Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Naona kabisa Hedes ataanza rasmi darasa la mambo ya anga, hapo atakuwa amekamilika rasmi na Athena atakiona Cha moto
 
mkuu singanojr hongera na asante kwa hii kazi......
ila mkuu ungekua unashusha vitu walau mara 3 kwa wiki ili wasomaji tusipoteze muunganiko wa matukio.....

hii kukaa siku 5 bila bila mtu unasahau hata ulipoishia, unakosa ule mvuto wa hii simulizi yako,...... mtu anakua anasoma as if kila kipande kinajitegemea,

btw, simulizi yako ni nzuri sana, tamu wala haichoshi, sema changamoto ni hio ya kukaa muda mrefu bila mwendelezo, inaondoa ladha ya simulizi kwa mfuatiliaji
 
umesikika mkuu ila najitahidi kupost zaidi ya vipande 12 kwa wiki ni rate nzuri , ninaweza igawa 12 mara tatu ikawa vipande vinne nne na kupost mara tatu ila muda upande wangu si rafiki sana , kwanj lazima nitumie laptop kupost ili simulizi isipoteze Aya . na mtiririko mzuri wa usomaji hivyo naweza toa ahadi halafu nikashindwa tekeleza ndio maana nikishusha nashusha vya kutosha .

Leo itaendelea inshallah
 
Ahsante kwa burudani mkuu...utukumbuke na weekend hii kaka tupunguze stress za maisha.
 
umeeleweka mkuu, ilikua ushauri tu na nashukuru kwamba umechukulia positive, maana angekua mwingine angekuja na matusi/kejeli.........

story yako ni nzuri sana,
 
Ohooooo
 
SEHEMU YA 310

Muda huo huo ambao Roma alikuwa akiingia Kigamboni , upande wa Ikulu ya Dar Es salaam , alionekana mheshimiwa Raisi Senga akiwa kwenye ofisi yake akiendelea na majukumu yake kama kawaida, alionekana kuwa bize mno.

Mheshimiwa huyu licha ya kwamba alikuwa na baadhi ya madhaifu , lakini likija swala la kulitumikia taifa alikuwa akijitahidi mno, kwani ni ahadi nyingi sana ambazo aliahidi kwa wananchi na kuziteleza.

Wakati akiendelea kusoma baadhi ya nyaraka zilizokuwa kwenye meza yake kwa haraka haraka , mara simu yake ilianza kuita na aliichukua na kuangalia jina la mpigaji na kugundua lilikuwa ni la rafiki yake Senior.

Senior Habari za majukumu?”

“Salama Senga , Habari za majukumu pia?”

“Salama rafiki yangu , ninaendelea kuwapambania watanzania”

“Ni vyema sana Senga , juhudi zako zinaonekana”

“Nashukuru sana Senior”

“Senga nimekupigia kutaka kujua msimamo wako juu ya yale ambayo Linda ameweza kutuambia”Aliongea Senior kwenye simu na kumfanya mheshimiwa Senga kuegamia kiti chake cha kibosi.

Ukweli ni kwamba siku kadhaa nyuma kabla ya Raisi Jeremy kurudi nchini Rwanda , Linda aliweza kuwaeleza kila kitu ambacho aliambiwa na Mchungaji Cohen Pamoja na Sheikh Assad , maelezo ya Linda yaliwashangaza sana viongozi hawa wa juu wa nchi, hususani stori yote iliokuwa ikihusiaa na viumbe vilivyokuja miaka mingi nyuma , lakini pia namna ambavyo Hades wa Zamani mmoja wa miungu hio kumrithisha Roma jina lake , kila kitu walichopata kusikia kilikuwa cha kushangaza , lakini cha kutoaminika kwa wakati mmoja.

Linda hakueleza kila kitu , kuna baadhi ya mambo ambayo hakupaswa kueleza kama alivyopewa maelekezo na Mchungaji Cohen, maelezo ambayo yalipaswa kubakia kwa wanachama pekee ambayo walikuwa na chata kwenye miili yao ambalo lilikuwa likiwatambulisha kama wanachama wa Ant- Illuminat, lakini pia Linda hakumueleza mheshimiwa Jeremy juu ya namna ambavyo Zoe kovac aliweza kukutana na Seventeen katika visiwa vya Maldives.

Katika kikao chake na wanachama wenzake Linda kwanza kabisa aliweza kufahamu mambo mengi ambayo hakuwa akiyajua , kwanza kabisa aliweza kumfahamu mtu ambaye alimchora Tatoo kwenye mwili wake ni Hades wa zamani lakini pia aliweza kufahamu kwamba yeye Pamoja na wanachama wengine walikuwa kwenye misheni kubwa sana , misheni ambayo ni kupunguza makali ya jamii ya siri ya Iluminat ulimwenguni.

Sasa baaada ya Linda kuwaelezea maelezo yoote alihitimisha kwa kuwaambia kuwa wanatakiwa kuchagua upande, yaani upande wa Illuminat au ule upande wa Anti- Illuminat.

Sasa hapo ndio maraisi hawa walishindwa kufanya maamuzi ya moja kwa moja , ukweli ni kwamba kuna mambo mengi sana ambayo walipaswa kuyazingatia kama viongozi wa nchi kabla ya kufanya maamuzi.

Sasa zilikuwa zimepita siku kadhaa bila ya wao kufanya maamuzi na hapo ndio mheshimiwa Jeremy anajaribu kumpigia simu Raisi Senga kumuuliza ni maamuzi gani ambayo anapanga kuyachukua , yaani kwa maneno marahisi ni upande upi ambao alikuwa akipanga kubakia.

Raisi Senga ukweli ni kwamba hakuwa kabisa na Imani ya kubakia upande wa Ant-Illuminat , aliona ni kichaa peke yake ambaye anaweza kufanya hivyo kwani Illuminat Pamoja ni jamii ya watu wenye nguvu sana duniani na ni ngumu sana Kwenda nao kinyume , lakini kubwa Zaidi ni kwamba hata The Doni mwenyewe ambaye alikuwa akiogopeka Dunia nzima alikuwa upande wa Illuminat.

“Senior nimepanga kuchagua upande wa Illuminat”Aliongea Raisi Senga na kupelekea kimya kwenye simu upande wa pili.

“Una uhakika na maamuzi yako Senga?”

“Ndio Senior , siwezi kukaa upande ambao ni Dhahiri kabisa hauna nguvu na muda wowote utashindwa”Aliongea Raisi Senga.

“Senga ni uamuzi mzuri uliochukua kwa maslahi mapana ya nchi yako

“Asante Senior , lakini hujanieleza na wewe ni upande upi ambao umechagua”

“Nipo upande wako Senga , tuko Pamoja”Aluongea Raisi Jeremy na kumfanya Senga kutabasamu na hawakuongea sana na simu palepale ilikatwa. Lakini palepale simu yake ya ofisini ilitoa mlio kuashiria inaita na alinyanyua mkonga na kuweka sikion.

“Hongera sana Raisi Senga Camilius Kweka kwa kuonyesha nia yako ya kujiunga na sisi, simu hii ni ya ukaribisho katika ibada ya mpasuko wa Mwezi”Ilisikika sauti ya mwanamke kwenye simu na kumfanya Mheshimiwa Senga kushangaa.

“Who Are you”

“Nitakuwa msaidizi wako siku na saa utakapowekewa Wakfu kama mwanachama halali wa Freemason”

“Nataka kujiunga na Illuminat sio Freemason”Aliongea Raisi Senga huku jasho likimtoka

********

Hali ya wanajeshi wake haikuwa nzuri , wengi wao walionekana kuomboleza kwa kiasi kikubwa kicho cha mwenzao Chiara , Roma aliembatana na Rose , waliwapa pole wanajeshi wake.

Upande wa Rose alijisikia Faraja sana kuwa karibu ya Roma na kutambulika kwa wanajeshi hao kama mwanamke wa Roma, ukweli ni kwamba baada ya Rose kusikia kifo cha Chiara hata yeye pia alihuzunika kwani mwanadada huyo alishawahi kukutana nae mara nyingi kwenye Bar yake ya Club B , sasa hata kufika kwenye makao hayo ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa pole, na Rose alikuwa na ruhusa kuingia kwenye kambi hio kwani Roma alishamtabulisha kwa wanajeshi hao.

“Ma Afande najua mnahasira sana kwa kile kilichotokea kwa Chiara mwanajeshi mwenzetu na hata mimi pia nina uchungu vilevile , jambo ambalo ni zuri na linaashiria kuwa sisi ni wamoja na siku zote sisi the Eagles hatujawahi kupotezea kifo cha mwanajeshi mwenzetu Kwenda bure pasipo yakulipiza kisasi na swala hili ndio linanifanya nisimame hapa niongee na nyie”Roma aliongea na kisha akavuta pumzi.

“Watu waliomuua Chiara ni maiti zilizofufuka” Aliongea Roma na kuwafanya The Eagles kushangaa , kwani walishindwa kumuelewa Roma mara moja anataka kumaanisha nini.

“Mfalme Pluto hatujapata kuelewa unacho maanisha , ni kweli kwamba tulikuwa tukiangalia namna tukio lilivyotokea kupitia mkanda uliochukuliwa na Camera , na tulichogundua wavamizi walikuwa na mafunzo ya ajabu, lakini pia walionekana kama hawakua na akili nzuri , lakini swala la kwamba ni maiti zilizofufuka limetuchanganya Mfalme”Aliongea Diego na Roma alimegukia Bram.

“Bram Carcia unaelewa nini kuhusu teknolojia ya Resurrection Fluid?”Aliuliza Roma na kumfanya Bram kushangaa na kupatwa na mzuka mara moja.

“Mfalme usiniambie….”

“Waelezee wenzako unachoelewa kuhusu Ressuration Fluid”Aliongea Roma na Bram alimeza mate na kisha kuwageukia wanajeshi wenzake.

Maelezo ya Bram hayakutofautiana sana na aliyongea Christine, utofauti wa maelezo ya Bram ni kwamba yeye hakugusia Dark Parliament kuwa moja ya taasisi ya siri ambayo ilisimamia kutengenezwa kwa teknolojia hio.

Ukweli Roma mara baada ya kukumbuka Bunge la Kiza , alijikuta akianza kufikiria maneno ya Lilith aliyomwambia kule ufaransa wakati akipambana na Vampire’s waliokuwa wakiongozwa na Madam Viscount.

Moja ya misheni kubwa ya Vampire’s ilikuwa ni kutafuta teknolojia ambayo inaweza kuwafanya kuishi milele(Eternity) jambo ambalo Roma hakuwahi kuliamini hata maramoja.

Sasa Bram maelezo yake hayakuwa yameshiba sana kwani pia hakueleza kwamba Teknolojia hio iliibiwa na Athena ndio maana ikapotea kwa miongo kadhaa kabla ya kuonekana tena.

“Teknolijia hii kama alivyosema Afande Bram Carcia ilipotea kwa miongo kadhaa na kwa bahati mbaya mara ya pili ilivyokuja kuonekana ilileta madhara makubwa sana, mtu ambaye anaaminika aliiba teknolojia hii ni The Doni”Aliongea Roma na kuwafanya wanajeshi wote kushangaa akiwemo pia Rose ambaye alikuwa akisikilia pembeni pasipo ya kuchangia chochote.

Ukweli Roma hakutaka kuwaeleza wanajeshi wake kwamba The Doni alikuwa ni Athena moja ya miungu kumi na mbili , aliamini kama angewaambia basi kuna uwezekano kwa wao kuanza kuogopa hatakutokufanya kazi vyema.

“Nyie wenyewe ndio mlifanya uchunguzi na mkagundua The Doni ni mtu mkubwa sana duniani ambaye ana kila mbinu ya kufanya serikali nyingi kumugopa , hivyo swala la kuiba teknolojia hio ni jambo linalowezekana , lakini sitaki kumsifia sana kwa uwezo wake , ila ninachowaambia ni kwamba tunaingia kwenye kazi nyingine ya kufahamu imekuwaje maiti zinazotembea zikaonekana hapa Tanzania mpaka kushambulia familia yangu lakini pia kumuua mwanajeshi wetu, hilo ni moja ,pili nataka mchunguze kifo cha Raheli Adebayo mama wa mke wangu”Aliongea na kuwafanya kutokuelewa sababu ya kuambiwa wanapaswa kuchunguza kifo cha Raheli Adebayo.

“Mfalme Pluto unahusisha kifo cha Mama wa Madam Persephone kinahusiana na hiko kimiminika?”Aliuliza Dieo kwa mshangao.

“Ndio maana nataka swala hili mlifanye kwa Pamoja , Miss Christine yupo hapa Tanzania na atawapatia mwanga katika uchunguzi huu, niwakumbushe tu kwamba jambo hili kufanikiwa kwake ndio namna ya kumfikia adui aliesababisha kifo cha mwanajeshi wetu Chiara”Aliongea Roma na wote kwa pamoja walisimama na kupiga saluti wakiashiria kukubariana nae.

“Babe kwenye maneno yako yale , ulikuwa ukimaanisha mkeo mama yake aliuliwa au sijaelewa vizuri?”Aliuliza Rose mara baada ya wote kutoka eneo la bustanini.

“Ndio mwili wake ulifanyiwa majaribio ya kisayansi , ambayo yalifeli na kupelekea kifo chake , hivyo nataka kujua ilikuwaje mpaka akawa sehemu ya watu waliochaguliwa kufanyiwa majaribio , maana hakuwa mtu mdogo , alikuwa ni mfanyabiashara ambaye alikuwa na pesa nyingi hivyo kulikuwa na hatari kubwa kwa wanasayansi hao kumtumia”Aliongea Roma na Rose alishangaa na kuhuzunika kwa wakati mmoja.

“Sipati picha Edna akilifahamu hili atakuwa kwenye hali gani ,natamani kipindi hiko niwe nimezoeana nae ili niwe sehemu ya watu wanaomfariji”Aliongea Rose na kumfanya Roma kutabasamu.

“Kuzoeana nae itategemea na juhudi zako mwenyewe babe Rose”Aliongea Roma huku akitembea na kumfanya Rose kusimama na kumwangalia kwanyuma.

*******

Saa kumi kamili mrembo Dorisi ambaye alikuwa akitoka kazini , alionekana kuegesha gari lake ndani ya jumba lake kubwa la kifahari, licha ya kwamba alikuwa amechoka lakini alivutia kumwangalia.

Kwa ukubwa wa jumba hilo analoishi ilikuwa ni ngumu sana kuamini kama alikuwa akiishi peke yake.

Dorisi alitembea mara baada ya kutoa mkoba wake kwenye gari mpaka kuufikia mlango mkubwa wa jumba lake na kisha akafungua mlango na kuingia ndani.

Lakini sasa alijikuta akishangaa baada ya kugundua eneo la sebuleni kuna mwanamke ambaye ameketi , jambo ambalo lilimfanya kutetemeka mwili mzima.

“Karibu sana Dorisi”Sauti hio ya kike ilisikika kwenye maisikio ya Dorisi na kumfanya mrembo huyu kuzidi kushangaa na kujiuliza kwa wakati mmoja mwanamke huyo kaingiaje nyumbani kwake kwani mlango ulikuwa umefungwa , lakini kilichomshangaza Zaidi ni kwamba mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa mzungu.

“Wewe ni nani?”Aliongea Dorisi huku akirudi nyuma nyuma na kusimama kwenye mlango.

I
 
SEHEMU YA 311

Mwanamke yule aliinuka alipoketi pasipo yakuwa na wasiwasi kabisa , ni kama vile alikuwa nyumbani kwake na alipogeuka sasa ndio Dorisi aliweza kumuona mwanamke huyu mrembo sana ambaye kwa haraka haraka aliamini sio raia wa Tanzania.

“Who Are you?”Aliuliza Dorisi kwa lugha sasa ya kingereza.

“Jina langu ni Cleria Allisanto”Aliongea yule mwanamke huku akimsogelea Dorisi akiwa ameupamba uso wake na tabasamu na alitumia Lugha ya Kiswahili kuongea.

“Unafanya nini nyumbani kwangu na umewezaje kuingia?”Aliuliza Dorisi kwa mara nyingine huku akishikilia kitasa cha mlango , ukweli ni kwamba alikuwa akiogopa sana na muda wowote alikuwa akijiandaa kukimbia.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi Dorisi , mimi ni rafiki yake na Naira Ryani kama alivyo rafiki yako”Aliongea yule mwanamke na hapo sasa Dorisi alitoa macho.

“Unamfahamu Naira?”Aliongea Dorisi na mwanamke yule alitabasamu.

“Dorisi unaonaje ukiacha kutetemeka , nishasema Naira ni Rafiki yangu kama alivyo rafiki yako”Aliongea yule mwanamke.

Huyu mwanamke hakuwa mwingine bali alikuwa ni Athena au The Doni na haikueleweka kwanini siku ya leo alikuwa amekuja ndani ya nyumba ya Dorisi.

Athena ambaye anajiita sasa kwa jina la Cleria Allisanto alimwangalia Dorisi kwa dakika kadhaa na kisha akaachia tabasamu na kurudi nyuma mpaka kwenye masofa na akainua bahasha moja ambayo ni Dhahiri alikuja nayo na kisha akamsogelea Dorisi na kisha kumpatia.

Dorisi kwa kutetemeka aliichukua ile bahasha huku akimwangalia Athena machoni na Athena baada ya kuona Dorisi anamwangalia sana alimpa ishara ya kufungua bahasha alioshikilia mkononi.

Dorisi baada ya kufungua ile bahasha alijikuta akishangaa mno mara baada ya kuona picha ya rafiki yake wa utotoni , ambaye kwake alikuwa ni kama ndugu , picha zile zilikuwa zikimuonyesha N aira akiwa kwenye mapozi tofauti akiwa amepiga na mwanamke aliekuwa mbele yake.

Athena baada ya kuona mshituko wa Dorisi alitabasamu na kisha akamsogelea Dorisi tena.

“Nafikiri umeamini sasa ninapokuambia mimi ni rafiki wa karibu na rafiki yako Naira”Aliongea Athena kwa lugha ya Kiswahili na Dorisi alitingisha kichwa , alikuwa bado na wasiwasi , licha ya kwamba mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa mrembo sana , lakini kwake wasiwasi hakumuishia , kwani kwanza alikuwa akijiuliza maswali , kama kweli mwanamke huyo hakuwa mbaya kwake , aliingiaje kwanza ndani ya nyumba yake pasipo ya kutumia mlango , kwani milango yote imefungwa.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Dorisi.

“Nishakutajia jina langu , naitwa Cleria Allisanto au ushasahau Dorisi , unapaswa ukalili jina langu kwani ujio wangu siku ya leo ni wa maana kubwa”Aliongea Athena na kumfanya Dorisi kumwangalia tena mwanamke huyu ambaye alikuwa amevalia suti ya rangi nyeusi huku miguuni akiwa amevalia viatu aina ya skuna , alikuwa amependeza haswa na hakuna aina ya uovu uliokuwa ukionekana kwenye sura yake Zaidi ya tabasamu la ucheshi.

“Naira rafiki yangu yuko wapi nahitaji kumuona”Aliongea Dorisi

“Unampenda rafiki yako kwa kiasi gani?”Aliuliza Athena.

“Kwangu ni Zaidi ya ndugu”

“Kama ilivyo kwangu , Naira ni rafiki yangu wa kwanza hapa Duniani”Aliongea yule mwanamke na kumfanya Dorisi kushangaa , ni kama hakuwa akiamini maneno ya mwanamke ambaye yuko mbele yake.

“Usishangae ninachosema namaanisha Dorisi na wewe unakwenda kuwa rafiki yangu wa pili, lakini kama ilivyokuwa kwa Naira alivyokuwa na msaada mkubwa kwangu , basi na wewe nahitaji uwe na msaada mkubwa kwangu”Aliongea Athena na kumchanganya Zaidi Dorisi.

“Msaada gani unataka kutoka kwangu ambao ndio unatufanya tuwe marafiki”Aliongea , ukweli Dorisi bado woga ulikuwa juu sana.

“Njoo tuketi maana swala ambalo tunakwenda kuongea ni kubwa mno”Aliongea Athena huku akimpa ishara Dorisi ya kusogea kwenye masofa na Dorisi kwa kusita alisogea.

“Dorisi nimekuja kukusaidia”

“Kunisaidia kivipi?”

“Unampenda kwa kiasi gani Roma Ramoni?”Aliuliza Athena na kumfanya Dorisi kushangaa hakuelewa inakuwaje mwanamke huyu wa kizungu kumfahamu Roma mpenzi wake.

“Dorisi sina muda mrefu wakukaa hapa , najua una maswai mengi ila jibu kila swali ninalokuuliza pasipo kuuliza swali”Aliongea Athena kwa usiriasi kidogo.

“Nampenda sana”

“Kiasi cha kutaka kumzalia mtoto?”Aliuliza Athena na Dorisi macho kodo.

“Mapenzi yako yanatosha kumzalia mtoto?”Aliuliza kwa mara nyingine na Dorisi alitingisha kichwa kuashiria ndio , ijapokuwa hajawahi kufikiria kuhusu kumzalia mtoto Roma , lakini aliishia kujibu kwamba yupo tayari kumzalia Roma mtoto.

Athena alitabasamu baada ya kuridhishwa na jibu la Dorisi.

“U?tajisikiaje kama nikikuambia kwamba huana uwezo wa kumzalia Roma mtoto?”Aliuliza tena.

“Unamaanisha nini?”

“Nafikiri ushawahi kushuhudia uwezo wa ajabu wa Roma si ndio?”Dorisi aliitikia kwa kichwa.

“Basi kwa maneno marahisi ni kwamba hakuna mwanamke yoyote ndani ya dunia hii mwenye mwili wa kawaida wa kibinadamu ambaye ataweza kushika Mimba ya Roma”Aliongea Athena na kumfanya Dorisi kushangaa Zaidi na Zaidi.

“Ila tu ninao uwezo wa kukufanya uweze kubeba mimba ya Roma kabla hata ya mke wake”Aliendelea kuongea.

“Dorisi unaonaje kama utamzalia mwanaume unaempenda mtoto? , kwa haraka haraka?, ni dhahiri kwamba hata mapenzi yake kwako yataongezeka na kuwa makubwa Zaidi kuliko hata kwa mke wake”Aliongea Athena kwa namna ya kumshawishi Dorisi.

Dorisi alikaa chini paispo ya kuongea chochote huku akifikiria , na alijiuliza maswali mengi na moja ni juu ya kwamba itakuwaje kama ataweza kumzalia Roma mtoto , lakini pia kama maneno ya mwanamke aliekuwa mbele yake ni ya kweli itakuwaje kama Roma akikosa mtoto Maisha yake yote , Dorisi alijijibu kwamba Roma hatokuwa na furaha kwenye Maisha yake yote na sio kwake tu hata kwa yeye ambaye ana mpenda hatokuwa na furaha.

“Dorisi upo tayari kumzalia Roma mtoto?”Aliuliza tena Athena

“Kwanini unataka kunisaidia kumzalia Roma mtoto , ni jambo gani la faida unalotaka kutoka kwangu”Aliuliza Dorisi , alijiambia hawezi kutokea mtu ghafla tu na kukutaka kukusaidia.

“Sina haja ya kunufaika kwa chochote kutoka kwako Dorisi mimi kama rafiki wa rafiki yako nataka kukusaidia kuwa na furaha , ndio ahadi niliowekeana nae ya kukusaidia”Aliongea na kumfanya Dorisi aanze kumkumbuka Naira , alikumbuka kipindi cha utoto wao namna ambavyo Naira alikuwa akimjali kama mdogo wake , huku akimwahidi mambo mengi.

“Dorisi nitahakikisha kwenye Maisha yako unakuja kuwa na furaha kuliko kiumbe chochote ndani ya dunia hii , hii ni ahadi ninayoweka mbele yako”Dorisi aliweza kukumbuka moja ya kauli ya Naira , kauli ambayo Naira aliongea wiki moja kabla hajaondoka na wazazi wake.

“Unamfahamu vipi Roma?”Aliuliza Dorisi , ukweli ni kwamba bado hakuwa akimwamini mwanamke aliekuwa mbele yake licha ya kwamba alikuwa rafiki wa Naira, swali lile lilionekana kumkera Athena , kwani palepale alikunja uso.

“Nishasema hupaswi kuuliza swali bali unatakiwa kujibu, kama unahitaji muda wa kufikiria ninaweza kukupatia , lakini lazima tukubaliane jambo moja”Aliongea Athena na Dorisi alitingisha kichwa akiashiria kwamba alikuwa akihitaji muda wa kufikiria.

“Ninakupa muda wa siku kumi kufikiria nikirudi unipatie majibu , na tulichokiongea hapa inapaswa kuwa siri yangu mimi na wewe”Aliongea Athena na palepale Dorisi ambaye alikuwa amekaa kwenye sofa aliegamia akiwa kama ni mtu ambaye amepitiwa na usingizi, alionekana kutokuelewa kinachoendelea.

“Dorisi nilikuwa nikikuandaa kwa muda mrefu kwa misheni yangu na lazima utimize kile ninachokipanga nje ya hiari yako”Aliongea Athena na kumshika shika Dorisi mashavu yake huku akionyesha kutabasamu , alikuwa ni kama mtu ambaye alikuwa akifurahishwa na uzuri wa Dorisi na alitumia dakika kama mbili hivi kumkagua Dorisi na palepale alipeleka mkono wake wa kushoto tumboni kwa Dorisi chini kidogo ya kitomvu na kuanza kuminya(palpating) kama mtu anaetafuta uvimbe kwenye tumbo la Dorisi na baada ya dakika kama tatu kuendelea kufanya kitendo kile alisimamisha mkono wake huku akiachia tabasamu , ni kama kitu ambacho alikuwa akikitafuta kwenye mwili wa Dorisi alikipata.

Aliendelea kushikilia vilevile mpaka hali ya Dorisi ilivyoanza kubadilika , kwani Dorisi alifumbua macho na kumwangalia Athena pasipo ya kuongea neno, alimwangalia kwa dakika kama mbili hivi na palepale macho yake yakajifumba tena na kumfanya Athena kutabasamu na zoezi lake ambalo alikuwa amefanya lilionekana kukamilika kwani alisimama na kuweka suti yake vizuri.

“Nitakuja kwa ajili ya matokeo Dorisi”Aliongea Athena na kisha aliangali picha ambazo amempatia Dorisi na kuzichukua na kufumba na kufumbua Athena akatoweka.

Sasa haikueleweka kwamba alifanya kitendo gani ila ni uhakika kwamba katika zoezi lake lile alifanya kitendo maarufu kinachofahamika kwa lugha ya kingereza kama ‘Channeling’.







SEHEMU YA 312

Roma baada ya kuagana na Rose alichukua uelekeo wa Kwenda Moroco , yalipo makao makuu ya kampuni ya Vecto Media , alikuwa akihitaji kujua ni nini kinaendelea.

Wakati akiwa anatoka kwenye makazi hayo ya The Eagles alikuwa ashawasiliana na Sophia na kumpa maelekezo ya kukutana Moroco.

Roma alijiambia angalau anapaswa kuwa kama kichwa cha familia , kwani Sophia tayari alikuwa ni mwanafamilia na Edna na Sophia ni kitu na mdogo wake , hivyo aliona hapaswi kumuachia Sophia kujitegemea kwa kila kitu na hata kumpigia , madhumuni yake ni Kwenda kumsikia Sophia akiimba , kwani tokea Sophia aseme kwamba ana kipaji cha kuimba Roma hakuwahi kumsikia kabisa akiimba.

Alitumia nusu saa tu kufika ndani ya jengo la kampuni yake na mara baada ya kuegesha gari yake alijongea mpaka ndani ya jengo hilo kwa ajili ya kuziendea lift, lakini alijikuta akisimama mara baada ya kumuona Sophia mbele yake , kilichomfanya Roma kusimama ni namna ambavyo Sophia alikuwa amevaa , yaani alikuwa amependeza kiasi kwamba ni kama alikuwa akitoka mtoko na mpenzi wake.

“Unamiadi mingine mara baada ya kuonana na mim?”Aliuliza Roma mara baada ya kumfikia Sophia ambaye alikuwa ameachia tabasamu.

“Mfalme Pluto miadi yangu ni kuonana na wewe”Aliongea Sophia kwa namna ya utani na kumfanya Roma kutabasamu

“Ndio ukaamua kuvunja kabati kisa unakuja kuonana na mimi?”

“Hii ndio staili yangu ya uvaaji , mfalme Pluto si useme tu umevutiwa na mimi maana hata sijajiandaa muda mefu”Aliongea Sophia na kumfanya Roma asitake kuongea tena na kumpita.

Sophia alionekana kufurahia kweli, ukweli ni kwamba tokea afike ndani ya famili ya Edna hakuwahi kutoka nje ya familia na Roma kabisa wala kupigiwa simu , sasa Roma alivyompigia simu na kumwambia wakutane Moroco alifurahi mno.

Taarifa za ujio wa Christine bado zilikuwa hazijatangazwa kabisa na haikueleweka Christine aliwezaje kupita ndani ya uwanja wa ndege pasipo ya kushitukiwa.

“Director , karibu tena kazini”aliongea Daudi kwa bashasaha baada ya kumuona Roma na hata Wendy alimsogelea na kumlaki na Roma alitabasamu kwa namna ambavo alikuwa akipewa heshima yake kama kiongozi wa kampuni.

Roma alipewa muongozo kwa haraka haraka kwa kile ambacho kiliendelea kwa siku zote nne ambazo hakuwa hapo kazini na aliliridhishwa na kazi kubwa ambayo Wendy na Daudi walikuwa wakifanya , kwani kampuni ilionekana kama sio mpya tena.

Sophia mwenyewe alipendezeshwa sana na mpangilio wa kampuni na alijiambia hakika Edna alikuwa na akili kufungua kampuni hio.

Baada lisaa kupita Sophia alipelekwa kwenye chumba cha Studio ya muziki, Roma pamoja na Daudi wote walitaka kumsikiliza Sophia uwezo wake wa kuimba.

Studio ilikuwa ya kisasa mno kiasi kwamba ilimtia mzuka mno Sophia , kwani Studio za namna hio alikuwa akiziona kwenye lebo kubwa sa muziki duniani , tena kwa kupitia mitandao ya kijamii tu.

“Studio hii ni ya kisasa kabisa , mmejitahidi sana”Aliongea Sophia akishindwa kuzuia hisia zake.

“Miss Edna kawekeza kiasi kikubwa sana kwenye hii kampuni na ndio maana tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha kila kitu kinakuwa ndani ya matarajio yake”Aliongea Daudi na Sophia akatabasamu.

“Huyu ni Producer wetu mpya , anafahamika kwa jina la Elisha Kagi ni Producer mzoefu sana na amefanya kazi zake nyingi nchini Marekani”Aliongea Daudi na Roma alimwangalia bwana aliekuwa mbele yake na kuridhishwa na namna ambavyo anajiamini.

“Elisha kutana na Director wa kampuni”Aliongea Daudi na Elisha alijikuta akikodoa macho na kusimama vizuri na kumpa heshima yake Roma , mwanzoni hakumfahamu kama kiongozi wa kampuni kwani Roma alikuwa na muonekano wa kawaida sana , hivyo akajua ni mfanyakazi wa kawaida na alikuwa akifanyiwa orientation.

“Producer Elisha nina dada yangu hapa , kila siku ni mwenye kujigamba ana kipaji nataka leo nimsikie ndio maana nimemleta kwako”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi akunje uso mara baada ya kusikia neno ‘Dada’ alionekana kabisa kutolipenda neno hilo.

Producer alikuwa akimwangalia Sophia kwa kuibia sana , lakini alikuwa amehusudu uzuri wake kwa kiwango kikubwa sana na kwa jinsi Sophia alivyokuwa amependeza ndio alichafua kabisa hali ya hewa , ukizingatia na uzuri wa kipekee aliokuwa nao.

“Miss Sophia unaimba wimbo wako mwenyewe au unafanya Cover Version?”Aliuliza Produza.

Cover Version ni neno la kingereza ambalo katika tasnia ya muziki linamaanisha kwamba msanii kuimba wimbo wa msanii mwingine aidha kama ulivyo au kwa kuongezea baadhi ya maneno yake(Remake).

“Nitafanya Remake ya wimbo wa Calum Scott -You are the reason”Aliongea Sophia na kumfanya Roma kutabasamu , alikuwa akiufahamu huo wimbo mwimbaji alikuwani mwanaume , sasa Sophia kuchagua wimbo wa namna hio aliamini kwake ni mgumu sana kuiimba.

Produza hakuwa na mwembe sana , alimpa maelekezo Sophia kupita upande wa pili, hatua ya kwanza ni Sophia kuimba bila ‘instrument Beat’:

“There goes my heart beating………cause you are the reason .. I am Losing my sleep”

Sio kwa upande wa Roma tu kila mmoja aliekuwa ndani ya studio hio alivutiwa mno na sauti ya Sophia , yaani wimbo ulikuwa ukiimbwa utadhania yeye ndio kautunga , Pruducer mwenyewe bila kupenda alijikuta akiachia Beat palepale na hapo ni kama alimfanya Sophia azidi kuongeza mbwembwe.

Upande wa Sophia alikuwa akiimba kwa hisia kali mno huku macho yake yote akiwa ameyaelekeza kwa Roma ,yaani ilikuwa kama ndio anamwimbia huo wimbo , kitendo ambacho Roma alikiona ila alipotezea

Kusema ukweli Sophia alikuwa na kipaji kikubwa sana cha uimbaji na kwa jinsi ambavyo alikuwa akiimba ilionyesha dhahiri kabisa atakuja kuwa mwimbaji mkubwa sana.

Sophia baada ya kumaliza kuimba wimbo wa Calum Scott alihamia wimbo ambao ni wa kwake sasa , ambao alipoulizwa jina lake aliishia kwamba hajapendekeza jina bado.

“This is Hit Song …. Paah !!... Paah !!”Producer alijikuta akishindwa kujizuia na kusimama na kushangilia ,Daudi aliishia kupiga makofi na kuridhishwa na uwezo wa Sophia , huku upande wa Roma yeye akiwa ameachia tabasamu akimwangalia Sophia.

“Director nadhani haina haja ya mashindano kwani namuona Miss Sophia kama mshindi”

“Uko sahihi Daudi , lakini mashindano haya yana maana kubwa sana kwa kampuni , lakini pia kwa mshindi atakaeshinda , tunamtengenezea jina ndio maana nikamwalika Christine kuboost mashindano yetu kuwa maarufu Zaidi”Aliongea Roma na Daudi alitingisha kichwa kukubaliana nae.

“Vipi maendeleo ya Chanelli yetu Pamoja Redio?”

“Tunasubiria vibali kutoka TCRA ili tuanze kufungua rasmi channeli yetu , wametuahidi jumatatu tutakuwa na vibali vyote”

“Tunahitaji Coverage ya kiwango cha juu sana kama malengo yetu ni kuteka soko la Habari na burudani, unaonaje siku ya ufunguzi wa Channeli yetu tukamfanyia Interview Christine?”Aliongea Roma na kumfanya Daudi kumaka.

“Lakini Director manajement ya miss Christine imetuambia ratiba yake ni kuja tu kwenye fainali ya mashindano peke yake?”

“Director samahani , unamaanisha Christine kutoka Marekani?”Aliuliza Producer kwa shauku ,kwani aliweza kusikia maongezi ya wakubwa hao wa kampuni na Daudi aliitikia kwa kichwa kwamba ndio mwenyewe.

“No..Siwezi kuamini Christine kuja hapa Tanzania?”Aliongea Elisha na Daudi alitabasamu.

“Hata mimi nilikuwa kwenye mshangao kama wako , lakini kila kitu kinawezekana kwa msaada wa Director hapa”Aliongea Daudi na kumfanya Elisha kumwangalia Roma kwanzia juu hadi chini na haikueleweka alifikiria nini bali alinyamaza na kuendelea kufanya kazi yake.

“Daudi anza na matangazo ya siku ya uzinduzi wa chaneli yetu,nitaongea na Christine kufanya Interview na chaneli yetu”Aliongea Roma na Daudi alitaka kuongea neno lakini aliishia kati.

“Cling!!..Cling..!!”Simu ya Roma ilitoa mlio wa kuita na kumfanya kuitoa haraka na kuangalia jina la mpigaji na alijikuta akishangaa na kutabasamu kwa wakati mmoja mara baada ya kuona aliekuwa akipiga ni Neema Luwazo.

“Neema kuna nini mbona unalia?”Aliuliza Roma kwa wasiwasi baada ya kupokea simu , lakini Neema Luwazo tofauti na kuongea yeye alikuwa akilia.

“Roma Mzee Chino kashambuliwa na majambazi…..”

“Niambie uko sehemu gani nifike haraka”Aliongea Roma, hakutaka kusikiliza Zaidi mpaka hapo alijua kuna tatizo la kiafya ambalo limemkumba Mzee Chino.

“Nipo hospitali ya Aghakhani, Roma nakuhitaji”Aliongea Neema kinyonge huku bado akilia na kumfanya Roma amgeukie Sophia aliekuwa chumba cha kurekodia.

“Nakuja”Aliongea Roma na kisha akakata simu na kumgeukia Daudi.

“Utamueleza Sophia nimepata dharula… “Aliongea Roma.

“Director ..” alijaribu kuita Daudi lakini Roma alishatokomea nje

Roma alitumia muda mchache sana kusafiri kutoka Morocco Kwenda hospitali ya Aghakhani , baada ya kufika na kuegesha alitoa simu yake na kupiga simu kwa Neema ili kujua yuko upande gani na alielekezwa na haraka haraka aliingia kwenye hospitali hio.

Roma mara baada tu ya kuingia upande wa VIP aliweza kumuona Neema Luwazo ambaye alikuwa Pamoja na wamama wawili ambao hakuwa akiwafahamu , Pamoja na vijana wawili wa kiume rika lake.

Neema baada ya kumuona Roma , alimkimbilia na Kwenda kumkumbatia huku akianza kulia kwa kwikwi , kama mtu ambae alikuwa amefiwa.

“Neema nini kimetokea?” Aliongea Roma huku akijaribu kumtuliza Neema.
 
SEHEMU YA 313

Kwa maelezo ya Neema ni kwamba Mzee Chino alishambuliwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na kumjeruhi kwa kumpiga risasi na baada ya tukio hilo ndio Neema aliekuwa kazini kwake katika kampuni ya Maple ndio aliweza kupata taarifa ya tukio hilo na kuja mpaka hospitali ya Aghakhani na kukuta tayari mzee Chino akiwa katika chumba cha matibabu..

Kwahio muda ambao Roma alifika ndani ya hospitali ya Aghakani ni kwamba ndio Mzee Chino alikuwa na saa moja tokea afikishwe hapo na madaktari walikuwa wakiendelea na zoezi la kuokoa Maisha yake.

Roma alishangazwa na tukio hilo la kupigwa kwa lisasi kwa Mzee Chino na kujiuliza ni jambo gani ambalo linendelea hapa Tanzania mpaka matukio ya namna hio kutokea.

“Roma nitafanya nini mimi Mzee Chino na yeye akipoteza Maisha,, nitabaki mwenyewe Roma, Mzee chino ni ndugu pekee niliebakiwa nae hapa Duniani”Aliongea Neema huku akilia kwa kwikwi na kumfanya Roma kumuonea huruma mwanamke huyu , kwani alikuwa akimjua Neema kwa siku kadhaa alizoweza kufahamiana nae alikuwa ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kutawala hisia zake , sasa tukio hili na kwa jinsi ambavyo alikuwa akionekana ilikuwa ni dhahiri kwamba Mzee Chino alikuwa mtu muhimu sana kwake.

Roma kwa wakati huo kwa kweli hakuwa akijua cha kufanya na hata baadhi ya watu walioambatana na Neema walionekana kutuoelewa uhusiano uliokuwepo kati ya Neema na Roma , ila hakuna hata mmoja aliepata ujasiri wa kuuliza.

Roma ilibidi asubirie akiwa nje na Neema ili kuona ni kipi kitajili kwa afya ya Mzee Chino, wakati wote Neema alionekana kuomba baya lolote lisimkute mzee huyo na kumfanya Roma ajitahidi kumfariji Neema.

Lisaa limoja mbele hatimae Dokta Shukuru Omary mganga maarufu ndani ya hospitali hii alitoka kwenye chumba cha upasuaji , huku akionesha kuchoka mno lakini licha ya hivyo Neema hakutaka kumpa ahueni , alichotaka kujua muda huo ni maendeleo ya Baba yake wa hiari , yaani Mzee Chino.

Dokta alimwangalia Waziri na kuonyesha hali ya kukata tamaa na hilo Roma aliweza kulishuhudia.

“Tumeweza kutoa risasi mbili zilizompata begani , lakini moja iliompata kwenye uti wa mgongo imeshindikana kutoka na naweza kusema kwamba kwa sasa hatuwezi kabisa kuitoa na kuna uwezekano mdogo sana kutembea hata kama atapona”Aliongea Dokta Shukuru kwa hali ya huruma na kumfanya Neema kuangua kilio upya.

“Dokta nini kinapaswa kufanyika juu ya hali yake?”Aliuliza bwana aliekuwa amekuja na Neema ambaye amevalia Suti.

“Tunaweza kuitoa risasi kwa kumfanyia upasuaji lakini kwa hali aliokuwa nayo hata kama itatoka hakuna namna ya yeye kupona”

“Sasa Daktari kwanini msiitoe hio risasi muda huu na kuacha ikiendelea kubakia kwenye mwili kama uwezo huo mpo nao?”Aliuliza Roma.

“Kwa hali aliokuwa nayo hatuwezi kumfanyia upasuaji mkubwa wa namna hio , tunapaswa kumuacha kuona kama atarejewa na fahamu ndio tuanze utaratibu wakumfanyia upasuaji kwenye uti wa mgongo ,lakini…”

“Lakini nini Dokta?”Aliuliza Neema na Dokta Shukuru alimeza mate kidogo.

“Kadri risasi inavyobaki kwenye mwili wake ndio madhara Zaidi kwenye afya yake yanavyozidi kuongezeka anaweza akawa in ‘Vegetative condition’ Maisha yake yote”Aliongea na hapo ni kama alirusha bomu lingine kwa Neema kwani machozi yalimtoka mfululizo.

Vegetative state ni hali ambayo inaelezea mgonjwa ambaye hana uwezo wa kufanya chochote ilihali ya kwamba bado yupo hai , yaani hatokuwa na uwezo wa kuongea kutumia akili yake , au kufanya chochote kile kama binadamu wa kawaida.

“Dokta kwahio kama kuna uwezekano wa mgonjwa kurejewa na hali yake ya kawaida mnaweza kumfanyia upasuaji wa uti wa mgongo na kumuokoa katika madhara makubwa yanayoweza kumkumba?”Aliuliza Roma na kumfanya Dokta amwangalie kidogo kwa mshangao kwani swali la Roma lilionekana kuwa la kipumbavu.

“Kama kungekuwa na uwezekano huo, basi ninaweza kuandaa upasuaji wa haraka sana na matumaini ya hali ya afya yake kurudi kama zamani yanaweza kupanda kutoka asilimia sifuri mpaka sabini na tano”Aliongea lakini hata hivyo maneno hayo hayakuwa na nafuu kwa Neema kwani uwezekano huo wa kimiujiza haukuwepo.

“Nipelekeni nikaonane na mgonjwa”Aliongea Roma na kumfanya hata Neema aliekuwa akitoa machozi kushangaa.

“Roma hakuna jinsi ya kumsaidia ninapaswa kuukubali ukweli nitahakikisha waliohusika wanakamatwa na vyombo vya dola na kufia Gerezani”aliongea Neema.

“Mzee Chino anaonekana kuwa wa muhimu sana kwako Neema na mimi siwezi kukuangalia ukilia na kukosa furaha kwa ajili yake , nitafanya ambalo lipo kwenye uwezo wangu kuhakikisha anapona ,Dokta tusipoteze muda nataka kuonana na mgonjwa sasa hivi”Aliongea Roma na kumfanya Dokta Shukuru kushangaa ,kwani alishindwa kuelewa Roma anataka kufanya nini.

“Dokta muonyeshe Roma mgonjwa ,ni mpenzi wangu hivyo hakuna shida kama atamuona”Aliongea Neema tena awamu hii akimtambulisha Roma kama mpenzi, jambo ambalo lilimfanya Dokta Shukuru kushangaa mno , hakuamini kijana mdogo kama huyo anatoka kimapenzi na mwanamke mwenye heshima ndani ya taifa hili mwanbamke Tajiri na mwanasisiasa Neema Luwazo lakini kubwa Zaidi ni namna wawili hao walivyotofautiana umri ,hata kwa wale mabwana wawili waliokuwa pembeni walijikuta wakishangaa mno.

Ukumbuke maongezi haya yalikuwa yakifanyikia ndani ya ofisi ya Dokta Shukuru na watu wote waliomsindikiza Neema walikuwa kwenye chumba hiko , na hivyo neno mpenzi lilisikika kwa kila mtu, Roma mwenyewe baada ya neema kumtambulisha kama mpenzi licha ya tofauti kubwa kati yao , alijikuta kipande cha mahaba kwa Neema kikiongezeka , hio ilikuwa na maana kubwa kwamba Neema alishamkubali moja kwa moja kama mwanamke wake na yupo tayari kuuwaambia ulimwengu anatoka nae kimapenzi.

Dokta Shukuru kwasababu alikuwa na heshima kubwa kwa Mheshimiwa Waziri , basi aliona afanye kama alichoomba Roma na alinyanyuka na kuwaambai wamfate nyuma mpaka ICU.

Muda ambao Roma anatoka na Neema , madaktari wengine walikuwa wakitoka kwenye chumba ambacho Mzee Chino alikuwa akifanyiwa matibabu.

Itifaki za kuona mgonjwa ndani ya chumba cha ICU zilifuatwa na Roma pamoja na Neema waliweza kuingia sehemu ambayo Mzee Chino alikuwa akifanyiwa matibau kilikuwa ni chumba ambacho kimezungukwa na mashine nyingi za kufanyia upasuaiji wa dharula , hakukuwa na mwanga mwingi Zaidi ya taa kubwa zilizofungwa hapo ndani.

Neema baada ya kuona hali ya Mzee Chino , Chozi lilimtoka kwa kuona huruma kwa hali aliokuwa nayo , kwani alikuwa amelazwa kifudifudi , huku majeraha ya Risasi yakiwa yameelekezewa juu.

“Naomba mniache mwenyewe na mgonjwa ,Neema utanisubiri nje baada ya nusu saa nitatoka”

“Mr Roma nimeweza kukuruhusu kumuona mgonjwa , lakini siwezi kukuacha ukabaki nae kwani sio utararibu na unaweza fanya jambo baya Zaidi likahatarisha afya yake Zaidi”Aliongea Dokta Shukuru na Roma alimwangalia Neema kama kumpa ishara na Neema baada ya kuangaliwa kwa namna hio na Roma, akili zake haraka haraka zilisafiri siku ya kwenye kusanyiko, namna ambavyo Roma alipigwa risasi mgongoni , lakini licha ya hivyo kuonekana hana tatizo lolote.

“Dokta mimi kama ‘Guardian’ wa mgonjwa wangu ninaomba umpatie Roma ruhusa ya kubaki na mgonjwa kwa muda wa nusu saa”Aliongea Neema Luwazo huku akionyesha kuwa siriasi kwa maneno ambayo ameongea.

Dokta Shukuru kwakuwa ndio aliekuwa ameongoza kumhudumia Mzee chino basi hakuwa na haja ya kukataa ombo la Mheshimiwa Waziri, licha ya kwamba alikuwa akikiuka taratibu za hospitali.

“Roma sijui unataka kufanya nini , ila nakuombea unachotaka kufanya kifanikiwe”Aliongea Neema na kisha akaungana na Dokra Shukuru na wote kwa pamoja walitoka wakimuacha Roma akibaki na mgonjwa.

Roma baada ya kubaki mwenyewe alianza kuchunguza chumba chote na kuangalia Camera zilizofungwa kwenye chumba hiko na hakupata tabu ya kuzitafuta kwani alitumia uwezo wake wa kihisia na kuzipata zote na alijikuta akitabasamu mara baada ya kugundua kuna Camera Zaidi ya zile ambazo zinaonekana.

Upande mwingine katika ndani ya hospitali hii katika chumba cha kuongezea Camera ,anaonekana Yan Buwen akiwa peke yake akiangalia Skrini ambazo zilikuwa zikionyesha moja kwa moja chumba ambacho alilazwa Mzee Chino.

Haikueleweka waongozaji Camera wengine wako wapi , lakini ni Dhahiri kwamba alitaka kuona kila kinachofanywa na Roma yeye peke yake , pasipo mtu mwingine kushuhudia.

Sasa alikuwa ndani ya chumba hiko kwa takribani lisaa limoja , tokea muda ambao Roma anapita anaongea na Dokta Shukuru , lakini pia Roma alivyoingia kwenye chumba cha IC?U alicholazwa Mzee Chino, Yan Biuwen alikuwa akiona kila kitu.

Ukweli Yan Buwen ndio ambaye aliagiza watu kumjeruh Mzee Chino , huku akiamini kwamba kama Mzee Chino atakuwa kwenye hatihati ya kufa na Roma akapewa taarifa hizo basi ni lazima angechukua hatua ya kumponya kwa kutumia damu yake , huo ndio mpango wa Yan Buwen , kutumia ukaribu wa Neema Luwazo na Roma ili kumponya Mzee Chino na baada ya hapo ndio damu ya Roma ipatikane ili akaweze kufanya Cloning na kutumia jiwe la Kimungu.

Sasa baada ya kuona Roma kaachwa kwenye chumba cha matibabu alijikuta akitabasamu mno,na kujiona kama mshindi na alijiambia mafanikio yake ndio yanakaribia..

“F****ck! Ameziharibu Camera”Aliongea Yan Buwen mara baada ya Skrini zote kuwa giza na kuonyesha chenga chenga.

Yan Buwen mara baada ya kuona Camera zimezima alivuta tarakishi iliokuwa pembeni na kisha baada ya kuifungua aliandika mistari kadhaa ya kodi kwenye tarakishi hio na baada ya dakika mbili tu , Mawasiliano ya Camera yalirudi na Roma alionekana ndani ya chumba alicholazwa mzee chino na Yan Buwen kutabasamu huku akijipiga piga kifuani kwa kujiona yeye ndio jiniasi.

“Hades unajifanya mjanja sana , ndio maana nime install undetected Camera”aliongea mwenyewe huku akikaza macho yake kwenye tarakishi yake.

Roma alionekana kuchukua bomba la Sindano ambalo halikuwa limetumika na kisha akachukua na Sindano na kuunganisha na lile bomba , baada ya kumaliza kitendo hiko alikunja shati lake la mikono mirefu mpaka kwenye kiwiko cha mkono na baada ya kumaliza alitafuta mshipa wa damu kwenye mkono wake na ndani ya dakika alionekana kuupata na kwa kutumia mkono wake wa kushoto aliweza kujidunga ile sindano huku akiwa amekuja ngumi na alivyoachia tu alianza kuvuta na bomba lile lilionekana damu ikiwa inajaa.

Kitendo kile kilimfurahisha mno Yan Buwen kiasi cha kurusha mikono juu kwa furaha , hakuamini jambo lake linakwenda kuwa rahisi hivyo , kwani kitendo cha Roma kutoa damu yake kwenye mwili ndio alichotaka.

Roma alifanya kitendo kile cha kujitoa damu na kisha damu yake kuingiza kwenye Dripu ya damu ambayo alikuwa ametundikiwa Mzee Chino , alifanya kwa Zaidi ya mara tatu mpaka alipoweka bomba na sindano chini,.

Baada ya kumaliza alimsogelea tena mzee Chino na akamshika kwenye mbavu zake huku akiwa amefumba macho , na alianza kuongea maneno ambayo hayakueleweka yalikuwa yakimaanisha nini , lakini ni kama vile mchungaji anavyomwombea mtu.

Kadri alivyokuwa akifanya vile , kupauka kwa Mzee Chino kulianza kupotea na sasa alikuwa akionekana kama mtu ambaye yupo usingizini , Roma baada ya kukamilisha zoezi lile alitoa bendeji zote zilizofungwa mgongoni na hapo ndipo alipoachia tabasamu baada ya kuona majeraha yake yalikuwa yakivutana kwa kasi mno , yaani nyama za mwili za Mzee Chino ni kama zilikuwa zikicheza cheza kwa kuvutana..

Neema Luwazo aliekuwa nje , alionekana kuwa na wasiwasi kweli licha ya kwamba alikuwa akiamini huenda Roma akaweza kufanya maajabu kwa Mzee Chino , lakini hata hivyo aliogopa jambo hilo kutokufanikiwa na ndio maana alikuwa akikaa na kunyanyuka.

Baada ya lisaa limoja mbele hatimae mlango wa chumba cha ICU ulifunguliwa na kufanya watu wote waliokuwa wakimsubiri nje kusimama, akiwemo Neema Luwazo, wakitaka kujua hali aliokuwa nayo Mzee Chino.







SEHEMU YA 314.

HONGKONG

Ni moja ya mgahawa mkubwa na maarufu sana ndani yajiji la HongKong ,mgahawa unaofahamikakwajina la Ling Sichuan King anaonekana mrembo Clark akiwa kwenye meza moja na mwanaume kwenye Kona ndani ya mgahawa huo, mwanaume huyo akiwa ni mzungu, mwanaume huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Edward kutoka ukoo wa Rothchild.

Huyu Edward ni yule aliekuwa akiambata na Malkia Catherine na tulimuona kule Ufaransa wakati akimleta Catherine katika chumba cha Roma kwa ajili ya ‘kunyanduliwa’.

Clark na Edward walionekana kuwa katika mazungumzo , huku wakijipatia nyama ya kopo , huku pembeni wakiwa na vinjwaji vya moto.

“Hades alikuwa na shida gani?”Aliuliza Edward huku akimwangalia mrembo Clark alievalia koti la manyoya aina ya leather , jaketi ambalo limtengenezwa na kampuni moja maarufu kutoka Italy.

“He is fine Edward , alikuwa na tatizo na lishaisha”Aliongea Clark .

“Nimesikia alikuwa Hokkaido kwa ajili ya mwanamke?”Aliongea Edward huku akimwangalia Clark usoni na Clark alitingisha kichwa kukubaliana nae.

“That isn’t good sign for you Clark”Aliongea Edward akimwambia Clark kwamba hio sio ishara njema kwake.

“That is none of your business I have said this before, I will decide myself on how I am getting along with Roma”

“Hio sio biashara yako , nishasema nitaamua mwenyewwe namna ambavyo nitakuwa naelewana na Roma”Aliongea Clark.

Unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba , alichokuwa akimaanisha Edward ni kwamba kitendo cha Roma kuongeza mwanamke mwingine ilihali kwa upande wa Clark hakuna maendeleo yoyote ndio alichokuwa akizungumzia na ndio maana akamwambia sio ishara njema kwa Roma kuongeza mwanamke mwingine ilihali kwake yeye kaachwa.

“Clark tatizo hujawahi hata kuongea nae juu ya hili swala , unafikiri ni kwa namna gani mahusiano yako na yeye yataimarika , kwa staili hio hauwezi kuuteka moyo wake na itafikia kipindi ushachelewa tayari hata kama ukichukua hatua”

“Hata kama mimi ndio daktari wake Edward na hatoweza kuniacha”Alijitetea Clark.

“Unafikiri ugonjwa wake usiporudi ataendelea kuwa na wewe, Clark unatakiwa kuelewa kwamba viongozi wa ukoo macho yao yote yapo upande wako kumteka Roma kihisia ili kuwa upande wetu”

“Edward katika ukoo nimechangia kwa kiasi kikubwa , kwanini natakiwa kuendelea kuishi kwa kutimiza malengo ya familia siku zote sio ya kwangu?”

“Clark unatakiwa kuelewa kwamba kwenye ukoo wetu wa Rothichild kuna Zaidi ya ndoa therathini mpaka sasa lakini licha ya hivyo damu yetu ya kifalme katika ukoo inazidi kupungua kutokana na miingiliano na makabila mengine ,tunachotaka sasa ni damu mpya katka ukoo wetu ambayo inachimbuko la kifalme moja kwa moja na macho yetu yapo kwa Hades na wewe ndio mwanamke pekee mrembo kwenye ukoo wetu ambaye unanafasi kubwa sana, urafiki wetu na Hades hautoshi bali akiwa mmoja kati yetu itakuwa rahisi Zaidi na hata makabila mengine hayatakuwa na nia ya kumsogelea na tutaendelea kuwa kabila kubwa ndani ya ulimwengu huu”Aliongea Edward kwa msisitizo.

“Edward najua wewe na Roma ni marafiki wa mudamrefu, je umekuwa na urafiki na yeye ili tu kupata faida kutoka kwake?”Aliuliza Clark.

“Ofcourse not , but other than being his friend , I am also a proud member of Rothchild clan, as well as a brother who hopes for his sister to be happy , Clark Stop being so cowardly ,this doesn’t look like you , you should confess to him since you love him, Even if he has Persephone as his wife and has other lovers at the same time ,it doesn’t mean you cant also be his love”

“Hapana , lakini licha ya kuwa rafiki yake , lakini pia mimi ni mwanaukoo wakujivunia wa Rothchild , lakini pia mimi ni kaka ambaye nataka dada yangu kuwa na furaha , Clark acha kuwa muoga , unaonekana kama sio wewe , unatakiwa kufunguka na kumueleza hisia zako kwasababu unampenda , hata kama anae Persephone kama mke wake lakini pia kuwa na wanawake wengine hii haimaanishi kwamba huna nafasi ya kuwa mpenzi wake pia”

“Edward nimechoka ninaondoka”Aliongea Clark huku akiinua mkoba wake na kuanza kupiga hatua kutoka nje ya mgahawa huo , lakini ile anakaribia kutoka alijikuta akigongana na mtu.

“Ooh!! Sorry”Aliongea mwanaume na kumuokotea mkoba wake Clark , sasa kitendo kile Edward alikiona na mtu aliekuwa mbele yake alikuwa akimfahamu sana kama moja ya mpishi namba moja duniani ambaye anamiliki pia mgahawa ambao walikuwa wakifanyia maongezi pamoja na migahawa mingine ndani ya China ,HongKong na Japani.

Mwaaume mwenyewe hakuwa mwingine bali alikuwa ni Poseidon , ambaye tulimuona kipindi kwenye siku ya kusanyiko la wafanyabiashara , mwanaume ambaye alimkamata Afshar Bahman.

“It`s okey”Aliongea Clark na kisha alichukua mkoba wake na kuanza kupiga hatua kutoka ndani ya eneo hilo pasipo kugeuka nyuma na Poseidon mara baada ya Clark kuondoka aliishia kumwangalia mpaka alipotokomea ndipo alipogeuza macho yake na kumwangalia Edward.

“Shemeji Edward kutoka Rothchild Family ni heshima kwangu umefanya mgahawa huu kama sehemu salama kutembelea hapa HongKong”Aliongea Poseidon mara baada ya kusogelea meza ya Edward.

“Mr Kelphin haina haja ya kuwa ‘humble’ kila mtu anatamani kuingia kwenye mgahawa wako ,na kwasisi ambao tunapesa siku zote tunajua hii ndio sehemu salama”Aliongea Edward na Poseidon ambaye sasa anafahamika kwa jina la Kelphin alitabasamu huku akiangalia nje.

“Niliona ulifanya makusudi kumgonga dada yangu”Aliongea Edward huku akitabasamu.

“Edward niseme tu nimetokea kuvutiwa sana na dada yako na ndio maana nilitanguliza neno Shemeji katika salamu yetu”Aliongea kwa Kingereza na kumfanya Edward kucheka.

“Macho yako yanaonyesha ,lakini nasikitika kukuambia kwamba moyo wake upo kwa mtu mwingine kabisa”Aliongea Edward.

“Unamaanisha moyo wake upo kwa yule mtanzania mpuuzi Hades?”Aliongea na Edward alitingisha mabega na Kelphin alitabasamu kwa kejeli.

“Koo zote za dunia hii mmekuwa mkitaka kuwa na ushirikiano na Hades kuliko sisi wengine ni kwanini?”

“Majibu yote yanajieleza Mr Kelphin ,ijapokuwa asilia yenu sio hapa duniani, lakini mkumbuke uwezo wenu ni mdogo pia , licha ya kwamba mmekuwa na uwezo mkubwa likija swala la kupambana lakini mchango wenu kwenye maendeleo ya dunia ni mdogo sana”Aliongea Edward

“Binadamu mnadharau sana lakini huyu Hades ambaye mnamuona wa maana nitamuua muda si mrefu”

“Ukifanikisha hilo siku moja, then dada yangu atakuwa ni wa kwako”Aliongea Edward huku akitabasamu na akanyanyuka baada ya kupiga mkupuo mmoja wa kinywaji chake na kumuacha Kelphin akiwa amekunja ngumi.

Hades labda usikanyage maeneo ya China , ukijichanganya siku hio nitakuonyesha sitojali tena the Stupid “ Gods Treaty’ lazima nikuonyeshe kwamba wewe ni binadamu na sisi ndio miungu”Aliwaza Poseidon huku akinyanyuka haraka haraka baada ya kumuona mzee flani wa kichina alietangulizana na mabodigadi akiingia hapo ndani na Kelphin alimsogelea yule mzee na kuanza kumkaribisha kwa kumuinamia kwa heshima kubwa.

Kwa maigizo aliokuwa akiyafanya Poseidon usingejua miaka Zaidi ya Elfu moja iliopita alikuwa akiabudiwa mpaka pale alipokuja Christ Pamoja na mtumbe Muhamad.

******

Ulikuwa mshangao mkubwa sana kwa madaktari wote waliokuwa wakimtibia Mzee Chino , na sio kwao tu hata kwa Neema Luwazo mwenywe alijikuta akishangazwa na jambo hilo ,licha ya kwamba hakujua Roma amefanyaje , lakini afya ya Mzee Chino iliimarikika kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba hata zile oksijeni ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye pua zake kuondolewa.

“This is more than Miracle”Aliongea Dokta Shukuru Omary kwa mshangao mkubwa huku akiamini kilichotendeka sio kwa uwezo wa kisayansi bali ni kwa uweza wa kimungu Zaidi na aliamini huenda Roma alikuwa nabii , kwani amekuwa ni moja ya watu ambao washawahi kusikia Habari za miujiza , ila kwa kuwa alikuwa ni mwanasayansi hakuwahi kabisa kuamini , lakini kwa tukio ambalo limefanyika ,kwake aliona ni ile miujiza ambayo siku zote alikuwa akiidharau.

Neema Luwazo baada ya kushuhudia afya ya Mzee Chino kutengemeaa kwakiasi kikubwa alijikuta akitoka haraka haraka ndani ya chumba hiko ili kumuwahi Roma aliemuacha nje kwa ajili ya kumpa shukrani , lakini ile anafika hakuweza kumuona tena na ilibidi awasogelee vijana wawili waliokuwa eneo la kusubiria.

“Allly Roma kaelekea wapi?”Aliongea Neema Luwazo mwanamama huyu ambaye licha ya kwamba alikuwa akionekana kuwa mtu mzima lakini hakuacha kuvutia kwa kila anaemtazama.

“Amesema anaondoka anamuwahi mke wake”Aliongea Ally na kumfanya Neema Luwazo kupumua mara baadaya kusikia Roma kaondoka na alijiambia atampigia simu kwa ajili ya kumshukuru , licha ya kwmaba alikosa namna nzuri kwenye kichwa chake ambayo aliamini inaweza kuielezea na kwa jinsi gani amegusw ana msaada ambao Roma kafanya kwa ajili yake.

“He is right person for me ,Roma I will always love you”Alifikiria Neema Luwazo mpaka pale aliposhituliwa na madakrari waliokuwa nyuma yake.

“Mheshimiwa kwa hali ya mgonjwa ilivyotengemaa naweza kusema kwamba tunayo kila sababu ya kuandaa upasauaji ili kuitoa risasi iliopo kwenye uti wake wa mgongo”Aliongea Dokta Shukuru.

“Atakuwa na asilimia ngapi za kupona baada ya upasuaji huo?”Aliuliza Neema na Dokta shukuru akatabasamu.

“Shukrani ziende kwa mpenzi wako , nimeshangazwa sana na kilichotokea na mpaka hapa naweza kusema kwamba mafanikio yatakuwa ni Zaidi ya asilimia themanini”Aliongea kwa furaha na Neema Luwazo alitingishwa kichwa kukubaliana na madaktari.

Upande mwingine ndani ya chumba ambacho amelazwa Mzee Chino alionekana daktari mmoja wakihindi akimtoa damu mzee Chino na kuihifadhi kwenye kijichupa , alionekana kufanya haraka haraka mno , baada ya kutoa damu kwemye mkono, aligeukia Drip ambayo ilikuwa na kiasi kidogo cha damu iliokuwa ikiingia kwenye mwili wa mgonjwa na alitumia sindano na kuifyonza yote na akaihifadhi kwenye kijichupa kingine na baada ya zoezi lake kukamilika alichukua vile vijichupa viwili vyenye damu na kuweka kwenye koti lake na kutoka.

Dokta huyu hakushitukiwa kutokana na kwamba alikuwa ni moja ya madaktari ambao walikuwa wakimfanyia matibabu mzee Chino , hivyo wakati wenzake wanatoka yeye aliachwa ndani.

Dakika kama tano mbele wakati Neema Luwazo akiwa ndani ya ofisi ya Dokta Shukuru , upande wa maegeshoni dokta yule mhindi alisogelea gari moja aina ya V8 na kuingia ndani upande wa dereva na hapo ndio anaonekana Yan Buwen alieketi kwenye gari hilo akiwa hana wasiwasi kabisa.

“Hii hapa Mr Yan Buwen”Aliongea yule daktari na Yan Buwen alitabasamu na kupokea vile vijichupa.

“Kazi nzuri Dokta Jamshid, Mstaafu ataingiza kiasi cha pesa kama mlivyokubaliana”Aliongea Yan Buwen na Jamshid alitingisha kichwa na kisha akatoka kwenye gari hilo.

Yan Buwen baada ya kuangalia damu ile kwenye vile vijichupa alijikuta akiachia tabasamu flani hivi la kukera na kisha akawasha gari kwa mbwembwe kama zote.

“Kazi yangu hapa Tanzania imeanza , mrembo wangu The Doni muda si mrefu utanikubali kwa kitu ambacho ninakwenda kutengeneza “Aliwaza yan Buwen kwenye kichwa chake na dakika mbili mbele alitoa gari lake kabisa na kuingia barabarani.





SEHEMU YA 315.

Siku hio hio ya ijumaa ndani ya ofisi ya mrembo Edna , alionekana Amiri akiwa katika maongezi na Boss wake na maongezi hayo yalionyesha kuwa muhimu Zaidi kwani kuna muda Amiri alikuwa akimpatia baadhi ya karatasi na Edna alizisoma na ambapo hajaelewa ,Amiri alikuwa akipatolea maelezo.

Kitu ambacho Amiri alikuwa akimwabia Edna ilikuwa ni swala juu ya mkataba wa kibiashara uliovunjwa na serikali ya Jamhuri pamoja na kampuni yake juu ya ujenzi wa jengo la Bima ya Taifa miaka kadhaa nyuma.

Katika maelezo ambayo yalitokana na uchunguzi uliofanywa na Amiri akishirikiana na kikundi chake cha Athena , alibaini kwamba Innova haikuwa kampuni ya ujenzi wa magorofa , hivyo ni kama haikustahili kupewa tenda ya kumalizia jengo la Bima mara baada ya serikali kuvunja mkataba.

Amiri aliweza kumuonyesha Edna baadhi ya kazi ambazo zilikuwa zikihusiana na kampuni ya Innova na kwa maelezo hayo ilionyesha Dhahiri kabisa kwamba kampuni ya Innova haikuwa na uhusikaji wowote na ujenzi wa majengo.

“Kama hii kampuni inajihusisha Zaidi katika maswala ya utafiti wa kisayansi waliwezaje kupata tenda kutoka serikalini?”Aliuliza Edna

“Boss kilichofanyika kwa Innova ilikuwa ni kufungua kampuni ya kwenye makaratasi(Shell Company) , kampuni ambayo imesajiliwa kama ya ujenzi ambayo ipo chini ya uongozi wa taasisi ya Innova na hio kampuni ndio iliosaini mkataba wa umaliziaji wa jengo la Bima ya Taifa, lakini jambo la kufurahisha ni kwamba nina ‘data’ nyingine ambazo tulizichambua na kugundua huenda kuna Zaidi ya ujenzi uliokuwa ukikusudiwa kufanyika ndani ya jengo la Bima ya Taifa na ndio maana serikali ikavunja mkataba”

“Sababu zipi?”Aliuliza Edna na . Amiri alitoa karatasi na kumpatia Edna.

“Hayo ndio makubaliano ambayo Boss Raheli aliingia na serikali baada ya mkataba wa ujenzi na Vexto Construction kuvunjwa na hii ya pili ni karatasi ya pesa iliolipwa kwa ajili ya kuvunja mkataba”Aliongea Amiri na kumpatia karatasi za aina mbili Edna na akaanza kuzisoma na alijikuta akitoa macho.

“Why the government were this desparate?”Aliuliza Edna kwani serikali ililipa fidia kubwa mno kwa ajili tu ya kuvunja mkataba.

“Boss hilo ndio swali ambalo na sisi tulijiuliza kwanini walikuwa wakitaka kuvunja mkataba kwa namna yoyote ile , jambo la pili mkataba huu haukuvunjwa na Wizara bali ni mheshimiwa raisi mwenyewe ndio aliehusika, kwa maneno marahhisi maamuzi yote yalifanyikia ikulu na hata Boss Raheli alisaini ‘Breach of Contract’ na serikali akiwa Ikulu”Aliongea Amiri na Edna alikagua sahihi na kweli ilikuwa ni sahihi ilioasaniwa na Mheshimiwa Mstaafu Kigombola.

“Boss angalia pia na hii taarifa”Aliongea Amiri na kisha akampatia Edna karatasi nyingine na Edna alianza kuisoma kwa umakini , ilikuwa ni kaatasi iliokuwa ikionyesha pia kwamba licha ya kampuni ya Innova kuwa taasisi ya maswala ya kiutafiti lakini pia ilikuwa ikihusika na ujenzi wa ‘Laboratory facilities’ , na karatasi hio ilikuwa ni maelezo ya kina namna ambavyo Innova iliweza kuingia mkataba na kujenga maabara ya kiututafiti nchini Canada , maabara ambayo inamilikiwa na kampuni ya Maya.

Edna licha ya maelezo hayo aliona bado swala ambalo anataka kulifikia lilikuwa mbali, alikuwa akitaka kusikia ni kisasi gani ambacho mama yake alikuwa nacho mpaka kumwachia Flash ambayo ilikuwa na orodha ya makampuni mengi ndani ya Tanzania huku moja ya kampuni kubwa ikiwa ni Maya Group.

“Boss hitimisho ambalo tumeweza kufikia moja kwa moja ni kwamba katika kampuni ya Innova ilifanya ujenzi wa maabara ndani ya jengo la Bima ya Taifa na baada ya ukamilishaji wa ujenzi huo ndio wakaingia mkataba na Maya constructor kumalizia ujenzi wa jengo upande wa juu hivyo ninaamini sababu ya kampuni ya Vexto kutolewa kwenye mkataba wa ujenzi na serikali huenda ni kwa ajili ya kulinda siri ya maabara hio”Aliongea Amiri na Edna alifikiria kidogo.

“Amiri vipi kuhusu taarifa ya Dokta Hubery juu ya kifo chake?”aliuliza Edna na Amiri alinyamaza kidogo na kuonyesha sura ya huzuni kidoo.

“Tumejaribu kufatilia ndani ya familia yake na tumeweza kupata kugundua ni kweli alikuwa na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao?”Aliongea Amiri na Edna alikubali kwa kichwa.

“Amiri nashukuru kwa kazi kubwa mnayoifanya, kwasababu kazi ambayo niliwapa ni kujua kwanini kampuni yetu ilitolewa katika mkataba wa ujenzi wa jengo la Bima imekuwa na majibu ya kuridhisha, sidhani kama kuna faida ya kuendelea kuchimba Zaidi , kwani naamini jambo hili linaweza kuleta matokeo hasi kwa kampuni”Aliongea Edna na Amiri alielewa boss wake anachoongea.

Dakika kadhaa baada ya kupita baada ya Amiri kutokandani ya ofisi yake , Edna alimpigia simu Monica kumuita Benadetha ofisini kwake na ndani ya dakika tano tu , Benadetha alionekana akiingia ndani ya ofisi ya Edna.

“Boss nimeitikia wito”Aliongea Benadetha na Edna pasipo ya kubadili muonekano wake alivuta bahasha kwenye mtoto wa meza na kisha akamnyooshea Benadetha na vile anataka kuichukua Edna alirudisha mkono nyuma.

“Benadetha nakupatia hii Document uihifadhi kama mkuu wa idara ya Public Relation, ni nyaraka muhimu sana kwa kampuni ,imejaa mipango yote ya kampuni ya miaka mitano ijayo, nyaraka hii ikifika mikononi mwa makampuni ambayo ni washindani wetu wa kibiashara jua kwamba kampuni itaingia matatizoni”Aliongea Edna na kisha akamnyooshea Benadetha ili aichukue na mwanadada huyo kwa kutetemeka aliipokea , hakuelewa kwanini Boss wake alikuwa akimwamini na nyaraka muhimu namna hio.

“Nitaihifadhi vizuri boss”

“Okey unaweza Kwenda ni hayo tu niliokuitia”Aliongea Edna na Benadetha aliitikia kwa heshima na kisha kutoka.

“Benadetha…!!!”Benadetha ambaye alikuwa akiikaribia Lift alijikuta akigeuza macho nyuma mara baada ya kusikia jina lake linaitwa , aliemuita alikuwa ni Ernest Komwe CEO msaidizi wa kampuni ya Vexto.

“Naam!!”Aliitikia Benadetha kwa upole na Ernest Komwe alitabasamu , huku akimsogelea.

“Nimekuona unazikaribia lift ndio maana nikakuita tushuke wote , mimi naelekea Chini”Aliongea Ernest Komwe kwa bashasha huku akitabasamu na Benadetha na yeye alitabasamu na wote kwa Pamoja waliingia kwenye Lift macho ya Ernest Komwe muda wote yalikuwa kwenye nyaraka alioshikilia Benadetha.

“Benadetha kesho wikiend utakuwa na ratiba gani?”

“Mh! Mara nyingi wikiend naenda Beach kupunga upepo”Aliongea Benadetha.

“Na boyfriend wako?”

“Haha… sijui nisemeje ila naendaga mwenyewe”Aliongea Benadetha na Ernest Komwe alitabasamu.

“Kesho unaonaje nikikusindikiza nina siku nyingi sijaenda baharini , tukiwa wote itakuwa vizui Zaidi , isitoshe sio mwenyeji sana wa Tanzania”Aliongea Ernest na Benadetha alikubali kwa kichwa.

Dakika chache mbele Ernest alionekana akiongea na simu eneo la mapumziko chini kabisa ya jengo hili la kampuni.

“Boss nafikiri nishapata namna ya kuyumbisha hisa za kampuni, kuna Audio nimekutumia kupitia mtandao wa Watsapp”Aliongea .

“Ngoja niisikilize”Sauti upande wa pili ya mwanamke ilisikika na palepale simu ilikatwa na Ernest alitabasamu huku akinywa kidogo soda ya Pepsi ilio kwenye kopo na kabla hata hajamaliza soda yake simu iliita na alipokea mara baada ya kuona jina ni Boss.

“Hilo faili linaonekana kuwa muhimu pia kwa kampuni , licha ya kwamba ninachotaka ni Zaidi ya hiko”

“Boss napaswa kufanya nini?”

“Hilo sio swali , hakikisha unaipata hio nyaraka na mtafute Matilda na atajua cha kufanya”Aliongea mwanamke aliekua kwenye simu na Eresti Komwe aliitikia na kisha simu ilikatwa,

******

“Wife jumapili Mzee Kweka anataka tukamtembelee, unaonaje ukinisindikiza wewe na Lanlan”Aliongea Roma muda wa usiku baada ya kumkuta Edna akiwa amekaa kwenye masofa akiangalia taarifa ya Habari ITV.

“Sawa!!”Alijibu Edna pasipo hata ya kufikiria na Roma alitabasamu na kumsogelea.

“Halafu babe unapaswa umsikilize mdogo wako jinsi anavyo imba , Sophia ana kipaji kikubwa sana na namtabiria kuwa mwimbaji mkubwa”Aliongea Roma huku akikaa karibu na Edna na kupitisha mkono kwenye kiuno chake na kumfanya Edna aangalie mkono wa Roma jinsi ulivyotokeza upande wa pili.

“Mhmh sijamsikiliza , ila mama yake alishaniambia kama anakipaji cha kuimba na aliniomba nimsapoti”Aliongea Edna huku akijikausha akiacha mkono wa Roma uliokuwa ukimtekenya , lakini wakati huo huo akiomba mama yake na Roma asijitokeze hapo sebuleni kwani kitendo anachofanya Roma ni cha aibu..

Sasa Roma baada ya kusikia Edna akimtaja mama yake Sophia ni kama alikumbuka kitu , alikumbuka siku aliomdanganya Edna kama Sophia alikuwa mdogo wake waliotoka nae Marekani , lakini pia alikumbuka siku ambao Sophia alimwambai kwamba Edna alikuwa anajua wamemdaganya na Roma hakuwahi kuzungumza swala hilo na mke wake na pia hakuwahi kumuuliza Sophia waliyamaliza vipi na dada yake.

“Halafu mke wangu kwanini uliamua kujikausha mara baada ya kujua siku ile nilikudanganya?”Aliongea Roma na Edna alishika mkono wa Roma uliomshika kiuno na kuutoa na kisha akaegamia vizuri sofa.

“Kwaho ulitaka nije nianze kukulalamikia kwanini wewe na Sophia mlinidanganya , kwanza kwa taarifa yako nikueleze tu mama yake na Sophia alishaniambia kila kitu mlichopanga na balozi ila niliamua kukaa kimya”Aliongea Edna na kumfanya Roima kushangaa.

“Kakuambia nini Balozi?”

“Sophia alikuja kuishi na sisi kwasababu gani kuwa mkwel?”Aliuliza Edna, sasa wasichokujua ni kwamba Sophia pia alikuwa amesimama nyuma yao.

“Balozi alitaka nimfanye Sophia mke wangu wa pili , ila sikukubaliana nae ndio akaniomba niishi na Sophia kwa muda”Aliongea Roma bila kumungunya maneno.

“Sister Edna…!!!”Aliiita Sophia na kukimbia kupiga magoti mbele ya Edna na Roma na kumfanya Edna kushangaa kwani Sophia pia alianza kulia kwa kwikwi
ITAENDELEA SIKU YA JUMANNE.
wATSAPP CONTANCT:0687151346
 
huku Yan Buwen kapata damu ya hades, kule Anthena keshaanza kucheza karata zake na Dorisi, ........ aisee hii kitu inakoelekea sijui
 
Ewhuuu! I've succeeded to catch up with you. I started reading this stuff 4 weeks ago. Congrats to me, but more congrats to the author- Your majesty Singanojr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…