Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

“Bado nasisitiza kuwa tusithubutu wala kujaribu kufanya lolote kabla ya kuhakikisha kuwa Joram Kiango yu marehemu”, ilidai sauti moja nzito.

“Naam, lazima afe”, sauti nyingine iliunga mkono. “Afe kabla hatujainua mikono kufanya lolote tulilokusudia. Hakuna asiyefahamu jinsi kijana huyu alivyo hatari anusaye shari na kuingilia kati kuharibu harakati zote. Hajasahaulika alivyowakorofisha wale mashujaa waliotaka kuuangusha utawala wa nchi ya Ngoko katika tukio lile lililoitwa Dimbwi la damu. Kadhalika bado hatujasahau alivyosababisha vifo na kuharibu mipango ya majasusi waliotaka kuiharibu nchi hii katika mkasa ambao mtu mmoja aliuandikia kitabu na kuuita Najisikia kuua tena. Kwa kila hali Joram Kiango ni mtu hatari zaidi ya hatari zote zinazoweza kutokea, Hana budi kufa”.

Kicheko kikavu kikasikika kidogo, kikafuatwa na sauti iliyokwaruza ikisema.

“Atakufa. Lazima afe. Na atakufa kifo cha kisayansi kabisa. Mpango huu tumeuandaa kwa uangalifu mkubwa, Na watekelezaji wake pia ni watu ambao wamehitimu vizuri katika nyanja zote zinazohusika na kazi hii, Tuondoe shaka kabisa. Mpango huu utafanikiwa kwa asilimia mia”.

“Kwa hiyo ndugu Mwemyekiti”, ilisema sauti ya mtu wa kwanza. “Niwie radhi kwa kukukata kauli. Ninachokuomba ni kuuahilisha mkutano huu na tusisubutu kukutana tena hadi hapo Joram Kiango atakapokuwa kaburini, Pengine mtaniona mwoga kupindukia, Lakni mimi sipedi kabisa kufanya jambo lolote wakati kijana yule akiwa hai. Mnajua jinsi alivyo na miujiza. Anaweza kuwa hapa akisikiliza mazungumzo yetu, kesho tukajikuta mahakamani bila kutegemea”.

Ilizuka minong’ono, sauti mbili tatu zilimuunga mkono msemaji aliyemaliza kusema. Jina la Joram liliamsha hofu katika mioyo yao. Wakatazamana…

Walipenda pia kumwona Mwenyekiti wao uso kwa uso. Kwa bahati mbaya, hawakuweza kuona uso wake isipokuwa kiwiliwili tu, ambacho kilifunikwa kwa mavazi ya thamani kama walivyokuwa wamevaa wao. Mwanga mkali uliotokana na taa ya umeme iliyowekwa kwa namna iliwachoma macho kila walipotamani kumtazama Mwenyekiti usoni. Ni yeye tu aliyekuwa na nafasi nzuri ya kuwatazama wote mmoja baada ya mwinginge kikamilifu na kuwasoma nyuso zao. Wakati wa kumtambua Mwenyekiti ulikuwa bado haujawadia hivyo hawakupaswa kumuona kabisa isipokuwa sauti yake tu.

Mkutano huo ulifanyika katika chumba cha siri, chini ya ardhi katika mojawapo ya majumba ya kifahari yaliyoko Jijini Dar es salaam.

Kila aina ya tahadhari iliwekwa kuhakikisha usalama wa mkutano huu wa awali. Mkutano ambao ulikuwa umeitishwa ghafla, kwa njia za kutatanisha, hata wajumbe hao walijikuta wamefika kwenye mkutano bila kufahamu kilichowaleta hapo
 
Tukimsubiri ndugu mwandishi. Nimeamua kuposti kipande cha kazi ya mwandishi NAMBA WANI kwa heshima kuu. BEN!!!! Mwandishi wa Karne! Watakaokasirika..........🤣🤣🤣
 
Kumbe hakuna udhamin mpaka leo? Ina maana hamna watu wa marekani humu?
 
Simulizi : Jiue Mwenyewe

Sehemu Ya Kwanza (1)

UTANGULIZI….

TRACEY TASHA Muuaji hatari mwanamke kutoka nchi ya Marekani, anafanikiwa kumuua tajiri mkubwa wa Afrika Kusini, The Great Khumalo…

Ni mara tano na zaisdi ameshindwa kumuua tajiri huyo, lakini sasa anafanikiwa baada ya kubadili mbinu.

Zaidi ya huyo anafanya mauaji mengine katika miji tofauti ya ulimwengu, na hii inamfanya awekwe kwenye orodha ya watu hatari duniani ambao labda hawakutakiwa kuzaliwa.

Mashirika ya kipelelezi na Kijasusi ulimwenguni yanamsaka mwanamke huyu na kushindwa kumkamata.

siku chache baadae anapata kazi nyingine ya kufanya mauaji katika Afrika Mashariki, Tanzania…

Je ni nani huyo anayetakiwa kuuawa? Fuatilia kisa hiki mpaka mwisho….
 
Karibuni nitaanza uzi kuhusu simulizi hii. Be sure ufuatilie huku ukimngoja singanojr achukue karne mzima kuposti Roma huku. Ninapromoti kazi ya mwandishi bingwa R.MWAMBE!!!! Sitaikata.🤣🤣
It goes without saying wenye watauzika na hii stori am sorry in advance👍👍👍
 
safi sana Mkuu, ila Itapendeza ukianzisha uzi mwingine
 
KIJASUSI
Ep 01: Jiue Mwenyewe

Jiue Mwenyewe Sehemu ya Kwanza
IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE

Simulizi : Jiue Mwenyewe

Ni mara tano na zaisdi ames

CHAPISHO LA 01

1

DURBAN – AFRIKA KUSINI-Saa 3:21 asubuhi

NDANI ya jengo refu kuliko yote, Monte Blanc, lililopo katika jiji la Durban, jimbo la KwaZulu Natal, Afrika ya Kusini, ni mtu mmoja aliyekuwa akiwindwa kwa udi na uvumba. Ni mara sita kama si tano mtu huyo kakoswakoswa na muuaji hatari wa kike kutoka Marekani, Tracey Tasha. Mara hii kamfuata hukohuko katika ardhi ya nchi yake, Afrika ya Kusini.

Lamborghini Veneno, gari ya gharama kabisa duniani iliegeshwa taratibu katika maegesho Monte Blanc, nyuma yake ikasimama gari nyingine, BMW nyeusi, vijana wane wakakamavu waliovalia suti nyeusi zilizotanguliwa na mashati meupe na shingoni mwao kila mmoja alining’iniza tai ndefu nyeusi. Walikuwa kikazi zaidi; macho yao yakitazama kila upande kwa umakini wa hali ya juu, mmoja wao aliiendea ile gari, Lamborghini, akaufungua mlango na kuukinga upande wa juu kwa kiganja cha mkono wake wa kushoto ili atokaye ndani asijigonge. Kwa mtindo huu ilionekana atokaye ndani ya gari hiyo ni Mheshimiwa sana, delicate person.

The Great Khumalo kama alivyojiita, alitoka nje ya gari ile, akajiweka vizuri suti yake ya gharama, huku mkono wake wa kulia ukiwa kwenye kifundo cha tai ili kuirekebisha alianza kuvuta hatua ndogo ndogo na mwamvuli ukiwa umeshikiliwa juu yake ili manyunyu ya mvua yaliyokuwa yakinyurunyuta mudaasubuhi hiyo yasimletee tabu. Viajana wake walifuata nyuma wawili na mbele wawili, yeye alikuwa katikati. Ilikuwa ni ngumu kumgusa mtu huyu, tajiri sana katika jiji la Durban; nani asiyemjua Khumalo? Hakuna shule ambayo hajawahi kuifadhili katika jiji hilo, alijulikana, alipendwa, alitazamwa kama almasi. Anaitwa Gervas Khumalo aliyezaliwa na kukulia katika kitongoji cha Berea, alizaliwa katika familia yenye maisha ya kati, lakini iliyoweza kumlipia masomo yake ndani na nje ya nchi mpaka akawa mtu mkubwa.

Hatua zake zilimfikisha katika mlango mkubwa wa jengo hilo, ukafunguliwa kwani yeye hakutakiwa kushika sehemu yoyote, kila mtu alimhusudu, lakini hakukuwa na nafasi ya kumpa hata mkono kwani alikuwa akilindwa vilivyo, moja kwa moja wakaingia katika lifti ili kupanda juu katika ofisi Fulani ya jengo hilo. Monte Blanc, jengo lenye urefu wa mita 133, sakafu (ghorofa) 40, lililojengwa hapo tangu mwaka 1985. Ndani ya lifti hiyo alizungukwa pande zote na vijana wake waliosheheni silaha ndani ya makoti yao.

23, mmoja wao alibofya kitufe kilicho katika kuta ya dude hilo na mara tu likaanza kupanda juu. Lilipofika mahala lilipoamrishwa likasimama kitu kama kengele kikagonga kwa pigo moja laini, mlango ukafunguka, wakateremka na kutembea kuelekea mahala Fulani, wakaipita milango kadhaa. Kila mtu alipisha tajiri huyo apite. KwaZULU Beauty and Massage, wakasimama hapo, mlango wa kioo ukafunguka wawili wakaingia na tajiri wao na wawili wakabaki mlangoni kuhakikisha ulinzi. Khumalo moja kwa moja alienda katika kochi kubwa na kulikalia mara baada ya vijana wake kulihakikisha kuwa lina usalama wa kutosha. Muda huo huo mwanamke mrembo mweupe wa Kiafrika alijitokeza kwenye mapazia yaliyokuwa na nakshi za kumetameta. Ndani ya ofisi hiyo pana na nzuri kulikuwa na wasichana wane waliokuwa katika kazi zao za kila siku, mwingine mapokezi, mwingine kupokea pesa na kutoa risiti, mwingine usafi na mwingine kuongoza wageni kule wanakotakiwa kwenda.

“You are welcome Sir,” (karibu sana mheshimiwa) yule mwanamke akamsalimu. Ukimwangalia alivyo, utasema ni Malaika kashushwa kutoka Mbinguni lakini alikuwa ni Binadamu kama wengine.

“Thank you so much,” (asante sana) The Great Kumhalo akaitikia karibisho hilo, yule Mwanamke akampa ishara ya kumfuata naye akafanya hivyo.

Haikuwa mara ya kwanza kwa tajiri huyo na matajiri wengine wengi kufika sehemu hiyo, wote walifika hapa kwa minajiri ya kupata huduma ya kukandwa mwili, ili kuirudisha miili yao katika hali nzuri ya kiafya. Bwana Khumalo alikwishazoea mara nyingi kuja mahala hapo kwa ajili ya huduma hiyo, alikuwa amejipangia ratiba kabisa ya tendo hilo.

Akainuka na kumfuata yule mwanamke huku walinzi wake nao wakiwa nyuma yake, wakaingia katika mlango ule wa mapazia na kufuata korido ndefu, waliipita milango mingi ya vioo ambayo ndani yake kulikuwa na wanawake waliokuwa wakifanyiwa urembo wa mwili na nywele, vyumba vingine vilikuwa ni vya mazoezi ya viungo, kulikuwa na mabafu maalum kwa ajili ya wanaotaka kuusafisha mwili kwa mvuke.

Walifika kwenye moja ya milango ambayo daima huingia hapo, wale walinzi wakasimama nje ya mlango na bosi wao akaingia ndani pamoja na yule mwanamke kwa ajili ya kumpa huduma hiyo. Juu ya mlango ule kuliandikwa V.I.P.
 
Ukipendezwa nayo ensure umeifuatilia profile yangu utaiona thread yenyewe!!Nitaposti sehemu zake baada ya siku mbili!!! Shukran!!!
 
Ukipendezwa nayo ensure umeifuatilia profile yangu utaiona thread yenyewe!!Nitaposti sehemu zake baada ya siku mbili!!! Shukran!!!
Simulizi ni nzuri lakini itapendeza kama utateta jambo na Dokta singanojr kwanza kabla hujamkatizia kwa mbele kama hivi, mm ni shabiki mkubwa wa simulizi ni mlevi haswa lakn napenda mabingwa wasigombane wala kuingiliana mipaka, ongea na singano mfanye jambo
 
@moderator huyu mtu anahiharibia uzi kupost thread nikioanzisha naomba content zake zifutwe tafadhar
 
Hiii sehemu ni kwa ajili ya simulizi ya NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA pekee kama unataka kupost simulizi yako anzisha thread yako then upost ,Mods naomba mnisaidie kwa huyu ndugu JIMWANGI wanaovuruga utaratibu wa huu uzi.
Huyo jamaa ni wa kupigwa Ban anataka kutuvurugia uzi wetu. Yeye aanzishe wa kwake na si kuvamia kwenye nyuzi za wengine na kuleta story yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiii sehemu ni kwa ajili ya simulizi ya NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA pekee kama unataka kupost simulizi yako anzisha thread yako then upost ,Mods naomba mnisaidie kwa huyu ndugu JIMWANGI wanaovuruga utaratibu wa huu uzi.
Pole mkuu. Lengo langu lilikuwa kuwavutia watu kwenye uzi wangu. Yaani, at least wakingoja uposti kazi yako wakuwe wakisoma Uzi wa kwangu.Otherwise kuna wale wanashinda wakikuja kwenye uzi wako kila saa, lakini wapi.Hujaposti!!! Ashakum si matusi, hatimaye unaposti baada ya karne kadhaa.
 
Simpingi Singanojr. Ni mwandishi aliyebobea na pengine simulizi ya kwake imeishinda ya kwangu. Mimi mwenyewe nilianza kusoma simulizi hii ya Roma kitambo sana. KALI!!!Lakini ikizingatiwa utashinda siku nzima, wiki nzima ukiangalia kama ameposti. Niliudhika na huu unyama.Unakuwa addicted na kitu lakini unakatiziwa, hupewi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…