Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Mnapenda vya bure mnoo
unajua we ni kiumbe wa ajabu halafu kihere here! Kwa upendo mkubwa singanojr aliamua kutushirikisha stor yake! Hata we cjui ndo cag ulikuwa hujui kama kuna stor ya roma! Humu! Angekuwa na roho mbaya kama ww si angeiacha huko huko wasap? Acha hzo bhana! Kwanza umejuaje kama hatuchangii? Unaa huu!
 
Changia usipende dezo
 
Nahisi atakuwa katekwa na The Don au kikosi cha Dhoruba Nyekundu.
Namuaminia kamanda singanojr akiamua anaweza ua hata mmbu kwa nyundo! Kumbuka alivyoenda kumuokoa amina japan! Ka sumu tu alikolishwa akajitwalia kikosi kizima cha mayakuza na pesa zao? I know he was somewhere very busy ila atatia kwato hapa jamvin soon atakapoona hii notification! Just pray for him
 
Changieni pesa muache porojo
 
SEHEMU YA 347

Wote kwa pamoja walitega masikio yao wakimsikiliza Denisi mpango ambao unakwenda kufanyika kwa ajili ya Roma kudhibitiwa, Denisi alionekana kuwa na akili licha ya kwmaba pombe zilikuwa zimemkaa kichwani.

“Kuna mpango unaandaliwa na mtu mmoja mkubwa sana , siwezi kuwaambia kila kitu , lakini mnachaotakiwa kuelewa muda si mrefu yule choko atadhibitiwa”Aliongea Denisi.

“Tupe hata fununu , nini kinaendelea Mr Denisi , wote hapa Roma ni adui yetu namba moja na hakuna ambaye anaweza kutoa siri”Aliongea Elvice na Denisi alimwangalia kwa dakika akiwa kama mtu ambaye anafikiria.

“Kwasasa siwezi kuwaeleza chochoke kinachoonedelea ila tambueni tu Roma muda wowote ata…”Aliongea huku akionyesha ishara ya kuchinja na aliweka ‘Solo Cup’ kwenye meza na kisha akatoka nje na alionekana safari ya kurudi nyumbani ilikuwa imeiva.

“Desmond unafikiri kuna mpango gani unaendelea?”Aliuliza Abubakari na Desmond alimwangalia Elvice na kisha akatabasamu.

“Sina haja ya kujua kinachoendelea , ninachofaamu mimi nina mipango yangu kichwani na ikikamlika Edna atarudi kwenye himaya yangu kama alivyokuwa akinipenda mwanzo”Aliongea Desmond na kumfanya Elvice na Abubakari kuangaliana.

Ukweli mabwana hawa ni kama walikuwa wakiambana ni bora wao wawili wakose ila sio kwa Roma kuishi na Edna na kilichowafanya wakubali kumsapoti Edna ni kutokana na nnamna ambavyo Desmond aliwasimulia namna ambavyo yeye alikutana na Edna Chuoni na mrembo huyo kumpenda kiasi kwamba yeye mwenyewe akachukua hatua ya kumuleza , sasa Desmond aliongezea uongo mwingi ilimradi stori yake ionekane yeye ndio mwenye makosa kwa kutozingaria hisia za Edna kipindi cha nyuma.

“Desmond nyie watoto wa maraisi mbona mnapenda kutuweka gizani kwa kila kinachoendelea , hebu tueleze chochote”Aliongea Elvice huku akiweka sura ya usiriasi kwenye macho yake na Desmond aliwaangalia mabwana hao wanne waliokuwa mbele yake na alionekana kama alikuwa akijishauri na kwa dakika moja tu baada ya kupita alitoa simu yake ya Smartphone kisha akenda upande wa picha na kuwaonyesha.

Ilikuwa ni picha ya Edna akiwa anapokea maua kutoka kwa Desmond huku upande wa Desmond akiwa amepiga magoti.

“Huo ni mwanzo tu”Aliongea Desmond na kumfanya Elive kutabasamu mara baada ya kuona hio picha.

“Lakini hii haiwezi kutosha kumchukua Edna”

“Unachoongea ni sahihi, hebu sikieni , najua mpo hapa Tanzania , lakini hamjui mambo mengi yanayoendelea ndani ya familia ya Edna , mathalani upande wa bibi yake”Aliongea Desmond wa sauti ya chini na kuwafanya Abubakari na wenzake kujawa na shauku.

“Unamaanisha kuna siri ambayo inahusiana na bibi yake Edna?”

“Ndio tena nzito sana, ambayo itamfanya Edna kutokuwa na uhalali wakumiliki kampuni ya Vexto kama itawekwa hadharani”Aliongea Desmond huku akiachia tabasamu na kukaa vizuri na kisha akachukua pombe iliokuwa kwenye glass na kunywa kidogo”

“Inahusiana na nini hio siri?”

“Siwezi kuwaeleza mapema , ila tambueni kuna mpango wa kufukua mashimo ya zamani na kama mpango huo utafanikiwa Edna hatakuwa tena na uhalali wa kumiliki kampuni ya Vexto na kubwa Zaidi anaweza akaachia kampuni yeye mwenyewe kutokana na siri hio”Aliongea Desmond na alionekana ndio amekwisha kumaliza kusema hivyo kwani hata yeye alisimama akiashiria anataka kuondoka.

“Ninarejea nyumbani leo hii nikirudi ni kwa ajili ya kukamilisha mpango ,, mpaka wakati huo kaeni kwa amani kabisa , awamu hii kila kitu lazima kiende kama kilivyopangwa”Aliongea na wote kwa pamoja walitingisha kichwa wakiashria kukubali na Desmond alichukua koti lake la suti juu ya Sofa na kisha akaondoka kwenye nyumba hio.

“Unafikiri kuna siri gani inayoendelea?”Aliuliza Elvice.

“Siwezi kufahamu , ngoja tusubiri, mwenyewe nimechoka na haya Maisha, unajua mpango wangu ni kurudi kwenye kampuni lakini Matilda yule Malaya anajifanya mjanja , ila dawa yake ipo jikoni”

“Lakini aliemuweka Matilda pale kama Raisi wa kampuni ni Edna anaweza kuwa na nguvu ya kuongoza kampuni lakini mwenye uwezo wa kupinga maamuzi anayoyafanya ni Edna peke yake , nadhani sasa hivi umeona kilichotokea juzi , Matilda hakupenda bodi kupitisha swala la ufunguzi wa benki , lakini kwakua maamuzi yalitoka kwa mwenyekiti ambaye ni Edna swala hilo limefanikiwa”

“Hahaha. Umeongea kweli , lakini swala lile halina shida sana kwa upande wangu, Mzee nilipomuambia kuhusu hili swala alionekana hata yeye hakuafiki kabisa na alishindwa kumuelewa Matilda kwanini ameshindwa kumdhibiti Edna”.

“Abubakari yule Edna sio demu wa kawaida kama hawa mademu wa kunywa bia tunazo wanunulia , Edna namjua tokea akiwa mdogo na nimesoma nae, darasani yule aliekuwa akimzidi kiakili ni Ashley tu dada yake Denisi.”

“Hahaha.. kwahio unaniambia kwa akili zake ndio maana aliweza kuolewa na yule choko?”

“Abubakari hizo ni hasira zako , unajua mimi nimeamua kutokuwa kama wewe , ijapokuwa Roma namdharau lakini yule ni ligi tofauti na sisi na anajifanyisha kuwa ‘Humble’ tu , hivi unafikiri yule jamaa ni wa kawaida mpaka kuweza kumchukua Madam Neema au yule mwandishi wa Habari mtoto wa Mzee Kanani, Vipi kuhusu Dorisi au Edna mwenywe ?, Lazima tubadilike ,ili kumshinda lazima tumfahamu kwanza”

“Nyie mnaongea sana , ila kwangu mimi huyu Roma ambaye mmnazungumzia amekuwa ni kama ‘Role Model’ wangu na nataka nimtumie Sister Neema kufahamiana nae vizuri”Aliongea kiijana mmoja ambaye ana mwili wa kibonge ambaye muda wote alikuwa akiongea na Sali mjukuu wa raisi kigombola.

“Msechu unazingua”Aliongea Abubakari akionyesha kukasirika.

“Sio nazingua nyie ndio mnazingua , Elvice unafikiri Sister Neema ni mwanamke wa kujirahisisha tu kwa mwanaume?, nimejaribu kukaa na Baba yangu Mzee Chino na kupata habari mbili tatu kuhusu Roma unajua amenijibu nini?”

“Amekujibu nini?”Waliuliza wote watatu kwa pamoja na kumfanya Msechu kutabasamu na kisha kusimama.

“Oya sikieni wanangu, kuhusu mipango yenu juu ya huyu Roma mimi siwezi kumueleza chochote na nitakaa kimya , ila mtanisamehe kwanzia sasa hivi licha ya kwamba nina hela na urithi, lakini najitolea kuwa Chawa wa Roma”Aliongea na kisha huyo akaanza kupiga hatua na kuondoka akiwaacha Elvice na wenzake kuwa kwenye mshangao,

********

Naam ni siku ya jumamosi tena , katika wiki ya mwisho ya mashindano ya Kizazi nyota ambapo fainali za mashindano hayo zilitarajiwa kufanyika siku ya kesho yake, yaani jumapili, maandalizi yalikuwa makubwa sana kiasi kwamba jiji la Dar lilikuwa na shamra shamra nyingi , moja ya mambo makubwa ambayo yalikuwa yakitarajiwa siku ya kesho ni Christine kushiriki kama jaji kwenye fainali za maishindano hayo , lakini kitu kingine siku hio ni ujio wa mwanadada maarufu mrembo msanii kutoka Korea Kusini, ambaye alikuwa akitaajiwa kutumbuiza siku ya fainali hio akiwa kama mgeni rasmi, lakini pia siku hio hio watu walikuwa na hamu ya kumuona Sophia akitangazwa mshindi wa mashindano hayo ya Kizazi nyota kwani kwa namna ambavyo alionyesha kipaji kikubwa kipindi chote cha mashindano ilileta hamasa kubwa sana kwa mashabiki wengi na pia kwa wale ambao walikuwa wakipenda muziki.

Kampuni ya Vexto Media kupitia chaneli yao ya V TV ilitangazwa kwa mara ya kwanza kuwa kampuni ya kwanza kufatiliwa na watu wengi duniani kwa muda mfupi sana tokea kufunguliwa kwake, mafanikio ambayo yaliipaisha sana kampuni mama ya Vexto Group lakini pia kulifanya taifa la Tanzania kujitangaza Zaidi kimataifa.

Umaarufu wa kampuni ya Vexto Media , sambamba na mkataba mnono wa malighafi mpya ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa ndani ya mwezi wa kumi na mbili ulifanya hisa za kampuni ya Vexto kuzidi kupamda thamani kwa kiasi kikubwa sana na kumfanya Edna utajiri wake kuzidi kuongezeka kwa asilimia kubwa, jambo ambalo liliwaacha midomo wazi baadhi ya matajiri na wafanyabiashara wakubwa wa Afrika wenye uzoefu, huku wakijiuliza imewezekanaje msichana mdogo kama Edna ambaye ndio kwanza alikuwa kwenye umri wa kati ya miaka ishirini Kwenda therathini kuweza hayo yote.

Wakati matajiri hao wakiendelea kujiuliza juu ya mafanikio ya Edna kwa mwaka huo , upande wa nyumbani kwa Edna ,Osterbay, Edna alionekana kutojali sana kile ambacho kilikuwa kikiendelea au kilichokuwa kikizungumziwa juu yake , mrembo huyo siku hio alionekana kuwa na wasiwasi mno kuliko siku zote ambazo ashawahi kuonekana kuwa ni mwenye wasiwasi.

Kulikuwa na jambo kubwa ambalo lilikuwa likitegemewa ndani ya familia hio kwa siku hio ya jumamosi , jambo ambalo lilimfanya Edna kushindwa kabisa Kwenda kazini, jambo lenyewe lilikuwa ni juu ya ahadi ya ya babu yake Lanlan.

Kabla Lanlan hajaanza kuishi na familia ya Edna, babu yake aliacha ahadi kwa kupitia Mama Issa wa kituo cha Son And Daughter, kwamba kama asipoteokea baada ya siku ishirini na tisa basi Lanlan rasmi angekuwa mzazi halali wa Edna na Roma.

Sasa siku hii Edna pamoja na Roma walibakia nyumbani kwa ajili ya kusubiria ujio wa babu yake Lanlan , upande wa Roma alikuwana hamu ya kumuona babu yake Lanlan kwani alikuwa na maswali mengi juu yake huku upande wa Edna alikuwa akiomba babu yake Lanlan kutotokea kabisa siku hio , upande wa Qiag Xi yeye alikuwa akitamani kumuona babu yake Lanlan siku hio kwani kwake ilikuwa ndio njia pekee ya kujua kama babu yake Lanlan atakuwa salama au amekufa , kwa lugha nyepesi Qiang Xi alikuwa akijua kama babu yake Lanlan asipotkea siku hio basi ni dhahiri kwamba misheni yake imefeli hivyo hawezi kumuona tena na kama atatokea basi misheni imefanikiwa , sasa yeye alikuwa akiomba atokee siku hio.

Hivyo katika wanafamilia ambao walikuwa na wasiwasi Zaidi ni yeye pekee , yeye ndio aliekuwa akijua nusu ya ukweli wote wa kila ambacho kinaendelea na ndio maana alikuwa ni mwenye wasiwasi sana kuliko mtu yoyote yule na hata Blandina na Bi Wema waliweza kuona wasiwasi wa Qiang Xi na waliishia kumtia moyo na kumwambia babu yake Lanlan atatokea.

Upande wa Yezi yeye alikuwa ashaenda kwenye mgahawa anaofanyia kazi kwa ajili ya kujipatia riziki kama kawaida yake na kwa upande wa Sophia yeye alikuwa kambini tokea mashindano yaanze.

Asubuhi hio Edna, Roma na Lanlan walikuwa wamepumzika juu kabisa ya nyumba yao kwenye ‘Living Lounge’ Roma alikuwa akicheza gemu na Lanlan, upande wa Edna yeye alikuwa amejiegamiza kwenye sofa akiwa anasoma kitabu , licha ya kuwa na wasiwasi lakini kwa namna moja ama nyigine mrembo huyo alionekana sura yake kuwa na furaha, kila alipokuwa akisoma peji kama nne hivi alikuwa akiangalia watu waliokuwa mbele yake wakicheza gemu.

Lanlan na Roma walikuwa bize wakicheza gemu kwenye PS5 ambayo ililetwa kama zawadi na Kasimu mtoto wa Tajiri Azizi alipokuja kuwatembelea Edna na Roma siku ya jumapili, akiwa ameambatana na mrembo Donyi.

Siku hio ya jumapili Roma , Kasimu , Lanlan na Donyi walishindia kucheza gemu , ukweli Roma alipenda sana magemu yaliokuwa kwenye hio PS5 kiasi kwamba alidhamiria kununua ya Kwenda nayo ofisini , kwani gemu la kulipwa alililokuwa akicheza ofisini halikuwa likisisimua kama magemu yaliokuwa kwenye PS5, moja ya gemu ambalo lilimvutia Roma pamoja na Lanlan ni gemu moja lililofahamika kwa jina la Multiversus.

Siku hio ya jumapili upande wa Donyi alikuwa akimwangalia Roma pasipo ya kummaliza na yote hayo ni kutokana na kujua mahusiano yaliokuwepo kati ya mama yake na Roma , alikuwa ni kama haamini mama yake ambaye alikuwa mtu wa kujiheshimu anaweza kutoka na Roma , ukweli kwake sio kwamba Roma hakuwa na hadhi ya kutoka na mama yake , kitu ambacho kilimfanya kutokuamini ni kutokana na kupishana kwa umri wa mama yake na Roma , yeye ndio aliejiona kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutoka kimapenzi na Roma na sio mama yake , sasa jambo hilo kwake lilikuwa lina mchanganya kwani ni kama alikuwa na hasira ndani ya moyo wake mara baada ya kungundua jambo hilo, upande wa Roma aliona mabadiliko ya Donyi kwa namna ambavyo alikuwa akimwangalia ila hakujali sana , alijua huenda Donyi alikuwa ashafahamu uhusiano uliokuwepo kati yake na mama yake, hivyo alipotezea mpaka pale walipoondoka.

Sasa Lanlan tokea kuletwa kwa hilo gemu nyumbani wiki nzima alikuwa akicheza tu, alimlazimisha hata Bibi yake Blandina pamoja na Qiang Xi kukaa kwenye runinga kucheza nae , lakini kutokana na wote wawili kutokuwa na uzoefu wowote kuhusu magemu waliishia kumkatisha tamaa Lanlan kabisa kwani hakuwa akipata msimsimko unaotokana na ushindani.

Lanlan alikuwa na kichwa chepesi mno , Kasimu alimwelekeza kidogo tu namna ya kutumia Pad na baada ya lisaa limoja tu ya Lanlan kushika Pad hizo ni kama alikuwa mzoefu wa miaka mingi kucheza magemu, jambo ambalo lilimshangaza sana Kasimu na Donyi , lakini pia lilimshangaza Edna na Roma kwa uwezo mkubwa aliokuwa nao , kwani halikuwa jambo la kawaida kwa mtoto ambaye hata darasa la Awali hajaanza kuweza kumudu kucheza magemu mazito mazito yaliokuwa kwenye PS kama vile Call Of Duty na mengineyo magumu.

Sasa siku hii wakati wakiendelea kusubiria ujio wa babu yake Lanlan , Roma alikuwa akishindana kucheza gemu na Lanlan huku Edna akiwa ameketi nyuma yao akijisomea kitabu, kwani yeye hakuwa mpenzi wa magemu.

Kwa jinsi Roma na Lanlan walivyokuwa siriasis kucheza gemu la Multversus , huku wakionekana kufurahia kile walichokuwa wakikifanya mrembo huyo aliishia kutabasamu na hali ya kuombea babu yake Lanlan asifike ikizidi kuongezeka, Edna alijiambia ni jambo zuri sana kuwa na familia.

Roma alishangazwa na uwezo wa Lanlan wa kuelewa vitu kwani kwa jinsi ambavyo alikuwa akicheza gemu hilo ni kama alikuwa akicheza na mtu mzima mwenye uzoefu, upande wa lanlan alionekana kuwa na msisimko kweli , kila alichokuwa akikifanya kwenye gemu hilo ni kama akili yake ilikuwa ikikifanya laivu na sio gemu , hali hio ilimpelekea kumpa upinzani mkubwa sana Roma , lakini upande wa Roma kwakuwa hakua tayari kushindwa alijitahidi kutokupoteza mbele ya mtoto mdogo kama Lanlan.

“Wife njoo ucheze kidogo”Aliongea Roma huku akimgeukia Edna.

“Sipendelei kucheza magemu”

“Ushawahi kucheza?”

“Sijawahi”

“Sasa unasemaje hupendelei wakati hujawahi kucheza , njooo nikuelekeze ushindane na Lanlan” Aliongea Roma na kumfanya Lanlan aliekaa pembeni kumwangalia mama yake kwa namna ya kuomba na Edna mara baada ya kuona nammna ambavyo Lanlan amemuangalia ilibidi asogee.

Roma alibadili gemu na kuweka la F1 na kisha akaanza kumuelekeza Edna namna ya kucheza.

Sasa wakati hayo yakiendelea upande wa mlango wa kuingilia alionekana Blandina akiwa amesimama huku akiwa ameshikilia glass za juisi na alionekana alikuwa akiingia hapo ndani kwa ajili ya kuwaletea.

Blandina alijikuta machozi ya furaha yakimtoka , alionekana kushindwa kujizuia kwa namna Roma alivokuwa akipatana na Edna hapo ndani , lakini pia pamoja na uwepo wa Lanlan, alitamani kuona Maisha ya aina hio kwa wawili hao yakiwa endelevu.

Hata zile juisi alizoshikilia aliamua kurudi nazo ,kwani hakutaka kusumbua watu ambao walikuwa kwenye starehe yao.

Baaada ya lisaa la Roma kumuelekeza Edna na kumuoneysha namna ya kucheza , Edna alijikuta akivutiwa mno na sasa ni kama ashaanza kuzoea namna ya kucheza na alijikuta hata mawazo ya babu yake na Lanlan yakimpotea kwa muda.

………………..

Naam hatimae ikafika mpaka usiku pasipo ya babu yake Lanlan kutokea , Edna alionekana sasa kuanza kupata amani ya moyo , ijapokuwa siku haikuwa imeisha kwa minajiri ya kwamba inaisha saa sita kamili usiku, bado babu yake Lanlan alikuwa na nafasi ya kutokea kwenye muda huo , bado hakuwa na amani na masaa yaliobaki kupita kwani hakuwa tayari kumuona mtoto wake Lanlan akichukuliwa na mtu mwingine , kwani alitokea kumpenda sana , Lanlan alikuwa mtoto wa kike na ni kama alikuwa akijiona yeye mwenyewe kenye utoto wake kupitai Lanlan , uwezo wa akili wa Lanlan pia ulimfurahisha sana na kuzidi kumpenda , lakini pia namna ambavyo walifanana na kufiti sana kuwa mwana na mama.

“Wife huna haja ya kuwa na wasiwasi tena , babu yake Lanlan hawezi kutokea kwa muda uliobaki”Aliongea Roma wakati wanafamilia wote wakiwa kwnye meza wakijipatia chakula cha usiku na Roma aliona amtoe wasiwasi Edna kutokana na kwamba mrembo huyo muda wote alikuwa akimwangalia Lanlan aliekuwa bize na chakula.

Sasa kauli ya Roma ni kama imemgusa Qiang Xi , kwani palepale alijikuta akianza kutoa machozi na kuwafanya wanafamilia hao akiwemo Yezi kuwa kwenye mshangao.

“Qiang Xi nini tatizo?”Aliuliza Blandina aliekuwa karibu yake na Qianq ni kama alichokozwa kwani alianza kulia kwa kwikwi na kuinuka kwenye meza na kukimbilia juu na kuwafanya watu wote kuwa na mshangao kwa kutoelewa ni nini kinaendelea , kwani kwa namna ambavyo mrembo huyo alionekana , ni kama mtu ambaye amempoteza mtu muhimu sana kwenye Maisha yake.

“Ngoja nikaongee nae”Aliongea Edna huku akinyanyuka.







SEHEMU YA 348.

Edna baada ya kuingia chumba anacholala Qiang Xi ilibidi amsogelee kwanza na kuanza kumbembeleza , Qiang Xi alionekana alikuwa akijikaza tu tokea asubuhi ila hakuwa na amani kabisa na muda huo kwake ilionena ilikuwa muda sahihi wa kuanza kuangaua kilio , mwanamke huyo wa kichina alionekna kuwa kwenye hali ya majonzi.

“Qiang Xi niambie ni nini kinaendelea, kwanini unalia hivi kama umefiwa?”Aliuliza Edna kwa upole na Qiang alizidi kulia kiasi kwamba ilibidi Edna amkumbatie ili kumpatia Faraja.

Baada ya kama nusu saa hatimae Qiang Xi alimuelezea Edna ahadi aliowekeana na Master juu ya kile kinachoendelea. Alimwambia kwamba kama babu yake Lanlan asipotokea mpaka ikifika asubihi maana yake ni kwamba kuna jambo baya ambalo limemkuta, maneno hayo yalimfanya Edna kuelewa kwanini Qiang Xi alikuwakwenye hali hio , hakuelewa kwamba yeye kufurahia kwake kulikuwa kukimuumiza Qiang Xi kwani kutoonekana kwa Master Chi ilikuwa ikimaanisha kwamba atakuwa amekumbwa na jambo baya,

“Kwahio unasema babu yake Lanlan ameondoka kwenda kulipiza kisasi, je ni kisasi gani?”Aliuliza Edna kutokana na maelezo ya Qiang Xi.

“Master amekuwa msiri sana kwa kila anachokifanya , hivyo sijui kinacheondelea , ila kutokana na nilivyoagana nae naamini adui ambaye anashindana nae ana nguvu kubwa kuliko yeye na ndio maana akaniambia kama nisipotokea atakuwa amekufa”

“Miss Edna siwezi tena kumuona Master wangu mimi..”Aliongea Qiang huku akianza kula tena na ilibidi Edna aendelee kumbembeleza , hakujua ni namna gani anapaswa kumfarijji Qiang X.

“Qiang Xi sikiliza ninaamini kwa asilimia mia moja babu yake Lanlan atakuwa salama , kutofika siku ya leo kama alivyoahidi haimaanishi kwamba amepatwa na jambo baya , au kuna kilichomtokea , muda mwingine tunapanga hiki na Mungu anapanga kingine , hivyo hupaswi kuwa na huzuni , kwanzia sasa wewe ni mwanafamilia na utaendelea kuishi na sisi , hupaswi kuwa na huzuni sawa”Aliongea Edna huku akibahatisha , hakuwahi kubembeleza mtu kumfariji hivyo alijitahidi kadiri ya uwezo wake , lakini maneno yake yalionekana kuwa na nguvu , kwani Qiang Xi alionekana kidogo kupata tumaini jipya , alijiambia huenda ni kweli kama Master yake hatofika siku hio , basi huenda ni mpango wake umechelewa kukamilika , kwani siku zote mambo hayawezi Kwenda kwa muda unaopangwa na kuna dharula pia, hivyo aliona ashikilie kwenye maneno chanya ya Edna.

Roma baada ya kumaliza kula ilimbidi kurudi kwenye ‘Living Lounge’ ya upande wa juu kuendelea kuangalia taarifa ya Habari na dakika chache mbele Edna alikuja pia na kuketi na yeye kwenye sofa na ilibidi Roma amuulize kile ambacho kilikuwa kikimsumbua Qiang , na Edna aliweza kumuelezea ,Roma alishangazwa na maelezo hayo , kiasi cha kuzidi kupelekea shauku ya kutamani kumjua Zaidi kuhusu huyo babu yake Lanlan, kwa namna moja ama nyingine alihisi kabisa babu yake Lanlan hakuwa mtu wa kawaida , kutokana na namna ambavyo pia Lanlan alivyokuwa na uwezo usiokuwa wa kawaida.

“Romaa..!!”Aliita Edna kwa kivivu na Roma alimgeukia na kumwangali na Edna alionekana kusita sita.

“Unataka kuongea nini Babe”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu.

“Errmm.. unaonaje ukihamia chumbani kwangu”

“Hehe… Wife usiniambie unataka tu..”

“Ushaanza kufikiria mambo ambayo hayapo, unaweza kuhamia tukawa tunalala pamoja lakini…”

“Wife nipo tayari lakini hatufanyi , si ndio unachotaka kusema”Alimalizia Roma mara baada ya kuona Edna anashindwa kuongea na Edna aliitikia kwa kichwa.

Upande wa Roma aliachia tabasamu la kifedhuli , alijiambia inawezekana vipi akalala na mrembo kama huyo na asifanye nae , ila hakutaka kuongea sana alijiambia kila kitu kitaeleweka wakiwa kitandani , lakini pia aliamini huenda Edna amelazimishwa na mama yake walale chumba kimoja , hivyo aliona Edna anaweza kuwa kwenye wakati mgumu.

Roma alinyanyuka kwenye sofa alilokalia na Kwenda kukaa karibu na Edna na kisha akapitisha mkono kwenye bega la Edna na kisha kumwangalia usoni.

Upande wa Edna alijihisi mapigo ya moyo yakienda kasi mno , alijiambia yaani kabla tu hawajaanza kulala pamoja mtu tayari ashaanza mambo yake , alijiambia kitandani itakuwaje.

“Wife usiwe na wasiwasi najua unafikira yale mambo hehe..”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuona aibu na kuangalia pemben.

“Wewe ndio umefikiria hayo sio mimi usinisingizie”Aliongea Ednana Roma alitabasamu.

“Wewe ndio unanisingizia , Babe wife niangalie usoni kama kweli haujawaza mambo ya kichumbani chumbani”Aliongea Roma na Edna aliinua usona kumwangalia Roma na kukaza macho.

“Nimekuambia sina mawazo mengi ya kihuni kama wewe mimi , haya umeamini”Aliongea Edna Edna akijifanyisha kumkodolea Roma macho na dakika moja ilikuwa nyingi kwani alijishitukia amepigwa busu. kwenye lipsi na kumpelekea Edna kuona aibu .

“Naona unanichokoza sasa”Aliongea Edna huku akimfinya kwenye paja ,Roma alijikuta akichekeshwa na aibu za Edna na alisogeza mkono wake na kushika mkono wa kushoto wa Edna.

“Wife unaonaje tukifunga ndoa , sio ya makaratasi bali ya kanisani kabisa kwa kuvishana pete?”Aliongea Roma huku akiwa ameshika mkono wa Edna na maneno yake yalimwingia vizuri Edna , alijihisi ni kama anachumbiwa sasa, sasa hisia zilikuwa za aina yake , kwani yeye tofauti na wanawake wengine ni kwamba aliolewa kwanza kabla ya kuchumbiwa na sasa yupo kwenye ndoa na ndio anachumbiwa, aliona mambo yanaenda kinyume nyume na kimbelembele.

“Ofcourse mke wangu sio lazima unijibu sasa hivi , unaweza ukafikiria kwa mud ana ukanipa jibu”Aliongea Roma na Edna alimwangalia Roma usoni na kisha akatingisha kichwa kwamba anakubali , yaani kwamba atafikiria na Roma alitabasamu na wakaendelea kuangalia runinga wakiwa vilevile lakini baada ya nusu saa tu Edna alipotelea usingizini na kichwa chake kuegamia bega la Roma.

Roma alimwangalia Edna na kutabasamu na kisha alitumia uchawi wake kwa kumshika Edna kwenye shavu na usingizi wa Edna ukakolea Zaidi, alimbeba na kumpeleka mpaka chumbani kwake na akamlaza kitandani na baada ya kumaliza alishuka chini na kumchukua Lanlan ambaye pia alionekana kusinzia kwenye mikono ya bibi yake na kumpadisha juu na Kwenda kumlaza karibu na Edna , baada ya kuwafunika wote na kurekebisha AC alifunga chuumba na kutoka kabisa nje na kuingia kwenye chumba chake na alitoa simu yake na kisha akamtafuta Mage.

“Babe Afande umelala?”Aliuliza Roma mara baada ya kutuma ujumbe ulijjibiwa palepale.

“Sijalala , nipo nje ya Balconi inayoangaliana na upande wa nyumba yenu”ilisomeka na Roma alitabasamu na kisha akarudisha jibu kwamba anakuja na alivyoweka simu kwenye mfuko tu palepale akapotea.

********

Ni asubuhi ya saa moja kamili Edna ndio aliekuwa wa kwanza kuamka na baada ya kuangalia pembeni na kumuona Lanlan alitabasamu na kuendelea kujiuliza ni muda gani jana alipotelea usingizini.

Baada ya kukumbuka matukio ya jana usiku , ndipo alipokumbuka mara ya mwisho alikuwa eneo la sebule ya juu akiwa ameketi na Roma na ndipo alipopotelea usingizini, mpango wake jana ulikuwa ni kukaa mpaka saa sita usiku ndio alale , yaani ahakikishe siku hio inapita , lakini mpango wake haukuenda kama alivyopanga kwani alisinzia na sasa ni asubuhi ya siku nyingine , lakini uwepo wa Lanlan pembeni yake ulimwambia kwamba babu yake Lanlan hajafika na kwanzia muda huo Lanlan ni mtoto wake kamili na kilichobaki ni Kwenda kusaini karatasi kwenye kituo cha Son And Daughter Orphanage na baada ya hapo kumsajili Lanlan kama mtoto wake kabisa.

Edna alijikuta moyo wake ukiwa mwepesi sana , ni kama akili yake ilikuwa sasa ishatulia kwani wiki kadhaa nyuma alikuwa akiishi kwa kuhofia babu yake Lanlan anaweza kutokea muda wwote na kumchukua , lakini hatimae siku za ahadi zimekwisha isha na sasa alikuwa na maamuzi yote juu ya Lanlan.

“Ni muda wa kukutafutia shule sasa”Aliongea Edna huku akimshika Lanlan kichwani kwa kumbembeleza na kisha akanyanyuka.

Kwasababu ilikuwa jumapili aliona aende moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha Roma ili amuambie waelekee wote Kiwangwa kwa ajili ya kumsalimia MaMa Issa na pia kukamilisha taratibu za kumlea Lanlan.

Edna baada ya kufika kwenye chumba cha Roma alisukuma mlango taratibu na alitabasamu mara baada ya kumuona Roma bado akiwa amelala,alisogea mpaka kwenye kitanda na kumwangalia Roma kwama dakika kadhaa na alijikuta akighaili kile ambacho kimemleta na alitembea na kutoka kabisa nje.

Sasa wakati wa anatoka tu nje Roma alifumbua macho na kutabasamu na kisha alijifunua shuka na kuamka na mavazi aliokuwa nayo jana ndio hayo hayo na ilionyesha kabisa ndio alikuwa akirudi kutoka kwenye harakati zake.

“Ningechelewa dakika chache tu , asingenikuta humu bora nimewahi”Aliongea Roma kisha akavua nguo na kuingia bafuni kwa ajili ya kuuweka mwili wake safi.

Saa mbili kamili wote walijumuika kwenye meza na kujipatia kifungua kinywa.

“Mama leo tutamsajili Lanlan kama mtoto wetu na kuanza kumlea”Aliongea Edna na Blandina alimwangalia na kisha akamgeukia Roma ,nikama alikuwa akiwaaangalia kusoma kitu kabla ya kutoa jibu.

“Kama ndio mlivyokubaliana hakuna shida , mwenyewe nimetokea kumpenda Lanlan na nafurahi nitaitwa bibi”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kutabasamu.

“Ni rahisi sana kumpenda Lanlan kwasababu ni mtoto asie msumbufu lakini pia ana akili nyingi sana na isitoshe anafanana kwa asilimia kubwa na Edna mama yake ”Aliongea Roma.

“Anko Roma , Lanlan pia anafanana na wewe , hebu angalia hicho kichwa na midomo”Aliongea Yezi.

“Lanlan hafanani na anko , Lanlna anafanana na mama yake”

“Chubi Girl unafanana na mimi”

“Mimi sio Chubi na sifanani na wewe nafanana na mama”Aliongea Lanlan huku akimwangalia Roma kwa macho flani ya mtoto aliekasirika.

Bi Wema aliekuwa kimya muda wote alikuwa akitoa tabasamu ambalo liliashiria huzuni ndio pekeeambaye hakuwa akielewa kingereza vizuri.

“Bi Wema hatimae umepata mjukuu”Aliongea Edna kwa tabasamu.

“Miss Edna uwepo wa Lanlan umekubadilisha sana umekuwa muongeaji , nimefurahi Mungu kukubaliki kwa kumpata mtoto mzuri kama Lanlan”Aliongea Bi Wema na wote walitabasamu kumuunga mkon.

Qiang Xi upande wake licha ya kwamba alikuwa na mawazo , lakini alijiambia Lanlan anabahati kuwa kwenye familia kama hio , alitamani hata Maisha yake ya utoto awe na familia kama hio ambayo watu wote walionekana kujaa upendo , ijapokuwa alificha kile anachokijua kuhusu Lanlan lakini aliona ni vilevile tu hata kama wasipofahamu , Lanlan bado atabakiwa kuwa mtoto wao.

“Nilikuja asubuhi chumbani kwako tuongee kuhusu Kwenda kusaini zile karatasi , ila ulionekana kulala”Aliongea Edna baada ya kumsimamisha Roma aliekuwa akitaka kuingia chumbani kwake.

“Wife unaona hatia kutomjulisha mumeo kwanza? How obedient.”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa kuashiria jibu ni ndio na Roma alimsogelea karibu.

“Kajiandae twende tukasaini wote , ili kupata haki kamili ya kumlea Lanlan kama mtoto wetu, Lanlan ni mtoto mzuri sana na mawazo yako ya kumlea yalikuwa sahihi tokea mwanzo”Aliongea Roma na Edna alitabasamu na kutingisha kichwa na kisha akaelekea chumbani kwa ajili ya kujiandaa.

Jumapili mara nyingi wanaenda na Yezi, lakini kwasababu Yezi siku hio alitakiwa Kwenda zamu kwenye mgahawani kazini kwake , basi ilibidi Roma na Edna waende pamoja na Qiang Xi.

Baada ya masaa mawili kupita Roma na Edna waliweza kufika kituoni na kuonana na mama Issa ambaye alikuwa ndio kwanza anatoka kanisani na waliweza kusaini karatasi zote kama ilivyokuwa ahadi na Lanlan Rasmi akawa na wazazi yaani Edna na Roma.

Ni jambo la ajabu kweli ambalo Mungu amefanya kwa wawili hao kwanzia siku wanakutana mpaka miezi sita hio yote kamili, ni mengi sana ambayo yamewatokea kwa muda mfupi sana.

“Wife tunaanza maisha mapya mimi na wewe , mkataba wetu wa ndoa tarehe yake ya mwisho ni leo , Unakumbuka?”Aliongea Roma akiwa ameshika Lanlan mkono mmoja wa kulia huku na Edna akiwa ameshika mkono mmoja wa kushoto , wote walikuwa wamesimama kwenye pozi la kupiga picha.

“Nakumbuka”Alijibu Edna.

“Maisha yetu yamekuwa ya kipekee siku ambayo tulipanga kuachana ndio siku rasmi tunakuwa baba na mama , Hehe .. babe inaonekana Maisha yetu mimi na wewe yameamuliwa muda mrefu sana”

“Unahisi hivyo?”

“Ndio”Alijibu Roma na Edna alitabasamu.

“Bado nakumbuka ahadi yako tuliowekeana siku narudi na Lanlan, nadhani umesahau?”

“Nakumbuka mke wangu , unaonaje siku ya harusi yetu ndio nikatimiza ahadi?”

“Mbona unaongea kama nimekubali, si uliniambia nifikirie ndio nikupe jibu”

“Hehe… kwahio unapanga kunikatalia, hautaki kuvaa pete ya ndoa?, Babe napanga harusi yetu tukaifungie visiwa vya wafu , unaonaje? , utapata nafasi ya kujua kwanini naitwa mfalme Pluto”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumwangalia.



SEHEMU YA 349.

Edna baada ya kusikia maneno ya Roma alijikuta akifikiria kwa dakika kadhaa , ni kama alikuwa akisharabu maneno yake na aliishia kumwangalia Roma na kutoa tabasamu pasipo ya kutoa jibu na kumchanganya Roma Zaidi , kwani alishindwa kujua ni jibu gani Edna alikuwa akilifikisha kwake kwa kutumia tabasamu.

“Tuaongea kuhusu hili , Lanlan twende tukacheze na marafiki zako wapya”Aliongea Edna pasipo ya kusubiria neno kutoka kwa Roma ambaye alikuwa akikuna kichwa.

Edna alimchukua Lanlan na wakaungana na watoto wengine kuanza kucheza kwa furaha , Edna alisahau shida zake zote kwa madakika kadhaa na alijikuta akiwa kwenye ulimwengu wa Watoto.

“Mr Roma hongera sana , una bahati kweli, Lanlan na Edna ni baraka kubwa kwenye Maisha yako”Aliongea Mama Issa na kumfanya Roma kutabasamu na kumwangalia Edna aliekuwa mita kadhaa kutoka walipokaa.

“Asante sana Mama Issa”

“Kila ninapowaangalia hawa Watoto walivyokuwa na furaha sura ya mama yako Blandina inanijia akilini , Mr Roma nashukuru sana kwa kumsaidia mama kulinda kile alichokupambania kwa miaka mingi”.

“Huna haja ya kunishukuru nilichokufanya ni kidogo sana tofauti na kazi ambayo mmeifanya miaka na miaka, nitaendelea kuhakikisha vituo vyote ambavyo mama amevianzisha vinaendelea kudumu na kuimarika kihuduma ili kuendeleza ‘Legacy’ yake”Aliongea Roma na Mama Issa alijikuta akitabasamu.

“Mama Issa mtoto wako wa kwanza, Issa yeye yuko wapi?”Aliuliza Roma na mama Issa alitabasamu.

“Mtoto wangu wa kwanza sio Issa , mtoto wangu wa kwanza ni wa kike anaitwa Eunice ni nesi huko kisarawe, Issai ni mtoto wangu wa kiume wa kwanza na yeye ni daktari hospitali ya Mloganzila”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Dokta Issai!!”

“Unamfahamu?”

“Ndio , wakati nafika Dar kwa mara ya kwanza nilibahatika kupata lift kutoka Morogoro kwa mama mmoja anafahamika kama Mama Aisha na alinikaribisha kwake na ndipo nilipokuja kufahamiana na Dokta Issai”Aliongea Roma na Mama Issa alishangaa na kutabasamu kwa wakati mmoja.

“Ndio ni kweli , Familia ya mzee Mohamedi ni wakwe zangu , kumbe mlishawahi kukutana?”Aliongea na Roma alitingisha kichwa lakini muda huo huo simu yake ndogo ilianza kutoa mlio.

Roma licha ya kupewa simu kubwa lakini aliendelea kutumia simu yake ndogo ya Tecno sasa haikueleweka hakuwa akipenda simu kubwa au alifanya hivyo kwa ajili ya usalama kwani inaaminika simu za batani ni salama Zaidi kuliko Smartphone.

Aliekuwa akimpigia ni Daudi moja ya msaidizi wake kutoka kwenye kampuni ya Vexto Media , Roma kuona simu hio aliamini kuna jambo ambalo limetokea , kwani jumapili hio ilikuwa ni siku kubwa sana kwa kampuni , ndio siku ambayo kilele cha mashindano ya Kizazi nyota yanafanyika usiku.

“Director Can you return to the company immediately? , There is VIP that wants to meet you”Aliongea Daudi akimwambia Roma kama anaweza kurudi kwenye kampuni haraka, kwani kuna mtu muhimu ambaye anatakiwa kuonana nae.

Sasa Roma alishangazwa na swala hilo la mtu muhimu kwani kwenye mashindano hayo ya kizazi nyota mtu ambaye kwake alikuwa akimchukulia kama mtu muhimu ni Christen.

“Is it someone I know?”Aliuliza Roma kama ni mtu ambaye anamfahamu.

“Hahaha.. Director ni malkia kutoka Asia , Queen Yoo YeonHe Kutoka Korea Kusini”Alijibu Daudi na hapo sasa Roma alikumbuka juu ya huyu msainii kutoka Korea Kusini, tabia yake ya kutozingatia sana watu maarufu ndio iliomfanya kumsahau huyu msanii.

Ni kweli wiki zilizopita alitangazwa kuhudhuria kwenye mashindano hayo ya Kizazi nyota , lakini swala hilo alilichukulia kawaida tu , lakini kwa namna ambavyo Daudi alikuwa akiongea ilimfanya kushangaa kidogo , kwani alionyesha mchecheto wa hali ya juu ukiashiria kwamba msanii huyo alikuwa akimpa heshima zake.

Sasa kitu ambacho hakuwa amekifahamu Roma ni kwamba licha ya msanii huyo kutaka kuhudhuria mashindano ya Kizazi nyota , lakini pia alikuwa akipanga kufanya show ndani ya jiji la Dar es salaam , sasa menejimenti yake iliomba kampuni ya Vexto Media kuhusika katika maandalizi ya Show hio, hivyo ilibidi Daudi amuelezee kwa haraka haraka Roma , ili kuelewa umuhimu wa msanii huyo.

“Bado sijaelewa unachogusia ni nini , ushasema ni mtu muhimu, lakini hujanielezea kwaninni anahitaji kuonana na mimi?”Alijibu Roma kwa Kingereza.

“It’s the first time Miss Yoo visiting Tanzania and our Company and as Diretor , you have to personally answer her Questions about the Show as a sign of respect”

“Ni mara ya kwanza Miss Yoo anaitembelea Tanzania na kampuni yetu na kama Mkurugezni unapaswa kujibu majibu yake kuhusiana na Show yake moja kwa moja kama ishara ya heshima”Aliongea Daudi na kumfanya Roma kutabasamu, maneno ya Daudi yalimfanya ahisi msanii huyo ni mwenye maringo sana kwani hata kwa Daudi peke yake alikuwa akitosha sana kujibu maswali yake na sio lazima yeye.

“Okey nitafika muda si mrefu”Aliongea Roma na kisha akamgeukia Mama Issa na kumuelezea kuwa ana dharula , alimfuata na Edna nakumuelezea dharula yake na Edna alimwambia atangulie tu na gari kwani angemuita dereva wa kampuni na familia kuja kuwachukua.

Ndani ya dakika arobaini na tano tu Roma aliweza kufika Moroco na Kwenda moja kwwenye ofisi yake, na ile anakaribia nje ya mlango wa kuingia kwenye ofisi, kulikuwa na mabodigadi wanne wa kikorea waliovalia mavazi meusi na miwani za jua, huku wakiwa na nyuso ambazo hazikuonyesha utani.

Roma baada ya kuwafikia hakujihangaisha sana kuongea nao Zaidi ya kuruhusiwa kuingia , mabodigadi hao walionekana kuwa na uzoefu wa kutosha katika kufahamu watu ndio maana hawakumzuia Roma.

Roma baada tu ya kufungua mlango alikutana na hali ya utulivu isiokuwa ya kawaida , Daudi alionekana kuketi kwenye kona kwenye sofa huku Wendy akiwa ameketi katikati , wote wakionekana kuwa kwenye hali isiokuwa kwenye utulivu ni kama walikuwa na Raisi ndani ya ofisi hio..

Kwenye kiti chake cha kibosi cha mzunguko alionekana mwanamke mrembo ambaye amekikalia , alikuwa ni mwanamke mwenye nywele ndefu nyeusi alievalia blazia ya mkato wa chini kifuani rangi nyeusi , sketi fupi ya Rangi ya Zambarau isiokolea , pamoja na viatu vya rangi nyepe vya High heels, alikuwa amefumba macho akiupa mgongo mlango huku akiwa ameweka Earpods masikioni , alionekana alikuwa akiburudika kusikiliza mziki kutoka kwenye simu yaje ya kisasa.Alionekana kuvutia sana.

Daudi na Wendy baada ya kumuona Roma kafika walisimama na kisha walimpa heshima yake.

“Would you be Miss Yoonhee?”Aliuliza Roma akisema je wewe ndio Miss Yoonhee na yule mwanamke mwenye mwili mwembamba aligeuka na kumwangalia Roma , alikuwa amevalia miwani pia ya jua ukijumlisha na weupe wake alionekana kuwa mrembo Zaidi.

Alitoa miwani yake na kisha kabla ya kujibu alimwangalia Roma kuanzia chini mpaka kichwani na mwonekano wa Roma ni kama hakuwa ameridhishwa nao kabisa kwani alivuta mdomo, alionekana ni mwanamke mwenye maringo na kujisikia sana kwa kumwangalia tu.

Roma kwa haraka haaka baada tu ya kumwangalia aliamini YoonHee miaka yake sio mingi sana ni juu ya miaka ishirini Kwenda ishirini na tano.

“Are you Director Roma?”

“Yes I am. I was dealing with some urgent matters , so I was late as I didn’t know you would be visiting , Miss Yoo.. my apologies”

“Ndio ni mimi , nilikuwa na kazi muhimu hivyo nimechelewa kwani sikufahamu kama utatutembelea , Miss yoon niwie radhi”

“Huna haja ya kuomba msamaha Director nadhani unajiuliza kwanini nimekuja hapa kwenye kampuni ,labda pia unawaza nimekuja kujionyesha tu kwako juu ya ukubwa wangu, si ndio?”

“Sio kweli Miss , nilipaswa kukutembelea Malkia kama wewe baada ya kufka hapa nchini kukushukuru kwa kushiriki kwenye mashindano yetu kwani umetuongezea umaarufu”

“Oh!, Kwaninni unaniita hivyo Mkurugenzi?, Haufahamu kama nachukia sana kuitwa jina la ‘Malkia’ , linanifanya nionekane kama nina maringo sana na kuwa wa matawi ya juu na wengine”Aliongea kwa mapozi na Roma alitamani kucheka , yaani mwanamke mwenyewe alionekana kujiona wa matawi ya juu na mwenye maringo lakini wakati huo huo anajifanyisha sio wa matawi , matendo na maneno vilikuwa vitu viwili tofauti , ndio alichoweza kuona Roma , ukweli Roma alikuwa akijitahidi sana kujishusha ili asimkasirishe mgeni wake lakini aliona kunakoelekea atakaosa uvumilivu kwani alikuwa akichukia mno dharau.,

“Oh ! kwasababu Miss Yoon hupendi kuitwa Malkia basi sitorudia tena kukuita hivyo, nilikuwa nikijaribu kukupamba tu”Aliongea Roma.

“Hahaha.. Director mbona unaonekana kama ni mwenye kukasirika , nafikiri unahisi mimi ni ngumu sana kunifurahisha , si ndio?”Aliongea yule mrembo wa kikorea na Roma na yeye aliishia kucheka pasipo kujibu chochote na kisha akamgeukia Daudi ambaye anatokwa na jasho muda wote.

“Tunapaswa sasa kuongea kabla ya chakula cha mchana ,Miss Yoon tuongee hapa hapa au tuelekee kwenye ukumbi wa mkutano?”Aliongea Daudi baada ya kusimama.

“Subirini kwanza.., sijasema nataka kuongelea mambo ya kikazi kwanza , naona nyie watu hamnipi heshima ninayostahili , nadhani mnaelewa mchango wangu kwenye kampuni yenu kupitia umaarufu wangu, Director nataka kuonana na CEO mwenyewe”Aliongea YoonHe na akaendelea

“You are the only director of branch company and therefore you do not possess the qualities and status to talk to me”

“Wewe ni mkurugezi wa kampuni hii tanzu pekee na huna viwango na hadhi ya kuongea na mimi mambo ya kibiashara”Aliongea kwa maringo huku akimwangalia Roma.

Alichokuwa akimaanisha huyo mwanamke ni kwamba alikuwa akitaka kuonana na Edna ambaye ndio CEO wa makampuni yote na sio Roma ambaye ni Director tu wa kampuni ndogo kama Vexto , yaani alimuona Roma wa kawaida sana.

“Miss Yoon , mpangilio wa kazi utachelewa kutokana na sababu zako ambazo hazina msingi”Alijibu Roma.

“Mr Roma nataka kwanza utambue wazi , nafanya kile ambacho nataka siku zote na sijali kama kazi zenu zitachelewa au lah, hayo hayanihusu ninataka kuonana na Boss wako”Aliongea kwa sauti ya kunyari huku akitoka kwenye kiti na kumsogelea Roma .

Daudi na Wendy walijikuta kwenye wakati mgumu mpaka hapo , lakini kwa upande wa Roma alionekana kutokuwa na wasiwasi, Rom alimsogelea YoonHe karibu kabisa na kuanza kumchunguza kwenye uso wake kama vile mtu anaetafuta chunusi.

“Unafikiri nitakuogopa kwa kunisogelea karibu , nataka kongea na boss wako na sio wewe mwajiriwa, la sivyo sitashiriki usiku wa leo”

“Tsk!.. huu uso wako sehemu ulipoutengeneza, nikiri kwamba madokta wa kikorea kwenye kufanya Plastic surgery ni wabobezi , mtu wa kawaida unaweza kumdanganya kwamba umezaliwa na hii sura kumbe ni ya kutegeneza”Aliongea Roma huku akiweka na yeye mwonekano wa kijeuri. Yaani maneno yake ni kama aikuwa akimwambia Yoon He kwamba ni mbaya na nido maana akafanya plastic surgery.

“Mbwa wewe , sijawahi kufanya upasuaiji wowote kubadilisha mwonekano,niko hivi hivi tokea nipo mdogo usiniangalie kwa macho yako mabaya ,nashangaa imekuwaje mwanaume mshamba kama wewe ukawa mkurugezi wa kampuni ya burudani na Habari, hili taifa limejaa vituko na ufisadi tu”Aliongea kwa kebehi ,lakini kwa namna ambavyo alikasirika Roma alijiona mwamba kwani amegusa penyewe.

“Sijali sana kama umefanya upasuaji au lah ,kwanza utanifanya nini wewe, hutaki kuongea kuhusu kazi na umejileta kwenye kampuni yangu , nani wa kufanya kazi na mwanamke mbaya kama wewe uliefanya upasuaji ili uonekane mrembo,Daudi na Wendy tumuache kama aliyvyo na tuendelee na majukumu yetu”Aliongea Roma na kuwafanya Daudi naWendy kuangaliana,huku wakisita sita kunyanyuka , lakini mwishowe walisimama na kutoka kwenye ofisi hio , lakini ile wanafunga tu mlango, walijkuta wakisikia ukulele wa kilio kutoka ndani.

“Wewe nyani unapata wapi , ujasiri wa kunidharau , unanifahamu mimi ninakotoka ni nani?”Ilisikika sauti kwa nje , kwani aliongea kwa sauti mpaka mabodigadi wake wakaingia ndani.

“Mkurugenzi litakuwa jambo zuri kumwacha?”Aliongea Daudi kwa wasiwasi.

“Msiwe na wasiwasi, kama ataendeleza tabia yake,mnaweza mkamtoa kwenye mashindano yetu , kama kutatokea lawama basi nitazibeba mimi”Aliongea Roma na kuondoka.
 
SEHEMU YA 350.

Saa kumi kamili za jioni Edna , Qiang na Lanlan waliweza kurudi kwa kutumia gari la familia , kwa jinsi ambaho walikuwa akionekana ilionyesha ni dhahiri walitoka kituoni muda mrefu na baada ya hapo walipitia Shopping, kwani ukiachana na Lanlan ambaye alibeba mdoli mkubwa wa Simba , lakini Qiang na Edna walikuwa wamebeba mifuko mingi ambayo ndani yake ilionyesha kulikuwa na nguo na vitu vingine.

Wakati Edna anafika , Roma alikuwa asharudi muda mrefu tokea asubuhi na hata chakula cha mchana alipatia hapo hapo nyumbani.

Edna baada ya kuingia ndani sebuleni alimuona Roma akiwa amekaa peke yake sebuleni akiangalia runinga na alisogea na mifuko yake na kuiweka kwenye meza na kisha akamgeukia Roma.

“Babe Wife mbona unaniangalia kwa macho makali hivyo nilitegemea utanipa busu la motomoto mumeo?”Aliuliza Roma mara baada ya kuona Edna anamwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida.

“Kwanini ukafanya makosa ya kuharibu uhusiano wa kibiashara na YoonHee msanii mkubwa kutoka Korea, hujui umuhimu wake kwetu”Aliongea Edna kwa sauti ya chini lakini iliojaa usiriasi na Roma baada ya kusikia Edna anamzungumzia mwanamke yule wa asubihi aliishia kutojibu na Edna alikaa kwenye sofa karibu yake.

“Ila nimeshangazwa imekuwaje kwa mara ya kwanza ukashindwa ku’mhandle’ vyema mwanamke mrembo kama YoonHee mpaka mkaishia kwenye ugomvi”Aliongea Edna huku akikagua mifuko iliokuwa juu ya meza., sasa kauli yake ilimfanya Roma kukohoa kuzuga.

“My Dear wife , mimi sio jogoo wa kudandia kila mwanamke ninaemwona”.

“Jogoo anadandia kuku tetea na wewe sio kuku”Aliongea Edna huku akipotezea maneno ya Roma.

“Babe unachotakiwa kuelewa yule YoonHee ni mtu mbaya sana na mwenye maringo , kwahio sikutaka kujihangaisha nae , hata hivyo hatumuhitaji siku zote nitu akinionyesha dharau na mimi namuonyeshea dharau”.

“Wewe ni mkurugenzi wa kampuni na unapaswa kujua sio watu wote utakaofanya nao kazi watakuwa na tabia unazotaka , inabidi uepushe matatizo kwani yataharibu taswira ya kampuni”

“Babe unaongea kama vile ushakutana nae,kakuletea shida na wewe?”

“Hajaniletea shida , ila baada ya uongozi wake kuwasiliana na mimi ilibidi niende na Lanlan mpaka hotelini kwao kukutana nae na kutatua changamoto ulioisababisha”Aliongea Edna na kisha akatoa mifuko miwili kati ya mitano aliokuja nayo na kumpatia Roma.

“Kuna suti za aina tatu nimekadiria vipimo vya mwili wako, hivyo jaribu ipi itakupendeza na baadae ndio utakayovaaa tukienda kwenye mashindano,hivi ni viatu pia nimekuchagulia kwa msaada wa Mama T , naamini vitakukaa vyema”Aliongea Edna na kumuonyesha mifuko mitatu yenye suti na mmoja wenye viatu.

“Mke wangu mtiifu , kumbe unajali sana mwonekano wa mume wako , unaonaje ukinisogezea shavu nikikupa busu kama zawadi”Aliongea Roma n kumfanya Edna kuona aibu na kumpiga kwenye paja , alijikuta akishukuru Qiang Xi hajui Kiswahili kwani maneno ya Roma aliona ni kama ya kutia aibu.

“Sio lazima muda wote uongee maneno yanayotia aibu, halafu nishakubaliana na Yoonhee na usiku wa leo tofauti na kuimba atakuwa jaji pamoja na Christen na siku atakayo imba ni siku ya Show ambayo kama kampuni utaisimamia , wasiliana na wafanyakazi wako kuwapa maagizo, sitaki kuingilia madaraka yako ya kiuongozi kwenye kampuni ndio maana sijawasiliana na Daudi,Muda umebaki mchache fanya mawasiliano sasa hivi ili waweke utaatibu”Aliongea Edna na kisha hakusubiri jibu alinyanyuka na kuchukua alivyokuja navyo na kumchukua Lanlan na wakapandisha juu.

……..

Ni muda wa saa moja za jioni Edna alikuwa ashajiandaa tayari, alikua amependeza haswa na vazi ambalo amechagua siku hio, alijiangalia kwenye kioo na kujikuta akitabasamu , ijapokuwa hakutumia vipodozi kwa wingi , lakini sura yake ilionekana kama ya mtoto kwa ulaini wake.

Upande wa Roma suti za bei ghali zote ambazo Edna alizinunua zilimkaa vyema kwenye mwili wake na alitabasamu na kuona kumbe Edna licha ya kuwa mwanamke kauzu anaejali biashara lakini anajua namna ya kupima mavazi yake,suti ya samawati ndio aliona inafaa kwa ajili ya usiku huo.

Blandina , Yezi ,Qiang na Bi Wema wao hawakuwa wakienda, walikuwa wakitaka kufatilia wakiwa hapo hapo nyumbani kupitia runinga , hivyo walikuwa wakichukua jukumu la kukaa na Lanlan.

Wakati wakiwa wapo sebuleni wakiendelea kuangalia matangazo kutoka kituo cha televisheni cha V Tv ,hatimae walijikuta wakishtushwa na sauti za viatu kutoka juu na wote waliikuta wakigeuza macho kuangalia , kila mmoja alijikuta akishangaa namna ambavyo Edna na Roma wamependeza, haikueleweka ilikuwaje wakashuka wote kwa wakati mmoja, lakini kwa jinsi ambavyo walipendezana ilimfanya Blandina kusimama kabisa na kuwaangalia Watoto wake kwa tabasamu.

“Edna mwanangu umependeza sana ,upo kama Malaika ,hakika mmefana sana kuitwa mume na mke ”Aliongea Blandina na kumafanya Edna kutabasamu kiaibu aibu.

“Asante mama”

“Nisubirini mara moja nakuja”Aliongea Blandina na kisha alipanda ngazi mpaka gorofa ya pili na kuingia chumbani kwake na ndani ya dakika moja tu alirudi akiwa ameshikilia kiboksi. Cheusi.

Roma alimwangalia mama yake kwa sintofahamu , lakini Blandina alitabasamu na kisha alimsogelea Roma.

“Roma Shika hii , mvishe mkeo shingoni , ni zawadi yangu kwa Edna ila nataka umvishe wewe kama mume”Aliongea Blandina na Roma alipokea kiboksi chenye nembo ya ‘Tiffany’ juu,Roma baada ya kufungua kile kiboksi alijikuta akipagawa baada ya kuona mkufu wa madini ya almasi pamoja na dhahabu.

“Nilipewa kama zawadi na malkia wa Sweeden miaka miwili iliopita ni mkufu alioununua kupitia mnada kupitia kampuni ya Tiffany, ni zawadi yangu kwa mwanangu Edna”Aliongea Blandina kwa tabasamu na baada ya kuongea vile Yezi ndio aliekuwa wa kwanza kusogea ili kuangalia na macho yalimtoka , kwa kuaagalia tu ulionyesha ni mkufu wa bei sana.

“Mama asante sana lakini siwezi kuchukua kitu cha thamani kama hiki kutoka kwako”Aliongea Edna aliekuwa kwenye mshangao.

“Ni kweli Edna ni kitu cha thamani sana kutoka kwangu na ndio maana nakupatia kama zawadi, Roma mvalishe mkeo”Aliongea Blandina na Roma alitingisha kichwa na kusogea nyuma ya Edna aliekuwa akinukia kama jini.

Mkufu huo ni kweli Blandina alipewa na malikia wa Sweden kama zawadi kutokana na mchango wake aliokuwa akiufanya kwa jamii , wakati akiwa ni First Lady wa Kenya, ni mkufu ambao una mkanda wa dhahabu tupu huku ukiwa na jiwe la Almasi nyekundu, ni aina ya mikufu ambayo thamani yake haipungui wala kuongezeka hio ni kutokana na kwamba huwezi kukuta unauzwa kiholela na hata kama unauzwa basi huwa ni kwenye mnada maalumu na unaambiwa almasi hio wakati malkia wa Sweeden anainunua ilikuwa ni bilioni tano za kitanzania na ni miaka mingi , sasa kwa wakati wa sasa bei yake inaweza kuwa Zaidi ya hapo kwani madini ya Almasi nyekudnu ni adimu sana.

Roma alimvalisha ule mkufu Edna na baada ya kumaliza Edna alijikuta hata pumzi zikitoka kwa shida , alikuwa akijua amevaa kitu cha thamani kubwa kwenye shingo yake, ijapokuwa alikuwa na hela nyingi , lakini kupata mkufu kama huo ni kitu ambacho hela haiwezi kununua bali ni konekesheni.

Ndio duniani kuna vitu hela haiwezi kununua , kutokana na kwamba vitu hivyo thamani yake ni ‘priceless’ yaani kitu ambacho huwezi kukipigia mahesabu kutokana na uadimu wake.

“Babe wife huu mkufu sio kwamba tu unakuonyesha kama mtu mwenye hela , bali unaashiria heshima,mtu yoyote akiuangalia lazima atasema ni feki kutokana na thamani yake”Aliongea Roma kwa tabasamu.

Na alichoongea kilikuwa na maana , ni kweli hakuna mtu ambaye anaweza kuamini mkufu wa Edna ungekuwa ni origino, kutokana na kwamba sio watu wote wanaweza wakaununua kwa thamani ya pesa.

Kitendo alichokifanya Blandina ilikuwa ni kuonyesha kwamba alishamchagua kabisa Edna kama mke wa mwanae , kwa kutoa moja ya kitu chake cha thamani kubwa.

…………….

Roma na Edna waliweza kufika eneo la Mlimani City sehemu ambayo fainali za mashindano ya Kizazi Nyota ndio hufanyika kwa usiku huo tofauti na Kunduchi beach.

Eneo lote lilikuwa limejaa watu wengi sana ambao wamefika kumshuhudia Christine, ambaye alitarajiwa kuhudhuria kama jaji kweye mashindao hayo ya mwisho.

Waandishi wa Habari walikuwa wametapakaa kila kona , wakiangalia kila gari inayoingia na inayotoka.

Roma na Edna baada ya kutoka kwenye gari moja ya Roll Royce waliokuwa wakiendeshwa , licha ya kwamba hawakufahamika kwa watu wengi ,lakini kila mtu aliwaangalia kwa macho ya kuwashangaa kutokana na namna walivyopendeza, lakini pia gari waliotumia kufika nayo kwenye ukumbi huo iliwaheshimisha, ni watu wachache sana ambao walikuwa wakimjua Edna, lakini pia kilichowafanya wasifuatiliwe sana ni kwamba walikuja muda sawa na msanii YoonHe, hivyo waaandishi wahabari walikuwa bize kumpiga picha msanii huyo kutoka Korea..

“Babe umaarufu ni mzuri sana , unaona hata wewe uliefanikisha haya yote hakuna anaekujali”Aliongea Roma baada ya kushuhudia kundi la wanahabari likiwapita kwa haraka wakisogea eneo la maegesho baada ya kusikia ujio wa YoonHe.

“Umaarufu ni mzigo kwa mfanyabiashara kama mimi , ukiwa maarufu Maisha yako muda wote yanakuwa ya mashaka mashaka , nitaendelea kuwekeza kwa watu maarufu lakini sio mimi kuwa maarufu ni ‘liability’ kwangu”Aliongea Edna.

“Vipi kwa upande wa Sophia , mpaka sasa ashakuwa maarufu na anafatiliwa kwa kila kitu na yote yametokana na mchango wako wa kuwekeza katika maswala ya burudani , je ni hasara kwa Sophia au faida?”

“Kipaji na umaarufu vinaenda sambamba , muwekezaji kama mimi hakuna ulazima wa kuwa maarufu kwani hauna faida kubwa mimi ni muwezeshaji na tena umenikumbusha baada ya mashindano ya leo kama Sophia atashinda inabidi mfanye utaratibu wa kumuandalia menejimenti itakayomsaidia katika kazi zake za kisanii”

“Mke wangu kuhusu hilo usiwe na wasiwasi , nitamtafutia menejimenti ya viwango vya Christen”Aliongea Roma na walikuja kusimamishwa njiani na Amina.

Amina mara baada ya kumuona Edna alimkimbilia na kumkumbatia na kwakua Edna hakutegemea swala hilo ilibidi akubali tu na Roma alijikuta akifurahishwa na matendo ya Amina, aliamini kama Amina ataendelea hivyo basi itakuwa rahisi kwa wao kupatana.

“Wow! Miss Edna unaonekana kama malkia , natamani ningekuwa mzuri kama we….”Aliongea lakini aliishia njiani mara baada ya kuona mkufu aliovaa Edna kwa ukaribu.

“Edna huu…..”Aliongea lakini aijikuta akiishia njiani baada ya kuitwa na na Director wa mashindano. Hayo na aliishia kuangalia kwa mshangao ni kama hakuwa akiamini alichovaa Edna .

………..

Wakati Edna akisalimiana na baadhi ya wageni wanaomfahamu ,upande wa Roma aliweza kukutana na Daudi pamoja na Wendy ambao wamekuja pamoja , waionekana kama vile walikuwa wapenzi.

Muda huo huo wakati Roma akiongea na Daudi , mita kadhaa kutoka kwenye Red Carpet Roma alisogelewa na mrembo YoonHe, mrembo huyo kwa jinsi alivyokuwa akimsogelea Roma ni kama kuna jambo ambalo alitaka kuongea lakini vile vile alionekana kumsogelea Roma kwa hasira.

Sasa ile Daudi wanampisha YoonHe , Roma aliingiza mkono wake kwenye mfuko akitoa simu yake kubwa iliokuwa ikivibrate ,sasa kitendo cha kuivuta juu ilitoka na kitu ambacho kilidondoka chini paisipo ya uelewa wake.

Mrembo YoonHe wakati akishangawa na watu akimsogelea Roma, alijikuta akichuchumaa chini mara baada ya kuona kitu ambacho kimedondoka chini kilichotoka kwenye mfuko wa Roma na alionekana kukodoa macho.

Upande wa Roma baada ya kuona aliekuwa akipiga ni Sauroni alisogea kidogo pembeni pasipo ya kujua kuna kitu ambacho amedondosha na aliongea kidogo tu kwa lugha ambayo anaijua yeye na ile anageuka , alijikuta akikutana na sura ya mrembo Yoonhee ambaye amezingirwa na mabodigadi.

YoonHe muonekano wake wa sasa haukuwa wa kawaida hata kidogo tofauti na wakati alipoanza kumsogelea Roma , mwonekano wake ulibadilika mara baada ya kuokota kitu ambacho Roma amedondosha.

“Director this….!!!”Aliongea Yoonhe kwa mshangao huku akimnyooshea Roma kidani cha rangi ya platinum ya kung’aa, sasa Roma mara baada ya kugundua Yoonhee ameshika ‘pendant’ ambayo alipewa na Yezi kama mbadilishano na hela alizompatia siku yao ya kwanza kukutana ilibidi kumpokonye haraka Yoonhe kwenye mikono yake.

“Director hicho kidani ni cha kwako?”Aliuliza YoonHe kwa namna ya upole na kwa mara ya kwanza alionekana kuongea na Roma kwa heshima na Roma hakumjibu Zaidi ya kukirudisha mfukoni.

“That is a souvenir given by someone really important to me I don’t plan to show it to others but thank you, I almost lost it without knowing”Aliongea Roma akimaanisha ni kitu ambacho kinawakilisha kumbukumbu muhimu kutoka kwa mtu muhimu aliempatia na hana mpango wa kukionyesha kwa watu , wakati huo huo akimpa shukrani YoonHe kwa kukiokota kwa ajili yake kwani ni kidogo tu angekipoteza.

Sasa baada ya kujibu vile YoonHe alimwangalia Roma kwa mshangao mno , mkufu wenye kidani uliokuwa kwenye mikono yake aliuona kama kitu cha thamani sana.





SEHEMU YA 351

Roma tokea apewe mkufu wenye kidani na Yezi kule kigamboni, kwanzia siku ile alikuwa akitembea nao kwa kuuvaa shingoni mara kwa mara na alichukulia kama sehemu ya zawadi aliopewa na Yezi baada ya kubadilishana na pesa.

Roma alikuwa akikumbuka kwamba kidani hicho ndio kitu pekee kama kumbukumbu alichokutwa nacho Yezi akiwa kichanga mbele ya geti la kituo cha kulelea yatima Kiwangwa miaka iliopita , kitu ambacho ni kama utambulisho kwa wazazi wake waliomzaa.

Sasa Roma alikuwa akikichukulia kama kitu cha thamani sana kwake kutokana pia kwa Yezi ni kitu chenye thamani, wakati alivyokuwa nyumbani akijaribisha suti alizoletewa na mke wake kipini chake cha kufungia shingoni kilikatika hivyo akalazimika kukiweka mfukoni kwenye suruali yake.

Sasa wakati anatoa simu kubwa ya Smart , ndio kikadondoka nje ya uelewa wake , alivyomuona YoonHe amekishikiria ndio alishangaa na kuona kwamba angekipoteza na ingekuwa hasara kubwa kwa Yezi, kwani anakumbuka ndio kitu cha thamani sana kwa Yezi na alipanga siku moja kumrudishia , hivyo alimshukuru Yoonhee kwa kukiokota na kumrudishia lakini licha ya hivyo alijikuta akijiuliza maswali kwanini mwanamke huyo alikuwa akionyesha kukishangaa.

YoonHe hakuongea ,Zaidi ya kuondoka na mabodigadi wake kuelekea ndani , lakini ni muda huo huo Edna alimsogelea Roma na kumwangalia usoni , alikuwa ameona muda mrefu wakati YoonHe akiongea na Roma na alitaka kuuliza kama wamepatana.

………..

Kufika kwa Christine ndani ya maneno ya Mlimani City ilikuwa ni shangwe ya aina yake kwa mashabiki zake , kwani barabara yote ilikuwa imejaa kiasi ya kwamba magari yalizuiliwa kwa muda , Christine ilibidi ajitokeze juu ya gari kwa ajili ya kuwapoza poza mashabiki kwa kuongea nao.

Usiku huo alikuwa amependeza kweli kwa mavazi aliovaa, menejimenti yake kwa kushirikiana na kampuni ya Vexto Media walijitahidi sana kuhakikisha usalama wa Christine , watu waliridhika mara baada ya kumuona Christine alipojitokea kwa juu ya gari kwa dakika kadhaa, kilichowapagawisha Zaidi watanzania ni mara baada ya Christine kuongea nao kwa lugha ya Kiswahili kabisa, jambo hilo liliinua zogo kweli , kwani Christine aliongea bila kuchanganya maneno , ijapokuwa rafudhi yake ilikuwa imeathirwa na uzungu lakini aliongea vizuri.

“Nawapenda sana Watanzania Asanteni sana kwa mapenzi yanu kwangu , mmebarikiwa sana Tanzania”Aliongea Christen kwa nguvu kumalizia na hapo hapo aliingia kwenye gari na kuingia ndani ya uzio akiacha watu wakishangilia nje.

Ratiba kabla ya mashindano yenyewe kuanza ilibidi kwanza majaji kukutana na kuongea kwa nusu saa nzima kwenye ofisi ilioandaliwa ndio watokeze ukumbini, ilionekana walikuwa wakijadiliana namna ambavyo wanakwenda kugawa maksi.

Sasa baada tu ya kikao hicho cha majaji kumalizika , upande wa chooni(Restroom) alionekana mrembo Yonhee akipangusa simu yake kwa pupa kwa namna ya kutetemeka na dakika moja tu aliweka sikioni.

“My Daughter Yoonhee,aren’t you busy with your concert in Tanzania , why do you have time to call father?”

“Mtoto wangu Yoonhee si uko bize na Show yako huko Tanzania, kwanini umenipigia simu baba yako?”Sauti upande wa pili ilizungumza kwa lugha ya kingereza lakini iliojaa rafudhi ya kikorea yenye uzito.

“Dad, i… I seemed to have seen the other half Crescent”Aliongea akimaanisha kwamba ameweza kuona nusu ya kidani kingine chenye muundo wa mwezi. Akimaanisha kile kidani ambacho alimuokotea Roma. Na sauti upande wa pili ilikaa kimya.

“Tell Dad in detail and will take care of it”

“Niambie baba yako kwa maelezo marefu na nitachukua hatua”Ilisikika sauti upande wa pili nzito kidogo na palepale YoonHee alibadili lugha na kutumia Kikorea na kuelezea maelezo yote juu ya kidani hicho na kwa jinsi alivyoelezea hakukuwa na utofauti na mwonekano wa kile kidani cha Roma na baada ya kumaliza kuelezea alikata simu na kujiweka sawa na kisha akatoka nje.

Lisaa limoja mbeleni hatimae ukumbi ulikuwa ushajaa na majaji walikaa sehemu zao husika , Yoonhe akiwa upande wa kushoto huku Christen akiwa upande wa kulia na majaji wengine wakiwa katikati na kukamilisha jumla ya majaji watano.

Upande wa Roma alikaa mkabala kabisa na mke wake Edna eneo la VIP, wakati Edna akimtania Edna alionekana mwanaume mtanashati alievalia suti akapendeza akiwasogelea, mwanaume mwenyewe hakuwa mwingine bali alikuwa ni Denisi mtoto wa raisi Senga.

“Shemeji Edna , habari za kutokea siku ile?”aliongea Denisi akimsalimia Edna.

“Ni nzuri Habari za kwako Denisi?”

“Nzuri pia naona umependezana na Bro wangu nimpendae Roma Ramoni”Aliongea Denisi huku akimwangalia Roma,yaani Denisi alikuwa kama mtu ambaye alikuwa akitafuta tu ugomvi kwa jinsi aliavyokuwa mnafiki.

“Acha unafiki ,umekujakufanya nini hapa?”Aliuliza Roma.

“Mr Roma nadhani unajua kilichonileta , nimekuja kumuangalia mwanamke wa ndoto zangu akichukua ushindi”Aliongea Denisi.

“Kama ndio kilichokultea basi ondoka na kakae mbali na sisi na nikutahadharishe tu kwamba ukimfanyia Sophia jambo la kijinga nitakurudisha kitandani na hutoamka tena”Aliongea Roma akiwa siriasis na kumfanya hata Edna aliekuwa pembeni yake kuwa na wasiwasi.

“Huna maamuzi yoyote juu ya Sophia , siku ambayo nitaudhirishia ulimwengu kuwa ni mwanamke wangu , hutakuwa na haki ya kuongea maneno yako ya kipuuzi na kukuta hadharisha tu Mr Roma , kaa mbali na mimi pamoja na familia yangu”Aliongea Denisi huku akiweka tabasamu la dharau na Roma alitaka kuchukua hatua lakini Edna alimjua Roma angefanya hivyo na ndio maana alimshika mkono.

Edna alimwangalia Denisi kwa macho ya kumwambia kwamba aondoke na alifanya hivyo na kumfanya Edna kuvuta pumzi ya ahueni.

Naam hatimae mashindano yalianza rasmi na Sophia alikuwa ni msanii wa nne kuingia kuimba , jumla ya wasanii walikuwa watano tu walioingia fainali na wawili walitakiwa kuaga mashindano na kubakia watatu ambao kutapatikana mshindi wa kwanza mpaka wa tatu kwa kutumia upigaji kura wa mashabiki.

Hata hivyo mshindi alikuwa alishajulikana atakuwa muda mrefu kutokana na kipaji chake.

Upande YoonHe ni kama alifahamu Sophia ana uhusiano wa karibu na Roma , kwani alimwambia maneno ya kukatisha tamaa na kumpa maksi chache , lakini hata hivyo maneno yake hayakuwa na athari kubwa kwani majaji wote walimsifia Sophia.

Saa sita usiku wa manene ndio muda ambao Sophia aliweza kutangazwa kama mshindi , ilikuwa ni shangwe ukumbi mzima, Sophia alionyesha kustahili kutokana na juhudi zake pamoja na namna alivyoonyesha kipaji cha kuimba.

Baada ya Sophia kutangazwa kuwa mshindi ilibakia hatua ya kupewa zawadi yake rasmi , ambayo ilikuwa ni milioni mia moja za kitanzania kama mshindi wa kwanza , gari pamoja na mkataba wa kusainiwa na Vexto Media Record Label kama msanii , lakini pia na mkataba wa ubalozi wa kampuni hio.

Mshereheshaji ambae ni mrembo Amina Kanani alitoa utaratibu mzima wa namna zawadi zitakavyotolewa, wa kwanza kupewa zawadi alikuwa ni mshindi wa tatu ambaye alikuwa ni mwanaume na Naibu Waziri wa Sanaa Mheshimiwa Neema Luwazo ndio alipewa nafasi ya kumkabidhi mshindi wa tatu zawadi , mshindi namba mbili zawadi alikabidhiwa na Waziri kamili wa Sanaa na utamaduni , ndugu Sabiri jumbe .

Msindi wa pili alijinyakulia milioni hamsini za kitanzania , huku mshindi wa tatu akijinyakulia milioni ishirini na tano , baada ya zawadi hizo za awali kumalizika hatimae Sophia aliitwa stejini kwa ajili ya kupokea zawadi yake ya mshindi wa kwanza ,jambo ambalo liliibua shangwe kubwa sana.

Christen na YoonHee ndio waliopewa heshima ya kumpatia zawadi mshindi wa kwanza , ambayo ni hundi ya milioni mia moja.

Jambo hilo lilifanya watu kushangilia sana kiasi kwamba Sophia alishindwa kujizuia na kutoa machozi ya furaha , huku akipungia kila mmoja mkono, maua maua ya ushindi yalisambazwa hewani na kufanya tukio kupendeza sana na kuwa la aina yake kufanyika kwenye nchi yenye uchumi wa kawaida kama Tanzania.

Hatimae Sophia akakabidhiwa zawadi yake ya tuzo na hundi ya milioni mia moja kutoka kwa mastaa wa Dunia Christine pamoja na YoonHee.

“Mabibi na mabwana, hatua ya mwisho inayofuatia ni ya CEO wa kampuni kumkabidhi Sophia Athumani funguo ya gari , Miss Edna kwa heshima na taadhima tunakukaribisha stejini uongee machache yatakayohitimisha mashindano haya lakini pia kumkabidhi mshindi wetu zawadi”Aliongea Amina Kanani na kumfanya Edna kupagawa kwani huo utaratibu hakuwa akiufahamu na ilibidi amgeukie Roma aliekuwa pembeni yake na Roma alimtingishia mabega kwamba hajui chchocte , ukweli Edna hakupenda kuonekana kwani alijua tukio hili lilikua likifatiliwana mamilioni ya watu.

Roma baada ya kuona Edna anasita sita , alisimama yeye na kisha akamnyooshea mkono kijentleman kabisa na Edna aling’ata meno na kukusanya ujasiri na kisha akashika mkono wa Roma na kwa mwendo wa madaha kabisa walisogelea steji ya ukumbi huo huku wakipigiwa makofi.

Watu wengi walikuwa na shauku ya kumuona mrembo Edna Tajiri ,kwani ni wengi ambao walikuwa hawamjui kwa undani anaonekanaje , yaani Zaidi ya picha kadhaa zilizokuwa mtandaoni zilizokuwa zikionyesha sura tu ya Edna , hakukuwa na picha nyingi. Hivyo watu kushindwa kulijua umbo halisi la Edna.

Ukumbi ulitulia kimya ni muziki wa chini tu ndio uliokuwa ukisikika ,Edna kila hatua aliokuwa akipiga, kujiamini kulikuwa kukiongezeka na alishukuru sana uwepo wa Roma.

Upande wa Roma alikuwa akijiamini utadhani alikuwa mzoefu , yaani mwendo wake haukuonyesha hofu yoyote, lakini kutokana na kuwa’escort’ wa Edna watu walitaka pia kumtambua ni nani haswa kwani ni wachache sana waliokuwa wakimfahamu.

Wahudumu wawili ambao walikuwa na sahani iliokuwa na funguo ya gari ndani yake walikuwa washasimama kwa ajili y a kumruhusu Edna kuchukua ufunguo huo na kuendelea na hatua ya kumkabidhi Sophia, lakini kabla ya tukio hilo Christen alitoka sehemu aliokuwa ameketi na kusogea pia stejini na kufanya watu kuangalia ni kipi mrembo huyo anataka kufanya.

Amina alimpatia Christen maiki baada ya kupewa ishara.

“Mabibi na mabwana kabla ya hatua ya ugawaji Zawadi kwa Miss Sophia, lakini pia CEO wetu mrembo Edna kuhitimisha mashindano , ninajichukulia haki ya kuwatambulisha kwenu Miss Edna na Roma Ramoni kama moja ya watu wangu muhimu sana”Aliongea Christine na palepale ukumbu ukawa kimya na taa za rangi ziliangaza kwa kubadilika badilika na watu kusubiri Christine anakwenda kuongea nini.

Upande wa Roma alimwangalia Christen akishindwa kusoma anakwenda kuongea nini , na Edna hivyo moyo wake ulipiga kite hakufahamu ni jambo gani ambalo Christine anakwenda kuongea kama utambulisho.

Minong’ono ya sifa Kwenda kwa Edna ilikuwa ikiendelea ukumbi mzima Edna alionekana kama Malkia na kilichomfanya kupendeza Zaidi ni vazi lake lakni pia na kitu kilichokuwa iikitoa mwanga mwekundu kwenye shingo yake , wanawake wengi walijiuliza ni mkufu wa aina gani ambao mrembo huyo amevaa.lakini wakati huo huo wakishindwa kuzuia kusifia uzuri aliokuwa nao.

*********

Upande mwingine nyumbani anapoishi Nasra mama yake kutoka kijini alikuwa ashafika siku ya jana yake na kupokelewa na Nasra katika Stendi ya Mbezi Luis , Mama huyo tokea afike alikuwa akitaka kumuona Roma tu lakini Nasra alimpa kauli za uongo kumtuliza mama yake , Nasra hakutaka kumsumbua Roma kwakua alikuwa akifahamu alikuwa na majukumu ya kikampuni kutokana na mashindano makubwa yaliokuwa yakiendelea na mama Nasra baada ya kupewa sababu na mwanae ilibidi atulie .

Ukweli mama Nasra kwa jinsi nyumba ya mtoto wake ilivyokuwa nzuri , lakini pia namna ilivyokuwa mara yake ya kwanza kuishi juu ya Ghorofa , alijikuta akiona kama vile yupo pepo ndogo , Maisha hayo hakuwahi kuyaota wala kufahamu kama huko duniani kuna watu wana maisha mazuri kama hayo.

Nasra alijaribu kumtuliza mama yake kwa kumwambia kuna sehemu nzuri Zaidi ya hapo kwake , lakini mama huyo aliamini hakuna sehemu nzuri inayozidi nyumba anayoishi Nasra.

Apartment ya vyumba vitatu aliokuwa akiishi Nasra ilikuwa ni ya kwake kabisa aliinunua na sio kwamba amepangisha , hivyo ilikuwa sahihi kuita nyumbani kwake.

Sasa siku hio ya jumapili muda wa usiku Nasra na mama yake hawakulala walikuwa macho wakishuhudia shindano la Kizazi nyota, Nasra wakati akiwa ameenda chumbani kuchukua simu yake alioisahau akimwacha mama yake Sebuleni , mara alisikia akiitwa na mama yake mfululizo

“Mama kuna nini?”

“Mumeo mtarajiwa yupo kwenye Tv”Aliongea Mama Nasra kwa pupa huku akikaa vyema kwenye sofa akiwa kama mtu ambaye haamini anaemwangalia ni Roma mchumba wa mwanae .

Sasa Nasra baada ya kuangalia vzuri ndio anamwona Edna na Roma wakiwa jukwaan na moyo wake ulipiga kite.

“Nasra yule mwanamke ni nani?,mbona kama wanaonekana ni wachumba? Halafu mzuri huyo ”Aliongea Mama Nasra huku akikodoa macho kwenye runinga kuangalia kinachoendelea licha ya kusikia stori kuhusu Edna ila hakuwahi kumuona na ujio wa hapo Dar ni kufunga safari nyumbani kwa Edna na Kwenda kumpa shukrani kwa kumsaidia mtoto wake mpaka kuwa na mafanikio aliokuwa nayo.
 
SEHEMU YA 352.

“Ningependa niseme licha ya kwamba nilikuwa nikitamani kuja Tanzania , nchi hii ambayo imebarikiwa na vitu vingi vya kvutia macho , lakini sikuweza kujua ni siku gani ambayo natakiwa kufanya maamuzi ya kufanya safari mpaka nilipopata mualiko maalumu kutoka kwa rafiki yangu Mr Roma Ramoni”Aliongea Christen na kisha akamsogelea Roma na kumshika mkono na kufanya watu wote kushangazwa na maneno ya Christen juu ya Roma kumwalika Christen Tanzania , watu walianza kunong’ona na kujiuliza Roma ni nani haswa mpaka kuwa na urafiki na msanii mkubwa kama Christen, kwani hata maraisi wengi ndani ya ukanda wa Afrika washawahi kuonekana hadharani wakimualika mrembo huyu kutembelea kwenye nchi zao , lakini Christen hakuwahi kutii mualiko kutokana na ubize , lakini mtu aliekuwa akionekana wa kawaida sana kaweza kumfanya mwanamke huyo kuja Tanzania.

Ukweli Roma hakupenda sana Christen kuongea vile kwani aliona anamfanya kuwa maarufu na yeye hakuwa akipenda umaarufu na hio yote ni kutokana na jina lake , lakini pia historia iliokuwa nyuma ya Maisha yake, lakini hata hivyo hakuwa na uwezo wa kumzuia.

Sasa watu wanafahamu kwamba ujio wa Christen Tanzania uliwezekana kutokana na Roma kumwalika kuja Tanzania , lakini pia wanajua kwamba Roma ni mtu muhimu kwa Christen , lakini jambo moja ambalo wanashindwa kufahamu ni ukaribu ambao upo kati ya malkia wa biashara, Edna na Roma mpaka Chrsiten kuwatambulisha kama watu muhimu kwake.

Ukumbuke ndani ya tukio hili walikuwepo watu wakubwa sana , wakiwemo wafanyabiashara , wasanii wakubwa ndani ya Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla , lakini vile vile walikuwemo wanasiasa wakubwa , lilikuwa tukio kubwa hivyo kila ambaye alikuwa na uwezo wa kulipia kiingilio kuhudhuria aliweza kufika ,tofauti na wale ambao walikuwa na mwaliko maalumu.

“Najua kuna maswali mengi kwanini nimesema watu waliokuwa mbele yenu ni muhimu sana , licha ya alienialika Tanzania ni Mr Roma Ramoni ningeomba Miss Edna kunisaidia , Karibu Miss Edna”Aliongea Christen huku akiweka Tabasamu na kisha akamkabidhi Edna maiki huku akimwinamia sikioni.

“Prove them you are Queen Persephone”Aliongea kwa sauti ya chini aliweza kuisikia Edna na Christine alitoka kwa madaha na kurudi kwenye nafasi yake.

Kusema ukweli Christen ndio ulikuwa mpango wake haikueleweka kwanini alikuwa akifanya hivyo , ila yeye ndio aliweka utaratibu wa Edna kufunga mashindano hayo kama CEO wa kampuni na hata maneno yake ya kumwambia Edna aweke wazi kwanini Roma na yeye ni watu muhimu ulikuwa ni mtego, Christen alikuwa akielewa haikuwa ikifahamika kwa watu wengi kama Edna kaolewa na alitaka kumfanya mwanamke huyo atamke hadharani sasa haikueleweaka kwanini anataka Edna afanye hivyo kwani yeye ni kama wanawake wengine tu ambao walikuwa wakimtaka Roma, ilionekana alikuwa na sababu yake.

“Ladies and Gentlemen , it’s my great pleasure to acknowledge Miss Christen as our guest of honor, who has made significant impact on this project…… ,as you all may know , Miss Christen is a great artist with a busy schedule , but she made the effort and came to Tanzania for the first time , Her presence here is not only a benefit for our company but it also shows her love and commitment to all her fans worldwide ,on behalf of all Tanzanian Fans ,Miss Christen we love and appreciate you very much for coming to Tanzania”

“Mabibi na mabwana , ni furaha kwangu kumtambua Miss Christen kama mgeni wetu wa heshima ambaye ameweza kuleta matokeo chanya kwenye projecti hii, kama mjuavyo Christen ni msanii mkubwa ambaye ana ratiba ya kubana lakini amejitoa na kuja Tanzania kwa mara ya kwanza , uwepo wake hapa sio kwa manufaa ya kampuni tu bali pia ni namna ya kuonyesha mapenzi aliokuwa nayo kwa mashabiki zake wote dunia nzima, Miss Christen tunakupenda na tunashukuru ujio wako hapa Tanzania”Aliongea Edna na makofi mengi yakapigwa na kisha Edna akaendele.

“And also I would like to take a moment to specifically recognize and thank the director of Vexto Media , Mr. Roma Ramoni, his leadership have been instrumental in the success of this event, this is a first successful project of our new branch Company and all appreciation’s goes to all who participated in it”

“Na pia ningependa kuchukua nafasi kumtambua na kumshukuru mkurugenzi wa Vexto Media , Mr Roma Ramoni.. uongozi wake uliotukuka ndio sababu ya mafanikio ya tukio hili.., hii ni projekti ya kwanza ya mafanikio iliofanywa na kampuni tawi letu jipya la kampuni na shukrani ziende kwa wote ambao wamehusika”Aliondelea Edna kuongea , alimshukuru pia mwanadada YoonHe kwa kufika Tanzania , lakini pia kwa wafanyakazi wote pamoja na majaji waliofanikisha mashindano yote, lakini sasa moja ya jambo ambalo liliwaaacha watu kwenye mshangoa ni namna Edna alviyomaliza.

“Mwisho kabisa licha ya kupendelea kuyafanya maisha yangu kuwa binafsi sana , lakini naomba nitumie nafasi hii pia kuweka wazi, Mr Roma Ramoni na mimi ni familia , ni Zaidi ya miezi sita mpaka sasa tokea tufunge ndoa yetu, hivyo kuendeleza alichokisema Miss Christen , ni kweli sisi ni muhimu kwake kama familia, Miss Christen tunakukaribisha muda wowote kwenye familia yetu kwani wewe ni muhimu kwetu sana na Tanzania kwa ujumla”Aliongea Edna na makofi yalipigwa huku watu wasiokuwa wakifahamu kile kinachoendelea kushangazwa na kauli ya Edna na sio watu wa kawaida tu lakini pia mpaka kwa wafanyakazi wa kampuni ya Vexto.

Upande wa Roma kauli hio ilimshangaza sana , kwani hakutegemea kama Edna anaweza kupata ujasiri wa kuweka uhusiano wao wazi mbele ya kadamnasi ya watu wengi namna hio, Roma alimgeukia Edna na kumwangalia usoni na Edna alimwangalia kwa tabasamu na kisha akaendelea na ratiba inayofuata ya ugawaji wa zawadi kwa Sophia.

Edna alimtambulisha pia Sophia kama mdogo wake , jambo ambalo pia liliwashangaza wengi , kwani hakukuwa na ambaye alikuwa akifahamu, ila Edna alitoa sababu kwamba alijaribu kuweka siri ili isionekanae kama Sophia anapendelewa na kampuni katika mashindano hayo.

Baada ya ratiba za ugawaji zawadi kwa mshindi wa kwanza kuisha hatimae washiriki wote tano bora waliweza kusainishwa mkataba na kampuni ya Vexto Media kama wasanii rasmi na kazi zao zote ambao watahitaji kufanya zitakuwa chini ya udhamini wa kampuni ya Vexto Media , kila mtu alipendezwa sana na tukio hilo.

*********

“Mama naomba unisamehe”Ilikuwa ni kauli ya Nasra Kwenda kwa mama yake akimuomba msamaha.

Mama yake na Nasra alijukuta akipagawa mara baada ya kusikia Roma ni mume wa mtu , hakutaka kuamini kama mtoto wake alikuwa akitoka kimapenzi na mume wa mtu , moyo wake ulijikuta ukiuma na kilichomuuma Zaidi ni kwamba Roma hakuwa mume wa mtu tu, bali Roma alikuwa ni mume wa Edna , ambaye wazazi wake ndio walikuwa na mchango mkubwa kwa Maisha ya kimasomo ya mtoto wake Nasra.

Mama Nasra alijikuta akipandwa na Jazba kweli , hakuamini kama Nasra anaweza kumfanyia mwanamke mwenzake kwa kuiba mume wake , alijikuta akijawa na uchungu na alijiambia anakwenda vipi kutoa shukrani kwa familia ya Edna , ilihali mtoto wake amekosa shukrani .

“Nasra licha ya kwamba sijabahatika kukulea kwenye makuzi yako yote , lakini jambo hili siwezi kulikubali kabisa , Nasra hauwezi kumfanyia hivi Edna , familia yake imekusaidia na leo hii una Maisha mazuri kuliko familia yoyote kule kijijjini , kwanini Nasra , kwanini mume wa Edna mbona wanaume wapo wengi sana ndani ya jiji hili, kwanini usichague hao na ukamchagua mume wa mtu?”

“Mama nisamehe , ni kweli nimefanya kosa lakini nampenda sana Roma …”

“Nasra nyamaza , nakuambia nyamaza na sitaki kusikia maneno yako yasio na shukrani sijakulea hivyo mimi na unapaswa kujua ni dhambi”

“Lakini mam..”

“Nasra nisikilize kwa makini , tena nisikilize unielewe , kwanzia leo hii sitaki ujihusishe kabisa na Roma kimapenzi, Nasra Sitaki ujihusishe na mume wa mtu kabisa na ikitokea ukaendelea nae mimi sio mama yako mzazi na umtafute aliekuzaa”Aliongea Mama Nasra , alionekana kuwa na Hasira sana , kwani alikuwa amejaa kwa Jazba.

Nasra alishangazwa na maneno ya mama yake , hakuwahi kumuona mama yake akiwa na hasira hio kwenye Maisha yake yote aliomfahamu , swala la kusema kwamba asimfahamu kama mama kama atakubali kuendelea na Roma ni maneno ambayo hakuwa ameyategemea kama mama yake angeongea.

“Naomba upunguze Jazba mama yangu, ni kweli nimekosea lakini..”

“Nasra nishakueleza , ijapokuwa sijasoma kama wewe lakini najua ulichokifanya sio haki kwa Edna kabisa na unapaswa kumuomba msamaha na kuachana na mume wake , kama haupo Tayari kufanya hivyo nitaenda mimi na kupiga magoti kwa ajili yako , lakini sipo tayari kukuona ukiendelea na mume wa mtu Nasra , nilimkubali Roma kule kijijini kwakua niliamini hakuwa ameoa… Nasraa..”Mama huyu alijikuta akihema kwa nguvu na kukaa kwenye sofa, hasira zilionekana kumzidia.

“Mama naomba unisamehe, naomba unisamehe mama yangu”

“Nasra nitakusemehe kama utaachana na Roma huo ndio msimamo wangu , kama utaniambia haupo tayari kuachana nae kesho nitarudi kijijini na sitoendelea kukutambua kama mwanangu , Nasra chagua moja kabla ya kesho asubuhi”Aliongea Mama Nasra huku akijitahidi kuzuia hasira zake , kwani alisindwa kupumua vizuri.

Nasra alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu sana , hakuamini kama mama yake angekuwa hivyo juu ya swala lake na Roma ,siku zote aliamini mama yake angemuelewa kwa maamuzi yake ya kuwa na mahusiano na Roma licha ya kuwa mume wa mtu , lakini sasa anajikuta yupo kwenye mtihani wa kumchagua mama yake au Roma.

Nasra alijikuta alikaa kwenye sofa na kuinamisha kichwa chini na kuanza kulia , lakini hata hivyo kilio chake kwa Mama Nasra hakikumpa shida alichokifanya ni kulala kabisa kwenye sofa, mwanamama huyo hakutaka kabisa kumuona mwanae Nasra anaendelea kuwa na mahusiano na Roma.

Mama Nasra katika Maisha yake alitamani kumuona Nasra akiolewa kwa harusi na mwanaume wa kueleweka na sio kutoka na mume wa mtu na kuwa mchepuko tu na kukosa nafasi ya kuwa mke , Aliona kabisa Nasra anapotea , hivyo hakuwa tayari na aliona asipo simama yeye kama mama basi Nasra hawezi kumsikiliza.

“Wewe lia unavyolia , lakini kama mimi nitaendelea kuwa mama yako sitotaka kukuona ukiendelza mahusiano na mume wa Edna , Nasra sisi ni waislamu na tunafunzwa kuwa na shukrani kwa wale wanaotutendea mema , lakini unachokifanya wewe sio shuktani kabisa , unafikiri Mungu anatuoanaje , siwezi kukubali hili likiendelea , achana na Roma mara moja na kwa uzuri wako naamini utapata mwanaume atakae kupenda na kuanzisha familia”Aliongea na kisha alielekea chumbani akimwacha Nasra sebuleni, akiwa kwenye wakati mgumu.

Unafikiri Nasra atamuacha Roma?”
 
hamna mbona sema anachoongea nisahihi na ninamshukuru
Sisi kazi yetu huku ni kupush mzigo uende mbele wadau wengine uwafikie walipie huko. Sie mashabiki kindakindaki wa SinganoJr. Kaka unaupiga mwingi sana....
 
bwana singanojr anataka kusema huyu mkorea na yezi are somehow related?......... or possibly wakawa ndugu?

anyway, tunasubiri jumapili
 
bwana singanojr anataka kusema huyu mkorea na yezi are somehow related?......... or possibly wakawa ndugu?

anyway, tunasubiri jumapili
Yani familia mzima ya Edna ina muingiliano na watu mashughuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…