Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Daa!! muendelezoo mkuu
 
Naamini Mage atapigwa miti na Roma Romani [emoji23][emoji23][emoji23] na kiburi chote kitaisha[emoji23][emoji23][emoji23]
 
SURA YA ISHIRINI NA SITA A
Muda wa saa kumi na nusu Edna alifika nyumbani huku mwanadada huyu akionekana siku ya leo kuwa na furaha kuliko siku zote jambo ambalo Bi wema aliligundua , lakini hakuuliza Zaidi , kwake huyu mwanamke alitamani sana kumuona Edna akifurahi ndio iliokuwa ndoto yake kubwwa sana , alikuwa akiumizwa sana na tabia ya Edna muda wote kufanya kazi kiasi kwamba kwake hakuwa na siku ya kupumzika , Edna hakuwa kama wafanya biashara wengine ambao walikuwa wakipenda kula bata kila ifikapo wikiendi .

Edna yeye alikuwa ni aina flani ya wanawake ambao alikuwa akirudi nyumbani ni kusomana kulala.

Ndani ya chumba cha Edna kulikuwa na mavitabu mengi sana na karibia vitabu vyote hivyo alikuwa amevisoma , kwa mtu wa kawaida unaweza kushangazwa na swala hilo lakini kwa Edna lilikuwa swala la kawaida sana , ndio Maisha yake ambayo alikuwa amezoea , kwake kusoma vitabu ndio ilikuwa starehe yake kuliko kujichanganya na marafiki.

Edna alikuwa ni mtu wa kutabasamu mara chache sana , muda wote alikuwa yupo siriasi kiasi ambacho kilifanya hata wafanya kazi wenzake wamuogope kumsogelea, lakini leo hii mwanadada huyu anaonekana kutabasamu mbele ya Bi Wema , mwanamama huyu aliekula chumvi nyingi alitamani kujua ni kipi kinamfanya mwanae huyu wa hiari kutabasamu , ila hautaka kuuliza.

“Bi Wema leo niachie jiko nitapika mimi” aliongea Edna na kumfanya Bi wema kutumbua macho lakini Edna hakujali sana , alikaa kwenye sofa huku mkononi akiwa ameshikilia kitabu cha mapishi.

“Sawa Miss , lakini haujawahi kuingia jikoni utapika nini?”

“Bi Wema hio ni siri , wewe utaona wakati wa kupakua”Bi Wema alijikuta akitabasamu na katika akili yake alikuwa ashajua kilichokuwa kikiendelea kwa Edna , aliamini kuna jambo ambalo lilikuwa limetokea kazini na kusababisha mabadiliko hayo .

Saa moja kamili za jioni Edna alikuwa bize na mapishi huku Bi Wema akiendelea kuangalia tamthilia, muda nao ulisonga lakini Roma bado hakuwa amerudi.

“Bi Wema Roma hajarudi bado?”Aliuliza mwanadada huyu aliekuwa amevalia Apron na kumfanya apendeze sana , kiasi kwamba wewe ndio ungekuwa mume wa Edna na ungemuana jinsi alivyovalia Apron ni hakika ungenenepa kabla hata ya kula chakula.

“Hajarudi bado na hajatoa hata taarifa kama atachelewa kurudi”Aliongea Bi Wema na kumfanya Edna kuonyesha hali ya kuhuzunika.

“Ukute na hangaika hapa yupo na mwanamke”Aliwaza Edna huku akirudi jikoni kuendelea na upishi akitegemea Roma atarudi.

Muda wa saa tatu na nusu alionekana Bi Wema akiwa ndani ya chumba cha maliwato akitapika huku akisukutua maji.

“Nimewahi kula chakula kibaya ila hiki cha leo ni kiboko , Chakula kama mavi ya mtoto mchanga khaa.. Edna ananitia aibu jamani”Aliongea Bi Wema huku akisukutua .

“Nimekula kumridhisha tu ilia aone na yeye mwanamke , ila kile sio chakula”.

Wakati Bi Wema akiendelea kutapika huko ,Edna alikuwa amekaa kwenye sofa akimsubiria mwamba Roma arudi huku Mabakuli ya chakula akiwa ameyapangilia kwenye Meza , na kwa jinsi yalivyopangwa moja kwa moja utaamini kuwa kuna bonge la pishi limefunikwa.

Upande mwingine Nasra alionekana akiwa nyumbani kwake jikoni akiwa bize na mapishi , alionekana kuwa mtaalamu kweli , kwani kwa namna ambavyo alikuwa akikata kitunguuu Ungejiambia mwenyewe ndio hapa yupo mwanamke.

Bebi Nasra unajua sana kupika” Aliongea Roma huku akiwa amejipumzisha na pensi la kike na haraka haraka ukimwangalia lazima ugundue hilo pensi ni la Nasra maana lilikuwa na Marinda Marinda chepete , ila Roma hakuwa na habari huyu bwana , yaani hakuwa na aibu hata kidogo.

Baada ya kula na kushiba , hakukuwa na kilichoendelea zaidi ya kuingia kwenye mtanange .

“Bebi hii Staili inaitwaje?”Aliuliza Nasra huku akionekana kukosa pumzi maana alikuwa amelemewa na utamu.

“Mh! Mimi hata sijui ila umekaa kipopo popo ,, itakuwa ndio Popo kanyea Mbingu”Aliongea Roma huku akiongeza spidi.

Muda wa saa kumi na mbili za Asubuhi Roma aliingiza gari yake nyumbani bila wasiwasi kabisa na baada ya kuliegesha aliingia ndani na kumkuta Bi Wema.
Bi wema kama kawaida , alikuwa mzungu wa Roho maana alimpokea Roma na kuitikia salamu kama hakujatokea kitu ila kiukweli moyoni alikuwa na huzuniko , kwani kwa mara ya kwanza anamuona Edna akiingia jikoni jambo ambalo kwake aliliona kama hatua ya kwanza ya Edna kuwa kama mwanamke aliekamilika , lakini Roma hakuonekana nyumbani , aliona kitendo hicho kimemnyong`onyesha Edna juhudi zake , kwani Edna kwa mara ya kwanza alimsubiria Roma kwa muda mrefu jambo ambalo sio kawaida.

“Roma jana ulikuwa wapi , hukutoa taarifa Miss alipika na akakusubiri lakini hukutokea”Aliongea Bi wema wakati Roma akianza kupandisha ngazi kuelekea chumbani kwake , lakini baada ya kusikia maneno hayo alijikuta akisimama na kushangaa.

“Bi Wema unamaanisha Edna jana kaingia jikoni kupika?”

“Ndio chakula bado kipo mezani”Aliongea Bi Wema na Roma hakuendela kwenda juu ,, alirudi chini na kwenda meza ya kulia chakula na kufunua mabakuli yaliopikwa.

“Bi Wema nitakula kama kiporo na chai”Aliongea Roma na kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake na baada ya muda alishuka kwa aili ya Chai na Edna alikuwa amejaa mezani akinywa chai oamoja na Bi Wema.

“Wife hebu tuone leo ulichopika”Aliongea Roma na kisha alifunua mabakuli hayo huku Edna licha ya kwamba hakuwa akimwangalia Roma usoni lakini akili yake ilikuwa ni kusbiria nini ataongea Roma baada ya kula chakula chake.

Roma alipakuwa chakula na kisha alichota mtori huo na kupeleka kinywani na kula.

“Nilijua mtori kumbe ni tambi Looh! Hapa nina jipu sio mke”Roma aliwaza moyomi na kisha akachota kijiko kingine na kula , wakati huo Bi Wema alikuwa amekunja sura utadhani chakula kilikuwa kikiingia Tumboni kwake.

Roma alimwangalia Edna huku mrembo huyu akijifanyisha kunywa chai , lakini alikuwa akisubiri Roma atamke neno.

“Wife umejitahidi sana leo, ukiendelea hivi utakuwa mpishi mzuri”Aliongea Roma na kuendelea kula bila ya wasiwasi huku nia yake ni kutokumkatisha tamaa Edna na Bi wema alifurahishwa na maneno ya Roma na kule kukasirika kwa kutokurudi nyumbani kulipotea , lakini bado kuna kitu kilimshangaza , kwa jinsi chakula hiko kilivyokuwa na chumvi , alijiuliza Roma amewezaje kula.

“Okey ! ngoja nijipe adhabu ya kumaliza hiki chakula maana sio kwa huu utopolo”Aliwaza Roma , ila kwa Edna moyo wake ulitabasamu , licha ya kwamba hakuwa akionyesha usoni lakini alifurahia sifa hizo kutoka kwa Roma.

ITAENDELEA SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA B
 
SEHEMU YA 26 B.
Roma baada ya kumaliza kunywa chai ya asubuhi alipandisha chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika , siku hii ya leo aliona akae kidogo nyumbani , kwani tokea afike ndani ya familia hii hakuwahi kukaa nyumbani kwa muda mrefu , muda mwingi alikuwa misele ya hapa na pale.

Wakati akiwa amejilaza kwenye kitanda alijikuta akiachia tabasamu .
Edna mambo yake ni kama ya Seventeen nakiri kwa asilimia kubwa wanafanana”Aliwaza Roma huku akiwa ni mwenye tabasamu.

****
1998- KIGALI RWANDA March 8

Ilikuwa ni ndani ya ofisi ya mheshimiwa Jeremy Paul (JP),walionekana watu wanne wakiwa wameketi ndani ya ofisi hii na ilionekana kuna kikao kilichokuwa kikiendelea kati ya mheshimiwa Jeremy na wanaume watatu kukamilisha idadi ya wanaume wane ndani ya ofisi hii.

Wanaiume watatu walikuwa ni watu maarufu sana waliokuwa wakifahamika ndani ya jiji la Kigali na moja ya sifa kubwa ambayo ilikuwa ikiwafanya watu hawa kufahamika ni kutokana na michango yao katika taifa hili dogo.

Mtu wa kwanza aliekuwa amekaa upande wa kushoto wa mheshimiwa Jeremy alifahamika kwa jina la Uwimana ,huyu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana ndani ya taifa hili la Rwanda na alikuwa akimiliki visima vingi vya Mafuta , pamoja na kampuni kubwa ya usafirishaji .

Mwingine alikuwa ni Jean , Wengi ndani ya taifa hili wanapenda kumuita kwa jina la Profesa J , huyu nae licha ya kuwa mfanya biashara lakini pia alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Rwanda.

Mtu wa tatu hakuwa akifahamika sana ndani ya taifa la Rwanda kama alivyokuwa akifahamika ndani ya taifa la Tanzania ,Alikuwa akifahamika kwa ina la Aziz Mohamed huyu alikuwa ni moja ya wafanya biashara wakubwa sana kutoka taifa la Tanzania , lakini pia alikuwa ni moja ya wawekezaji wakubwa ndani ya taifa la Rwanda na ndio maana mchango wake ulikuwa ukiheshimika ndani ya taifa hili.

“Ndoto yangu yangu kubwa ni kuona Rwanda ikiwa nchi kubwa sana kiuchumi ndani ya bara la Afrika , na haya yote hayawezi kufanikiwa bila ya uwepo wenu”Aliongea. Huku mabwana hawa wakionekana kutingisha vichwa kuashiria kuwa wako pamoja na mheshimiwa na muheshimiwa.

“Mheshimiwa sisi tupo tayari kukuunga mkono katika safari ya ndoto yako ya kuifanya Rwanda kuwa kubwa na tutakuwa ni wenye kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha kuinua uchumi wa taifa hili”

Alingea Uwimana Kikao hiki kilionesha dhahiri kilikuwa ni cha mipango juu ya kuifanya Rwanda kuwa nchi kubwa kwa miaka ishirini ijayo, mipango ambayo mheshimiwa Jeremy aliona watu pekee wakufanikisha nao swala hilo ni hao mabwana watatu , haikueleweka ni kwanii Mheshimiwa akamwinginza mtu mwingine kutoka taifa la nje yaani Azizi Mohamed.

Baada ya kikao hiki kuisha Mheshimiwa huyu alionekana kuwa na maongezi binafsi na Aziz kwani wale mabwana wengine walikuwa washatoka ndani ya ofisi hii.

“Asante sana Aziz kwa kufanikisha kurudisha sehemu ya damu yangu mikononi mwangu”.

“Jeremy sisi ni marafiki wa muda mrefu sana hupaswi kunishukuru , lakini nisingependa kuona katika Maisha yako unakosa furaha , umemkosa Rahel , lakini naamini zawadi aliokupatia ni kubwa na angalau itakufanya usiishi kwa kujuitia”Aliongea Azizi huku akimtaja Rahel na Jeremy alionekana kukosa furaha mara baada ya kusikia jina la Rahel.

“Ni kweli Aziz.. lakini Maisha yangu bado naona kama hayajakamilika kwa kumkosa Rahel , katika Maisha yangu niliamini kwa kuwa raisi hakuna kitu ambacho ninaweza kukosa na kunifanya nisiwe na furaha , lakini Rahel amenifanya nione sikuwa nikifikiria kwa usahihi”.

“Ni kweli Jeremy, lakini kwa sasa unatakiwa kumsahau Rahel , yule mwanamke ni mke wa mtu kwa sasa na ni maamuzi ambayo aliyafanye yeye mwenyewe na akakuacha wewe , angalau sasa wekeza nguvu zako katika kulea kichanga alichokuachia kama zawadi”Aliongea Aziz lakini muda huo huo aliingia mwanadada makamu hivi, hakuwa mrembo sana , ila alionekana kuwa mtanashati

“Mheshimiwa kuna taarifa mbaya?”

“Unamaanisha nini Linda , unamaanisha nini kuhusu taarifa mbaya?”

Mwanadada huyu aliefamika kwa jina la Linda alisogelea Rimoti ya Tv na kisha akawasha Runinga na kuweka chaneli ya BBC .

BREAKING NEWS: NDEGE YA M AIRLINE ILIOKUWA IKISAFIRI KUTOKA KUAL LAMPUR KUELEKEA BEIJING CHINA YAPOTEZA MAWASILIANO.

Taarifa hii ilionekana kumshitua sana mheshimiwa pamoja na Aziz waliouwa wakiangalia Runinga hio lakini kati ya watu hao aliekuwa kwenye hali mbaya Zaidi ni Jeremy.

“Linda wasiliana na shirika la ndege la Malaysia wakupe orodha ya majina ya watu waliopanda kwenye hii ndege”Aliongea Mheshimiwa Jeremy huku akiwa ni mwenye wasiwasi mwingi sana.

“Jeremy punguza presha naamini huenda kuna tatizo la kawaida tu ambalo limetokea”

“Aziz siwezi kutulia kabisa ,unafikiri nitaishije kama kitu kibaya kikimkuta Lorraine ,Nitamwabia nini Rahel , hapana nitaishi kwa majuto makuu kwenye Maisha yangu yote , naomba jambo baya lisitokee”Aliongea Mheshimiwa Jeremy huku akishikilia kifua chake.

Ni ndani ya dakika tano Linda alirudi na kuingia ndani ya ofisi , huku wasiwasi ukiwa umejaa kwenye macho yake.

“Mheshimiwa hii ndio orodha ya abiria”Aliongea lakini Azizi aliona wasiwasi uliokuwa kwenye macho ya Linda na kwakuwa alikuwa karibu nae alichukua ile karatasi na kuangalia majina hayo na bwana huyu alijikuta akitumbua macho na kumwangalia Rafiki yake Jeremy.

“Azizi usiniambie Lorraine ni sehemu ya abiria walikuwepo kwenye hio ndege?”

“Jeremy taarifa inasema ndege imepoteza mawasiliano , lakini sio kuanguka tusubirie taarifa kamili , Acha kufikiria mambo mabaya”Aliongea Azizi lakini baada ya kumaliza sentensi yake…

“Mheshimiwa..!!”Aliongea linda kwa sauti mara baada ya Mheshimiwa Jeremy kudondoka na kuzimia.

SHEMU YA ISHIRINNI NA SABA
Taarifa za mheshimiwa Jeremy kuzimia zilikuwa ndani ya ikulu , hazikutoka hata kwa baadhi ya mawaziri Zaidi ya kitengo cha usalama ikulu pamoja na baadhi ya wanafamilia wa mheshimiwa Jeremy.

“Nini kimempata mheshimiwa Linda?”Aliuliza mke wa Raisi Jeremy huku akionekana ni mwenye wasiwasi sana , wakiwa nje ya chumba cha matibabu ndani ya ikulu.

Lakini Linda hakuwa na jibu la kuongea na kusema hakuwa akijua ni nini kimemkuta mheshimiwa Jeremy Zaidi ya kumwambia First lady huyu wasubiri majibu kutoka kwa daktari.

Baada ya masaa kadhaa ya hatimae daktarin wa ikulu alitoka katika chumba cha matibabu.

“Inaonekana mheshimiwa kapata mshituko”.

“Mshituko , unamaanisha nini mshituko dokta?”Aliuliza mama huyu kwa Jazba huku macho yake yakimgeukia Linda aliekuwa mlinzi wa karibu wa raisi na Linda jasho lilimtoka.

“Linda niambie ni jambo gani baya mheshimiwa kakumbana nalo mpaka kupata mshituko?”

“Madam ! hata mimi najiuliza swali kama hilo , lakini sina majibu sahihi ,maana mheshimiwa nilimkuta akiwa katika hali ya kupoteza fahamu”.

Bado haikuwa ikimwingia akilini mwanamama huyu mwenye PhD ya lugha , aliamini kuna jambo ambalo mme wake limemkuta na kumpelekea kupoteza fahamu.

Baada ya masaa mawili kadhaa kupita hatimae mheshimiwa Jeremy alirejewa na fahamu zake na swali la kwanza baada ya kuamka lilitoka kwa mke wake akitaka amueleze nini kimemkuta mpaka kupoteza fahamu , lakini mheshimiwa licha ya kuonyesha hali ya wasiwasi hakuwa tayari kuweka wazi ni jambo gani lilimkuta.

“Linda nipe taarifa ya kinachoendelea?”

“Mheshimiwa taarifa ni zile zile ni Zaidi ya masaa nane sasa ndege haijapatikana kwenye Rada na satelaiti , na wataalamu wa anga wanajaribu kuifatilia kwa ukaribu”Alijibu Linda na kumfanya mheshimiwa chozi la utu uzim limtoke.

“No .. no Lorraine you are not dead”Mheshimiwa aliongea kwa uchungu kiasi kwamba Linda alitoa machozi na kumuonea huruma mheshimiwa.

****
WHITE HOUSE -USA 1998 MARCH 8.

Ndani ya ofisi ya kiserikali ya Marekani ,alionekana mheshimiwa Raisi , mwenye jina maarufu The First Black akiwa ameketi kwenye kiti chake huku akiwa ameshikilia faili lililokuwa na nembo ya ‘Top Confidential’ ikimanaanisha Nyaraka ya Siri sana.

‘Life and Death Operation’(LADO) ndio jina la kichwa cha karatasi kilichokuwa kikisomeka juu kabisa ya karatasi alioshikilia mheshimiwa The First Black(TFB) huku akionekana ni mwenye umakini mkubwa sana kusoma karatasi hio ambayo imetoka kwenye faili lililokuwa mezani .

Ni ndani ya dakika kama kumi na moja tu alizotumia Mheshimiwa huyu kusoma , simu yake ilianza kuita mfululizo kiasi cha kumfanya mheshimiwa huyu aichukue na kuipokea .

“Yes Rogan whati is news?”

“Mr President the plane has landed safely on Life and Death Island”Ilisikika sauti na bwana huyu alitabasamu.

“Very Good Rogan Activate Project LADO and all Concealment Protocol should be followed strictly, I will deal with the Rest”

Baada ya kuongea maneno hayo simu ilikatwa na mheshimiwa huyu akachukua simu na kupiga na muda huo huo mlango wa ofisi ya mheshimiwa ulifungulikiwa na akaingia mwanadada wa kizungu mwenye umri kati ya miaka therathini hivi kupanda alievalia suti ya zambarau na blazia nyeupe na viatu vyenye kisigino kirefu ‘high heels’

“Christine nipe taarifa ya kinachoendelea huko ulimwenguni”

“Mheshimiwa hali sio shwari kwa sasa , mataifa mengi yanahitaji msaada kutoka kwetu , juu ya upoteaji wa ndege ya M Airlines, ufupi ni kwamba mheshimiwa dunia imesimama kutokana na tukio hili”

Mheshimiwa alisimama na kutembea kwa kuzunguka kwenye hii ofisi.

“Endelea kutoa taarifa kwa kila anaepiga simu, na waambie serikali yetu itafanya kila namna kuhakikisha ndege hio inapatikana”Aliongea mheshimiwa na kisha Christine alitoka na kwenda kuendelea na kazi .

Huyo mwanadada alikuwa ndio msemaji mkuu wa kurugenzi ya White House.
Baada ya Christine kutoka . mheshimiwa alivuta faili lingine kwenye droo ya meza , lililokuwa likifanna na lililopo mezani . utofauti wa faili hili na lile ni kwamba juu ya karatasi iliokuwa ndani ya faili hilo ilisomeka kwa jina la ‘The Agrement’ huku kukiwa na baadhi ya orodhesho la mashirika makubwa Duniani ya kijasusi na sahihi za wakurugenzi wakuu wa mashirika hayo.

The first Black aliangalia sahihi hizo, lakini kuna jambo moja ambalo lilionekana halikumridhisha.

“Shirika la Urusi pekee la kijasusi ndio Saini yao hapa haipo ,Beijing wamenihakikishia kwamba watashughulika na swala hili , lakini bado nina wasiwasi”Aliwaza mheshimiwahuyu na kurudisha mafaili yote kwenye Safe Box ndani ya ofisi yake.

****
DAR ES SALAAM ,TANZANIA 1998 -March 8.

Ni ndani ya familia moja ya kitajiri maarufu ndani ya Masaki , walionekana wanafamilia hii wakiwa kwenye hali ya furaha sana , na hii yote ni baada ya kiumbe kipya kuja duniani ndani ya familia hio.

Rahel pamoja na Bi Salome walionekana na furaha ilikuwa imewazidia kiasi kwamba muda wote walikuwa wakipokezana kubeba kitoto kichanga kalikozaliwa.

“Rahel umemleta mtoto mzuri sana duniani , anafanana kwa asilimia mia moja na wewe na hili limenifurahisha Zaidi , asante kwa kumlindia mwanangu Adebayo heshima yake”Aliongea mwanamama huyu huku akimwanglia mtoto aliekuwa kwenye mikono yake , muda huu ikiwa yapata saa mbili za usiku.

Wakati wanawake hawa wanaendelea kufurahia kiumbe kilichokuja duniani , alionekana kijana wa makamo umri wa Rahel akiingia ndani hapa huku akiwa amelewa chakali , baada ya kuingia ni kama hakuwa akijali waliokuwa sebuleni kwani alipandisha ngazi moja kwa moja.

“Adebayo utaacha nini kulewa hivyo wewe”

“Mama niache maamuzi ulioyafanya licha ya kwamba nimeyakubali ila ni yenye kuniumiza na njia pekee ya kujipoza ni kunywa”Aliongea kijana huyu na kisha alijikokota na kuingia chumbani kwake huku nyuma akimuacha Raheli aliekuwa akimwangalia kwa huzuni.

“Tutampa jina la Edna”Aliongea huyu mama mtu mzima na Raheli alitabasamu.

“Ni jina zuri mama”.

Upande mwingine mkoani Ruvuma manispaa ya Songea katika familia ya bwana Senga kulikuwa na majonzi makuu , huku mtu aliekuwa akilia kama mtoto alikuwa ni Senga, bwana huyu katika kilio chake alikuwa akitamka neno ‘Mke wangu na mtoto wangu mmeniacha ‘ bwana huyu alionekana watu wake muhimu walikuwa wamapatwa na jambo baya sana.

“Yote ni mipango ya Mungu Senga huna budi kumshukuru Mungu”.

“Hapana Desmond , ndio kwanza naanza kuyaona mafanikio lakini mafanikio yangu yanasababisha mke wangu na mtoto wangu Denis kufa , bora ningebakia maskini huenda wasingeweza kupanda ndege na haya yote yasingewatokea”

Senga alikuwa akilia sana , na katika kilio chake ilionekana yeye ni moja ya familia nyingi duniani ambazo ni wahanga wa upoteaji wa ndege ya M Airlines.

Hakuna alieweza kumfariji bwana huyu akapata unafuu , mapenzi yake kwa watu walipotea na ndege yalikuwa ni makubwa mno , kiasi kwamba hayakuweza kupimika kwa aina yoyote ile ya kipimio, alikumbuka safari ya kimaisha aliopitia na mke wake Blandina ya msoto hatimae kupata pesa na utajiri na Mungu akawabariki mtoto wao wa kwanza , lakini Mugnu huyo huyo akawachukua wote wawili na kumuacha Senga akiwa katika majonzi na machungu makubwa ndani ya moyo wake , hakika maumivu yake hayakuwa ya kupimika hata kidogo na na waliokuwa karibu yake hawakuweza kufanya jambo lolote Zaidi ya kumuonea huruma.

Bwana huyu hakujali tena mali alizokuwa nazo , alikuwa radhi kutoa kila kitu alichokuwa nacho iwapo mtu yoyote atatokea na kusema kwamba anaweza kuwarejesha wapendwa wake duniani , lakini bado jambo hilo halikuwa likiwezekana , na tumaini hilo likabakia kuwa ndoto ya mchana.Na waswahili wanakazia kwa msemo wao , alieenda ameenda na waliobaki Maish ya naendelea,

Ndio kwanza simulizi inaanza , so tuvumiliane ili niendeleee kuhakikisha mnafurahia hii simulizi NITAIWEKA HAPA IJUMAA NA JUMAMOSI NGOJA NIWASOGEZE WATI WA GRUPU

CHANGIA KAZI HII KWA KULIPIA KUANZIA 2000 KUENDELEA NIKUUNGANISHE NA GRUPU UIFATILIE KWA VIPANDE VITATU KILA SIKU TUPO SEASON 2 KWENYE GRUPU

GRUPU NI KWA AJILI YA SIMULIZI HAKUNA KUCHAT

LIPIA NAMBA 0687151346 AIRTEL AU 0623367345 HALOPESA AU 0657195492 TIGOPESA JINA ISSAI SINGANO UKILIPA TUMA MESEJI YA MUAMALA NAMBA 0687151346 WATSAPP
 
Umetutengenezea addiction...ikipita siku bila hii mtori basi mambo yanakuwa si mambo dah!

Sent from my SM-T555 using JamiiForums mobile app
 
Kwa tuliosoma literature la nne B hapa tunapewa historia ya Roma... kumjua Roma ni naniiiii.....

All in all big up sana Mkuu[emoji123][emoji123][emoji123][emoji2536]
 
Kwa tuliosoma literature la nne B hapa tunapewa historia ya Roma... kumjua Roma ni naniiiii.....

All in all big up sana Mkuu[emoji123][emoji123][emoji123][emoji2536]
ndio maana yake mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…