Rogers luyangi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2014
- 552
- 948
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda kesho haijafika bado
Jion ndo hiiLabda kesho haijafika
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ikawa jioni na ikawa usiku hatimae kukapambazuka
Nadhani anaanda
Imeisha hiyo !!!Ikawa jioni na ikawa usiku hatimae kukapambazuka
,[emoji3][emoji3][emoji3]nitaweka soon niko nipo kwa roadIkawa jioni na ikawa usiku hatimae kukapambazuka
Sikati tamaa nasubiri kwa hamu,[emoji3][emoji3][emoji3]nitaweka soon niko nipo kwa road
Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
Mrembo tuendelee kunywa mtori nyama zipo chini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Haaa, anawapa the big dickImeisha hiyo !!!
SAA hizi yupo kwa Doris kama siyo kwa Rose Au bint Maple the Don
usingizi umekata simulizi nayo punje 2 mateso tupuBonge la simulizi
ThenkyuuuuuuuuuSEASON 03
SEHEMU YA 61
MASAA MACHACHE NYUMA
Roma na Edna baada ya kumaliza kupata chakula ambacho walikiita chakula cha mchana kutokana na kuchelewa kwao kupata chakula hicho ,Roma alimchukua Edna mpaka My World Fashion Mall , kwa ajili ya kuchagua vazi la kuvaa kwenye kusanyiko la wafanyabiashara ambalo lilikuwa likitegemewa kufanyika usiku wa siku hio.
Ilikuwa ni wikiend na ndani ya eneo hili lilikuwa na watu wengi mno ambao walikuwa wakifanya ‘Shopping’ , kuna waliokuwa na wapenzi wao , kuna waliokuwa na marafiki zao jinsia moja , lakini pia kuna waliokuwa peke yao wakijinunulia nguo.
Kama kawaida baada ya Roma na Edna kuingia ndani ya eneo hili , walikodolewa macho na watu wengi , huku macho yote yakielekezwa kwa Edna ambaye licha ya kwamba hakuwa amepaka kitu chochote kwenye uso wake , lakini alionekana mrembo Zaidi kuliko mwanamke yoyote aliekuwa hapo ndani.
“Baby hivi unajifahamu kama ni mzuri sana , angalia wanaume wanavyokuangalia kwa kukutamani”Aliongea Roma kwa kumtania Edna wakati wakipanda kwenye ‘ Elevetor’ za jengo hili .
“Nishazoea, acha waniangalie”Aliongea Edna huku akionyesha kutojali kwa namna ya watu walivyokuwa wakimkodolea macho.
“Karibu Madam”Aliongea moja ya mfanyakazi ,ambaye leo alikuwa ni wa tofauti na wa siku kadhaa zilizopita ambapo Edna alifika hapo akiwa na Roma.
“Kuna nguo ipi ingizo jipya ambayo unaamini itanikaa vizuri Tusi?”Aliuliza Edna huku Roma akimwangalia mwanadada huyu ambaye alikuwa mzuri wa haja, aliekuwa akifahamika kwa jina la Tusi.
“Kuna aina mbili kutoka Ufaransa kampuni ya Luis Vuiton na nyingine ni kutoka Norf Italy”Aliongea mwanadada huyu na Edna akajikuta akijawa na shauku ya kuona nguo hizo .
“Edna karibu!”Aliongea mwanamama mmoja ambaye aliwasogelea , alikuwa ni mnene wa wastani mrefu kiasi , alikuwa ni wale wanawake wanaojipenda , kwani licha ya kuonekana kuwa na wa umri mkubwa lakini bado uzuri wake haujapotea..
“Mama T!”Aliita Edna kwamshangao , ni kama hakuwa amemtegemea mwanamama huyo ndani ya hili eneo ,huku mwanamama huyu akimkodolea macho Roma , alikuwa akijiuliza hiuyu ni mlinzi mpya wa Edna , maana kwa muonekano wa Roma hakuonyesha kama mtu wa ukaribu na Edna.
“Roma huyu ni Mrs Augustin ni mmiliki wa haya maduka,alikuwa jirani yetu Osterbay , tumezoea kumuita Mama T ,Mama T huyu ni Roma ni mume wangu”Aliongea Edna na kumfanya Mama T ashangae kwa kutoa macho na kisha akampa mkono Roma aliekuwa kwenye tabasamu namna ambavyo Edna alikuwa akimtambulisha.
“Ooh! Edna jamanii mbona hujanipa taarifa kama umeolewa?”Aliongea mwanamama huyu huku akishanga.
“Mama T ndoa yetu haina hata muda mrefu na tumeona tu bila hata ya kufanya sherehe”Aliongea Edna na kumfanya mama huyu kuonekana kuelewa.
“Hongereni sana Edna , Hongera Mr Roma kwa kupata mke kama Edna”Aliongea mama huyu na alionekana alikuwa akitoa pongezi zake kwa dhati kabisa.
“Asante sana na pia nafurahi kukufahamu Mama T , ila bado sijaelewa kwanini unaitwa mama T?”
“T maana yake ni kirefu cha Twin, mama T ana watoto mapacha”Aliongea na hapa Roma alionekana kuelewa na kuona maelezo hayo yanajitosheleza lakini pia ni sahihi.
“Edna kwasaabu leo ndio nimejua umeolewa , nataka nikupe Zawadi , nilishawahi kumwambia Rahel siku utakayo olewa lazima nikupe zawadi”Aliongea Mama T na kisha akamshika mkono Edna huku wakienda upande wa kulia kwenye duka kubwa ambalo lilikuwa limesheheni mavazi ya kike na hata Roma alifuatisha nyuma.
Roma aliona mwanamaa huyu alikuwa na pesa nyingi , kwani hili duka halikuwa la kawaida , japo kwenye jengo hili kulikuwa na maduka menginye ya nguo makubwa tu, ila la Mama T lilionekana kuwa kubwa Zaidi.
“Nina nguo mpya Edna , kwa uzuri wako kama utaivaa lazima ikupendeze na naamini utanisaidia kuitangaza leo usiku kwenye kusanyiko”Aliongea Mama huku Edna akikaa kwenye Sofa na mama huyu akienda upande wa ‘Store’ , alionekana hakuwa kabisa ameiweka kwenye nguo ambazo zinauzwa.
Baada ya kuitoa Edna alishangazwa mno na aina hio ya gauni lililokuwa la maua maua , kabla hata ya kulijaribu alikuwa ashalipenda tayari na hata kwa Roma pia alipendezwa na aina hio ya Gauni,na Edna alienda kujaribisha.
Roma alijikuta akiridhika na namna ambavyo mke wake alikuwa amependeza , Edna alionekana kama malaika mbele ya macho ya Roma , ni kama hakuwa akiamini kama ana mke mzuri kama huyo.
Mama T na yeye aliliridhishwa na vazi hilo kwa kiasi cha juu sana kwa namna ambavyo lilikuwa limekaa kwenywe mwili wa Edna , lilikuwa ni gauni jekundu lilikuwa na aina flani ya vimaua aina ya Rose`s vilivyokuwa vimeshonwa kimpangilio kwenye shingo , huku mbele ya kifua likiaacha uwazi kidogo wa mfumo wa V.
“Edna ungekuwa msanini hakika nadhani kila kampuni ingekutaka kuwa balozi wao kutangaza biashara ya mavazi”Aliongea Mama T .
****
“Diego Unamkumbuka Alfshar Bahman?”Aliuliza Bram aliekuwa akichezesha vidole vyake kwenye Tarakishi yake huku akitafuna bublish.
“Nishamsahau nikumbushe”Aliongea Diego kiongozi wa kundi la The Eagles.
“Unasahau sana Diego ,utamsahau vipi Afshar?,kumbuka tukio lililotokea miaka kumi na moja iliopita Dallas , siku ya Christimas?”Aliongea Bram na kumfanya Deigo kuonekana kukumbuka.
“Yes ! akili ilikuwa mbali , unamaansiha yule Gaidi aliye ua raia wa Kimarekani Zaidi ya ishirinni na tano kwenye mkesha wa sikukuu ya Christmas? Na akatoweka baada ya tukio lile na mpaka leo FBI wanamtafuta?”
“Ndio huyo huyo”
“Kwanini umetaja jina lake?”
“Notification yake imeletwa kutumia ‘Facial Recognition System’ na satilaiti ya Crogo”.Diego alishangaa kwani mtu ambaye alikuwa akitafutwa miaka na miaka na kundi la FBI kwa tukio la kutisha lilofanyika miaka kumi na moja nyuma siku ya sikukuu ya Christmas na kutoweka kusiko julikana baada ya tukio bila kuacha alama yoyote ya uwepo wake.
Ukiwauliza Raia wa Marekani ea Dallas juu ya mtu anaeitwa Afshar Bahman hakuna ambae atashindwa kumfahamu , kutokana na maumivu aliyoyasababisba kwa familia pamoja na Taifa la Marekani.
Tukio la Afshar Bahman linakuja miaka kumi na moja nyuma baada ya Afshar Bahman ambae alikuwa akitumia jina feki la Mahmood kumiminia waumini wa kanisa la The Forgiven chini Marekani na kuua raia 25 papo kwa papo na kujeruhi washirika kumi na moja huku kumi ya Raia kati ya ishirini na tano wakiwa ni watoto , tukio ambalo lilitokea miaka kumi na moja katika usiku wa mkesha wa sikukuu ya Christmasi saa saba kasoro ,baada ya waumini hao kuanza kutawanyika kuelekea majumbani baada ya ibada hio kuisha.
Kwa maelezo ya awali ya FBI baada ya tukio hilo la kutisha la kihistoria Mtuhumiwa huuyo ambae alikuwa akijiita Mahmood , alikuwa akitumia jina feki na jina lake halisi lilikuwa ni Afshar Bahman ,lakini taarifa ya kushangaza iliotolewa na idara hio ya usalama ya FBI ilisema Afshar Bahman baada ya kukamilisha tukio hilo alitoweka kwenye mazingira ya kutatanisha, jambo ambalo kwa zaidi ya muongo mmoja FBI walikuwa wakijiuliza bwana huyo alitoweka vipi pasipo kukamatika wala kuacha kivuli nyuma, swala hili liliwaumiza sana vichwa na kuanzia siku hio ya tukio Afshar Bahman akaingia lwenye jarada la watu wanaotafutwa zaidi na FBI(Most Wanted).
"Unamaanisha satilaiti yetu imeweza kumnasa Afshar ?"Aliuliza Diego huku akionesha hali ya mchecheto kwani aliamini kama swala hilo litakuwa la kweli basi litakuwa ni swala la mafanikio kwa kundi la The Eagles.
"Ndio amekmatwa na Rada na anaonekana kuwa hapa Tanzania , angalia hiii alama nyekundu ni eneo ambalo anaonekana kuwepo" Aliongea Bram.
"Sehemu hio ni wapi?”Aliuliza Diego na Bram alizoom na jina likasomeka Kunduchi. na wote waliangaliana.
"Hebu badilisha kwenda ‘Satelite View’ tuone eneo husika"Aliongea kwa haraka na Bram alifanya hivyo.
"Apple Apartment!"Aliongea Bram ,na ungeshangaa uwezo wa satelite kwani waliweza kusoma mpaka maandishi ya jengo refu la Apple Apartment ambalo linamilikiwa na Maple Group na muda huu haya yakiendelea ilikuwa ni Saa mbili za usiku kama dakika nane hivi.
Diego naamini kuna tukio linaenda kutokea ndani ya hili eneo na nadhani unakumbuka kunaa kisanyiko la wafanyabiashara wakubwa ndani ya hoteli ya Apple" Aliongea Bram na kumfanya Diego ashangae.
“Wasiliana na Chiara na John haraka tujue nia yake na wape maelekezo ya kutosha , ngoja niende na vijana na tuta ‘secure perimeter’ kabla hajatoroka,wape msisitizo tuunamtaka akiwa haoi"Aliongea Diego na kutoka hapo haraka huku Bram akifanya mawasiliano na Chiara na John.
*****
Suti ambayo Edna alimchagulia Roma ilikuwa imemkaa vizuri sana Roma , licha ya kwamba Roma alikuwa na mwonekano wa kawaida hata avae kitu cha thamani kubwa, lakini usiku huu alikuwa amependeza mno.
Roma na Edna walikuwa ni kama kusanyiko hilo lilikuwa la kwao , kwani kwa namna ambavyo walikuwa wakionekana ndani ya eneo hili la kuingilia ndani ya hoteli, waliwafanya watu watu kuwa midomo wazi , Madam T alionekana kufaulu katika zoezi zima la kumpamba Edna na vazi alilochagua.
“Roma usije ukaniangusha , hakikisha unaongea vizuri na wafanyabiashara , hii ni sehemu yako kwa kujenga kesho yako kupitia koneksheni”
Aliongea Edna aliekuwa ameshikilia mkono wa Roma huku wakiingia kwenye Lift kwenda Floor ya kumi na Sita ambayo ndio kulikuwa na ukumbi maalumu kwa ajili ya kusanyiko la wafanyabiashara.
"My wife usiwe na wasiwasi leo kwa jinsi ulivyopndeza nitahakikisha sikukasirishi usiku huu"Aliongea Roma na kumfanya Edna atabasamu na ndani ya dakika chache tu walikuwa nje ya mlango wa kuingilia ndani ya Ukumbi huu mkubwa unaotumiwakwa ajili ya hafla mbalimbali.
Eneo la ndani ya ukumbi lilikuwa limepambwa likapambika ,kwa namna ambavyo sehemu jii ilionekana ni dhahiri ilikuwa ikiwakilisha watu ambao walikuwa na pesa.
Wahudumu waliokuwa na vinywaji walipita huku na huko kuhakikisha wafanyabiashara hawa wanaumwagilia moyo vyema , lakini pia siku hii kulikuwa kumealikwa mpishi mkubwa sana Duniani kwa ajili ya kuandaa chakula kitamu kwa Wafanyabiashara hawa.
Wafanyabiashar wengi walikuwa washafika na ni wahcache sana ambao bado hawakuwa wamefika na walikuwa wakitarajiwa kufika , moja ya watu maarufun waliokuwa hapo ndani kwenye ukumbi alikuwa ni Neema luwazo huyu alikuwa ni Naibu waziri wa Sanaa na almaarufu kama Pisi ya mheshimiwa Kigombola , alikuwepo pia Abubakari Hamadi CEO , alikuwepo pia Meya wa jiji la Dodoma ndugu Bakari Juma , alikuwepo Mzee Alex mmiliki wa makampuni ya JR , Alikuwepo pia Balozi wa Tanzania nchini Japani , hao ni moja ya watu maarufu waliokuqepo ndani ya eneo hili lililopendeza na kuwakawaka taa nzuri za mapambo.
Abubakari kama kawaida yake leo hii alionekana kupendeza mno ,suti aliokuwa amevaa ilikuwa imemkaa vyema ,ukijumlisha na muonekano wake wa Kihandsome ulichangia kupendeza kwake , wakati huu alionekana kushikilia glass ya wine huku akiongea na wafanyabiashara wakubwa ndani ya taifa la Tanzania na muda wote alionekana kuachia cheko la kibiashara,cheko la pesa.
Neema Luwazo na yeye hakuwa nyuma katika kupendeza usiku huu , alionekana kama malaika , alikuwa amevaa akapendeza na kwa namna mwanamama huyu alivyokua akiongea na wafanyabiashara ungeona uzoefu uliokuwa ndani yake kwani muda wote alionekana kutabasamu na kutawala maongezi,alionekana kutumia fursa hiyo vyema kujijengea Koneksheni,ndio biashara ni koneksheni na hili linafahamika duniani kote , usipokuwa na koneksheni kwenye biashara huwezi kufanikiwa kirahisi lakini sio kwenye biashara tu , mambo mengi yanahitai Koneksheni .
Tajiri namba moja Tanzania Mohamed Azizi pia na yeye alikuwepo na bwama huyu alionekana kama kivutio kwa wafanyabiashara wengi , kwani kila mtu alionekana kutumia fursa yake vyema kuongea nae .
Ndani ya madakika kadhaa kupita hatimae hali ya hewa ilibadilika baada ya mrembo tajiri ndani ha Taifa la Tanzania kutokezea kwenye mlango wa kukngilia akiwa ameambatana na mtu ambae kwa wafanya biashara hawa walikuwa na hamu ya kumuona yaani mume wa tajiri mrembo Edna CEO .
Neema Luwazo alijikuta akipagawa na moyo wake kupiga kite mara baada ya kumuona Roma kwa mara ya tatu ,.Mwanaume ambae alikuwa akimuota kila siku akifanya nae mapenzi, hata muda mwingine kujimalizia mwenyewe , mwanaume ambaye alifanya amnyime kitumbua mheshimiwa Kigombola ,kilichomfanya mwanamama huyu kushangaa zaidi ni Mwanaume huyo kushikana mikono kimahaba na mtu ambae hakuwa akimtegemea yaani Edna Adebayo CEO,Malkia ndani yaulimwengu wa biashara, kwanini asipagawe .
“Mheshimiwa kutana na mume wangu Roma , Roma huyu ni Naibu waziri Neema na mmiliki wa kampuni ya Maple group nadhani mlikutana nchini Japan”
Edna alimtambulisha Neema kinafiki licha ya kwamba alikuwa akijua Roma na mwanamke huyo walikuwa na historia lakini hakutaka kuonyesha analifahamu hivyo kwani kwake ingekuwa udhaifu na alitumia nafasi hio kumuonesha Neema yeye ni mchepuko tu na yeye ameshikilia mpini , na kwa Roma aliona acheze ngoma alioanzisha mkewe kwani na yeye alifuata .
“Mr Roma hii ni mara yetu pili kukutana , nilidhani ni mfanyakazi pekee wa Vexto kumbe ni mume wa mrembo na Tajiri Edna”
“Ndio ndugu Waziri ! ,mimi ni mume wa huyu mrembo mzuri kuliko wanawake wote ndani ya hii dunia"Aliongea Roma na kumfanya Edna ajisikie utamu , lakini pia kumfanya Neema kuumia ndani kwa ndani na aliona ni kama Roma alikuwa akimfanyia makusudi mbele ya mkewe.
SEHEMU YA 62
Muda wote wakati Edna anaongea na Neema , watu wote hapa ndani macho yalikuwa kwa Edna na Roma , ni kama walikuwa kivutio usiku huu wa leo, na kwanini wasimwangalie sasa , kwani asilimia kubwa ya wanaume waliokuwa hapo ndani walishawahi kumtongoza Edna na kukataliwa , lakini jamaa wa kawaida sana asie Handsome kampata mrembo kama Edna , kwao ilikuwa ni pigo na aliekuwa akipumulia mashine ni Abuu,maana yeye ndie aliekuwa na juhudi lakini wapi.
Edna baada ya kusalimiana na Neema walihamia kwa wafanyabiashara wengine wakubwa wakubwa , na ni kama Edna alikuwa akichagua yupi wa kusalimiana nae na yupi wa kumuacha na hii ni kawaida sana , kwani Edna alikuwa matawi ya juu na pia asingeweza kusalimiana na kila mfanyabiashara kwani walikuwa wengi. .
“Edna sio pesa tu zilizoongezeka ila na wewe pia umezidi kuwa mrembo"Aliongea Tajiri Azizi na Edna alitabasamu .
“Asante Sann Mr Azizi , Kutana na Roma Ramoni mume wangu”
“Mr Roma nilikuwa nikisikia Edna kapata mume ,kumbe ndio wewe , Hongera sana kijana umekuwa kati ya vijana waliobahatika kupata mwanamke mrembo ndani ya taifa hili"
"Mr Azizi acha kumbania mke wangu , utapungukiwa nini ukitoa sifa zote , wewe sema dunia nzima ,halafu ongezea ,mbeba mizigo wa kwanza kupata mwanamke mrembo halafu tajiri"Aliongea Roma na kumfanya Mr Azizi acheke kama ilivyo kawaida yake ya kucheka na kufanya wafanya mbiashara wengine wawaangalie
Baada ya kutoka kwa Azizi walihamia kwa Mr Alex tajiri wa JR , Alex muda wote alikuwa akimtathimini Roma ni kama hakuwa akiamini maneno ya sifa aliokuwa akiambiwa , alimuona Roma kama kijana wak awaida sana na kujiuliza inakuwaje akawa anaogopwa na watu.
“Leo lazima utoe machozi wewe baada ya kumuona Edna akifa mbele yako”Aluwaza Alex huku akipokea mikono na Roma na wakaangaliana machoni ni kama walikuwa wakiwasiliana na Roma aligundua chuki kutoka kwa bwana huyu.
Baada ya kutoka kwa Alex walihamia kwa Abu ambae alikuwa akichemka muda wote kwa wivu , kwani alitamani nafasi ya Roma iwe yake na sio kutamani tu, aliona Roma amemuibia nafasi yake, Roms leo hii alionekannaa kufanya vyema sana mbele ya Edna na Edna alishukuru katika hilo kaani Roma hakuongea sana zaidi ya kupeana mikono.
“Muda si mrefu Edna utatoa machozi huyu kinyago ukimuona anakufan mbele yako”Aluwaza Abuu .
Na kwa namna ilivyonekana hapa ndani Abu alikuwa na mawazo tofauti na baba yake , kwani mzee Alex alikuwa akiwaza Kifo cha Edna na Abu alikuwa akiwaza kifo cha Roma ,kila mtu alikuwa na kipaumbele chake kati ya baba mlezi na mwana .
Neema Luwazo alikosa utulivu kabisa licha ya kwamba alikuwa akisalimiana na kundi lingine la wafanyabiashara , lakini akili yake ilikuwa kwa Roma , ni kama hakuwa akiamini kama mwanaume aliekuwa akimpenda, mke wake alikuwa ni Edna malkia wa biashara , alijiknta ile nafasi aliokuwa nayo ya ushindi ya kumpata Roma imeshika kwa asilimia kubwa sana na sasa alikuwa na silimia mbili tu za kumpata ,mpango wake wa kuwa mchepuki Grade A aliona umekutana na kikwazo , aliona hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa .
“Kwa Edna kanizidi kila kitu ,pesa na urembo ,kanipiga gepu pia kwenye umri ,mimi nina miaka mingi Edna bado mdogo hii ni changamoto kwangu ya kumpata Roma”Aliwaza Neema huku akisalimiana na baadhi ya wafanyabiashara .
Sasa ndani ya dakika chache aliingia mtu ambaye alifanya Roma atoe macho, huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Mama T ambae hakuwa peke yake na hili jambo lilimfanya Roma kushangaa zaidi , Mama T alikuwa ameambatana na mapacha wake, yaani Mage na Magdalena wadada hawa kwa namna walivyopemdeza katika vazi la aina moja ,na wao pia walikuwa kivutio kwa wafanyabiashara.
Mage ndie aliekuwa wa kwanza kumuona Roma lakini pia wakati huo macho yake yalishangaa zaidi kumuona Edna akiwa na Roma .
“Magdaelana yule si Edna!?”
Aliongea Mage huku akishangaa lakini wakati huo huo ni kama na Edna aliwaona kwani aliwasogelea kutoka alipokuwa amesimama na walikumbatiana , Edna na Mage walionekana kufahamiana jambo ambalo lilimuacha Roma mdomo wazi.
"Edna jamani ... ni siku nyingi hatujaonana kama hatuishi wote ndani ya nchi moja "Aliongea Mage huku akimwangalia usoni .
"Mambo ni mengi tokea nihame Osterbay, ni kama nilikuwa nje ya nchi kwa ubize... Magdaelana umerudi lini?"Aliuliza Edna na kumshitua Magdaelana ambae macho yake muda wote yalikuwa kwa Roma.
Kwa Magdalena hakua kama dada yake aliekuwa akimshangaa Roma kwanini yupo na Edna ,alichokuwa akishangaa ni wasiwasi wake wa kimaswali juu ya mtu anaeitwa Pluto kuwa mwanaume huyu ambae kwake ni mwanaume wa Kawaida sana na hakuwa akionesha upluto wowote kama alivyokuwa akisikia habari zake , aliona Afande Maeda huenda kamfananisha.
“Jamani huyu ni mume wangu anaitwa Roma Ramoni, Roma hawa ni marafiki zangu wa utotoni tumekuwa pamoja , majirani zetu”
Mage alianza kukumbuka siku ya kwanza alipokutana na Roma Vikindu mpaka kumpeleka kituo cha polisi Chalambe , alikumbuka akiongea na mwanamke kwenye simu ambaye kwa Roma alimtambulisha kwake kama mke wake.
“Kwanini sikuweza kuifahamu sauti ya Edna siku ile , ndi maana Mkuu alipaniki na kuniambia nimuachie “
Aliwaza Mage na pia akaanza kukumbuka tukio la Nadia Alfonso na hapa alizidi kuunganisha matukio na kuona kweli huyu mwanaume licha ya kwamba alikuwa akionekana wa kawaida , lakini hakuwa kawaida kama alivyokuwa anamdhania.
Roma aliwaangalia wanawake wakufanana waliokuwa mbele yake , na kisha akatabasamu na kuwapa mkono.
“Nafurahi kufahamina na ninyi japo sio mara ya kwanza , kwa Afande Mage na Afande Magdalena”Aliongea Roma na kumfanya Edna ashangae.
“Kumbe mashawahi kuonana?”Aliongea Edna kwa mshangao na Mage alitabasamu na kutingisha kichwa , lakini wakati wanaendelae kuaongesa mara alikuja Balozi wa Japani.
“Mr Roma , Miss Edna!”aliita mzee huyu na kumfanya Edna amwanagalie ,aliekuwa akiongea na Mage akitaka kujua namna ambavyo waliweza kukutana na mume wake
“Its been a while Edna since we last met, limekua jambo jema mara yetu ya pili kukutana umeshaolewa”Aliongea Balozi na Edna akaachia tabasamu lake ambalo lilizidi kuudhihirisha uzuri wake.lakini Roma akaingilia.
“Balozi tunaonana tena”.
“Ndio Mr Roma na moja ya sababu kubwa ya kufika hapa Tanzania ni kwa ajili ya kuonana na wewe”
Aliongea Balozi na kumfanya Roma ashangae na hata Edna , hakujua ni vipi Roma alikuwa akifahamiana nipi na Balozi , lakini alijisikia faraja kuona mume wake alikuwa akifahamina na baadhi ya watu wakubwa , aliona ni hatua nzuri , hakutaka kufikiria sana ni kwa namna gani wawili hao waliweza kufahamiana.
“Miss Edna naamini haitakuuzi nikimchukua mume kwa dakika kadhaa nina mazungumzo nae”Aliongea na Edna alitingisha kichwa kukubali huku Edna na Mage wakisogea mpaka ndani kabisa upande ambao ulikuwa ukiangaliana na jengo la Apple Apartment.
“Hades najua sio jambo jema kuongellea hapa , ila sina muda mwingi hapa Tazania , kesho inanibidi kurudi Japani”
“Haina haja ya kuzungukazukuka Balozi , nenda moja kwa moja kwenye swala lako”Aliongea Roma na bwana huyu alivuta pumzi kidogo na kuzitoa.
“Nimefikiria lile swala la wewe kuwa mkwe wangu , niseme kwamba nimeridhia kiroho safi , na sababu kubwa ni Sopha anasumbua sana , anasema anataka kuwa mke wako , na mimi pia baada ya kufikiria swala hili nimeona sio jambo baya , Hades sijui historia yako ya nyuma , lakini nasikia watu wanakutia Mfalme Pluto hii ni sifa tosha ya wewe kutomkataa Sophia”Roma alijikuta akishangaa , nikama alishindwa kumuelewa mzee huyu , kwani siku ile maneno aliongea kwake yalikuwa ni utani iweje kachukulia siriasi.
“Balozi sina mpango wa kuoa tena nishakuwa na mke tayari”
“Hades naelewa unachomaanisha ,sikuambii umuache mkeo, nachokuambia umuoe Sophia awe mke wako mdogo , wewe ndio mtu pekee ambae unaweza kumlinda Sophia , nimekua nikijiambia kwenye maisha yangu mwanaume ambaye Sophia atakuja kuolewa nae lazima awe na nguvu za kumlinda na wewe umejitokeza na pia Sophia anakupenda kiasi cha kunitishia Amani , anasema usipo muoa wewe haolewi na mimi mpaka sasa nashangaa umemfanya nini Sophia Hades mpaka kupenda kwa muda mfupi kiasi hicho”Roma aliona sasa hapa kinachoendelea ni jaribu, hakuelewa .
“Sophia atakuja kuishi hapa Tanzania Hades naamini utampa ulinzi wa kutosha m na pia kadri ukakavyokua nae karibu naamini lazima utampenda,Sophia ni mrembo na pia anakili nyingi”
Aliongea Balozi na kisha akageuka ni kama hakutaka kusikiliza jibu kutoka kwa Roma , lakini sasa wakati Balozi anageuka Roma macho yake yalitua kwa Chiara aliekuwa akiingia hapo ndani akihema , na kumfanya Roma kumwangalia Edna na ni kama macho yake yalikuwa na X-Ray kwani aliweza kuona Risasi inayotoka kwenye Bunduki upande wa pili , ilikuwa ni kitendo cha haraka sana kilichofanyika , kwani Roma alipokuwa amesimama alihama kama jini , na ile anaibuka , alikuwa amemkinga Edna na mgongo wake na palepale Risasi mbili zikatua kwenye mgongo wa Roma na hali ya hewa ikabadilika , huku dirisa likiwa na tobo la Risasi
Magdalena alikuwa ametoa macho ya mshangao , kwani jambo ambalo lilitokea alilishuhudia , kwani yeye pekee ndie aliekuwa akimwangalia Roma muda wote .
Roma alijikuta akimtemea Damu Edna , hali ya hewa ilibadilika ghafla , kila mtu alishindwa kuelewa kile ambacho kimetokea , watu walianza kuhaha , kwa tukio hilo , lilikuwa ni swala ambalo liliacha mshituko kwa kila mtu..
Upande wa pili chmba alichokuwa Seif , baada ya kuona mtu aliempiga risasi ni Roma alitoa tusi , lakini aliona sio mbaya pia, alikumbuka kuwa Abu tageti yake ni Roma na Mheshimiwa Kigombola na Mzee Alex tageti yao ilikuwa ni Edna.
“Not Bad” Aliwaza
Baada ya kumaliza tu alianza kukusanya bunduki lake kwa ajili ya kuondoka eneo la tukio , lakini ni kama alichelewa kwani muda huo huo aliingai John na Bastora yake mkononi na haikueleweka aliitoa wapi kwani Tanzania hawakuja na Siraha.
“Mikono juu Afshar Bahman! Jambo lolote la kijinga nakupasu”Aliamrisha John na kumshitua Seif ambaye alikuwa bize na kufunga bunduki lake, lakini bwana huyu hakugeuka , akili yake ilifanya kazi haraka , alikumbuka mkataba na mabosi wake haukuwa ukimtaka kukamatwa baada ya tukioo na kama itatokea amekaamatwa basi ahakikishe anajiua, lakini kubwa Zaidi lililomshangaza ni mzungu ambaye alimwita kwa jina lake halisi.
“FBI how did they found me?”Aliwaza
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana Seif alichokifanya , alijirusha nje kwenye gorofa hio ya floor Zaidi ya ishirini , ni kitendo ambacho John hakuwa amekitegemea.
“Sh***T!”Alitamka tusi na kisha akakimbilia Dirishani na kuangalia chini , lakini ajabu ni kwamba chini Seif hakuonekana , alizidi kuangalia kwa umakini , lakini Seif hakuonekana , lilikuwa jambo la kushangaza.
“Diego he is Disappered , our Target disappeared again just like eleven year ago with FBI”
“What.. how!”Ilikuwa sauti ya upande wa pili ya Diego”
“I just can`t comprehend , I need to confirm the situation , Back up is needed”
“Okey we are coming , we will secure the perimeter , he is not going to Escape again”Aliongea Diego kwenye simu huku John akikimbilia chini kwa kutumia ngazi.
UNAJUA NINI KIMETOKEA ..
ENDELEA KUTOA MCHANGO KUANZIA 2000 KUENDELEA KUNISAPOTI , UKILIPA UNATUMIWA SIMULIZI HII INBOX WATSAPP AU UNAUNGANISHWA NA GRUPU , TUKO SEHEMU YA 90 KWA SASA , UTATUMIWA VIPANDE VYOTE MPAKA TULIPOSIHIA
NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346