Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Daaaah!!!,, apo afadhari, sas ngoja 2one ka ROMA atachangamka mda huu, kwakua ameanza kupata SIRI alizokua azijui apo mwanzo.....
 
Akhsante sana mkuu, acha tu nije whatsapp
 
[emoji119]nitarudiii
 
SEHEMU YA 331

Zawadi ambayo Edna amemletea Roma ilikuwa simu ya Sumsung Galaxy S23 Ultra iliotengenezwa na madini ya Gold ,ni simu ambayo Edna aliweza kuinunua kwa spesho oda ya kiasi cha shilingi milioni tano, zawadi haikuwa moja tu lakini pia Edna alikuwa amemnunulia Roma Saaa ya Patek Phillipe saa ambayo ilimgharimu dollar elfu therathini na mbili za Kimarekani , ukizileta kibongo bongo ni Zaidi ya milioni sitini, hizo ndio zawadi ambazo Edna alimletea mume wake.

“Ushakuwa Diector wa kampuni sasa haileti picha nzuri kuendelea kutumia hio simu yako ya batani, mwonekano na biashara vinaenda sambamba”Aliongea Edna akimkabidhi Roma zawadi ambazo amemletea.

Roma kwa mara ya kwanza alikuwa akipokea zawadi kutokakwa mwanamke , , ukweli alikuwa na mahusiano na wanawake wengi katika historia yake , lakini hakuwahi kuzawadiwa zawadi ya saa , siku zote yeye ndio aliekuwa akitoa zawadi kwa wanawake wote.

“My Babe Wife nikajua hunipendi mumeo , kumbe una mahaba mazito kiasi cha kunikumbuka na kuniletea zawadi, Lanlan inaonekana licha ya mama yako kukupenda lakini na mimi pia ananipenda”Aliongea Roma na kumfanya Lanlan kumwangalia mjomba wake kwa macho ya wivu.

“Lanlan ulipanga nini na Anko?”Aliuliza Edna baada ya kumuona Lanlan kuonyesha wivu kwa Roma na ilibidi amwambie kile ambacho walipinga wakati wakiwa uwanja wa ndege na Edna Edna alijikuta akitabasamu na kisha kumwangalia Roma.

Ukweli Edna kwa mara ya kwanza alivyokuwa safarini nchini Hongkong alijawa na hamu ya kurudi nyumbani , mrembo huyu alijiona kama mwanamke ambaye alikuwa na sababu ya kuishi , mwanzoni kabla ya kukutana na Roma Maisha yake yote aliyaelekeza katika kuendesha kampuni aliaochiwa na mama yake pamoja na bibi yake , lakini miezi hii kadhaa alijikuta akiwa na sababu nyingine ambayo inamfanya kutamani kurudi nyumbani mapema na sababu hio ilikuwa ni uwepo wa Lanlan kwenye Maisha yake , lakini pia uwepo wa Roma.

Kwenye ndege mrembo huyu alikuwa akiwaza kwa mfano akiachana na Roma ni mwanaume gani ambaye anaweza kuishi nae na akamvumilia, Edna alijiona licha ya kwamba ni kweli ni mrembo na anaweza kupata mwanaume yoyote , lakni aliamini kutokana na staili yake ya Maisha, Kiburi cha kurithi na madhaifu aliokuwa nayo likija swala la mahusiano, lakini pia hofu ya kutopata mapenzi ya kweli kutokana na utajiri wake , aliona Roma ndio mtu sahihi wa kumfaaa, kwani licha ya kwamba hakuwa akimjali kama mume lakini mwanaume huyo alikuwa akimjali na muda wote yupo kwa ajili yake, lakini licha ya kuona Roma ndio mtu anaendana nae kutokana na yeye mwenyewe alivyo, aliamini siku ambayo atamkubali kabisa Roma kama mume na kuanza harakati za kutengeneza familia anapaswa kukubali pia wanawake wake wengine , kwani kwa jinsi alivyomuona Roma , lakini pia matendo yake kwa michepuko yake hakukua na dalili ya kuwaacha wanawake hao na alijiambia njia ni moja aidha ni kuwakubali huku akiendelea kuwa kama mke wa Roma au awafanye wao wenyewe wamuache mume wake , sasa Edna alikuwa akiwaza yote hayo kwa wakati mmoja katika safari yake ya kurejea Tanzania.

Inabidi nibadilike kidogo niwe angalau namuonyeshea kumjali”Aliwaza Edna kabla ya kuvaa mkanda wa ndege mara baada ya tangazo la kuvaa mikanda kutolewa kwani ndege ndio inakaribia kutua ndani ya uwanja wa mwalimu Nyerere.

Upande wa Mage licha ya kwamba mara nyingi hakuwa akionana na Roma , lakini sio kama hakuwa akimmbuka , mrembo huyu kila siku alikuwa akimkumbuka nakutamani sana kumuona na hata kurudia kile ambacho walikifanya kule kambi ya jeshi , lakini kutokana na kwamba hakutaka Edna kufahamu kwanza alichokianzisha na Roma , hivyo alijitahidi kutoenda nyumbani kwa Roma na kujiweka bize.

Upande wa mama yake Mage , yaani Mama T alikuwa akimlazimisha Mage kumwambia ni mwanamme gani ambaye alikuwa akitoka nae kimapenzi , mama huyu alikuwa akimtaka Mage kumwambia jina, lakini pia kumkaribisha huyo mwanaume kwenye familia ili wote wamuone , upande wa Kanali Tobwe licha ya mke wake kujawa na shauku ya kumtaka kumjua mwanaume alienzisha mahusiano na mtoto wake Mage , yeye alibakia kimya , aliona sio muda sahihi wa kumuelezea kile ambacho anajua , hivyo hivyo pia kwa Magdalena alikaa kimya, hivyo kumfanya Mama huyo kuwa mtu pekee ambaye hakuwa na uelewa na kile ambacho kilikuwa kikiendelea.

Mage alimuahidi mama yake kwamba atamtambulisha mwanaume huyo kwake siku ishirini zijazo na mama huyo alijikuta akiridhika, Mage alimuahidi mama yake hivyo kutoka na kwamba alikuwa akijua mkataba wa ndoa kati ya Edna na Roma unaisha wiki kadhaa zijazo , hivyo aliamini baada ya siku hizo kutimia atakuwa na haki ya kumfanya Roma kuwa mpenzi wake kamili.

Naam zikawa zimepita siku tatu yaani ijumaa , jumamosi na jumapili , katika siku hizo tatu hakuna kikubwa kilichotokea Zaidi ya Roma kumtembelea Dorisi na Rose.

Dorisi licha ya kukutana na mwanamke anaefahamika kwa jina la Clelia Allsanto hakumueleza jambo hilo Roma kabisa , ukweli alikuwa akiogopa mikwala ya yule mwanamke juu ya kukutana kwao kuwa siri na ndio maana hata Roma alivyofika nyumbani kwake kumtembelea alifanya jambo hilo kuwa siri yake, licha ya kwamba nguvu iliokuwa ikimtaka kumuelezea Roma kilichotokea kuwa kubwa.

Edna pia alionekana kuchangamka kidogo tokea alivyorudi Hongkong na kumfanya Blandina kufurahi, siku ya jumapili Edna kwa mara ya kwanza kwa hiari yake alimpakulia chakula Roma pamoja na mtoto wake wa hiari Lanlan , jambo ambalo lilimfurahisha sana Roma na kuona mke wake ashaanza kulegeza uzi.

Asubuhi ya siku hio Edna akiwa anaelekea kazini kichwani kwake alikuwa na mpango ikifika muda wa chakula cha mchana aende kumtembelea Roma ili wakapate Lunchi pamoja.

Edna alijiambia huo ndio muda mzurri wa kuweka ukaribu na Roma mume wake na alikuwa akiwaza kufanya mengi Zaidi ya kula chakula na Roma , alipanga kwenye kichwa chake kumuweka Roma bize kwa kuwa nae kila muda na ndio maana asubuhi hio wakati akiondoka kuelekea kazini alijiambia hatua ya kwanza mchana wa siku hio ni Kwenda kwenye kampuni ya Roma kwa ajili ya kupata nae chakula cha mchana.

Upande wa Roma alitoka akiwa ameambatana na Sophia kuelekea kazini , Sophia alikuwa akichukua mazoezi pamoja na kurekodi baadhi ya nyimbo zake kwenye studio za kampuni.

Roma baada ya kutia mguu ndani ya jengo la kampuni alipokelewa kwa salamu na Wendy pamoja na Daudi, wafanyakazi hao walikuwa wakimuona Roma sio mtu wa kawaida kabisa , kwani kitendo cha kuweza kuwa na koneksheni na Msanii bora duniani, Christine, halikuwa jambo la kawaida.

Roma baada ya kupewa maelezo ya hapa na pale na Daudi , pamoja na kusaini baadhi ya nyaraka hatimae alitoka nakuelekea kwenye Floor ambayo ndio kuna Studio za Tv Chaneli yao , Floor ya mwisho kabisa juu.

Roma alifanya ukaguzi na kuridhishwa , lakini jambo pia ambalo lilimfanya kufurahi ni mara baada ya kampuni yake kupata kibali cha kurusha matangazo kutoka TCRA.

“Boss Kesho ndio siku ambayo tunategemea kuanza kurusha matangazo, ofisi ya HR tayari washaweza kufanyia usaili watangazaji wenye ubobevu wa hali ya juu”Aliongea Daudi kwa Kingereza na Roma alitingisha kichwa kukubaliana nae.

Saa sita kamili Roma akiwa ndani ya ofisi yake hio kubwa ya kisasa , akiendelea kucheza game , aliingia Daudi akiwa na karatasi mkononi.

“Director , the secretary whom you want to interview is waiting outside now, Do I let her in now?”

“Mkurugenzi , Sekretary ambaye unataka kumfanyia usaili ameshafika na yupo nje sasa hivi , je ni mruhusu aingie?”Aliongea Daudi.

“Unamaanisha nini kuhusu Sekretary na usaili?”Aliongea Roma huku akiwa ni mwenye kushangaa , kwani hakuwa na taarifa za maswala ya usaili.

“Ooh kwaho huna hio taarifa , lakini mbona ofisi ya muajili imesema wewe ndio umemchagua mwenyewe kutoka kwenye orodha ya majina yalioletwa ofisini kwako?”

“Daudi unaongea vitu ambavyo havipo , sijawahi kuhitaji Sekretari na juu yayote ofisi ya muajili sijawahi kufika”Aliongea Roma huku akiwa ni kama mtu wa kupotezea swala hilo.

“It doesn’t matter now , Director I would advise you to meet the interviewee, the Lady isn’t an ordinary person..”

“Director nashauri umuone kwanza mtu mwenyewe kwani ni mwanamke ambaye sio wa kawaida..”Aliongea Daudi huku akikosa utulivu ni kama anachoongea hana uhakika nacho,. Roma alifikiria kidogo na kisha akampa ishara ya kumruhusu aingie nakumfanya Daudi kupumua kwa nguvu , alionekana ni kama mtu alietua mzigo na alitoka ndani ya ofisi hio kwa ajli ya kumkaribisha mtu huyo ndani ya ofisi ya Roma .

Roma alijikuta akipumua huku akiegamia kiti mara baada ya kugundua mtu aliekusudiwa alikuwa ni mrembo Amina.

Upande wa Amina alijifanyisha kama mtu ambaye hakuwa akimfahamu Roma na alifunga mlango na kisha alitembea mpaka karibu na meza ya Roma.

“Director Roma ,I’ m the new applicant for the secretary position , My name is Amina Kanani”

“Mkurugenzi, Mimi ndio mwombaji mpya wa nafasi ya usekretari , nafahamika kwa jina la Amina Kanani”Aliongea Amina huku akimkonyeza Roma kiaina.

“Mpenzi wangu Amina, ni mpango gani unapanga tena ?”Aliongea Roma na kumfanya Amina kutabasamu , huku akizungusha macho kukagua ofisi ya Roma na kisha alianza kutembea kimadaha mpaka karibu kabisa na meza ya Roma.

“This time ,I’m for real , I came to look for job”Aliongea Amina na Roma alitabasamu na kumpa ishara Amina ya kumuinamia ili ambusu shavuni na Amina alitabasamu na kisha alimsogelea na kumbusu Roma na midomo yake miekundu ambayo imepakwa Lipstick na Roma alitumia mkono wake wa kushoto na kufinya pua ya Amina.

“Ouch!”

“Nani kakuruhusu unifinye, ijapokuwa mimi ni mchepuko tu , lakini pia nina heshima zangu, huruhusiwi kunifinya”Aliongea Amina kwa kulalamika.

“Unaongea nini sasa, unataka kuniongezea matatizo Zaidi na niliokua nayo, Eti Amina baba yako anamiliki makampuni mengi tu hapa Tanzania , kwanini unakuja kwenye kampiuni yangu kwa ajili ya kutafuta kazi , mrembo kama wewe mwenye mzazi mwenye pesa ulitakiwa kuwa nyumbani na kula Maisha na sio kuja kufanya kazi hapa , au unataka kuutangazia umma kwamba unatoka na mimi mume wa mtu kimapenzi”

“Mbona unazungumza sana kuhusu Mapenzi , nimekuja kuomba kazi mimi, halafu kuna ubaya gani watu wakifahamu , au ndio unamuogopa mkeo”

“Acha kuongea mambo ambayo hayapo , hebu niambie kweli , umekuja kufanya nini?”

“Ni kweli nimekuja kutafuta kazi , siwezi kuishi bila kazi na kula na kulala tu kama nguruwe , zamani nilikuwa na kazi yangu na nilikuwa nikijihudumia pasipo kumtegemea baba , lakini kwasababu nilishaacha kazi yangu ya utanganzaji na siwezi kurudi tena , ni bora ukanipa kazi nikafanya , sijisikii kabisa kujihusisha na biashara za baba”

“Lakini kuna kampuni nyingine unaweza kuomba kazi na kwa koneksheni za baba yako ingekuwa rahisi , kwanini hapa?”

“Dear don’t you know how many men out there are trying to get close to me , a wealthy woman?”

“Mpenzi haufahamu ni wanaume wangapi huko nje wanataka kunipata , mwanamke kama mimi ambaye ni mtoto wa Tajiri?” Roma alishangaa kidogo huku akielewa pointi yake.

“Kwahio ukatumia koneksheni zako ukawasiliana na ofisi ya mwajiri na kujipangia usaili ili kuwa secretary?”

“Ndio ilinibidi kupitia hatua za kawaida mpaka kupata kazi , japo ya kutumia koneksheni , lakini kama hutaki nikifanya kazi kama secretary wako unaweza kunipangia kazi nyingine , ninaweza kusafisha vioo na kufagia na kudeki kama unamwogopa malkia wako kukasirika , ninachotaka ni kuwa karibu na wewe hivyo naweza kufanya chochote”Roma alijikuta akikosa namna ya kumkatalia mwanake aliekuwa mbele yake , ni kweli kabisa mrembo huyu alikuwa ameacha kazi yake n ani jambo la kawaida kway eye kutafuta kazi nyingine ya kufanya ka hapa nchini.

“Unaweza kweli kuwa secretary , unauzoefu na kazi hii?”

“Hehe.. Mpenzi nadhani umesahau kwamba nimesomea mambo ya uandishi wa Habari na nimeshawahi kuajiliwa na kampuni kubwa kama BBC, isitoshe kampuni yako pia inajihusha na maswala ya habari na burudani, sitaki kuwa mtangazaji bali nataka kukusaidia kutokana na uzoefu wangu na hilo linawezekana kama nitakuwa Sekretary wako”Aliongea Amina.

“Lakini mbona unaongea kama vile unataka kuwa CEO na sio usekretary?”Aliongea Roma huku akitabasamu kifedhuli.

“”My Dear Boss haven’t you heard off saying”

“Boss Wangu mpendwa haujawahi kusikia msemo mmoja maarufu?”

“Msemo gani?”

“The Secretary does the work while the boss..”

“Sekretari ndio anafanya kazi wakati boss..”

“The Boss Does the Secretary”

“Boss anamfanya Secretary”Aliongea Roma akimsaidia Amina kumalizia Sentensi yake. Huku akimeza mate , akianza kumkagua Amina mavazi ya kiofisi aliovalia , alijiambia kweli mrembo huyu anapaswa kuwa secretary kwa muonekano wake , kwanza ni boss gani anaweza kumkataa mrembo kama huyo kutokuwa secretary dunia hii.

“Kwahio Boss nimefaulu usaili?”

“Ndio lakini kuna jaribio la mwisho”Aliongea Roma huku akiegamia kiti chake.

“Matokeo mazuri yanatokana na majaribio mengi, Sekretari Amina tunatakiwa kufanya majaribio namna ya kazi yako inavyotakiwa kuwa”Aliongea Roma kifedhuli huku akisimama na kumsogelea Amina na ile anamkaribia alimvutia kwake huku akiwa ameshika kiuno na kumfanya Roma kufurahishwa na harufu nzuri ya manukato iliokuwa ikitoka kwenye mwili wa Amina.

“Siwezi kujizuia kwa kula nyama ambayo imejileta mwenyewe mdomoni mwangu ,Baada ya kazi tutaenda kula chakula cha mchana.”Aliongea Roma na kumfanya mrembo Amina kupitisha mikono yake kwenye shingo ya Roma na kisha akambusu kwa mara nyingine shavuni.

“Then should I call you Babe or Boss?”Aliuliza Amina.

“Kwahio niwe nakuita Babe au Boss?” Roma baada ya kuulizwa swali hilo kwa spidi ya hali ya juu alimnyanyua juu Amina na kumpandisha kwenye meza huku akimbana, lakini kabla hajaendelea na alichokuwa amekudida mara mlango uligongwa.
 
SEHEMU YA 332

Roma baada ya kusikia kugongwa kwa Mlango aliishia njiani na kisha akampiga Amina kibao kwenye makalio na kisha akamwambia ajiweke sawa nywele zake ambazo zimechanguka changuka.

Amina alielewa somo na haraka haraka alijiweka sawa na kisha akasimama kama Sekretary kweli karibu na meza ya Roma.

“Please Come in”Aliongea Roma na palepale mlango ulisukumwa taratibu mpaka ukawa wazi, Sasa sura ambayo ilikuwa mbele yake Roma hakuwa ameitegemea kabisa muda huo .

Ni mrembo alievalia suti ya ugoro , blazia nyekundu kwa ndani pamoja na viatu aina ya ya High Heels rangi nyeupe, nywele zake ndefu akiwa ameziachia pasipo ya kuzifunga na kibanio.

Edna alieshikilia mkoba wa rangi nyeupe , aliingia ndani ya ofisi ya Roma, na baada ya kuingia na kufunga mlango macho yake makavu yasio na utani yalitua kwenye sura ya Roma pamoja na Amina na baada ya kumwangalia Amina vizuri ni kama ukauzu aliokuja nao uliongezeka mara mbili.

Roma mapigo ya moyo ni kama yalikuwa yamesimama kwa sekunde alijiambia ni jambo gani la bahati mbaya kama hili linatokea , kwanini ghafla tu ajitokeze bila taarifa , ameanza lini kuja kwenye ofisi yake.

Amina alijikuta palepale akigundua mtu aliekuwa mbele yake ni Edna mke wake Roma , ijapokuwa ni mara chache sana Edna kuonekana kwenye jamii lakini kutokana na familia ya baba yake alishawahi kumuona hapo kabla licha ya kwamba hakuwahi kuoongea nae.

Edna pasipo ya kukaa chini alimwangalia Amina kwanzia juu mpaka chini , Ijapokuwa Edna alikuwa mzuri kuliko yeye mwenyewe , lakini Amina aliogopeshwa na ukauzu aliokuwa nao Edna lakini pia macho yaliokuwa yakimwangalia, matendo yote ya Edna hayakudumu kwa Zaidi ya dakika. Na kwa jinsi Edna alivyoonekana ni kama hakuwa akijilinganisha na Amina, ukweli ni kwamba Edna hakuwa kama wanawake wengine ambao siku zote wangejilinganisha uzuri wao na mtu mwingine , yeye hakuwa mtu wa kujali kama amekutana na mwanamke mwenye uzuri kumzidi yeye au yeye kumzidi kama ilivyokuwa tabia za wanawake wengine kujilinganisha.

Uzoefu wa kutembea nchi nyingi kwa upande wa Amina na kukutana na watu wengi Zaidi ulimfanya kuweza kumsoma kwa haraka Edna na kugundua ni mwanamke wa aina gani na aliweza kukisia mambo mawili kuhusu Edna , jambo la kwanza huenda Edna ni mwanamke ambaye alikuwa na ule ujinga wa kujilinganisha na kila mtu kwenye jamii au ni mwanamke ambaye ni ngumu sana kumsoma kile ambacho anafikiria , lakini hata hivyo kutokana na Edna anavyotambulika ,aliona sio mwanamke mjinga kwani kuongoza kampuni kubwa kama Vexto na kuifanya kutambulika kimataifa kwa miaka michache ni kosa kumdhania mke wa mpenzi wake ni mjinga na jibu lake likawa ni moja tu , kwamba Edna ni mwanamke ambaye haeleweki , yaani ni ngumu kusoma mawazo yake.

Lakini pia jambo lingine ambalo Amina aliweza kumsoma Edna ni kwamba alikuwa tofauti sana na yeye , kwa mfano Amina yeye alikuwa na uwezo wa kujishobokesha kwa mwaname ili mradi kuweza kupata hitajio lake kama ilivyokuwa kwa Roma siku ya kwanza walivyokutana , lakini kwa Edna aliona ni aina ya wanawake ambao hawawezi kujilegeza kwa mwanaume kwa ajili ya shida na sio kwamba Edna hataki kujilegeza kwa mwanaume , lakini alichoona ni kwamba Edna kwa muonekano hajui namna ya kujilegeza kwa mwanaume yaani kwa maneno marahisi huyupo ‘Romantic’.

Wanawake siku zote wana ‘Sharp instict’ likija swala la kumsoma mwanamke mwenzake na jinsi Amina alivyomsoma Edna , kila kitu kilikuwa kweli , Edna likija swala la mahusiano na mwanaume kama ni mtihani anapata sifuri.

Kwa mfano Edna angekuwa ni kama Amina kwa kipindi chote cha miezi mitano walioishi pamoja , huenda ingekuwa ngumu sana kwa Roma kutafuta mwanamke mwingine, na asingeenda hata Bar, kwani kutembelea kwa Roma Bar ndio kulimfanya akakutana na Neema Luwazo , lakini pia akakutana na mrembo Amina.

Edna kabla hajakaa ni kama sasa akili zake zilianza kufanya kazi vizuri , sura ya Amina ni kama alikuwa ameiona mahali , bali alikua hakumbuki, lakini hata hivyo hakutaka sana kujisumbua alimuona wapi mwanamke aliekuwa mbele yake , kilichomfanya kukasirika ndani kwa ndani ni alama ya Lipstick ambayo ipo kwenye shavu la Roma.

“Vipi hilo shavu umeumia?”Aliuliza Edna huku akikaa kwenye sofa.

“Mke wangu naumiaje wakati muda wote nilikuwa hapa nikiendelea na majukumu yangu ya kazi?” Aliongea Roma lakini palepale alikumbuka kwamba alibusiwa kwenye shavu na alipelekea mkono haraka haraka na kujifuta.

Roma alijikuta akigeuza macho yake kumwangalia Amina mara baada ya Lipstick ile kuiona kwenye mikono yake , na Amina aliekuwa pembeni yake alijifanysha hakuwa akifahamu kinachoendelea.

“Edna naweza kuelezea kilichotokea…..”

“Huna haja ya kujielezea , sio mara ya kwanza hata hivyo , ninachohitaji ni kumjua huyu mwanamke”Aliongea Edna huku akimwangalia Amina, Amina alikuwa akielewa Kiswahili bali hakuwa vizuri kwenye kuongea kutokana na kuishi sana nje ya nchi.

“Nice To meet you Boss Edna , I’m Amina Kanani a newly appointed secretary of Director”Aliongea na kitendo cha kumaliza tu sentensi yake , sasa Edna aliweza kumkumbua.

“Wewe ni mtoto wa Tajiri Kanani?”Aliuliza Edna kwa mshangao

“Ndio Mzee Kanani ni baba yangu , licha ya kwamba nachukia kufahamika hivyo”

“Kwahio habari za miezi iliopita juu ya kumchukua mchumba wa mtoto wa Tajiri Khalifa , lakini pia ukavuruga ndoa yao huko Japani , mwanamke mwenyewe ndio huyu?”Aliongea Edna na Amna kwasababu alijua Edna amekasirika ilibidi ajikalishe kimya, upande wa Roma alishindwa kujitetea.

“Roma niseme tu kwamba unajiamini sana na nadhani sikufanya makosa kukuchagua kuongoza hii kampuni , maana kupitia kujiamini kwako kwa kuweza kuchukuwa wachumba wa wanaume wengine , kama utatumia nguvu hizo kwenye maswala ya maana basi tutafika mbali, nafikiri nikuachie kabisa hata kampunbi ya Vexto uchukue nafasi yangu ya CEO, unaonaje ukaifanya kampuni yangu kwa koneksheni zako na ikawa kubwa Zaidi kimataifa, hata hivyo bado sisi ni wanandoa kishetia , hivyo sio mbaya ukanisaidia”Aliongea Edna na sauti yake ilionyesha kabisa alikuwa amekasirika mno, ila tu alikuwa akijizuia kiuongea maneno mabaya Zaidi.

“Edna mke wangu naomba usikasirike na naomba unisamehe kwa nilichokifanya “

“Kuna kipi sasa hapa cha wewe kuniomba msamaha, Wewe ni mtu mkubwa una konesheni kubwa huko duniani na unaweza kuwa na mwanamke yoyote yule unayetaka , kwanini nikufanye uniombe msamaha mtu mdogo kama mimi”

“Edna hizo ni lawama za kipuuzi , nipe angalau nafasi basi nijielezee, acha kuongea vitu ambavyo havina msingi”

“Unasema naongea upuuzi , Roma unamaanisha kweli nilichokuwa nikiongea ni upuuzi?”Aliongea Edna kwa sauti huku akisimama, alikuwa ni kama hakutarajia Roma anaweza kumwambia kwamba anaongea mambo ya kipuuzi mbele ya mchepuko wake.

“Okey si umesema naongea mambo ya kipuuzi sawa , nilikuja hapa kwa ajili ya kukualika tukapate chakula cha mchana wote na unielezee maendeleo ya kampuni , lakini sikujua kama nakuja kuharibu sherehe yako na Sekretary wako mpya , nitaacha kuongea upuuzi kwanzia leo”Aliongea Edna kwa hasira na kisha alinyakua mkoba wake kwenye sofa na kutoka kwenye ofisi hio kwa haraka.

Amina kwa jinsi alivyomuona Edna alivyokasirika , aliona kabisa ameyakoroga na alijilaumu kuja siku hio ndani ya ofisi ya Roma

“Sorry i.. didn’t mean to worsen your relationship..”Aliongea Amina akiomba msamaha kwa kuona yeye ndio chanzo.

“Na wewe unaongea ujinga , una kosa gani sasa mpaka uombe msamaha , haya ni matokeo ya mimi kufanya vitu bila kufikiria ndio maana , hupaswi kubeba makosa yangu kwa kuomba msamaha

“Basi mfuate angalau ukambembeleze hata kama ni mimi ningekuwa kwenye nafasi yake ningekasirik sanaa.. mfuate ukamuweke sawa”Roma alijikuta akipumua huku akikaa kwenye kiti chake na kumwangalia Amina.

“Unafikiri hata nikimfuata nitafanya nini , siwezi kumwambia kwamba nitaachana na wewe na hatutawasiliana tena au kuachana na wanawake wangu wengine pia , hapa wa kulaumiwa ni mtu mmoja tu na mtu huyo ni mimi mwenyewe kwa kushindwa kujizuia”Aliongea Roma na Amina aliona maneno yake ni sahihi kwani hata yeye hayupo tayari kabisa kuachana na Roma , hivyo hakuna cha kubadilisha hata kama amkimbilie.

Edna naomba unichukie uwezavyo , ni mimi ambaye nimeingilia mahusiano yenu , lakini siwezi kukata tamaa kirahisi kwasababu unaumia mimi kuwa na Roma ,,, nitaendelea kuwa nae hata kama hutaki”Aliwaza Amina kwenye kichwa chake.

I
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…