Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 495.
Roma alishangazwa na kupatwa na huzuni ya taarifa hio ya kifo kwani siku hio hio ndio walipanga kwenda yeye Edna na Lanlan kumtembelea, kwao ilikuwa ni kama wamechelewa kwenda , lakini hata hivyo hakujilaumu sana kwa kutowahi kwenda kumuona.
Mzee Atanasi ni moja wapo ya wazee waliokula chumvi nyingi na alikuwa akikaribia kutimiza miaka mia moja na moja na kwa uzito wake ndani ya serikali ya Tanzania ni sahihi kuitwa babu wa taifa.
Ndio mwanajeshi pekee aliebaki ambaye alipigania uhuru wa Tanzania pamoja na Raisi Nyerere.
Roma hakuwa na haraka ya kwenda moja kwa moja msibani , alitaka kwanza kumaliza kilichomfikisha hapo na kisha ndio arudi nyumbani na kuelekea huko , ile safari yao ya kwenda kwa ajili ya kusalimia iligeuka na kuwa safari ya kwenda msibani.
Roma baada ya kukata simu kwa kumpa mama yake pole aliwageukia Diego na kuwapa taarifa hio ya msiba na Diego na Bram walimpatia pole.
Roma aligeukia kwa mara ya pili picha iliokuwa ikionekana kwenye skrini , picha ya mwanaume aliefahamika kwa jina la Bikindi , alikuwa ni baba mzazi wa Lekcha na Roma alimkumbuka kwasababu ni moja ya wanasayansi wa Zeros organisaiton aliowaua.
“Mfalme Pluto unamfahamu huyu mwanaume?”Aliuliza Diego na Roma alitingisha kichwa kuashiria anamjua.
“Mmefanikisha kuchunguza taarifa za Joseph Bikindi za hivi karibuni”
“Ndio mfalme Pluto kwa taarifa tulizoweza kupata kutoka Rwanda mpaka miezi michache iliopita alikuwa mkufunzi wa chuo kikuu cha taifa lakini kwa wiki kadhaa sasa ameripotiwa kutoonekana chuoni bila ya taarifa”.
“Endeleeni kumchunguza kwa ukaribu zaidi na sura yake iunganishe na mfumo wetu wa ‘facial recognition’ ili kama itatokea akiwepo Tanzania tuweze kutambua mara moja”Aliongea Roma huku akipata hisia huenda Lekcha alikuwa Tanzania kwa kutafuta namna ya kulipiza kisasi na kwa muda huo ambao Kizwe alionekana kutokuwa wa kawaida aliamini huenda wapo wote na wanajiandaa na mipango ya kulipiza kisasi , hakusahau na Denisi alikuwa hivyo hivyo tu ndio maana alihitaji kuchukua tahadhari mapema.
Jambo lingine ambalo lilimfanya kuwa na wasiwasi ni juu ya Athena ,tokea apewe cheo cha Hades hakuwahi kujionyesha kwake na alikuwa akijua ana mzunguka lakini hakuwa akijua sababu ni ipi ,lakini alijiambia maadamu yupo hai basi kuna siku tu wataonana na atathibitisha maswali yake yote.
“Vipi kuhusu uchunguzi wa Chriss mlikamilisha?”
“Mfalme Pluto taarifa za Chriss imekuwa ngumu sana kuzipata na mpaka sasa hatujapiga hatua lakini kuna jambo moja tu ambalo tulifanikiwa kupata”
“Mmepata nini?”Aliuliza Roma kwa shauku na Diego alitoka ndani ya chumba hiko na ndani ya muda mfupi aliweza kurudi na mfuko wa plastic ambao ndani yake ulionekana kuwa na mkufu uliofungwa na kishaufu cha madini ya almasi.
“Huu ni…”
“Ni mkufu ambao unaonyesha Chriss alikuwa mwanachama wa Freemason”Aliongea Diego na kumfanya Roma kuchukua na kuangalia vizuri na kweli aliweza kugundua maana ya mchoro uliokuwa kwenye kishaufu(Pendant).
Ijapokuwa sasa ameweza kuanza kupata ukweli wa Chriss alikuwa akitokea jamii ya siri ya freemason lakini ilikuwa ngumu kwake kuweza kuamini kama watu wa jamii hio ya siri ndio walitaka kumuua mke wake na moja kwa moja alijua huenda majibu yapo kwenye mchoro.
Roma ilibidi kwanza amuelezee Diego na Bram kile ambacho alikuwa akitambua kuhusu Chriss.
“Mfalme Pluto hata sisi tunashindwa kuelewa kama Chriss alikuwa mwachama wa Ant- illuminat”
“Kwanini mnaamini hawezi kuwa mwanachama unajua taarifa zote za umoja huo?”
“Ndio mfalme Pluto najua taarifa zote zinazohusiana na umoja wa ant- illuminat na baadhi ya mipango yao ya mbeleni japo mpaka sasa hakuna uthibitisho kwani ni taarifa ambazo ni kama uzushi”
“Ni taarifa gani ambazo unafahamu?”
“Mfalme Pluto ushawahi kusikia kuhusu mpango TASAC?”
“Mpango TASAC!, si huu ulioanzishwa na serikali ya Urusi kuyafanya mataifa ya Afrika kutounga mkono wala kukataa vamizi anazozifanya Raisi wa Urusi nchini Ukraine?”
“Ndio mfalme Pluto lakini ni ngumu kusema mpango TASAC umeanzishwa na Urusi”
“Kwanini?”
“Taarifa za siri za daraja la tatu zinaonyesha mpango TASAC waanzilishi ni Ant- illuminat”Aliongea na kumfanya Roma kuguna ilikuwa habari mpya kwake na huenda angekuwa anafatilia sana maswala ya siasa angekuwa ashaijua , huenda ilikuwa sahihi kwa Christen kumwambia hayuko ‘flexible’ kama mtangulizi wake”
“Uzushi mwingine unaoenezwa kuhusu Ant-illuminat ni juu ya mataifa ya kiarabu kuwekeza zaidi katika mataifa yalioendelea ya kimagharibi katika nyanja ambazo zinagusa moja kwa moja hisia za watu mfano kwenye vilabu vya mpira na kadhalika”Aliongea Bram.
“Na pia ndio kinara wa mapambano ya sarafu ya Dola ya kimarekani kutaka kuiangusha”Aliongezea Diego.
“Inaongekana mnapenda sana uzushi”
“Your Majesty if no Somke no Fire “Aliongea Diego akiingiza msemo ambayo unaoendana na ule wa kiswahili usemao yasemwayo yapo na kama hayapo yaja au penye moshi hapakosi moto.
Roma hakutaka kukaa sana hapo kwani kuna msiba ambao ulikuwa ukimuhusu na mpango wake ni kuunganisha kwanza msibani kujua kile kinachoendelea na kujua taratibu zinazofuatia, hivyo alitoa msisitizo wa usalama zaidi wa watu wake wa karibu kuzingatiwa hususani muda huo ambao alijua na Lekcha ni adui yake mpya alieingia kwenye orodha.
Akiwa garini alijaribu kuwasiliana na mke wake kumuulizia kama kapata taarifa na ilionyesha Edna alikuwa na taarifa na alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kufika msibani pamoja na Bi Wema na Roma alimwambia angemkuta huko huko kwani anatangulia.
Baada ya kufika Masaki nyumbani kwa Tajiri Azizi aliweza kuona watu wengi waliokuwa wakiingia ndani ya nyumba hio na kutoka na pia kulikuwepo na baadhi ya waandishi wa habari.
Kwa haraka haraka Roma alishajua msiba huo ni wa kitaifa hivyo wageni wengi lazima wangefika kutoa salamu zao za pole.
Roma hakuingiza gari ndani ilibidi apaki pembeni kwa kuhofia ndani kusingekuwepo na nafasi na baada ya kuegesha aliingia moja kwa moja ndani na alikuta tayari maturubai yashasimamishwa pamoja na viti ambavyo vilikuwa vikipangwa.
Mtu wa kwanza kuonana nae alikuwa ni Kassimu mtoto mkubwa wa tajiri Azizi ambaye alikuwa akipokea wageni na alimkaribisha Roma na kumpeleka kuonana na mama yake pamoja na wanafamilia wengine.
Dakika chache mbele na Edna aliweza kufika na kutoa pole , msiba haukuwa na vilio sana zaidi ya sura za majonzi tu huenda ni kwasababu mzee huyo kaishi miaka mingi na muda wake umewadia hivyo alipaswa kutangulia mbele za haki .
Ratiba ya msiba ilikuwa ni siku inayofauta mwili kuagwa katika viwanja vya Karimjee na kisha safari ya kuelekea Kilosa kijijini ingeanza ili kumpumzisha Babu Atanasi.
Katika watu ambao walikuja kutoa salamu za pole ni Samweli Nguruma kiongozi wa kundi la ZoaZoa na ilikuwa ni kama amekuja kumtafuta Roma kuongea nae.
Roma alishawahi kuwasiliana na bwana huyo kwa kupitia simu ila hakuwahi kukutana nae ana kwa ana na siku hio ndio waliweza kufahamina kwa mara ya kwanza.
Samweli Nguruma baba yake na Benadetha alikuwa ni kama bosi mtu mwenye kitambi na kipara cha nywele na ilikuwa ngumu kuamini ndio ambaye alikuwa akijihusisha na biashara za magendo lakini hata hivyo Roma hakutaka kumtoa dosari ukizingatia hata Rose hakuwa na mwonekano wa kuongoza kundi la Tembo.
“Mr Roma unamwonaje mtoto wangu Benadetha?”Aliuliza Samweli Nguruma na kumfanya Roma kushangazwa na swali hilo.
Ilikuwa ni saa za mwisho mwisho za kuaga mwili ili safari ya kuelekea Morogoro ianze ndio maana Roma alishangaa.
“Kwanini unauliza hivyo mzee?”.
“Nataka kujua maoni yako, umefanya nae kazi kwa muda mrefu kidogo hivyo sio dhambi kutoa maoni yako unavyomuona na tabia yake kwa ujumla”Roma ijapokuwa muda huo aliona hakupaswa kujibu swali hilo kutokana na muda kutokuwa mzuri lakini aliona ni kheri kujibu kile anachokiona kwa Benadetha.
“Namuona kama msichana mzuri mwenye sheria zake na inaonyesha ashatambua mapema kama mwanamke anataka nini katika maisha yake”Alijibu Roma na kumfanya Samweli nguruma kutabasamu.
“Upo sahihi Benadetha ni binti mwenye msimamo na mara nyingi uwezo wake mkubwa wa kujielewa unanifanya hata mimi baba yake kumhofia”
“Hongera kwa malezi, kwa ninavyomuona atakuja kuwa na maisha yenye furaha sana mbeleni”
“Furaha ya mwanamke inakamilika pale akiridhika na kila kitu kunachomzunguka, asipo ridhika ataishia kutangatanga kukidhi haja ya moyo wake”Aliongea
“Ndio maana nikasema Benadetha atakuja kuwa na furaha kwasababu kama mwanamke ukishafahamu kwenye maisha unataka nini mapema ni rahisi pia kuridhika”
“Upo sahihi Mr Roma lakini ushawahi kujiuliza kwanini kipindi Benadetha alipopelekwa kituoni na mkeo nilitaka wewe ufanye kazi ya kumtoa?”
“Kwanini?””
“Nilijua tayari mkeo ashafahamu hisia za Benadetha kwako”Aliongea na kumfanya Roma ashangae.
“Mzee labda utakuwa haujamfahamu Benadetha vizuri , mimi na yeye hatuna ukaribu huo na hata kama Benadetha anipende mimi kama mwanaume siwezi kumpokea kwani tayari nina mke”Aliongea Roma bila ya wasiwasi.
“Haha.. Mr Roma nimekutana na vijana wengi ila ujasiri wako na kujiamini ni wa viwango”
“Na wewe pia ujasiri wako ni wa viwango kumnadi mtoto wako wa kike kwangu ilihali tayari nina mke sio jambo la kawaida kabisa kwa tamaduni za kiafrika”
“Upo sahihi imenichukua ujasiri kuongea na wewe kuhusu maswala ya binti yangu na nimetidhika pia kama huna nia ya kumfanya kuwa sehem ya wanawake wako”Aliongea na kumfanya Roma kumchanganya na kuona huenda habari za yeye kuwa na wanawake wengi zilikuwa zikifahamika kwa watu wengi.
*********
Tokea kumalizika kwa maziko ya Babu Atanasi siku zilienda haraka haraka mno na katika watu ambao walikuwa wako bize basi ni Roma ,kuna muda alijiambia uwepo wa Lanlan kidogo ulikuwa umesaidia sana kupunguza migogoro yake na Edna.
Kwani kitendo cha Lanlan kung’ang’ania kulala na mama yake ilimpa nafasi Roma ya kila usiku kutembelea wanawake wake kwa zamu na hilo pia lilisaidia sana kuyafatilia maendeleo yao.
Vidonge ambavyo aliweza kuvipata baada ya kuwaua watu wa hongmeng vilisaidia sana katika kumfanikisha Rose kupanda levo na Roma aliona kabisa muda si mrefu Rose angefanikisha kupata ufunuo wa nguvu ya mbingu na Ardhi jinsi ya kutumia elementi zote za dunia.
Katika mafunzo ya kijini kila mmoja alitofautiana na mwenzake katika kupata ufunuo wa namna ya kutengeneza maajabu kwa kutumia elementi za dunnia na hicho ndio ambacho kilimfanya Roma kupatwa na hamu kubwa ya kuwaona wakifikia levo ya kupata ufunuo.
Mage na yeye hakuwa mbali sana na ilionyesha juhudi zake zilionyesha manufaa kwani alianza kuelewa levo ya nusu mzunguko kikamilifu na Roma aliona kabisa muda si mrefu angeweza kuingia levo ya mzunguko na alijiambia kama atafanikisha mpango wake wa kutengeneza vidonge vyenye nguvu basi huenda ndani ya mwaka mmoja kila mmoja anaweza kuingia kwenye levo ya Nafsi na matumaini ya kuweza kupata mtoto yangekuwa juu.
Upande wa Amina msukumo wa ndani zaidi kujifunza mafunzo hayo ni kwa ajili ya kutunza urembo wake na kufanya tahajudi muda mrefu haikuwa kazi kubwa kwake, ,ijapokuwa maendeleo yake yalikuywa ya taratibu lakini alileta matumaini na hata hivyo Roma alifurahi kuona Amina alikuwa mzoefu wa mazoezi ya Yoga na hilo ndio lilirahisisha.
Neema Luwazo ndio ambaye alikuwa akijifunza kwa fujo sana na tamaa kubwa ya kufikia levo za juu na Roma aliona huenda ni kwasababau alikuwa akiukaribia utu uzima ndio maana alitaka kupanda levo kwa haraka ili asiendelee kuzeeka na kubakia na mwonekano wa ujana.
Lakini licha ya fujo alizokuwa nazo za kutaka kujifunza maendeleo yake yalikuwa ni ya taratibu mno kulinganisha na wengine wote kutokana na utu uzima wake kwani ilikuwa rahisi kwa vijana kujifunza na kupanda levo kwa haraka tofauti na watu wazima na Roma ilibidi achukue jukumu la kumtuliza.
“Roma nimeachia majukumu kabisa ya kampuni kwa Alhaji kwa ajili ya kujifunza”Aliongea Neema usiku Roma alipomtembelea.
“Umefanya vizuri lakini unatakiwa kwelewa mbinu hizi huwa zinaendana na utulivu wako wa akili ukiwa na tamaa ya kupanda levo kwa haraka utakosa utambuzi wa kunyaka kila viashiria vinavyokujia wakati wa kufanya Tahajudi na ndio maana nakushauri usichukulie sana hili swala siriasi lifanye kama ni moja wapo ya starehe, kama unavyokaa kwenye Jakuzi ukiwa umeshikilia glasi ya mvinyo ukiyafurahia mafanikio yako”Aliongea Roma nakumfanya Neema kutabasamu.
Na alfajiri Roma alijaribu kufanya nae mafunzo na sasa angalau aliona akili yake ilikuwa imetulia , ilionekana maneno yake ya jana usiku yalikuwa yamefanya kazi.
Upande wa Edna na Nasra maendeleo yao yalikuwa ya kinyonga lakini yalioleta mabadiliko kwenye miili yao.
Zamani Edna alikuwa akimhofia Lanlan kumrukia kutokana na uzito wake lakini kwa kipindi chote alichokuwa akichukua mazoezi alikuwa ameimarika na kumudu hata uzito wa Lanlan vizur.
*******
Ni baada ya wiki moja kupita hatimae Omari na Queen waliweza kufunga ndoa yao rasmi kwa tamaduni za dini ya kiislamu ambazo zilimtaka Queen kubadili dini jambo ambalo Mzee Alex hakupinga, hata hivyo ni Omari pekee ambaye alionyesha kumpenda mtoto wake kwa mapenzi ya dhati licha ya kwamba alikuwa mjamzito hivyo hata swala la Queen kubadili dini kuwekwa mezanni kwake hakuwa na kipingamizi.
Saa tano na nusu za usiku ndio muda ambao Roma na Edna walirudi kutoka kwenye sherehe ya harusi hio ya Omari na Queen na wakati Roma anaingiza gari ndani ya geti alishangazwa kuona nyumba bado inatoa mwanga wa taa kutokea sebuleni kwani kwa muda huo aliamini wanafamilia wote wangekuwa washalala.
Roma usiku huo akiwa njiani alikuwa akipanga kwenda kuburudika na mke wake Edna usiku kucha kwa kuamini muda huo Lanlan angekuwa tayari amekwisha kulala na Qiang Xi.
Lakini sasa ile wanaingia sebuleni lile tumaini lake lote lilipotea baada ya kumkuta Qiang Xi na Lanlan wakiwa wamekaa sebuleni na hata Edna mwenyewe alishangaa kuwakuta hapo kwani muda ulikuuwa umeenda.
“Qiang mbona mpaka muda huu Lanlan hajalala na asubuhi anatakiwa kuwahi kuamka”
“Madam nimejaribu kumfanya alale lakini hana usingizi na anasema anakusubiria”Aliongea Qiang Xi huku akionyesha hali ya uchomvu ilionekana alikuwa akijitahidi kuwa macho kwasababu ya Lanlan na alikuwa amechoka.
“Lanlan kwanini unashindwa kulala?”
“Mama sipati usingizi , Lanlan anataka kulala karibu na mama”Aliongea na kumfanya Roma akunje sura alijiambie kama watoto wake watakuja kuwa kama Lanlan basi maisha yake yangekuwa magumu sana.
Edna alimuonea huruma kuona alikosa usingizi na swala hilo lilikuwa likimsumbua kichwa namna ya kulitatua kuishia kujiuliza kama siku nyingine asingekuwepo na Lanlan angelala vipi.
Upande wa Roma alishajua kwanini Lanlan alikuwa akikosa usingizi , sababu ilikuwa ni kutokana na damu yake kuchemka kila wakati na kumfanya kukosa utulivu wa akili ndio maana alikuwa akikosa usingizi na njia pekee ambayo aliona huenda ingemsaidia Lanlan ni kumfundisha ya mbinu ya kimaandiko ya urejesho ili aweze kudhibiti uwezo wake lakini alimuona Lanlan ni mdogo na hata kama angejaribu kumfundisha kutamka maneno ya maandiko na kuyageuza kuwa nguvu ingekuwa ngumu kwake.
Hivyo suluhisho la muda mfupi ambalo aliona lingefaaa kwa muda huo ni Lanlan kuendelea kulala na Edna mpaka atakapogundua namna ya kumsaidia kupata usingizi bila ya uwepo wa Edna.
Roma mara baada ya kurudi kwenye chumba chake akijiandaa kwenda bafuni kujimwagia maji alale simu yake ilitoa mlio wa ishara ya mwaliko wa mtu kumpigia kwa njia ya Vidio Call.
Baada ya kuangalia inatoka kwa nani aligundua ni Sauron na alijikuta akiwa na shauku ya kumsikia maana ni kama mwezi unakaribia kuisha tokea ampatie Sauroni kazi ya kusambaza vijana kutafuta maeneo walioishi binadamu enzi za kale , maeneo ambayo yalifanikisha ukuaji wa mila na tamaduni za kijamii za mwanzo kabisa(Ancient Civilization) lakini baada ya muda maeneo hayo yakatelekezwa , aliamini upatikanaji wa maeneo hayo ingekuwa rahisi kwake kuweza kupata mimea anayojitaji itakayosaidia katika utengenezaji wa vidonge vya kijini.

SEHEMU YA 496.
Licha ya mwonekano wa kutisha kutokana na mtindo wake wa nywele nyingi alizokuwa nazo kwa upande wa Roma alikuwa ashamzoea na kumuona mtu wa kawaida lakini kwa mwingine huenda mwonekano wa Sauroni ungemkosesha amani hususani wakati anapokuwa siriasi.
Ilionekana muda huo Sauroni upande wa kwao kulikuwa ni mchana maana alionekana ndani ya ofisi huku kwenye meza yake kukiwa na mafaili mengi, huku yeye mwenyewe akiwa amevalia miwani ya kusomea.
Roma mara baada ya kupokea simu na kubadilishana salamu na Sautoni ilibidi amwambie aende moja kwa moja kwani alitaka kulala.
“Mfalme Pluto nishakutumia mafaili yanayohusiana na taarifa ulizo omba kupitia barua pepe yako , tumefanikisha kupata maeneo nane yanayofanana na sifa ulizotupatia”Aliongea Sauroni
“Asante sana Sautoni kwa juhudi zako zilizopelekea kufanikisha , vipi kuna changamoto yoyote uliweza kupata?”
“Sijapata changamoto kubwa mfalme Pluto lakini nina shauku ya kufahamu kwanini unahitaji taarifa za hayo maeneo kwani kwa uelewa wangu hayo maeneo sasa hivi hayakaliwi na binadamu na huenda hata uwepo wa hio mimea ni kwasababu hio na binadamu wa kawaida ambaye angesafiri kwenda kwenye hayo maeneo asingeweza kutoka hai”Aliongea na kumfanya Roma kucheka kidogo
“Maeneo ambayo watu waliishi na sasa hawaishi ndio ambayo ninayatafuta kwani naamini inaweza kufanikisha kupata kile ninachohitaji , najua una shauku lakini nitakuelezea siku nyingine kwasasa taarifa hii ulionitumia nitaipitia na kuanza na mikakati ya kuelekea huko”Aliongea Roma na Sauroni aikubali na kisha akakata mawasiliano
Roma alighairi kwanza kwenda kuoga na kuanza kupitia taarifa ambazo ametumiwa na Sauroni na ilionekana ziliandikwa vizuri ili kueleweka kwa urahisi, ni ‘Document’ ambayo ilikuwa na peji nane ambazo zilikuwa zikielezea maeneo husika ambayo yalikuwa yakikidhi vigezo.
Na mpaka anakuja kumaliza alikwisha kupata sehemu ambayo aliona inafaa kuanzia kutafuta mimea hio lakini kwakuwa hakuwa mzoefu sana alitaka kwanza kusikia maoni kutoka kwa Rufi na kwasababu muda huo ulikuwa ni usiku sana aliona angewasiliana nae asubuhi.
Siku iliofauta jambo la kwanza ilikuwa ni kuwasiliana na Rufi na akamtumia na faili la taarifa alizotumiwa na Sauroni na wote walijikuta wakiachana na baadhi ya maeneo yalio orodheshwa kwa sababu za aina moja, waliachana na eneo la Eveglades ambalo lipo kusini mwa Marekani , Msitu wa Panama , msitu wa Amazoni na maeneo mengine na wakaja kuchagua eneo lililofahamika kwa jina la Arnhem Land ambalo lipo kaskazini mwa bara na nchi ya Australia.
Arnhem Land ni eneo ambalo walichagua kutokana na historia yake kwani sio tu kwamba miaka ya hivi karibuni halikukalika lakini miaka mingi iliopita lilikaliwa na watu wa asili zaidi wa nchi ya Australia na ilikuwa ni eneo ambalo ni kama tamaduni nyingi zilizaliwa na hivyo ndio vigezo ambavyo Rufi alipendekeza.
Eneo ambalo lilikaliwa na watu wa asili na kuzaa tamaduni na mila ndio ambalo lingekuwa na mkusanyiko wa nguvu nyingi za kiroho ambazo zingefanikisha upatikanani wa malighafi za Alchemy.
Roma alikuwa akielewa Australia ilikuwa kusini mwa ncha ya dunia na kwa mwezi huo wa nne kwenda wa tano ni kipindi cha Vuli na kama angevuta muda vuta muda basi mwezi wa sita ingekuwa ni hatari zaidi kwenda kwani ingekuwa ni kipindi cha baridi kali na kwasababu hakuwa akienda mwenyewe alitakiwa pia kuzingatia hali ya kiafnya ya Rufi na ndio maana aijiambia ni kheti kuharakisha kufanya safari na kwenda kutafuta hio mimea na kuanza harakati zingine.
Rufi alikuwa ashakubali kuongozana nae kwani hakuwa na shughuli ya maana ya kufanya Tanzania na maisha yake yalikuwa ya upweke sana na aliona ingekuwa kama utalii kwake kusafiri mpaka Australia.
Tatizo ambalo Roma aliona ni changamoto ambayo alipaswa kuitatua ni kwa mke wake , alijua akimuaga kwamba anaelekea Australia na Rufi angemuwekea ngumu lakini hata hivyo aliona lazima akubaliane na matakwa yake kwani anachokifanya sio kwa faida yake mwenyewe bali ni kwa faida ya wote.
Usiku baada ya Roma kupata chakula aliona ndio wakati muafaka wa kumweleza Edna mpango wake wa kusafiri na Rufi na Roma alimsubiria kwanza Edna amalize kumwandaa Lanlan kwa ajili ya kulala na ndio aongee nae.
Roma mara baada ya kukaa chini na kumuelezea anachopanga mwanzoni hakushangazwa na taarifa hio lakini Roma alipokuja kusema anataka kwenda na Rufi alihisi hatari.
Tokea aanze kuwa na ukaribu zaidi na mume wake alikuwa mwangalifu mno hakutaka Roma aongeze mwanamke kabisa na ndio maana hakutaka mazoea kati ya Rufi na Roma kuongezeka kwani mwisho wake usingekuwa wa kheti kwake.
“Najua unaweza kuona sio sawa mimi kwenda na Rufi lakini hili ni swala ambalo napaswa kulifanya na hata hivyo Arnhem sio sehemu ambayo ipo kiburudani ni kama gereza na kila kitu ni msitu hivyo kwenda na Rufi kule ni kama nampeleka kuzimu, hivyo mke wangu usiwe na wasiwasi na toa ruhusa yako niweze kuondoka nae”Aliongea Roma kwa unyenyekevu baada ya kuona mabadiliko yake.
Edna alifikiria na alionekana kama mtu ambaye amechanganyikiwa, moyo wake siku hizo za karibuni ulikuwa tofauti na zamani, alikuwa tayari kuona Roma akiendelea na wanawake wale wale aliokuwa nao na asione wivu lakini kumuona mwaamke mwingine mpya kwake ilimuuma na kumuogopesha kwa wakati mmoja na hata yeye mwenyewe alijishangaa na hata Roma alivyoweka wazo hilo akili yake ilimwambia na yeye aungane nae ili aweze kumlinda vizuri , lakini alifikiria uwepo wa Lanlan aliona asingeweza kuongozana na Roma na kumuacha peke yake.
Wazo moja tu ambalo lilimjia katika akili yake na kuona ndio njia mbadala ni kumteua mtu mwingine wa kuongozana nae kwenda huko na ingekuwa rahisi kuzuia mahusiano kuibuka zaidi na zaidi
“Nimekubali unaweza kwenda nae lakini lazima uende na mtu mwingine pia”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.
“Mtu mwingine kwenda nae sio tatizo kwangu , nani unaona anafaaa kunisindikiza?”
“Mage”Aliomngea akiwa ni mwenye sura iliojaa usirias na kumfanya Roma moyo wake kupiga kite , alikuwa na mahusiano na Mage lakini alikuwa akiyafanya siri Edna asifahamu.
“Unashangaa nini Mage ndio mtu pekee ambaye unaweza kwenda nae ningewaruhusu mwingine lakini kwa walivyokuwa wadhaifu kwako wasingeweza kukuzuia kufanya jambo la kishenzi?”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa.
Roma alikuwa na mahusiano na Mage lakini hakuwahi luyaweka wazi na ndio maana alikuwa kwenye mshangao bara baada ya Edna kutaja mtu wa kuongozana nae kwenda Australia kuwa Mage, hali hio ilimfanya kuvhanganyikiwa yeye mwenyewe kwa kuona Edna alikuwa akifahamu siri yake halafu alikaa kimya.
"Mbona uko hivyo au Mage hafai ?"
"Sio kwamba hafai lakini kuna ulazima wa kutangulizana na mwanamke?"
"Ndio nataka utangulizane na mwanamke tena mwanamke huyo akiwa Mage ndio mtu pekee ambaye anaweza kukuzuia usifanye ujinga na Rufi na ndio sharti langu"Aliongea
"Edna ulifahamu lini?"
"Kuhusu nini?"
"Mimi na Mage tuna mahusiano" Aliongea Roma kwa ujasiri lakini kwa hofu ndani yake na swali lake lilimfanya Edna kucheka kidogo kwa uchungu.
"Hilo swali muulize Mage mwenyewe atakuwa na majibu" Aliomgea Edna na kisha hakutaka mazungumzo zaidi na kuondoka kwenye chumba hiko cha kujisomea na kumuacha Roma bado akiwa kwenye sintofahamu.
Ni kweli alikuwa na mahusiano na Mage lakini siku zote alikosa ujasiri wa kumuweka wazi Edna , lakini alishangaa Edna kutambua juu ya hilo bado lakimi aka kaa kimya bila ya kuzungumza.
Roma alijiuliza Edna alifahamu lini maana kama ingekuwa ni siku hio basi huenda angemnunia siku nzima lakini ajabu walikuwa sawa na hata siki yao iliisha bila shida.
Ila kitendo sasa cha Edna kuondoka wakiwa hawajamaliza mazungumzo alijua lazima angekuwa na hasira na yeye kutokumuambia ukweli lakini hata hivyi asingejuwa namna ya kujitetea kama hajui ni lini ameweza kujua ukweli.
Roma hapohapo aliona majibu ayapate kuroka kwa Mage mwenyewe , muda ulikuwa umeenda lakini alijua lazima Mage atakuwa macho na kweli baada ya simu yake kuita muda mfupi ilipokelewa haraka.
"Babe Mage mbona kama ulikuwa ukisubiria simu yangu"
"Mh ..! Roma vipi kuhusu Edna"
"Edna ana nini?"
"Mama leo kaharibu kila kitu"
"Kaharibu nini??"
"Sijui kaongea nini na Mkeo ila kamwambia kuhusu sisi baada ya Magdalena kakataa mchumba anaetaka kumuoa...."
Kwa maelezo ya Mage ni kwamba mtoto wa waziri wa sayansi na teknolojia afahamikae kwa jina la Jumbe alifika nyumbani kwa Mage na kuweka nia yake wazi ya kutaka kumuoa Magdalena jambo ambalo lilipokelewa kwa mikono miwili na Mama T.
Mwanamama huyu alikuwa ashachoshwa kuona watoto wake wa kike wakikosa ndoa ilihali wakina mama ambao ni marafiki zake watoto wao walikuwa wakiolewa na kuoa kwa sherehe kubwa na yeye kuishia kutoa michango pekee.
Na kilichompa shida zaidi ni kila mara alipofikiria Mage hawezi kuolewa tena kwa kuamua kuwa mchepuko wa Roma jambo ambalo hata mume wake alilibariki hivyo tumaini lake kubwa ilikuwa ni kwa Magdalena.
Alielewa watu wakiona Mage hajaolewa wangemnyooshea vidole na kumsema lakini kwasababu ilikuwa ni kwa ajili ya furaha yake hakutaka kumzuia lakini jambo hilo hilo hakutaka kuona likitokea kwa Magdakena pia na ndio maana Jumbe alupoweka nia yake wazi ya kutaka kumuoa mtoto wake alipokea taarifa hio kwa mikono miwili.
Lakini sasa kilichomshangaza ni baada ya Magdakena kukataa akisema hawezi kuolewa na Jumbe kauli ambayo ilimfanya kuhisi uchizi.
"Magdalena kama humtaki Jumbe inamaana tayari una mchumba kama ni hivyo mlete tumuone na nikiridhika nae nitakuruhusu uolewe nae" Aliongea Mama na kumfanya Mage aliekuwa amekaa upamde wa kushoto kushindwa kuongea chochote na kumuonea huruma dada yake kwani alikuwa akijua kike kilichokuwa kikiendelea kwenye moyo wake.
"Mama sina mchumba ila sipo tayari kuolewa na Jumbe" Alijibu Magdalena na kumfanya Mama T kushindwa hata kuelewa watoto wake wamekumbwa na nini , kwenye maisha ykje alijitahidi kuwalea kimaadili na kutegemea waje kuolewa na kuwa na furaha kakini imegeuka kuwa tofauti .
"Mume wangu mbona huongei chochote jamani hawa watoto wanataka kunitia uchizi?"
Afande Tobwe alikosa cha kusema kabisa kwani alikuwa ashajua muda mrefu sababu ya Magdalena kukataa ndoa na Jumbe , alikumbuka vizuri siku ya Roma alipokuwa akipambana na Yan Buwen namna ambavyo Magdalena alitaka kumuokoa Roma kwa kujitoa Muhanga yeye mwenyewe uhai wake.
Kwanzia kipindi hiko alikuwa akishindwa kujua tatizo la Magdakena linaisha vipi , kwenye maisha yake licha ya kuwa mwanajeshi likija swala ka familia yake alikuwa akizingatia zaidi watoro wake waje kuishi na furaha na ndio maana hata Mage alipo onyesha kuwa na mapenzi na Roma hakusita kumruhusu licha ya kujua Roma ana mke tayari na mwanae angekwenda kuwa mchepuko tu, lakini swala la Magdalena ilikuwa ngumu kumruhusu kuwa na mahusiano na Roma na wakati huo na pacha wake akiwa na mahusiano na Roma.
Jambo hilo kama angeruhusu jamii isingemuelewa na sio hivyo ru hata dini yake ilimzuia kuruhusu kitu kama hiko.
"Magdalena kama huna mahusiano, Jumbe anakufaa usikatae , najua kwa zama za sasa wazazi hawapaswi kuwachaguliwa watoto wao wachumba lakii siku zote mzazi anamuombea mtoro wake kuwa na furaha hivyo kuelewa ni kipi bora kwako , Jumbe anakupenda hivyo hata kama humpendi utajifunza"Aliongea Afande Tobwe kwa usiriasi na kisha akaamka na kuondokaneneo hilo la sebuleni.
Huku nyuma akiacha sura ya Magdalena kuwa katika hali isioelezeka , alitarajia baba yake kumuunga mkono lakini akaishia kumkandamiza kwa.kusimama upande wa mama yake.
Wakati wa mchana Edna alipofika dukani kwa ajili ya kutafuatilia mwenendo wa mauzo ya mavazi alioingiza sokoni kupitia kampuni yake kwa kutumia malighafi mpya ndio alipokutana na Mama T.
Walikuwa hawajaonana muda mrefu tokea Edna asafiri kwa ajili ya harusi yake hivyo waliongea sana huku Mama T akitaka kuona Edna alipendezaje na katika mwendelezo wa stori ndipo Mama T alipojikuta akiropoka kuhusu mtoto wake Mage kuwa na mahusiano na Roma.
Mwanzoni Edna alihisi kuna kitu kinaendelea kati ya Mage na mume wake lakini alikosa ushahidi wa wazi wa kuthibitisha kile anachowazia.
******
Upande mwingine nchini Rwanda mheshimiwa Jeremy alikuwa akizunguka zunguka kwenye ofisi yake huku na huko akionyesha kama mtu mwenye hasira nyingi na hio yote ni mara baada ya kupata taarifa ambazo zilithibitisha Kizwe ndio ambaye alimtorosha Desmond hospitalini wiki kadhaa zilizopita.
Raisi Jeremy mara baada ya kumtoa Desmond Tanzania moja kwa moja alimsafirisha mpaka India kwa ajili ya matibabu , hakuwa akiamini maneno ya daktari wa Tanzania kwamba mtoto wake hawezi kupona kiungo chake cha uzazi na ndio maana alikuwa radhi kufanya lolote kwa ajili ya mtoto wake huyo na isitoshe ndio ambaye alikuwa ni mrithi wake akitaratjia siku za usoni kumwachia nchi aiendeshe , lakini akajiuliza kama Demsond hatokuwa na uanaume wake je angeweza kuendesha nchi kisawasawa na jibu lilikuwa hapana.
Upande wa Desmond mara baada ya kushituka katika kupoteza fahamu na kujua hakuwa na uwezo tena wa kumfanya chochote mwanamke wakiwa kitandani alilia sana na kuomboleza na maumivu yake yalikuwa ni zaidi ya siku aliopokea taarifa za kifo cha mama yake.
Mpaka muda huo alijiona hakuwa ni wa thamani tena kama mwanaume na ndio maana alijawa na huzuni isiokuwa ya kifani huku lawama zote akimwangushia baba yake mzazi ,kwani aliamini kama sio matendo yake basi huenda asingepatwa na kadhia hio.
Ilikuwa ni adhabu kubwa mno ambayo Roma alikuwa amemfanyia , ilikuwa ni zaidi ya kifo kwake na hakujiona wa thamani kabisa.
Hata pale raisi Jeremy alipomtembelea katika wodi aliolazwa hakutaka kumuona kabisa na alitangaza waziwazi kwamba anamchukia na hali ilio iliamsha sana huzuni kwa Raisi Jeremy ,hakujua ni kwa namna gani angemsaidia mtoto wake kupona kwani alishakuwa tayari Eunuch ,kwa mtazamo wake hata kama angetaka kulipiza kisasi kwa Roma asingeweza na pia ingekuwa laana kwake kushindana na mkwe wake.
Kuna muda aliona huenda matendo yake ndio yaliokuwa yakimfikisha katika hali kama hio, alikuwa na mafanikio katika uongozi wake lakini likija swala la familia alikuwa amefeli pakubwa na alijiona kama mtu ambaye hakuwa na bahati.
Madaktari wa kihindi walijitahidi kufanya juhudi za kila namna ili kumponyesha Desmond tatizo lake lakini majibu hayakuwa na tofauti sana na yale ambayo yalitolewa Tanzania.
Kwa ufupi ni kwamba mtoto wake hakuwa mwanaume mwenye makali tena , taarifa ambayo ilikuwa mbaya sana na kuishia kumlaani Roma kwa kumfanyia hivyo mtoto wake.
Wakati akiendelea kutafakari namna gani ya kumsaidia Desmond akiwa nchini India kwa siri, ndipo alipopokea taarifa za Desmond kutoweka hospitalini kwa hali isiokuwa ya kueleweka jambo ambalo lilimshangaza mno na sio kwake tu hata vitengo vya ulinzi vya hospitali vilishangazwa na jambo hilo kwani hakukuwa na Kamera yoyote ilionasa tukio la Desmond kutoroshwa na kitu kingine zaidi ni kwamba CCTV Kamera zote zilikuwa zikifanya kazi.
Kwa maelezo hayo mafupi alioyapata Raisi Jeremy alijua moja kwa moja Kizwe atakuwa anahusika katika hilo.
Tokea siku ambayo aliweza kupata taarifa za Kizwe kuwa hai kutoka kwa Linda ilimshangaza sana Raisi Jeremy kwani ilikuwa ni taarifa ambayo kwake ni kama anaambiwa mfu kafufuka , alishuhudia yeye mwenyewe kifo cha mke wake na kumuona akizikwa inakuwaje akawa hai.
Linda hata yeye mwenyewe alishindwa kuamini kama Kizwe alikuwa hai , aliweza kupata kuigundua sura ya Kizwe siku kadhaa wakiwa wanafanya uchunguzi ndani ya chuo cha taifa cha Rwanda mara baada ya Lekcha kupotea na walipoangalia kamera za Chuo ndio walipoweza kuona sura ya mwanamke anaefanana na Kizwe kabisa akiwa katika ujana.
Tena inasemekana wakati Kizwe anaondoka na Lekcha katika chuo hicho Kizwe aliangalia Kamera ya ulinzi na kisha akatabasamu kifedhuli na kutamka maneno kwa namna ya kuonyesha ishara za midomo yake, alifanya hivyo kama mtu ambaye aliamini kabisa Footage za sura yake zingemfikia Jeremy.
Katika rekodi hio ya camera Kizwe alikuwa akionyesha ishara kama ya kumtahadharisha Jeremy kwa kumwambia kwamba anarudi kulipiza kisasi.
Baada ya taarifa ya mwanamke anaefanana na Kizwe kumfikia raisi Jeremy kwanza kabisa hakuamini na aliweza kupitia hatua zote tano za mshituko ili kujibu hali ya taarifa hio na baada ya masaa mengi ya kufikiria ndio uamuzi wa kufukuliwa kaburi(exhumation) la Kizwe kwa siri sana ufanyike nyakati za usiku kazi ambayo iliongozwa na Linda.
Na ilichukua siku tatu kwa mchakato wote kumalizika na mara baada ya raisi Jeremy kuwekewa majibu mezani alijikuta akipagawa , mwili ambao ulifukiwa haukuwa wa mke wake Kizwe kwani vinasaba vilithibtisha hilo.
Sio kwake tu ambaye alishangazwa na hilo lakini hata Linda pia alishangaa na kutaka kuthibitisha hilo na hapo ndipo walipoanza kuwasiliana na wanasayansi na vitengo vya serikali nyingine ili kuweza kuthibitisha uwezekano wa mtu aliefariki kufufuka na katika majibu mengi ambayo walipokea moja wapo ni kesi ya siri sana iliomtokea raisi mstaafu wa China lakini kesi hio hio ikajirudia nchini Tanzania baada ya mwili mtoto wa tajiri wa makampuni ya Maya kuonekana akiwa hai mara baada ya kifo chake kuthibitishwa.
Taarifa zilikusanywa kwa kutumia idara za kitelijensia na zilipomfikia Raisi Jeremy ndipo alipotambua sasa jina la mwanasayansi Yan Buwen ambaye alikuwa amepewa hifadhi ya kufanya majaribio yake nchini Tanzania.
Intellijensia ya Rwanda iliweka kila kitu wazi na kweli Yan Buwen wakati wa maombolezo ya kifo cha Firsr lady alionekana kuingia nchini Rwanda , muunganiko huo wa matukio ndio ulikamilisha uchunguzi wa kuamini Kizwe alikuwa hai bado na aliehusika kumrudisha hai ni Yan Buwen.
Na Raisi Jeremy alijiona mjinga kwa kuona alizidiwa akili na mke wake na hata kitendo cha Lekcha kumbakisha hai ulikuwa pia ni mpango uliosukwa , hatari aliweza kuiona mbele yake na kuanza kumuogopa Mwanamke aliekuwa ni mke wake na hata ulinzi wake aliongeza maradufu huku akihakikisha Desmond mtoto wake hafahamu ukweli wowote kuhusu hilo.
Asichokijua raisi Jeremy ni kwamba Desmond ndio moja wapo ya watu walioshuhudia mama yake mzazi akifufuliwa na Yan Buwen na hata nyakati za maombolezo ya taifa alikuwa akijifanyisha tu kuwa na huzuni.
Baada ya kifo cha raisi Kigombola pamoja na Yan Buwen Raisi Jeremy alipata unafuu na safari yake ya kuhudhuria maziko ya raisi Kigombola ilikuwa na sababu ya ziada ambayo ni kuona uwezekano wowote ambao ungemkutanisha na mke wake.
Siku ambayo Fredi aliandaa Party ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na Edna na Roma kualikwa ndio siku ambayo pia hata yeye mwenyewe aliweza kupokea ujumbe kutoka kwa Kizwe akimwambia afike Maple speed Resort kama anataka kuonana nae.
Lakini Kizwe hakuwa na mpango wa kuonana na Jeremy bali aliandaa mpango wa kumfanya Jeremy kushuhudia Kaka akimbaka mdogo wake kwa macho yake lakini kwa bahati mbaya mpango wake huo ukaja kufeli mara baada ya bangili aliovalishwa Edna kuingilia kati na matokeo yake ni Desmond kuharibiwa uanaume wake.
Sasa zikawa zimepita siku kadhaa tokea Desmond apotee nchini India huku akiamini moja kwa moja muhusika ni Kizwe ambaye amebadilika na kuwa wa tofauti sana , sio tu kwamba alikuwa amefufuka lakini pia akarudi ujana.
Asubuhi hio aliokuwa akizunguka katika ofisi yake ni mara baada ya Kizwe kumthibitishia Jeremy kwamba yupo na Desmond na ajiandae kuachia uongozi wa nchi , kauli ya Kizwe kwake ilikuwa kama ya vitisho na ndio maana alikuwa na hasira na kuzunguka huku na huko huku akikosa namna ya kumshughulikia mwanamke huyo ambaye muda huo hakumuona kama mke wake tena bali alimuona kama shetani.
Mbaya zaidi aliogopa kwa kuamini na Desmond atakuwa amejazwa ujinga na mama yake kwa wakati huo .
Ilikuwa kama laana kwake kwa baba wa familia kushindana na familia yake na jambo hilo lilimkosesha amani kabisa.
ITAENDELEA.
Matendo ya mapacha yanasikitisha. Haya ni matokeo ya KUWADEKEZA ktk malezi.

Boss Edna anao moyo kwa kweli. Michepuko ya Mfalme Pluto inamtia jakamoyo na simanzi ya hasira.

Ulinzi kwa Familia ndicho kipaumbele kwa kila Baba. Roma anauweka rehani usalama wa familia yake kutokana na arrogance na hivyo kuongeza wigo wa maadui.

Rufi ana lake jambo. Pamoja na kuleta hadithi za kuhuzunisha, shabaha ni kumnasa Roma na hatimaye kumtia msuko suko mkubwa atakapofika milki za Majini.

Hata hivyo, mwandishi na mtunzi ameonesha kipaji cha hali ya juu ktk kupangilia matukio na hivyo riwaya kuwa na mtirirko mzuri na hivyo kistahili PONGEZI nyingi sana.

Adios.
 
... mwandishi anaupiga mwingi kama Yanga
 
SEHEMU YA 568.

Stern mara baada ya kuona kitu kibaya kinakwenda kutokea , palepale alisogea na kumshika Ares ili asije kuleta malumbano na Magdalena.

“Kwasababu ni mwanamke wa karibu na Hades basi ni mmoja wetu , Ares hasira zako za haraka haziwezi kubadilika hata kama utapewa miaka elfu therathini ya kuishi , kwasasa wote turudini hotelini muda ambao Poseidon na Hermes watafika hapa tutasalimiana na marafiki zetu”Aliongea Stern

“Nitaacha hili lipite kwa leo”Aliongea Stern huku akimwangalia Magdalena kwa hasira kubwa na kisha akaondoka katika hilo eneo.

*********

Anga la Norway katika bahari licha ya kwamba kulikuwa na jua lakini bado kulikuwa na ubaridi wa aina yake.

Mbele yake ni bahari isionekana mwisho wake , na alichoweza kuona ni mawingu ambayo yanatawanyika kila pande.

Usiku ulikuwa ushapita tayari , Roma alikuwa ametafuta katika kila sehemu ambazo hazikuwa na watu wengi sana na kutofikika kwa urahisi hususani milimani na katika pembezoni mwa bahari katika maeneo yote ya Kaskazini mwa Ulaya

Alianzia Gotland katika bahari ya Baltic akaeda Stockholm halafu Oslo na Bergen , katika maeneo yote hayo kulikwa na vituo nane ambavyo vyote vilikuwa ni vya kimitengo ambavyo vimetengenezwa na wahalifu ili kuchanganya watu wanaowatafuta.

Roma aliweza kupata moja wapo ya kambi ya siri katika kijiji kimoja lakini licha ya hivyo hakuweza kuona dalili yoyote ya majaribio ya sayansi ya nyuklia .

Mpaka hapo aliona kabisa ilikuwa sahihi kuja yeye kutafuta , kwani kama ni watu wake wasingefanikisha chochote, yeye licha ya spidi yake kubwa lakini bado tu hakuwa amefanikisha kumpata Clark.

Roma alitoa simu maalumu aliokabidhiwa na Sauron ili kuwasiliana nae moja kwa kwa moja kupitia satilaiti.

“Sauron wapi kumebakia?”Aliuliza.

“Mfalme Pluto kutoka bahari ya Norway kwenda Kaskazin kuna kituo katika eneo la Wilwick na ukielekea magharibi zaidi kuna meli inayoelekea Iceland na nyingine inaelekea Nuuk Greanland , Kusini kutoka sehemu ulipo pia kuna kituo cha Rotterdam nchini Uholanzi , Leipzig nchini Ujerumani , Marseille nchini Ufaransa na Lodz nchini Poland na kuendelea”Aliongea Sauron kupitia simu na kumfanya Roma kung’ata meno yake kwa hasira.

“Pumbavu kabisa yaani wamefanya makusudi kutengeneza vituo hewa vingi ili wasikamatike kirahisi”.

Ukumbuke hapa kwamba Roma anachofatilia ni uelekeo wa madini adimu yalikosafirishwa hivyo vituo anavyozungumzia Sauron ni vile ambavyo wanaamini meli iliosafirisha mzigo ilisimama.

Kama kutakuwa na sehemu meli imesimama na kushusha mzigo moja kwa moja ingemaanisha kwamba katika ukanda huo wote kutakuwa na maabara ya siri na hicho ndio ambacho Roma alikuwa akitafuta.

“Mfalme Pluto nafikiria kwamba tachane na baadhi ya vituo , kwa mfano maeneo ya Ufaransa yapo karibu sana na bahari ya Mediterranian na yana idadi kubwa ya watu hivyo kukosa sifa kujificha na uwezekano wa wao kufanyia majaribio ya sayansi ya nyuklia katika maeneo hayo , lakini pia hawawezi kuyachagua kwani wangehofia kukamatwa haraka na jeshi , hivyo nashauri uelekee upande wa magharibi na mimi nitaamrisha vikosi kutafuta upande wa miji ya Kaskazini”

“Mimi nashauri tufanye kinyume chake , tutaanza kuafuta kutoka katika latitiudo za chini kwenda latitudo za juu , miji na maeneo ambayo yapo zaidi karibu na bahari ya Mediterranian tutaanza kutafuta huko kwanza”

“Mfalme Pluto unadhania kwamba wamefikiria kinyume makusudi kuchagua maeneo ambayo sisi hatwezi kufikiria kama wameyachagua si ndio?”

“Haiwezi kuwa rahisi Sauron , nakumbuka umesema haiwezekani kwa maabara kuwepo katika watu wengi waliozagaa , njia zuri kwa kundi la watu wengi kama hao kujificha basi kwa angalau miaka ni katika maeneo ambayo yana idadi kubwa ya watu, kwahio nafikiri maeneo sahihi ya kutengeneza maabara ni katika maeneo hayo , hata hivyo kwasasa ni makisio yangu tu lakini tunaweza pia kuotea baadhi ya maeneo tofauti na kutafuta bila uelekeo”

“Uko sahihi nitawaagiza vijana kuanza kutafua upande wa kusini sasa hivi?”Aliongea Sauron na palepale walikatisha maongezi yao

Baada ya Roma kukata simu palepale aliichukua safari ya kuelekea Marseille nchini Ufaransa , ijapokuwa anakwenda kuonekana katika maeneo hayo kukiwa mchana kweupe lakini hakujali kama anaweza kuibua taharuki , alijiambia akifika katika hayo maeneo atatumia spidi kubwa kuzunguka ili hata kama kuna mtu atakae weza muona asiweze kuamini kama ni mtu bali maluweluwe.

Alikuwa akifikiria kinachoendelea Sicilly kwa muda huo katika mashindano ya Caesar Conference na kwa haraka haraka alijua mpaka muda huo mashindano hayo yatakuwa yamefunguliwa rasmi , lakini hata hivyo alijituliza kwa kujiambia hakuna baya ambalo linaweza kutokea kama tu Christen atakuwa ametaarifu miungu wenzake kufika katika.

*******

Wakati Roma akielekea Ufaransa upande mwingine katika jiji la Palermo karibu na bandari kulikuwepo na Colloseum kubwa ya kizamani iliokuwa imejazwa na makelele.

Ukumbuke Colloseum ni uwanja au Ulingo unaotumika kwa michezo ambayo huhusisha damu na hicho ndio ambacho kilikuwa kikienda kuanza ndani ya uwanja huo.

Ulikuwa ni uwanja mkubwa sana uliokaa kama duara na kwa upande wa nje ulionekana kama vile ni jengo la Ghorofa la froo nne liliojengwa kama duara.

Licha ya kwamba ni jengo ambalo lipo kama makumbusho lakini lilikuwa limefanyiwa maboresho makubwa na umoja wa makundi ya kimafia ya Sicilly kwa kazi maalumu ya kufundishia watu wao , kwa nje ni jengo lililoonekana kuwa na muundo wa kizamani lakini ndani yake lilikuwa na mwonekano wa kisasa zaidi kama vile kiwanja cha mpira.

Ni Ulingo uliokuwa ukiruhusu zaidi ya watu elfu therathini kwa mpigo na cha kushangaza sana asilimia kubwa katika siti zote hujazwa na wanajeshi wa makundi mbalimbali duniani ambao hushiriki.

Ukichana na watu hao kuwa wanajeshi lakini kwa jinsi walivyoketi katika viti vyao ni kama vile ni mashabiki wa mpira , kwani waliongea lugha mbalimbali na kufanya zogo kubwa kusikikika katika rafudhi mbalimbali.

Katika eneo la VIP , Magddalena na Rose walikuwa tayari washachukua siti zao mapema sana , katika eneo hilo alikuwepo Stern na dada yake Alice , vilevile alikuwepo mrembo Christen na kwa upande wa Ron na mtoto wake Fidero walikuwa wapo pembeni yao wakihakikisha kuwahudumia kwa kila kitu watakachotaka.

“Wanaanza kupigana saa ngapi ni zadii ya lisaa tokea sherehe za ufunguzi kumalizika?”Aliongea Rose aliekuwa na shauku ya kuona mapambano haraka iwezekanavyo.

“Unaonaje tukicheza raundi moja ya kadi ili kupoteza muda?”Aliogea Magdalena kwa kutania huku akicheka na kumfanya Rose kubetua midmo.

“Cheka uridhike mama, nimepoteza hela nyingi kwenye kamari lakini kwangu sio tatizo , wale watu hata hivyo walikuwa na maprofesheno kwenye kucheza kamari ingeshangaza mimi kushinda”Aliongea , ilionyesha siku ya jana alikuwa amepoteza hela nyingi sana.

“Oh! Miss Christen nimekumbuka , je napaswa kukuita Venus si ndio?”Aliuliza Rose.

Wakati huo Christen na Alice alikuwa wameshikiria jarida na fasheni na mitindo wakiangalia baadhi ya picha za nguo ambazo zimewekwa.

“Vyovyote utakavyoniita sawa tu lakini usije kuniita Venus kwenye kundi la watu”Aliongea.

Kitendo cha Rose kuwa karibu na Roma kwenye maisha yake kimemfanya kujua uwepo wa hao viumbe kutoka sayari nyingine ambao serikali nyingi duniani kubwa hujaribu kuficha uwepo wao.

“Nataka nikuulize swali , je unafahamu wale watu wa mavazi meupe?”

Baada ya kuulizwa swali hio alionyesha upande wa kulia kwake katika eneo la VIP , kulikuwepo na wanaume watatu waliokuwa wamekaa , alikuwepo Poseidon ambaye amevalia kombati za jeshi la Marekani lakini pia Ares na Hermes ambao walikuwa wamevalia suti na viatu vya ngozi wakiwa kawaida.

Majamaa hao hawakuwa wakipendelea sana kukaa karibu na wanawake kutokana na kwamba hawakupenda sana kuongea ongea lakini kitu kingine ukiachana na Hermes , Ares na Poseidon walikuwa wakifanana kitabia walikuwa wakipenda sana fujo.

“Angalia na wale wanasubiri kama sisi tu , tutaweza kuthibitisha wakati watakapotokea na isitoshe Hades hayupo hapa na Athena pia hayupo , haitakuwa rahisi kama tutaweza kukutana na maadui wetu wa zama zile”Aliongea.

Maneno yake ni kama yalizidi kumuongezea Rose shauku ya kutaka kujua watu hao ni wakina nani na alitamani muda huo hata Roma aweze kurudi mapema baada ya kumpata Clark , lakini akili yake haikuwa mbali na kufikiria kama kuna uwezekano wa kitu kibaya kimetokea.

Wakati wa watu kuanza kuchoka hatimae msherehesaji katika jukwaa maarufu alitangaza kwamba raundi ya kwanza ya mapigano ingeanza .

Kutokana na timu nyingi ambazo zilikuwa zikishiriki siku ya kwanza kulikuwa na raudi ya mtoano , kulikuwa na timu sita ambazo zilikuwa zinacheza kila raundi na kila mshindi atakae toka katika kila pambano basi atakuwa ameingia katika nafasi ya kucheza siku inayofuata.

Mkutano wa Kaisari mara nyingi huzuia mauaji ndani ya ulingo lakini kama itatokea kifo cha bahati mbaya au kumpelekea mshiriki kupata ukilema basi hawezi kukosa vigezo kuendelea na hayo ni makubaliano ambayo yanasainiwa na kila timu kabla ya kuanza.

Ukweli ni kwamba licha ya kwamba kuna makundi ya wanajeshi wapiganaji ambao walikuwa na asilimia ndogo za kushinda lakini walikuwa na uwezo wa kibunifu wa kuweza kutoroka pale wanapozidiwa na hilo limesaidia sana kupunguza mauaji yanayotokea katika ulingo kwa zaidi ya miaka nane mfululizo.

Uwanja ulikuwa umegawiwa katika maeneo matatu na muda huo mwanajeshi mmoja baada ya mwingine aliweza kutoka na kwenda kusimama katika eneo ambalo ameelekezwa.

Kulikuwa na ulingo tatu ambazo zote zilipaswa kila timu kupigana na mshindani wake katika mgawanyo wa timu mbilimbili.

Kilichomkatisha tamaa Rose ni kuona The Eagles sio timu ya kwanza ambayo imeanza katika randi hio , lakini palepale alionekana mtu mmoja aliekuwa kwenye mavazi meupe ambae aliingia katika ulingo akiwa peke yake na kuonyesha kutaka kushindana na timu ya watu watano.

Yaani mtu mmoja wa mavazi meupe alikuwa akitaka kudili na timu ya watu watano na ilifanya hali ya hewa kuwa katika ukimya wa hali ya juu kuangalia kinachokwenda kutokea.

Baada ya watu hao kujitokeza Christne na wenzake wote walijikuta wakisimama na kumwaangalia mtu yule kwa mshangao.

“It is real hem .. how did they come back”Aliongea Hermes akisema ndio wenyewe , wamewezaje kurudi.

“Kuna haja gani ya kuwa na wasiwasi , hili ni jambo zuri pia, kipindi kile tuliwaacha hai nadhani muda huu itakuwa nafasi nzuri kuwamaliza kabisa”Aliongea Ares.

Upande wa Poseidon yeye alionekana mwenye kujiamini wala kutokuwa na mshangao mkubwa na alikunja sura baada ya kumuangalia namna ambavyo Ares anaongea kwa kujigamba.

“Unasema kuwamaliza , hivi unafikiri wewe ni Zeus au Athena?Unafikrii unaweza kuwamaliza wewe kama wao walishindwa? , kwasababu wameweza kurudi lazima watakuwa na njia yao maalumu ya kuingia na kutoka , kama sio hivyo wasingekuwa ni wenye kujiamini kujitokeza mbele yetu”Aliongea Poseidon mpishi huyo na mwanajeshi kwa wakati mmoja.

“Poseidon nafikiri unaishi nyuma ya muda na unazidi kupoteza kujiamini , hawa ni kundi tu la wezi na wauaji wa miungu , hata baada ya miaka elfu ishirini hawawezi kubadili kilichopo ndani yao”

“Acheni kulumbana mara moja, muda huu lazima tufikirie namna ya kumtaarufu Athena ,Wakati huu Zeus hayupo na hatujui kama Hera na Dionysus wameamka , kama hatokuja hapa sijui namna ya kudhibiti hali’Aliongea Hermes.

“Umeanza lini kumkubali Athena wewe , si siku zote ulikuwa ni mwenye kumchukia na kutaka kuonyesha una uwezo mkubwa kuliko yeye?”Aliongea Ares kwa kejeli huku akicheka.

“Hata kama namchukia lakini kwasasa tupo upande mmoja kushindana na adui mmoja”

“Acha unafiki”

“Hehehe ..vyovyote unavyofikiria”

Kila aina ya kelele na vifijo vilisikika katika uwanja mzima , watu wengine walikuwa kwenye mchecheto mara baada ya kuona labda ni majivuno na kujiamini kwingi kwa timu ya kundi la DEICIDE kutuma mtu mmoja kushindana na timu ya watu watano.

Ni wakati huo huo kundi la wapiganaji ambalo lilijiatambulisha kama wawakilishi wa Afrika kumvamia yule mtu wa mavazi meupe kwa fujo zote.

Hawa Masenari wa kiafrika walikuwa na miili mikubwa mno na ni wenye nguvu ,ijapokuwa namna wanavyopigana sio kwa utaratibu maalumu na kwa wepesi lakini walikuwa na spidi na walichagua maeneo muhimu ya kumpiga adui

Mtu wa mavazi meupe aliekuwa na sura iliofunikwa na Mask ya madini ya Dhahabu alisimama katika eneo moja bila ya kusogea na hata maadui zake walivyomsogela hakufanya chochote na aliwaacha wafanye wanachotaka, walijaribu kurusha ngumi kumpiga katika maeneo ya kifuani , usoni na kwenye kiuno kwa kuunganisha nguvu lakini hawakuweza kumsogeza hata inchi., ni kama vile mtu anapojaribu kupunguza maji chumvi ya maji ya bahari kwa kumwaga maji safi.

Tukio hilo liliwafanya wale watu kushindwa kujua ni kipi cha kufanya zaidi , maana wamepiga kwa kutumia mbinu zao zote , lakini hakukuwa na matokeo ya adui yake kuonysha kuumia ni kama wanajaribu kulima jiwe kwa kutumia majembe.

Muda uleule kulisikika sauti isiokuwa ya kawaida,ilioashiria dharau kutoka kwa yule mtu wa mavazi meupe na palepale wale waafrika wenzetu ni kama vile walikuwa wakivutwa kwani wote walirushwa pembeni na nguvu isiokuwa ya kwaida na kwenda kudondokea mbali nje ya ulingo.

Ijapokuwa hawakuwa wameumia , lakini mshindani wao aliwashangaza na kumuona sio wakawaida kabisa kwa namna ambavyo anapambana na walikosa ujasiri wa kueondelea na palepale kengere ya refarii kupitia vifaa vya Eletronik ilisikika na kutangaza timu ya DEICIDE imeshinda kuingia raundi nyingine.

Licha ya hivyo mtu wa mavazi meupe alionekana kama vile hakuwa hata na haja ya kuingia raundi nyingine bali alikuwa amesimama akiwa ameangalia upande mmoja ambao ni wa VIP.

Miungu sita iliokuwa katika eneo la VIP ndio walengwa wake wakuu na macho yake kama yalivyoonekana katika Mask yalikuwa ni yale aliokuwa na dharau lakini pia ya kiuchokozi.

“Haiwezi kuwa makosa , muonekano wao na nguvu bila ya kuwa na msisimko wowote wa nguvu ya kiroho , ni wao bila shaka”Aliongea Sten huku akikunja sura.

“Lakini kama kweli ni wao na wametoka walipokuwa , kwanini wameshiriki katika mashindano ya binadamu , si maadui zake ni sisi?”Aliuliza Alice.

“Sina uhakika kwasasa , lakini kwasababu tayari washatangaza vita basi haitakuwa rahisi kama miaka elfu ishirini iliopita na inaweza kusababisha dunia kuingia katika taharuki , tunapaswa kuona mambo yatakavyokwenda”Alijibu .

“Hao ni wakina nani , kwasababu unaonekana unajua kwanini na sisi usitutoe gizani?”Aliuliza Rose , yeye na Magdalena hawakuwa wakijua chochote na Christen alivuta pumzi na kuzishusha na kisha akaongea.

“Have you heard about .. A race named GIANT?”Aliuliza akisema je ashawahi kusikia kabila la watu waliofahamika kwa majina ya GIANT.

“Giant!!?”Aliongea Magdalena huku akionyesha mshangao na kuonekana akifikiri.

SEHEMU YA 568.

Magdalena mara baada ya kufikiria kwa muda alikumbuka maneno ya Roma na Ron walivyokuwa wakizungumzia kuhusu kundi la Kimasenari ambalo linajiia Ps linalohusiana na Cyclops.

“Nimesikia mshindi wa mashindano yaliopita ni kutoka kwa familia iliopewa jina la Cyclop ?”

“Upo sahihi , Cyclops ni sehemu ya Giants(Majitu) wana uhusiano wa karibu pia na Centimani , kulingana na historia Centimani iliwakirisha majitu mia moja katika vita , Hadithi za miungu kuna nyingine ni za uongo na nyingine ni za ukweli ambazo zilikuwepo enzi hizo zilizoandikwa na binadamu, kabila la Cyclop ni uzao mchanganyiko kati ya Giants na binadamu wa kawaida , hivyo unaweza kusema Cyclop wamerithi tu damu yao na sio muonekano. licha ya hivyo uwezo wao ulikuwa mkubwa kushinda makundi yote ya kimasenari katika mapigano.

Sasa basi hawa Cyclops halisi pamoja na Centmani wanatokea katika uzao mmoja ambao ni sawa na wa kwetu lakini hayo ni mambo ya zamani sana ambayo yametukia katika sayari yetu , nguvu zao za kimwili ni kubwa mno kuliko za kwetu lakini nguvu zao za kiroho hazikuwa kubwa kutupita hivyo wakawa na uwezo mdogo sana wa kutumia kanuni za anga na sio washindani wetu kabisa kipindi hicho na katika sayari yetu walikuwa ni kabila lenye hadhi ya chini kabisa ambalo lilikuwa chini yetu lakini mara baada ya sayari yetu kukosa uwezo wa kusapoti maisha sisi tlikuja duniani lakini wakati huo sio kama tulikuja duniani tukiwa peke yetu, baadhi ya Cyclops na Centiman walikuja duniani kwa kupewa msaada na Hepheastus ambaye alikuwa ni mwanasayansi aliebobea katika utengenezaji wa dhana , utofauti wa hawa Majitu na sisi wao walivyofika duniani waliweza kuhimili mazingira lakini kwetu sisi tulishindwa hivyo uwezo wetu wa kuendeleza kizazi chetu ukawa mdogo sana na ni kipindi ambacho waliweza kugundua tulikuwa tumeivaa miili ya binadamu ili kuweza kuishi walituchukulia kama dhaifu sana na baada ya kuona hilo hawakutaka tena kuwa chini yetu bali juu yetu na walianza kutuwinda ili watuue lakini matokeo yake Zeus akagundua mipango yao na akatumia kauuni za anga kupitia siraha yake ya Thunder na kuwafungia katika ‘Dimension’ mbalimbali na kwanzia hapo ndipo walipoweza kupotea katika uso wa dunia , lakini hakuna ambae alitarajia leo hii wataonekana tena kwa zaidi ya miaka elfu ishirini katika miili ya kibinadamu”Aliongea

“Kama ulivyosema ni sahihi , mbona hawaonekani kuwa na uwezo mkubwa, kwanini Zeus hakuwaua kabisa”Aliuliza Rose

“Ilikuwa ni ngumu sana kuwaua kwasababu ya miili yao ndio maana Zeus akaamua kuwafungia kwenye Dimension nyingine kwa kutumia kanuni za anga, ijapokuwa hatuwaogopi lakini ni ngumu sana kupambana nao na zaidi ya yote kama wametoka wakiwa hivi inamaana wanao uwezo mubwa na kama sio hivyo wasingetokea”

“Kama Zeus ndio aliekuwa na nguvu kuliko wote na alishindwa vipi kuhusu sasa hivi?”

“Kama tungekuwa na miili yetu kama kwenye sayari yetu na nguvu zetu kuwa asilimia mia moja wasingekuwa na ubavu hata wa kutusogelea”

“Unamaanisha nini?”

“Haha..Usiulize maswali mengi , Inabidi mjaribu kuwasiliana na Hades arudi haraka iwezakanavyo”Aliongea Christen huku akicheka

*****

Ni katika nchi ya Ujerumanni katika ukanda wa eneo la Bavaria , Roma ndio kwanza alikuwa amefika katika eneo hilo akitokea Marseille Ufaransa akijiandaa kuelekea Leipzig.

Sasa wakati akiwa anapita katika jiji la Munich alisimama ghafla , wakati huo alikuwa akiongea na Sauron ili kumpa maelekezo lakini mfumo wa mawasiliano ulionekana kuingiliwa na kumfanya Roma kusimama.

“Mfalme Pluto kuna kitu umepata?”Aliuliza Sauron mara baada ya kuona Roma yupo kimya.

“Sauron hii njia ya mawasiliano tunayotumia si mtandao wake unajitegema na tunatumia satilaiti binafsi?”

“Ndio Mfalme , njia hii inazuia baadhi ya taasisi nyingine kuingilia mawasiliano yetu na kutudukua, tumeweza pia kuweka nywira ili isiwe rahisi”

“Kwahio inamaanisha kwamba kama itatokea mawasiliano yakayumba inamaana kuna mtu alieingilia kutoka ndani si ndio anaejua mfumo wetu?”

“Ndio Mfalme na kama ni hivyo basi nakubaliana na wewe kwani mawasiliano yetu yalikuwa mazuri tokea tuanze msako”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria huku akianza kuchunguza kila upande na aliweza kusikia tena mawimbi ya frikwensi yakiingiliana na mawasiliano yao

“Hebu jaribu kuangalia kama kuna sehemu gani ndani ya eneo la ukanda wa Bavaria ambalo kuna uwezekano wa uwepo wa kambi”Aliongea Roma na Sauron alichukua agizo hilo na kulifanyia kazi.

“Mfalme Pluto hilo eneo ni mahususi kwa ajili ya Viwanda na hakuna kingine ukiachana na sehemu mbili zilizotelekezwa ambazo kuna migodi mwili ya makaa ya mawe iliotelekezwa kwa miaka mingi”

“Migodi ya makaa ya mawe , unamaanisha ambayo ilichimbwa miaka mingi iliopita?”

“Upo sahihi lakini hata kama ni ya zamani ilikuwa ni mikubwa mno na inaenda sana chini na imetawaliwa na joto la kiwango cha juu , hivyo eneo hilo haliwezekani kuwa sahihi kwa ujenzi wa maabara”

“Umekosea Sauron , huu ndio ufunguo kwasababu jotoridi kuwa juu inafanya eneo hili kuwa sahihi kujenga maabara”Aliongea Roma na kumfanya Sauron upande wa pili kushangaa.

“Could it be.. Geotharmal energy”Aliongea Sauron akimaanisha je wanatumia nguvu ya umeme wa mvuke.

Maabara ya siri ya utafiti wa siraha kubwa za nyuklia ingeweza kugundulika kwa haraka kama tu ingetumia umeme kutoka katika gridi ya taifa kwani wangekuwa na matumzi makubwa sana ya umeme hivyo wagetiliwa mashaka , lakini kama ni umeme unatokana na mvuke ingekuwa rahisi sana kwani ni wa kujitegemea.

Sauron alishngaa kuona Roma aliweza kufikira jambo la namna hio lakini upande wa Roma hakutaka kufikiria mara mbilimbili kwani aliweza kushuka moja kwa moja mpaka chini.

Eneo lote la Bavarian lilikuwa na utajiri wa kutisha ndio kitomvu cha utajiri wa taifa la Ujerumani , lakini licha ya kuwepo kwa viwanda vingi vinavyofanya kazi na maendeleo makubwa ya jiji lakini kulikuwepo na maeneo ambayo yalikuwa wazi , hususani yale ya migodi kama hio ya makaa ya mawe.

Roma mara tu baada ya kukanyaga chini na kukagua eneo hilo aliweza kutumia uwezo wake kukagua mazingira kutoka juu kwenda chini na hatimae aliweza kuona utofati wa eneo moja kuwa na muundo ambao ulikuwa ukitofautiana na baadhi ya migodi mingine na alijiambia huenda ikawa eneo ambalo alikuwa akitafuta.

****

Dakika kumi zilizopita lwenye maabara , alionekana Clark ambaye alikuwa amesimama kwenye kioo chenye uwezo mkubwa wa kuzuia mionzi akiangalia kwa umakini upande wa pili namna mkono wa Roboti ulivyokuwa ukifanya kazi kutoa majibu ya kikanuni ambayo umepewa maelekezo yake.

Mkono huo uliokuwa ukifanya kazi kiotomatiki ulikuwa ushafanikisha kudhalisha vitu viwili vyenye maumbo makubwa muundo wa risasi.

Jerry akiwa na macho ya furaha aliangalia matokeo hayo kwa tamaa huku muda wote akicheka cheka kama chizi.

“FURY hatimae upo mbele yangu , Profesa naamini unafuraha pia hii ni Masterpice ambayo itabadilisha kabisa ustaarabu wa dunia mzima wa kibinaadamu , hata miungu hawatoweza kuwa na nguvu ya kuhimili si ndio?”

“Sijawai kufikiria ingefika siku ningetengeeza kitu kama hichi , kama bado unanichukulia kama mwalimu wako fuata ushauri wangu , usije ukaitumia..”

“Haha..”Alicheka na muda uleule alibonyeza kitufe na kuruhusu zile Fury zilizokamilika kutoka katika eneo la matengenezo na kuingia upande mwingine kwa ajili ya matumizi.

“Usijali Profesa kama yule shetani atashuruti , bila shaka sitakuwa na haja ya kuitumia lakini kabla ya hapo lazima tutengeneze mtaji mkubwa ambao hata siku tukisema tuiharibu dunia inawezekana , kwasasa wafadhili wa hii projekti wanasubiri “

“Ijapokuwa sijui nani yupo nyuma yako na ni taasisi ipi lakini nguvu ya FURY haiwezi kuogozwa na binadamu , nakwambia utajutia hili”Aliongea kwa kujaribu kumbembeleza.

“Profesa au hapana kwanzia sasa nitakuita Clark , mimi nido napaswa kukushauri kuanzia sasa hivyo acha maigizo , wewe na mimi ni sawa tu , sisi wote ni watu ambao tunatumia juhudi kubwa kaika kufanya tafiti bila kujali athari zake na mwisho wa safari yetu ni pale ambapo tutapita vizingiti vyote alivyowekewa binadamu na kujua nini maana ya msingi wa ulimwengu , kama hukuwa na mpango wa kutengeneza FURY na kuvuka mipaka ya kibinadamu katika siraha za nyuklia basi usingethubutu hata kufikiria hii tafiti , wewe si ulisoma maswala ya tiba kwanini ukajiunga na maswala ya tafiti za siraha , Hawa binadamu wote ni wapuuzi kwako na unawachukulia kama vifaa vya majaribio , hawana utofauti na panya wa maabara waliofngiwa kusubiria wakati muafaka kufanyiwa majaribio kwani hakuna utofauti , kama hukutegneneza Fury kwa ajili ya kuharibu dunia nina uhakika ulikuwa ukisubiria madhara yake, Au nakosea Clark?”

“Sijatarajia utanifikiria mimi hivyo , nilisoma maswala ya tiba kwa ajili ya mwanaume ninampenda kuondokana na maumivu na nilitengeneza Fury nikiwa na matarajio kwamba itasaidia binadamu kuweza kutumia nishati kwa kiwango kikubwa zaidi ya ilivyosasa kupitia teknolojia iliopo lakini licha ya hivyo niliishia njiani kwasababu niliogopa kama itatumiwa na taifa kutengenezea siraha , upo sahihi maisha yangu yote yatakuwa ni kufanya tafiti lakini sio hapo tu , kuna vitu vingi katika dunia hii ambavyo vinahitaji hasira zetu lakini hatupaswi kuwa watumwa wa hasira na chuki”

“Acha kuongea upumbavu wako , usijifanye wewe ndio mtakatifu, unaweza kuwa mwalimu wangu lakini sasa wewe ni mateka wangu na mimi ndio master wako”Aliongea na palepale alimsogelea Clark na kisha akakikumbatia kiuno chake na Clark kwasababu alikuwa amengalia upande wa mbele yake hakuweza kutegemea kitendo kile kutoka kwa Jerry aliekuwa nyuma yake.

“Jerry unataka kufanya nini?”Aliongea huku akijitoa kwake.

“Unaiuliza tena , huu ni muda sasa wa kurelax baada ya kumaliza kazi yangu nzito , kwanini nisifurahie uzuri wako, itakuwa hasara kumuacha mtu mwingine”

“Wewe, mimi ni mwalimu wako uthithubutu”

“Acha ujinga , sijali wewe ni nani , kwanza kabisa wewe ni mdogo kwangu kwa miaka miatu , unafikiri nitakuabudu kwasababu tu ulikuwa mwalimu wangu na uwezo wako ni mkubwa , sahau katika kichwa chako na kwanzia sasa hivi hakuna kitu kinachoitwa mwalimu na mwanafunzi, hapa ni mwanaume na msichana ambaye anajiandaa kuwa mwanamke”Aliongea huku akimsogelea tena.

Clark alikuwa na uwezo wa kumdhibiti Jerry kwa wakati huo kwani alikua yupo peke yake katka hilo eneo kwasababu ya kuwa na mafunzo ya kujilinda lakini alisita kufanya hivyo..

Upande wa Jerry mara baada ya kuona Clark anakwenda kuleta ugumu palepale alichomoa bastora na kumnyooshea Clark.

“Samahani najua kabisa wewe ni mgumu hivyo niliandaa kabisa bunduki , kukwambia tu ukweli nje ya hii maabara kuna walinzi kibao wanalinda na hauwezi kutoroka”Aliongea na kumfanya Clark kukunja ngumi yake na kung’ata lipsi kwa wakati mmoja .

“Unaota nini , vua nguo haraka , nina sehemu ya kwenda pia kuonyesha mafanikio kwa wakubwa zangu, nimeisubiri hii siku kwa zaidi ya miaka mitatu kufanya mapenzi na wewe na hatimae leo ninapata nilichokuwa nikipania sana , hivyo naomba unirhuhsu nifurahi kistaarabu kabisa..”

“Nipige risasi kama una ujasiri huo”Aliongea Clark akiwa katika ukauzu.

“Kama unakitaka kifo utakipata lakini kama hutotoa ushirikiano basi wale watoto ndani ya kanisa la Santa Maria nitawaua kwa bomu tena nikuambie nitaenda mbali kuharibu shule ambayo umewekeza”

“Ushetani””

“Ndio ujue sasa mimi ni shetani , hivyo vua haraka”Aliongea na kumfanya Clark amwangalie kwa huzuni kubwa na palepale aliingiza mkono wake katika mfuko wa koti na kutoa kijichupa kidogo na kupeleka mdomoni na kuonekana alikuwa akinywa kimiminika.

“Unafanya nini?”Aliongea Jerry kwa mshangao na kumfanya Clark kucheka kwa dharau.

“Wewe huoni , ni kheri nife kuliko kuruhusu shetani kama wewe kuunajisi mwili wangu , kama hutojali mwili wenye sumu na wa baridi unaweza kunitumia utakavyo..”Aliongea na muda uleule sura ya Clark ilianza kubadilika na kupauka na alianza kuhema kwa shida na palepale alikosa mhimili na kudondoka chini huku povu likianza kumtoka mdomoni na palepale macho yake yaliongezeka ukubwa.

“Wewe umewezaje kupata sumu..”Aliongea kwa kutetemeka akiwa haamini.

Muda huo huo ndio aliweza kukumbuka kauli yake masaa kadhaa yaliopita kwamba anajaribu kuangalia usafi wa elementi.

Wakati ule hakuwa akielewa ni mchanganyo gani wa kemikali aliokuwa akitengeneza , lakini sasa anajua kumbe ilikuwa ni simu aliokuwa akitengeneza.

Baada ya kuona kwamba mwanamke huyu alimdaganya jana na kujitengenezea sumu alijikuta hasira zikimvaa na alimsogelea kwa kasi na kumpiga teke tumboni na kumfanya Clark kudhidi kutapatapa akielekea kupoteza maisha.

“Mh hata hivyo sina tamaa kihiivyo ya mwili wako , lakini siwezi kukuacha ukafia hapa ndani , tutakutoa na kufanya wanyama wakali wa msituni kukufanya chakula , itashangaza baade ikija kugundulika mwanamke mwenye busara kama wewe umejiua na sumu”Aliongea na baada ya kumaliza hakujali tena na alirudisha siraha yake kibindoni na kugeuka ili kuondoka hilo eneo.

BOOM!

Wakati akiwa anajiandaa kutoka alijikuta akisimama na kufunga masikio yake baada ya mlango wa kuingilia kudondoka chini kwa kuonyesha kwamba umepigwa na nguvu isiokuwa ya kawaida.

Na mpaka akili yake inamkaa sawa na kuamsha kichwa kuangalia knachoendelea , alijikuta akiachama mara baada ya kuona sura ya mtu ambaye hakuitarajia kuiona hapo ndani , alikuwa ni Roma.

ITAENDELEA.
Hatari
 
SEHEMU YA 570.

Jerry alidhani alikuwa akiota , mlango huo ulikuwa ni wa chuma kigumu sana , imewezekanaje ukabobolewa kirahisi namna hio.

Muda huo ni shoti pekee za umeme ambazo zilikuwa zikisikika ndani ya eneo hilo na Roma wala hakujali kabisa aliingia kama vile ni mnyama.

Nyuma yake kulikuwepo na damu nyingi ambazo zilikuwa zimetengeneza mfereji mkubwa wa damu kuingia ndani mara baada ya mlango kuvunjika.

Zilikwa ni damu za walinzi ambao walikuwa walilinda katika hilo eneo na ilionekana dhahiri kabisa Roma aliwapasua pasua viungo vyao pasipo huruma.

Roma mara baada ya kugundua eneo ni lenyewe , alitolea hasira zake zote za kutafuta usiku kucha kwa walinzi hao na aliwaua vifo vibaya sana, huenda ni aina ya vifo ambavyo havijawahi kutekelezwa hapa duniani , vilikuwa ni vya ukatili wa hali ya juu sana.

“Clark!!”Aliita mara baada ya kumuona Clark aliekuwa yupo chini sakafutni akitetema kama mgonjwa mwenye kifafa na palepale alimkimbilia na kumkalisha.

“Nini kimetokea ?Umepewa sumu?”Aliuliza Roma kwa wasiwasi mkubwa na hakuacha kujaribu kumchunguza kwa kumuingizia nguvu za kimaandiko.

“I… I knew it ..you.. would save me ..just like ten years ago..”Aliongea kwa tabu sana akisema kwamba alijua tu atakuja kumuokoa kama miaka kumi iliopita.

Roma macho yake yalianza kuwa mekundu hakuwa na uwezo wa kujua ni aina gani ya sumu ambayo ipo kwenye mwili wa Clark , alikuwa na uwezo wa kuhisia sumu iliokuwa kwenye mwili wake ilikuwa ikinyong’onyesha saa utendaji kazi wa mwili.

Lakini alishindwa kumponyesha kwani sumu iliokuwa kwenye mwili wake iliionekana tayari ishaingia kwenye mfumo wa damu moja kwa moja na wakati akiwa amemshikilia palepale alitema damu nyingi nje mara baada ya Roma kujaribu kumponyesha.

“Ni sumu ya aina gani hii , niambie namna ya kukuponyesha”Aliongea Roma akijaribu kumtingisha lakini Clark aliishia kutingisha kichwa chake akimuonyesha ishara kwamba hakuna namna ya kumponyesha.

“Ni sumu ambayo niliiandaa dakika ya mwisho kabisa na ili kuhakikisha hawawezi kuniponyesha nilitumia mbinu ya kipekee ambayo inafanya viungo vya mwili kutofanya kazi sawasawa .. kwasasa haiwezekani kitu”Aliongea kwa tabu na kumfanya Roma palepale kumgeukia Jerry ambaye alikuwa amemsahau kwa muda.

“Wewe mnyama , yote haya ni kwasababu yako , kama utafanikisha kumponyesha mwalimu wako nitakuua lakini mwili wako sitouharibu”Aliongea Roma kimkwara huku akisambaza msisimko wa hali ya juu wa nguvu za kijini ili kumuogopesha Jerry.

Muda huo Jerry alikuwa ameshikwa na ubaridi wa aina yake hasa baada ya kuona damu nyingi zikiingia ndani kutokea nje , lakini licha ya hivyo chuki yake zidi ya Roma ziliifunika hofu yake na kaunza kucheka kama kichaa.

“Wewe shetani ijapokuwa sijui namna ulivyoipata hii sehemu lakini nakuambia hivi hakuna namna ya kumuokoa , sumu ambayo Clark ametengeneza anaweza kutengenza dawa yeye mwenyewe , inatia huruma kwamba anakufa kwenye mikono yako ukiwa huwezi kumsaidia “

“Unakiomba kifo wewe..”Aliongea Roma huku akitaka kumshambulia lakini Jerry alimzuia kwa kumpigia makelele.

“Usinisogelee, ukinigusa tu hii maabara yote italipuka na zile FURY mbili zitalipuka, madhara hayatakuwa kwako tu lakini kwa ukanda wote wa eneo la Bavaria, Ujerumani yote itageuka na kuwa toharani ya dunia, Je upo tayari kutoa kafara mamilioni ya watu kwa ajili ya kuniua mimi?”Aliongea na kumfanya Roma kunasa neno FURY.

“FURY siraha aliotaja je ndio sababu ambayo imewafanya wakuteke?”Alimuuliza Clark.

“Ndio .. niliipatia jila hilo ikimaanisha neno kisasi”Aliongea .

“Inahusiana na nini?”

“Ni aina ya siraha ya nyuklia ambayo teknolojia yake imeboreshwa zaidi … risasi yake moja ni sawa na risasi mia tano za bomu la Hydrojeni”

“Nini..!!”

Roma alishangaa kwa uhatari wa siraha hio , kama kweli risasi moja ni sawa na risasi mia tano za bomu la Hyrdrojeni si ni hatari hio , maana kama siraha hio ikatumika basi mionzi yake isingeathiri tu Ujerumani huenda na nchi za karibu.

Alijiuliza inakuwaje watu wa North Buyeo na kundi la kigaidi kutafuta teknolojia ya namna hio, ni kipi ambacho wanalenga?.

“Hehe.. sasa nadhani tayari ushajua ukuu wake, ninataka kuona kama utathubutu kuniua …Wewe shetani utapata maumivu makubwa sana baada ya mwanamke unaempenda akifa mbele yako …Hahaa, nimesubiria hii sku kwa muda mrefu sana , na unastahili kwa kila kitu , unapaswa kwenda jehanamu”Aliongea kwa hasira .

Roma alikuwa katika kiwango cha juu cha hasira na alitamani kumfanya kitu kibaya , lakini hakuweza kuthubutu kufanya maamuzi ya haraka kwani maisha ya watu zaidi ya mamilioni yalikuwa hatarini.

“Nini tatizo , Umekosa ujasiri tena?, Umejileta mwenyewe hata hivyo , ninakwenda kulipiza kisasi cha vifo vya familia yangu , baba yangu , mama yangu na dada yangu ambaye alikuwa na miaka mitatu tu”

“Kisasi? Ni kipi nimekufanyia mpaka kutaka kulipiza kisasi?”

“Bila shaka hukumbuki , umeua watu wengi sana unawezaje kuwakumbuka wote , umesahau ulichokifanya miaka mitano iliopita pale Simbokrog nchini Belarus kwenye kijiji cha Wozic si ndio?”

“Kijiji cha Wozic ?”Aliongea Roma huku akikunja sura , hakuwa akikumbuka kabisa kama kuna sehem kama hio na isitoshe kulikuwa na maeneo mengi madogo madogo aliopita ambayo hakuyakumbuka na kote hhuko huenda aliua.

“Unaonekana hukumbuki , Kijiji chetu kilikuwa na watu 186, kati yao therathini walikuwa ni watoto na wakati huo ni mimi pekee ambaye sikuwepo nyumbani kutokana na kwamba nilienda shuleni kwenye mji mwingine wa pembeni , lakini wewe ukaja na kufyeka kila mtu uliemkuta kijijini bila kujali wana hatia au hawana kwasababu tu adui yako alikuja kwenye kijiji chetu , kwanini usingeacha hata maisha ya watoto wadogo ambao walikuwa hawana hatia , kwanini ulivyomaliza ukawachoma na moto…”Aliongea Jerry kwa hasira kubwa na kauli yake ilimfanya Roma sasa kukumbuka lakini hakuwa akikimbuka vizuri sana , kipindi anafanya hivyo alikuwa katika hali ya ukichaa na ugonjwa wake ulikuwa ndio unaitawala akili yake.

Alikumbuka kabisa kitendo cha kuua watu wa kijiji kile ndio kilichosababisha Seventeen kumkimbia na mwisho wa siku akaingia kwenye mikono ya maadui na kumuua akiwa na ujauzito tumboni mbele ya macho yake.

Roma alishindwa kujizuia kusikia uchungu kutokana na maelezo ya Jerry , haikujalisha alikuwa akitamani kuwa na maisha ya amani , lakini mambo ambayo ameyafanya miaka iliopita yalimfanya kutengeneza maadui wengi ambao muda wowote watataka kulipza kisasi na aliona hata kwa Jerry ni mwanzo tu.

Lakini licha ya hayo yote , kipindi hicho akili yake ni kama ilikuwa ikiendeshwa kwa rimoti , ugonjwa wake ulikuwa mkubwa kiasi kwamba alikuwa ni kama shetani na bila kumwaga damu kwa siku hakuweza kutulia.

“Naona sasa unakumbuka ..?”Aliongea Jeryy huku akifuta machozi .

“Unapaswa kuadhibiwa pia , mwanzoni wakubwa waliniahidi watanisaidai katika kulipiza kisasi , na nikaamua kuishi na chuki na kuvumilia mpaka leo hii , lakini kwa leo kwasababu umepajua hapa sina mpango wa kuondoka hapa nikiwa hai”

“Unapanga kufanya nini , je unafikiri kulipua hilo bomu la FURY na kuniua kutakufanya ulipize kisasi cha ndugu zako , sahau kabisa hizo ni ndoto za kufikirika utaua watu wengi kuliko mimi”

“Inanihusu nini , ni matendo yako ya kishetani ndiio ambayo yamenifanya kuwa katika hali hii , usijaribu kunidanganya, hata kaam nitaondoka leo utanitafuta na kuniua , ni kheri niende na mamia ya watu katika kaburi langu , maisha ya hawa watu yatakuwa yametolewa kafara kwa sababu yako hahahaa..”

Baaada ya kuongea huku akicheka kwa kejeli palepale alisogea upande wa kulia wa kile kioo cha kuzuia mionzi na kukipiga ngumi kwa nguvu kubwa.

“Twiii , Twi, Twiit”

Ilionekana ndio namna maabara ilivyotengenezwa ili kuilipua njia ya mkato ya kuwasha bomu ni kupiga ngumi kioo na hicho ndio ambacho kilikuwa kikienda kutokea , hata hivyo maabara nyingi za kufanya majaribio ya siraha hutegeshewa bomu la kuiharibu kabisa pale panapotokea tatizo.

Muda uleule alivyoopiga ngumi kile kioo sauti kutoka kwenye tarakishi humo ndani ilisikika ikiwatahadharisha.

“Destruction Mode has been turned on , the labaratory will be exploding after the countdown , thirty .. twenty nine…”

“Ni mwisho haha , hatimae imekuwa mwisho”Aliongea Jeryy.

Roma alishangaa , hakutaka kumuua Jerry kwasababbu aliogopa siraha hio ya FURY ingelipuka , lakini sasa hivi maabara yote inakwenda kulipika , ilikuwa haiwezekani kwa yeye kuzuia kutokulipuka kwa bomu hilo la nyuklia.

Roma aligeuza macho yake na kumwangalia Clark aiekuwa kwenye mikono yake ambaye afya yake inaelekea ukingoni alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira

Baada ya kuona hana uwezo wa kuzuia mlipuko wa maabara hio pamoja na mlipuko wa FURY kitu pekee ambacho aliona angeweza kufanya ni kujiuoko yeye na Clark kuondoka katika hilo eneo.

Kufumba na kufumbua alikuwa ashatoka nae na kwenda kutua mbali kabisa na eneo hilo katika mlima na msitu usiokaliwa na watu, Kusini mwa nchi ya Austria.

Alikadiria kwa umbali huo hata kama bomu hilo la nyuklia litalipuka upande wa Ujerumani halitowaathiri kwa muda kupitia mionzi yake.

Baada ya kutafuta sehemu yenye majani makavu aliamua kumuweka Clark chini na kuanza kumfanyia uchunguzi wa mwili wake.

Haikuleta maana kwake kuomba msaada kwa muda huo , kwani aliona asingepata msaada huo ndani ya muda , hivyo kitu pekee ambacho alitaka kujaribu kufamnya ni kumpontysha yeye.

Mapigo ya moyo ya Clark yalikua ya chini mno na yalikuwa yakiendelea kuwa ya chini na muda wowote yangeacha kabisa kudunda na kupelekea kifo chake.

Roma alijikuta akijikatia tamaa mara baada ya kumungizia nishati ya mbingu na Ardhi kwa kuunganisha na ya Urejesho lakini bado alishindwa kumponyesha.

Mwili wake ulikuwa ni kama vile seli zake zinaoza ndani kwa ndani na hiko ndio kilichomuogopesha zaidi , kwani aliona dakika yoyote Clark angeweza kufa kwenye mikono yake maana tayari alishaanza kuwa wa baridi.

“Damn it … Clark , jarobu hata kuongea kidogo , ninaweza vipi kukuokoa?”Roma ujasiri wake wote ulimwishia na aliishia kuukumbatia mwili wa Clark huku akishindwa kuzuia machozi yaliochanganyika na hofu.

Ni mwanamke huyo ambaye hakulala usiku na mchana kwa ajili tu ya kumtengenezea dawa, na katika kipindi chote ambacho alihisi kuwa mpweke ni yeye pekee ambaye alifanya kila liwezekanalo kumsaidai , lakini sasa mwanamke huyo anafia kwenye mikono yake bila ya kuwa na msaada kwake.

Aliogopa kwamba bado hakuwa amelipa fadhila zake zote kwa yale aliomfanyia , alijilaumu na kuona yatakuwa makosa yake kuruhusu akifariki kwenye mikono yake kwani itamaanisha kwamba alishindwa kumlinda na maadui ambao aliwatengeneza yeye mwenyewe.

Clark alijitahidi kuamsha kinyonge sana mkono wake akimfuta machozi roma ,Roma hakujua hata alikuwa akilia alihisi maji yanaririka katika mashavu yake , lakini hakujua kama ni machozi yake .

“Ni sawa … wewe .. usilie tena .. nina furaha , mtu wa mwisho ninaemuona .. ni wewe”Aliongea Clark kwa kukata kata maneno.

Alishindwa kujizuia zaidi na zaidi mara baada ya mwanamke huyo kuongea kauli hio na alizidi kutoa machozi na kulia kwa kwikwi.

“Huwezi kuondoka hivi … utakuwa umenikatili sana ,,,, siwezi kujisamehe tena , umeniokoa mara nyingi sana na umefanya mambo mengi kwa ajili yangu ,, lakini mimi nashindwa kukukoa ,, sina thamani kabisa kwako , mimi ni mjinga”Aliongea huku akiinua mkono wake na kujipiga kibao kwa nguvu na kutokana kutumia nguvu za kijini ilisababisha mpaka majani ya miti kuanza kudondoka lakini bado aliendelea kujipiga vibao mara nyingi zaidi na kumfanya Clark azidi kutoa machozi ya kumuonea huruma na huzuni kwa wakati mmoja.

“Usi.. usi , fanye hivyo”Alijitahidi kuongea.

“Clark naomba usife , naomba usife tafadhari , siwezi kufikiria nitakuwa na maisha ya namna gani ukishaniach…”Alianza kulia kama mtoto huku akimwangalia mwanamke huyo kwa kuomba.

“Na.. naomba,, nikuulize swali na unijibu kabla sijafa?”

“Niulize chochote na nitakujibu”Aliongea haraka haraka.

“Roma … nataka tu .. kujua kama .., je .. unanipenda?”

“Ndio , Nakupenda , siku zote nilikuwa nikikupenda sana ,… wewe ni moja wapo ya wanawake ninaowapenda sana..”Roma aliongea bila kujiuma uma , hayo ni maneno ambayo hakupanga kumwambia mwanamke huyo katika maisha yake.

Zamani hakutaka kabisa kumsogelea mwanamke huyo kutokana na madhambi ya umwagaji damu alioyafanya, lakini baada ya kurudi Tanzania na kujipatia mke ndio kabisa hakutaka kumfanya mwanamke huyo mchepuko kwa kuamini alistahili kitu kikubwa zaidi.

Roma hakuwa na mashaka kabisa juu ya mapenzi yake kwa Clark, ni mapenzi ambayo hayakuanza jana wala leo , ni tokea alivyokuwa mdogo na kadri mrembo huyo alivyokuwa anakuwa alizidi kumpenda.

Mapenzi yake kwa mwanamke huyo yalikuwa sio ya kawaida ambayo yanaweza kueleweka kirahisi kwa binadamu.

Pengine katika dunia kuna wanawake wengi ambao aliwapenda na wao pia kumpenda na kumpa kila kitu na yeye kufanya kila kitu kushinda magumu yote kwa ajili yao lakini mapenzi yake ya kweli katika kumbukumbu zake yapo kwa Seventeen na katika uhalisia yapo kwa Edna na mpenzi anaemuona kama ndoto ni Clark.

“Kweli!?”Aliuliza Clark akiwa kama haamini na alijitahidi kufumbua macho yake ..

“Ni kweli , nilichokwisha kukisema ni ukweli , na unapaswa kuniamini , sijawahi kukuweka wazi kwasababu tu niliona hustahili kuwa na mtu kama mimi , … samahani sikukuambia hili mapema”Macho ya Clark yalionyesha kabisa kufurahishwa na kauli yake na tabasamu la furaha lilifunika uso wake .

“Honey … I knew it , you loved me..”Aliongea.

Roma alikuwa akilia hivyo hakuwa akiongea zaidi ya kutingisha kichwa tu kumwaminisha ni namna gani anamkubali huyo mwanamke.

Clark alipanua mdomo wake huku akiinamisha kichwa chini na alionekana kama anataka kung’ata kitu flani..”

Roma aliweza kuona lakini hakujua Clark anataka kufanya nini na alimwangalia kwa kuchanganikiwa.

“Collar …”Aliongea Clark kwa sauti dhaifu akimaanisha Kola ya koti lake.

Roma palepale alielewa sasa anataka kung’ata nini na alifanya haraka na kumsaidia kumpelekea karibu Kola ya koti ili kuweza kugusanisha na lipsi zake.

“Clark unafanya nini, kwanini unamg’ata Kola ya koti, ni kwa ajili ya nini?”Aliuliza lakini Clark hakuongea neno na muda huo alikuwa kama mtoto anaetafuna nguo kwani alifyonza kwa nguvu ule ukola wa koti mpaka ukaanza kujaa mate.

Ni muda huo huo aliweza kuona Ukola ule wa shati ukibadilika rangi na kuwa wa bluu ambayo haijakolea sana na kama sio kwa kuloana basi isingetokea

Wakati akishangaa palepale aliweza kushangaa mara baada ya Clark kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha baada ya kuonekana kumaliza alichokuwa akifanya na kadri dakika zilivyokuwa zikisogea ndio ambavyo alizidi kurudi katika hali yake ya kawaida.

“Unashangaa nini mpenzi? , sijafufuka ni kwamba tu sijafa”Aliongea huku akitabasamu.

“Wewe , umewezaje kufanya hivyo.. nini..?”

“Unataka kuuliza nimewezaje kurudi katika hali ya kawaida si ndio , basi ni kwasababu nimejiponyesha mwenyewe”Aliongea huku akijaribu kukusanya nguvu na kukaa mwenyewe chini.

Roma aliangalia ile Kola ya koti kwa mara nyingine jinsi ilivyokuwa na doa la rangi ya bluu na kisha akamgeukia Clark aliekuwa na uso wa furaha .

“Ulinidanganya?”

“Nani kakuambia udanganyike kizembe , mimi ni nani , mimi ni Profesa Clark, mwalimu wa mwanafunzi mjinga kama Jerry , hivi unadhani naweza kuzidiwa akili na mwanafunzi niliemfundisha mimi?”

Roma alikosa cha kusema, alimwangalia mwanamke huyo namna ambavyo aliweza kurudi katika hali yake ya kawaida kwa haraka sana na alijikuta akichoka kabisa na kujikalia chini.

“Huu ulikuwa ni mpango wako?”Aliuliza Roma.

“Ndio , hivi unafikiri ungeweza kunipata kwa kubahatisha , wakati nilipokuwa nikitumia tarakishi zao nilituma Link kwa siri katika satilaiti yenu , kama mwalimu nilimjua Jerry hakuwa vizuri kwenye maswala ya Compyuta hivyo hakuweza kujua ninachokifanya kabisa , nilijua tu kama mtafika maeneo ya karibu na nilipo basi mngehisi mawasiliano ni kama yameingiliwa kutoka ndani”Aliongea na kumfanya Roma asipinge kwani ndio alivyoweza kumpata.

“Kama ni hivyo vipi kuhusu Sumu ni nini kile?”

“Ile ni sumu kweli , niliweza kuchanganya aina mpya ya sumu nilioitengeneza pale, ni sumu ambayo inavilegeza viungo vya mwili na kukufanya uonekakane kama umekufa na kama hutachukua dawa yake basi utakuwa wa baridi kwa masaa ishirini na nne na ikiisha makali yake mwili utarudiwa na joto lake na utaweza kuamka , nilipanga kama wataniona nimekufa watatafuta sehemu ya kunizika au kunipatia matibabu na ndio nitajua namna ya kutoroka ,lakini hio ilikuwa ni mpango wangu wa mwisho kabisa kwani sikuwa na uhakika kama hawatachoma mwili wangu lakini nilipanga kama hakuna ambae atakuja kuniokoa basi moja kwa moja nitadanganya nimekufa ili kuepuka wasinidhuru, lakini bahati nzuri umeweza kuja ndani ya muda hivyo nikatumia mpango B”Aliongea na kisha akashika Kola ya koti lake.

“Nililoanisha hii Kola na dawa maalumu ya sumu ,ilihitajika tu mimi kunyonya na ndani ya lisaa limoja ninarudi kuwa sawa tena”

“Kama ni hivyo kwanini ulinichezea hila hata mimi , hivi ulijua ni kwa kiasi gani moyo wangu uliuma?”Aliongea Roma huku akisimama na palepale mrembo huyo alisimama na kupitisha mikono yake yote mwili katika shingo ya Roma na kumbusu kwenye paji la uso..

“Kama nisingetumia fursa hii , usingeweza kuniambia nilichotoka kusikia kutoka kwako kwa muda mrefu”Aliongea na wakati Roma anataka kuongea neno alizuiwa na lipsi laini za mwanamke huyo.

Baada ya busu jepesi , Clark alionyesha uso wa kuomba huku macho yake yakionyesha hali ya kutia huruma.

“Honey usinikasirikie , nilitaka tu kuwa na wewe kama mpenzi wako , nilijua kama hutoniambia nitakuwa na huzuni milele”

Roma alijiambia ile siku ambayo alikuwa akiiepuka kwa miaka mingi hatimae imewadia na hakujua anakwenda vipi kumwelezea mke wake kwa maneno marahisi na kumuelewa.

“Umeandaa mpango wako , ili kunifanya niingie katika mtego na ukanifanya nilie kama mtoto , aisee inatia aibu Daah”Aliongea Roma huku akitabasamu kwa uchungu na kumfanya Clark amwangalie kwa macho ya utani huku akimtolea ulimi nje kama anamcheka.

“Nilikuwa nikienda na hali inavyoruhusu , Jerry alinitishia kwenda kuwaua wale watoto wsio na hatia , sikuwa na chaguo lingine..”Baada ya kusikia hivyo alijikuta akikumbuka kitu alichosahau.

“Oh nimesahau kuhusu FURY Ujerumani ndio kwaheri”Aliongea.

“Haha.. nilikuambia kila kitu nilipanga mimi , unadhani ninaweza kutengeneza kitu hatari namna hio”

“Kwahio ulichotengeneza ni nini , ni feki pia?”

“Hebu fikiria , unadhani ninaweza kuhatarisha maisha ya mamilioni ya watu kwasababu ya watoto , hata kama niwe kwenye hali gani siwezi kwenda mbali kiasi hivyo , teknolojia ya FURY kwasasa ipo katika nadharia tu , inawezekana vipi kuitengeneza ndani ya siku mbili au moja? , kutengeneza tu elementi ya mwisho inayokamilisha kanuni inahitajika mchanganyo wa kikemia ambao unaweza kuchukua mwaka mzima kutoa matokeo”

“Kwahio unasema sasa hivi Jerry atakuwa na hasira sana mara baada ya kuona umemdanganya?”

“Labdal , Ujerumani naamini watashughulika na tatizo hilo , kwasasa ninafuraha ya nilichoweza kutimiza baada ya muda mrefu , Roma naomba unibusu japo kidogo tu”

“Nini!”

“Umesema unanipenda hivyo unapaswa kunifidia kwa miaka yote nilioteseka kwa ajili yako”Baada ya kuongea alifumba macho na kunyanyua kichwa chake juu kuweka mdomo vizuri ubusiwe.

Roma aliangalia Lips zake zilizokuwa nyekundu kutokana na weupe wake wa kizungu na kisha palepale alitoa tabasamu la kifedhuli na kumshika kiuno kisha akamvutia kwake.

Clark mpaka hapo alijua kabisa alikuwa amefanya kosa kwa kujirahisisha mbele ya mwanaume ambaye alikuwa kama Simba mwenye njaa.

Dakika moja mbele wote walikuwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa ulioitwa Busu, inasemekana wazungu wapo vizuri sana kwenye Kubusu na hicho ndio kilichompagawisha Roma.

MWISHO WA SEASON YA 19

SEHEMU YA 571.

Katika jiji la Palermo giza tayari lilikuwa lishatawala na katika uwanja wa kivita uliokuwa ukifanyia mashindano , ulikuwa mtupu kwa wakati huo ikimaanisha kwamba mashindano kwa siku hio yamesha mpaka siku inayofuata.

Katika siku hio ya kwanza hakukua na maajabu makubwa kwani wale wanajeshi kutoka mashindano yaliopita wote kwa pamoja wameweza kuingia raundi inayofuata na kwa wale wahudhuriaji wenyewe wanasema mapigano yenyewe yanaanza siku inayofuata katika raundi ya pili.

Katika Moja ya Balkonni ya hoteli ya Cassano , mwanaume wa makamo mzungu alievalia mavazi ya upishi meupe alionekana akiwa bize kucharanga samaki aina ya Salmoni kwa haraka sana na kwa ufanisi mkubwa.

Kila kipande cha samaki kilikuwa kikilingana na kingine ni hivyo tu kwamba vilikuwa na ukubwa kidogo ambao unamuwezesha mlaji kutafuna kipande kimoja chote kwa wakati mmoja.

Mbali kidogo na alipokuwa anafanyia kazi mwanaume huyo kulikuwa na meza kubwa ambayo wahudumu wawili walionekana wakiwa bize kumsaidia kuhudumia kila anachokamilisha kupika na kuweka mezani.

Katika meza Christen alinyanyua Glasi yake ya Champagne na kumnyooshea Rose kugonga zao Cheers ambaye alikuwa karibu yake.

“Aphrodite, unaonekana kutokuwa kabisa na wasiwasi , vipi kuhusu hiko kinywaji?”Ares ambaye alikuwa ameegamia kwenye kiti kivivu aliongea kwa kuonyesha sura ya dhihaka.

“Wasiwasi wa nini , nipo hapa kwa ajili ya burudani sio kuteseka”Baada ya kusema hivyo alimgeukia Poseidon ambaye alikuwa akikomaa na upishi.

“Poseidon vipi hiko chakula bado tu? Nina njaa mimi”

“Hakuna mtu kugusa chakula kabla sijamaliza ,atakae fanya hivyo nitahakikisha hali chakula nilichopika mimi”

Upande wa Magdalena aliekuwa kimya alikuwa kwenye mshangao , bila shaka alikuwa akimjua Poseiodon ni mpishi maarufu duniani aliefahamika kwa jina la Mr Kelphin lakini hakuwahi kuwaza mtu huyo huyo kuwa mwanajeshi wa jeshi la Marekani upande wa majini.

“Christen kuna haja gani ya kusubiria amalize kila kitu , kwanini tusianze kula?”Aliuliza Magdalena ambaye alikuwa na njaa.

“Ndio sheria ya Poseidon hio kama atajitolea kupika chakula basi hataki mtu akiguse mpaka aridhike kimekamilika , anajali sana mlo kamilifu kuliko kitu kingine chochote”

“Kwa maneno marahisi Miss Magdalena ni kwamba bwana huyo ni mpishi Mbishi sana kwahi kutokea”Aliongezea Stern na Rose na Magdalena waliishia kushangaa tu.

Dakika chache mbele Poseidon aliweza kukamilisha sahani za Sashimi na kuwekwa kwenye meza hio kubwa , katika meza hio kilichoonekana ni aina mbalimbali ya vitoweo vya baharini ambavyo vimepikwa katika ubora wa hali ya juu.

Na kabla ya kuwaruhusu kula aliwaambia wasiguse kwanza chakula chake mpaka apige Selfie na palepale alitoa simu yake ya I Phone Toleo la juu na kupiga picha mbalimbali ya chakula chake na kisha kupost mtandaoni kwenye akaunti yakeiliokuwa ikifuatiliwa na watu zaidi ya milioni.

Baada ya kutaniwa na ndugu zake kutoka sayari nyingine , hatimae aliweza kukaa sasa na kuwaambia wale wahudumu waondoke.

Ukweli Magdalena na Rose walipata fursa ya kushiriki kwasababu ya heshima ya Roma pekee , lakini chakula hicho cha usiku ni kama vile kimeandaliwa kwa ajili ya ndugu hao ambao ni mara chache sana hukusanyika pamoja kama hivyo.

“Hermes tayari upo ndani ya hoteli , kwanini usivue hilo lisuti lako , huoni kwamba ni wewe tu hapa ulievaa suti na joto lote hili?”Aliongea Christen huku akimwangalia Raphaeli aliekuwa amekaa pembeni yake.

“Kuwa na amani sisi Vampire miili yetu ni ya baridi”

“Mwacheni nani anajali kama anahisi baridi au Joto , kwanza unaweza kunywa damu na ukaishi , kuna haja gani ya kula na sisi?”

“It’s recognition to Poseidon ‘s Culinary arts”Alijibu.

“Haina haja , chakula changu kipo Perfect”Aliongea Poseidon akijigamba.

Rose na Magdalena waliishia kuangaliana pasipo kuongea chochote , na walijiambia Poseidon na yeye ni kama Roma tu hana aibu kabisa kwa matendo yake.

Chakula kilichokuwa mbele ya Ares kilipotea kwa haraka sana na baada ya kumaliza kila kitu alisimama na kuelekea upande wa Balkoni.

“Ares unaenda wapi?”Aliuliza Stern.

“Hilo nalo ni swali gani?”

“Sio muda sahihi wa kuwatafuta, au unadhania unaweza kuwashinda?”

“Sina muda wa kupoteza kula na nyie mpaka usiku wa manane mimi wala sitamani kuangalia mapigano ya kibinadamu ya Caesar Conference nipo hapa kwa ajili ya kupigana nao”

“Hey Bro unataka kuzaliwa upya katika mwili mwingine labda?”

“So what , nevet try never know , I am not interested in their conspiracies , I dare to go if you don’t”(“Kwani vipi , usipo jaribu huwezi kujua , sina matamanio ya uzushi wao , ninathubutu kwenda kama wewe huwezi”Aliongea na kumfanya Stern na Alcie kukunja sura zao kutokana na ukichaa wa Ares.

Muda huo huo Rose na Magdalena waliweza kuhisi msisimko maalumu ambayo ni kama vile ni mawasiliano yao na Roma na walijikuta wote wakiangalia upande wa nje na waliweza kumuona Roma akiwasogelea kwa kasi na walijikuta wakiwa na furaha.

Kufumba na kufumbua Roma aliweza kutua katika Balkoni huku akiwa na tabasamu pana.

“The Annoying Hades , you finally came back , we thought you run away in fear”Aliongea Christen akimtania kama walidhania amekimbia kutokana na uoga.

Roma aliangalia kila mmoja aliekuwepo na alionekana kuridhika kupitia macho yake.

“Naona kila mmoja ameweza kufika , hakuna chochote kilichotokea wakati nilipokuwa sipo, nilienda Scotland ndio maana nimchelewa kuja”Aliongea.

Alikuwa amempeleka Clark Scotland kwani walikuwa na jukumu la kushiriki katika sherehe za Summer Bank Holliday , yeye na mama yake.

“Kwasasa bado lakini ni swala la muda tu”Aliiongea Stern huku akimwangalia Ares.

Baada ya hapo Roma aliongea na wanawake wake na kuwatoa hofu kwamba tayari alifanikiwa kumpata Clark na kumrudisha nyumbani.

Baada ya kuelezea kwa ufupi kwa upande wake na yeye alimuuliza Christen kile kilichotokea wakati ambao hakuwepo na alielezewa kila kitu kwa ufupi na namna ambavyo Ares anapanga kutoka hapo na kwenda kuwatafuta akiwa peke yake.

Upande wa Roma hakuwa na msingi mzuri wa historia nzuri juu ya hadithi ya miungu ya kigiriki hivyo hakuwa na uelewa mkubwa na licha ya kusikia stori zinazohusiana na majitu hakuwahi kuamini kama kweli walikuwepo.

“Nakushauri usiende kwanza mpaka ufahamu mbinu zao zote”Alishauri Roma.

“Acha kunidharau , Hades usijifanye wewe una nguvu kunishinda mimi kwasababu tu mara ya mwisho ulinishinda , kipindi kile sikuwa makini na nilikudharau na mbinu zako za kichawi”

“Kama unajiamini basi hakuna wa kukuzuia kufanya kile unachotaka, ni sawa kama unataka kufa lakini haitakuwa vizuri kwasisi kuja kuulizwa baadae”Aliongea Roma na kisha akajifanyisha kufikiria.

“Unaonaje ikawa hivi , kwasababu una uhitaji wa mtu wa kupigana nae , kwanini usipigane na Raphaeli”

“Damn it Hades , unanitania , nani anataka kupigana nae?”Alijitetea Hermes.

Ares baada ya kuambiwa pigane na Raphaeli alionyesha kuwa katika hali ya furaha mno , ukweli ni kwamba mikono yake ilikuwa ikimuwasha muda wote , hakujali kama angeweza kushinda au kushindwa alitaka kupigana tu.

“Hehe.. Hermes wewe ndio ulijifanyisha kuwa Farid kule Tanzania si ndio?”

“Farid !!, yupi huyo?”

“Haishagazi kwa mtu kama wewe kukosa makando kando na haina haja ya kujifanyisha hujui ninachomaanisha, ijapokuwa sijui kwanini ulileta mkanda wa kichawi feki Tanzania lakini haitokei tu ukaamua kunichokoza mimi peke yangu”

“Unamaanisha nini? , Hermes ule mkanda wangu feki ulionekana Tanzania wewe ndio uliehusika na kuzusha habari hizo?”Aliuliza Christen kwa mshangao.

“Aphrodite unaamini vipi anachoongea , kwanini nifanye kitu cha namna hio kwa faida ipi kwa mfano?”

“Acha kongea ujinga , Hades hawezi kuongea bila kuwa na ushahidi na zaidi ya yote Hermes tumejuana kwa muda mrefu tokea katika syari yetu, siku zote ukidanganya unakuwa na utulivu wa hali ya juu mno”

“Wewe..”Alitaka kuongea lakini aliishia kimwangalia Poseidon na wengine wanavyochukulia swala hilo.

“Mnaonaje na nyie , mnadhani ni mimi niliefanya kitendo hiko , mnamuamini Hades anachoongea tofauti na mimi , nitapata faida gani nikifanya hivyo kwanza?”Alijitetea. na Stern na Alice hawakuongea chochote na kuweka sura za maigizo.

“Hermes your skills in deception is not as good as your illusions”Aliongea Poseidon akimwambia uwezo wake wa kudanganya ni mdogo kuliko uwezo wake wa kutengeneza udanganyifu.

“Poa, nakubali kwamba wote nyie mnanijua vizuri , na nakubali nilifanya mimi , lakini sababu kubwa ni kwamba nilikuwa ninajisikia vibaya hivyo nikaona nikamchokoze Hades , kuna ttatizo juu ya hilo?”Aliongea kinafiki alikuwa akijua anadanganya.

“Hehe.. Hermes sijali sana kuhusua mambo yako ya kishenzi unayoyafanya , kama kweli umekasirika sasa hivi kwanini usitolee hasira zako kwangu kwa kujaribbu kunipiga”Aliongea Ares.

“Pumbavu , nina hasira kweli , lazima nikufundishe adabu wewe mshenzi”Aliongea kwa hasira huku akisimama na alimwangalia Roma kwa dakika kadhaa na kisha alisogelea Balkoni na kupotea nje na mabawa yake kama vile ni Makerubi akimfukuzia Ares.

“Aphrodite , Hermes ndio aliezusha uzushi juu ya mkanda wako wa kichawi , huna mpango wa kwenda kuungana na Ares kumshikisha adabu Hermes?”Aliuliza Alice akitania.

“Hapana, uwezekano wa sisi kushinda au wa Hermes kutushinda ni asilimia hamsini kwa hamsini, nilikuwa nikijaribu kukaa upande wa Hades tu hapa , sijali kati yenu anaetumia jina langu kwa mambo yenu”

“Vyovote vile , lakini kumuacha Hermes kwenda kushindana na yule kichaa ili tu kutoa hasira zake ni sawa na kupigana na yale Majitu tu”Aliongezea Stern huku akicheka.

“Ni wazi kabisa wametuleta hapa kwa makusudi , vinginevyo wasingeenda ndani ya hoteli ambayo ulipanga kukaa Hades , inaonekana wanasubiria wote tuwe sehemu moja ndio watushambulia , hivyo kwa muda kama huu kama tutakuwa na haraka na kukosa mpango lazima tutaingia kwenye mtego wao , hivyo tunapaswa kusubiri kuona ni nini wanatuandalia , isitoshe Athena hayupo hapa na hatuwezi kujihakikishia ushindi wa moja kwa moja”Aliongea Poseidon.

“Mbona unamuamini sana Athena?”Aliuliza Roma.

“Tayari nasikia umekutana nae na kuona uwezo wake , je sipaswi kujiamini?”Aliuliza na kumfanya Roma kushindwa kuongea chochote , ukweli ni kwamba katika nyakati zoe ambazo aliweza kukutana na Athena hakuweza kufanya chochote mbele yake , tukio la Korea kusini halikuwa limefutika katika akili yake na kila siku alikuwa akifikiria ni kwa namna gani anaweza kuwa katika levo za juu kumpita Athena.

Lakini kwa wakati mmoja alishindwa kuelewa ni kwa namna gani hao watu wenye asili ya Ujitu wametoa wapi hali ya kujiamini mpaka kujitokeza na kuanza kuwachokoza makusudi.

****

Siku nyingine ya mashindano iliwadia katika jiji la Palermo , watu wengi walikuwa wakitarajia kwanzia siku hio mashindano yangekuwa ya moto sana kwani makundi makubwa makubwa ndio ambayo yalikuwa yakikutana.

Kila mmoja aliekuwa akimfahamu Roma alifurahi kwamba amerudi na alikuwa akishiriki , Kwa Sauron alonekana kama vile amezeeka tu ndani ya siku mbili zilizopita lakini mara baada ya kumfuata Roma hotelini asubuhi kidogo hali yake ya utulivu ilimrejea.

Roma hakuwazuia wasiendelee na uchunguzi, alihitaji kujua zaidi kuhusu tukio lile , alitaka kujua kuhusu kundi la kigaidi ambalo limemteka Clark na kutaka kuunda siraha ya kimaangamizi ya teknolojjia ya FURY.

Kwa wakati huo uchunguzi ulikuwa ni rahisi kutokana na kwamba Umoja wa Norh Buyeo kutoka Korea ulikuwa ukijihusisiha , hivyo Roma alimpa kazi Makedon na wengine kujaribu kutafuta nguvu ambayo ipo nyuma yao na pamoja na mipango yao yote.

Wakati mashindano yanaanza Roma alikuwa eneo la VIP huku kulia na kushoto akiwa na Mage na Magdalena.

Upande wa Magdalena alikuwa na aibu sana asubuhi hio kumwangalia Roma usoni , pengine huenda ni kwasababu ya kile kilichotokea usiku kucha.

Ukweli ni kwamba baada ya chakula cha usiku Rose yeye alichukuana na Christen na kusingizia wanaenda kufanya Shopping , ilikuwa ni usiku ndio kakini maduka katika jiji la Palermo yalifanya kazi masaa ishirini na nne na watu ambao walikua ni maarufu maarufu wanaofika katika jiji hilo walikuwa wakifanya Shopping usiku ili kuepuka macho ya wengi.

Sasa kilichotokea ni kama kuna mpango ambao Rose na Magdalena walikuwa wamepanga , kwani wakati Rose alivyotaka kwenda kufanya Shopping Magdalena yeye alisema amechoka na alitaka kulala, upande wa Roma na yeye alikuwa amechoka kwa kutolala siku mbili mfululizo hivyo alitaka kupumzika.

………….

Kutokana na wote kupewa chumba kimoja basi ilitokea , Roma na Magdalena wakalala kitanda kimoja.

“Magdalena vinauma?”Ni sauri ya mwanaume iliosikika usiku wa jana katika chumba cha hadhi ya juu alichokuwa akilala mfalme Pluto.

Licha ya mwanaume kuuliza swali la namna hio , hakukuwa na majibu kutoka kwa mwanamke mrembo aliekuwa amelaliwa kwa juu na mwanaume aliejengeka mwili kimazoezi, upande wa yule mwanamke alionekana kuwa katika raha ya ajabu kiasi kwamba alitumia miguu yake na kuipitisha katika kiuno cha mwanaume yule.

“Arggh..”Mwanamke alitoa mguno huku akiachama kama vile kabanwa na mlango , alionekana alikuwa akipitia hali ya maumivu na raha kwa wakati mmoja

“Samahani , lakini inaonekana kubanwa sana ndio maana unasikia maumivu”Aliongea mwanaume kwa sauti ya kunong’ona, ilionekana kwa upande wa mwanamke kinachoendelea kwake kilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanyiwa.

“Ni sawa tu , nitapona kwa haraka , isitoshe na mimi pia sio wa kawaida”Ilisikika sauti nyororo ya mwanamke.

“Kama ni hivyo basi nitaanza kuchezesha kiuno”

“Sawa , usije kunifanya niijutie hii siku”

“Usijali , nitahakikisha hii siku unaikumbuka katika maisha yako yote”Aliongea yule mwanaume kwa besi na kisha makalio yake yalionekana kubonyea chini.

“Argh…!!”

…………….

Naam hayo ndio maongezi yaliosikika nje ya mlango wa chumba cha mfalme Pluto usiku wa jana.

Sasa wakati wakisubiria pambano lianze , ndio Roma alimuuliza mrembo Rose namna usiku wake wa Shopping ulivyokuwa na mrembo huyo alimwelezea kwa ufupi.

“Hakuna kikubwa kilichotokea”Alijibu Rose.

“Pengine anaona aibu , jana kanunua nguo za ndani kibao ambazo zimekaa kiuchokozi uchokozi”Aliongea Christen bila aibu na kumfanya Rose amkazie macho na alijikuta akiona aibu, Bahati tu waliokuwepo karibu yao ni Stern na Alice , angejisikia aibu sana kama Ron na Sauron wangekuwepo hapo.

Christen hakujali namna Rose alivyokuwa akimwangalia na alitoa ulimi kumtania na kisha akageuza shingo yake mbele.

“Kama ni hivyo , hakikisha unanunua za kutosha”Aliongea Roma akiwa na uso uliokaa kifisi.

“Haikuwa hivyo..Usimsikilize Christen”

“Najua , mimi natoa maoni yangu tu , ila usisahau usiku wa leo nataka kuona namna utakavyopendez… sawa Babe?”

………………

Wakati wakiendelea kuongea hatimae ilifikia zamu ya The Eagles , washindani wao ilikuwa ni kundi la Kimasenari lifahamikalo kwa jina la Odin Mercenary Corp, walikuwa na makazi yao Kaskazini mwa ncha ya dunia.

Rose na Magdalena mara baada ya kuona ni watu wa Roma waliweza kuongeza umakini , lakini upande wa Roma alionekana kabisa kutopenda sana kuangalia maishindano ya aina hio kwani yalikuwa ya kawaida sana kwake.

Lakini licha ya hivyo alifurahi kuona wanajeshi wake walikuwa wameimarika sana , hususani Maninja upande wa New Zero kwani walionyesha uwezo mkubwa katika kupambana na wapiganaji wa kundi la Odin, mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa The Eagles waliibuka washndi na kuigia katika hatua inayofuatia.

Roma ndio aliekuwa wa kwanza kuondoka na hakuwa na mpango kabisa wa kurudi tena, upande wa Rose mara baada ya kuona Roma kaondoka katika hilo eneo na yeye alifuata nyuma nyuma lakini kwa Magdalena yeye alisema ataangalia mashindano hayo mpaka mwisho

Ukweli ni kwamba alitaka kuendelea kuangalia , ila tu kumpa nafasi na Rose kuwa karibu na Roma kwani usiku wa jana kama sio Rose basi huenda asingeweza kuonja dunia ya mapenzi kwa mara ya kwanza katika maisha yake, alikuwa na raha na akili yake yote ilikuwa ikiwaza usiku wa jana wote aliofanya mapenzi na Roma.

Hakuwaza rena kama Roma alikuwa mpenzi wa pacha mwenzake au mume wa rafiki yake wa utotoni Edna , bali muda huo alijiambia amefanya maamuzi sahihi kufata kile moyo wake unachotaka.

Wakati Roma na Rose wanakaribia hotelini waliweza kukutana na mwanaume wa Kijapani , Rose alionekana kumfahamu mwanaume huyo na upande wa Roma pia alikuwa akikumbuka sura ya mwanaume huyo, alikumbika kipindi alichosafiri kwenda Japani akiwa na Dorisi aliweza kukutana na huyo mwaname katika kambi ya jeshi wakati akienda kumpatia mateso Kapteni Kisu Mvunjiko na alishangaa kumuona akiwa hapo kwani alikuwa na cheo kikubwa mno serikalini.

Roma ilibidi kwanza amhoji Rose inakuwaje akawa anamfahamu huyo Mjapani na ndipo alipomuelezea kwamba alikutana nae usiku wa jana akiwa na Christen na huyo mwanaume ndio aliewasogelea na kuwachombeza kwa ajili ya kwenda kumpa huduma usiku kucha kwa malipo ya hela , lakini Christen akamjibu kwa kumwambia yeye atamlipa kwa kila pigo atakalompiga na ndio akaondoka na kuwaacha.

Roma mara baada ya kusikia hivyo aliguna , aliona sio jambo la kawaida kigogo wa serikali kutoka Japani ghafla tu kumsogelea Christen na Rose na kuwataka wampatie huduma.

Baada ya kuingiwa na wasiwasi ya uwepo wa mwanaume huyo hapo Sicilly haraka sana alimpigia simu Sauron na kumpa maelekezo ya kumfanyia uchunguzi , hisia zake zilimwambia huenda alikuwa akihusika na wale watu wa mavazi meupe au kundi la Cyclops.

*****

Ikiwa ni muda wa jioni kabisa wakati Roma akiwa ameuchapa usingizi mara baada ya kazi nzito alioifanya na Rose mlango wa chumba chao ulifunguliwa na Magdalena.

Mara baada ya kuona namna Rose na Roma walivyolala wakiwa hawana nguo mwilini alijikuta akiona aibu , lakini alijitahidi kujikaza na kwenda kumuamsha Roma.

Roma mara baada ya kuamka hakuona aibu licha ya kwamba alikuwa uchi yeye na Rose na alienda mbali kumtania Magdalena na kumwambia ajiunge na yeye lakini Magdalena aligoma na kumwambia kwamba amekuja hapo kumpa taarifa kwamba wenzake wanamuhitaji katika eneo lileile la siku ya jana kwa ajili ya maongezi.

Roma mara baada ya kupewa taarifa hio hakuwa na muda wa kupoteza , alikuwa na hamu kubwa ya kuwajua kiundani watu alioambiwa wana aasii ya Ujitu ndani yake hivyo ndani ya dakika chache tu alikuwa tayari amekwisha kujiandaa na kutoka.

Roma mara baada ya kufika aliweza kukuta kila mmoja alikuwa amekaa katika nafasi yake na yeye pia alisogelea kiti na kuketi , lakini wakati huo akiangalia barua iliokuwa juu ya meza.

“Nini kinaendelea hapa , hio ni nini?”Aliuliza Roma na kumfanya Christen aliekuwa akimwangalia Roma muda wote katika eneo la chini ya kiuno chake palivyotuna kuvuta mdomo na kisha kuchukua ile barua na kumpatia.

“Je ungependa kujifunza lugha yetu?”Aliuliza na kumfanya Roma kuangalia ile barua ilioandikwa kwa herufi zisizoeleweka na kumrudishia Christen.

“Haina haja , ninajua lugha nyingi sitaki kuongeza nyingine kwenye kichwa changu , niambie barua hii inahusu nini”

“Ni rahisi tu , ni kwamba kiongozi wa Cyclops anaefahaika kwa jina la Brontes ametutumia mwaliko , anatualika sisi wote kwenda kupata chakula cha mchana katika mgahawa siku ya kesho baada ya awamu ya kwanza ya mashindano ya asubuhi”Aliongea Poseidon.

“Kwanini wanataka kukutana na sisi? , hawajawahi kututafuta hapo kabla”Aliuliza Roma.

“Hata sisi imetushagnaza pia , wanaonekana kama hawatafuti kulipiza kisasi na wanajaribu kutualika namna hii , wanajaribu kufanya nini?”Aliongea Stern.

“Kwanini tujali wanachotaka , huenda wametualika kwa ajili ya kumaliza tofauti zetu , lakini kama wanataka kupigana na sisi tutapigana na kama wanataka amani tutawaacha waendelee kuishi”Aliongea Ares na kufanya wote wamwangalie kwa mshangao kidogo lakini haa hivyo washazoea Ares amekaa kifujo fujo.

“Hivi wasiwasi wenu ni kwamba tunaweza tusiweze kupambana nao?”Aliuliza Roma baada ya kimya cha muda mfupi.

“Kama tungekua kwenye sayari yetu , wasingethubutu hata kutusogelea na ningewapiga mimi mwenyewe, lakinii sasa hivi mambo ni tofuati bila ya Athena na Zeus tunaweza tusifanikiwe kuwashinda ijapokuwa tutakuwa na uwezo wa kujilinda”Aliongea Hermes.

“Mimi nipo , yupo pia Rose na Magdalena ambao wote wapo katika levo ya Nafsi , je bado tu haitoshi , kwanini tuwaogope?”Aliuliza Roma.

“Hades unawachukulia poa hawa majitu , ngoja nikuambie Cyclops na Hecatoncheires wanao uwezo mkubwa kuliko jamii zote za majini na hawaathiriki na nguvu za mbingu na ardhi kwasababu wana damu ya kizazi chetu , Damu ya Titan”Aliongea Artemis.

“Damu ya Titan!!?”Aliuliza Roma kwa mshangao.

“Ndio …”Alice aliwaangalia wenzake kuona kama kuna ambaye anajaribu kumzuia na baada ya kuona wapo kimya aliendelea.

“Damu ya Titan ndio asili yetu kamili na sisi ni mwendelezo wa kizazi cha damu yake , ndio chanzo kikubwa cha nguvu zetu wakati tulipokuwa kwenye sayari yetu m sababu ambayo imetufanya uwezo wetu kushuka kufikia asilimia therathini ni kwasababu tulikosa miili yetu yenye asili ya damu ya Titan , hawa Majitu wenyewe ni sehemu ya uzao wetu hivyo wana asili ya damu ya Titan na kama tulivyosema mwanzo, wao walikuja duniani na wakaweza kuishi kwa miili yao lakini sisi ikashindikana, Mpaka sasa hivi damu yetu ipo Sealed”

“Hebu subiri kwanza , nilikuwa nataka siku zote kuuliza ilikuwaje miungu mkapoteza uwezo wenu kwa kiasi kikubwa , kama kweli hii damu ya Titan ndio chanzo cha nguvu zenu , kwanini ipo ‘Sealed’ mpaka sasa , je swala hili lina uhusiano na moyo wa Gaia?”Aliuliza Roma.

“Kuhusu hilo..”Alice alitaka kuongea lakini alisita lakini palepale Christen na yeye aliingilia.

“Usiulize maswali Hades , kwetu kumbukumbu hizo ni maumivu makali kila zinapojirudia .. nitaendelea kukuelezea kwa niaba ya Alice, hawa majitu wanao uwezo mkubwa kutokana na kuwa na damu ya Titan na ndio maana hawaogopi kabisa watu wanaovuna nishati za mbingu na ardhi , kwasababu ni nishati ya muunganiko wa dunia hii , Damu ya Titan unaweza kusema ina nguvu ya Kiroho kama mnavyopenda kuita hapa duniani , sasa unatakiwa kujua ni Zeus pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kutumia mwanga kuifubaza nguvu za damu hio na kuwafanya wawe dhaifu , hivyo hakuna mtu ambaye anaweza kuwashinda hata Athena mwenyewe hakuwa na uwezo huo”

“Kwa maelezo yenu mnaamaanisha kwamba tunapaswa kufa kwenye mikono yao si ndio?”Aliuliza Roma huku akitabasamu kwa uchungu

“Hatuwezi kwenda mbali hivyo , kwasasa hatujui ni ipi mipango yao na isitoshe una nafasi kubwa , angalau unaweza kutumia kanuni za anga pamoja na nguvu za nishati ya mbingu na ardhi , lakini hata hivyo inatia huzuni kwasababu haupo kwenye levo ya juu zaidi ya kuweza kudhibiti Radi kama Majinni tuliokutana nayo kipindi tunafika la sivyo ungekuwa tishio kwao”Aliongea Poseidon.

Roma alijiambia hata kama hakuwa katika levo za juu kama watu waliowakuta miaka hio , lakini yeye alikuwa na chungu cha maafa hivyo alijiambia kwamba mwisho wa kila kitu bado haujulikani kama watapambana.

Hao watu kilichomuudhi sana ni kwamba ni wasiri sana kuhusu hio damu ya Titan na alijua kabisa ameelezwa nusu na ni kitu ambacho kinahusiana na moyo wa Gaia

Baada ya mazungumzo ya muda mfupi Poseion alimtaka Hermes kunagalia Ulingo kama haujawekwa mtego ili kuwa salama na haikuwa tatizo kwa Hermes kulingana na spidi yake

******

Siku ya tatu hatimae iliweza kuwadia na makundi therathini na mbili yalikuuwa ndo yamebakia , wawakilishi mbalimbali kutoka serikalini walikuwepo.

Kama kawaida Poseidon , Hermes na Ares walikuwa katika eneo lao la sku zote na Roma , Magdalena , Rose Alice , Stern na Christine wlaikuwa wamekaa katika eneo moja.

Kabla ya mashindano kuanza Roma aliweza kupokea ripoti kutoka kwa Makedoni juu ya baadhi ya chunguzi alizomwambia Sauron afanyie kazi.

Na kwa maelezo yake ni kwamba mwanaume wa Kijapani aliemuona katika hoteli ya Cassano alikuwa akifahamika kwa jina laKagawa Chusho na ni waziri wa ulinzi wa Japani na hana uhusiano wowote na kundi la watu wa mavazi meupe , lakini alimwambia kwamba wakati ambao alimuona hotelini ilionekana kulikuwa na kikao kilichokwisha kufanyika hivyo hawakuwa na uelelwa nini kilitokea au kilizungumzwa katika kikao hicho ndani ya hoteli ya Cassano.

Roma kuna hisia ambazo zilimwambia kabisa huenda serikali ya Japani ilikuwa ikihusika kabisa na uwepo wa hawa Majitu hapo Sicilly lakini hakuwa na namna ya kuthibtisha dukuduku lake kutokana na kwamba alijua fika kikao ambacho kilifanyika ndio kilikuwa na taarifa kamili lakini kwa bahati mbaya walichelewa kugundua mapema..

Wakati ambao Roma alikuwa katika mawazo alikuja kushituliwa na Sauron aliekuwa anakuja mbio mbio kwake .

“Your Majesty Pluto something is wrong”Aliongea Sauron akimwambia kuna tatizo.

“What are you saying?”(Unaongea nini?”);

‘Hapa , hebu angalia wahusika ambao wanakwenda kushiriki katika mecho inayofuatia”Aliongea Sauron na kushika Kishikwambi alichokuwa ameshikilia Sauron.

“Mechi inayofuata ni The Eagles na Deicide?”Aliongea Roma kwa mshangao akimaanisha kwamba mechi inayokwneda kuanza ni kati ya Majitu wanaojiita godkiller na wanajeshi wake wa The Eagles.

“Nini kimetokea , nilijua wanakwenda kukutana katika nusu fainali tu?”Aliuliza Roma huku akiwa na wasiwasi na kuanza kupitia orodha ya wanajeshi wake ambao wanakwenda kushindana katika mechi inayofuata.

“Kuna mtu ambaye amebadilisha na meneja anasema ni makosa tu yaliofanyika , nadhani ni makusudi kabisa wanataka tukutane kwanza na hao wauaji ili watudhalilishe kututoa katika mashindano mapema“Aliongea Sauron kwa hasira.

Lakini licha ya hivyo ni kama washachelewa , kwani tayari wanajeshi wa The Eagles walionekana wakiingia kwenye ulingo na walionekan kuwa na mchecheto mara baada ya kusikia wanakwenda kupambana na kundi la Deicide watu waliowaonyeshea kiburi katika hoteli ya Federico.

Wakati Nasri na wenzake wakiwa na shauku ya kulipiza kisasi kwa kuwashikisha adabu watu hao, upande wa Roma alikuwa na wasiwasi kwa kile kinachokwenda kutoktea kwa kuamini kwamba wanajeshi wake hao hawana uwezo wa kushinda na kwa mara ya kwanza jeshi lake linakwenda kudhalilishwa.

Makofi ya shangwe na vifijo yalisikika pande zote baada ya wanajeshi wa mavazi meupe kuingia kwa mbwembwe zote na baada ya kufika katikati waligeuka upande ambao wamekaa Poseidon , Roma na ndugu zake na kuwaangalia , ijapokuwa sura zao hazikuwa zikioneana kwa kuvaa Mask lakini likuwa ni kama vile walikuwa na sura za kejeli.

ITAENDELEA WIKIEND NJOO WATSAPP TUPIGE STORI NAMBA 0687151346
Naaam
 
[emoji15][emoji15][emoji7]
 
Yaan nyie mmeshajihesabia haki kwamb lazm awaburudishe hiv hamuon anachoka kuandk na kutunga event nzr kweny stor
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR
Mono no aware.

SEHEMU YA 629.
Ijapokuwa Najma alikuwa amepata kazi ya hadhi yake lakini bado mshahara wake haukumtosha kununua gari pamoja na kuweza kulihudumia, hivyo kitendo cha kutumia Taxi pamoja na Uber kwenda na kurudi kazini ni kama ilimpa nafasi Naibu waziri Salihi kujenga nae ukaribu kwa kumpatia Lift.
Roma sasa baada ya kupata wazo hilo ndio aliona umuhimu wa kumnunulia gari Najma.
Najma alitaka kuchagua IST gari ya kawaida lakini Roma aligoma kwa kuona gari hio haikuwa na usalama mzuri lakini pia haikuwa ikiendana nae kimuonekano kama mwanamke wake ,hivyo aliamua kumchagulia Mercedenz benz E class Amg 53 ya rangi ya pollar white mettallic ambayo iligharimu zaidi ya Dollar elfu tisini.
Najma alihofia kwa kuogopa gari hio inauzwa hela nyingi lakini Roma alimtoa hofu na kumwambia anao uwezo wa kumnunulia ya thamani zaidi ya hio ili mradi tu iwe na vipengele vya kiusalama wakati wa kuitumia.
Roma hakujali sana kuhusu bei alichojali ni usalama wa gari wakati wa kuendesha ndio maana aliichagua , alifurahi pia kuona Najma alikuwa akijua kuendesha gari hivyo alimwambia aanze kufuatilia leseni.
Roma alikuwa na hela ambazo alizipata Korea kusini baada ya kumuuzia babu yake Yezi vidonge hivyo haikuwa shida kwake kufanya malipo ya haraka haraka na ilikuwa kama bahati kwani Fredi alimwambia gari hio ipo Showroom na ni mpya kabisa Zero kilometer na waende wakaikague, upande wa Roma aliona ni bora wachukue hio kuliko kuagiza nje ya nchi jambo ambalo lingeifanya kufika kwa kuchelewa.
Fredi alikwua ni ndugu yake Roma aliekuwa akijihusisha na uuzaji wa magari kutoka Ulaya , ndio yule ambaye aliwaalika Edna na Roma kwenye sherehe yake ya kuzaliwa na kumfanya Desmond kutaka kumbaka Edna akisaidiwa na Kizwe ndani ya Maple Speed resort.
Upande wa Najma hakuwa na shida na alikuwa tayari kupokea chochote ambacho anapewa na mpenzi wake Roma.
Juma yeye alifurahi kuona dada yake kapata gari ambalo linaendana na muonekano wake lakini kwa wakati mmoja alishangazwa na wepesi wa Roma kutoa zaidi ya milioni miambili za kitanzania kwa ajili tu ya kununua gari.
Roma hakukaa sana nyumbani kwa Juma na baada ya sherehe kukaribia mwisho mwisho alimchukua Najma na kuondoka nae kuelekea posta waterfront sehemu ambayo alielekeza Fredi ndio Showroom yake ya magari inapopatikana.
Roma alikuwa na mpango wa kurudi Iringa siku hio hio kwa gari hivyo hakutaka kupoteza muda mrefu kubakia Dar , isitoshe kile kilichomleta alikuwa ameshakifanyia kazi.
Wakiwa ndani ya gari Roma alimuuliza Najma juu yamaendelo yake ya kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi na alisema anaendelea vizuri japo hakuwa akijua yupo levo ya ngapi lakini ashaanza kuelewa vitu vichache na Roma alimtia moyo kwa kumwambia ajipe muda wa kufikiria ndio ingekuwa rahisi kwake kuweza kujifunza kwa haraka na ubongo wake kupanuka na kuweza kuelewa siri juu ya uhusiano wa mbingu na ardhi.
Upande mwingine mara baada ya Naibu waziri Salihi kuachana na Roma moja kwa moja alielekea ofisini kwani ilikuwa ni muda wa kazi bado, ijapokuwa hata kama asingerudi hakuna ambaye angemuuliza lakini kutokana na kutaka kuweka mfano mzuri kwa wafanyakzi walio chini yake basi alijitahidi kuonekana kazini muda mwingi.
Hata hivyo hakuwa na muda mrefu tokea ateuliwe kuwa naibu waziri , alikuwa na miezi mitatu tu ofisini , yaani yeye na Najma walipishana mwezi mmoja tu yeye akiwa amemtangulia.
Bwana huyo mara baada ya kuwasha tarakishi yake na kufanya kazi kwa muda mfupi aliishia kuegamia kwenye kiti chake huku akionekana kukosa utulivu wa kimawazo.
Picha ya Najma kukumbatiana kimahaba na Roma
ilikuwa ikimsumbua katika akili yake na kumpelekea kukosa utulivu wa kimawazo.
Ukweli ni kwamba mwanzoni aliona pengine Sophia alikuwa akimdanganya juu ya kuwa na mpenzi , aliona huenda ni mbinu tu za Najma kutaka kumkataa pamoja na aibu za kike na hilo lilimpa hamasa zaidi kwani kwa muonekano wake pamoja na hela alizokuwa nazo ni wanawake wachache sana ambao walikuwa na uwezo wa kumkataa hivyo kitendo cha Najma kumkataa kilimpa hamasa ya kuweka juhudi ya kumpata zaidi na zaidi.
Lakini siku hio aliweza kuthibitisha maneno ya Najma mara baada ya kumuona akikumbatiana na mwanaume mbele yake kimahaba , kwake ni kama amepigwa kofi la uso jambo ambalo kwenye maisha yake halijawahi kumtokea.
Lakini licha ya hayo bado hakuwa amekata tamaa , ukweli ni kwamba sura ya Roma ilikuwa ikija na kupotea katika akili yake na hakuwa akimjua vizuri na hio yote pengine ni kutokana na kuishi nje ya nchi kwa muda mrefu akifanya kazi ubalozini pamoja na Umoja wa mataifa kabla ya kurudi Tanzania.
Alikuwa amekariri namba ya gari ya Roma pamoja na jina lake fupi na wakati akiwa njiani aliweza kuwasiliana na mtu aliemfahamu yeye ili kumsaidia
kumchimba Roma ni nani kwa kuamini kama angepata kujua jina la usajili wa gari yake basi
angepata jina lake kamili na kuweza kufatilia taarifa zake, hakutaka kumpotezea kutokana na kwamba alionekana ni wa kawaida katika macho yake.
Wakati akiendelea kuwa katika hali ya mawazo kuwaza namna ya kuushinda moyo wa mrembo Najma simu yake ilianza kuita na haraka haraka aliichukua na kuangalia jina la mpigaji na aliishia kutoa tabasamu.
“Umefanikiwa?”Aliuliza mara tu baada ya kupokea simu.
“Ndio mheshimiwa, Gari hio ilisajiliwa kwa jina la Shedrack Kengeu kabla ya kuhamishiwa usajili wake kwenda kwa Roma Ramoni mmiliki wa sasa , kwa taarifa nilizoweza kupata ni kwamba ni mume wa Edna Adebayo mwenyekiti na mmiliki wa kampuni ya Vexto international , hakuna taarifa kubwa zaidi kuhusu yeye ila alishawahi kuwa mgurugenzi wa kampuni ya Vexto Media”
“Vipi kuhusu familia yake?”
“Taarufa ambazo zipo kwenye Database ya serikali zinaonyesha alikuwa ni Yatima kabla ya kulelewa nchini Marekani , amemaliza pia ndani ya chuo cha Harvard shahada yake ya kwanza ya masoko, tofauti na hivyo hakuna kitu cha maana sana kuhusu CV yake”Aliongea na kumfanya Naibu waziri Salihi kushangaa kidogo
Ukweli ni kwamba taarifa aliopatiwa haikuwa kamili kutokana na cheo chake hivyo asingeweza kupewa kila taarifa inayohusiana na Roma, ijapokuwa Roma alishatambulika kwa baadhi ya watu kama mtoto wa Raisi Senga lakini bado ni taarifa ambayo haikuwa ikijulikana kwa watu wengi na watu baadhi waliishia kukisia tu Raisi Senga alikuwa na mtoto mwingine wa kiume lakini haikufahamika moja kwa moja kama alikuwa ni Roma Ramoni, pengine ni kutokana na kwamba jina hilo halikuwa na uhusiano wowote na familia ya Afande Kweka.
Ukiachana na kwamba hakuwa ameishi Tanzania kwa muda mrefu lakini alikuwa akifahamu kampuni ya Vexto, kwani ndio kampuni kubwa ndani ya Afrika ambayo imeweza kufikia Ulaya katika maswala ya ki uwekezaji, lakini pia alikuwa akimsikia Edna kutokana na kuwa katika orodha ya watu matajiri kutooka Afrika akiwa ndani ya kumi bora
Taarifa ya Roma kuwa mume wa Edna ilionekana kumshangaza na kumgusa bwana huyo , kwani ni jambo ambalo hakuwa ametegemea , ijapokuwa hakuwa akimfahamu Edna vizuri lakini alijua ni mwanamke wa hadhi ya juu sana ndani ya Tanzania.
Ijapokuwa hakuelewa kwanini Edna amekubali kuolewa na mwanaume kama Roma ambaye
alionekana hajatulia lakini kwake aliona ni taarifa nzuri sana kama ingevuja mitandaoni kama Roma alikuwa akichepuka na Najma.
Baada ya kupata wazo mujalabu alitoa tabasamu la kifedhuli na kisha aliinua simu yake na akaingia mtandaoni na kutafuta mawasiliano ya kampuni ya Vexto katika website yao na kisha akaipiga na iliita ndani ya dakika kama mbili hivi bila kupokelewa na alipojaribu mara ya pili ndio iliweza kupokelewa na sauti nyororo ya mwanamke.
“Hello , naongea kutoka makao makuu ya kampuni ya Vexto international , kuna lolote nikusaidie tafadhari”Sauti ilisikika hivyo katika masikio ya naibu waziri Salihi.
“I am Salihi Ibuyawanga , The Vice minister of education , I would like speak to one of chairman , Miss Edna Adebayo, this is urgent matter , please contact her on my behalf”
“Mimi ni Salihi , naibu waziri wa elimu , ningependa kuongea na mwenyekiti wa bodi , miss Edna Adebayo , hili ni jambo la muhimu tafadhari wasiliana nae kwa niaba yangu”
Mtu wa mapokezi hakuwa mjinga , watu wengi walikuwa wakipiga simu wakitaka kuongea na Edna kwa sababu mbalimbali , kuna ambao walikuwa wakipiga huku wakijinadi na kusema wanauza gunduzi za kiteknolojia za hali ya juu, kuna ambao pia walikuwa wakisema wanatokea katika kampuni kubwa za kifedha na wanataka ubia wa kibiashara , kuna wengine ambao wanasema ni ndugu wa vigogo flani serikalini , kuna wengine walijitambulisha ni maraisi wa mataifa ya madogo ya Afrika.
Hivyo kwake haikuleta mantiki kwa naibu waziri wa Elimu kupiga simu mapokezi, hivyo mrembo huyo wa mapokezi aliongeza umakini katika kusikiliza maelezo yake.
“Waziri Salihi , naomba taarifa zako zaidi ili kutambua uhusika wako tafadhari”
“Jambo langu ni kuhusiana na mume wake Roma
Ramoni , gari yake ina namba za usajili kutoka wilaya
ya Bagamoyo 0067BN Lexus Rx 450, unaweza kuthibitisha na nitakupatia dakika moja tu , utawajibika kama kuna jambo baya litatokea kwa kushindwa kuunganisha simu yangu”Aliongea Waziri Salihi kikauzu , alionekana kuchafukwa na roho pengine wivu ndio ambao ulikuwa ukimsukuma kufanya yote hayo.
Upande wa dada wa mapokezi alishangazwa na jambo hilo kwani ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mtu kupiga simu na kuzungumzia kuhusu mume wa boss Edna.
Roma alikuwa maarufu kwa wafanyakazi hao kwani alikuwa mume wa mwanamke mrembo na tajiri Edna hivyo hakuna ambaye hakuwa akifahamu jina lake.
Dakika ileile aliwasiliana na idara ya usalama ya kampuni na kuthibitisha taarifa za Roma na ndani ya sekunde chache tu taarifa ilimrudia ikiwa imethibitishwa na palepale aliwasiliana na Recho.
Ijapokuwa Recho hakuwa teka sekretari wa Edna lakini alikuwa bado akihusika na ku’manage’ simu zote ambazo zinamuhusu Edna.
Baada ya Recho kuongea na Waziri Salihi ambaye taarifa yake ilikuwa ikihusiana na Roma, alijikuta akipatwa na shauku lakini aliamua kujituliza na kutouliza maswali mengi na aliuliza maswali ili kumtambua Salihi kama kweli ni Naibu waziri na baada ya kuthibisha ni yeye kweli palepale alihamisha simu ile kwenda kwa Edna.
Upande wa Edna alikuwa Iringa na muda huo alikuwa akiongea na simu na Daudi mkurugezi wa kampuni ya Vexto Media juu ya maandalizi ya show ambayo imepangwa kufanyikia Iringa , Show ambayo ilikuwa inakwenda kuutanganzia uma kwamba Sophia amerejea katika kiwanda cha muziki, sasa wakati akiwa bize katika kutoa maelekezo ndio namba mpya ilionekana ikipiga kupitia namba yake maalumu ambayo hupokea simu zinazohusiana na maswala ya ofisi.
Aliipotezea namba ile na kuendelea na maongezi yake na Mkurugenzi lakini mtu aliekuwa akipiga alionyesha hali ya kutokata tamaa hata mara baada ya kumaliza mazungumzo yake.
Baada ya simu kupigwa kama mara tano mfululizo bila kukoma palepale alisita kidogo kuipokea lakini baada ya kujishauri kwa dakika kadhaa aliamua kuipokea na kuweka sikioni.
“Is this chairman Edna from Vexto
international?”Sauti ya mwanaume ilisikika na Edna aliitikia kivivu kwa namna ya kuguna.
“Mimi naitwa Salihi , naibu waziri wa elimu , nina jambo nataka kukuelezea kuhusiana na mume wako Roma Ramoni , nimeona ni busara kama utajua kuhusu hili”Aliongea na kumfanya Edna kukunja ndita huku akionyesha mshangao, hakutarajia kama simu hio ilikuwa ikihusiana na Roma.
Alijiuliza imekuwaje Roma akajiingiza kwenye migogoro na Naibu waziri wa Elimu.
“Unaweza kuendelea”
“Tuna mtumishi wa kiserikali afahamikae kwa jina la Najma Waziri ambaye ana mahusiano ya kimapenzi na Mr Roma Ramoni , jambo ambalo linaweza kupelekea uchafuzi wa taswira ya wizara, nadhani kama taarifa hii itasambaa kwenye vyombo vya habari itakuletea pia aibu wewe pamoja na kampuni yako”
Edna mara baada ya kusikia maelezo hayo moyo wake uliuma na alijihisi shoti za umeme za baridi zikisambaa kuanzia kwenye magoti, taarifa hio ni kama ya onyo kwake lakini kwa wakati mwingine ilikuwa kama ya kikandamizi, lakini kwa wakati mmoja alishindwa kuikataa kwani ni jambo ambalo ana uelewa nalo , ilikuwa kidogo tu akae kwenye sakafu.
Baada ya kuvuta pumzi ndefu na kuishusha alijitahidi kujituliza kadri awezavyo lakini alipotaka kuongea ni kama kuna kitu kimemkaba kooni na macho yake yalimuwasha ikionyesha muda wowote machozi yanaweza kumtoka.
Ijapokuwa alikuwa akielewa uhusiano huo lakini kusikia habari hizo kutoka kwa mtu mwingine ilikuwa ikiuma sana kwani ni kama dhihaka kwake.
“Ndugu Mwenyekiti, je unanisikiliza?”Salihi aliuliza mara baada ya kuhisi kimya kirefu kutoka kwa mwenyekiti.
“Nimekusikia…”
Edna alijitahidi na kutoa kauli hio na kisha akakata simu palepale , hakujua sauti yake ingesikika vipi kama tu angeendelea kuongea ndio maana aliikata.
Edna alishindwa hata kujielewa ni kipi anajisikia moyoni mwake na alijiuliza tangu lini akawa hivyo , ni lini kaanza kupoteza utulivu wake ambao ni sifa kubwa ya jina lake.
Alijikuta akikimbilia chooni kwenye sinki na kufungua maji na kisha akatumbukiza sura yake ndani ya maji akijaribu kujituliza na kisha akainua uso wake ulioloana na maji kujiangalia kwenye kioo.
Macho yake mazuri yaliangalia kioo akijaribu kujiangalia lakini kwa wakati huo ni kama hakuwa akijiona vizuri.
Palepale alijikuta kichwa kikianza kumuuma na kama vile kuna kengere zinazosikika katika kichwa chake na alijikuta akifumba macho akisikilizia maumivu lakini wakati huo ilikuwa ni kama vile yupo ndotoni , kwani ile ndoto ambayo ilikuwa ikijirudia rudia kila anapolala usiku ilianza kujitokeza tena katika akili yake.
Dakika hio hio mlango wa chumba chake uliweza kufunguliwa kwa nguvu huku sauti ya Lanlan ikisikika kumuita akiwa ameshikilia
Lambalamba(Icecream) mbili mkononi za kampuni ya Azam.
Edna mara baada ya kusikia sauti ya Lanlan alijikuta akitoka katika mawazo ambayo yalikuwa kama ndoto kwake na kujiweka sawa na kufungua mlango na kutoka.
“Bibi kamnunulia Lanlan icecream nikamuomba amnunulie na mama yake”Aliongea Lanlan huku akimwangalia mama yake ambaye aliekuwa na maji usoni.
Edna muonekano wake ulionyesha kutotaka kupokea Lambalamba hizo lakini Lanlan aliendelea kumnyooshea mama yake kama ishara ya kupokea.
Edna hali yake ya kimawazo palepale ilipungua na aliweza kulazimisha tabasamu akimwangalia Lanlan na uso wake wa kitoto uliojaa ukarimu ndani yake , alijikuta akichuchumaa na kisha kushika nywele zake ndefu.
“Lanlan nitang’ata hii ya kwako kidogo na unaweza kula zote , ina sukari na meno ya mama yatauma”Aliongea Edna na kushika ile ya Lanlan aliokuwa akilamba na kuing’ata kipande.
Lanlan mara baada ha kuridhika na maneno ya mama yake palepale alikimbilia nje kwenda kutafuta mtu mwingine wa kushirikiana nae kula hizo lambalamba , alikuwa tayari ashazoea mazingira na alichukulia hapo ni kama nyumbani kwako na alikuwa ashazoeana na kila mu.
Edna alijikuta akifumba macho yake mara baada ya
Lanlan kuondoka na palepale michirizi ya machozi iliweza kuonekana katika mashavu yake lakini hakuna ambaye alikuwa akijua kama alikuwa akilia kutokana na ubaridi wa lambalamba aliopewa na Lanlan au ni ubaridi uliopo kwenye moyo wake.
Wakati mrembo huyo akionekana katika hisia za uchungu palepale simu yake iliweza kuiita na aliichukua na mara baada ya kuangalia na kuona anaepiga ni Wendy alipokea na kuweka sikioni.
“Boss tayari maandalizi ya show yashakamilika na Meneja Ummy atakuwa Airport Iringa na Sophia usiku wa leo na baada ya hapo ratiba ya tukio lenyewe itaanza kujadiliwa”
“Ni muda gani ambao Sophia atafika Airport?”
“Itakuwa ni saa mbili kamili usiku , tayari tushatuma mtu wa kumpokea kumpeleka hotelini”
“Haina haja , nitaenda kumpokea mdogo wangu mimi mwenyewe , sijaonana nae kwa muda mrefu , hivyo uliowaagiza wanaweza kufanya kazi nyingine”Aliongea Edna.

SEHEMU YA 630.
Baada ya Edna kufanikiwa kumshawishi Sophia kurudi kuendelea na maswala ya usanii alipanga show yake ya kwanza aifanyie jijini Iringa , ijapokuwa ni show iliopangwa kwa haraka kufanyika lakini kutokana na hela pamoja na koneksheni ya vyombo
vingi vya habari jijini Dar es salaam iliweza kutangazwa kwa haraka sana na ikawa habari kubwa na show hio ikawa inategemewa na kila mmoja.
Sophia alikuwa ashaanza safari ya kurejea Tanzania tokea siku ya jana , hivyo moja kwa moja alipaswa kutua Mwanza akitokea Dubai na kuanza safari ya moja kwa moja kwenda Iringa kwa ndege kwani Show ilipaswa kufanyika siku iliofuatia hivyo maandalizi ya mapema kabla ya show hio yalipaswa kufanyika wakati Sophia mwenyewe akiwepo.
Wendy mara baada ya Edna kusema yeye ndio ataenda kumpokea mdogo wake , basi hakutaka kupinga na aliishia kukata simu na kutoa maagizo kwa wale ambao wameagizwa kwenda kumpokea Sophia kutoenda.
Edna alijiambia asingemwambia chochote Roma kuhusu Naibu waziri Salihi alichoongea , alijua kama akisema basi Roma ni lazima angelipiza kisasi pengine cha kumuua kabisa.
Edna hakuona maneno ya Waziri yalikuwa na uongo
, ni kweli kabisa Roma alikuwa akijihusisha kimapenzi na Najma ,hivyo anawezaje kuwa na kinyongo kwa kauli yake, hivyo aliamua kupotezea licha ya kwamba bwana huyo alionekana kama vile alikuwa akimtishia na kumfikishia ujumbe kwamba amkanye mume wake kuachana na Najma la sivyo angevujisha taarifa.
Edna aliamua kujituliza na alijiambia pengine Roma akirudi anapaswa kuongea nae kuhusu hilo na hakupaswa kumfanya mama mkwe wake kujua hilo , pengine ingeonekana labda anawatumia ili kumpa presha Roma.
Edna alikuwa ukingoni, maswala ya kifamilia kwake yalikuwa ni magumu sana kuliko hata maswala ya kibiashara na alijiona muda wowote anaweza kupata uchizi.
Ijapokuwa hakuwa akijivunia na maisha yake ya miaka michache iliopita , maisha ya kutokuwa katika mahusiano lakini kwa wakati huo alikuwa akipitia furaha na huzuni kwa wakati mmoja, alikuwa na furaha alikuwa na familia , lakini alikuwa na huzuni kutokana na michepuko ya mume wake.
Edna mara baada ya kujikalisha chini na kuwaza kwa muda aliishia kung’ata meno yake kwa hasira huku akijituliza na baada ya hapo alichukua simu yake na kuanza kupiga kudili na maswala mengine.
Saa moja kamili Edna alikuwa ashamaliza kula chakula cha usiku na aliweza kuaga anaelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea Sophia.
Familia hio haikumzuia kwani walijua Edna na Sophia ukaribu wao ni wa kindugu zaidi.
Lanlan mara baada ya kusikia habari za mama yake kwenda kumpokea Sophia alianza na yeyekulilia kuongozana na mama yake kumpokea Aunt Sophia na ilimfanya Edna kukosa chaguo lingine na kuondoka nae.
******
Ili kurahisisha ukuaji wa maendeleo ndani ya Tanzania Raisi Senga aliweza kuingia madarakani na sera yake ya kujenga miundo mbinu ili kurahisisha usafiri kati ya mikoa na mikoa.
Miongoni mwa mikoa ambayo ilipewa kipaumbele katika miundo mbinu ni pamoja na Iringa ambayo ilipendelewa kwa kujengwa uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa.
Mwanzoni mwa ujenzi huo Raisi Senga alipingwa na wengi kwa kusema anapendelea ukanda wa anakotokea kwani kulikuwa na uwanja wa Songwe tayari ambao upo karibu na Iringa lakini mara baada ya kiwanja hicho kufunguliwa yale maoni hasi yalizima kwani kiliweza kuwa kiwanja maarufu ndani ya muda mfupi na kiliweza kupokea wasafiri wengi kwa siku na kuongoza kwa kuwa kiwanja chenye ubize mkubwa namba tatu nchini.
Ni kiwanja kikubwa ambacho kilikuwa na uwezo wa kuruhusu ndege mbili za abiri za ukubwa wa wastani kutua kwa wakati mmoja huku zile kubwa zikipeana nafasi ya kutua baada ya nyingine kwa zaidi ya dakika kumi tu.
Hviyo ni rahisi kusema kilikuwa na uwezo wa kuhudumia ndege tatu mpaka nne kwa wakati mmoja.
Ijapokuwa hakikuwa kikihudumia ndege za usafiri wa moja kwa moja kutoka mataifa makubwa lakini wasafiri wa kutoka nchi za Afrika jirani na Tanzania zilikuwa zikitua mara kwa mara katika kiwanja hicho.
Kulikuwa na Terminal mbili ya kwanza ilikuwa karibu kabisa na maegesho ya magari ambayo ilihudumia wasafiri wa kimataifa na nyingine ya kuzunguka upande wa pili yake ilikuwa ni terminal ya kuhudumia wasafiri wa ndani.
Hivyo ukiingia ndani ya kiwanja hicho unaanza kukutana na Terminal ya kimataifa ndio unaelekea Terminal ya wasafriri wa ndani.
Edna mara baada ya kufika kiwanjani hapo aliingia mpaka ndani ya jengo la kusubiria wageni wa ndani wanaowasili akiwa amevalia miwani yake ili kuzuia watu wengi wasimfahamu.
Hata hivyo licha ya eneo hilo kuwa na watu wengi wanaotoka na kuingia haikuwa kama uwanja wa ndege wa Dar es salaam.
Baada ya kusubiria ndani ya dakika kumi hatimae makundi ya wasafiri yaliweza kutoka kwa awamu , huku wengi wao wakiwa ni wazungu na watu wa kiasia , waafrika walikuwa wachache sana katika makundi hayo.
Kati ya kundi hilo la waliokuwa wakiwasili alikuwepo Sophia ambaye alikuwa amejichanganya katikati ya watu akiwa amevalia miwani ya jua pamoja na barakoa usoni na sweta la kofia, ilikuwa ngumu kumjua lakini Edna aliweza kumuona kwa haraka na hata kwa Sophia aliweza kumtambua Edna kwa haraka, pengine ni kutokana na mafunzo yake ya kijini aliokuwa nayo.
“Aunt…!!”
Lanlan aliekuwa amesimama alitoka kwenye mikono ya mama yake na kukimbia upande wake.
Sophia hakuonyesha kushangazwa na uwepo wa Lanlan na aliishia kuongeza spidi kumsogelea akitoka katika kundi la watu na alishukuru mara baada ya kuona hakuna mtu ambaye alikuwa akiwaangalia wala hakukua na mapaparazi.
Ijapokuwa alikuwa na aibu kutokana na hatia yake ya kuwa na mahusiano na Roma lakini alikuwa na furaha kumuona Edna kwa mara nyingine.
“Sis , wewe ndio umekuja , ungetuma mtu kuja kunipokea haikuwa na haja ya kuja mwenyewe kwani naenda hotelini moja kwa moja”
“Haina shida , sijakuona muda mrefu hivyo niliona nije mwenyewe , isitoshe ulikuwa katika hali ya hatari ndio maana , Lanlan amekumis pia”Aliongea Edna akitoa tabasamu.
Sophia alijua Edna alichokua akimaanisha mara baada ya kusema mazingira ya hatari , alijua alikuwa akizungumzia juu ya ulimwengu wa majini pepo.
Sophia hisia zake zidi ya Lanlan sasa zilikuwa za tofauti kwani alikuwa akifahamu ni mtoto wa Roma.
Kutokana na kuona Edna hakuwa na uelewa wowote alijiuliza sijui ni lini Roma angemuweka wazi Edna juu ya Lanlan kuwa mtoto wake na Seventeen.
Kwa wakati huo Sophia hakutaka kufikiria sana na alimbeba Lanlan kwenye mikono yake huku akimpiga busu la shavuni.
“Lanlan unakula nini, mbona umekuwa mzito hivi jamani?”Aliuliza Sophia mara baada ya kumpakata , lakini Lanlan alitingisha kichwa chake kukataa kama hajaongezeka uzito.
“Hapana , Lanlan ni mtoto mzuri, mama anakataa nikila mpaka nikishiba”
Kwa kauli yake pengine watu wangesema Edna anamnyanyasa Lanlan lakini kwa Sophia aliekuwa akijua ulaji wa Lanlan alijua maana ya maneno hayo.
Sophia hakuwa peke yake , alikuwa ametangulizana na meneja wake Ummy na alishangazwa na maneno ya Lanlan na kujiambia Edna ni mtu makini kujaribu kuzingatia ulaji wa chakula cha binti yake ili asinenepe vibaya.
Edna hakutaka sana watu wa nje ya familia yake kusikiliza maongezi yao na alimwambia Ummy kwa kauli kavu achukue Taksi kumpeleka moja kwa moja hotelini yeye ataondoka na Sophia.
“Boss , nashukuru sana umekuja kutupokea lakini sidhani kama ni sawa kukusumbua”
“Nimesema nitaondoka nae mwenyewe ,, kuna haja ya mimi kurudia rudia?”Aliongea kikauzu kwa kuona meneja huyo anashindwa kujiongeza.
Meneja Ummy alijikuta akiogopa macho ya kikauzu ya Edna na aliishia kutingisha kichwa kwa kuitikia na alichukua begi lake akiondoka, hakutaka kusubiri tena kwani aliogopa kupoteza kazi yake.
Sophia alimuonea huruma Meneja wake lakini kwa wakati mmoja akionea wivu namna Edna alivyoongea kibabe kwani ni kitu ambacho yeye hakuwa akiweza , ukali wa Edna uliwafanya wafanyakazi wengi kumtii kila anapotoa agizo bila ya kuuliza mara mbili mbili.
“Tuondoke nitakupeleka moja kwa moja hotelini na tutakuwa na kikao cha muda mfupi na nitakuacha , najua kwanzia kesho utakuwa bize ndio maana nimeandaa kikao usiku huu huu”Aliongea Edna huku wakitembea kurudi upande wa magari yanakoegeshwa.
“Sis , unafikiri ninaweza kufanya vizuri kama mwanzo , naona kama watu wanachuki na mim?”Aliongea Sophia akiwa na wasiwasi kutokana na skendo yake ya mwanzo.
“Utafanya vizuri ndio , ilimradi tu nyimbo zako na uigizaji wako utakuwa mzuri basi naamini utarudi katika ubora wako na kupanda juu zaidi , kupitia hela itakuwa rahisi pia kusafisha jina lako na kila mtu atakukubali tu , wasanii mnapaswa kuushawishi umma na kazi zenu na si vinginevyo , nina imani na wewe..”
“Kumbuka pia nimetumia zaidi ya mabilioni ya hela kuanzisha kampuni yote ya burudani na habari , unataka kweli kampuni yangu kufirisika , ninaweza
kuwa tajiri lakini pia sipendi hasara , ninataka kuendelea kukutegemea kama mgongo wa kamapuni upande wa burudani”
Sophia alijua Edna alikuwa sahihi na maneno yake ni kwa ajili ya kumpa motisha lakini hakuacha kujisikia vihaya , alitamani ni kheri Edna kumlaani ili mradi tu ajisikie vizuri .
Lakini licha ya yote Sophia alipanga kufanya kazi vizuri ili tu kutokumuangusha Edna ambaye ameweka tumaini kwake.
Wakati wakielekea upande wa maegesho ya magari waliweza kupita nje ya mlango wa wasafiri wa nje ya nchi wanaowasili na Edna alijikuta akisimama baada ya kuona kitu na Sophia hivyo hivyo alisimama na kuangalia upande ambao Edna alikuwa akiangalia.
Alikuwa ni Roma ambaye alionekana mbele yao akitembea kuingia jengo hilo la wageni wanaowasili, ijapokuwa hakuwa na muonekano wa kuvutia kama wengine kutokana na staili yake ya uvaaji lakini Edna na Sophia waliweza kumuona kwa haraka kutokana na kwamba alikuwa mtu muhimu kwenye maisha yao.
“Isn’t that daddy?”AliulizaLanlan mara baada ya kumuona Roma pia.
Edna na Sophia waliangaliana huku wakiwa kama na mshangao kwenye macho yao .
“Mbona inashangaza, ni yeye ndio lakini kwanini ameshindwa kugundua uwepo wetu?’Aliongea Edna akionyesha kuchanganyikiwa, alijua kutokana na Edna na Sophia kuwa na mafunzo ya kijini na Roma kuwa na uwezo wa juu wa kimafunzo basi lazima angehisia uwepo wao , hususani kwa Sophia ambaye alikuwa katika levo ya Nafsi.
“Inaonekana kuna mtu kaja kumpokea”Aliongea Sophia mara baada ya kumuona Roma kazama
ndani ya jengo la wasafiri wa kimataifa wanaowasili.
Edna licha ya kwamba alikuwa na hasira na Roma lakini mara baada ya kumuona akielekea jengo la wasafiri wa kimataifa wanao wasili alijikuta akijawa na shauku ya kutaka kujua Roma anampokea nani na kwanini ashindwe kuwaoana.
Roma hakuwa na habari kama kuna watu waliokuwa wakimfatilia nyuma yake na yote hio ni kutokana na kwamba hakuwa akitumia kabisa uwezo wake wa kijini kutokana na hatari ya kupatwa na uchizi kwasababu ya Cauldron.
Mpango wa Roma ni kumpokea Clark na kumpeleka Hotelini kabla ya kwenda nyumbani na muda ambao alifika hapo ndio alikuwa akitokea Dar.
Ni ndani ya dakika tano tu kupita hatimawe kundi la wazungu ambao walionekana kuwa ni watalii liliweza kuonekana likitoka na haikumchukua muda mrefu kwani Roma aliweza kumuona Clark aliekuwa nyuma peke yake na alimpungia mkono.
“Clark!!!”
Clark aliweza kumuona pia Roma mara baada ya kusikia sauti yake , hakuwa amebeba begi kubwa kama wasafiri wengine.
“Roma..!!”
Aliita Clark huku akiweka tabasamu usoni na kufanya watu kuzidi kumwangalia kwa macho ya matamanio kutokana na urembo wake huku wakiangalia ni mtu gani ambaye amekuja kumpokea huyo mrenbo , lakini dakika chache walijikuta wote wakishikwa na hasira na kutoa matusi mara baada ya kumuona Clark akimkimbilia mwanaume ambaye alikuwa ni wa kawaida mbele ya macho yao tena mweusi.
Clark hakuwa na aibu pengine ni kutokana na uzungu wake kwani mara baada ya kumfikia Roma palepale alijirusha kwenye mikono yake huku akimpa mabusu moto moto.
Roma alishangazwa na mabusu ya kushitukiza ya Clark lakini hakuweza kukwepa kwani Clark mwenyewe hakuwa na wasiwasi na macho ya watu yaliokuwa yakiwaangalia.
Roma alimshika kiuno mrembo Clark na kisha akampiga kibao cha makalioni kwa namna ya uchokozi na muda huo huo walijikuta wakipeana french kiss.
End of season 21

NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

SEASON 22

SEHEMU YA 631.
Pengine ingekuwa tukio la kuvutia kwa wenza kubusiana ndani ya airport kama tu Edna , Sophia na Lanlan wasingekuwa wakiwafahamu watu hao.
Lakini kwa bahati mbaya , wenza hao walikuwa wakifanya mambo yao pasipo ya kujua kama kuna watu muhimu wanawaangalia.
Sophia na Edna sasa waliweza kujua uwepo wa Roma ndani ya eneo hilo ni kwa ajili ya kumpokea Clark.
Kama Clark angekuwa makini basi angeweza kumuona Edna na Sophia lakini kutokana na umakini wake kuelekezea kwa Roma basi alishindwa kuwaona lakini kwa wakati mmoja kama usingemjua Clark ungesema anafanya makusudi kwani alienda mbali na kupitisha mikono na kuiloki nyuma ya shingo ya Roma akibembea huku akifurahia busu nyevu.
Ijapokuwa kwa tamaduni za kiafrika kupeana denda hadharani ni jambo la mshangao kidogo lakini katika mazingira kama hayo ambayo wageni wengi walikuwa ni wazungu na wasomi basi halikuwa jambo kubwa sana zaidi ya kuonekana kivutio hususani kwa mrembo kama huyo kubusiana na mwanaume wa kawaida kama Roma, wengi waliwaelewa kwa kuona kwamba siku zote hisia hazivumiliki hususani pale unapommisi umpendae.
Edna palepale alimrudhisha Lanlan nyuma yake ili tu asione kile baba yake anachokifanya.
Uso wake mwanzoni ulikuwa umepauka lakini ulianza kujikunja kwa hasira kiasi cha kumfanya Sophia kuanza kupatwa na hofu.
Wakati huo Sophia alianza kumchukia Roma na kujiuliza kwanini ameshindwa kujua uwepo wao ndani ya hilo eneo , au anafanya yote hayo makusdi kumkomoa Edna na yeye?.
Kwa kile alichokuwa akikikumbika ni kwamba Roma hakupaswa kuwa na mahusiano na Clark hivyo alijiuliza kam yameanza yalianza lini.
Sophia alikuwa na wivu pia wakati huo lakini ulifunikwa na wasiwasi wake aliokuwa nao juu ya Edna , ijapokuwa Sophia hakuwa na ukaribu mkubwa na Clark lakini alijua mrembo huyo alikuwa na sehemu yake pekee katika moyo wa Roma.
Clark alikuwa ni rafiki wa muda mrefu wa Roma kwa zaidi ya muongo mmoja na uzuri wake pamoja na umuhimu katika maisha ya Roma haukupishana sana na Edna.
Yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba katika uzuri Edna na Clark wameachana kidogo sana , ukija kwenye mafanikio pia Clark alikuwa amepishana na Edna kidogo hivyo ni sawa na kusema kama Edna ungemchagulia mshindani basi Clark ndio mshindani wake mkubwa , isitoshe pia ni Princess wa Wales cheo ambacho ni cha ziada lakini kinachompa ‘status’ ya hali ya juu.
Mwanamke wa aina hio Edna alimuogopesha mno kuliko hata wale wanawake wengine wa kule Dar es salaam , kwa mfano Neema Luwazo licha ya mafanikio makubwa lakini alikuwa sio mzuri kumshinda Edna na pia alikuwa akikaribia kuuaga ujana.
Wanasema baadhi ya watu wamezaliwa katika kimo cha juu ambacho watu wa kawaida hawawezi kufikia hata wapambane vipi basi ndio kwa Clark.
Kama vile ndio sasa ameridhika kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea palepale alimwambia Sophia waondoke haraka.
Upande wa Edna ni kama alikuwa ndotoni na huku akitamani baada ya kufumbua macho ajue kile alichoona hakina ukweli wowote .
Upepo wa ubaridi wa hali ya juu ulitawanyisha machozi yake kiasi cha kumfanya akili yake kurudi katika uhalisia.
Ilikuwa ni ukatili mkubwa kwa yeye kama mke kuangalia tukio hilo laivu na ilizidi kuuma kwa kuona kwamba haikuwa ndoto.
“Mommy ..”Aliita Lanlan mara baada ya kuhisi kuna kitu hakipo sawa na Edna alimwangalia.
“Who is that aunt daddy ‘s kissing? Is she onother aunty..?”Aliuliza Lanlan akimaanisha kwamba yule shangazi ni ambaye baba yake anamkiss ni nani , je ni shangazi mwingine.
Lanlan alikuwa akiwatia wanawake wa Roma mashanganzi zake , hivyo mara baada ya kuona tukio la baba yake kufanya vile alijua lazima atakuwa ni shangazi mwingine kama Rose , Nasra na wengineo.
“That is not your dad..”(Yule sio baba yako)
“But he …”(Lakini ni..)
“I said he isn’t, Can’t you listen to me”Aliongea Edna akipandisha sauti akimkatisha Lanlan kwa kumfokea.
Lanlan aliishia kunyamaza lakini bado alionekana kushangazwa na maneno ya mama yake kwani asingeweza kutokumfahamu baba yake.
Baada ya kuingia kwenye gari Edna aliendesha kuelekea hoteli ya Iringa Highland bila ya kuongea neno lolote.
Sophia alikuwa na wasiwasi sana akiwa kwenye gari , alijiambia Edna alikua amemuona Roma na Clark na yupo kwenye hali hio vipi akigundua kuhusu yeye.
Alijiambia atamwambia Roma wawe makini kuyafanya mahusiano yao kuwa siri kwa kugopa kumuumiza Edna.
“Sis , pengine Princes Clark alikuwa na shauku kubwa ya kumuona Roma ndio maana, hata hivyo hawezi kukaa kwa muda mrefu hapa
Tanzania”Aliongea Sophia akijairbu kumtuliza
“Huna haja ya kumtetea , nimeona vya kutosha na namjua alivyo , mimi sio kipofu”Aliongea Edna kwa kikauzu.
Sophia aliishia kujikunyata huku akijua kabisa hana kingine cha kuongea kutuliza hali ya Edna.
“Sikia Sophia huna haja ya kuwa na wasiwasi na mimi , cha msingi zingatia kazi yako na ukifanya vizuri itanifurahisha”Aliongea Edna mara baada ya kuona hali ya wasiwasi isiokuwa ya kawaida kwenye uso wa Sophia.
Ukweli ni kwamba hakuwa na wasiwasi juu ya tukio ambalo limetokea , kilichokuwa kikimpa wasiwasi ni kwamba na yeye alikuwa kwenye mahusiano ya kutatanisha pia.
Dakika chache tu waliweza kufika na kuingia ndani ya hoteli na waliweza kumkuta Ummy akiwasubiria na alimpokea Sophia begi lake na kutangulia mbele.
Upande mwingine Roma mara baada ya kusabahiana na Clark alimchukua na kuelekea moja kwa moja mpaka Kigombola Medical Research University, moja wapo ya chuo kilichozinduliwa miaka mitatu iliopita ndani ya jiji la Iringa chini ya uongozi wa Raisi Senga lakini kikapewa jina la raisi msataafu Kigombola kutokana na yeye ndio mwasisi wa ujenzi wake, kilikuwa chuo kikubwa mno ambacho kimejengwa kwa ajili ya mafunzo ya kitafiti katika maswala ya magonjwa yasioambukiza kama vile Saratani , moyo na mengineyo.
Ijapokuwa Clark alikuwa na furaha kumuona Roma lakini bado alijali sana kuhusu afya yake .
Ndani ya gari Roma aliweza kuelezea kuhusu hali yake na maswala ya Chaos Cauldron na Clark aliweza kuelewa vizuri kutokana na kuanza kujifunza mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
Hakuwa na mpango wa kumponyesha Roma bado hivyo alichokuwa akidhamiria ni kumfanyia vipimo vya awali na ndio aanze kufikiria namna ya kumsaidia.
Upande wa Roma matumaini yake yalikuwa chini kutokana na kwamba alijua mafanikio ya teknolojia kuweza kufubaisha nguvu ya Roho ya mnyama huyo ilikuwa ni ngumu kufanikiwa, lakini alitaka kuona kama Clark anaweza kutibu dalili za uvimbe(Benign) kichawni basi angeweza kuwa na uwezo wa kuitawala akili yake kwani uvimbe huo ndio kichocheo cha yeye kupatwa na uchizi.
Baada ya kufika nje ya geti kuingia chuoni hicho walielekezwa na mfanyakazi na kwenda kusimamisha gari chini ya jengo refu kwenda juu ambalo chini yake lilikuwa na kibao cha utawala.
Kilikuwa chuo lakini pia kulikuwa na hospitali ndani yake hivyo eneo lilikuwa limechangamka.
“Clark unapanga kukaa hapa?”Aliuliza Roma.
“Ndio , mkuu wa chuo amenikubalia kutumia vifaa vya maabara nipendavyo , nimezoea kukaa ndani ya maabara kuliko hotelini”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa kidogo lakini pia hakuacha kuangalia mandhari ya kuvutia ya chuo hicho na kujiambia Tanzania imepiga hatua kwa kuwa na taasisi hio.
“Na yeye ni mwanafunzi wako?”
“Sio mwanafunzi wangu , ana miaka tisini tayari niliweza kumfahamu kupitia Profesa Shelukindo na alinikubalia moja kwa moja mara baada ya kumwambia nitampatia kanuni ya matibabu ya saratani ya ini bure , nina kanuni nyingi za kimatibabu hivyo sikiuona shida”
“Kwahio kwa kurahisisha ni kwamba kukualika kwangu kumesaidia taifa katika maswala ya kitafiti?”Aliongea Roma akijaribu kumtania.
“Ninaweza kufanya chochote kwa ajili yako kwasabab nishakuwa wako tayari”Aliongea na kumfanya Roma aone siku hizi Clark amezidi kuwa muwazi katika kuongea kimitego.
Baada ya kuingia ndani na kutembea umbali mfupi kukaribia mlango wa kuingia waliweza kupokelewa na daktari mwenye muonekano wa kizee ,Alikuwa ni Profesa maarufu Tanzania aliefahamika kwa jina la
Justice Damiani Mandu , wanafunzi wengi hupendeleea kumwita Profesa Mandu au Dokta Mandu.
Hakuwa peke yake alikuwa na madaktari wengine pamoja na baadhi ya watu wa utawala na mara baada ya kusalimiana nao Clark aliwapa ruhusa wengine kuondoka na kisha aliongozana na Profesa Mandu na walihamia kwenye jengo lingine lililojengwa kwa vioo upande mmoja na ndani ya dakika chache walifika kwenye floor ya nne na Profesa Mandu alitoa maelezo kwa ufupi juu ya eneo hilo la maabara na kisha Profesa Clark mara baada ya kuridhika alitoa karatasi iliokunjwa na kumpatia na kisha wakaagana huku Profesa huyo akionyesha furaha ya waziwazi huku akijiambia anakwenda kustaafu kwa heshima.
Roma aliishia kupumua kwa ahueni na kukumbuka msemo wa kingereza unaokwenda kwa jina la ‘knowledge is power’.
Clark hakutaka kufikiria sana kuhusu vitu vilivyokuwa hapo ndani na palepale aliingia kazini bila ya kuchelewa licha ya kwamba ilikuwa ni usiku sana.
Alionekana kuwa siriasi wakati akianza kukadiria vifaa kwa ajili ya kuanza vipimo.
Roma alisubiria kwa uvumilivu kutokana na kwamba aisngeweza kusaidia chochote na mara baada ya lisaa limoja kupita , Clark alianza vipimo pamoja na kufanya uchambuzi.
Mpaka anakuja kumaliza ilikuwa ishatimu saa tano na inaelekea saa sita za usiku na Clark alimharakisha Roma kuondoka kwenda nyumbani kwasababu alihitaji muda wa kufanyia kazi vipimo vyake.
Roma alimuaga baada ya kumkiss kwenye paji la uso akionyesha kuwa ni mwenye shukrani kubwa kwa kile anachomfanyia na kisha akaondoka .
Wakati Roma anakaribia kufika nyumbani gari la Edna na lenyewe lilikuwa nyuma yake na baada ya kuingia ndani na kusimamisha Edna alishuka na kisha akafungua mlango wa nyuma na kumtoa Lanlan ambaye alionekana kuwa usingizini.
Roma kwa haraka haraka alijua Edna alikuwa ametoka kufanyia kazi maswala ya Sophia kurudi katika usanii lakini alishangaa kuona alikuwa ameenda na Lanlan.
Roma alitoka na yeye haraka haraka kwenye gari yake na kumsogelea Edna huku akionekana kuna kitu alikutwa kiutaka kumwambia.
“Babe wife.. je tunaweza ..”Kabla hata hajamaliza sentesi yake Edna alimpita kama vile hamjui.
Haikuwa mara ya kwanza Edna kufanyiwa hivyo lakini siku zote alikuwa akijua sababu ni nini lakini wakati huo hakujua ni kipi kinaendelea maana walikuwa vizuri tu juzi yake.
“Wife nini tatizo , nimefanya kosa gani awamu hii?”Aliuliza Roma mara baada ya kukimbilia mbele akijaribu kumzuia Edna.
Walinzi waliokuwa zamu waliweza kuhisi kuna kinachoendelea lakini walijifanya hawaoni chochote na kujiweka bize na wanachofanya.
Edna hakujisumbua hata kumwangalia usoni zaidi ya kumpita kwa mara nyingine.
Roma aliishia kukuna kichwa chake akionekana kuchanganyikiwa huku akimfuata nyuma nyuma, baada ya kuona namna ambavyo Edna alikuwa na ukauzu hakujua namna ya kuanza nae mazngumzo. “Edna usiwe hivyo , niambie chochote nitabadilika kama nimefanya kosa , kama huna furaha juu ya jambo niambie na nitajirahidi kukufurahisha , nilikuwa nikiwaza kuwatoa out wewe na Lanlan siku ya kesho”Roma alijitahidi kumbembeleza lakini Edna hakuonyesha nia yoyote ya kutaka kumjibu , baada ya kuingia ndani ya chumba chake palepale alifunga mlango na Roma aliishia kusikia ufunguo ukizungushwa kwa ndani na kumfanya Roma kuishia kushika ukuta huku akikosa cha kufanya.
Ilikuwa tayari ni usiku sana hivyo wanafamilia wote walikuwa wamekwisha kulala muda mrefu na hakuna ambaye alikuwa akijua kinachoendelea.
Roma alijikuta akipigwa na bumbuwazi , huku akijiuliza kwanini ana mikosi , alikuwa tayari amechanganyikiwa kutokana na uwezo wake wa kijini na sasa na mke wake alikuwa akimpa kisogo, lakini licha ya hivyo hakuwa akijua kosa lake ni nini.
Dakika hio hio kabla ya kujua agonge mlango Edna afungue au achukue uamuzi gani simu yake ilitoa ‘notification’ ya ujumbe wa meseji na alivyoangalia ni Sophia aliemtumia.
“Roma , upo huru kuongea sasa hivi?”Roma aliishia kutabasamu kutokana na umakini wa Sophia na palepale alitoka mbele ya mlango wa chumbani kwake na kutafuta eneo tulivu na kumpigia,
“Upo Iringa tayari?”Aliuliza Roma na Sophia aliitikia kwa kuguna.
“Ndio unajiandaa kwa kurudi kwenye mziki ndio maana mpaka sasa hivi hujalala tu?”Aliuliza Roma lakini Sophia hakujibu.
“Roma Sister asharudi tayari?”Aliuliza na Roma macho yake yalichanua na kuamini pengine Sophia alikuwa anajua nini kimetokea.
“Kidogo tu nisahau kukuuliza , nini kimempata , alikuwa na ukauzu kiasi cha kuogopesha , nimefanya kosa gani awamu hii?”
“Ndio nilichokuwa nataka tuongee , alikuja kunipokea Airport na tuliweza kukuona wewe na Clark ..”Aliongea Sophia kwa kusita sita na Roma macho yalimtoka.
“Mliniona mimi na Clark .. unamaanisha anajua mimi na Clark?”Aliuliza Roma huku akikunja ngumi kwa hasira.
“Ndio , alionekana ametulia lakini inaonyesha amekasirika mno , Roma Seriously, kwanini umeshindwa kujua kama tupo nyuma yako?”Aliuliza Sophia huku akionyesha na yeye kukasirika.
Roma alijiambia mwenyewe hata mimi sikutaka mnione , ni kwamba sikuwa na uwezo wa kutumia uwezo wangu, lakini licha ya hivyo hakuwa na ujasiri wa kumuweka wazi Sophia juu ya hilo.
“Sijui nilikuwa nikiwaza nini kiasi cha kushindwa kuwaona ,,, asante lakini kwa kuniambia la sivyo ningepata uchizi wa kutafuta makosa yangu”Aliongea na kumfanya Sophia kupumua kwa nguvu.
“Mimi kwa upande wetu nadhani ni vizuri tukiendelea kufanya siri naogopa anaweza akashindwa kuvumilia , isitoshe yupo Lanlan pia , unapaswa kusubiri kwa muda pia kabla hujamwambia chochote kuhusu Lanlan”
Roma alikuwa na mawazo sawa na ya Sophia lakini bado aliona ni swala la muda tu kwani hisia mara nyingi hazijifichi kwani itafikia mahali Sophia asingeweza kujificha mbele ya Edna.
Roma alijaribu kufikiri njia ya kuweza kumbembeleza Edna lakini hata hivyo aliona ni kheri kusubiri apate nafasi kwani Edna hakutaka hata kumwangalia usoni.
Roma baada ya kuona hana pakulala alitafuta chumba chochote cha wageni ambacho kilikuwa wazi na kisha akajitupia kitandani huku akikosa hata hamu ya kuoga na alijitahidi kuutafuta usingizi lakini alishindwa kabisa.
Ni masaa machache kabla ya kupambazuka , Edna alionekana akitingishika akiwa usingizini huku akiongea.
“Hapana,,, sio mimi,, siwezi ,,, Hubby …ah!!!”
Edna palepale alishituka kwa nguvu na kukaa kitandani huku jasho likimtoka akiwa katika mavazi ya kulalia.
Baada ya kuona yupo ndani ya chumba chake alijikuta akipatwa na ahueni .
Lanlan aliekuwa amelala pembeni yake aliishia kutingishika kidogo huku akiwa kama amesikia Edna akiongea akiwa ndotoni.
Blanketi lilikuwa limefunika tumbo tu huku miguu yote ikiwa wazi , kwasababu ilikuwa ngumu kwake kuugua Edna hakumlazimisha kumfunika.
Lanlan alionekana na yeye kuongea kwa dakika chache maneno yasioelewweka na kisha aliendelea kuuchapa usingizi
Edna aliishia kumshika shika Lanlan nywele zake za Ki’half-cast huku akionekana kuogopa kulala tena kwa kuogopa kuota tena.
Edna alikuwa ameshapoteza hesabu ya mara ngapi aliweza kuota ndoto hio ya aina moja , kwani alikuwa akiota mchana na usiku , mwanzoni alijua pengine alikuwa akiota kwasababu ya kuwa na wasiwasi na Roma mara baada ya kupotea , lakini hata baada ya kurudi alikuwa akiota kitu cha aina moja.
Edna alivuta pumzi nyingi kabla hajaangalia saa na kuona ilikuwa ni saa kumi na moja alfajiri , muda ambao kwa Iringa ilikuwa mapema sana lakini alijiambia muda huo anaweza kuamka na kuendelea na kazi.

SEHEMU YA 632.
Asubuhi wanafamilia wote walikusanyika eneo la nje katika kiambaza kwani kulikuwa na padri aliefika kwa ajili ya kuongoza sala maalumu.
“Edna huyu mtukutu yupo wapi?”Aliuliza Afande Kweka alikuwa akijua kurudi kwa Roma kwani jana yake alimpigia simu.
Edna mara baada ya kuulizwa swali hilo alishindwa hata ajibu nini kwani hakujua hata alilala wapi na asingeweza pia kusema jana alimfukuza kwenye chumba chake.
“Babu si..”Edna alikosa jibu na Blandina palepale aliona kuna tatizo na aliamua kuingilia.
“Ngoja nikamwite”Aliongea Blandina huku akijiandaa kutoka lakini alisimama mara baada ya kusikia sauti kutoka upande wa kulia.
“Nipo hapa”Aliongea Roma huku akiwa na mavazi ya jana lakini lakini utofauti ni kwamba alikuwa amevaa Apron ya upishi akionekana alikuwa jikoni.
“Roma kwanini..”
“Hahaha… niliamka mapema niliamua leo kuhusika na maandalizi ya kifungua kinywa”Aliongea Roma na kumfanya Afande Kweka misuli yake ya uso kukaza kidogo.
“Huyu ni father Selestin kutoka parokiani na leo amefika hapa kwa ajili ya maombezi maalumu na sisi wanafamilia wote”Aliongea Afande Kweka.
“Ah…unamaannisha yupo kwa ajili ya kutuombea kwa Bodhidhativa?”
“Acha upuuzi na maswala yako ya Bozitavazi ni kwa ajili ya kutuombea kwa Mungu”Aliongea Afande Kweka , hakumlaumu Roma kutoongea maneno yake ya kipuuzi maana alijua pengine hata kanisa halijui.
Aliishia kumtambulisha Roma kwa Father Selestin na kisha maombezi yalianza kwa muda mfupi na kisha aliaga huku akikataa kubakia kwa ajili ya kifungua kinywa na kusema yupo kwenye maombi.
Asubuhi hio wanafamilia wakiwa mezani Roma alijitahidi kuongea na Edna kwa kumpatia chakula maalumu alichomwandalia lakini majibu yalikuwa yale ya kimikato mikato na hakugusa chakula alichopewa na kufanya wanafamilia hao kuona kuna kitu hakipo sawa kati yao.
“Edna mmegombana , kwanini hamuongeleshani?”Blandina alijikuta akikosa uvumilivu mara baada ya kuona vituko vinavyoendelea kati ya Roma na Edna
“Hatujagombana..”Aliongea Edna huku akiwa ni mwenye kulazimisha tabasamu.
“Vijana wa siku hizi mna’complicate’ mambo sana , hamjui namna ya kuvumiliana , mkikoseana wekeni wazi na ongeeni myamalize na ndio namna pekee ya kujirekebisha na kusonga mbele , nyie mna bahati sana mpo pamoja katika umri mdogo , mkishazeeka mnaweza msiweze kuonana tena na kujutia nafasi ambazo mlipaswa kumaliza sintofahamu zenu na kuishi kwa furaha”Aliongea Afande Kweka ambaye licha ya uzee wake alijua kuna vita ya baridi iliokuwa ikiendelea kati ya Roma na Edna.
Kila mmoja alikuwa kimya juu ya maongezi yake , ilikuwa ni kama vile anamkumbuka mke wake marehemu.
“Edna mimi siwezi kusimama upande wowote kati yenu , Roma anaweza kuwa kichwa kigumu lakini sio mjinga , anajitahidi kukubembeleza ili uweze kumsikiliza na kumsamehe , hivyo leo wote kwa pamoja ondokoni na binti yenu mkatembee , Roma mchukue mkeo na mpeleke duka lolote na mnunulie anachotaka ,Edna usisahau kununua na nguo pia kwa ajili ya kesho kwenda kutembelea ndugu, mpe nafasi mumeo ya kurekebisha makosa yake , na wewe Roma jitahidi kumfanya mkeo kuwa ni mwenye furaha ili kuyaziba madhaifu yako , Edna nataka ukirudi leo nikuone unatabasamu sawa?”Aliongea Afande Kweka na Edna alijisikia vizuri na kuitikia kwa kichwa.
Upande wa Roma alimshukuru mzee huyo kumpigia pasi maana ni kweli kama asingekuwa akijutia makosa yake asingeamka asubuhi asubuhi na kuwaambia wafanyakazi wamuachie yeye jiko kwani anataka kumpikia mke wake.
Upande wa Blandina alimwangalia mzee huyo na kuona huenda anafanya yote hayo kutokana na kumuonea huruma Roma kutokana na juhudi alizoweka.
Lakini hakuacha kuwaza na kusema pengine Edna ndio mwenye makosa na Edna anambebesha Roma mzigo wote , aliwaza hivyo maana aliona ni kama Edna anamtawala mtoto wake.
Upande mwingine kwenye mitandao habari za Sophia kurudi kwenye kazi zake za kisanii zilikuwa zikienea kwa kasi sana huku show yake ilioandaliwa kufanyika Iringa ikivuma huku kubwa zaidi ni uhusikaji wa wasanii wengine wakubwa ambao wangemsindikiza .
Zote hizo zilikuwa ni juhudi za Edna kutaka kumfanya Sophia kufanya kitu anachokipenda lakini kwa wakati huo akiifanya kampuni yake ya habari na burudani kufanya vizuri
Mpango ulikuwa ni kumtambulisha amerudi na hapo ndipo angeweza kupewa ofa ya kuigiza katika muvi ambayo kampuni ya Vexto Production walikuwa wakipanga kuidhalisha.
*****
Ilikuwa ni asubuhi ya siku ya jumamosi katiak jengo la wizara ya elimu iliingia gari kali aina ya Mercedenz Benz E Class Amg 53 , siku hio ndani ya jengo hilo hakukuwa na watu wengi pengine ni kutokana na kwamba ilikuwa ni wikiendi.
Baada ya gari ile kuegeshwa katika eneo husika aliweza kutoka Najma ambaye asubuhi hio ni kama vile uzuri wake umeongezeka mara mbili zaidi ya jana yake , pengine ni kutokana na kutembelea gari nzuri ndio maana ilimfanya kupendeza.
Siku hio hakuwa amevalia Shungi na kufanya kuzidi kupendeza na mtindo wake wa nywele wa twende kilioni, ni aina ya msuko wa kawaida lakini uliendana sana na muonekano wake.
Roma alikuwa ni mwepesi sana , jana mara baada ya kwenda kukagua gari na kuridhika nayo palepale alitoa zaidi ya milioni miambili kwenye akaunti yake na kuziingiza kwenye akaunti ya Fredi na kukamilisha malipo na baada ya hapo alimwambia Fredi kuagiza mtu kulipeleka nyumbani kwa Najma baada ya usajili kukamilika huku yeye akiondoka nae.
Upande wa Najma hakuwa na tabia za majigambo na wala hakuona ni jambo kubwa sana kuendesha gari ya bei ghali lakini hakuweza kujizuia kutaka kuonyesha kwa watu ni gari gani ambayo mpenzi wake amemnunulia.
Dakika ileile wakati akifungua mlango wa kushoto wa abiria akitoa begi la laptop yake ya mapakato ili afunge mlango kuelekea juu , gari aina ya Lamborgin iliingia eneo la maegesho na kwenda kusimama kando yake.
Baada ya gari ile kusimama kioo cha mbele kilishushwa na Naibu waziri Salihi alionekana na alishangaa mara baada ya kuona gari hio mpya ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Najma na aliishia kulazimisha tabasamu.
“Najma hii ni gari yao?”Aliuliza.
“Ndio Mheshimiwa Naibu waziri , asante kwa kunipa
lift kwa kipindi chote nadhani kwanzia sasa sitokusumbua tena”Aliongea Najma huku akiweka tabasamu ambalo lilizidi kumnyong’onyesha waziri. “Roma ndio kakununulia?”
“Ndio”
“Je unajua kwamba ameoa na mke wake ni mmiliki wa kampuni ya Vexto?”Aliuliza na kumfanya Najma kushangazwa na hilo.
“Nadhani hilo ni swala ambalo halikuhusu mheshimiwa , ni ukorofi kwa wewe kuanza kufatilia maisha ya wengine , ninaondoka kama huna kingine cha kuongea”
“Simama hapo hapo”Aliongea kwa namna ya kufoka huku akitoka nje ya gari.
“Ni kipi kizuri umekiona kwake , nimekuwa nikikubembeleza kwa muda mrefu kwa moyo wangu mkunjufu lakini umeshindwa hata kunipatia nafasi , yule ameoa tayari lakini bado tu unamng’ang’nia , ni upande upi ni mzuri sana kuliko mimi?”Aliongea kwa sauti na kumfanya Najma kuwa na wasiwasi kwani alikuwa akiona hasira yake.
“Sitaki kumlinganisha mpenzi wangu na mwanaume mwingine , mapenzi sio sawa na kununua kitu kwamba utachagua kwa muonekano wa vipimo maalumu, Mheshimiwa mimi nakuheshimu sana lakini naomba pia uyaheshimu maisha yangu binafsi hususani ukiwa hujui chochote kuhusu mimi”Aliongea kijeuri na wakati huo huo wakati Naibu waziri akijiandaa kuanza kuongea tena gari nyeusi aina ya Bentley iliweza kuingia na kwenda kusimama kando ya gari ya Salihi.
Wakati Salihi akikunja sura kutokana na ujio wa gari hio upande wa Najma alishangazwa kwani ilikuwa ni gari ya muonekano wa kifahari.
Dakika hio hio mwanamke mtu mzima mwenye muonekano wa kujipenda aliweza kutoka nje ya gari.
Alikuwa amevalia mavazi ya kuvutia mno , ijapokuwa sura yake ilionekana kuwa haijajikunja lakini kwa haraka haraka kwa mtu mwenye uzoefu angeweza kugundua mwanamke huyo ametumia ‘Botox injection’ kwa ajili ya kuzuia makunyanzi.
“My dear son , thank goodness you’re still here , the traffic was pretty bad and I thought I’ ll miss you”Aliongea yule mwanamke na kumfanya Najma kushangaa na kujiuliza inawezekanaje mwanamke huyo akawa mama kwa mheshimiwa ilihali muonekano wake ni kama vile ana miaka arobaini. “Unafanya nini hapa?”Aliuliza Salihi kwa kingereza.
“Nilitaka kuwa na muda mzuri na wewe , hatujaonana muda mrefu na nimekuja nchini lakini umekuwa ni wa kuniepuka”
“Hapana , nenda nyumbani nitakuja huko huko nina maswala ya kushughulikia sasa hivi”Aliongea na kumfanya yule mwanamke kumwangalia Najma kwa macho ya dharau.
“Oh , you found yourself a b*tch, what is wrong ? It sees like you two were quarrelling , she doesn’t like you”
“Oh nakuona umejipatia Ma**ya , tatizo ni nini , mlionekana mlikuwa mkigombana , hakupendi?”
“Asha jaribu kukaa kimya , ingia kwenye gari yako uondoke na uache kuongea ujinga”
“Mimi ni mama yako , kwanini nipotezee matatizo yako? Najua jina lake anaitwa Najma Waziri, najua hata mahali anapoishi”Aliongea kwa majigambo.
Najma alijisikia vibaya kwani macho ya huyo mwanamke yalikuwa ni ya kijeuri mno. “Ulikuwa ukimfuatilia , wewe Asha umechoka kuishi maisha mazuri?”
“Unapenda kunifokea kwasababu tu nashindwa kukupotezea, wewe ni mkatili sana , hakupendi lakini bado tu unanikatli , fanya utakavyo lakini jua mimi ni mama mzuri kwako , babu yako na wajomba watafika kwa ajili ya chakula cha usiku leo hii hakikisha unakuwepo , ole wako uache huyu Ma..ya akucheleweshe”
Baada ya kumsonya Najma alirudi kwenye gari yake na kisha liligeuzwa kijeuri na kutolewa ndani ya hilo eneo.
Upande wa Salihi alionyesha kuna kitu hakipo sawa na alimwangalia Najma kwa macho makali kwa muda mfupi na kisha na yeye aligeuza gari yake na kuondoka.
“Edna nimekuonya kuhusu mumeo lakini ukanipotezea na ukaaenda mbali na kumruhusu amnunulie gari mpenzi wake …,, , Roma kwahio unajaribu kunidhalilisha kwa kumnunulia mpenzi wako gari kwa kutumia hela za mke wako , ni ujinga wa namna gani huu , hebu ngoja tutaona ni karata gani nyingine unaweza kucheza , unathubutu vipi kuniibia mwanamke wangu?”Aliongea kwa hasira huku aking’ata meno
Roma na harakati zake nini kitajili? Vipi kuhusu ndoto za Edna ,Usikose.
ITAENDELEA.

Sent from my 23021RAAEG using JamiiForums mobile app
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI : SINGANOJR
WATSAPP : 0687151346.

Mono no aware.

SEHEMU YA 634.
Salihi wakati akiwa kwenye gari lake akiendesha kwa pupa kusonga mbele alijikuta akipata wazo na kutoa simu yake haraka haraka na kutafuta namba flani alioisave kwa jina la Uncle na kuipiga.
“Hahaha ...Mheshimiwa Naibu kwanini unapiga tena kuna tatizo, nimealikwa leo kwa ajili ya kufika nyumbani kwenu kwa ajili ya chakula cha usiku” Sauti upande wa pili ilisikika .
“Mjomba haina haja ya kuongea kwa matani na kujishusha, wewe ni mkubwa kwangu na sijakupatia heshima yako inavyostahili tokea nirudi nchini” “Kwanini unaongea kwa upole hivyo?, Au kuna kitu unataka kuniomba, pengine kama ni swala la kukupigia debe kwa baba yako hilo niachie mimi”Aliongea na kumfanya bwana Salihi kutoa tabasabu la uovu.
“Mjomba najua wewe ni Mkurugenzi msaidizi , kwanini nikuhangaishe na maswala yangu madogo kwa kwenda kumtaarifu baba”
“Kama ni hivyo basi niambie tatizo lako nikusaidie mwenyewe”
“Mjomba shida yangu ni kwamba nimejikuta nakuwa na kinyongo na Edna Adebayo bosi wa kamouni ya Vexto , najua moja ya kampuni yake tanzu inajihusisha na maswala ya udhalishaji wa kemikali, unaonaje ukinisaidia kwa kumtengenezea tatizo katika kiwanda chake ili tu kuharibu maswala ya kiudhalishaji”Aliongea na kufanya upande wa pili kusikia mguno na ukimya wa sekunde kadhaa.
“Hapana Bwana mdogo , sio kama sitaki kukusaidia lakini mtu unaemzungumzia hapo ni Edna , ingekuwa kampuni nyingine tofauti na ya Kanani, Vexto na Maple ningekusaidia, Edna sio mfanyabiashara wa kawaida , Nguvu ambayo ipo nyuma yake sio ya kawaida kabisa hivyo ni ngumu sana kugusa kampuni yake , kwanini una kimyongo nae., mbona haupo makini mjomba??”Aliongea mwanaume alieitwa Mjomba akiwa siriasi.
Salihi alijikuta akishikwa na mshangao kwani mjomba wake huyo hakuwahi kuogopa mtu na siku zote ni mtu wa kutii kila analomwambia kwa kuogopa anaweza kumuongelea vibaya mbele ya baba yake.
“Kwanini Mjomba , Si Edna ni mfanyabiashara mwenye akili tu ambaye amezoea kuonea kampuni za chini yake , sidhani kama kuna haja ya kuogopa kwani ninachokijua hata ndugu zake karibia wote wamefariki”
“Upo sahihi Edna anaweza kuwa mfanyabiashara wa kawaida mwenye akili na familia yake kufariki lakini hebu jiulize mwenyewe ni kwa muda.mrefu kampuni yake imekuwa ikifanya vizuri bila hata ya kupatwa na changamoto ambazo kampuni nyimgine hapa nchini zinapitia , Kampuni yakr haigusiki sio kwasababu yake tu bali ukweli ni kwamba mume wake Roma Ramoni ni mwanafamilia wa ukoo wa Kweka ambae inasemekana anatarajia kufanywa mrithi,huwezi kujua haya maana umekaa sana nje ya nchi na network yako ya taarifa ni ndogo , umefanya vizuri kuanza kuawasiliana na mimi”
“Nini!!, unasema mwanafamilia wa ukoo wa Kweka,
Kwahio unamaana ya kwamba Roma ndio mtoto wa Raisi Senga kama inavyosemwa??”
“Upo sahihi nadhani licha ya kuishi kwako nje ya nchi una fununu ya nguvu ya familia hio kwa sasa”
Salihi alijikuta akipigwa na mshangao wa aina yake na alilaani kukaa kwake nje ya nchi kumemfanya kutojua mambo mengi yanayoendelea nchini , pengine ni kutokana na tabia yake ya kutopendelea kufatilia maswala ya siasa.
Hata kurudi kwake nchini alilazimishwa na familia yake kuingia katika ulingo wa siasa, lakini ukweli ni kwamba sio aina ya maisha alioyataka .
Alikuwa na uelewa mchache juu ya familia ambazo zinanguvu kubwa nchini , familia ya Mzee Atanasi ambayo ndio imemtoa Tajiri Azizi , familia ya Kweka ambayo ndio.imeshikilia jeshi na familia ya kigombolana ndio inakuja familia yao ambayo imelishikilia taifa kiroho(Hapa utaelewa baade kidogo)..
Sasa Salihi alikuwa amekwisha kuzisikia habari za wanajeshi kushambuliwa mkoani Iringa , ijapokuwa taarifa hio ilikuwa ni ya siri lakini kwa nafasi yake ya kiungozi aliweza kuzipata lakini sasa hakujua kama mtu ambaye amehusika ndio Roma Ramoni.
“Bwana mdogo , nadhani tufanye kama hujazungumzia kabisa hili swala , hatuwezi kunufaika nalo , sio kwangu tu pengine hata ukoo wetu wote hauwezi kushindana na yule shetani”
“Mjomba huu ni ujinga ,kwanini tumuogope Roma na ukoo wake , hawamiliki hii nchi na hata kama watataka kutushambulia chama hakiwezi kuruhusu kwani ni swala ambalo linaweza kuibua mpasuko wa kitaifa , usisahau baba pia ndio alifanya juhudi kubwa ya kutoa ufadhili kwa ajili ya kumfadhili raisi Senga”
“Hehe ,, upo sahihi kabisa haiwezi ikatokea familia yetu kushambuliwa kirahisi , isitoshe na sisi pia tuna mizizi ndani ya taifa hili ambayo haionekani kwa macho”Aliongea mjomba wake Salihi.
“Sema mjomba ni bora nimejua hili mapema, la sivyo ningejiingiza kwenye matatizo, naomba usimwambie chochote baba maana hakawii kukasirika”
Waziri Salihi mara baada ya kujua kwa udani kuhusu ukoo wa Roma alona haikuwa na haja kwenda mbali
zaidi kwa ajili tu ya kujiridhisha na hasira yake ili hali athari zinaweza kuwa kubwa.
Aliwaza pengine atafute nafasi ya kuweza kumbembeleza Najma ili apotezee ugomvi wao uliotokea, Waziri Salihi alijiambia ni kheri aendelee kuwa rafiki wa kawaida wa Najma kuliko kuwa na adui aliejificha.
“It is better to be a cautious crow than fearless one, for the cautious crow lives a long life” Aliwaza akijiambiani kherikuwa kunguru muoga kwani anaishi miaka mingi.
******
Kama Edna na Roma walivyoambiwa na Afande Kweka kutoka pamoja na Lanlan kwenda kutembea ndio kilichotokea.
Ijapokuwa Edna alikuwa na hasira na Roma lakini hakutaka kabisa kupotezea uwepo wake , akiwa kanuna hivyo hivyo aliamua kuondoka nae , hakutaka pia kuonekana kama mwanamke kiburi asietii wakubwa na mume wake, isitoshe alikuwa kwenye mazingira ya ukweni hivyo ilimaanisha asingeweza kufanya kila anachotaka.
Ikiwa ni muda wa jioni ya saa kumi na mbili na nusu wakati Edna na Roma bado hawajarudi nyumban, alifika mgeni ambaye alimshangaza kidogo Afande Kweka kwani ni kwa kipindi kirefu sana hajawahi kuonana nae.
Babu yake Sophia, yaani Jenerali mstaafu wa jeshi aliepokea kijiti kutoka kwa Afande Kweka , mara baada ya kumtelekeza Mariaum bibi yake Edna akiwa mjamzito alioana na mwanamke aliefahamika kwa jina la Sumaiya ambaye alikuwa ni mwanajeshi mwenzake katika kitengo cha wachawi.
Ni sahihi kusema Afande Athumani kipindi hicho akiwa chini ya uongozi wa Afande Cammilius Kweka kama mkuu wa jeshi ndio aliekuwa Kanali akisimamia kitengo kipya kilichoundwa jeshini maalumu kwa ajili ya kupambana na nguvu za giza, yaani kikosi cha wachawi.
Kipindi hicho wakati kikosi hiko kinaanzishwa hakukuwa na mwanajeshi yoyote ambaye alikuwa na mafunzo ya kichawi , hivyo ni kama lilikuwa ni wazo ambalo lilianza kutekelezwa na jeshi na msimamizi mkuu alikuwa ni Kanali Afande Athumani.
Wakati kitengo hichi kinaanizishwa tayari Kanali
Athumani ashafunga ndoa na mwanajeshi mwenzake aliefahamika kwa jina la Kapteni Sumaiya Mbale, au Kapteni Mbale kama alivyofahamika sana , mwanajeshi machachali sana jeshini ambaye pia alikuwa mtoto wa kigogo wa kiserikali wakati huo.
Kati ya wanajeshi waliochaguliwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo ni Kapteni Mbale mke wa Afande Athumani ambaye alijitolea mwenyewe
,ilikuwa ni wakati ambao tayari ashamzaa
Ramadhani ambaye alikuwa ndio mtoto wa pili kwa Afande Athumani ukiachana na Adebayo ambaye alikuwa ni mtoto wa nje ya ndoa aliezaliwa na Marium.
Inasemekana mara baada ya Kapteni Mbale kurudi mafunzoni alimkuta Afande Athumani alishaoa mke wa pili afahamikae kwa jina la Fatuma ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari na habari hio mara baada ya kumfikia, Kapteni Mbale ambaye alipandishwa cheo na kuwa Meja mara baada ya kurudi nchini alikasirika sana na kuitaka talaka mara moja na mgogoro ulikuwa mkubwa mno kiasi cha kupelekea Afande Athumani kumpa talaka yake licha ya kwamba alichokifanya sio kosa kwani ilikuwa ni sheria ya dini yake ya kiislamu kumruhusu kuoa wake zaidi ya wawili lakini kwa Afande Sumaiya Mbale hakusikia la mwadhini.
Miaka kadhaa baada ya Afande Athumani kupandishwa cheo na kuwa mkuu wa majeshi upande wa Sumaiya alikuwa ashajiunga na kikosi cha usalama wa taifa na kupewa misheni maalumu akiwa undercover katika kivuli cha ubalozi nchini China.
Na kwanzia hapo maisha ya Sumaiya mara nyingi yalikuwa nje ya nchi , alikuwa jasusi mbobezi ambaye alihamishwa kwenda nchi mbalimbali kijasusi mara baada ya kukaa China kwa muda mrefu na ilisemekana rafiki yake mkubwa alikuwa ni Abbess Yumiao Master wa dhehebu la Shushan ambaye alikutana nae wakati wa mafunzo ya kichawi katika dhehebu hilo.
Sifa kubwa ya Sumaiya ni hasira za haraka na kutojali , inasemekana ni aina ya tabia alioweza kuipata mara baada ya mume wake kuoa mke wa pili, wazungu wanaweza kuita tabia ya Sumaiya kama ‘Bad temper’.
Lakini licha ya hivyo alikuwa akimpenda mtoto wake Athumani sana na pia vilevile alikuwa akimpenda mjukuu wake Sophia kwa viwango na ndio aliempa presha AbessYumiao kukaa macho katika Dehebu la Shushani ili tu kumpata Sophia mara baada ya kupotea kwake.
Sasa jambo moja unalotaka kuelewa ni kwamba kitendo cha Ramadhani baba yake Sophia kulazimisha Sophia kuolewa na Roma nyuma yake alikuwepo huyo Sumaiya bibi yake Sophia, jasusi mbobezi ambaye ana historia yake kwa mchango alioweza kufanya katika upande wa usalama wa taifa.
Maisha ya Sumaiya kwa miaka yake yote ni nchini Marekani na mara baada ya kustaafu kwa hiari yake alihusishwa kuwa jasusi chini ya kikosi cha Dhoruba nyekundu japo habari hizo hazikuwahi kuthibitishwa na yeye mwenyewe alipinga vikali kuhusishwa na shutuma hizo miaka ya nyuma , lakini kutokana na sintofahamu serikali ya Tanzania iliacha kabisa kumuhusisha na maswala ya kiserikali na kwanzia hapo alionekana mara chache sana nchini Tanzania.
Afande Kweka alikuwa akimuheshimu sana Sumaiya kutokana na ujasusi wake, mwenyewe alikuwa akijiita jasusi lakini kwa Sumaiya alikuwa pia ni Konkodi lakini hata hivyo bado hakuwa akimzidi hata kidogo.
“Bi Sumaiya ni siku nyingi hatujaonana, je upo hapa Iringa kwa ajili ya Sophia?”Aliuliza Afande Kweka mara baada ya kusalimiana na mgeni.
“Unaweza sema hivyo Mr Cammillius , lakini nipo pia hapa kwako kwa ajili ya Sophia”Aliongea na kumfanya Blandina kushindwa kuelewa anataka kumaanisha nini.
“Madam kuna shida yoyote kuhusu Sophia?”Aliuliza Blandina alikuwa akimjua vizuri.
“Mjukuu wangu Sophia na Roma ni wapenzi na hiki ndio ambacho kimenileta”Aliongea na kumfanya Blandina kushika mdomo huku Afande Kweka misuli yake ya uso ilicheza.
Wote walijua hio sio taarifa nzuri kwani kama Edna ataijua basi matatizo makubwa yanaweza yakajitokeza , isitoshe muda huo walikuwa wameenda kutembea kwa ajili ya kumaliza hali ya kimigogoto ambayo ilikuwa ikiendelea kati yao.
“Inaonekana hamna taarifa juu ya hilo , lakini Sophia mara aada ya kurudi kutoka huko alikopotea aliweza kusema kila kitu , mimi licha ya kwamba sijaishi muda mrefu na Sophia lakini namjua vizuri na hata mwanangu Ramadhani anamjua Sophia vizuri , ni msichana mwenye aibu sana na sio jambo rahisi kuziweka hisia zake wazi , labda niwaeleze tu Sophia kuacha kwake usanii ilikuwa ni kutokana na hisia zake za kimapenzi juu ya Roma, ninachomaanisha ni kwamba Sophia yupo siriasi kuhusu uhusiano wake na kwasababu tunajua tabia ya Sophia ni ya upole basi nimeamua kuingilia hili kati”Aliongea kwa kujiamini tena kwa sauti kubwa, alionekana ni wale wanawake ambao hawana upole ndani yao.
“Nadhani ukiachana na hilo kuna lingine pia unataka kutoka kwetu si ndio, maana sidhani kama kuna haja ya kuingilia mahusiano yao kama ndio wameamua?”Aliongea Afande Kweka.
“Upo sahihi ukiachana na mahusiano yao pia nina sababu nyingi”
“Unaweza kutuelezea tukusikie”Aliongea Afande Kweka huku akinywa kidogo kahawa yake, ijapokuwa taarifa hio ni mbaya lakini alionyesha utulivu.
“Mwanzoni nilitaka Sophia kuwa mke wa pili kwa Roma , lakini hilo kwa sasa nadhani haliwezekani hivyo nimekuja na ombi lingine”Alipozi na kisha akaendelea.
“Kwa ninavyojua ni kwamba Roma hana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito mpaka afikie mwishoni mwa levo ya nafsi kwenye mafunzo ya kijini, sidhani kama mnalijua hilo?”
“Upo sahihi”Alijibu Blandina.
“Basi nadhani pia mnapaswa kuelewa kwamba
Sophia mpaka sasa amekwisha kufikia katika levo ya
Nafsi hivyo uwezekano wa yeye kupata ujauzito wa Roma ni mkubwa na kama itatokea, tunataka mtoto wa Sophia kuwa chini ya ukoo wetu”Aliongea na kumfanya Blandina kushangaa lakini upande wa Afande Kweka hakuonyesha mshangao ni kama alitarajia hilo.
Afande Kweka alikuwa akijua uzao wa Roma sio wa kawaida, pengine ni sawa na kusema ni mwanzo wa kizazi kipya katika uso wa dunia.
Mwanzoni alipoambiwa maneno hayo na Paster Cohen hakuwa akiamini lakini mara baada ya kurudi kwa Lanlan ndio aliweza kujua maana ya maneno yake.
“Uzao wa Roma ni mwanzo wa kizazi kipya chenye uwezekano wa kuwa na thamani kubwa au cha hatari kwa dunia”Kauli hio ilitoka kwa Paster Cohen siku moja mara baada ya kumuona Lanlan.
Ukweli ni kwamba siku ambayo Paster Cohen alifika nyumbani kwa Afande Kweka malengo yake makuu ni kuweza kumuona Lanlan na kuthibitisha matarajio yake na mara baada ya kumuona ndio sasa aliweza kuyaelewa maelezo ya Hades wa Zamani ambaye alimwambia kauli sawa na aliomwambia Afande Kweka ya kizazi cha Roma kinaweza kuwa cha hatari au chenye uthamani mkubwa kwa dunia.
Pastor Cohen ndio watu waliokuwa wakijua kama mpango LADO ungeweza kufanikiwa basi moja kwa moja ndio mwanzo wa kizazi kipya na katika maisha yake alitamani kuona kizazi chenyewe kabla ya siku zake hapa duniani kufika mwisho na mara baada ya kumuona Lanlan ndio sasa aliweza kuridhika.
Upande wa Afande Kweka tokea mwanzo alijua haikuwa bahati mbaya kwa familia ya Athumani kumtaka Sophia kuwa na mahusiano na Roma alijua tu Sumaiya alikuwa akivuta kamba kwa siri akimtangulizia mtoto wake mbele.
Roma anaweza kuja kuwa na watoto wengi zaidi ya ilivyotarajiwa lakini kumfanya mtoto mmoja kutokuwa sehemu ya ukoo ilikuwa ni stori nyingine kabisa.
Afande Kweka alionekana kuwaza kwa muda na kisha akafumba macho yake na kuyafumbua.
“Ninaweza kuelewa nia yako na pia ninaweza kuruhusu hili ila lazima kuwe na masharti” “Nipo tayari kuyasikiliza”
“Kama mtoto huyo atakuwa nje ya ukoo wetu inamaanisha kwamba jina lake la ukoo haliwezi kuwa la Kweka hivyo moja kwa moja atakuwa na jina la ukoo kutoka familia yenu na pia hawezi kupata urithi wowote kutoka kwetu , familia yenu itahusika na elimu yake pia jamboa ambalo linamaanisha hata mbinu ya kipekee ya Roma ya mafunzo ya kijini hawezi kupata”Aliongea Afande Kweka na alimfanya Bi Sumaiya kuonyesha kutoridhishwa na jambo hilo.
“Afande nakuelewa unachomaanisha lakini ninachojua ni kwamba mbinu hio asili yake ni kutoka taifa la China katika dhehebu la Tang hivyo moja kwa moja ni kwamba haiwezi kuwa ya familia yako kama urithi”
“Upo sahihi lakini ni raia kutoka taifa la Tanzania ambaye ameweza kujifunza hii mbinu na ikaonyesha mafanikio , hivyo ni sawa na kusema ni Roma pekee ambaye anaijua , hivyo moja kwa moja itaendelea kubakia chini ya ukoo wetu”
“Lakini huyu mtoto atakaezaliwa atakuwa ni mtoto wa Roma pia?”
“Upo sahihi atakuwa ni damu ya Roma na hio ni faida kubwa kwenu kwani atakuwa ni mtoto wa tofauti , nadhani hicho ndio unacholenga hivyo kuhusu mbinu ya kijini hatoweza kuipata”Aliongea Afande Kweka akiwa siriasi na kumfanya Bi Sumaiya sura yake kujikunja.
“Hilo haliwezekani”Aliongea.
“Madam huwezi kulazimisha huo ndio msimamo wa kifamilia”Aliongea Blandina na kumfanya Afande Kweka kupata ahueni maana hakutaka kujibishana na mwanamke huyo ilihali msimamo wake upo wazi.
Dakika hio hio akiwa hajui aendeleze vipi maongezi hayo akipandwa na hasira kama kawaida yake aliweza kupata ahueni mara baada ya kuweza kuhisi ujio wa Roma, alikuwa na nguvu za kijini pia katika levo ya Nafsi pengine ndio maana hakuonekana kuzeeka sana.
“Vizuri Roma amerudi mwenyewe nitaongea nae yeye nione kama anakubaliana na hili au lah, hakuna mtu mwingine anaepaswa kuingilia kama akikubali”Aliongea na ilikuwa ni kama alivyoongea kwani Roma palepale aliweza kutokea akiwa ameshikilia mifuko mkononi.
Alikuwa ametangulizana na Edna ambaye alionekana amechangamka kwani walikuwa wakiongea na Roma muda huo wakati wakiingia ndani ya nyumba hio huku akiwa amemshikilia Lanlan mkono na uso wake ulipambwa na tabasamu na lilipotea mara baada ya kumuona bibi yake Sophia.
Wataalamu wa mahusiano wannasema mbinu pekee ya kuweza kumpa mwanamke furaha pale unapomkosea ni kumpeleka Shopping anunue kila kitu kinachomfurahisha na mwanamme kulipia na hilo lilionekana kufanya kazi kwa Edna.
Edna alikuwa akimjua bibi yake Sophia nje ndani na alishawahi kukutana nae na sifa zake pia alishawahi kuzisikia kutoka kwa bibi yake na karibia zote hazikuwahi kuwa taarifa nzuri ,pengine bibi yake alikuwa ‘biased’ kutokana na kwamba ndio mwanamke aliemchukulia mwanaume anaempenda huku yeye akitelekezwa.
Ukweli ni kwamba Edna alikuwa akijua fika kwamba bibi yake Sophia hakuwa akimpenda.
Kila mtu aliekuwa hapo ndani alionekana kupatwa na ahueni mara baada ya kuona Roma na Edna wamepatana lakini uwepo wa bibi yake Sophia walijua kabisa utageuza hali ya hewa muda wowote.
Roma mara baada ya kumuona huyo mwanamke mapigo yake ya moyo yalidunda , alikuwa akimjua ni bibi yake Sophia licha ya kwamba hajawahi kuonana nae na habari zake alikuwa akizisikia juu juu.
Sophia alishawahi kumuonyesha picha yake na hata
Edna pia alikuwa akimjua na alishawahi kumdokezea , ukiachana na wasiwasi wake juu ya uwepo wake hapo nyumbani lakini alishangazwa na namna ambavyo alionekana kuwa kijana licha ya kuwa na umri wa miaka mingi na alijua pengine alikuwa na mafunzo ya kijini.
“Mr Roma nadhani sina haja ya kujitambulisha kwani Sophia amesema unanifahamu , mimi ndio bibi yake na nitaenda moja kwa moja katika swala ambalo limenileta hapa kuhusu Sophia”
“Bibi nakujua ndio lakini hatujawahi kuonana , nadhani tunapaswa kusalimiana vizuri kabla hatujafanya maongezi”Aliongea Roma huku akiweka ile mifuko ya nguo chini sakafuni akitaka kusalimiana nae.
“Tutafahamina rasmi kama utajibu maswali yangu kwanza ,Je utawajibika moja kwa moja kwa watoto wako na Sophia?”Aliuliza mwanamke huyo huku akimpotezea Edna kama hajamuona vile.
Swali hilo lilikuwa kama bomu na halikumpiga yeye tu lakini pia lilimgusa Edna aliekuwa nyuma ya Roma.
Roma alimwangalia mwanamke huyo katika muonekano usiokuwa wa kawaida wa huzuni lakini pia muoneknao wenye maswali na kujiuliza imekuwaje huyo mwanamke akajua uhusiano wake na Sophia.
Roma hakuwa akijua kwamba Abbess na Bibi yake Sophia walikuwa marafiki na ndio maana Sophia alienda kuchukulia mafunzo katika Dhehebu la Shushani , pengine ni uzembe wake kutouliza au ni kosa la Sophia kutokumweleza.
Moyo wake ulitetemeka mara baada ya kumpiga macho Edna aliekuwa nyuma yake na kujiambia ni balaa gani hii inakwenda kumtokea tena.
“Nini tatizo? Ulikuwa ukifanya siri, kwanini unaonekana kuwa katika hali ya mshituko, Au ulikuwa ukimdanganya Sophia kwa kumridhisha kuwa nae katika mahusiano kwasababu anakupenda , Roma nadhani hunijui vizuri nitakuua kama ukimuumiza mjukuu wangu kihisia, mimi ndio Afande Mbale muulize babu yako ananijua vizuri nilivyo mapepe”

SEHEMU YA 635.
Edna mara baada ya kusikia maneno ya bibi yake na Sophia uso wake ulibadilika palepale huku akikumbuka siku ambayo Sophia alikuwa akijaribu kumfariji mara baada ya kumuona Roma akibusiana na Clark.
Edna siku ile alijaribu hata kumwambia maneno ya kumtia moyo ili tu apunguze wasiwasi juu yake.
Edna mpaka hapo alijua kabisa siku ile yeye ndio mjinga , alianza kuchukia, kumbe alikuwa akifanywa mjinga hata na Sophia , alijaribu hata kuji ‘assert’ kwa kujiambia kila kitu kipo sawa na anaelewa kila kitu.
Mbele yake kulikuwa ni kiza na mwanaume aliekuwa pembeni yake ni kama vile hakuwa akimjua , kwake ilikuwa ni kama vile ndio mwisho wa dunia.
“Edna!! Edna… naomba unisikilize”Roma aliweza kyaona mabadiliko ya Edna, mabadiliko ambayo hayakuashiria uhai badala yake yamejazwa na chuki ya kifo.
Bi Sumaiya aliweza kujua amefanya kosa kubwa, maneno yake yameonekana kuwa bomu kwa Edna kuliko hata alivyotegemea.
Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kunyanyuika alipokuwa amekaa na kumkimbilia Edna na kumshikilia mkono .
“Edna usiwe kama hivi , ndio tumejua sasa hivi kama Rima amekusaliti , tutamuadhibu kwa ajlili ya hiloo … Edna kwanini mikono yako ni ya baridi hivyo , unaumwa?”Aliongea Blandina huku akihisi mshangao kutokana na ubaridi wa Edna ni kama vile ameshika maiti.
Edna hakuongea chochote alikuwa amesimama kama sanamu , hakuwa akitoa machozi,hakuwa akionekana kama alikuwa akiumia ila alikuwa amesimama kama vile ni msukule uliokosa nafsi na kufanya kila mtu aliekuwa akimwangalia kujawa na wasiwasi.
“Unafanya nini , umebadilika hivyo kwasababu tu ya Sophia, hata hivyo Sophia sio mwanamke wa kwanza
Roma kukusaliti nae , kwa maoni yangu ulipaswa kujiandaa kwa hili”Aliongea Bibi yake Sophia huku akikunja sura.
“Inatosha”
Roma aliongea kwa nguvu , pengine kama Mwanamke huyo hakuwa na uhusiano na Sophia basi angekuwa ashamuua hapo hapo au penginge kumchapa kibao.
“Sijafanya kosa lolote , Edna hana undugu wowote na mjukuu wangu , hivyo haileti maana kuwa kama hivyo”
“Madam unaenda mbali , unafikiri hatujui kwamba ulifanya hila na kumpokonya bibi yake Edna mume wake , lakini uliishia wapi wakati alipooa mwanamke mwigine ukamkimbia , yaani wewe ya kwako yamekushinda unataka na Edna kuwa sawa”Aliongea Blandina baada ya kukosa uvumilivu.
“Kimya”Aliongea kwa nguvu bibi yake Sophia huku akionyesha hasira waziwazi .
“Hivi unajua wewe ni kama mtoto kwangu , usitake niende mbali na kuweka wazi ujjinga wako uliofanya miaka na miaka”.
“Una mdhalilisha Edna tena akiwa nyumbani, unadhani naogopa ukiyasema mabaya yangu , unaweza kuongea chochote lakini siwezi kukuruhusu kumdhalilisha Edna”
Blandina na Bi Sumaiya walianza kuwakiana, upande wa Roma alishindwa kujua namna ya kumbembeleza Edna kwa muda huo kwani asingeweza pia kusema kama hakuna kinachoendelea kati yake na Sophia.
Alijua kusema hana mahusiano na Sophia isingekuwa kudanganya wengine bali angejidanganya mwenyewe na pia angemuumiza Edna na Sophia kwa wakati mmoja.
Dakika hio hio ni kama Edna alijua nini cha kufanya kwani alimpiga Roma jicho kali na kisha akageuka akitupa kila alichoshikilia chini.
“Edna unaenda wapi?”Aliongea Roma akitaka kumsogelea na kumzuia kwa kumshika mkono lakini alionekana kuchelewa kwani Edna alikuwa fasta na ndani ya dakika chache tu alikuwa nje ya nyumba.
Lanlan alitaka kumfuata mama yake lakini Roma palepale alimpakata na kumuweka kwenye mikono ya mama yake.
“Lanlan kuwa mtoto mtiifu ,baki hapa usubirie chakula cha usiku ule ulale”Aliongea Roma na palepale alikimbilia nje kumfuata Edna.
Blandina alitaka kumuita Roma lakini aliishia njiani kwani alishindwa hata kutoa sauti.
Lalan anaweza kua mtoto lakini alikuwa ashajua wazazi wake wapo katika migogoro , akiwa na mwonekano wake ambao muda wote ni kama mtoto mwenye furaha aliishia kuangalia upande wa nje baba na mama yake wakipotea bila ya yeye kutoka kwenye mikono ya bibi yake.
Roma ile anafika nje aliweza kumfikia Edna ambaye tayari ashaingia kwenye gari ya Audi nyekundu na Roma alitaka kumzuia kwa mbele lakini alipigwa jicho hilo ambalo licha ya kwamba aliona kupitia kwenye kioo cha gari lakini ilitosha kumuogopesha.
Edna hakujali kusimama kwake mbele na aliendesha gari kwa kasi kama anataka kumgonga na Roma alikuwa mwepesi kwani alisogea pembeni na gari ikapita.
Roma hakutaka kusubiri na palepale alikimbia upande wa nyuma magari yanapo egeshwa na palepale alichukua gari ya BMW ya Afande Kweka na kisha aliliwasha na kulitoa nje ya geti.
Roma mara baada ya kutoka nje ya geti gari ya Edna ilioekana ikikata kona kwa ustadi wa hali ya juu kuingia barabara kuu ya kuelekea mjini.
Roma alishangazwa na uwezo wa hali ya juu wa Edna kuendesha gari lakini hata hivyo alijua kwa uwezo wake wa kuendesha gari basi angeweza kumfikia , alijiambia kama aliweza kumshinda Tusiman mwendesha magari maarufu wa dunia anashindwaje kumshinda Edna.
Lakini sasa Roma mara baada ya kuingia kwenye barabara kuu alikuwa ameachwa umbali mrefu sana huku akisikia mngurumo wa gari ya Edna ukiwa sio wa kawaida kabisa namna ambavyo gari ilikuwa ikibadilisha gia zake na kusonga mbele.
Roma jasho lilimtoka na kujiuliza au uwezo wa Edna kuendesha gari unahusiana na kile kilichotokea wakati akiwa hayupo mpaka kuua wanajeshi.
Ilichukua dakika kama tatu tu walikuwa wapo mjini kuingia kwenye ‘Raundi about’ na ile Edna anapita tu taa za kuongoza magari ziliwaka na kumzuia Roma na Semi Traller iliokuwa ikitokea upande wa kushoto kwake ilimzibia njia na kujikuta aking’ata meno yake kwani mpaka hapo alijua kabisa Edna kamchezea mchezo wa hila.
Mpaka ile gari yenye makontena mawili juu kupita Roma hakuweza kuiona gari ya Edna mbele yake na ilimfanya Roma kukosa chaguzi nyingine na kuanza kuifukuzia kwa mara nyingine.
Kwa wakati huo Roma hakuwa na wasiwasi kwa Edna kupata ajali kwani kwa uwezo wake ule aliamini haukuwa wa kawaida kabisa kuweza kupata ajali.
Roma aljikuta akilaani kutokuweza kwake kutumia uwezo wa kijini , pengine muda huo angeamua kusafiri kwa kuteleport na ingemuokoa kwenye taabu zote za kukimbizana na mke wake.
Roma hakuwaza ingekuja siku kukimbizana na Edna kwenye barabara kama hivyo , ilikuwa ni kituko na ilionekana ni kama Roma na Edna wamegeuka na kuwa maadui.
Dakika kama kumi tu gari ya Edna iliweza kufika katika hoteli ya Iringa Highland , sehemu ambayo ndio ambapo show ya Sophia inayoonyeshwa laivu kupitia V-TV ilikuwa ikipaswa kufanyika masaa machache yajayo.
Roma mara baada ya kufika nje ya hoteli hio alijua pengine Edna amekuja kwa ajili ya Sophia na alishindwa kuelewa nini anakwenda kufanya na palepale aliona aharakishe kuingia.
Lakini sasa Roma ile anataka kuingia alizuiwa na walinzi na kutakiwa kuonyesha kadi ya mwaliko , tiketi au kitambulisho lakini Roma hakuwa na chochote mfukoni.
Ilikuwa rahisi kwa Edna kupita kwani alikuwa ndio mmiliki wa wa kampuni ya Vexto Media lakini kuhusu yeye hakuwa akifahamika sana.
Roma aliamua kuegesha gari pembeni ya barabara na alitumia njia nyingine kuingia ndani , ijapokuwa sehemu ambayo alikuwa ameegesha palikuwa na kibao cha kuonyesha hapuruhusiwi kuegesha lakini hakuona haja ya kutafuta sehemu nyingne , aliamini hakuna shida ili mradi gari yake ilikuwa na Plate namba za jeshi.
Roma mara baada ya kuingia ndani ya hoteli hio alianza kukimbia kuelekea upande wa ukumbi ulipo kwani ni eneo ambalo lilikuwa limetanganishwa na hotel.
Alikuwa akikimbia huku akipiga simu kwa Sophia na bahati nzuri iliweza kupokelewa.
“Sophia .. ulimwambia bibi yako kuhusu sisi?”Aliuliza Roma.
“Sijamwambia mimi , MasterYumiao na bibi ni marafiki, hivyo aliniuliza kuthibitisha tu na sikuwa na jinsi”aliongea Sophia.
Roma alijikuta akijutia mara baada ya kusikia maelezo ya Sophia , alijua pengine Sophia alielezea kuhusu ulimwengu wa majini tu kumbe alielezea kila kitu mpaka mahusiano yao, lakini hakumlaumu na aliona yeye ndio mwenye makosa , alipaswa kumuuliza Sophia kuhusu bibi yake au angempa tahadhari tokea walipokuwa kwenye ulimwengu wa majini pepo.
“Dada yako Edna yupo eneo la ukumbini anajua kila kitu na amekasirika mno, sijui anapanga kufanya nini lakini nisaidie niweze kumdhibiti , usiruhusu afanye jambo lolote la kijinga”Aliongea Roma.
Alijua kabisa Sophia angeweza kumdhibiti Edna kwani tayari alikuwa levo ya Nafsi.
Upande wa Sophia alijuta , alijua bibi yake alikuja Iringa kwa ajili ya show yake kumbe kilichomleta ni jambo lingine.
Upande wa Edna ambaye alifika mapema aliweza kufika ndani ya hoteli hio na kutoka kwenye gari na kuanza kupiga hatua kuelekea upande wa ofisi za ukumbi huo jengo maalumu ambalo maandalizi hufanyikia.
Edna alikuwa kauzu mno, muonekano wake ni kama wa gaidi ambaye muda wowote angejitoa muhanga kwa kujilipua na bomu.
Edna mara baada ya kuingia katika chumba maalumu cha kubadilishia na maandalizi kilichojumuisha wanawake alianza kuangalia watu waliokuwemo ndani humo huku akiitafuta sura ya Sophia na haikumchukua dakika nyingi mpaka kuiona.
“Chukua watu wako ondoka nao”Aliongea Edna kikauzu akimpa maagizo Ummy Meneja wa Sophia.
Ummy hakuthubutu kuongea chochote na aliwapa ishara wafanyakazi waliokuwa wakimlemba Sophia na wote kwa pamoja walikimbilia nje na sasa waliobaki alikuwa ni Edna na Sophia peke yao.
“Sis…. Najua .,. najua unanichukia , nimekusaliti lakini siwezi kuzuia hisia zangu ,,,, nime..”Sophia alianza kutetemeka huku akiogopa macho ya Edna.
Edna alisogea bila kuongea nae lolote na palepale alimchapa kofi Sophia la uhakika kiasi cha kumyumbisha na kurudi nyuma mpaka kushikilia kioo ukutani.
Kofi hilo halikuwa la kawaida kabisa kwani lilimpeleka Sophia kuhisi kengele kwenye masikio yake.
Sophia alikua na uwezo wa kulikwepa lakini hakufanya hivyo , alitaka kumruhusu Edna kutuliza hasira zake hata kama ni kwa kumpiga lakini hakutegemea kofi lake lingekuwa na maumivu makali kiasi hicho kiasi cha kumfanya kuwa katika hali ya kizunguzungu licha ya kwamba alikuwa tayari kwenye levo ya Nafsi.
Kwa Edna ambaye alikuwa mwanzoni mwa levo ya mzunguko kamili asingeweza kuwa na nguvu za aina hio , lakini kwa Sophia aliona pengine ni kwasababu hakujizuia ni kama aliamua kumzimisha kabisa.
Sophia mara baada ya kuona amepigwa kibao cha aina hicho alishikwa na huzuni na kuona Edna hakuwa tena na zile hisia za undugu wa udada kati yao na hio ilimaanisha ni kwa kiasi gani amekasirika.
“Sister najua umekasirika ,, nipige kama ndio njia pekee ya kukufanya ujisikie vizuri”
“M*laya mkubwa wewe”Aliongea Edna kwasauti ya kusikika kabisa na Sophia hakutegemea Edna anaweza kuongea hivyo na moyo wake uliuma na alishindwa kuzuia machozi .
“Nadhani unaniona kama mjinga si ndio , nimetengeneza mpango wote wa wewe kurudi katika tasnia ya sanaa na kukutia moyo kufanya kazi kwa juhudi nikifikiria upo upande wangu lakini kumbe ulikuwa ukinionea hurma, Sophia maigizo yako ni ya hali ya juu sana , ulikuwa ujinga wangu kufikiria kwamba wewe huwezi kunisaliti , nilishawahi kuwaza na kujisemea wewe ni mwanamke mwaminifu na mpole kuliko wote ambao nishawahi kuwaona ,,, nilikuamini sana na nikafanya mambo makubwa kwa ajili yako kwa hiari yangu kabisa lakini mwisho wa siku ukaamua kumtega mume wangu kimapenzi kama wale wanawake wengine , hivi huna aibu hata kidogo , Dhamiri yako ipo wapi , hebu jiulize unautoa wapi ujasiri wa kuongea hayo maneno yasio na aibu mbele yangu , unaitafuta huruma yangu si ndio?”Aliongea Edna na Sophia alikuwa akilia kwa kwiki.
“Dada ,, sijawahi kuitaka huruma yako , najua nimekukosea na sina chaguo lingine zaidi ya kukuruhusu kunipiga na kunifokea ,,, nitakuacha unifanye chochote ili mtadi tu kukufanya ujijisikie vizuri”
“Unanijaribu ukidhania sitokufanya chochote”Baada ya kuongea hivyo palepale Edna alimchapa vibao vingine viwili kulia na kushoto tena kwa nguvu kiasi cha kumfanya Sophia kurudi nyuma kwa maumivu na aliishia kushika ukuta ili kujizuia asidondoke chini.
Ilikuwa bahati kwake alikuwa na mafunzo ya kijini kwani uvimbe na vidole mashavuni kwake viliweza kuponyeshwa kwa haraka, lakini Edna alionekana hakuwa na mpango wa kuishia hapo.
“Unajitia huruma ukidhani nitakuacha , kwahio hutaki kupigana na mimi , unafikiri nitaacha eh , sio kwamba nina mpango tu wa kukupiga na kuliacha lipite, Lazima nikuue leo mshenzi wewe”Aliongea na sauti yake ile ilimfanya Sophia kujua kuna kitu cha hatari kina kwenda kumtokea
Macho ya Edna yalikuwa ya mejaa ukatili wa hali ya juu mno , ni kama vile sio yeye na hali hio ilimuogofya.
Ilikuwa ni kama Edna ametawaliwa na pepo la giza na alimwangalia Sophia ka macho ambayo hayakuwa yale ya Edna anapokuwa na hasira bali macho hayo yalikuwa ni yale ya kimauji.
Sophia aijiuliza ilikuwa kweli mpango wa Edna kuja hapo kwa ajili ya kumuua.
Sophia hakuwa na muda wa kujiuliza maswali mara mbili mbili na alijiuliza imekuwaje Dada yake akabadilika ndani ya muda mfupi na kuwa hivyo.
Edna alikuwa ni kama wale wacheza Karate kwani palepale alimshambulia Sophia akilenga shingo yake eneo ambalo mtu yoyote akipigwa hawezi kupona na Sophia palepale alikwepa kwa ustadi.
Sophia mara baada ya kukwepa alipulizwa na upepo wa sauti namna ambavyo mkono huo uliweza kuikata hewa na alijua kabisa Edna ametumia nguvu zake zote kufanya shambulio la aina hio.
Lakini haikua mwisho, Edna alionekana kuwa mwepesi sana kwani baada ya shambulizi lake kukata hewa palepale alifyatuka na mguu wa kulia na kumpiga Sophia kifuani.
Teke lile lilikuwa na nguvu isiokuwa ya ajabu kwani Sophia alirushwa na kwenda kujipigiza kwenye ukuta huku akiishia kuugulia maumivu.
Halikuwa pigo la kuweza kumuumiza kivile kutokana na uwezo wake , lakini wakati akiugulia maumivu alisogelewa tena huku Edna akiwa ametanguliza ufunguo wa gari mbele akinuia kumtomboa macho Sophia.
Sophia alitumai uwezo wa kijini kukwepa mashambulizi ya Edna lakini pigo la kifuani ni kwamba alishindwa kulikwepa na alishangaa kuona kwamba ilikuwa ni kama alitegemea namna anavyokwepa. Alijiambia haikuwa kawaida hii.
Sophia palepale alijua asingeweza kupambana na Edna kwa njia za kawaida na palepale aliita nguvu ya kijini ili kujilinda.
Edna mara baada ya kumkaribia Sophia alikumbana na wimbi la nguvu ya kijini ambalo lilimrudisha nyuma na alionekana kukosa balansi na kwenda kujibwaga kwenye sakafu.
“Sister..!!”
Sophia alijua alishamuumiza Edna na pigo lile na kuanza kumkimbilia lakini ni kama alikuwa akitegwa kwani ile anakaribia Edna alifyatua mguu wake wa kushoto na kumfyeka Sophia kuanzia katika eneo la kwenye magoti akinuia kumpiga mtama na pigo lake lilionekana kufanya kazi kwani Sophia alishindwa kukwepa ndani ya muda na alijikuta akidondoka chini na kupigiza makalio chini.
“Umesema utaniacha nikupinge nitakavyo , ili nitulize hasira zangu , mbona sasa hivi unanizuia”Aliongea Edna huku akitoa tabasamu la uovu na muda huo alishamrukia Sophia ili kutompa nafasi nyingine ya kutumia nguvu zake za kijini na kumkaba shingoni huku kigoti cha miguu yake akiwa amekibana tumboni kwake kwa kulenga Meridian za mwili sehemu ambayo ndio senta ya kutawala nguvu za kijini mwilini.
Sophia aliishia kufurukuta tu huku machozi yakimtoka, Edna hakuwa na utani kabisa palepale aliinua ufunguo wa gari yake na kupelekea uswa wa Koromeo la Sophia akinuia kummaliza kabisa.

SEHEMU YA 636.
Kama sio Roma kuwahi kuingia ndani ya eneo hilo na kumsukumia Edna mbali basi pengine angemuua Sophia.
Roma mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi mno huku akijawa na hatia kumuona namna Sophia alivyokuwa katika hli ya mshituko.
Edna mara baada ya kusukumwa kwa nguvu alisimama palepale na kumpiga macho Roma na wote walijikuta wakiangaliana kama mabeberu.
Upande wa Roma alimwangalia Edna kwa macho yaliojaa utofauti wa kihisia , lakini upande wa Edna alikuwa na macho ya chuki, pengine macho ambayo hajawahi kumwangalia nayo Roma.
Ilikuwa ni bahati kwa Roma aliweza kukutana na Ummy mpaka kuja kutafuta na kufika hilo eneo ndani ya muda na kama sio hivyo pengine angemkuta Sophia akiwa mfu.
Roma alishindwa kabisa kumjua Edna kihisia, alikuwa ni kama mwanamke tofuati kabisa na anavyomjua , uhatari wake ,sumu yake iliomjaa , ukali wake na sura yake alikuwa akifanana kwa asilimia mia moja na mwanamke ambae kwenye maisha yake pengine asingeweza kumsahau.
“Edna umekuwa kichaa , ni kweli ulikuwa ukitaka kumuua Sophia?” Aliuliza Roma lakini ajabu Edna alianza kucheka huku akionyesha dharau za waziwazi.
“Kwani hukujionea mwenyewe , vipi kwani wewe mnyama? , ndio tuseme upo kwenye maumivu sasa hivi kumuona mpenzi wako mpya akitaka kufa mbele yako,, bado hajafa haina haja ya kuumia”
Roma mara baada ya kusikia maneno ya mnyama aliweza kukumbuka onyo la Edna kwamba akimgusa na Sophia basi atakuwa ni mnyama ,ilionekana mwanamke huyo hakuwa akisahau anachoongea.
Alijikuta palepale hasira zake zidi ya Edna zikishuka zenyewe na kugeuka kuwa hatia , alikuwa ni yeye ambaye amepelekea hayo yote kutokea.
Roma aliachana na Edna na kisha aliinama na kumsaidia Sophia kusimama na alijikuta akiumia kumuona namna ambavyo alikuwa kama amechanganyikiwa.
“Sophia na wewe umekuwa mwehu , ulipaswa kujilinda na nguvu za kijini hata kama hukuwa na mpango wa kushindanna nae”
“Si…”Alijikuta machozi mengi yakimtoka kiasi cha kutia huruma mbele ya Roma.
“Niliogopa nitamuumiza”Aliongea.
“Wewe unafiikiri huyu ni mwepesi kuumia ilihali katumia mbinu zangu za mafunzo , anaweza kuwa katika levo ya mwanzo mwa mzunguko kamili,
hivyo ngao yako ya kijini haiwezi hata kumsababishia mchubuko”
Sophia aliishia kuinamisha kichwa chake chini , uwezo wa kupigana alikuwa nao lakini alishindwa kushindana nae kwani alimuona ni dada yake.
Pengine katika hali kama hio ni mawazo ya kinafiki kufikiria kama Edna ni dada yake ilihali amemua kutoka kimapenzi na mume wake , lakini ile heshima ya udada aliokuwa nayo zidi ya Edna ndio iliomzuia kutoshindana na kumtaka ampige atakavyo huku akishindwa kuelewa Edna alikuwa siriasi akitaka kumuua.
“Edna usifanye hivi tena , haijalishi ni hasira kiasi gani unazo unapaswa kuzitolea kwangu , ni kweli Sophia anakuita dada lakini sio dada yako ,huoni sio halali kutolea hasira zako kwake?”
“Kwahio unamaanisha kwamba utafanya ngono na kila mwanamke ambaye hana undugu na mimi?” “Unajua kabisa sijamaanisha hivyo , najua nimekukosea na kukusaliti lakini si ndio wewe ambaye ulimsukumia Sophia kwangu?”
“Kwahio unanilaumu si ndio?”
“Nakuelezea ukweli , tokea siku ambayo ulijua Sophia sikuwa na mahusiano nae kama nilivyokuambia na ana hisia na mimiza kimapenzi ulichukua uamuzi gani , wewe ndio uliemruhusu mwenyewe kuishi na sisi na ukaenda mbali na kufungua kampuni kwa ajili yake na kunifanya mkurugenzi , ulijua ana hisia za kimapenzi na mimi lakini hukuwahi kumchukulia siriasi. Mimi naona wewe ndio umetufunga tuwe pamoja , au ndio ulikuwa ukinijaribu ,ulikuwa ukipima uwezo wa Sophia kujizuia , nilimkataa mara kibao kwa ajili yako na nikamuumiza lakini yeye yupo siriasi na hisia zake na siwezi kumuacha aendelee kuteseka , huna haja ya kumuamulia nani wa kumpenda kwasababu sio mdogo wako , ukiachana na kunipenda hakuna kitu kingine ambacho amekufanyia ni kibaya , lakini wewe unataka kumuua , mbona hujafanya hivyo kwa wengine , amekuruhusu umpige utakavyo haikumaanisha kwamba hakuwa na uwezo wa kujilinda ,ana mafunzo ya Kung Fu huyu na ana uwezo wa nguvu za kijini mkubwa kulikowa kwako , kwanini unakuwa mkatili kwake?”
“Kwahio unamaanisha napaswa kumshukuru kwa kuvumilia kwa ajili yangu , hebu nyooka ueleweke sitaki maneno mengi”
“Namaanisha hupaswi kumshukuru lakini vilevile hupaswi kumchukia , kama unataka nichome kisu moyoni nife mimi lakini yeye usimuumize”
“Haha.. nikuchome na kisu wewe , unaniona mimi mjinga , nikishakuchoma na hicho kisu si utakichomoa na kupona hapo hapo , naamini naweza hata kuutoa moyo wako na kuutupa na ukautufauta na kuuweka na ukaendelea kufanya kazi”Aliongea kwa macho ya kejeli na kisha alichukua funguo zake na kumpita Roma kuelekea mlangoni.
“Unaenda wapi?”
“Haikuhusu”
“Nifuatae twende nyumbani”Aliongea Roma akijaribu kumzuia asipite. Mlangoni lakini macho ya Edna yalibadilika palepale na alikunja ngumi yake na kumrushia Roma akinuia kumpiga tumboni lakini Roma alikuwa mwepesi kukwepa.
Roma alikuwa mwepesi kwani licha ya kukosa uwezo wake alikuwa na mafunzo ya hali ya juu ya zaidi ya miaka sita hivyo ilikuwa ngumu kumgusa kwa shambulizi kama hilo , lakini sasa Roma baada ya kukwepa alitaka kumshika mkono ili kumzuia lakini Edna alimpiga Roma teke la mzunguko na kumsukumia mbali na mlango na Edna hakuishia hapo tu.
Roma mara baada ya kuinama kuugulia maumivu ya teke lile Edna alileta lingine usawa wa kiuno lakini Roma alikuwa ameliona na alijikuta akipigwa na mshituko na kuishia kulikwepa huku akitaka kumshika Edna mabega lakini ni kama alitarajiwa angefanya hivyo kwani Edna alimkwepa na kurudi nyuma.
“Mashambulizi yako ni makali mno na ya haraka , kama ungekuwa kwenye uwanja wa vita ungekuwa na uwezo wa kuua kila mtu na shambulizi moja kutokana na maeneo unayolenga , sio mashambulizi yaliozidi bali ni ya kimahesabu ambayo yameunganika katika mtindo kamilifu, huwezi kufikia levo ya aina hii kwa mazoezi yako ya muda mfupi ulioyafanya , ndio maana haishangazi ulifanikiwa kumzidi Sophia”Aliongea Roma akitafsiri mashambulizi ya Edna.
Roma sasa aliweza kuelewa hali ilivyokuwa lakini hali ya wasiwasi iliweza kukijaza kichwa chake huku akikunja ndita.
“Edna nani kakufundisha mapigano?”
“Nimesema hayakuhusu”Aliongea na palepale Sophia alikuwa amesogea karibu yake na kabla hata hajaelewa nini kinachotokea alipokea shambulizi lingine la kiwiko cha mkono ambacho kilimrudisha nyuma kwa kasi ya ajabu
Kwasababu hakuwa ametegemea hilo alijikuta akikosa balansi na kudondoka kama furushi na kujjigonga kwenye meza na kudondokea kwenye kapeti.
Kitafsiri ni kwamba pigo hilo lilikuwa ni la kihisia zaidi , Sophia alikuwa nyuma ya Edna akitaka kumuomba msamaha wakati huo Edna alikuwa ameangaliana na Roma lakini Edna alijua Sophia yupo umbali gani kutoka kwake na kuachia pigo la ajabu namna hio.
“Edna umekuwa kichaa?”
Roma alijikuta akitetemeka na alitaka kumpiga Edna kibao lakini mkono uliishia hewani huku akianza kutetemeka , alishindwa kabisa kumpiga.
Angewezaje kumpiga mwanamke anaempenda kwa kiasi kikubwa , Edna alimwangalia kwa jicho la dharau na kisha alisogelea mlango na kutoka.
Awamu hii Roma hakuwa na uwezo wa kumzuia tena na alimuacha aondoke huku akijaribu kutuliza akili yake na hasira zake kabla ya kumsogelea Sophia.
Sophia upande wake alijitahidi kusimama huku akishika kiuno chake kilichokuwa na maumivu akikwepa Roma kumshika.
“Niko sawa”
“Sophia ni…”Roma hakujua hata ni kipi aongee katika hali kama hio na aliishia katikati.
“Nipo sawa ninachopaswa ni kujipaka makeup tu kwa ajili ya kufanya show, Roma nenda sasa kabla mtu hajaingia hapa”
“Show tena … Sophia wewe ni mpole au ni mjinga?”
“Mimi sio mjinga ,najua ana hasira sana lakini pia nina uhakika hakuwa akitaka kuniua .. nitafanya kazi kwa bidii ili uwekezaji wake usiende bure ,, huwezi jua pengine akipata hela za kutosha kupitia mimi anaweza kuwa na furaha , siwezi kumuomba msamaha wowote , hivyo ndio kitu pekee ambacho naweza kufanya kwa ajli yake”
Roma alijikuta akishika kiuno huku akivuta pumzi nyingi na kuzishusha, akili yake wakati huo ilikuwa imejaa maswali kibao pamoja na wasiwasi.
Katika mapambano bila ya kutumia mbinu zozote za kijini Roma alikuwa akijiamini mno na kujiita Master wa mbinu, lakini kitendo cha kupigana kwa muda mfupi na Edna mashambulizi yake ni ya kiwango cha juu mno na mbaya zaidi hakuwa akipambana kujilinda alikuwa akipambana kuua ,ilikuwa ni afadhali ru kwamba alikuwa hana siraha ya aina yoyote la sivyo ingekuwa ni habari nyingne.
Edna kufikia uwezo huo haikumhitaji mazoezi tu ya kimwili bali kulihitajika kipaji na uzoefu wa kimafunzo , katika dunia ya leo Roma alikuwa akijua watu wa mapigano ya mbinu hio walikuwa ni wachache sana akiwemo Noriko Okawa Master wa kundi laYamata Sect aliemuua na yeye mwenyewe.
Roma alijiuliza kuna mangapi Edna alikuwa akimficha au kuna kitu kingine kisicho cha kawaida ambacho hakijui.
Bila ya kujali ukweli Roma sasa anaamini kwamba Edna ndio muhusika ambaye ameua wale wanajeshi mara baada ya yeye na Lanlan kutekwa , kwa uwezo ambao ameonyesha aliona kabisa isingekuwa tatizo kwa Edna kupambana na watu kumi wenye siraha.
Baada ya Roma kumwambia Sophia ajilinde mwenyewe , aliamua kuondoka kumtafuta Edna akihofia anaweza kufanya jambo lingine la kijinga.

SEHEMU YA 637.
Roma wakati akitoka nje kabisa ya geti la hoteli hio Edna ndio kwanza alikuwa akitokomea barabarani akichukua uelekeo wa kurudi nyumbani.
Roma hakujiuliza mara mbilimbili na aliingia kwenye gari yake na kuanza kumfatilia kwa nyuma , awamu hio umbali kati yao ulikuwa mkubwa sana na hakuwa na uhakika kama anaweza kumpita.
Dakika chache mara baada ya kutoka eneo la mjini Roma aliweza kuwa na uhakika Edna alikuwa akielekea nyumbani , lakini kwa wakati mmoja hakujua kama alikuwa na mpango gani maana kwa alvyokuwa na hasira hakuwa na uhakika kama swala hilo linaweza kuisha kwa kumbembeleza.
Baada ya gari kusimama nje ya geti , Edna hakujisumbua hata kuliingiza ndani na alishuka na kisha akachoma moja kwa moja mpaka ndani akiwa na uso uliojaa usiriasi.
Walinzi waliishia kumpisha kwa tahadhari kwani alionekana kutokuwa wa kawaida ,ijapokuwa alikuwa mrembo wa sura lakini ule msisimko aliokuwa akisambaza haukua wa kawaida kabisa.
Ilikuwa ni usiku na familia yote ilikuwa mezani kwa ajili ya chakula cha usiku wakiongozwa na Afande Kweka mwenyewe na hawakuwa na haja ya kuwasubiri tena kwani hawakuwa na uhakika kama maswala yao yanaweza kutulia.
Bibi yake na Sophia hakuwepo tena ilionekana alikwisha kuondoka katika hilo eneo , lakini hata kama alitaka kubaki uwezekano wa kukaribishwa ungekuwa mdogo kutokana na hali ya hewa alioichafua.
Edna mara baada ya kuingia eneo la sebuleni kila mmoja alishituka na walishikwa na wasiwasi kutokana na ukauzu wake kama vile ni Jemadari anaejiandaa kumwangamiza adui.
Edna macho yake yalikuwa kwa Lanlan tu ambaye alikuwa amekalishwa juu ya kiti miguu ikining’inia akijiandaa kuanza kula .
Alikuwa na furaha ya kuona chakula licha ya kwamba wazazi wake hawakuowepo , hamu yake ya kula haikuathirika hata kidogo lakini mara baada ya kumuona mama yake alitoa tabasamu.
“Mama amerudi , Mama njoo ule chakula”
Edna mara baada ya kusikia sauti ya Lanlan muonekano wake ulibadilika kutoka katika hali ya ukauzu na kuwa katika hali ya kimaamuzi.
Na bila kujali wanafamilia waliokuwa wakimwangalia alimsogelea Lanlan na kumbeba juu juu.
“Eh! Edna unafanya nini?”
“Nini kinaendelea , Roma yupo wapi?”
Waliuliza wanafamilia wote waliokuwa wakijiandaa kupata chakula cha usiku lakini Edna hakujali mshangao na kuchanganyikiwa kwao.
Lanlan aliekuwa amebebwa juu juu aliangalia chakula kilichokuwa kwenye meza kwa macho ya huruma.
“Simama hapo hapo”
Roma aliekuwa anakuja kwa kukimbia mara baada ya kuingia tu alimzuia Edna kwa sauti ya kufoka na alijua kumbe kuja nyumbani mpango wake ni kucmchukua Lanlan.
“Wapi unampeleka?”Aliuliza Roma kwa sauti ya chini.
“Tunakuacha”Aliongea Edna kwa sauti kavu.
“Huna haki hio”Aliongea Roma huku akikunja ngumi yake.
“Hustahili kuwa mume wangu wala kuwa baba wa binti yangu , nina mchukua kwa ajili ya kumuweka mbali na wewe”
Roma aliona huu ni ujinga , anasemaje hana haki ya kuwa baba wa Lanlan ilihali yeye ndio amemzaa na Seventeen.
Roma hakuwa na mpango wa kutangazia familia kama Lanlan ni mtoto wake , lakini pia hakuwa tayari kumuona Lanlan akiiishi mbali na yeye tena, hivyo alibakiwa na chaguo moja tu kumwambbia Edna ukweli.
Alijiambia anaweza kukubali hasira zake na laana zake pamoja na kudharauliwa lakini sio kuruhusu mtu yoyote kumchukua mtoto wake hata kama ni Edna.
“Nyie wawili mnafanya nini ?Kwahio mnapanga kupena talaka na giza lote hili mbele yangu?”Aliuliza Afande Kweka kwa sauti ya juu ya mikwaruzo akishindwa kuvumilia.
“Roma, nini kimetokea ,kwanini hali imefikia hivi?”Aliuliza Blandina kwa wasiwasi akiogpa hasira za Afande Kweka.
“Alitaka kumuua Sophia na nikamzuia”Aliongea Roma mara baada ya kuvuta pumzi na kuzito.
“Nini!!!?’
Kila mtu alishangazwa na kuali ya Roma kwani ni kama vile hawajamsikia vizuri na kuishia kutoa midomo.
“Nipishe huko , ninaondoka na Lanlan”
“Nimesema huwezi , Lanlan ni binti yangu , hata kama unataka kuondoka ondoka peke yako na huwezi kuondoka nae”
“Mimi ndio niliefanya maamuzi ya kumuasili na nitakuwa mimi ninaeondoka nae , huna haki ya kumchukua kutoka kwangu”Baada ya kuongea hivyo alimpita.
Lanlan masikini aliishia kutoa kilio cha kwikwi akishindwa kuelewa ugomvi huo wa wazazi wake , kwani mpaka hapo alishajua wanaachana.
“Lanlan ni binti yangu wa kumzaa!!”Roma alishindwa kujizuia kabisa mara baada ya kuona Edna anakaribia mlango kutoka.
Ilikuwa ni kama kumetokea tetemeko la Ardhi huku kauli yake ikizuia muda kutokuendelea.
Edna ambaye alikuwa ndio anataka kutoka alijikuta akiganda huku akiwa amempatia Roma mgongo.
Afande Kweka ndio wa kwanza kutoka kwenye mshangao , ukweli ni kwamba mzee huyo hakuwa kwenye mshangao bali alikuwa kwenye maigizo ya mshangao maana alikuwa akijua kila kitu lakini hakutegemea jambo hilo lingekuja kujulikana katika mazingira ya ugomvi.
“Wewe mtukutu umesema nini… Lanlan ni mtoto wako wa kumzaa?”Aliuliza na Roma aliishia kutingisha kichwa huku ni kama mzigo uliokuwa umemlemea kifuani kwake ukishuka na kumpa ahueni ya kupumua.
“Ndio Lanlan amezaliwa na mwanamke ambaye nilikutana nae nje ya nchi , jina lake anaitwa Seventeen , alipoteza maisha mara baada tu ya kumzaa Lanlan na babu yake Lanlan ambaye alikuwa ni mwalimu wangu ,Master Tang Chi ndio ambaye alimlea.. kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake hakuweza kumleta Lanlan kwangu mapema kama alivyoagizwa na Seventeen, nilivyopotea niliweza kukutana nae kwa bahati mbaya na akaniambia ukwel..”
Yalikuwa maneno machache lakini ujumbe wake ulikuwa mwingi sana kuusharabu wote kwa dakika moja , mwili wa Edna kwa wakati huo ulikuwa ukitetemeka.
“Unaongea upuuzi, una ushahidi gani?”Aliongea Edna huku machozi yakianza kuloanisha macho yake
Roma kwa wakati huo hakuwa na huruma tena kwani alishaamua kuweka ukweli wote wazi , alijiambia kwasasa anapaswa kujifikiria yeye na mtoto wake kwanza.
Baada ya kujitahidi kudhibiti maumivu yaliokuwa kwenye moyo wake , Roma aliingia upande wa Email katika simu yake na kisha kutafuta picha za barua alizozichukua kwa Qiang Xi , barua ambayo iliandikwa na Master Chi na baada ya hapo alitoa Ushanga wa kibudha na kumuonyesha Lanlan.
“Grandpa’s Beads”Aliongea Lanlan kwa sauti ya mshangao huku macho yake yakichanua akimaanisha kwamba ushanga huo ni wa babu yake.
Edna tumaini lake la mwisho ambalo alikuwa nalo ni kama limebomoka, alikuwa kama mtu ambaye amejenga ukuta wa bwawa la maji kwa kutumia saruji ambayo haina ubora na sasa maji yamebomoa na kuanza kukauka.
“Hii barua imepigwa picha na Qiang Xi baada ya kupoteza ya karatasi na ina majibu yote kwani ni Master Chi ambaye ameaindika na kumkabidhi
Qiang kwaajili ya kunipatia baada ya siku ishirini na tisa kupita, lakini hakufanya hivyo kwani aliogopa ukweli unaweza kuharibu familia yangu, kwasasa siwezi kujizuia zaidi kwasababu unajaribu kunipokonya binti yangu , nisamehe kwa kukuumiza kwa mara hii nyingine lakini siwezi kuuficha huu ukweli , ninapaswa kufanya hivi kwa ajili ya Lanlan”
Roma aliweka simu iliokuwa na picha katika mikono ya Edna,iliokuwa na picha ya barua na kisha akamchukua Lanlan.
Edna hakusita kusoma kilichokuwa kikionekana , ilikuwa ni barua ilioandikwa kwa kingereza lakini alielewa na kadri alivyokuwa akisoma machozi yalizidi kumtoka na kugonga kwenye kioo cha simu na alishindwa kumaliza na palepale simu aliomnunulia Roma kama zawadi ilidondoka kwenye tailizi na kutengeneza ufa.
Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kukurupuka kutoka kwenye kiti na kwenda kuichukua ile simu na kuangalia yaliyomo na kadiri na yeye alivyokuwa akisoma ndio wasiwasi na hatia ilivyoanza kumjaa.
“Roma unasema kweli Lanlan … , Namaanisha
Lanlan kumbe wewe ni mjukuu wangu kabisa, Roma nataka kusikia kwako mwenyewe kwa mara nyingine hebu rudia”Aliongea Blandina huku mikono ikimtoka jasho na aliishia kumshika Roma mkono na Lanlan kwa wakati mmoja.
Upande wa Afande Kweka aliishia kuegamia kiti chake kivivu akiangalia kinacheondelea kwa hamu zote lakini kwa wakati mmoja akimuonea huruma Edna.
“Mmeona wenyewe , Lanlan ameweza kuujua ushanga huu lakini pia Qiang Xi anaujua ukweli wote , Seventeen pia alituma Lanlan kuja kwangu kwa kuweka uthibitisho wa kisu kilichovunjika na zaidi ya yote Lanlan kazaliwa tofauti na watoto wa kawaida kama mwili wangu ulivyo, mnadhani hii inatokea kwa bahati mbaya , siku zote nilikuwa nikihisi muunganiko na Lanlan nadhani yote haya ni kufanana kwetu kwa damu”Aliongea Roma kwa kirefu.
“Lanlan babu yako amesema huu ushanga wa kibudha ni kwa ajili yako , ameenda sehemu ya mbali kucheza na rafiki yake na itachukua muda mrefu mpaka kurudi , lakini usijali kwa sababu mimi baba yako nipo hapa, utakula kila chakula kitamu utakacho kipenda na hakuna mtu wa kumchokoza binti yangu tena”
Lanlan alikuwa ni jiniasi na alishaaelewa maneno ya Roma na aliishia kugeuza kichwa chake na kumangalia mama yake kwa huruma.
“But daddy isn’t mommy Lanlan’s too?”Aliuliza akisema lakini baba si hata mama ni mama wa Lanlan.
“No , I’ m not your monny , your mother’s name is Seventeen and she is dead , From now on . I won’t have anything to do with you two anymore”
“Hapana mimi sio mama yako , mama yako anaitwa Seventeen na ameshafariki, na kuanzia leo sitohusika na chochote kwenu nyie wawili tena”
Edna aliongea manenno yake kwa sauti ya kusikika kwa kila mmoja na kisha aligeuza na kutoka nje kimya kimya.
Afande Kweka anahadithia na kusema kivuli cha
Edna kilikuwa ni kile cha mtu ambaye ametelekezwa na aliekosa tumaini lakini kwa wakati mmoja kilikuwa ni kivuli kilichojaa ujeuri ndani yake.
Unadhani huo ndio mwisho wa Edna na Roma , usikose yajayo.

Sent from my 23021RAAEG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom