Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Mkuu tunathamini sana kazi yako, binafsi nakupongeza sana, kwa sasa naona umeamua kupost mara moja kwa wiki, weka wazi kama ni ijumaa au jumamosi basi tujue kuliko kutoa ahadi halafu hutimizi
Akijibu nitag
 
SEHEMU YA 470B

“Inatosha Ron , maana sitokuongezea mshahara hata kama uninyenyekee kwa kiasi gani”Aliongea Roma kwa kingereza kwa kuweka utani na kumfanya Edna atamani kumuweka Roma ngumi.

“Mfalme Pluto unaonekana ni mwenye furaha , nimefarijika na mabadiliko yako”Aliongea na Roma alitabasamu na kisha akampita akimgusa gusa kwenye bega na kisha akamtambulisha Ron kwa Edna na Blandina.

“Huyu ndio kiongozi mkuu wa ukoo wa Konstantin kutoka Italy , ni uzao wa Kaisari alietawala kipindi cha utawala wa Kirumi , Lakini nani anafahamu ni vizazi vingapi vimepita tokea kufa kwa Kaisari lakini Ron bado yupo”Aliongea Roma kwa Kingereza.

“Mr Ron nimefurahi kukutana na wewe , nimesikia umemchagulia Bi Wema vazi la kuvaa, inaonekana upo vizuri kwenye fasheni za kimavazi?”Aliuliza Edna kwa urafiki.

“Nimefurahi sana kukutana na wewe pia Madam Persephone ,ubunifu wa mitindo ya kimavazi pia ni moja kati ya kazi zangu nyingi na nimeweza kupata heshima ya kuandaa gauni lako la harusi”Aliongea Ron na kumfanya Edna kuhisi aibu kidogo mara baada ya kusikia gauni la harusi , lakini wakati huo huo jina la Ron’s ni kama lilikuja na kupotea kwenye kichwa chake na kumfanya kumwangalia Bi Wema na vazi alilovaa palepale aligundua gauni la Bi Wema ni ubunifu maarufu ya mitindo ya mavazi ya Bohemia na jina la Ron ni miongoni mwa majina ya wabunifu ambao ashawahi kuwasikia.

“Nina kampuni inayohusiha ubunifu na udarizi wa mavazi , nishawahi kusikia jina lako lakini sijawahi kukuona kwa sura ,mimi nishabiki wa mavazi ya mtindo wa kibohemia”Aliongea Edna akitumia mbinu ya ushawishi kukubalika kwa haraka hakuna binadamu asiependa kusifiwa au kutambulika kwa kile anachokianya hata kama ni kidogo vipi.

“Ni heshima kwangu kupata kutambuliwa na wewe Madam Persephone”Edna alifurahi na kisha alimgeukia Rom.

“Nakumbuka mara yako ya kwanza kuanza kazi kwenye kampuni , uliulizwa swali linalohusiana na mtindo wa kimavazi mathalani kampuni za kiitaliano na uliweza kutoa majibu mazuri kumbe chanzo ni Ron?”Aliongea Edna na kumfanya Roma kucheka sana baada ya kukumbuka.

“Upo sahihi nguo zangu nyingi Ron ndio ananitengenezea na kuna muda tukipiga stori huingizia maswala ya mavazi hivyo kidogo nilikuwa na uelewa?’Aliongea Roma mara baada ya kusafisha koo.

“Master Ron umesema ubunifu ni sehemu ya kazi zako nyingi, je unajihususha na kazi gani nyingine?”Aliuliza Edna na kumfanya Rona kuwa na wasiwasi kidogo na kumwangalia Roma kwani swali la Edna lilikaa kimtego.

“Usiwe na wasiwasi , unaweza kumwambia”

“Nitakuwa mkweli kwako Madam Persephone , ukoo wangu ndio wamiliki wa kundi kubwa la Kimafia nchini Italy na mimi ndio nilikuwa kiongozi kabla ya kustaafu”Aliongea na kumfanya Edna kushangaa akiwa kama haamini.

“Hakuwa kiongozi tu wa kundi la Mafia , lakini pia alipewa cheo cha heshima cha Uraisi na Mafia Alliance in Cicilly”Aliongezea Roma.

“Lakini hayo yote yalikuwa ni zamani , kwa msaada wa Mfalme Pluto niliweza kuanza maisha mapya ndani ya hivi visiwa na sasa kazi yangu kubwa ni kutunza mali zake”Aliongea.

Roma alimtambulisha mama yake mzazi kwa Ron na Blandina alifuahi kukutana na Ron hasa pale alipofahamu ndio rafiki mkubwa wa Roma.

“Vizuri sana rafiki yangu , ngoja tusalimie wengine na tuondoke hapa ili tusisubirishe wanaotaka kuniona kwa muda mrefu ”Aliongea Roma huku akimgusa bega Ron na kumpita.

Waliingia kwenye gari aina ya SUV mara baada ya kumaliza kusalimiana na kila mmoja , Ron alikaa siti ya mbele kabisa huku akiendelea kuongea na Roma kwa kukumbushiana habari za muda wote ambao hawakuonana.

“Madam Persephone harusi yako imepangwa kufanyika kesho , nitakuomba baada ya chakula cha mchana ujaribishe gauni lako , unaweza ukashangaa ni kwa namna gani nimeweza kupata vipimo vyako lakini ukweli ni kwamba ujuzi wangu umenifanya kukadiria kwa kuangalia picha yako tu……”Aliendelea kuongea na Edna huku habari kubwa ni namna anavyofanya kazi yake ya ubunifu wa mavazi na Edna alichangia.

Bi Wema na Blandina waliishia kutabasamu baada ya kuona Ron anavyoongea kwa ishara , ijapokuwa Bi Wema hakuwa akielewa kingereza lakini ni kama alikuwa akielewa kile kinachoongelewa.

“Ron unaongea kuhusu picha ya mke wangu kama vile ugonjwa wako wa macho umepona , naamini msaidizi wako ndio ambaye alikadiria vipimo”Aliongea.

“Mfalme Pluto unaishi kizamani sana”

“Nini?”

“Natumia ‘Contact lenses’ , unaweza kuona macho yangu kwa kiasi fani yamebadilika rangi”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie na aligundua kwenye macho yake yamebadilika kwa kiasi flani na kiini cheusi kuonekana kama kimepauka.

“Mr Ron naomba uache kuniita hilo jina , sijisikii vizuri kila ninapolisikia”Aliongea Edna.

“Bila shaka Miss Edna, hivi nilishia wapi kuongea ., Oh nimekumbuka nilikuwa nikizungumzia kuhusu gauni lako , ukweli ni kwamba ni mara yangu ya kwanza kuandaa gauni la harusi hivyo nilikuwa na mengi ya kujifunza , nilienda hadi New York kutafuta ushauri kwa rafiki yangu , Madam Vera Wang..”Kabla hajaendelea Edna alimwingilia.

“Unamaanisha Madam Vera Wang mwanamitindo maarufu wa magauni ya harusi ni rafiki yako?”Aliuliza Edna kwa mshangao.

“Upo sahihi ni rafiki yangu na ni mtaalamu wa viwango likija swala la mavazi ya harusi , nilimuuliza baadhi ya vitu ili kunisaidia kuandaa la kwako”

“Ron nafikiri hujaweka urembo wa almasi na dhahabu kwenye hilo gauni maana litatumika mara moja tu”Aliongea Roma na kumfanya Edna amgeukia.

“Acha ubahiri”

“Mfalme Pluto wala usiwe na wasiwasi , niseme ukweli nilikuwa na chaguzi nyingi namna ya gauni hilo lionekanaje lakini mwisho wa siku nilifikia na hitimisho kulitengeneza kwa kutumia vitambaa maarufu vya kiasili ili kidogo liwe jepesi kuvalika”Aliongea na kumfanya Roma kutingisha kichwa kwa kukubali na kisha akamgeukia Edna.

“Mke wangu sio ubahiri kwani kila mtu anatumia madini ya Almasi na dhahabu kupamba magauni, hivyo la kwako lingekosa ule upekee , Si nilikupaga Henrygraves kutoka kampuni ya Patek Phillipe ni zaidi ya almasi au dhahabu kwa thamani yake”

“Saa ulionipa ni vitu viwili tofauti , wanawake tunapenda sana vitu vinavyong’aa na kumetameta na kuonekana vizuri kwa macho , kwanza umeniambia kuna zawadi yangu umeniandalia sijasahau”Aliongea Edna bila ya kuwa na wasiwasi ya uwepo wa watu kwenye gari na kumfanya Roma kucheka.

“My dear wife inaonyesha siku hizi umekuwa mhitaji wa zawadi kuliko siku za nyuma”

“Kama nisipotaka zawadi , wengine wanaweza kupata zawadi nilizopaswa kupewa mimi hivyo lazima kuhakikisha nafasi yangu inakuwa salama”Aliongea Edna kwa sauti ndogo na kumfanya Roma kutabasamu.

“Zawadi yako nimeiandaa lakini usubiri mpaka baada ya harusi kuanza”

“Bado unanificha na unachotaka kunipa?”Aliongea Edna kwa kutingisha mabega lakini aliishia kutoendelea kuuliza kama kwa kuona Roma anataka amfanyie Surprise.

Kadri gari waliokuwa wamepanda ikiendelea kusonga sasa waliweza kuona mandhari ya kisiwa hicho na baadhi ya visiwa ambavyo vilikuwa kwa mbali , ambavyo kuna vilivyokuwa vikitoa moshi wa kulipuka kwa Volkano kwenye vilele vya mlima huku vikizungukwa na msitu.

Edna aliweza kuangalia mazingira mathalani namna maisha yanayovyendelea na aliweza kuona nyumba ambazo zimejengwa kwa kuezekwa na mapaa yaliopakwa rangi nyekundu huku asilimia nyingi ya rangi zilizotumika kupamba kuta za nje ni rangi nyeupe lakini pia vioo vya madirisha vilikuwa ni vile vigumu lakini vya rangi ya bluu mtindo wao wa maisha haukuonyesha tofauti na watu wa bara la Ulaya.

Waliweza kuona kundi la watu waliokuwa pembezoni mwa fukwe wakifurahia upepo , ilikuwa muda wa mchana lakini watu walikuwa wengi

“Mr Ron kuna wakazi wangapi kwenye hiki kisiwa?”Aliuliza Blandina.

“Madam kuna zaidi ya watu elfu mbili wenyeji wa hapa na kwa wale ambao wapo chini ya utawala wa mfalme Pluto wanafikia zaidi ya elfu tatu ambao wapo tu kwenye hiki kisiwa ukiachana na vingine”

“Kuna ambao wapo nje ya hiki kisiwa?”

“Meli za watu binafsi pamoja na watu wanaopenda kuona visiwa hivi huwa wanakaribia , hivyo ulinzi umekuwa kitu makini sana kwetu na mpaka sasa kuna wanajeshi baharinni zaidi ya elfu moja wakipiga doria kwenye meli za kivita wote hao wapo chini ya Mfalme Pluto”Aliongea na Blandina alionekana kumuelewa na hakuuliza swali lingine

Dakika kama kumi mbele waliweza kuingia kwenye eneo lililokuwa limepandwa maua mengi na bustani za kuvutia , ni eneo ambalo halikuwa na geti ila kwa mbele zilionekana nyumba nzuri ambazo zilikuwa za rangi nyeupe na ndefu kwenda juu , ilikuwa ngumu kukadiria ni za ghorofa kutokana na aina ya ujenzi wake haukuwa ule wa kisasa zaidi , juu ya mapaa moshi mzito ulikuwa ukitoka..

Katikati ya bustani kulikuwa na Fountain ambayo imejengwa kwa mtindo wa kizamani sana , ni aina ya Fountain ambazo unaweza kuzikuta zaidi kwenye miji ya Italia kwa muundo wake.

Baadhi ya watoto walionekana kukaa pembeni mwa hio Foutain wakicheza kwa fuaraha kwa kuzunguka wakiwa wameshikana mikono , hakika maisha yalionekana kuwa ya amani sana na kila kitu kilivutia kwa macho,alichokipenda zaidi Edna ni usafi wa mazingira hakukuwa hata na dalili ya aina yoyote ya uchafu unaozagaa zaidi ya moshi tu unaotoka kwenye baadhi ya nyumba.

Ki ufupi ni kisiwa ambacho kilikuwa kikubwa lakini wakazi walikuwa wachache na nyumba zilijengwa kwa mtindo wa kimakundi makundi , yaani ndani ya eneo moja kulikuwa na nyumba mbili au zaidi na zote hushirikiana eneo la nje kwa usawa na barabara za Zege ziliingia kwa kila nyumba.

“Karibu tena nyumbani mfalme Pluto” Mwanamke mmoja wa kizungu alipaza sauti mara baada ya wote kushuka kutoka kwenye magari na watu wengi wanaume na wanawake walikuwa wamesimama na kuwapungia mkono.

“Hongera kwako kwa harusi”Aliongea mwingine na baadhi ya wengine pia waliungana kumpongeza Roma.

Roma alisalimiana nao kwa kupeana mikono huku akiwasalimia kwa lugha tofauti tofauti , ilikuwa ni kama anajua huyu anazungumza lugha hii na huyu ile na ndio alichofanya.

Edna na Blandina hawakuelewa hata lugha ambayo Roma anaongea kwani kuna muda aliongea Kirusi kuna mara aliongea kireno na kuna muda aliongea kijerumani.

“Mr Rona hawa ndio wazawa wa hapa?”Aliuliza Edna.

“Hapana , Wazawa wanaishi upande wa mashariki kutoka kwenye hiki kisiwa , hao unao waona hapo wote waliomba kuishi kwenye hivi visiwa kupitia kwa mfalme Pluto , kuna zaidi ya vijiji vitano vikubwa ndani ya hiki kisiwa na wote wamemfahamu Mfalme Pluto kwa muda mrefu sana, yule mwanaume alieanza kusalimiana nae anafahamika kwa jina la Schachenleer alikuwa ni kiongozi wa kundi la kigaidi na anatafutwa sana na serikali ya Marekani , mume wake pia anafahimika kwa jina la Saab na yeye pia alikuwa ni kiongozi wa kikundi cha kigaidi kutoka Iraq m hivyo hapa wapo kama mafichoni?”Aliongea Ron lakini Blandina na Edna walijikuta wakipatwa na mshangao kwa maelekezo yake

“Mfalme Pluto hakika unaonyesha mabadiliko makubwa unaonekana kuwa na furaha kuliko ulivyoondoka”

“Labda ni kwasababu ndio anafunga ndoa, Mfalme Pluto hakika umekuwa mtu mzima sasa”Waliongea watu waliosimama na Roma wanaume na wanawake na kuishia kucheka.

Roma alionyesha maisha yake hapo visiwani yalikuwa yale ya ukaribu sana na raia kwani walionyesha kumzoea mpaka kuingizia utani.

Kuna muda Edna alionyesha kutokuelewa kingereza chao kutokan ana rafudhi ila alifanikiwa kuwasalimia , mwanzoni alihofia kwasababu watu hao walikuwa na historia mbaya wangekuwa na roho mbaya , lakini walionyesha urafiki mkubwa na ule ukarimu wa kipekee na hata Bi Wema na Blandina pia waliweza kuwapenda.

Baada ua kufika mje ya nyumba hizo waliweza kuona watoto wawili wa kike na kiume wanafukuzana , walikuwa watu wazima rika la miaka kama kumi na moja na mwingine kama kumi na tano , wote walikuwa wazungu .

“Isabella ..Brewster ?!”Aliita Roma huku akionyesha mshangao kwani walionekana kuwa watu wazima na walikuwa wote wakigeuka na kumwangalia Roma.

“Mfalme Pluto hatukufahamu umekwisha kufika ..oh huyu lazima atakuwa ndio Madam Persephone , si ndio , karibu sana, unaonekana mrembo kuliko tulivyokuona kwenye picha”Aliongea yule mkubwa wa miaka kama kumi na tano huku akimwangalia Edna kwa tabasamu, alikuwa na kiini chake cha macho kimefifia na nywele nyeupe aina ya Blonde.

“Isabella imekuwaje ukawa mnene kiasi hichi na wewe Brewster naona umekonda”Aliongea Roma , alikuwa akiwafahamu vizuri kwani walikuwa ni watoto wa kike wa Sauroni.

Wote kwa pamoja walikaribishwa kwenye nyumba ya Ron na Edna alishangazwa ,ijapokuwa mwonekano wa nje haukuwa mzuri sana , lakini ndani yake kulikuwa kukipendeza mno, lakini alishangazwa pia kuona siraha aina ya bunduki pamoja na bastora zikiwa zimening’inizwa karibu na jiko alishangaa kwani nchi kama Tanzania siraha kama hizo huwezi kuona zikiweka kiholela namna hio..

Nyumba za hilo eneo zilikuwa kidogo na utofauti na nyumba za kitanzania , karibia zote zilikuwa na majiko makubwa eneo la sebuleni ambayo huchoma kuni kwa ajili ya kupasha nyumba joto na hii yote ni kutokana na majira ya hali ya hewa , kulikuwa na kipindi cha baridi kali mno..

Familia ya Sauroni na Ron waliishi ndani ya ‘compaund’ moja na kwa sherehe ya harusi hio nyumba ya Ron ndio ilichaguliwa kwa ajili ya wageni kutumia na baada ya harusi Roma kwenda kwenye makazi yake na mke wake.

Edna aliweza kutambulishwa kwa Makedon ambaye alifika kwa ajili ya kuhudhuria harusi lakini pia aliweza kukutana kwa mara nyingine na Sauroni , wageni wote walikuwa wapya kwa Blandina hivyo Roma alichukua nafasi ya kumtambulisha mama yake vizuri na wote walifurahi kukutana nae.

“Jamani eh kwanini muendelee kuongea kuhusu habari za vita mbele ya Edna , Kesho ni siku ya harusi ya mfalme Pluto nadhani tuongelee hio”Aliongea mke wa Sauroni afahamikae kwa jila la Bellaih

“Nakubaliana na wewe” Alijibu Ron na wakaacha habari za vita na kuanza kuongea habari nyingine huku chakua kikiandaliwa.

“Vipi wakina Edward , hawajafika bado?”Aliuliza Rom.

“Edward alifika hapa na Makeddon lakini karudi kwenda kumchukua Malkia Catherine na Clark, watafika hapa usiku”Aliongea Sauron.

“Catherine yupo bize sana na maandalizi ya Olimpiki hivyo atahudhuria matukio mawili kwa wakati mmoja kesho atahudhuria tukio la harusi na atageuza siku hio hio kwa ajili ya siku inayofata ya ufunguzi wa mashindano hayo”Aliongea Sauroni.

Baada ya kumaliza chakula Ron alimchukua Edna akimuacha Roma kuendelea kongea na baadhi ya watu waliofika kumsalimia.

Ofisi ya Ron haikuwa mbali sana na nyumbani kwake , ilikuwa mita kadhaa , lilikuwa ni jengo la ghorofa mbili kwenda juu, ambalo lilijaa kila aina ya michoro , kwa maelezo ya Ron ni kwamba kampuni yake ya mavazi ipo Palermo na hapo hutumia tu katika ubunifu na utekelezwaji unakuwa ni sehemu nyingine na hata gauni la harusi alibuni kwa kuchora michoro na kutiuma Palermo ambako ndio ukamilishaji ulifanyika.

Edna baada ya kuonyeshwa gauni lake alijikuta akilipenda hapo hapo na ilionekana Sauroni alikuwa sahihi kwenye vipimo vyake , kwani lilimkaa vizuri sana mwilini mara baada ya kujaribisha.

“Naweza kusema wewe ni moja ya bibi harusi mrembo ambao nimeweza kushuhudia kwenye maisha yangu”Aliongea Rona mara baada ya kumuona Edna alivyopendeza.

“Asante sana Master Ron”Aliongea Edna huku akitoa tabasamu hafifu , alionyesha kulipenda.

“Kuna jina lolote umelipatia hili gauni?”Aliuliza Edna.

“Swali zuri , nimepenga kulipatia jina la Demeter na kwasababu huu ni mtindo wa kipekee litapatikana sokoni baada ya ndoa yako”

“Demeter nahisi nishawahi kusikia kuhusu hilo jina?”

“Katika historia za hadithi za kigiriki Demeter alikuwa ni mama wa Persephone , mungu wa mavuno , nimeamua kulipatia jina hilo kwasababu ndie anapaswa kukusindikiza wakati wa kuingia eneo lililoandaliwa kwa ajili ya harusi yake”Aliongea na Edna alitingisha kichwa kukubali.

“Niseme kwamba kuna mtu unafanana nae , naweza kusema ni kama pacha wako”Aliongea Sauron

“Unamzungumzia nani?”

“Kuna mwanamke ambaye alitokea kupendwa sana na Mfalme Pluto , anafahamika kwa jina la Seventeen”Aliongea na kumfanya Edna kupoteza raha kidogo.

“Inasikitisha sijawahi kukutana nae”Aliongea huku akiwa amelazimisha tabasamu.

“Miss Edna naomba usifikirie kama Mfalme Pluto anakutumia kama mbadala , unaweza kufanana na Seventeen lakini ninyi ni watu wawili tofauti”Aliongea na kumfanya Edna kuridhika na maneno yake na muda uleule aliingia mtoto mwenye rangi mchanganyiko wa mwafrika na mzungu.

Edna alimfahamu mtoto huyo kwani ametambulishwa kwake na Bi Wema , alikuwa ni mtoto mmoja wa mhamiaji wa hapo ambaye alikuwa raia wa Kenya na ndio ambaye Bi Wema alisema anajua kuongea kiswahili, lakini hata hivyo huyo mkenya alionekana kutokijua sana kwani alichanganya mara nyingi ne kingereza na kwa maelezo ya Ron mkenya huyo alikuwa ni mhalifu anaetafutwa na serikali ya Ugiriki.

“Master Ron , Madam Persephone anaitwa na Mfalme Pluto , anasema kuna sehemu wanapaswa kwenda”Aliongea yule mtoto kwa Kingereza.









SEHEMU YA 471.

Edna mara baada ya kupewa taarifa ya kuitwa na Roma hakukawia kwani hata hivyo gauni alishajaribisha hivyo angesubiri kuvaa kesho siku ya harusi.

“Vipi ulikuwa unasemaje” Aliongea Edna mara baada ya kumfikia Roma aliekuwa amesimama nje ya gari dogo kampuni ya Fyatt.

“Naelekea mlimani kwa ajili ya kumtembelea Seventeen”Aliongea Roma na kumfanya Edna moyo wake kwenda mbio.

“Unamaanisha nini kwenda kumtembelea?”

“Namaanisha naenda kuzuru kaburi lake , wakati anakufa sikuweza kupata mwili wake hivyo nilizika baadhi ya vitu vyake alivyokuwa akitumia na ni zaidi ya miaka miwili sijatembelea , nadhani ni muda muafaka kwangu kumpa salamu ya kwaheri na kuacha yaliopita yapite na kuanza maisha mapya”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushindwa kutoa jibu la haraka.

“Hakuna shida , unaweza kwenda lakini nina ombi moja”

“Ombi gani?”

“Nataka kwenda pia”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa kidogo lakini alishia kumfungulia mlango na kuingia na kisha wakaondoka.

Hewa ya mlima ilikuwa ya kuvutia lakini isiokuwa ya ubaridi sana , hata hivyo kipindi hicho kilikuwa ni cha joto , gari iliingia ndani ndani kwenye msitu na walikuja kuisimamisha chini ya kijimlima ambapo wasingeweza kuendelea kwenda juu kwa kuendesha, walishuka na kuanza kutembea .

“Huu ndio msitu ninaotumia kuwazika wanajeshi pamoja na watu wangu wa karibu , ni msitu wa heshima sana ndani ya hivi visiwa vyote na ukiona amezikwa hapa jua alikuwa na mchango mkubwa sana kwenye kundi …..”Aliongea Roma.

“Ni kama msitu wa mashujaa sio?”Aliuliza Edna.

“Upo sahiihi”Aliongea Roma huku akiendelea kumwelezea baadhi ya mambo mengine hususani watu waliokuwa wamezikwa ndani ya hilo eneo.

Edna alijikuta akikmbuka mara ya kwanza alivyokutana na Roma ,ijapokuwa alionekana kuwa mtu wa kawaida kati ya wanajamii lakini macho yake yalionyesha kitu kisichokuwa cha kawaida na huenda maisha yake ya nyumba ndio yalimvutia zaidi.

Waliendelea kutembea kimya kimya pasipo kuongeleshana , Edna yeye alikuwa akishangaa na Roma alikuwa akikumbuka mambo yaliopita.

“Ah!”

Edna aliteleza na kidogo tu aanguke kama isingekuwa Roma kumuwahi kumshika mkono.

“Kuwa makini nitakushikilia”Aliongea Roma huku akimshika Edna mkono lakini aliutoa kwake.

“Edna una tatizo gani , ninajaribu kukushikilia usije kudondoka”

“Usiniguse , nitakuwa makini lakini sitaki unishikilie wala kunivuta”Aliongea kwa kiburi na kumfanya Roma kushangaa , yeye mwenyewe ndio alietaka kuja lakini alionyesha kukasirika, lakini alijiambia hawezi kusitisha safari yake ya kwenda kumuona Seventeen.

Roma hakujua Seventeen yupo hai , alipotezea hata maneno ya wale watu waliokuwa wakimwambia kwamba yupo hai na wamekutana nao , alikuwa mgumu kuwaamini kutokana yeye mwenyewe alishuhudia kifo chake.

Upepo mkali uliendelea kuwapuliza , Edna na gauni lake lilipulizwa na kuwa kama fuko na nywele zake ndefu pia zilipeperushwa na upepo kiasi cha kupeleka mkono kila mara kuzitoa usoni.

Kijimlima kilikuwa kirefu na kuchongoka kwenda juu , lakini kutokana na kuchukua mazoezi alionyesha kuweza kuhimiri vizuri mwinuko huo na kutembea pasipo ya Roma kumuacha hatua .

Baada ya muda mfupi waliweza kufikia mwisho kabisa juu na kuweza kuona kaburi moja tu eneo hilo.

Kwa maelezo ya Roma ni kwamba kadiri kaburi linavyopelekwa juu zaidi ndio ilimaanisha mtu aliekufa alikuwa na cheo au muhimu zaidi.

Hivyo kwa Seventeen ni kama alikuwa na cheo kikubwa kuliko wote ndio maana alizikwa juu kileleni kabisa.

Kabuli lilikuwa kama ubao uliojengwa kwenda juu , lakini ukiwa umapakwa rangi nyeusi huku ukiwa na maelezo ya kirumi pamoja na namba 30 ilioandikwa pia kwa Kirumi.

“Hili ndio kaburi lake?”

“Ndio”Akijibu Roma na kutembeea mpaka kufikia mbele yake.

“Hio therathini inamaanisha jumla ya mimi na yeye, nilifahamika kwa jina la Thirteen tokea nilipojitambua kuwa mtu mzima na yeye aliitwa namba kumi na saba”

“Kwahio ukijumlisha inakuwa ni therathini ndio inawakilisha muungano wenu?”Aliongea Edna huku sauti yake ikiwa ya kitetemeshi lakini Roma alitingisha kichwa.

“Nikupishe , naamini una mambo mengi ya kutaka kumwambia”

“Haijalishi , unaweza pia kusikiliza kama utapenda”Aliongea Roma na kisha alishika ule ubao wa zenge na kuanza kupitisha mkono kama vile anashika mtu kutokana na upole aliokuwa akitumia.

“Imepita zaidi ya miaka miwili sasa tokea mara ya mwisho nilipokutembelea , unaendeleaje , umekuwa mpweke sana tokea niondoke, kwa ninavyokujua muda huu ungeshanniwekea kisu kwenye koo langu ukitaka kuniua kwa hasira za kukuacha mwenyewe kwa muda mrefu..”Aliongea Roma huku akicheka mwenyewe lakini hakukuwa na jibu hata moja

“Nilienda nchiniTanzania , uliniambia napaswa kuona nchi yangu inavyoonekana , nilifika na kuwa mbeba mizigo , niliishi nyumba ya kupanga , maisha hayakuwa mazuri sana lakini yalikuwa ya upekee , nilikutana na watu wengi ambao hawakuhitaji kuua ili kuweza kuishi kama ilivyokuwa falsafa yangu , Oh! tena nimesahau sasa, nimefanya kazi kwenye kampuni iliokuwa na warembo wengi , unaweza kunilaumu lakini ndio hivyo tabia haipotei haraka…..”Aliongea Roma Pumba zote alizojisikia kuongea huku kubwa akielezea maisha yake nchini Tanzania.

“Nimekuja na mke wangu nilieweza kumpata na kuishi nae kwa zaidi ya miezi sita sasa, niliamini ungependa kumuona ndio maana nikaja nae”Aliongea Roma mara baada ya kumwangalia.

“Nimekuwa mke wake lakini sitomfanya akusahau . nitamruhusu muda wowote kuweza kuja hapa na kukusalimia mara kwa mara , lakini hii ndio mara yangu ya mwisho kufika hapa , siku nyingine nitamsindikiza mpaka chini ya mlima na nitasubiri”Aliongea Edna na baada ya hapo Roma alitabasamu na kumwambia waondoke na Edna hakuongea chochote na kutangulia mbele

“Mpenzi!”Aliita Roma kwa nyuma lakini Edna hakuitikia zaidi kutembea lakini alijishtukia tu akiwa kwenye mikono ya Roma akiwa amebebwa juu juu.

Roma alianza kumzungusha kwa haraka mpaka Edna akajihisi kizungu zungu na kisha akamshusha chini huku akihema kwa shida na kabla hajalalamika alijishutikia tu midomo yake ikibusiwa .

“Aah.. midomo yako ina radha ya samaki .hebu niache”Aliongea Edna huku akiona aibu.

“Hehe My wife you are so cute , unapendeza zaidi ukiwa hivyo”

“Unaongea nini , mbona umebadilika haraka na kuwa na furaha wakati ulikuwa na huzuni kwa ajili ya mchumba wako”

“Kulikuwa na utofauti gani sasa?”

“Wewe unaonaje ulikuwa upo siriasi mno , halafu kama unanipenda kweli kwanini unaendelea kuwa na wanawake wengine , hunionei huruma mimi mkeo”

“Ninaweza kuwa siriasi pia na hata hivyo Seventeen sio taarifa yako ya kwanza na ni kweli na kuonea huruma”

“Kama ni hivyo kwanini…”

“Edna siwezi kuwaacha kwani ni kama kuwasaliti tu , Edna unaweza kuniita majina yote utakayo lakini kuhusu hili lazima hisia tuzuweke pembeni na kufikiria kimantiki, ninachojua kukutana kwetu sio kwa bahati mbaya na ndio maana leo hii tupo hapa kwa ajili ya harusi , hivyo tufurahie harusi yetu na baada ya hapo unaweza kunilaumu utakavyo na kunisema vibaya, ila usije ukataka talaka tu kutoka kwangu maana harusi za kila muda ni gharama”Aliongea Roma na kumfanya Edna kug’ata meno kwa hasira.

“Ndio maana hakuna hata mmoja alietaka kushiriki harusi yangu , naaini hawakutaka kukasirika kwasababu mimi ndio naolewa”

“Turudi nyumbani kwa Ron kwanza, utalala na Mama pamoja na Bi Wema na mimi nitaenda kukamilisha taratibu za kesho na baada ya hapo tutahamia kwenye nyumba ambayo ina chumba maalumu kwa ajili ya usiku baada ya ndoa”Aliongea Rom.

‘Chumba maalumu kwa ajili ya usiku baada ya ndoa””Alirudia Edna maneno ya Roma kwa mshangao.

“Acha kuwa mwanamke mjinga basi , laizma tulalae pamoja baada ya harusi kwenye chumba maalumu nilichokiandaa”

“Wewe ndio mjinga” Aliongea Edna kwa kiburi na kuanza kushuka haraka haraka na ndani ya muda mfupi waliweza kuingia kwenye gari na kuondoka.

Hatimae siku ya kwanza ndani ya visiwa vya watu ilifikia mwisho na giza kuingia.

*******

Mwanga wa jua ulitokeza kwenye mawingu na kufanya kisiwa chote kuwa angavu.

Kundi la ndege wa baharini wafahamikao kwa jina la Shakwe(sea gull) waliruka kimakundi makundi juu ya bahari iliokuwa ikifoka kutokana na wingi wa mawimbi asubihi hio.

Ki kawaida ni watu walioishi ndani ya hilo eneo asubuhi kama hio wangekuwa wakiota jua na wengine kwenda kwenye shughuli zao, lakini siku hio ilikuwa tofauti kwenye kiwanja kikubwa kilichokuwa kikipakana na msito kulia na bahari kushoto.

Uwanja ulipambwa na maua ya aina nyingi yenye kuvutia na kuonyesha mwonekano wa kupendeza ulioashiria sherehe.

Kati ya mapambo ni maua meupe yafahamikao kwa jina maarufu la kingereza la Madonna Lily yalipambwa kwenye njia iliokuwa ikielekea kwenye steji ya uwanja huo ambao ni kama ulikatwa katikati kwa namna viti vilivyopangwa , kulia na kushoto kulilingana na katikati ikaachwa nafasi ambayo ndio njia atakayopita bibi harusi na bwana harusi.

Steji ilikuwa imepambwa na kupendeza sana huku spika kubwa zikiwa zimefungwa pande zote za steji, kwa haraka haraka ungetoa mapambo ungeamini moja kwa moja kuna show ya msanii mkubwa inayotarajiwa kufanyika siku hio , kazi yote ya ujenzi ilifanyika usiku na mpaka asubuhi hio ilikuwa ikimalizikia.

Watu waishio hapo walikusanyika ndani ya eneo hilo huku wakionyesha shauku ya kuona kile ambacho kinakwenda kutokea siku hio lakini kwa muda huo walisaidia kazi ndogo ndogo za upambaji.

Kuna ambao walikuwa wamebeba vikapu vya maua, kuna waliokuwa wamebeba kreti za mvinyo na kuna wale waliokuwa wamebeba glasi huku wakiongea kwa furaha.

Katikati ya uwanja karibu na steji alikuwa amesimama mzungu mmoja aliekuwa ni wa kike alievalia gauni la kawaida la rangi ya pink , alikuwa ndio kiongozi kwani alionekana kuagiza watu wafanye hivi na vile kukamilisha zoezi ,alionekana alikuwa mjuzi pia wa lugha kwani kuna muda aliagiza kwa lugha hii na kuna muda aliagiza kwa lugha nyingine ili kuelewana na watu aliokuwa akiwaongoza , alikuwa mrembo haswa licha ya kwamba alivalia kikawaida.

Muda ule ule aliongezeka mwanadada mwingine mrembo , lakini aliekuwa ni mwafrika rangi ya chocolate na kusalimiana nae huku wakionyesha kucheka kwa furaha.

Mwanamke mzungu alikuwa ni Profesa Clark na mwanamke mwafrika alikuwa ni Ashley mdogo wake Roma na dada yake Denisi , ndio mgeni pekee aliefika kwenye sherehe hio upande wa baba yake.

“Peleka mbele hizi meza mpaka pale zisikaribiane sana maana itakuwa ngumu kwa watu kutembea katikati lakini pia zisikaribie hayo maua na kuyaharibu , leteni zaidi Pina Colada(Coctail), msilete tu pia mvinyo wa matunda wengine wanaweza wasipende”

“Unafanya vizuri Profesa ,sikudhani una ujuzi pia wa kupamba majukwaa”Aliongea Ashley.

“Ukiachana na kuwa Profesa mimi mia ni mtoto wa malkia hivyo mambo kama haya ni sehemu ya utamaduni ndani ya familia za kifalme” Aliongea huku akiachia tabasamu murua lililomfanya kuzidi kuwa mrembo.

Clark alikuwa ndio amepewa jukumu la kuongoza upambaji na mpangilio wa eneo zima , alikuwa ni mtoto wa malkia hivyo wengi waliamini angefanya vizurri , alikuwa pia na uwezo wa kuwatambua watu kwa makabila yao au nchi walizotoka ndio maana kuna muda alitumia lugha mbalimbali kuongea nao, ijapokuwa hakujua ligha nyingi lakini lugha kubwa duniani alikuwa akizijua.

Upande mwingine wakati wengine wakiendelea kupamba , kuna mwanamke mrembo lakini mtu mzima aliekuwa amekaa kwenye viti pasipo ya kujishugulisha , huku alionekana kuwa na sahani iliojaa vipande vya nyama na pembeni yake kulikuwa na glasi ya mvinyo , hakujali watu walikuwa wakihangaika ile yeye alijali tumbo lake.

“Catherine unaonaje ukienda kula ndani kule kuliko hapa tunapofanyia kazi”Aliongea Clark akijaribisha maiki kama zinafanya kazi vizuri , lakini maneno yake yalikuwa yakimlenga mama yake ambaye ndio mwanamke aliekuwa akiburudika na kula asubuhi hio.

“Clark unaonaje ukiniacha na umtafute Edward akusaidie, nimekaa hapa bila bughuza ya kumsumbua mtu yoyote” Aliongea huku akionyesha kulalamika.

“Inashangaza pia unavyohangaika kupamba eneo la harusi ya mwanaume unaempenda akimuoa mwanamke mwingine” Aliongea na kumfanya Clark maneno hayo kumgusa, alijua mama yake alikuwa akimwonea huruma.

Aliweka maiki chini na kisha akamsogelea mama yake na kumuinamia karibu.

“Mwanaume unayemzungumzia ni Roma, ni mtu ambaye ametusaidia kuwa na kila kitu tulichonacho leo hii , aliniomba nimsaidie kupamba hili eneo na sikuwa na nguvu ya kumkatalia”Aliongea na Catherine alisimama na kumbusu shavunni.

“Baby je unataka mama yako nikamtege wakati akielekea nyumbani kwa ajili ya kulala na bibi harusi?”Aliongea na kumfanya Clark akose usemi.

“Nenda kabadili haya mavazi angalau uonekane mrembo , Edna ni mrembo hivyo sidhani kama utamzidi”

“Wewe ni mtoto wangu na kama unalitaka nyonyo sema, maana ulivyokuwa mdogo ulikuwa unanyonya kidogo sana na umeyaacha maziwa ndio maana sasa hivi nateseka na haya manyonyo huenda ningekuwa mrembo kuliko wanawake wote dunia hii” Aliongea bila aibu

“Kimya, naomba uondoke” Aliongea kwa amri na kumfanya mama yake kuondoka huku akicheka , walionekana walikuwa wakitaniana sana na hata hivyo walitofautiana umri kiasi kidogo sana hivyo ilikuwa rahisi kuwa marafiki licha ya kuwa mama na mwana.

Baada ya maandalizi ya ukumbi kumalizika Ron aliweza kufika na kutangaza kwamba harusi ingeanza muda si mrefu ujao .

Kwasababu ndoa ilikuwa ikimuhusu Roma, mwanaume ambaye aliletea uhuru visiwa hivyo kutoka serikali ya Uingereza lakini pia kuvilinda na zidi ya uvamizi wa serikali nyingine , basi kwa heshima kubwa watu karibia wote walihudhuria kwenye harusi hio na ndio maana harusi ilifanyikia kwenye uwanja..

Mwanzo kabisa wa viti vya mbele waliketi wale watu wazito wazito , walianza kuweka ndugu wa Roma ambaye alikuwa ni Ashley na Blandina na kisha wakafuatia marafiki zake ambaye aikuwa ni Makedon na Sauroni na kisha Catherine na Clark wote walikaa mstari wa mbele.

Nyuma yao walikaa viongozi wa kundi la Kininjua la New Zero pamoja na makamanda wa jeshi la Sea Eagles , lakini pia Edward wa Rothchild alikaa mstari wa nyuma pamoja na mataiiri mbalimbali na wawakilishi kutoka mataifa rafiki na Roma.

Eneo hili halikuhitajika ulinzi wa mabodigadi na ndio ilikuwa sheria ambazo hazikumbagua mtu kutokana na cheo, hivyo hata watu waliokuja walifika peke yao huku wakihakikishiwa ulinzi wa kutosha kwenye hilo eneo.

Ron alipanda juu ya jukwaa na kisha akashikilia maiki , alikuwa ni EMCEE tokea asubuhi lakini muda huo alitaka kutoa tangazo huku kadamnasi ya watu walimwangalia.

“Now focus everyone , Your Majesty Pluto has requested to emcee his own wedding..”Aliongea akimaanisha kwamba Roma anataka kuwa Emcee wa harusi yake mwenyewe, baada ya kusema hivyo alipiga makofi na kisha akatoka juu ya jukwaa.

Watu walichanganyikiwa, inakuwaje mtu kuwa Emcee wa harusi yake yake mwenyewe , lakini pia Roma aliezungumziwa hakuwa akionekana na kila mgeni alikuwa ameshaketi , lakini ghafla watu wote waliangalia juu.

Roma alikuwa akishuka kutoka angani huku akiwa ameachia tabasamu mwanana ,alikuwa amevaa suti nyeusi na tai nyeupe ilionakishiwa na rangi nyekundu , alikuwa akishuka kutoka angani lakini hakutumia parashuti.

Alikuwa pia ameshikilia kamba ambayo imefungwa kwenye puto kubwa lakupulizwa na hewa maalumu (hellium ballon) ambalo lilikuwa limetengenezwa kwa shepu ya moyo likiwa la rangi nyekundu, lakini pia lilikuwa na mikanda(ribbon) yenye maandishi makubwa ya neno LOVE.

Roma kama ilivyokuwa tabia yake ya kujiamini , alionyesha kutokuwa na hofu ya aina yoyote mpaka anatua kwenye steji na kuanza kupungia watu mikono , lakini hadhira ilikuwa kwenye mshangao maana ni tukio ambalo sio la kawaida kwenye sherehe licha ya kwamba wengi wao walikuwa wakifahamu kuhusu uwezo wake usiokuwa wa kawaida ndio maana swala la kupaa halikuwachanganya sana.

“Clark mimi mama yako nashukuru sio wewe unaolewa na huyu mwanaume ambaye amekaa kivituko na kutokuwa wa kawaida..”Aliongea Malkia Catherine

“Sijaona .. sijaona…” Blandina aliekuwa kwenye mshituko haya yeye ni moja wapo wasiotegemea kuona tukio la Roma kushuka kutoka mawinguni kama malaika.

Roma alivuta maiki na kisha akasafisha koo kidogo mara baada ya kuachia lile Baluni.

“Kwanza kabisa nataka niwashukuru kila mmoja wenu kwa kuja , naona kila mmoja amefurahishwa na staili yangu ya kipekee niliofika nayo kwenye jukwaa ……”Aliongea na kufanya eneo lote kuwa kimya.
 
SEHEMU YA 472.

“Mnaweza pia kushangaa inawezekanaje bwana harusi akawa Emcee wa harusi yake mwenyewe, ukweli hata mimi mwenyewe sijui. kikawaida Emcee kazi yake ni kuongoza mtiririko wa matukio ya sherehe, lakini hio si inaamaanisha natakiwa kumsikiliza mtu mwingine, sio kwamba sipendi lakini hakuna mtu ambaye nimeona anafaa kuingoza hivyo nitaongoza mwenyewe”.

Ashley alitakiwa kuongoza kama Emcee, lakini alikosa kujiamini kwani hakuwahi kufanya hivyo na ndio maana Roma hakuona mtu mwingine anfaa kuongoza harusi yake, hivyo akajiambia atakuwa Emcee.

“Madam His Pluto is hilarious..”Aliongea Ron

“Which part is hilarious?” Alijibu Blandina na kumfanya Ron kucheka na wote waliendelea kumwangalia Roma.

“Kuna jambo lingine pia, nadhani mmegundua hapa hakuna mchungaji wala Padri wa kufungisha ndoa au kuwa kama shihidi?”Aliongea Roma na kufanya hadhira kushindwa kuelewa ni kweli hakukuwa na kasisi au mtu wa dini wa kusimamia hio ndoa na walianza kujiuliza maswali.

“Sikuona kama nahitaji mtu wa kusimamia ndoa yangu , huwa nilijisikia vibaya kila niliposhiriki kwenye ndoa za watu wengine , mtanzamo wangu mimi ndoa ni baina ya bibi harudi na bwana harusi , kwanini iongozwe na mtu mwingine , siwezi kuingilia ndoa za wengine zinazofanyika lakini ya kwangu nitaifanya kwa staili yangu , hivyo hapa hakuna mchungaji wala shahidi , unaweza kuniita Fafher Roma au Paster Roma kwani najifungisha ndoa mwenyewe“Aliongea Roma huku akijinyooshea kidole kwamba atakuwa yeye ndio mchungaji au shekhe wa kufunga ndoa yake mwenyewe

Watu walijikuwa wakicheka mno, watu waliokuwa mbele walijikuta wakipiga makofi bila haya ya kujielewa huku wakicheka .

“Alright as the groom and witness and emcee, please welcome the bride”

“Vizuri kama bibi harusi , shahidi na Emcee tafadhari karibu sana bibi harusi”Aliongea Roma akimkaribisha sasa bibi harusi na muda huo huo mara baada tu ya kumaliza kuongea spika zote zilianza kutoa sauti ya wimbo maalumu wa kumsindikiza bibi harusi jukwaani.

Song by Ryani Darling

You’re my always.

You’re my forever.

You’e my sunshine .

You’re my best times.

You’re my anomaly.

And I would choose you in a hundred lifetimes, I would choose you in a hundred worlds , I ‘d find you…….

I would say ‘I do’ for the rest of my life with all that I have ……”



Ni wimbo wa msanii wa Ryani Darling ulioanza kusikika , wanawake waliokuwa ndani ya hilo eneo walishindwa kujizuia na kuanza kuimba wenyewe kwa hisia huku wakiwa wamesimama wakipiga makofi.

Haikueleweka kundi la ndege mfano wa njiwa wametokea wapi, lakini waliamka kwa kupeperuka kwenda angani huku mziki bado ukidunda.

Muda huo huo watu wote walijikuta wakishindwa kupumua kwa mwonekano wa bibi harusi na gauni lake , lilikuwa ni gauni ambalo hakuna ambae alitarajia kutokana na upekee wake , lakini kubwa zaidi ni kuhusu bibi harusi mwenyewe.

Alionekana kama ua la rangi ya light blue la mmea maarufu wa lotus ambalo linaanza kuchanua.

Gauni lake refu liliburuzika kwa nyuma huku kila pande ikiwa imeshonewa na mfano wa maua ya waridi lakini rangi nyeupe, unyororo wa kitambaa cheupe kilichotumika kilichanganya vizuri na nakshi za maua

Kulikuwa na mkanda flani wa kitambaa cha hariri umefungwa kiunongi na kuning’inia huku ukishonewa pia na maua flani ya rangi ya pink, gauni lilimkaa vyema mwilini na kumfanya umbo la mwili wake kuonekana vyema

Staili ya nywele pia licha ya kwamba zilifungwa kawaida, lakini ni kama zilifanyiwa hivyo kuendana na gauni lenyewe.

Uzuri wake ulikuwa ni wa kukosesha pumzi na kufanya wengi wao kuvutiwa sana lakini pia kuusifia uumbaji.

Edna alikuwa akijitahidi kutembea, mapigo ya moyo wake hayakuwa sawa , kuna muda alitamani kulia kutokana na kuangaliwa na macho ya watu wengi.

Ukwei alitamani harusi iishe mapema, wakati Roma alipokuwa akiongea pumba ilimfanya hata kukasirika maana alisimama muda mrefu kwenye eneo a kuingia kwenye uwanja kutembea kuelekea stejini.,

Lakini baada ya kuingia kwenye njia ya kuelekea kwenye steji, akili zake alizihamishia kwenye kutembea.

Zaidi ya macho ya watu elfu tatu yalikuwa yakimwangalia na alijihisi vinyweleo vikimsimama kutoka na wingi wao kwani ni kama hakutegemea wangekuwa wengi kiasi hicho na mbaya zaidi wote walikuwa wazungu.

Shukrani kwa Bi Wema alikuwa pembenni yake , Bi Wema alijihisi kama mwanamke aliekuza , hakujihisi aibu bali alijihisi kuwa mwenye mafanikio kushuhudia Edna akiolewa , nafasi hio ilitakiwa iwe ya Raheli mama yake Edna lakini imekuja kuwa ya kwake.

Kila hatua ilikuwa na hisia zake, huku akimwangalia mwanaume aliekuwa mbele yake huku akihisi yupo mbali sana mpaka kumfikia.

Edna alikuwa akitembea katikati ya uwanja , kulia kwake kulikuwa na watu na kushoto kwake kulikuwa na watu ambao walikuwa wakimwangalia..

Mwanaume aliekuwa mbele yake akimsubiria wlaishaishi zaidi ya miezi nane sasa pamoha , lakini siku hio ni kama alikuwa mgeni kwake na ndio kwanza baada ya hapo wanakwenda kuishi pamoja.

Matukio mbalimbali tokea anaanza kukutana na Roma yalianza kuibuka kwenye kichwa chake, alikumbuka wakati alipozimia ndani ya hoteli na kujishutikia akwia kwenye chumba akiwa juu ya godoro uchi akiwa amepteza usichana wake, alikumbuka alivyopendekeza kufunga ndoa kwa mkataba na mwanaume huyo , alikumbuka wakati waliposaini makaratasi ya ndoa na Roma kuhamia nyumbani kwake.

Licha ya mziki wa kuvutia uliosikika , makofi na shangwe zilizokuwa zikirindima , lakini pia upepo wa baharini uliokuwa ukipuliza kwa kasi hakuna chochote alichoweza kukisikia , alikuwa kwenye mawazo na alijitahidi sana kuwaza yale ambayo yatamfanya awe ni mwenye furaha na ndio alivyojiambia na aliamini muda huo bibi yake na mama yake wanamwangalia huko walipo na kufurahi kwa ajili yake.

“Natoa onyo kwa wanaume wote msikodolee sana macho mke wangu , mnaruhusiwa kumwangalia kwa sekunde kumi tu na kisha macho yote mbele , ukizidisha utajikuta upo kule baharini unaogelea”Aliongea Roma kwa onyo na kufanya wanaume wote kutoka kwenye mshituko na kuangalia mbele maana kauli yake ilikuwa ya kibabe na siku zote waliamini anachoongea anamaanisha.

“Madam don’t you think they are very lovey d-dovey?”Aliongea Ron

“Again wich part?”Alijibu Blandina na kumfanya Ron kucheka.

“Miss usikasirike , unajua mwenyewe Roma ndio alivyo na anafanya yote hayo kwasababu anakupenda”Aliongea Bi Wema mara baada ya kumuona Edna kakasirika kutokana na ubabe Roma hata sehemu kama hio alihisi anatia aibu.

“Bi Wema nataka kuondoka sasa hivi” Aliongea Bi Wema.

“Huwezi kufanya hivyo, si ulikuwa ukitarajia sana hii siku, amekuahidi zawadi katikati ya harusi hutaki kuiona” Aliongea Bi Wema kwa kumfarji na kumfanya Edna kuongeza mwendo na hatimae kuweza kuifikia stejini na Bi Wema kumkabidhi kwa Roma.

Kadamnasi ilipiga makofi ya pongezi mara baada ya bibi harusi kupokelewa na bwana harusi.

Roma alimkonyeza Edna na kumfanya kuona aibu huku akizidi kuwa mwekundu , kumbuka Roma alikuwa Emcee mwenyewe na pia alikuwa akijita Padri kwa muda huo.

“Now it’s time for us to exchange our token of love , I’ve spent a lot fo effort to prepare mine so I’ll allow the cameras to show off my gift , Take close look at the screens around you”

“Sasa hatimae ni muda wa kubadilishana ishara ya upendo, nilitumia juhudi kubwa kuandaa ya kwangu na nitaruhhusu Camera kuonyesha zawadi yangu , angalia kwa ukaribu skrini(Tv) zinazowazunguka”

Maneno yale yaliamsha hisia za wengi kutaka kushuhudia ni zawadi gani ameandaa , hata Edna mwenyewe aliangalia kwa shauku.

Roma alimwangalia mke wake na kujikuta akitamani kumvaa na kumbusu palepale kutokana na alivyokuwa mrembo , lakini alijiambia kwenye nafsi yake ‘Roma bado kitambo kidogo tu unakwenda kupata haki ya tendo la ndoa usiku kucha’.

Roma alimwachia Edna huku akimpa tabasamu na kisha akasimama katikati ya steji na palepale alikunjua kidole cha mwisho na kukionyesha hewani kuelekea upande uliokuwa na msitu na palepale watu waligeuka kuangalia na waliweza kuona kitu kama kidoti cheusi kikiwasogelea kwa kasi na ilipokaribia waliweza kugundua ni ndege isiokuwa na rubani mfano wa Drone chini yake ilikuwa imefungwa na vitu kama kikapu kilichoning’inia.

“Sijawahi kuona harusi ya namna hii..”Aliongea Blandina.

“Edna alikuwa akitegemea sana hio zawadi, naamini ataipenda” Aliongea Bi Wema akiangalia juu angani na yeye.

“Hata mimi naamini hivyo”

“Clark wewe ndio ulietengeneza kile kindege si ndio? , kutokana na kutembea kwenye mstari mnyoofu kutoka umbali mrefu siamini kama mtu yoyote anaweza kuitengeneza”Aliongea Catherine.

“Haikuwa hata kitu kigunu kutengeneza, ni kwamba kumsaidia ilikuwa kipaumbele changu”Alijibu Clark

“Seriously!, wewe sio bibi harusi lakini umejichoosha na maandalizi ya shrehe kama yako vile”Aliongea lakini Clark alijifanyisha hajamsikia na Catherine aliacha kuongea na kuangalia mbele.

Muda ule ule mara baada ya kindege kukaribia usawa wa steji , Roma alichukua rimoti kubonyeza na kamba ilishusha kile kikapu mpaka kikatua kwenye steji na Roma aliweza kutoa boksi la mbao dogo lililonakshiwa na kupendeza na kisha akampatia Edna.

Edna na yaye alipokea kimashaka mashaka huku akiwa na shauku pia ya kutaka kujua ni zawadi gani ambayo Roma alikuwa amemchagulia mpaka kuiandaa kwa muda mrefu..

Watu na wao walijawa na shauku huku wakiangalia kile kinachotokea, waliweza kuona kwa ukaribu kwa kutumia zile skrini kwanni ziliwamulika vizuri Edna na Roma waliosimama stejini,

Edna mara baada ya kufungua ndani alijikuta akipigwa na butwaa kwa kile alichokiona, hakuamini Zawadi ambayo Roma amemuandalia ni kijikeki , vijikeki ambavyo alikuwa akipendelea kula wakati alipokuwa mdogo na hata alipokuwa mkubwa pia alikuwa akipenda kununua na kula akiwa ofisini.

“Uliniambia unaniandalia zawadi , unamaanisha ni hii keki?”

“Niliitengeneza hio keki jana usiku, ndio kitu pekee ulichopenda sana ulivyokuwa mtoto, hivyo nikaona nikutengenezee kama zawadi” Aliongea Roma.,.

Edna alijikuta likimshuka, hakuamini hio ndio zawadi ambayo ameahidiwa alionyesha kutoipenda kabisa.

Wageni na wao walijikuta wakiangalia kuchanganyikiwa pasipo kuelewa nini kinaendelea.

Bi Wema na Blandina walikuwa wakijitahidi kujituliza kwani wenyewe hawakuelewa nini kinaendelea na kujiuliza kwanini Roma amletee Edna Kijikeki.

“Inawezekana kuwa zawadi nzuri kwangu kwani ninaweza kununua zawadi yoyote kwani nina pesa hata hivyo keki hii ndio kitu ambacho ninakipenda tokea nikiwa mtoto , hivyo naizingatia kama zwadi nzuri pia kwangu”Aliongea Edna lakini sauti yake ilionyesha kabisa hajaridhika. Walichokuwa wakifanya stejini ni kama walikuwa wakiigiza.

“Ndio unavyowaza hivyo , unafikiri hii inakutosha?”Aliuliza Roma

“Umeniangusha sana kunipa zawadi hii , lakini naweza kusema leo ni zawadi nzuri ambayo sitosahau kwani nimepewa kwenye harusi yangu”Aliongea huku machozi yakianza kumtoka , alishindwa kujizuia kuwa na hasira mbele ya watu na Roma.

“Kwahio unalia nini mpenzi?”Aliongea Roma huku akimshika shavu na kutabasamu.

Watu wenyewe walikuwa kwenye hali ambazo hazilezeki , ni kama waliona harusi inaharibika.

“Wewe ndio uliyapandisha matarajio yangu , ulitakiwa kuniambia kama zawadi ulioandaa ni hivi vikeki , kwanini umechukua muda mrefu , tungeifanya harusi hata kule kule nyumbani pasipo ya kuja huku”Aliongea Edna ila sauti ilisikika kwao tu kwani maiki ameizima.

Minong’ono nayo ilianza kuibuka katikati ya watu kwa kuona bibi harusi na bwana harusi wanarumbana.

“Umekasirika?”

“Ndio nimekasirika”

“Basi naomba niendelee na kutoa zawadi” Aliongea Roma.

“Zawadi gani tena?”

“Zawadi ya keki ulioshikilia ni kasehemu tu kati ya zawadi nilioandaa , nilikuwa nakupa kionjo tu na sasa nakuonyesha nini maana ya zawadi , imenitia wasiwasi kukasirika kisa ya kionjo tu”Aliongea Roma kiutani na kumfanya Edna atamani kumfinya

“Unependa sana kunitega si ndio hata mbele ya watu?” Aliongea Edna huku awamu hii akiona aibu

“Sithubutu nilitaka kukuona tu utakavyo onekana ukiona vijikeki ulibvyo kuwa ukipenda , okey sasa ni muda wa kuendelea na zawadi niliopanga”

“Achana nayo kama itakuwa ni kindege kingine ”Alionea Edna.

“Naahidi haiwezi kuwa hivyo tena lakini naomba upokee hii zawadi kwa kuweka viganja vya mikono yako kuelekea juu”Aliongea Roma akimwashiria Edna aweke viganja vya mikono yake kuelekea juu kama mtu ambaye alikuwa akikinga maji ya mvua.

Edna hakujua ni igizo gani Roma anataka kufanya lakini alifanya kama alivyoambiwa .

“Kama hivi?” Aliuliza na Roma alitingisha kichwa.

Watu pia walikuwa wamechangayikiwa maana wanashindwa kuelewa kile kinachotokea ni Ron na Sauroni ambayo walikuwa wakitabasamu tu na kumfanya Edward awaangalie na kisha akaigizia kutabasamu na yeye.

Kila mmoja macho yalikuwa kwenye skrini kuangalia mikono ya Edna maana steji ilikuwa mbali na macho yao.

Dakika hio hio kila mmoja alijikuta akitoa macho ya mshangao na kuziba midomo kwa wale wanawake walioshindwa kujizuia.

Ukisikia maana halisi ya neno ‘nipeni maua yangu’ kutoka kwa msanii Roma mkatoliki basi ndio kilichoanza kutokea.









SEHEMU YA 473.

Yalikuwa ni maua aina ya waridi, lakini yote yakiwa ni ya rangi nyekundu tupu , ni sahihi kusema ni mvua ya maua ya waridi ya rangi nyekundu.

Kiganja chake cha mkono kilipojaa maua ndio alijua nini maana Roma alichokuwa akimaanisha.

Yalikuwa ni maua fresh kabisa ya waridi ambayo yalikuwa na ubaridi mno kama yametoka kwenye friji.

Edna alijikuta akiinua macho yake angani na kuangalia na hapo ndipo alipojikuta akishindwa kuzuia mshangao na tabasamu kutokana na namna yalivyokuwa yakishuka , hayakuonekana yanatokea wapi , lakini yalitoka juu kama mvua.

Karibia anga lote la kisiwa lilijaa vipande vya maua ya waridi(rose petal), eneo lote lilinukia maua hayo na yalikuwa mangi kiasi kwamba ni kama Mungu amaeamua kushusha mvua ya maua tu kwa binadamu wake.

Wageni wenyewe kila mmoja alikuwa kwenye mshituko kwani mandhari ya anga ilibadilika kabisa na kuwa ni yenye kuvutia mno na kilichovutia zaidi chanzo cha maua hakikionekana kutokana na wingu lililotanda juu ghafla.

Blandina, Bi Wema na Ashley walishindwa kujizuia na kujikuta machozi yakianza kuwatoka, kwani surprise hio ilikuwa ni ya aina yake na hakuna ambaye alitarajia.

Waliosimulia anasema anga liligubikwa na harufu ya maua lakini pia liligubikwa na harufu ya upendo.

Akiwa bado anaangalia anga kwa kuinua shingo yake alijikuta mikono imara ikimvuta kwake kwa na kumgeuza na kisha kumwangalia usoni.

“Mpenzi nadhani umependa zawadi yangu, niliandaa kwa zaidi ya miezi kadhaa mpaka kufanikiwa kutengeneza mvua ya maua” Aliongea Roma na Edna alikosa usemi na machozi yalianza kumtoka palepale, ilionyesha ameguswa.

Wahenga wanasema zawadi ni zawadi, lakini zawadi inayodumu kwenye kumbukumbu za wengi ni ile isio ya kutarajiwa hivyo Edna alikuwa sehemu ya binadamu waliokuwa wakizungumzia na wahenga, mwingine anaweza kutafsiri kama uharibifu lakini kikubwa zaidi ni ile maana iliokusudiwa na ndio maana watu wengi walishindwa kujizuia.

Edna alimwangalia Roma kwa dakika kadhaa na kujiuliza ni zawadi gani anapaswa kumpa mwanaume aliekuwa mbele yake na palepale alitabasamu na kumpelekea mdomo Roma na walijikuta wakidendeka hadharani, kwa Blandina na Bi Wema ilionyesha kama sio utamaduni lakini kwa wazungu lilikuwa tukio la pekee.

Kiss wakati wa mvua ya maua , huenda ndio kichwa cha habari kwa kile kilichokuwa kikifanyika.

Watu walisimama na kuanza kupiga makofi kwa shangwe, Catherine na Clark wenyewe walishangazwa lakini mioyo yao ni kama haikujisikia vizuri , wote walitamani ile nafasi.

“Umewezeje kufanikisha hili, umepata wapi maua yote haya?”Edna alijikuta akiuliza huku akisahau kabisa kuna watu waliokuwa wakimwangalia.

“Nimetumia jet kusambaza angani na kwasababu ya upepo tulianza kuyaloanisha na kioevu maalumu ili yaweze kushuka kwampangiio maalumu kama mvua , nilikusanya maua yote karibia miezi minne”

“Miezi minne na hayakuharibika?”

“Ilikuwa kazi ya Clark hio, alitengeneza maji maalumu ambayo yametumika kuyahifadhi na Ron ndio aliekuwa akiyakusanya pande zote za dunia , yatasabambazwa kwa awamu kumi na sita ambazo ni kila baada ya nusu saa , hivyo kwa makadirio mvua ya maua itadumu kwa zaidi ya masaa kumi na tatu”

“Masaa kumi na tatu umesema?”

“Ndio mpenzi, ila kama hutaki ninaweza kuwaambia waache”

“Hapana, ni kwamba si yatakuwa mengi, umefanikishaje kukusanya yote hayo”

“Inawezekana kabisa, nimetoa dora bilioni moja ya ajili ya kuandaa , hivyo ni swala linalowezekana na Ron alifanya kazi yote na ndio maana mara ya mwisho Omari alisema maua ya waridi yalipanda bei sana na mengi yalikuwa yakisafirishwa nje ya nchi , ilikuwa ni kazi yangu”Aliongea Roma huku akimkonyeza.

Edna alishangaa na kujiambia jambo hilo lisingewezekana tu kwasaabu ya mtu kuwa na pesa hata matajiri wakubwa wasingeweza kufanya hivyo kwani ili kuyasafirisha ni mpaka serikali zikubali.Baada ya muda Roma alisogelea tena maiki na kutoa tangazo .

“Kila mmoja sasa anaweza kufurahia chakula kilichoandaliwa kwani nimehitimisha kwa kumkiss mke wangu, kuleni mshibe na vyoo mnaweza kutumia huo msitu, kuhusu vinywaji tumeandaa mvinyo wa matunda na Pina Colada’s kwa ajili ya kuhamashisha wazalishaji wetu wa ndani, angalizo naomba msinywe sana vilevi maana sitohusika mtu yoyote akipata mimba siku ya leo”Aliongea Roma na kufanya watu wacheke mno.

Edna alishindwa kuvumilia na kumpa ishara aache kuongea pumba mara moja na baada ya hapo watu walianza kushereheka sasa , sherehe ni vyakula asikudanganye mtu eti ni mamiziki na udambwi udambwi mwingine.

Siku nzima ilijawa na vifijo na furaha , watu waligonga cheers , ilikuwa ni harusi ya kitaifa hivyo maandalizi yalikuwa makubwa na hata chakula kilipikwa kwa malengo ya watu wengi.

Muda wa jioni ulivyokaribia muda wa zawadi uliwadia na watu walitoa zawadi nyingi kwa wale walioandaa na zote zilipokelewa na wawalishi kwa ajili ya Edna.

Sherehe haikuwa na mwisho, hivyo baada ya watu kulewa sana na kusinzia ndio ukawa mwisho wa sherehe na kila mmoja aliondoka kuelekea nyumbani na wale wageni kwenda mahotelini.

Siku hio ndio Edna alioweza kukaa meza moja na Malkia Catherine na aliweza kumkumbuka mara baada ya kumwangalia kwa karibu , alikumbuka ndio mwanamke alietoka kwenye chumba cha Roma siku ile kule ufaransa ndani ya hoteli ya Sofitel.

Baada ya kuhitimisha Bi Wema, Ashley na Blandina walirudi nyumbani kwa Ron huku Roma na Edna walipandishwa kwenye gari kama utamaduni wa kizungu na kurusha maua angani na baada ya mmoja ya wahudhuriaji kulidaka wote walishangilia wakimaanisha ndio ambaye anafuatia na kisha wakaondoka kwenda kwenye nyumba waliopangiwa kulala usiku huo huku watu wakiwapungia mikono ya kwaheri na maisha mema.

Roma aliendesha gari aina ya Dune Buggy kuelekea upande mwingine kabisa kulia mwa msitu kwenye barabara ya rami, ilikuwa na kigiza na upepo wa baharini uliwapiliza kutokana na gari alilotumia kutokuwa na bodi zaidi ya kioo cha mbele tu.

Kila kitu kilionekana kuwa amani kadri walivyokuwa wakisonga mbele , ilikuwa raha kuendesha gari huku ukiangalia nyota angani na Edna ndio alichokua akifanya , aliangalia nyota wa angani huku akitafakari mambo mengi yaliotokea siku hio.

Dakika chache mbele waliweza kufika chini ya kilima kilichogubikwa na miti mingi ya mipine , lakini iliopandwa kwa mpangilio mzuri mno , lakini chini yake pia kulikuwa kusafi na kuwa na nyasi kama zile za viwanja vya mpira mbele yao kulikuwa na geti kubwa ambalo lilifunguliwa bila ya Roma kupiga honi, Edna alijikuta akipigwa na butwaa mara baada ya kuona nyumba anayokwenda kulala ni Ngome , haikuwa imejengwa kama ngome bali ilikuwa ni ngome halisi tena ilionyesha haikujengwa hivi karibuni bali miaka mingi iliopita.

Alitarajia kwamba nyumba ambayo wangetumia katika usiku wao wa ndoa ingekuwa ya kipekee lakini hakutegemea ingekuwa ni ngome., ilikuwa kubwa mno huku ikiwa imependeza sana kutokana na kupanda kwa kijimlima juu yake , lakini jambo la kuvutia zaidi ilikuwa imezibiwa na maua maua na miti mirefu , ilikuwa na minara(Towers) mitatu moja ikiwa imeenda hewani juu zaidi , yote imejengwa kwa staili ya zamani yaani Gothic style na kuchanganywa na mtindo wa Baroque staili.

“Mpenzi hii nyumba kama ni kule Tanzania ungeuza zaidi ya mabidlioni ya pesa”

“Hii sio nyumba bali ni ngome kama zile wanazoishi malkia wa Uingereza haiziki hata utake kufanya hivyo”Aliongea Edna huku akizungusha shingo kulia na kushoto.

“Upo sahihi hii ilijengwa kama ‘Palace’ kwa ajili ya familia ya kifamle kuishi na aliwahi kuishi mtoto wa mfalme , kipindi Uingereza ilivyotawala hili eneo , baada ya vita ya pili ya dunia iliharibiwa ule upande wa kulia na ilijengwa baadae upya na ilipokuja kuwa chini yangu haikuwa nzuri kimwonekano wa ndani hivyo nikaanza kuitengeneza upya , mwishowe nilikata tamaa kwani nilikuja huku mara moja moja , lakini Ron alisisitiza aendelee na projekti ya kuitengeneza upya mwonekano wa ndani ili yawe makazi yangu rasmi kila ninapotembelea huku”Aliongea Roma.

“Mbona unaongea kwa huzuni?” Aliuliza Edna huku akiangalia hizo ngazi za kupandisha mpaka juu na kisha kumgeukia Roma.

“Hii gauni ni refu , litanipa shida kupandisha mpaka kule”Aliongea Edna kwani bado alikuwa amevalia gauni la harusi.

“Nitakubeba mpaka ndani lakini mimi sio punda” Alitania Roma na kumfanya Edna kucheka.

“Unaongea kama mtoto “Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu na kisha kumnyakua na kupandisha nae kwa spidi na ndani ya dakika chache tu waliweza kufika nje ya mlango na alimshusha, Roma aliweka jicho sehemu maalumu(Iris scanning system na kisha akatumia kidole pia kuingiza finger print na hatimae mlango ulifunguka.

Edna aligeuka nyuma kuangalia eneo la nje na kuona kwa juu mazingira yalikuwa yakipendeza kuliko walivyokuwa chini licha ya kwamba taa zilimulika kwa mwanga haififu , bustani zilizopandwa kwa mpangilio pamoja na maua yaliokuwa kam fensi yalipendezesha mno.

“Ni mimi pekee na Ron ndio tunao uwezo wa kufungua huu mlango kwa kutumia macho”Aliongea

Edna alishangaa maana ni mara yake ya kwanza kuona mtu akifungua mlango kwa jicho na Roma alitaka pia Edna kuweza kufungua mlango huo kwa kutumia jicho na finger print hivyo alimsajili palepale kama mmiliki wa ngome.

“Kwasasa umekuwa mtu wa tatu ambaye unao uwezo wa kufungua huu mlango” Aliongea Roma na mpango palepale ulifunguka taratibu wenyewe na muda ule ule jengo lote liliwansha taa zote za eneo la nje na ndani na kumfanya Edna kushangaa huku akigeuka na sasa kuna mandhari ya nje hususani taa zilizotengenezwa kwenye bustani za maua.

Ni kama vile lilikuwa imelala na sasa limeamka kutoka usingizini na sasa Edna.

Roma hakutaka kumpa nafasi Edna ya kushangaa bali alimshika kiuno na kumwingiza ndani.

Eneo la ndani lilikuwa safi mno ni kama muda mchache tu lilifanyiwa usafi , taa za rangi ya njano ziliendana sawia na mtindo wa ubunifu wa upambaji wa eneo lote , mwonekano wa nje ulikuwa wa tofauti sana na wa ndani.

Eneo la sebuleni lilikua kubwa kama vile kiwanja cha basketi ball , madirisha yalikuwa na vioo flani vilivyotengenezwa kwa ajili ya kuingiza mwanga wa aina ya kipekee wakati wa mchana kupendezesha eneo lote , madirisha yote jengo liliangalilina na bahari upande wa kulia, Ceiling board ilikuwa ni ya kipekee huku ikiwa na taa zilizotengenezwa na kioo pamoja na madini ya dhahabu na kufanya kuvutia macho kuangalia , eneo hilo la sebuleni lilikaa kama duara huku likiwa limezungukwa na ngazi ambazo zinapandisha juu na kila kona ya sebule kulikuwa na vyumba vilivokuwa vimejipanga na milingo yake ilikuwa ni ya uhunzi wa aina yake.

Edna alijjikuta akizungusha macho kulia na kushoto kwake, sio sofa sio kapeti na sio meza sio vifaa vya umeme kila kitu kilitengenezwa ili kuleta radha sawia ya ubunifu , ilikuwa ni sahihi kwake kusema alikuwa ndani ya jumba la kifalme.

“Umesema kuna watu wawili tu wenye uwezo wa kufungua humu ndani?”

“Ndio, kwanini umeuliza hivyo?”

"Kuna vyumba vingi sana , itakuwa hasara kama hakuna wanaotumia " Aliongea Edna.

"Haiwezi kuwa hasara , siku moja vitajaa wote watu" Aliongea Roma. na Edna alimkata jicho na kugundua ameongea bila kufikiria.

Mawazo yake ya ndani kabisa ni kama yameshtukiwa sasa, Roma hakuwa na ndugu zaidi ya therathini wa kuweza kujaza vyumba vyote hivyo, Edna alijua kabisa Roma anazungumzia wanawake wake ndio wangevijaza.

"Malizia sentensi yako, unamaanisha kwamba niwarihusu waje wakae na sisi hapa?"

"Mpenzi sijamaanisha hivyo"Roma alijitetea lakini ukweli wa ndami kabisa ndio alichokuwa akikiwazia , kama hakupanga kuleta wanawake hao kwanini vyumba vyote vipo na vitanda ni lazima alishawaza jambo hilo , lakini wakati huo hakuwaza kuhusu warembo wake wengine ila alichokifikiria ni kufanya mapenzi na mke wake ili kitimiza kiu aliokaa nayo kwa muda mrefu.

"Kama hukua ukimaanisha hivyo ulikuwa ukimaanisha nini?”

"Ah..!, nilikuwa nikimaanisha kwamba naweza leta ndugu na marafiki na wakavijaza"Aliongea kwa kijibaraguza huku akijua sababu yake ni ya kipuuzi hasa mbele ya mwanamke kama Edna.

" Oh.!. vipi kuhusu vingine maana siamini unaweza kuvijaza vyote , wapo wakina Amina , Dorisi , Nasra , Rose na wengine naamini utawaleta wote hapa na ndio ulichomaanisha, na kama nikikumbuka vizuri wote walikuwa an shauku ya kuja kuutembelea ufalme wako na walikuwa sriasi katika hilo , nakuhakikishia kama vitajaa sitoshindwa kujenga Kota nyimgime upamde wa kule chini waishi kwa amani"

"Mke wangu Edna hili swala nadhani ni vizuri kama tukizungumza kesho, muda umeenda sana na tunatakiwa kuumaliza usiku wetu kwa kufanya tendo la ndoa , ni utamaduni kufanyika mara baada ya usiku wa ndoa"

Ndio Roma aliona kama mazingumzo hayo yakiendelea yatafikia hatua ambayo anaweza asipewe kitumbua, jambo ambalo alilisubiria kwa muda mrefu sana tokea aanze kuishi na Edna na sio hivyo tu naweza kusema alivumilia sana maana kwa urembo wa Edna ilikuwa ngumu kwa mwanaume rijali kutomgusa kabisa.

Edna mara baada ya kusikia kihusu tendo la ndoa ni kama sasa anaanza kukumbuka alishawekeana ahadi na Roma kufanya kitendo hicho mara baada ya harusi na kama ni ndoa ndio ishamalizika hivyo ahadi ilipaswa kutimizwa .

"Lakini si tulishafanya siku yetu ya kwanza kukutana , sidhani kama ni jambo la lazima kufanyika sasa hivi , kwanza nimechoka ninapaswa kupumzika"Aliongea Edna na kisha akashililia gauni lake na kuanza kupandisha ngazi kutafuta chumba chovhote cha kuweza kulala .Roma uso ulimshuka , alitaka kuongea neno lakini mdomo ulikuwa mzito.

"Edna hatuwezi kumaliza hii siku vibaya huenda tukajutia huko mbeleni , tumeanza vizuri tokea asubuhi itakuwa sahihi kumalizia vizuri"Aliongea Roma na kumfanya Edna kusimama na kumwangalia kwa chini .

"Siku ishaisha tayari na hata hivyo tumefurahi wote na sherehe imeenda vizuri na nimevaa gauni la harusi na kupokea zawadi na nimeridhika"

"Lakini hatujafanya bado.. na ni muhimu"Aliongea Roma kwa upole na huenda kwenye maisha yake hakuwahi kuwa hivyo.

" Nitapata ujauzito kama tutafanya sasa hivi ?”

" Uwezekano huo ni mdogo sana, mwili wangu ulivyo ni ngumu kwa miili yya kawaida kuweza kubeba ujauzito , labda utakapofikia levo ya Nafsi ninaweza kusema uwezekano utakuwa mkubwa"

" Kama siwezi kupata ujauzito basi haina haja ya mimi kufanya hiko kitendo"Aliongea Edna , ni kama alikuwa akimaansiaha kwamba tendo la ndoa ni kwa ajili ya kutafuta mtoto na kama hakuna uwezekano wa kupata mimba basi haina haja ya kufanya .

"Unasemaa..!” Roma hakuamini Edna angembadilikia ndani ya muda mfupi hivyo tena siku ya harusi , usiku ambao alikuwa akiusubiria kwa hamu zote.

"Edna tendo la ndoa halifanyiki kwa ajili ya ndoa tu na isitoshe uliniahidi mwenyewe"

"Mimi ni mwanamke na unapaswa kuelewa sisi wanawake ni vigeugeu"

"Uko serious?"

" Naonekana sipo siriasi? , hata hivyo naamini ukinifosi siwezi kukuzuia maana sio mara ya kwanza kunifanyia hivyo, lakini nakushauri usijekujaribu"Aliongea kibabe.

"Huna haja ya kuongea hivyo , unajua kabisa sitokulazimisha kama hutaki kufanya" Aliongea Roma , hakika ungemuona Mfalme Pluto ungemuonea huruma sana , Roma anaomba tunda kwa mke wake lakini anakataliwa.

"Najua unaweza kuona sikufanyii haki, lakini kila nikifikiria unakwenda kujaza wanawake kwenye hii ngome siwezi kujizuia kuchukia, Sitaki kugombana na wewe wala kukudharau lakini naomba unielewe leo siwezi kulala na wewe"

"Kwanini ulianzisha sasa hayo maongezi kama huyapendi , hata hivyo sio kama jambo hilo litatokea hivi karibuni"

"Kuna utofauti gani leo na siku zijazo, kila ninapoangalia msururu wa hivi vyumba nahisi kabisa kuna siku watakuwa wamevijaza, najua huwezi kuwaacha na pia nitakutana nao huko bnje lakini kuishi nao kabisa!? , siwezi vumilia"Aliongea.

Ukweli Roma alipanga siku moja kuja kuishi nao wote pamoja na hakuna namna mawazo yake Edna asingeshindwa kuyasoma mapema tu lakini alilaumu maana huo muda ulikuwa mbaya kwake.

"Edna siwezi kukufosi kama hutotaka kuishi nao, nitawakusanya wote na kuishi na wewe utakuwa na nyumba yako"

" Roma naomba uache maneno yako tafadhari , tushaishi pamoja muda mrefu na nilikuwa napanga mwanzoni kuwapuuzia . mimi na wewe tunajua huwezi kuwaacha, na pia siwezi kukuacha, kwa hivyo mimi na wewe tupige hatua moja nyuma. Nilipoona vyumba hivi, niligundua siwezi kabisa kukubali kuishi nao kwa namna yoyote matarajio yangu ni kinyume kabisa na uhalisia. Roma Akili yangu imechanganyikiwa niache nipumzike”

"Okey sitokusumbua tena , nitakupeleka chumbani upumzike"Aliongea Roma huku akilazimisha tabasamu

"Sawa"

Walipandisha wote ngazi na Roma aliweza kumuonyesha chumba kikubwa zaidi kuliko vyote , baada ya kuingiza Edna alianza kukichunguza , kilikuwa chumba kikubwa mno kilichopambwa na samani za kuvutia pamoja na mapambo , madirisha yake pia yalikuwa na upekee wake , kilikuwa Master bedroom , lakini licha ya uzuri haukunfurahisha Edna hata kidogo , macho yake yote yalikuwa kwenye kitanda , kilikuwa kikubwa mno kwa haraka haraka ni mita sita kwa sita ,godoro lake pamoja na kitanda vyote vilitengeneza kwa oda maalumu.

Haikueleweka kwanini alipata mabadiliko ya namna hio, alimgeukia Roma na kumwangalia na macho makali, akiangalia hicho kitanda ni kama anaona namna mwanamke zaidi ya mmoja akifanya mapenzi na Roma huku akijihisi na yeye kujumuishwa kutokana na ukubwa wa kitanda.

"Naona umewaza mbali sana kuandaa kitanda kikubwa namna hii" Aliongea Edna lakini ni dhahiri maneno yake yalikuwa ya kejeli na sio ya kusifia , Roma alitamani kupiga ukuta ngumi huku akijihisi aibu mbele ya mke wake.

Hiko kitanda alikiandaa maalumu kwa kulala na wanawake zaidi ya mmoja na hata malighafi zilizotumika kutengenezea zilitoka Myanmar, wakati ujenzi unamalizikia alimwambie Ron akiweke kwenye chumba kikubwa zaidi kabla ya kuanza safari ya kwenda Tanzania , mawazo ya kufanya hivyo ni pale alipojiambia kuna siku angekuja kula bata na wanawake zaidi ya mmoja.

Sasa alisahau kumwagiza Roma kukibadilisha na kuweka cha saizi ya kati kinachotosha watu wawili tu , yaani yeye na mke wake.

Hivyo Edna mara baada ya kukiona rayari alishafikiria mbali kwamba Roma anapanga kumlaza kwenye kitanda kimoja na wanawake wengine , lilikuwa kosa la kiufundi ambalo amesahau kulifanyia kazi , ukizingaria Edna ni mwanamke anaeweka heshima yake mbele.

Edna alijikuta akifungua mlango na kutoka kwenye hiko chumba na kisha akageuka na kumwangalia Roma.

“Naweza kuwa na madhaifu kama mwanamke , lakini mimi ni mwanamke ninaojali sana utu wangu , Roma you are wrong if you think I can let my husband have an orgy , ni kweli nakupenda lakini haimaanishi ninaweza kupuuzia mipango yako”Aliongea na kisha akaufunga mlango kwa nguvu kwa nje.

Roma alijikuta akishika kiuno hakuamini mambo yangefikia katika hatua hio , tena usiku wa ndoa yao.Aliijiuliza ni nanni mwenye makosa , yeye kwa kutokuwa makini au yeye kwa kuwa mbishi na mwenye kuchukia haraka.

Ilikuwa stori nyingine kama ashafanya hiko kitendo , lakini hata mchakato wenyewe haujaanza , alikaa huku akitafakari namna ya kumtuliza Edna na hatimae kula tunda lakini alikosa namna , ilikuwa habari mbaya sana kama usiku wao wa ndoa ukimalizika kwa ugomvi.

Edna baada ya kuingia kwenye chumba kingine alijikuta akikosa hata nguvu ya kukaa kitandani , alijua fika kwamba Roma hakufanya makusudi lakini wazo la kufikiria kwamba siku zijazo jumba lote hilo lingejazwa na wanawake , alikosa hamu na kuhisi maumivu makali.

Alijikuta akianza kulia kwa kwikwi na Roma aliesimama nje ya chumba aliweza kusikia kinachoendelea , Roma alijikuta akiwa kwenye mawazo na kuja kushituka mara baada ya simu yake kuita mfululizo.

Aliitoa na kuangalia jina la mpigaji , namba ilikuwa ilikuwa ni ya Omari Tozo na alikasirika mara baada ya kuona huyo mpuuzi anampigia wakati muhimu kama huo ambao anapaswa kuyamaliza na mke wake , lakini hata hivyo aliishia kupokea.

“Bro..!!”Sauti hafifu ilisikika kutoka upande wa pili na Roma aliweza kutambua ni ya Omari Tozo.

“Kuna nini wewe mtoto unapiga muda huu muhimu?”

“Goddamn! Roma nakufa,,, ni dharula njoo uniokoe nakufa ndugu yako…”Sauti upande wa pili ilisikika na anaongea alionekana kuwa kwenye maumivu makali na Roma alijikuta akibung’aa.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

MTUNZI SINGANO JR

WATSAPP:0687151346



VOLUME TWO

SEHEMU YA 474.

Roma kichwa kilianza kumuwaka moto, alijua kabisa Omari hakuwa akitania kama yupo kwenye matatizo, kwani mpaka kuchukua hatua ya kupiga simu licha ya kwamba alifahamu yupo nje ya nchi haikuwa swala la utani.

Roma alijiambia anapaswa kumuokoa, alipaswa kubakia hapo visiwani ndio kwa ajili ya honeymoon na mke wake , lakini hawezi kupuuza hatari aliokuwa nayo Omari.

“Uko wapi?”

“Nipo Muheza mkoa wa Tanga , sehemu moja inaitwa Magoroto”Aliongea na Roma alikata simu , hakupafahamu Tanga vizuri lakini aliamini atafika kwa kutumia mbinu za kichawi kumpeleka licha ya kwamba aliogopa radi njiani kwani kutoka hapo visiwani mpaka Tanzania ulikua ni umbali mrefu sana hivyo ni lazima angekiuka kanunu za asili za anga.

Alifungua mlango wa chumba alichoingia Edna na kumkuta akiwa ameketi kwenye zulia chini akilia kwa kwikwi, lakini alijiambia huo sio wakati wa kujali machozi yake.

“Edna ninarudi Tanzania kuna tatizo , nitakuomba msamaha nikirudi sitochelewa”Aliongea Roma na hakusubiri jibu kwani alitoka na kufunga mlango na kupotea palepale.

Edna alijikuta akiwa haamini kama Roma kaondoka, alijua wakati anafungua mlango labda anaingia kwa ajili ya kubembelezwa kumbe alikuwa akiondoka na kumuacha mwenyewe.

******

Kilichompa ahueni Roma, Tanzania bado ilikuwa ni mchana wa kama saa sita hivi kutokana na utofauti wa muda , hivyo haikumuwia ugumu kufika Magoroto kwa njia ya kuteleport.

Ile anatua eneo la msitu aliweza kuhisi msuguano wa hewa kwa mbali na aliamua kufuatisha na kweli mbele yake kando na bwawa aliweza kumuona Omari akiwa amelala chini akiwa ameshikiliwa na Queen ,alikuwa amezungukwa na watu waliovalia suti, lakini wote walionekana kutokuwa watu wa kawaida kutokana na mwonekano wao lakini pia Aura waliokuwa wakisambaza.

Omari alionekana kuumia eneo la tumboni na alikuwa akivuja damu nyingi mno, yeye na Queen haikueleweka walikuwa wakifanya nini Magoroto lakini kwa haraka haraka huenda walifika kwa ajili ya kutalii.

Wale watu mara baada ya kumuona Roma walianza kumshambulia , hawakuwa na siraha za moto bali walikuwa na mapanga na wawili walikuwa ni weupe jamii ya Asia kama wajapani na mmoja alikuwa mweusi.

Roma alijikuta akikunja sura baada ya kuwagundua kutokana na mkao wao wa kuanzisha mashambulizi, ni ninja wa kundi la Yamaguchi na mmoja kati yao alikuwa ni Scorpion mlinzi wa raisi Kigombola lakini hata hivyo Roma hakumtambua kwa uharaka.

Scorpion aliwaonyesha ishara ya vidole ambayo Roma aliweza kuelewa kwani hata yeye ashapitia mafunzo ya uninja , walikuwa wakiambiana kwamba adui sio mwepesi na wanapaswa kushambulia wote kwa pamoja.

Wote walianza kumshambulia Roma na walitoka kwa spidi huku mapanga wakitanguliza mbele na Roma alisimama eneo moja na ile wanamsogelea karibu aliita nguvu za kijini ambazo ulikuwa kama upepo ulioambatana na wingu na kuwapiga wote kwa pamoja na walirushwa nyuma na kujipigiza kwenye miti huku wakiugulia maumivu na kutema damu.

Roma hakutaka tena kucheleweshana nao kwani aliwaona dhaifu , Yamaguchi walikuwa na mbinu yao hatari ya kushambulia maarufu kama Tansu lakini ilikuwa dhiafu sana kwa mtu mwenye mafunzo ya kijini katika levo ya kuipita dhiki , lakini pia mbinu yao ili iwe vizuri kwenye kufanya kazi ni wakati wanapokuwa karibu na maji na bahati mbaya ni kwamba bwawa lilikuwa mbali.

Aliachia pigo lingine la kijini na awamu hii hakuna ambaye aliweza kuhimili bali mifupa ilivunjika vunjika na damu ndio zilioonekana kuruka hewani.

Queen alijikuta akitoa macho kwa tukio lile , ijapokuwa ashashuhudia mara moja uwezo wa Roma lakini kuona mwili wa binadamu ukisambaratika ilikuwa mara yake ya kwanza na ilimtoa macho.

“Roma naomba umsaidie tafadhari, anakufa”Aliongea huku akionyesha wasiwasi na michirizi ya machozi ilikuwa inaonekana kwenye mashavu yake, Roma alitingisha kichwa na kumwambia amwachie.

“Dhibiti mtiriko wa nguvu zako kwenda kwenye Meridian za tumbo nitakusaidia kuweza kupona haraka”Aliongea Roma akimwangalia Omari aliekuwa amelala chini.

Omari alifanya kama alivyoambiwa na kisha Roma aliweka mkono wake eneo la tumboni ambapo alikatwa na upanga na aliweza kugundua alikuwa na sumu mwilini hivyo alitumia nguvu za ziada kuikusanya hivyo kumsababishia maumivu makali Omari.

“Roma unafanya nini , Unaniua.?”Aijikuta akitoa ukulele mara baada ya nguvu ya kimaandiko ikiingia kwenye eneo la jeraha lake na kusambaa mwilini.

“Acha woga mtoto wa kiume mwili wako sio dhaifu na unaweza kuvumilia maumivu”Aliongea Roma na kumfanya Omari atake kumtukana kutokana na maumivu aliokuwa akiyahisi.

Dakika chache mbele Roma aliweza kutoa mkono mara baada ya kuona kazi yake imeisha.

“Unajisikiaje?”Aliuliza Queen baada ya Roma kumuacha.

“Nipo vizuri , ila nitajisikia vizuri zaidi kama utanipa hata busu shavuni”Aliongea na kumfanya Queen kushangaa lakini aliishia kuangalia pembeni , bado alionekana hajamfungulia Omari milango ya kuingia kwenye moyo wake.

“Roma asante sana , nilipatwa na wasiwasi usingeweza kuja haraka kwani upo kwenye harusi”Aliongea na kumfanya Roma kukumbuka namna alivyonyimwa kitumbua.

“Hakikisha unanilipa sijakutibu bure , licha ya kwamba juhudi kubwa zimetokana na nguvu zako za kijini”Aliongea Roma na ni kweli Omari aliweza kuwa hai mpaka Roma amefika kutokana na kuwa na uwezo wa nguvu za kijini na kama angekuwa binadamu wa kawaida angeshakufa,maana alichomwa na panga tumboni lakini si hivyo tu ilionyesha pambano lilichukua muda mrefu kidogo kwani Roma alitumia zaidi ya dakika kumi na tano mpaka kufika.

“Usiwe na wasiwasi kabisa , umenisaida mimi lakini pia umemsaidia Queen , nitahakikisha nakununulia msosi wa nguvu kwenye hoteli ya kimataifa”Aliongea na kumfanya Roma atamani kumpa kibao amempotezea muda na kuja mpaka hapo halafu anataka kumlipa kwa kumnunulia chakula.

“Vizuri malipo ni malipo , lakini sasa nataka uniambie nini kimetokea?, kwanii walikuwa wakikushambulia?”.

“Hata mimi sijui chochote , lakini nia yao ilikuwa ni kumuua Queen”

“Kama wanataka kumuua Queen unamaanisha Yan Buwen anaweza kuhusika?”Aliuliza Roma.

“Hapana Yan Buwen hawezi kuniua , ananipenda”Aliongea Queen na kumfanya Roma amshangae , inakuwaje mpaka muda huo bado alikuwa akimtetea, Omari na yeye alijikuta akiumia mara baada ya kusikia Queen anamtetea hata kwa wakati huo licha ya kujali alivyopambana kumlinda, ama kweli mapenzi ni upofu.

“Queen inawezekana Yan Buwen kahusika , lakini hatuna uhakika hivyo hatuwezi kuhitimisha kama ni yeye , lakini nakushauri tu kwamba Yan Buwen ni hatari kwako na sio mtu mzuri”Aliongea Roma , alijua Queen hakuwa na makosa bali alimuona Yan Buwen kama mtu mpole na huenda ndio maana akatokea kumpenda , lakini aliamini kama sio leo , kesho au kesho kutwa Queen angeweza kushuhudia ukatili wa Yan Buwen.

Walitembea kutoka kwenye msitu na kwenda kutokezea kwenye uwanja na muda uleule simu ya Roma ilianza kuita na alipoangalia jina la mtu anaepiga ni Ron kutoka visiwa vya wafu, alipokea na kuweka sikioni haraka.

“Mfalme Pluto Madam Persphone anataka kurudi Tanzania siku ya kesho , ameniambia nimwandalie usafiri wa ndege na nimeshindwa kumpa majibu ya moja kwa moja”Aliongea Ron na kumfanya Roma kuguna.

“Yupo karibu yako? Mpe simu niongee nae”

“Mfalme Pluto anasema hana chochote cha kuongea na wewe”Aijibu Ron na kumfanya Roma kuwaza kidogo , alijua sifa ya Edna ni kiburi hivyo alipaswa kumzoea na isitoshe hawezi kuanza safari tena ya kurudi visiwani kwani alikuwa hajamaliza , aliamini kuna uwezekano kushambuliwa kwa Omari ni mipango ya Yan Buwen.

“Basi hakuna shida mfanyie kama anavyohitaji aweze kurudi , kuhusu mama na Bi Wema haina haja ya kuwasumbua”Aliongea Roma na kisha akakata simu.

“Ineonyesha kuwa na wanawake wengi hakuyafanyi maisha yako kuwa marahisi?”

“Haya yasingetokea kama usingejiingiza kwenye matatizo , kwanza imekuwaje mpaka ukaja huku?”

“Nilikuja kupumzika na Queen kwenye hio hoteli huoni hili eneo ni zuri sana na kushauri siku umlete mkeo”Aliongea na kumfanya Roma kuanza kukagua eneo lote na kweli sasa aliona lilikuwa na mandhari nzuri ya kuvutia.

“Vipi umewaonaje wale watu walionishambulia uwezo wao?”

“Ni ninja wa kundi la Yamaguchi , nina uhakika inawezekana wametumwa na Yan Buwen”.Aliongea Roma na muda huo huo waliangalia wote angani mara baada ya kusikia sauti ya Chopa ikikaribia hayo maeneo.

“Kabla ya kukupigia simu niliwasiliana na baba kwanza na kumuaga kabisa kabla sijafa , ndio nilipokukupigia kwa kubahatisha , nadhanni ndio anafika kuniokoa”Aliongea Omari huku akitabasamu kwa uchungu.

“Nisingefika wangebeba maiti”

“Upo sahihi”Aliongea Oamri na muda ule ule chopa ilishuka na kutua kwenye eneo la uwanja na wanajeshi wawili makomandoo walishuka haraka haraka na mwishoni akatangulia kushuka mwanaume aliekuwa amevaa suti.

Alikuwa ni Afande Gambino Tozo , mkuu wa majeshi, na ile anatua chini tuna magari ya kijeshi yaliingia ndani ya hilo eneo kwa haraka na wanajeshi walitoka na kumzingira.

Afande Tozo mara baada ya kumuona Omari akiwa mzima alijikuta akipumua kwa ahueni na hata Roma aliona mzee huyo alivyokuwa na wasiwasi , ilionyesha alikuwa akimjali sana mtoto wake.

“Wewe mpuuzi kwanini unataka kujiingiza kwenye matatizo kwa ajili ya mwanamke ambaye ana ujauzito wa mwanaume mwingine , unataka kutuletea aibu familia”

“Baba huyu sio mwanamke bali ni mchumba wangu , ni mkwe wako mtarajiwa”Aliongea na kumfanya Afande Tozo kutaka kumpiga kibao , lakini alijitahidi kujizuia, ukweli hakupenda kabisa Omari akijihusisha na Queen kwani alikuwa mjamzito na mbaya zaidi Queen hakutaka kutaja ni mwanaume gani ambaye amempa mimba na Omari hivyo hivyo licha ya kwamaba alikuwa akiufahamu ukweli lakini hakutaka kuwaeleza wazazi wake kwamba ujauzito wa Queen ni wa Yan Buwen.

Afande Tozo alimshukuru sana Roma kwa msaada ambao ametoa kwa mtoto wake na kumuahidi muda wowote akihitaji msaada wa kijeshi atampatia.

“Queen mheshimiwa Kigombola anataka kuonana na wewe muda huu?”Aliongea Afande Tozo na kumfanya Omari kushangaa.

“Unamaanisha nini Mheshimiwa Kigombola kumuita Queen?”

“Sijui chochote na unavyoniona hapa nilikuwa kwenye sherehe ya Sendoff ya mtoto wake mkubwa, Amesema ana ujumbe wake”Aliongea na Omari alimwangalia Queen na kuona mshituko wake.

“Nitaenda kuonana nae” Aliongea Queen na kumfanya Roma kuhiusi kuna mchezo unaendelea na alijiambia itakuwa busara kwake kwenda na yeye kuhudhuria hio sherehe, hata hivyo Kigombola alikuwa adui yake na alijiambia kwasababu ashajileta mwenyewe ataenda kumpatia anachostahili.

“Afande nadhani inanipasa na mimi kuhudhuria, huenda ninaweza kupata hata mvinyo kupunguza mawazo”

“Bila shaka Mr Roma”Aliongea na wote walipanda kwenye chopa na kuondoka , huku wanajeshi aliokuja nao wakipanda magari kwani chopa ilikuwa ina uwezo wa jumla wa kubeba watu wa nne tu pamoja na Rubani.

Masaa kadhaa mbele waliweza kufika kwenye uwanja wa shule ya msingi na magari yaliwabeba na moja kwa moja safari ya kuelekea kwenye jumba la Raisi mstaafu Kigombola ilianza.

******

Mstaafu raisi Kigombola alikuwa asharudi nchini Tanzania , mara ya mwisho aliondoka haraka haraka kutokana na kuogopa Roma kumshambulia , lakini awamu hii amerudi akionekana ni mwenye kujiamini sana.

Ndio alikuwa akijiamini kiasi kwamba aliweza kufanya sherehe ya mtoto wake mkubwa wa kike ambaye alikuwa akiolewa , hivyo alikuwa akimfanyia sherehe ya Sendoff.

Watu mbalimbali siku hio walikuwa wamealikwa na wengi wao walikuwa na nyazifa kubwa serikalini , wakiwemo mawaziri , wanajeshi na wafanya bishara.

Moja wapo ya watu waliohudhuria ni Neema Luwazo , Afande Tobwe na familia yake yote yaani Mage na Magdalena walihudhuria pamoja na mama yao.

Sherehe ilikuwa ya kifahari kutokana na pesa alizokuwa nazo Kigombola , kwanza sifa yake kubwa mbaya kwa raia ni ufisadi alioweza kufanya kipindi akiwa kiongozi.

Ulinzi ulikuwa imara kweli na sherehe ilikuwa ni kama inakaribia mwisho mwisho kwani baadhi ya watu walikuwa wakianza kuondoka hivyo kubakia wachache sana ambao wengi walikuwa ni wale waliokaribu zaidi na raisi huyo.

Muda huo wakati mheshimiwa akiondelea kuongea na kucheka na wageni wake , mara alisogelewa na mlinzi alievalia suti na vifaa vya mawasiliano masikioni.

“Mheshimiwa Afande karudi lakini yupo na mgeni wa ziada”Aliongea yule bwana.

“Mgeni wa ziada?”

“Ni Roma Ramoni mtoto wa raisi Senga” Aliongea na kumfanya mheshimiwa mstaafu kigombola kutabasamu.

“Unaweza kumruhusu ndio niliekuwa nikimsubiria”Aliongea na yule bodigadi alionyesha kushangaa kidogo lakini aliinama kwa heshima na kuondoka.

Moja ya watu pia ambao hawakuondoka alikuwa ni Matilda na baba yake Mzee Alex , wote walikuwa ndani ya hilo eneo.

Mtu wa kwanza kumuona Roma akishuka kwenye gari na kumfanya kushangaa ni Magdalena na Mage , lakini hata hivyo mwonekano wa Omari ndio uliwafanya watu kumwangalia kwa wasiwasi kwani alikuwa amechafuka damu.

Magdalena m Mage na Afande Tobwe walifahamu kilichomkuta Omri na hata sababu ya mkuu wa majeshi kuondoka hapo ndani kwa dharula waliweza kuambiwa.

Kitendo cha Roma kufika hapo ndani kwa wale waliokuwa wakimjua iliwafanya kukosa amani, akiwemo Neema Luwazo ambaye alikuwa akijua Kigombola alikuwa na ugomvi mkubwa na Roma.

Upande wa raisi Kigombola kwanza hakuonyesha wasiwasi wowote, alionyesha kijiamini mno na haikuelewa kwanini alikuwa akijiamini maana kama Roma angeamua kulipiza kisasi kwa yale aliomfanyia basi hakuna mtu ambaye angeweza kumzuia.

Upande wa Roma aliamini hio ndio nafasi nzuri ya kumkomesha Raisi Kigombola , alijiambia alijileta mwenyewe nchini hivyo kama ataondoka hapo bila hata ya kumvunja mguu atakuwa hajajitendea haki , kwani raisi huyo ndio chanzo cha yeye kutaabika na Yan Buwen.

Mage ndio aliekuwa wa kwanza kumsogelea Roma mara baada ya kumuona , lakini ile anamkaribia alijikuta akibung’aa kwani Roma alipotea aliposimama na ile kuja kuibuka alikuwa mbele ya raisi Kigomboa na tayari alishashika shingo yake.

Watu wote walishangazwa na tukio lile na walinzi walikusanyika haraka na kumzingira Roma huku siraha wakiwa washazikoki tayari kwa mashambulizi.

“Roma punguza jazba”Aliongea Afande Tobwe na Omari alijikuta akimsogelea Roma ili kumsihi , lakini alijikuta akishindwa kuongea mara baada ya kusikia kauli ya Raisi kigombola.

“Nimekutafuta sana na hatimae leo umeingia kwenye kumi na nane zangu”Aliongea Roma huku akimwangalia Mheshimiwa Kigombola aliekuwa akihema kwa shida.

“Hu…huniwezi Roma , sikuwa mjinga kurudi nchini bila kuchukua tahadhari”Aliongea huku akikunja sura kwa maumivu na kauli ile ilikuwa ni kama imempa Roma ruhusa ya kumaudhibu kwani palepale alimtupia kwenye viti na kudondoka chini.

“Babaa..!!!!” Sauti ya Donyi ndio iiokuwa ya kwanza kugonga kwenye masikio ya Roma , lakini muda huo alijiapiza hawezi kutoa msamaha hata kama Donyi aingilie.

“Bro punguza jazba”Omari aliongea kwa wasiwasi na Roma alimwangalia.

“Omari kuna kitu labda hujagundua na nilitaka nikuthibitishie nikishafika hapa”

“Unamaanisha nini?”Aliuliza Omari.

“Kati ya watu waliokuwa wakikushambulia mmoja wapo anafahamika kwa jina la Scorpion ni mlinzi wa raisi mstaafu Kigombola na ndio aliehusika kumuua Profesa Shelukindo”Aliongea Roma na kumfanya Afande Tozo kushangaa na hapo hapo akili yake ilifanya kazi.Kwa jinsi ambavyo Roma alivyokuwa akimshambulia Raisi Kigombola ni dhahiri kama Scorpion alikuwepo angekua ashachukua hatua.

Kuna walioelewa maneno ya Roma na kuna ambao hawajaelewa , lakini kwa wanajeshi wote walikuwa wakimfahamu mlinzi wa kike wa raisi Kigombola afahamike kwa jina la Scorpion walielewa.

Roma pia alikuwa akimfahamu Scorpion kwani alishawahi kuingia kwenye rada za The Eagles kipindi walipokuwa wakifanya uchunguzi juu ya kifo cha Profesa Shelukindo , Scorpion ni moja ya watu ambao walikutana na Yan Buwen.

Roma aliamini kwa kumtumia Raisi Kigombola lazima angempata Yan Buwen na ndio maana wakati alipokuwa akipambana nao hakutaka kumwambia kwanza kuhusu Scorpion , lakini kubwa zaidi ambalo lilimhakikishia hisia zake ni pale Afande Tozo aliposema kwamba Kigombola anataka kuongea na Queen.

Tokea siku ambayo Roma alifahamu Queen alikuwa na ujauzito wa Yan Buwen alijiuliza maswali , Queen alimfahamu vipi Yan Buwen mpaka kuanzisha mahusiano , lakini jambo ambalo alikumbuka familia ya Queen kupitia mzee Alex walikuwa na ukaribu zaidi na familia ya Raisi mstaafu Kigombola.

Roma aliamini huenda Queen alikutana na Yan Buwen kwa kupitia Kigombola.

Roma alikuwa ashaanza kusambaza nguvu za kijini na kuwafanya watu kushindwa kumsogelea , licha ya kwamba alikuwa amemshikilia mstaafu kigombola kwa kumminya kwenye shingo kiasi cha kumsababishia maumivu.

“Muachie baba yangu mara moja la sivyo nitaruhusu wanajeshi wakushambulie”Aliongea mwanaume mmoja na kumfanya Roma kumwangalia na kutabasamu kifedhuli na palepale alimrusha tena Mstaafu ambaye alijipigiza kwenye nguzo ya turubai na kulifanya liyumbe palepale na kudondoka , watu walikimbia kujihami.

“Mama, baba anakufa,,, “Donyi alianza kutoa machozi huku akimsihi mama yake afanye jambo kumsaidia baba yake , lakini Neema Luwazo hakutaka kuingilia kwasababu alikuwa akijua mwenye makosa sio Roma bali ni Kigombola.

Afande Gambino Tozo palepale alishika siraha yake na kumsogelea raisi Kigombola, hakuamini mtoto wake alitaka kuuliwa na watu waliotumwa na mstaafu.

“Afande usiniangalie kwa macho ya chuki, mtoto wako ndio mwenye makosa”Aliongea Raisi Kigombola huku akijitahidi kusimama.

“Unamaanisha nini ndio mwenye makosa ilihali ulipanga kumuua , kama sio Roma huenda sasa hivi tungezungumza habari za msiba”

“Sio mimi nilimwagiza Scorpion bali ni Yan Buwen alietaka kumuua Queen”Aliongea na sauti yake iliweza kusikika lakini alieisikia zaidi ni Queen.

“Yan Buwen!.. unamaanisha nini Yan Buwen anataka kuniua?”Aliongea na kumfanya Queen kuanza kutokwa na machozi, lakini wengine hawakuelewa, kwanini Queen atake kuuliwa na Yan Buwen , moja wapo alikuwa ni Mzee Alex , alikuwa akifahamu Queen ni mjamzito lakini hakujua ujauzito ni wa Yan Buwen kwani Queen hakutaka kuweka wazi.

“Baba ujauzito wa Queen ni wa Yan Buwen”Aliongea Omari na kufanya watu wote kushangaakwa wale tu ambao walikuwa wakimfahamu Yan Buwen , wengine walijiuliza huyo Yan Buwen ni nani maana hata hawakuwahi kumuona.

Afande Tozo licha ya kwamba alikuwa akimfahamu Yan Buwen , lakini mambo makubwa aliokuwa akiyajua kuhusuYan Buwen ni kwamba anafanya utafiti wa kisayansi kusaidia siraha jeshini, hata kifo cha Profesa Shelukindo hakujua kama Raisi Kigombola alihusika na sio hivyo tu hakushiriki pia kwenye swala la Roma damu yake kuchukuliwa , yeye alitii kauli ya mstaafu kama mkuu wa majeshi tu na hata maamuzi aliyafanya mara baada ya kupata ruhusa kutoka kwa raisi.

“Roma nadhani unajihisi kuwa na nguvu , lakini hata hivyo umekwisha kuchelewa , kwani kila kilichotokea leo hii ni mpango wa kukuangamiza”Aliongea Raisi Kigombola na Roma wala hakutishika na maneno yake , lakini wengine walishangazwa hususani wale waliokuwa wakimjua Roma.

“Nilijua tu”Aliwaza Roma kwenye akili yake na kisha alitabasamu , ile siku ambayo alikuwa akiisubiria hatimae imewadia.

“Hades…!”Sauti kama ya mwangwi ilisikika kwenye masikio ya kila mmoja na kuwafanya wote waanze kuitafuta imetokea wapi..

“Yan Buwen!!” Omari ndio aliekuwa wa kwanza kuangalia juu angan huku akitamka jina la Yan Buwen.

Muda ule ule walitokeza wanaume kutoka pande zote za nyumba huku wakiwa na siraha mfano wa makombora ya Bazooka, lakini hayo yalikuwa ya rangi ya silver.
 
SEHEMU YA 475.

Kutokea kwa Yan Buwen kulishangaza wengi na kuwafanya warudi wote nyuma kwa tahadhari kwani suti yake aliovaa lakini pia miale ya Godstone ilileta msuguano ambao haukuwa wa kawaida.

Raisi Kigombola mara baada ya kumuona mwokozi wake alitoa tabasamu la kejeli.

Ndio kitendo cha kurudi Tanzania ilikuwa ni kwa ajili ya kumuondoa kabisa Roma, hakupenda Roma akiendelea kuishi Tanzania kwani alikuwa akimkosesha amani.

Hivyo kushambuliwa kwa Omari ulikuwa ni mpango wa Yan Buwen na mstaafu Kigombola kumrudisha Roma Tanzania na kukutana na kifo chake.

Hata Roma mwenyewe aliweza kugundua hilo kutokana na watu waliomzunguka , wote walionyesha kutokuwa wanajeshi wa kawaida na kwa haraka haraka alijua watakuwa na miili ambayo imechakachuliwa hivyo kushindana na wanajeshi wa kawaida ingekuwa kama misheni ya kujitoa muhanga, mbaya zaidi walikuwa wengi.

“Damn it Roma hawa wote si miili yao imechakachuliwa?”Aliuliza Omari huku akiwaangalia.

Unajua nini wakati wote wa harusi hao watu waliokuwepo lakini walikuwa wamevalia mavazi ya kihudumu na ndio maana hata muda huo walikuwa wameshikilia siraha lakini wakiwa na mavavi yaleyale ya wahudumu , Raisi Kigombola aliwaweka maalumu kwa ajili ya vita vya kummaliza Roma.

Roma hakujisumbua nao kwanza aliwachukulia wa kawaida , lakini tatizo ni moja eneo hili kuna watu wake wa muhimu hivyo ingekuwa ngumu kudili na Yan Buwen na wakati huo huo kudili na hao wanajeshi.

“Mheshimiwa waziri mkuu , Meja Tobwe na Mkuu wa majeshi mnaonekana hamna wasiwasi kwasababu mnadhani Roma anaweza kumdhibiti Yan Buwen si ndio?”Aliuliza Raisi Kigombola huku akimwangalia mwanaume aliekaa kwenye kona.

Roma aligeuka na kugundua kumbe kuna waziri mkuu , alijikuta akitukana ndani kwa ndani , ilionyesha dhahiri raisi Kigombola alialika watu wake muhimu pamoja na maadui zake ili kufanya vita iwe rahisi , kwani alikuwepo Mage , Magdalena ,Neema Luwazo na wengine wote ambao kama Yan Buwen anapanga kuwadhuru basi itamchukua kazi ya ziada kufanikisha usalama wao.

“Ninapenda niwaeleze moja kwa moja , ujio wenu kwenye hii sherehe ni wa kupangwa nyie wote ndio maadui wakubwa wa Kigombola hivyo nitahakikisha hakuna ambaye anatoka hapa akiwa hai”Aliongea Yan Biuwen.

“Mara ya mwisho ulijigamba kwamba unataka kuniua lakini uliishia kukimbia au sio wewe?”Aliongea Roma.

“Lakini nilifanikisha kukuumiza kwa kiasi kikubwa , nadhani hapo upo na shauku nimeweza vipi kufanyia kazi jiwe la Kimungu kufikia hatua ambayo sikuogopi tena , usijali kabisa kijana nimefanikisha kuweza kutumia nguvu yake yote na leo nina kwenda kutumia uwezo zaidi ya mara mia niliotumia wakati tunapambana kule China”Aliongea kwa majigambo na kumfanya Roma kwanza kukagua mazingira na wale watu ambao wamemnyooshea makombora aina ya Bazooka.

“Unafikiri mimi ni mjinga , kilichopo ndani ya hayo makombora sio kitu cha kawaida , ngoja nikuonjeshe utamu wa siraha yangu mpya”Aliongea na palepale Kombola la mmoja wa wale watu lilipuka palepale lakini halikutoa mlipuko kama ilivyotengemewa bali lilitoa miale kama ya mionzi rangi ya samawati lakini ya kung’aa sana kuumiza macho.

Roma alichukua tahadhari na kuwakinga watu wote na ngao na ilikuwa rahisi kwani wote walikuwa upande mmoja lakini sasa kwa wale wanajeshi wa Yan Buwen baadhi yao walianza kubabuka ngozi kwa spidi kubwa na ndani ya dakika mbili tu walidondoka chini na kupoteza maisha huku miili yao ikiwa kama imeyeyuka na kuwa maji na kilichoweza kuonekana ni skeletoni tu , kwani nyama zote zilibadilika na kuwa uji uji.

“Thanatos!” Roma alibwabwaja ndani kwa ndani mara baada ya kugundua teknolojia iliotumika ndani ya makombora hayo ilikuwa ni Thanatos kwani ndio pekee ambayo ilikuwa ikiweza kuyeyusha miili ya kiupe hai na kuwa ujiuji.

Akili zake zilimrudisha ufaransa namna alivyoweza kukwapulia siraha hio mara baada tu ya kuweza kuipata kutoka kwa serikali ya Ufaransa, jambo la kutisha zaidi ni kwamba hii iliokuwa na uweze zaidi ya mara mbili (Enhanced) kuliko alivyokuwa akiijua uwezo wake.

Tukio lile liliwafanya watu kutoa ukulele na kuhema kwa shida na hata Roma mwenyewe alishangazwa, ilikuwa ni siraha ya hatari mno ikigusana na miili ya binadamu na mbaya zaidi Yan Buwen ashaigueza na kuwa mionzi isiokuwa ya kawaida.

Wakati anapambana na Yan Buwen nchini China aliweza kuhisi hio mionzi lakini hakugundua kama ilikuwa ni ya siraha ya Thanatos kutokana na kwamba ili uweze kuitambua teknolojia hio ni pale inapoleta athari.

Roma kitu kingine pia alichokigundua wale watu waliozingira hawakuwa binadamu , walikuwa misukule na haraka haraka alijua lazima ni maiti zilizofufuliwa na Yan Buwen kwa kutumia kimiminika cha ufufuo na hili lilikuwa pia hatari zaidi.

Hivyo kwa haraka haraka ni kwamba walikuwa wakiongozwa akili zao maana hawakuonyesha hata hofu licha ya Yan Buwen kuyeyusha wenzao.

Afande Tozo na wengine sasa walielewa hatari na mbaya zaidi hakuna kifaa chochote cha kiletroniki kinachofanya kazi muda huo hivyo wasingeweza kufanya mawasiliano ya kuomba msaada na kwa mpango wa Raisi kigombola wa kutaka kuwaangamiza kwa kuwachukulia kama maadui basi ni hakika alikuwa amehakikisha hakuna mianya ya kutoroka.

“Yan Buwen unaweza kufanya majaribio ya siraha yako, lakini hapa ndani kuna baadhi ya watu wangu muhimu sitaki wapoteze maisha”

“Usijali mzee watu wako muhimu hawawezi kuguswa kama tulivyokubaliana” Aliongea huku akitabasamu na kisha akamgeukia Roma.

“Hades what do you think, Beutifull isn’t it?”

“Roma unaonaje, inavutia si ndio?”

“Wewe ni mshenzi , Wewe ni binadamu kichaa”Aliongea Neema Luwazo kwa hasira.

“Haha…Miss Neema nasikia umemsaliti Mzee Kigombola na kwenda kutoka kimapenzi na Hades , Huenda umechangia zaidi katika hili na leo unakwenda kuona mpenzi wako nikimuua mbele yako”Aliongea.

“Yan Buwen nataka ufanye kazi , Neema hapaswi kuguswa ninachotaka nikuona huyu mpuuzi wake anaejivunia nae anakufa mbele yake”Aliongea Kigombola.

“Kigombola kwanini unafanya hivyo , kwanini umeamua kufanya kazi na huyo shetani sio kama nilivyokujua tokea mwanzo”

“Umeyataka mwenyewe Neema na sina chaguo zaidi ya kufanya maamuzi magumu, umeutesa moyo wangu sana kutoka na huyo mtoto sasa wajibika kwa matendo yako” Aliongea.

“Muda wa kuongea porojo ushaisha naingia kazini sasa, nitaanza na Afande Flamingo nasikia una mafunzo kutoka China, hebu tuone kama unaweza kuhimili pigo moja” Aliongea na palepale msukule wake mmoja uliachia bomu la Thanatos kutoka kwenye Bazooka.

“Magdalena kuwa makini” Aliongea Roma na uzuri Magdalena alikuwa mwepesi hivyo alipotea aliposimama na miale haikumpata.

Ilikuwa ikitisha sana, yaani misukule yake alikuwa akiwaongozakwa kutumia akili yake , kwanni akifikiria kufanya hiki na mmoja wapo angechukua hatua.

“Hahaha… nishasahau unasemekeana kidogo una spidi kubwa labda nianze kwanza na baba yako pamoja na pacha wako” Aliongea na palepale wanajeshi wake wanne waliinua kombola kulenga waliposimama Afande Tobwe na Mage lakini palepale ngao kama kioo ilijitengeneza mbele yao na kuwakinga na mlipuko wa mionzi ya Thanatos.

Uzuri ni kwamba miale ile ilikuwa na sifa moja ya pekee haikuwa na uwezo wa kusambaa , ilikuwa ni mionzi tofauti sana na iliozoeleka, hivyo athari zake zilikuwa za dakika moja tu na kuisha lakini hata hivyo zilikuwa na nguvu mno kwani ile ngao ilionekana mbele yao baada ya kugongana na bomu la mionzi la Thanatos ulitokea mtikisiko wa ardhi wa aina yake.

Afande Tobwe alimwangalia Roma kuona kama ndio yeye aliewakinga kwani alikuwa ashakata tamaa , lakini Roma alimwonyeshea ishara kwamba sio yeye lakini sasa muda huo huo walisikia sauti kutoka mbali kidogo angani lakini ikiongea kwa lugha isiokuwa ya kawaida lakini Roma alipata kuifahamu kilikuwa ni kihindu.

“Ninakwenda kukumaliza leo hii, wewe ni uzao wa shetanni kutoka familia ya Yan” Aliongea hivyo.

“Master!”

Omari ndio aliekuwa wa kwanza kuangalia hewani na kujikuta akitabasamu na kuita jina la Master.

Roma na yeye aliangalia hewani na palepale aliweza kuona mwanaume aliekuwa jamii ya wahindi hakuwa mchina licha ya kuweza kuongea kichina , alikuwa mhindi lakini alienyoa kipara huku akiwa na shanga kama Rozari alizokuwa amevalia shingoni , alikuwa pia amevalia mavazi ya kitamaduni maarufu kama Kisaya ambayo huvaliwa na Monk wale wanaosalia Budha.

Ni Monk lakini ni sahihi kusema alikuwa monk mwenye kutisha maana kwa dunia ya leo hakuna mtu ambaye anaweza kuwa na mwonekano mbaya wa sura kama mtu huyo alieweza kufika.

Roma alijikuta akishangaa, mara moja aliweza kutambua mtu aliefika hapo sio binadamu wa kawaida , licha ya kuonekana kama binadamu , alikuwa ni watu jamii ya Hongmeng kama hajakosea ambaye alikuwa anakaribia kuvuka Levo ya Nafsi na kuingia levo ya Dhiki.

Ilionyesha yeye ndio ambaye alihusika kuwakinga Afande Tobwe kwa kutumia dhana ya kimaajabu ambayo kwanza ilimshangaza sana Roma.

“Nilijua kabisa Hongmeng lazima mngekuja kabla sijawafuata huko huko, lakini nasikitishwa kuona umekuja peke yako” Aliongea Yan Buwen.

“Amitabhaa , hili tukio tusingeweza kukaa na kuangalia unafanya utakavyo kwani unaifanya nchi yetu kuwa na uadui na mataifa mengine , Mimi mjumbe kutoka Hongmeng leo nakwenda kukuadhibu kwa niaba ya dunia nzima, kutana na Dhana yangu ya kishetani”

Monk hakutaka kupoteza muda na palepale alianza kumsogelea Yan Buwen kwa kasi, ilionekana alikuja kwa kazi maalumu tu nchini Tanzania , kupambana na Yan Buwen na kisha kusepa maana hakumzingatia hata Roma.

Wakati anamsogelea Yan Buwen alikuwa ameshikilia kiutu kama kijichupa cha rangi nyeusi lakini ajabu ni kwamba palepale kilibadilika na kuwa kama mkuki wenye ncha kali kwa mbele ambao ulitoa msisimko wa ajabu mno.

Yan Buwen wala hakusogea zaidi ya kumwangalia kwa kebehi na ile Monk anapeleka mkuki wake akidhamiria kumchoma nao Yan Buwen eneo la kifuani , Yan Buwen palepale alibadilika na kuwa kama sanamu ya Chuma lakini rangi ya Silver na palepale mlio wa chuma kugongana na chuma ulisikika , lakini Monk alionyesha kuwa na akili zaidi kwani palepale alichia pigo lingine na Yan Buwen alirudi kwenye ubinadamu na Monk alimkata mkono na mkuki wake palepale.

“Yes,, Yes…!!”Omari alishangilia mara baada ya kuona lile pigo na kumfanya Roma kumwangalia.

“Roma huyu ndio Master wangu ndio anaesifika kuwa sehemu ya wazee watano wenye uwezo mkubwa ndani ya Hongmeng”Aliongea Omari na kuwafanya watu wote kupata ahueni.

Lakini upande wa Roma aliona ilikuwa mapema sana kushangilia ushindi kwani hakutegemea Yan Buwen kuja na uwezo mdogo kiasi cha kuweza kushindwa na Monk kama ni hivyo alijimbia asingeumiza kichwa.

Yan buwen alionyesha kutougulia maumivu na mkono wake ulipona palepale na kisha akamsogelea Monk kwa spidi na kumwachia wimbi la shoti ambayo ilimlipua na mlio wake ulikuwa kam Transfoma inapiga shoti.

BOOM!

Watu walijikuta wakichuchumaa chini kwa woga mara baada ya mlipuko ule kwani ni kama Roho zilitaka kuwatoka ni Roma , Magdalena na Omari ambao hawakuonyesha hofu na kuendelea kuangaia angani.

Monk alijitahidi kuhimiri mlipuko wa Shoti kwa kutumia nguvu za kijini lakini nguvu yake ilimzidi na kumfanya kutupwa mbali kalibu aiguse ardhi na palepale shoti ikapotea na Yan Buwen alirekebisha mkono wake uliojiponyesha kwa haraka na kucheka.

Monk alijikuta akimwangalia Yan Buwen huku akiwa kama haamini alijihisi mtiririko wa nguvu zake za kijini kwenye mwili wake zimepungua sana kwa kufonzwa na shoti.

Roma mpaka pale aliona kabisa Yan Buwen nguvu zake zilikuwa za viwango vikubwa mno na ilionyesha hakuna pigo la kawaida la kijini ambalo lingeweza kummaliza na mwenyewe alijiambia asingemsaidia Monk kwa namna yoyote ile aliacha kwanza aone mwisho wake alitaka kwanza atumie nafasi hio kuona Hongmeng wanavyopambana ili apate kujifuza.

Roma alianza kudili na wanajeshi misukule wa Yan Buwen maana asingefanya hivyo wakati wa kupambana na Yan buwen angeshindwa kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja na alishukuru sana kutokea kwa Monk maana huenda ingekuwa shida kwake.

Roma aliachia pigo moja ambalo liliambatana na upepo wa kisulisuli na kuwazoa wanajeshi watatu kwa wakati mmoja na walikwenda kujipigiza kwenye ukuta na kombola lao lilipuka palepale na walianza kuyeyuka nyama zao zote na kubakia maskeletoni.

Afande Tozo , Afande Tobwe waliona kabisa hapa uwepo wao ungekuwa mzigo kwa Roma hivyo wanapaswa kuondoka kwenye hilo eneo na watu wote , lakini Yan Buwen alionekana ameshayasoma mawazo yao mara baada ya kushuhudia Roma akiangamiza wanajeshi wake , palepale wanajeshi wawili waliachia bomu la Thanatos kuelekea upande wao , lakini Roma alikuwa fasta sana kwani ni kama alitegemea na kuwafunika na ngao ya kijini na kilichotokea ni mtikisiko.

“Msifanye chochote maana nawahakikishia hakuna ambaye anaweza kuondoka hapa akiwa hai , mpango ni mimi kuwamaliza maadui zangu wote na msifikiri uwepo wa Monk unaweza kuwasaidia , mpango wa Yan Buwen pia ni kumalizana na Hongmeng ili aitawale China”Aliongea Kigombola na kumfanya Roma aone kweli binadamu yoyote wa kawaida akipata uwezo wa ajabu kuzidi wengine basi uwezo wa kufikiria hupungua kwa kiasi kikubwa mno. Alimjua Kigombola alikuwa akisifika kwa mbinu lakini hakuamini angekuwa na uwezo mdogo wa kufikiria namna hio.

Ukweli Kigombbola alimwamini kwa asilimia zote Yan Buwen , ni kama aliamua kubetia maisha yake kwenye uwezo wa Yan Buwen aliamini kama Yan Buwen angeweza kumdhibiti Roma basi taifa lingekuwa la kwake milele na angefanya mpango na kumaliza na maadui zake ambao hawakuwa hapo ndani na kisha kumuweka raisi ambaye angefanya kile anachotaka yeye.

“Tianyin Dhamachakra!!”

Monk alionekana kurejewa na nguvu zake na kuanzisha upya mashambulizi kumlenga Yan Buwen.

Ghafla tu palepale monk alionekana mara ishirini zaidi na wote wakiongea ‘Mantra’ kwa nguvu na sauti ya Brahma ilisikika mara mbilimbili kama mwangwi.

Kumbuka hapa alikuwa ni Monk mmoja lakni alijitengeneza kuonekana zaidi ya mara hamsini na ndio maana sauti zao zilionekana kama vile ni watu waliopo kanisani au msikitini wakisali kwa kuongea na sauti zake kujaa mwangi , waliopo hapo ndani ni kama walihisi uchizi kutokana na makelele yasioeleweka.

Yan Buwen alikuwa katikati na Monk alionekana kufanya vile ili kumchanganya Yan Buwen asiweze kumshambulia kwani asingejua yeye halisi ni yupi kati ya ‘illusion’ aliotengeneza.

“Hahaha.. unachokifanya ni ujinga kwangu”Aliongea Yan Buwen na kuachia shoti ya aina yake kumlenga Monk aliekuwa kushoto kwake na alikuwa ndio origino lakini bahati nzuri alikuwa amejiwekea ngao na ile dhana yake ya kijini hivyo hakupata majeraha lakini alishangaa Yan Buwen amewezaje kumfahamu.

Monk alichokosea ni kuamini kwamba Yan Buwen alikuwa akipambana kwa kutumia sayansi na yeye alikuwa akipambana kwa kutumia uchawi hivyo kama angemuwekea Yan Buwen mtego ingekuwa rahisi kumdhibiti.

Roma aliweza kudhibiti baadhi ya wanajeshi , lakini hata hivyo walionekana kuwa wengi sana kwake kuwamaliza kwa muda mfupi huku pia akilinda watu wasidhurike.

Yan Buwen alionyesha kuwa mjanja sana kwani wanajeshi aliokuja nao kwa mahesabu ya haraka haraka ni therathinni, mwanzoni waliokuwa wamemzingira walikuwa wachache lakini baada ya muua waliongezeka.

Omari hakuweza kupambana pia kutokana na jeraha eneo la tumboni.

Donyi aliekuwa akitaka baba yake asiuliwe na Roma alikuwa kwenye wasiwasi kwa kile ambacho kingetokea muda huo.

Roma mbinu pekee ambayo aliona ingeweza kumaliza kazi ni kumshambulia Yan Buwen , kwani ilionyesha wale wanajeshi pasipo ya Yan buwen hawawezi kuchukua hatua kwasababu walitegemea akili yake.

Hivyo mara baada ya kuona Monk anapokea kichapo fasta alimsogelea Yan Buwen kwa kasi.

“Naona umekuja , lakini muda bado”Aliongea huku akiangalia chini na ilionekana Magdalena alifanya kosa kutaka kuwashambulia wale mazombie , ilikuwa sahihi kuwaita mazombie maana akili hazikuwa zao na walishakufa na kufufuliwa na kimiminika.

Sasa kumbe Yan Buwen aliona hilo , hivyo palespale aliruhusu wale mazombie kumshambulia Magdalana lakini hata hivyo alionyesha kuwa spidi kwani aliweza kukimbia kwa spidi na kuepuka shambulizi na ile miale iliwaua wahudumu wawili wa kike na nyama zao kuyeyuka palepale walibakia kuwa skeleton.

Neema Luwazo alikosa uvumilivu na alijikuta akianza kutapika palepale na ilibidi Donyi amshikilie mama yake kwani alianza kukosa pumzi.

“Unaweza kuwa na spidi lakiini haimaanishi kwamba unaweza kupona kama watashambulia wote”Aliongea Yan Buwen mara baada ya Magdalena kutudi aliposimama baba yake , lakini lilikuwa kosa kubwa.

“Shiti tupo karibu sana”

“Mshachelewa , Firee..!!”Aliongea Yan Buwen akiwaamrisha misukule yake kushambulia.



SEHEMU YA 476.

Roma alikuwa na spidi, mwanzoni alitaka atumie ile Dhana ya Ganyua alioipata kutoka kwa lile jini lililomteka Edna na kumpa laana ya minyoo lakini hakujua kama ingekuwa na nguvu kiasi gani hivyo hakutaka kubahatisha na aliita nguvu ya kimaandiko na kuwafunika na alifanya ndani ya muda kabla ya kuguswa na mionzi ya Thanatos.

Lakini sasa wakati Roma akiwalinda wengine yeye alipokea pigo kutoka kwa Yan Buwen na alihisi maumivu makali mno, ilikuwa ni kama viungo vyake vya ndani vinakamuliwa kama nguo inayotolewa maji.

Roma ilibidi kwanza arudi chini ili kushindana na maumivu na ilionekana mbinu ya Yan Buwen kumalizana kwanza na Monk na kisha ndio adili na Roma.

“Roma uko sawa?”Aliuliza Mage ambaye aliishia kutoa machozi pasipo ya kujua cha kufanya.

“Inabidi mjiwazie usalama wenu kabla ya wa kwangu , Babe Mage nikimaliza hapa hakikisha unanihudumia vizuri”Aliongea Roma huku akilazimisha tabasamu kuwaonyesha kwamba yupo sawa.

“Unapata wapi ujasiri wa kufanya utani wakati upo kwenye hatari” Aliongea Magdalena lakini maneno yake yalikuwa sahihi , ijapokuwa hakuwa na woga lakini aliamini kushindana na Yan Buwen inahitajika akili ya ziada kwani uwezo wake ulikuwa mkubwa huenda kumzidi hata Poseidon.

Wakati akiangalia namna ya kushinda pambano lililokuwa mbele yake , ghafla kuna wazo lilimjia na kuamini huenda linaweza kufanya kazi kumsaidia kumshinda Yan Buwen.

“Simameni wote hapa hakikisheni mnakaribiana na msiulize maswali kama mnataka kuishi” Aliongea Roma kwa kuamrisha na palepale Roma alipotea na ile anakuja kuibuka alikuwa nyuma ya wale wapiganaji wa Yan Buwen na alimvunja shingo mmoja na mwingine aligeuka kwa kuhamaki kujilinda kwa kufyatua bomu lakini aliishia kumdhuru mwenzake.

Upande wa juu Monk alikuwa akiendelea kupamaban na Yan Buwen , lakini ukweli Monk alikuwa amezidiwa alichokuwa akifanya ni kukinga mashambulizi tofauti ya kushambulia na Yan Buwen alionekana kutulia na alifanya kazi mbili kwa wakati mmoja , baada ya kuona Roma anashambulia wanajeshi wake , alianza kuwapa maelekezo ya kumshambulia.

Muda ule ule haikueleweka wanajeshi walitokea wapi lakini waliwaznguka Afande Tozo kwa kuwakinga huku wakiachia risasi mfululizo kuelewa kwa misukule , lakini licha ya risasi zile kuwapiga hazikuwaletea madhara makubwa.

“Kipaumbele ni ulinzi kwa Generali na waziri mkuu” Mmoja wapo wa wale wanajeshi alitoa amri walikuwa na sare za kikomandoo.

Roma aliendelea kuwashambulia wale wanajeshi wa Yan Buwen kwa spidi kubwa huku akiwakausha, alionekana alitaka kumaliza ndani ya dakika chache na kumfanya hata Omari kushangaza.

“Damn it huyu Roma ni zaidi ya shetani”Aliongea Omari.

“Tunatakiwa kujua namna ya kumsaidia na sio kumsifia”Aliongea Magdalena.

“Kwani naongea uongo , Magdalena hata wewe unaonekana kumpenda”Aliongea na kumfanya Magdalane kumwangalia kwa macho makali Omari na alianza na yeye kushambulia kwa kasi , ilionyesha tokea maarifa mapya ya kijifunza mbinu za kijini kwa kufundishwa na Roma aliimarika kwani aliachia mapigo kwa kasi mno na aliweza kuwamaliza wawili na kuwaua kabisa.

Omari na yeye alichana kitambaa na kisha akajifunga nacho eneo la tumboni kwa nguvu na kisha akaanza kushambulia kwa spidi.

Upande wa Queen yeye macho yake ni kwa Yan Buwen tu hakujali kilichokuwa kikiendelea kumzunguka bali alikuwa akimwangalia Yan Buwen huku akitoa machozi , alionyesha kama hakuwa akiamini ni yeye, alitamani Yan Buwen amwangalie lakini hakufanya hivyo zaidi ya kuendelea kupambana.

Afande Tozo hakutaka tena kukaa na yeye kwenye ngao , alichokifanya ni kuchukua bunduki na hivyo hivyo kwa Afande Tobwe walichokifanya ni kupambana wakiendelea kubaki nyuma ya ngao.

“Nimegundua kuhusu siraha zao , haziwezi kuachia mashambulizi mfululizo lazima watulie kwanza ndio waachie tena , tunaweza kutumia udhaifu kushambulia kabla hawajaachia na kurudi kwenye ngao”Aliongea Afande baada ya kupewa siraha na wanajeshi waliofika kumlinda.

Upande wa mstaafu Kigombola alikuwa hana wasiwasi kabisa alikuwa amesimama upande mwingine akiwa amesimama na watu wake wakiwaangalie wenzao wakitaabika.

Yan Buwen mara baada ya wanajeshi wake wawili kupasuliwa vichwa aliweza kugundua washajua udhaifu wa siraha yake. Aliangalia chini kwa kebehi.

“Inaonekana mshaanza kuzifahamu siraha zangu , lakini niwaambie tu hizo Ant-matteer Bazooka zipo kwenye majaribio tu nimezitegeneza kwa kuigizia nguvu ya nishati ya jiwe la Kimungu na kuchanganya na teknolojia ya Thanatos, hivyo hio ni ‘Prototype’ tu , lakini naona mnavyo hangaishwa , kama ningeamua kutumia ‘pure antimatter energy’ kutoka kwenye Godstone kutengeneza miozi ya Thanatos msingeweza hata kuwa levo ya kushindana na mimi”Aliongea

Antimatter energy?”Roma alijikuta akishangaa..

“Huna akili wewe, siku zote ulikuwa ukimiliki jiwe la kimungu lakini umeshindwa kufahamu ndani yake kulikuwa na Antimatter , tena mionzi hio ilitumika kukumulika lakini ulishindwa kung’amua”Aliongea Yan Buwen akimkebehi Roma.

“Kukutoa tongo tongo nishati ant- matter ndio ambayo inatumika kutengeneza usawa kati yake na maada na kufanya dunia iendelee kuwepo , hivyo usije ukajinadi na kujiona mwenye nguvu, nishati ya mbingu na ardhi ni upuuzi mtupi mbele ya Godstone na kadri itakayokuwa kwenye umiliki wangu nitakuwa mungu wa dunia yote na wewe lazima ufe”Aliongea.

Roma licha ya kuonyesha kutoathirika kwa muonekano wa nje , lakini ndani kwa ndani alikuwa akihofia matokeo.

Tokea kupatikana kwa jiwe la kimungu miaka mingi iliopita hakuna mwanasyansi ambaye alifanikisha kuweza kuvuna nguvu yake kwa asilimia mia moja, jambo pekee ambalo walifanikisha ni kumtengeneza Roma, hivyo Yan Buwen sio tu kugundua siri iliokuwa nyuma ya teknolojia ya jiwe la Kimgunu lakini ameweza pia kugeuza na kuwa siraha ya maangamizi.

Lakini ukweli ambacho hakuwa akifahamu Roma ni kwamba Yan Buwen sio ambaye alikamilisha kila kitu, walioweza kufanikisha ni Athena, Profesa Shelukindo na Naira na Yan Buwen alipewa tu baadhi ya kanunni na Athena lakini pia aliweza kugundua siri mara baada ya kuiba tafiti za Profesa Shelukindo baada ya kumuua.

Lakini Yan Buwen asingeweza kusema amepokea msaada kwasababu alitaka kuchukua sifa zote yeye.

“Mtoto mjinga sana wewe usie na aibu” Aliongea Monk kwa hasira huku akimsogelea Yan Buwen kwa kasi na kuanza kuongea Mantra tena.

“Isio na umbo ,yenye nguvu ya uharibifu ,kwako Asura Dharmakaya

Aliongea kwa nguvu Monk kuita nguvu za kichawi na palepale watu waliweza kushangaa kuona moshi mweusi ukijitengeneza angani ulikuwa ni moshi kama mtu kwani ulikuwa na kichwa na mikono pasipo ya kuwa na miguu na ulianza kumsogelea Yan Buwen kwa spidi , walikuwa juu angani lakini waliochini nywele ziliwasimama.

Alichokiita ndio kinafahamika kwa jina la Asura Dharmakaya ni sehemu ya miungo ya kipepo ya wahindu na ina nguvu kweli.

Monk hakutaka kuendeleza mapambano kwani huko alikotoka alikuwa na uhakika angemwangamiza Yan Buwen kwa pigo moja tu , lakini sasa ni zaidi ya lisaa bado anapambana nae bila mafanikio.

Lile pepo Asura mara baada ya kumsogelea Yan Buwen , ghafla upepo mkali ulimkumba Yan Buwen kiasi cha kusababisha suti yake eneo la kifuani kuchanika na palepale lilionekan jiwe la Kimgu kwenye kifue eneo la moyo.

Monk hakujali tena kuhusu lile jiwe alichotaka ni kuhitimisha pambano kwa kumdhibiti Yan Buwen , hivyo aliongezea nguvu lile pepo Asura kwa kutumia nguvu za kijini na nguvu iliokuwa kwenye dhana alioiita Tianyi na kisha kutengeneza pigo zito kama bomu kuelekea kwa Yan Buwen huku akiwa na uhakika anammaliza kutokana na kutumia nguvu zake zote.

Lakini sasa baada ya kuachia lile shambulizi zito kulitokea vinyuzi nyuzi vidogo kama kamba kutoka kwenye lile Godstone , havikuwa vinyuzi kabisa ni kama mstari wa vinyuzi lakini vingi na vilizingira kichwa cha pepo Asura na kukifanya kama mpira na palepale liliishiwa nguvu , lakini Monk akiwa amehamaki kwa tukio lile pepo lake lilimgeukia mwenyewe na Yan Buwen aliachia na bomu kama shoti kumpiga nalo, ijapokuwa aliwahi kujitengenezea ngao lakini alikuwa karibu hivyo aliweza kupata majeraha kwenye mwili wake na kurudi chini huku akimwangalia Yan Buwen kwa mshangao.

Katika maisha yake hakuamini kama Sayansi inaweza kudhibiti pepo au uchawi, aliamini uchawi unadhibitiwa kiroho lakini Jiwe la Kimugnu liliweza kumeza nguvu yote ya Asura.

Roma mwenyewe alishangazwa na tukio lile , ilikuwa mara yake ya kwanza kuona kitu kama kile.

“Hahaha… Vipi bwana Hades unaogopa mbona umetoa macho hivyo naamini unajihisi kukata tamaa , zamu yako bado , Firee.!!.”Aliongea baada ya kumwangalia Roma kwa jeuli.

Roma hakujalishwa na kejeli zake na hasira iliongezeka maradufu na alianza kuwashambulia wale wanajeshi kwa kushirikiana na Omari na Magdalena.

Yan Buwen alimwangalia Monk ambaye alikuwa akijiponyesha na kucheka , kwani ni kama alikuwa akiangalia kituko , hakujali hata wanajeshi wake chini walikuwa wakiangamia bali alichokuwa akijali ni uwezo wake.

“Hongmeng wamekuleta mpaka huku Tanzania, nani atapeleka taarifa ya kifo chako?”

“Wewe mtoto muda wako wa kufa umewadia”Aliongea Monk kwa kiburi na kuanza kuongea lugha isioeleweka kama vile ana mapepo na palepale mikono yake ilionekana ngao ya kichawi kwenye mikono yake pamoja na mkuki wake na alimsogelea Yan Buwen kwa kasi huku akidhamiria kumchoma tumboni , lakini Yan Bvuwen ni kama alikuwa akisubiria amfikie kwani palepae ulitokea miale mikali sana kuangalia kwa macho na kumfunika Monk kiasi cha kusababisha eneo lote kuwa na mwanga wa tofauti licha ya kwamba ilikuwa mchana na mpaka mwanga unapotea Monk hakuonekana tena zaidi ya mkuki wake kudondoka chini.

Na huo ndio ukawa mwisho wake , kwani Yan Buwen aliweza kumyeyusha mara moja.

“Nguvu ya mionzi ambayo ipo kwenye hizi Bazooka chanzo ni wewe mwenyewe si ndio?” Aliongea Roma.

“I guess there is no harm telling you this , I’m Godstone and Godstone is me”Aliongea Yan Buwen akimaanisha kwamba yeye jina lake ni Jiwe la kimungu na Jiwe la Kimungu ndio yeye, yaani yeye ndio chanzo cha nishati yote ya ant- matter.

Palepale kuthibitisha majigambo yake alishika eneo la kifua chake na kisha akaingiza mkono eneo la moyo na kuchomoa kitenesi kinachong’aa sana , lilikuwa jiwe la kimungu na Roma alishangazwa mno.

“You fused God’s stone into your body?”Aliuliza Roma kwa mshangoa kwa lugha ya kingereza , kwamba ameunganisha jiwe la kimungu na mwili wake.

“Hahaha…. Unaogopa? , Frequency za mfumo nishati wa mawimbi ya mwili wangu unafanana kabisa na Frequency za jiwe la kimungu, hivyo moyo kwangu hauna kazi kubwa kwani nishati safi inayotokana na anti- matter inafanya seli za mwili wangu kuwa ‘active’ , wewe si ulifanya jiwe hili kuwa kama kajiwe kakuchezea nako , mpuuzi mkubwa wewe ngoja wenye akili tukuonyeshe”Aliongea

“Only I , Yan Buwen deserve to own the world’s greatest creation”

Aliongea huku akinyanyua mikono hewani kama vile watu wa dunia nzima walikuwa wakimuona lakini baada ya kushusha mikono yake chini alichia na shoti ambazo zilikaa kama boriti na kuwashambulia Roma na watu wake.

Baadhi ya makomandoo wa kijeshi walipoteza maisha palepale na Misukule ya Yan Buwen ilibakia mitano tu na walinyanyua makombola yao ya Bazzoka na kuachia miale ya yenye mionzi ya Thanatos.

BOOM , BOOM , BOOM.

Ngao ya kichawi iliowafunika Neema Luwazo na wengine iliyumba na kuonyesha muda wowote ingeachia na Roma alitumia nguvu nyingi sana kuidhibiti na kila inapopokea mashambulizi maumivu aliyasikia yeye.

Sasa shoti alipiga Yan Buwen ilikua na nguvu mno na ilimfanya Roma kuhishi kama yupo Jehanamu, ni maumivu ambayo mara ya mwisho aliyahisi wakati akipambana na Poseidon kwenye bahari ya kusini ya China, Roma alijikuta akitapika damu lakini hata hivyo aliendelea kudhibiti ngao isiondoke kwani ingekuwa ndio vifo vya watu wake muhimu, yeye alijiambia ni kheri wafe wengine lakini sio Mage na Neema Luwazo.

“Romaa..!!”Mage na Magdalena na Donyi awamu hii walimlilia Roma mara baada ya kutapika damu.

Roma alijitahidi kuita nguvu ya kimaandiko kumponyesha haraka na alijihisi ahueni mara baada ya maumivu kupungua.

“Nipo sawa ni majeraha madogo tu “Aliongea kuwaondoa hofu maana Mage alitoa kilio , alikuwa akijilaumu kukosa uwezo wa kumsaidia Roma”

“Mhmh!.. nimetumia nishati ya ant- matter halafu unasema hujaumia sana , ngoja tuone kama unaweza kubwabwaja baada ya hili pigo”Aliongea Yan Buwen na kunyanyua mkono akitaka kumpiga tena Roma.

“Hapana , Yan Buwen naomba uache”Sauti ya kike ilisikika na alikuwa ni Queen alietoka kwenye ngao na kumpita Roma kwa mbele bila hofu.

“Yan Buwen naomba uache tafadhari , usifanye hivi jamani.. acha kuwa mkatili kiasi hicho unataka kumuua na mtoto wako?”alianza kuongea huku akilia

“Bitch” Aliongea Yan Buwen na kuanza kuandaa pigo la kumkausha Queen.

“Queen!!!”

“Wewe mpuuzi hujafa tu?”Aliongea Yan Buwen.

“Nini?”

“I am calling you a bitch , bitch , bitch …..Unafikiria nakuona kama binadamu, kwangu wewe mwili wako ulikuwa kama kipozeo tu usijifanyishe najali sana kuhusu huyo mdudu alieoko tumboni kwako”Aliongea Yan Buwen.

“Kaa kimya wewe mpuuzi, wewe ni chizi na huna akili ndio maana unataka kuua mtoto wako”Aliongea Omari

“Hahaha unajitekenya….naomba nitangaze hadharani , labda haieleweki , nasema hivi hakuna binadamu ambaye anavigezo vya kubeba mimba yangu, Shenzi labda nikifa na kufufuka ninaweza kufikiria upya”Aliongea kwa jeuri na maneno yalikuwa makali kiasi kwamba yalimnyong’onyesha Queen nakujikuta akikaa chini na kuanza kulia.

Siku zote aliishi kwa tumaini na kujiambia Yan Buwen anaweza kuwa kichaa lakini hawezi kumdhuru mtoto wake , lakini tumaini ambalo alikuwa nalo mpaka hapo alihisi lishafutika.

“Yan Buwen unapoteza muda , ushamuua tayari Monk malizana na hawa waliobaki , malizana na Roma na baada ya hapo tukaimalize na familia yake , hakuna wa kutuzuia kwa sasa”Aliongea Raisi Kigombola.

“Kigombola wewe msaliti usifikirie hilo linaweza kuwezekana kirahisi kama unavyodhani , jeshi letu lipo imara”Aliongea Afande Tozo lakini maneno yake yalipokelewa kama upuuzi na Kigombola na alimwangalia Neema na mtoto wake Donyi.

“Neema njoo huku upande wangu wewe na mtoto wetu, nitakusamehe kwa usaliti ulionifanyia na nitaendelea kukusapoti wewe na mtoto wangu pia”Aliongea kwa kubembeleza akimtaka Neema Luwazo na Donyi kwenda kusimama upande wao , lakini Neema alitingisha kichwa kukataa, hivyo hivyo na Donyi alikataa, aliekuwa mbele yake ni kama hakuwa baba yake , mwanzoni hakutaka kushuhudia akifa lakini kwa ushetani alioweza kuona kwa macho yake hakutaka kabisa kuungana nae hata kama ni baba yake.

“Wewe ni shetani tena zaidi ya shetani , huwezi kunitumia kwa ajili ya faida kama kweli ulikuwa ukinipenda , nakuchukia zaidi ya mara milioni moja, bora Yan Buwen aniue kuliko kuungana na wewe kwenye ushenzi wako”

“Hahaha. Mzee naona mwanamke wako na mtoto wako wamekukataa waziwazi, lakini usiwaze nitahakikisha vifo vyao sio vya maumivu” Aliongea Yan Buwen kwa kebehi.

“Mwanamke ni mwanamke tu na akishapata mwanaume mwingine anaekidhi haja zake anasahau kila kitu , sijali kama atakufa lakini naomba mtoto wangu awe hai”Aliongea na kisha akageukia kundi ambalo lilikuwa limemzuguka wakiwemo baadhi ya mawaziri ambao walikuwa ni mashushu wake serikalini.

“Ambaye haniungi mkono kwa misheni yangu anaweza kupita hapo katikati na kulifuata geti na kuondoka Waziri mkuu kama unataka kuungana na mimi njoo upande wangu , yoyote pia anaetaka kuja huku afanye hivyo na ataendelea kuishi”Aliongea lakini hakuna ambaye alikuwa na ujasiri huo , hawakuwa wajinga , ilimaanisha ambaye angeweza kuondoka hapo ndio ingekuwa kifo chake hivyo waliishia kuangalia chini kama kuku tetea , upande wa waziri mkuu na wengine hakuna ambaye alikuwa na mpango wa kusaliti nchi , waliamua kama ni kufa ngoja wafe kiume.

Kigombola mara baada ya kuona hakuna ambaye anataka kuondoka ,alitabasamu kwa kuridhika na kisha alimgeukia Yan Buwen.

“Tekeleza vifo vya wote ambao wanapaswa kufa leo hii tumalize kazi mapema”

“Haina haja ya kuniambia mara mbili mbili mzee”Aliongea Yan Buwen na palepale aliachia pigo.

“Omarii..!!!”Waliita kwa nguvu.

Roma alijikuta akibung’aa na kushindwa kuchukua hatua mara baada ya Omari kumkimbilia Queen na kuondoka nae , Omari alikuwa na spidi lakini hata hivyo miale ilikuwa na spidi zaidi yake na ile anampakua Queen alipigwa na shoti mgongoni kiasi cha kuchana shati lake ambalo amevaa.

Isingekuwa uwezo wake wa kijini huenda angeyeyuka kama wale wengine, Queen hakuamini kama Omari angemuokoa, hata hivyo alishajichokea na alitaka tu kufa ili kupunguza maiumivu ya moyo.

Alijikuta akimwangalia Omari ambaye alikuwa akiugulia maumivu , hakuamni licha ya kumkataa huyu mwanaume lakini alikuwa tayari kumuokoa kwa kumkinga na mwili wake.

“Omari….Omari kwanini unakuwa mjinga wewe mpumbavu”Alifoka Afande Tozo lakini Omari hakujali hata hivyo alikuwa akijihisi maumivu makali kiasi cha kutaka kupoteza fahamu.

Roma hata yeye alishangazwa na kitendo cha Omari na kukasirika kwa wakati mmoja lakini hakuwa na namna , alichokifanya ni kuita uwezo wake wa kijini na kisha akawakausha wanajeshi watatu wa Yan Buwen na kumuachia wawili wa mwisho Magdalena amalizane nao maana hawakuwa na siraha.

Roma aliamua kumfuata juu Yan Buwen , alijiambia ndio muda muafaka wa kumalizana nae , maana kama hatofanya hivyo kwa ukichaa wa Yan Buwen basi huenda hata taifa kutokuwa salama kama sio dunia nzima na hata hivyo yeye ndio mwenye makosa kupoteza jiwe la kimungu kwa hayawani.

“Hades unatakiwa kuelewa mpaka sasa huniwezi kwa chochote , nina kwenda kuwa mtu mwenye nguvu zaidi duniani mara baada ya kumaliza majini yote husuani Hongmeng, ninaweza kukusamehe leo hii kama tu utajisalimisha kwangu na kuwa mmoja ya watu wangu”Aliongea na kumfanya Roma kujawa na hasira na kukunja ngumi.

“Sina uhakika kama ninaweza kukuua , lakini nakuhakikishia wewe pia huwezi kuniua bila ya kufahamu nani anakupa nguvu , maana najua wewe ni mbwa ambaye unatumika tu kwa ajili ya bosi wako”Aliongea Roma

“Unasemaje?”Aliongea Yan Buwen huku akimwangalia kwa macho makali alionekana kukasirika.

“Nimekosea? , ninaweza kukusifia kwa kuweza kujificha lakini pia umeweza kuwa na uwezo mkubwa lakini naamini kabisa usingefikia hapo ulipo bila kupata msaada kutoka kwa mtu ambaye alinipokonya jiwe la kimungu , Thanatos na Hollygrail”Aliongea Roma , ijapokuwa hisia zake zilimwambia ni Athena lakinni alitaka Yan Buwen akiri wazi , kwanza alishindwa kuelewa kwanini Athena alikuwa akishirikiana na mpumbavu kama Yan Buwen ndio maana alitaka kujua zaidi nia yake.

“Sijui nia yako kwangu kunishambulia lakini naamini moja kwa moja wewe ni mbwa tu unaefanya kazi kwa malengo yao na hao ndio ambao ni maadui zangu ninaowalenga na ninaotaka kumalizana nao”Aliongea na kumfanya Yan Buwen kuanza kupandwa na hasira maradufu kwani alichosikia yalikuwa matusi kwake , ijapokuwa maneno ya Roma yalikuwa ya ukweli lakini yalikuwa yakiuma , aliguswa penyewe.

“Unajua nini wewe mpumbavu , kwanza sitaki hata kupoteza muda kwa kuongea na mpuuzi kama wewe nitakuonyesha leo ni kiasi gani nimekuzidi uwezo , nitakusambaratisha na kubakia vipande vipande na baada ya hapo wanawake wako wote nitawakusanya na kuwapeleka kwenye gereza la mateso kwa ajili ya kuchezewa na kila mwanaume, nadhani nikiyaona machozi yao nitafarijika”Aliongea na palepale jiwe la kimungu ambalo lipo kwenye kifua chake lilianza kutoa miale mingi ni kama lilikuwa likimpongea kwa kuwa na hasira

Roma aliamua sasa kuwa siriasi na aliiita kiwango cha juu cha nishati ya mbingu na ardhi kwa ajili y a kujiweka tayari kukumbana na Anti-matter, hata hivyo alihisi kani kubwa kutoka aliposimama kutokana na msunguano wa nguvu ya jiwe la kimungu.

Mawingu yalianza kujitengeneza na kuashiria mvua ilitaka kuanza kunyesha lakini sio hivyo tu ngurumo za radi hazikuwa kimya pia

Upande wa chini Magdalena aliweza kumaliza misukule yote ya Yan Buwen na sasa macho yake yalikuwa juu akiangalia pambano.

Hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kukimbia kwa kuogopa Yan Buwen anaweza kuwashambulia hivyo waliishia kuangalia kile ambacho kinakwenda kutokea.

Yan Buwen alikuwa na hasira mno , muda ule ule mpira wa shoti ulijitengeneza kwenye mikono yake huku ukizunguka zunguka kana kwamba unaogopa kugusana na kiganja chake .

“Go to hell!”Aliongea kwa sauti na kisha alirusha ule mpira kuelekea aliposimama Roma na palepale ulibadilika kutoka kuwa mpila na kuwa kama miale ya shoti ya umeme , lakini Roma alikuwa na spidi kwani palepale aliweza kutengeneza ngao na kuizuia na kufanya atomu kusuguana angani na kutengeneza mwanga wa rangi tofauti wa kuvutia.

Lakini hata hivyo pigo la Yan Buwen lilimfanya kuhisi maumivu makali maana ilihitajika nguvu kubwa kuweza kudhibiti ngao yake , lakini wakati huo huo kudhibiti ngao iliowafunika Neema na wenzake.

Yan Buwen baada ya kuona Roma kakinga , aliachia pigo lingine na lingine na kudhidi kumsababishia Roma maumivu makali na kuishia kutema damu.

Yan Buwen alitabasamu kwa kebehi baada ya kuona mbinu sahihi ya kumuua Roma ni kushambulia kwa kasi ngao zote mbili , kwani Roma hakuwa na uwezo wa kushambulia zaidi ya kukinga mapigo yake kwasababu aikuwa akijilinda yeye na waliochini yake.

“Roma shambulia na wewe na usikinge tu mapigo yake”Aliongea Magdalena ambaye alianza kukosa uvumilivu na chozi kuanza kumtoka.

“Nimetumia robo tu ya nguvu zangu kushambuia lakini naona upo hoi taabani”Aliongea Yan Buwen na kuachia mapigo mawili kwa wakati mmoja kwa kutumia mikono yake yote , moja alilenga chini kwenye ngao iliowafunika Neema na nyingine alimlenga Roma.

Alishangundua kadri alivyokuwa akishambulia ngao ndio ambavyo Roma anapoteza nguvu na hivyo alitumia mbinu hio hio kuongezea dawa.

Roma alijihisi roho yake inataka kuacha na mwili wake kwa maumivu ambayo anayasikia, muda huo ambao alipaswa kuwa Honeymoon ndio muda ambao alikuwa akiugua , tena hata nguo za harusi hakuvua.

“Daah..Roma anateseka kwa ajili yetu , sijui kwanini tukaingia mkenge na kuja hapa”aliongea Afande Tobwe huku akijidharau kwa kutoweza kufanya chochote , kauli yake ilisikika na baadhi ya watu waliokuwa wakimsapoti Kgiombola na kuishia kucheka.

Roma alikuwa ashaita uwezo wake wote wa nguvu ya kijini katika levo ya kupita dhiki na alijiambia kadri ambavyo atakuwa anakinga mapigo ya Yan Buwen basi anaweza kushindwa kuendelea kuhimili na kupoteza uhai.

Kuna muda alitamani hata kupigwa na radi kama ilvyotokea wakati akipambana na Poseidon na huenda angejitoa muhanga kufa na Yan Buwen moja kwa moja , lakini hata hivyo dalili ya radi ilionyesha kuwa mbali sana licha ya kwamba wingu kubwa lilikuwa limetanda angani.

Tegemeo lake la mwisho ni kuchukua ile dhana ya Ganyua ili kujikinga nayo kama ngao halafu atumie nguvu ya kijini kuwakinga waliochini yake , aliamini ndio mbinu pekee ambayo ingepunguza nafasi ya kushindwa pambano lakini pia maumivu.

Roma aliita kwenye mikono yake , lakini muda ule na Yan Buwen aliachia pigo kubwa kuliko la mwanzo na ile dhana palepale ilitengeneza ngao yenyewe , lilikuwa kosa kubwa sana , kwani ngao aliotegneneza ilionyesha kutokuweza kuhimili vizuri na palepale ilijizima yenyewe na kulitokea mlipuko ambao haukuwa wa kawaida ni kama anga lilikuwa likitaka kudondoka na kufanya watu wote kuziba masikio.

“Romaa…!!!!!”Omari na Magdalena ndio walioweza kushuhhudia Roma akipigwa pigo takatifu na Yan Buwen na kupoteza balansi na kudondoka chini kama embe.

Roma alijitahidi kuiweka akili yake sawa asipoteze fahamu lakini mwili haukutaka kwani maumivu yalikuwa makali mno na palepale alianza kuona nyota nyota na hatimae ukungu na mwili wake ulipoa kabisa na akalegea na kutua chini kama furushi.

ITAENDELEA. IJUMAA - WATSAPP 0687151346
 
Duuuuh mpka ijumaa
 
Roma kwishney
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…