SEHEMU YA 238.
“Kabla sijaendelea kuelezea naomba kuuliza swali?”Aliongea The First Black kwa wasiwasi.
“Unaweza kuuliza , lakini ni swali moja tu nakuruhusu”Ilisikika sauti ya Athena ndani ya chumba hiko cha hoteli na The First Black alivuta pumzi.
“Kwa miaka mingi nimekuwa nikiishi chini yako na kukutii kwa kila maelekzo uliokuwa ukinipatia na kuhakikisha nakupatia majibu ambayo yanakuridhisha , lakini pia niliamini katika kichwa changu unao uwezo wa kujua kila kitu ndani ya dunia hii na kutokana na hilo nimekuwa nakuheshimu sana , lakini kazi hii ya kuwafuatilia wanachama wote wa Illuminat imenishangaza, hivyo swali langu ni kutaka kujua kwanini unawatafuta hawa wanachama?”Aliuliza The First Black.
“Nikitaka kujibu swali lako kwa ufahasa , lazima uelewe historia yangu ya nyuma miaka mingi tokea kufika kwetu ndani ya uso wa dunia, nadhani unakumbuka mara ya mwisho nilikueleza kuwa sikufika kwenye dunia hii peke yangu?”
“Ndio nakumbuka?”
“Basi jibu ni kwamba nawatafuta ndugu zangu niliokuja nao na naamini kwa asilimia mia moja wamejificha chini ya hili kundi la Illuminat, nina mpango unaoendelea na ili kufanikiwa kwa mpango wangu nikuhakikisha nakuwa na kila jina la mwanachama wa Illuminat ndani ya dunia hii”Aliongea Athena.
“Asante kwa jibu lako”
“Huna haja ya kunishukuru , nimekujibu kwakua nataka majibu yangu kukusaidia katika kazi yako , hivyo huu ni wakati wako wa kunielezea Illuminat ni kundi lipi na Freemason ni kundi lipi”Aliongea .
“Mimi ni mwanachama wa Illuminat , naomba unisaheme kwa kukuficha juu ya hilo”Aliongea The First Black kwa wasiwasi mkubwa lakini muda ule ule aliijikuta akikosa hewa na kuanza kukohoa mfululizo huku akiwa ameshikilia shingo yake kama mtu anaekabwa.
“Nao..mba uni..sa.. mehe , nilikuwa na sababu ya kutokukueleza”Aliongea huku akilala kwenye sofa kwa namna ya kurusha rusha miguu kama mtu anaekata roho na tukio hilo lilidumu kwa muda wa dakika chache tu na alimuachia.
“Biuadamu tabia yenu ya kusema uongo inaniudhi sana na inanipelekea kuwachukia kila siku”Ilisikika sauti ya kike , licha ya kwamba ilikuwa ikiashria hasira , lakini bado ilikuwa nyororo.
“Nitakueleza ninachokijua kuhusu Illuminat , naomba unisamehe kwa kukuficha”Aliongea The First Black na kisha akavuta pumzi na kuweka akili yake sawa.
“Illuminat kama nilivyosema kiasili sio waanzilishi wa kundi la Freemason , bali Illuminat waliomba hifadhi ya kujificha ndani ya kundi hili la Bavarian la wajenzi huru , ambao enzi hizo walikuwa na utajiri mkubwa, sababu iliowafanya wajifiche chini ya kundi la Freemason ni kutokana na kwamba walikuwa wakiwindwa sana na serikali ya Kirumi… “Aliongea na kisha akaendelea.
Kwa maelezo yake ni kwamba Mwaka kati ya 1700 kuendelea ndani ya mamlaka ya Rumi kuliibuka wanasayansi wengi ambao walikuwa wakifanya gunduzi mbalimbali , kulikuwa na wanasayansi wabobezi katika maswala ya hesabu , kuna waliokuwa wamebobea katika maswala ya biolojia na mashine lakini pia kulikuwa na wanasayansi walibobea katika maswala ya anga.
The First Black anaelezea kwamba baada ya gunduzi hizi kufikia serikali ya kirumi ambayo ilikuwa ikiongozwa kwa misingi ya dini, walikasirishwa na baadhi ya gunduzi za wanasayansi hao kutokana na kwamba zilikuwa zikipingana na maandiko matakatifu na hili liliibua uhasama sana kwa watu wa dini na kuona wanasayansi hao wanapingana moja kwa moja na dini kutokana na tafiti zao ,na hapo ndipo serikali ilipoanza msako wa kukamatwa kwa watu waliokuwa wakijiita wanasayansi , na serikali iliwakamata na kuwatesa huku ikiwataka wanasayansi hao wabatilishe baadhi ya kauli zao.
Sasa basi baada ya serikali kuzidi kutesa na kuua wanasayansi wengi , ilipelekea hofu kwa wanasayansi wengine ambao hawajafikiwa na serikali na kupitia hofu yao iliwafanya wakusanyike kwa siri sana kwa ajili ya kuzungumza mustakabali wao wa kuendeleza sayansi na teknolojia, baada ya kufanikiwa kukutanika kwa siri waliamua kujipatia jina kwanza ili kujiongezea hamasa na ujasiri ,na ndipo walipojipatia jina la ‘Enlightened ones’ yaan Illuminat.
The First Black anaelezea kwa kusema kwamba dhumuni ambalo liliwafanya wanasayansi hawa kukutana ni kwa ajili ya kutaka kuanzisha vita na watu wa dini kutokana na tabia yao ya kuwakamata na kuwatesa , jambo ambalo lilipingwa vikali na mwanasayansi mmoja maarufu ambaye pia alikuwa ni mtu wa dini kindakindaki , mwanasayansi ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Galilei Galilleo.
Gallileo aliwapinga wenzake kwa mpango wao wa kuanzisha vita kwa madai ya kwamba sayansi na Dini ni vitu viwili vinavyotegemeana na kwamba Sayansi ipo kwa ajili ya kuimarisha na kuipa nguvu dini , hivyo akawaasa wanasayansi wenzake wasifanye fujo bali yeye yupo tayari Kwenda kuzungumza na watu wa dini juu ya kwamba sayansi haipingi uwepo wa mungu Zaidi ya kwamba inaipa nguvu dini kimaarifa.
Sasa kwasababu Gallileo ndio aliependekeza swala hilo , wanasyanasi wakaona wajaribu kuongea na watu wa dini.
Kabla ya hapo Gallieo alikuwa tayari ashagundua kwamba dunia ilikuwa ni duara lakini pia Dunia ndio inazunguka jua na sio jua kuzunguka dunia na aliweza kugundua kutumia darubidni yake.
Sasa gunduzi yake ilikuwa ikipingana na watu wa dini waliokuwa wakiamini kwamba dunia ni tambarare na haiwezi kuwa duara na jua ndio linaiuzunguka dunia, sasa Baada ya Gallieo kutangaza gunduzi yake alianza kuwindwa na watu wa dini na alionekana kama kichaa na mtu anaeenda kinyume na mafundisho ya dini , hivyo akaingia kwenye orodha ya watu wanaotafutwa na watu wa dini.
First Black anaelezea kwa kusema kwamba kundi lote la Illuminat ambao sasa ni wanasayansi , walipendekeza Galileo Kwenda kuongea na watu wa dini juu ya pendekezo lake, na Gallielo hakupinga kwanza alikuwa akipenda sana dini licha ya kuwa mwanasayansi hivyo alifanya maamuzi ya Kwenda kuongea na watu wa dini, na alipoweka swala lake wazi , palepale alikamatwa na kuingizwa kwenye chumba cha mateso huku akilazimishwa kubatilisha kauli yake ya kwamba dunia ni duara, lakini Galileo hakuwa tayari kubatilisha kauli yake na alisimamia msimamo wake , jambo ambalo liliwaudhi watu wa kanisa na kuamua kumfunga ndani ya chumba cha gereza lenye giza mpaka umauti wake.
Sasa huku wa kundi la illuminat baada ya kuona mpango umebuma walianza kutoroka nje ya mamlaka ya kirumi na Kwenda mbali Zaidi nje ya mkono wa serikali , wakitafuta eneo zuri Zaidi kwa aijili ya kujunda upya, na katika heka heka zao ndipo walipokuja kukutana na kundi lingine linalofahmika kwa jina la Freemason na Kundi la Illuminat ndipo walipamua kujiunga nao kwa kuomba hifadhi ndanni ya kundi hilo.
Na kwanzia hapo kundi hilo la wanasayansi walitumia jina la Freemason kuendeleza Imani yao ya kuamini katika sayansi na kipindi ambacho wanakubaliwa kuingia , kundi la Freemason lilikuwa na wafuansi wengi mno kuanzia Amerika yote mpaka kufikia baadhi ya nchi za Ulaya na walikuwa washajenga mpaka Lodge za kufanyia ibada zao.
“Kwa maelezo yako Illuminat waliamua kutumia jina la Freemason kuendeleza mipango yao ya maendeleo ya kisayansi?”Aliuliza Mrembo The Doni.
“Ndio na baada ya wao kujiunga na Freemason kundi lao lilipote na kuwa Dormant”
“Kwa maelezo yako ni Dhahiri kwamba huwezi kutenganisha Freeason na Illuminat?”
“Ndio kwasababu Freemason , licha ya kwamba hatuamini uwepo wa Mungu , lakini pia Freemason tunaamini Zaidi katika utajiri na huo ndio msingi wa dunia hii”
“Kwenye vikao vyenu mnazungumza nini kuhusu mimi?”
“We Believe you are one of us”
“Tunaamini wewe ni mmoja wetu”Aliongea The First Black.
********
Mheshimiwa Senga alimkaribisha Kigombola kwa tabasamu la kinafiki mtangulizi wake mara baada ya kufika ndani ya ukumbi wa ikulu wa kuonana na wageni na kwa upande wa Mheshimiwa Kigombola , alikuwa akijua kuwa tabasamu la Senga ni la kinafiki kwasababu Mheshimiwa Kigombola hakuwa chaguo lake katika kumrithisha uongozi , ni hivyo tu kwamba wazee wachama ndio waliokuwa na nguvu Zaidi , hivyo kumfanya ashindwe kushindana nao na kuweka mtu anaemtaka yeye.
Baada ya kusalimiana kwa dakika kama kumi na tano huku vicheko vya kinafiki vikiendelea, Mheshimiwa Kigombola alienda kwenye jambo ambalo limemfaya kuja hapo ikulu.
“Nina uhakika ushapata taarifa juu ya mimi kuonana na baadhi ya viongozi wakubwa wa ulinzi , akiwemo jenerali Tozo?”Aliongea Mheshimiwa Kigombola na kumfanya Senga kushangaa kidogo na kushindwa kufahamu nia ya mtangulizi wake.
“Ndio nimeipata na imenichanganya sana mimi kama mkuu wa Nchi kuona viongozi wa chini yangu wanafanya mambo pasipo kunishirikisha”Aliongea Senga na kumfanya Mheshimiwa Mstaafu kutabasamu.
“Nazifahamu hizo hisia kwasababu hata mimi nishawahi kuwa katika nafasi yako, niende moja kwa moja , kwanza kabisa mimi ndio niliowaita kwa ajili ya kuzungumza nao na swala ambalo tumezungumza ni kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa hili”
“Wiki kadhaa nyuma nilipokea ugeni kutoka taifa la China na sikuelewa kwanini Jenerali wa jeshi la wananchi wa China aliagiza mgeni kuja moja kwa moja kwangu, lakini naweza kukisia dhumuni lao”Mheshimiwa Senga alishangaa maana hakuwa na taarifa hio.
“Mheshimiwa Senga kuna siri ambayo sikukuambia baada ya kuachia madaraka na leo hii nipo hapa kwa ajili ya kuiweka wazi”
“Siri!!!”Mheshimiwa Senga alishangaa .
ITANDELEA JUMAPILI MCHANA
0687151346 .WATSAPP NICHEKI TUONE NAMNA YA WEWE KUENDEKEA KUBURUDIKA