Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 188

Edna alionekana kuwa na hasira , alionekana alikuwa na mambo mengi ambayo alikuwa ameyaweka moyoni muda mrefu , mrembo huyu kama ilivyokuwa tabia yake , tabia ya kutopenda kuuliza , lakini pia tabia ya kutopenda kujielezea ilimfanya kuficha mambo mengi sana na kuyakalia kimya , kwa mfano Edna tokea anafika Ufaransa alikuwa akifikiria swala la Roma Kwenda kujitambulisha nyumbani kwa Nasra, lakini swala lingine Edna alikuwa akifahamu Roma alichokifanya mara baada ya kupotea kwake , siku ambayo alienda kupigana na Ares na baada ya kurudi akaenda kuua watu wa kundi la Fupa Faru kwa ajili ya Rose, mambo yote hayo Edna yalikuwa kwenye moyo wake na hakuyatafutia maelezo kabisa licha ya kuyafahamu, wala kutaka kuuliza Zaidi ya kukaa kimya, lakini mbaya Zaidi ni baada ya kumuona mwanamke akitoka kwenye chumba cha Roma asubuhi, Edna alijiambia Roma hakuwa siriasi na yeye na alikuwa akimchukulia kabisa kama mwanamke wa mkataba pekee ndio maana anafanya mambo anavyotaka hata kumuahidi Nasra Kwenda kujitambulisha ukweni .

Roma mwenyewe alishangaa , hakuwa akifahamu kama Edna alikuwa akijua kama aliua watu wa kundi la Fupa Faru kwa ajili ya Rose, alijiuliza ni mambo mangapi Edna alikuwa akiyajua na ameyakalia kimya.

Lakini alijiambia huenda Edna pointi yake ni ya msingi , alijiuliza kama Edna atajua ukweli wote wa Maisha yake ya nyuma ni kipi ambacho angefanya ,Je angekuwa na furaha na kumkumbali yeye kama mume na kujitoa jumla jumla kwake , hilo ni moja ya maswali mengi yaliopita katika kichwa cha Roma.

“Edna maneno yako yanaumiza”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie Roma na kisha kuvuta pumzi ndefu kama mtu ambaye anakusanya ujasiri.

“Kama kweli unapenda nikuulize , basi naomba nikuulize swali moja tu”Aliongea Edna

“Unaweza kuuliza?”alijibu Roma.

“Niambie kuhusu Seventeen?”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae hapo hapo na kujiuliza Edna aliwezaje kujua hilo jina,kwani katika kumbukumbu zake hakuwahi kulitamka , lakini katika kufikiria hapo hapo jina la Clark liliibuka katika kichwa chake , aliamini kama Edna amejua hilo jina basi ni kupitia Clark.

*******

WIKI KADHAA NYUMA

Ni siku ambayo Edna alikuwa hospitalini , siku ambayo Roma , Sophia na Profesa Clark walienda kumtembelea Edna baada ya kupewa taarifa ya Edna kudhirai akiwa ndani ya hoteli ya Paridise siku ambayo aliweza kugundua kuwa baba yake mzazi ambaye alikuwa akimchukia kwa miaka mingi alikuwa sio baba yake mzazi.

Sasa muda huu wa jioni wakati Roma anaongea na simu nje mpaka kusimamishwa na Queen baada ya kugongana nae , upande wa ndani Sophia Edna na Clark walikuwa wakiongea.

“Edna nikiri kwamba unafanana kila kitu na Seventeen”Aliongea Profesa Clark na kumfanya Edna kushangaa , kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kusikia hilo jina na sio kwake tu hata kwa Sophia.

“Profesa!, Seveenteen ni nani?”Aliuliza Edna na kumfanya Clark kushangaa na mpaka hapo alijua ameropoka neno ambalo hakupaswa kuongea , maana kama Edna hakuwa akimjua Seventeen, basi ni hakika kwamba Roma hakuwa amemueleza Edna juu ya jambo hilo.

Sophia ilibidi waangaliane na Edna na kisha wakageuza macho yote kwa Profesa Clark wakitaka maelezo ya kumjua Seventeen ni nani.

“Jamani kama hamumjui Seventeen basi naamini Roma hajawaambia bado na naamini anayo sababu ya kutofanya hivyo”

“Profesa tuambie Seventeen ni nani?”Aliongea Sophia huku akimshika mkono Profesa Clark ili kueleza Seventeen ni nani.

“Edna naamini siku moja Roma atakwambia kuhusu Seventeen kwa undani Zaidi , ninachoweza kukuambia tu ni kwamba Seventeen ndio mwanamke pekee ambaye Roma aliwahi kumpenda sana.. Sijui nini kilitokea ila kwa maelezo ya Roma Seventeen alijiua akiwa mjamzito”Aliongea Profesa Clark huku akionyesha kujutia kwa kitendo chake cha kuropoka mbele ya Edna.

“Kwanini alijiua?”Aliuliza Sophia. Na kumfanya Edna amwangalie Clark.

“Kuhusu hilo sifahamu ,jamani najua sikupaswa kuwaambia juu ya hili ,Roma akijua nimewaambia anaweza kukasirika, naombeni msiongee chochote kwa sasa mpaka atakapotaka kuwaambia yeye mwenyewe”Aliongea na kuwafanya Sophia na Edna watingine vichwa kubaki na siri hio moyoni.

Na hata pale Roma aliporudi ndani ya chumba alicholazwa Edna hakuweza kuona mabadiliko ya aina yoyote , Zaidi ya Edna na Sophia kumuangalia.

Sasa hii ndio siku ambayo Edna alipata kujua jina la Seventeena kwenye Maisha ya Roma , lakini licha ya mrembo huyu kupata kujua kuna mtu anaeitwa Sventeen kwenye Maisha ya Roma , hakuwa tayari kumuuliza Roma juu ya huyo mtu na kukaa na jambo hilo moyoni.

“Sipo tayari kuona mwanamke wa pili anapoteza uhai

kwa ajili yangu”
Edna alikumbuka hio kauli ya Roma , siku ambayo alionana kwa mara ya pili na Roma na kupendekza swala la Roma kumuoa na pale Roma alipokataa na kutishia kujirusha na ndio Roma alipomzuia na kutamka kauli hio.

Edna baada ya kuunganisha matukio aliamini huenda maneno hayo yalikuwa yanamhusu Seventeen, lakini kama kawaida ya Edna hakuuliza , alilihifadhi moyoni.

*******

Taswira ya mto Seine ndani ya siku hii ilionekana kuvutia macho ya wengi waliokuwa wamekaa kandokando yake ,ni mto ambao umezungukwa na miti mikubwa aina ya London Platanus, miti iliogubikwa na majani ya kijani kibichi na manjano , huku kila upepo unapovuma juu ya miti hii hufanya majani ya manjano kupeperuka , kuna yale yaliokuwa yakitua kwenye reli na kuna yale yaliokuwa yakienda moja kwa moja ndani ya mto, Roma alikuwa ni moja ya watu waliokuwa wakiangalia namna majani hayo yalivyokuwa yakipeperushwa , huku akionekana kuingia kwenye mawazo, huku Edna akiwa upande wake wa kulia akiwa anasubiria jibu.

“Kwahio ushamfahamu tayari?”Aliuliza Roma.

“Vipi!,unaonekana haujapenda nilipotaja hilo jina , huenda nisingepaswa kukuuliza” Aliongea Edna.

“Sidhani kama napaswa kushangaa juu ya hilo,naamini Clark ndio kakuambia”

“Alitamka hilo jina tu , huku akianiambia nafanana kwa asilimia kubwa na mtu anaefahamika kwa Seventeen , hakunipa maelezo mengine , nataka nisikie kutoka kwako kuhusu Seventeen , lakini kama haupo tayari kuniambia usijilazimishe”Aliongea Edna.

“Nadhani sipaswi kukuficha juu ya hilo, ni mambo yaliopita na kila mtu katika Maisha lazima awe na kumbukumbu za maisha yaliopita , sio swala la mtu kuona aibu kuwa na kumbukumbu za nyuma , ziwe za kusikitisha au za kufurahisha,kuhusu Seventeen sidhani kama nitakuja kumsahau kwenye Maisha yangu na angalau imekuwa vyema umeweza kumfahamu kupitia Clark”

“Bado unampenda?”Aliuliza Edna.

“Mapenzi!, Sina uhakika kama bado nampenda au lah,Nimejuana na Seventeen miaka Zaidi ya ishirini na mbili iliopita kabla sijarudi Tanzania , Seventeen kwangu alikuwa ndio kila kitu , alikuwa ndio sababu ya mimi kuishi licha ya kupitia kipindi cha maumivu makali nikiwa katika utoto wangu , kila nilipofikiria kukata tamaa na kumwangalia Seventeen ambaye bado alinihitaji nilipata nguvu upya , hatukuwa wapenzi kwasababu hatukuwahi kutongozana na kuambiana tunapendana wala kupeana zawadi , muunganiko wetu ulikuwa ni Zaidi ya wapenzi , ,Seventeen alinihitaji ili aishi na mimi nilimhitaji vilevile ili niweze kuishi,huenda ningemwambia kama nampenda na akawa mpenzi wangu , huenda asingechukua maamuzi ya kijinga alioyafanya… Seventeen ni mwanamke wa kipekee sana kwenye Maisha, aliebaki katika kumbukumbu zangu…”Roma alijikuta akiishia njiani , kwa mara ya kwanza aliongea pasipo kuwa na tabasamu kwenye macho yake, huku macho yakiwa mekundu mno , ilionesha Maisha alioishi na Seventeen yalikuwa ya kuumiza sana , kiasi kwamba hakutaka kabisa kukumbuka yaliowatokea, Edna na yeye alijihisi moyo kuuma kwa jinsi Roma alivyokuwa akiongea.

“Umeuliza kama na mpenda! , kwangu Seventeen sikuwahi kumtamkia neno nampenda hata siku moja na yeye hakuwahi kuniambia ananipenda, tulizungumza maneno machache sana kuhusu mapenzi , vitu tuulivyongea ni namna ya kuweza kushinda kiza kilichokuwa mbele yetu , kwangu kuwa karibu yake ilikuwa ni Faraja, ukiniuliza kama nampenda ukweli sijui namna ya kujibu hilo swali”Aliongea Roma.

“Clark alisema nafanana nae kwa kiasi kikubwa , hilo ni kweli?”

“Ndio mnafanana kwa asilimia kubwa sana na Seventeen , ila utofauti wenu ni kwamba wewe ni mtembo Zaidi kuliko Seventeen , usisikilize maneno ya Clark , hana anachojua kuhusu Seventeen Zaidi ya kuona picha yake tu”Aliongea Roma.

“Kwahio unavyoniona kwako unanichukulia kama mbadala wa Seventeen?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kushangaa kidogo.

“Seventeen ni Seventeen na wewe ni mke wangu kwa sasa, Seventeen kwangu amebakia kuwa kumbukumbu nisizoweza kuzisahau, kama ningekuwa nakuchulia kama Seventeen nisingejali hisia zako”Edna alionekana kuridhishwa na jibu alilipewa na Roma.

“Unakumbuka mara yangu ya pili na wewe kukutana ndani ya hoteli , wakati nilivyokuambia kuwa nataka unioe na ukanikataa , na hata pale nilipolazimisha kujirusha kwenye lile jengo ukabadilika ghafla na kunizuia, nahisi ile siku nilikukumbusha kuhusu Seventeen , ndio maana ulikiubali kunioa”Roma alifikiria kidogo , ukweli siku ile ni kweli kitendo cha Edna kutaka kujirusha kwenye lile jengo la hoteli kilimrudishia kumbukumbu za nyuma juu ya kitendo alichokifanya Seventeen.

“Siwezi kupinga , ulinifanya nikumbuke kilichotokea miaka ya nyuma ndio maana nikakubaliana na wewe , lakini hata hivyo sijawahi kukuchukulia kama mbadala wa Seventeen”

“Kama ni hivyo basi naamini ninapaswa kushukuru uwepo wa Seventeen kwenye hii dunia, kama sio yeye huenda Maisha yangu mpaka sasa yangekuwa yashabadilika , huenda baba yangu mzazi angeniua , lakini pia hunda ningekuwa kwenye Maisha ya ndoa na mtu nisiekuwa nikimpenda…”Aliongea Edna na kuishia njiani huku akianza kulia na kumshangaza Roma na kumfanya ageuze macho kuangalia watu waliokuwa ndani ya eneo hili , kwani aliogopa watu wakishuhudia Edna akilia mbele yake,aliamini Wazungu wangemshangaa kwa kumfanya mwanamke mrembo kama Edna kulia na alishukuru uwepo wa Sauroni , kwani watu walikuwa wametawanyishwa.

“Edna nyamaza basi , kama kuna sehemu hujaridhika na majibu yangu niambie”Aliongea Roma , huku akishindwa ni hatua gani azichukue kwa wakati huo , siku zote amemzoea Edna kuwa kauzu na mtu wa kuficha hisia zake , lakini mabadiliko ya leo ya Ghafla yamemfanya kushangaa kidogo.

Licha ya Edna kumwambia Edna anyamaze , lakini Edna hakunyamaza Zaidi ya kuangalia chini na kudondosha machozi.

“Edna nishasema wewe ni Edna na Seventeen ni Seventeen, Sijui unafikiria nini lakini sijui cha kufanya kwenye hali uliokuwa nayo”Aliongea Roma na Edna alinyanyua kichwa chake na kumwangalia Roma.

“Clark aliniambia kuwa Seventeen alikuwa na ujauzito wako, Ni kweli?”Aliuliza Edna na Roma alitingisha kichwa kukubali.

Ukweli kwa upande wa Roma hakupenda kukumbuka tukio la miaka kadhaa iliopita , kitendo cha Seventeen aliekuwa na ujauzito wake kujirusha kwenye bahari iliokuwa imejaa mabarafu ,tena mbele yake kilikuwa ni cha kuumiza sana na kwake ndio sababu nyingine iliomfanya Roma kuchukulia wanawake kama chombo cha Starehe , Alikuwa akitumia wanawake kwa ajili ya kujipoza na maumivu , lakini maumivu hayakupita na kadri maumivu ya moyo yalivyozidi kumuendesha ,ndipo tatizo lake la ubongo kuwa kubwa Zaidi , Profesa Clark alijaribu kumsaidia Roma ili aweze kupunguza mawazo , lakini alishindwa kabisa na kuogopa mno na kushindwa kujua cha kufanya, na hata pale Roma alipompa taarifa ya kuondoka nchini hakuwa tayari , lakini pia hakuweza kumzuia Roma.

Hivyo ndio ilivyokuwa, moja ya sababu kubwa ya Roma kurudi Tanzania , aliamini kwa kuishi Maisha ya kawaida , huenda ingekuwa rahisi kwake kumsahau Seventeen na hata pale aliporudi nchini hakuwa tayari kujihusisha na wanawake kabisa , kwani aliona wanawake hawakuwa wakimsaidia Zaidi ya kumfanya kumkubuka Sevcenteen.

“Kama ni kweli Seventeen alikuwa na ujauzito wako , naomba nikuulize swali la mwisho”

“Okey unaweza kuuliza”

“Kama Seventeen yupo hai na akajitokeza kwako , akiwa na mtoto wako na yupo tayari kwa ajili ya kuanza upya na wewe ,je utaendelea kuwa na mimi au utaenda kwa Seventeen?”

“Nyamazaa….!!!!”Aliongea Roma kwa sauti kubwa na mwonekano wake ulibadilika palepale na hata macho yake yalibadilika na kuwa ya kijani.







SEHEMU YA 189.

Edna licha ya Roma kubadilika , alionekana kutohofia kitu chochote , alimwangalia Roma pasipo hata ya kupepesa macho na alionekana alitaka jibu lake licha ya Roma kubadilika.

“Seventeen….. Seventeen na mtoto wake walishakufa zamani na sitaki tena kusikia ukilitamka hilo jina mbele yangu”Aliongea Roma kwa sauti isio ya kawaida.

“Huna haja ya kuzificha hisia zako, unaonekana kabisa kwenye moyo wako unashindwa kututofautisha mimi na Seventeen , ndio maana unaonesha kunijali na kutaka kunilinda”Aliongea Edna huku akiangaliana na Roma kwenye macho, pasipo ya kuogopa kabisa , ni kama mtu aliekuwa akijiambia licha ya Roma kubadilika asingeweza kumdhuru..

“Edna nakuambia kwa mara nyingine kaa kimya”Roma aliongea huku akimsogelea kabisa Edna karibu kama mtu ambaye anajaribu kumuogopesha kwa muonekano wake.

Roma mwenyewe alishindwa kujielewa kwanini alikuwa na hasira za namna hio, baada ya Edna kutaja jina la Seventeen mfululizo.

“Roma acha kujidanganya, ninachojua huwezi kunitofautisha mimi na Seventeen na unajishawishi tu kusema kama sisi ni tofauti , ila unafanya hivyo kwa ajili ya kujipozapoza maumivu yako yakuachwa ,hukutaka kuwa na mwanamke mwingine kwasababu ulihisi utakuwa dhaifu ,kutokana na kumbukumbu za Seventeen na kwako mimi ni kama kitulizo cha mateso yako, Kama kweli unaweza kunitofautisha na Seventeen kwanini ukaamua kumuacha Rose , mwanamkie ambaye naamini anakupenda na wewe unampenda na kukubali kuoana na mimi ambaye kwangu ninachojali zaidi ni kazi , sikuwahi kukupa hata nafasi ya kuingia kwenye chumba changu wala kuonyesha ishara yoyote ya kukupenda upo na mimi kwasababu nafanana na Seventeen huo ndio ukweli.

Maneno ya Edna yalikuwa ni makali kiasi kwamba yalikuwa yakipita kwenye masikio ya Roma kwa kujirudia rudia na kumfanya kichwa chake kuanza kuuma.

“Edna tafadhari , nakuomba uache kuongea tena kuhusu Seventeen”

“Nisamehe kama maneno yangu yanaonekana kuwa makali , lakini huo ndio ukweli haukuwahi kunichukulia mimi kama mimi , najua ni mengi umenisaidia kwa muda mfupi tuliokuwa Pamoja , lakini tokea siku Clark aliponiambia kuhusu Seventeen , nilikuwa nikiwaza sana , haikuwa rahisi kwangu kama unavyofikiria na angalau leo hii nimeweka wazi kile kilichopo ndani ya moyo wangu”Aliongea Edna ila kwa upande wa Roma alishindwa kujibu chochote , aliona anaweza kushindwa kujizuia muda wowote ndio maana akaugeukia mto.

“Mimi nishamaliza na narudi ndani kuendelea kuangalia maonyesho , kama hujisikii kuungana na mimi unaweza kurudi kupumzika ila naamini pia rafiki yako yupo hapa kwa ajili ya kuongea na wewe”Aliongea Edna na kujiweka sawa na kuanza kupiga hatua kurudi ndani.

Edna licha ya kujiweka sawa , lakini macho yake hayakujificha kama alikuwa akilia , Stern na Alice waligundua pia hilo , ila hawakutaka kuuliza lolote na kuendelea kuangalia mbele.

“Miss Edna tunaweza kuanza tukio?”Aliuliza Meneja na kumfanya Edna amwangalie.

“Kwanini unaniuliza mimi?”

“Tulikuwa tukisubiri uwepo wenu ndio tuanze”Aliongea Meneja.

“Mnaweza kuanza tu , kilichotokea hapa ni maswala binafsi”Aliongea Edna na Meneja alitabasamu na kisha kuinamisha kichwa chake kwa heshima na kusogea jukwaani na kumnong`oneza mshereheshaji kuanza tukio.

Upande wa nje Roma alitulia kwa dakika kama mbili hivi mpaka alipoinua mkono wake na kumpa ishara Sauroni ya kumsogelea na Sauroni alifanya hivyo.

“Sauron, I’m going to ask you something, be honest with me.”

“Sauroni nitakuuliza kitu na naomba uwe mkweli na mimi”

“Your Majesty Pluto, I never lie.”

“Mfalme Pluto , Mimi sidanganyi”

“Tell me then, in your eyes, am I someone who will cower in the face of my own weaknesses…”

“Hebu niambie kwenye macho yako ,naonekana kama mtu ambaye naweza kuogopa kudili na udhaifu wangu”

“Mfalme Pluto ijapokuwa mimi ni mshirika wako , lakini kwa umri wako naamini hilo swali ni la kitoto”Aliongea Sauroni na kumfanya Roma kucheka.

“Kwa kauli hio naamini Swali langu ni la kijinga”

“Mfalme Pluto ninachoamini ni kwamba muda mwingine inakuwa ngumu kwa mtu kuutambua uongo na ukweli , ila ilimradi unaweza kutambua kusudio halisi ndani ya moyo wako basi hupaswi kujiuliza maswali , Nguvu ya kweli haitegemei nguvu ya kimwili bali ni ule uwezo wa kukabiliana na matatizo na kuyatafutia ufumbuzi”

“Haha.. Sauroni nadhani kweli swali langu lilikuwa la kipumbavu , ulichoongea ni sahihi , kama kweli nina uwezo wa kukabiliana na matatizo yangu , kuwa imara au dhaifu sio swala la kujionea aibu”Aliongea Roma na Sauroni alitabasamu baada ya kuona mapokeo ya Roma.

“Mheshimiwa Pluto,Sidhani kama unataarifa juu ya mkutano wa siri wa Kimataifa unaofanyikia hapa Paris chini ya DGSE?”Aliuliza Sauroni na kumfanya Roma kushangaa.

“Mkutano wa siri?” Sijawahi kusikia juu ya hilo Sauroni”

“Nadhani umechelewa tu kupata taarifa juu ya huu mkutano Mfalme Pluto , kiufupi ni kwamba huu ni mkutano ulioandaliwa na Serikali ya Ufaransa na unahusisha , mashirika ya kijasusi , Vikosi maalumu na baadhi ya mashirika pia yanayotumia nguvu za ziada na kwa kile tulichogundua ni kwamba moja ya ajenda za mkutano huo pia unahusika”

“Unamaanisha nini Sauroni kama nahusika?”

“Your Majest!, “It’s about the gods”

“Kwanini kikao kiwe ni kwasababu ya The Gods Sauroni”

“Mfalme kwa maelezo ambayo hatuna uhakika nayo ni kwamba Mataifa ya Ulaya Pamoja na Marekani wanajiandaa kuingia Vitani na Appolo, licha ya kwamba ni tetesi tu kwa sasa , ila naamini kuna jambo kubwa linaendelea”

“Sauroni sijafautalia maswala haya kwa muda mrefu kidogo”

“Ndio Mfalme Pluto ,Tokea umerudi nchini Tanzania , Appolo Pamoja na jeshi lake waliweza kushambulia baadhi ya kambi za kijeshi za Urusi , EU pamoja na NATO, lakini mbaya Zaidi ni kwamba Appolo ameenda mbali na kuanza kuandikia barua za vitisho baadhi ya viongozi wa kubwa wa nchi , akiwemo Raisi wa Ufaransa, , Kwa taarifa tulizopata ni kwamba Appolo pia amehusika na kuteka baadhi ya matajiri wakubwa waliohudhuria maonyesho ya Fasheni hapa Paris”

“Sauroni hata mimi pia pamoja na mke wangu ni moja ya wahanga wa tukio hilo”Aliongea Roma na Sauroni akatabasamu.

“Sikudhani Umeweza kukutana na mkasa huo Mfalme Pluto , Nimefika hapa kwa ajili ya kumuona Madam Persephone lakini pia kulizungumzia swala hili”

“Haha.. Sauroni hebu niambie kwanza mmeweza kumfahamu Appolo mpaka sasa hivi?”Sauroni alitingisha kichwa akimaanisha Hapana.

“Mfalme ninachotaka kukuambia ni kwamba kwenye mkutano utakaofanyika siku ya kesho licha ya ajenda kuu ni juu ya kutafuta namna ya kumuangamiza Appolo na kundi lake , lakini pia kuna swala ambalo linahusiana na wewe?”

“Swala gani tena Sauroni?”

“Ni juu ya majadiliano juu ya umiliki halali wa teknolojia iliotumika kutengenezea siraha aliopoteza Mfalme Pluto wa kwanza”

“Sauroni unamaanisha Thanatos!?”Roma alishangaa , alikuwa akijua sana juu ya Teknolojia iliokuwa imepewa jina la Thanatos , Teknolojia ambayo ilivumbuliwa na wanasayansi kutoka kisiwa cha wafu na mfalme Pluto wa kwanza kabla hajamrithi.teknolojia ambayo ilikuwa ikifanyika kwa kucheza na DNA za mwili na kumfanya mtu kuwa kama sumu kwa Maisha ya binadamu , kwani kama mwili wako utatengenezwa kwa tekonolojia hio basi utakuwa hata na uwezo wa kumuua mtu kwa kumgusa tu ndio maana ikaitwa kwa jina la Thanatos.

Sasa kwa kumbukumbu za Roma ni kwamba, Mfalme Pluto wa kwanza alipoteza kanuni za kutengeneza siraha hio , huku mwanasayansi aliehusika na utafiti kufariki .

“Ndio mfalme Pluto ,kwasasa taarifa zinaonyesha teknolojia hio ipo chini ya Serikali ya Ufaransa na Appolo ni moja ya watu wanaotaka hio teknolojia kwa nguvu ndio maana akatishia hata kuteka baadhi ya matajiri , lakini pia kumpa siku saba Raisi wa Ufaransa kusalimisha hio Teknolojia kabla ya kuvamia ikulu na kumuua”

“Sauroni nina hamu ya kutaka kuona uwezo wa hio teknolojia , lakini nahisi kwangu haina matumizi makubwa”

“Mfalme naamini hio teknolojia ni moja ya sehemu ya Urithi wako kutoka kwa Mfalme Pluto wa kwanza na ni haki yako kuimiliki, Mfalme Pluto kama unaona hutaki kujiingiza kwenye matatizo sisi The Eagles tutakusaidia katika hilo na kuhakikisha Teknolojia hio inarudi kwenye mikono yako”

“Sauroni unaweza usinielewe ila kwangu hio teknolojia haina maana , nadhani Appolo anaitaka kwa ajili ya kujiongezea nguvu , lakini sio kwa upande wangu”Aliongea Roma.

“Naamini kwa asilimia kubwa mtu aliechukua HollyGrail ile siku na kwenye huu mkutano anaweza akawepo ,ni muhimu nikashiriki na mimi ili kama atawepo niweze kumjua zaidi”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake.

“Sauroni kikao kinafanyikia sehemu gani?”

“Sauron, where will the secret meeting be held tomorrow night?”

“Kitafanyikia ndani ya kambi ya kijeshi ya Le Havre ,usafiri Kwenda hujo ni kwakutumia meli ya Louis XVI mfalme”

“Sauroni nadhani kuna umuhimu wa mimi kuhudhuria”

ITAENDELEA





ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 190

Muda ambao Roma na Sauroni walikuwa wakiongea upande mwingine kaskazini mwa jiji la Paris,katika bandari ya Le Havre ,inaonekana meli kubwa ya kifahari ikiwa imesimama , meli iliokuwa ikifahamika kw ajina la Louis XVI, ilikuwa ni meli ya kifahari kubwa yenye urefu unaolingana na nusu ya kiwanja cha mpira iliopakwa rangi ya Silver.

Upande wa kuingilia ndani ya meli hii kuna ngazi ndefu zilizofungwa kutoka nchi kavu mpaka kwenye meli , huku zikiwa zimefunikwa na zulia la rangi nyekundu , Pamoja na kupendezeshwa na maua mazuri yaliokuwa yamewekwa pande zote , watu waliokuwa ndani ya hili eneo hawakuweza kufahamu kama Meli hio ilikuwa ikisubiria kukaribisha watu wazito sana katika medani za usalama ndani ya dunia , ila walichokuwa wakifahamu ni kwamba meli hio ililikuwa ikikaribisha watalii.

Muda huu Fodesa Pamoja na Depney waliokuwa wamevalia mavazi ya kawaida , walioekana wakitoka kwenye meli hii na kwa haraka haraka tu walionekana walikuwa wakifanya ukaguzi, wakati wakishuka kwenye ngazi Depney aliangalia ukubwa wa meli hii na kisha alionekana kuridhika na kumgeukia Fodesa.

“Vipi Thanatos ishapelekwa tayari kisiwani?”Aliuliza Depney.

“Ndio ,Jana tuliweza kuituma chini ya uangalizi wa idara ya ‘Ant Spy’ kwa kutumia meli ya kivita na mpaka sasa ulinzi mkali umeimarishwa kambini”Aliongea Fodesa

“Hapo sawa , awamu hii tuhakikishe hakuna makosa yanafanyika , teknolojia hii ipo kwenye mikono yetu hivyo lazima tuwe wanufaika ndani ya kikao tunachokwenda kufanya”Aliongea Depney na kumfanya Fodesa kutingisha kichwa.

“Boss hivi ni lini serikali yetu ikawa na teknolojia ya siraha kama hii ya kimauaji?”

“Fodesa licha ya kwamba wewe upo chini yangu , lakini huwezi kujua kila kitu kinachoendelea kwenye hii nchi , ninachokushauri ni kujikita Zaidi katika kuhakikisha mkutano huu unafanikiwa na Appolo haleti madhara ya aina yoyote, kesho sitokuwepo moja kwa moja kwenye mkutano,kuna baadhi ya mambo ninatakiwa kuyafanyia kazi , nyuma ya pazia wakati mkutano unaendelea”Aliongea Depney na ilimbidi Fodesa asiendelee kuuliza.

“Director kwanini usihudhurie?”

“Hio kazi ya kuhudhuria utafanya wewe Fodesa , ndio maana ukaitwa msaidizi wangu”Aliongea Depney na kisha kumuacha Fodesa nyuma.

“Chifu naona Director anaogopa kuhudhuria mkutano ndio maana anakusukumizia majukumu yake, naamini huenda kuna jambo baya linaweza kukutokea , kwanini usikatae”Aliongea Boltoni aliekuwa nyuma ya Fodesa.

“Boltoni hatupaswi kumsimanga Depney juu ya hili , kwanza hili kwangu ni kama fursa”Aliongea Fodesa na kumfanya Boltoni atingishe kichwa.

“Boltoni unajua mpaka sasa sijui kwanini huu mkutano tuna uandaa, licha ya hivyo naamini pia kuna jambo kubwa linaendelea na Serikali imeona kukaa na Teknolojia ya Thanatos ni mbaya kwani tunaweza tusiwe na uwezo wa kuilinda”

“Lakini kama tutaachia teknolojia hii Kwenda kwenye baadhi ya mataifa makubwa kama Marekani si inaweza ikawa shida kwetu”

“Sidhani kama swala hili linaweza kuleta shida , kuna jambo kubwa Zaidi ya mazungumzo ambalo litatokea siku ya kesho na ninatamani sana kushuhudia”Aliongea Fodesa.

*****

Ratiba ya maonyesho ya fasheni ilienda haraka haraka na kampuni kubwa za mtindo ziliweza kuonyesha kile walichokiandaa kwa siku hio..

Roma hakurudi kabisa ndani ya maonyesho hayo , kwanza haikuwa moja ya hobi yake kuangalia mitindo , baada ya kuachana na Sauroni aliishia kutembea tembea ndani ya eneo hilo huku akiwa ameshikilia kahawa yake mkononi, katika kichwa chake hakuwa akifikiria mambo aliongea Sauroni , bali yeye alikuwa akifikiria namna ya kuendelea kuishi na Edna na kukomaza uhusiano wao , Maneno alioongea mke wake yalikuwa yakijirudia rudia kwenye kichwa chake , licha ya kwamba walikuwa wameishi muda mfupiu sana na Edna , lakini ni mengi ambao yametokea hapo katikati na aliona Edna ashaanza kutegeneza hisia za mapenzi na yeye ndio maana akaongea maneno aliokuwa akiongea na hilo halikumshangaza sana , lakini bado alitaka kujua ni namna gani ataweza kuyajenga na Edna na kuendelea kuishi nae , huenda hata kubatilisha mkataba wao wa ndoa na kuona kihalali, Roma baada ya kuona kufikiria kwake hakuna majibu , aliona aachane na swala hilo na hata hivyo muda ulikuwa umeenda na watu walikuwa wakitawanyika kwa ajili ya chakula cha mchana , hivyo alipiga hatua kurejea ndani kwa ajili ya kumchukua Edna.

Edna baada ya kughairishwa kwa tukio kwa ajili ya chakula cha mchana , alichukua mkoba wake na kutaka kuanza kupiga hatua , lakini ile anageuka nyuma aliona Stern na Alice walikuwa wamekumbatiana wakiwa kwenye usingizi mzito na walionekana kutojua kile kinachoendelea , Edna alifikiria kidogo na kuona sio vyema kuwaacha wakiendelea kulala , alichofanya ni kumshitua Stern kwa mkono , lakini bado hakukuwa na majibu.

“Babe Edna hapo wenzio wapo kwenye ulimwengu wa mapenzi na sio rahisi kuwaamsha kwa staili hio”aliongea Roma na kumfanya Edna amgeukie Roma na kumwangalia machoni na kisha kuangalia chini , alionekana kukumbuka maneno yake ya kulalamika muda mcgache uliopota , jambo ambalo hakuwahi kulifanya katika Maisha yake , hivyo alihisi aibu mbele ya Roma.

“Ngoja nikusaidie kuwaamsha”Aliongea Roma na kisha aliwasogelea Alice na Stern na kisha akainua mguu wake wa kulia na kupiga teke kiti na wote kwa Pamoja walidondoka kama mafurushi na wakashituka wakiwa chini.

“Mr Roma wewe ni mkatili sijapata ona”aliongea Alice kwa kulalamika huku akiamka kivivu na kumshika mkono mpenzi wake.

“Baada ya kunishukuru mnaniona kama mkatili , ni roho yangu nyeupe ndio ilionifanya niwaamshe la sivyo ningewaacha hapa na kuondoka”Aliongea Roma

“Okey Mr Roma tutaacha hili lipite maana tunamtegemea Miss Edna kwa ajili ya chakula cha mchana”Aliongea Stern na kumfanya Roma amwangalie Edna.

“Mh! Walipoteza kadi zao za benki hivyo hawana pesa za kutumia siku ya leo”Aliongea Edna.

“Hata kama kuna haja gani ya kuwasaidia , ukoo wao si unapesa nyingi, hata tusipo wasaidia hakuna ambacho kitawapata”Aliongea Roma , ukweli hakutaka kuongozana na hao wapenzi , yeye alitaka kuwa karibu na mke wake Edna ili kumpeti peti na kuyajenga.

“Miss Edna Roma anaonekana hatupendi , ni kweli hatuna pesa”Aliongea Alice kwa kulalamika

“Alice msijali sana na maneno yake , tutaenda Pamoja kwa ajili ya chakula cha mchana, mimi sio mwenyeji sana wa Paris mnaonaje mkachagua wapi tunapaswa kwenda”

“Kuna mgahawa mzuri wa kiitaliano upo Avenue des Champs-élysées, napendekeza hapo”Aliongea Alice.

Roma aliwaangalia hawa kaka na dada na kutoa tabasamu la kifedhuli , kuna kitu ambacho sio cha kawaida ambacho ameweza kukigundua kutoka kwao ila kwa upande wa Edna hakuweza kukigundua , yeye alichoona kutoka kwa hao wapenzi ndugu, ni kwamba walionekana kama Watoto.

“Okey ! basi tunapaswa kuwahi , nina mpango wa kurudi kuendelea na maonyesho”aliongea Edna.

“Mke wangu kama kawaida na juhudi zako”

“Nipo Paris kwa ajili ya kazi”Aliongea Edna kwa kiswahili huku akianza kupiga hatua kutokaa ndani ya ukumbi huu.

Dakika chache mbele Roma aliekuwa akiendesha alikuja kupaki gari ndani ya mtaa huu wa Avenue des Champs-élysées, ni moja ya mitaa mizuri mno ndani ya jiji la Paris , ni sehemu ambayo kwa hapa Tanzania huwezi kuipata, mpangilio wa miti midogo midogo na bustani zilizopandwa kwenye mtaa huu zilifanya uvutie kwa kiasi chake , na hii ilidhihirisha namna Wazungu walivyokuwa wakiheshimu usafi wa mazingira.

Edna mwenyewe alijikuta akitoa tabasamu kwa utulivu na uzuri wa mitaa hii , huku akiangalia namna watu walivyokuwa bize , huku kila mmoja kuvaa mavazi ya kimtindo wake , Stern na Alice pia walionekana kufurahishwa sana na namna mtaa huu ulivyokuwa ukionekana , walikuwa wapo mbele yao huku kila wakitembea mita kadhaa walikumbatiana na kupigana mabusu na kumfanya Edna atabasamu na utoto wanaofanya.

“Mke wangu naona kama unawaonea wivu kwa namna wanavyoendana na kupatana, hata mimi sijali kukubusu na kukukumbatia mbele za watu”Aliongea Roma na kumsogelea Edna , lakini aliishhia kupigwa na mkoba tumboni na Roma kujifanyisha kaumia.

“Siwezi fanya matendo ya kichafu mbele za watu”Aliongea Edna.

“Haijalishi kama ni matendo ya kichafu, waangalie Alice na Stern wanachokifanya , licha ya watu kuwaona wachafu , lakini wanafurahia Maisha yao”Aliongea Roma

“Unajua maana ya jina la huu mtaa?”

“Sijui , Maana yake ni nini?”

“Elysee maana yake ni baraka ,Kwa hapa Ufaransa ndio wanaita mtaa huu sehemu ya kuwa na furaha ndio maana unaona watu wengi wanaonekana kuwa na furaha”

“Maelezo yako yanaonekana kuwa na maana kubwa , lakini kuna jambo naona kama halijakamilika”

“Unamaanisha nini?”Aliongea Edna lakini jibu alilopata lilikuwa la aina yake kwani Roma alimsogelea pasipo ya uelewa wake na alijikuta ameshikwa mkono upande wa kulia.

“Unafanya nini?”Aliuliza Edna akiwa kwenye hali ya aibu.

“Hebu angalia namna watu wanavyotembea ndani ya hili eneo”Edna alingalia na kuona watu wakiwa wanatembea wakiwa wameshikana mikono na wengine kukumbatiana kabisa.

“kutembea namna hivi tukiwa tumeshikana mkono ndio inakamilisha maana ya huu mtaa, hata hivyo sisi ni wanandoa ambao tuna safari ndefu”

“Nani kakuambia nina safari ndefu ya kuwa mke wako”Aliongea Edna na kumfanya Roma atabasamu.

“Wife Stern na Alice wanatusubiria”Aliongea Roma kupotezea mada huku wakitembea wakiwa wameshikana mikono.

“Inabidi kuwachana na mawazo ya kufanana na Seventeen”Aliwaza Edna na kutabasamu kisiri siri pasipo ya Roma kumuona, alionekana kufurahia kufanana na watu wengi waliokuwa katika eneo hilo.
 
SEHEMU YA 191

Edna alihusudu mgahawa ambao Alice na Stern walaikuwa wameuchagua , ulikuwa umetengenezwa kwa mtindo wa aina yake , wapo watu mbali mbali waliokuwa ndani ya hilo eneo , wengine hawakuwepo hapo kwa ajili ya kula bali kupiga tu picha , huku jamii nyingi ya kiafrika ndio waliokuwa wakiongoza kwa kuwa wengi wakipiga picha kwa ajili ya kuoshea watu mtandaoni.

Edna alijitoa kijanja kwenye mikono ya Roma wakati wakiwa wanaingia ndani ya hili eneo , lakini kabla hawajaingia kabisa , walisimamishwa na mtoto wa kizungu aliekuwa amesimama mlangoni akiwa ameshikilia maua.

“Anko nunua maua”Aliongea yule mtoto kwa kifaransa, Roma aliangalia maua yaliokuwa yameshikiliwa na mtoto huyo na kuona ni maua ya kawaida sana yanayopatikana pembezoni mwa barabara , ambayo mtoto huyu alikuwa ameyachuma na kuyafunga na Kamba, alikuwa ni mtoto makadirio ya umri wa miaka kama tisa hivi.

“Unauza shilingi ngapi?”Aliongea Edna huku akimsogelea yule mtoto baada ya Roma kutaka kupita na Roma baada ya kuona Edna yupo tayari kumuungisha mtoto na maua yake alikumbuka kituo cha kulelea yatima , ambacho Edna alikuwa akitembelea mara kwa mara.

“Dada,unaonekana kuwa mrembo sana”Aliongea yule mtoto wa kiume baada ya kusogelewa na Edna na kumfanya Edna atabasamu baada ya kusifiwa na mtoto.

“Hata wewe unavutia pia , Unaitwa nani?”

“Naitwa Harry , Sister wewe ni mgeni?”

“Ndio mimi ni mgeni natokea Tanzania”Alijibu Edna.

“Tanzania ni wapi Sister?”

“Ni mbali na hapa, inakupasa kupanda ndege ili kufika”

“Ndege!, Sister sijawahi kupanda ndege, marafiki zangu wananihadithia tu raha ya kupanda ndege natamani siku na mimi niweze kupata uzoefu wa kupanda ndege , lakini baba yuko bize sana na kazi, lakini kaniahidi kabla ya mwezi kuisha tutaenda Disnyland , nitaweza kuona magari yanayoruka kama ndege , Sister wewe ushayaona?”Aliongea yule mtoto na kingereza chake cha kuunga uunga na kumfanya Edna asielewe vizuri na kumgeukia Roma na Roma alimsaidia kutafsiri.

“Sijawahi kufika Disnyeland na kuona magari yanayotembea angani , naamini baba yako akikupeleka utafurahia”aliongea Edna.

“Ndio sister nitaenda na mama pia”Harry alionekana kufurahishwa na maongezi , ila kwa upande wa Roma alionekana kukosa uvumilivu.

“Dogo uza maua acha kupiga stori na mteja”Aliongea Roma.

“Una nini wewe , ,mbona unaingilia maongezi yetu , unaweza kutangulia”Aliongea Edna kwa kumshushua Roma.

“Harry usimjali “Aliongea huku akimpotezea Roma.

“Sister unataka mua yapi hapa”

“Unauzaje?”

“Euro moja tu kwa kila moja”

“Okey , nitanunua , ila kama utaniambia kwanini unauza maua sehemu kama hii nitakupa Euro tano”

“Nataka kumnunulia baba Soksi , jana nimeona moja ya Soksi yake ina tobo mguuni ,nataka iwe kama Surprise hivyo sikutaka kumuomba mama pesa”Aliongea Harry na kumfanya Edna atabasamu kwa mtoto kuwa na mapenzi makubwa kwa baba yake ,Edna alitoa noti na kisha akampatia Harry.

“Asante sana Sister , sasa hapa nishapata pesa ya kutosha”

“Soksi haziuzwi kwa Euro tano”aliongea Edna huku akitoa hela nyingine na kumpatia Harry.

“Harry ongezea na hii ndio itatosha kumnunulia baba yako Soksi”Aliongea Edna lakini Harry aliikataa.

“Mama kaniambia nisipokee pesa kwa mtu nisie mjua pasipo kuifanyia kazi”Aliongea Harry na kumfanya Edna atamani kucheka , hakujua mtoto alikuwa na utiifu kwa kile alichokuwa akiambiwa na mama yake.

“Okey Harry basi tufanye hivi , unaonaje ukinipa busu shavuini na mimi nikulipe”Aliongea Enda na kumfanya Roma aliekuwa pembeni ashangae.

“Mke wangu sikubaliani na jambo hilo , kwanini uruhusu mtu akukiss halafu tena umlipe kirahsi hivyo wakati mimi natafuta hio nafasi hata siipati”

“Kwahio unataka kushindana na mtoto,Wewe ni mtu mzima ila Harry ni mtoto ila anakuzidi kwa tabia nzuri, Ungekuwan na tabia nzuri kama Harry ningekuruhusu”Aliongea Edna na kisha na kumuinamia Harry na kupewa busu na kisha akampatia Hela na Harry alifurahi na kupokea kwa shangwe zote na kisha akaacha kazi yake ya kuuza maua na kuondoka.

“Kama unapenda sana Watoto kwanini tusitafute mmoja?”Aliongea Roma , lakini Edna ni kama hajamsikia , kwani alimpita na kuingia ndani ya mgahawa hu wa kisasa na kuwafuata Alice.

Roma baada ya kuongea maneno hayo , alijjikuta akipata mawazo ambayo hata yeye hakujua yametokea wapi , alifikiria kafanya mapenzi na Nasra, Dorisi Pamoja na Rose pasipo ya kutumia kinga yoyote lakini hakuna hata mmoja ambaye amepata ujauzito wake.

Au ni athari za kumiliki Godstone,Ila Hapana ngoja nitaongea na Clark kujua tatizo nini”Aliwaza Roma, ukweli alikuwa akitamani sana kupata na mtoto hususani kwa kupitia Rose , kwani aliamini ingemfanya kuwa na furaha, lakini ajabu kwa muda wote hakukua na dalili za Rose au wanawake wengine kushika mimba.

“Hey Miss Edna We are here , They’re known for their butter garlic giant lobster…we’ve ordered one, should we get one more?”Aliongea Stern baada ya Edna kuwafikia huku wakimwambia kuwa hapo ndani kunapatikana Kamba kochi wakubwa waliotengenezwa kwa kukaangwa na kuchanganywa na kitunguu swaumu.

“Miss Edna unataka kuagiza nini , kuna pia nyama wazuri wanaotoka Kobe Japan”Aliongea Alice huku Edna akiketi.

“Mimi sijui aina ya vyakula vinavyopatikana , naomba mnisaidie kuagiza”Aliongea Edna wakati huo huo Roma na yeye alikuja na kukaa pembeni yake na kisha akaangalia chakula walichoagiza Alice na Stern na kujikuta akitoa macho.

“Mke wangu unajua gharama ya chakula walichoagiza?”

“Mr Roma acha kutuchawia ,Miss Edna katuahidi mwenyewe kutununulia tunachopenda”Aliongea Stern na kumfanya Rma achukue kisu na kutaka kumrushia na Stern na yeye alinyanyuka na kuweka pozi la ki Bruce lee.

“Tulieni bwana”Aliongea Edna , kwani wahudumu walikuwa wakisubiria oda yao na yeye aliwaona wanacheza na Roma alirudisha kisu kwenye meza.

“Hawa Kamba waliogiza wanatolewa Canada na ni gharama sana hapa Ufaransa kwa chakula alichoagiza Stern kinagharimu Zaidi ya milioni nne ,Nyama aliogiza Alice ni Zaidi ya Milioni tatu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangaa , hakujua chakula hiko kilikuwa na bei kiasi hiko.

“Mr Roma unaonekana kujua bei ya hivi vyakula , nadhani umeshawahi kuvitumia, unaonaje ukimuacha na Mke wako akajaribu”Aliongea Alice na kumfanya Edna aone aibu.

“Alice… mmejua kwa muda gani kama sisi ni wanandoa?”Aliuliza Edna , alikuwa ashasau Roma kumuita Mke wake mbele ya Alice.

“Miss tulijua tokea kule msituni m kwa mtu makini lazima ajue uhusiano wenue sio wa kawaida, mnaonekana kuwa familia tayari”Aliongea Stern.

“Edna mnaendana sana”Aliongezea Alice

“Hahaha… hakika mke wangu pesa yako haijaendi bure”Aliongea Roma kwa kucheka na kumfanya Edna amfinye kwenye paja , na ukucha ulimwingia kisawa sawa Roma.

Edna aliona kama Stern na Alice walikuwa na uwezo wa kugundua kwa kuwaangalia tu , vipi kuhusu kwenye kampuni yake , aliamini lazima watu watakuwa washagundua ila wameamua kukaa kimya.

“Wife haina haja ya kuwa na aibu siku moja watu watafahamu tu , hata kama ujitahidi kuficha”Aliongea Roma

“Miss Edna Do you know, In this world, there are two things that people always want to cover up although it is impossible to do so.”

“Miss Edna, unajua kwenye huu ulimwengu kuna vitu viwili watu wanajaribu kuficha , ijapokuwa haiwzekani kufanya hivyo?”

“Vitug ani?”Aliuliza Edna akimwangalia Alice.

“The first is poverty. No matter how hard poor people try, they can never change their depressing reality. and the second thing… well, it’s when one person loves another….with their heart.”

“Kitu cha kwanza ni Umasikini ,Kwa vyovyote vile mtu masikini atakavyojitahidi kuuficha , hawawezi katu kuficha uhalisia wao wa kunyongea na kitu cha pili .. ni pale mtu anapompenda mwingine kwa moyo wake wote”

“Hehe ..Miss Edna unaona aibu … naamini nimepatia”Aliongea Alice huku akimtania Edna ambaye ni kweli maneno aliongea yalimwingia vizuri.

Roma aliekuwa pembeni hakutaka kumtania Edna ila alimwangalia tu mabadiliko yake na kutabasamu , na Edna alijikuta akigeuza macho yake na kumwangalia Roma , lakini aliishia kuyarudisha chini baada ya Roma kutabasamu huku akitingisha mabega.

Baada ya nusu saa waliletwa chakula chao aina ya Kamba Kochi wakubwa na Nyama , Edna , Alice na Stern walikula kidogo tu , ila kwa upande wa Roma alimaliza chakula chake chote.

“Huu ni uharibifu wa chakula”Aliongea Roma huku akiangalia vyakula vilivyokuwa mezani ambavyo wenzake wameacha.

“Mbona pesa zinakuuma sana wewe”

“Bebi unatakiwa kukumbuka mumeo nilikuwa mbeba mizigo kabla hatujaoana,siwezi kushindana na wafanyabishara kama nyie”Aliongea Roma bila aibu.

“Jaribu kuwa na aibu hata za maigizo basi, kwanini unapenda kujishusha wakati hapa wewe ndio mwenye pesa nyingi”Lakini Roma kabla hajajibu Muhudumu aliekuwa na bili yao alifika na mhudumu sijui alimwonaje Roma , ila bili ndio alimpatia , Roma baada ya kuichukua na kuona kiasi cha pesa kilichotakwa kulipwa alimsogezea Edna.

“Wife utalipia”Aliongea Roma lakini Edna hakujali , alichokifanya ni kufungua mkoba wake na kuchukua burungutu la pesa na kutoa kiasi cha pesa , huku akiongeza pesa kidogo kama ‘Tip’ na kumpatia muhudumu.

Mhudumu na yeye alishindwa kujizuia baada ya kuona burungutu kubwa la midola kwenye mkoba wa Edna, aliishia kuondoka huku akiwa yupo kwenye mshangao , ni kama tu ambaye hakuwai kuona pesa nyingi.

Baada kama ya nusu saa kupita , wakati wanatoka ndani ya mgahawa , walisogelewa na mwanaume mmoja hivi mzungu , alievalia Tisheti ya Levi, aliekuwa na ndevu nyingi kwa muonekano wake tu alionekana mtumiaji wa madawa ya kulevya.

“This beautiful lady over here, do you have time to talk?”

“Wewe mwanamke mrembo tunaweza kuongea kama una muda”

“Who are you?”Aliuliza Edna maana ndio aliekuwa ameangaliwa na kuongeleshwa.

“Miss, please take a look at this.”

“Miss , hebu jaribu kuangalia”Aliongea yule mwanaume na kumpatia Edna furushi la maua na hapo hapo Edna alikumbuka aliekuwa ameshikiria hayo maua ni Harry mtoto aliemsaidia kiasi cha pesa.

“Unataka kusema kuna jambo umemfanyia Harry?”

“Hehe .. Yule mtoto mpaka sasa yupo kwenye mikono ya boss wangu, na nimeagizwa hapa kuwaambia kama mnataka mtoto aachiwe akiwa salama basi unapaswa kuongozana na rafiki zako tukaongee na kama tutafikia kwenye makubaliano , Mtoto ataachiwa”Aliongea yule mzungu.
 
SEHEMU YA 192

Sio Edna peke yake ambaye alikuwa kwenye mshangao , ila hata kwa Stern na Alice pia walishangazwa na jambo hilo , waliona kabisa huo ni uhalifu unaokusudiwa kufanywa kwa ajili yao kupitia mtoto Harry.

“Nyie watu kweli mnaonekana kuijua kazi yenu vyema , kwa kuweza kunusa harufu ya pesa kutoka kwetu, lakini naamini mmekosea kabisa kwani hatuna uhusiano wowote na huyo mtoto,sidhani kama tunaweza kutii matakwa yako”Aliongea Roma akiwa kwenye muonekano wa kawaida.

“Hehe ..Wewe ndio unaongea , lakini siamini kwa huyu mrembo anaweza akamuacha mtoto kupata shida , tulimuona namna alivyoonekana kumjali mtoto wakati ananunua maua kutoka kwake”Aliongea huku akiweka tabasamu la kifedhuli.

“Mr Roma nafikiri wanawahitaji nyie wawili , sisi hili halituhusu hivyo tutaondoka , naamini utaweza kumlinda mkeo”Aliongea Stern huku wakitaka kuondoka walijikuta wakizuia na wanaume wawili waliongezeka wenye rangi nyeusi.

“Hili swala lazima libakie siri , tukiwaachia muondoke , linaweza kutuletea shida”Aliongea mmoja ya wale wanaume wa kiafrika na kumfanya Alice na Stern kuona hamna namna ya kukimbia.

Kwa upande wa Roma yeye hakuwa na wasiwasi , alikuwa akimsikiliza Edna yeye ndio amafanye maamuzi.

Edna alimwangalia mwanaume wa kizungu aliekuwa mbele yake kwa namna ya kumkata jicho.

“Ongoza njia tuelekee kwa bosi wako , na ole wako kuwe na madhara yoyote kwa Harry”Aliongea Edna, na Roma hakushangaa , alitegemea maamuzi ya aina hio kutoka kwa mke wake , lakini hata hivyo kutoka na kuijua Paris vizuri , utekaji wa aina hio haikuwa kawaida kabisa na aliamini hapo anaetafuwa ni yeye.

Mzungu aliongoza njia huku wale waafrika wawili wakibakia nyuma na kuwaweka Edna katikati,Walikuja kuingia upande wa maduka yanayouza vito na kukunja kulia , sehemu ambayo haikuwa na watu wengi Zaidi ya kuwa na nyuma pekee na baada ya kutembea kwa mita kama miatano hivi walikuja kutokezea , sehemu iliokuwa wazi kabisa , sehemu iliozungukwa na nyumba na kufanya eneo lisiwe na jua kwa kuzibwa na majengo na hapo hapo wakasimama.

“Harry yuko wapi?”aliuliza Edna baada ya kuona wamesimama sehemu ambayo ina uwazi na hakukuwa na dalili zozote za kuonekana kwa Harry.

“Cool Down madam , our Boss is here”Aliongea yule mwafrika huku akiangalia angani, na kuwafanya wengine waangalie angani vilevile,Na muda ule ule kilionekana kitu mfano wa Furushi likitoka juu likija upande waliosimama na kumfanya Edna arudi nyuma kumsogelea Roma, lakini wakati huo huo Edna alijikuta ni kama akili yake ipo sehemu nyinine kabisa isiokuwa ya kawaida, alihisi mwili wake ni kama vile ulikuwa ukielea angani , ni hisia ambazo hakuwahi kuzipata kwenye Maisha yake.

Lakini ajabu baada ya furushi kufika chini lilibadilika na kuwa mtu , tena mwanamke alievalia mavazi ya rangi nyeusi tupu , ikiwemo Koti la Leather

Edna alipatwa na mshangao wa ajabu kwani hakuwahi kukutana na tukio la ajabu kama hilo na sio kwake tu hata kwa Alice na Stern wote walikuwa kwenye mshangao tofauti na Roma ambaye alikuwa akionekana kuwa kawaida.

Harry alionekana kuwa kwenye mikono ya yule mwanamke ambaye alionekana kuwa mtu mzima , kutokana na Ngozi yake kuwa na mikunjo, Edna aliekuwa mbele ya Roma macho yake yote yalikuwa kwa Mtoto Harry ambaye alionekana kuwa hajitambui.

“Umemfanya nini Harry”Aliongea Edna kwa wasiwasi.

“Usiwe na wasiwasi , bado yupo hai huyu,nisingeweza kummaliza kumla ndani ya muda mfupi”Aliongea huku akilamba lamba midomo kama shetani , akimwangalia Harry aliekuwa kwenye mikono yake na macho yake yaliokuwa na wekundu wa kutisha.

“Kumla..!!”Aliongea Edna na kuogopa , hakuelewa alikuwa anamaanisha nini.

“Edna usiogope nipo nyuma yako,Anakutania tu”Aliongea Roma akimwinamia Edna sikioni.

“Ouch.. nyie ni majini?”Aliuliza Stern kwa mshangao akiwa amekumbatiaa na dada yake , hata wao waliweza kuhisi miili yao kukosa nguvu na waliweza kuhisi kama vile wapo anga za mbali , kutokana na kuhisi kama hawajakanyaga ardhini.

“Mpo kwenye ‘Dimension’ inayowatenganisha na ulimwengu wa kawaida hakuna mtu atakaeweza kuwaona hapa wala kuwasikia , hivyo msilete shida”

“Nyie watu ni wakina nani , kama mnataka pesa , nipo tayari kuwapa na mumuachie Harry”Aliongea Edna. Na kumfanya yule mwanamke amwangalie kwanzia juu mpaka chini.

“Gais hakika mmejua kuchagua,nimependa huo mwili, mmefanya kazi kubwa”Aliongea yule mwanamke akimwashiria yule mwanaume wa kizungu.

“Hahaha… Madam Viscount mimi nitatumia mwili wa huyo mwanaume mwenye nywele nyeupe, huu mwili ninaotumia sasa hivi, unazeeeka kwa spidi kubwa”Aliongea Gais.

“Gais ombi lako limekubwaliwa , utachukua utumie mwili wake , ile wa huyo mwanamke nitautunza kwa ajili ya kupelekea wazee wetu”Aliongea Madam Viscount.

Edna ukweli hakuelewa hata wanachomaanisha kabisa , aliona ni kama watu ambao wapo kwenye maigizo, ila kwa upande wa Roma alikuwa akifuatilia maneno yao kwa ukaribu sana.

“Naona mnagombania miili ya wazungu tu Pamoja na wa mke wangu , mbona mimi mmeniacha au hamna mpango wa kutumia mwili wangu?”Aliongea na kumfanya yule mwanamke Pamoja na Gais wamwangalie Roma.

“Binadamu , unajua unachoongea , kwa muonekano wako unafaa kuwa chakula pekee kwa wasaidizi wangu”Baada ya kumaliza kuongea palepale alinyoosha mkono wake mbele yao na kukunjua kiganja cha mkono wake na moshi flani hivi wa rangi ya Pink ulitoka kwenye mikono yake na kusambaa eneo lote na palepale Edna alilegea na kumfanya Roma amzuie na kumuweka chini , alionekana kupoteza fahamu , lakini pia hata kwa Alice na Stern walidondoka chini kama mafurushi na kupoteza fahamu.

Kitendo cha Roma kutoathirika na ule moshi kiliwafanya wale watu wote wanne kushangaa huku Gais na Madam Viscount kushangaa Zaidi.

“Wewe ni nani… Hapana haiwezekani”Walionekana kupatwa na wasiwasi baada ya kuona Roma hajaathirika.

“Ijapokuwa sijui ni kipi mnataka kufanya kwa uhakika , ila naamini mmefanya makosa makubwa sana katika kuchagua watu wa kuwatumia awamu hii”

“Unaongea Ujinga ,Gaisi muueni”Aliongea Madam Viscount kwa hasira na pale pale wale watu wote watatu walianza kubadilika muonekano wao kwa asilimia mia , Meno yao yalichomoka huku Ngozi zao zikitengeneza Ngozi ya mabakamabaka kama vile Ngozi ya nyoka huku kucha zikianza kurefuka na macho yao kubadilika na kuonekana kama vile kidonda kilichovimba na kutoa usaha.

“Sijawahi kupambana na jamii ya Majini kwa muda mrefu”Aliwaza Roma kwenye akili yake huku sasa vile viumbe vya ajabu vikimjia kwa kasi huku wakitanguliza mikono yao yenye kucha ndefu , huku majini ambayo yalikuwa yamevalia Ngozi za watu Weusi walimfata Roma kwa kasi usawa wa shingo huku yakipanua midomo yao ambayo ilikuwa ikitema ute ute mzito na mate mengi hewani kiasi cha kuonekana.

Sasa kabla hawaijaifikia shingo ya Roma , palepale walijikuta wakiganda hewani bila kubadilka kwa staili yao , ni kama vile muvi iliosimamishwa kwa muda ndio walivyonekana

“Pfffs”

Wale wanaume wawili wote walitema damu kwa wakati mmoja na hapo hapo kama vile jani linalopeperushwa na upepo walitoweka na Kwenda kudondokea mbali.

“Hamjazuiwa kufanya mawindo yenu , lakini siku zote ukikosea wa kumuwinda utajikuta wewe ndio unawindwa”Aliongea Roma kwa sauti yenye kitetemeshi na kumfanya Gais Pamoja na Madam Viscount kushangaa.

“Hahaha…Hahaha…Acha dharau, Ijapokuwa sikufahamu ila huwezi kuzuiwa mpango wangu kutofanikiwa kwa leo”Aliongea kwa sauti inayoumiza masikio na pale pale macho yake yalibadilika na kuwa kama kitenesi chekundu ambacho muda wowote kinaweza kudondoka chini , yaani halikuwa jicho lakini ni kama vile uvimbe flani hivi , huku mwili wa yule mwanamke ukianza kutanuka na kuanza kutoa harufu kali kama ya kitu kilichooza kiasi kwamba hadi Roma alianza kupata shida kwenye kuvuta hewa.

“Blood Race!!”Alitamka Roma baada ya kuona amefanya makosa ya kutambua maadui zake , hawakuwa majini kama alivyotegemea bali ni viumbe jamii ya Vampire`s
 
0687151346 WATSAPP NICHEKI , ITAENDELEA JUMAANE
Mfalme Singano. Hongera simulizi matata Sana hii.

Ikifika mahala nasomo sehemu za Edina na mfalme Pluto tu.

Kwa Sasa kule Whatsapp. Sehemu tulipofikia nafurahia Sana, kule jeshini na maamuzi ya Edina yanani sumbua Kwa sabab kwanini mfalme mzima hapewi kitumbua??


Na je hivi the dong anaweza kumuuwa mfalme Pluto au Hawa hawawez Kupigana nahisi mfalme hamuwez the Don. Na ni kama vile wote ni katika wale watu 12.

Hii Hadith is amazing.

Tulio soma stori za kale za kijasusi hii imetulia pia.

Ninakusihi Singano. Kama sio hii lkn toa kitabu Cha Hadith. Na hakikisha kinakuwa kinene kikubwa. Chenye habari ndefuuuu.


Hivi ndio vile vitabu unamkuta MTU anakisoma hapa Hadi Marekani bila kuchoka
 
Mfalme Singano. Hongera simulizi matata Sana hii.

Ikifika mahala nasomo sehemu za Edina na mfalme Pluto tu.

Kwa Sasa kule Whatsapp. Sehemu tulipofikia nafurahia Sana, kule jeshini na maamuzi ya Edina yanani sumbua Kwa sabab kwanini mfalme mzima hapewi kitumbua??


Na je hivi the dong anaweza kumuuwa mfalme Pluto au Hawa hawawez Kupigana nahisi mfalme hamuwez the Don. Na ni kama vile wote ni katika wale watu 12.

Hii Hadith is amazing.

Tulio soma stori za kale za kijasusi hii imetulia pia.

Ninakusihi Singano. Kama sio hii lkn toa kitabu Cha Hadith. Na hakikisha kinakuwa kinene kikubwa. Chenye habari ndefuuuu.


Hivi ndio vile vitabu unamkuta MTU anakisoma hapa Hadi Marekani bila kuchoka
Shukrani mkuu
 
Wakuu challenge: pachikeni uhusika kwa wahusika kutoka bongomovie
Kwangu mimi EDNA nikimleta kwa bongomovie nampa Welusengo
 

Attachments

  • FB_IMG_16696251805756259.jpg
    FB_IMG_16696251805756259.jpg
    44 KB · Views: 126
Huyo mwanamke mnene mnene , bado hamfikii Edna , kwanza huyo kajipodoa , Edna hajipaki ma makeup , Natural beuty
Kabisa,kwaninavyoimagine Edna yupo sample zakina Paula Ila kiuzur Paula bado Sana nataman hii story ingekua yakweli ili mtunzi s singanojr atuwekee picha ya Edna na mwamba Roma ao wengine sina issue nao labda mrembo Najma
 
Kabisa,kwaninavyoimagine Edna yupo sample zakina Paula Ila kiuzur Paula bado Sana nataman hii story ingekua yakweli ili mtunzi s singanojr atuwekee picha ya Edna na mwamba Roma ao wengine sina issue nao labda mrembo Najma
Edna baba yake ni Mrwanda mama yake ni kabila la Wairaq kutoka Babati Manyara , She is very introverted and workhollic .
She is not romantic , likija swala la mahusiano ni kama mtoto wa darasa la saba , she is dumb ...
Edna ana high ability ya kukontrol hisia zake , she is intelligent woman .... Mkishamuona The Don nitaendelea
 
Edna baba yake ni Mrwanda mama yake ni kabila la Wairaq kutoka Babati Manyara , She is very introverted and workhollic .
She is not romantic , likija swala la mahusiano ni kama mtoto wa darasa la saba , she is dumb ...
Edna ana high ability ya kukontrol hisia zake , she is intelligent woman .... Mkishamuona The Don nitaendelea
Edna huyu
73d15f07784b4b05d38e0f31780ca5af.jpg
 
Edna baba yake ni Mrwanda mama yake ni kabila la Wairaq kutoka Babati Manyara , She is very introverted and workhollic .
She is not romantic , likija swala la mahusiano ni kama mtoto wa darasa la saba , she is dumb ...
Edna ana high ability ya kukontrol hisia zake , she is intelligent woman .... Mkishamuona The Don nitaendelea
Edna atakuwa anafanana na madam Ritha akiwa kijana, ama klyne, na kama ni mweusi basi anafanana na yule binti wa kagame ama mke wa Ay
 
Back
Top Bottom