Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Safi sana nipo na nishaagiza katoni ya popcorn kwa ajili ya kesho.
 

.
 
SEHEMU YA 57

Roma alitabasamu na aliona kabisa amejiingiza kwenye mtego wa Edna , na kujilaumu kwa kutokuwa makini na maneno yake , lakini alijiwazia kuwa sheria yake kubwa ni kuongea ukweli pale inapobidi kufanya hivyo.

“Nimelala na Dorisi ,Nasra , Rose na Neema Luwazo”Aliongea na kumfanya Edna akunje sura , kitendo cha Roma kujibu swali lake bila hatia kilimuuzi sana na alitamani agonge geti na gari

“Bebi wife umeridhika na jibu?”

“Ndio”Aliibu Edna na kisha hakutaka maoangezi tena , baada ya kuingiza gari ndani ya uzio , alichukua mkoba wake na kuingia ndani na hakuhangaika hata kuegesha gari.

“Bi Wema nimerudi”Roma alimsalimia Bi Wema kwa tabasamu.

“Karibu sana Mr Roma nyumbani kwako”

“Asante sana Bi Wema nimemisi chakula chako sana”Bi Wema alitabasamu.

“Karibu Mezani Mkeo leo aliamka mapema kukuandalia chai nzito na sasa ipo mezani”aliongea Bi Wema huku akiwa ni mwenye kutabasamu , lakini kwa Roma alishangaa kidogo , alijua Edna alikuwa akitiania alivyosema amemuandalia chakula.

Roma alijongea mezani huku akiwa na hamu ya kujua ni kipi Edna awamu hiia amepika.

“Bi Wema kaandaa Edna hizi tambi?”Aliuliza roma baada ya kula kidogo , alishangazwa na tambi hizo kuwa nzuri licha ya kwamba hazikuwa tamu kwa kiwango cha juu lakini zilikuwa tamu.

“Ndio Miss amekuwa akijifunza kupita tokea uondoke na amesema amepata rafiki anaemfundissha kupika”

Roma alijikuta akizidi kushangaa , alijiuliza ni rafiki gani huyo Edna mke wake amempata , kwani kwa namna ambavyo mke wake alikuwa kauzu, ilikuwa ni ngumu sana kuwa na marafiki kwani hata Dorisi ambaye alikuwa ni rafiki yake walionekana kama sio marafiki.

“Bi Wema ni rafiki gani Edna kampata?”

“Mimi sifahamu lakini ninachofahamu ni kwamba huyo rafiki yake ni mwalimu mpya ndani ya shule ya kituo cha kulelea yatima”.

Roma alitingisha kichwa hakutaka kuuliza sana maswali , lakini alikuwa na shauku ni rafiki Gani Edna kaweza kumpata ndani ya muda mfupi aliosafiri kuelekea Japai , alishangaa.

*****

Upande mwingine ndani ya makao makuu ya kampuni ya JR alioneakna Abuu akiwa ameketi kwenye kiti chake huku sura yake ikiwa katika hali ya wasiwasi sana na jambo ambalo lilimfanya bwana huyu kuwa na wasiwasi ni kutokana na Hisa za kampuni yao zinavyoendelea kushuka , kutokana na kushindwa kusaini mkataba wa Dili la Yamakuza, akiwa amekalia anaangaia tarakishi yake iliokuwa ikimuonesha chati ya Candlestick .

Mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na alionekana Isack Makamu wa raisi wa Makapuni haya ya JR, huku mkononi akiwa ameshikilia karatasi.

“Kuna nini Isaack?”

“Abu kuna swala hapa ambalo sio la kawaida”

“Unamaanisha nini?”Aliuliza na Isack alimpatia Abu karatasi aliokuwa ameshikilia.

“Kama unavyona kwenye hio orodha ni baadhi ya watu ambao wamenuunua Hisa zetu baada ya kushuka kwa Thamani , lakini kuna mtu anaejiita Athena anaonekana kununua kiasi kikubwa sana cha hisa na hii ni hatari kwa kampuni , kwani mpaka sasa mtu huyu ana asilimia Zaidi ya therahini za umiliki wa kampuni”Abu macho yalimtoka , aliangalia na ni kweli kuna mtu kanunua hisa zao kwa kiwango kikubwa sana Zaidi ya bilioni mia mbili.

“Kana hisa zikiendelea kushuka Thamani kwa muda wa wiki , anaweza kununua Zaidi”Aliongea Abu.

“Ndio , inatakiwa kuwa na mpango wa kutatua hili tatizo zisishuke thamani Zaidi ya hapa”

“Huyu mtu unafikiri a anampango gani wa kununua hisa zote hizi?”Aliuliza Abuu

“Kuns mawili hapo huenda anataka kuwa na sehemu kubwa ya umiliki wa Kampuni , pili labda ni mtu ambaye ana matarajio chanya ya hisa za kampuni yetu kupanda thamanni baadae ,hivyo anatafuta faida”

“Okey Isack , lakini lazima tuwe makini na pesa yote hii ambayo imeingia kwenye Kampuni yetu , jaribu kutafura namna ya kuwasiliana na huyu mtu , ili tuweze kujua nia yake”

“Sawa boss” Baada ya Abuu kuongea na Isack ,aliingia marasta .

“Vipi Seif anaendeleaje Jose?”

“Anaendelea vizuri , bado yupo hospitalini anaendelea kuongezea Glucose na virtubisho mbalimbali ili mwili kupata nguvu”

“Okey Kazi nzuri”

“Lakini Boss hujaniambia , kwanini tunamtibu kizee kama yule?, sio kawaida yako”

“Jose wewe fanya kama ninavyoelekeza na acha maswali megni sawa”

“Sawa Bosi, Halafi Roma asharudi nchini leo asubuhi , kapokelewa na mke wake uwanja wa ndege na waliongea na Raisi”.Abu alitafakari kwa muda.

“Okey , waambie vijana waendelee kumfatilia kwa kila kitu anachokifanya na nataka taarifa zote zinazomuhusu”

“Sawa bosi”

Baada ya Marasta kutoka , aliingia Elvice ndani ya ofisi hii na kumfanya Abu atabasamu na kumkaribisha.

“Halafu Elvice haujaniambia kwanini mpango wa kumteka Edna ulishindwa kwa mara nyingine wakati nikiwa Japani , nilisahau hata kukuuliza maana niikuuwa nimechanganyikiwa.

“Nilituma vijana wangu kama kawaida , kutoka jeshini , lakini jambo la kushagnaza ni kwamba mpaka sasa sijui walipo , kwani mara ya mwisho niliwasiliana nao wakiwa nje ya nyumba ya Edna”Abuu alishangaa.

“Kwahio unamaanisah kwamba wamekukimbia au imekuwaje , sijaelewa mpaka hapo”.

“Sio wamekimbia , nilijaribu kufatilia kupitia polisi na majibu nilioyapata ni kwamba waliingia kabisa na kuwadhibiti walinzi wa Edna , lakini kwa maelezo ya polisi waliofika kwenye tukio ,Edna alieleza kuwa walidhibitiwa na Wazungu na kisha wakawabeba na kuondoka nao”

“Mh! , hii inaweza ikawa shida kwa upande wetu Elvice kama watakutaja?”

“Hawawezi , ni vijana kutoka jeshini ninao waamini sana na nina uhakika hawawezi kuniuza nimewatumia katika kazi nyingi”Abuu alitikia kwa kichwa kuonesha kuwa amekubali jibu hilo.

“Mpango wetu ni wikiend hii?”

“Ndio bado siku mbili tu kumuondosha yule shetani , japo bado nina wasiwasi?”

“Hupasi kuwa na wasiwasi , licha ya kwamba ulisema alibadillika kama shetani , lakini naamini Roma ni mwanadamu na hawezi kupona na risasi ya moyo”

“Naunga mkono hoja , cha msingi ni kuhakikisha tunamwandalia mazingira seif mazuri ya kufana kazi”

“Hilo muhimu”

*****

Ni Kaskazini mashariki ya Kiimwa kimwe na Kaskazini Mashariki ya Kirawe katikati ya haya maeneo ndipo ilipo Ikulu ya Wananchi wa Kenya , makazi ya mtawala wa Kenya aliemadarakani ndugu Kamau Kamau.

Ndani ya jengo hili ndani ya chumba wanachotumia kulala wanandoa, yaani mheshimiwa Kamau Kamau na mke wake Maina aliemaarufu kama ‘First lady’. Alionekana mheshimiwa Kamau Kamau kwenye kioo kikubwa huku akiwa anaweka suti yake sawa huku nyuma yake akiwa amejilaza mke wake Maina.

“Blandina , utamuepuka mpaka lini Senga , jambo hili linanikasirisha mara kwa mara, na kumuepuka kwako kunanifanya nione bado una hisia nae”

“Kamau hayo ni mawazo yako , ni miaka mingapi mpaka sasa tuwepamoja?”

“Miaka ishirini na tano ya ndoa yetu”

“Sasa nimeishi kwa miaka yote hio na wewe , kwanini bado hujiamini kama nakupenda?”

“Sio sijiamini Blandina , lakini huyu ni kiongozi na inapaswa tumpokee kwa pamoja, nataka ujiamini mbele ya Senga”.

“Sio kama sijiamini mbele ya Senga , lakini wewe ndio umenifanya kuwa hivi , miaka ile nilivyokuambiaa tumuambie Senga ukweli wote ukataka tumfiche huku ukinilazimisha kuishi kwa sura bandia , unafikiri napenda eh”Alianza kulia.

“Am sorry Blandina , yote nimefanya kwa ajili yako na mapenzi yetu , sikutaka Senga ayaingilie”

“You are Selfish Kamau , its always you as you , kwanini unaijali sana nafsi yako kuliko yangu Kamau , ni mapenzi ya aina gani hayo unayo juu yangu ,nimekuwa wakuishi kwa mateso miaka na miaka Kamau, lakini mpaka sasa hats mtoto wa kutoka kwenye tumbo langu sina….”Aliongea na kulia mno mwanamke huyu.

“Nisamehe sana Blandina ,, najua umeishi na mimi miaka na miaka na umekuwa ni mwenye kunifariji , huku ukiacha kuziishi ndoto zako , ni mapenzi makubwa sana ambayo umenipatia , Blandina naahidi baada ya mimi kustaafu I will make evertihing up for you mpenzi , nakupenda sana na nitaendelea kukupenda naomba usinikatie tamaa mapema hivi mke wangu sawa mama”

Kamau alionekana kumbembeleza mwanamama huyu ambaye ana majina mawili , yaani lile la Maina , ambalo lilikuwa likifahamika na watu wengi kama mke wa raisi , lakini pia alikuwa akifahamika kama Blandina , jina ambalo ni watu wachache sana waliokuwa wakilifahamu, na pia ni watu wachache ambao walikuwa wakijua kuwa Maina waliekuwa wakimjua ni feki.

Baada ya kubembelezana muda mrefu ,Maina kinyonge alikubali kujiandaa kwa ajli ya kuelekea uwanja wa ndege kumpokea Raisi senga, ambaye atakuwa hapo nchini kwa ziara ya siku moja.

Ni ndani ya nusu saa wanandoa hawa na baadhi ya viongozi wajuu walikuwa ndani ya uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyata kusubiria ujio wa Raisi senga.

Ilichukua takribani dakika kumi kwa ndege ya ATCL kutua na kusimama kabisa na pia kutoka kwa mheshimiwa Senga.

Maina alijikuta akigonganisha macho na Senga na Senga na yeye alimwangalia Maina huku kwenye kichwa cha Maina mambo mfululizo yakipita , haikueleweka mwanamke huyu alikuwa akifikiria nini kwa wakati mmoja .
 
SEHEMU YA 58

Mheshimiwa Senga baada tu ya kushuka kwenye Ndege alianza kusalimiana na mwenyeji wake Raisi Kamau ,aliekuwa ameambata na mke wake Maina .

Muda wote Maina alikuwa akimwangalia Senga , mwanamama huyu alionekana kuwa na majuto makuu , alionesha hali ya kujutia kwa kitendo cha kujivika sura bandia ili mradi asifahamike uwepo wake duniani kwa Senga.

Senga nae licha ya kwamba alikuwa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa juu wa taifa hili la Kenya , lakini akili yale ilikuwa kwa Maina ,Senga alikuwa akijihisi kitu cha ajabu kila anapokutana na mke wa raisi mwenzake , hakujua ni kwanini anapata hisia ambazo ni kama amezisahau katika maisha yake .

"Karibu sana Kenya Mheshimiwa Senga"

"Asante sama Komredi , kila ninapokuja ndani ya taifa hili hua natoka na kitu kipya ni kama kuna nguvu ya Kimungu iliopo ndani ya hili taifa, nakiri Kenya imebarikiwa sana"

"Hahaha.. ni kweli ,Senga hata mimi mara ya mwisho kuja Tanzania niseme nilijisikia Amani na natamani baada ya kuachia madaraka nihamie Kwenye nchi yako" Aliongea Kamau na kwa namna ambavyo alikuwa akionekana kuongea usingemdhania kuwa alikuwa akificha mengi moyoni .

Waswahili wanasema Moyo wa mtu ni kichaka, na hili ndio lililokuwa likijidhihirisha mbele ya Maraisi hawa wa nchi jirani.

Baada ya salamu na mapokezi ya aina yake ya Raisi Senga hatimae walianza mazungumzo yao baada ya kuingia ndani ya Ikulu.

"Senga umekuwa sio wa kuambatana na mkeo mara kwa mara unapofika Kenya Au Damasi anakataa kuja Kenya , nimemkumbuka sana "

"Kamau yule mwanamke acha tu ni mvivu kupindukia na hapendi sana kuonekana hadharani na hio imekuwa tabia yake tokea namuoa".

"Ndio nakumbuka sana ,Sema tumetoka mbali sana Senga, ile mitihani tuliopitia kipindi kile katika kutafuta maisha ilikuwa ni ya aina yake , nakumbuka kila hali ilivyokuwa mbaya kwako na kujihisi kukata tamaa, Blandina ndio aliekuwa akikutia nguvu na neno moja la Blandina kwako la faraja ,ulionekana kuwa mpya na kupambana zaidi".

"Umenikumbusha mbali sana yaani, kama sio Blandina kufariki kwenye ile ajali pamoja na mwanangu Denisi huenda maisha yangu yangekuwa ya tofauti sana"Aliongea huku akiwa ni mwenye Huzuni na muda huo hio aliingia Maina.

Maina alionesha hali ya kutojiamini kabisa mbele ya raisi Senga , alikuwa ni mwenye kukwepesha macho kila mara wanapoangaliana.

"Maina niseme sana Asante kwa kujenga kile kituo kule Bagamoyo , hakika kimesaidia sana jamii ya wenye uhitaji , kimekuwa tumaimi kwa watoto ambao walipoteza wazazi wao wakiwa wadogo".

Asante sana Senga , moyo wangi unafarijika pale ninapo ona watoto wakiwa na furaha na kuishi katika mazingira salama"

"Ni kweli mchango wako kwa jamii za Afrika ni mkubwa sana na unapaswa kupewa tuzo"Maina alitabasamu namuda wote Kamau alikuwa akiwaangalia wawili hao walivyokuwa wakiongea ni kama alikuwa akitafuta jambo flani kupitia kukutana kwao.

Kwa namna ambavyo Senga alikuwa akiongea na raisi Kamau mabwana hawa walionekana kuwa na stori yao ambayo bado watu hawakua wakiifahamu, kwani kwa namna ambavyo waliweza kukumbushiana mambo yaliowatokea miaka ya nyuma , ilionekana walifahamiana kabla hata ya kufanikiwa ,haikueleweka mara moja ilikuwaje mpaka wote wakawa maraisi.

"Sijajua kwanini najisikia wa tofauti kila ninapokutana na Maina".Aliwaza Senga huku akiwa ameshilia picha ilioonekana kuchakaa , picha ambayo ameitoa kwenye mfuko wa koti lake ,ni picha ambayo ilikuwa ikimuonesha mwanamke mrembo , licha ya kwamba picha hio ilikuwa imechakaa , lakini mwanamke aliekuwa kwenye pivha hio alikuwa akionekana vyema kwa urembo wake.

***

Roma baada ya kumaliza kunywa chai ilioandaliwa na mke wake Edna , aliingia chumbani kwake na ndani ya madakika kadhaa alionekana kubadilisha nguo na sasa alikuwa amependeza huku mkononi akiwa ameshikilia ufunguo wa gari yake .

“Bi Wema mimi natoka kidogo nitarudi jioni”Aliongea Roma na Bi Wema akaitikia.

Wakati Roma anatoka Edna kama kawaida yake alikuwa juu ya Balconi akimwangalia Roma ambaye alikuwa akielekea uelekeo wa yalipokuwa yakiegeshwa magari.

“Zishaamka , yaani sijawahi pata ona mwanaume Malaya hivi , kama wanaume wote wako hivi , bora hata mimi niliolewa kwa mkataba, katumia zaidi ya siku tatu zote kuwa na Dorisi lakini saivi pale ni kwenda kutafuta mwanamke mwingine”Aliwaza Edna huku akiangalia Gari ya Roma inayotokomea nje .

Nimemmisi Rose , japo ni asubuhi ngoja nikaonanane nae”Aliwaza Roma huku akikanyaga pedeli kuchanja mbuga kuelekea Mbagala.

Dakika chache mbele kama nusu saa hivi , Roma alikuwa akiingiza gari ndani ya Club B.

Aliegesha gari yake na moja kwa moja aliingia kwenye Bar hii ambayo wakati wa mchana ni wateja wachache sana wanaokuwepo hapo.

“Mr Roma karibu sana”Aliongea Zonga mara baada ya kumuona Roma akiingia hapo ndani , lakini Roma kuna kitu alikiona kwenye macho ya Zonga , aliona hali ya wasiwasi.

“Rose yuko wapi na mbona leo naona hali ni kama nisivyoizoea?”

“Ndio Roma na bora hata umekuja , kwani Boss yupo kwenye hali mbaya”

“Nini kimempata Rose?” aliongea Roma kwa kushangaa huku akianza kupiga hatua kuelekea ilipo ofisi ya Rose.

“Boss yupo nyumbani kwake kajeruhiwa na risasi ya tumbo”Aliongea Zonga na kumfanya Roma ashangae na kuwa na wasiwasi pia , aligeuza na kutoka nje na kisha akaingia kwenye gari na kuipeleka mpaka ilipo nyumba ya mwanadada Rose.

Baada ya kuingia hapa ndani ,aliona kweli Rose alikuwa kwenye shida , kwani kulikuwa kimya mno , kiasi ambacho ungedhania kuwa wenyeji wamehama.

“Rose!”Aliita Roma mara baada ya kuingia kwenye sebule hii kubwa na kumkuta Rose ambaye amejilaza kwenye sofa huku akionekana kupauka kweli , ule uzuri wake ulikuwa umefifia na huyu alikuwa ni Roze anaeumwa.

“Huby!”Aliitikia Rose kwa sauti dhaifu na kumfanya Roma amuonee huruma mchepuko wake.

Roma baada ya kumsogelea , hakutaka kuongea sana alivuta juu blazia aliokuwa amevalia Rose na kuangalia jeraha la Risasi , na hapo Roma alijikuta akikumbuka siku alioingia Tanzania kwa mara ya kwanza ,alianza kukutana na Rose akiwa kwenye hali mbaya , hali ambayo ilikuwa ikifanana na hii anaiona sasa , kwani sehemu aliojeruhiwa Rose ni hio hio.

“Kwanini hujaenda hospitalini?”

“Ni jeraha la risasi , sikutaka kwenda hospitalini ingeleta shida kwa upande wangu na pia maadui zangu wangenimaliza kabla hata sijapona”

“Unamaanisha nini, mbona unaongea kama upo kwenye Vita?”Aliuliza Roma na Rose alionekana kusikia maumivu makali akongea na alijikuta akikohoa na Roma alilitambua hilo , na alichokifanya ni kumuwekea Rose mkono kwenye shavu la kulia na kushoto na palepale Rose alifumba macho , ni kama amepewa sindano ya ganzi.

Roma baada ya kuona Rose kalala , alienda mpaka jikoni na kisha akachukua kisu na kurudi nacho sebuleni, baada ya kukaa alifyonza kidole chake na kisha akamuweka Rose kwa kumlaza chali na kisha akafunua blazia na kutoa bendeji iliokuwa imeloana na damu nyingi.

Roma alichukua kisu na kuchana kiganja chake kwa kutumia kisu na damu zilianza kumtoka na hapohapo akasogeza mkono wake usawa wa jeraha la Rose na damu ile kuingia kwenye jeraha.

Ilikuwa ni kama kidonda cha Rose kilikuwa kikiungua kwa moto kwani ile sehemu ya jeraha kadiri Roma alivyokuwa akiruhusu damu kuingia , mvuke flani hivi mfano wa moshi ulianza kutoka , Roma alikata kiganja kingine na akaweka tena na mvuke ulizidi kuongezeka na ndani ya dakika tano alikuwa ashamaliza na sasa jeraha la Rose lilianza kuvutana na lilionekana kufunga taratibu na kadri dakika zilivyokuwa zikisogea ndipo jeraha lilipozidi kujifunga na ndani ya dakika kumi tu , ile sehemu iliokuwa na jeraha ilifanana na sehemu nyingine za mwili.

“Bebi Rose sasa hivi damu yako sio ya kawaida , umekuwa mtu wa kwanza kuhimili damu yangu yenye maambukizi ya kirusi kwa Zaidi ya mara mbili” .

Aliongea Roma huku akiwmangalia Rose aliekuwa amelala bila ya fahamu.

“Roma!!”Aliita Zonga aliesimama mlangoni , akimwangalia kwa hali ya wasiwasi , haikueleweka alisimama hapo kwa muda again.
 
SEHEMU YA 60

Roma Na Dorisi walipewa mapumziko ya siku mbili kabla ya kurejea kazini , hivyo Roma muda wote alibakia nyumbani , kiufupi hakukua na jambo kubwa sana ambalo lilikuwa limetokea ndani ya siku nzima.

Edna alionekana kuwa bize sana tokea Roma arudi nchini , Roma mwenyewe alishangazwa na ubize wa nke wake, Edna alikuwa akirudi usiku sana kwani alikuwa akifanya kazi Overtime,Kwa Roma hakutaka sana kumuuliza nini kinaendela kwenye kampuni mpaka mke wake kuwa bize kiasi hicho.

Siku ya ijumaa nzima Roma hakuwa ameonana na Edna , kwani ile anaamka mwanadada huyu alikuwa tayari ashaenda kazini.

Roma jambbo hili lilikuwa likimshangaza sana , hakuelewa Edna ni mwanamke wa aina gani , kwani alikuwa na pesa nyingi lakini alikuwa akifanya kazi Zaidi ya wale waliokuwa hawana hela na pia wafanyakazi wake yaani yeye ndio kama ameajiriwa.

Edna na Bi wema ni kama walikuwa wamesahau tikio la wao kuvamiwa , kwani Roma hakuwa na taarifa nalo , hakuwa akijua kama kuna watu ambao walikuja kuingia ndani ya nyumba yake, kwani hata jeshi lake hawakumpatia taarifa na Roma hakuwa ameenda kuwatembelea, alijiambia katika nafsi yake ngoja awape muda kidogo wa kufanya uchunguzi , ili akienda kuchukua ripoti iwe imeshiba.

Naam ni siku ya jumamosi,Roma aliamka vizuri na kujinyoosha na kisha alishuka kuelekea kwenye chumba cha mazoezi na ile anafika sebuleni , alikuta Bi Wema kama kawaida yake alikuwa ashaamka na sasa alikuwa akifanya usafi, na Roma alimsalimia.

“Bi Wema Edna jana alirudi?”Aliuliza Roma maana alienda kulala mapema kabla ya Edna kurudi.

“Miss jana hajarudi , alinipa taarifa kama atalala ofisini”Alijibu Roma na kushangaa.

“Bi Wema hii ya kulala ofisini imeanza juzi au ni mazoea?”.

“Ndio kuna siku hakuwa akirudi kabisa , na hii ni kama kuna jambo kubwa linaendelea ndani ya kampuni”

Alijibu Bi wema na Roma hakutaka kuongea Zaidi , licha ya kushangazwa na ufanyaji kazi wa Edna , hakujua k mke wake alikuwa akihitati kiasi gani cha pesa mpaka kuridhika , kwani kwa Roma ilikuwa ni jana tu aliweza kupata kuona taarifa ya Edna utajiri wake kuongezeka kwa dola bilioni moja kutokana na hisa za kampuni kupanda .

“Ilimradi wanajeshi wangu wapo makini na usalama wake , haina shida, ngoja afanye kazi”Alijiwazia Roma baada ya kuingia kwenye chumba cha mazoezi.

Baada ya kufanya mazoezi kwa madakika , alitoka na akaenda kuoga, kujiandaa kwa ajili ya kifungua kinywa na alitumia dakika chache tu alishuka na kukaa ,na leo hii alikuwa peke yake, kwani Bi Wema na yeye alitoa sababu za kutokunyuwa chai asubuhi hio na Roma hakujali sana , aliendelea kunywa zake chai taratibu, lakini chai ya hio ilionekana sio tamu kwake na mwenyewe alijishangaa kwanini leo hajisikii kunywa chai.

Wakati Roma anaendelea kunywa chai taratibu huku akiwa ni mwenye kukosa hamu , mara Bi Wema aliekuwa ameshikilia mfuko alionekana kushuka kutoka juu na alionekana alikuwa akitoka kwenye chumba cha Edna.

“Bi Wema mbona unaonekana kama unasafari?”Aliuliza Roma huku akimwangalia

“Nampelekea Miss chai, na baadhi ya nguo za kubadilisha,Jumamosi hakuna utaratibu wa wafanyakazi kufika kazini mpaka jumatatu”Aliongea Bi Wema na Roma alikuwa akielewa kuwa wafanyakazi wa Vexto Jumamosi walikuwa hawalazimishiwi kufika kazini na ni mara chache sana kukuta Kantini ya kampuni kuwa na wapishi siku za jumamosi.

“Bi Wema ngoja nimpelekee mimi , kwanza sina hamu ya kunywa chai leo”.Aliongea Roma na Bi Wema alitabasamu.

“Angejua nilikuwa nilikuja kumpa ampelekee asingeniomba maana ningemlazimisha”Aliwaza Bi Wema na alionekana alikuwa na mpango wake kichwani.

“Itakuwa vyema ukipeleka ndio”Aliongea Bi Wema na kisha aliandaa vitu ambavyo Roma antakiwa kwenda navyo, na ndani ya dakika kumi Roma alikuwa tayari kwa safari ya kuelekea kazini kwa mke wake huku Jasusi wa mapenzi akiwa ni mwenye kufarijika baada ya kumuona Roma akitoka na gari.

“Hivi ndio inatakiwa iwe”Aliwaza Bi Wema na kisha alirudi ndani kuendelea na majukumu yake ya kazi.

“Dakika chache mbele, Roma aliingiza gari yake sehemu ya maegesho , siku hii kweli aliona ni tofauti kwani magari yalikuwa machache mno,lakini kuna jambo moja lilimfurahisha Roma ni baada ya kuona Gari ya Chiara iliokuwa imepaki na Chiara alimuona Roma wakati anatoka na Roma alitabasamu na kutingisha kichwa kama ishara ya salamu.

“Wanajitahidi sana kumlinda Edna , nitamwambia Sauroni awaongeze mshahara”Aliwaza Roma wakati akiingia kwenye Lift.

Kampuni leo ilikuw imetulia kimya sana , ni wafanyakazi wachache sana ambao walionekana kuhudhuria siku ya leo.

Lift ilimchukua Roma mpaka Floor ya ofisi za wafanyakazi wa juu wa kampuni.

“Leo Miss Airport anaoneakana na yeye hajaja kazini”Aliwaza Roma huku akiwa na mfuko wake.

Roma hakujisumbua kugonga , alisukuma mlango na ulionekana kuwa wazi na akazama ndani , lakini alijikuta akishangaa na hii ni mara baada ya kumkuta Edna aliekuwa amejifunika na khanga , kwenye sofa akiwa amelala , Roma alishangazwa na jambbo hili na kuwaza kama mtu amechoka kwanini harudi nyumbani kulala.

Alisogea mpaka kwenye meza ya mke wake na kisha akaweka ule mfuko, na kugeuka na kutembea mpaka kwenye masofa na kumwangalia Edna alivyokuwa amelala.

“Mke wangu anaonekana mrembo Zaidi wakati akiwa amelala”Aliwaza Roma huku akivuta Khanga aliojifunika Edna na kumuweka vizuri kwani ilikuwa imeacha mwili na kuburuzika kwenye marumaru.

Roma hakutaka kumuamsha Edna , aliona ngoja amuache kwanza apumzike , na yeye alienda kukaa kwenye kiti cha mke wake.

Lakini Edna alionekana kuwa macho , kwani Roma ile anakaa kwenye kiti cha mzunguko cha mke wake ,Edna alifumbua macho na kumuangalia Roma na kisha akaendelea kulala.

Roma wakati anafungua tarakishi ya mke wake kwa ajili ya kucheza gemu , kuna karatasi juu ya faili ambalo lilikuwa pembenni , mbalo lilimvutia, alilichukua na kuanza kusoma.

Ilikuwa ni karatasi ambayo ilikuwa na majina ya kampuni za kitanzania ambazo zimezungushiwa kwa Wino , lakini sio zote, moja ya kampuni ambayo ilikuwa imezungushiwa kwa wino ilikuwa ni JR , alishangazwa na karatasi hio na kushindwa kuelewa ilikuwa ikihusu nini , hakutaka kujisumbua sana kama ilivyo kawaida yake, hakupenda kufikiria fikiria.

Edna ilionekana wakati alipokuwa peke yake alikuwa akikosa usingizi kutokana na wasiwasi , kwani kitendo cha Roma kuingia hapo ni kama ameruhusiwa , alilala muda mrefu mno kiasi kwamba hata Roma alijikuta akipitiwa na usingizi baada ya kuchoka kucheza gemu.

Mpaka inafika saa tisa na nusu bado hakuwa ameshituka,Roma alimwangalia Edna na kuishia kutabasamu , ukweli ni kwamba Roma aliona alikuwa na safari ndefu sana ya kumfahamu mke wake.

“Anaonekana hakulala usiku mzima, sijui ni kipi kinachomfanya kuwa bize kiasi cha kutolala” Aliwaza Roma na muda huohuo Edna alishituka huku akionekana ni kama alikuwa amekurupushwa.

“Wife unaonekana ulikuwa umechoka sana”Aliongea Roma huku akianza kuachama , kwani alihisi njaa.

“Saa ngapi?”Aliuliza Edna.

“Saa Tisa”Edna alijikuta akitoa macho hakujua kuwa amelala muda wote huo , alijishngaa kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala ofisini Zaidi ya masaa sita.

“Nimepitiliza”Aliongea Edna huku akimwangalia Roma na macho yaliokuwa na usingizi bado.

“Ndio umelala sana mke wangu, yaani huwa nakushangaa Edna kwanini unafanya kazi kama huna hela”aliongea Roma lakini Edna hakutaka kumsikiliza alinyanyuka na kisha akazama kwenye mlango upande wa kulia , ulikuwa mlango wa maliwato kwani ofisi ya Edna ilikuwa imeunganishwa na choo na bafu kwa ndani.

Baada ya dakika kumi hivi kupita Edna alitoka huku akiweka nywele zake vizuri,ile chai ambayo Roma ameleta haikuwa na maana tena kwani muda ulikuwa umeenda na ilishapoa , Roma aliona jambo la maana hapo ni kutoka na Edna kwenda kupata chakula cha mchana.

“Wife nina njaa twende tukale kabla ya kwenda nyumbani”Aliongea Roma na nikama Roma alishitua njaa, na Edna alikumbuka hakuwa ameweka chochote tumboni tokea jana usiku, alimwangalia Roma na kisha akatingisha kichwa kukubali.

“Leo saa mbili nadhani hujasahau Roma”Aliongea Edna baada ya kuingia barabarani.

“Nishasahau mke wangu unaonaje ukinikumbusha”Aliongea Roma na ni kweli alikuwa ashasahau.

“Kusanyiko la wafanyabiashara ni leo , tukitoka kula unipeleke nikatafute nguo ya kuvaa maana nimesahau kuandaa”Aliongea

“Usijali mke wangu , nitaenda kukuchagulia mimi mwenywe , nguo itakayokupendeza , nataka usiku wa leo uonekane kama malkia kwa kupendeza , na hivyo ulivyomzuri mke wangu”Edna aliishia kutabasamu na kuangalia mbele.

Roma hakuwa akijua wapi asimamishe kwa ajili ya wao kupata chakula cha mchana , aliendesha taratibu , huku akiangaza macho kulia na kushoto na baada ya dakika kumi aliona sehemu ambayo ilikuwa ni nzuri kwa wao kukaa kwa ajili ya kula.

Ulikuwa ni mgahawa uliokuwa ndani ya posta , uliokuwa ukifahamika kwa jina la Rachel Dishes , ni mgahawa maarufu sana na ulikuwa umepakana na Mgahawa wa vyakula vya kichina.

Edna alipenda piam azingira ya mgahawa huo na waliangalia sehemu ambayo inawafaa kwa wao kukaa , sehemu hii ilikuwa na watu , licha ya kwamba sio wengi sana , maana muda ulikuwa umeenda.

Leo ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Roma kutoka na mke wake kwa ajili ya chakula tokea wafunge ndoa yao.

“Bebi unajua leo ndio siku yetu ya kwanza kutoka pamoja kama hivi kupata chakula”Aliongea Roma na Edna alimwangalia na kisha hakuongea chochote huku akiangalia chakula cha kuagiza kwenye kitabu cha orodha.

Baada ya dakika kama kumi na tano waliwekewa chakula chao na kuanza kula ,Roma alimwangalia Edna na wakakutanisha macho na Roma akatabasamu na kuendelea kula.

“Natamani maisha yangu yangekuwa hivi , ila naona kama nina safari ndefu”Aliwaza Roma.

****

Naam ni muda wa Saa mbili kamili za jioni ndani ya hoteli iliokuwa pembezoni mwa ufukwe wa Kunduchi , hoteli iliokuwa ikimilikiwa na Maple Group , hoteli ambayo ilikuwa maarufu sana ambayo ilikuwa ikifahamika kwa jina la Apple hoteli.

Hoteli hii ilikuwa imepakana na majengo mawili yaliokuwa yakifanana na yote yalikuwa yakimilikiwa na kampuni ya Maple , jengo la kulia lilikuwani la Apartment na jengo la kushoto kwake ndio ilikuwa hoteli hii nzuri ya kimataifa.

Hapa ndani ya hii hoteli ndio mahali ambapo kusanyiko la wafanyabiashara lilikuwa likifanyika na sasa ni muda wa saa mbili kamili za usiku gari za kifahari zilionekana kuingia ndani ya eneo hili kwa kupishana na kuegeshwa katika eneo maalumu,

Ni saa mbili kamili dakika kumi na tano,Gari ya kifahari aina ya Roly Royce iliingia hapa ndani na kwenda kusimama katika eneo la maegesho na baada ya gari hii kusimama, alishuka dereva ambaye alikuwa ni Roma Ramoni na kuzunguka upande wa pili na kufungua mlango na hapa ndipo alipoonekana mwanamke Mrembo sana akiingia na mwanamke huyu hakuwa mwingine bali ni Edna

Upande kulia wa jengo hili alionekana Seif Ramadhani mwanajeshi kutoka jeshi la Irani aliezamia nchini Tanzania kwa sababu ambazo hazikuwa zikifahamika , bwana huyu alionekana akiwa ndani ya jengo hili huku akiweka bunduki yake vizuri aina ya Assault Sniper Riffle Koflo 64 iliotengenezwa nchini Urusi.

Bwana seif alionekana kujiamini mno , baada ya kuweka standi ya kusapoti bunduki lake , aliweka jicho kwenye Lensi ya bunduki hii na na kuvuta pumzi kwa ishara ya ahueni.

“Target is clear in Position 12 O Clock”Alionekana alikuwa akiongea na mtu na kumwambia kuwa tageti yake inaonekana.

“Fanya haraka na kisha utoweke sehemu ya tukio”Ilisikika sauti ya upande wa pili.

Baada ya Seif kuruhusiwa , alimlenga vizuri , huku mtu aliekuwa akionekana kwenye lensi yake alikuwa ni mrembo Edna , bwana huyu alivuta pumzi nyingi na kuzizuia na kisha akazilekeza kifuani na palepale akavuta Triga na Risasi ikachomoka kuelekea ndani ya ukumbi uliokuwa ukifanyia kusanyiko.

MWISHO WA SEASON 02

UNAJUA NINI KIMETOKEA ..
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 84 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
 
Jaman imeishia patamu hivi pls kimoja tu[emoji120][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…