SEHEMU YA 209
Mwanamke aliekuwa mbele ya Roma alikuwa ni Lilith , haikueleweka alifikaje hapo ndani ila nia yake ilionekana wazi kabisa mbele ya Roma , Lilith alionekana kuja hapo ndani kwa ajili ya kuomba mchezo na mfalme Pluto.
“Nikajua ushaondoka na baba yako kuelekea Uingereza?”Aliuliza Roma akijongea kivivu mpaka kwenye kitanda na kuketi.
“Nisingeweza kuondoka kabla hatujaonana?”Aliongea Lilith huku akijirembulisha.
“Lilith najua kwanini upo hapa , ila nikuambie tu sipo kwenye mudi nzuti kabisa na nitapenda uondoke”aliongea Roma.
“Mfalme Pluto huwezi kunifukuza na nimekuja mpaka hapa naomba japo kidogo ulichofanya na Malkia wa Wales”aliongea Lilith na kumfanya Roma amwangalie , hakua akifahamu kama Lilith alikuwa akijua kuwa ana mahusiano na Catherine.
“Lilith haina haja ya kujilinganisha na Catherine , Kuwa na mahusiano na Catherine haimaanishi kwamba kila mwanamke nitakubali kuwa nae”Aliongea Roma , lakini kwa upande wa Lilith alionekana kutokata tamaa , mpango wake ni kuhakikisha anashusha kiu yake usiku huo.
“Mfalme Pluto sijilinganishi na Catherine , ila naomba unipokee kama sehemu ya shukrani kwa kile ambacho umetutendea mimi na baba yangu”
“Kuhusu nilichokifanya kule kisiwani kisikusumbue kichwa kabisa , sijawaua Wavatican kwasababu yenu , ila nimefanya vile kutokana na Vatican walichonifanyia miaka kadhaa nyuma , hivyo hauna haja ya kunilipa na naomba uondoke”Aliongea Roma huku akiweka uso wa usiriasi.
“Mfalme Pluto hivi unajua tofauti ya wanawake Vampire na binadamu wa kawaida?”Aliongea Lilith huku akiacha paja wazi na Roma alionekana kutokumuelewa.
“Binadamu damu yao ni ya moto , hivyo pia kwa miili yao kuwa ya moto ndani na nje , lakini kwetu sisi Vampire damu yetu ni ya baridi kama barafu nje na ndani”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie Lilith.
Ukweli baada ya maneno hayo kutoka kwa Lilith Roma alijikuta akifikiria kwamba hajawahi kukutana na kitu cha baridi , hivyo shauku ya kujaribu kitu kipya ilimvaa palepale na kwa upande wa Lilith alijua maneno yake yamemgusa penyewe Mfalme Pluto , na alimsogelea na kisha akamkalia mapajani.
“Mfalme Pluto sidhani kama haifanyi kazi”Aliongea Lilith huku akimsogelea Roma kwenye uso na kama ilivyokuwa kwa wanaume wote wasivyopenda kauli ya kudharauliwa ndio kilichotokea kwani Lilith alichapwa bakora za kimkakati.
*******
Saa saba mchana siku iliofuat, ndio muda ambao Edna na Roma waliiacha ardhi ya Ufaransa kurejea Tanzania kwa kutumia ndege ya kampuni ya Fly Emirate.
Edna alishamaliza kile ambacho kilimpeleka Ufaransa ,licha ya kusaini mkataba mnono na kampuni ya mavazi na mitindo ya Luis Vuitton ,lakini pia aliweza kuchagua mtu mwingine wa kuongoza kampuni yake ya Athena na hakubadili tu viongozi wa juu , lakini pia aliweza kupangua mfumo wote wa kiuongozi wa kampuni yake na hii ni kuhakikisha anaepusha ufisadi ndani ya kampuni kutokana na kile kilichotokea kwa Goodman na kwa jinsi alivyoweza kubadili uongozi wa kampuni ilimshangaza Roma kwani ni kama Edna alikuwa na mpango huo tokea anatoka Tanzania , kwani swala la kubadili uongozi kama ni kufanyika lingechukua muda , lakini kwa pande wa Roma hakuuliza.
Taarifa za Goodman kufariki alizipata , lakini licha ya kupata taarifa hizo hakumuuliza Roma chochote , kwani alijua fika kifo cha Goodman ni lazima kimetelekezwa na Roma.
Ukweli tokea siku ya jana yake ya kujikuta kwenye meli ya kivita hakuongea neno lolote na Roma ,yaani alikuwa amemchunia moja kwa moja na hata safari yao ya kurudi Tanzania ilikuwa ni ya kimya kimya, licha ya Roma kiuingiza maneno ya utani kwa Edna lakini hakukua na majibu na Roma hakuona namna ya kumaliza hio vita baridi ilioanzishwa na mke wake na ilimuwia kuwa ngumu mno kutokana na kwamba hakuweza kujua Edna anafikiria nini kwa wakati huo.
Saa tatu kamili Edna na Roma walikamilisha taratibu zote baada ya kufika ndani ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere na walitoka nje ya jengo la kufikia wageni na kupokelewa na Innocent ambaye alikuwa ni dereva wa kampuni na moja kwa moja safari ya Kwenda Kigamboni ilianza.
Kwa upande wa Roma safari nzima alikuwa akiwaza mambo mawili mpaka anafika ndani ya jiji la Dar , jambo la kwanza alilokuwa akiwaza ni juu ya mwanamke aliekuwa amekutana nae ndani ya meli ya Loius XVI, mwanamke aliejitambulisha kwake kama Zoe Kovac , kilichomfanya Roma kumfikiria huyu mwanamke ni kutokana na kwamba aliguswa na sehemu ya Stori ya Zoe pale aliposema alikutana na mwanamke anaemfahamu ndani ya visiwa vya Maldives , jambo hilo lilimfikirisha kwani kwa wanawake wake wote ambao alikuwa nao hapo kabla hawakuwa wakimfahamu kwa jina la Hades na hata wale wanawake ambao alikuwa na uhusiano nao wa karibu ambao walikuwa wakimfahamu, ni ngumu sana Kwenda visiwa vya Maldives na kuamza kuzungumza Habari zake.
Swala la pili ambalo Roma alikuwa akilifikiria ni juu ya mtu ambaye amehusika na kumpokonya HollyGrail Pamoja na Teknolojia ya Thanatos, hisia mbalimbali ziliibuka katika kichwa cha Roma kila alipokumbuka nguvu aliokuwa nayo mtu huyo kiasi cha kwamba hata namna ambavyo alikuwa akitokea alishindwa kabisa kuilelewa.
“Nitatumia Godstone chambo cha kupambana nae tena?”Aliwaza Roma huku akijiambia atatumia Jiwe la kimungu kama chambo kwa ajlii ya kupambana nae tena , na wazo hili lilimjia baada ya kufika Kigamboni.
“Sister Edna..!!!”Ilikuwa ni sauti ilioambatana na kivuli kilichojitokeza mbele ya Edna ambaye ndio kwanza alikuwa akipiga hatua kuelekea ndani huku Roma akiwa nyuma yake.
“Yezi..!”Aliita Edna na kukumbatia na Yezi , hakufahamu ilikuwaje Yezi akawa yupo nyumbani kwake.
*****
Damasi mke wa Raisi Senga alishangazwa na maneno ya mume wake , hakuamini kama siku zote hizo baba mkwe wake alikuwa akifahamu Denisi na Blandina walikuwa hai na alikuwa kimya muda wote pasipo kumwambia mtoto wake..
Alimuonea sana huruma Mume wake , kwani aliamini ni maumivu makubwa sana kudanganywa kwa miaka mingi na mtu ambaye alikuwa akimpenda, kiufupi aliona ni watu wengi ambao walihusika kumdanganya mume wake , Afande kweka mkwe wake , Blandina na Mheshimiwa Kamau ni watu ambao mme wake alikuwa akiwaheshimu sana na kuwapenda sana , lakini watu hao walimuweka kizani kwa miaka yote hio , aliona ni jambao la ajabu sana ambalo wamelifanya na alimuonea huruma sana mume wake juu ya jambo hilo , na aliona ana haki kuwa katika hali aliokuwa nayo, lakini licha ya hivyo yeye alikuwa ndio mke halali wa Senga hivyo hakutaka kumuoana Senga akiumia Zaidi, aliona pasipo kumpa ushauri mzuri mume wake, lakini pia maneno ya Faraja kwa ajili ya kumtuliza , huenda akafanya jambo ambalo sio zuri na likampelekea kuwa katika matatizo.
Na hata pale ambapo Senga alipomueleza mke wake juu ya safari ya Kwenda Kenya siku inayofuata alipinga sana swala hilo.
“Senga sipo tayari kukuona ukienda Kenya?”Aliongea Damasi kwa msisititizo.
“Damasi lazima hili swala nilimalize ,siwezi kuendelea kukaa hapa bila kufanya lolote”
“Baba Ashley, mume wangu , najua ni kipindi kigumu unapitia sasa , lakini licha ya hivyo unatakiwa kutambua kuwa kuna Denisi na Ashley ambao wanakutegemea kama baba , lakini pia usisahau pia kuwa wewe ni raisi wangu wa taifa hili , mimi Pamoja na Raia wote tunakutegemea, maamuzi ya Kwenda Kenya siyaafiki kabisa”Aliongea Damasi kwa msisitizo.
“Damasi unataka nifanye nini kwenye hali kama hii , nikikaa kimya watazidi kuniona mpumbavu na dhaifu ,lazima hili swala nilimalize kwa namna yoyote ile”Aliongea Senga kwa hasira huku akipumua kwa kasi mno na kusababisha kifua chake kupanda na kushuka kwa kasi.
“Kama kweli unataka Kwenda Kenya , ni hatua gani unakwenda kuichukua , je utakwenda kuanza kupigana na Kamau kwa ajili ya kukusaliti au unakwenda kumgombeza Blandina kwa ajili ya kujificha kwa sura ya Maina , Nipe sababu ya kueleweka Senga kwa ajili ya wewe Kwenda Kenya?”Aliongea Damasi huku akianza kupandwa na hasira hata yeye, lakini maswali yake yalionekana kuwa ya maana sana mbele ya raisi Senga , ni kweli alikuwa akitaka Kwenda Kenya , ila mpaka wakati huo hakuwa nasababu maaliuamu ya Kwenda kenya na alishindwa hata kumjibu Damasi swali lake.
“Damasi sijui hata nini napanga kufanya mpaka sasa”
“Ni haki yako Senga kutokufahamu kipi unapaswa kufanya kwa wakati huu , ni kwasababu unapitia wakati mgumu na mimi kama mkeo nipo hapa kwa ajili ya kukusaidia kuvuka katika hali hii unayopitia , ukishatulia utakuwa na majibu sahihi”Aliongea Damasi na kumfanya Senga amwangalie mke wake kwa dakika kadhaa na kisha akamsogelea na kumkumbatia.
“Nakupenda sana mke wangu”Aliongea Mheshimiwa Senga kwa hisia kubwa.
“Nakupenda sana mume wangu”
Maongezi ya Damasi na mume wake Raisi Senga yaliishia kwa Senga kughairisha safari yake ya Kwenda Kenya.
*******
Raisi Kamau tokea siku ambayo Gumilla alirudi pasipo kukamilisha misheni aliompatia hakuwa na amani kabisa , moyo wake ulikuwa kwenye wasiwasi na maumivu mengi , licha ya kwamba ni maamuzi yake mwenyewe aliofanya miaka kadhaa nyuma ya kuhakikisha Blandina anakaa mbali na Senga na hata kuamua kumuoa kabisa , lakini bwana huyu leo hii baada ya rafiki yake wa muda mwingi Senga kuambiwa juu ya uwepo wa Blandina ulimfanya kukosa amani na kujutia kwa matendo yake.
Leo ni siku ya tano mke wake Blandina hakuwa tayari kuongea nae kabisa na alikuwa amemchunia na msimamo wake wa kutotaka kuendelea kubaki hapo ikulu ukiwa upo vilevile.
“Njiro hakikisha ulinzi unaongezeka kwa mke wangu sitaki mtu yoyote kuonana nae”
“Sawa mheshimiwa” Aliitikia Njiro mara baada ya kuitwa ofisini na mheshimiwa Kamau.
“Pia haruhusiwi kupata kifaa chochote cha mawasiliano ukitokea uzembe wa aina yoyote kama uliotokea Tanzania basi jua kazi huna tena”
“Sawa mheshimiwa nitazingatia”
“Okey unaweza Kwenda”Aliongea na Njiro alievalia suti na viatu vyake vya Skuna alitoka ndani ya ofisi hio ya mheshimiwa kwa ajili ya Kwenda kuendelea na majukumu ya kumlinda Maina ili asiweze kuonana na mtu yoyote.
Baada ya Maina kutoka , aliingia na Deo ndani ya ofisi ya mheshimiwa na alionekana na yeye aliitwa ndani ya ofisi hio.
“Nipe Ripoti”
“Hakuna hatua yoyote ambayo mheshimiwa Senga amechukua mpaka sasa”Aliongea Deo.
“Okey , hakikisha unanipa taarifa ya kile kinachoendelea , wasiliana na wanausalama wetu Tanzania kuongeza umakini”
“Sawa mheshimiwa”
“Deo..!!”Aliita Mheshimiwa baada ya Deo kukaribia mlango wa kutokea.
“Ndio mheshimiwa”
“Nataka pia taarifa zinazomuhusu Roma Ramoni kwa kila anachokifanya ndani ya Tanzania , Tafuta mtu kwa ajili ya kazi hio”
“Sawa mheshimiwa”Alijibu Deo na kisha akatoka nje.
Licha ya Kamau kumfungia Maina , lakini alikuwa na hofu na Roma mno aliamini yeye ndio enaeweza kuwa kikwazo cha kumzuia Blandina kubakia ndani ya ikulun, taarifa ya Roma aliokuwa nayo haikuwa ndogo kabisa na alijua kwa uwezo aliokuwa nao Roma kama atajua mama yake amefungiwa ndani ya ikulu yake ni Dhahiri angechukua hatua