SEHEMU YA 141
Edna aliendelea na matibabu ndani ya hospitali kama daktari alivyoshauri.licha ya Edna kutaka kuendelea na matibabu akiwa nyumbani , lakini Bi Wema alikataa kwa msisitizo mkubwa sana kwa Edna kutorudi nyumbani na Edna kwakua alikuwa akimheshimu Bi Wema kama mama yake alitii na kuamua kubakia hospitalini huku majukumu yake ya kazi akiyafanyia ndani ya Wodi kama kawaida , upande wa kampuni majukumu yake yalibebwa na CEO msaidizi bwana Ernest Komwe.
Upande wa Roma siku ya Wikiendi usiku hakuimalizia nyumbani bali alilala usiku kucha nyumbani kwa Rose wakifanyana , Hakua na wasiwasi juu ya Edna aliekuwa hospitalini kwani walinzi wake walikuwa wakifanya kazi yao kwa ufasaha , lakini pia kutokana na sheria za hospitali ya Aghakhani kwa uande wa VIP hawakuruhusu watu kulala hospitalini ambao sio wagonjwa , kulikuwa na manesi ambao walikuwa wako karibu na wagonjwa kwa masaa ishirini na nne.
Jambo pekee ambalo kama familia walikuwa wakifanya ni kuhakikisha Edna anapelekewa baadhi ya mahitaji muhimu kama vile nguo na mengineyo , chakula kilikuwa kikitolewa hospialini.
Ni Muda wa Asubuhi wakati Roma ndio kwanza anatoka kuoga mara baada ya kumaliza kupiga cha Asubuhi na mrembo Rose , simu yake ilianza kuita mfululizo na kumfanya Roma aichukue na kuangalia ni nani aliekuwa akipiga na baada ya kuona jina ni Bi Wema alipatwa na wasiwasi na kuona huenda kuna jambo ambalo limetokea hospitalini hivyo alipokea haraka haraka.
“Bi Wema kuna nin?”Aliuliza Roma moja kwa moja akiwa na wasiwasi huku akimwnagalia Rose.
“Sio jambo kubwa Roma , ni kwamba Sophie hayupo na nimejiumiza mguu asubuhi hii ya leo na nashindwa kumpelekea baadhi ya mahitaji yake Edna , ndio maana nimekupigia”Aliongea Bi Wema na kumfanya Roma apumue kwa afadhali.
“Nakuja Bi Wema muda si mrefu nitakupeleka na hospitalini”Aliongea
“Hapana Roma ninachotaka unisaidie kumpelekea mkeo tu mahitji yake”
“Sawa Bi Wema nakuja sasa hivi”Aliongea Roma na kisha akakata sim una kumwangalia Rose.
“Bebi Rose Ngoja niwahi nyumbani nikampelekee mke wangu baadhi ya mahitaji ya asubuhi”Aliongea Roma
“Usijali naelewa mke ni muhimu Zaidi kuliko mchepuko , wewe nenda uwahi sawa”Aliongea Rose na kumfanya Roma atabasamu.
“Usijali kila mtu ana umuhimu wake , kama utapenda nitakuja tena jioni ya leo?”
“Hapana , nitakuwa bize sana usiku wa leo juu ya maswala ya biashara yangu nitakupigia tu simu”Aliongea Rose na kisha Roma alimsogelea na kumbusu shavuni na kuchukua ufunguo wake na kuondoka.
Roma aliendesha gari yake kwa mwendo kuelekea Kigamboni , huku akiwa na mawazo mchanganyiko , ukweli ni kwamba alikuwa akiwaza Maisha ya baadae yatakavyokuwa juu ya wanawake wake, yaani alimuwazia Rose , Nasra ,Dorisi na Neema kwa wakati mmoja , alijua hakuwa na mpango wa kuachana kabisa na Edna hata kama siku mkataba wao utaisha ,lakini sasa aliamini ili hilo liwezekane ni mpaka Edna atakaporidhia kwa asilimia mia moja kuwa mume wake kabisa na sio kwa mkataba bali kwa mapenzi , lakini aliwaza kama hilo likienda kutokea vipi kuhusu michepuko yake, baada ya kuona anawaza mambo ambayo mpaka muda huo hayana majibu aliachana nayo na kuendelea kuendesha na ndani ya muda mfupu tu alikuwa ndani ya nyumba yao na Bi Wema nadhani baada ya kusikia gari ya Roma alitoka kabisa , kwani alikuwa amesimama mbele ya mlango huku akiwa na mfuko mkubwa umefungwa nadhani ni ili vitu vya ndani visionekane.
“Vipi mguu hauumi sana?”aliuliza Roma baada ya kupokea ule mfuko.
“Hapana nikijipaka dawa leo na kesho utakuwa sawa , hua sio mara moja Napata majeraha mara kwa mara , Nadhani uelekee hospitalini sasa umpelekee Miss huo mzigo maana ukichelewa hatokuwa sawa”Aliongea Bi Wema na kumshangaza kidogo Roma hakujua kwanini Bi Wema alikuwa akimwambia kama akichelewa Edna hatokuwa sawa , ila hakutaka kuuliza sana aliingia kwenye gari yake na kuliondoa kuelekea hospitalini.
Ndani ya madakika kadhaa tu Roma alikuwa nje ya chumba alicholazwa Edna , baada ya kugonga mlango aliusukuma na kuingia , ilikuwa ni mapema ya jumapili lakini Edna alionekana kuamka muda tu na alikuwa ameshikilia kitabu akisoma na Edna alisalimiana nae kwa kumpa tabasamu.
“Wife muda kama huu ukiwa hapa hospitalini nategemea kuona ukiacha kusoma hayo mambo yanayohusu kampuni , hauchoki tu , mwanamke unatakiwa kujipenda bwana”Aliongea Roma na hii ni baada ya kutopendezwa na namna Edna alivyokuwa bize akisoma kitabu kilichokuwa kwenye mikono yake , aliona anapaswa kumuelekeza Edna baadhi ya mambo.
“Unafikiria nisiofanya kazi kwa juhudi nini kitatokea , familia nyingi zinategemea kampuni yangu lakini pia walioniachia kampuni walikuwa wakitegemea kitu kikubwa kutoka kwangu ,Roma mpaka sasa najua una hela nyingi hata kunizidi lakini mimi ni tofauti na wewe utajiri wako upo kwa mfumo wa pesa taslimu lakini kwangu mimi hela zipo kwenye kampuni na kupitia hela zangu watu wanapata mishahara na kuendesha Maisha yao nikikaa legelege unafikiri nini kitatokea…”Aliongea Edna.
“Sio kama nakuambia uwe legelege mke wangu ninachomaanisha ni kwamba sio kila kitu lazima ufanye wewe kwenye kampuni , gawa majukumu kwa waliochini yako , fanya kazi lakini kuwa na muda wa kupumzika wikiend kama hivi unaenda hata nje ya nchi ;Vacation’ unapumzika, tafuta muda wa kukaa na marafiki zako , sasa kuna utofauti gani kati ya masikini na wewe kama huna muda wa kumumzika?”Aliongea Roma lakini Edna alionekana hata kutojali alinyooshea mkono mfuko alioshikilia Roma.
“Humo ndani umeleta nini?”
Roma aliishia kutabasamu baada ya kuona Edna anapotezea Topic na alichokifanya ni kumsogezea mfuko aliokuwa ameubeba, na Edna baada ya kuupokea , kwakua ulikuwa mkubwa yeye hakujali kutoa kitu kimoja moja alichofanya ni kumwaga kila kitu kitandani huku Roma akimwangalia, na hapo ni kama joto la chumba limeongezeka kwani vitu ambavvyo vimewekwa ndani ya mfuko huo vilikuwa ni vya siri kwa upande wa Edna , kulikuwa ni nguo nyingi za ndani za rangi tofauti lakini pia kulikuwa na pedi na hapa baada ya Roma kuona vitu hivyo alikumbuka maneno ya Bi Wema kwamba akichelewesha Edna hatokuwa sawa.
Roma hakuwa na aibu aliendelea kuangalia kila kitu kilichokuwa kipo juu ya kitanda, na alivyoona nguo za ndani ,bwana huyu alianza kuwaza ile siku aliomchukua Edna na kumpeleka geto kwake , sasa akaweka picha kwa kila nguo iliokuwa hapo kitandani kwa kumuona nayo Edna akiwa ameivaa na kujikuta mapigo yake ya moyo yakiendelea kuongezeka.
“Hutakiwi kuangalia..”Aliongea Edna kwa aibu huku akifunika kwa shuka , mrembo huyu alishangazwa na namna Bi Wema alivyomfungashia kwani ilikuwa ni tofauti na alivyoagiza , yeye aliagiza nguo za kawaida tu , lakini Bi Wema alichagua nguo za ndani mpaka zile zenye maua maua.
“Khoo,,, Mh. Mh!”Alikohoa Roma baada ya kushushuliwa na Edna ambaye alikuwa akiona aibu na lawama zote kumpelekea Bi Wema , alijiambia kama angejua kwenye huo mfuko kulikuwa kumewekwa hivyo vitu basi asingevimwaga moja kwa moja kwenye kitanda.
“Nadhani mzigo nimeleta nirudi sasa , nikuache upumzike”.
“Yeah..itakuwa vizuri”Alijibu Edna kwa sauti ndogo na Roma ukweli hakutaka kubakia hapo hospitalini na ndio maana aligeuka kwa ajili ya kutoka lakini alivyofikia mlango aligeuka na kumwangalia Edna.
“Wife Hio ya Rangi ya pink yenye maua maua hapo mbele nimeipenda”
“……”
Edna aliishia kumwangalia Roma na kushindwa hata kuongea chochote na Roma alitoka na kufunga mlango huku akitabasamu , alipenda muonekano wa Edna baada ya kumtannia.
Edna baada ya Roma kutoka alirudi kwenye hali yake ya utulivu na kuvuta mkoba wake uliokuwa pembeni yake na baada ya kuuchukua alitoa pete mbayo siku mbili nyuma alikuwa amepewa na Roma , aliangalia pete hio ambayo ilikuwa sio ya kawaida na kuisugua na kidole chake huku mawazo mchanganyiko yakimuandama , ukweli ni kwamba usiku mzima hakuweza kulala Zaidi ya kufikiria ni historia gani ya nyuma ambayo ipo kwenye Maisha ya Roma..
Usiku aliweza kufikiria kwanzia siku ya kwanza kuoana na Roma akiwa kwenye chumba cha kupanga akiwa ametandika godoro chini akiwa uchi , siku ambayo aliweza kupoteza usichana wake ,tukio mbalo lilisababishwa na Abubakari mpaka kuingia kwenye mikono ya Roma.
Edna hakuishia hapo tu aliwaza namna mara ya pili yake alivyokutana na Roma kwa ajili a kuweka wazi nia yake ya kutaka kuolewa nae, lakini pia namna Roma alivyomkamata mara baada tu ya kutania kutaka kujirusha nje ya Ghorofa ili kumfanya Roma kukubali kumuoa baada ya kukataa.
Mrembo huyu lifikiria mambo yote ya kushangaza yaliotokea yale ya kushangaza kuoneakana kwa binadamu wa kawaida, Edn alifikiria muda wa mambo hayo yote kutokea na aliona ni mwezi sasa kwa mambo yote hayo kutokea na kujikuta mwenyewe kushangaa , kwani ilikuwa ni kipindi kidogo sana walichoishi na Roma lakini ni mambo mengi ambayo yametokea ambayo mengi sio ya kawaida kabisa , kwa jinsi alivyoishi na Roma kwa muda wote huo ni kama aliishi nae kwa muda wa mwaka mzima , kwani alikuwa amepata hisia zote kwa wakati , aliweza kupata uzoefu wa kuwa na mwanaume karibu wakati wa shida, aliweza pia kupata uzoefu wa kukasirika na kujisikia vizuri kwa wakati mmoja, Edna pia hakuacha kufikiria michepuko yote ya Roma , akaja kuhitimisha kwenye maneno ya Meneja mkuu wa benki ya Swiss juu ya Roma kumiliki Zaidi ya mabilioni ya pesa , mrembo huyu alianza kuzipigia hela hizo hesabu na kuona ni nyingi mno na Roma angetaka hata kununua nusu ya Bara la Afrika angeweza , lakini alishangaa kwannini Roma akaamua kushi Maisha ya kawaida ilihali alikuwa na pesa nyingi kiasi hiko benki zimekaa tu , kwani aliamini kama pesa hizo zingekuwa kwenye mikono ya watu ambao wanahamasa ya kufanya biashara basi majina yao yangesikika duniani kote kwa kumiliki kiasi kama hiko cha pesa
“Maybe kukutana kwetu sio jambo la bahati mbaya”aliwaza Edna na kisha alijiegamiza na kujikuta kupotelea usingizini.
Edna baada ya kuangalia pete iliokuwa kwenye mikono yake kwa dakika kadhaa alijikuta akifunua nguo ambazo Roma ameziona na kisha alitafuta ile ambayo Roma aliisemea kwa kuisifia na kisha akaanza kuikagua na kuishia kutabasamu na haikueleweka alikuwa akitabasamu nini.
SEHEMU YA 142
Upande mwingine siku hio ya jumapili , alionekenana Tajiri Azizi akiwa ndani ya gari aina ya Range Rover Sport nyeusi iliokuwa barabara ya Bagamoyo road ikielekea upande wa Bunju B, kwani muda huo akiwa anaendeshwa na dereva wake alikuwa ndani ya eneo la Bunju A ,baada ya madakika kadhaa , Walikuja kukunja kushoto mara baada ya kufika mita kadhaa kutoka ilipokuwa Shule ya Sekondati ya Baobab na kuelekea juu Zaidi, na gari yake ilikuja kusimama nje kabisa ya geti kubwa la Rangi nyeusi lililonakishiwa na rangi ya Shaba na baada ya kusimama kwa dakika kaa mbili baada ya dereva kupiga honi , hatimae geti lilionekana likifunguliwa kwa kusukumwa na kijana alievalia gwanda za Jeshi la JWTZ.
Baada ya gari kweenda kusimama eneo maalumu , Tajiri huyu ambaye leo hii alikuwa amevalia kawaida tu kwa kupigilia Tishti yake iliomkaa vyema mwilini pamoja na Jeans, alianza kupiga hatua kuingia ndani ya jumba kubwa lililokuwa mbele yake , ilikuwa ni nyumba kubwa ya kifahari mno yenye mazingira ya kuvutia na nidhahiri mtu aliekuwa akiishi hapo ndani hakuwa kinyonge kabisa likija swala la pesa, lakini pia uwepo wa wanajeshi hapo ndani uliashiria mtu aliekuwa akiishi hapo ndani anahusiana moja kwa moja na jeshi.
“Denisi!!!”Aliita Tajiri Azizi baada ya kukutana na kijana Denisi mtoto wa Raisi Senga akiwa anatoka ndani ya mlango wa kuingilia.
“Si Azizi Shikamoo”
“Marhaba!, Naona leo umakuja kumsalimia babu yako?”
“Ndio nimekuja kumsalimia mzee lakini pia kumuaga”
“Kumuaga tena unarudi masomoni?”Aliuliza Tajiri Azizi.
“Ndio ”Aliongea Denisi huku akionekana kuwa na haraka na Tajiri Azizi aliagana nae na kumtakia safari njema.
Baada ya dakika kadhaa wakiwa wanaingia barabara kuu , Denisi alionekana kuwaza kidogo.
“Diki unadhani Tajiri Azizi ni kwanini ameenda kuonana na Babu?”aliuliza Denisi akimwangalia Dereva wake Diki kwa kutumia kioo cha juu.
“Bosi siwezi kufahamu ila kama unataka nifuatilie nitafahamu”
“Fanya hivyo nataka kujua kila kinachoendelea kwenye ukoo wetu, kila kinachoendelea unipatie taarifa angalia namna ya kuweka mtu wetu karibu na babu”
“Sawa bosi, lakini nataka kuuliza!!!”
“Uliza”
“Kwanini unakuwa makini Zaidi na Babu yako kuliko baba yako ambaye ndio raisi”Aliuliza Diki na kumfanya Denisi kutabasamu.
“Babu ni sehemu ya msingi wa hii nchi na sio mwanasiasa , baba yeye ni mwanasiasa tu na nguvu yake inaisha baada ya kumaliza mihula yake ya kiuongozi lakini nguvu ya babu inaendelea hata atakapofariki , wewe huoni muda wote nyumbani kwa babu kuna wanajeshi wanaomlinda?”
“Ni kweli lakini bado baba yako anabakia kuwa kiongozi mkubwa ndani ya taifa”
“Baba alikataa matakwa ya Babu kwenda jeshi na akakimbilia kuwa mwanasiasa, lakini kama unavyojua baba ndio mwanaume pekee kwenye uzao wa babu , unafikiri kwa ukoo wetu ambao nguvu yake ipo jeshini babu aataweza kumrishitsha baba nafasi yake katika jeshi ilihali ni mwanasiasa?”
“Kwahio bosi ndio maana ukaamua kujiunga jeshini baada ya kutoka Tanzania na ukaidanganya familia yako kuwa mwanafunzi wa kawaida chuoni?, ni kwasababu unataka kuwa mrithi wa babu yako?”
“Unaonekana sasa kuwa na akili Diki , mimi ni mwanajeshi hivyo siwezi kumrithi baba katika shughuli zake za kisiasa na ndio maana sina matamanio yoyote kwa kile anachokifanya”
“Ila siku mheshimiwa akifahamu kama ulimdanganya kwa miaka yote hio kuwa upo chuoni sidhanii atachukua uwamuuzi gani?”
“Hilo lisikuumize kichwa , ilihali babu mwenyewe ndio alinishauri niende nikasomee jeshi nchini China na sio kwenda chuo basi sina haja ya kuogopa chochote, baba anamuheshimu babu na hata nafasi yake ya uraisi imetokana na nguvu ya Babu kwenye taifa hili”Aliongea Denisi na kisha akaegamia kwenye kiti chake na alionekana hakutaka maongezi Zaidi.
“Vipi niendeshe kuelekea wapi Bosi?”
“Twende Rotana nahitaji kuonana na Sophia”Aliongea Denisi
*****
Upande wa huku nyumbani Tajiri Azizi alipokelewa na mwanamama mmoja hivi mwanamke mchina alievalia suti na kisha akamuongoza kwenda ndani kabisa upande wa kulia mara baada ya kuacha upande wa Sebuleni na baada ya Tajiri huyu kuingia aliweza kumuona Mzee mbaye hakuwa amezeeka sana , alikuwa na umri kama wa miaka themanini na tano hivi kuendelea, akiwa amevalia sweta zito na miwani ya macho huku akiwa amekaa kwenye sofa.
Hapo ndani ilikuwa ni kama ofisi ndogo ya mzee huu , kwani kwa mbele kulikuwa na meza na tarakishi, lakini pia na shelfu kubwa iliojaa mavitabu mengi , upande wa kushoto wa chumba hiko kulikuwa na bendera ya Tanzania harafu pembeni yake kuna Kombati ya jeshi yenye vyeo vingi iliokuwa imening`nizwa kwenye ‘Hanger’.
“General Camilius Kweka”Ndio jina lililokuwa likisomeaka kwenye kombati hio ya jeshi.
“Shikamoo mzee”Alisalimia Tajiri Azizi na kumfanya Generali Senga Kweka kuweka gazeti alilokuwa akisoma pembeni na kuvua miwani yake na kumpatia yule mwanamke wa kichina.
“Marhaba! Karibu sana Azizi nilikuwa nikikusubiria”
“Asante sana”Aliongea Tajiri na kisha akakaa vizuri.
“Nadhani twende moja kwa moja Azizi kwenye ujumbe ambao umepewa na Raisi Jeremy”Aliongea huyu mzee na alionekana afya yake bado ilikuwa imara kwani licha ya kuwa mzee hakuonyesha unyonge katika kuzungumza kwake , na hii inaonyesha jeshi ndio limemfanya mzee huyu kutokuwa myonge.
Tajiri baada a kuambiwa aende moja kwa moja alielewa , alikuwa akielewa wanajeshi hawakuwa wafanyabiashara au wanasiasa, wao walitaka kwenda moja kwa moja kwenye jambo husika na ndio maana alitoa Bahasha ndogo na kumpatia Afande Mstaafu Camilius Kweka na mzee huyu mara baada ya kupokea bahasha hio alitoa picha na kuziweka mkononi na kisha akampa ishara Mchina ampatie miwani yake na mzee huyu alionekana kuona mbali vizuri ila alikuwa akishindwa kuona karibu.
“Hii picha inaonekana kama ya Denisi , licha ya kwamba imekuwa miaka mingi lakini naikumbuka picha ya mjukuu wangu wa kwanza”Aliongea mzee na kisha akampatia yule mchina ile picha na yeye akaingalia kwa dakika kadhaa.
“Hakika hii ni yenyewe Sir”Aliongea Mchina huku mzee huyu akiendelea kuangalia picha ya pili kwa umakini nikama kuna jambo aligundua ila hakuwa na uhakika na ndio maana alimpatia yule mchina ile picha na baada ya yule mchina kuichukua ile picha alianza pia kuikodolea macho.
“Hawa ni watu wawili Camilius”Aliongea yule Mchina na muda wote huu Tajiri Azizi hakuwa akiongea lolote.
“Kwa jinsi ninavyoona tarehe za hizi picha zote mbele zinashangaza”
“Nini kimekushangaza Zhenzei?”
“Hii ya kwanza inaonekana ni ya mwaka 1998 na hii ya pili inaonekana kuwa ya hivi karibuni na picha zote hizi ni za tu mmoja kwa maana hio……”Kabla hajamaliza mzee alimpa ishara asimalize kuongea na akamgeukia Tajiri Azizi.
“Nadhani tunahitaji maelezo yaliobaki kutoka kwako , mpaka hapa nipo kwenye mshangao na nahitaji majibu”Aliongea Mwanajeshi huyu wa Zamani na kumfanya Tajiri kwanza ashangaae kwani alichokuwa akitegemea ni kuona mzee huyu kuwa katika mshangao mkubwa sana , lakini kwa hali anayoiona kwa sasa hapo mdani ni kwamba yeye ndio aliekuwa akishangaa.
“Ndio Mzee huo ni Ushahidi wa kwamba ndege ya shirika la M Airline haikuwa ajali bali swala la kupangwa na Roma Ramoni ndio Denisi”
Aliongea Tajiri kwa ufupi huku akimwangalia Mzee , lakini bado mzee huyu hakuwa akionyesha mshangao hata kidogo na kuzidi kujiuliza maswali inakuwaje huyu mzee haonyeshi hisia zozote za mshangao na alishindwa hata kuelewa.
“Azizi nadhani mpaka hapa unamaswali ya kwanini hatuonyeshi aina yoyote ya kushituka na hii taarifa?”Aliuliza Afande mstaafu Kweka na Tajiri alitingisha kichwa kukubali na Mzee alitabasamu na kisha akampa ishara Mchina anafahamika kwa jina la Zhenzei.
Na mchina yule alitoa picha mbao ya mzee mmoja ambaye hakutambulika kwa haraka ukutan mbele yao na kikaonekana kijimlango , rangi nyeusi kilichofnngwa na pembenni yake kulikuwa na sehemu flani ya kuingizia namba na Mchina yule mara baada ya kuweka picha chini aliingiza namba na kufungua na zikaonekana faili mbalimbali zilizopangwa kwenye hiko kijiboksi na bila ya kuzigusa alivuta bahasha ya khaki iliokuwa juu kabisa na kuitoa na kisha akasogea mpaka alipokaa Azizi na kumpatia na kumfanya Tajiri huyu kushangaa maana hakujua ni nini kinaendelea hapa ndani.
“Unaweza kuangalia kitu gani kipo ndani ya hio bahasha”Aliongea Mchina kwa Kiswahili safi kabisa.
SEHEMU YA 143
SIKU CHACHE NYUMA.
Ilikuwa ni siku ambayo Edna alitekwa na Kundi la Yamata Sect na kumpelekea hadi Roma kwenda mpaka hadi Msitu wa Mabwepande kwa ajili ya kuwapa kundi hilo jiwe la Kimungu.
Sasa siku hii muda wa asubuhi ndani ya nyumba hii hii ambayo Tajiri ameingia kuonana na mwanajeshi mstaafu Kweka , ndio muda ambao Jenerali mstaafu Athumani alikuwa akiingia hapo ndani na gari yange aina ya V8 huku akiwa ameshikilia bahasha mkononi na baada ya kupokelewa na mchina na baadhi ya wafanyakzi wa jumba hili moja kwa moja aliingia ndani ya chumba cha Afande Kweka na akabana T*ko kama ishara ya salamu na akapewa ishara ya kulegeza na Mzee kweka.
“Umefanikiwa?”Aliuliza Mzee Kweka na kwa Afande Athumani hakuongea Zaidi kwani alimkabidhi ile bahasha Zhenzei na aliifungua na kuangalia kilichokuwemo humo ndani.
“DNA PATERNITY TEST, ROMA VS KWEKA”
Ndio yalikuwa ni majibu ya DNA kati ya Roma na Mzee Kweka na haikueleweka ni lini kipimo hiko kilifanyika.
“Zhezhei majibu yanasemaje?”
“Ni mwanafamilia kwa asilimia mia moja Camilius”Aliongea huku akitabasamu na hata kwa Afande Athumani kutabasamu.
“Sio jambo la kushangaza sana kwasasa tushapata uhakika wa asilimia mia moja kwamba Roma ndio Denisi”Aliongea Mzee Kweka .
“Afande nini kinafuata?”
“Hakuna haja ya kuwa na haraka juu ya hilo , Roma karudi nchini kuitafuta familia yake naamini atatutambua muda sio mrefu”Aliongea Mzee huyu.
“Lakini mzee vipi kuhusu mheshimiwa Raisi”
“Kuhusu Senga Achana nae kwa sasa atajua muda ukifika nitakapoamua kumwambia ukweli wote uliotokea miaka iliopita”Aliongea mzee huyu huku akufumba macho ni kama tu ambaye alikuwa akitafuta hisia.
“Nadhani Afande kabla ya kumwambia Senga nini kilitokea miaka iliopita utanipa kipaumbele cha kuujua ukweli kabla yake?”
“Athumani usijali sana , sisi wote hapa ni wanajeshi, muda sio mrefu nitakuambia kwa sasa nataka uendelee kuwa makini na usalama wa taifa hili wewe pamoja na Majenerali wengine wote sisi ni wahimili wa taifa hili , ndio walinzi wa misingi yake na ndio wenye nguvu hatuwezi tukawafanya wanasiasa kua na nguvu juu yetu, usijali kuhusu Roma nitaweka ukweli wote wazi”Aliongea Mzee huyu na kumfanya babu yake Edna atabasamu.
“Hata hivyo Athumani usisahau kuwa familia zetu zinaunganishwa na mjukuu wako Edna , nadhani ni muda muafaka wa kuhakikisha Edna anakuita babu hatutaki arejee kwenye mikono ya koo za Rwanda”Aliongea Mzee .
“Ni kweli usemayo Afande ninalifanyia kazi hilo na mpaka sasa mpango wangu wa kumfanya Edna arudi kwenye familia yetu unaendelea”Aliongea na kumfanya Mzee huyu kutabasamu kivivu na kisha wakaagana.
******
Tajiri alishindwa kuamini alichokuwa akikiona na mpaka kufikia hatua hio alijua ni kwanini huyu mzee hakuwa na mshangao.
“Tajiri Azizi najua wewe ni moja ya wafanyabiashara wakubwa ndani ya taifa hili ambao uchumi wetu unakutegemea sana kwa uwezo wako, lakini pia najua kuwa una urafiki kubwa sana na Raisi wa Rwanda na ndio maana nimekupa usome hayo ajibu”Aliongea Mzee.
“Kwannini umeamua kunipatia haya majibu?”
“Kwasababu nataka ukamwambie Jeremy kwamba Msingi wa Taifa la Tanzania sio lelemama kama anavyofikiria , tunajua mambo mengi yanayoendelea ndanni ya taifa hili na nje ya mipaka yetu , swala la Roma tunalijua muda mrefu tu na kila anachofahamu sisi ndio tumeruhusu kwa yeye kukifahamu”Aliongea mzee huyu na kumuacha Tajiri kwenye mshituko.
“Mzee unamaanisha kwamba unajua kila kitu ambacho mheshimiwa Jeremy anakifanya?”
“Najua hata tukio la wewe kumuiba pacha wake Edna na kumpelekea Jeremy kwa makubaliano yenu na Rahel”Aliongea huku akitabasamu kwa uvivu na kusaidiwa na Mchina na kumfanya Tajiri ashindwe hata kuongea neno.
“Mpaka hapo nadhanni unaweza kufahamu kwanini nakuambia na kwanini nasema sisi Wazee , ndio msingi wa hili taifa?”Aliongea na Tairi kusema ukweli maka hautua hio tajiri aliogopa kwa wakati mmoja na mbele yake hakumuona babu bali alimuona kijana wa kijasusi , na alijiambia kweli wazee huficha mengi , kwani kwa miaka yote aliomfahamu Afande huyu hakuonyesha namna yoyote ile ya kujua kile kilichokuwa kikiendelea.
“Asante sana Afande kwa kunifumbua macho , nadhani leo ndio naamini nguvu yenu ndani ya taifa hili , siku zote nilikuwa nikisikia taarifa tu juu juu”Aliongea na kumfanya Mchina kutabasamu.
“Vizuri na nikusisitizie Taifa la Tanzania na Rwanda ni kama ndugu wanaoishi sehemu tofauti tofauti na mwisho wa siku tutakutana sehemu moja ambayo ndio chimbuko letu ,Kenya ,Uganda, Rwanda Burundi na baadhi ya mataifa mengine ambayo tunapakana nayo tulipaswa kuwa taifa moja lakini kutokana na watu waliofika ndani ya ukanda wetu na malengo yao ndio jambo ambalo linatufanya leo hii kutengenashiwa na majina , lakini licha ya hivyo lazima kuishi kwa kutosahau kwamba asili yetu wote ni moja , nakuambia meneno haya ili umshauri vyema Rafiki yako kwamba hatupaswi kuhujumiana”Aliongea Mzee huyu na kisha akanyamaza na kumpa ishara Tajiri kuondoka kwa siku hio.
“Nipeleke Maple hoteli”aliongea Tajiri Azizi maa baada ya kujibwaga kwenye gari , bwana huyu alionekana kuwa na hali tofauti na aliokuwa nayo wakati akiingia ndani ya jumba hili kwenye macho ya Dereva wake.
Ukweli siku hii ya jumapili kwaTajiri Azizi amegundua mambo mengi sana , unajua siku zote alikuwa akijihisi kama mtu ambaye alikuwa akimiliki taifa kutokana na kuwa Tajiri mkubwa , lakini leo hii mbele ya Mzee Kweka alijiona ni kapanya tu, mbele yake na kuna watu waliokuwa na nchi , waliokuwa wakijua kila jambo linalofanyika. Na leo hii ndipo alipoweza kuamini ni nini maana ya msingi wa taifa, siku zote aliamini mtu pekee ukiwa na pesa nyingi .taifa linaweza kua chini yake lakini leo hii Imani yake iligeuka na kuona kwamba unaweza ukawa Tajiri mkubwa sio kwamba una akili nyingi za kuwa Tajiri ndani ya taifa lakini ni kwasababu wenye nchi ndio wamekuruhusu kuwa Tajiri na kuneemeka.
Tajiei huyu alijikuta akikumbuka msemo wa Harold Wallace uliuokuwa ukisomeka hivi:
‘Then We Promote both sides of the issue as confusion Reigns ,with their eyes fixed on the issues ,they fail to see who is behind every Scene”
Hio ni moja wapo ya kauli Tajiri huyu alikuwa akiipenda san ana ilikuwa ikibeba mambo mengi sana , Dunia ye leo unaweza ukaona tukio zuri na baya kwa wakati mmoja , lakini ukijua nani yupo nyuma ya matukio hayo utashangaa , kwani utakuta mtu huyo huyo alietengeneza tukio zuri ndio huyo huyo aliesababisha tukio baya na hii ni kuwafanya Raia wasielewe ni nini kinaendelea ili macho yao yote kuwa katika matukio na sio ukweli uliokuwa nyuma ya matukio , ni matukio mangapi ndani ya dunia ya sasa yanatokea mazuri na mabaya lakini mwisho wake ukweli wa chanzo wa matukio hayo ukikosekana , hio ndio maana ya kauli ya Harold .
Tajiri Azizi alijikuta akiwa na mawazo, mpaka kufikia hapo aliamini kuna jambo kubwa ambalo huenda yeye na raisi Jeremy hawakua wakilijua ambalo lilitokea miaka mingi ya nyuma , kwani kitendo cha Mzee yule kufahamu kuwa hata kitendo chake alichofanya miaka ya nyuma kilikuwa kikifahamika alijikuta akichanganyikiwa.
“Jeremi vijana wangu wamenipa ripoti kutoka hospitalini”
“Wanasemaje?”
“Raheli kajifungua salama Watoto mapacha wa kufanana kama vipimo vilivyonyesha awali”
“Basi mpango uendelee kama tulivyopanga Azizi , nenda wewe mwenyewe kamchukue mtoto na kumleta Kenya , tuntaonana huko”
“Jeremy unauhakika hili jambo nu sahihi kufanya , tunamkoseha mtoto nafasi ya kuwa karibu na mama yake?”
“Azizi mbona hayo tushaongea tayari na tukakubaliana na hata Rahel mwenyewe , sistahili kukosa kila kitu kutoka kwa Rahel , nilimpigania kwa miaka mingi na nikakubali aolewe ndani ya familia ya Adebayo , lakini angalau sasa nipate kuitwa baba na mtoto akutoka kwenye tumbo la uzazi la mwanamke ninaempenda”
“Okey Jeremi, tukutane Kenya” ……
…………..
“Nakupenda sana Lorraine , popote utakapoishi ukiwa mbali na mimi mama yako utaishi ndani ya moyo wangu daima” Tajiri Azizi alikumbuka maneno ya Raheli miaka ya nyuma wakati akimchukua Lorraine kwenye mikono ya mama yake kabla ya kumsafirisha na hio ni mara tu ya Lorraine kunyonyeshwa kwa mara ya mwisho.
Tajiri huyu machozi ya Raheli hakuwahi kuyasahau katika Maisha yake yote , alikumbuka uchungu uliokuwa ukionekana kwenye macho ya Raheli kutenganishwa na mtoto wake.
“Bosi tushafika”Ni suati ambayo ilimgutusha Tajiri Azizi na kumfanya aangalie nje na kuona ni kweli walikuwa nje ya jengo la Maple hotel.
Huku nyuma ndani ya chumba cha mzee Kweka , alionekana akiwa amefumba macho yake kama mtu ambaye alikuwa akifanya ‘meditation’ , pembeni yake akisimama huyu mwanamke wa kpchina alikuwa akifhaamika kwa jina la Zhenzei.
“Camilius nadhani ni muda ya Roma kuitambua familia yake”Aliongea Mchina.
“Yeah ni kweli lakini kabla ya hatua hio kufikia lazima tumalizane na swala la Senga kwanza ,ndio mtu wa kwanza kutakiwa kufahamu kabla ya kujua mtoto wake Denisi yupo hai”
“Naungana na wewe, lakini swala hili halitomuathiri sana?”
“Vyovyote vile ni lazima autambue ukweli na mimi sitaki sana kuchelewesha swala hilo , napanga kumrithisha mjukuu wangu Roma kila kitu, ana tabia ambazo huwa zinanifurahisha sana”
“Kuhusu Denisi itakuwaje?”
“Denisi ataisambaratisha familia kama nikimuachia , unajua sisi familia yetu imejengwa kijeshi , Denisi ni mwanajeshi ila bado ni muoga. na uoga ni dalili kubwa ya udhaifu kama mwanajeshi, na siku zote wanaaokuzunguka hawatakutii ,tunahitaji ‘Charistmatic leader’ mfano wa Roma… Aaa yeah anaitwa Hades na upuuzi mwingine hahaha…”Aliongea mzee huyu na kwa mara ya kwanza alitoa kicheko cha kujiachia na kumfanya mchina huyu ambaye haikueleweka ana miaka mingapi bongo na yeye aungane kwa kucheka.
Ila nadhani maamuzi ulioyachukua miaka ile ni yakibusara juu ya Denisi?
“Ni kweli na sijutiii kwa kile nilichokifanya, ningemuacha Denisi na hali yake akarudi nchini angekuwa mfu mpaka sasa hivi, halafu Zenzhei nadhani ni muda wa kumtambua Denisi kama Roma a.k.a Hades sasa. maana Denisi ni jina tayari ambalo lipo ndani ya familia”
“Naunga mkono hoja Camilius”
“Usijali Zhenzei , siku moja nitategeneza nafasi upambane na Hades kupima uwezo wako kimapigano uliojifunza kwamiaka mingi”
“Camilius natamani siku hio ifike,nina hamu ya kumshikisha Adabu Hades na aache kujiamini”
“Hahahahaha…. Hahahaha… sidhani kama litatokea ,Usisahau kuna wanaomuiota god.. hahaha”Aliongea mzee huyu na kicheko chake cha kizee.
“Ila naamini utatokeamtifuano mkubwa sana kati ya Denisi na Roma?”
“Naamini hivyo , Denisi na yeye anauwezo wa juu kimapigano pande zote za uchawi pamoja na kijeshi lakini siku atakaposhuhudia hamuwezi kaka yake atakata tamaa na kukubaliana na mimi”
SEHEMU YA 144
Denisi ndani ya madakika kadhaa alikuwa ndani ya hoteli Rotoana , bwana huyu tofauti kati yake na Roma licha ya kuwa ndugu wa damu , ilikuwa ni Sura , Denisi alikuwa na Sura ya kuwachanganya wanawake ukijumlisha na muoneaknao wake wa kimazoezi, lakini pia Denisi Pesa ilikuwa imemkubali , sio kama Roma ambaye ana mabidlioni ya hela lakini bado alionekana kama mkulima wa Tumbaku.
Wakati Denisi anaingia ndani ya hili eneo la mapokezi moja kwa moja aliweza kumuona Sophia ambaye alionekana kumsubiria na bwana huyu baada ya kumuona mwanamke huyo mrembo aliishia kutabasamu na kumsogelea huku akitaka kumkumbatia Sophia lakini mrembo huyo alimkwepa.
“Tukaongelee sehemu ya mgahawani , nimetokea nyumbani bila kunywa chai”aliongea Sophia kwa sauti yake nyoroiro, Sophia alikuwa akionekana mrembo kweli, mchanganyiko wa makabila kati ya Mwarabu na mbongo ulikuwa umekumbali kwa asilimia kubwa sana na kuonekana mrembo mno na kila mtu aliekuwa akimwangalia ndani ya eneo hili la hotelini , alimtamani.
Denisi alitoa tabasamu la uchungu huku akiongozana na Sophia , bwana huyu aliishia kula kwa macho kamtingishiko ka Sophia ambaye licha ya kuvalia Traucksuti lakini bado umbo lake lilijichora vizuri.
“Umesema una jambo la kuniambia , nataka unieleze sasa hivi Denisi sitaki kukaa muda mrefu sister ni mgonjwa”
“Come on Sophie , yaani unaongea na mimi kama vile ndio mara yetu ya kukutana , ushasahau kuwa mimi na wewe ni marafiki wa muda mrefu?”
“Denisi nakubali kwamba sisi ni marafiki wa muda mrefu , lakini uliharibu ulipo anza kunitongoza wakati nilikuchukulia kama kaka yangu tu ambaye ulikuwa bega kwa bega na mimi nilipojiunga na mafunzo ya Kung Fu , usisahau kuwa tabia yako ndio imenisababishia kuacha mafunzo?”
“Sophie kama nikunichukia unichukie tu na nadhani utanichukia milele kwasababu siwezi kuwa mnafiki mbele yako , nakupenda na ndio maana nakuambia nakupenda , hizo ndio hisia zangu kwanini niewe mnafiki , kwanini unakasirika kwa mimi kukupenda?”
“Sijakataa wewe kunipenda hata siku moja , lakini tabia yako ya kibinafsi ndio iliokuwa ikinifanya intake kukaa na wewe mbali , umenipenda sawa lakini vipi kuhusu mimi, vipi kuhusu hisia zangu?”.
“Kipindi kile sikuwa nikifikiria vizuri ndio maana , nilikuwa mbinafsi ndio maana nilikuwa nikikulazimisha kuwa na mahusiano na mimi”
“Kwahio sasa hivi imekuwaje?”
“Sasa hivi nakupenda lakini naziheshimu hisia zako hivyo usinikimbie Sopia tena ,sawa mama..”
“Denisi nenda moja kwa moja kwanini unataka kuonana na mimi ,sidhani tupo hapa kuambiana mambo yaliopita?”
Denisi alijikuta hata kule kujiamini kukipotea , ukweli ni kwamba Sophia na yeye walikutana kitambo sana tokea Sophia akiwa nchini China akijifunza mafunzo ya Kung Fu ,na Denisi baada ya kugundua kuwa Sophia ni mtanzania ndio ukaribu wao ulianza , lakini sasa kadri Denisi alivyoishi na Sophia ndio alivyozidi kuvutiwa na urembo wake na kutamani kumvua nguo na kujilia tunda , lakini kwa upande wa Sophie hakuwa hata na mawazo hayo , Sophiealikuwa akimchukulia Denisi kama kaka na rafiki wa kawaida tu waliokutana ndani ya Tempo kwa ajili ya mafunzo ya kimapigano. , lakini urafiki wao ulikoma pale Denisi alivyomalizmisha Sophie wafanye mapenzi kabla hata ya kutongozana kitendo ambacho kikamkasirisha sana mrembo Sophia na kufanya wawili hao wasiongee kwa Zaidi ya wiki mbili , lakini mwishowe Sophia alimsamehe Denisi na wakaendelea kuwa marafiki lakini Denisi hakutaka kuishia hapo tu aliendelea kumnunulia zawadi ndogo ndogo Sophia kila aendapo mjini , vimaua maua , nguo za ndani, na matendo hayo yote Sophia aliona Denisi hajaacha tabia yake na kwa upande wake hakuwa na hisia nae hata kidogo.
“Denisi sina mpango wa kuwa na wewe kwenye mahusiano , yaani siwezi nakupenda kama Rafiki , kama kaka yangu hivyo naomba uache mambo yako”aliongea Sophia siku moja akimrudishia Denisi zawadi zake za pichu wakiwa ndani ya Tembo mbele ya wanafuzi wenzake na kufanya Denisi awe na aibu sana, lakini kwa Denisi hakujali aliendelea na kulazimisha , aliamini wanawake mwanzonni ni wagumu , hasa kwa Sophia ambaye alikuwa bikra bado, hivyo aliamini muda ukifika atakubali , lakini siku alikuja kuishia kusikia Sophia karudi Japani baada ya baba yake kuteuliwa kuwa balozi huko na hapo ndio waliishia kuwasiliana kwa njia za simu huku Denisi akiendelea kupiga simu kumshawishi Sophia.
“Sophie nimeshangazwa na wewe kurudi Tanzania ghalfla na kwenda kuishi na Edna na ndio maana niliihitaji tuongee nataka nijue kwanini unaishi kule?”
“Ni maamuzi yangu Denisi na ya familia yetu ka ujumla”
“Familia!?”
“Ndio naandaliwa kuoelewa na Roma”Aliongea Sophie bila kujiuma uma na kumfanya Denisi kutoa macho.
“Unamaanisha nin kuolewa na Roma , licha ya kwamba najua wewe na Edna sio ndugu wa Damu lakini kwako yule ni kama dada yako , kwanini untaka kuolewa na Roma wakati tayari ameshaoa?”Aliongea Denisi huku sura ya hasira haikujificha.
“Denisi sitaki kukuficha ila ukweli mimi nampenda sana Roma, na nipo tayari kuoelewa kama mke wa pili na leo hii nimekuja kukuambia kile ninachojisikia moyoni mwangu kwa mara ya kwanza ili kama nikutafuta mwanamke mwingine ufanye hivyo ,Roma atakuja kuwa mume nwangu kwa namna yoyote ile kwasababu nampenda”.
Denisi hakuweza kuamini maneno ya Sophia mara moja , yaani jamaa huyu alikuwa akichemka kwa hasira na kujiambia kwa wakati mmoja Roma ananini mpaka kupendwa na wanawake wote ambaye yeye ashawahi kuwapenda kwenye Maisha yake , mara ya kwanza ni Edna na sasa Sophia , bwana huyu alijikuta akimchukia Roma maradufu na kuendelea kumuua kwenye mawazo yake.
“Denisi nadhani baada ya leo utaacha kunisumbua m kwaheri”Aliongea Sophia ambaye hakujali hata chakula kilichokuwa mbele yake kwamba hajakigusa hata kidogo.
“Damn you Roma , sitokuacha hai haiwezekani , wewe ni mchawi na lazima nikuue kwa mikono yangu yote”Aliongea Denisi huku akiwamgalia Sophia aliekuwa akitokomea upande wa pili akimuacha yeye kwenye mshanagao.
*******
Upande mwingine nchini Rwanda , alionekana mheshimiwa Jeremy akiwa ameshililia simu yake kubwa akiwa nje ya jengo la ikulu kwenye balconi , mzee huyu ni kama hakuwa akiamini kile ambacho alikuwa akikisikia upande wa pili.
“Jeremy hivyo ndio ilivyokuwa Rafiki yangu, siku zote tulidhania sisi ndio ambao tulikuwa tukijua kile kinachoendelea duniani , lakini ukweli ni kwamba sisi ndio ambao hatukua tukifahamu kinachoendelea , sisi ndio tupo gizani mpaka sasa hivi na lazima tutafute namna ya kutoka kwenye giza”
“Azizi hii habari ni kubwa sana kwangu kwa asubuhi hii ,imenishangaza na maneno yako yana maana kubwa , lakini bado Napata ukakasi”
“Ukakasi gani tena Jeremy wakati kila kitu kipo wazi?”
“Umesema wamekupatia karatasi za DNA tu lakini pia ukasema wanafahamu tukio la Lorraine nadhani hatupaswi kwnda kwenye hitimisho moja kwa moja kama walikuwa wakijua kile kinachoendelea , huenda hata wao wamefahamu hilo hapa majuzi tu”
“Kwahio unataka kumaanisha kuna watu ambao wamewapatia taarifa?”
“Ndio naamini hivyo , kama ni kweli walikuwa wanajua swala hilo wasingekaa kimmya miaka yote hio?”
“Kama mawazo yako ni sahihi kwanini ufikirie hivyo , sababu gani unayo?”
“Sijui kwasasa , ila naamini Kamau Kamau ana majibu yote juu ya hili , unakumbuka stori yao na Blandina miaka ya 98 ilivyokuwa?”
“Naelewa hio stori yao”
“Sasa unafikiri mpaka hapo Kamau alijuaje , lazima kuna mtu alimpatia tu taarifa na huyo ndio wa kuanza nae , lakini siwezi pia kuwapuuzia wazee wa Tanzania huenda maneno yao yapo sahihi , lakini pia huenda na Wazee wa Kenya au Uganda wapo wanajua hili, ngoja nijaribu kuwasiliana na Rasi Mjumaane nione ananiambia nini , nimefanya makosa siku zote kumpuuzia kwenye mipango yangu na kumuona kama mzee asie na mawazo mapana , huenda angerahishisha kazi yangu”aliongea Jeremy.
“Kazi kwako Jeremy , huu ndio muda wa kuongeza umakini Zaidi , na nafikiria hata Urusi wanacheza na akili yako tu muda wote”
“Ni kweli kabisa nadhani inawezekana kuwa hivyo , ila ngoja nifuatilie ila naaapa kwa majina yote kama Tanzania inahusika na tukio la Ndege na kutoniambia mpaka mwanangu Lorraine akaingia ndani ya ile ndege , hatutaelewana kabisa nitatumia ‘Resources’ zangu zote kuiparanganisha”Aliongea Jremy na kukata simu , alionekana kuwa na hasira mno sana mpaka wakati huo.
*******
Roma baada ya kutoka ndani ya jengo la hospitali ya Aghakhani moja kwa moja alinyoosha kwenda Jogoo na hio ni baada ya kuwasiliana na Profesa Clark juu ya kumuhitaji , alitaka kuangalia maendeleo ya Roma juu ya ugonjwa wake na ndio maana wakati siku ile wanaachana ndani ya hospitali ya Aghakani , Profesa alimuambia atampigia muda si mrefu akipata eneo sahihi kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya kina kujua ni nini kimebadilika tokea mara ya mwisho kumpima.
Dakika chache mbele Roma alikuwa akiingia eneo hili la Tegeta Jogoo na kwenda kuegesha gari yake mita kadhaa tokea mlango mkubwa wa kuingia hospitali na Chuo cha IMTU.
“Nipo hapa kwa ajili ya kuonana na Profesa Clark”Aliongea Roma baada ya kufika eneo la mapokezi na ajabu leo hii licha ya kuwa jumapili ni kwamba Hospitali ilikuwa wazi.
“Romaa…!!!”Kabla mtu wa mapokezi kujibu Roma aliitwa nyuma yake na sauri aliokuwa akiifahamu na kugeuka , alikuwa ni Profesa Clark akiwa kwenye koti la kidaktari na glovuzi mkononi.
Walikumbatiana kizungu na kumpigana mabusu huku Clark akiweka mikono yake juu asimguse Roma.
“Kuna sehemu ya kuweza kunipimia hapa?”
“Hiki ni chuo cha IMTU maana yake ni cha kimataifa na siku zote kinapata ufadhili mkubwa sana kutoka Uingereza na kuna maabara chini ya Ardhi yenye kila aina ya kifaa ninachohitaji kujua afya yako”Aliongea Clark kwa kingereza na kumfanya Roma kutabasamu na kuingia ndani ya eneo hili , ni kweli baada ya kushuka kwa Lift , Roma aliweza kushushudia Maabara kubwa ailiokuwa imejengwa kwa kisasa kabisa ikiwa na vyombo vikubwa tu kama CT Scan na vifaa vingine vya kisasa vyenye teknolojia kubwa kupangwa kimpangilio na kupendezesha sehemu hio.
“Nitaangalia kwanza picha ya ubongo wako na mahusiano yake ya taarifa zake mwilini hivyo inabidi uvue nguo zote uingie kwenye hio mashine”Aliongea Clark bila ya aibu, na Roma wala hakujali sana , alivua haraka haraka , mpaka boksa na kumfanya Clark aangalie dudu ya Roma.
“Mh! Imeongezeka ukubwa?”
“Acha utani iko vilevile” Aliongea Roma pasippo wasiwasi na kumfanya Clark atabasamu.
“Ndio maana mama hasahau mambo yako kila siku”Aliongea Clark huku akibonyeza bonyesha mashine iliokuwa mbele yake na ndani ya dakika chache ru kulichomoka kifaa kama kitanda kwenye mashine hio na Clark alimpa ishara Roma kulala kwenye hiko kitada na Roma alitii na ndani ya dakika chache tu kitanda kiliriudi ndani ya lijimashine hilo na Clark akafunga na kuzunga upande mwingine wa chumba, kilichokuwa na skirni kubwa.
“Ding! Initilizing Scaning, please press Pink Button to start”Mashine hio ilitoa sauti ndogo ya kike na Clark alibonyeza kitufe cha pinki na hapo hapo ubongo wa Roma ukaonekana wote kwenye Skrini , na kumfanya mrembo huyu kutoa macho baada ya dakika moja kupita , kuna jambo ambalo aliona na lilimshangaza.
ITAENDELEA IJUMAA
WATSAPP 0687151346 NICHEKI UPATE UTARTIBU WA KUIFATILIA KWA SPIDI YA 4G