Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 225

Kusanyiko lilikuwa ni Zaidi ya lilivyokusudiwa , kwani licha ya kwamba sababu kubwa ilikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza Roma kwa ajili ya kupanda cheo, lakini wafanyakazi walionekana kufurahia Pamoja na kufanya ukaribu wao kuongezeka, hususani kwa wafanyakazi na bosi wao Edna kwani siku zote walikuwa wakimuona kwa mbali.

“Jamani tumepoa sana , usiku huu ungekuwa mzuri kama tungekuwa na msanii wa kutuburudisha”Aliongea Ernest Komwe na kufanya kila mtu amwangalie anachotaka kusema.

“Mnaonaje mmoja wetu anaejua kuimba akatoka mpaka pale mbele na kutuburudisha ninazo instrumental Beat za nyimbo maarufu kwenye simu lakini pia nina hiki”Aliongea Ernest Komwe huku akionyesha kijispika kidogo kampuni ya Anker alichoshikilia mkononi na alifika nacho wakati wa kuja , lakini hakuna ambaye alifahamu kuwa ni kijispika.

“Nitaanza..!”Ni Sauti ya Recho ndio ambayo ilisikika na kufanya kila mtu kufurahi , Recho alionekana wine alizokunywa zishaanza kumuingia kisawa sawaa na na hata ile hofu aliokuwa nayo mbele ya Boss wake ilikuwa imemwishia.

Watu walipiga makofi baada ya Recho kusogea mbele kabisa kwenye ukumbi huu na uzuri ni kwamba ukumbi ambao walikuwa wameuchukua kwa ajili ya mkusanyiko wao ulikuwa ni binafsi , hivyo kilichokuwa kikiendelea ndani hakikuweza kusikika nje.

Wakati watu wote macho yao wakiyaelekeza kwa Recho kwa ajili ya kusikiliza kile ambacho anakwenda kuimba , Nadia Alfonso alinyanyuka kutoka sehemu alikuwa amekaa na kisha akamsogelea Roma.

“Roma tunaweza kuongea?”Aliuliza Nadia na kumfanya Roma aliekuwa akisubiria kwa hamu kumuona Recho akiimba ageuze shingo na kumwangalia Nadia.

“Nadia si unaona tupo katikati ya burudani , hatuwezi kusubiri?”Aliuliza Roma huku akimwangalia Nadia.

“Ni muhimu sana , hatuchukui muda mrefu… pleaese”Aliongea Nadia kwa namna ya kubembeleza na Roma alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha.

Ukweli hakujua Nadia alikuwa akitaka kuongea nini na yeye , kwani tokea alivyomuacha Nadia kwenye mikono ya Stern na Alice kule Ufaransa hakuongea nae tena na hata pale alipofahamu ukaribu uliokuwepo kati ya Nadia na Depney hakuona haja ya kutafuta maelezo Zaidi na aliondoka kurejea Tanzania na kumuacha pasipo kuonana nae tena, lakini kwa jinsi Nadia alivyokuwa akionekana mbele yake aliona kabisa huwenda kuna jambo Zaidi ya lile ambalo anahisi kwenye akili yake Nadia anataka kumwambia.

Roma alimwangalia Edna ambaye alionekana muda wote macho yake yalikuwa yakimwangalia Recho ambaye ashaanza kuimba kwa madaha na kisha akamgeukia Nadia.

“Wapi unataka tukaongee?”

“Naomba unifuate”Aliongea Nadia huku akianza kupiga hatua kuelekea nje ya ukumbi huo na Roma bila ya kufikiria mara mbili mbili aliamua kunyanyuka na kumfuata.

“Nadia hatupaswi Kwenda mbali sana , sijamuaga Edna”Aliongea Roma baada ya kuona Nadia anazifuata Lift.

“Roma hatuchukui muda mrefu naomba unifuate”Aliongea Nadia huku akibonyeza Lift na kusubiria ifunguke na ndani ya dakika moja ilifunguka na Roma ilibidi aingie kwenye Lift hio Pamoja na Nadia.

“Roma nafahamu unayo maswali mengi ya kilichotokea Paris and I real need to Explain it”Aliongea Nadia.

“Nadia kama unataka kuongea juu ya hili nikuambie tu, huna haja ya kujielezea kabisa , ijapokuwa sijui ukweli wote lakini naaminini halina maana tena kwani Depney alishafariki na ulishuhudia kwa macho yako”Aliongea Roma na muda huo huo Lift ilifunguka juu kabisa kwenye korido yenye vyumba vingi vya kulala.

“Kwahio kweli hutaki nikijielezea…?”Aliongea Nadia huku wakitembea ki upande upande.

“Nadia nishakuambia hauna haja ya kujielezea na sidhani ndio swala ambalo ni muhimu ambalo unataka kuniambia”Aliongea

“Ndio kuna swala lingine muhimu, ila najihisi uhitaji wa kujielezea natumaini utanipa nafasi , I need you to see the reason”Aliongea Nadia na muda huu walikuwa washafika kwenye mlango wa chumba namba 117 ndani ya hoteli hii na Nadia alitoa kadi yake kwenye mkoba wake na kuchomeka kwa kutumia mkono wa kushoto.

Ndio Nadia alikuwa akitumia mkono wa kushoto hata kwenye maswala ya kuandika na mkono wake wa kulia haukuwa na nguvu kabisa.

Baada ya mlango kufunguka Nadia alimpa ishara Roma kuingia na Roma ni mtu ambaye alikuwa akijiamini na hakusita sita kwani aliingia na akafuatia Nadia.

Ni chumba aina ya Super Deluxe , See View na Roma aliendezwa na mpangilio na uzuri wa chumba , mbele kabisa ya chumba hiki alionekana mwanamke ambaye amevalia taulo akiwa amesimama akiangalia upande wa baharini , alikuwa ni mwanamke wa Kizungu na kwa haraka haraka Roma kwa kuangalia nywele zake aligundua kabisa mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa si chini ya miaka sitini na tano ki umri.

“Madam Roma has arrived”Aliongea Nadia kwa Kingereza na Roma alienda moja kwa moja kukaa kwenye masofa huku akimwangalia mwanamke aliekuwa mbele yake , akisubiria ageuka amuone.

“Thank you Nadia for this, now we can talk”Aliongea yule mwanamke kwa sauti yake ya kiutu uzima na akageuka na kisha akatembea kwa kujiamini na kumsogelea Roma.

“Mr Roma naitwa Joyce Donald naomba nitangulize radhi kwa kuingilia ratiba yako usiku huu”Aliongea yule mwanamke wa Kizungu huku akinyoosha mkono kumpatia Roma kama salamu , lakini Roma hakuupokea.

“Joyce umeingilia ratiba zangu usiku huu, lakini siwezi kuendelea kupoteza muda kama utaendelea kujitambulisha kwangu kwa jina feki na sura bandia”Aliongea Roma kwa pasipo kubadili miuonekano wake na kumfanya Joyce kushangaa kidogo na kisha akatabasamu.

“Hakika wewe ni Hades mwenye kusikika na sifa nyingi , sikuweza kudhania unaweza kunitambua kwa sura bandia ilihali ni mara yetu ya kwanza kuonana , tafadhari naomba uniwie radhi na nitajirambulisha kwa majina yangu halisi”Aliongea kwa Kingereza huku akiketi na kukunja nne kwenye sofa na kumfanya hadi mapaja yake kuwa wazi kutoka na kuvaa taulo tu , lakini kwake hakuona shida.

Upande wa kule ukumbini licha ya kwamba Edna alikuwa bize akimwangalia Recho aliekuwa akiimba , lakini wakati Nadia alivyonyanyuka na kumsogelea Roma aliona kitendo hiko na hata wakati wanatoka pia aliona na Edna baada ya kupita kama dakika nne za Roma na Nadia kutoka na yeye alinyanyuka na kuusogelea mlango wa kutokea na kufanya baadhi ya wafanyakazi wamwangalie , lakini hawakujali kwani waliamini huenda Edna anaenda maliwatoni.

Edna baada ya kutoka nje kabisa , alikumbana na Korido ndefu ambayo haikuonekana kuwa na mtu anaefanana na Roma wala Nadia , alijiuliza Roma kaelekea wapi.

Ukweli hali ya wivu ilimwingia baada ya kumuona Nadia akitoka na Roma hivyo aliamini huenda kuna jambo la kishenzi ambalo Nadia na Roma walikuwa wakipanga kulifanya na ndio maana alitoka kwa ajili ya kuangalia usalama wa mume wake , lakini sasa anajikuta kuwa na wasiwasi Zaidi baada ya kutokumuona Roma ndani ya hilo eneo.

Baada ya kuangalia kulia na kushoto pasipo ya kuona dalili ya Roma alianza kupiga hatua kuelekea upande wa Lift na haikueleweka alikuwa akipanga kufanya nini, lakini alienda na akabonyeza kitufe na lift ilionekana kutokuwa na mtu kwani ilifunguka na aliingia.

“Damn you Roma , umeelekea wapi na yule mwanamke”Aliwaza Edna huku hasira na wivu vikianza kuutekenya moyo wake , Edna hakuwa tayari kumuona Roma akiongeza mchepuko mwingine na ndio maana mpango wake wa kuja kwenye hilo kusanyiko nje ya utaratibu yake ni kumchunga Roma , lakini muda huo alijikuta akiwa amepigwa chenga.

“Ding!”Lift iligonga kengere kuashilia inafunguka eneo la Ground Floor na Edna aliangalia mbele baada ya mlango kuachiana , lakini alijikuta akishangaa baada ya kumuona mwanaume aliekuwa mbele yake.

“Edna… how Unfortunates!”Ilikuwa ni sauti ya mwanaume , nzito iliosikika mbele ya Edna.
 
SEHEMU YA 226

“Kwa majina yangu halisi niliozaliwa nayo na nilio acha kuyatumia kwa miaka mingi ni haya”Aliongea mwanamke aliekuwa mbele ya Roma na kisha kuvuta pumzi ,hata kwa upande wa Nadia alionekana kushangaa , kwani mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa akimfahamu kwa jina la Joyce lakini pia hakuweza kufahamu mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa amevaa sura bandia.

“Naitwa Mellisa Luiz Veteran Undercover Agent with RedStorm”Mwanamke huyu alijitambulisha kwa jina la Mellisa Luiz akijieleza kama alikuwa Ajenti kutoka shirika la Kijasasi la Dhoruba Nyekundu

Roma alishangazwa na utambulisho huo na alijiuliza kwanini Ajenti wa zamani wa Kitengo cha Dhoruba Nyekundu akataka kuonana nae , lakini pia kuwa na mahusiano na Nadia.

“Endelea Kuongea Miss Mellisa , kwanini AJenti wa zamani wa Dhoruba Nyekundu unataka kuonana na mimi kwa siri”

“Mpaka hapa Mr Roma nadhani utakuwa umeelewa aina ya mazungumzo ambayo ninakwenda kuzungumza na wewe pamoja na Nadia hapa ,ni mazungumzo ya muhimu sana na huenda pia kuwa ya hatari , lakini hakuna haja ya kuwaza juu ya hili kwani swala hili nishalichukulia tahadhari na mazungumzo yetu yataendelea kwa namna ya siri sana”Aliongea Mellisa na kisha alichukua chupa ya Moet na kumimina kilevi kwenye Glass yake na kisha akanywa kidogo na kurudisha Glass chini.

“Nadia I am So Sorry for lying to you for many years of our relationship but I will Explain Everything now and I am sure you will learn the reason”

“Nadia unisamehe sana kwa kukudanganya kwa miaka mingi , tokea kwa kuanza kwa uhusiano wetu lakini nitaelezea kila kitu sasa na utakwenda kujifunza sababu”Aliongea mwanamke huyu na kumfanya Nadia kuanza kutokwa na machozi.

“Mr Roma nina simulizi ndefu sana ya Maisha yangu , ambayo inanifanya kutoweza kutumia jina langu kwa Zaidi ya miaka therathini sasa , lakini kwakuwa nimeomba kuonana na wewe ukiwa katikati ya ratiba zingine nitafupisha stori yangu ili Kwenda moja kwa moja kwenye pointi ya msingi ilionifanya leo hii tukutane”

“Litakuwa jambo zuri Mellisa Luiz, sitaki kumfanya mke wangu kuwa na wasiwasi”Aliongea Roma.

“Mr Roma ushawahi kusikia popote katika harakati zako kuhusu Project Pro Human?”Aliuliza Mellisa na kumfanya Roma akili yake ifikirie na alijikuta akikumbuka ashawahi kusikia kuhusu Project Pro Human kutoka kwa Sauroni.

“Nishawahi kusikia juu ya hilo , lakini ni mara moja pekee na sijui chochote kuhusu hio Projekti”Aliongea Roma na kumfanya Mellisa kutabasamu.

“Unaweza kunieleza kwa uchache juu ya kile unachokifahamu juu ya Projekti hio?”

“Kwanini napaswa kukuelezea?”

“Kwasababu stori yote ya Maisha yangu inahusiana na Projekti hio , unavyoniona leo hii kwa kutumia sura yangu hii ya bandia na jina la bandia lakini pia kuishi kwa kujificha miaka mingi ni kutokana na Projekti Pro Human”

“How far do you know about me?”Aliuliza Roma na Mellisa alitabasamu.

“You are Hades , Pluto , Agent 13 , King From Island`s of Dead , First Human to reach Master Level of Hongmeng Scripture Power, Founder of Mercenary Group , The Eagles…. that is less I know about you”

“Hades , Pluto , Ajenti 13 , Mfalme kutoka visiwa vya wafu , binadamu wa kwanza kufikia ngazi ya juu ya nguvu za kimaandiko kutoka Hongmeng….mmiliki wa kundi la Marcenary la The Eagles , hivyo ni kwa uchache ninayofahamu kuhusu wewe”Aliongea Mellisa na kumfanya Roma kutabasamu.

“Unaonekana kujua mambo mengi kuhusu mimi , sio mbaya unaonekana ulikuwa Afisa mzuri ndani ya Dhoruba Nyekundu”Aliongea Roma na kumfanya Mellisa kutabasamu.

“Your Majest Pluto , I appreciate for yor Aknowledgement”Aliongea Mellisa na kisha alisimama na kutoa heshima mbele ya Roma na kumfanya Nadia kushangaa kwa kila neno ambalo amelisikia.

“Nadhani twende moja kwa moja kwenye mazungumzo , sitaki kutumia muda mwingi ndani ya hiki chumba, Projekti Pro Human nimeisikia kutoka kwa kiongozi wa Kundi la The Eagles na kwa maelezo ya taarifa hio ni kwamba mtu anaefahamika kwa jina la Carlos ndio aliekuwa akizungumzia juu ya Project Pro Human”Aliongea Roma na kumfanya mwanamama huyu kutabasamu.

“I know Carlos, Your Majest Pluto. He was CIA Agent who terminated Project Pro Human, I Was Manager”

“Namfahamu Carlos mfalme Pluto , alikuwa ni afisa wa CIA ambaye aliizimisha Projekti Pro Human , mimi nilikuwa meneja”Aliongea Mallisa na kumfanya Roma aanze kuvutiwa na maongezi ila kwa upandee wa Nadia alizidi kushangaa.

“Unachotaka kusema ni nini Mellisa?”Aliuliza Roma na kumfanya Mellisa Luiz kuvuta kumbukumbu.

Dhoruba Nyekundu ni shirika la kijasusi la Pamoja , nikimaanisha kwamba ni shirika ambalo limeundwa kwa umoja wa mashirika makubwa ya kijasusi duniani ya nchi ishirini zenye nguvu kasoro Urusi pekee , shirika hili lipo chini ya taasisi ya siri ya Zeros Organisation ,kama ilivyo kwa Zeros kuwa taasisi ya siri sana duniani ndivyo ilvyo kwa Shirika hili la Dhoruba nyekundu kuwa la siri vilevile , japo sio kwa vyombo vingi vya usalama kufahamu kwa undani kuhusu shirika hili lakini jina hili haliwezi kuwa geni kwenye masikio ya wengi , kuna madhumuni mengi ambayo yameundwa kwa ajili ya shirika hili ambayo hayakuwa yakifahamika kwa uwazi, kutokana na namna ya uendeshaji.

Sasa kwa maelezo ya Mellisa nikwamba yeye ni moja ya majasusi ambao walikuwa chini ya shirika la Dhoruba na kabla ya Mellisa kujiunga na Shirika hili alikuwa akifanya kazi chini ya kundi la kijasusi la CIA kwa miaka mingi akiwa ni Undercover Ajent.

Kilichomfanya Mellisa kujiunga na kundi la Dhoruba chini ya Zeros ni kwa ajili ya kusimamia Projekti Pro Human na ombi la kusimamia projekti hio lilitoka moja kwa moja kutoka kwa raisi wa 42 wa Marekani, Projecti ambayo ilikuwa ikifanyikia ndani ya msitu wa Amazoni kwa upande wa Nchi ya Bolivia.

Mellisa anaendelea kumuelezea Roma namna ambavyo Project hio ilivyoanza na mpaka mwisho wake, yaani mpaka siku Carlos alivyolipua kambi ambayo ilikuwa ikifanyikia Project hio.

Anaendelea kusema kwamba licha ya kwamba alikuwa akisimamia Projekti hio , lakini hakuwa na maelezo ya kile ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya maabara na hio ni kutokana na kwamba wanasayansi waliokuwa wakifanya kazi hio hawakuwa tayari kuongea chochote mpaka miezi kadhaa mbele alipoweza kujua kile ambacho kilikuwa kikiendelea.

“Ilikuwa inahusu nini hio Project?”Aliuliza Roma.

“kwa maelezo nilioyapata Project hio ilikuwa ikihusisha Watoto wadogo kundungwa na sindano za virusi”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Virusi vya aina gani?”

“Sina uelewa mkubwa juu ya virusi hivyo , lakini ninachojua ni kwmaba ni virusi ambavyo vilikuwa vimepewa jina la Al na mtu aliehusika katika kutengeneza vitrusi hhivyo ni mwanasayansi mmoja anaefahamika kwa jina la Banosi”Aliongea.

“Ni maelezo gani mengine ambayo unayafahamu kuhusu aina ya virusi hivyo?”

“Taarifa nyingine juu ya virusi hivyo sina , ila ninachojua kuhusu Project Pro Human ilifanikiwa kwa asilimia nane nukta tatu”

“Unamaanisha nini?”

“Katika Watoto kumi na mbili waliodungwa sindano ya Virusi ni mmoja pekee ambaye aliweza kuhimili , hivyo kukamilisha asilimia nane ya mafanikio hayo na sijui nini kilichotokea baada ya kulipuka kwa kambi ila naamini Watoto wote kumi na moja walifariki dunia kasoro mtoto mmoja pekee”Aliongea Mellisa na kumfanya Roma kukuna kichwa.

“Kabla hatujaendelea na kilichotokea , nataka kwanza unielezee ni kwa namna gani uliweza kupona kwenye mlipuko, kwa jinsi ulivyoelezea siamini kabisa mtu wa kawaida unaweza ukaepuka mlipuko kwa sekunde ambazo umepewa kujiokoa, labda kama ulikuwa na nguvu za ziada”Aliongea Roma na kumfanya Mellisa kutabasamu.

“Ni kweli nisingeweza kupona kwa uwezo wangu wa kibinadamu”Aliongea na kisha akasimama na kufungua mkanda wa taulo ambalo kalivaa na kisha akaliachia likadondoka chini na akabakia uchi kitendo ambacho kilimfanya hata Nadia kushindwa kuelewa anataka kufanya nini.
 
SEHEMU YA 227.

Mellisa baada ya kuwa uchi aliweka mguu wake kwenye Sofa kwa kujipanua na kisha alimpa ishara ya Roma kuangalia na Roma alijikuta akishangaa baada ya kuona Tatoo ambayo alikuwa akiifahamu.

“Umeipataje hii kwenye mwili wako?”Aliuliza Roma kwa mshangao na hata Nadia ambaye alikuwa akiwaza ni jambo gani ambalo Mellisa anataka kufanya sekunde kadhaa nyuma alishangazwa na aina hio ya Tatoo kwani hakuwahi kuiona popote na ilionekana sio ya kawaida..

Mellisa alitabasamu na kisha alivaa upya taulo lake na kuketi chini na kumwangalia Roma.

“Nikitaka kujibu swali lako la kwanza , nitakujibu kwamba kutokana na aina ya mlipuko wa mabomu ambayo yalikuwa yametegwa ndani ya kambi ya Projekti Pro Human ilikuwa ngumu sana kwa mimi kuokoka ule mlipuko hivyo mtu ambaye aliniokoa aliniachia hii alama ya tatoo , lakini kwa mshangao wako mfalme Pluto naamini umeifahamu”Aliongea Mellisa na kumfanya Roma kumeza mate.

“Raia wote wa Visiwa vya wafu wana hio alama katika miili yao ni utambulisho kama ilivyokuwa kwa kitambulisho cha taifa, imenishangaza kuiona kwenye mwili wako”Aliongea Roma na kumfanya Mellisa kutabasamu.

“Kwahio inamaanisha na mimi ni moja ya raia wa Visiwa vya wafu na wewe ndio mfalme wangu?”

“Hilo siwezi kusema kwa uhakika , ila nahitaji unielezee tukio lilivyokuwa”

“Sijui namna ya kukuelezea nilivyoweza kupata hii alama , lakini baada ya mlipuko huu kunipata nilijikuta nikiwa nchini Brunei ndani ya jumba la kifahari na mpaka leo hii sitambui nilivyofika na nimeishi ndani ya jumba hilo kwa miaka mingi”Aliongea Mellisa na kumfanya Roma kushangaa Zaidi.

Brunei ni nchi ambayo ipo ndani bara la Asia , ni nchi ambayo inapakana na Malaysia na kusini mwa bahari ya China , ni moja ya nchi ya kiislamu ambayo inasifika kwa utajili mkubwa lakini pia kwa amani.

“Kwahio baada ya kujikuta ndani ya Brunei nini kilifuatia?”

“Niliishi kwa kumfikiria mtu ambae ameniokoa kwenye mlipuko kwa namna ambayo sio ya kuelezeka , lakini pia niliishi kwa kisasi moyoni kulipiza kwa kile ambacho Serikali yangu ilidhamiria kunifanyia”

“Unaamini Serikali yako ilitaka kifo chako?”Aliuliza Roma.

“Kila kitu kipo wazi , Serikali ilinitaka nijiunge na Dhoruba nyekundu na wakanipatia kazi ya kuongoza Project Pro Human , lakini baadaya mafanikio wakalipua kambi pasipo kujali uhai wangu , hii inamaanisha kwamba hawakunihitaji na serikali ilikuwa ipo kwa ajili ya kunitumia tu kukamilisha mipango yake”

“Kwanini unaamini ni serikali , je kama maamuzi hayo yalifanywa na mtu mmoja peke yake?”

“Siamini juu ya hilo na ni lazima nilipize kisasi”Roma alitabasamu , aliona Mellisa anachekesha , mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa na umri mkubwa lakini pia adui yake alikuwa ni taifa kubwa kama Marekani , ilikuwa ni ndoto ya mchana kwa mtu kufikiria kulipiza kisasi juu ya taifa kama Marekani lenye kila aina ya Rasilimali.

“Kwanini umeamua kuniambia juu ya haya yote?”

“Mfalme Pluto nimeishi kwa kujificha miaka mingi ndanii ya taifa la Brunei, lakini kujificha kwangu haikunizuia kutoendelea na mpango wangu wa kulipiza kisasi,alama iliokuwa kwenye mwili wangu lilikuwa dhumuni langu la kwanza kuipatia maana yake na nilitumia elimu yangu niliokuwa nayo ya kijasusi kufanya uchunguzi mpaka kuja kugundua kuwa Alama hii inahusiana na wewe mfalme Hades, hivyo kukutafuta leo hii ni kutaka kujua ni nani ambaye amehusika na kuniokoa kule msituni hilo ni la kwanza na kwakua unaijua hii alama basi hutoshindwa kufahamu mtu ambaye ameniokoa , swala la pili nataka kumpata Carlos . nahitaji kujua kila kitu kilichoendelea , najua Carlos kakimbilia visiwa vya wafu na namhitaji nianze nae katika kisasi changu”Aliongea kwa hasira Mellisa na kumfanya Roma atabasamu.

“Mellisa nishakuambia tayari kwamba alama hio ni kama sehemu ya utambulisho wa uraia ndani ya visiwa vya wafu , kuhusu namna ulivyoipata alama hio sijui kama vile wewe usivyojua, kuhusu kisasi chako pia nadhanini swala ambalo halinihusu kabisa”Aliongea Roma huku akisimama.

“Mr Roma .. Mfalme sijamaliza bado..”

“Mellisa umeniambia kwamba shida yako kubwa ilikuwani kutambua hio alama inamaana gani katika mwili wako na ndio maana ukaamua kunieleza historia yako , hitajio lako nishalikamilisha ,mimi na wewe hakuna deni”

“Mfalme Pluto nipo tayari kwa ajili ya kubadilishana taarifa na wewe”Aliongea Mellisa huku akiwa amesimama na kumfanya Roma kutabasamu kwa namna ya kukereka.

“Mellisa sidhani kama unataarifa ambayo inaweza kunifanya kubaki hapa na kuendelea kukusikiliza na kujibu maswali yako, ninakutakia mafanikio mema juu ya kisasi chako zidi ya Serikali ya Marekani”Aliongea Roma na kuendelea kupiga hatua kuufuatia mlango.

“Mfalme Pluto nadhani umekutana na Mwanamke aliejitambulisha kwako kwa jina la Zoe Kovac”Aliongea na kumfanya Roma kusimama na kumwangalia.

“Kwahio unataka kusema kwamba wewe na Zoe Kovac mnamahusiano ya karibu na wote mnataka kulipiza kisasi zidi ya serikali ya Marekani? ,maana hata mwenzako anahisi kaka yake yupo hai , lakini naamini baada ya kugundua kama ni mfu ataungana na wewe kwenye mapambano , Melissa naonba nikutahadharishe sina mpango wowote wa kushirikiana na wewe kwenye visasi vyako vya kipuuzi”Aliongea Roma na kuufungua mlango.

“Wait.. Mfalme kuna mwanamke ambaye Zoe Kovac alikuwa akimzungumzia anafahamika kwa jina la Seventee..” Kabla hajamaliza Mellisa alijikuta akining`inia hewani akiwa amekwabwa shingoni na Roma na haikuelewa amefikiwaje , lakini alijihisi kifo kinamkaribia , aliishia kupiga piga mikono ya Roma kwa ajili ya kujitetea.

“Roma muachie Madam… utamuua tafadhari”Aliongea Nadia kwa woga mno huku akimshika Roma shati akibembeleza , lakini Roma alionekana kama hajamsikia kwani alizidi kumkaba Mellisa kiasi kwamba alianza kutoa ulimi nje.

“Roma…..naomba usimuue , Madam ni kama mama kwangu naomba uniadhibu mimi”Aliongea Nadia huku akiwa amepiga magotr na Roma alimtupia Mellisa kwenye sofa huku akihema kwa kasi. Mellisa aliishia kukohoa mfululizo huku akivuta hewa kama mbwa.

Na Roma hakusubiri tena , kwani alipiga hatua kutoka ndani ya chumba hiko huku akifunga mlango kwa kasi.

Roma baada ya kuingia kwenye Lift alijituliza hasira mpaka pale Lift ilipofunguka na alitoka moja kwa moja kuelekea sehemu ambayo alikuwa amewaacha wafanyakazi wenzake , Pamoja na mke wake.

Roma baada ya kuingia ndani ya ukumbi alikuta hakuna mtu Zaidi ya wahudumu wa hoteli ambao walikuwa wakisafisha na aliamini washaondoka na alijikuta akishika kiuno na kuvuta pumzi alijilaumu kwa kupoteza muda mwingi na mwanamke mpuuzi anaeitwa Mellisa.

“Kwa staili hii Edna ataninunia wiki nzima”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake huku akianza kupiga hatua kuelekea upande wa Lift.

Upande wa nje eneo la Maegesho ya Gari alionekana Edna akiwa amesimama kwa kuegamia gari ya Roma, mbele yake alionekana mwanaume ambaye amevalia suti ya rangi nyeusi , mrefu maji ya kunde ambaye alikuwa na nyweele ndefu mno ila zilizochanwa vizuri.

“Edna mpenzi , hivi unajua ni kwa kiasi gani chuoni nilikuwa nikilitafuta penzi lako, huwezi kunikatili kwa kuniambia tayari umeolewa najua nimechelewa kurudi kwenye Maisha yako kutokana na kuwa na mambo mengi ila ujio huu hapa Tanzania ni kwa ajili yako”Aliongea yule mwanaume huku akimwinamia Edna kwa kutaka kumbusu mdomoni.

“Paah…!!!” Kilikuwa ni kibao kutoka kwa Edna Kwenda kwa mwanaume ambaye tulimfahamu kwa jina la Desmond.

“Naomba ujiheshimu Desmond…”Aliongea Edna huku macho yake yakianza kubadlika na kuwa mekundu.

“Edna..”Aliongea huku akimsogelea tena , ukweli haikueleweka hayo mazungumzo yalianzaje mpaka kufikia hapo maana Desmond mwanamme ambaye hajulikanni ametokea wapi alionekana kumbembeleza mrembo Edna na walionekana kuwa na historia.

“Puuh!!!”

Ni kishindo cha mtu kudondokea gari na Edna alipangalia vizuri alimuona Desmond akiwa ndio aliedondoka mita kadhaa kutoka aliposimama yeye huku damu puani zikimtoka kwa fujo.

“Roma..muachee!!!”Aliongea Edna huku akikimbia na kumzuia Roma kwa mbele huku akipanua mikono.. haikueleweka Roma alifika muda gani ila macho yake hayakuonyesha namna yoyote ya Desmond kuchoropoka akiwa hai.
 
SEHEMU YA 228

DAKIKA CHACHE NYUMA

“Desmond umefika lini Tanzania?”Aliongea Edna baada ya kumsogelea Desmond na hata Desmond alighairisha kuingia kwenye Lift na Desmond alijikuta akitabasamu.

“Edna ndio kwanza naingia Tanzania lakini sikudhani mtu wa kwanza kukutana hapa nchini ni wewe”Aliongea Desmond kwa uchangamfu.

“Ndio unafika ?”

“Yeah masaa mawili yaliopita , nimefikia kwenye hoteli hii”Aliongea Desmond huku akimwambia Edna wakaketi kwenye eneo la mgahawa kwa ajili ya kuongea na Edna licha ya kwamba alikuwa eneo hilo kwa ajili ya kumtafuta Roma , ila aliona sio mbaya kuongea na Desmond rafiki yake wa kitambo.

Desmond na Edna walikutama miaka kumi nyuma kwa mara ya kwanza na walikutana kwenye ndege nchini Kenya wakati Edna akielekea Masomoni kwa mara ya kwanza ngazi ya shahada nchini Uingereza.

Wakati Desmond na Edna wanakutana kwa mara ya kwanza Desmond kwa upande wake alikuwa akirudi Uingereza kuendelea na masomo yake ya ‘Masters’kozi ya political Science baada ya likizo kumalizika.

Na kutokana na kwamba wawili hawa walikuwa wamekaa siti za Pamoja , lakini pia kuelekea wote Uingereza kwa ajili ya masomo , ilikuwa rahisi kwao kuongea na jambo hili lilikuwa rahisi sana kwa Desmond kutokana na kwamba ndio kwanza Edna anakwenda kuanza masomo yake.

Upande wa Edna alifurahi kukutana na Desmond kutokana na kwamba angekuwa mwenyeji wake kwenye safari na upande wa Desmond yeye alitokea kuvutiwa na uzuri wa Edna na kwake aliona ni bahati kubwa kukutana na Edna.

Desmond yeye alikuwa akitokea nchini Rwanda na ni mtoto wa kwanza wa Raisi Paul Jeremy Pamoja na mke wake Kizwe.

Desmond ndio aliemsindikiza Edna na kufanya taratibu zote za usaili mpaka akamaliza Pamoja na kushirikiana na mama yake Goodman yaani Nahita, mwanzo wa Edna kufahamiana na Desmond ndio mwanzo wa urafiki wao wa muda mrefu , Desmond yeye alikuwa akisoma chuo cha Manchester na Edna alikuwa akisoma chuo cha Oxford , lakini hio haikuwazuia wawili hao kutotembeleana.

Edna kwa mara yake ya kwanza tokea kuzaliwa alijikuta akimpenda Desmond kisirisiri(Secret Admirer) na hio haikuwa kwa Edna tu hata kwa Desmond alitokea kumpenda Edna lakini changamoto ya wakati huo ni kwamba Desmond alikuwa na mpenzi tayari ndani ya chuo cha Manchester na hata Edna alikuwa akimfahamu , hivyo kila mmoja alikuwa akimpenda mwenzake kisirisiri , hivyo kwa maneno marahisi ‘First Crush’ wa Edna ni Desmond mtoto wa raisi wa Rwanda.

Kutokana na utofauti wa kimasomo , Desmond ndio aliekuwa wa kwanza kumaliza masomo yake na kujiunga na Shirika la UN maswala ya wakimbizi kwa kujitolea huko nchini Sudan na kwanzia hapo ndio mara yao ya mwisho ya Edna na Desmond kuonana.

Sasa licha ya Edna kutomtamkia Desmond kwamba anampenda, lakini Desmond alikuwa akilifahamu hilo na hata Edna alikuwa akijua Desmond anafahamu hisia zake na hii ni kutokana na rafiki wa Edna wa kike aliefahamika kwa jina la Zainabu aliekuwa akisoma nae Chuoni kumwambia Desmond siri ya Edna na jambo hili lilimuuzi sana Edna baada ya kugundua Zainabu katoboa siri yake na kuanzia siku hio Edna aliishi kwa kumkwepa Desmond huku akisingizia ubize wa masomo.

Hivyo tokea Desmond anamaliza masomo yake alikuwa akijua anapendwa na Edna na kwake ilikuwa ni kama bahati kwani hakudhania kama anaweza kupendwa na mwanamke mrembo kama Edna.

……..

Desmond alikuwa akimkagua Edna kwanzia chini mpaka juu na kumfanya Edna aone aibu hakuzoea kuangaliwa na mwanaume kwa muda mrefu.

“Mbona unaniangalia sana Desmond nimebadilika?”

“Sana Edna , umebadilika mno sio kama tulivyoachana mara ya mwisho”Edna alishangaa.

“Nimekuwaje?”

“Umezidi kuwa mrembo Edna na unaonekana kuwa more matured”Aliongea Desmond na Edna alitabasamu.

“Umekuja kufanya nini hapa Dar?”Aliuliza Edna na kumfanya Desmond kutabasamu.

“Nimekuja kwa ajili yako Edna”Aliongea Desmond na kumfanya Edna kushangaa hakumuelewa Desmond kwanini aseme amekuja Tanzania kwa ajili yake.

“Unamaanisha nini kuja kwa ajili yangu?”

“Edna najua hatujaonana muda mrefu sasa, na ni Zaidi ya miaka kumi tokea tuonane but Trust me tokea niachane na Elizabeth nimekuwa wa kukufikiria kila siku , and I was shocked and happy baada ya kupata taarifa ya wewe kupewa cheo cha CEO ndani ya kampuni ya Vexto ,So Edna to answer your Question, yes nipo hapa Tanzania kwa ajili yako , nataka tuendeleze tulipoishia..”Aliongea Desmond na aliona hana muda wa kuremba kuweka madhumuni yake wazi moja kwa moj.

“Desmond wait… unamaanisha nini kusema unataka tuendelee tulipoishia?”Aliuliza Edna huku moyo wake ukidunda kwa kasi.

“Edna nadhani ushanielewa tayari , I know I was foolish back then baada ya kupewa taarifa na Zainabu juu ya hisia zako juu yangu…”

“Stop.!, Desmond usiendelee kuongea”

“Why ! Edna I am ..”

“Desmond I am Married now , I did not got a chance to refute what she told you back then, but its true sikuwa na hisia na wewe kama unavyojiaminisha hivyo naomba uache kuongelea mambo yaliopita na kama huna jambo lingine la kuongea naondoka”Aliongea Edna huku akionyesha kukasirika.

Kwa upande wa Desmond alijikuta akipigwa na kitu Kizito kichwani , ni kama hakuwa amemuelewa Edna vizuri juu ya maneno yake hasa kwenye neno ‘Married’ na alikuwa kwenye mshangao kiasi kwamba hata Edna alivyoanza kupiga hatua kuondoka ndani ya hilo Eneo hakuona na ile akili zake zinarudi kawaida alishangaa kutokumuona Edna.

“Noo.. Edna noo.., how sijasikia kama umeolewa , unatania kama ilivyokuwa miaka ile, Wewe ni CEO mkubwa na ningefahamu kama tayari ushaolewa”Aliongea Desmond peke yake huku akionyesha hali ya kuchanganyikiwa.

Ni kweli Desmond hakuwa akifahamu chochote juu ya Edna kuolewa na hii ni kutokana na kwamba Edna hajawahi kuweka wazi swala hilo na hata kwenye mtandao wa Wikipedia. ‘Profile’ ya Edna ilikuwa ikionyesha yupo Single bado.

Desmond aliachana na mpenzi wake Elizabeth Thambo miaka miwili baada ya kuanza kazi yake ndani ya shirika la kimataifa la UN upande wa wakimbizi, na tokea aachane na Elizabethi alijiingiza kwenye mahusiano tofauti tofauti na wanawake wengi warembo na alifanikiwa juu ya hilo kutokana na kwamba alikuwa na hela , kwani baba yake alikuwa ni raisi, na mama yake Kizwe licha ya kuwa First Lady lakini alikuwa mfanyabiashara mkubwa ndani ya Taifa la Rwanda na nje ya mipaka yake , hivyo jina kubwa alikuwa nalo lakini pia pesa alizokuwa nazo, na moja ya wanawake ambao alitoka nao kimapenzi ni msanii wa kike maarufu kutoka Nigeria afahamikae kwa jina la Misu, licha ya kwamba uhusiano wao ulikuwa wa chini chini , lakini vyombo vya kishilawadu nchini Nigeria vishawahi kuripoti mara moja moja juu ya uhusiano huo lakini Misu alikanusha madai hayo.

Sasa baada ya miaka mingi ya Desmond kufanya kazi kwenye mashirika makubwa duniani , baba yake Paul Jeremy alimtaka arudi nyumbani ili ajiingize kwenye maswala ya kisiasa kwa ajili ya kumuandaa kama mrithi wake na hio yote ni kutokana na Jeremy kumpenda sana Desmond kutokana na uwezo wake wa akili.

Sasa Desmond tokea aliporudi nchini Rwanda mama yake na baba yake walikuwa wakimkalia vikao vya kumtaka aoe kwani umri ulikuwa ukienda, lakini pia haikuwa picha nzuri kwa kuwa na cheo kikubwa serikalini pasipo ya kuwa na mke.

Desmond baada ya kuona kelele zimekuwa nyingi ndio akaanza kufikiria mwanamke ambaye anaweza kumuoa na alianza kufikiria wanawake wake wote aliotoka nao kimapenzi na alianza na Elizabethi mtoto wa Tajiri mmoja kutoka Afrika kusini na kumfikiria kwake kulimfanya kuanza kumfatilia mwanamke huyo mrembo , lakini alijikuta akipatwa na ganzi baada ya kugundua kuwa Elizaethi ashafunga ndoa na Dj mmoja maarufu nchini mwao hivyo alimkatia tamaa na kuanza kufikiria warembo wengine ambao ashawahi kutembea nao , lakini kila mwanamke ambaye alikuwa akimfikiria na kumpembua aliona hakuwa na vigezo vya kuwa nae kwenye mahusiano ya ndoa na katika kufikiria sana pasipo kupata jibu ndipo akili yake iliporudi miaka kumi nyuma chuoni, na jina la Edna Adebayo liliibuka kwenye kichwa chake na hapo hapo alichukua simu yake na kuanza kutafuta jina la Edna mtandaoni na mtandao wa ‘Google’ ulimletea mapendekezo(Keywords) mengi baada tu ya kuandika jina la Edna kwenye ‘Searching Engine tap Bar’.

“What age Edna get Rich?, Is Edna Self made Billionare ,Why Edna is So Famous? , Who is in Love with Billionare Edna, Is it true Edna is no 1 Beutifull Woman in World , Does Edna have Instagram Account?, What are 3 interesting facts about Edna Adebayo?”

“Damn It She is so Famous”Aliwaza Desmond baada ya kuona maswali mengi yanayomuhusu Edna yaliokuwa yakiulizwa mtandaoni na Desmond alipitia kila swali ili kujua taarifa nyingi ambazo zilikuwa zikimuhusu Edna na kila taarifa aliokuwa akiisoma alijjikuta penzi likichipuka , maana hakuna neno baya ambalo limezungumzwa juu ya Edna Zaidi ya Sifa zilizotukuka ambazo zilikuwa zipo kwenye mitandao , lakini jambo ambalo lilimfurahisha Zaidi ni baada ya kugundua Edna bado hajafunga ndoa kwa maana ya kwamba ni Single.

“Maskini ukute alikuwa akinisubiria muda wote … Desmond wewe ni mjinga kwanini unaacha mrembo kama huyu anateseka juu yako … Edna mrebo wangu nisamehe mimi kwa kuchelewa kujua penzi lako juu yangu … Shujaa ,mwokozi majaliwa nipo njiani kwa ajili ya kukuokoa kwenye dimbwi la mateso”Hayo ni maneno ya kipuuzi machache ambayo Desmond alikuwa akiyafikiria kwenye kichwa chake , aliamini Edna hakuwa na mume kwasababu alikuwa akimsubiria yeye.

Sasa jambo hilo lilimfurahisha mno Desmond kwanza alijiambia litakuwa jambo zuri kama atamuoa Edna , kwasababu mrembo huyo anapesa za kutosha , pili aliamini umaarufu wake utazidi kupamba moto na hata ushawishi wake utaongezeka maradufu.

Na Desmond hakutaka kuchelewesha jambo hilo alipanga safari ya kuja Tanzania haraka sana kwa ajili ya kuonana na Edna na siku hii , usiku ndio ana bahatika kuonana na Edna ndani ya hoteli ya Kilimajaro.

Hivyo hata maneno ya kumwambia Edna juu ya kama alifurahishwa na namna alivyopata u’CEO ndani ya Vexto , zilikuwa swaga tu za kumuingia mrembo Edna , ila ukweli ni kwamba hakuwahi kumfatilia kabisa Edna mpaka aliporudi Rwanda.
 
SEHEMU YA 229

Edna baada ya kurudi kwenye Lift , hata lile wazo alilokuwa nalo mwanzo la kumtafuta Roma lilikuwa limepotea , mrembo huyu alikuwa akijionea aibu na kuwa na hasira kwa wakati mmoja , ni kweli kabisa alikuwa na hisia na Desmond kipindi alipokuwa akianza chuo lakini jambo hilo hakutaka kabisa limfikie Desmond , lakini Zainabu Mdomo Mpana, ndio akaharibu kila kitu na Kwenda kutoboa siri yake kwa Desmond na kwanzia kipindi hiko Edna aliishia kumpiga chenga Desmond mpaka pale ambapo alimaliza chuo na hakupata hata nafasi ya kukanusha maneno ya Zainabu.

Na hata urafiki kati ya Zainabu na Edna ulikufa kutokana tu na jambo hilo , hivyo Edna sio kama alikuwa bize kwenye Maisha yake yote , alikuwa pia ni binadamu mwanamke, hivyo hisia za mapenzi mara moja moja zilimtawala , lakini hisia zake zilipotea baada ya kupata taarifa za kifo cha mama yake na tokea Edna aliporithi kampuni hakuwahi kufikiria tena kuhusu mwanaume yoyote mpaka siku anakutana na Mfalme Pluto.

Mwanaume ambaye mpaka muda huo hakujua yuko upande gani na mrembo Nadia.

“Roma mpuuzi wewe , Shetani wewe , Nguruwe mkubwa wewe , Bata mzinga Mchafu , nimekuja na wewe kwa ajili ya kukulinda usiongeze mchepuko lakini ushanipiga chenga na kuondoka na kimada Nadia , Pumbavu kabisa”Edna alikuwa akimsuta na kumtukana Roma kimoyo moyo wakati akiwa ndani ya Lift , huku akipotezea swala zima la Desmond.

Edna baada ya kurudi ndani ya chumba alichowaacha wenzake , aliona Roma bado hakurudi na kuzidi kukasirika moyoni , licha ya kwamba alikuwa akionekana kawaida , lakini alikuwa akiugua na hata ile mudi ya kubakia hapo ndani ilikata kabisa na alikaa kwa dakika kumi na tano tu alichukua mkoba wake na kutoka, wafanyakazi wenzake baada ya kuona bosi wao anaondoka na wao walianza kutawanyika kwani walikuw washakula na kushiba , lakini hata hivyo walishangaa kupotea kwa Roma , lakini hawakuuliza wala kutaka kutafuta majibu mengi ,Dorisi na Nasra ndio ambao walikuwa wakijua kinachoendelea na pia walikuwa wakihisi wivu kweenye mioyo yao , kwani walimuona Roma akiondoka na Nadia.

Upande wa Desmond licha ya Edna kumwambia kuwa ameolewa hakutaka kabisa kukubaliana na hilo , aliona Edna ana mtania na ni mbinu tu za nataka sitaki za wanawake wengi , hivyo alijiapia haondoki Tanzania pasipo kuhakikisha Edna akuwa mpenzi wake na hakujisumbua kuendelea kumfuatilia , bali alienda mpaka juu kwenye chumba chake na kujimiminia wine pasipo kuvua suti yake na kisha alisogelea dirisha ndani ya chumba hiko cha kifahari cha Super Deluxe na kuangalia nje.

Dirisha la chumba alichokuwepo, limeangaliana na baharini , lakini pia alikuwa akipata kuweza kuona eneo la Maegesho , licha ya kwamba kulikuwa na giza , lakini hakushindwa kumuona Edna aliesimama kwa kuegamia gari akionekana kumsubiria mtu, na palepale aliweka glasi chini na kufungua chumba chake haraka haraka na kutoka nje.

…………………….

“Roma huruhusiwi kupita na kumdhuru”Aliongea Edna kwa amri.

“Yaani mtu alikuwa akikulazimisha kukubusu halafu nimuache , anatoa wapi ujasiri wa kusogelea mke wa mtu”Aliongea Roma kwa hasira na Desmond aliweza kuelewa sasa mwanaume aliemtupa kama furushi na kujigonga kwenye gari alikuwa ndio mume wa Edna , moyo wake ulipiga kwa nguvu na hata maumivu yalianza kumpotea.

Aliinua macho yake na kumwangalia Roma na kuona mwanaume aliekuwa mbele yake hana vigezo vyovyote vya kuwa mume kwa mwanamke mrembo kama Edna na ujasiri ulimvaa na alisimama na kujifuta futa suti yake.

“Desmond ondoka?”Aliongea Edna kwa ukali , huku baadhi ya watalii waliokuwa ndani ya hoteli hii wakishangazwa na kile kinachoendelea , lakini baada ya kuona anaegombaniwa ni mwanamke mrembo kama Edna hawakushangaa Zaidi ya kusifia namna Edna anavyotatua tatizo la wanaume wawili wanaomtaka na walikuwa na hitimisho kwenye vichwa vyao kwamba Edna kagonganisha wanaume.,

Desmond kwa jinsi alivyomuona Edna alivyo na wasiwasi , lakini pia kwa namna ambavyo aliweza kuvutwa kwa nguvu kitendo ambacho hakujua kimefanyikaje , aliona hakuna usalama wa kuendelea kubakia hapo na alimwangalia Roma kwa macho ya hasira na kisha aliondoka kuelekea ndani. Na Edna alijikuta akivuta pumzi ya ahueni.

“Kwanini unamlinda mwanaume ambaye alikuwa akitaka kukudhalilisha?”Aliuliza Roma huku akimwangalia na Edna alimwangalia Roma kwa macho makali huku akili yake ikitengeneza picha za Nadia na Roma kufanya matendo ya kishenzi, na Edna hakuongea neno lolote Zaidi yakuchukua mkoba wake ulidondoka chini na kutembea kuelekea getini.

“Edna subiri….”Licha ya Roma kuita lakini Edna hakusikiliza Zaidi ya kukimbia kabisa na ile anatoka nje ni kama taksi ilikuwa ikimsubiria kwani ilisimama kwenye miguu yake na aliingia ndani na ikaondolwa na kumuacha Roma ashindwa kujua cha kufanya.

Upande Desmond alitembea mpaka kwenye Litf na kuingia ndani , huku baadhi ya wahudumu na wageni wakimshangaa kwa hali aliokuwa nayo , kwani alikuwa akivuja damu , lakini hakujali na baada ya lift kufunguka moja kwa moja alienda mpaka kwenye chumba chake na alivua koti la suti kwa hasira na kulitupa kwenye sofa.

“F***uuuck!” nitakuonyesha”Aliongea Desmond na kisha alitoa simu yake mfukoni na kupiga”

“Kesi upo kazini bado?”Aliuliza kwa Kingereza huku akijibwaga kwenye sofa.

“Ndio boss”

“Kuna taarifa juu ya mtu hapa Tanzania naitaka muda huu , nadhani kitengo chetu cha usalama kina weledi wa kufanya kazi kwa haraka sana”

“Ndio boss nitajie jina?”

“Jina sina , ila nataka umfuatilie Edna Adebayo , tafuta taarifa za mwanaume ambaye yupo nae kimahusiano , kila kitu kwanzia elimu yake , uchumi wake na kila kitu, nakupa dakika nne tu”

“Boss ,kuhusu Edna mbona taarifa yake ipo hapa Ikulu subiri nakutumia faili la mume wake sasa hivi”

“Okey fanya hivyo na hakikisha swala hili linakuwa siri , baba yangu hapaswi kufahamu”

“Sawa boss”Alikata simu na kisha akachukua chupa ya Hennessy na kumimina kilevi kwenye Glass na kugida kilevi chote kwa hasira na kuweka glass chini juu ya meza na simu yake ilitoa mlio wa ‘notification’ , na aliichukua na kuingia Watsapp na kuona faili ambalo limetuwa na Kesi IT wa kitengo cha usalama ndani ya ikulu ya baba yake.

Kadiri alivyokuwa akisoma taarifa iliokuwa ikihusiana na Roma Ramoni , uso wake ulipambwa na tabasamu la kifedhuli ambalo lilikuwa likiashiria dharau.

“Yaani mpuuzi mmoja , mbeba mizigo kutoka soko la Mbagala anishinde , haya ni matusi na nikishindwa kumdhibiti Roma sifai hata kumrithi baba , licha ya kwamba anaonekana kuwa na elimu ya Harvard ila inaonyesha haijamsaidia chochote. Roma Ramoni mimi ndio Desmond Jeremy kila kitu nimerithi kutoka kwa mama yangu sio kwa baba yangu mpole mpole , najua ninachohitaji kwenye Maisha yangu na hivvyo siwezi kushindwa hata kidogo , nitakuua na nitamchukua Edna na nitamfanya kuwa mke wangu”Aliwaza huku akisimama na kuanza kufungua vifungo vya shati na ile anamalizia kifungo cha mwisho mlango wake ulingongwa na kumfanya kukunja sura kwa hasira na kutembea mpaka mlangoni na alitumia Peephole kuchungulia nje na aliona sura ya mwanaume ambaye hamfahamu.

“Wewe ni nani?”Aliuliza kwa sauti ya kibesi.

“Naitwa Elvisi Temba , Mtoto wa Mkuu wa mkoa wa Dodoma na kiongozi mpya wa kundi la Black Mamba”

“Unataka nini kutoka kwangu?”

“Nahitaji tuongee juu ya namna ya kumuadhibu Roma Ramoni , nimeona kila kitu kilichoteka dakika chache nyuma , eneo la maegesho ya magari”Aliongea Elvisi Temba na kumfanya Desmond kufikiria kidogo na kisha akashika kitasa na kufungua mlango na kumkaribisha Elvice Temba.

Mwanaume aliekuwa mbele yake hakuwa akimfahamu lakini alimfungulia kwasababu aliamini kuna manufaa ya kufanya hivyo.

******

Upande wa Nasra baada ya kuachana na wafanyakazi wake ikiwemo bosi wake Edna , aliendesha gari yake aina ya BMW M4 huku akiwa na mawazo lukuki ,huku jambo kubwa ambalo lilikuwa likimsubua Zaidi ni juu ya mapenzi yake na Roma , licha ya kwamba mrembo huyu mchana wa siku hio alimpigia Edna magoti kwa ajili ya kumuomba msamaha kwa kutembea na mume wake , lakini moyo wake muda huo ulikuwa kwenye maumivu makali mno , hakujielewa kabisa , kwani alihisi kumpenda sana Roma na moyo wake haukuwa tayari kabisa kumuachilia.

Kwa jinsi alivyokuwa na mawazo alishindwa kabisa kuelewa namna ambavyo aliweza kufika ndani ya Apartment yake ambayo alikuwa akiishi, ndani ya eneo la Mikocheni kwa Warioba , alipaki gari kivivu na kisha akaziendea lift ambazo zilimchukua moja kwa moja mpaka juu na kuingia kwenye Apartment yake,

Na baada ya kuwasha taa alijongea kivivu na kisha kutupia mkoba wake kwenye sofa na ksiha akasogelea jokofu na kutoa chupa ya maji ya Afya na kufungua kizibio na kunywa kidogo na kisha akarejea na kuketi kwenye sofa na ile anakaa tu , simu yake kubwa ilianza kunguruma ikiashiria ilikuwa ikiita na aliichukua haraka haraka kwa kutoa kwenye mkoba na kuangalia jina la mpigaji na aliona ni Mama yake na kujikuta akishangaa kwanini anampigia muda huo kwani ilikuwa ni takribani saa tatu Kwenda saa nne usiku.

“Mom…. Kuna nini?”Aliuliza Nasra huku akitawaliwa na wasiwasi.

“Hakuna kitu Nasra , nimeota ndoto mbaya hapa ndio maana nikakupigia usiku huu kujua hali yako”Ilisikika sauti upande wa pili na kumfanya Nasra kuvuta pumzi ya ahuenni.

“Nilipatwa na wasiwasi mama , huna tabia ya kunipigia usiku wa manane , nimejisikia vizuri kama uko sawa, lakini umeota nini mama?”

“Nasra mwangangu nimeota juu ya mwanaume ambaye unampenda” Nasra alijikuta akishangaa.

“Umeota nini….”

“Nimeota umeachwa siku ya harusi yako na ukaamua kuchukua maamuzi ya kujiua kwa kujichoma kisu tumboni, nimepatwa na woga kweli juu ya ndoto hii”Ilisikika sauti ya kiutu uzima upande wa pili na kumfanya Nasra kushangaa na kukaa kimya .

“Nasra hebu niambie , kuna kinachoendelea kati yako na huyo mwanaume ambaye umesema unakuja nae kumtambulisha?”

“Mama…”

“Niambie Nasra ,, nina wasiwasi mwenzio, kama mambo hayaendi vizuri unieleze tuangalie namna ya kumtegeneza ili asikuache, mimi nimeogopa eti ,nighambia mwanangu iji fukundo jiniikae vyedi”Sauti ya mama mtu mima ilisikika huku akimalizia kwa kisambaa kabisa.

“Mama tutaongea kesho , hakuna kilichotokea , ulale salama”Aliongea Nasra na kumkatia simu mama yake na kisha kuvuta pumzi.

“Nijiue kwa ajili ya Roma?”Alijiuliza Nasra huku akianza kupima kwenye kichwa chake siku ambayo Roma kama atachukua maamuzi ya kumuacha lakini kabla hajapata jibu , kengele ya mlango wake ilisikika chumba kizima na kumfanya ainuke huku akijiuliza ni nani amekuja usiku huo , kwani haikuwa kawaida.

“Najmaa…!!!”Aliita Nasra huku akifungua mlango haraka haraka baada ya kuona mwanamke aliesimama kwa nje akiangalia Kamera inayomuonyesha kwa ndani.

ITAENDELEA JUMAPILI BAADA YA MECHI 0687151346 NICHEKI WATSAPP USIACHE AROSTO IKUTESE WAKATI TIBA IPO[emoji1787]
 
Shukran Mkuu
 
Nitakuwa anyonymous [emoji1787]
hii kitu inatupa arosto hatari kabisaa..Sema mimi sijaelewa kuhusu group ya watsap..ukilipia unanunua episode kadhaa au hiyo payment unakua unakaa kwa group kupata post ahead bila ku renew payment??
 
SEHEMU YA 228

DAKIKA CHACHE NYUMA

“Desmond umefika lini Tanzania?”Aliongea Edna baada ya kumsogelea Desmond na hata Desmond alighairisha kuingia kwenye Lift na Desmond alijikuta akitabasamu.

“Edna ndio kwanza naingia Tanzania lakini sikudhani mtu wa kwanza kukutana hapa nchini ni wewe”Aliongea Desmond kwa uchangamfu.

“Ndio unafika ?”

“Yeah masaa mawili yaliopita , nimefikia kwenye hoteli hii”Aliongea Desmond huku akimwambia Edna wakaketi kwenye eneo la mgahawa kwa ajili ya kuongea na Edna licha ya kwamba alikuwa eneo hilo kwa ajili ya kumtafuta Roma , ila aliona sio mbaya kuongea na Desmond rafiki yake wa kitambo.

Desmond na Edna walikutama miaka kumi nyuma kwa mara ya kwanza na walikutana kwenye ndege nchini Kenya wakati Edna akielekea Masomoni kwa mara ya kwanza ngazi ya shahada nchini Uingereza.

Wakati Desmond na Edna wanakutana kwa mara ya kwanza Desmond kwa upande wake alikuwa akirudi Uingereza kuendelea na masomo yake ya ‘Masters’kozi ya political Science baada ya likizo kumalizika.

Na kutokana na kwamba wawili hawa walikuwa wamekaa siti za Pamoja , lakini pia kuelekea wote Uingereza kwa ajili ya masomo , ilikuwa rahisi kwao kuongea na jambo hili lilikuwa rahisi sana kwa Desmond kutokana na kwamba ndio kwanza Edna anakwenda kuanza masomo yake.

Upande wa Edna alifurahi kukutana na Desmond kutokana na kwamba angekuwa mwenyeji wake kwenye safari na upande wa Desmond yeye alitokea kuvutiwa na uzuri wa Edna na kwake aliona ni bahati kubwa kukutana na Edna.

Desmond yeye alikuwa akitokea nchini Rwanda na ni mtoto wa kwanza wa Raisi Paul Jeremy Pamoja na mke wake Kizwe.

Desmond ndio aliemsindikiza Edna na kufanya taratibu zote za usaili mpaka akamaliza Pamoja na kushirikiana na mama yake Goodman yaani Nahita, mwanzo wa Edna kufahamiana na Desmond ndio mwanzo wa urafiki wao wa muda mrefu , Desmond yeye alikuwa akisoma chuo cha Manchester na Edna alikuwa akisoma chuo cha Oxford , lakini hio haikuwazuia wawili hao kutotembeleana.

Edna kwa mara yake ya kwanza tokea kuzaliwa alijikuta akimpenda Desmond kisirisiri(Secret Admirer) na hio haikuwa kwa Edna tu hata kwa Desmond alitokea kumpenda Edna lakini changamoto ya wakati huo ni kwamba Desmond alikuwa na mpenzi tayari ndani ya chuo cha Manchester na hata Edna alikuwa akimfahamu , hivyo kila mmoja alikuwa akimpenda mwenzake kisirisiri , hivyo kwa maneno marahisi ‘First Crush’ wa Edna ni Desmond mtoto wa raisi wa Rwanda.

Kutokana na utofauti wa kimasomo , Desmond ndio aliekuwa wa kwanza kumaliza masomo yake na kujiunga na Shirika la UN maswala ya wakimbizi kwa kujitolea huko nchini Sudan na kwanzia hapo ndio mara yao ya mwisho ya Edna na Desmond kuonana.

Sasa licha ya Edna kutomtamkia Desmond kwamba anampenda, lakini Desmond alikuwa akilifahamu hilo na hata Edna alikuwa akijua Desmond anafahamu hisia zake na hii ni kutokana na rafiki wa Edna wa kike aliefahamika kwa jina la Zainabu aliekuwa akisoma nae Chuoni kumwambia Desmond siri ya Edna na jambo hili lilimuuzi sana Edna baada ya kugundua Zainabu katoboa siri yake na kuanzia siku hio Edna aliishi kwa kumkwepa Desmond huku akisingizia ubize wa masomo.

Hivyo tokea Desmond anamaliza masomo yake alikuwa akijua anapendwa na Edna na kwake ilikuwa ni kama bahati kwani hakudhania kama anaweza kupendwa na mwanamke mrembo kama Edna.

……..

Desmond alikuwa akimkagua Edna kwanzia chini mpaka juu na kumfanya Edna aone aibu hakuzoea kuangaliwa na mwanaume kwa muda mrefu.

“Mbona unaniangalia sana Desmond nimebadilika?”

“Sana Edna , umebadilika mno sio kama tulivyoachana mara ya mwisho”Edna alishangaa.

“Nimekuwaje?”

“Umezidi kuwa mrembo Edna na unaonekana kuwa more matured”Aliongea Desmond na Edna alitabasamu.

“Umekuja kufanya nini hapa Dar?”Aliuliza Edna na kumfanya Desmond kutabasamu.

“Nimekuja kwa ajili yako Edna”Aliongea Desmond na kumfanya Edna kushangaa hakumuelewa Desmond kwanini aseme amekuja Tanzania kwa ajili yake.

“Unamaanisha nini kuja kwa ajili yangu?”

“Edna najua hatujaonana muda mrefu sasa, na ni Zaidi ya miaka kumi tokea tuonane but Trust me tokea niachane na Elizabeth nimekuwa wa kukufikiria kila siku , and I was shocked and happy baada ya kupata taarifa ya wewe kupewa cheo cha CEO ndani ya kampuni ya Vexto ,So Edna to answer your Question, yes nipo hapa Tanzania kwa ajili yako , nataka tuendeleze tulipoishia..”Aliongea Desmond na aliona hana muda wa kuremba kuweka madhumuni yake wazi moja kwa moj.

“Desmond wait… unamaanisha nini kusema unataka tuendelee tulipoishia?”Aliuliza Edna huku moyo wake ukidunda kwa kasi.

“Edna nadhani ushanielewa tayari , I know I was foolish back then baada ya kupewa taarifa na Zainabu juu ya hisia zako juu yangu…”

“Stop.!, Desmond usiendelee kuongea”

“Why ! Edna I am ..”

“Desmond I am Married now , I did not got a chance to refute what she told you back then, but its true sikuwa na hisia na wewe kama unavyojiaminisha hivyo naomba uache kuongelea mambo yaliopita na kama huna jambo lingine la kuongea naondoka”Aliongea Edna huku akionyesha kukasirika.

Kwa upande wa Desmond alijikuta akipigwa na kitu Kizito kichwani , ni kama hakuwa amemuelewa Edna vizuri juu ya maneno yake hasa kwenye neno ‘Married’ na alikuwa kwenye mshangao kiasi kwamba hata Edna alivyoanza kupiga hatua kuondoka ndani ya hilo Eneo hakuona na ile akili zake zinarudi kawaida alishangaa kutokumuona Edna.

“Noo.. Edna noo.., how sijasikia kama umeolewa , unatania kama ilivyokuwa miaka ile, Wewe ni CEO mkubwa na ningefahamu kama tayari ushaolewa”Aliongea Desmond peke yake huku akionyesha hali ya kuchanganyikiwa.

Ni kweli Desmond hakuwa akifahamu chochote juu ya Edna kuolewa na hii ni kutokana na kwamba Edna hajawahi kuweka wazi swala hilo na hata kwenye mtandao wa Wikipedia. ‘Profile’ ya Edna ilikuwa ikionyesha yupo Single bado.

Desmond aliachana na mpenzi wake Elizabeth Thambo miaka miwili baada ya kuanza kazi yake ndani ya shirika la kimataifa la UN upande wa wakimbizi, na tokea aachane na Elizabethi alijiingiza kwenye mahusiano tofauti tofauti na wanawake wengi warembo na alifanikiwa juu ya hilo kutokana na kwamba alikuwa na hela , kwani baba yake alikuwa ni raisi, na mama yake Kizwe licha ya kuwa First Lady lakini alikuwa mfanyabiashara mkubwa ndani ya Taifa la Rwanda na nje ya mipaka yake , hivyo jina kubwa alikuwa nalo lakini pia pesa alizokuwa nazo, na moja ya wanawake ambao alitoka nao kimapenzi ni msanii wa kike maarufu kutoka Nigeria afahamikae kwa jina la Misu, licha ya kwamba uhusiano wao ulikuwa wa chini chini , lakini vyombo vya kishilawadu nchini Nigeria vishawahi kuripoti mara moja moja juu ya uhusiano huo lakini Misu alikanusha madai hayo.

Sasa baada ya miaka mingi ya Desmond kufanya kazi kwenye mashirika makubwa duniani , baba yake Paul Jeremy alimtaka arudi nyumbani ili ajiingize kwenye maswala ya kisiasa kwa ajili ya kumuandaa kama mrithi wake na hio yote ni kutokana na Jeremy kumpenda sana Desmond kutokana na uwezo wake wa akili.

Sasa Desmond tokea aliporudi nchini Rwanda mama yake na baba yake walikuwa wakimkalia vikao vya kumtaka aoe kwani umri ulikuwa ukienda, lakini pia haikuwa picha nzuri kwa kuwa na cheo kikubwa serikalini pasipo ya kuwa na mke.

Desmond baada ya kuona kelele zimekuwa nyingi ndio akaanza kufikiria mwanamke ambaye anaweza kumuoa na alianza kufikiria wanawake wake wote aliotoka nao kimapenzi na alianza na Elizabethi mtoto wa Tajiri mmoja kutoka Afrika kusini na kumfikiria kwake kulimfanya kuanza kumfatilia mwanamke huyo mrembo , lakini alijikuta akipatwa na ganzi baada ya kugundua kuwa Elizaethi ashafunga ndoa na Dj mmoja maarufu nchini mwao hivyo alimkatia tamaa na kuanza kufikiria warembo wengine ambao ashawahi kutembea nao , lakini kila mwanamke ambaye alikuwa akimfikiria na kumpembua aliona hakuwa na vigezo vya kuwa nae kwenye mahusiano ya ndoa na katika kufikiria sana pasipo kupata jibu ndipo akili yake iliporudi miaka kumi nyuma chuoni, na jina la Edna Adebayo liliibuka kwenye kichwa chake na hapo hapo alichukua simu yake na kuanza kutafuta jina la Edna mtandaoni na mtandao wa ‘Google’ ulimletea mapendekezo(Keywords) mengi baada tu ya kuandika jina la Edna kwenye ‘Searching Engine tap Bar’.

“What age Edna get Rich?, Is Edna Self made Billionare ,Why Edna is So Famous? , Who is in Love with Billionare Edna, Is it true Edna is no 1 Beutifull Woman in World , Does Edna have Instagram Account?, What are 3 interesting facts about Edna Adebayo?”

“Damn It She is so Famous”Aliwaza Desmond baada ya kuona maswali mengi yanayomuhusu Edna yaliokuwa yakiulizwa mtandaoni na Desmond alipitia kila swali ili kujua taarifa nyingi ambazo zilikuwa zikimuhusu Edna na kila taarifa aliokuwa akiisoma alijjikuta penzi likichipuka , maana hakuna neno baya ambalo limezungumzwa juu ya Edna Zaidi ya Sifa zilizotukuka ambazo zilikuwa zipo kwenye mitandao , lakini jambo ambalo lilimfurahisha Zaidi ni baada ya kugundua Edna bado hajafunga ndoa kwa maana ya kwamba ni Single.

“Maskini ukute alikuwa akinisubiria muda wote … Desmond wewe ni mjinga kwanini unaacha mrembo kama huyu anateseka juu yako … Edna mrebo wangu nisamehe mimi kwa kuchelewa kujua penzi lako juu yangu … Shujaa ,mwokozi majaliwa nipo njiani kwa ajili ya kukuokoa kwenye dimbwi la mateso”Hayo ni maneno ya kipuuzi machache ambayo Desmond alikuwa akiyafikiria kwenye kichwa chake , aliamini Edna hakuwa na mume kwasababu alikuwa akimsubiria yeye.

Sasa jambo hilo lilimfurahisha mno Desmond kwanza alijiambia litakuwa jambo zuri kama atamuoa Edna , kwasababu mrembo huyo anapesa za kutosha , pili aliamini umaarufu wake utazidi kupamba moto na hata ushawishi wake utaongezeka maradufu.

Na Desmond hakutaka kuchelewesha jambo hilo alipanga safari ya kuja Tanzania haraka sana kwa ajili ya kuonana na Edna na siku hii , usiku ndio ana bahatika kuonana na Edna ndani ya hoteli ya Kilimajaro.

Hivyo hata maneno ya kumwambia Edna juu ya kama alifurahishwa na namna alivyopata u’CEO ndani ya Vexto , zilikuwa swaga tu za kumuingia mrembo Edna , ila ukweli ni kwamba hakuwahi kumfatilia kabisa Edna mpaka aliporudi Rwanda.
Desmond Edna ni dada yako, pita nae mbali kabisa
 
hii kitu inatupa arosto hatari kabisaa..Sema mimi sijaelewa kuhusu group ya watsap..ukilipia unanunua episode kadhaa au hiyo payment unakua unakaa kwa group kupata post ahead bila ku renew payment??
Simulizi inael3kea tamari so ukishalipia ni moja kwa moja
 
“Nijiue kwa ajili ya Roma?”Alijiuliza Nasra huku akianza kupima kwenye kichwa chake siku ambayo Roma kama atachukua maamuzi ya kumuacha lakini kabla hajapata jibu , kengele ya mlango wake ilisikika chumba kizima na kumfanya ainuke huku akijiuliza ni nani amekuja usiku huo , kwani haikuwa kawaida.

KUMBE AMELIA MACHOZI YA BURE KWA EDNA ANGALI MOYO HAUPO TAYARI KUACHWA NA ROMA
 
Back
Top Bottom