SEHEMU YA 475.
Kutokea kwa Yan Buwen kulishangaza wengi na kuwafanya warudi wote nyuma kwa tahadhari kwani suti yake aliovaa lakini pia miale ya Godstone ilileta msuguano ambao haukuwa wa kawaida.
Raisi Kigombola mara baada ya kumuona mwokozi wake alitoa tabasamu la kejeli.
Ndio kitendo cha kurudi Tanzania ilikuwa ni kwa ajili ya kumuondoa kabisa Roma, hakupenda Roma akiendelea kuishi Tanzania kwani alikuwa akimkosesha amani.
Hivyo kushambuliwa kwa Omari ulikuwa ni mpango wa Yan Buwen na mstaafu Kigombola kumrudisha Roma Tanzania na kukutana na kifo chake.
Hata Roma mwenyewe aliweza kugundua hilo kutokana na watu waliomzunguka , wote walionyesha kutokuwa wanajeshi wa kawaida na kwa haraka haraka alijua watakuwa na miili ambayo imechakachuliwa hivyo kushindana na wanajeshi wa kawaida ingekuwa kama misheni ya kujitoa muhanga, mbaya zaidi walikuwa wengi.
“Damn it Roma hawa wote si miili yao imechakachuliwa?”Aliuliza Omari huku akiwaangalia.
Unajua nini wakati wote wa harusi hao watu waliokuwepo lakini walikuwa wamevalia mavazi ya kihudumu na ndio maana hata muda huo walikuwa wameshikilia siraha lakini wakiwa na mavavi yaleyale ya wahudumu , Raisi Kigombola aliwaweka maalumu kwa ajili ya vita vya kummaliza Roma.
Roma hakujisumbua nao kwanza aliwachukulia wa kawaida , lakini tatizo ni moja eneo hili kuna watu wake wa muhimu hivyo ingekuwa ngumu kudili na Yan Buwen na wakati huo huo kudili na hao wanajeshi.
“Mheshimiwa waziri mkuu , Meja Tobwe na Mkuu wa majeshi mnaonekana hamna wasiwasi kwasababu mnadhani Roma anaweza kumdhibiti Yan Buwen si ndio?”Aliuliza Raisi Kigombola huku akimwangalia mwanaume aliekaa kwenye kona.
Roma aligeuka na kugundua kumbe kuna waziri mkuu , alijikuta akitukana ndani kwa ndani , ilionyesha dhahiri raisi Kigombola alialika watu wake muhimu pamoja na maadui zake ili kufanya vita iwe rahisi , kwani alikuwepo Mage , Magdalena ,Neema Luwazo na wengine wote ambao kama Yan Buwen anapanga kuwadhuru basi itamchukua kazi ya ziada kufanikisha usalama wao.
“Ninapenda niwaeleze moja kwa moja , ujio wenu kwenye hii sherehe ni wa kupangwa nyie wote ndio maadui wakubwa wa Kigombola hivyo nitahakikisha hakuna ambaye anatoka hapa akiwa hai”Aliongea Yan Biuwen.
“Mara ya mwisho ulijigamba kwamba unataka kuniua lakini uliishia kukimbia au sio wewe?”Aliongea Roma.
“Lakini nilifanikisha kukuumiza kwa kiasi kikubwa , nadhani hapo upo na shauku nimeweza vipi kufanyia kazi jiwe la Kimungu kufikia hatua ambayo sikuogopi tena , usijali kabisa kijana nimefanikisha kuweza kutumia nguvu yake yote na leo nina kwenda kutumia uwezo zaidi ya mara mia niliotumia wakati tunapambana kule China”Aliongea kwa majigambo na kumfanya Roma kwanza kukagua mazingira na wale watu ambao wamemnyooshea makombora aina ya Bazooka.
“Unafikiri mimi ni mjinga , kilichopo ndani ya hayo makombora sio kitu cha kawaida , ngoja nikuonjeshe utamu wa siraha yangu mpya”Aliongea na palepale Kombola la mmoja wa wale watu lilipuka palepale lakini halikutoa mlipuko kama ilivyotengemewa bali lilitoa miale kama ya mionzi rangi ya samawati lakini ya kung’aa sana kuumiza macho.
Roma alichukua tahadhari na kuwakinga watu wote na ngao na ilikuwa rahisi kwani wote walikuwa upande mmoja lakini sasa kwa wale wanajeshi wa Yan Buwen baadhi yao walianza kubabuka ngozi kwa spidi kubwa na ndani ya dakika mbili tu walidondoka chini na kupoteza maisha huku miili yao ikiwa kama imeyeyuka na kuwa maji na kilichoweza kuonekana ni skeletoni tu , kwani nyama zote zilibadilika na kuwa uji uji.
“Thanatos!” Roma alibwabwaja ndani kwa ndani mara baada ya kugundua teknolojia iliotumika ndani ya makombora hayo ilikuwa ni Thanatos kwani ndio pekee ambayo ilikuwa ikiweza kuyeyusha miili ya kiupe hai na kuwa ujiuji.
Akili zake zilimrudisha ufaransa namna alivyoweza kukwapulia siraha hio mara baada tu ya kuweza kuipata kutoka kwa serikali ya Ufaransa, jambo la kutisha zaidi ni kwamba hii iliokuwa na uweze zaidi ya mara mbili (Enhanced) kuliko alivyokuwa akiijua uwezo wake.
Tukio lile liliwafanya watu kutoa ukulele na kuhema kwa shida na hata Roma mwenyewe alishangazwa, ilikuwa ni siraha ya hatari mno ikigusana na miili ya binadamu na mbaya zaidi Yan Buwen ashaigueza na kuwa mionzi isiokuwa ya kawaida.
Wakati anapambana na Yan Buwen nchini China aliweza kuhisi hio mionzi lakini hakugundua kama ilikuwa ni ya siraha ya Thanatos kutokana na kwamba ili uweze kuitambua teknolojia hio ni pale inapoleta athari.
Roma kitu kingine pia alichokigundua wale watu waliozingira hawakuwa binadamu , walikuwa misukule na haraka haraka alijua lazima ni maiti zilizofufuliwa na Yan Buwen kwa kutumia kimiminika cha ufufuo na hili lilikuwa pia hatari zaidi.
Hivyo kwa haraka haraka ni kwamba walikuwa wakiongozwa akili zao maana hawakuonyesha hata hofu licha ya Yan Buwen kuyeyusha wenzao.
Afande Tozo na wengine sasa walielewa hatari na mbaya zaidi hakuna kifaa chochote cha kiletroniki kinachofanya kazi muda huo hivyo wasingeweza kufanya mawasiliano ya kuomba msaada na kwa mpango wa Raisi kigombola wa kutaka kuwaangamiza kwa kuwachukulia kama maadui basi ni hakika alikuwa amehakikisha hakuna mianya ya kutoroka.
“Yan Buwen unaweza kufanya majaribio ya siraha yako, lakini hapa ndani kuna baadhi ya watu wangu muhimu sitaki wapoteze maisha”
“Usijali mzee watu wako muhimu hawawezi kuguswa kama tulivyokubaliana” Aliongea huku akitabasamu na kisha akamgeukia Roma.
“Hades what do you think, Beutifull isn’t it?”
“Roma unaonaje, inavutia si ndio?”
“Wewe ni mshenzi , Wewe ni binadamu kichaa”Aliongea Neema Luwazo kwa hasira.
“Haha…Miss Neema nasikia umemsaliti Mzee Kigombola na kwenda kutoka kimapenzi na Hades , Huenda umechangia zaidi katika hili na leo unakwenda kuona mpenzi wako nikimuua mbele yako”Aliongea.
“Yan Buwen nataka ufanye kazi , Neema hapaswi kuguswa ninachotaka nikuona huyu mpuuzi wake anaejivunia nae anakufa mbele yake”Aliongea Kigombola.
“Kigombola kwanini unafanya hivyo , kwanini umeamua kufanya kazi na huyo shetani sio kama nilivyokujua tokea mwanzo”
“Umeyataka mwenyewe Neema na sina chaguo zaidi ya kufanya maamuzi magumu, umeutesa moyo wangu sana kutoka na huyo mtoto sasa wajibika kwa matendo yako” Aliongea.
“Muda wa kuongea porojo ushaisha naingia kazini sasa, nitaanza na Afande Flamingo nasikia una mafunzo kutoka China, hebu tuone kama unaweza kuhimili pigo moja” Aliongea na palepale msukule wake mmoja uliachia bomu la Thanatos kutoka kwenye Bazooka.
“Magdalena kuwa makini” Aliongea Roma na uzuri Magdalena alikuwa mwepesi hivyo alipotea aliposimama na miale haikumpata.
Ilikuwa ikitisha sana, yaani misukule yake alikuwa akiwaongozakwa kutumia akili yake , kwanni akifikiria kufanya hiki na mmoja wapo angechukua hatua.
“Hahaha… nishasahau unasemekeana kidogo una spidi kubwa labda nianze kwanza na baba yako pamoja na pacha wako” Aliongea na palepale wanajeshi wake wanne waliinua kombola kulenga waliposimama Afande Tobwe na Mage lakini palepale ngao kama kioo ilijitengeneza mbele yao na kuwakinga na mlipuko wa mionzi ya Thanatos.
Uzuri ni kwamba miale ile ilikuwa na sifa moja ya pekee haikuwa na uwezo wa kusambaa , ilikuwa ni mionzi tofauti sana na iliozoeleka, hivyo athari zake zilikuwa za dakika moja tu na kuisha lakini hata hivyo zilikuwa na nguvu mno kwani ile ngao ilionekana mbele yao baada ya kugongana na bomu la mionzi la Thanatos ulitokea mtikisiko wa ardhi wa aina yake.
Afande Tobwe alimwangalia Roma kuona kama ndio yeye aliewakinga kwani alikuwa ashakata tamaa , lakini Roma alimwonyeshea ishara kwamba sio yeye lakini sasa muda huo huo walisikia sauti kutoka mbali kidogo angani lakini ikiongea kwa lugha isiokuwa ya kawaida lakini Roma alipata kuifahamu kilikuwa ni kihindu.
“Ninakwenda kukumaliza leo hii, wewe ni uzao wa shetanni kutoka familia ya Yan” Aliongea hivyo.
“Master!”
Omari ndio aliekuwa wa kwanza kuangalia hewani na kujikuta akitabasamu na kuita jina la Master.
Roma na yeye aliangalia hewani na palepale aliweza kuona mwanaume aliekuwa jamii ya wahindi hakuwa mchina licha ya kuweza kuongea kichina , alikuwa mhindi lakini alienyoa kipara huku akiwa na shanga kama Rozari alizokuwa amevalia shingoni , alikuwa pia amevalia mavazi ya kitamaduni maarufu kama Kisaya ambayo huvaliwa na Monk wale wanaosalia Budha.
Ni Monk lakini ni sahihi kusema alikuwa monk mwenye kutisha maana kwa dunia ya leo hakuna mtu ambaye anaweza kuwa na mwonekano mbaya wa sura kama mtu huyo alieweza kufika.
Roma alijikuta akishangaa, mara moja aliweza kutambua mtu aliefika hapo sio binadamu wa kawaida , licha ya kuonekana kama binadamu , alikuwa ni watu jamii ya Hongmeng kama hajakosea ambaye alikuwa anakaribia kuvuka Levo ya Nafsi na kuingia levo ya Dhiki.
Ilionyesha yeye ndio ambaye alihusika kuwakinga Afande Tobwe kwa kutumia dhana ya kimaajabu ambayo kwanza ilimshangaza sana Roma.
“Nilijua kabisa Hongmeng lazima mngekuja kabla sijawafuata huko huko, lakini nasikitishwa kuona umekuja peke yako” Aliongea Yan Buwen.
“Amitabhaa , hili tukio tusingeweza kukaa na kuangalia unafanya utakavyo kwani unaifanya nchi yetu kuwa na uadui na mataifa mengine , Mimi mjumbe kutoka Hongmeng leo nakwenda kukuadhibu kwa niaba ya dunia nzima, kutana na Dhana yangu ya kishetani”
Monk hakutaka kupoteza muda na palepale alianza kumsogelea Yan Buwen kwa kasi, ilionekana alikuja kwa kazi maalumu tu nchini Tanzania , kupambana na Yan Buwen na kisha kusepa maana hakumzingatia hata Roma.
Wakati anamsogelea Yan Buwen alikuwa ameshikilia kiutu kama kijichupa cha rangi nyeusi lakini ajabu ni kwamba palepale kilibadilika na kuwa kama mkuki wenye ncha kali kwa mbele ambao ulitoa msisimko wa ajabu mno.
Yan Buwen wala hakusogea zaidi ya kumwangalia kwa kebehi na ile Monk anapeleka mkuki wake akidhamiria kumchoma nao Yan Buwen eneo la kifuani , Yan Buwen palepale alibadilika na kuwa kama sanamu ya Chuma lakini rangi ya Silver na palepale mlio wa chuma kugongana na chuma ulisikika , lakini Monk alionyesha kuwa na akili zaidi kwani palepale alichia pigo lingine na Yan Buwen alirudi kwenye ubinadamu na Monk alimkata mkono na mkuki wake palepale.
“Yes,, Yes…!!”Omari alishangilia mara baada ya kuona lile pigo na kumfanya Roma kumwangalia.
“Roma huyu ndio Master wangu ndio anaesifika kuwa sehemu ya wazee watano wenye uwezo mkubwa ndani ya Hongmeng”Aliongea Omari na kuwafanya watu wote kupata ahueni.
Lakini upande wa Roma aliona ilikuwa mapema sana kushangilia ushindi kwani hakutegemea Yan Buwen kuja na uwezo mdogo kiasi cha kuweza kushindwa na Monk kama ni hivyo alijimbia asingeumiza kichwa.
Yan buwen alionyesha kutougulia maumivu na mkono wake ulipona palepale na kisha akamsogelea Monk kwa spidi na kumwachia wimbi la shoti ambayo ilimlipua na mlio wake ulikuwa kam Transfoma inapiga shoti.
BOOM!
Watu walijikuta wakichuchumaa chini kwa woga mara baada ya mlipuko ule kwani ni kama Roho zilitaka kuwatoka ni Roma , Magdalena na Omari ambao hawakuonyesha hofu na kuendelea kuangaia angani.
Monk alijitahidi kuhimiri mlipuko wa Shoti kwa kutumia nguvu za kijini lakini nguvu yake ilimzidi na kumfanya kutupwa mbali kalibu aiguse ardhi na palepale shoti ikapotea na Yan Buwen alirekebisha mkono wake uliojiponyesha kwa haraka na kucheka.
Monk alijikuta akimwangalia Yan Buwen huku akiwa kama haamini alijihisi mtiririko wa nguvu zake za kijini kwenye mwili wake zimepungua sana kwa kufonzwa na shoti.
Roma mpaka pale aliona kabisa Yan Buwen nguvu zake zilikuwa za viwango vikubwa mno na ilionyesha hakuna pigo la kawaida la kijini ambalo lingeweza kummaliza na mwenyewe alijiambia asingemsaidia Monk kwa namna yoyote ile aliacha kwanza aone mwisho wake alitaka kwanza atumie nafasi hio kuona Hongmeng wanavyopambana ili apate kujifuza.
Roma alianza kudili na wanajeshi misukule wa Yan Buwen maana asingefanya hivyo wakati wa kupambana na Yan buwen angeshindwa kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja na alishukuru sana kutokea kwa Monk maana huenda ingekuwa shida kwake.
Roma aliachia pigo moja ambalo liliambatana na upepo wa kisulisuli na kuwazoa wanajeshi watatu kwa wakati mmoja na walikwenda kujipigiza kwenye ukuta na kombola lao lilipuka palepale na walianza kuyeyuka nyama zao zote na kubakia maskeletoni.
Afande Tozo , Afande Tobwe waliona kabisa hapa uwepo wao ungekuwa mzigo kwa Roma hivyo wanapaswa kuondoka kwenye hilo eneo na watu wote , lakini Yan Buwen alionekana ameshayasoma mawazo yao mara baada ya kushuhudia Roma akiangamiza wanajeshi wake , palepale wanajeshi wawili waliachia bomu la Thanatos kuelekea upande wao , lakini Roma alikuwa fasta sana kwani ni kama alitegemea na kuwafunika na ngao ya kijini na kilichotokea ni mtikisiko.
“Msifanye chochote maana nawahakikishia hakuna ambaye anaweza kuondoka hapa akiwa hai , mpango ni mimi kuwamaliza maadui zangu wote na msifikiri uwepo wa Monk unaweza kuwasaidia , mpango wa Yan Buwen pia ni kumalizana na Hongmeng ili aitawale China”Aliongea Kigombola na kumfanya Roma aone kweli binadamu yoyote wa kawaida akipata uwezo wa ajabu kuzidi wengine basi uwezo wa kufikiria hupungua kwa kiasi kikubwa mno. Alimjua Kigombola alikuwa akisifika kwa mbinu lakini hakuamini angekuwa na uwezo mdogo wa kufikiria namna hio.
Ukweli Kigombbola alimwamini kwa asilimia zote Yan Buwen , ni kama aliamua kubetia maisha yake kwenye uwezo wa Yan Buwen aliamini kama Yan Buwen angeweza kumdhibiti Roma basi taifa lingekuwa la kwake milele na angefanya mpango na kumaliza na maadui zake ambao hawakuwa hapo ndani na kisha kumuweka raisi ambaye angefanya kile anachotaka yeye.
“Tianyin Dhamachakra!!”
Monk alionekana kurejewa na nguvu zake na kuanzisha upya mashambulizi kumlenga Yan Buwen.
Ghafla tu palepale monk alionekana mara ishirini zaidi na wote wakiongea ‘Mantra’ kwa nguvu na sauti ya Brahma ilisikika mara mbilimbili kama mwangwi.
Kumbuka hapa alikuwa ni Monk mmoja lakni alijitengeneza kuonekana zaidi ya mara hamsini na ndio maana sauti zao zilionekana kama vile ni watu waliopo kanisani au msikitini wakisali kwa kuongea na sauti zake kujaa mwangi , waliopo hapo ndani ni kama walihisi uchizi kutokana na makelele yasioeleweka.
Yan Buwen alikuwa katikati na Monk alionekana kufanya vile ili kumchanganya Yan Buwen asiweze kumshambulia kwani asingejua yeye halisi ni yupi kati ya ‘illusion’ aliotengeneza.
“Hahaha.. unachokifanya ni ujinga kwangu”Aliongea Yan Buwen na kuachia shoti ya aina yake kumlenga Monk aliekuwa kushoto kwake na alikuwa ndio origino lakini bahati nzuri alikuwa amejiwekea ngao na ile dhana yake ya kijini hivyo hakupata majeraha lakini alishangaa Yan Buwen amewezaje kumfahamu.
Monk alichokosea ni kuamini kwamba Yan Buwen alikuwa akipambana kwa kutumia sayansi na yeye alikuwa akipambana kwa kutumia uchawi hivyo kama angemuwekea Yan Buwen mtego ingekuwa rahisi kumdhibiti.
Roma aliweza kudhibiti baadhi ya wanajeshi , lakini hata hivyo walionekana kuwa wengi sana kwake kuwamaliza kwa muda mfupi huku pia akilinda watu wasidhurike.
Yan Buwen alionyesha kuwa mjanja sana kwani wanajeshi aliokuja nao kwa mahesabu ya haraka haraka ni therathinni, mwanzoni waliokuwa wamemzingira walikuwa wachache lakini baada ya muua waliongezeka.
Omari hakuweza kupambana pia kutokana na jeraha eneo la tumboni.
Donyi aliekuwa akitaka baba yake asiuliwe na Roma alikuwa kwenye wasiwasi kwa kile ambacho kingetokea muda huo.
Roma mbinu pekee ambayo aliona ingeweza kumaliza kazi ni kumshambulia Yan Buwen , kwani ilionyesha wale wanajeshi pasipo ya Yan buwen hawawezi kuchukua hatua kwasababu walitegemea akili yake.
Hivyo mara baada ya kuona Monk anapokea kichapo fasta alimsogelea Yan Buwen kwa kasi.
“Naona umekuja , lakini muda bado”Aliongea huku akiangalia chini na ilionekana Magdalena alifanya kosa kutaka kuwashambulia wale mazombie , ilikuwa sahihi kuwaita mazombie maana akili hazikuwa zao na walishakufa na kufufuliwa na kimiminika.
Sasa kumbe Yan Buwen aliona hilo , hivyo palespale aliruhusu wale mazombie kumshambulia Magdalana lakini hata hivyo alionyesha kuwa spidi kwani aliweza kukimbia kwa spidi na kuepuka shambulizi na ile miale iliwaua wahudumu wawili wa kike na nyama zao kuyeyuka palepale walibakia kuwa skeleton.
Neema Luwazo alikosa uvumilivu na alijikuta akianza kutapika palepale na ilibidi Donyi amshikilie mama yake kwani alianza kukosa pumzi.
“Unaweza kuwa na spidi lakiini haimaanishi kwamba unaweza kupona kama watashambulia wote”Aliongea Yan Buwen mara baada ya Magdalena kutudi aliposimama baba yake , lakini lilikuwa kosa kubwa.
“Shiti tupo karibu sana”
“Mshachelewa , Firee..!!”Aliongea Yan Buwen akiwaamrisha misukule yake kushambulia.
SEHEMU YA 476.
Roma alikuwa na spidi, mwanzoni alitaka atumie ile Dhana ya Ganyua alioipata kutoka kwa lile jini lililomteka Edna na kumpa laana ya minyoo lakini hakujua kama ingekuwa na nguvu kiasi gani hivyo hakutaka kubahatisha na aliita nguvu ya kimaandiko na kuwafunika na alifanya ndani ya muda kabla ya kuguswa na mionzi ya Thanatos.
Lakini sasa wakati Roma akiwalinda wengine yeye alipokea pigo kutoka kwa Yan Buwen na alihisi maumivu makali mno, ilikuwa ni kama viungo vyake vya ndani vinakamuliwa kama nguo inayotolewa maji.
Roma ilibidi kwanza arudi chini ili kushindana na maumivu na ilionekana mbinu ya Yan Buwen kumalizana kwanza na Monk na kisha ndio adili na Roma.
“Roma uko sawa?”Aliuliza Mage ambaye aliishia kutoa machozi pasipo ya kujua cha kufanya.
“Inabidi mjiwazie usalama wenu kabla ya wa kwangu , Babe Mage nikimaliza hapa hakikisha unanihudumia vizuri”Aliongea Roma huku akilazimisha tabasamu kuwaonyesha kwamba yupo sawa.
“Unapata wapi ujasiri wa kufanya utani wakati upo kwenye hatari” Aliongea Magdalena lakini maneno yake yalikuwa sahihi , ijapokuwa hakuwa na woga lakini aliamini kushindana na Yan Buwen inahitajika akili ya ziada kwani uwezo wake ulikuwa mkubwa huenda kumzidi hata Poseidon.
Wakati akiangalia namna ya kushinda pambano lililokuwa mbele yake , ghafla kuna wazo lilimjia na kuamini huenda linaweza kufanya kazi kumsaidia kumshinda Yan Buwen.
“Simameni wote hapa hakikisheni mnakaribiana na msiulize maswali kama mnataka kuishi” Aliongea Roma kwa kuamrisha na palepale Roma alipotea na ile anakuja kuibuka alikuwa nyuma ya wale wapiganaji wa Yan Buwen na alimvunja shingo mmoja na mwingine aligeuka kwa kuhamaki kujilinda kwa kufyatua bomu lakini aliishia kumdhuru mwenzake.
Upande wa juu Monk alikuwa akiendelea kupamaban na Yan Buwen , lakini ukweli Monk alikuwa amezidiwa alichokuwa akifanya ni kukinga mashambulizi tofauti ya kushambulia na Yan Buwen alionekana kutulia na alifanya kazi mbili kwa wakati mmoja , baada ya kuona Roma anashambulia wanajeshi wake , alianza kuwapa maelekezo ya kumshambulia.
Muda ule ule haikueleweka wanajeshi walitokea wapi lakini waliwaznguka Afande Tozo kwa kuwakinga huku wakiachia risasi mfululizo kuelewa kwa misukule , lakini licha ya risasi zile kuwapiga hazikuwaletea madhara makubwa.
“Kipaumbele ni ulinzi kwa Generali na waziri mkuu” Mmoja wapo wa wale wanajeshi alitoa amri walikuwa na sare za kikomandoo.
Roma aliendelea kuwashambulia wale wanajeshi wa Yan Buwen kwa spidi kubwa huku akiwakausha, alionekana alitaka kumaliza ndani ya dakika chache na kumfanya hata Omari kushangaza.
“Damn it huyu Roma ni zaidi ya shetani”Aliongea Omari.
“Tunatakiwa kujua namna ya kumsaidia na sio kumsifia”Aliongea Magdalena.
“Kwani naongea uongo , Magdalena hata wewe unaonekana kumpenda”Aliongea na kumfanya Magdalane kumwangalia kwa macho makali Omari na alianza na yeye kushambulia kwa kasi , ilionyesha tokea maarifa mapya ya kijifunza mbinu za kijini kwa kufundishwa na Roma aliimarika kwani aliachia mapigo kwa kasi mno na aliweza kuwamaliza wawili na kuwaua kabisa.
Omari na yeye alichana kitambaa na kisha akajifunga nacho eneo la tumboni kwa nguvu na kisha akaanza kushambulia kwa spidi.
Upande wa Queen yeye macho yake ni kwa Yan Buwen tu hakujali kilichokuwa kikiendelea kumzunguka bali alikuwa akimwangalia Yan Buwen huku akitoa machozi , alionyesha kama hakuwa akiamini ni yeye, alitamani Yan Buwen amwangalie lakini hakufanya hivyo zaidi ya kuendelea kupambana.
Afande Tozo hakutaka tena kukaa na yeye kwenye ngao , alichokifanya ni kuchukua bunduki na hivyo hivyo kwa Afande Tobwe walichokifanya ni kupambana wakiendelea kubaki nyuma ya ngao.
“Nimegundua kuhusu siraha zao , haziwezi kuachia mashambulizi mfululizo lazima watulie kwanza ndio waachie tena , tunaweza kutumia udhaifu kushambulia kabla hawajaachia na kurudi kwenye ngao”Aliongea Afande baada ya kupewa siraha na wanajeshi waliofika kumlinda.
Upande wa mstaafu Kigombola alikuwa hana wasiwasi kabisa alikuwa amesimama upande mwingine akiwa amesimama na watu wake wakiwaangalie wenzao wakitaabika.
Yan Buwen mara baada ya wanajeshi wake wawili kupasuliwa vichwa aliweza kugundua washajua udhaifu wa siraha yake. Aliangalia chini kwa kebehi.
“Inaonekana mshaanza kuzifahamu siraha zangu , lakini niwaambie tu hizo Ant-matteer Bazooka zipo kwenye majaribio tu nimezitegeneza kwa kuigizia nguvu ya nishati ya jiwe la Kimungu na kuchanganya na teknolojia ya Thanatos, hivyo hio ni ‘Prototype’ tu , lakini naona mnavyo hangaishwa , kama ningeamua kutumia ‘pure antimatter energy’ kutoka kwenye Godstone kutengeneza miozi ya Thanatos msingeweza hata kuwa levo ya kushindana na mimi”Aliongea
“Antimatter energy?”Roma alijikuta akishangaa..
“Huna akili wewe, siku zote ulikuwa ukimiliki jiwe la kimungu lakini umeshindwa kufahamu ndani yake kulikuwa na Antimatter , tena mionzi hio ilitumika kukumulika lakini ulishindwa kung’amua”Aliongea Yan Buwen akimkebehi Roma.
“Kukutoa tongo tongo nishati ant- matter ndio ambayo inatumika kutengeneza usawa kati yake na maada na kufanya dunia iendelee kuwepo , hivyo usije ukajinadi na kujiona mwenye nguvu, nishati ya mbingu na ardhi ni upuuzi mtupi mbele ya Godstone na kadri itakayokuwa kwenye umiliki wangu nitakuwa mungu wa dunia yote na wewe lazima ufe”Aliongea.
Roma licha ya kuonyesha kutoathirika kwa muonekano wa nje , lakini ndani kwa ndani alikuwa akihofia matokeo.
Tokea kupatikana kwa jiwe la kimungu miaka mingi iliopita hakuna mwanasyansi ambaye alifanikisha kuweza kuvuna nguvu yake kwa asilimia mia moja, jambo pekee ambalo walifanikisha ni kumtengeneza Roma, hivyo Yan Buwen sio tu kugundua siri iliokuwa nyuma ya teknolojia ya jiwe la Kimgunu lakini ameweza pia kugeuza na kuwa siraha ya maangamizi.
Lakini ukweli ambacho hakuwa akifahamu Roma ni kwamba Yan Buwen sio ambaye alikamilisha kila kitu, walioweza kufanikisha ni Athena, Profesa Shelukindo na Naira na Yan Buwen alipewa tu baadhi ya kanunni na Athena lakini pia aliweza kugundua siri mara baada ya kuiba tafiti za Profesa Shelukindo baada ya kumuua.
Lakini Yan Buwen asingeweza kusema amepokea msaada kwasababu alitaka kuchukua sifa zote yeye.
“Mtoto mjinga sana wewe usie na aibu” Aliongea Monk kwa hasira huku akimsogelea Yan Buwen kwa kasi na kuanza kuongea Mantra tena.
“Isio na umbo ,yenye nguvu ya uharibifu ,kwako Asura Dharmakaya”
Aliongea kwa nguvu Monk kuita nguvu za kichawi na palepale watu waliweza kushangaa kuona moshi mweusi ukijitengeneza angani ulikuwa ni moshi kama mtu kwani ulikuwa na kichwa na mikono pasipo ya kuwa na miguu na ulianza kumsogelea Yan Buwen kwa spidi , walikuwa juu angani lakini waliochini nywele ziliwasimama.
Alichokiita ndio kinafahamika kwa jina la Asura Dharmakaya ni sehemu ya miungo ya kipepo ya wahindu na ina nguvu kweli.
Monk hakutaka kuendeleza mapambano kwani huko alikotoka alikuwa na uhakika angemwangamiza Yan Buwen kwa pigo moja tu , lakini sasa ni zaidi ya lisaa bado anapambana nae bila mafanikio.
Lile pepo Asura mara baada ya kumsogelea Yan Buwen , ghafla upepo mkali ulimkumba Yan Buwen kiasi cha kusababisha suti yake eneo la kifuani kuchanika na palepale lilionekan jiwe la Kimgu kwenye kifue eneo la moyo.
Monk hakujali tena kuhusu lile jiwe alichotaka ni kuhitimisha pambano kwa kumdhibiti Yan Buwen , hivyo aliongezea nguvu lile pepo Asura kwa kutumia nguvu za kijini na nguvu iliokuwa kwenye dhana alioiita Tianyi na kisha kutengeneza pigo zito kama bomu kuelekea kwa Yan Buwen huku akiwa na uhakika anammaliza kutokana na kutumia nguvu zake zote.
Lakini sasa baada ya kuachia lile shambulizi zito kulitokea vinyuzi nyuzi vidogo kama kamba kutoka kwenye lile Godstone , havikuwa vinyuzi kabisa ni kama mstari wa vinyuzi lakini vingi na vilizingira kichwa cha pepo Asura na kukifanya kama mpira na palepale liliishiwa nguvu , lakini Monk akiwa amehamaki kwa tukio lile pepo lake lilimgeukia mwenyewe na Yan Buwen aliachia na bomu kama shoti kumpiga nalo, ijapokuwa aliwahi kujitengenezea ngao lakini alikuwa karibu hivyo aliweza kupata majeraha kwenye mwili wake na kurudi chini huku akimwangalia Yan Buwen kwa mshangao.
Katika maisha yake hakuamini kama Sayansi inaweza kudhibiti pepo au uchawi, aliamini uchawi unadhibitiwa kiroho lakini Jiwe la Kimugnu liliweza kumeza nguvu yote ya Asura.
Roma mwenyewe alishangazwa na tukio lile , ilikuwa mara yake ya kwanza kuona kitu kama kile.
“Hahaha… Vipi bwana Hades unaogopa mbona umetoa macho hivyo naamini unajihisi kukata tamaa , zamu yako bado , Firee.!!.”Aliongea baada ya kumwangalia Roma kwa jeuli.
Roma hakujalishwa na kejeli zake na hasira iliongezeka maradufu na alianza kuwashambulia wale wanajeshi kwa kushirikiana na Omari na Magdalena.
Yan Buwen alimwangalia Monk ambaye alikuwa akijiponyesha na kucheka , kwani ni kama alikuwa akiangalia kituko , hakujali hata wanajeshi wake chini walikuwa wakiangamia bali alichokuwa akijali ni uwezo wake.
“Hongmeng wamekuleta mpaka huku Tanzania, nani atapeleka taarifa ya kifo chako?”
“Wewe mtoto muda wako wa kufa umewadia”Aliongea Monk kwa kiburi na kuanza kuongea lugha isioeleweka kama vile ana mapepo na palepale mikono yake ilionekana ngao ya kichawi kwenye mikono yake pamoja na mkuki wake na alimsogelea Yan Buwen kwa kasi huku akidhamiria kumchoma tumboni , lakini Yan Bvuwen ni kama alikuwa akisubiria amfikie kwani palepae ulitokea miale mikali sana kuangalia kwa macho na kumfunika Monk kiasi cha kusababisha eneo lote kuwa na mwanga wa tofauti licha ya kwamba ilikuwa mchana na mpaka mwanga unapotea Monk hakuonekana tena zaidi ya mkuki wake kudondoka chini.
Na huo ndio ukawa mwisho wake , kwani Yan Buwen aliweza kumyeyusha mara moja.
“Nguvu ya mionzi ambayo ipo kwenye hizi Bazooka chanzo ni wewe mwenyewe si ndio?” Aliongea Roma.
“I guess there is no harm telling you this , I’m Godstone and Godstone is me”Aliongea Yan Buwen akimaanisha kwamba yeye jina lake ni Jiwe la kimungu na Jiwe la Kimungu ndio yeye, yaani yeye ndio chanzo cha nishati yote ya ant- matter.
Palepale kuthibitisha majigambo yake alishika eneo la kifua chake na kisha akaingiza mkono eneo la moyo na kuchomoa kitenesi kinachong’aa sana , lilikuwa jiwe la kimungu na Roma alishangazwa mno.
“You fused God’s stone into your body?”Aliuliza Roma kwa mshangoa kwa lugha ya kingereza , kwamba ameunganisha jiwe la kimungu na mwili wake.
“Hahaha…. Unaogopa? , Frequency za mfumo nishati wa mawimbi ya mwili wangu unafanana kabisa na Frequency za jiwe la kimungu, hivyo moyo kwangu hauna kazi kubwa kwani nishati safi inayotokana na anti- matter inafanya seli za mwili wangu kuwa ‘active’ , wewe si ulifanya jiwe hili kuwa kama kajiwe kakuchezea nako , mpuuzi mkubwa wewe ngoja wenye akili tukuonyeshe”Aliongea
“Only I , Yan Buwen deserve to own the world’s greatest creation”
Aliongea huku akinyanyua mikono hewani kama vile watu wa dunia nzima walikuwa wakimuona lakini baada ya kushusha mikono yake chini alichia na shoti ambazo zilikaa kama boriti na kuwashambulia Roma na watu wake.
Baadhi ya makomandoo wa kijeshi walipoteza maisha palepale na Misukule ya Yan Buwen ilibakia mitano tu na walinyanyua makombola yao ya Bazzoka na kuachia miale ya yenye mionzi ya Thanatos.
BOOM , BOOM , BOOM.
Ngao ya kichawi iliowafunika Neema Luwazo na wengine iliyumba na kuonyesha muda wowote ingeachia na Roma alitumia nguvu nyingi sana kuidhibiti na kila inapopokea mashambulizi maumivu aliyasikia yeye.
Sasa shoti alipiga Yan Buwen ilikua na nguvu mno na ilimfanya Roma kuhishi kama yupo Jehanamu, ni maumivu ambayo mara ya mwisho aliyahisi wakati akipambana na Poseidon kwenye bahari ya kusini ya China, Roma alijikuta akitapika damu lakini hata hivyo aliendelea kudhibiti ngao isiondoke kwani ingekuwa ndio vifo vya watu wake muhimu, yeye alijiambia ni kheri wafe wengine lakini sio Mage na Neema Luwazo.
“Romaa..!!”Mage na Magdalena na Donyi awamu hii walimlilia Roma mara baada ya kutapika damu.
Roma alijitahidi kuita nguvu ya kimaandiko kumponyesha haraka na alijihisi ahueni mara baada ya maumivu kupungua.
“Nipo sawa ni majeraha madogo tu “Aliongea kuwaondoa hofu maana Mage alitoa kilio , alikuwa akijilaumu kukosa uwezo wa kumsaidia Roma”
“Mhmh!.. nimetumia nishati ya ant- matter halafu unasema hujaumia sana , ngoja tuone kama unaweza kubwabwaja baada ya hili pigo”Aliongea Yan Buwen na kunyanyua mkono akitaka kumpiga tena Roma.
“Hapana , Yan Buwen naomba uache”Sauti ya kike ilisikika na alikuwa ni Queen alietoka kwenye ngao na kumpita Roma kwa mbele bila hofu.
“Yan Buwen naomba uache tafadhari , usifanye hivi jamani.. acha kuwa mkatili kiasi hicho unataka kumuua na mtoto wako?”alianza kuongea huku akilia
“Bitch” Aliongea Yan Buwen na kuanza kuandaa pigo la kumkausha Queen.
“Queen!!!”
“Wewe mpuuzi hujafa tu?”Aliongea Yan Buwen.
“Nini?”
“I am calling you a bitch , bitch , bitch …..Unafikiria nakuona kama binadamu, kwangu wewe mwili wako ulikuwa kama kipozeo tu usijifanyishe najali sana kuhusu huyo mdudu alieoko tumboni kwako”Aliongea Yan Buwen.
“Kaa kimya wewe mpuuzi, wewe ni chizi na huna akili ndio maana unataka kuua mtoto wako”Aliongea Omari
“Hahaha unajitekenya….naomba nitangaze hadharani , labda haieleweki , nasema hivi hakuna binadamu ambaye anavigezo vya kubeba mimba yangu, Shenzi labda nikifa na kufufuka ninaweza kufikiria upya”Aliongea kwa jeuri na maneno yalikuwa makali kiasi kwamba yalimnyong’onyesha Queen nakujikuta akikaa chini na kuanza kulia.
Siku zote aliishi kwa tumaini na kujiambia Yan Buwen anaweza kuwa kichaa lakini hawezi kumdhuru mtoto wake , lakini tumaini ambalo alikuwa nalo mpaka hapo alihisi lishafutika.
“Yan Buwen unapoteza muda , ushamuua tayari Monk malizana na hawa waliobaki , malizana na Roma na baada ya hapo tukaimalize na familia yake , hakuna wa kutuzuia kwa sasa”Aliongea Raisi Kigombola.
“Kigombola wewe msaliti usifikirie hilo linaweza kuwezekana kirahisi kama unavyodhani , jeshi letu lipo imara”Aliongea Afande Tozo lakini maneno yake yalipokelewa kama upuuzi na Kigombola na alimwangalia Neema na mtoto wake Donyi.
“Neema njoo huku upande wangu wewe na mtoto wetu, nitakusamehe kwa usaliti ulionifanyia na nitaendelea kukusapoti wewe na mtoto wangu pia”Aliongea kwa kubembeleza akimtaka Neema Luwazo na Donyi kwenda kusimama upande wao , lakini Neema alitingisha kichwa kukataa, hivyo hivyo na Donyi alikataa, aliekuwa mbele yake ni kama hakuwa baba yake , mwanzoni hakutaka kushuhudia akifa lakini kwa ushetani alioweza kuona kwa macho yake hakutaka kabisa kuungana nae hata kama ni baba yake.
“Wewe ni shetani tena zaidi ya shetani , huwezi kunitumia kwa ajili ya faida kama kweli ulikuwa ukinipenda , nakuchukia zaidi ya mara milioni moja, bora Yan Buwen aniue kuliko kuungana na wewe kwenye ushenzi wako”
“Hahaha. Mzee naona mwanamke wako na mtoto wako wamekukataa waziwazi, lakini usiwaze nitahakikisha vifo vyao sio vya maumivu” Aliongea Yan Buwen kwa kebehi.
“Mwanamke ni mwanamke tu na akishapata mwanaume mwingine anaekidhi haja zake anasahau kila kitu , sijali kama atakufa lakini naomba mtoto wangu awe hai”Aliongea na kisha akageukia kundi ambalo lilikuwa limemzuguka wakiwemo baadhi ya mawaziri ambao walikuwa ni mashushu wake serikalini.
“Ambaye haniungi mkono kwa misheni yangu anaweza kupita hapo katikati na kulifuata geti na kuondoka Waziri mkuu kama unataka kuungana na mimi njoo upande wangu , yoyote pia anaetaka kuja huku afanye hivyo na ataendelea kuishi”Aliongea lakini hakuna ambaye alikuwa na ujasiri huo , hawakuwa wajinga , ilimaanisha ambaye angeweza kuondoka hapo ndio ingekuwa kifo chake hivyo waliishia kuangalia chini kama kuku tetea , upande wa waziri mkuu na wengine hakuna ambaye alikuwa na mpango wa kusaliti nchi , waliamua kama ni kufa ngoja wafe kiume.
Kigombola mara baada ya kuona hakuna ambaye anataka kuondoka ,alitabasamu kwa kuridhika na kisha alimgeukia Yan Buwen.
“Tekeleza vifo vya wote ambao wanapaswa kufa leo hii tumalize kazi mapema”
“Haina haja ya kuniambia mara mbili mbili mzee”Aliongea Yan Buwen na palepale aliachia pigo.
“Omarii..!!!”Waliita kwa nguvu.
Roma alijikuta akibung’aa na kushindwa kuchukua hatua mara baada ya Omari kumkimbilia Queen na kuondoka nae , Omari alikuwa na spidi lakini hata hivyo miale ilikuwa na spidi zaidi yake na ile anampakua Queen alipigwa na shoti mgongoni kiasi cha kuchana shati lake ambalo amevaa.
Isingekuwa uwezo wake wa kijini huenda angeyeyuka kama wale wengine, Queen hakuamini kama Omari angemuokoa, hata hivyo alishajichokea na alitaka tu kufa ili kupunguza maiumivu ya moyo.
Alijikuta akimwangalia Omari ambaye alikuwa akiugulia maumivu , hakuamni licha ya kumkataa huyu mwanaume lakini alikuwa tayari kumuokoa kwa kumkinga na mwili wake.
“Omari….Omari kwanini unakuwa mjinga wewe mpumbavu”Alifoka Afande Tozo lakini Omari hakujali hata hivyo alikuwa akijihisi maumivu makali kiasi cha kutaka kupoteza fahamu.
Roma hata yeye alishangazwa na kitendo cha Omari na kukasirika kwa wakati mmoja lakini hakuwa na namna , alichokifanya ni kuita uwezo wake wa kijini na kisha akawakausha wanajeshi watatu wa Yan Buwen na kumuachia wawili wa mwisho Magdalena amalizane nao maana hawakuwa na siraha.
Roma aliamua kumfuata juu Yan Buwen , alijiambia ndio muda muafaka wa kumalizana nae , maana kama hatofanya hivyo kwa ukichaa wa Yan Buwen basi huenda hata taifa kutokuwa salama kama sio dunia nzima na hata hivyo yeye ndio mwenye makosa kupoteza jiwe la kimungu kwa hayawani.
“Hades unatakiwa kuelewa mpaka sasa huniwezi kwa chochote , nina kwenda kuwa mtu mwenye nguvu zaidi duniani mara baada ya kumaliza majini yote husuani Hongmeng, ninaweza kukusamehe leo hii kama tu utajisalimisha kwangu na kuwa mmoja ya watu wangu”Aliongea na kumfanya Roma kujawa na hasira na kukunja ngumi.
“Sina uhakika kama ninaweza kukuua , lakini nakuhakikishia wewe pia huwezi kuniua bila ya kufahamu nani anakupa nguvu , maana najua wewe ni mbwa ambaye unatumika tu kwa ajili ya bosi wako”Aliongea Roma
“Unasemaje?”Aliongea Yan Buwen huku akimwangalia kwa macho makali alionekana kukasirika.
“Nimekosea? , ninaweza kukusifia kwa kuweza kujificha lakini pia umeweza kuwa na uwezo mkubwa lakini naamini kabisa usingefikia hapo ulipo bila kupata msaada kutoka kwa mtu ambaye alinipokonya jiwe la kimungu , Thanatos na Hollygrail”Aliongea Roma , ijapokuwa hisia zake zilimwambia ni Athena lakinni alitaka Yan Buwen akiri wazi , kwanza alishindwa kuelewa kwanini Athena alikuwa akishirikiana na mpumbavu kama Yan Buwen ndio maana alitaka kujua zaidi nia yake.
“Sijui nia yako kwangu kunishambulia lakini naamini moja kwa moja wewe ni mbwa tu unaefanya kazi kwa malengo yao na hao ndio ambao ni maadui zangu ninaowalenga na ninaotaka kumalizana nao”Aliongea na kumfanya Yan Buwen kuanza kupandwa na hasira maradufu kwani alichosikia yalikuwa matusi kwake , ijapokuwa maneno ya Roma yalikuwa ya ukweli lakini yalikuwa yakiuma , aliguswa penyewe.
“Unajua nini wewe mpumbavu , kwanza sitaki hata kupoteza muda kwa kuongea na mpuuzi kama wewe nitakuonyesha leo ni kiasi gani nimekuzidi uwezo , nitakusambaratisha na kubakia vipande vipande na baada ya hapo wanawake wako wote nitawakusanya na kuwapeleka kwenye gereza la mateso kwa ajili ya kuchezewa na kila mwanaume, nadhani nikiyaona machozi yao nitafarijika”Aliongea na palepale jiwe la kimungu ambalo lipo kwenye kifua chake lilianza kutoa miale mingi ni kama lilikuwa likimpongea kwa kuwa na hasira
Roma aliamua sasa kuwa siriasi na aliiita kiwango cha juu cha nishati ya mbingu na ardhi kwa ajili y a kujiweka tayari kukumbana na Anti-matter, hata hivyo alihisi kani kubwa kutoka aliposimama kutokana na msunguano wa nguvu ya jiwe la kimungu.
Mawingu yalianza kujitengeneza na kuashiria mvua ilitaka kuanza kunyesha lakini sio hivyo tu ngurumo za radi hazikuwa kimya pia
Upande wa chini Magdalena aliweza kumaliza misukule yote ya Yan Buwen na sasa macho yake yalikuwa juu akiangalia pambano.
Hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kukimbia kwa kuogopa Yan Buwen anaweza kuwashambulia hivyo waliishia kuangalia kile ambacho kinakwenda kutokea.
Yan Buwen alikuwa na hasira mno , muda ule ule mpira wa shoti ulijitengeneza kwenye mikono yake huku ukizunguka zunguka kana kwamba unaogopa kugusana na kiganja chake .
“Go to hell!”Aliongea kwa sauti na kisha alirusha ule mpira kuelekea aliposimama Roma na palepale ulibadilika kutoka kuwa mpila na kuwa kama miale ya shoti ya umeme , lakini Roma alikuwa na spidi kwani palepale aliweza kutengeneza ngao na kuizuia na kufanya atomu kusuguana angani na kutengeneza mwanga wa rangi tofauti wa kuvutia.
Lakini hata hivyo pigo la Yan Buwen lilimfanya kuhisi maumivu makali maana ilihitajika nguvu kubwa kuweza kudhibiti ngao yake , lakini wakati huo huo kudhibiti ngao iliowafunika Neema na wenzake.
Yan Buwen baada ya kuona Roma kakinga , aliachia pigo lingine na lingine na kudhidi kumsababishia Roma maumivu makali na kuishia kutema damu.
Yan Buwen alitabasamu kwa kebehi baada ya kuona mbinu sahihi ya kumuua Roma ni kushambulia kwa kasi ngao zote mbili , kwani Roma hakuwa na uwezo wa kushambulia zaidi ya kukinga mapigo yake kwasababu aikuwa akijilinda yeye na waliochini yake.
“Roma shambulia na wewe na usikinge tu mapigo yake”Aliongea Magdalena ambaye alianza kukosa uvumilivu na chozi kuanza kumtoka.
“Nimetumia robo tu ya nguvu zangu kushambuia lakini naona upo hoi taabani”Aliongea Yan Buwen na kuachia mapigo mawili kwa wakati mmoja kwa kutumia mikono yake yote , moja alilenga chini kwenye ngao iliowafunika Neema na nyingine alimlenga Roma.
Alishangundua kadri alivyokuwa akishambulia ngao ndio ambavyo Roma anapoteza nguvu na hivyo alitumia mbinu hio hio kuongezea dawa.
Roma alijihisi roho yake inataka kuacha na mwili wake kwa maumivu ambayo anayasikia, muda huo ambao alipaswa kuwa Honeymoon ndio muda ambao alikuwa akiugua , tena hata nguo za harusi hakuvua.
“Daah..Roma anateseka kwa ajili yetu , sijui kwanini tukaingia mkenge na kuja hapa”aliongea Afande Tobwe huku akijidharau kwa kutoweza kufanya chochote , kauli yake ilisikika na baadhi ya watu waliokuwa wakimsapoti Kgiombola na kuishia kucheka.
Roma alikuwa ashaita uwezo wake wote wa nguvu ya kijini katika levo ya kupita dhiki na alijiambia kadri ambavyo atakuwa anakinga mapigo ya Yan Buwen basi anaweza kushindwa kuendelea kuhimili na kupoteza uhai.
Kuna muda alitamani hata kupigwa na radi kama ilvyotokea wakati akipambana na Poseidon na huenda angejitoa muhanga kufa na Yan Buwen moja kwa moja , lakini hata hivyo dalili ya radi ilionyesha kuwa mbali sana licha ya kwamba wingu kubwa lilikuwa limetanda angani.
Tegemeo lake la mwisho ni kuchukua ile dhana ya Ganyua ili kujikinga nayo kama ngao halafu atumie nguvu ya kijini kuwakinga waliochini yake , aliamini ndio mbinu pekee ambayo ingepunguza nafasi ya kushindwa pambano lakini pia maumivu.
Roma aliita kwenye mikono yake , lakini muda ule na Yan Buwen aliachia pigo kubwa kuliko la mwanzo na ile dhana palepale ilitengeneza ngao yenyewe , lilikuwa kosa kubwa sana , kwani ngao aliotegneneza ilionyesha kutokuweza kuhimili vizuri na palepale ilijizima yenyewe na kulitokea mlipuko ambao haukuwa wa kawaida ni kama anga lilikuwa likitaka kudondoka na kufanya watu wote kuziba masikio.
“Romaa…!!!!!”Omari na Magdalena ndio walioweza kushuhhudia Roma akipigwa pigo takatifu na Yan Buwen na kupoteza balansi na kudondoka chini kama embe.
Roma alijitahidi kuiweka akili yake sawa asipoteze fahamu lakini mwili haukutaka kwani maumivu yalikuwa makali mno na palepale alianza kuona nyota nyota na hatimae ukungu na mwili wake ulipoa kabisa na akalegea na kutua chini kama furushi.
ITAENDELEA. IJUMAA - WATSAPP 0687151346