singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
-
- #2,541
SEHEMU YA 464.
Roma mara baada ya kumwambia Diego kwamba atashughulikia kumuokoa mke wake , alisimamisha gari na kisha akaunganisha simu yake na GPS kwa kutumia Code maalumu , alifungua Aplication maalumu kwenye simu na kisha akaingiza herufi mfano wa Serial number na palepale simu ilianza kutafuta kwa kasi na ndani ya dakika kidoti cha rangi nyekundu kilionekana juu ya Ramani nje kidogo na jiji la Dar es salaam.
Namba alizoingiza kwenye simu zilikuwa za kifaa maalumu ambacho aliwapatia wanawake wake kubonyeza pale watakapokutana na Clone ya Yan Buwen , ni kama Panick Button lakini ambacho kinatoa mawimbi ambayo yanaweza kunaswa na mfumo wa GPS.
Roma baada ya kuona kifaa hicho kinafanya kazi alifikiahitimisho moja kwa moja mtekaji aliacha kiwe kinafanya kazi kwa ajili ya yeye kumtafuta.
Ali’zoom’ ramani kusoma jina la eneo ambalo kidoti chekundu kunaonyesha na jina lilisomeka Lugoba , ni sehemu ambayo haikuwa akiifahamu lakini alijua ipo ndani ya mkoa wa pwani na ni kilomita kadhaa kutoka Dar.
Hakutaka kujishauri mara mbili alishuka kwenye gati akaangalia kulia na kushoto na aliona hakuna mtu anaemwangalia na palepale alipotea .
Roma alikwenda kutokezea kwenye kichaka mita kadhaa kutoka barabara inayoelekea Tanga kutuokea Chalinze , sehemu alitokezea kulikuwa na sheli ambayo ilionyesha kutelekezwa lakini upande wa kulia kwake kulikuwa na boma la kanisa ambalo lilionyesha halitumiki.
Alitumia uwezo wake wa kijini kukagua enelo lote na kisha alitembea kufuata uelekeo wa kanisa.
Edna hakuwa amefungwa lakini alikuwa amejikunyata kwenye kona upande wa kushoto huku akionyesha kutetemeka kwa woga na hata sura ilimpauka, alitia huruma kwa mwonekano wake.
Upande wa kulia kwake eneo liliojengwa kama kimbweta alionekana mwanaume mweusi tii aliekuwa amenyoa kipara na kuvaa mavazi ambayo yalikuwa ni kama ya wale watu wanaosalia Budha , alikuwa na shanga nyingi amezivaa kwenye shingo na mwili wake ulionyesha kuwa ni wenye kushiba mazoezi.
Mkononi alionyesha kushikilia kitu kama Medali lakini ambacho kimefungwa na mkufu au Chain na kuandikwa kwa ligha isiokuwa ya kawaida.
Edna alikamatwa muda ambao alikuwa akitoka nyumbani akianza safari ya kuelekea kazini , alisimamishwa njiani kabla hajaingia ndani ya barabaa ya Bagamoyo na aliposimamisha gari alijikuta akipoteza fahamu bila hata ya kujielewa na alipokuja kushituka alikuwa ndani ya jumba hilo bovu ambalo aligundua lilikuwa ni kanisa.
Edna alijaribu kukimbia lakini miguu yake ni kama ilikuwa imefungwa kwani alishindwa kupiga hatua, ni kama alikuwa ameshikiliwa na kamba kutoka nyuma yake.
“Inaonyesha mpenzi wako hakujali kabisa , kwanini mpaka muda huu hajajitokeza tu bado”Aliongea yule mwanaume kwa lugha ya kingereza huku akionyesha sura ya kukosa uvumilivu, alikuwa na rafudhi ambayo Edna alishindwa kujua mtu huyo ni wa nchi gani au kabila lipi, alijua sio mtanzania kutokana na kushindwa kuzungumza kiswahili.
Edna alishindwa kujibu zaidi ya kuendelea kujikunyata kwenye kona huku akitamani Roma atokezee , hata hivyo kwa muonekano wa huyu mtu alionyesha kabisa alikuwa na uadui na Roma, maana hakuonekana mtu wa kawaida kabisa kwake.
Baada ya mwanaume yule kuona Edna haongei chochote alimsogelea na kuanza kumchunguza kwa kumwangalia vizuri na alijikuta akitabasamu kifedhuli na kilichonekana zaidi ni meno , alikuwa mweusi kuliko isivyokuwa kawaida ni kama amepakwa masinzi.
“Unaonekana kuwa mrembo sana , kwenye maisha yangu sijakutana na mwanamke Kiafrika mwenye muonekano kama wako , kama nisingekuwa na kitu kingine ninachohitaji nisingekuacha salama”Aliongea na kumfanya Edna kuzidi kutetemeka alijiambia akibakwa na huyu mwanaume atajiua kuliko kuishi na kumbukumbu ambayo hatoweza kuvumilia maisha yake yote, alishasahau kabisa hata Roma alimfanya bila ya ridhaa yake.
“Ineonyesha umechoka kuishi”Sauti nyuma yake ilisikika na kumfanya Edna kunyanyua macho haraka na kuangalia mbele na alijikuta akijawa na ahueni mara baada ya kumuona Roma.
Yule mwanaume mara baada ya kumwangalia Roma alianza kuongea mwenyewe kwa lugha ambayo haikueleweka ilikuwa ni ya kabila gani , lakini palepale kile kichuma mfano wa medali alichoshikilia kilianza kutoa mwanga mkali , ni kama vile kioo kinapolengeshwa na jua na kuakisi mwanga wake..
Muda ule ule yalionekana maputo kama ya kupuliza lakini haya yalikuwa ya kichawi yakijitengeneza hewani na kuanza kumsogelea Roma na palepale aliinua mkono na yale maputo ni kama yalipulizwa na upepo kwani yalimsogelea Roma kwa kasi , lakini kabla hata hayajamfikia Roma aliyabadilisha mwelekeo.
“BOOM!”
Yalipasuka yote lakini nguvu yake ilikuwa kama ya bomu kwani yalibomoa kipande cha dirisha kuruka nje.
Roma aliguna baada ya kuona maajabu hayo , alimkagua yule mwanaume na kugundua hakuwa binadamu wa kawaida, alikuwa ni jini kabisa ambalo limejitengenezea mwili, lilikuwa kwenye levo ya Nafsi kwa Roma alivyopima uwezo wake.
Roma mara baada ya kitedo kile cha maputo kupasuka alisogea kwa kasi kumsogelea yule Jini, lakini alipokaribia yule Jini mweusi aliinua mkono na kunyoosha kile kimedali na Roma alikumbana na nguvu ambayo ilikuwa kama upepo ambayo ilimrudisha nyuma kwa nguvu.
Roma alijikuta akishangaa mno kwa tukio lile , hakuamini anaweza kudhibitiwa na kifaa ambacho kilionekana kama kijichuma tu kwake.
Alijikuta akikumbuka baadhi ya maneno ya Zenzhei kuhusu uwepo wa Dhana katika miliki za kijini, aliamini huenda alichoshika yule mwanaume ndio moja wapo ya dhana hizo.
“Chukua hio”
Aliongea yule mwanaume na palepale macho ya Roma yaliweza kuona Rungu la kichawi ambalo lipo kama chuma likija kwa kasi huku likitoa msisimko wa kuwa na nguvu isiokuwa ya kawaida.
Roma hakutaka kuzembea aliita nguvu za kijini na kisha kutengeneza ngao na kuzuia lile Nyundo na alifanikiwa kwani baada ya nyundo ile kugongana na nguvu yake ya kijini lilirudishwa nyuma kwa spidi kurudi kwa alielituma lakini kabla halijamfikia yule jini mweusi palepale lilirudi tena kwa kasi kwenda kwa Roma kwa mara nyingine
“Hehe… ngoja uonje nini maana ya nguvu halisi Kivimbo , unafikiri nimekuja bila ya kujipanga”Aliongea huku akichekelea
Roma alikasirishwa na kauli yake , alimdharau adui yake kwa kuwa katika levo ya nafsi lakini aligundua kile alichoshikilia mkononi ndio siraha yake kubwa ambayo ni kama imeongeza uwezo wake kwa zaidi ya mara mbili.
Roma alijiambia kama kweli ujinini kuna vitu vyenye nguvu kubwa kama hivyo , basi kama atakutana na jini ambalo lipo kwenye levo sawa na yake na kumiliki dhana za namna hio huenda anaweza asifanikiwe kushinda.
Edna alikosa ujasiri wa kuangalia yale mapigano na alipofungua macho na kuona Roma hajapatwa na madhara yoyote alijikuta akiwa mwenye ahueni.
“Edna usiogope tena nipo hapa kwa ajili yako”Aliongea Roma mara baada ya kuweza kupita upande wa Edna .
“Jamani inaonyesha mnapendana sana hadi nawaonea wivu mimi”Aliongea yule mwanaume na Lipsi zake hazikuweza hata kuonekana zaidi ya meno , Roma alijiambia kama utakutana na mtu mweusi namna hii muda wa usiku basi kama huna ujasiri unaweza kukimbia nduki.
“Wewe ni nani?”Roma aliuliza.
“Jina langu halina umuhimu kwako , ambacho ni muhimu ni kile ninachotaka kutoka kwako”Aliongea .
“Unataka nini kutoka kwangu?”
“Andiko la Urejesho”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa na palepale maswali yalibuuka na kujiuliza je huyu ndio yule aliekutana nae nchini China wakati alipoenda na Magdalena.
“Na kwanini nikupatie?”
“Tusema ni kama biashara, nitamuacha mkeo kuwa hai na mimi utanipatia ninachotaka”
“Unadhani unaweza ukanishinda, sijatumia hata robo ya uwezo wangu wote nitakupatia kifo ambacho hakitakuwa na maumivu kama utaniambia ninachotaka kujua kutoka kwako”
“Kama unapanga kuniua basi mkeo atatangulia kwanza”Aliongea.
“Unamaanisha nini?”Aliongea Roma na kumfanya Edna aliesimama kumsogelea Roma.
“Ushawahi kusikia laana ya kutupiwa ya kichawi inayohusiana na minyoo?”Aliuliza na kumfanya Roma kuanza kufikitia.
“Unamaanisha umemtpia mke wangu Laana?”Aliongea na kumfanya Edna kuchanganyikiwa baada ya kusikia kauli hio.
“Nimetumia mbinu yangu maalumu niliokuwa nayo kwa muda mrefu, ni laana ya minyoo ambayo akitupiwa binadamu na kuingia kwenye mwili wake inaweza kumuua kwa kutoboa moyo”Aliongea
Edna baada ya kusikia ndani ya mwili wake kuna minyoo alijikuta akihisi kichefu chefu muda ule ule.
“Tokea nimesafiri mpaka kufika hapa nilikuwa najua ungeniua kirahisi ndio maana nikawa mbele ya muda , nasikia unasifika kwa ukatili wa kutosamehe maadui zako hivyo ukinua na mkeo anatangulia”
Roma alimuwekea Edna mkono kwenye eneo la kifua kujaribu kumpima kama kuna nguvu ya ziada ndani ya mwili wake na kweli aliweza kuhisi vitu visivyokuwa vya kawaida vikitambaa ndani ya kifua, Roma alijikuta akijawa na wasiwasi mpaka Edna akaogopa kwani hajawahi kumuona Roma akiwa na wasiwasi wa namna hio.
“Niko sawa Roma , sio kama anavyoongea”
“Binti nadhani huelewi hata ninachoongea , unajihisi uko sawa kiafya, ni kwasababu sijawapa maelekezo watoto wangu kukutoboa ndani kwa ndani”
“Sijisikii chochote ndani ya mwili wangu, ninaweza vipi kukuamini kama unaongea ukweli?”Aliongea Edna huku awamu hii akiwa na hali ya kujiamini , ile hali dhoelefu ya kiburi cha kuzaliwa ilianza kujionyesha.
“Nadhani huelewi , nimesema ni laanna na sio sumu”Aliongea na kisha akatabasamu kifedhuli.
“Arrgh!!”
Edna alijikuta akitoa kilio cha maumivu huku akishikiria shingo yake , alijihisi ni kama vile anameza watoto wa nyoka kwenda tumboni , maumivu yake hayakuwa yakielezeka na alijikuta akitapika palepale na kilichoonekana sio chakula kutoka tumboni bali alitema damu.
“Ednaa!!”
Roma alijikuta akishistushwa na kitendo kile na kumshikilia haraka na kisha kumwingizia nguvu za kijini kutuliza maumivu.
“Umemfanyia nini?”Aliuliza Roma huku jicho lilikuwa jekundu mno.
“Punguza presha nimeruhusu minyoo itoboe kidogo ili kukuaminisha kwamba siongei utani”Aliongea
Roma alikuwa na hasira kiasi ambacho alitamani kumuua palepale , lakini alishindwa kufanya hivyo kwani usalama wa Edna ulikuwa ni kipaumbele.
“Roma .. naogopa .. sitaki kufa na kumuacha Lanlan”Aliongea Edna huku akianza kulia.
“Edna huwezi kufa , utaondoka hapa ukiwa salama”Aliongea Roma kwa kumfariji na palepale alijikuta akipata tumaini baada ya kufikiria kitu , alijiambia vipi kama atatumia uwezo wake wote kumwingizia Edna nguvu ya kimaandiko ndani ya mwili wake na kuua laana hio ya kutupiwa ya minyoo.
“Nakushauri usije ukatumia nguvu za kijini ukidhamiria kuwaua ,watapasuka ndani kwa ndani na mkeo atakufa kifo cha maumivu makali mno”Aliongea jini mwuesi.
Roma ilibidi amwingizie kiasi kidogo cha nguvu ya kijini kwenye mwili wake ili kumponyesha maumivu na ilisaidia kwani maumivu yalipotea lakini hakuacha kutoa kilio ,Edna kwenye maisha yake hakuwahi kuhisi maumivu ya aina hio , aliogopa kile kilichopo ndani ya mwili wake kwani alihisi kabisa vitu kama nyoka vikitembea tembea ndani ya mwili wake, Roma ilibidi amkumbatie huku akimuonea huruma.
“Kama nitakupatia unachotaka , je unanihakikishia utamwondolea hio Laana?”Aliuliza
“Hakika , Hao ni watoto wangu na nimewakuza kwa zaidi ya miaka kumi nitapata hasara kama nitawatumia kwa binadamu wa kawaida kama mkeo , lakini..”
“Lakini nini?”
“Sikuamini kabisa , ninachotaka uniruhusu kwanza nikufungie uwezo wako wa kijini kwanza ili kuhakikisha kwamba huwezi kunishambulia , nitakapona sio tishio kwangu na kupata ninachotaka basi nitamwoneolea mkeo laana yangu”Aliongea
“Kwahio unaniona mimi ni mjinga , kama nitakuruhusu ufungie uwezo wangu wa kijini utaniua kirahisi”
“Kwahio una chaguzi ipi nyingine , hapa tunazungumzia ni aidha ukubaliane na mimi nifungie uwezo wako wa kijini nichukue ninachotaka au mkeo afe ukiwa unamwangalia”.
Roma alijikuta akipandwa na hasira kwani hakujua huyu mwanaume anaenda kufanya nini kufungia uwezo wake wa kijini , aliogopa anaweza kuvuliwa nguvu zake zote za kijini na alijiambia hata kama anao uwezo wa kutumia kanuni za anga kama alivyofanya kwa Drogba na Mourihno kwa jini ambalo lipo kwenye Levo ya Nafsi asingeweza kufanikisha ndani ya muda.
“Roma usimsikilize anachotaka ni kukuua tu , anataka kunitumia mimi kama chambo kwasababu hana uwezo wa kukuzidi , Roma najua unao uwezo mkubwa hivyo unaweza kumua na kisha kuniokoa na mimi”Aliongea Edna kwa msisitizo huku akiwa amemshika mkono.
Roma alijikuta akimwangalia Edna kwa uchungu mwingi.
“Edna mke wangu nisamehe tu kwa leo nitakuangusha , lakini siwezi kukuangalia ukifa , nitampatia anachotaka”Aliongea Roma kwa huzuni huku akimfuta machozi kwa mkono wake wa kushotO
SEHEMU YA 465
Edna alikuwa kama haamini maneno ya Roma , hakuwa pia tayari kuona Roma anapoteza nguvu kwa ajili yake, ni kama aliogopa ataishi kwa kuwa na deni maisha yake yote.
“Kwahio unamaanisha utamuachia afanye kama anavyotaka?”
“Nina uhakika ninaweza kumuua kwa pigo moja tu , lakini siwezi kuhatarisha maisha yako , natamani nikusikilize lakini siwezi , sio kwa muda huu..”
“Wewe usifanye hivyo ..”
“Najua nimekuumiza mara kibao nadhani hiki ndio ninachostahili kama adhabu , kama sio mimi usingekuwa kwenye hali hii ya hatari hivyo siwezi kuruhusu ukipoteza maisha”Aliongea Roma na kumfanya Edna machozi kuanza kujitengeneza kwenye macho yake.
“Usifanye chochote cha hatari kama nitakufa naamini atakuacha hai, anachotaka ni nguvu zangu za kijini na nitampatia , ukishatoka hapa tumia simu yangu kupiga simu namba ya mwisho nilioipigia”Aliongea Roma na kisha alitoa simu yake na kumpatia Edna ambaye aliipokea kwa wasiwasi, baada ya kuipokea aliitupa chini.
“Sitaki simu yako , huwezi kuniambia unataka kufa halafu umeniumiza sana na kunikasirisha, ukifa kabla sijakusamehe nitakuchukia milele”
“Edna usifanye hivyo , nisikilize tafadhari ..”
“Mimi sitaki, unaruhusiwa kufa baada ya sisi kufunga ndoa , huwezi kuniahidi kitu halafu usitimize”Aliongea huku akianza kukasirika na kutoa machozi kwa wakati mmoja.
“Edna kaa pembeni na kaa kimya, nishafanya maamuzi tayari na ukinizuia nitakufosi ufanye ninavyotaka”Aliongea Roma kwa kumfokea na kumfanya Edna kumwangalia kwa wasiwasi akiwa haamini kama Roma kweli anataka kufanya kama alivyopanga.
“Hahaha.. nyie ndege wawili mpendanao , mshamaliza kuongea?”Aliuliza yule mwanaume .
“Fanya unachotaka”Aliongea Roma.
“Ndio ndio”Alijibu na palepale kisu mfano wa daga rangi ya silver kilionekana kwenye mikono yake , haikuwa Dagger ya kawaida bali ya kichawi ,ilikuwa ikitoa msisimko wa ajabu mno.
“Hii ni Dhana ya zama za kale inafahamika kwa jina la Dragoni Dagger , ni sehemu ya siraha nne za kijini ambazo zina uwezo wa kuzuia nguvu za kijini kwenye mwili wa mtu ambaye amefikia kwenye levo ya kuipita dhiki , ni kama sumu hivyo kama utajifanyisha mjanja kutaka kuutumia uwezo wako basi utakufa hapo hapo, najua Nguvu ya kimaandiko inaweza kuponyesha moyo wako hivyo..”Aliongea
“Kwahio unataka kunichoma kwenye moyo wangu?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“Ndio ninachomaanisha”
“Sasa nakupaje nguvu zangu za kimaandiko?”
“Ni rahisi sana”Aliongea na kisha akatoa kifaa flani kama kibuyu lakini kilichotengenezwa na malighafi ya Jade.
“Unachotakiwa kufanya ni kuruhusu nguvu zako zote za kijini kuingia kwenye hii dhana na mimi nitaweza kuthibitisha kama nguvu ya kimaandiko ni halisi ili usije ukanidanganya na baada ya hapo nitamwondolea mkeo laana”Aliongea
Roma alishangazwa na mwonekano wa kile kijifaa baada ya kukishika, ni moja wapo ya Dhana ambazo aliweza kusikia kutoka kwa Zenzhei na alijiambia hawezi kutegemea uwezo wake pasipo kuwa na moja ya wapo ya Dhana kama atahitaji kuwa na nguvu nyingi za kushinda hata majini kutoka Hongmeng.
Roma alishindwa pia kumjua mwanaume aliekuwa mbele yake ni miliki gani anatokea mpaka kumiliki Dhana za aina hio.
“Nitaingiza nguvu yote ya kimaandiko kwenye hii Dhana na nitakupatia kuithibitisha na utakapoweza kuona ni halisi basi nitatumia hio Daga kujichoma moyoni na utakaporidhika nimekuwa dhaifu utamuondolea mke wangu Laana”Aliongea Roma.
“Deal”Aliongea kwa shauku baada ya kuridhika na maelezo ya Roma .
Edna alijikuta ngozi yake ikiota vipele mara baada ya kusikia Roma angejichoma na Daga kwene eneo la moyo.
“Roma jamani acha kuwa mjinga, huoni anataka kukuua”Aliongea Edna kwa kufoka.
“Kimya! , ninafanya haya kwa ajili ya maisha yako hivyo usiingilie”Aliongea Roma na kumfanya Edna kujawa na hasira huku machozi yakitiririka kwenye macho yake.
Yule jini mweusi alionyesha kufurahishwa na maongezi hayo , mpaka hapo alijiambia anayakaribia mafanikio.
“Fanya haraka unipatie nguvu za kimaandiko , Minyoo yangu ninaweza kushindwa kuiongoza ikihisi njaa”Aliongea na kumfanya Roma kupandwa na hasira lakini hata hivyo hakuwa na namna kwa wakari huo zaidi ya kutiii shuruti kwani kwake Edna alikuwa muhimu.
Alifumba macho huku akiwa ameshikilia ile Dhana ya kibuyu na kulengesha mkono karibu na mdomo wa ile Dhana na palepale kulionekana mfano wa mvuke ukiingia ndani.
Baada ya dakika kumi za Roma kuwa makini kuhamisha nguvu zake za kimaandiko alifumbua macho na kisha alimrushia yule mtekaji kile kibuyu baada ya kuona amemaliza.
Baada mtekaji kuridhika ilikuwa nguvu halisi ya kimaandiko alimrushia Roma ile Daga.
“Hakikisha unafanya kama tulivyokubaliana”Aliongea Roma.
“Fanya hivyo haraka sina muda wa kupoteza”Aliongea na Roma alifumba macho na kisha alijidunga na ile Daga eleo la kifuani akilenga moyo na palepale damu ziliruka mara tatu .
Roma alishindwa kuvumilia maumivu na palepale alidondoka chini kwa kupiga magoti huku uso wake ukionyesha kupauka kwa haraka sana.
“Romaa...!!” Edna aliita akimkimbilia pale chini kwa wasiwasi.
Roma alikuwa akijihisi maumivu, ijapokuwa nguvu ya kimaandiko haikuwa imetoka yote hivyo kujaribu kumponyesha, lakini alihisi maumivu makali kwani spidi yake ilikuwa ya chini mno kupona.
Dakika kadhaa mbele mwili wake ulianza kupoteza nishati ya mbingu na Ardhi na kuendelea kuwa dhaifu.
Sasa hapa utofautishe vitu viwili, kuna nguvu ya kijini ya kimaandiko ambayo inamsaidia kupona lakini pia kuna nguvu ya kijini ya kinishati ya mbingu na Ardhi , ni kama ilivyo kwa Omari au kwa jini ambalo lipo mbele yake , ijapokuwa lilikuwa na nguvu ya Nishati ya mbingu na Ardhi lakini halikuwa linamiliki nguvu ya kimaandiko kutokana na kutumia njia fupi ya kujifunza mbinu za kijini.
Hivyo Daga ilikuwa ikimzuia Roma kutumia nguvu zake za nishati za mbingu na Ardhi ili bwana aliekuwa mbele yake aweze kumponyesha Edna kwa kumuondolea laana na baada ya hapo aweze pia kutoroka kwani Roma hatokuwa na uwezo wa kumdhibiti kwasababu angekuwa ni dhaifu sana kufanya hivyo.
Yule mtekaji mara baada ya kupokea kile kibuyu, alitoa kijisahani kama cha Plastiki lakini ambacho kilionyesha kutengenezwa pia na madini ya Jade na kisha aliruhusu zile nguvu ambazo zipo kwenye ile Dhana ya kibuyu kutoka na kuvamia kile kisahani na palepale maandishi yalianza kujitengeneza kwenye kile kisahani , yalikuwa ndio maandiko ambayo yanaitwa nguvu ya urejesho.
“Nitasoma kwanza haya maandishi na baada ya hapo ndio nitamuondolea mkeo laana”Aliongea akimwangalia Roma ambaye amepiga magoti huku akiugulia maumivu.
“Hakikisha unatimiza ahadi yako”
“Haupo kwenye nafasi ya kuniambia kipi nifanye , wewe ni binadamu wa kawaida ambaye hukupaswa kumiliki kitu muhimu kama hichi , tamaa zako za kutaka kumiliki visivyo vyako ndio zinakuua sasa”
Edna alipatwa na wasiwasi na kisha akashika ile daga
“Unataka kufanya nini?”Aliuliza Roma
“Utakufa Roma kama damu zitaendelea kukutoka, ninaitoa hii daga , anakudanganya tu hawezi kuniondolea laana”
“Edna nisikilize mimi usifanye hivyo”Aliongea Roma kivivu na kumfanya Edna kuanza kulia akiamini Roma anakwenda kufa.
Yule mwanaume mara baada ya kusoma maandishi na kuridhika alioneysha tabasamu.
“Nadhani tumefikia mwisho wa kubagain”
“Okey fanya haraka na mwondolee mke wangu hio laana”
“Sio mbaya nitafanya hivyo , uwezo wako naona umeshuka mpaka kufikia nusu mzunguko , ngoja tumalizane sasa”Aliongea.
Palepale alianza kuongea maneno yasioeleweka kwa spidi kubwa kwa zaidi ya dakika mbili na Edna alijihisi kutapika kwani kuna vitu ambavyo vilikuwa vikitoka tumboni kwa fujo namna ambayo hata yeye alishindwa kuelewa lakini ajabu hakuweza kuona chochote zaidi ya kuhisi mwepesi baada ya vitu kumtoka.
Roma alijikuta akivuta pumzi ya ahueni mara baada ya kuona Edna ashaondolewa ile laana ya minyoo.
Edna alijikaza na kisha akamshikilia Roma vizuri na kumsimamisha, Roma alikuwa dhaifu mno.
“Roma usije kufa kwenye mikono yangu sasa hivi tafadhari jikaze”Aliongea Edna kwa kubembeleza, hakuwa tena CEO wa kampuni kubwa bali muda huu alikuwa akifanana na mtoto ambaye anaomba hela kutoka kwa mzazi.
Alijikuta akianza kujutia kwa kosa lake la siku ya jana la kumfukuza kuondoka nyumbani, alijiambia huenda yote hayo yasingetokea
“Usijali mke wangu siwezi kufa, nitaweza kupona”Aliongea Roma akimfariji.
“Huwezi kujiponyesha , nimesema ninaweza kumuondolea mkeo minyoo lakini kuhusu wewe siwezi kukuacha hai”Aliongea yule mtekaji.
“Wewe muuaji?”Edna alijiktua akitetema kwa hasira mara baada ya kusikia ile kauli.
“Haha..Sijaahidi chochote mimi”Aliongea na kumfanya Roma kufumba macho yake na kisha alishikilia ile Daga na kuichomoa kwa nguvu na damu zilitoka kidogo tu na kuacha, lakini hata hivyo Roma alijaribu kuita nguvu za kijini lakini ilionyesha sumu ya ile Daga ilikuwa ikimzuia kufanya chochote.
“Huwezi kuepuka kifo siku ya leo”Aliongea huku akianza kuminya vidole vyake na palepale aliita nguvu za kijini na kunyoosha ile medali kuelekea aliposimama Roma na Edna, palepale lile Rungu la kichawi liliibuka tena hawani likimsogelea Roma kwa kasi.
BOOM!
Kabla lile Rungu halijamkaribia Roma mlipuko ulitokea kwenye mikono ya yule mtekaji na kilicholipuka hakikuwa kingine bali kile kibuyu Roma alichoingiza nguvu ya kimaandiko.
Ulikuwa ni mlipuko mkubwa ambao uliondoka na nusu ya mkono wa metakaji huku yeye mwenyewe akirushwa na kwenda kutua kwenye ukuta wa kanisa na kufanya uchafu uliokuwa juu kuanza kudondoka chini kwa mtikisiko.
Edna alijikuta akiziba mdomo wake kwa mshangao akiwa haamini kile ambacho alikuwa akiangalia.
Roma alitoa tabasamu la kifedhuli na kisha aliruhusu nguvu ya kijini na kisha akakusanya sumu ya Daga iliokuwa ndani ya mwili wake na kisha akaikausha yote mara moja na palepale mwili wake ulianza kujiponyesha kwa kasi mno.
Upande wa mtekaji alikuwa ametapakaa damu zake yeye mwenyewe akiwa chini akigulia maumivu , ashapoteza mkono lakini pia ilionyesha damu zilikuwa zikivilia ndani kwa ndani ya mwili baada ya kukohoa na kutema damu.
“Umenifanyia .. nini?”Alianza kuongea huku akijikaza na maumivu akiwa haamini kila kitu kimebadilika.
“Ni kama ulivyosema wewe , sijakuahidi chochote baada ya kuondoa laana kwenye mwili wa mke wangu, ushajua mimi ni mtu wa aina gani lakini ukatoka huko ulikotoka na kuja kunichokoza , unaonekana unakipenda kifo kuliko uhai na nitatimiza unachotaka”aliongea Roma huku akitembea kwa kumsogelea.
Edna macho yalimtoka hakuamini yule Roma dhaifu alikuwa sawa kama vile hakuna kilichomtokea.
“Hapana haiweizekani, uwezo wako ulikuwa upo kabisa kwenye nusu mzunguko” Aliongea kwa hamaki na Roma baada ya kumkaribia alikanyaga ule mkono uliokatika.
“Arrgh!”
Edna alijikuta akigeuka nyuma pasipo ya kupenda yeye mwenyewe, kilichokuwa mbele yake kilimuogopesha kuangalia,
“Haujui hata ni kwa namna gani nilivyoweza kugeuza maandishi kuwa nguvu lakini bado unahitaji nguvu zangu” Aliongea Roma huku akitabasamu kwa kejeli.
“Unamaanisha nini?”
“Nilichokupatia sio maandiko halisi bali nilikuwekea mtego kwa kutumia maandishi, upo levo ya chini mno kuelewa nilichokifanya ndio maana ukaamini kweli nilichokupatia ni kitu halisi , sio kweli bali nilikutengenezea bomu” Aliongea Roma na kumfanya yule mtekaji kuanza kukata tamaa , mpaka hapo alijua hana cha kufanya zaidi ya kusubiri kifo chake kwani keshazidiwa ujanja.
Alimdharau Roma kwa kuona kwamba walikuwa kwenye levo sawa na yeye ndio maana hakuchukua tahadhari na hilo ndio kosa lake , Roma akamdhibiti kwa kutumia mpango wake mwenyewe.
“Sasa ni muda wa kuniambie wewe ni nani , na nani kakutuma”Aliongea Roma.
“Niue tu”
Crack!
Roma aliongea kwa vitendo , alipindisha mguu wake kwa nguvu na kukatika palepale. Na kumfanya kupiga ukulele.
Roma aligeuka nyuma na aliona ni afadhali Edna hakuwa akiangalia kile alichokifanya maana alikuwa akidhamiria kufanya ukatili wa hali ya juu.
“Utaniambia au niendelee”
“Siwezi kukuambia chochote , hata hivyo ninakwenda kufa”
Roma alichukua ile daga iliotumika kumchoma kifuani na kisha alimchana mtekaji eneo la tumboni kama anafanya upasuaji na kufanya damu kutoka nyingi huku viungo vya ndani vikionekana ikiwemo Ini.
“Argg!”
“Uniambie usiniambie ni chaguo lako , ila nitahakikisha nakata kiungo kimoja kimoja kadri utakavyoshindwa kujibu swali langu , nakushauri ufanye maamuzi maana unaweza kuongea mwishoni na vivungo ukawa huna”Aliongea Roma na kumfanya Mtekaji kuanza kujawa na hofu mno.
Roma alipanga kukata maeneo ambayo yasingemfanya adui yake kupoteza maisha haraka kwani alikuwa akiijua vizuri anatomi ya mwili.
“Wewe ni pepo kichaa na huwezi kupona kwa sumu iliopo kwenye mwili wako”Mtekaji aliongea kwa hasira.
“Wrong answer “Aliongea Roma na kukata kwa mara nyingine, ile daga ilikuwa na makali mno kama wembe.
“”Nishafeli kwenye misheni yangu tayari, kama sitokufa kwa mikono yako nitakufa kwa mikono ya walionituma, hivyo kuna haja gani ya kukupatia majibu ili uridhike”Aliongea na palepale mwili wake ulianza kukakamaa na damu zilianza kumtoka mfululizo kwa kila tundu kama vile mgonjwa wa Ebola na ndani ya dakika chache tu mwili wake ulianza kuoza kwa spidi kubwa kiasi cha kusababisha harufu kali mno.
Roma alijikuta akishangazwa na jambo kama hilo , alijuwa mwanaume huyo alikuwa na uwezo wa kutawala minyoo ambayo inaweza kula moyo wake lakini hakuamini kama anaweza kujiua mwenyewe kwa kuozesha mwili wake aliona ni kama alishajiwekea mtego wa kujimaliza mambo yatakapoenda kombo.
Alijikuta akiwa na wasiwasi na kujjiuliza kaama mtu huyoa metumwa kwa ajili ya nguvu zake za kijini , je hao waliomtukma anaogopa wangeuuwa wana uwezo mkubwa kiasi gani.
Roma alijiktua akiwaza kwa muda mfupi huku moyo wake ukiwa mzito, alijiambia kwanzia muda huo ni kuwalazimisha wanawake wake kuanza mazoezi ya kujifunza mafunzo ya kijini kwa haraka , kwani kama maadui zake wangekuwa na nguvu kubwa asingeweza kuwalinda.
Aliangalia lile rungu la kijini likiwa bado lipo chini na ile medali pia ilikuwepo chini , aliinama na kuviokota vyote . Roma alishika ile Medali na kuanza kusoma maandishi yake, lakini lugha ilikuwa ngumu kuielewa hivyo aliachana nayo , alitumia kanuni za anga na kisha alificha kwenye Space storage
Baada ya kuhakikisha hajaacha kitu muhimu aligeuka na kumsogelea Edna ambaye bado alikuwa upande wa nyuma kabisa akiogopa kusogea mbele kwani hata harufu ilikuwa ikimfikia.
Alimwangalia Roma kwa wasiwasi, hata hivyo alishaanza kumzoea Roma kwani kwake kuua ni jambo la kawaida.
“Edna umepata mshituko mkubwa kwa yaliotokea siku ya leo , Vipi unajisikia vizuri sasa?”
“Maneno ambayo ulikuwa ukiongea, je kila kitu ulipanga..?”Aliuliza Edna.
“Unaweza kusema hivyo , nisingemwaminisha asingekuwacha hai ndio maana nilikuigizia hata wewe uamini natoa nguvu zangu kweli”Aliongea Roma.
“You bastard”Aliongea Edna kwa kufoka , hakuamini alikuwa amechezewa akili bila ya kujitambua na kulia vyote vile.
SEHEMU YA 466
Edna alijikuta akiinua mguu wake wa kulia na kisha kumpiga teke Roma kwa hasira.
“Umeufanya moyo wangu kuumia kwa kujua kabisa unakwenda kufa , kama ilikuwa mpango kwanini hukuniambia hata kwa ishara, ulikuwa ukifurahia mimi kulia mbele yako au ndio kinilipizia kisasi?”
“Sikuwa na chaguzi nilitakiwa kumfanya aniamini kwa namna yoyote ile , ilitakiwa aamini kweli ninakufa kwa kuona machozi yako, ningekutarifu angeshitukia mchezo”
“Vipi kama angekataa kuniondolea laana alioniwekea ya minyoo ungekubali kufa kwa ajili yangu?”Aliuliza Edna.
“Edna mke wangu nishakuambia kwamba kadri nitakavyokuwa naishi nitahakikisha na wewe unaishi vilevile”
“Kwahio ndio unachotaka, tuseme kwamba tungekufa wote hukoi kuzimu bado ningekuwa na deni kubwa kwako kwa kujua umekufa kwa ajili yangu. si ndio ilikuwa mpango wako?”
“Muone sasa , kuna haja gani ya kuanza kukumbuka yaliopita wakati muda huu tupo salama”Aliongea Roma.
“Kwako hili linaweza lisiwe la umuhimu ila kwangu ni muhimu sana , umetumia maisha yako kuokoa ya kwangu”
“Hukumbiki hata wewe ulinidanganya kwa kuniaminisha kampuni yako inafilisika?”
“IIe ni kwasababu..”Alikosa usemi
“Niliamini usingekasirika baada ya kuekuelezea baada ya matokeo”
“Upo sahihi baada ya siku ile kugundua ukweli sikuweza kuwa na kinyongo juu yako licha ya kwamba sikupenda njia yako , kwasababu nilikuwa nikielewa nia yako halisi , naamini hata wewe pia utaweza kunielewa kwa nilichokifanya”
“Vyovyote vile kikubwa uhai”Aliongea Edna
Roma alitaka kumkumbatia Edna kwa nyuma lakini alikumbuka bado walikuwa kwenye ugomvi na hawakuwa wamesameheana na alikuwa akijiuliza kama Edna ameshasamehe.
“Tunapaswa sasa kuriudi , Recho alikuwa na wasiwasi kweli , ni kheii ukampigia simu muda huu”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa na kuokota simu ya Roma na kumpigia na baada ya hapo Roma alimvuta kwake na kumkumbatia kifuani.
“Nitafanya hivi kwa ustaarabu , fumba macho yako kwani unaweza kushindwa kuvumilia utakachoona”Aliongea Roma.
“Unamaanisha tunapaa kurudi mjini?”Aliongea Edna pasipo kuamini kama angepaa kwa mara yake ya kwanza.
“Unafikiri ni kwa usafiri upi tutaondoka nao hapa kurudi hii ndio njia pekee rahisi”
Edna alijikuta akifumba macho yake na ndani ya muda mfupi tu Roma aliweza kutua nje ya eneo la bustani kwenye nyumba yao.
“Unaweza kuangalia sasa tumefika”Aliongea Roma
Edna baada ya kufumbua macho yake alijikuta akishangaa mno , hakuamini kama ni kweli wapo nyumbani, ulikuwa ni uzoefu wa mara ya kwanza kuupata katika maisha yake.
Roma alinwangalia Edna ambaye alionyesha hali ya kushangaa kwa muda na Edna alivyogeuka kumwangalia Roma aliona alikuwa akimwangalia.
“Mbona kama unataka kuongea”
Roma alikuwa amefukuzwa nyumbani hivyo hakujua kama anapaswa kuingia ndani au aondoke na ndio maana alikuwa akisubiria maamuzi ya Edna.
“Ah… nishakufikisha nyumbani salama , nadhani napaswa kuondoka sasa”Aliongea Roma kimtego.
Edna alishindwa kuongea chochote zaidi ya kushikilia gauni lake la maua maua ambalo limechafuka kwa vumbi na damu.
Licha ya Edna kuishi na wazungu lakini mavazi yake muda wote yalikuwa yakivuka magoti, vazi pakee ambalo alikuwa akivaa kuonyesha umbo lake labda suruali, lakini alikuwa akiheshimu sana utu wake ,ni heshima ambayo wafanyakazi wake walimpendea lakini Edna yote hayo ni kutokana na malezi
Katika wanawake wa Roma ni Amina ambaye alikuwa akivaa kihasara hasara , ile hali ya kuishi Uingereza mpaka kutokijua kiswahili vizuri ilimjengea maisha ya kizungu.
Roma alitamani Edna aongee neno kwani alikuwa ashaanza kupiga hatua kuelekea getini, kwenye maisha yake hakuwahi kujihisi mdogo mbele ya mwanamke , hata kipindi alipokuwa na Seventeen alikuwa mbabe lakini kwa Edna maisha yake yalikuwa ya tofauti sana,
“Edna ndio naondoka hivyo kweli ujue”Aliongea Roma lakini Edna alimwangalia tu na alipogikia geti tu Edna aliongea na kumfanya Roma kusimama.
“Kwahio ndio unaondoka kweli?” Edna alivunja ukimya.
“Sitaki kukaa hapa huku nikiamini nitakukasirisha tena”
“Roma tangu lini ukawa mvivu wa kufikiria , wewe si umesema mwenyewe mara kibao unanipenda?, kama kweli unanipenda kwanini usingenibembeleza hata mara nne ile jana uliponikosea , Ulitakiwa kuniomba msamaha mara nyingi nyingi na kunibembeleza na ningejifanyisha kukusamehe , Roma wewe ni muongo sana hata hunipendi”Aliongea kwa hasira.
Jana hakudhamiria kumfukuza Roma ila alifanya vile ili Roma ahangaike kuomba msamaha, ilikuwa tabia ya wanawake kupendwa kubembelezwa pale wanapokosewa.
Roma mara baada ya Edna kuongea maneno yale alishangazwa na palepale alimsogelea na kumsukumia kwenye ukuta huku akimwangalia kwa ukaribu.
“Mimi sio muongo bali ni mwizi.. nimeiba moyo wako”Aliongea Roma na palepale alimkisi Edna mdomoni
Edna alishindwa kumzuia kufanya vile kwani viongo vyake ni kama vimepalalaizi , licha ya kuogopa Bi Wema angetoka na kuwaona lakini bado aliacha Roma afanye atakavyo.
“Ijapokuwa kuna mtu ameniambia sipaswi kumuambia mke wangu ‘I am sorry’ lakini naomba nikwambie ‘I am sorry’ kwa mambo mengi mabaya niliokufanyia , nakuahidi hakutatokea Rufi mwingine kwenye maisha yetu”
“Sitaki kusikia jina lake?”Aliongea Edna na kumfanya Roma kumuachia Edna baada ya kuhisi mlango wa kuingilia ndani unafunguliwa,
“Miss Edna usharudi”
“Ndio nimerudi Bi Wema”Aliongea Edna na palepale mlango ulifunguliwa na Bi Wema akatoka nje.
“Mr Roma nini kimetokea mbona nguo zenu zimejaa damu?”Aliuliza Bi Wema kwa mshangao.
“Bi Wema tulipata ajali ila tupo sawa , usiwe na wasiwasi”Aliongea Roma.
Bi Wema alijitahidi kutulia licha ya sababu ya Roma kumtia wasiwasi kwani damu zilikuwa nyingi mno ni kama wametoka buchani.
“Lakini kwa mwonekano huo mtakutana vipi na mgeni?”
“Kuna mgeni ? ni nani Bi Wema”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“Kuna mdada amefika hapa amejitambulisha kwa jina la Rufi”Aliongea Bi Wema na kauli yake ilimpa Roma ubaridi wa moyo.
Alishindwa kuelewa Rufi alikuwa akimtafutia nini mpaka kuja tena nyumbani kwake , ndio kwanza alikuwa ameyajenga na mke wake lakini ana haribu kila kitu , alijiambia awamu hii hawezi kumsamehe.
Edna na yeye baada ya kusikia kauli hio alijikuta akikasirika na kumwangalia Roma , moja kwa moja alijua huenda Roma alikuwa hajamalizna na huyo mwanamke, kama ni hivyo kwanini apate ujasiri wa kuja mpaka nyumbani.
“Ondoka” Aliongea Edna kwa hasira na kisha akaingia ndani , Bi Wema alishindwa kuelewa hasira za ghafla za Edna zinatoka wapi , aliijua lazima kuna tatizo.
Roma hakuondoka alifuata ndani ili kujua Rufi kaja nyumbani kwake kufanya nini , hakuwa tayari kumuacha Edna kuongea nae peke yake.
Rufi alikuwa amekaa kiwasiwasi ndani ya jumba hili huku akizungusha macho , kulia na kushoto ilikuwa nyumba nzuri mno kwa macho yake.
Mbele yake kulikuwa na glasi ya juisi lakini alionyesha hakuigusa hata kidogo , baada ya kumuona Edna ameingia hapo ndani alisimama kwa wasiwasi na kumwangalia kwa mshangao kutokana na kuchafuka kwake.
Alishangaa zaidi alipomuona |Roma na yeye akiingia akiwa amechafuka na damu mwili mzima.
“Ondoka nyumbani kwangu”Aliongea Edna kwa kingereza na Rufi alijikuta akivuta pumzi alitegemea Edna kuwa hivyo.
Roma aliekuwa nyuma alishangazwa na kauli ya Edna na kujikuta akivuta pumzi na kuangalia juu kwenye ceilingboard, akitafakari namna ya kudhibiti hali hio pasipo kugombana zaidi na Edna.
“Mlikuwa mmeenda wapi , Boss Edna kwanini unoanekana kuchafuka hivyo na Roma kutapakaa damu?”
“Hayakusu, niimesema ondoka , hujanisikia”Aliendelea kuongea kwa hasira
“Hatuwezi kukaa chini na kuongea?, nipo hapa kwa ajili ya kuongea swala muhimu”
Edna ni kama hajamsikia, alimgeukia Bi wema ambaye hakuelewa mazungumzo kwani ligha iliokuwa ikitumika ni kingereza.
“Bi Wema mgeni wetu anaondoka, naomba umsindikize nje”Aliongea Edna na kumfanya Bi Wema kushangaa.
Mgeni aliekuwa mbele yake alimuona mpore sana na alitamani hata kufahamiana nae, lakini lugha ilikuwa tatizo
“Rufi nitakusindikiza kwenda, nje unaweza kuja wakati mwingine” Aliongea BiWema kwa ishara na Rufi alijikuta aking’ata lipsi zake kwa hasira na kumwangalia Roma kwa macho ya kuomba kuhurumiwa.
“Roma hata wewe unanifukuza?” Aliongea.
“Kwanini uniulize hivyo , nilikusaidia kuponyesha sumu iliokuwa kwenye mwili wako , nikakupatia pesa lakini bado umekuja kuharibu mahusiano yangu , unatakiwa kushukuru upo hai mpaka sasa”Aliongea Roma huku akionyesha chuki.
“Unamaanisha nini kumponyesha sumu?”Aliuliza Edna mara baada ya kusikia Roma anataja maswala ya sumu.
Roma alimwelezea kwa ufupi kile kilichotokea mpaka kumponyesha Rufi sumu ilipo kwenye mwili wake.
“Rufi kama hivyo ndio ilitokea unapaswa kushukuru badala ya kutaka kuharibu familia yangu ili kufanikisha matamanio yako”
“Upo sahihi , nimekuja hapa kwa ajili ya kuomba msahamaha”Aliongea na palepale alisogea mpaka katikati sehemu ya wazi na kupiga magoti mbele ya Edna, kitendo kile kilimshangaza hata Roma.
“Ni makosa yangu , akili zangu ziligubikwa na kisasi na kushindwa kufanya maamuzi yaliosahihi , Nilitaka kuharibu familia yako Edna kwa kutumia gistoria yangu na Roma , maisha yangu ya ukimbizi na kuyahofia maisha yangu ndio kilichonifanya nikafika mpaka hapa Tanzania , Boss Edna natamani kuendelea kuishi naomba uniokoe, bila ya wewe kunisaidia siwezi kwenda popote”Aliongea huku akianza kulia kama mtoto mdogo , ilionyesha alikuwa akijikaza muda wote.
Kitendo cha Rufi kulia kama mtoto kilimuumiza sana Bi Wema na alimkimbilia na kumwambia asipige magoti akae kwenye sofa lakini Rufi alikataa.
‘Nitaendelea kupiga magoti mpaka nisikie Edna amenisamehe” Aliongea
Roma alishangaa kwani ni mara ya kwanza kumuona Rufi akiwa na mwonekano wa aina hio , leo hii mwanamke huyu alionyesha kweli kuhitaji msamaha na mwonekano wake ndio uhalisia wake ambao hakuwahi kuona tokea walipokutana..
Edna alikuwa mwepesi wa kuguswa na wenye uhitaji hivyo licha ya kwamba alijua Rufi ndio chanzo cha migororo yake na Roma lakini kumuona analia alijikuta akimuonea huruma.
“Umesema akili zako ziligubikwa na roho ya kisasi , unamaanisha nini?”Aliuliza Edna.
“Nilikimbia kutoka kwenye nchi yangu niliozaliwa , familia yangu pamoja na wakwe zangu wananitafuta na wanapanga kunirudisha nyumbani”Aliongea na kumfanya Bi Wema kumwangalia Roma alihitaji kutafsiriwa na Roma alifanya hivyo.
“Kwanini?, kwanini umekimbia familia yako na wakwe zako , si ndio ndugu zako?”Aliuliza Bi Wema na Roma alitafsiri.
“Kwangu siwachukulii kama familia yangu , natamani ningekuwa na uwezo kuwararua rarua wote”
Aliongea huku akionyesha hasira waziwazi na Roma mabadiliko ya Rufi aliweza kuyatafsiri kama uhalisia na sio maigizo.
Alikuwa ashaanza kuelewa kwani ashaongea na Rufi kabla , hivyo kwa kuunganisha kauli zake alihisi ni kweli kuna kinacheendelea kwenye maisha ya huyu mwanamke.
“Inuka na ukae kwenye sofa”Aliongea Roma kwa kuamrisha
“Miss Edna Umenisamehe?”Aliuliza
“Kaa na unieleze kila kitu kuhusu wewe ni wapi unapotokea”Aliongea Roma lakini Rufi alitaka kwanza kusikia kauli kutoka kwa Edna.
Edna aliekuwa amesimama alimwangalia Roma na mwonekano usoelezeka .
“Fanya kama alivyosema ,nitakusamehe kama utaongea kila kitu”Aliongea Edna mara baada ya kuona Rufi ameshindwa kuamka akisubiria kali yake.
“Thank you..”Alijibu kwa kutabasamu na kisha alisimama na kukaa kwenye sofa na wote kwa pamoja waliketi ili kuweza kumsikiliza.
“Mngefanya hivi tokea mwanzo jamani kuliko kumfanya akalia, Edna kwanini usiende kwanza kubadili mavazi? , hata Mr Roma sio vizuri kuendelea kuw ana mavazi hayo yalichafuka”Aliongea Bi Wema akivuta pumzi ya ahueni baada ya kuona Rufi amekwisha kusamehewa.
“Babe twende tukaoge pamoja”Aliongea Roma akimshika Edna kiumo ni kama alikuwa akifanya makusudi mebele ya Rufi.
“Sawa twende”Edna na yeye alisoma mchezo na kuitika lakini alijitoa kwenye mikono ya Roma , bado alionyesha kama alikuwa na chuki , ijapokuwa alimsamehe Rufi lakini hakutaka kuendelea kumuona hapo ndani.
“Bi Wema muda umeenda sana ni bora tukapata chakula kabisa” Aliongea Edna na Bi Wema aliwaambia alikuwa katikati kuandaa chakula na Qiang Xi yupo barabarani akisubiria gari ya shule ili kumpokea Lanlan..
Edna alitamani kwenda kumpokea Lanlan mwenyewe lakini kutokana na maongezi, aliona kwanza wahitimishe kilichpo mbele yake, hata hivyo Qiang Xi alikuwa barabarani tayari.
Rufi aliwaangalia Roma na Edna wakipandisha ngazi kwenda juu na alimfanya Bi Wema kumwangalia na kisha alitabasamu na kuondoka kuelekea jikoni, alitamani kumshauri Rufi jambo lakini kwakuwa lugha ilikuwa kikwazo alishindwa kuongea lolote.
Baada ya nusu saa kupita Edna na Roma walimwita Rufi juu kwenye chumba cha kujisomea kwa ajili ya maongezi.
Edna alikaa kwa umakini kutaka kusikiliza stori ya Rufi, alijiambia sasa hivi atataka kujua kila kitu kinachomzunguka Roma kutokana na tukio la kukamatwa leo na mwanaume ambaye alikuwa jini.
“Tuambie kila kitu, usije ukapanga kudanganya tena kama unataka kweli msaada wetu” Aliongea Roma kwa tahadhari na Rufi alivuta pumzi nyingi na kuzishusha.
“Sina uhakika kama mshawahi kusikia kuhusu miliki za kijini?” Aliongea Rufi
********
KIGALI NATIONAL UNIVERSTY
Ni ndani ya chuo kikuu nchini Rwanda katika jiji la Kigali, leo hii ilikuwa tofauti kidogo na siku zote kutokana na uchache wa wanafunzi wanaotoka ndani ya chuo hicho na kuingia kwa ajili ya masomo na yote hio ni kutokana na wanafunzi kwenda likizo fupi, lakini licha ya hivyo bado kuna wanafunzi waliokuwepo ndani ya Campus ambao walikuwa wakiingia na wale ambao walikuwa wakitoka makundi makudi na kuna wale waliokuwa peke yao.
Katika geti la kuingilia chuoni hapo alionekana mwanadada aliekuwa amevalia vazi la kisasa kama gauni rangi nyekundu na nyeupe na kofia aina ya Hat pamoja na mkoba wa bei ghali , alikuwa amependeza haswa.
Alikuwa amevalia miwani ya jua huku miguuni akiwa amevalia viatu vya high heels, alitembea kwa madaha na kujiamini huku akiingia ndani ya chuo hicho na kwa muonekano wake ilionyesha kabisa hakuwa mgeni.
Baada ya kukata kwenye viunga vya chuo hicho alikuja kusimama kwenye jengo moja refu kwenda juu la ghorofa kama tano hivi ambalo lilikuwa na maandishi ya Jengo la Utawala kwa liugha mbili, moja ya Kifaransa na Kingereza.
Mwanamke yule aliingia ndani ya jengo hilo huki akipishana na baadhi ya watu kadhaa na ndani ya dakika chache aliingia ndani kabisa ya jengo hilo na kupandisha kwa ngazi na kuingia kwenye Floor namba tatu ambayo ilikuwa na ofisi za wakufunzi wa chuo hiki.
Alitembea akionyesha kujua kilichompeleka hapo na alikwenda kusimama kwenye idara ya Sayansi na kusimama nje na kisha akajiweka sawa na kugonga mlango.
Mwanaume aliekuwa na mwonekano wa kipekee alievalia suti alikunja sura mara baada ya kusikia mtu kugonga mlango , alikuwa na mengi aliokuwa akifikiria na kubwa zaidi alikuwa akisoma kitabu, na kwakuwa wanafunzi wengi wamefunga chuo hakuwa akitegemea mtu kuja kwenye ofisi yake hasa kwa muda kama huo ambao alihitaji utulivu.
Alijinyanyua kutoka kwenye meza iliokuwa imepangiliwa kwa vitabu vingi na kusogelea mlango na kuufungua , alijikuta akitoa mshangao mara baada ya kumuona mwanamke mrembo sana akiwa mbele yake , kilichomshangaza zaidi na kurudi nyuma kama kaona mzimu ni mara baada ya yule mwanamke kuvua ile miwani.
“You. you..!!”Aliongea kwa mshangao
“Why!, little Cripple , its me Am I that scary?”Aliongea akimwita yule mwanaume kilema huku akisema kama alikuwa akiogopesha.
“Mwanamke yule alitoa kofia aliokuwa amevalia na kuonyesha nywlee zake ndefu ambazo zimechanwa vyema kurudishwa nyuma, alikuwa na ngozi laini mno , unaweza kusema ni msichana wa miaka therathini.
Naam hakuwa mwingine mwanamke huyu bali alikuwa ni Kizwe, yule ambaye aliombolezwa kitaifa kwa kufa kwa tatizo la moyo.
Mwanaume aliekuwa mbele yake alikuwa ni Lekcha, ambaye alionyesha mshangao wa hali ya juu mno kama ameona mzimu.
Hakuamini mwanamke ambaye alimshuhudia kwa macbo yake akipoteza maisha ni huyu aliesimama mbele yake , ilikuwa ngumu sana kuamini kile alichokuwa akikishuhudia.
Huenda kama Lekcha hakuwa ameshuhudia mambo makubwa kwenye maisha yake , angepoteza fahamu hapo hapo , lakini hata hivyo kwa kumchunguza Kizwe aliona kuna jambo ambalo halipo sawa.
Kizwe alimpita Lekcha aliekuwa akishangaa shangaa na kuingia ndani kabisa na kisha akatupa mkoba wake kwenye sofa huku akianza kunyoosha mwili wake na kumgeukia Lekcha ambaye alikuwa akihema kwa shida na kuanza kucheka
“Lekcha , why are you still in a daze , Are you so excited to see me that you can’t talk?”
“Lekcha kwanini unashangaa shangaa , au ni mshituko wa kuniona ndio umekufanya kushindwa kuongea”
Lekcha alijikuta akimeza mate mengi na kuvuta pumzi nyingi na kisha kuzitoa huku macho yake yakimwangalia mwanamke aliekuwa mbele yake kwa tahadhari
“Kwanini … nilifikiria ulikufa?”Aliongea Lekcha kwa mshangao kidogo huku akishusha sauti yake na kujitahidi kujituliza ,
Kizwe alitabasamu na kisha alikunjua mikono yake akimpa ishara Lekcha kumkumbatia na Lekcha bila kujielewa anakumbatia mzimu alimsoogelea Kizwe na kisha wakakumbatiana.
“Naomba unisamehe kwa kukufanya kuwa na wasiwasi , ilikuwa kweli kidogo tu nipoteze maisha lakini Mungu alinionea huruma na kunifanya niendelee kuwa hai”Aliongea
“Kama ni hivyo wapi ulikuwa umeenda?, Nilikumisi sana na kukufikria kila wakati”Aliongea Lekcha.
“Nilikumisi pia mpenzi “Aliongea na kisha akambusu Lekcha kwenye shavu kimahaba.
“Nimefurahi mpaka sasa unaendelea kuishi , nilikuwa na wasiwasi yule shetani kakuua , Nimempata mtu wa kunisaidia kulipiza kisasi changu”Aliongea
“Kulipiza kisasi ?Nani?”Aliuliza Lekcha kwa mshangao lakini Kizwe hakumjibu.
‘”Hatujaonana kwa muda mrefu , huoni kama nimebadilika na kuzidi kuwa mrembo?”
Lekcha alimwangalia Kizwe kwa kumchunguza kwa mara nyingine huku hofu ikiwa imepungua na alijiktua akimeza fundo la mate maana Kizwe alikuwa mrembo mno , alikuwa kama mwanamke ambaye ndio kwanza anatimiza miaka therathini.
“Nimemisi sana.” Aliongea Lekcha huku akiweka tabasamu la kifedhuli.
“Acha haraka mara ya mwisho hukunikoleza vizuri”Aliongea Kizwe huku akiweka tabasamu la kimtego.
“Nitafanya vyema awamu hii” aliongea na palepale alimsogelea na kisha kuanza kubusiana mdomoni kwa dakika na Kizwe alimwangalia Lekcha kwa tabasamu.
“Najua wewe ndio mwanaume pekee ambaye ulitokea kunijali na kunipenda kwa madhaifu yangu , Nimeweza kuishi kwa sababu yako tu na sasa nimekupata nataka niwe wako milele”Aliongea Kizwe na kauli ile ilikuwa kama kichocheo kwa Lekcha kwani alimtupia Kizwe kwenye sofa na kuacha gauni lake liache wazi mapaja yake, alilipandisha juu zaidi na kisha akashusha nguo ya ndani kwa spidi na kisha akazama chumvini.
Dakika chache mbele ni migunio ya kimahaba pekee iliotawala ofisi nzima , Lekcha alionyesha kufanya kazi njema kabisa pasipo ya kujiuliza mwanamke aliekuwa mbele yake aliponaje katika tundu la kifo.