Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Tatizo WhatsApp haurespond kwa wakati mkuu, unatuangusha.
 
Jumanne ndo hii mjomba nimeshachoka kusubiri
 
SEHEMU YA 193

Kilichomfanya Roma kutogundua mapema juu ya maadui wake kuwa jamii ya kundi la wanywa damu ni kutokana na aina ya hisia walizokuwa wakisambaza.

Moja ya sifa kubwa ya kutofautisha viumbe wa ajabu ndani ya dunia hii ni aina ya msisimko(Aura) wanayokuletea pale wanapokukaribia , kwa mfano hisia ambazo hupata pale mtu anapokutana na jini ni tofauti na hisia ambazo mtu hupata pale anapokutana na mchawi usiku na hapa wengi watakwambia nywele kusisimka baada ya kuhisi nguvu isiokuwa ya kawaida, hio ni kweli kabisa , kama unayoelimu ya kutofautisha aina ya hisia unazopata ukikutana na viumbe wa aina hii basi hakika utaweza kuwatofautisha kwa asilimia kubwa.

Mwanamke ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Madam Viscount ndio aliemfanya Roma kugundua kuwa maadui zake hawakuwa kwenye kundi la Majini bali ni kundi la wanywa damu yaani Vampires, lakini hata hivyo Roma aliweza kuhisi aina ya msisimko(Aura) uliofifia sana na hii ilimuwezesha kuwatofautisha maadui waliokuwa mbele yake kutofautiana pakubwa na jamii ya kawaida ya wanywa damu, kundi hili lilikuwa ni tofauti na wale aliokutana nao Tanzania ambao wanaunda kundi la Dark Parliament, hili ni kundi ambalo hawana umbo maalumu la ubinadamu , yaani kwamba ili waweze kuonekana kuwa na maumbo ya binadamu ni lazima watumie miili ya viumbe wengine wakiwemo binadamu.

Madam Viscount baada ya kuona namna wenzake walivyodhibitiwa na nguvu isio ya kawaida kutoka kwa Roma, alimwangalia Gais na kumpa ishara ya kumpokea mtoto Harry aliekuwa kwenye mikono yake na muda huo huo alimrusha hewani na Gais alimdaka na kumshikilia huku akirudi nyuma akiwapa nafasi Roma na Madam Viscount kupambana.

Madam Viscount baada ya kumrusha kuelekea kwa Gais palepale alikusanya mikono yake kwa Pamoja na kuibuka na Donge la Damu kubwa kama mpira kwenye mikono yake na kumfanya Roma kushangaa, lakini muda huo huo wale Weusi wawili ambao aliamini kuwaua kutoka na aina ya mapigo aliowapatia , waliibuka tena huku wakiotoa mkandamizo wa hewa ambao ulifanya Roma ahisi kifo , ni aina ya msisimko wa kutisha sana ambao walikuwa wakitoa.

“Umetibua wakati wetu mzuri wa kupata chai ya mchana ,Wewe funza ulierogwa”Aliongea Madam Viscount huku jicho lake kama kitenesi likizidi kuogopesha na alijiambia kama Edna angeshuhudia muonekano wake, asingeweza kuishi tena kwa amani.

Kitendo cha kufufuka kwa wale wawili Weusi na pia kitendo cha Madam Viscount kutengeneza Donge la Damu kilimfanya Roma kuchanganyikiwa na hii ni kutoka na kwamba kwa alivyokuwa akijua kundi la wanywa damu wengi hawakuwa na uwezo wa kutengeneza nguvu ya kichawi kwa kutumia damu(Blood Spell) , lakini vile vile hawakuwa na uwezo wa kufufuka kama utawapatia pigo la moja kwa moja kwenye moyo.

“Leo nina kazi kubwa ya kupambana nao”Aliwaza Roma lakini palepale Madam Viscount alipotea sehemu aliokuwa amesimama na ile anakuja kuibuka alikuwa juu ya kichwa cha Roma huku akilenga lile Donge la Damu kwenye utosi na ilionekana alidhamiria kummaliza kabisa Roma palepale na Roma hakutaka kuwa mzembe kwani wakati lile Donge linamkaribia kwa spidi kubwa kama jiwe, alichuchumaa na kisha akainua mkono juu na likatua kwenye kiganja cha mkono na kupasuka pasuka kama vile ni Glass iliotua sakafuni , kwani donge lile liliacha vipande vipande vikisambaaa , kitendo kile alichokifanya Roma kilimuogopesha Madam Viscount na kumpelekea kurudi eneo aliliokuwa amesimama mwanzo , alishangaa Binadamu aliekuwa mbele yake kawezaje kupasua siraha yake ya kichawi(Blood Spell).

“All of us now”Aliongea Madam Viscount huku akiwapa amri wale Weusi waungane Pamoja kushambulia na Wote kwa pamoja waliachia madude flani hivi kama mapovu au Maputo yaliokuwa kwenye mfumo wa kioo kueleka aliposimama Roma , lakini kabla hayajamfikia Roma, ni kama yalikuwa yakikutana na Joto kali kwani yaliyeyuka na kupotelea hewani na kumfanya Madam Viscount kuja kwa kasi hukua akitanguliza kucha na Roma ni kama alikuwa akimsubiri amfikie , kwani Madam Viscount aliweza kabisa kumshika kwa nguvu nyingi Roma kwenye Bega kwa kutumia kucha zake huku akidhamiria kumrarua , lakini ni kama amekutana na chuma kwani kucha hazikuzama hata nusu inchi na kufanya eneo lote litegeneze kama tetemeko kwani alikuwa ametumia nguvu nyingi sana kushuka kutoka juu, sasa tukio lile la kushindwa kumrarua Roma na kucha zake lilimuacha kwenye mshangao na kukosa hatua nyingine ya kushambulia na hapo ni kama alitoa nafasi kwa Roma.

“Ngoja nione awamu hii kama mtaweza kufa”Aliongea Roma na kwa kutumia mikono yote miwili aliachia ngumi nzito akilenga wale Weusi wawili maeneo ya kifuani , na kwakua walikuwa wakija kwake kwa spidi walishindwa kumkwepa na ngumi zile zilitua kisawa sawa na kurushwa umbali mrefu , lakini ikawa nje ya matokeo ya Roma , kwani licha ya wale Weusi kuwapiga na nguvu kubwa , lakini ni kama hawakupata madhara yoyote kwani walitema damu na kunyanyuka tena na kumsogelea.

“Wakoje hawa….”Roma aliongea kwa mshangao , lakini muda huo huo akisahau kuwa Viscount yupo karibu na bega lake na Vicount alitumia mwanya huo kupeleka mdomo wake wenye meno marefu usawa wa shingo ya Roma,lakini ni kama Roma alitegemea tukio hilo kwani pale pale macho yake yalibadilka na kuwa kama balbu ya wati hamsini iliowashwa , kwani macho yake yalikuwa ya njanoo kama jua , na palepale alizunguka kama Pia na kumpiga Vicount ngumi nzito ambayo ni kama vile ilikuwa imeambatana na umeme, kwani ilivyotua ilimfanya afyatuke umbali mrefu Kwenda juu huku akizunguka zunguka.

“Arghh…!”Alitoa ukulele wa maumivu baada ya kudondoka chini , lakini kama ilibyokuwa mategemeo ya Roma , alinyanyuka tena akiwa mpya akionekana kupona maumivu.

“Hahaha… Mshenzi wewe huwezi kuniua .. ninakumaliza”Aliongea kwa sauti kali inayoumiza masikio.

Sasa kwa namna hio Roma aliona hapa kazi ishakuwa kubwa , ukweli hakutaka kutumia uwezo wake wote kupambana na aina hio ya viumbe , aliona njia pekee iliobaki ni kutumia nguvu ya kuyeyusha , aliona ajaribu kuyeyusha miili yao na kuona kama wataweza kurudi tena kuwa hai.

“Ha,,Hahaha.. hahaha…Manny kwanini unakuwa na hatari mpaka kupambana na mtu ambaye sio saizi yako”Ilisikika sauri ya kike ambayo Roma aliweza kuitambua, sauti ambayo ilikuwa nje ya uzio wa kichawi (dimension) ambao Madam Viscount aliutengeneza na kumfanya Roma asimuone huyo mwanamke , lakini muda huo Roma aliweza kuona mtikisiko wa hewa kama vile mafuta ya Petroli yakipotelea hewani au gesi, na hapo ndipo alipoweza kumuona mwanamke wa kizungu alievalia koti refu la suti manyoya lililokuwa limemfikia mpaka miguuni huku akiwa na nywele zake nyeupe.

“Lilith..mpumbavu wewe , umekuja kufanya nini?”Aliongea Viscount huku akiuonyesha hasira kali kuelekea kwa Lilith ambaye wala hakujali macho yake Zaidi ya kumwangalia Roma.

“Long time no see, Your Majesty Pluto.”Aliongea Lilith huku akimsogelea Roma

“It’s not that long. Plus, now is no time for reminiscing.”

“Sio muda mrefu hivyo , ukijumlisha huu sio muda wa kukumbushiana”Aliongea Roma huku akimwangalia Lilith pasipo kubadili macho yake.

“Kwangu ni muda mrefu , nilikuwa nikikumbuka tokea tulivyoachana”Aliongea Lilith huku akimgeukia Madam Vicount ambaye alimwita Manny muda mfupi uliopita.

“Manny unabahati mara ya mwisho ulinikimbilia kabla ya kubadilisha mwili, awamu hii huwezi kunikimbia Viscount Manny”

“Acha kujigamba Lilith nina mateka kwenye mikono yangu”Aliongea Vicount huku akimwangalia Gais aliemshikiria Harry.

“Mfalme Pluto , unataka kumuokoa yule mtoto?”Aliuliza Lilith huku akimwangalia Gais ambaye alionekana kutetemeka kwa uwepo wa Lilith ndani ya hilo eneo.

“Kwakua umekuja , nadhani nikuachia upambane na mtu wako , mimi nitamuokoa mtoto kwanza”Aliongea Roma na pale pale alipotea alipokuwa amesimama , na ile anaibukia alikuwa mbele ya Gais na kabla Gais kumkwepa , Harry alikuwa tayari yupo kwenye mikono ya Roma.

“Asante kwa kumshikilia”Aliongea Roma na paleple aliachia bonge la ngumi ambayo iliambatana na kufuka mvuke mkali na palepale Fais aliyeyuka na kupotea na kumfanya Vicount kutoa macho , unajua wakati alivyokuwa akipambana na Roma hakudhani kama Roma alikuwa na uwezo wa kupotea na kuibuka(Teleporting ability).

Lilith baada ya kuona Roma ashamwangamiza Gais na yeye alitoa upanga wake kimazingara uliokuwa na mgumo wa muundo wa mwezi(Massacre blade) na kufanya eneo lote litoe harufu ya damu mbichi kama ya myama .

“Shambulieni”Aliongea Viscount na wale Weusi bila ya woga walijipeleka kwa Lilith , lakini kilichowakuta ni panga lile kuwafyeka kwa wakati mmoja na ni kama vile wamefyekwa na radi kwani ni moshi pekee ndio uliofuka na kufanya watu wale kuwa majivu palepale na kudondoka chini.

“Kumbe ilikuwa rahisi hivyo , kwa kutumia moto tu unawamaliza , basi ngoja nijaribu kutumia uwezo wangu wa kutengeneza moto kufanya majaribio”Aliongea Roma na pale pale mkono wake ulionekana kuwa na umbo Flani hivi kama mpira ila uliokuwa kama mfano wa moto uliokuwa ukizunguka na palepale alirusha kwa nguvu zote kuelekea upande ambao Viscount alikuwa amesimama na kabla hata hajaukwepa alijikuta akiyeyushwa mzima mzima na kupotea palepale na kumfanya Roma atabasamu.

“Hawa ni Wanywa damu kama wewe sio?”Aliuliza Roma.

“Mfalme Pluto usinifananishe na hao Wanyama , Viscounty Manny ni aina ya jamii kutoka katika kundi la muungano wa kishetani kutoka koo ya Tzimisce”Aliongea Lilith na kumfanya Roma kushangaa.

“Tzimisce clan!?”

“Ndio mfalme Pluto , Tokea enzi za kale jamii hii ya wanywa damu kutoka kundi la Tzimisce ndio ambao wameishi Maisha ya kutokuwa na Imani ya aina yoyote ile na ni wakatili mno na ndio pekee ambao wamefanya jamii ya Vampires kuogopwa sana na binadamu na kututengenezea sifa mbaya , sifa yao kubwa nzuri ni juu ya kiu yao ya kuendeleza Sayansi na teknolojia,masalani katika sayansi inayohusiana na uwezo wa kuwafanya kuishi milele(Eternity), Hivyo kwa maneno marahisi Imani yao imejikita katika Umilele”

“Umilele tena , nilijua wanambinu pekee za kurefusha Maisha yao , kwanini waamini katika umilele?”

“Umilele na kurefusha Maisha ni vitu viwili tofauti mfalme Pluto , kwa sasa hii jamii inaweza kurefusha Maisha yao , lakini sio kuweza kuishi milele na ndio maana wamejikita katika sayansi inayohusiana na kuishi milele pasipo kubadilika kutoka hali ya ujana”Roma alijikuta akishangaa , yalikuwa mambo mapya kwake , licha ya kwamba hata yeye mwili wake DNA zimechakachuliwa na kumfanya kuweza kuhimili sumu ya aina yoyote ile , lakini sio katika kuweza kurefusha Maisha yake.

“Usishangae sana , zipo tafiti mbalimbali ambazo wameweza kufanya kwa kulinganisha binadamu na wao wenyewe kibaiolojia na utofauti wao na binadamu ni kwamba wao hawategemei moyo kuishi kutokana na uwezo wao wa kuweza kukusanya seli za mwili kwa Pamoja na kurudi hai ndio maana ni ngumu sana kuwaua, lakini pia wanayon teknolojia walioipa jina la ‘shell reconstruction,hio ni jina ambayo wanafanya kwa kuharibi miili ya binadamu kabla ya kuweka seli zao kwenye hio miili na hapo watakuwa na uwezo wa kuhama kutoka kwenye mwili mmoja Kwenda kwa mwingine”Aliongea Lilith.

“Ndio maana yule mwanamke alisema anataka kutumia mwili wa mke wangu”Aliongea Roma kwa kushangaa.

“Ndio mfalme Pluto hii ndio maana imewaongezea nguvu kubwa sana kwa jamii zote za Illuminat(Devil Worshipers) na wamekuwa pasua kichwa sana kwa wanachama wote wa Dark Parliamnent na mimi ni moja ya watu waliopewa jukumu la kihakikisha ninawapunguza kwenye uso wa dunia ili wasije kuleta madhara makubwa Zaidi”

“Lilith umesema kwamba Manny na wenzake wanatoka kutoka Tzimisce ,je wewe na kundi lote la Camarilla asili yenu inatoka kwenye kundi lipi la wanywa damu?”

“Sisi asili yetu ni ukoo wa Venture,Baba yangu Prince Sargaras ndio mkuu wa ukoo wetu”Aliongea Lilith na Roma alionekana kutokuwa na swali lingine na Lilith alimuaga kwamba anaondoka.

“Lilith hebu subiri”

“Ndio mfalme ?”

“Nataka kujua hospitali isiokuwa na gharama kubwa ndani ya jii la Paris , najua wewe ni mzoefu hivyo unaweza kunisaidia”

“Kwanini mfalme , kuna mtu unataka kumpeleka?”

“Yeah!Nataka nikamuache huyu mtoto hospitalini , hivyo naona nikimuacha kwenye hospitali kubwa wazazi wake wanaweza wasimudu gharama na sitaki hela zinitoke”Aliongea Roma lakini Lilith ni kama hahamsikia kwani alimpuuza na kupotea.

NB: Camarilla , Savath na Dark Parliament hizi ni taasisi tu mfano wa Illuminati ,Freemason na jamii nyingine za kimakundi , hizi taasisi zote ni za siri ,nguvu pekee inayofanya taasisi hizi kutawala dunia ni kutokana na uwepo wa watu ambao sio wa kawaida ambao wapo kama viongozi(Noble) wanaotofautishwa na damu zao ‘Pure Blood’.

Sasa Vampire unachotakiwa kuelewa ni kwamba wenyewe wamegawanyika katika makundi mbalimbali kutokana na tabia zao , kuna jamii ya binadamu ya Vampire ambao kuishi kwao hawategemei damu kabisa na hata kama wakitumia damu ni kwa mwaka mara moja na unaambiwa hata tone moja tu linawatosha kabisa kuendesha Maisha yao.

Hakuna uthibitisho wowote wa Vampire kuwa majini kabisa licha ya kwamba majini na yenyewe kuna ambayo yanategemea damu ili kuishi.



Sasa kama utataka kutofautisha hizi jamii zote ni kutokana na Alama , nenda google andika Camarilla utaona alama yao , andika pia Savathh utaona alama yao , andika Freemason utaona alama yao ya kipekee kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…