SEHEMU YA 347
Wote kwa pamoja walitega masikio yao wakimsikiliza Denisi mpango ambao unakwenda kufanyika kwa ajili ya Roma kudhibitiwa, Denisi alionekana kuwa na akili licha ya kwmaba pombe zilikuwa zimemkaa kichwani.
“Kuna mpango unaandaliwa na mtu mmoja mkubwa sana , siwezi kuwaambia kila kitu , lakini mnachaotakiwa kuelewa muda si mrefu yule choko atadhibitiwa”Aliongea Denisi.
“Tupe hata fununu , nini kinaendelea Mr Denisi , wote hapa Roma ni adui yetu namba moja na hakuna ambaye anaweza kutoa siri”Aliongea Elvice na Denisi alimwangalia kwa dakika akiwa kama mtu ambaye anafikiria.
“Kwasasa siwezi kuwaeleza chochoke kinachoonedelea ila tambueni tu Roma muda wowote ata…”Aliongea huku akionyesha ishara ya kuchinja na aliweka ‘Solo Cup’ kwenye meza na kisha akatoka nje na alionekana safari ya kurudi nyumbani ilikuwa imeiva.
“Desmond unafikiri kuna mpango gani unaendelea?”Aliuliza Abubakari na Desmond alimwangalia Elvice na kisha akatabasamu.
“Sina haja ya kujua kinachoendelea , ninachofaamu mimi nina mipango yangu kichwani na ikikamlika Edna atarudi kwenye himaya yangu kama alivyokuwa akinipenda mwanzo”Aliongea Desmond na kumfanya Elvice na Abubakari kuangaliana.
Ukweli mabwana hawa ni kama walikuwa wakiambana ni bora wao wawili wakose ila sio kwa Roma kuishi na Edna na kilichowafanya wakubali kumsapoti Edna ni kutokana na nnamna ambavyo Desmond aliwasimulia namna ambavyo yeye alikutana na Edna Chuoni na mrembo huyo kumpenda kiasi kwamba yeye mwenyewe akachukua hatua ya kumuleza , sasa Desmond aliongezea uongo mwingi ilimradi stori yake ionekane yeye ndio mwenye makosa kwa kutozingaria hisia za Edna kipindi cha nyuma.
“Desmond nyie watoto wa maraisi mbona mnapenda kutuweka gizani kwa kila kinachoendelea , hebu tueleze chochote”Aliongea Elvice huku akiweka sura ya usiriasi kwenye macho yake na Desmond aliwaangalia mabwana hao wanne waliokuwa mbele yake na alionekana kama alikuwa akijishauri na kwa dakika moja tu baada ya kupita alitoa simu yake ya Smartphone kisha akenda upande wa picha na kuwaonyesha.
Ilikuwa ni picha ya Edna akiwa anapokea maua kutoka kwa Desmond huku upande wa Desmond akiwa amepiga magoti.
“Huo ni mwanzo tu”Aliongea Desmond na kumfanya Elive kutabasamu mara baada ya kuona hio picha.
“Lakini hii haiwezi kutosha kumchukua Edna”
“Unachoongea ni sahihi, hebu sikieni , najua mpo hapa Tanzania , lakini hamjui mambo mengi yanayoendelea ndani ya familia ya Edna , mathalani upande wa bibi yake”Aliongea Desmond wa sauti ya chini na kuwafanya Abubakari na wenzake kujawa na shauku.
“Unamaanisha kuna siri ambayo inahusiana na bibi yake Edna?”
“Ndio tena nzito sana, ambayo itamfanya Edna kutokuwa na uhalali wakumiliki kampuni ya Vexto kama itawekwa hadharani”Aliongea Desmond huku akiachia tabasamu na kukaa vizuri na kisha akachukua pombe iliokuwa kwenye glass na kunywa kidogo”
“Inahusiana na nini hio siri?”
“Siwezi kuwaeleza mapema , ila tambueni kuna mpango wa kufukua mashimo ya zamani na kama mpango huo utafanikiwa Edna hatakuwa tena na uhalali wa kumiliki kampuni ya Vexto na kubwa Zaidi anaweza akaachia kampuni yeye mwenyewe kutokana na siri hio”Aliongea Desmond na alionekana ndio amekwisha kumaliza kusema hivyo kwani hata yeye alisimama akiashiria anataka kuondoka.
“Ninarejea nyumbani leo hii nikirudi ni kwa ajili ya kukamilisha mpango ,, mpaka wakati huo kaeni kwa amani kabisa , awamu hii kila kitu lazima kiende kama kilivyopangwa”Aliongea na wote kwa pamoja walitingisha kichwa wakiashria kukubali na Desmond alichukua koti lake la suti juu ya Sofa na kisha akaondoka kwenye nyumba hio.
“Unafikiri kuna siri gani inayoendelea?”Aliuliza Elvice.
“Siwezi kufahamu , ngoja tusubiri, mwenyewe nimechoka na haya Maisha, unajua mpango wangu ni kurudi kwenye kampuni lakini Matilda yule Malaya anajifanya mjanja , ila dawa yake ipo jikoni”
“Lakini aliemuweka Matilda pale kama Raisi wa kampuni ni Edna anaweza kuwa na nguvu ya kuongoza kampuni lakini mwenye uwezo wa kupinga maamuzi anayoyafanya ni Edna peke yake , nadhani sasa hivi umeona kilichotokea juzi , Matilda hakupenda bodi kupitisha swala la ufunguzi wa benki , lakini kwakua maamuzi yalitoka kwa mwenyekiti ambaye ni Edna swala hilo limefanikiwa”
“Hahaha. Umeongea kweli , lakini swala lile halina shida sana kwa upande wangu, Mzee nilipomuambia kuhusu hili swala alionekana hata yeye hakuafiki kabisa na alishindwa kumuelewa Matilda kwanini ameshindwa kumdhibiti Edna”.
“Abubakari yule Edna sio demu wa kawaida kama hawa mademu wa kunywa bia tunazo wanunulia , Edna namjua tokea akiwa mdogo na nimesoma nae, darasani yule aliekuwa akimzidi kiakili ni Ashley tu dada yake Denisi.”
“Hahaha.. kwahio unaniambia kwa akili zake ndio maana aliweza kuolewa na yule choko?”
“Abubakari hizo ni hasira zako , unajua mimi nimeamua kutokuwa kama wewe , ijapokuwa Roma namdharau lakini yule ni ligi tofauti na sisi na anajifanyisha kuwa ‘Humble’ tu , hivi unafikiri yule jamaa ni wa kawaida mpaka kuweza kumchukua Madam Neema au yule mwandishi wa Habari mtoto wa Mzee Kanani, Vipi kuhusu Dorisi au Edna mwenywe ?, Lazima tubadilike ,ili kumshinda lazima tumfahamu kwanza”
“Nyie mnaongea sana , ila kwangu mimi huyu Roma ambaye mmnazungumzia amekuwa ni kama ‘Role Model’ wangu na nataka nimtumie Sister Neema kufahamiana nae vizuri”Aliongea kiijana mmoja ambaye ana mwili wa kibonge ambaye muda wote alikuwa akiongea na Sali mjukuu wa raisi kigombola.
“Msechu unazingua”Aliongea Abubakari akionyesha kukasirika.
“Sio nazingua nyie ndio mnazingua , Elvice unafikiri Sister Neema ni mwanamke wa kujirahisisha tu kwa mwanaume?, nimejaribu kukaa na Baba yangu Mzee Chino na kupata habari mbili tatu kuhusu Roma unajua amenijibu nini?”
“Amekujibu nini?”Waliuliza wote watatu kwa pamoja na kumfanya Msechu kutabasamu na kisha kusimama.
“Oya sikieni wanangu, kuhusu mipango yenu juu ya huyu Roma mimi siwezi kumueleza chochote na nitakaa kimya , ila mtanisamehe kwanzia sasa hivi licha ya kwamba nina hela na urithi, lakini najitolea kuwa Chawa wa Roma”Aliongea na kisha huyo akaanza kupiga hatua na kuondoka akiwaacha Elvice na wenzake kuwa kwenye mshangao,
********
Naam ni siku ya jumamosi tena , katika wiki ya mwisho ya mashindano ya Kizazi nyota ambapo fainali za mashindano hayo zilitarajiwa kufanyika siku ya kesho yake, yaani jumapili, maandalizi yalikuwa makubwa sana kiasi kwamba jiji la Dar lilikuwa na shamra shamra nyingi , moja ya mambo makubwa ambayo yalikuwa yakitarajiwa siku ya kesho ni Christine kushiriki kama jaji kwenye fainali za maishindano hayo , lakini kitu kingine siku hio ni ujio wa mwanadada maarufu mrembo msanii kutoka Korea Kusini, ambaye alikuwa akitaajiwa kutumbuiza siku ya fainali hio akiwa kama mgeni rasmi, lakini pia siku hio hio watu walikuwa na hamu ya kumuona Sophia akitangazwa mshindi wa mashindano hayo ya Kizazi nyota kwani kwa namna ambavyo alionyesha kipaji kikubwa kipindi chote cha mashindano ilileta hamasa kubwa sana kwa mashabiki wengi na pia kwa wale ambao walikuwa wakipenda muziki.
Kampuni ya Vexto Media kupitia chaneli yao ya V TV ilitangazwa kwa mara ya kwanza kuwa kampuni ya kwanza kufatiliwa na watu wengi duniani kwa muda mfupi sana tokea kufunguliwa kwake, mafanikio ambayo yaliipaisha sana kampuni mama ya Vexto Group lakini pia kulifanya taifa la Tanzania kujitangaza Zaidi kimataifa.
Umaarufu wa kampuni ya Vexto Media , sambamba na mkataba mnono wa malighafi mpya ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa ndani ya mwezi wa kumi na mbili ulifanya hisa za kampuni ya Vexto kuzidi kupamda thamani kwa kiasi kikubwa sana na kumfanya Edna utajiri wake kuzidi kuongezeka kwa asilimia kubwa, jambo ambalo liliwaacha midomo wazi baadhi ya matajiri na wafanyabiashara wakubwa wa Afrika wenye uzoefu, huku wakijiuliza imewezekanaje msichana mdogo kama Edna ambaye ndio kwanza alikuwa kwenye umri wa kati ya miaka ishirini Kwenda therathini kuweza hayo yote.
Wakati matajiri hao wakiendelea kujiuliza juu ya mafanikio ya Edna kwa mwaka huo , upande wa nyumbani kwa Edna ,Osterbay, Edna alionekana kutojali sana kile ambacho kilikuwa kikiendelea au kilichokuwa kikizungumziwa juu yake , mrembo huyo siku hio alionekana kuwa na wasiwasi mno kuliko siku zote ambazo ashawahi kuonekana kuwa ni mwenye wasiwasi.
Kulikuwa na jambo kubwa ambalo lilikuwa likitegemewa ndani ya familia hio kwa siku hio ya jumamosi , jambo ambalo lilimfanya Edna kushindwa kabisa Kwenda kazini, jambo lenyewe lilikuwa ni juu ya ahadi ya ya babu yake Lanlan.
Kabla Lanlan hajaanza kuishi na familia ya Edna, babu yake aliacha ahadi kwa kupitia Mama Issa wa kituo cha Son And Daughter, kwamba kama asipoteokea baada ya siku ishirini na tisa basi Lanlan rasmi angekuwa mzazi halali wa Edna na Roma.
Sasa siku hii Edna pamoja na Roma walibakia nyumbani kwa ajili ya kusubiria ujio wa babu yake Lanlan , upande wa Roma alikuwana hamu ya kumuona babu yake Lanlan kwani alikuwa na maswali mengi juu yake huku upande wa Edna alikuwa akiomba babu yake Lanlan kutotokea kabisa siku hio , upande wa Qiag Xi yeye alikuwa akitamani kumuona babu yake Lanlan siku hio kwani kwake ilikuwa ndio njia pekee ya kujua kama babu yake Lanlan atakuwa salama au amekufa , kwa lugha nyepesi Qiang Xi alikuwa akijua kama babu yake Lanlan asipotkea siku hio basi ni dhahiri kwamba misheni yake imefeli hivyo hawezi kumuona tena na kama atatokea basi misheni imefanikiwa , sasa yeye alikuwa akiomba atokee siku hio.
Hivyo katika wanafamilia ambao walikuwa na wasiwasi Zaidi ni yeye pekee , yeye ndio aliekuwa akijua nusu ya ukweli wote wa kila ambacho kinaendelea na ndio maana alikuwa ni mwenye wasiwasi sana kuliko mtu yoyote yule na hata Blandina na Bi Wema waliweza kuona wasiwasi wa Qiang Xi na waliishia kumtia moyo na kumwambia babu yake Lanlan atatokea.
Upande wa Yezi yeye alikuwa ashaenda kwenye mgahawa anaofanyia kazi kwa ajili ya kujipatia riziki kama kawaida yake na kwa upande wa Sophia yeye alikuwa kambini tokea mashindano yaanze.
Asubuhi hio Edna, Roma na Lanlan walikuwa wamepumzika juu kabisa ya nyumba yao kwenye ‘Living Lounge’ Roma alikuwa akicheza gemu na Lanlan, upande wa Edna yeye alikuwa amejiegamiza kwenye sofa akiwa anasoma kitabu , licha ya kuwa na wasiwasi lakini kwa namna moja ama nyigine mrembo huyo alionekana sura yake kuwa na furaha, kila alipokuwa akisoma peji kama nne hivi alikuwa akiangalia watu waliokuwa mbele yake wakicheza gemu.
Lanlan na Roma walikuwa bize wakicheza gemu kwenye PS5 ambayo ililetwa kama zawadi na Kasimu mtoto wa Tajiri Azizi alipokuja kuwatembelea Edna na Roma siku ya jumapili, akiwa ameambatana na mrembo Donyi.
Siku hio ya jumapili Roma , Kasimu , Lanlan na Donyi walishindia kucheza gemu , ukweli Roma alipenda sana magemu yaliokuwa kwenye hio PS5 kiasi kwamba alidhamiria kununua ya Kwenda nayo ofisini , kwani gemu la kulipwa alililokuwa akicheza ofisini halikuwa likisisimua kama magemu yaliokuwa kwenye PS5, moja ya gemu ambalo lilimvutia Roma pamoja na Lanlan ni gemu moja lililofahamika kwa jina la Multiversus.
Siku hio ya jumapili upande wa Donyi alikuwa akimwangalia Roma pasipo ya kummaliza na yote hayo ni kutokana na kujua mahusiano yaliokuwepo kati ya mama yake na Roma , alikuwa ni kama haamini mama yake ambaye alikuwa mtu wa kujiheshimu anaweza kutoka na Roma , ukweli kwake sio kwamba Roma hakuwa na hadhi ya kutoka na mama yake , kitu ambacho kilimfanya kutokuamini ni kutokana na kupishana kwa umri wa mama yake na Roma , yeye ndio aliejiona kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutoka kimapenzi na Roma na sio mama yake , sasa jambo hilo kwake lilikuwa lina mchanganya kwani ni kama alikuwa na hasira ndani ya moyo wake mara baada ya kungundua jambo hilo, upande wa Roma aliona mabadiliko ya Donyi kwa namna ambavyo alikuwa akimwangalia ila hakujali sana , alijua huenda Donyi alikuwa ashafahamu uhusiano uliokuwepo kati yake na mama yake, hivyo alipotezea mpaka pale walipoondoka.
Sasa Lanlan tokea kuletwa kwa hilo gemu nyumbani wiki nzima alikuwa akicheza tu, alimlazimisha hata Bibi yake Blandina pamoja na Qiang Xi kukaa kwenye runinga kucheza nae , lakini kutokana na wote wawili kutokuwa na uzoefu wowote kuhusu magemu waliishia kumkatisha tamaa Lanlan kabisa kwani hakuwa akipata msimsimko unaotokana na ushindani.
Lanlan alikuwa na kichwa chepesi mno , Kasimu alimwelekeza kidogo tu namna ya kutumia Pad na baada ya lisaa limoja tu ya Lanlan kushika Pad hizo ni kama alikuwa mzoefu wa miaka mingi kucheza magemu, jambo ambalo lilimshangaza sana Kasimu na Donyi , lakini pia lilimshangaza Edna na Roma kwa uwezo mkubwa aliokuwa nao , kwani halikuwa jambo la kawaida kwa mtoto ambaye hata darasa la Awali hajaanza kuweza kumudu kucheza magemu mazito mazito yaliokuwa kwenye PS kama vile Call Of Duty na mengineyo magumu.
Sasa siku hii wakati wakiendelea kusubiria ujio wa babu yake Lanlan , Roma alikuwa akishindana kucheza gemu na Lanlan huku Edna akiwa ameketi nyuma yao akijisomea kitabu, kwani yeye hakuwa mpenzi wa magemu.
Kwa jinsi Roma na Lanlan walivyokuwa siriasis kucheza gemu la Multversus , huku wakionekana kufurahia kile walichokuwa wakikifanya mrembo huyo aliishia kutabasamu na hali ya kuombea babu yake Lanlan asifike ikizidi kuongezeka, Edna alijiambia ni jambo zuri sana kuwa na familia.
Roma alishangazwa na uwezo wa Lanlan wa kuelewa vitu kwani kwa jinsi ambavyo alikuwa akicheza gemu hilo ni kama alikuwa akicheza na mtu mzima mwenye uzoefu, upande wa lanlan alionekana kuwa na msisimko kweli , kila alichokuwa akikifanya kwenye gemu hilo ni kama akili yake ilikuwa ikikifanya laivu na sio gemu , hali hio ilimpelekea kumpa upinzani mkubwa sana Roma , lakini upande wa Roma kwakuwa hakua tayari kushindwa alijitahidi kutokupoteza mbele ya mtoto mdogo kama Lanlan.
“Wife njoo ucheze kidogo”Aliongea Roma huku akimgeukia Edna.
“Sipendelei kucheza magemu”
“Ushawahi kucheza?”
“Sijawahi”
“Sasa unasemaje hupendelei wakati hujawahi kucheza , njooo nikuelekeze ushindane na Lanlan” Aliongea Roma na kumfanya Lanlan aliekaa pembeni kumwangalia mama yake kwa namna ya kuomba na Edna mara baada ya kuona nammna ambavyo Lanlan amemuangalia ilibidi asogee.
Roma alibadili gemu na kuweka la F1 na kisha akaanza kumuelekeza Edna namna ya kucheza.
Sasa wakati hayo yakiendelea upande wa mlango wa kuingilia alionekana Blandina akiwa amesimama huku akiwa ameshikilia glass za juisi na alionekana alikuwa akiingia hapo ndani kwa ajili ya kuwaletea.
Blandina alijikuta machozi ya furaha yakimtoka , alionekana kushindwa kujizuia kwa namna Roma alivokuwa akipatana na Edna hapo ndani , lakini pia pamoja na uwepo wa Lanlan, alitamani kuona Maisha ya aina hio kwa wawili hao yakiwa endelevu.
Hata zile juisi alizoshikilia aliamua kurudi nazo ,kwani hakutaka kusumbua watu ambao walikuwa kwenye starehe yao.
Baaada ya lisaa la Roma kumuelekeza Edna na kumuoneysha namna ya kucheza , Edna alijikuta akivutiwa mno na sasa ni kama ashaanza kuzoea namna ya kucheza na alijikuta hata mawazo ya babu yake na Lanlan yakimpotea kwa muda.
………………..
Naam hatimae ikafika mpaka usiku pasipo ya babu yake Lanlan kutokea , Edna alionekana sasa kuanza kupata amani ya moyo , ijapokuwa siku haikuwa imeisha kwa minajiri ya kwamba inaisha saa sita kamili usiku, bado babu yake Lanlan alikuwa na nafasi ya kutokea kwenye muda huo , bado hakuwa na amani na masaa yaliobaki kupita kwani hakuwa tayari kumuona mtoto wake Lanlan akichukuliwa na mtu mwingine , kwani alitokea kumpenda sana , Lanlan alikuwa mtoto wa kike na ni kama alikuwa akijiona yeye mwenyewe kenye utoto wake kupitai Lanlan , uwezo wa akili wa Lanlan pia ulimfurahisha sana na kuzidi kumpenda , lakini pia namna ambavyo walifanana na kufiti sana kuwa mwana na mama.
“Wife huna haja ya kuwa na wasiwasi tena , babu yake Lanlan hawezi kutokea kwa muda uliobaki”Aliongea Roma wakati wanafamilia wote wakiwa kwnye meza wakijipatia chakula cha usiku na Roma aliona amtoe wasiwasi Edna kutokana na kwamba mrembo huyo muda wote alikuwa akimwangalia Lanlan aliekuwa bize na chakula.
Sasa kauli ya Roma ni kama imemgusa Qiang Xi , kwani palepale alijikuta akianza kutoa machozi na kuwafanya wanafamilia hao akiwemo Yezi kuwa kwenye mshangao.
“Qiang Xi nini tatizo?”Aliuliza Blandina aliekuwa karibu yake na Qianq ni kama alichokozwa kwani alianza kulia kwa kwikwi na kuinuka kwenye meza na kukimbilia juu na kuwafanya watu wote kuwa na mshangao kwa kutoelewa ni nini kinaendelea , kwani kwa namna ambavyo mrembo huyo alionekana , ni kama mtu ambaye amempoteza mtu muhimu sana kwenye Maisha yake.
“Ngoja nikaongee nae”Aliongea Edna huku akinyanyuka.
SEHEMU YA 348.
Edna baada ya kuingia chumba anacholala Qiang Xi ilibidi amsogelee kwanza na kuanza kumbembeleza , Qiang Xi alionekana alikuwa akijikaza tu tokea asubuhi ila hakuwa na amani kabisa na muda huo kwake ilionena ilikuwa muda sahihi wa kuanza kuangaua kilio , mwanamke huyo wa kichina alionekna kuwa kwenye hali ya majonzi.
“Qiang Xi niambie ni nini kinaendelea, kwanini unalia hivi kama umefiwa?”Aliuliza Edna kwa upole na Qiang alizidi kulia kiasi kwamba ilibidi Edna amkumbatie ili kumpatia Faraja.
Baada ya kama nusu saa hatimae Qiang Xi alimuelezea Edna ahadi aliowekeana na Master juu ya kile kinachoendelea. Alimwambia kwamba kama babu yake Lanlan asipotokea mpaka ikifika asubihi maana yake ni kwamba kuna jambo baya ambalo limemkuta, maneno hayo yalimfanya Edna kuelewa kwanini Qiang Xi alikuwakwenye hali hio , hakuelewa kwamba yeye kufurahia kwake kulikuwa kukimuumiza Qiang Xi kwani kutoonekana kwa Master Chi ilikuwa ikimaanisha kwamba atakuwa amekumbwa na jambo baya,
“Kwahio unasema babu yake Lanlan ameondoka kwenda kulipiza kisasi, je ni kisasi gani?”Aliuliza Edna kutokana na maelezo ya Qiang Xi.
“Master amekuwa msiri sana kwa kila anachokifanya , hivyo sijui kinacheondelea , ila kutokana na nilivyoagana nae naamini adui ambaye anashindana nae ana nguvu kubwa kuliko yeye na ndio maana akaniambia kama nisipotokea atakuwa amekufa”
“Miss Edna siwezi tena kumuona Master wangu mimi..”Aliongea Qiang huku akianza kula tena na ilibidi Edna aendelee kumbembeleza , hakujua ni namna gani anapaswa kumfarijji Qiang X.
“Qiang Xi sikiliza ninaamini kwa asilimia mia moja babu yake Lanlan atakuwa salama , kutofika siku ya leo kama alivyoahidi haimaanishi kwamba amepatwa na jambo baya , au kuna kilichomtokea , muda mwingine tunapanga hiki na Mungu anapanga kingine , hivyo hupaswi kuwa na huzuni , kwanzia sasa wewe ni mwanafamilia na utaendelea kuishi na sisi , hupaswi kuwa na huzuni sawa”Aliongea Edna huku akibahatisha , hakuwahi kubembeleza mtu kumfariji hivyo alijitahidi kadiri ya uwezo wake , lakini maneno yake yalionekana kuwa na nguvu , kwani Qiang Xi alionekana kidogo kupata tumaini jipya , alijiambia huenda ni kweli kama Master yake hatofika siku hio , basi huenda ni mpango wake umechelewa kukamilika , kwani siku zote mambo hayawezi Kwenda kwa muda unaopangwa na kuna dharula pia, hivyo aliona ashikilie kwenye maneno chanya ya Edna.
Roma baada ya kumaliza kula ilimbidi kurudi kwenye ‘Living Lounge’ ya upande wa juu kuendelea kuangalia taarifa ya Habari na dakika chache mbele Edna alikuja pia na kuketi na yeye kwenye sofa na ilibidi Roma amuulize kile ambacho kilikuwa kikimsumbua Qiang , na Edna aliweza kumuelezea ,Roma alishangazwa na maelezo hayo , kiasi cha kuzidi kupelekea shauku ya kutamani kumjua Zaidi kuhusu huyo babu yake Lanlan, kwa namna moja ama nyingine alihisi kabisa babu yake Lanlan hakuwa mtu wa kawaida , kutokana na namna ambavyo pia Lanlan alivyokuwa na uwezo usiokuwa wa kawaida.
“Romaa..!!”Aliita Edna kwa kivivu na Roma alimgeukia na kumwangali na Edna alionekana kusita sita.
“Unataka kuongea nini Babe”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu.
“Errmm.. unaonaje ukihamia chumbani kwangu”
“Hehe… Wife usiniambie unataka tu..”
“Ushaanza kufikiria mambo ambayo hayapo, unaweza kuhamia tukawa tunalala pamoja lakini…”
“Wife nipo tayari lakini hatufanyi , si ndio unachotaka kusema”Alimalizia Roma mara baada ya kuona Edna anashindwa kuongea na Edna aliitikia kwa kichwa.
Upande wa Roma aliachia tabasamu la kifedhuli , alijiambia inawezekana vipi akalala na mrembo kama huyo na asifanye nae , ila hakutaka kuongea sana alijiambia kila kitu kitaeleweka wakiwa kitandani , lakini pia aliamini huenda Edna amelazimishwa na mama yake walale chumba kimoja , hivyo aliona Edna anaweza kuwa kwenye wakati mgumu.
Roma alinyanyuka kwenye sofa alilokalia na Kwenda kukaa karibu na Edna na kisha akapitisha mkono kwenye bega la Edna na kisha kumwangalia usoni.
Upande wa Edna alijihisi mapigo ya moyo yakienda kasi mno , alijiambia yaani kabla tu hawajaanza kulala pamoja mtu tayari ashaanza mambo yake , alijiambia kitandani itakuwaje.
“Wife usiwe na wasiwasi najua unafikira yale mambo hehe..”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuona aibu na kuangalia pemben.
“Wewe ndio umefikiria hayo sio mimi usinisingizie”Aliongea Ednana Roma alitabasamu.
“Wewe ndio unanisingizia , Babe wife niangalie usoni kama kweli haujawaza mambo ya kichumbani chumbani”Aliongea Roma na Edna aliinua usona kumwangalia Roma na kukaza macho.
“Nimekuambia sina mawazo mengi ya kihuni kama wewe mimi , haya umeamini”Aliongea Edna Edna akijifanyisha kumkodolea Roma macho na dakika moja ilikuwa nyingi kwani alijishitukia amepigwa busu. kwenye lipsi na kumpelekea Edna kuona aibu .
“Naona unanichokoza sasa”Aliongea Edna huku akimfinya kwenye paja ,Roma alijikuta akichekeshwa na aibu za Edna na alisogeza mkono wake na kushika mkono wa kushoto wa Edna.
“Wife unaonaje tukifunga ndoa , sio ya makaratasi bali ya kanisani kabisa kwa kuvishana pete?”Aliongea Roma huku akiwa ameshika mkono wa Edna na maneno yake yalimwingia vizuri Edna , alijihisi ni kama anachumbiwa sasa, sasa hisia zilikuwa za aina yake , kwani yeye tofauti na wanawake wengine ni kwamba aliolewa kwanza kabla ya kuchumbiwa na sasa yupo kwenye ndoa na ndio anachumbiwa, aliona mambo yanaenda kinyume nyume na kimbelembele.
“Ofcourse mke wangu sio lazima unijibu sasa hivi , unaweza ukafikiria kwa mud ana ukanipa jibu”Aliongea Roma na Edna alimwangalia Roma usoni na kisha akatingisha kichwa kwamba anakubali , yaani kwamba atafikiria na Roma alitabasamu na wakaendelea kuangalia runinga wakiwa vilevile lakini baada ya nusu saa tu Edna alipotelea usingizini na kichwa chake kuegamia bega la Roma.
Roma alimwangalia Edna na kutabasamu na kisha alitumia uchawi wake kwa kumshika Edna kwenye shavu na usingizi wa Edna ukakolea Zaidi, alimbeba na kumpeleka mpaka chumbani kwake na akamlaza kitandani na baada ya kumaliza alishuka chini na kumchukua Lanlan ambaye pia alionekana kusinzia kwenye mikono ya bibi yake na kumpadisha juu na Kwenda kumlaza karibu na Edna , baada ya kuwafunika wote na kurekebisha AC alifunga chuumba na kutoka kabisa nje na kuingia kwenye chumba chake na alitoa simu yake na kisha akamtafuta Mage.
“Babe Afande umelala?”Aliuliza Roma mara baada ya kutuma ujumbe ulijjibiwa palepale.
“Sijalala , nipo nje ya Balconi inayoangaliana na upande wa nyumba yenu”ilisomeka na Roma alitabasamu na kisha akarudisha jibu kwamba anakuja na alivyoweka simu kwenye mfuko tu palepale akapotea.
********
Ni asubuhi ya saa moja kamili Edna ndio aliekuwa wa kwanza kuamka na baada ya kuangalia pembeni na kumuona Lanlan alitabasamu na kuendelea kujiuliza ni muda gani jana alipotelea usingizini.
Baada ya kukumbuka matukio ya jana usiku , ndipo alipokumbuka mara ya mwisho alikuwa eneo la sebule ya juu akiwa ameketi na Roma na ndipo alipopotelea usingizini, mpango wake jana ulikuwa ni kukaa mpaka saa sita usiku ndio alale , yaani ahakikishe siku hio inapita , lakini mpango wake haukuenda kama alivyopanga kwani alisinzia na sasa ni asubuhi ya siku nyingine , lakini uwepo wa Lanlan pembeni yake ulimwambia kwamba babu yake Lanlan hajafika na kwanzia muda huo Lanlan ni mtoto wake kamili na kilichobaki ni Kwenda kusaini karatasi kwenye kituo cha Son And Daughter Orphanage na baada ya hapo kumsajili Lanlan kama mtoto wake kabisa.
Edna alijikuta moyo wake ukiwa mwepesi sana , ni kama akili yake ilikuwa sasa ishatulia kwani wiki kadhaa nyuma alikuwa akiishi kwa kuhofia babu yake Lanlan anaweza kutokea muda wwote na kumchukua , lakini hatimae siku za ahadi zimekwisha isha na sasa alikuwa na maamuzi yote juu ya Lanlan.
“Ni muda wa kukutafutia shule sasa”Aliongea Edna huku akimshika Lanlan kichwani kwa kumbembeleza na kisha akanyanyuka.
Kwasababu ilikuwa jumapili aliona aende moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha Roma ili amuambie waelekee wote Kiwangwa kwa ajili ya kumsalimia MaMa Issa na pia kukamilisha taratibu za kumlea Lanlan.
Edna baada ya kufika kwenye chumba cha Roma alisukuma mlango taratibu na alitabasamu mara baada ya kumuona Roma bado akiwa amelala,alisogea mpaka kwenye kitanda na kumwangalia Roma kwama dakika kadhaa na alijikuta akighaili kile ambacho kimemleta na alitembea na kutoka kabisa nje.
Sasa wakati wa anatoka tu nje Roma alifumbua macho na kutabasamu na kisha alijifunua shuka na kuamka na mavazi aliokuwa nayo jana ndio hayo hayo na ilionyesha kabisa ndio alikuwa akirudi kutoka kwenye harakati zake.
“Ningechelewa dakika chache tu , asingenikuta humu bora nimewahi”Aliongea Roma kisha akavua nguo na kuingia bafuni kwa ajili ya kuuweka mwili wake safi.
Saa mbili kamili wote walijumuika kwenye meza na kujipatia kifungua kinywa.
“Mama leo tutamsajili Lanlan kama mtoto wetu na kuanza kumlea”Aliongea Edna na Blandina alimwangalia na kisha akamgeukia Roma ,nikama alikuwa akiwaaangalia kusoma kitu kabla ya kutoa jibu.
“Kama ndio mlivyokubaliana hakuna shida , mwenyewe nimetokea kumpenda Lanlan na nafurahi nitaitwa bibi”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kutabasamu.
“Ni rahisi sana kumpenda Lanlan kwasababu ni mtoto asie msumbufu lakini pia ana akili nyingi sana na isitoshe anafanana kwa asilimia kubwa na Edna mama yake ”Aliongea Roma.
“Anko Roma , Lanlan pia anafanana na wewe , hebu angalia hicho kichwa na midomo”Aliongea Yezi.
“Lanlan hafanani na anko , Lanlna anafanana na mama yake”
“Chubi Girl unafanana na mimi”
“Mimi sio Chubi na sifanani na wewe nafanana na mama”Aliongea Lanlan huku akimwangalia Roma kwa macho flani ya mtoto aliekasirika.
Bi Wema aliekuwa kimya muda wote alikuwa akitoa tabasamu ambalo liliashiria huzuni ndio pekeeambaye hakuwa akielewa kingereza vizuri.
“Bi Wema hatimae umepata mjukuu”Aliongea Edna kwa tabasamu.
“Miss Edna uwepo wa Lanlan umekubadilisha sana umekuwa muongeaji , nimefurahi Mungu kukubaliki kwa kumpata mtoto mzuri kama Lanlan”Aliongea Bi Wema na wote walitabasamu kumuunga mkon.
Qiang Xi upande wake licha ya kwamba alikuwa na mawazo , lakini alijiambia Lanlan anabahati kuwa kwenye familia kama hio , alitamani hata Maisha yake ya utoto awe na familia kama hio ambayo watu wote walionekana kujaa upendo , ijapokuwa alificha kile anachokijua kuhusu Lanlan lakini aliona ni vilevile tu hata kama wasipofahamu , Lanlan bado atabakiwa kuwa mtoto wao.
“Nilikuja asubuhi chumbani kwako tuongee kuhusu Kwenda kusaini zile karatasi , ila ulionekana kulala”Aliongea Edna baada ya kumsimamisha Roma aliekuwa akitaka kuingia chumbani kwake.
“Wife unaona hatia kutomjulisha mumeo kwanza? How obedient.”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa kuashiria jibu ni ndio na Roma alimsogelea karibu.
“Kajiandae twende tukasaini wote , ili kupata haki kamili ya kumlea Lanlan kama mtoto wetu, Lanlan ni mtoto mzuri sana na mawazo yako ya kumlea yalikuwa sahihi tokea mwanzo”Aliongea Roma na Edna alitabasamu na kutingisha kichwa na kisha akaelekea chumbani kwa ajili ya kujiandaa.
Jumapili mara nyingi wanaenda na Yezi, lakini kwasababu Yezi siku hio alitakiwa Kwenda zamu kwenye mgahawani kazini kwake , basi ilibidi Roma na Edna waende pamoja na Qiang Xi.
Baada ya masaa mawili kupita Roma na Edna waliweza kufika kituoni na kuonana na mama Issa ambaye alikuwa ndio kwanza anatoka kanisani na waliweza kusaini karatasi zote kama ilivyokuwa ahadi na Lanlan Rasmi akawa na wazazi yaani Edna na Roma.
Ni jambo la ajabu kweli ambalo Mungu amefanya kwa wawili hao kwanzia siku wanakutana mpaka miezi sita hio yote kamili, ni mengi sana ambayo yamewatokea kwa muda mfupi sana.
“Wife tunaanza maisha mapya mimi na wewe , mkataba wetu wa ndoa tarehe yake ya mwisho ni leo , Unakumbuka?”Aliongea Roma akiwa ameshika Lanlan mkono mmoja wa kulia huku na Edna akiwa ameshika mkono mmoja wa kushoto , wote walikuwa wamesimama kwenye pozi la kupiga picha.
“Nakumbuka”Alijibu Edna.
“Maisha yetu yamekuwa ya kipekee siku ambayo tulipanga kuachana ndio siku rasmi tunakuwa baba na mama , Hehe .. babe inaonekana Maisha yetu mimi na wewe yameamuliwa muda mrefu sana”
“Unahisi hivyo?”
“Ndio”Alijibu Roma na Edna alitabasamu.
“Bado nakumbuka ahadi yako tuliowekeana siku narudi na Lanlan, nadhani umesahau?”
“Nakumbuka mke wangu , unaonaje siku ya harusi yetu ndio nikatimiza ahadi?”
“Mbona unaongea kama nimekubali, si uliniambia nifikirie ndio nikupe jibu”
“Hehe… kwahio unapanga kunikatalia, hautaki kuvaa pete ya ndoa?, Babe napanga harusi yetu tukaifungie visiwa vya wafu , unaonaje? , utapata nafasi ya kujua kwanini naitwa mfalme Pluto”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumwangalia.
SEHEMU YA 349.
Edna baada ya kusikia maneno ya Roma alijikuta akifikiria kwa dakika kadhaa , ni kama alikuwa akisharabu maneno yake na aliishia kumwangalia Roma na kutoa tabasamu pasipo ya kutoa jibu na kumchanganya Roma Zaidi , kwani alishindwa kujua ni jibu gani Edna alikuwa akilifikisha kwake kwa kutumia tabasamu.
“Tuaongea kuhusu hili , Lanlan twende tukacheze na marafiki zako wapya”Aliongea Edna pasipo ya kusubiria neno kutoka kwa Roma ambaye alikuwa akikuna kichwa.
Edna alimchukua Lanlan na wakaungana na watoto wengine kuanza kucheza kwa furaha , Edna alisahau shida zake zote kwa madakika kadhaa na alijikuta akiwa kwenye ulimwengu wa Watoto.
“Mr Roma hongera sana , una bahati kweli, Lanlan na Edna ni baraka kubwa kwenye Maisha yako”Aliongea Mama Issa na kumfanya Roma kutabasamu na kumwangalia Edna aliekuwa mita kadhaa kutoka walipokaa.
“Asante sana Mama Issa”
“Kila ninapowaangalia hawa Watoto walivyokuwa na furaha sura ya mama yako Blandina inanijia akilini , Mr Roma nashukuru sana kwa kumsaidia mama kulinda kile alichokupambania kwa miaka mingi”.
“Huna haja ya kunishukuru nilichokufanya ni kidogo sana tofauti na kazi ambayo mmeifanya miaka na miaka, nitaendelea kuhakikisha vituo vyote ambavyo mama amevianzisha vinaendelea kudumu na kuimarika kihuduma ili kuendeleza ‘Legacy’ yake”Aliongea Roma na Mama Issa alijikuta akitabasamu.
“Mama Issa mtoto wako wa kwanza, Issa yeye yuko wapi?”Aliuliza Roma na mama Issa alitabasamu.
“Mtoto wangu wa kwanza sio Issa , mtoto wangu wa kwanza ni wa kike anaitwa Eunice ni nesi huko kisarawe, Issai ni mtoto wangu wa kiume wa kwanza na yeye ni daktari hospitali ya Mloganzila”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.
“Dokta Issai!!”
“Unamfahamu?”
“Ndio , wakati nafika Dar kwa mara ya kwanza nilibahatika kupata lift kutoka Morogoro kwa mama mmoja anafahamika kama Mama Aisha na alinikaribisha kwake na ndipo nilipokuja kufahamiana na Dokta Issai”Aliongea Roma na Mama Issa alishangaa na kutabasamu kwa wakati mmoja.
“Ndio ni kweli , Familia ya mzee Mohamedi ni wakwe zangu , kumbe mlishawahi kukutana?”Aliongea na Roma alitingisha kichwa lakini muda huo huo simu yake ndogo ilianza kutoa mlio.
Roma licha ya kupewa simu kubwa lakini aliendelea kutumia simu yake ndogo ya Tecno sasa haikueleweka hakuwa akipenda simu kubwa au alifanya hivyo kwa ajili ya usalama kwani inaaminika simu za batani ni salama Zaidi kuliko Smartphone.
Aliekuwa akimpigia ni Daudi moja ya msaidizi wake kutoka kwenye kampuni ya Vexto Media , Roma kuona simu hio aliamini kuna jambo ambalo limetokea , kwani jumapili hio ilikuwa ni siku kubwa sana kwa kampuni , ndio siku ambayo kilele cha mashindano ya Kizazi nyota yanafanyika usiku.
“Director Can you return to the company immediately? , There is VIP that wants to meet you”Aliongea Daudi akimwambia Roma kama anaweza kurudi kwenye kampuni haraka, kwani kuna mtu muhimu ambaye anatakiwa kuonana nae.
Sasa Roma alishangazwa na swala hilo la mtu muhimu kwani kwenye mashindano hayo ya kizazi nyota mtu ambaye kwake alikuwa akimchukulia kama mtu muhimu ni Christen.
“Is it someone I know?”Aliuliza Roma kama ni mtu ambaye anamfahamu.
“Hahaha.. Director ni malkia kutoka Asia , Queen Yoo YeonHe Kutoka Korea Kusini”Alijibu Daudi na hapo sasa Roma alikumbuka juu ya huyu msainii kutoka Korea Kusini, tabia yake ya kutozingatia sana watu maarufu ndio iliomfanya kumsahau huyu msanii.
Ni kweli wiki zilizopita alitangazwa kuhudhuria kwenye mashindano hayo ya Kizazi nyota , lakini swala hilo alilichukulia kawaida tu , lakini kwa namna ambavyo Daudi alikuwa akiongea ilimfanya kushangaa kidogo , kwani alionyesha mchecheto wa hali ya juu ukiashiria kwamba msanii huyo alikuwa akimpa heshima zake.
Sasa kitu ambacho hakuwa amekifahamu Roma ni kwamba licha ya msanii huyo kutaka kuhudhuria mashindano ya Kizazi nyota , lakini pia alikuwa akipanga kufanya show ndani ya jiji la Dar es salaam , sasa menejimenti yake iliomba kampuni ya Vexto Media kuhusika katika maandalizi ya Show hio, hivyo ilibidi Daudi amuelezee kwa haraka haraka Roma , ili kuelewa umuhimu wa msanii huyo.
“Bado sijaelewa unachogusia ni nini , ushasema ni mtu muhimu, lakini hujanielezea kwaninni anahitaji kuonana na mimi?”Alijibu Roma kwa Kingereza.
“It’s the first time Miss Yoo visiting Tanzania and our Company and as Diretor , you have to personally answer her Questions about the Show as a sign of respect”
“Ni mara ya kwanza Miss Yoo anaitembelea Tanzania na kampuni yetu na kama Mkurugezni unapaswa kujibu majibu yake kuhusiana na Show yake moja kwa moja kama ishara ya heshima”Aliongea Daudi na kumfanya Roma kutabasamu, maneno ya Daudi yalimfanya ahisi msanii huyo ni mwenye maringo sana kwani hata kwa Daudi peke yake alikuwa akitosha sana kujibu maswali yake na sio lazima yeye.
“Okey nitafika muda si mrefu”Aliongea Roma na kisha akamgeukia Mama Issa na kumuelezea kuwa ana dharula , alimfuata na Edna nakumuelezea dharula yake na Edna alimwambia atangulie tu na gari kwani angemuita dereva wa kampuni na familia kuja kuwachukua.
Ndani ya dakika arobaini na tano tu Roma aliweza kufika Moroco na Kwenda moja kwwenye ofisi yake, na ile anakaribia nje ya mlango wa kuingia kwenye ofisi, kulikuwa na mabodigadi wanne wa kikorea waliovalia mavazi meusi na miwani za jua, huku wakiwa na nyuso ambazo hazikuonyesha utani.
Roma baada ya kuwafikia hakujihangaisha sana kuongea nao Zaidi ya kuruhusiwa kuingia , mabodigadi hao walionekana kuwa na uzoefu wa kutosha katika kufahamu watu ndio maana hawakumzuia Roma.
Roma baada tu ya kufungua mlango alikutana na hali ya utulivu isiokuwa ya kawaida , Daudi alionekana kuketi kwenye kona kwenye sofa huku Wendy akiwa ameketi katikati , wote wakionekana kuwa kwenye hali isiokuwa kwenye utulivu ni kama walikuwa na Raisi ndani ya ofisi hio..
Kwenye kiti chake cha kibosi cha mzunguko alionekana mwanamke mrembo ambaye amekikalia , alikuwa ni mwanamke mwenye nywele ndefu nyeusi alievalia blazia ya mkato wa chini kifuani rangi nyeusi , sketi fupi ya Rangi ya Zambarau isiokolea , pamoja na viatu vya rangi nyepe vya High heels, alikuwa amefumba macho akiupa mgongo mlango huku akiwa ameweka Earpods masikioni , alionekana alikuwa akiburudika kusikiliza mziki kutoka kwenye simu yaje ya kisasa.Alionekana kuvutia sana.
Daudi na Wendy baada ya kumuona Roma kafika walisimama na kisha walimpa heshima yake.
“Would you be Miss Yoonhee?”Aliuliza Roma akisema je wewe ndio Miss Yoonhee na yule mwanamke mwenye mwili mwembamba aligeuka na kumwangalia Roma , alikuwa amevalia miwani pia ya jua ukijumlisha na weupe wake alionekana kuwa mrembo Zaidi.
Alitoa miwani yake na kisha kabla ya kujibu alimwangalia Roma kuanzia chini mpaka kichwani na mwonekano wa Roma ni kama hakuwa ameridhishwa nao kabisa kwani alivuta mdomo, alionekana ni mwanamke mwenye maringo na kujisikia sana kwa kumwangalia tu.
Roma kwa haraka haaka baada tu ya kumwangalia aliamini YoonHee miaka yake sio mingi sana ni juu ya miaka ishirini Kwenda ishirini na tano.
“Are you Director Roma?”
“Yes I am. I was dealing with some urgent matters , so I was late as I didn’t know you would be visiting , Miss Yoo.. my apologies”
“Ndio ni mimi , nilikuwa na kazi muhimu hivyo nimechelewa kwani sikufahamu kama utatutembelea , Miss yoon niwie radhi”
“Huna haja ya kuomba msamaha Director nadhani unajiuliza kwanini nimekuja hapa kwenye kampuni ,labda pia unawaza nimekuja kujionyesha tu kwako juu ya ukubwa wangu, si ndio?”
“Sio kweli Miss , nilipaswa kukutembelea Malkia kama wewe baada ya kufka hapa nchini kukushukuru kwa kushiriki kwenye mashindano yetu kwani umetuongezea umaarufu”
“Oh!, Kwaninni unaniita hivyo Mkurugenzi?, Haufahamu kama nachukia sana kuitwa jina la ‘Malkia’ , linanifanya nionekane kama nina maringo sana na kuwa wa matawi ya juu na wengine”Aliongea kwa mapozi na Roma alitamani kucheka , yaani mwanamke mwenyewe alionekana kujiona wa matawi ya juu na mwenye maringo lakini wakati huo huo anajifanyisha sio wa matawi , matendo na maneno vilikuwa vitu viwili tofauti , ndio alichoweza kuona Roma , ukweli Roma alikuwa akijitahidi sana kujishusha ili asimkasirishe mgeni wake lakini aliona kunakoelekea atakaosa uvumilivu kwani alikuwa akichukia mno dharau.,
“Oh ! kwasababu Miss Yoon hupendi kuitwa Malkia basi sitorudia tena kukuita hivyo, nilikuwa nikijaribu kukupamba tu”Aliongea Roma.
“Hahaha.. Director mbona unaonekana kama ni mwenye kukasirika , nafikiri unahisi mimi ni ngumu sana kunifurahisha , si ndio?”Aliongea yule mrembo wa kikorea na Roma na yeye aliishia kucheka pasipo kujibu chochote na kisha akamgeukia Daudi ambaye anatokwa na jasho muda wote.
“Tunapaswa sasa kuongea kabla ya chakula cha mchana ,Miss Yoon tuongee hapa hapa au tuelekee kwenye ukumbi wa mkutano?”Aliongea Daudi baada ya kusimama.
“Subirini kwanza.., sijasema nataka kuongelea mambo ya kikazi kwanza , naona nyie watu hamnipi heshima ninayostahili , nadhani mnaelewa mchango wangu kwenye kampuni yenu kupitia umaarufu wangu, Director nataka kuonana na CEO mwenyewe”Aliongea YoonHe na akaendelea
“You are the only director of branch company and therefore you do not possess the qualities and status to talk to me”
“Wewe ni mkurugezi wa kampuni hii tanzu pekee na huna viwango na hadhi ya kuongea na mimi mambo ya kibiashara”Aliongea kwa maringo huku akimwangalia Roma.
Alichokuwa akimaanisha huyo mwanamke ni kwamba alikuwa akitaka kuonana na Edna ambaye ndio CEO wa makampuni yote na sio Roma ambaye ni Director tu wa kampuni ndogo kama Vexto , yaani alimuona Roma wa kawaida sana.
“Miss Yoon , mpangilio wa kazi utachelewa kutokana na sababu zako ambazo hazina msingi”Alijibu Roma.
“Mr Roma nataka kwanza utambue wazi , nafanya kile ambacho nataka siku zote na sijali kama kazi zenu zitachelewa au lah, hayo hayanihusu ninataka kuonana na Boss wako”Aliongea kwa sauti ya kunyari huku akitoka kwenye kiti na kumsogelea Roma .
Daudi na Wendy walijikuta kwenye wakati mgumu mpaka hapo , lakini kwa upande wa Roma alionekana kutokuwa na wasiwasi, Rom alimsogelea YoonHe karibu kabisa na kuanza kumchunguza kwenye uso wake kama vile mtu anaetafuta chunusi.
“Unafikiri nitakuogopa kwa kunisogelea karibu , nataka kongea na boss wako na sio wewe mwajiriwa, la sivyo sitashiriki usiku wa leo”
“Tsk!.. huu uso wako sehemu ulipoutengeneza, nikiri kwamba madokta wa kikorea kwenye kufanya Plastic surgery ni wabobezi , mtu wa kawaida unaweza kumdanganya kwamba umezaliwa na hii sura kumbe ni ya kutegeneza”Aliongea Roma huku akiweka na yeye mwonekano wa kijeuri. Yaani maneno yake ni kama aikuwa akimwambia Yoon He kwamba ni mbaya na nido maana akafanya plastic surgery.
“Mbwa wewe , sijawahi kufanya upasuaiji wowote kubadilisha mwonekano,niko hivi hivi tokea nipo mdogo usiniangalie kwa macho yako mabaya ,nashangaa imekuwaje mwanaume mshamba kama wewe ukawa mkurugezi wa kampuni ya burudani na Habari, hili taifa limejaa vituko na ufisadi tu”Aliongea kwa kebehi ,lakini kwa namna ambavyo alikasirika Roma alijiona mwamba kwani amegusa penyewe.
“Sijali sana kama umefanya upasuaji au lah ,kwanza utanifanya nini wewe, hutaki kuongea kuhusu kazi na umejileta kwenye kampuni yangu , nani wa kufanya kazi na mwanamke mbaya kama wewe uliefanya upasuaji ili uonekane mrembo,Daudi na Wendy tumuache kama aliyvyo na tuendelee na majukumu yetu”Aliongea Roma na kuwafanya Daudi naWendy kuangaliana,huku wakisita sita kunyanyuka , lakini mwishowe walisimama na kutoka kwenye ofisi hio , lakini ile wanafunga tu mlango, walijkuta wakisikia ukulele wa kilio kutoka ndani.
“Wewe nyani unapata wapi , ujasiri wa kunidharau , unanifahamu mimi ninakotoka ni nani?”Ilisikika sauti kwa nje , kwani aliongea kwa sauti mpaka mabodigadi wake wakaingia ndani.
“Mkurugenzi litakuwa jambo zuri kumwacha?”Aliongea Daudi kwa wasiwasi.
“Msiwe na wasiwasi, kama ataendeleza tabia yake,mnaweza mkamtoa kwenye mashindano yetu , kama kutatokea lawama basi nitazibeba mimi”Aliongea Roma na kuondoka.