SEHEMU YA 235.
Ilikuw ani siku ya jumapili , Edna aliamka asubuhi kama kawaida , huku akichangamkiwa na Blandina mama yake Roma wakati anashuka mezani kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.
Blandina tokea ujue ukweli kwamba Edna aliolewa akiwa Bikra basi alitokea kumpenda mno na kuona pia mtoto wake ana bahati sana kupendewa na mwanamke mrembo kama Edna.
Sasa tokea siku hio alikuwa akihakikisha anamuonyeshea Edna mapenzi ya aina yake ili asijione mpweke na ahisi yupo kwenye familia sahihi na mume wake Roma nichaguo bora.
Sasa muda wa asubuhi Roma alikuwa na wanafamilia wengine kwenye meza wakijipatia kifungua kinywa , ili baada ya hapo ratiba zingine ziendelee.
“Edna bado unaendelea na utaratibu wa Kwenda kule kituoni kila siku ya jumapili?”Aliongea Blandina na kumfanya Edna atabasamu na kumwangalia mama mkwe wake.
“Ndio na nishajiandaa nataka kuelekea huko asubuhi ya leo”Aliongea Edna na kumfanya Blandina atabasamu.
“Edna mwanangu , najua sijawahi kukuambia haya , lakini nashukuru sana kwa msaada wako juu ya kuwasaidia wale Watoto, baada ya mama yako kufariki nilikuwa na wasiwasi mno ya kupata mfadhili mwingine , lakini nashukuru haujaacha kuendeleza kile ambacho mama yako na bibi yako walikuwa wakikifanya”
“Mama huna haja ya kunishukuru zaidi ya kwamba pongezi nizielekeze kwako kwani kituo kile kimekuwa sehemu ya familia yangu na nafarijika kila ninapo waona wale Watoto wakiishi kwenye mazingira safi na salama”Aliongea Edna na Blandina alijikuta akitabaamu na kujiambia yes huyu ndio mkwe.
“Leo tutaenda wote, nina siku nyingi sijaonana na Mama Issa”Aliongea huku akimwangalia Yezi na Edna aliitikia kwani hakuona ubaya na isitoshe Blandina alikuwa ni mwanzilishi wa kile kituo.
Saa tatu kamili Edna ndio aliekuwa akiendesha gari kuelekea Kiwangwa na walikuwa washanunua mahitaji maalumu tayari kwa ajili ya Watoto na ilikuwa ni kazi ya kupeleka tu.
“Edna niseme tena asante…. Nakushukuru sana mwanangu”Aliongea Blandina na kumfanya Edna kupunguza mwendo.
“Mama kwanini unanishukuru hivyo”
“Edna hujui ni kiasi gani nimefurahishwa na wewe kumkubali mwanangu na kumpenda na kuvumilia madhaifu yake , mimi kama mama yake nakushukuru sana kwa kumpenda Roma na kumvumilia , hata nikiondoka kwenye huu ulimwengu najua anazaidi ya mama”Aliongea Blandina na kumfanya Edna ashindwe jinsi ya kujibu , kwanza aliona aibu na kukosa utulivu pia na alijua pia Blandina atakuwa ashaona Maisha yao wanavyoishi na mume wake Roma.
Lakini wakati huo Edna alikumbuka kuwa licha ya kwamba ni kweli anajihisi kuwa na hisia za kimapenzi na Roma , lakini ndoa yao ni ya kimkataba na ndio maana wanaishi kama sio wanandoa.
“Edna nitajitahidi kuhakikisha Roma anabadili tabia yake , nimesikia kila kitu kutoka kwa Bi Wema juu ya Roma kutoka nje ya ndoa , naomba umvumilie nitamrekebisha , nimeomba tuje wote huku kwasababu nilitaka kukuambia hivyo”Aliongea na Edna akatabasamu na kuitikia kwa kichwa na muda huu tayari walikuwa wakiingia kituoni.
Mama Issa alikuwa na taarifa za ujio wa rafiki yake Blandina na alionekana kusimama nje ya jengo lake kwa kumsubiria kwa hamu na ile gari inaingia hapo ndani kituoni alisogelea na walikumbatiana na Blandina baada tu ya kutoka.
“Edna karibuni sana..”Aliongea Mama Issa kwa furaha huku akiwakaribisha na Edna aliacha ufunguo kwa wafanyakazi kwa ajili ya kutoa mizigo nyuma,
Stori za bapa na pale kati ya Mama Issa zilianza na Edna kama kawaida yake alijichanganya na Watoto na kuanza kucheza nao kwa furaha , alionekan kufika kwenye ulimwengu wake , kwani alicheka kama sio yeye vile na kumfanya kupendeza na Mama Issa na Blandina walifurahia kwa jinsi walivyokuwa wanamuangalia.
“Blandina hongera sana kwa kumpata mtoto wako Denisi, unajua baada ya kupewa taarifa na Jestina nilianza kufikiria siku ya kwanza Edna na Mr Roma walivyofika hapa ndani ya kituo”Aliongea Mama Issa na kumfanya Blandina amuangalie kama mtu ambaye akisubiria Blandina aendele kuongea.
“Unakumbuka kuwa kuna picha yako ambayo ipo pale ofisini kwani?”
“Ndio nakumbuka na ile picha ipo kwa kila kituo nilichofungua”Aliongea Blandina.
“Sasa siku ya kwanza Mr Roma kuangalia ile picha nilihisi mabadiliko yake ila niliyapotezea kwani nilimuona kama mtu mzuri”Aliongea Mama Issa.
“Unazungumzia mabadiliko ya aina gani?”
“Kwanza aliangalia picha yako kwa muda mrefu sana, lakini kuna kitu sio cha kawaida ambacho kilimtokea , niliona macho yake yakibadilika kwa kupitia kioo cha ofisini kwangu”Aliongea Mama Issa na kumfanya Blandina kushangaa
“Macho kubadilika , mbona sijakuelewa hapo Tabea”Aliongea na kumuita jina lake halisi.
“Sijui nielezeje , ila macho yake yalibadilika na kuwa na kiini cha rangi ya kijani , japo sikuwa na uhakika sana ila alishindwa kuendelea kuangalia picha yako na kukimbilia nje na mimi sikutaka kuuliza na nilijifanya sijaona kitu na ilibidi niitoe ile picha kwa muda nikihofia mabadiliko yake”Aliongea na kumfanya Blandina kukumbuka tukio la Roma kudhibiti wanausalama wakati anakuja kuonana na familia yake , lakini pia aliweza kukumbuka namna Roma kule Kenya namna alivyoweza kuzuia risasi.
“Tabea hata mimi nahisi Roma sio wa kawaida kabisa , lakini ninafuraha kwamba nimeonana nae kwa wakati mwingine na huzuni yangu ya kukosa mtoto imepungua kwa sasa , Namshukuru sana Edna kwa kumpokea Roma licha ya kwamba sio wakawaida”Aliongea na kumfanya Mama Issa atabasamu.
“Nampenda sana Edna na hata siku ambayo alimtambulisha Roma kwangu , nilimpenda mume wake pia , niliamini chaguo lake sio baya na kweli Imani yangu ilikuwa sahihi , huyu mtoto namuona kama baraka tokea alivyokuwa mdogo”Aliongea Mama Issa na wote wakageuka na kumwangalia Edna aliekuwa akikimbizana na Watoto kuelekea getini , lakini walishangaa pia Edna akisimama ghafla na macho yake yote kuyaelekeza getini na Watoto wote pia.
Edna alikuwa amemuaona mtoto aliekuwa amesimama kwenye geti , mtoto ambaye sura yake hakuweza kuisahau , alikuwa ni Lanlan.
“Yule mtoto ni nani?”Aliuliza Blandina baada ya kugundua Edna alikuwa akimwangalia mtoto.
“ Ni zadi ya mara tatu namuona sasa , anaishi upande wa pili na siku zote akija anasimama pale getini pasipo ya kuingia ndani”Aliongea Mama Issa na kumfanya Blandisha kushangaa.
“Ni kazuri jamani nakaona kwa mbali lakini anaonekana kufanana na Edna kabisa”
“Ni kweli hata mimi nilikuwa nikisema hivyo , kumbe hata wewe mwenzangu umeona?”Aliongea na wote wakacheka.
“Lanlan..!1”Aliita Edna huku akimsogelea Lanlan.
“Mom..!”Alita Lanlan huku akimsogela Edna kwa kusita sita , lakini Edna baada ya kusikia anaitwa Mama kwa mara nyingine na mtoto huyu moyo wake ulijihisi kitu cha ajabu.
“Lanlan njoo unikumbatie”Aliongea Edna kwa Kingereza kwani alikuwa akifahamu Lanlan hakuwa akijua Kiswahili, sasa kwa upande wa Lanlan ni kama alikuwa akisikia suati mbilimbili , sauti zinazofanana kabisa na ya mama yake mzazi na alionekana kuchanganyikiwa.
“Mom..!”Aliitakwa mara ya pili na Edna ilibidi achuchumae na kumkumbatia Lanlani ambaye machozi yanaanza kumtoka.
“Lanlan usilie tena.. niangalie machoni”Aliongea Edna huku akimwangalia Lanlan machoni na kumfuta machozi kwa mkono.
Sasa kitendo cha Lanlan kumwangalia Edna machoni , sijui nini kilitokea ila miale mnyoofu kama ya jua ilitoka kweye macho ya Lanlan na kutua kwenye macho ya Edna kitendo ambacho kilimfanya Edna kukosa nguvu na palepale alidondoka na kuzimia .
“Moo..om…”Aliita Lanlan kwa sauti na kumfanya Blandina na Mama Issa kukimbia baada ya kuona tukio lile.
*******
GENEVA -USWISI.
Ni ndani ya hoteli ya nyota tano ndani ya hoteli kubwa ya nyota tano , katika chumba cha Presidential Suite , anaonekana The First Black akiwa amekaa kwenye sofa kwa mkao ambao ni kama alikuwa akiongea na mtu , na kwa jinsi alivyokuwa akionekana ni Dhahiri kwamba wasiwasi ulikuwa umemjaa kwenye macho yake.
Na kwa watu ambao walikuwa wamemzoea The First Black , basi wangeshangaa kwa namna ambavyo alikuwa akionekana , Raisi huyu katika kutawala kwake miaka kadhaa nyuma alikuwa akijimini sana na ni mtu ambaye alikuwa akisifika kwa uongozi thabiti ambao umeleta maendeleo makubwa ndani ya Marekani na nje pia na hii ilifanya watu wengi kumkubali sana,
“Have you accomplished the task?”Ilisikika sauti ya kike chumba kizima na haikuelweka sauti hio ilikuwa ikitokea upande gani, lakini kwa mtu ambaye angeweza kuisikia angeifahamu mara moja , ilikuwa ni sauti ya Mwanamke Mrembo Athena na ilionekana alikuwa akitumia mbinu ya kuongea na The First Black pasipo kujionyesha.
“Miss sijakamilisha bado , lakini mpaka sasa hivi kuna mafanikio makubwa”Aliongea The First Black kwa wasiwasi.
“Your taking too much time for small issue like this Mr First Black , I Installed you as head of Zeros Organisation because I belived, you are smart…”
“Unachukua muda mrefu kwa jambo dogo kama hili Mr First Black , nilikufanya kuwa mkuu wa Zeros organization kwasababu niliamini una akili…”
“No.. no..”
“Sitaki uniingilie wakati nikiwa na zungumza”aliongea Athana asieonekana kwa namna ya kuamrisha na First Black mzee huyu mwenye mvi alikuwa mdogo kama Piritoni.
“Tell me about Illuminat?”Aliongea Athena au The Doni na kumfanya Mr First Black kumeza mate na hata hali ya kujiamini ikaongezeka.
“Malaika! .. tafadhati naomba nikueleze hili baada ya kukuona, nimeishi miaka mingi tokea nikiwa Director wa CIA mpaka kuwa raisi kwa kukutii , lakini kwa miaka yote hio sijapata hata nafasi ya kuona unavyofanania, kama tunataka kufanya jambo kubwa kwa dunia hii mimi na wewe naamini huu ni wakati mzuri wa kujionyesha kwangu”Aliongea The Fisr Black.
“Hahaha… kwahio unadhani unanidai kwa kazi uliofanya , unatakiwa kuelewa mimi na wewe hatudaiani , umekuwa mtu mwenye nguvu sana ndani ya Zeros Organisation kwasababu yangu , umekuwa raisi wa Marekani licha ya Ngozi yako kwasababu yangu na mpaka sasa nimekufanya kuwa mtu kuogopeka kwa sababu yangu , unafikiri kwa nilioyafanya unapaswa kunidai au unakitafuta kifo”Aliuliza Athena huku sauti yake ikidhihirisha kukasirika.
“Hapana Malaika .. naomba unisamehe , ni kwamba nimekuwa mtu wa kutamani sana kukuona , sauti yako kila siku imeendelea kuishi kwenye fikra zangu miaka na miaka na nimetengeneza taswira nyingi sana tokea siku ya kwanza naisikia sauti yako”Aliongea.
“Acha kuongea upumbavu , misheni niliokupa ukiweza kuikamilisha nitajionyesha kwako , lakini itakuwa ni kwa mapenzi yangu , kwangu wewe ni binadamu tu ambaye ninaweza kuchukua Maisha yako muda wowote , hivyo jitahadhari sana unavyotaka kupata kitu kutoka kwangu”Aliongea The Don .
“Naomba unisamehe , hili halitajirudia tena Malaika”
“Tell me about Illuminat”Aliongea kwa amri na The First Black alimeza mate na kisha akakaa vizuri.
“They are not Freemason`s”Aliongea The First Black kwa utulivu akimaanisha kwamba Illuminat sio mafreemason
“Endelea kuongea na hakikisha una Ushahidi”
SEHEMU YA 236.
2005- UNKNOWN PLACE
Ni mwaka 2005 anaonekana Athena akiwa amembeba Msichana mdogo rika la miaka kumi na moja hivi akiwa ndani ya kambi ya Kisayansi ambayo bado haikufahamika kambi hio ipo sehemu gani katika uso wa dunia.
Athena baada ya kuingia ndani ya kambi hii ya kufanyia majaribio ya kisayansi , kambi ambayo ilikuwa na teknolojia ya hali ya juu , alimuweka msichana huyo mdogo kwenye sofa ndani ya chumba ambacho kimezungukwa na Skrini nyingi zilizokuwa zikionesha maeneo mbalimbali ya dunia.
Baada ya kumuweka Msichana kwenye sofa , alimpiga kichwani eneo la utosini na palepale msichana yule alishituka kutoka usingizini.
“Where am I?”Ndio swali la kwanza lililotoka kwa mwanadada yule Kwenda kwa Athena ambaye alikuwa akimwangalia kwa kutabasamu kwa namna msichana huyo alivyokuwa akishangaa mazingira mapya aliokuwepo.
“Your in Atarctica Continent Naira” Aliongea Athena huku akimwangalia kwa kutabasamu msichana aliekuwa mbele yake.
Naira hapa alikuwa na miaka kumi na moja tu na kwa jinsi alivyokuwa akionekana ilionyesha ni Dhahiri alikuwa ndani ya maabara akifanya majaribio ya kisayansi, kwani kwa nguo zake alizovalia zilikuwa zikimtambulisha kama mwanasayansi licha ya umri wake mdogo.
Naam sasa tunajua sasa kwamba eneo ambalo Naira ameletwa na Athena ni ndani ya bara la Atarcticta bara ambalo hakuna makazi ya muda mrefu kwa binadamu kutokana na hali ya hewa yake kuwa ya baridi kali.
Naira alishangaa kuambiwa kuwa alikuwa ndani ya bara la Atarctica, kwani dakika kadhaa nyuma alikuwa ndani ya maabara chini ya Zeros Organisation akifanya kazi zake kama kawaida , lakini pia mwanamke mrembo aliekuwa mbele yake hakuwahi kuonana nae kwenye Maisha yake na jambo hilo lilimfanya kushangaa Zaidi.
“Kama kweli nipo ndani ya bara la Antarctica nimefikaje hapa?”Aliuliza Naira huku akishangaa maeneo yote ya chumba alichokuwemo na alijjiambia licha ya kambi ya Zeros aliokuwa akifanyia kazi kuwa na teknolojia kubwa , lakini hapa ndani teknolojia yake ilikuwa sio ya kawaida na akili zake za kisomi zilimwaminisha hivyo kwa asilimia kubwa.
“We teleported”Aliongea Athena huku akisogelea Friji upande wa kushoto kwake na kutoa chupa ya bia mfano wa zile za konyagi na kisha akaweka kilevi kwenye glass mbili na kumsogelea Naira na kumpa ishara ya kupokea, lakini Naira bado alikuwa akiogopa kwani mtu aliekuwa mbele yake hakuwahi kumuona , lakini pia alimwambia mambo ambayo hayawezekani.
“We..tele.. ported , how!”Aliongea kwa namna ya kubabaika na kumfanya Athena kutabasamu huku akimpa ishara ya kupokea kwanza glass ya kilevi na Naira alipokea kwa mikono miwili huku akitetemeka.
“Unaonekana kutokuniamini?” Aliuliza na Naira alishindwa kujibu lakini kwa Athena akatabasamu.
“I can utilize space laws to teleport from one point to onether with maximum speed , I can even manipulate space time”Aliongea athena akimaanisha kwamba anauwezo wa kutumia kanuni za anga kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine na spidi ya juu na pia anao uwezo wa kuendesha muda.
Licha ya meneno hayo kufika kwa msichana mdogo Naira , lakini alishindwa kuelewa na kuyapokea kwa wakati mmoja , lilikuwa ni jambo kubwa kwake na alishindwa hata kuliamini na katika Maisha yake hakuwahi kuwaza kwamba atakutana na mtu wa aina hio , licha ya kwamba ni miaka minne tu aliokuwa ameingizwa ndani ya Zeros kwa ajili ya mafunzo ya kisayansi , lakini swala la kutumia kanuni za anga kusafiri lakinii pia kuongoza muda lilikuwa kubwa kwake.
Athena pia alitambua kuwa Naira alikuwa kwenye wakati mgumu kusharabu maneno yake na ndio maana hakutaka kuongea nae Zaidi ya kumuonyesha kwa vitendo na ile Naira anapeleka Glass ya wine mdomoni palepale Athena alisimamisha muda na kisha akamsogelea Naira na kuchukua glass yake ya wine na kuishika mkononi na kisha hali ikarudi kama ilivyokuwa kawaida na Naira alijikuta akiduwaaa huku akisimama na kujiangalia mikono yake.
“Umewezaje kuchukua Glass yangu pasipo mimi kujua?”Aliuliza kwa shauku.
“Timespace manipulation”Aliongea Athena na wakati Naira anaendeelea kumwangalia , palepale akapotea alipokuwa amesimama na kilikuwa ni kitendo cha kupepesa macho mara moja Athena alikuwa nyuma yake na kumfanya Naira kuzidi kuchanganyikiwa.
“Wewe ni nani….?”Aliuliza Naira huku akijituliza.
“No there is no Woman God , She Cant be God , maybe an Angel”Aliwaza kwenye kichwa chake Naira akimaanisha kwamba hakuna mwanamke Mungu , na hawezi kuwa mungu labda awe Malaika.
“Swali zuri Naira, mpaka hapo nadhani ushaanza kuamini na nitajibu maswali yako kila nitakapokuwa na muda”
“I am alien,Arrived on Earth many years Ago”Aluiongea Athena kwamba yeye ni kiumbe kutoka sayari nyingine ambaye amefika hapa duniani miaka mingi iliopita.
“Unaweza kuniita utakavyo , watu wa dini wananifahamu kama Athena kwa upande wa Ugiriki, watu kutoka Rumi wananifahamu kama Minerva , kwa Underworld t wananiita The Doni”Aliongea Athena na kumfanya Naira kushindwa kuelewa na kusharabu maneno hayo.
Athena , Minerva , The Doni , yalikuwa ni maneno yaliopita kwenye kichwa chake.
“Naira nitakujibu maswali yako taratibu kwasababu wewe ni binadamu ambaye sio wa kawaida na nimekuchagua ili kunisaida katika misheni yangu”Aliongea Athena huku akiketi na kukunja nne kwenye Sofa.
“This place will be your new home, New Lab , New Task with great cause, you are going to learn undiscovered knowledge about universe, and maybe in future you will be like me”
“Hii sehemu itakuwa ndio makazi yako mapya , maabara yako mya , kazi mpya yenye malengo makubwa , unakwenda kujifunza maarifa kuhusu ulimwengu ambayo hayajagunduliwa na labda baadae unaweza kuwa kama mimi”Aliongea Athena na kumfanya Naira kudhindwa kuelewa mara moja point ya msingi.
“Unanifahamu vipi mimi?”Aliuliza Naira kwa wasiwasi na Athena alitabasamu.
“Nakufahamu kwa muda mrefu sana , tokea ulipozaliwa na makuzi yako ndani ya Afrika , namfahamu rafiki yako kipenzi Doris Alex, namfahamu baba yako Ryan , namfahamu mama yako Epholia , nilikuwa nikikuangalia kila siku katika ukuaji wako”Aliongea Athena.
“Kwanini ulikuwa ukiniangalia?”
“Najua mama yako na baba yako hawakukueleza kwanini walikuwa ndani ya bara la Afrika na sio ndani ya nchi yao uliozaliwa”Aliongea Athena na kumfanya Naira akumbuke kuwa ni kweli hakuwahi kuelezwa na wazazi wake kwanini walikuwa ndani ya taifa la Tanzania ,na kwanini yeye pekee ndio alikuwa mtoto mwenye rangi tofauti na Watoto wengine.
Kwa maelezo ya Athena Kwenda kwa Naira ni kwamba Athena alifika ndani ya dunia hii miaka mingi iliopita kipindi kabla hata ya dini kuenea na wakati anafika hapa Duniani hakuwa peke yake bali alikuwa na kundi la watu wengine waliotoka katika sayari nyingine lakini baada ya kufika hapa duniani mategemeo yao yalikuwa nje ya matarajio, kwani walikuja kugundua kuwa miili yao haiendani na hali ya hewa na Mazingira ya binadamu , hivyo walishindwa kuendana na mazingira na walikuwa katika hatihati ya kupoteza maisha , jambo ambalo hawakauwa tayari kulikubali hata kidogo , kwani walikimbilia ndani ya dunia hii kwa ajili ya kupata makazi mapya.
Katika namna ya kutafuta mbinu za kuishi ndani ya dunia , ndipo kwa kutumia akili zao waliposhauriana kuachana na miili yao ambayo haina uwezo wa kuendana na mazingira ya dunia na kutumia miili ya binadamu kuhifadhi nafsi zao , na wakati wanapanga hayo yote walikuwa juu angani kwenye mzingo wa dunia kwenye vifaa vyao na baada ya kushauriana kwa malumbano ya siku kadhaa ndipo walipofikia makubaliano ya kuendelea na wazo la kuacha miili yao na Nafsi zao zikavae miili ya binadamu.
Athena anaendelea kuelezea kwamba , katika jaribio la kuvaa miili ya binadamu lilifanikiwa kwa asilimia kubwa lakini pia mpango wao ulitokeza dosari.
“Dosari gani zilijitokeza?”Aliuliza Naira kwa shauku.
“Tulipotezana lakini pia kupoteza rasilimali tulizokuja nazo”Aliongea Athena kwa huzuni.
“Ilikuwaje mpaka mkapotezana kama mpango ulikuwa unawezekana”
“Because we underestimated human?”Aliongea akimaanisha kwamba kwasababu tuliwadharau binadamu.
“ Kivipi?”
“Tuliwadharau binadamu kwa kuwaona kama viumbe dhaifu sana na tungeweza kutawala miili yao tutakavyo kwa kutumia nafsi zetu , lakini jambo hili lilishindikana kwa asilimia kubwa , kwani licha ya kwamba binadamu walionekana dhaifu kutokana na muonekano wao , lakini Nafsi zao zilikuwa na nguvu kuzidi za kwetu na hilo ndio kosa letu”
“Kwahio nini kilitokea?”
“Asilimia tisini za nafsi zilizoshuka duniani kwa ajili ya kuvaa miili ya binadamu zilimezwa na nafsi za binadamu kwa maneno marahisi unaweza kusema kwamba nafsi zetu zilibakia kuwa ‘Defunct’Aliongea Athena na kumfanya Naira kushangaa Zaidi.
“Na vipi asilimia moja iliobaki?”
“Swali zuri Naira , nafsi kumi na mbili tu ndio ziliweza kushindana na nafsi za binadamu na kuuteka mwili lakini licha ya hivyo tulipoteza uwezo wetu mkubwa wa kumbukumbu”Naira alishangaa Zaidi.
Athena anaendelea kusema kwamba baada ya wao kumi na mbili kuweza kufanikiwa kuteka nafsi za binaadamu na hatimae kuuteka mwili walipoteza nguvu zao , lakini pia walipoteza rasilimali zao ambazo zingewarudishia uwezo wao , lakini pia akasema kwamba wao kumi na mbili ambao waliweza kuteka miili ya binadamu na nafsi zao iliwezekana tu kutokana na kwamba walikuwa wakitokea kwenye koo moja ya kifalme katika sayari yao ambayo bado hajaiweka wazi.
“Rasilimali gani ambazo mlipoteza?”
“Swali zuri Naira , tofauti ya sayari yetu na ya kwenu ni Energy”
“Energy!!?”Aliuliza kwa mshangao.
“Yes kwenye sayari yetu tunatumia ‘Pure Energy nikimaanisha kwamba energy ambayo haitokani na maada ya aina yoyote”Aliongea.
“You mean Ant-Matter energy?” Aliuliza Naira kwa mshangao.
“Exactly”