Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Best sorry of all the time
 
[emoji482][emoji15]
 
[emoji482][emoji1635][emoji120]
 
SEHEMU YA 651.
Roma alimlaani Mzee Kweka kwa kupenda kumuweka hewani na palepale alirusha simu yake pembeni.
Roma mara baada ya kupiga mswaki na kujiweka sawa , alikumbuka Hazina ambayo aliiba huko Kilimanjaro na palepale alichukua lile boksi na kuangalia kilichopo ndani.
Roma alishangaa , kilikuwa ni kitu cheusi kilichokuwa kimewekwa ndani kinacholingana na kokoto lakini yenye muonekano wa kuvutia kidogo.
“Hiki ni kitu gani?”Roma alijiuliza huku akijiambia pengine ni Dhana ya kijini na hakuweza kuhisi nguvu yake kwasababu hakuwa na uwezo wa kutumia nguvu za kijini.
Lakini bado ilimfanya Roma kutodhania ni kitu cha kawaida mpaka kuitwa Hazina kutokana na muonekano wake, maana kitu hicho kilikuwa kama vile ni ishara ya kitu flani lakini hakuweza kujua ni kitu gani.
Roma hakutaka kufikiria sana , alirudisha kama ilivyokuwa hazina hio ambayo hakujua maana yake na kisha akapotezea swala hilo kwa muda.
Baada ya kushuka chini aliweza kumuona Lanlan akiwa tayari ashaanza kunywa chai kwa kushikilia chapati za maji huku Qiang akiwa anamsaidia kumnywesha maziwa.
Kwa jinsi mashavu yake yalivyotuna ilikuwa ngumu kuamini kama alikuwa akimeza vizuri kile ambacho anakula.
Roma pia alishagazwa na uwepo wa Amina na Rufi waliokuwa wamekaa eneo la sebuleni wakiangalia runinga.
“Nyie mnafanya nini hapa asubuhi yote hii?”Aliuliza Roma huku akifinya mashavu yao.
“Ushasahau nimemuahidi Lanlan kumpeleka kucheza , napaswa kutimiza hadi yangu kwani leo ndio nipo free”Roma alimwangalia Lanlan na kuona alikuwa akimwangalia kwa namna ya kumwambia asikatae.
“Hubby , unaonaje tukienda pamoja , tukiwa wengi ndio itakuwa vizuri zaidi”Aliongea Rufi.
“Lazima niende pia , vipenzi vyangu nyie mnaenda pamoja na binti yangu lazima niwasindikize kama bodigadi , wote nyie ni warembo hivyo nina wasiwasi mtaibiwa”
“Unapaswa kuwa na wasiwasi labda na sisi tu lakini sio Lanlan , itakuwa vizuri kama wavulana wa huko hawatamuogopa Lanlan”Aliongea Nasra.
“Nasra wewe hujui tu , lakini Lanlan akishakuwa mkubwa atakuwa mrembo haswa , naamini majitu isiokuwa na adabu itamsumbua sana ili kumharibu mapema iwezekanvyo”Aliongea na kumfanya wote wamwangalie namna ambavyo amekosa aibu.
Baada ya Roma kupata kifungua kinywa aliingia kwenye gari ya Amina na kuendesha kuelekea Kawe eneo maalumu ambalo limekuwa maarufu kwa ajili ya michezo ya watoto.
Baada ya kufika watoto walikuwa wengi mno maana ilikuwa ni kipindi cha likizo ya mwisho wa mwaka.
Lilikuwa ni eneo lenye hali ya hewa nzuri kutokana na kuwa ufukweni na Roma alipata muda mzuri wa Kurelax maana tokea arudi ni mwendo wa hekaheka.
Baada ya Lanlan kucheza kwa muda mrefu ilikuwa ishatimia saa saba mchana na alirudi na kumwambia baba yake njaa inamuuma na Roma aliwachukua na kisha wakasogea upande mwingine eneo hilohilo sehemu yenye mgahawa wa kisasa na kisha walikaa na kuagiza chakula.
Wakati wakiendelea kula Lanlan aliacha kula na kuangalia upande wa nje huku akionekana kama kuna kitu amekiona na kukitamani, ilimfanya na Roma kuangalia upande wa nje na kugundua pembeni yao kuna mtu aliekuwa akichoma mishikaki.
Rufi aliweza kugundua alichokuwa akihitaji Lanlan na palepale alisimama na kuchukua pochi lake.
“Mnaweza kuendelea kula nitaenda kununua kwa ajili ya Lanlan”
Lanlan mara baada ya kusikia kauli ya Rufi aliinua kijiko chake kwa furaha zote na Roma aliishia kutabasamu na kufuta punje za pilau zilizokuwa zimemgandia pembeni.
Ni mara baada ya Rufi kumaliza kupewa mzigo wake wa mishikaki sasa wakati akijiandaa kulipia palepale alisikia sauti pembeni yake.
“I want those two”
Sauti ya kike pembeni yake iliweza kusikika , ijapokuwa mtu alieongea hio kauli alitumia kingereza lakini kidogo tu Rufi adondoshe mishikaki kwenye mchanga lakini alijizuia, hata hiyo alikuwa amechelwa kwani pochi lake lilimponyoka na kudondoka chini kutokana na kutetemeka.
Haraka haraka aliinama na kuchukua pochi lake na kumpatia muuza mishikajji hela yake na kutaka kuondoka bila ya kugeuza sura yake.
“Subiri”
Sauti ya kike ambayo iliagiza mshikaki ilimzuia kuondoka na yule mwanamke palepale alikimbia na kwenda kusimama mbele ya Rufi ambaye hakugeuka.
“Hey! Ni wewe kweli.. Aaa..Shemeji!!!”Aliongea yule msichana huku akionyesha hali ya kuwa furaha na mshangao kwa wakati mmoja.
“Miss utakuwa umenifananisha”Aliongea Rufi huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Shemeji kwanini unajifanya hunijui , ni mimi Xiao Xiao , tulikutana wakati ulipochumbiwa na kaka yangu”Aliongea huku akiinamisha kichwa chake kutaka kumwangalia Rufi ambaye alikuwa na mabadiliko.
“Hapana sio mimi umennifananisha” Rufi alionekana kutetemeka mno.
Ukweli alilaani sana katika hali kama hio , hakujua imekuwaje akakutana na Xiao Xiao msichana ambaye alikuwa akimjua fika kwani alikutana nae katika ulimwengu wa kijini kabla ya kutoroka.
*******
Nje ya hoteli ya Serena alionekana Suzzane akishuka kwenye gari aina ya Audi ya rangi nyekundu na kisha kumpatia Valet ufunguo baada ya kutoa pochi yake.
Baada ya kuweka mkoba wake kwenye kwapa palepale alianza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo la hoteli huku akigeuka nyuma akiangalia kama kuna mtu anamwangalia.
Suzzane alikuwa amebadilisha mtindo wa nywele , siku hio alikuwa amevalia Wigi na kumfanya kuonekana mtu mwingine kabisa.
Baada ya kuingia eneo la mapokezi na kupokelewa na mwanadada aliepamba uso wake kwa tabasamu palepale aliongea kidogo na mwanadada yule alichukua simu yake na alionekana alikuwa akiongea na ndani ya dakika chache alitabasamu na kisha akampa ishara Suzzane ya kuendelea kutembea.
Suzzane mara baada ya kuingia kwenye Lift alivuta pumzi kwa kutuliza presha yake na kisha alibonyeza kitufe kuruhusu Lift hio kumpeleka katika Floor husika.
Alijiangalia mavazi yake kwa kujichunguza na kuona yupo vizuri na na amependeza , kwa jinsi ambavyo alikuwa na wasiwasi ni kama mwanamke ambaye anaenda kukutana na mpenzi wake kwa mara ya kwanza.
Baada ya Lift kupandisha na kufika floor ya tatu , ilisimama na kufunguka na alionekana mwanaume alievalia suti na miwani nyeusi.
Suzzane alimpiga mwanaume huyo jicho la pembeni kumchunguza lakini hakuonyesha hofu na yule mwanaume hakuonyesha kumjali Suzzane kwani aliingia kwenye lift na kisha kutulia bila ya kubonyeza kitufe chochote.
Suzzane hakuwa mshamba , alijua pengine mwanaume huyo alikuwa akielekea Floor sawa ndio maana hakugusa vitufe lakini hakuacha kuwa na wasiwasi.
Baada ya Lfit kufunguka katika Floor namba sita wote kwa pamoja walitoka na mwanaume yule alichukua upande wa kushoto na Suzzane alichukua upande wa kulia.
Suzzane alijikuta akipatwa na ahueni na kisha alitembea kwenye Korido yenye msururu wa vyumba na ndani ya dakika chache tu aliweza kufika katika mlango wenye namba 123 na aligonga mara moja na dakika hio hio mlango ulifunguliwa na kisha akaingia.
“Shosti unaonekana kuwa na presha juu juu”Sauti nyororo ilisikika ikiongea na kumfanya Suzzane kuhema kwa nguvu kwa hali ya ahueni.
“Sijui nakua paranoid au nini lakini niseme hata nikienda chooni tu nakuwa na wasiwasi”Aliongea Suzzane huku akilazimisha tabasamu na kujaribu kuangalia mazingira.
Nadia alitoa tabasamu na kisha alimsogelea Suzzane na kumpa ishara ya kutaka kumkumbatia na Suzzane hakuwa na hiyana ya kukataa kumbatio.
“Unafanya vizuri Suzzane , ukishazoea kila kitu utaona ni kawaida”Aliongea na Suzzane lile kumbatiao kidogo lilionekana kuwa dawa kwake kwani aliweza kutulia.
“Unaonekana kuwa mzoefu Nadia , ulishawahi kufanya kazi ya hatari kama hii?”Aliuliza Suzzane na kumfanya Nadia kutoa tabasamu.
“Nishawahi kufanya kazi ya hatari mara tatu ya hii, mwanzo wakati napewa misheni ya kufanya nilikuwa kama wewe tu ndio maana nimesema unafanya vizuri”Aliongea na kisha Suzzane alimimina maji kwenye glasi na kisha akampatia Suzzane huku akimwambia akae.
Suzzane baada ya kunywa maji yale alijihisi angalau ameweza kupoa.
“Presha ilipanda zaidi mara baada ya kukutana na mtu kwenye Lift , alikuwa amekaa kama mwanausalama, aliniogopesha mno , nikajua ni watu wa Raisi Senga”
“Oh .,.. huyo atakuwa ni mwanasalama kweli , hakika unafanya kazi nzuri Suzzane , lakini hupaswi kuwa na wasiwasi , kuna raisi kachukua makzi ndani ya hii hoteli”
“Raisi!!!”
“Ndio , ni taarifa za siri sana za kiusalama , nimejua hayo kutokana na kwamba nimekutana nae kwa ajili ya mazungumzo, kwasasa sitokuambia ni raisi wa taifa gani”Aliongea Nadia huku akitoa tabasamu.
Na kisha alisimama na kwenda kutoa mvinyo kwenye jokofu na ksha akafika nao na kuuweka mezani na kuanza kujimiminia.
“Hongera Suzzane kwa mara nyingine, kila kitu kimeenda kama tulivyopanga”Aliongea Nadia na huku akimpatia Suzzane glasi ya mvinyo na mara baada ya Suzzane kupokea alimpa ishara ya kugongesheana Cheers.
Baada ya Suzzane kunywa ile Wine kidogo alijikuta akitoa macho kutokana na utamu wake.
“Vipi umeipenda?”
“Ina radha tamu kweli?”
“Yeah hii ni Chateu Margaux, nilipanga kushare hii zawadi na wewe siku ya leo”Aliongea na kumfanya Suzzane kutabasamu na kuangalia chupa ya Wine hio.
Hakuwa mshamba alijua huo ni mvinyo wa bei ghali sana , pengine kama angetaka kuununua basi angefilisika.
Waliongea kwa dakika kadhaa huku wakionyesha kucheka na kufurahi kwa pamoja kama marafiki na kumfanya Suzzane kupotezea hofu yake.
“Kila kitu kimeenda kama tulivyopanga Suzzane, unajisiije mara baada ya kufikia hatua hii?”
“Wakati naanza kufanyia kazi huu mpango sikuwahi kudhania kama ungefanya kazi, yaani hapa hisia zangu siwezi kuzielezea”
“Suzzane kila kitu ndani ya dunia hii kinawezekana ukiwa una taarifa sahihi”Aliongea.
“Ilikuwaje mkaweza kuja na huu mpango?”
“Ni maswala ya kisaikolojia Suzzane , kama ungekuwa na mafunzo ya kijasusi basi ungejua mambo mengi yanawezekana sana kwa kusoma saikolojia ya mtu na tabia zake, tulichofanya ni kufaitlia maisha ya Salihi ya kila siku ili kujua tabia zake, we did it randomly at first without any plan lakini mara baada ya Asha kuingia kwenye Equation tuliweza kufinilize kila kitu na here we are”Aliongea .
“Unajua mpaka sasa kuna baadhi ya vitu nashindwa kuelewa , Salihi kutoka kimapenzi na mama yake wa kambo ni swala ambalo nashindwa kuliprocess kabisa”Aliongea Suzzane na kumfanya Nadia kutoa kicheko.
“Hii dunia Suzzane ina mambo mengi na huwezi kuyajua yote , laiti ungejua hata nusu robo tu basi maisha yako yangebadilika kabisa, anyway tunapaswa kuachana na hayo , leo nataka kukuambia kwamba kesho ndio siku yako ya mwisho ya misheni yako”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha kesho ndio siku ya kumshawishi Raisi Senga kujiunga na Umoja wa Ant- Illuminat , lazima iwe kesho Suzzane kabla hajalazimishwa kusaini mkataba wa kishenzi”
“Sijakuelewa swala hili linahusiana nini na Mkataba wa kishenzi?”
“Suzzane we are Ant – lluminat, ikimaanisha kwamba tunaenda kinyume na namna dunia inavyoendeshwa , hiki ndio tunachopambana nacho, kuna kitu kikubwa sana kimepangwa kukamilishwa hapa Tanzania na mimi misheni yangu ni kukizuia kwa namna yoyote lakini kabla hilo halijatokea wewe unapaswa pia kukamilisha misheni yako, kumbuka ulichoambiwa kule Qatar”Aliongea na kumfanya Suzzane kumwangalia Nadia kwa macho ya kuuliza.s
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 652.
Rufi licha ya kwamba alijuwa uwepo wa Xiao Xiao ndani ya jiji la Dar lakini bado hakuamini kama angeweza kukutana nae katika eneo kama hilo la Kawe Beach.
Upande wa Xiao Xiao ukweli ni kwamba haikuwa mara ya kwanza kumuona Rufi, mara ya kwanza alivyomuona hakuamini kama anaweza kuwa Rufi lakini siku hio mara baada ya kumuona kwa mara nyingine hakutaka kudharau hisia zake na aliweza kuthibitisha ni yeye kweli.
Ilimshangaza kumuona Rufi nchini Tanzania mara baada ya miaka mingi ya kutoroka kutoka katika ulimwengu wa kijini.
Rufi licha ya kukamatika hakutaka kabisa kuongea na Xiao na palepale alikimbia kurudi ndani ya mgahawa na Xiao Xiao na yeye alimkimbilia kumfuata.
Roma mara baada ya kumuona msichana huyo wa kichina alikumbuka alivyokutaka nae mara ya mwisho mpaka kuja maeneo hayo hayo na kuachana .
Alikumbuka namna mrembo huyo alivyokuwa akimsumbua kwa kumtumia jumbe za meseji za kumtaka kimapenzi ambazo alidharau na kutomjibu mpaka akajikatia tamaa.
“Nini kinaendelea , kwanini Rufi anakimbiiana na yule mdada?”Aliuliza Amina ambaye alikuwa kwenye mshangao kama Roma .
Muda huo huo kabla Roma hajajibu Rufi alishawafikia na Roma alisimama mbele ya Rufi akimkinga na Xiao Xiao.
Mrembo yule wa kichina mara baada ya kumuona Roma alijikuta akijawa na mshangao kwani ni kama hakutegemea kumuona katika maeneo hayo.
“Hata wewe pia upo hapa , aisee kweli kilichopangwa hakikwepeki nadhani imepangwa tuoanane kwa mara nyingine”Aliongea Xiao Xiao akimwangalia Roma kwa furaha.
“Ndio nipo hapa pia , lakini kwanini unamfukuza Rufi?”
“Rufi!!?Oh.. nafahamiana nae ni shemeji yangu kwa kaka yangu”
“Huyo kaka yako ndio anaefahamika kwa jina la Xiao Hang?”Aliuliza Roma na kumfanya Xiao kutoa macho.
“Umejuaje jina la kaka yangu , au Rufi kakuambia kila kitu?”Aliuliza huku akiwa na mshangao , ingekuwa ngumu kwa Roma kujua jina la kaka yake kwani alikuwa akiishi huko katika jamii ya majini.
Roma hakujibu swali lake na palepale alimshika mkono yule mchina na kisha alianza kumvuta kumtoa nje ya mgahawa huo na ndani ya dakika chache tu walionekana wakiingia upande wa kushoto kwenye vyoo na mabafu ya kubadilishia nguo kwa watu wanaoenda kuogelea.
Amina yeye alikuwa kwenye mshangao kuona Roma amempeleka yule mchina kwenye mabafu .
Upande wa Lanlan hakushangaa kile kilichokuwa kikiendelea na alisimama na kwenda kuchukua kifurushi cha mishikaki na kurudi juu ya meza na kuendelea kula.
Upande wa yule mchina Xiao Xiao hakuelewa Roma anataka kumfanya nini na namna ambavyo alimshika mkono hakuwahi kufanyiwa hivyo na mwanaume na alijikuta mapigo yake ya moyo yakienda spidi spidi.
Pengine alijua labda Roma kadhamiria kwenda kufanya nae bafuni ndio maana anamwingiza huko.
Alikuwa mwekundu kama yai la kisasa kutokana na uzungu wake na aliishia kujiuliza ni kipi ambacho anapaswa kufanya ,ijapokuwa alikuwa akitamani kuonana na Roma kwa mara nyingine na kufanya nae mapenzi ili kuweza kumtumia kupanda levo lakini katika hali kama hio ya kushitukiza alijiona ni kama hakuwa tayari.
Upande wa wanaume ambao walikuwa kwenye mgahawa huo waliishia kumwangalia Roma kwa mshangao na wivu , ukweli ni kama walimdhania Roma na mchina huyo ni wapenzi kwani Xiao Xiao hakuleta ukinzani wakati wa kuvutwa na Roma mpaka kuingiziwa ndani ya mabafu.
Roma hakujali sana macho ya wengi yaliokuwa yakimwangalia , kwani mara baada ya kumfikisha Rufi kwenye bafu ambalo hutumiwa na wanaume aliwapa ishara vijana wadogo waliokuwa wakibadilisha mavazi kuondoka na walifanya hivyo haraka haraka na kisha wakakimbilia nje lakini mmoja wapo ambaye alikuwa mkubwa kidogo aligoma.
“Wewe kama nani mpaka kutuamrisha tuondoke?”Aliongea
Roma alikuwa na hasira na palepale alipiga ngumi ukuta kiasi cha kutengeneza ufa na jambo lile lilimuongopesha yule wmanaume na palepale alikimbia kuelekea nje akiwa kwenye mshangao.
Upande wa Xiao Xiao alikuwa akimwangalia Roma na macho ya aibu , huku akishindwa kuzuia kulegea kutokana na macho yake pamoja na uso ambao ulikuwa umetakata na kumfanya kumuona mtanashati.
Yeah Roma alikuwa amebadilika uso sana tofauti na mwanzo ambapo alikuwa mbeba mizigo , kipindi hicho alionekana kuwa Handsome sana , pengine ni kutokana na kupanda levo, kilichokuwa kikimpunguzia pointi ni aina ya uvaaji wake tu.
Roma alimshika na kumsukumia Xiao kwenye chumba kilichokuwa pembeni kushoto kwake na kisha akafunga mlango na palepale alikwenda kumkandamiza ukutani huku akimwangalia usoni kwa macho yasiokuwa yakielezeka.
Xiao alikwepesha macho kwa aibu huku akiwa na msisimko wa aina yake na alikuwa akisubiria kwa hamu hatua ya pili ambayo Roma anakwenda kufanya.
Ijapokuwa Roma alionekana kuwa siriasi hali ile ya ki uwanaume ilimfanya kuvutiwa zaidi na aliona kitakacho fanyika hapo ni yale mapenzi ya vurugu na hio ndio ilikuwa ‘Fantasy’ yake.
“Kufanyia hapa sio vizuri , kama vipi tufanye haraka haraka tuondoke…”Aliongea huku akionyesha hali ya aibu za kike na kumfanya kuzidi kupendeza..
Wanawake wa rangi nyeupe ni tofauti kidogo na wanawake wa kiafrika hususani katika swala la mahusiano , ni wawazi sana likija swala la mahusiano na anaweza akaruhusu ngono kufanyika hata na mtu ambaye hamjui vizuri.
Upande wa Roma mawazo yake yalikuwa mengine kabisa muda huo alikuwa akijiuliza ni kipi anapaswa kumfanyia , aliogopa kwamba kama ataenda kusema huko kwenye ulimwengu wao kama Rufi yupo Tanzania basi ingekuwa tatizo.
Roma hakutaka matatizo kwa wakati huo kwani nguvu zake za kijini hakuwa na uwezo wa kuzitumia kwa wakati huo na asingeweza kumlinda Rufi kama atakamatwa.
Mbaya zaidi kama itajulikana alikuwa na mahusiano na Rufi ndio ingekuwa tiketi ya majini hayo kuja kumvamia na kutaka kumuua maana alijua tabia yao namna moja ni kutopenda kudharaulika.
“Unataka nifumbe macho kwanza kabla hujaanza kunikiss… najihisi sipo tayari lakini unaonekana una hamu, hivyo sijali kama unataka tufanye , isitoshe nilikuwa nikikufikiria sana”Aliongea Xiao huku akiona pengine Roma alikuwa akiona aibu ndio maana alikuwa akimwangalia tu bila kuchukua hatua yoyote.
Xiao Xiao alikuwa ni mzuri haswa wa sura ijapokuwa alikuwa na rangi ya kichina lakini macho yake yalikuwa tofauti kidogo na wachina wa kawaida , kitu pekee ambacho hakuwa nacho ni umbo tu.
Roma alijiwazia alikuwa ameua watu wengi ambao pengine kati yao hawakuwa na hatia hivyo kujiongezea dhambi kwa kuua na mwanamke mrembo kama Xiao lisingekuwa tatizo.
Alijiambia kama mwanamke huyo ataendelea kuwepo hai basi siri ya uwepo wa Rufi nchini Tanzani itafichuka na ili kuficha siri hio kwa wakati huo hatua ya kwanza ni kumuua.
Baada ya kuwaza kwa muda palepale akili yake ilifanya maamuzi na shetani mtoa roho alimvaa na sura yake iligeuka na kuwa ile ya kikatili na palepale alipeleka mkono kwenye shingo yake.
Xiao alijua Roma alikuwa akitaka kuinua kidevu chake , hio pia ni moja wapo ya staili ambayo alipenda kufanyiwa na mwanaume , kunyanyuliwa kidevu na kuangaliwa usoni na mwanaume mwenye uchu kabla ya kubusiwa.
“Xiao Xiao kama utakuwa na kinyongo na mimi kwa kukuua leo hii basi naomba ukiwa kuzimu roho yako initafute na ulipize kisasi, hili halina uhusiano wowote na Rufi hivyo usije kumchukia”Aliongea Roma.
“Unamaanisha nini?”Xiao Xioa alijikuta akiwa katika mshangao huku akichanua macho yake lakini palepale aliweza kugndua kwamba Roma hakuwa akipanga kufanya nae mapenzi bafuni.
Roma hakutaka kuchelewesha muda na palepale alimshikilia shingo kwa nguvu kumkaba na Xiao Xiao alijihisi kuanza kukosa pumzi.
“No .. usinifanyie hivi..”Aliongea lakini Roma kabla hajakaza mkono mlango palepale mlango ulisukumwa kwa nguvu na aliingia Rufi ambaye alionekana kuhema kwa nguvu.
“Hubby usifanye hivyo , tafadhari naomba umuache ,, huyo sio tishio kwetu”Aliongea Rufi kwa kubembeleza.
Wakari Rufi na Amina wakimuona Roma akimwingiza Xiao kwenye bafu palepale waliangaliana na kisha wakapeana ishara ya kwenda kuchungulia nini kinafanyika.
Baada ya kusikia Roma alikuwa akipanga kumuua Xiao Xiao palepale alisukuma mlango kumuokoa.
Xiao Xiao mara baada ya kujua Roma alikuwa akitaka kumuua na sio kufanya nae mapenzi machozi yalianza kumtoka palepale.
“Uli.. ulikuwa ukitaka kuniua?”Aliuliza huku akionyesha mshangao na uso wake wa kirembo ulibadilika na kuwa mwekundu , pengine angekuwa na nguvu za kijini katika levo ya nafsi basi moja kwa moja angekuwa ashampiga Roma.
“Rufi huyu anatokea katika ulimwengu wa kijini , ukoo uliolazimishwa kuolewa nao , kama ataenda kutoa taarifa ..”
“Najua ...”Rufi alijikuta akimeza mate huku akionyesha huruma.
“Najua ni hatari lakiki sitaki kukuona ukimuua mtu ambaye hana hatia .. pengine hujui hili lakini wakati nilipochumbiwa kwenye ukoo wao walinidharau sana na kuniona kama kiumbe cha ajabu lakini ni Xiao Xiao pekee ambaye hakuoneysha kunidharau, sio mtu mbaya na hawezi kufanya kitu ambacho kitaniathiri”
Roma alimwangalia Rufi na kuona anapaswa kutii kile anachomwambia kwani asingefanya hivyo angeziumiza hisia zake.
“Okey fine”Aliongea Roma na kisha akamwachia Xiao Xio
Xiao Xiao alijikuta akichuchumaa na kuanza kulia kilio cha kwikwi huku akiwaangalia wote na kuangalia mkono wake ambao ushavimba kutokana na kushikiliwa kwa nguvu.
“Umenikatali sana , mimi sio kama baba yangu wala kaka yangu , kama yeye mwenyewe hataki kurudi kwanini aende , kwanini umeshindwa kuongea na mimi vizuri tu”Aliongea na kisha palepale akasimama.
“Kama hunipendi si ungesema tu kwamba hunipendi , kwanini ya kutaka kuniua , nilipatwa na furaha baada ya kukuona kwa mara nyingine kutokana na kukuwazia muda wote tokea mara ya mwisho tuonane kwanini unapenda kucheza na hisia zangu hiv, nakuchukia sana , sitaki kukuona tena kwenye maisha yangu”Aliongea awamu hio kwa Kichina kabisa na kisha alitoka nje kwa kukimbia huku akitoa machozi .
“Hubby asante kwa kunisikiliza”Aliongea Rufi akivuta pumzi ya ahueni.
“Natumaini maamuzi yako ni sahihi na hakuna kibaya ambacho kitatokea”Aliongea Roma.
“Kama mambo yatabadilika nitaondoka kuelekea Mediyerranian kuishi na Sister Rose , nadhani hawawezi kuvuka mpaka kuja mpaka kule”Aliongea
“Rufi unarahisisha mambo , kama watataka wanaweza kwenda mahali popoate hata kama ni kwa kupigana na miungu hawatojali , mwili wako ni hazina kubwa kwao kukupoteza kirahisi , isitoshe majiini ni viumbe ambavyo havipendi kushindwa kirahisi”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kutoa machozi.
“Jamani tumekuja hapa kwa ajili ya kumsindikiza Lanlan kucheza hebu tuachane na hayo kwasasa , Nasra ,Dorisi na Lanlan wanatusubiria”Aliongea Amina kwa kingereza huku akitangulia.
“Hubby nimefurahi , tulijua ulitaka kufanya nae kwasababu alikuwa mrembo lakini kumbe ulitaka kumuua kwa ajili yangu , namuoea huruma Xiao Xiao lakini nimefurahi kuona unanijali , Thanks a lot love”Aliongea.
“Nyie warembo siku moja mtaniua”Aliongea Roma huku akimfinya mashavu huku akitoa tabasamu.
Baada ya chakula Lanlan alienelea kucheza michezo akiungana na Nasra na Dorisi na walijikuta wakifurahi sana siku hio.
Ilifikia hatua mpaka Nasra akajiuliza imekuwaje Edna akamuacha mtoto mzuri kama Lanlan kwani uwepo wake tu ulikuwa ukileta furaha.
Roma wakati huo hakuacha kumkumbuka Edna na alijiaribu kupiga simu nyumbani kumuulizia Edna kama amerudi lakini Bi Wema alimwambia bado hajarejea.
“Pengine atarudi jumatatu kwani ndio siku ambayo inatarajiwa kuwa na kikao cha kutangaza mabadiliko ya kampuni ya Vexto”Aliongea Nasra mara baada ya kumuona Roma amekuwa mnyonge.
“Mimi sitaki hata kujisumbua na maswala yake mengine , ninachotaka ni kuongea nae na kuweka mambo sawa tu basi , nimefikiria sana katika hizi siku na nimegundua kuna kitu alikuwa akinificha”Aliongea Roma na Nasra alimshika begani kumtuliza huku akimwangalia kwa kumuonea huruma.
Muda wa jioni wote walirudi nyumbani kwao wakimuacha Amina anapoishi na Roma alichukuana na Lanlan kueleka nyumbani kwa Nasra
Wakati wanaingia getini walishangazwa na uwepo wa magari matatu ambayo hawakuwa wakiyajua, mawili yalikuwa ni Aud rangi nyeusi na moja wapo ilikuwa ni gari aina ya Maserati ya rangi nyekundu.
“Ineonekana tuna ugeni hapa”Aliongea Rom.
“Naona hivyo pia”Alijibu Nasra aliemshika Lanlan mkono.
“Nasra wewe ondoka na Lanlan moja kwa moja kwenda juu akapumzike mimi nitaonana nao”Aliongea Roma na Nasra alitingisha kichwa kumwelewa na kisha alitumia mlango wa nyuma wakati Roma akielekea eneo la seubuleni.
Mtu pekee amaye aliachwa nyumbani alikuwa ni Qiang na mara baada ya kuingia ndani Roma aliweza kumuona mwanadada huyo ambavyo amekosa utulivu kwani alikuwa akizunguka zunguka huko na huko , lakini alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kumuona Roma.




SEHEMU YA 653.
Roma mara baada ya kuingia ndani aliweza kuona sura anazozifahamu , mmoja wapo alikuwa ni Afande Jamali na mwingine alikuwa ni mwanamke kutoka familia ya Sharif.
Alikuwa amevalia suti nyeusi na viatu rangi nyekundu aina ya skuna, nywele zake alikuwa amezifunga kurudi nyuma na kumfanya kuwana mwoneknao wa kujiamini pamoja na wa kuvutia kwa wakati mmoja.
Alikuwa ni mwanadada mrembo Maimuna Sharif ambaye alionekana kama vile ni ofisa kutoka benki kwa muonekano wake kiasi ambacho kama wewe ni mwanaume wa kawaida ingekufanya kukosa hali ya kujiamini mbele yake.
Afande Jamali mara baada ya kumuona Roma palepale alisimama kwa heshima.
“Mr Roma naomba unipe ruhusa yako kukutambulisha , huyu ni Miss Maimuna Sharif Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bale Group na mtoto wa kwanza kutoka kwa mzee Hafidh Sharif”Aliongea Jamali.
“Tunakutana tena Mr Roma”Aliongea Maimuma huku akionyesha tabasamu na kunyoosha mkono wake kumpatia Roma.
Roma aijiuliza mwanamke huyu anafanya nini , alikuwa akikumbuka alimuona siku ya jana yake mkoani Kilimanjaro , lakini licha ya kutoelewa nia ya ujio wake hakuwa akimuogopa hivyo alinyoosha mkono wake kumsalimia.
Roma mara baada ya kugusana na mkono wa mrembo huyo alijikuta akijiambia alikuwa na mkono mlaini mno ijapokuwa haikuwa mlaini kama wa Rufi lakini bado ulikuwa mlaini wa kumpagawisha mwanaume yoyote rijali.
Roma kwa kumwangalia ru Maimuna alijua kabisa sio mwanamke wa kawaida , ilionekana kabisa alikuwa na mafunzo ya kimapigano na alijiambia hakika alikuwa akijua kujijali.
Moja ya mbinu ya kupima kama mtu ana mafunzo ya kimapigano ni kupitia pumzi yake, watu ambao wana mafunzo ya kimapigano hususani ya Kung fu mara nyingi upumuaji wao ni wa tofauti na watu kawaida wanapumua kama vile wanahesamu pumzi inayvoingia na kutoka, kitu kingine pia katika utembeaji wao au pale wanapokuwa wamesimama hii huwatofautisha sana.
Kwa mfano wakati wa kutembea ni kama vile kuna mstari anaofuatisha kwani hatua zake hazipindishiki huku mikono yake yote ikiwa usawa wa mwili , mtu wa kawaida tembea yake inateneza mstari wa Zigzag huku vidole vya miguu yake vinatengeneza angle
Sasa sifa hizo zote alikuwa nazo huyu mwanadada Maimuna ambaye alikuwa mbele ya Roma na kujikuta akimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida na kujiambia alikuwa na urembo wa mwili na ngozi yake ni laini mno , pia ni mkurugezi wa kampuni ya Bale lakini pia wakati huo huo alikuwa na mafunzo ya mapigano.
Ilikuwa ngumu sana kumkutana mwanamke mwenye mafunzo ya mapigano kuwa na ngozi laini hususani ya mikono.
Wakati wakiwa wameshikana mkono Roma alijikuta akihisi mtekenyo kwenye kiganja chake na palepale aligundua Maimuna alikuwa amemtekenya kwa kutumia ukucha wa kidole cha mwisho.
Jambo lile lilimshangaza na kumfanya Roma ajulize mwanamke huyo anafanya nini , au yupo hapo kwa ajili ya kumtega.
Baada ya kuachiana wote watatu waliweza kuketi chini huku Qiang akiandaa juisi.
“Afande Jamali nadhani hujamleta hapa kwa ajili ya kunisalimia tu”Aliongea Roma akitaka maongezi yaende moja kwa moja katika topiki ambayo imewalata.
“Ndio Mr Roma , sitozunguka zunguka , nipo hapa kama mwakilishi wa wizara ya ulinzi?”Aliongea.
“Mzee Hashim Tozo ndio kakuagiza?”Aliogea Roma akimaanisha waziri wa ulinzi ambaye alikuwa ni ndugu yake Afande Tozo, Roma alishawahi kukutana nae mara kadhaa nyumbani kwa Afande Kweka na alikuwa amezoeana nae japo sio sana,
“Ndio Mr Roma , nipo hapa kufikisha ujumbe kutoka serikalini , serikali ya Tanzania inaheshimu familia yako pamoja na familia ya Mzee Sharif kwani mchango wenu kwa taifa ni mkubwa , Mstaafu jenerali ametoa taarifa yake kwamba familia yake haihusiki na swala lolote lililotokea siku ya jana na kusema unapaswa kuwajibika kwa kila kitu binafsi, hivyo ndio maana tupo hapa kwa ajili ya maongezi”Aliongea.
“Nenda moja kwa moja kwenye pointi”
“Ngoja niseme mimi… Mr Roma nipo hapa kwa ajili ya kutafuta haki ya familia yangu”Aliongea Maimuna
“Haki ya familia yako?”
“Ndio , nimekuja hapa kwa ajili ya kukutaka urudishe hazina yetu , kisha ujenge upya jengo la ibada na baada ya hapo usujudie roho za miungu wetu mara nne”Aliongea Maimuna huku akiwa na uso wenye urafiki.
“Kwanza nikueleze kwamba hio hazina sijui nini maana mimi sina , pili mmefikiria nini kudhania kwamba ninaweza kwenda kusujudia miungu yenu ilihali mimi ndio niliochoma moto jengo lenu la ibada”
“Mr Roma watu waliokukosea ni Salihi naibu waziri wa elimu pamoja na Asha na kama ni kisasi ulitakiwa kuwalipiza wao , kwanini ukahusisha familia nzima katika kisasi chako kwa kuchoma jengo letu la ibada pamoja na kuiba hazina yetu huku ukiharibu makazi yetu , mpaka kuja kwangu hapa ni kwamba familia yetu imekaa chini na viongozi wa kiserikali na kukubali jambo hili kuisha kwa amani na kusahaulika kama utatii matakwa yetu , urudishe hazina yetu na kisha usujudie miungu yetu kuiomba msamaha”
“Kama hiki ndio ambacho kimewaleta mnaweza kuondoka”aliongea Roma akisimama na kisha kunyoosha kidole kuelekea mlango wa kutokea nje.
Maimuna wala hakuonyesha kuathirika , yaani alikuwa akiongea kirahisi mno na palepale alisimama na kisha akamsogelea Roma karibu zaidi kimadaha na kufanya marashi yake makali ya bei ghali kuathiri pua za Roma.
“Mr Roma , siku ya jumatatu jioni nimeandaa sherehe ndani ya hoteli ya Wache Kigamboni, wageni wangu ni wabia wa kibiashara ambao wanashirikiana kwa ukaribu zaidi na kampuni yetu ya Bale Group , unaonaje ukishiriki na wewe?”Aliongea huku akiwa na tabasamu la kiuchokozi.
“Kwanini nihudhurie?”
“Kwasababu nitakupa sababu ambayo itakufanya ushindwe kukataa kuhudhuria , nina uhakika utaweza kukubaliana na matakwa yetu baada ya hio hafla”
“Vipi kama nisipo hudhuria?”Aliuliza Roma na kumfanya Maimuna kutingisha mabega.
“Nina uhakika mwanaume jasiri kama wewe hutopenda kuonekana Muoga mbele ya familia ya Sharif .. Besides I’ m just a frail woman .. alright that is settled, nitakuja kukuchukua mwenyewe hio siku”Aliongea huku akimkonyeza na kisha alimpita kimadaha na kuelekea nje huku akitingisha makalio yake ya wastani kwa fujo kama zote.
Roma aliishia kushika kiuno na kujiambia hakika ameweza kuamsha shauku yake.
“Vipi mmeshawazuia kutumia njia ya fujo katika kulipiza kisasi?”Aliuliza Roma akimwangalia afande Jamali.
“Hata mimi mwenyewe sijui na nafuata tu maagizo ninayopewa na wakuu wangu , lakini nakushauri Mr Roma hii familia haiwezi kuliacha hili lipite hivi hivi kuna nguvu kubwa ambayo ipo nyuma yao , lakini inaonekana hawataki kufanya fujo kudai haki yao , unapaswa kufikiria mara mbili ili kulimaliza kimya kimya”Aliongea Afande Jamali
“Babu alisema kwasababu mimi ndio msababishaji nitawajibika mwenyewe na hakuna mtu wangu wa karibu ambaye ataguswa “
“Inaonekana kuwa hivyo , isitoshe wanawake wako wote sio raia wa kawaida , serikali haitaki hili swala kuingiliana usalama wa raia … maagizo yashatoka kama famili ya Sharif itafanya jambo lolote la kutaka kudhuru familia yako basi tutaingilia”Aliongea Jamali.
“Nimefarijika kusikia hivyo , isitoshe adui yao ni mimi hivyo nipo tayari kuona nini wananniandalia, ninashauku ya kutaka kujua mchezo wao utazaa nini”Aliongea Roma na kumfanya Afande Jamali kushindwa kumuelewa Roma kabisa kwani alionyesha kutokuwa na hofu kabisa.
Baada ya wageni kuondoka na walinzi wao, Roma alikaa hapo sebuleni kwa muda mpaka Nasra aliposhuka na kukaa pembeni yake.
“Hii familia ya Sharif ina nguvu sana?”Aliuliza Nasra.
“Inaonekana , ila kwa sasa nahitaji kufanya maandalizi”
“Unahitaji msaada wangu?”
“Ndio”
“Nini nikusaidie?”Aliongea Nasra akionyesha shauku.
“Simu yangu imeisha chaji , nichajie na kisha niletee laptop yako hapa , kuna mtu nahitaji kuwasiliana nae kwa njia ya online”Aliongea Roma.
Nasra alijikuta furaha yake ya kutaka kumsaidia Roma ikipotea, na kujiambia alijawa na shauku ya bure.
Ukweli ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kutohitaji msaada wowote kutoka kwao iliwafanya kuwa na shauku kama atataka msaada.
Licha ya kuchukia alichukua simu ya Roma na kwenda nayo juu kuichomokea chaji na kisha alishuka na Mackbook Pro na kumpatia na Roma aliunganisha na internet palepale na aliingia mtandaoni na kulipia VPN na kisha akapakua kivinjari cha Tor na kisha akaingia mtandaoni.
“Naweza kuangalia unachofanya?”Aliuliza Nasra akiwa makini na kumfanya Roma kumwangalia na kutabasam.
“Unaweza ndio kuangalia wewe ni mwanamke wangu”Aliongea
Roma hakuona haja ya kumficha Nasra kile ambacho alikuwa akipanga kufanya , mpango wake ni kutaka kuomba msaada kutoka nje ya nchi kufika Tanzania kwa ajili ya kumsaidia jambo lake.
Roma baada ya kuingia kwenye mtandao wa Deep Web palepale aliandika link ambayo alikuwa ameikariri na dakika hio hio yaliweza kuonekana mawasiliano ya watu mbalimbali na ajabu kila mtu ambaye Roma alikuwa akiwasiliana nae ilimhuhiaji kwanza kuingiza Passcode.
Licha ya kukaa na kuangalia lakini Nasra hakuelewa chochote kwani Roma alikuwa akiwasiliana na watu kwa kutumia lugha tofauti tofauti.
Kitu pekee ambacho aliweza kugundua ni kwamba kila mtu ambaye aliwasiliana nae alionekana kumuheshmu sana Roma
Ilimchukua nusu saa Roma mpaka kumaliza .
“Babe you were so cool”Aliongea Nasra huku akijikumbatisha kwenye kifua cha Roma.
“Umeelewa chochote nilichokuwa nikiongea?”
“Sijaelewa lakini , ulivyokuwa ukiongea inapendeza sana”Aliongea akirembua na kumfanya Roma mzuka kumpanda.
“Lanlan ashalala?”Aliuliza Roma.
“Ndio na anakoroma huyo”Aliongea na kumfanya Roma kutoa tabasamu na kuingiza mkono kwenye kifua cha mrembo Nasra na kuchoropoa embe dodo.
“Kama kashalala unaonaje tukifanyia hapa hapa kwenye sofa na kisha tukaoge wote”Aliongea Roma lakini hakusubiri jibu kwani paleplae alimnyanyua na kisha akamlalia kwa juu na kilichoendelea masofa yatahadithia.
Siku ilofuata ilikuwani jumapili na Roma hakuwa na mpango wa kumpeleka Lanlan kucheza tena.
Siku hio aliona kitu pekee ni kuangalia maendelo yake katika kujifunza mbinu ya Andiko la urejesho, maana aliona Lanlan ni mwendo wa kula bata tu tokea arudi ulimwengu wa majini pepo.
Kutokana na Roma kutokuwa na nguvu za kijini hakuweza kumwangalia Lanlan amefikia levo ya ngapi hivyo kitu pekee ambacho alitaka kujua ni kumchukua na kisha wakaenda hadi msituni na wakati huo akiwa na matofali ya zege.
Baada ya kuyapangilia chini kwa mstali maalumu mawili mwili matatu mtatau na manne nne alimwambia Lanlan aanze kuyapasua kutoka mwanzo mpaka mwisho kwa kutumia ngumi.
Lanlan misuri ya mwili wake ilianza kutuna kama vile ni puto na palepale alianza kuyapasua kwa kasi na ndani ya dakika yote alikuwa ameyapiga na pigo moja moja mpaka kupasuka.
Roma alijikuta akiridhika na alijiambia kutokana na nguvu aliotumia pengine atakuwa katika levo ya Uchoyo au wanaita levo ya kujijali mwenyewe na muda wowote angeingia katika levo ya Takdiri au Hatima kwa lugha nyingine.
Hii ni levo muhimu sana katika mafunzo ya kijini lakini ukiachana katika mafunzo ya kijini lakini pia katika maisha ya binadamu ni moja wapo ya hatua ambayo ni muhimu kwa mafannikio ya binadamu yoyote , ni binadamu wachache sana ambao wanajua Takdiri yao nini katika ulimwengu huu na hao ambao wamebahatika kuijua mafanikio yao ni ya juu sana kuliko wale ambao hawaijui Takdiri yao ni nini.
Kila binadamu huzaliwa na kuwepo katika uso wa dunia kwa kusudi maalumu na ndio maana katika hatua za kujitafuta ili kujua wewe ni nani tofauti na jina lako hutakiwi kuuliza maswali mtu wa nje bali unatakiwa kujiuliza wewe mwenyewe maswali na kutafuta majibu na hapa ndipo utaweza kujua nini Takdiri yako.
Maendeleo ya Lanlan yalimshangaza sana Roma , ijapokuwa yeye wakati wa kujifunza hakutumia vidonge vyvoyote kujibust lakini kwa Lanlan spidi yake ilikuwa ya juu na alikuwa na shauku ya kutaka kujua kitamtokea nini mpaka kupita levo ya kifo na uhai halafu kuzaliwa upya.
Roma alijikuta akimsifia Lanlan kwa kazi nzuri huku akimwahidi mambo mengi lakini Lanlan alitaka kupaishwa juu angani lakini Roma uwezo huo hakuwa nao na alijikuta ile hali ya kutaka kurudisha uwezo wake na kumuondoa mdudu aliekuwa akimtawala kumvaa.
Roma aliona kwamba haijalishi Lanlan uwezo wake unaongezeka kwa spidi namna gani lakini bado tu alikuwa akipaswa kumlinda.
Roma mara baada ya kurudi na kumaucha Lanlan mojakwa moja alielekea katika maabara ya Clark eneo la Makongo juu , maabara ambayo ilikuwa urithi kutoka kwa Profesa Shelukindo.
Roma mara baada ya kufika aliweza kugundua pia Rufi yupo na wote walikuwa bize kupitia baadhi ya vitabu.
“Kuna chochote ambacho mmepata?”Aliuliza Roma akiwaangalia warembo hao namna ambavyo wapo bize.
Clark alikuwa amevalia simple huku nywele zake alikuwa amezifunga na lastick kwa nyuma, muda wote mwanamke huyo alionekana kuwa bize.
“Kulingana na maarifa ya Rufi kuhusu roho mnyama wa maafa , hakuna aina yoyote ya nguvu ya kiroho ambayo inaweza kushindana nayo kwasababu ni mnyama aliewahi kuwepo katika kipindi cha dunia kuwa katika hali ya ukiwa na machafuko , inawezekana alikuwa ni mnyama mwenye nguvu kubwa duniani”
“Dear nipo hapa kwa taarifa nzuri lakini kwanini unaongea kuniogopesha?”
“Mimi ni mwanasayansi na sio motivation speaker , ninachokuambia ni fact , mambo hayapo mazuri sana kwa upande wetu”
“Hubby huna haja ya kujali sana kuhusu alichoongea Clark , ijapokuwa sina wazo namna ya kuishinda lakini tunaweza kushinda kutokana na hasira yake”
“Hasira yake?”
“Ndio”
“Hio ni roho ya mnyama mkali sana ambaye sifa yake kubwa ni kukasirika na kutokuwa na huruma , hivyo tunapaswa kutafuta roho nyingine ambayo ni ya mnyama lakini mpole ili tu kuiamsha ndani yako , ijapokua roho hio inaweza kuwa na nguvu kidogo kushindana na Chaos, hivyo kabla ya jaribio hilo tunapaswa kuanza na nguvu zako za kijini , tunapaswa kuibadili nguvu yako ya kijini na kuiweka katika kitu ambacho kitakandamiza roho yake ya ukali”Yalikuwa ni maelezo mengi ambayo Roma alishindwa kuyaelewa.
“Umeongea vitu vingi , je una mpango wowote?”
“Tuna mawazo tofauti , nilikuwa nikiwaza vipi kama utaombewa kanisani au kusomewa swala msikitini , watu wa dini wana upako wa kutosha, ninachojua nguvu iliopo ndani yako ni ya kipepo hivyo inaweza kusafishwa na nguvu ya kiroho ya nuru ya kidini ambayo ni safi”
“Clark tangu lini wewe kama mwanasayansi ukaanza kuamini katika maombezi”Aliongea Roma kwani siku zote Clark kila mama yake alipokuwa akimlazimisha kwenda kanisani alimwambia hakuna Mungu kwasababu hakuna uthibitisho wa kisayansi.
“Mimi najua mambo mengi kuliko unavyodhania , ijapokuwa sijawahi kuamini katika imani yoyote lakini kuna nguvu ya kiroho ambayo sio ya kawaida katika misikiti pamoja na kanisani ndio maana watu wana imani kali, nimeamini baada ya kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi”Aliongea na Roma alitingisha kichwa kwani hata yeye alikuwa akikubalaina nae.
“Vipi kuhusu wewe Rufi?”
“Mimi nimeona labda ujaribu kusali kibudha au kihindu, kuna Monk ambao wana uwezo mkubwa wa kufanya ‘Exorcism’ lakini kazi kubwa ni kuwapata na kuwa na utayari kufanya hio kazi, nimeshindwa kujua ni aina gani ya nguvu ya kiroho ambayo inaweza kushindana na nguvu ya Chaos”
“Kwahio mwishowe tuna uelekeo lakini mpango hatuna”
“Sio kabisa , kama tutashindwa kukusaidia kwa njia za maombezi au Exorcisim basi angalau tunapaswa kupata Dhana za kijini za kiwango cha juu kabisa ambazo zina uwezo wa kushindana na roho ya mnyama wa maafa”
Baada ya Rufi kuongea vile mawazo ya Roma yalimkumbusha kitu kimoja ambacho aliiba katika madhabahu ya Mzee Sharif.
“Nimekuja hapa kwa kitu kingine pia , hebu ngoja niwaonyesheni muone..”Aliongea Roma na kisha palepale alitoa ile Kokoto iliokuwa na jina la Hazina na kisha akampatia Rufi.
“Unaijua hii maana yake?”
Write Note:Exorcism ni kama vile wanavyofanya waganga wa kienyejji katika kufukuza mapepo , sasa katika imani ya Kibudha na Kihindu hufanya hicho kitendo pia kwa muumini mwenye mapepo.




SEHEMU YA 654.
Rufi na Clark walikuwa wameshangazwa sana na neno Hazina na palepale walijikuta wakifungua kile kijiboksi kuangalia kilichopo ndani.
Lakini mara baada ya kuona kitu chenyewe walijikuta wakikosa yale matamannio yao, walijiuliza kokoto inaweza vipi kuwa hazina.
“Ndio nini hiki , ndio Hazina uliokuwa ukisemea , mbona inaonekana kama pande la mkaa lakini uzito wake ni mkubwa kuliko wa mkaa , au ni jiwe?”Aliuliza Rufi.
Clark hakuonyesna kukupurukuka na aliishia kuangalia kwa umakini kujaribu kukagua na kulipatia maana yake kwani palepale aliliweka katika Darubini na kuanza kulikagua kisayansi na ndani ya dakika tano tu alionekana kupata majibu kadhaa.
“Linaonekana kama vile ni ‘Carbide’, kuna aina ya madini ndani yake lakini ajabu pia kuna protini , au ni Fossi , asili mara nyingi inakuwaga na vitu ambavyo vinaonekana kama vimekufa lakini bado vipo hai , hata hivyo vitu vya aina hio sio vingi lakini sio adimu pia”(Fossil ni mabaki ya kale)
Roma alijikuta pia na yeye kuchukia na kujiambia hio takataka kwanini iwe ndio Hazina , lakini kwa wakati mmoja alijiambia familia ya Sharif ni matajiri na hata kiboksi kilichotumika kuihifadhia ni cha madini ya Dhahabu, alijiuliza au ni kumbukumbu.
Roma mara baada ya kuona hakuna majibu ya haraka haraka alificha hazina yake alioona kama takataka na kisha akawaambia waondoke pamoja kwa ajili ya chakula cha mchana
Roma wakati akiwa njiani kurejea nyumbani aliweza kupokea simu kutoka kwa Sophia na kumweleza kwamba yupo Afrika ya kusini anashoot matangazo ya Promosheni ya filamu na angerejea Tanzania hivii karibuni kwa ajili ya Show ya siku ya usiku wa Christmas na Roma alimuahidi kwamba atahudhuria show yake.
Roma mara kutoka nje ya gari aliweza kumkuta Lanlan ambaye alikuwa amelalia tumbo kwenye kibaraza huku makaratasi mengi na penseli za kuchotea zikiwa zimezagaa huku pembeni yake akiwa amesimama Qiang Xi.
Muda huo ilikuwa ni jioni na Nasra alikuwa ameenda Supermarket kwa ajili ya kununua vitu vya kupika usiku.
Roma alimsogelea Lanlan na kisha aliinua karatasi ambazo alikuwa amemaliza kuchora na kisha aliona sura ya Superman na chini yake kuna jina la Daddy.
“Lanlan mimi ndio Superman?”Aliuliza Roma huku Lanlan akiwa bize kukoleza rangi ya mti aliochora na alimgeukia Roma na kutingisha kichwa kukubali kwamba ndio yeye.
“Na huyu mwanamke na msichana ni nani ?”
“Huyo msichana mdogo ni Lanlan na msichana mkubwa ni mama yake Lanlan , Mama ana nwele ndefuu mpaka shingoni”
“Umekosea, Lanlan wetu ni kibonge lakini huyu hapa ni mwembamba”
“Lakini Lanlan hapo amekonda kwasababu amemmisi mama yake”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu.
“Umekonda vipi wakati ulikuwa ukila chakula chote ambacho Aunt Nasra anakuandalia , hujakonda bwana”
“Lakini Lanlan atasikia njaa asipokula , ila anammisi mama yake”Aliongea huku akiwa kama vile anaona aibu kuumbuliwa na kumfanya Roma kutoa cheko.
“Aunt yako Nasra atakasirika , yaani amekupikia chakula kitamu lakini hujamchora?”
“Kwasababu mama simuoni na nammiss ndio maana nimemchora”Aliongea na kumfanya Roma kukaa kimya.
Sio kwa Lanlan ambaye tu alikuwa amemmisi Edna bali hata yeye mwenyewe alikuwa amemkubuka sana .
“Daddy ,Je Mama hatutaki tena?”Aliuliza huku akitia huruma na kumfanya Roma kushangaa.
“Lanlan , unapaswa kukumbuka kwamba mama yako anakupenda na kwasasa hana furaha ndio maana , kila kitu kitakuwa sawa muda si mrefu”
“Nina uhakika Mama ananipenda kwasasabu yeye ndio amenizaa”Aliongea Lanlan akiwa na uhakika na Roma hakuelewa ujasiri wake unatokana na nini.
Ilimfanya kuingiwa na majonzi kwa kuona pengine Lanlan ameshindwa kumtofautisha mama yake mzazi na Edna, Roma alishindwa kujizuia na kumkumbatia.
Qiang ambaye alikuwa akisikiliza maongezi hayo alijikuta akitokwa na machozi tu na kuishia kuyafuta kwa siri.
Hakuna ambaye angeweza kuamini kwamba Lanlan alikuwa ameficha kile anachojisikia na kujitahidi kuonekana ni mwenye furaha muda wote.
Usiku wa jumapili uliweza kuisha vizuri na Roma mara baada ya kuamka alijua ndio siku ambayo Edna atakuwa amerudi na ataenda kazini kama alivyosema Nasra.
Kuhusu hafla ambayo Maimuna aliongea hakutaka sana kuwazia maana ingemfanya tu kuwa na wasiwasi.
Roma alitaka kumsubiri Edna atakaporudi ndio aongee nae lakini alijiambia anapaswa kuchukua hatua yeye kwanza kama mwanaume , alijiambia pengine Edna anasubiria yeye aanze.
Hivyo mara baada ya wazo hilo kumuingia alienda moja kwa moja mpaka nyumbani na aliweza kukutana na Bi Wema ambaye alimwambia Edna alirudi lakini ameelekea kazini.
Roma palepale alifanya maamuzi ya kuelekea huko huko kazini kuonana nae.
Roma mara baada ya kufika ndani ya jengo la makao makuu ya kampui ya Vexto moja kwa moja alienda mpaka Floor ambayo ndio rasmi ofisi ya Mwenyekiti wa kampuni inapatikana , ni ofisini ileile ya Edna lakini ilikuwa imebadilsihwa tu hadhi.
Ijapokuwa Ernest ndio alikuwa CEO lakini hakuwa akitumia ofisi ya Edna ya mwanzo.
Roma mara baada ya kutoka kwenye lift moja kwa moja alitembea mpaka kwenye mlango wa kuingilia ofisni huku akipata burudiko la kiyoyozi na harufu ya kuvutia na kisha aligonga mlango lakini hakuweza kupata mrejesho.
Dakika ileile mlango wa ofisi ya Sekretari ulifunguliwa na aliweza kutoka msichana mrembo kiasi alievalia kinadhifu.
“Wewe ni Mr Roma?”Aliuliza.
“Ndio , wewe ni nani?”
“Mimi ni Sekretari mpya , naitwa Yulia , naamini hunifahamu , upo hapa kwa ajili ya kuonana na Mwenyekiti”Aliongea kwa namna ya heshima.
Ilionekana alikuwa na taarifa zote kuhusu Roma ni nani , ni kama kawaida mfanyakazi mpya lazima ajue Hidden rules za mazingira ya kazi ili kuepuka kufanya makosa na kuwa upande mbaya na watu wakubwa.
Roma aliishia kutabasamu kumuondolea woga , alijua atakuwa ni mbadala wa Recho ambaye alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa idara.
“Ndio yupo wapi?”
“Yupo kwenye kikao na Bodi ya wakurugenzi , wapo chumba namba tatu cha mikutano”
Kama ilivyotarajiwa , mwanamke mchapakazi ambaye hana mpango wa kuacha.
Roma hakuwa mgeni hivyo alijua chumba namba tatu cha mikutano kipo upande upi na mara baada ya kufika aliweza kuona viti vyote vilikuwa vimejaa na wafanyakazi wa juu wa makampuni pamoja na wanahisa , wote wakiwa na sura za kitaaluma.
Edna alikuwa amekaa mbele kabisa kawenye kiti cha kibosi akiwa kauzu kama kawaida yake , hakukuwa na ishara zozote kama alikuwa na mawazo na ilikuwa ni kama ukauzu wake uliongezeka zaidi na zaidi.
Kila mfanyakazi aliekuwa ndani ya hilo eneo alikuwa akimhofia Edna huku wengine wakionyesha heshima zao , ilikuwa ni kama mawaziri wanavyomheshimu mheshimiwa Raisi.
Baada ya Roma kufungua mlango na kuingia macho yote yalimgeukia huku baadhi ya Sura zikimwonyeshea tabasamu , akiwemo Ernest Komwe na Monika.
Upande wa Dorisi na Nasra walishangazwa na ujio wake kwani hawakutegemea kama angeweza kuja hapo mapema hivyo.
Roma aliwaonyeshea tu tabasamu na ksiha akageuza uso wake kwa Edna na kumwangalia kwa namna isiokuwa ikielezeka.
Kama sio jasiri usingeweza kuingia ndani ya chumba kama hicho ambacho kilikuwa na zaidi ya watu therathini.
Edna alionekana kukunja sura tu mara baada ya kumuona Roma lakini hakukuwa na mabadiliko makubwa , yaani alimwangalia kwa sekunde tu na kisha akampotezea kama hamjui.
Baadhi ya watu tayari walishagundua mabadiliko hayo na kuishia kuwaangalia kwa namna siokuwa ya kawaida.
Roma baada ya kuona namna Edna alivyomwangalia alijikuta akikosa furaha na aliishia kushika kidevu chake na kufunga mlago na kisha akaegamia ukuta kama bodigadi.
Ijapokuwa alitamani kuongea na Edna lakini hakuona haja ya kumsumbua akiwa katika kazi kama hivyo.
“Recho , please continue with your presentation”Aliongea Edna akimwashilia kwa kunyanyua karamu.
Kampuni hio ilikuwa ikitumia mara nyingi lugha ya kingereza katika vikao vyote na mara nyingi hata wafanyakazi wakifanyiwa usaili wanapimwa uwezo wao wa kuongea kingereza kwa ufasaha na kukielewa pia. Isitoshe lazima iwe hivyo kwani kulikuwa na wafanyakazi na baadhi ya wanahisa ambao ni wazungu wasiokuwa wakijua lugha ya kiswahili , akiwemo Rich pamoja na Ernest mwenyewe.
Recho alionekana kukosa utulivu mara baada ya kumuona Roma lakini alijakaza na kisha aligeukia Projector.
“Kutokana na kuundwa kwa Vexto group kimataifa , itahitajika kugawa majukumu kwa wafanyakazi wakubwa wa kampuni kwenda kufanya kazi katika matawi Tanzu ambayo yapo nje ya nchi ili kurahisisha mwenendo mzuri wa kampuni pamoja na kugundua fursa nyingine za kibiashara, Mwenyekiti wetu wa bodi anaamini sisi wafanyakazi wa ngazi ya juu tunapaswa kuwa mfano katika kutoa mchango wa maendelo katika kampuni hivyo , Mwenyekiti amependekeza Dorisi kupandishwa cheo kuwa sawa na Nasra na watapaswa kuondoka nchini kwenda kufanya kazi katika matawi yafuatayo , Dorisi ataelekea Cape Town Afrika ya kusini na Nasra ataelekea Buenos Aires Argentina, watakuwa ndio Wakurugenzi wa makampuni haya yote mawili ambayo yameanzishwa rasmi na kazi zao ni kujenga msingi wa kibiasara katika masoko hayo mapya.











SEHEMU YA 655.
Dorisi na Nasra ni kama vile hawakuwa wamesikia vizuri , hata Roma ambaye alikuwa amesimama vilevile ni kama hajasikia vizuri.
Afrika ya Kusini , Argentina?!!
Roma hakushangaa sana uwezo wa Edna kuchanja mbuga kimataifa hususani kutokana na mtaji waliokuwa nao , hivyo sio jambo la kushangaza kampuni ya Edna kuanzisha tawi jipya Argentina na Afrika ya kusini lakini alijiuliza kwanini anataka kuwatuma Dorisi na Nasra.
Bila shaka kama wataenda huko ilimaanisha kwamba madaraka yao pamoja na malipo yangekuwa makubwa zaidi lakini kuwaagiza wanawake hao wawili kwenda nje ya nchi ni sawa na kuwafukuza tu ndani ya Tanzania.
Dorisi na Nasra waliweza kuhisi kitu na waliishia kumwangalia Edna kwa macho yasiokuwa ya kawaida lakini Edna hakuwaangalia hata kidogo.
“Mwenyekiti , sote sisi tunajua michango mikubwa na uwezo wao mkubwa katika maendeleo ya kampuni na ni sahihi kuwa wakurugenzi wa kampuni tanzu lakini nadhani wangeweza kufanya kazi nzuri zaidi kama wangebakia hapa makao makuu kutokana na uzoefu wao”Aliongea Ernest Komwe akitoa mchango wake.
“Wanapaswa kuongoza kampuni kama ishara ya kutoa mfano kwa wengine watakaochukua nafasi zao , sitojisikia vizuri kama nikituma mtu ambaye sio mdhoefu na biashara zetu , isitoshe kwenda huko kutawafanya kupata uzoefu wa kimazingira , CEO Ernest vipi unataka kwenda wewe?”Swali hilo lilimfanya Ernest kufunga bakuli lake.
Monika ambaye alishawahi kufanya kazi kama msaidizi wa Edna alikuwa akijua tabia yake hivyo alimwangalia mume wake na kumpa ishara ya kutulia.
Kila mmoja alijua kama Dorisi na Nasra wataenda huko watafanya kazi nzuri sana lakini isingekuwa rahisi kwao kwani walikuwa wakienda kukutana na mazingira mapya.
Roma aliekuwa amesimama kwenye kona ya mlango alijikuta akikunja ngumi na kujiambia je anafanya hayo yote kwa ajili ya kumlipizia.
Alijiambia sio tu kwamba wakati huo alikuwa akimpotezea lakini ameenda mbali na kuanza kuwaondoa wanawake wake karibu na kuwatuma nchi ya mbali.
Bila shaka , kama kiongozi mkuu wa kampuni Edn alisifika kwa kutopenda kupingwa akiamua jambo lake , kwa jinsi ambavyo alimwagiza Recho kusoma mapendekezo yake ilikuwa ikimaanisha kwamba alishafanya maamuzi tayari.
“If there is no objection from the vice presidents , we can proceed with the voting process , raise your hand if you approve of this proposal”Aliongea akimaanisha kama hakuna pingamizi kutoka kwa watendaji wasaidizi wa kampuni basi anaekubaliana na pendekezo lake anyooshe mkono kupiga kura.
Kati ya wakurugenzi ambao walikuwepo ni Mzee Alex mmiliki wa zamani wa kampuni ya Jr ambaye ipo chini ya Edna kama mwanahisa mkuu na wote kwa pamoja waliangaliana na kisha walionekana hakuna ambaye alikuwa akipinga kwani walinyoosha mikono kupiga kura ya ndio.
Yaani kwa jinsi wanahisa hao walivyonyoosha wote pasipo ya yoyote kutopinga ni kama vile walikuwa washajiandaa,
Recho alisimama kwa ajili ya kuhesabu kura hizo lakini Edna alimzuia.
“Hakuna haja ya kuhesabu , tayari tuna asilimia hamsini ya kura zote wanaokubali kabla sijatoa kura yangu , inaonyesha wengi wenu mmekubaliana na pendekezo langu , Miss Dorisi na Miss Nasra matawi yote mawili hayajamaliza hata miezi sita tokea yafunguliwe hivyo tunategemea kazi kubwa yenye mchango chanya kutoka kwenu”
Dorisi aliishia kuwa kimya huku macho yake yakiwa tayari ni makundu , ni kama vile muda wowote angetoa machozi , upande wa Nasra alionyesha hasira na wasiwasi kwa wakati mmoja.
“Edna kuna haja ya kwenda mbali hivi , inaonyesha hapa kabisa ulishaongea na Shareholders kupiga kura ya ndio ili sisi kwenda nje ya nchi mbali na Tanzania , umefurahi sasa?”Alisimama Nasra na kubwata huku akimwangalia Edna kwa macho makavu.
Watu wote kimya , hakuna ambaye alikuwa tayari kuongea lolote , ni kama walikuwa wakitarajia dhoruba kuamka muda wowote.
Ilionekana kwa watu hao ni kama kweli Edna alikuwa akifanya makusudi kabisa na hakujisumbua hata kuficha dhamira yake na ilionekana ni kama kuwadhalilisha mbele ya kila mtu.
Lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alikuwa tayari kupinga maamuzi ya Edna , licha ya kwamba maamuzi yake yalionekana kuwa na ukakasi.
Mtu pekee ambaye hakupiga kura ya ndio au hapana alikuwa ni Mzungu Richie peke yake , alikuwa amefumba macho kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza.
“Sijaelewa unachotaka kumaanisha”Aliongea Edna akimwangalia Nasra.
“Edna acha maigizo , unakasirisha ujue”Aliongea Nasra akiwa amepaniki hatari.
“Kama hukubaliani na maamuzi ya bodi , tunakukaribisha muda wowote kuleta barua yako ya kujiuzulu”
“Unadhani nnitashindwa kufanya hivyo?”
“Sidhanii hivyo , najua zipo kampuni nyingi ambazo zinakuhitaji”Aliongea Edna bila ya kuonyesha hisia zozote ni kama vile hakuwa akimjua Nasra,
“Benadetha utadili na hili swala , kama Mkurugenzi Mtendaji Nasra akitaka kujiuzlru nipo tayari kununua hisa zake zote kwa thamani mara mbili iliopo sokoni”Aliongea na Benadetha ambaye alikuwa kimya muda wote aliishia kutingicha kichwa tu.
“Edna unafikiri nimesema haya kwasababu ninajali sana kuhusu hisa zangu , unafikiri nitakuwa na furaha kama utanipa hela?”
“Furaha yako hainihusu , asante kwa mchango wako uliotoa kwa kampuni , sitokutendea vibaya kama utaamua kujiuzulu”Aliongea na kumfanya Nasra kujibwaga kwenye kiti huku akimuona kama Edna sio yule ambaye alikuwa akimjua.
“Nasra huna haja ya kuwa hivi , Mwenyekiti wa bodi ashafanya maamuzi lakini ni kweli hatuwezi kwenda nchi za mbali hivyo kwa ajili tu ya kazi hivyo chaguo lililobaki ni kujiuzulu”Aliongea Dorisi.,
“Dorisi unamaanisha nini kwamba hatuwezi , tatizo hapa sio kwenda mbali hivyo , shida ni kwamba hajaongea na sisi kabla , anatuchukulia sisi kama takataka kututupa kila mahali anapoona panafaa , nimeamua kufanya kazi hapa sio kwasababu sina sehemu nyingine ya kwenda kufanya kazi , sijali sana kuhusu nafasi yangu wala mshahara ninaopata wala hisa ninazomiliki, lakini mimi pia kama mfanyakazi wa hii kampuni nina kanuni zangu na utu wangu ambao unapaswa kuheshimiwa”
Dorisi aliishia kukunja sura , alikuwa akijua Nasra alikuwa sahihi lakini ilionekana haiwezekani kuweka mstari kati ya maswala ya kazi pamoja na mambo binafsi.
Dorisi mara baada ya kuwaza hivyo alijikuta akimgeukia Roma na kumpiga jicho na aliweza kugundua alikuwa kwenye mawazo pia kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza , kwani alikuwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Edna tokea siku ambayo nilijiunga na kampuni hii , sijawahi kuwaza kama nitapata chochote , , bibi yako na mama yako ndio watu ambao wamenifanya kuwa Nasra wa leo hii kwa kila kitu nilichokuwa nacho na siku zote nitaendelea kuwa mwenye shukrani , kama shukrani zingeweza kupimwa katika kipimio cha hela basi ningesema faida ambayo nimeingiza kwenye hii kampuni imepita deni ambalo mama yako ananidai , kama sio wewe kuongoza hii kampuni nisingejisumbua kufanya kazi ndani ya kampuni moja kwa miaka yote hio , sikuacha kufuata ndoto zangu na kufanya bidii kwa ajili ya mafanikio ya hii kampni kwa ajili ya mtu yoyote bali nimefanya yote hayo kwa ajili yako , Edna najua ni kweli kabisa nimekukosea wewe binafsi lakini kwanini unataka kunidhalilisha kazini , sijui wengine watanionanje lakini mimi kama mwanamke mwenzio nimekudharau”
Roma alijikuta akiinua uso wake na kumwangalia Nasra ambaye hakutaka kuonekana mnyonge mbele ya Edna , hali yake ya kujiamini na ujasiri wake ilimkumbusha na kumuona kama mwanajeshi.
Edna muonekano wake haukuadilika kabisa , ni kama vile hajamsikia kwa chochote kile alichoongea .
“Kama Miss Nasra na Miss Dorisi watachukua maamuzi ya kujiuzuru , majukumu yao ambayo walikuwa wakiyafanyia kazi kwasasa yatakuwa chini ya Recho , Benadetha pamoja na Rich , nitapenda kuona kila mmoja wenu kuanza kufikiria ni nani ambaye anafaa kurithi kazi zao kabla ya kikao kingine au vinginevyo nitafanya hio kazi mwenyewe”Aliongea kwa kujiamini kabisa.
Ukauzu wake na hali ya kujiamini na kutoathirika iliwaanya wafanyazi kumhofia na kujiuliza inakuwaje akawa haathiriki kwa chochote kutokana na kubweka kwa Nasra.
Nasra alijikuta akimpiga jicho la chuki Edna na palepale alikusanya kila kilichokuwa chake na kisha aliondoka akiwa wa kwanza, ilikuwa ni kama vile alikuwa amepoteza muda mwingi wa kufanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto.
Ni Dorisi peke yake ambaye alijitahidi kuzuia hisia zake zisimvae na palepale na yeye alikusanya vitu vyake na kumsogelea Roma na kumpa ishara ya kumfuata.
“Bado tu unataka kubakia hapa?”Aliuliza Dorisi na Roma alijikuta moyo wake ukijinyonga, katika mazingita kama hayo kama angeonyesha kusita sita ingewafanya kujisikia vibaya zaidi hivyo aliuvaa ujasiri na kisha akawashika mkono na kuondoka nao.
“Tutaenda kwenye hoteli yoyote, na nitawaruhusu mywe bia hadi mlewe mpunguze mawazo , mnaonaje?”Aliongea Roma na wote walitingisha kichwa na kuondoka.
Roma alifanya kama alivyowaambia na aliwapeleka katikati ya jiji na kisha akawaagizia chakula pamoja na vilevi na siku hio Dorisi na Nasra walikichafua haswa kiasi kwamba walilewa chakali.
Baada ya kuelwa wote hakuna ambaye alitaka kuondoka na Nasra na Dorisi wote walitaka kulala hotelini na Roma licha ya kwamba ilikuwa mchana bado.
Roma mara baada ya kujifikiria kidogo aliona awape kile walichotaka na palepale alienda kuchukua chumba na kisha aliwabeba wote kwa pamoja na ulevi wao na kuwabwaga kitandani na kupiga Treesome ya nguvu kwa muda mrefu na mpaka anakuja kumaliza wote walionekana kutosheka na bakora za kimkakati na waliishia kukumbatiana na kisha wakapitiwa na usingizi.
Roma alijikuta akitingisha kichwa na palepale aliangalia saa na kuona ni saa kumi na moja kuelekea saa kumi na mbili.
Ijapokuwa Edna alionekana alikuwa amebadilika nje kabisa ya mategemeo yake lakini hakutaka kupitisha hio siku bila ya kuongea nae , hivyo aliingia bafuni na kuoga na kisha akavaa na kuwaacha.
Kwa spidi aliotumia kuendesha ilimchukua dakika chache tu kufika Ununio na ile anaingia katika barabara ya Ununio Road aliweza kuona gari ya Edna kwa mbele akionekana ndio anarudi kazini.
Dakika chache tu gari iliweza kuruhusiwa kuingia ndani ya geti tena kilichomshangaza zaidi Roma ni kwamba ijapokuwa geti lilikuwa likijifungua lenyewe lakini lilifunguliwa ‘Manual’ tena aliefungua ni Lanlan ambaye pembeni yake alikuwa amesimama Bi Wema.
Roma hakujisumbua kuingiza gari ndani kwani alitoka palepale na kukimbilia ndani,.
“Edna subiri”Aliongea Roma mara baada ya Edna kutoka nje ya gari baada ya kuliegesha lakini ni kama hajamsikia Roma.
Lanlan ambaye alikuwa ndio anamalizia kufunga geti alijikuta akitoa tabasamu la furaha na kuanza kumkimbilia mama yake kwa shangwe huku akimwita Mama.. Mamaaa..
Edna mara baada ya kuitwa vile alisimama na ksiha akamgeukia Lanlan na kumwangali kama vile hamjui.
“Umemuita Mama mtu asiesahihi , mimi sio mama yako”Aliongea kwa Kingereza huku akimtoa Lanlan mikono ambayo imemshikilia.
Kitendo cha Edna kumwambia Lanlan vile kilimfanya kumwangalia kwa macho ya kutia huruma na palepale aliishia kuchuchumaa na kuanza kudondosha machozi chini.
Roma alietaka kuongea tena alijikuta mdomo wake ukiishia hewani na hasira zilimpanda mara baada ya kumuona binti yake akilia.
Lanlan alikuwa na furaha ya kumuona mama yake kwa mara nyingine na hata ujio wake hapo ni kutokana na kujua huo ndio muda wa kurudi kazini lakini jibu la Edna lilimnyong’onyesha , alikuwa ni kama vile amemwagiwa ndoo ya maji ya baridi.
Roma alikubali Edna kumchukia yeye lakini alijiuliza kwanini anamfanyia hivyo na Lanlan ambaye anamchukulia kama mama, uvumilivu palepale ulianza kumpotea.
“Edna naona sasa unavuka mpaka”Aliongea Roma kwa namna ya kufoka huku akimpakata Lanlan na kumfanya machozi yake yaloanishe kifua chake
“Mommy doesn’t want Lanlan again …Mommy doesn’t like me anymore..”Aliongea Lanlan akilia akisema kwamba mama hamtaki tena na mama yake hampendi.
Kilio cha Lanlan kiligusa moyo wa Bi Wema na alijikuta akimsogelea Edna na kumwangalia usoni.
“Edna unafanya nini , huwezi kutolea hasira zako kwa mtoto kisa tu mna ugomvi”Aliongea Bi Wema na palepale alimsogelea Lanlan kwa jaili ya kumtuliza lakini ilikuwa ngumu kutulia.
Lanlani alikuwa na kumbbukumbu za kuachwa na mama yake kwa mara ya kwanza hivyo hicho kinachotokea ni kama alikifananisha na kumbukumbu zake mbaya zilizopita ndio maana kilio hakikiwa cha kawaida.
“Bi Wema mimi sitaki kuhusika nao tena , huyo ni mtoto wake na sisi tumeachana, ni kwamba tu hatujasainishiana maswala ya talaka kwani kuna taratibu za kuchukua”Aliongea
Roma alikuwa akitetemeka kwa hasira mno kutokana na kilio cha Lanlan na alijihisi ni kama ule uchizi wake wa siku nyingi unaanza kumvaa.
“Edna ,,, unaweza kunichukia utakavyo na sitolaumu lakini umemuumiza binti yangu kihisia ,, na hii ni sababu ambayo inanifanya nitake kukua sasa hivi..”
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR
WATSAPP:0687151346.

Mono no aware.


SEHEMU YA 655
Bi Wema licha ya kwamba alikuwa na hali ya kutoridhishwa na tabia ya Edna kutolea hasira zake kwa Lanlan lakini hakutaka kumuona akidhulika kwa namna yoyote ile mara baada ya kusikia kauli ya Roma kwamba anataka kumuua.
“Hapana Mr , usiwe mwepesi hivyo , Edna anakufanyia makusudi tu”Aliongea Bi Wema kumtuliza Roma, hakujua kama Roma alikua kwenye hali isiokuwa ya kawaida kwani haikuwa swala tu la kuchanganywa na Edna kwa kukosa huruma lakini kilio cha Lanlan kilikuwa ni pigo lingine ambalo liliathiri moyo wake.
Watu wawili muhimu kwenye maisha yake waliweza kumpa pigo katika akili yake, ilikuwa ni kama vile hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kuziba shimo ambalo limejitengeneza katika moyo wake.
Muda huo akili yake ilikuwa katika hali hatarishi ya kuweza kumezwa na nguvu ya roho ya mnyama iliokuwa ndani yake , ni kama ilichukulia wakati huo ambao hakuwa sawa kiakili kutaka kujaribu bahati ya kuutawala mwili wa Roma.
Roma uwezo wake wa kujidhibiti ulikuwa umepungua kutokana na hali aliokuwa nayo ndio maana alisema anataka kumuua Edna licha ya kwamba hakuwa akidhamiria kufanya hivyo.
Nia ya roho ya kipepo ya mnyama ilikuwa wazi kabisa kile ambacho ilikuwa ikitaka kufanya, ilikuwa ikimsukuma Roma kumuua Edna ili baada ya hapo Roma awe kwenye majonzi makubwa na mwisho wa siku kukosa mhimili na kuchukua mwili wake.
Roho ya kipepo ya mnyama huyo mpango wake ilikuwa ni kuiba uwezo wa kijini wa Roma na baada ya hapo kutawala akili yake na kurudi hai tena kwa kuua roho ya kibinadamu ya Roma na ndio ingekuwa mwisho wa kuishi katika gereza la Cauldron.
Roma akili yake ilicheza haraka sana na kuona roho hio inachotaka kukifanya na alijitahidi kukunja ngumi pamoja na kung’ata meno kwa nguvu kujizuia akili yake isimpotee.
Hakuwa akishindana na Edna bali alikuwa akishindana yeye mwenyewe na Edna hakuwa akilijua hilo, pengine angekuwa na uelewa angepunguza jeuri.
“Unadhani naogopa kufa , kama ningekuwa naogopa nisingeomba Talaka”Aliongea Edna kijeuri.
“Wewe…
Roma alikuwa akipambana na akili yake na maneno yake ni kama yalikuwa yakimsaidia zaidi roho iliokuwa ndani yake kushinda , ijapokuwa asingeweza kumuua lakini hakutaka kujizuia kumpiga kibao.
Lakini kabla hajamkaribia tu Lanlan alianza kumpigia makelele kumtaka asimpige mama yake.
“Daddy don’t hit mommy , Don’t hit her”
Sauti ya Lanlan iliokuwa kali kwenye masikio yake ni kama neno la upako katika akili ya Roma kwani palepale aliweza kuidhibiti akili yake na kuiweza nguvu ya mnyama wa maafa.
Uhusiano wa mtoto na baba katika ulimwengu wa kiroho siku zote unakuwa na nguvu mno , nguvu ya kuweza hata kushinda roho za giza na hiki ndio kilichotokea , sauti ya Lanlan ni kama maneno ya kichungaji au kishekhe.
Katika maisha unahitajika kuwa na sababu kubwa ya kuweza kukupa motisha ya kuendelea kuishi hivyo Roma mara baada ya kuisikia sauti ya Lanlan ni kama ukumbusho kwake kwamba ana mtoto wa kumlea.
“Lanlan hakuwa mtoto mzuri….Lanlan hatakuja kumtafuta mama tena”Lanlan aliongea huku akifuta makamasi yaliochaanganyika na machozi huku akimwangalia Edna kwa mara ya mwisho na kisha kukificha kichwa chake asimuone tena.
Kauli ya Lanlan ilimpa Roma uchungu mwingi moyoni lakini hakuwa na la kufanya, angewezaje kumpiga Edna mbele ya mtoto wake.
“Ninaenda kupumzika ndani kama huna kingine cha kuongea , nipo bize”Aliongea Edna huku akibana vizuri mkoba wake kwapani.
“Subiri..”
Roma hakutaka kumruhusu kuondoka kirahisi , alikuwa bize kushindana na mnyama wa maafa hivyo hakuweza kupata muda wa kuuliza maswali.
“Edna , unasababu yoyote … siamini kama unaweza kuwa mkatili hivi , kama unasababbu kwanini usiniambie , tumepitia magumu mengi pamoja , hivi huamini uwezo wangu , kwanini tusikae chini tukaongea hili likaisha kama wanandoa ?”Roma alongea akiwa katika hali ya matarajio ya jibu la Edna.
Bi Wema hata yeye aliona alichoongea Rioma ni sahihi na kutamani Edna kuurudisha moyo nyuma na kuyamaliza.
Kama kawaida Edna alimwangalia Roma kwa sura ya kejeli huku akitoa tabasamu la kuchukiza.
“Acha kuwa kichekesho, mkataba wangu wa ndoa na wewe ushaisha na sasa nafanya ninachotaka”
“Siamini kama umebadilika hivi ghafla tu”
“Kama unataka tuendelee kua pamoja sawa , lakini lazima nikwambie ukweli hapa hapa uelewe , ni aidha unichague mimi au binti yako”Aliongea akiwa siriasi kabisa.
Roma na Bi Wema walijikuta wakibumg’aa , hakuna ambaye aliweza kuamini masikio yake kama yamesikia vizuri , yaani Edna anamwambia Roma kwamba achague kuishi na Lanlan au amuache aishi na yeye.
“Hapana huyu ni mtoto pekee wa Seventeen na pia ni binti yangu , nawezaje kumuacha ?”
“Kama ni hivyo kesi imeisha ..”Aliongea huku akimwangalia kwa tabasamu la kumdhihakki
“Nina weza kukubaliana na michepuko wako kwasababu hawana uwezo wa kushindana na mimi na ninajiamini, lakini siwezi kukubali kushindania penzi na mwanamke aliekufa ukijumlisha na mtoto alieacha .. kila saa ninapomfikiria Lanlan ninajihisi ni kama vile namuona huyo mwanamke pembeni yako , hata kama umesema mimi sio mbadala wake lakini kwangu nakuona kama mnafiki tu , kuendelea kumuona mbele yangu ni kama tusi kwangu na najihisi kama vile ndoa yetu ni kichekesho kiasi cha kunipatia maumivu makali ambayo sijawahi kuyapitia hapo kabla , maadam huyo mtoto atakapoendelea kuwa na wewe huwezi kumsahau Seventeen kwasababu ndio mwanamke ambaye unampenda sana, mwanamke ambaye ameweza kukuzalia mtoto”
Maneno ya Edna yalikuwa makali mno kuyasikia , ni kama yalikuwa yakiurarua moyo wake.
Alishindwa kuamini ni kweli kwake akimuona Lanlan alikuwa akijisikia kama anateswa kwasababu tu ya Seventeen.
Dakika hio Roma alijiuliza je lilikuwa kosa kumtambua Lanlan kama binti yake kwa kumzaa lakini aliona bado alikuwa sahihi asingemfanya Lanlan kutambulika kama mtoto wa kuasili ilihali yeye ni baba yake mzazi, isingekuwa haki.
“Nadhani tamaa yangu imeniponza , upo sahihi , sijui kama nakupenda sana wewe kuliko Seventeen lakini jambo moja ambalo nina uhakika nalo ni kwamba siwezi kumuacha mtoto wangu kwa namna yoyote ile”
“Ni afadhali umelitambua hilo kwaheri”Aliongea na kisha aliingia ndani bila ya kuangalia nyuma.
“Mr hakuna chochote kingine ambacho unaweza kufanya?”Aliuliza Bi Wema ambaye alikuwa kwenye majonzi.
“Bi Wema najua wasiwasi wako na unahitaji hili liishe lakini nakuomba usiwe na huzuni , unapaswa kuwa na furaha kwa ajili ya Rufi”
“Kwanini niwe na furaha kwenye hali kama hii , hata Rufi mwenyewe hawezi kukubali wewe kuachana na Edna”Aliongea
“Bi Wema nadhani ni muda sahihi kumuacha sasa aende , ni makosa kuendelea kubakia hapa na kumsumbua, isitoshe ndoa yetu imeanza na sintofahamu nyingi , ni kama wakati unapofundishwa kuendesha baiskeli kwa mara ya kwanza unaambiwa unapaswa kugeukia upande unaotaka kudondokea na sio upande mwingine , hivyo ninachoweza kufanya kwasasa ni kuendana na hali ilivyo tofauti ya kuwa king’ang’anizi wa kubadilisha mueleko wa hali , Edna anaweza kunidharau kwa kumchagua binti yangu na kumuacha yeye, anaweza kutokuwa sawa japo siwezi kuona lakini ninachojua hana rafiki wa kuongea nae , naomba umsikilize kile ambacho ataongea , kama akilia msaidie kufuta machozi, kama ataniongelea vibaya muunge mkono , kama akikuuliza nimekuambia chochote naomba umwambie …’ I am sorry’ kwa kila kitu”Aliongea Roma na maneno yake pamoja na muonekano wake vilimfanya Bi Wema na utu uzima wake kushindwa kujizuia kutoa machozi kwani Roma alikuwa akitia huruma.
“Edna anachofanya ni utoto , kitu muhimu kuwafanya wenza kudumu ni upendo , ujuaji una athari ya vitu vingi”
“Kila mtu ni tofauti Bi Wema..”Aliongea Roma na muda huo huo macho yake yaligeukia upande wa getini nje mara baada ya kuona gari aina ya Bentley ikisimamishwa na akili ya Roma haraka haraa ilimwambia huyo lazima atakuwa ni Maimuna kwani alikuwa na miadi nae ya kukutana siku hio.
“Bi Wema kuna sehemu napaswa kwenda , naomba unisaidie kumpeleka Lanlan nyumbani kwa Nasra na umwambie Qian Xi kwenda nae mgahawanni kumnunulia chochote anachotaka maana Nasra hatorudi”Aliongea Roma huku akimkabidhi kwa Bi Wema.
Dakika hio hio Maimuna aliweza kusimamisha gari nje ya geti ambalo halikuwa limefungwa vizuri na kutoka nje ya gari na kuingia ndani kabla hata hajakaribishwa.
Alikuwa amevalia gauni refu rangi nyekundu na kikoti cha rangi nyeusi juu yake , nywele zake hakuwa amezifunga zaidi ya kuzichana kuzirudisha nyuma na miondoko yake ilikuwa ile ya kushawishi macho ya watu kumwangalia.
Baada ya kuingia ndani aliweza kumuona Lanlan na Bi Wema ambao wote walikuwa na dalili ya kulia na kuonyesha mshangao kwa sekunde lakini dakika ileile aliupotzea kwa kuupamba uso wake na tabasamu na kisha alimkimbilia Roma na kwenda kujirusha kwenye mikono yake , kwa jinsi ambavyo aliweza kujikumbatisha kwa Roma ni kama vile alishawahi kufanya hivyo mwanzo.
Roma aliweza kunusa harufu kali ya marashi ya kuvutia kutoka kwa mwanamke huyo na ukweli alishindwa kumkwepa ndani ya muda na kuishia kushika ngozi yake laini , ilikuwa ni kwasababu hakumtegemea kama angekuja kumkumbatia.
Roma ile anataka kujitoa kwake palepale alipitisha mikono yake kwenye shingo huku miguu yake akiipitisha kwenye kiuno cha Roma na kuning’inia kama mtoto mdogo, alienda mbali zaidi na kusugua manyonyo yake yaliosimama katika kifua cha Roma.
Mrembo huyu hakujali sehemu hio ni nyumbani na Edna alikuwepo , ilikuwa ni kama vile alikuwa akifanya makusudi.
Roma jambo lile lilimshangaza na kujiuliza huyu mwanamke anafanya nini , kwanini anafanya haya yote ghafla tu.
“Hehe… Roma huyo ndio binti yako ? She is cute”Aliongea huku akimwangalia Lanlan kwa tabasamu.,
Bi Wema alikuwa kwenye mshituko mara baada ya kumuona mwanamke mrembo kama huyo ambaye hakuwa akimjua akimkumbatia Roma kama vile wanafahamiana na aliishia kumwangalia Roma kwa maswali mengi.
Roma alijikuta akijisikia vibaya kutokana na kitendo hicho kwani pia alikosa maelezo ya kutosha ya kujielezea na aliihisa kujitoa katika mwili wa Maimuna.
“Sidhani kama tuna ukaribu wowote” Aliongea Roma akijaribu kuweka usiriasi kwenye uso wake kutokana na kutokuwa kwenye mudi nzuri lakini maneno yake ya moja kwa moja hayakumuathiri Maimuna.
“Najua jina lake anaitwa Lanlan Ramoni Kweka, ana jina zuri mno , linaendana na muonekano wake”Aliongea na kumfanya Roma kukunja ndita.
“Inaonekana umefanya utafiti wa kutosha”
“Sio vibaya kujua maisha ya mwanaume ninaemtamani”Aliongea huku akimkonyeza Lanlan .
“Acha maneno mengi , nipeleke kwenye hio sherehe”
“Tunaenda babu lakini haina haja ya kuharakisha ..”Aliongea na palepale alitoa Bracelet(bangiri ) ya Dhahabu ambayo juu yake ilikuwa imetengenezewa ua la kumeta meta la madini ya rangi ya Samawi, ilikuwa ni Bracelet ya ajabu mno kuangalia na mwanga wa jua linalozama uliifanya kuwaka wake pale mbele.
Baada ya kuishikilia mkononi alimsogelea Lanlan huku akiwa na tabasamu na kumpa ishara ya kupotkea.
“Lanlan hii ni zawadi yangu kwako”
Hata kama alikuwa ni mdogo lazima angejua kitu kilichokuwa mbele yake kilikuwa kizuri na cha thamani na pengine mtoto yoyote asingekataa lakini kwa Maimuna ilionekana ni kosa alilofanya mbele ya Lanlan.
Zawadi yake hio pengine kwa watoto wa kike wa kawaida wangeipokea lakini ilikuwa ni tofauti kwa Lanlan ambaye alishazoea kuona vitu vizuri kama hiyo hususani alikuwa akiona Bracelet ya Almasi ya Nasra ambayo alikuwa akivaa na pia Edna alikuwa akimiliki jiwe kubwa la madini ya Rubi ambalo alipewa na Roma baada ya kutoka ulimwengu wa maijini pepo.
“Its not tasty , I don’t want it”Aliongea huku akigeuzia kichwa chake pembeni akionyesha ishara ya kutotaka kabisa hata kumwangalia.
Tabasamu lote ambalo lilikuwa limeupamba uso wa Maimuma lilipotea palepale na kubakia kuwa katika mshangao.
Alijiambia inakuwaje zawadi yake isiwe tamu , kwani hiko ni chakula.
Alijiambia hakika mtoto wa kichaa ni kichaa vilevile.
Bi Wema alijikuta akifurahishwa na jambo lile na alitatami kucheka na aliishia kukakamaa mwili kujizuia mbele ya mgeni.
Roma pia alitamani kucheka lakini hakutaka kucheka kwani angeharibu taswira yake , lakini hata hivyo ili kumuonyesha kama Lanlan amefanya jambo la maana palepale aliigiza kama anaingiza mkono mfukoni na alipoibuka alitoka na jiwe lingine la Yakuti ambalo alitoka nalo katika ulimwengu wa majini pepo.
“Yaani unatumia hio takataka yako kutaka kumhonga mtoto wangu , inaonekana familia yenu ya Sharif sio matajiri kama nilivyoambiwa”Aloiongea Roma huku akihakikisha Maimuna anaona lile jiwe la kung’aa sana na kupendeza , kwani alilipitisha taratibu taratibu kama vile yupo kwenye slow motion.
“Lanlan binti yangu ninaekupenda hili jiwe zuri ni kwa ajili yako , Daddy anatoka leo hivyo kuwa mtoto mzuri na kaa nyumbani na aunt Qiang sawa, utaenda nae mgahawani kula chakula chakula cha usiku sawa”Aliongea Roma
Lanlan alijikuta akitoa meno yake madogo huku akitoa kicheko wakati wa kupokea jiwe la thamani , lilikuwa dogo kuliko la mama yake lakini alipenda rangi yake.
Maimuna macho yake yalikuwa kodo kwenye jiwe hilo la ajabu ambalo ni kama vile ni mara yake ya kwanza kuliona .
Alijiambia mbona jiwe hilo ni kubwa hivyo …My goodness ,, the purity and size it would’ve cost 50 million dollar on the Market and he just gave it to a kid as a toy!?
Maimuna hakutaka kuamini , ijapokuwa alijua familia ya Roma ilikuwa na uwezo mkubwa ndani ya taifa hili lakini nguvu yake kubwa ilikuwa ni kwenye maswala ya kijeshi tu na sio maswala ya utajiri., kitu pekee ambacho aliona pengine hakuwa akikijua basi ni Roma wenyewe ndio tajiri,
Maimuna alijikuta aking’ata lipsi zake huku kijasho chembamba kikianza kumtoka , alijiambia pengine hakuwa akimjua Roma vizuri .
Alijiambia pengine alichokuwa akikijua ni kidogo sana kuliko kile ambacho alikuwa akimjua nacho na jambo hilo lilimfanya kumpenda na kumchukia kwa wakati mmoja.
Kwa mwanamke kama huyo hakuwa na matamanio na mwanaume wa kawaida anaetokea katika familia yenye utajiri mkubwa lakini asingeweza kujizuia kutoka kimapenzi na mwanaume wa ajabu na kushangaza kama Roma.
Utajiri na madaraka ni vitu vya juu juu na kitu cha kutamanika zaidi ni nguvu halisi pamoja na haiba ya mwanaume ilivyo.
Hata hivyo hakutaka kujilaumu kwani babu yake mwenyewe hakuwa na taarifa zote kumuhusu Roma nje ya nchi.
Inasemekana kwamba licha ya familia ya Mzee Sharif kuabudu majini ambayo ni chanzo cha utajiri wao lakini pia walikuwa na uhusiano wa karibu na jamii za siri kama vile Freemason na walikuwa wakishirikiana kwenye mambo wanayoendana nayo sambamba ki ajenda.
Familia hio haikuwa na ukubwa kwama wa familia ya Rothchild ambayo ilikuwa ipo kila kona ya dunia lakini walikuwa wamejitengenezea sehemu yao ndani ya dunia.
Maimuna alijua pengine ndio maana Afande Kweka alitangaza kilichotokea aadhibiwe Roma mwenyewe , lakini akiwa na uhakika kwamba Roma ana nguvu ya kushinda.
“Huna ubahili wa aina yoyote … vipi tunaweza kuondoka”Aliongea Maimuna huku awamu hii akiwa mpole lakini hakuacha kutaka kujigusisha na Roma.
Roma alijiambia sjui huyo mwanamke ana kiu ya mwanaume ndio maana matendo yake yapo hivyo au ni nini.
Baadaa ya kumuaga Bi Wema na Lanlan Roma alitoka na kuingia ndani ya gari.
Upande wa Maimuna kabla hata hajaingia ndani ya gari aligeuza shingo yake ndefu na kuangalia nyumba hio na kisha akatoa tabasamu la kejeli.
Baada ya kuingia hatimae gari iliweza kutoka eneo hilo kuelekea katika hoteli ya Wache ambayo ilikuwa Kigamboni.
Asichokijua Roma ni kwamba mara baada ya gari yao kuondoka pazia la dirisha katika Floor ya pili lilionekana kufungwa vizuri na Edna ambaye alikuwa akichungulia.

SEHEMU YA 656.
Ni ndani ya jumba moja la kifahari ambalo lilikuwa lipo Kawe , jumba hilo siku hio lilionekana kuwa na ulinzi mkali kuliko siku zote.
Hio ni moja wapo ya nyumba ambayo mmiliki wake ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Senga Cammilius Kweka , ilikuwa ndio nyumba yake ya mapumziko mara nyingi anapokuwa ndan ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya maswala ya kikazi,
Siku hii ndani ya nyumba hio kulikuwa na ugeni kwani mheshimiwa alikuwa akitarajiwa kufika hapo muda wa jioni ya saa moja usiku.
Ijapokuwa wengi waliamini Raisi Senga anafika hapo kwa ajili ya mapumziko kama kawaida yake lakini ukweli ni kwamba alikuwa na miadi ya kukutana na mtu kwa ajili ya kufanya kikao cha siri.
Raisi Senga hakuwa akiamini eneo la Ikulu hata mara moja mathalani kwa wale watu ambao wanamlinda ndio maana kila linapotokea swala nyeti sana ambalo linahitaji usiri mkubwa mara nyingi angesafiri kwenda mikoani kwenye ikulu ndogo au angetoa kisingizio cha kwenda kupumzika katika nyumba yake hio , huku akihakikisha watu anao ambatana nao ni wachache tu wale ambao alikuwa akiwaamini.
Saa moja kamili gari kadhaa za rangi nyeusi za brandi tofauti tofauti zilionekana zikiingia ndani ya jengo hilo.
Uzuri wa mazingira ya eneo hilo yalikuwa yametengena sana na maeneo ya makazi ya uswahilini ya watu hivyo ni watu wachache sana ambao walikuwa wameshuhudia gari hizo.
Baada ya saa moja kupita baada ya gari hizo kuingia hatimae ilionekan gari nyingine ikiingia ndani ya hilo eneo , gari hio ilikuwa ni gari aina ya Aud SUV rangi nyeusi.
Baada ya kusimama eneo la getini kwa dakika kama tano hatimae gari ile iliweza kuruhusiwa kuingia ndani.
Baada ya kuingia ndani hatimae aliweza kuonekana mwanadada Suzzane na Nadia Alfonso wakishuka.
Wote kwa pamoja walikuwa wamevalia mavazi ya suti zinazofanana za rangi nyeusi na walionekana kama vile ni wanausalama.
Suzzane ndio ambaye alionekana kidogo kuwa na wasiwasi lakini kwa upande wa Nadia Alfonso hakuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi , pengine ni kutoana na uzoefu wake.
Baada ya kushuka hawakuacha kukaguliwa na walinzi na kisha dakika chache alitokea Kabwe msaidizi wa karibu zaidi wa raisi kaatika kitengo cha ndani cha siri cha raisi na kuwapokea.
Kabwe mara baada ya kusalimiana nao kwa ufupi aliwapa ishsara ya kumfuata huku yeye akitangulia kuelekea mbele.
Mazingira ya eneo hili hakika yalikuwa yakivutia mno , ni sahihi kusema eneo hilo ni maalumu kwa ajili ya mapumziko kwani lilikuwa limejengwa kwa ufanisi mzuri mno , mtu yoyote ambaye angefika hapo lazima angesema ni ufahari wa juu sana kuwa raisi wa nchi.
Lakini upande mwingine kama kauli hio angeisikia Raisi Senga pengine angepingana nayo , kwani kuwa raisi kwake alichukulia ni kama swala la kujitoa, ni kweli kuna faida zitokanazo na uraisi lakini baadhi ya siri ambazo anazibeba kwa ajili ya taifa zilikuwa kubwa mno ambazo zilihitaji akili yenye utimamu mkubwa.
Nadia alimwangalia Suzzane kwa ishara ya kumwambia kwamba anapaswa kujiamini na kisha waliendelea kusonga mbele.
Ukweli ni kwamba mwanzoni Suzzane ndio alipanga kuja kuonana na Raisi Senga peke yake lakini maagizo tofauti yalikuja yakimtaka Nadia kuhusika katika maongezi hayo ili kuweza kumshawishi Raisi Senga kwa namna yoyote ile kuweza kujiunga na umoja wa Ant Illuminat.
“Mheshimiwa Wageni wamekwisha kufika”Aliongea Kabwe mara baada ya kuingia katika eneo la sebule yenye samani za kuvutia.
Mheshimiwa Raisi alionekana kuongea na simu na kadri alivyokuwa akiongea sura yake ilizidi kujikunja na palepale hasira ilimvaa.
******
Wache Grand Hotel ilikuwa imejengwa juu ya kilima , mwanzoni mwanzilishi wa eneo hilo alihitaji kujenga nyumba za makazi kwa ajili ya biashara lakini kutokana na mazingira ya muinuko aliona ni gharama zaidi kuliko eneo la tambarare hivyo hoteli hio ndio ikajengwa.
Hoteli hio ilinufaika kwa kuwa juu ya kilima hivyo kufanya kuweza kutengeneza mandhari mazuri ya bahari huku ikizungukwa na msitu wa miti.
Unaweza kusema hili ndio eneo pekee ambalo ndani ya kigamboni halijaguswa wala kukaliwa na raia wa kawaida, ni eneo ambalo pia limeuzwa kwa Mzee Sharif kwa ajili ya ujenzi hivyo unaweza kusema kwamba hoteli hio ya Wache ni moja ya hoteli ambazo zimejitenga sana katika mji huo wa Kigamboni.
Roma alishawahi kuona kibao cha hoteli hio lakini ukweli ni kwamba hakuwahi kufika ndani ya hoteli hio kabisa na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kujua kumbe eneo hilo lote lilikuwa likimilikiwana familia hio ya Mzee Sharif.
Roma mara baada ya kufika ndani ya eneo la hoteli hio ya nyota tano aliweza kuona sehemu zaidi ya mia moja za kuegeshea magari lakini katika sehemu hizo ni ishirini pekee ambazo zilikuwa zimechukuliwa.
“Kulingana na magari haya naamini kuna watu zaidi ya ishirini huko ndani”Aliongea Roma.
“ Hupaswi kuanza kujutia sasa hivi kuja hapa , vipi umeguswa kwa familia yetu kukuandalia sherehe?”Aliuliza Maimuna na kumfanya Roma kutingisha mabega , alikuwa akitegemea jambo la namna hio , isitoshe familia hio mara nyingi ilikuwa ikilinda siri zao hivyo mambo yao yalikuwa yakiendeshwa kisiri siri hivyo alikuwa amejipanga kuja kukutana na watu wasiokuwa wa kawaida katika eneo hilo.
Yaani kwa kwa haraka haraka ni kwamba hoteli nzima ilionyesha kutokuwa na wageni wengine zaidi ya familia ya Sharif pekee.
Dakika ileile anatoka kwenye gari kabla hata hajapiga hatua kuingia ndani ghafla tu aliweza kushuhudia wanaume wawili waliovalia majoho ya rangi nyeupe wakiibukia kutoka pande mbili tofauti kwa namna ya kupaa, walikuwa katika umri wa miaka arobaini na hamsini kimakadirio huku wakiwa na vipara pamoja na masharupu mengi usoni.
Walikuwa na macho makali ambayo hayakuwa ya kawaida , licha ya Roma kutokuwa na uwezo wa kutumia uwezo wake wa kijini akili yake ilishamwambia hao sio binadamu wa kawaida, walikuwa na muonekano wa kiarabu lakini kwake aliwaona kama sio waarabu.
Roma moja kwa moja aliamini pengine watakuwa katika levo ya kuipita dhiki katika mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi au mafunzo ya kijini.
“Acha kukodoa macho wewe mjjinga”Aliongea jini Imrah ambaye alitokea ndani na Roma alimkumbuka vyema kwani alipambana nae kule Kilimanjaro.
“Jinni Marid na Jinn Iftir wapo hapa kwa ajili ya kukuangalia na wote wapo katika levo ya kuipita dhiki wakiwa na uwezo wa kudhibiti moto wa rangi tatu , watahakikisha huondoki hapa kwa namna yoyote”Aliongea .
Roma alijikuta akishangazwa na kauli ya Jinn Imrah , hakutegemea angeweza kukutana ndani eneo hilo na watu wa levo ya juu katika mafunzo ya kijini.
Roma alijiuliza inakuwaje hii familia ikawa na uhusiano mkubwa na viumbe hawa wa kijini kiasi cha kuweza kuita watu wenye uwezo wa juu namna hio ndani ya muda mfupi.
“Acheni kusimama hapo , wewe mlete huyo ndani anasubiriwa”Aliongea akimpa amri mtoto wake wa kike kumwingiza Roma ndani ya hoteli.
Maimuna aliishia kumwagalia Roma kwa tabasamu huku akimpa ishara ya kutembea kuingia ndani.
“Ukoo wenu hauendeshwi kulingana na nani mwenye nguvu zaidi si ndio?””
“Kwanini unauliza hivyo?”
“Jinn Iftiri na Marid wana nguvu kubwa za kijini kuliko Imrah lakini bado tu wanaonekana kusikiliza maagizo yake”Aliongea Roma na kumfanya Maimuna kutabasamu.
“Mr Roma tatizo unatuchukulia poa , yule Master Iftir na Maridi wote ni washirika kutoka matawi yaliopo katika nchi kadhaa , ukizungumzia swala la madaraka Imrah ana madaraka makubwa kuliko wao , wapo watu wenye nguvu za kijini wengi sana pamoja na majini wenyewe na ni wengi kiasi kwamba hata babu mwenyewe hajui idadi yao”
“Unajaribbu kuniogopesha?, kama ni hivyo si mngeweza kutawala hii nchi?”
“Hatuna haja ya kukutisha kwani tuna nguvu ya kukushinda na kuhusu unachokisema kuhusu kutawala taifa hio ni nje ya sheria za kijini, nguvu yetu ipo katika maswala ya nguvu isioonekana tu”Aliuongea kwa kujiamini
Roma mara baada ya kuingia kabisa ndani ya Korido ya hoteli hio aliweza kukutana na mabodigadi waliokuwa wakilinda, ilimshangaza Roma kwani eneo hilo lilikuwa na ulinzi mkali kama vile kuna kiongozi mkubwa wa dunia aliekuwa yupo katika eneo hilo.
Kwa haraka haraka tu Roma aliweza kuamini mabodigadi hao wapo katika levo za chini za mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi na mbaya zote wote walikuwa ni Waraanbu tupu.
Ilionekana dhahiri kabisa familia hio ilikuwa imeandaa maandalizi makubwa ya kutaka kumdhibiti.
Ukiachana na ulinzi mkali hoteli hio ilikuwa na mazingira ya kuvutia mno , kuna hisia zilimwambia Roma pengine hii hoteli haipo wazi kwa kila mgeni ambaye anataka kuja kupumzika ndani ya eneo hilo.
Hisia za Roma zilikuwa sahihi , tokea ujenzi wa hoteli hio kukamilika hakuna Mtanzania wa kawaida ambaye alishawahi kwenda kulala ni watu wachache sana ambao walikuwa wakijua hata muoenekano wake kwani eneo hilo lilikuwa na ulinzi mkali sana kuanzia getini mwanzoni kabisa wa kuingia kwenye eneo hilo mpaka upande wa Fukwe.
Inasemekana kwamba katika vipindi flanni vya mwaka waarabu wengi pamoja na wahindi huonekana wakiingia ndani ya hoteli hio na hata mpaka leo hoteli hio iliaminika kama hoteli ya Waraabu kwani ndio ngozi pekee ambazo zilikuwa zikifika hapo.Lilikuwa kama eneo mbadala tofauti na lile la kule Kilimanjaro
Pengine ni sahihi kuiita Hoteli ya Majini kwani viumbe ambavyo vinafika hapo havikuwa vya kawaida, aidha ni binadamu mwenye nguvu za kijini au majini yenyewe.
Sasa jambo ambalo Roma hakuwa akilijua ni kwamba kulikuwa na ulimwengu wa majini lakini alishindwa kuelewa huyu Mzee Sharif yeye anatokea katika koo ipi ya kijini na alichosalia ni hao majini au kuna kingine zaidi ya kile anachokidhania.
Roma mara baada ya kuingizwa katika ukumbi mkubwa hatimae sasa aliweza kuona sura za watu tofauti tofauti wengi ambao walikuwa wameketi kwenye Zuria la kuvutia huku katikati yao kukiwa na kifaa flani ambacho Roma hata hakuelewa maana yake ila kilikuwa kikitoa moshi wa pink wenye harufu flani ambayo hakuweza kuielewa.
Sura zote zilikuwa ni nyeupe tupu huku kila mmoja akiwa na ndevu nyingi na masharubu, kuna ambao Roma alikuwa akiwahafamu kwani alishawaona lakini kuna wengine ambao hakuwa akiwafahamu kwani sura zao zilikuwa mpya, wote walikuwa wamevalia mavazi ya tamaduni za kiarabu.
Mzee Sharif alikuwa amekaa katikati kabisa kama kiongozi huku akiwa na kiremba cha rangi ya bluu kichwani, pembeni yake alikuwa ameketi jini Imrah , kushoto kwake kulikuwa na mhindu ambaye amevalia tofauti na wengine wote , yeye alikuwa amevalia joho la rangi nyeusi.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba kila mmoja alikuwa amevalia kitamaduni kasoro Maimuna peke yake ambaye amevalia kisasa zaidi lakini vazi lake likiwa la heshima.
Roma alimwangalia Mzee huyo ambaye amevalia Joho la rangi nyeusi kwa kumchunguza , alikuwa mzee zaidi kuliko Imrah mwenyewe na alikuwa amefumba macho, Roma kwa haraka haraka alijua tu huyo ndio mtu hatari zaidi hapo ndani kuliko wengine wote.
“Mrithi wa ukoo wa Kweka , hatimae tunakutana tena”Aliongea Mzee Sharif.
“Naona watu wengi wapo hapa kwa ajili ya kunikaribisha , kwanini mmejikalisha hapa kizembe tofauti na ukumbi wa chakula kuanza sherehe”Aliongea Roma huku akiwa na tabasamu kama kawaida yake.
“Acha kuigiza wakati unakiona kifo chako”Aliongea mdogo wake Maimuna afahamikae kwa jina la Meki huku akimwangalia Roma kwa kejeli.
Roma hakutaka hata kuongea nae kwani palepale alimsogelea na kisha akampiga teke na kumfanya avamie kimeza iilichokuwa na glasi pamoja na vikombe.
Hakua ambaye alitegemea hilo na walijikuta wakishangaa na kujiuliza au amekuja akiwa amelewa , kwanini ameamua kushambulia kwa kuchokozwa kidogo tu.
Yule mzee mwenye Joho jeusi hatimae aliweza kufumbua macho yake mara baada ya kusikia purukushani hio ya mtu kupigwa kiasi cha kuvamia meza.
“Unafanya nini , unadhani tunakugopa?”Aliuliza Mzee Sharif huku akionyesha hasira za wazi.
“Mjukuu wako ana mdomo mchafu sana na kama ningetaka kumuua mpaka muda huu angekuwa ni kifusi cha nyama tu , nadhani unanielewa mwenyewe”Aliongea Roma.
Meki alijikuta akimwangalia Roma kwa uchungu huku akiugulia maumivu makali.
“Meki ondoka hapa ndani”Aliamrishwa kuondoka
Mwanaume huyo mwenye jina la Meki alimwangalia Mzee Sharif kwa kuchanganyikiwa lakini aliishia kusimama na kisha akatoka nje.
“Roma hatukufanyi chochote kwasababu tunahitaji kufanya na wewe mazungumzo ya kina , hivyo jitahidi kujiuzuia”Aliongea akitoa onyo kwa uso uliokuwa na usiriasi.
“Mnataka kuongea na mimi kuhusu nini? , au ni kuhusu hazina yenu?, niwaambie mapema tu kwamba sijachukua hazina yenu na msije hata kufikiria kutaka niwaombe msamaha”Aliongea Roma lakini hata hivyo hakuna ambaye alikuwa akiamini kauli yake , kila mmoja ni kama walikuwa wakimjua anaigiza tu.
Mzee Sharif alimwangalia kwa ishara mtoto wake mkubwa na palepale alitingicha kichwa na kisha akatoka ndani ya eneo hilo na ndani ya dakika tatu waliweza kufikishwa Naibu waziri Salihi pamoja na Asha huku wakiwa na hofu zaidi mara baada ya kumuona Roma.
“Sikumfundisha vizuri mkwe wangu na mjukuu wangu na wakakuchokoza , unaweza kuwa na kinyongo juu yao na mimi nipo tayari kuwafanya wakuombe msamaha na naahidi hawatolipiza kisasi tena”Aliongea mzee huyo na kisha aliinua uso wake na kumwangalia Roma.
“Unaonaje , ninachoongea hapa nina maanisha kabisa”
“Sijali tena kuhusu wao kuomba msamaha, kama ni fidia nishajilipa kwa kuharibu makazi yenu pamoja na kuchoma jengo lenu la ibada”Aliongea Roma.
“Hakuna shida , kama ni hivyo basi ni zamu yetu”Aliongea na palepale alitoa ishara ya Skrini iliokuwa imefungwa mwishoni kabisa ukutani iwashwe.
Dakika ileile ilionekna vidio katika Tv ile na Roma alipoangalia kwa umakini alijikuta akikunja ndita bila ya kupenda.
Samweli Nguruma ambaye ni baba yake na Benadetha pamoja na mke wake ndio ambao walioneana katika hio vidio wakiwa wapo chini ya ulinzi wa wanaume ambao wameshika mitutu ya bunduki.






SEHEMU YA 658.
Katika vidio iliokuwa ikionekana kwenye skrini hio ilikuwa ikimuonyesha Samweli Nguluma akiwa amefungwa na kamba kwenye kiti huku akiwa amezibwa mdomoni, haikuwa hivyo kwake tu hata kwa mke wake pia.
Ilikuwa bahati kwamba Benadetha na kaka yake hawakuwa nyumbani wakati huo pengine na wao wangeunganishwa katika utekwaji huo .
“Kwa taarifa ambayo tumeweza kuipata ni kwama kundi la Zoa Zoa ambalo lipo chini ya Samweli Nguluma ndio waliokupatia yale mabomu ,je nimekosea?”Aliuliza na kumfanya Roma kushindwa kujibu lile swali na palepale alitoa simu yake na kutafuta namba ya Afande Jamali na kuipiga.
“Mr Roma najua hali ilivyo kwasasa”Aliongea mara tu baada ya simu ile kupokelewa.
“Unajua nini , si wewe ndio ulieniambia kwamba hakuna mtu mwingine ambaye ataweza kuguswa zaidi yangu?”
“Mr Roma sikujua ulikuw ana uhusiano na Mzee Nguluma mmiliki wa kundi la ZoaZoa , Mzee Nguluma amehusika katika maswala ya kihalifu mengi sana na kukamatwa kwake hakuathiri usalama wowote wa jamii”
“Acha kuongea ujinga , hata kama ni mhalifu haina maana kwamba anaweza kukamatwa na watu ambao sio polisi”
“Ni ,.. Hakuna maagizo yoyote ambayo nimepokea kutoka juu , hivyo hatupaswi kuingilia katika hili swala”Roma aliishia kulaani na kisha palepale alikata simu.
Roma alijiambia kutokana na kukosa uwezo wake wa kijini asingeweza kuwaokoa kwa wakati lakini pia hakutaka chochote kiwatokee kwani asingeweza kumwangalia Benadetha usoni kwani ni yeye ndio aliemhusisha baba yake licha ya kwamba mzee huyo alionyesha wasiwasi wake mwanzo.
Mabwana wote waliokuwa hapo ndani walionyesha sura za furaha kumuona namna ambavyo Roma alikuwa akiteseka.
“Unaonaje sasa, wewe ni mtu wa kukurupuka sana lakini unapaswa kuelewa hii dunia sio yako peke yako , kila mtu ana udhaifu wake, kama utatoa ushirikiano, basi tutapotezea swala la Mzee Nguluma kukusaidia mabomu lakini kama utaendelea na ukiburi wako wewe pamoja na Mzee Nguluma mtalipia gharama”
“Unataka nitoe ushirikiano gani?”Aliuliza Roma na kuwafanya wote kutoa tabasamu wakiona Roma hatimae anaenda kujisalimisha.
“Tutakupa machaguo matatu”
“Oh.. hebu yataje tuone“
Chaguo la kwanza , rudisha hazina yetu m jenga upya madhabahu yetu na kisha omba msahama miungu yetu , nadhani ushaambiwa kuhusu hilo, kuhusu chaguo la pili …”Alisita kwanza na kisha akamgeukia Maimuna na kutoa tabasamu hafifu.
“Chaguo la pili unapaswa kumuoa mjukuu wangu Maimuna Sharif na sisi kuwa wakwe zako”
Kidogo tu Roma adondoke chini kutokaa na mshituko , alitaka kujiambia hajasikia vizuri lakini baada ya kumwangalia Maimuna ambaye alikuwa akionyesha viabu vya kike alijua ni kweli kile alichosikia.
Kauli hio ilimfanya Roma kukumbuka matendo ya mrembo huyo , kumbe alikuwa akijua mpango wa mababu zake ndio maana alikuwa akijilengesha.
“Hebu kwanza tuachane na chaguo la kwanza kwani sitofuata na kuhusu chaguzi ya pili na yenyewe niseme kwamba mimi nishaoa tayari hivyo tupotezee”Aliongea Roma akikataa.
“Kwanini isiwezekane , si tayari ndoa yako na Edna imefikia ukingoni, tunajua aliondoka Iringa akiwa ameweka wazi kabisa anataka talaka mbele ya babu yako na habari hii inajulikana ndani ya familia nyingi ndani ya Dar , kama una wasiwasi na maswala ya mgawanyo wa mali sisi tutampatia kitu cha kuridhisha ili talaka yenu iwe rasmi”Aliongea Maimuna.
“Ndoa sio kama mnavyofikiria wewe, kwamba ni mambo ya kusainishana makaratasi na kufikia mwisho , uhusiano wetu hausiani na makaratasi wala ndugu ,sawa?”
“Acha kuniona mjinga , najua ameshindwa kuvumilia wanawake wako , inashangaza kwamba licha ya urembo wake ameshindwa kukulinda kama mke mpaka ukawa na wanawake wengi lakini sasa hivi anaanza kuchafua hali ya hewa , sioni kama ana stahili kuwa mmoja wa familia yenu wala kuendelea kuwa mkeo”
“Kaa kimya wewe hilo halikuhusu , hivyo acha kuongea ujinga”Alifoka Roma
“Unakasirika nini sasa , ninachokuambia ni ukweli , mimi ni mwanamke na nawajua wanawake wenzangu pia kuliko wewe , kwanini unanifokea kwa kuongea ukweli , nenda kamfokee Edna sio mimi”Aliongea na kumfanya Roma kushindwa hata amfanye nini kwani alioneana kujiamini sana.
“Eti dada ndio tuseme kwamba unataka kuolewa na mimi sana au?”
“Mimi sio dada yako unikome… , tunalingana umri ..”Aliongea huku muonekano wake ukibadilika huku kifua chake kikipanda na kushuka , alionekana kama amewezwa kuitwa dada na Roma.
Lakini hata hivyo muonekano wake wa aibu na kukasirika ulimfanya Roma kumshangaa kidogo na alijiambia pengine kama ni miaka kadhaa iliopita asingekataa mwanamke mrembo kama huyo , lakini kwa kipindi kama hicho ambacho alikuwa akitaka kurudiana na Edna kwa namna yoyote ile hakutaka kuongeza matatizo.
Isitoshe ndoa ni tofuati na kulala na kuamka pamoja hivyo Roma aliamini kama angemgusa huyo mwanamke hatua nyingine lazima ingefuata.
Upande wa Roma alijua kabisa familia hio pengine ilikuwa ikitaka kujikita zaidi ndani ya taifa la Tanzania kwa kutaka kuanzisha undugu na familia yake jambo ambalo aliona ni kichekesho.
“Mjukuu wangu sio wa kawaida , ukiachana na muonekano wake , akili pamoja na kutokuwa binadamu wa kawaida , nina wasiwasi huwezi kupata mwanamke wa aina yake maisha yako yote , unapaswa kujiona wa bahati yupo tayari kuolewa na wewe, Edna anaweza kuwa mtoto wa raisi wa Rwanda lakini bado atabakia kuwa mtoto wa nje ya ndoa , tunaweza kukusaidia kwenye mambo mengi tofauti na familia yake itakavyokusaidia , kama utamuoa Maimuna tutahakikisha familia yenu ni ya kuogopwa sio tu hapa Tanzania bali Afrika mashariki kwa ujumla , tuhakikisha tunawapa nguvu ya kuamua kiongozi wa mataifa ya Afrika mashariki awe nani na biashara nyingi zitakuwa chini yenu”AliongeaMzee Huyo.
Roma alijikuta ni kama akili yake haifanyi kazi vizuri , alijiammbia hata kama atakuja kuachana na Edna basi hawezi kuoa mwanamke mwingine.
“Inatosha , haina haja ya kumsifia mjukuu wako kwani simtamani kwa lolote”Aliongea Roma
Ukweli ni kwamba Maimuna ndio mwanamke pekee ambaye miungu ya ukoo imekumkubali kuwa kama kiongozi wa ukoo baada ya Mzee Sharif mwenyewe na walitaka kumjengea nguvu zaidi kwa kumuozesha kwa Roma ambaye alikuw ana uwezo mkubwa wa nguvu za kijini.
Kitu kingine Maimuna hakuwa msichana wa kawiada kama ambavyo amesema Mzee Sharif , inasemekana mrembo huyo mama yake sio binadamu wa kawaida hivyo waliamini kama wataweza kupata mtoto kupitia Maimuna na Roma basi anaweza kuwa sio wa kawaida na kufanya ukoo wao pamoja na dini yao kuzidi kusambaa duniani kote.
Maimuna alijikuta akikasirika na jambo lile na kung’ata lipsi zake nyekundu kwa hasira kwani kitendo cha Roma kumwambia hamtamani kwa lolote kwake ni kama amedhalilishwa, hakuwahi kuwaza kama kuna mwanamme katika dunia hii ambaye anaweza kumkataa kirahisi kama alivyofanya Roma, alianza kujifananisha ana kasoro gani na Edna kwani wote ni warembo huku yeye weupe wa kiarabu ukimbeba.
“Nsihakuambia hivyo huyu Maimuna atakuwa na msaada kwako , ndio anaekwenda kurithi utajiri wote wa familia yetu , acha kuwa mjinga na kumkataa hii ni bahati siojirudia mara mbilimbili”Aliongea na kuwafanya wale wazee ambao hawakuwa wakijua ukweli kuhusu mrithi wa familia kumwangalia kwa mshangao.
Maimuna licha ya kwamba alikuwa mwanamke lakini ndio mmoja wapo ya wanafamilia ambaye alikuwa ameonyesha uwezo mkubwa wa akili na kumfanya Babu yake kumkubali, isitoshe alikuwa ametii sheria za ibada kwa kuendelea kuwa bikra mpaka wakati huo.
“Vipi kuhusu chaguo la mwisho?”Aliulizia Roma na kuwafanya waamini kabisa kwamba bwana huyo ameamua kukataa chaguzi ya kumuoa Maimuna.
“Hakuna shaka , kama ijulikanavyo viijana wa siku hizi ni wenye kukurupuka , chaguo la tatu ni rahisi sana , hatujawahi kujizuia kudili na adui yetu , familia ya Mzee Nguluma wote watauliwa halafu wewe utakuwa mateka chini ya familia yetu na tutakuvua nguvu zote za kijini ulizokuwa nazo na tutakutesa mpaka utoe hazina yetu na kisha kukulazmisha kusujudia miungu yetu”
Roma alijikuta akichezesha ulimi wake kwa kutoa sauti kutokana na namna walivyokuwa wakijiamini mpaka kuongea kauli hio.
“Usituchukulie poa , familia yako inaweza kuwa na nguvu ndani ya taifa hili lakini haimiliki nchi , isitoshe jeshi haliwezi kuwasikiliza kwa kila kitu , tunaweza kuimaliza familia yako kwa kuagiza wazee wetu hapa wa kijini kwenda kuua familia yako yote lakini hatuna mpango wa kwenda mbali hivyo”
Roma hakutaka sana kumwamini huyo kikongwe , alijiambia kama kweli alikuwa jasiri wa kufanya makubwa kwanini alikimbia nchi yake na kuja kujificha hapa Tanzania.
“Nitakupa dakika tatu tu za kufikiria , hili ni swala ambalo lazima limalizike leo hii hii”Aliongea .
Roma alijikuta akitoa kicheko cha kebehi na kisha aliingiza mkono mfukomi na kuibuka na simu na kisha alionekana kuandika namba flani flani hivi.
Kila mmoja alionekana kumshangaa na kujiuliza anampigia nani katika wakati kama huo.
Upande wa Roma haikuonekana kama alikuwa akipiga simu hali namna alivyokuwa akiandika ilionekana kama alikuwa akituma ujumbe wa maandishi.
“Roma usije ukafanya janja…”
Dakika ambayo alitaka kuongea ulisikika mtetemeko na mlipuko mkubwa kama vile ni wa ngurumo ya radi.
Dakika hio hio ndege walionekana wakiambizana kukimbia katika mazingira hayo yenye miti.
Sauti haikuonekana kutokea na kuisha bali iliendelea kusikika mfululizo na ndani ya dakika chache tu ndani ya eneo hili lilianza kuzingirwa na moshi mzito sana huku mawe yakianza kuingia ndani ya jengo hilo la hoteli kiasi cha kupasua pasua vioo.
Magari yaliokuwa yameegeshewa nje yalianza kuwika kwa kutoa ving’ora vya alamu na mengine yalianza kulipuka mara baada ya matanki ya mafuta kupasuliwa na mawe,
“Pumbavu alikuwa akituma signal , inaonekana alikuwa ametega mabomu?” Mmoja wapo alipiga kelele mara baada ya kugundua mlipuko uliokuwa ukiendelea ndani ya eneo hilo ni wa mabomu.
Dakika ileile wakati mabomu hayo yakipiga wakiwa katika hali ya kushangaa Roma alimshikilia maimuna kwa spidi kiasi cha kumfanya kushindwa kuchukua hatua ya kumkwepa .
Maimuna alikuwa na nguvu za kijini lakini zilikuwa za chini sana kulinganisha na uwezo wake.
Roma palepale hakutaka kumcheleweshwa kwani alipitishia vidole shingoni kwa spidi na palepale aliweza kupoteza fahamu na kisha akamuweka begani.
“Wewe mzee wa kiarabu Kikongwe usie na aibu , nimeshindwa kuamini kama ulikuwa na mpango wa kunichokoza kwa mara ya pili , kabla ya kutia mguu ndani ya hii hoteli ishatembelewa na vjana wangu muda tu na kutegesha mambomu aina ya C4., nenda kuzimu”Aliongea Roma kwa kufoka.
“Mjingaaa sana wewe!!, unataka tufe wote kwa pamoja hapa , umekuwa kichaa?”
“Haha si ndio mlichokuwa mkikitafuta, siogopi bomu la nyuklia sembuze hivi vibomu vya kawaida nitaondoka na mjukuu wako , mwachie Mzee nguluma na mke wake la sivyo nitahakikksha namtupia baharini sehemu yenye papa na kisha nitaua kila mwanafamilia mwenye jina la ukoo la Sharif na kufuta mizizi yako ndani ya hili taifa , Shwain..”Aliongea Roma na palepale alikimbilia nje.
Kabla hajapiga hatua yule mhindu aliekuwa kimya muda wote akiwa na mavazi yake meusi palepale alipotea alipokuwa amesimama na ile anakuja kuibukia ni mbele ya Roma.
Ilikuwa kama alivyotegemea huyo mzee alionekana anaenda kumletea ngumu katika kushindana nae., spidi yake na msisimko ulikuwa umezidi ule wa jini Imrah.
Lakini hata hivyo Roma alishajua hana namna ya kumkimbia zaidi ya kupigana nae uso kwa uso
“Unakimbilia wapi?”Aliuliza kwa sauti kali ya kuumiza masikio kwa mtu wa kawaida.
“MODAO!!!”
Dakika ileile mkono wake ulianza kuzungukwa na mwanga wa njano na ndani ya dakika tu kulionekana kitu kama chungwa lililoiva likitokea mkononi mwake.
Roma alijikuta akishangaa kwani aliweza kugundua hio ilikuwa ni dhana ya kijini ambayo hakuwahi kuiona ambayo inaitwa Modao , Dhana ile ilikuwa ikitoa msisimko wa ajabu mno na kutengeneza kimbunga cha upepo mkali sana.
Ijapokuwa mabomu bado yalikuwa yakiripuka kuzunguka hoteli hio lakini eneo waliliiokuwa ni kama lilikuwa haliathiriki na milipuko hio.
“Kaeni ndani ya ngao , msisogee la sivyo hamtokuwa salama”Aliongea mara baada ya jengo hilo kuanza kutingishika likionekana linataka kudondoka muda wowote.
Familia hio ambayo ilikuwa na watu ambao wana uwezo mdogo wa nguvu za kijini walijikuta wakipatwa na ahueni mara baada ya kuona wana ulinzi wa kuwatoa ndani ya eneo hilo wakiwa salama.
Dakika ileile jini Iftiri , Imrah na Maridi waliingia ndani na kumzingira Roma huku kila mtu amelipukwa na nguvu isiokuwa ya kawaida ya kijini.
“Unajikuta jasiri kujitengenezea njia ya kutoroka si ndio, lakini nikwambie tu pengine umedharau sana uwezo wetu , leo ndio mwisho wako, hebu onja kwanza uzito wa thamani ya paundi elfu sitni”Aliongea yule mzee wa vazi jeusi,
Roma alijikuta akianza kulaani kimoyo moyo kwani aliona hao majjini hawakuwa na nia ya kumuacha salama kabisa na hawakuonyesha kujali usalama wa Maimuna tena , pengine tayari walikuwa washajua kwamba Roma asingeweza kumua kwani kifo chake ingemaanisha kifo cha Mzee Nguluma.
Wakati majini hao wakiwa na nia ya kumua, familia ya Mzee Sharif ilikuwa katika hali ya wasiwasi kwani waliogopa kifo cha Maimuna ingemaanisha kwamba wangepoteza mrithi aliekubaliwa na miungu wao.
Roma mara baada ya kuona nguvu ya ajabu inamsogelea alitaka kujikinga na mwili wa Maimuna lakini alihofia angeweza kufariki wakati bado alikuwa akimhitaji , aliona pengine akwepe pigo hilo lakini bado spidi yake ilikuwa ndogo na alijikuta akikosa chaguo na palepale alinyoosha mkono kupokea lile shambulizi.
“Modao!!!”
Aliongea kwa nguvu yule Mzee mwenye vazi jeusi na palepale ulitokea mlipuko wa aina yake ambao ulitengeneza mtetemeko wa ardhi ya aina yake.
Sehemu ambayo alikuwa amesimama Roma hakuonekana zaidi ya shimo kubwa la mita moja kwenda chini ndio na palepale ukuta wa hoteli hio uliokuwa umebakia ulidondoka.
Upande wa Roma bado alikuwa amesimama vilevile akiwa chini ya shimo na bado mkono wake ulikuwa ukishindana na nguvu ya kijini ilioruhusiwa kutoka katika Dhana ile ya Modao..
Yule mze mwenyewe alijikuta akiwa kwenye mshangao kwani hakuamini Roma hajathiriwa na pigo lale na aliishia kujiuliza inakuwaje akawa hajaathirika , mwili wake umetengnezwa na chuma.
Upande wa Roma alikuwa kwenye maumivu makali mno , ijapokuwa hajawahi kuyaogopa maumivu lakini alichokuwa akipitia hakikuwa cha kawaida , ni damu pekee ambazo zilikuwa zinaonekana kwenye mkono wake.
Shambulizi lote lile la Modao alikuwa amelizuia na mkono mmoja ndio maana aliweza kupitia maumivu makali kama hayo.
Yule Mzee wa kijiini aligundua maumivu yake , ijapokuwa alionekana kuweza kuhimili shambulio lake kwa mkono lakini bado aliona mikono yake ilikuwa ikimtetemeka na hili lilikuwa udhaifu ambayo ulimpa tumaini la usihindi.
“Sijajua umewezaje kuwa na mwili wa aina hio lakini hainizui kukuua na shambulizi langu la thamani ya paundi elfu sitini”Aliongea huku akitoa tabasamu la kejeli na palepale aliita moto wa rangi ya njano na kisha aliunganisha na kile kitenesi kama chungwa kwenye mikono yake na kufanya nguvu yake kuzidi kuwa kubwa maradufu.
Roma alijikuta sasa akihisi ile nguvu ya ile Dhana ikiongezeka uwezo wake kwa zaidi ya mara mia moja na alijihisi mifupa yake inataka kumvunija kutokana na presha aliokuwa akiihisia.
“Mlete Maimuna , huwezi kuvumilia shambulizi langu lingine”Aliongea
“Unapambana na Jinn Ghula ambaye uwezo wake ni mkubwa zaidi katika kuipita dhiki na kwenda mpaka levo ya kudhibiti maji kwa kuyabadilisha mara sita kimuundo . atakuua na shambulizi moja tu”Aliongea jini Imrah kwa tahadhari.
Roma alijikuta akishangazwa na kauli ile na kujiambia inakuwaje akawa na uwezo mkubwa namna hio , alijiambia kama angejua familia hio haikuwa ya kawaida basi asingechoma madhabahu yao.
Shauku yake ya kutaka kuijua hio familia chimbuko lake ilizidi kumjaa,
Roma alijiuliza au pengine kna kitu hakijui kuhusu majini ndio maana yupo kwenye hatari kama hio.
“Acha kuwa mbishi wewe binadamu , Master Ghula hio dhana yake ya Modao inao uwezo wa kukusanya nguvu za kiroho za kikosmiki na kuwa na uzito mkubwa ambao huwezi kuhimili”Aliogea kuzidi kumtia hofu Roma.
“Nitakuuliza mara ya mwisho , je upo tayari kurudisha hazina yetu?”Aliuliza Master Ghula.
Roma damu yake ilikuwa ikichemka mno na aliweza kuhisi namna ambavyo ile Dhana ilikuwa ikikusanya nvuvu ya kiroho ya giza kwa kasi mno.
“Niue tu kama unaweza” Aliongea Roma kijeuri kama kawaida yake na kumfanya Master Ghula macho yake kubadilika rangi palepale na kuwa na kutisha.
“Ukiburi ulioje kutoka kwa binadamu kama wewe , ni hasra kukuua lakini sina namna”Aliongea na palepale upepo mkali ulianza kuvuma na uchafu ulianza kujikusanya katika mikono yake kiajabu , kile kitenesi kama chungwa kilianza kutengeneza kimbunga cha ajabu na palepale alianza kuongea lugha ya kiajabu ambayo Roma alichoweza kusikia ni Mlima wa Tai, Viani Dao…
Ilikuwa ni nguvu ambayo haikuwa ya kawaida kwani katika lile eneo ambalo amesimama Roma kulitengeneza shimo kubwa na pengine kulikuwa na eneo la Ardhini ambalo lilikuwa limechimbwa kaitka hoteli hio kwani Roma alisukumwa kwenda chini mara baada ya mpasuko huku akisindikizwa na pigo takatifu la Modao na hakuonekana tena yeye pamoja na Maimuna na palepale yalifuatia maporomoko ya mawe pamoja na vifusi kufunika lile shimo kwa kasi na ndani ya dakika tu majabali na vifusi viliweza kufunika na kufanya eneo lote kujaa vumbi ambalo sio la kawaida.





SEHEMU YA 659.
Hoteli yote ya Wache ilikuwa imeharibika na kwa mtu mwenye uchungu wa mali pengine angekuwa kwenye masikitiko maiubwa kwani ilikuwa na mvuto usio wa kawaida ndani yake.
Wale wazee wa kijini wote watatu walionyesha kukunja ndita zao , ijapokuwa Roma alionekana kufunikwa na kifusi lakini bado waliweza kuhisi kabisa bado alikuwa hai na pia Maimuna alikuwa hai jambo ambalo lilimfanya ajawe na ahueni.
Kwao Maimuna alikuwa na thamani kubwa zaidi ya Mzee Nguluma na mke wake.
“Baba tayari ashafukiwa na kifusi chini ya Ardhi , Maimuna atakuwa sawa kweli?”Aliuliza baba yake Maimuna aliekuwa katika hali ya wasiwasi.
“Punguza presha , hebu waangalie wazee muonekano wao , inaonekana huyo mwanaharamu bado yupo hai na anamtumia Maimuna kama mateka na chochote kikimtokea Maimuna basi anajua fika familia ya Mzee Nguluma itakuwa halali yetu”Aliongea Mzee Sharif.
“Lakini anaweza kuwa hai lakini vipi kuhusu kupatwa na majeraha”
“Kaa kimya , wazee wanajua wanachokifanya”Aliongwa kwa kufoka.,
“Anatumia mbinu gani ya kimafunzo , mwili wake sio wa kibinadamu kabisa”Aliuliza jini Marid kwa mshangao.
Upande wa Mzee Ghula alionekana kushanga pia na kujiuliza kwa nguvu ya kijini aliotumia kwanini huyo mwanaharamu bado tu hajafa.
Mzee Ghula palepale hakutaka kuamini kama hawezi kumuua Roma kwani alianza kuchanel nguvu nyingine ya kijini ili kuweza kuisindilia kwenye lile shimo ambalo Roma alifunikwa lakini kabla hajamaliza anachotaka kufanya ghafla tu alianza kukumbwa na hali ya woga kwenye akili yake na kujikuta akigeuza macho yake na kuangalia angani.
Wale wenzake pia walikuwa washainusa hatari na walijikuta wakigeuza macho yao wote kwa pamoja kuangalia angani na walijikuta wakiwa hawamini wanachokiona angani.
“Nini kile?”Kila mtu alikuwa kwenye mshhitiko kuangalia kitu ambacho kilikuwa kikiwasogelea kwa kasi.
Kabla hata hawajaelewa waliweza kuona kitu kingine kiibuka kutoka baharini na kupaaa angani na kuanza kusafiri kuelekea upande wao.
“Oh ,. Hapana ni Makombora yale”
“Shit .. hili linawezekana vipi?”Baadhi ya mabodigadi waliokuwa nje ya eneo hilo walijikuta wakijawa na kiwewe.
Mzee Sharif mara baada ya kugundua kinacho wasogelea ni makombora ya kivita alijikuta akipagawa na kujiuliza vitu hivyo si vya kijeshi.
Halikuwa kombora moja , ilionekana yalikuwa yakirushwa kutoka chini ya baharii kuja eneo walipo kutokana na trajectori zao na ilikuwa ni swala kufumba na kufumba yote yashakaribia eneo walipo.
Ilikuwa ni maamuzi ya haraka sana walioyafanya kwani palepale walitengeneza ngao ya kijini na kuwafunika watu wote na wao pia kwa kuunganisha nguvu na makombora yale yalitua yote kwenye ngao na kutoa mlipuko wa aina yake na kuanza kugeuza kile kijimlima kuwa tambarare,
Naibu waziri Salihi , Asha na wengine wote walikuwa wakihisi ngoma za masikio yao zinawapasuka kutokana mlipuko huo huku kila mtu akilaani ni balaa gani hilo wamejitengenezea.
Wale wazee licha ya kwamba walifanikiwa kutengeneza ile ngao lakini hawakuacha kutema damu nyingi chini huku nguvu zikiwa zikiwaishia.
Ilikuwa ni kama vile kuna kambi ya kijeshi ambayo ilikuwa ikiangamizwa moja kwa moja na adui katika hilo eneo kwani yalikuwa yakishuka mfululizo tena kwa kasi bila ya kukosa shabaha.
Baada ya yote kutulia hatimae walianza kupumua lakini muda huo hawakupewa kwani kijimlima chote kilianza kuporomoka kutoka juu kwenda chini baharini na wale majini wote hawakuwa na muda wa kupoteza hata wa kujiuliza Roma na Maimuna wapo wapi kwani waliweza kuwachukua wale wasiokuwa na nguvu za kijini na kuwatorosha kwenye eneo hilo kwa haraka sana.
“Pumbavu zako Roma , nitahakikisha nakuua kwa namna yoyote ile”Aliongea Mzee Ghula kwa hasira akiwa haamini kama amezidiwa ujanja na kuishia kukimbia na Mzee Sharif, alitaka kutumia uwezo wake wa kijini kumchunguza Roma alipo lakini hali ilikuwa tete.
“Huyu mwanaharamu yupo wapi , mbona kapotea siwezi kupata msisimko wake”Aliongea Mzee Ghula kwa hasira mara baada ya kutua eneo la mbali.
“Master si atakuwa na yeye amepasuka pasuka vipande na Maimuna?”Aliuliza Marid.
Mzee Sharif mara baada ya kusikia jina la mjukuu wake likitajwa alijikuta akipatwa na huzuni kubwa na kujiambia pengine lilikuwa kosa kumchokoza Roma.
“Hapana , hawezi kufa yule , inaonekana huu ni mpango aliotuandalia hivyo kuna njia ya kujiokoa ameitegneneza tokea mwanzo”Aliognea
Mzee Sharif hakujua namna ya kuongea kwa wakati huo kwani alikuwa amechafuka na vumbi hatamaniki , zile sura za majigambo zote kwisha na kilichokuwa kimebakia ni hasara nyingine ambayo wameipata siku hio,walikuwa wakijiamini wanakwenda kummaliza Roma lakini ni kama vile wamejipalia makaa
Lakini bado mzee huyo alikuwa akijiuliza mabomu hayo nani ambaye ameyarusha , aliamini kabisa serikali ya Tanzania haiwezi kwenda mbali na kufanya kitu cha namna hio kwani ungekuwa ni ukichaa.
Kama sio serikali ya Tanzania je katoa wapi makombora ya kijeshi , vipi amewezaje kufukia mabomu ndani ya jengo lao la hoteli bila wao wenyewe kujua.
Alijiuliza hata kama serikali ya Tanzania haikuhusika jeshi la Tanzania linafanya kazi gani kulinda mipaka ya bahari.
Aliishia kukumbwa na fedheha kubwa na kujiambia habari hio ikifikia watu itakuwa ni dharau kubwa wamefanyiwa.
Wakati wote wa Kigamboni waliweza kusikia milipuko hio na wengine walikuwa washaanza kukimbia na kudhania taifa linavamiwa.
Ilikuwa ni kwa haraka sana baada ya tukio hilo wanajeshi ndio sasa wanaamka huku simu nyingi na maelekezo yakitolewa kutoka mamlaka ya juu ili kujua nini kinatokea.
Ni ndani ya nusu saa tu taarifa ziliweza kufikia jeshi la Tanzania kuhusu Kichaa afahamikae kwa jina la Roma Ramoni alikuwa akiisambaratisha familia ya Sharif kwa mabomu na makombora na taarifa hio ilipelekea kila mtu kupigwa na mshutuko , ijapokuwa ni habari zilizoenea kwa baadhi ya vongozi lakini zilikuwa za kushitusha mno kwani ni mara ya kwanza raifa kupitia milipuko ya aina hio.
Sasa mjuda ambao Suzzane na Nadia alfonso wanafika ndani ya nyumba ya mapumziko ya Raisi Senga ndio wakati ambao anapokea taarifa ya makombora kurushwa ndani ya kigamboni katika eneo linalomilikiwa na Mzee Sharif huku jeshi likishindwa kujua swala hilo limetokea vipi na makombora hayo yametokea wapi.
Kuna wengine walianza kufananisha milipuko hio na mabomu ya mbagara yaliotokea miaka kadhaa iliopita.
*****
Upande mwingine giza likiwa limetanda juu ya maji ya bahari huku upepo ukivuma kwa kasi kiasi cha kusababisha mawimbi makubwa.
Kilomita kumi katikati ya bahari lilionekana dude la chuma kama lisamaki likubwa la baharinni likiambaa ambaa kwa kasi likielekea katikati ya bahari huku likitoa mkonga wake kwa juu.
Ilikuwa ni manuari ya kijeshi yenye urefu zaidi ya mita moja na kadri ilivyokuwa ikijitokeza juu chuma chake kilichopakwa rangi nyeusi kilionekana vizuri tena bila kupiga sauti yoyote ile.
Ndani ya manuari hio katika eneo la Deck kulikuwa na mwanamke mjapani aliekuwa mrembo akiwa amevalia mavazi ya kawaida , huku nywele zake ndefu akiwa amezifunga kuzirudisha nyuma.
Pembeni yake alikuwa ni mwanaume wa kizungu ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kijeshi ya kiwana majji.
Kombati zake za kijeshi hazikuwa na isignia yoyote ile kuashiria ni jeshi la wapi zaidi ya kuwa na chata kubwa la fuvu.
Mwanaume yule alionekana kuwa katika tabasamu pana huku akimwandalia mwanamke wa kijapani aliekuwa mbele yake na aliweza kuona wasiwasi wake.
Nyuma yake pia kulikuwa na wanajeshi waliokuwa na sura za kikauzu wengine wakiwa ni Wafrika , wengine ni Warabu na wengine wakiwa ni Wazungu wakiwa wamesimama wima kikakamavu.
“Madam Tanya huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani misheni imekamilika kwa asilimia mia moja , kwa mahesabu tuliopiga itachukua zaidi ya nusu saa mpaka jeshi la maji la Tanzania kutushitukia na mpaka wakati huo tutakua kwenye maji ya kimataifa”Aliongea kwa kingereza.
“Colonel Brewester, I don’t care about the Navy , all I care is about His Majesty Pluto’s Safety”Aliongea na kumfanya Kanali Brewester kutoa tabasamu ambalo halikuwa na hofu kabisa alikuwa katika hali ya mchecheto kwani misheni iliomfikisha hapo alikuwa ameikamilisha kikamilifu bila hata jeshi la Tanzania kuwashitukia na muda huo wanaenda kujiegesha kusubiri maelekezo mengine zaidi.
Haya njooni watsapp mmalizie 0687151346
 
Ulishatuma hii
 
Shukhran mkuu mzigo umetufikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…