Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akhsante sana mkuu, acha tu nije whatsappSEHEMU YA 330.
Ni muda wa saa kumi za jioni Roma na Lanlan walionekana wakiwa ndani ya jengo laTerminal namba tatu , sehemu ya kusubiria wageni wanaowasili, uchangamfu wa Lanlan wakati akiongea na mjomba wake Roma Ramoni ulifanya baadhi ya watu waliofika kwa ajili ya kupokea wapendwa wao kuwaangalia kwa namna ya wivu , uzuri wa Lanlan ulifanya kuwa kivutio ndani ya eneo hilo.
“Anko Mama mbona hafiki , Lanlan amemmisi sana mama yake”Aliongea Lanlan kama kawaida yake na kumfanya Roma atabasamu , wakati huu Lanlan ameshikilia Ice Cream huku kila akiilamba macho yote yalielekea sehemu ya kutokea wageni.
“Chubi Anko pia amemisi mke wake na mke wangu ni wa kwangu peke yangu”
“Anko mimi sio Chubi na Mama ni wa Lanlan peke yake na mama anampenda Lanlan ndio maana atamletea zawadi”
“Lanlan unaonaje tukapinga, mama yako ananipenda mimi na ataniletea zawadi na wewe hakuletei”
“Mama yake Lanlan ataniletea zawadi na wewe Anko hakuletei”Alijibu Lanlan huku akipitisha kidole kwenye kidole cha Roma wakipinga.
“Mh kuna watu wanabahati jamani ,nitafurahije nikipata katoto kama kale”
“Hehe.. Suzy kwa mwonekano wako na mchumba wako Kibwengo hio ndoto ifute kwenye kichwa chako”
“Halafu Dorca usiniaze nishasema uache kumuita mpenzi wangu kwa jina la Kibwengo, unapenda kunichokoza”
“Heheh ,, kinachokukasirisha nini wakati mchumba wako jina lake ni Kibwengo Khamisi, kuna muda nafikiria wazazi wa mchumba wako walikuwa wakiwaza nini mpaka wakaamua kumwita mtoto wao jina la Kibwengo”
Hao ni wadada wawili waliokuwa wameketi karibu na alipokaa Roma na Lanlan na hayo ndio ilikuwa mitazamo yao juu ya Roma na Lanlan bila kusahau mpenzi wa Dorca afahamikae kwa jina la Kibwengo.
Dakika kama kumi na tano mbele hatimae tangazo la ndege ya Emirate kutua ndani ya uwanja huo ilisikika na Roma alimshika Lanlan mkono, wote kwa pamoja wakiwa na hamu ya kumuona Edna.
Upande wa Roma maneno aliozungumza na Christine ni kama aliyapotezea kama ilivyo kawaida yake , Roma alikuwa na sheria moja tu katika Maisha yake kutojisumbua na mambo ambayo hana uhakika nayo, alipenda kudili na yale tu ambayo anauhakika nayo na ambayo yapo mbele ya macho yake , lakini sio yale ambayo ni ya kufikirika na ndio maana aliamua kupotezea maneno ya Christine na alijiambia katika akili yake kama maneno yake ni sahihi basi yeye anaisubiria hio siku ya utabiri kwa hamu zote.
Upande wa kampuni yake ya Vexto siku hio alikuwa ashatoa taarifa ya uthibitisho juu ya Christine kukubali kufanya interview siku ya uzinduzi wa Tv Channeli yao m jambo ambalo lilipokelewa kwa shangwe na Daudi pamo ja na Wendy na walihakikisha watatumia kila nyenzo kuhakikisha kila mtu anaufahamu na siku hio yenyewe na hio ni kwa ku’promote’ kwenye mitandao pamoja na kwenye chaneli za Tv Tofauti tofauti,
Matangazo mbalimbali pia yanayohusiana na shindano la vipaji vya uimbaji wa muziki pamoja na uigizaji yalikuwa yamesambaa kwenye barabara nyingi katikati ya jiji la Dar , lakini pia kwenye baadhi ya mitandao , huku mirejesho ya watu wanaojiandaa na kujiingiza kwenye mashindano hayo ukiwa ni mkubwa mno na hilo lilidhihirisha kazi nzuri ambayo wafanyakazi wa Vexto Media upande wa Marketing walikuwa wakifanya.
Ni ndani ya dakika ishirini mara baada ya ndege kutua , Lanlan ndio aliekuwa wa kwanza kumuona mama yake akitokezea sehemu ya kusubiria wageni.
“Anko mama wa Lanlan yule”Aliongea Lanlan huku akijaribu kutoa mkono wake wake kwenye kiganja cha Roma , lakini Roma alikuwa ameshikilia vizuri , alikuwa akitegemea Lanlan akishamwona mama yake atamkibilia hivyo kuweza kugonga watu na ndio maana hakutaka kumuachia.
Upande wa Edna mara baada tu ya kufika ndani ya eneo hilo alijikuta akisimama mara baada ya kumuona Roma aliesimama na Lanlan , alionekana mrembo huyu ni kama hakutegemea kuwaona watu hao wawili wakiwa pamoja , moyo wake ulipata joto ambalo sio la kawaida , kwake picha hio ilimfurahisha sana.
Edna alikuwa amependeza mno na hakuwa amevalia mavazi ya suti kama alivyoondoka bali alivalia kama mdada wa kileo, suruali na Jeans pamoja na tisheti ndio mavazi Edna aliovalia na kumfanya kuonekana mrembo kuliko wanawake wote waliokuwa ndani ya hilo eneo.
Edna hakuwa peke yake bali alikuwa ametangulizana na Alhaji CEO kampuni ya Maple na bwana huyu baada ya Edna kusimama alijikuta akiangalia mbele na hapo ndipo alipomuona Roma akiwa amesimama na mtoto ambaye alimshangaza kutokana na uzuri wake , lakini pia namna ambavyo anafanana na Edna , sasa jambo hilo lilimshangaza kwani hakuwa na taarifa , wala hakuwahi kusikia popote Edna ashawahi kuwa na mtoto.
“Madam Boss kumbe una mtoto mzuri vile?”Aliongea Alhaji na kumfanya Edna kutabasamu na kuanza kutembea huku akiwa ameshikilia mkoba wake akiwasogelea Roma na Lanlan huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu.
Watu wote waligeuza macho kuangalia ni nini kimemfanya mrembo huyo kuwa na tabasamu mwanana namna hio na kuzidi kupendeza.
Upande wa Roma alijiambia lilikuwa wazo zuri sana lililopendekezwa na Sophia kuja na Lanlan kumpokea Edna , kwani matokeo yake alikuwa akiyaona laivu.
“Mom,,,!!!:Lanlan baada tu ya kuachiwa mkono wake alimkimbilia Edna na kumkumbatia na Roma ilibidi na yeye asogee mpaka waliposimama.
“Mr Roma tunaonana tena “Aliongea Alhaji kwa tabasamu na kisha alimpatia Roma begi dogo la kuburuza akimpa ishara ni la Edn.
“Hongera sana Mr Roma kwa kuwa na familia nzuri”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu na kisha walipeana mkono na Alhaji akatangulia.
Edna alimwangalia Roma na alijikuta akiachia tabasamu bila kupenda alionekana kufurahishwa na kitendo cha Roma kuja na Lanlan , licha ya kutokuwategemea.
“My Babe Wife umeenda siku hizi mbili lakini umerudi urembo wako ukiwa umeongezeka kwa kiwango kikubwa, usiniambie umerekebisha kidogo sura ili mume nizidi kukupenda”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu na Edna alitabasamu kidogo .
“Una makengeza labda”Alijibu Edna huku akimshika mkono Lanlan na kuanza kutembea huku wakiongea na dakika chache tu mbele waliweza kufika kwenye gari aliokuja nayo Roma.
“Lanlan nimekuletea zawadi za kutosha tukifika nyumbani nakuonyesha”Aliongea Edna na kumfanya Lanlan kushangilia na kumwangalia Roma kwa macho ya ushindi.
“Wife inamaana unayemkumbuka ni Lanlan tu na mimi mumeo niliepiga magoti usiku mzima kupiga maombi urudi salama haujanikumbuka”Aliongea Roma huku akijifanyisha kaonewa na Edna alimwangalia.
“Ukweni hawajambo?”Aliuliza Edna na Roma badala ya kujibu aliwasha gari na kukaza macho barabarani na kuanza kusogeza gari , ni kama alikuwa akielewa Edna anakoelekea kwenye mazungumzo aliotaka kuanzisha na mpaka hapo aliamini Lanlan ndio kamzidi.
“Vipi safari imekuwa ya mafanikio?”Aliuliza Roma.
“Shukrani kwako Hades safari imekuwa ya mafanikio”Aliongea Edna kwa namna ya utani akitumia jina la Hades na kumfanya Roma kutabasamu na mpaka hapo aliamini kuna jambo ambalo limetokea.
“Nielezee kilichotokea basi wife sio kuishia kuniita Hades”Aliongea Roma.
“Nikajua unataarifa na kila kilichojili nadhani sio kama nilivofikiria Hades”Aliongea Edna na kuanza kumuelezea safari ilivyokuwa namna alivyokutana na Tanya na kujua kile kilichotokea Japani namna alivyoweza kumiliki kundi la Yamata Sect, lakini pia hakuacha kuelezea namna ambavyo alikutana na Clark ,Edward na Mr Alfin Kelphin pamoja na zawadi aliopatiwa , ambacho hakuelezea Edna ni kilichomtokea hotelini , kitendo cha kudondoka na kupoteza fahamu.
“Alfin Kelphin ndio mmiliki wa kampuni ya Aba?”
“Nikajua unamjua vizuri , inaonekana maneno yake juu ya wewe kuwa rafiki yake ni ya uongo”
“Sijasema ni ya uongo ila juu ya umiliki wake wa makampuni ya Aba sijawahi kufahamu hilo , hata hivyo mke wangu nimefurahi umetatua shida zako kwa haraka na kurejea nchini maana kwa jinsi nilivyokumisi huenda ningefanya safari ya dharula kuja Hongkong”
“Mbona unaruka baadhi ya mambo?”
“Nimeruka nini sasa mke wangu”
“Hujaongea chochote kuhusu Tanya mwanamke ambaye aliniteka Tanzania lakini Ghafla tu akawa kijakazi wako”Aliongea Edna na kumfanya Roma akune kichwa ukweli aliona hakuna maelezo ya kuongea hapo.
“Kule Ufaransa ukajinasibu kwamba utanieleza kila kitu unachofanya , lakini matokeo yake ukavunja ahadi yako , ilianza kwa Apollo na Artemis na baada ya pale ukawa umesahau, kumbe ulienda Japani ukakamatika na Seventeen feki, lakini sio hivyo tu kumbe mwenzetu unakitu cha thamani ‘Godstone’ unakaa nacho hatuambiani”
“Kwahio sababu ya kuninunia siku ile Ufaransa ilikuwa ni kwasababu sikukueleza kuhusu Alice na kaka yake, lakini ulijuaje kama wanaitwa Apollo na Artemis nakumbuka ulikuwa umepoteza fahamu”Aliongea Roma.
Ukweli hakuelewa ilikuwaje Edna akamfahamu Alice kuwa Artemis na Stern kuwa Apolo kwani alichokuwa akikumbuka ni kwamba Edna alikuwa hana fahamu zozote.
“Waulize Apollo na Artemiss watakua na majibu ya swali lako”Aliongea Edna na kumfanya Roma sasa kuelewa huenda Siku ile Alice na Stern hawakumfanya Edna kupoteza fahamu , lakini kama ni kweli Roma aliona basi Edna ni mtu hatari sana kwenye kuweka mambo moyoni , kwani mambo yaliotendeka siku ile hayakuwa ya kawaida , kwa mfano kitendo cha Roma kuongea na Roho ya Depney lilikuwa ni jambo ambalo sio la kawaida kwa binadamu wa kawaida kulishuhudia na kutulia tuli.
Roma alikuwa na shauku kujua ni kwa kiasi gani ambacho Edna alieweza kuelewa siku ile.
“Wife kuhusu Japa..”
“Huna haja ya kujitetea Roma yalishapita”Aliongea Edna akimkatisha Roma kuongea na Edna alimgeukia Lanlan aliekuwa bize kuchezea simu.
Dakika chache mbele waliweza kufika nyumbani na kupokelewa na Roma alibeba begi la Edna na Kwenda nalo chumbani , huku Lanlan akifuata nyuma nyuma kuagalia ni Zawadi gani alizoletewa na mama yake , alionekana kuwa na shauku kubwa na hata Roma alilitambua hilo.
Baada ya Roma kutua begi kitandani alimwangalia Lanlan na kisha akapiga hatua kutoka Kwenda kwenye chumba chake.
“Nimekuletea Zawadi pia Rma usiondoke”Aliongea Edna kwa sauti kavu huku akimpita Roma na Kwenda kuketi kitandani kichomvu na kumfanya Roma amwangalie kwa mshangao , hakuamini kama kweli Edna mke wake kabisa na ukauzu wake amemkumbuka mpaka kumletea zawadi, tabasamu lilikuwa nje nje.
Unafikiri kwanini Edna akapatwa na kichwa cha ghalfa , Jiwe lingine analozungumzia Aphrodite liko wapi?
ITAENDELEA ALHAMISI NINAWEKA RATIBA ILI USITESEKE NA AROSTO KWANI SIO MAKUSUDI YA KULETA SIMULIZI HII HAPA JUKWAANI .
UKITAKA KUNIUNGA MKONO UNAKARIBISHWA , NICHEKI WATSAPP 0687151346 NITAKUJIBU NA KUKUPA UTARATIBU WA MWENDELEZO KWA ANAETAKA
[emoji119]nitarudiiiSEHEMU YA 51
Upande wa Chini kabisa ndani ya Mashua, kwa nje kabisa alikuwa amesimama mzee mmoja hivi aliekuwa ameshikilia panga lake Refu akiwa anaangalia Chopa iliokuwa hewani , mzee huyu alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa , alikuwa amevalia mavazi ya kitamaduni ya kichina huku akiwa na kipara chake, alikuwa na macho flani hivi ya kutisha kama ana makengeza na mboni za macho hazikuonekana ni rahisi kusema anajicho lisilokuwana kiini cheusi..
Ndani ya mashua hio walionekana vijana wanne hivi wote wakorea waliokuwa wameketi kwenye visturi huku wakinywa kilevi ambacho kilikuwa kikifanana na ulanzi , huku pembeni yake kukiwa na Sanamu Varicana ambalo walikuwa wamelifunika na nguo.
Upande wa kushoto ndani ya mashua hii kulikuwa na maboksi flani ya mbao , kama yale ya kuhifadhia Nyanya wakati wa kuzisafirisha kutoka shambani , chakushangaza ni kwamba maboksi hayo yalikuwa yakitingishika na nikama kulikuwa na mnyama ndani ya maboksi hayo na watu hawa hawakuwa wakijali sana kutingishika kwa maboksi waliendelea kunywa kwa furaha huku wakiongea , lakini muda huohuo ndio walipoanza kusikia mngurumo wa Chopa na wote kwa pamoja walikurupuka na kubeba Bunduki zao na kutoka nje haraka na walimkuta kama kawaida Tzeng akiwa anaingalia ile chopa huku akionekana ni mwenye kukata tamaa , ni kama mtu ambaye alikuwa akisubiria kitu kikubwa Zaidi na hakijatokea.
“Master Tzeng”Aliita kijana mmoja wa kikorea huku akimwangalia Monk kwa wasiwasi.
“Mtu ninaemsubiria hayupo kwenye hio chopa , naona wale makafir wamenidanganya,imenikatisha moyo , walitaka kunitumia tu kukamilisha mambo yao ,Inasikitisha sana”Aliongea Tzeng.
“Master lakini haujatuambia unaemsubiria kila siku umekuwa wakutuambia kuna mtu unaemsubiria”.
“Unafikiri kwa miaka yangu yote niliohudumu kusalia Budha ninaweza kuisaliti huduma yangu kuja kuiba sanamu,Nimewakubalia Dhoruba Nyekundu kuiba hilo sanamu kwasababu wamenihakikishia nitapata nafasi ya kupambana na Hades ,Inasikitisha sana”
“Master Hades ni nani?”
“Huna haja ya kumjua , kwangu ni mtu ambaye natamani kuupima uwezo wangu wa kimapigano kwa kupambana nae , lakini nimekatishwa tamaa na kutoonekana kwake, nahisi sitoweza kuufamu uwezo wangu wa kimapigano mpaka nakufa inasiikitisha sana”.
Upande wa Chopa kule juu wakati wakiendelea kushangaa chini baharini kama watamuona Roma , Mara walijikuta wakianza kushambuliwa kwa mbele.
“Sh**t Ni ni kikosi cha watu wa Dhoruba Nyekundu washafika, Kapteni kuwa makini wasiharibu chombo”.
“Pumbavu tulishindwaje kuwagundua wamekaribia? , Boti yao ile”
“Sio Boti wewe mpuuzi , ile ni SubMarine(Manuari)”Aliongea Kobota akimrekebisha Mbwa Mwitu , lakini wakati huohuo lilirushwa kombola na ilibakia kidogo tu ligonge Chopa yao na Rubani alionekana kuwa mtaalamu kweli , kwani aliipindisha Ndege na kugeuza kushoto, mashambulizi yalikuwa makali sana na watu wa Dhoruba Nyekundu walionekana kudhamiria kuidondosha kabisa hio chopa.
“Bang .. Bang !!”Ni milio ya risasi iliokuwa ikigonga chopa huku na waliokuwa kwenye ndege wakirusha Risasi.
“Hawa wajamaa wanateknolojia kubwa ndio maana ndege yetu imeshindwa kuwanasa kwenye Radar, tusipokuwa makini hii misheni itafeli”Aliongea Rubani msaidizi kwa kijapani.
“Sema Pluto naamini ashakufa mpaka sasa , niliwaambia hana lolote yule, na nimeshangaaa kumuhusisha kwenye hii misheni”Aliongea Kibonge huku akimdharau Hades na hio ni kutokana zimepita Zaidi ya dakika tano bila ya kumshuhudia Roma.
“Mother***ker!”
Rubani alijikuta akitoa tusi mara baada ya kurushiwa Kombora kiasi kwamba Chopa ilianza kutoa mlio wa Alarm lakini ile anataka kulikwepa kwenda kulia , wa kwanza kuruka alikuwa ni kibonge , alionekana kuwa shapu na akafatia Kobota na Mbwa mwitu na hapohapo ulisikika mlio wa ‘BOOM’ Chopa ilikuwa imelipuka ikiwa na Sunami na Rubani msaidizi Jani ,na wengine , ulikuwa ni mlipuko mkubwa uliosababisha mwanga kutawala kwa sekunde kadhaa mpaka kufifia huku mabaki ya ndege yakidondokea baharini.
“Haya yote hayana maana ,Inasikitisha sana”Aliongea Tzeng baada ya kuona mlipuko wa ndege , lakini ile anageuka tu Roma alietoka kwenye maji kama samaki jamii ya Dolphin ,kama mshale huku akijilenga kwa Tzeng , lakini Tzeng alikuwa mwepesi mno kwani aliinama chini kama mti ambao umepindishwa na kichwa kugusa chini huku miguu haijasogea hata kidogo , yaani ni kama mti ulikuwa umechomekwa kwenye shimo na ukapindishwa na Roma akapita na kumvaa kijana aliekuwa akiuliza maswali na akaenda kudondokea baharini .
“Amitabha.. Hades”Aliongea Mzee huku akikunja mikono miwili , alionekana kushukuru ujio wa Hades.
“Inashangaza kuona Monk kuwa mwizi”Aliongea Roma.
“Kuna Muda inapaswa kuwa hivyo , kama unania ya kutimiza dhumuni kuu kwenye maisha yangu”Aliongea huku wale Wakorea wakiwa wamemzingira na Bunduki zao ila Roma hakuwa ni mwenye kuwajali.
Wakati huo huo ile Submarine(Manuari) ilikuwa ishafika usawa wa mashua na walikuwa wakimshuhudia Tzeng na Roma waliokuwa wakiangaliana.
“Jason ni Hades , inapaswa kuchukua Sanamu tuondoke wakati akiendelea kupambana na Tzeng”
“Jessy tulia kwanza tuone mtanange , tukiona dalili za kushindwa kwa Tzeng tunakimbia ”Aliongea Jason wakati huu chombo chao kikiwa
Upande wa Kibonge alionekana kusalimika hukuu akiogelea upande wa ilipokuwa mashua ,aliangalia nyuma na kuwaona wenzake pia wanatapatapa kwenye maji.
“Okey!Tzeng nataka nikamuokoe mpenzi wangu,kwasababu umeshindwa kutumikia Budha na kugeukia njia Ovu nikikuua nitakuwa nimefanya jambo la kiimani kwa Mungu wa Budha”Aliongea Roma.
“Bothisativa Sabejatha” Alitamka Tzeng huku akimnsogelea Roma akiwa amenyoosha upanga wake , akilenga tumbo na Roma hakuondoka alipokuwa amesimama na ile Tzeng anafika Roma alisogea kidogo na Upanga ukapita kwenye kwapa , lakini Tzeng alionekana kutumia nguvu isiokuwa ya kawaida , kwani alimsukuma Roma na wote walitumbukia kwenye maji huku wakiwa katika staili kama ya kukumbatina ,Tzeng baada ya kutua kwenye maji mita kadhaa chini kabisa , alimsukuma Roma na kujitoa kwake na kisha akaleta tena pigo huko akizungusha upanga wake kwa spidi kiasi kwamba ulikuwa ukionekana kama sinndano na ile anamfikia Roma kwa nia ya kumchoma Roma aliuzuia na viganja vya mikono kwa kuubana , kitendo ambacho kilimfanya Tzeng kuuvuta ila Alishindwa na kujikuta akishangaa ni uwezo gani wa nguvu za mikono za Roma, lakini ile anashangaa Roma aliruka sarakasi na miguu ikawa juu na mikono ikiwa chini imeshikilia lile panga na kisha akazunguka kama Pia kitendo kilichomfaya Tzeng kukosa mhimili wa kushikilia lile Panga,Baada ya Tzeng kuona Roma anazunguka na yeye alizunguka vilevile kwa spidi kiasi kwamba Jason ,Jessie ,Kibonge na wenzake kushangazwa na Wimbi lililojitengeneza juu sehemu ambayo wametumbukia.
****
ATLANTIC OCEAN-ISLAND X
PROJECT LADO MONITORING CENRE(PLMC)
Ni ndani ya kisiwa ambacho kilipewa jina la Kisiwa X,kisiwa hiki kilipewa jina hilo kutokana na kwamba kimetolewa kwenye Ramani , yaani ni kisiwa , lakini kwenye Ramani ya dunia hakionekani na ndio maana kikapewa jina la Kisiwa X.ni kisiwa ambacho kipo kwenye bahari ya Antlantic.
Ni sehemu ambayo ina ulinzi mkubwa sana kiasi kwamba kama upo habarini kilomita 60 kutoka ndani ya kisiwa hiki utaona mkanda mkubwa wenye maandishi ya DON’T GET CLOSER ,IT`S DANGEROUS yalioandikwa kwa Rangi nyekundu kuzunguka eneo lote la kisiwa ,ni sehemu ambayo inabaridi kali sana na mkondo mkubwa wa maji na ni mara nyingi kuona meli zinapita karibu na eneo hilo na kama itatokea mtu akifika kwenye eneo hilo ni ngumu sana kutoka hai.
Ndani ya eneo hili la kisiwa kuna jengo ambalo kwa juu linaonekana kama kibakuli kilichofunikwa, na jengo hilo lina rangi nyeupe huku pembezoni mwa jengo hili kukiwa na Bendera zinazopepea za mataifa ishirini yenye nguvu, ambazo zimepangiliwa kwa umbali sawia kiasi kwamba zilifanya jengo hilo kupendeza.
Basi ndani kabisa ya jengo hili ndani ya hiki kisiwa , walionekana watu wanaume na wanawake walio na utofauti wa umri ,yaani kuna wale ambao walionekana kuwa na miaka hamsini na kuna wale ambao walikuwa na miaka Therathini kimakadirio , hapo ndani hapakuonekana mtu ambae yuko chini ya miaka ishirini.
Watu hawa wote walikuwa wamevalia tisheti za rangi ya Bluu huku kila mmoja ikiwa na chata la ‘O’ na jicho katikati ambalo limenakishiwa kwa rangi nyekundu, halafu chini ya tisheti hio kuna maneno yanayosomeka Zero`s Organisation.
Ni jengo ambalo kwa ndani lilikuwa limejengwa kitaalamu sana , jengo hili lilikuwa limetenganishwa mara mbili upande wa kulia kuna vyumba ambavyo vimejengewa kwa mfumo wa nusu duara , lakini pia kwa upande mwingine kuna vyumba ambavyo vimejengwa kwa mfumo wa nusu duara huku katikati pakiachwa wazi huku juu yake kukiwa na paa ambalo lilikuwa likipitisha mwanga na matundu ambavyo yametengenezwa kwa muundo wa nyota.
Ukiachana na hili jingo kwa pembeni yaani nje kabisa kulikuwa kumejengewa pia nyumba ambazo zilikuwa kwenye muundo tofauti tofauti ,zilizofanya eneo hili kupendeza sana ukijumlisha na bustani zilizokuwa zimetenezwa kwa muundo wa kuvutia.
Sasa ndani ya hili jengo kuna Idara inayofahamika kwa jina la PLMC(PROJECT LADO MONITORING CENTER), ndani ya hii idara walionekana jumla ya watu kumi na mbili , watano wanawake na saba wanaume wenye umri tofautt tofatui , ndani ya hii idara mbele kabisa kuna ukuta mkubwa ulionjengwa huku ukiwa na skrini kubwa ambayo ilikuwa ikionesha eneo la baharini , lakini ajabu ni kwamba mazingira yanayoonekana ndani ya hili eneo ni yale yale ambayo Roma na Tzeng wakipigana.
“Unafikiri Agent 13 atashinda Carlos?”Aliuliza mwanamke mmoja wa kizungu makadirio ya miaka hamsini hivi kupanda ambaye alikuwa akila Popcon zake zilizokuwa kwenye kopo bila habari huku akiangalia mpambano kati ya Roma na Tzeng , mwanamama huyu alikuwa amekaa huku pembeni yake kulikuwa na bwana mmoja mweusi kijana, akiwa amekaa pamoja na mwanamama anaekula Popcorn huku nyuma yao wakionekana wenzao ambao wamesimama wakiwa wanangalia mtanange huo , kwa jisi walivyo makini ni kama walikuwa kwenye ukumbi wa sinema wanaangalia muvi.
“Sina mashaka na Agent 13 Dyana, Tzeng ni mtu ambaye ana mafunzo ya juu na ndio maana tukamchagua kupambana na Agent 13 lakini haimaanishi kama anaweza kushinda ni uwekezaji mkubwa na maarifa yaliofanyika kumtengeneza Agent 13 na hatakiwi kushindwa na Tzeng”Aliongea bwana huyu aliefahamika kwa jina la Carlos huku akirudisha umakini wake kwenye pambano.
“Sema Agent 13 tokea Agent 17 kufariki , ukatili wake umepungua kwa asilimia mia moja ,nadhani mpango wa kumuua Agent 17 ulikuwa bora sana”Aliongea mwanamama huyu lakini bwana Carlos hakujibu.
Alisema leo Alhamis ila kimya
Mkuu mapema ya lini jana au leo?nipo mbali kidogo nitaishusha mapema
Mkuu fanya muujiza moja tujue yaliojiri kwa headsnipo mbali kidogo nitaishusha mapema
<<<tafadhali leo jaribu kushusha mzigo uliotuna. Yah ili mtu ahisi kuwa amemsoma Roma sio paragraph kadhaa eti ndio mzigo!!! Fanya makuu Singanojrnipo mbali kidogo nitaishusha mapema
Mapema Ni saa ngap mkuunipo mbali kidogo nitaishusha mapema
Tunasubr ap mkuu fany kwernipo mbali kidogo nitaishusha mapema