Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Baada ya Iftar leo tunaendelea Inshallah
Daaah mkuu upo? maana tukikuita tukiwatag wana waje kwenye chama letu...kuna viumbe wanaluka nasi, so tunaona bora tukupe mikausho mikali maana kujibizana na wana sio mpango...

Dondosha vitu...
 
NDO MUDA HUU SHEKHE
Kama ww ni mwislam unafunga utakuwa unajua nin kinaendelea kwa mtu aliefunga! Hapo kuna kuswal magharibi, kisha kufuturu , ukimaliza tu swala ya insha ipo mlangon then tarawehe rakhaa 26! Be humble story ni baada ya tarawehe mkuu! Na nna imani singanojr anapitia hizo hatua za kiiman! Na hatatuacha yatima wa stor usiku wa leo! Tumpe muda aongee na Mwenyez muweza wa yote inshallah
 
SEHEMU YA 362.

Kwenye kampuni ni wengi walikuwa wakimfahamu Roma kama mume wa Edna , lakiini hata hivyo hawakushangaa sana uwepo wake, kwani yeye pia ni moja ya wafanyakazi wa ngazi ya juu wa kampuni , walichotegemea ni kutaka kusikia Roma alikuwa akitaka kuongea nini kwa kuingia kwa kuchelewa.

“Nilikuwa nikiwasikiliza kwa muda nikiwa nje ya mlango na maongezi yenu sijaona yakibeba suluhisho la maana juu ya swala hili , kwanini msitawanyike na Kwenda kufanya kazi zenu ili kusubiria mapambano ya kuikoa kampuni siku ya jumatatu? , kuhusu kazi ya kumjua muhuisika mnaonaje hio kazi nikaifanya mimi”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumwangalia huku chumba kikiwa kimya .

“Mpango wako wa kumpata muhusika ni upi?”Aliuliza Edna kwa sauti kavu.

“Wife , hebu kwanza acha kuniangalia na macho ya usiriasi kiasi hicho , unanifanya nikuogope”Aliongea Roma nbila hata ya aibu

“Tupo siriasi hapa , hii ni kampuni na tupo kwenye matatizo Director Roma”Aliongea Edna na kumfanya Roma kukuna kichwa na kisha kuangalia watu wote.

Ukweli Roma licha ya kwamba alijua mke wake yupo siriasi na kazi yake , swala la kumtoa Benadetha aliona hakuna namna ya kulifanikisha pasipo kwanza ya kumtambua muhusika mkuu , alichokifanya asubuhi kwanza ni kuwasiliana na Mage ili atumie upolisi wake kuhakikisha anakuwa na ukaribu na Benadetha huku yeye akimtafuta muhusika, huo ndio mpango wake.

“Sijajua namna ya kuanza uchunguzi wangu bado.. lakini si kuna Camera , kwanini tusianze kuangalia hizo kwenye ofisi ya Benadetha kujua kama kuna mtu aliingia na kugusa kiboksi cha kuhifadhia nyaraka tofauti na yeye ?”Aliongea Roma

“Director Roma nadhani haujafahamu kwamba kwenye ofisi zote za wakuu wa idara hakuna Camera inafungwa?, huo ni utaratibu wa kampuni ulioweka kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kibiashara yanakuwa siri kwa kila idara”Aliongea Nasra

“Director Roma , I highly suggest you consult your thought process before speaking”Aliongea Ernest Komwe kwa kingereza , mara nyingi vikao vyote vilikuwa vikifanyika kwa lugha ya kingereza kutokana na kwamba kuna baadhi ywa wafanyakazi sio watanzania, hivyo hata Roma alitumia Kingereza pia.

“Director Roma nashauri sana kuushirikisha ubongo wako kabla ya kuongea”Hilo ndio jibu ambalo alitoa Ernest

“Kama unafikiri nimekosea , je ni wazo gani lingine unashauri?”Aliuliza Roma.

“Mimi , natamani ningekuwa na wazo lakini kwa bahati mbaya unachoniuliza kipo nje ya fani yangu”Alijibu Ernest.

“Kama ni hivyo , unaonaje ukifunga bakuli lako, Wif.. Boss Edna kaa kwa kutulia kabisa nakuhakikishia ndani ya siku mbili nitakuwa nimemkamata muhusika, hivyo naomba umtoe polisi Benadetha kwani naamini kabisa hahusiki katika hili”Aliongea Roma na kufanya watu wote kuangaliana, kwa namna ambavyo Roma anamtetea Benadetha.

“Kikao hiki nakiahirisha kwa muda , kwanzia sasa kila mmoja arudi kwenye nafasi yake na kuangalia namna gani tunazuia hasara Zaidi , kuhusu Benadetha ataendelea kua chini ya uchunguzi”Aliongea Edna na wafanyakazi wote walisimama na kutawanyika huku akibakia Roma na Edna.

“Edna nakuahidi uchunguzi nitaukamilisha ndani ya siku mbili na nitamkamata muhusika , unaonaje ukimtoa Benadetha kituo cha polisi?”

“Roma nishafanya maamuzi Benadetha ataendelea kukaa polisi , labda nikueleze tu swala hili sio la kikampuni tu , bali ni kwa uchumi wa taifa pia , ushahidi unamfunga kwa sasa na ataendelea kukaa polisi , kama unataka kuendelea kufanya uchunguzi kwa upande wako , ni wewe ila maamuzi yangu ni ya mwisho”Aliongea Edna na kisha kukusanya vitu vyake.

“Edna unajua jinssi Benadehta alivyojitoa kwenye kampuni , kwanini unashindwa hata kumpa siku moja tu ili nithibitishe hahusiki”.Aliongea Roma na kumfanya Edna kusitisha alichokifanya na kumwangalia .

“Una jambo gani linaendelea na Benadetha, na yeye ni mwanamke wako?, hivi kabla ya kumfikiria Benadetha ushawaza najisikiaje muda huu , kwanini haupo upande wangu?”Aliongea Edna.

“Lakini kila mtu anamuona kama mtuhumiwa na namfahamu Benadetha kama mfanyakazi mzuri wa kampuni hii , unadhani akikosa mtu hata mmoja wa kumtetea atajisikiaje?”.

“Kwahio vipi kuhusu mimi , kila mtu anajua wewe ni mume wangu , lakini wewe kutwa kumtetea hahusiki ,nina umuhimu mdogo sana kwako mpaka kushindwa kusapoti maamuzi yangu?”Aliongea .

“Kwahio unaona wivu nikikuambia kwamba hahusiki?”Aliuliza Roma

“Unaweza kufikiria unachotaka Roma , kwanza una hela na una nguvu kubwa , kwanini usiende ukamtoa polisi huku ukiendelea na uchunguzi, lakini nikutahadharishe tu jambo hili ni kwa ustawi wa kampuni , hivyo usije ukatumia hela zako kutatua hili tatizo , nahitaji kujua nani kahusikana kama hakuna Ushahidi Benadetha ataendelea kuwa polisi , nina kazi nyingi sitaki kujibishana na wewe”Aliongea Edna akiwa amekasirika na Roma hakutaka kumjibu Zaidi Edna, aliona asiruhusu hisia kumpanda na kufikiria namna ya kumsaidia Benadetha, ijapokuwa jana alipigwa mikwala na mwanaume aliejitambulisha kama baba wa Benadetha lakini kumsaidia Benadetha sio kwasababu ni kumuogopa mtu , bali ilikuwa ni wajibu wake kufanya hivyo , kwani Benadetha alimuona kama msichana mwenye roho nzuri.

Roma mtu wake wa kwanza ambaye alimhisi kama muhusika ni Ernest Komwe , kwanza kabisa ndio aliekuwa akionekana kinara cha kusema Benadetha anahusika , lakini pia kabla ya kuja hapo alijairibu kufanya uchunguzi wake na kusikia mara nyingi Ernest komwe alikuwa karibu sana na Benadetha hata kuingia ofisini kwake mara kwa mara.

Roma kwakua hakuwa sana mtaalamu na maswala ya kiuchunguzi ilibidi kuwapigia wanajeshi wake.

“You mejest Pluto , ar you calling in regard of what is happening in Vexto ?”

“Yes! I need you to stop by Vexto hq right now , I require your professional wisdom to clarify some of my doubts”Aliongea Roma akimaanisha kwamba anamhitaji Diego kufika kwenye kampuni ili kumpa ushauri wa kitaalamu ili kuweza kuthibitisha wasiwasi wake.

“Your Majest Pluto Forgive me , I am not adept in crime scene investigation but I will assign one of our best to pay you a visit now”

“Utanisamehe mfalme Pluto siko vizurri sana kwenye maswala ya uchunguzi wa kesi , ila nitampa kazi moja ya vijana wabobevu kuja hapo”Aliongea Diego.

“Chagua yoyote na aje muda huu”

“Got it”

Baada ya nusu saa hivi aliweza kufika mwanadada wa kizungu, mwanadada mrembo kiasi aliekuwa amebeba mkoba mweusi , akiwa amevalia suti iliomkaa vyema mwilini , alionekana kama ajenti wa CIA kutokana na kujiamini kwake na aliweza kukutana na Roma ambaye alikuwa akimsubiri kwenye korido floor za chini.

“Mfalme Pluto , kabla sijaanza kazi yangu nahitaji kujua itifaki za ulinzi zinavyofanya kazi ndani ya jengo hili”Aliongea yule mwanadada kwa kingereza baada ya kusalimiana na Roma , alikuwa akifahamika kwa jina la Fanny.

“Kwenye korido zote na ofisi za wakuu wa idala hakuna Camera za ulinzi, lakini kumbi zote za mikutano kuna kamera kila kwenye kona ,kama uchunguzi anzia kuangalia kwa watu walioingia na kutoka kabla ya tukio kwenye ofisi ya muhusika”Aliongea Roma na mwanadada huyo aliitikia kwa heshima.

“But Fanny why are you so coiled up around me , am I that terrifying to you?”Aliuliza Roma mara baada ya Fanny kumtegea Roma kuingia kwenye Lift , alikuwa akikosa kujiamini na muda huu walikuwa wakifanya safari ya Kwenda idara ya masoko na uhusiano.Sasa Roma aliuuliza kwanini anaonekana kukosa kujiamini mbele yake , kwani yeye anatisha?’

“No , definitely not , your Majest just that its my first time meeting you alone and I would never want to fail you”

“Hapana Hakika Hapana , ni kwamba mfalme imekuwa siku yangu ya kwanza kukutana na wewe peke yangu , hivyo naogopa nisije kukufelisha”

“All you need to do is support my claim that the safe was manipulated or cracked open by a third party , I’ll handle the rest myself”

“Uanchotakiwa ni kusaidia kujua kama Safe ilichokonolewa au kuvunjwa na mtu yoyote na kitakachobakia nitajua mwenyewe”

“Understood , I know exactly what to do”Aliongea Fany akimaanisha kwamba anajua cha kufanya na ndani ya dakika kama tatu tu waliweza kuingia upande wa idara ya PR. Wafanyakazi baadhi walikuwepo , ikiwemo Recho na wengine ambao Roma hakuwatambua na nafasi ya Benadetha ilipewa mmoja ya mfanyakazi wa kike ambaye hakuwa akimtambua na ndio huyo ambaye aliwafungulia ofisi kuingia ndani.

Baadhi ya wafanyakazi walishangazwa na uwepo wa mzungu huo ambaye ametambulishwa kufika hapo kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Fanny alifungua mkoba wake na kisha akatoa tarakishi mpakato yake na kisha akaiweka mezani karibu na boksi la kuhifadhia nyaraka hizo na kisha akatoa nyaya flani zilizounganishwa mwishoni na viachuma vya rangi ya shaba na akaanza ufanya mautundu yake , huku akichezesha password za boksi hilo.

Roma baada ya kuona Fanny atachukua muda , yeye alitoka na kuelekea chumba cha kuongozea kamera na aliweza kuwapa maagizo waongozaji wa kamera hizo kuangalia matukio ya siku kadhaa nje ya ofisi ya Benadetha.

Roma baada ya kukagua sana hatimae aliweza kuona pia sura ya Ernest Komwe ikiiingia na kutoka ndani ya ofisi ya Benadetha siku ya ijumaa, lakini kilichomfanya Roma kushangaa ni kwamba alionekana kuingia kwa muda mchache sana na kutoka na ilionekana pia Benadetha hakuwepo ofisini. Roma alijuliza kama ni yeye kahusika atakuwa amewezaje kufungua boksi hilo la usalama ndani ya ofisi ya Benadetha bila kuwa na nywira , baada ya kuona hana majibu anayotaka alitoka ndani ya chumba hicho na kurejea.

Roma baada ya kuingia ndani ya ofisi alimkuta Fanny akifuta jasho, ilionekana ni kazi kubwa sana aliokuwa amefanya.

“Mfalme Pluto nisamehe kwa kuchelewa kukamilisha kazi , ugumu wa kufungua hili sanduku la usalama , unazidi teknolojia zinazotumiwa kufunga maboksi ya benki , inashangaza teknolojjia hii kutumika ndani ya kampuni…”

“Kwanini unasema hivyo?”

“Mfumo wake wa ulinzi umetengenezwa na kampuni maarufu ya Ulaya ifahamikayo kwa jina la Casa, ni mfumo wa mizunguko mingi ya moja kwa moja(Mult turn free range lock) kwa maana hio kwa uchaguzi wa mtumiaji lazima aweze kuweka mpangilio wa kimuunganiko wa namba usiofanana na hiki kizungushio chake kinaenda kwanzia namba sifuri mpaka tisini na tisa kwa maana ya kwamba kuna muunganiko wa Zaidi ya kodi mia moja kwa kila mzunguko, kwa urahisi Zaidi ni kwamba ili mtu kuweza kuotea namna ya kufungua bila password lazima abunie namba moja ya kodi kati ya namba milioni moja”

“Kwahio unachotaka kumaanisha ni..”

“Ili mtu kuweza kuchokonoa na ifunguke basi kwanza kabisa unatakiwa kuwa na mfumo wa calculator wenye teknolojia kubwa ili kuweza kukadilia muunganiko wa hizi kodi na wakati huo huo hiki kizungushio lazima kigeuke upande mwingine” hapo anamaanisha kwamba makadirio ya nywira yanatakiwa kufanyika Kwenda kinyume nyume , anachojaribu kuelezea ni kwamba ni ngumu sana kwa mtu kuweza kuiba faili ndani ya hilo sanduku pasipo ya kuwa na password.

“Ukiachana na meaelezo yako ya kitaalamu ,je itamchukua mbobezi wa hali ya juu muda gani kuweza kuiba vitu kwenye sanduku kama hili?”

“Masaa manne au Zaidi , lakini kwa uelewa wangu watu wenye uwezo huo wapo watano tu ndani ya dunia hii ambao waliweza kuripotiwa na Casa , hivyo wa mtu wa kawaida hata apewe wiki nzima hawezi kuiba kitu “

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba ili kufungua lazima uwe na password na kwa mtu ambaye hana hakuna uwezekano wa kufungua?”

“Ndio Mfalme” Baada ya kujibiwa hivyo , ilibidi Roma aanze kutafuta kila kona ya chumba

“Your Majesty , are you searching for micro Camera?”

“Mfalme Pluto je unatafuta camera ndogo

“You guessed it , the only othe possibility of this happening is if our thief was watching the safe be unlocked”

“Umepatia , njia pekee iliobaki ni uwezekano wa haya yote kuwezekana kama tu mwizi wetu alikuwa akiangalia namna sanduku linavyofunguliwa”Aliijibu Roma na kumfanya Fanny kutabasamu kidogo.

“Naomba unisamehe mfalme Pluto kwa kutokukumbia ,ukweli niliscan chumba kizima na sijaona kitu chochote ambacho kinaweza kutumika kama Camera”

“Nini.!”Roma alijikuta akishangaa huku akihema, ukweli aliamini huenda kuna Camera yoyote ambayo imefungwa kwa siri ndani ya hio ofisi, lakini kumbe Fanny ashafanya tayari ukaguzi , aliona ni kweli mtu alieletewa yuko vizuri kutokana na alivyobobea katika kazi yake

“Naomba unisamehe mfalme , sijakusaidia chochote”Aliongea huku akiinamisha kichwa chake chini, ilikuwa ni ngumu sana kuona mzungu kama huuyo kumnyenyekea Roma tena ndani ya Tanzania.

“Usiwe na wasiwasi , umefanya kadri ya uwezo wako , kwasasa unaaweza kurudi , mueleze Diego kukamilisha kwa haraka nilichomuelezea jana”Aliongea Roma na wakaagana.

Wakati huo huo Roma akiwaza ni hatua gani aichukue kwenye uchunguzi wake , simu yake ilianza kuita na alaivyoitoa ni namba iliompigia jana, ilibidi aipokee tu.

“Najua mzee ni mwenye hasira , lakini nafanya kila linalowekezaka kumsaidia mtoto wako”Aliongea Roma.

“Acha kuongea ujinga, Mr Roma nina Habari za kutosha kuhusu wewe ndio maana nataka umtoe mtoto wangu polisi , kama nilioyasikia ni uongo basi nilete kikosi changu”

“Mzee kwanza kabisa punguza jazba , pili siktaki vitisho , tatu kumtoa mtoto wako polisi kibabe sio suluhisho , ninachofanya sasa hivi ni kuthibitisha mwanao hahusiki katika hili, hilo ndio lengo , kama unataka Benadetha kuwa mhalifu basi fanya unachotaka”

“Okey nakupa siku moja tu uwe umekamilisha , la sivyo nitaanza na mkeo” na Roma ile anataka kumuuliza mzee huyo kwanza ni nani na vitisho vyeka simu ilikatwa , lakini ile anawaza simu ilianza kuita tena na jina kwenye simu lilionekana ni Rose.

“Hubby kuna nini kinaendelea, Boss wa kundi la ZoaZoa amenipigia simu na ananipa vitisho”Aliongea Rose.

“Boss wa ZoaZoa ndio nani?”

“Anafahamika kwa jila la Samweli Nguluma ni tajiri maarufu ndani ya Kahama, ndio mmiliki wa kundi la uuzaji wa madawa ya kulevya katika mipaka ya Zambia na Congo , kundi lake linafahamika kwa jina la ZoaZoa, inasemekana ni moja ya wafadhili wakubwa ADF kundi la magaidi ndani ya Congo, ananitishia usipomtoa mwanae polisi ataanza na mimi”Aliongea Rose na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli , aliona ndio maana mzee huyo alikuwa akijiamini kumtishia Maisha kumbe alikuwa mhalifu.

Roma ilibidi amtulize kwanza Rose ili kuendelea na uchunguzi wake , hakutaka kujifikirisha kuhusu Samweli Nguluma , kwanza kabisa hakuwa akihofia vitisho vyake.

Roma baada ya kutulia ndani ya ofisi hio akiwa anajiuliza maswali ya kipi ameshindwa kunasa kumuwezesha kwenye uchugnzi wake , kuna jambo lilimjia akilini na hapo hapo alitoa simu yake na akapiga Kwenda kwa Edna.

“Umepata nini?”

“Nataka kujua kati ya taarifa zilizoibiwa ni muda gani ziliandaliwa lakini pia ni kopi ngapi mnazo?”Aliongea Roma.





SEHEMU YA 363.

“Kwaasababu nyaraka zote ni za kimipango ya kampuni tulianza kuziandaa kwanzia mwezi wa sita mwanzoni na za hivi karibuni tulimaliza mwezi huu wa kumi mwanzoni , watu wawili tu ndani ya kampuni mimi na Benadetha ndio wenye kopi, ijapokuwa pia baadhi ya wafanyakazi wengine wa idara walikuwepo kwenye vikao wakati wa kuandaa , lakini katika uundaji wa kopi hawahusiki na pia kopi zote huwa hazihifadhiwi katika mfumo wa kompyuta bali ni kwa nakala ngumu , lakini zinazosambaa mtandaoni zipo kwenye mfumo wa komputa lakini zote ni za kwetu, vipi kuna ulichogundua?”Aliuliza Edna mwishoni.

“Vipi kuhusu taarifa za wiki mbili zilizopita , nimeona pia zenyewe zipo mtandaoni?”

“Mbona unaongea kama unanishuku mimi ndio nimezisambaza mtandaoni , lakini upo sahihi hata mimi ninazo hizo nyaraka , hivyo nisahihi kusema na mimi ni muhusika lakini pia sio kwamba nakosa nia ya kufanya hivyo naweza kufanya pia , Roma uko sahihi kunishuku na mimi”Aliongea Edna na sauti yake iliojaa kinyongo..

“Edna huu sio muda wa maneno hayo , asiliamia tisini zote za hisa ni zako kwenye kampuni . unawezaje kuvujisha taarifa upate hasara , sio kama nakushuku ila nafanya uchunguzi kupata suluhisho , najua unahisi labda natembea na Benadetha lakini hata kama iwe kweli huwezi kumsingizia Benadetha , mke wangu wewe ni mwanamke unaelinda heshima yako siku zote”Aliongea Roma na kimya kigogo upande wa Edna.

“Nina hisa asilimia hamsini tu za kampuni mpaka sasa”

“Unamaanisha nini , haiwezekani kushuka kwa hisa ukapoteza hisa zote hivyo”

“Mwezi uliopita niliziuza ili kujipanua Zaidi kibiashara ukizingatia na ujio wa malighafi mpya , lakini pia nilifanya uwekezaji kwenye maswala ya Recreation, hivyo nilihitaji pesa , lakini pia nililipa hela zote nilizokopa kutoka kwake kwenye benki ya Swiss , nilichukua maamuzi hayo baada ya hisa za kampuni kupanda kwa kiasi kikubwa , lakini hata hivyo niliona haiajlishi kiasi ninachomiliki kwakua mimi ndio ninaongoza kampuni”

“Hakukua na ulazima wa kulipa hela uliochukua benki ya Swiss , kwani Meneja wa benki hakukuelezea , kulikuwa na haja gani ya kujibebesha deni, kama unashida na hela wewe niambie mume wangu nataka pesa muda wowote , haikuwa na ulazima kuuza hisa zako”

“Mhmh , unaongea kama vile mimi sina hela zangu , kwanini niombe hela zako wakati nina zangu ”Aliongea Edna huku sauti yake ikioneysha kama hakupendezwa na kuambiwa aombe pesa .

“Kwahio ulifikiria nitakudai , unafikiria najali sana kuhusu pesa mimi , haya sasa una hisa asilimia hamsini za kampuni , vipi kama kuna mtu anafanya vita na wewe na akanunua hamsini zilizobaki?”

“Unafikiri mimi ni Mungu mpaka kujua kampuni itaingia kwenye matatizo , mimi ni CEO wa makampuni tu , kuna wengine pia waliopo kwenye nafasi kama yangu kwa mafano boss wa Amazoni anamiliki asilimia chache tu , mimi kushikilia hisa asilimia hamsini , yenyewe ni kiwango kikubwa sana “

“Okey haina haja ya kubishana sasa hivi , ninachotaka kufahamu kama sijakosea ni Monica peke yake anayehusika kutoa photocopy za hizo nyaraka peke yake , si ndio?”

“Unahisi Monica kahusika?”

“Ninachotaka kufahamu ni wapi zipo mashine zinazotumika kutolea photocopy”

“Katika ofisi yake , lakini hilo haliwezekanai kwani wakati alipotoa photocopy nilimsimamia na nikaondoka nazo, hivyo kama kuna kitu alifanya ningefahamu”

“Okey swali la mwisho hizo kopi orijino bado zipo kwenye hili sanduku ndani ya ofisi ya Benadetha?”

“Umeweza kuifungua?”

“Siajafanikiwa ninachouliza ni kama hazipo au zipo?”

“Zipo ndio hazijatolewa , kama amehusika basi ni kwa njia ya kuzikopi”Aliongea Edna.

“Basi mpaka hapo kila kitu kinajielezea , Monica hakugusa kabisa nyaraka hizo kwa makusudi kabisa , ila bila kujua amemsaidia mtu ambaye amehusika na kuvuja kwake”Aliongea Roma , lakini kabla tu hajamaliza , alisikia kishindo upande wa pili wa simu.

“Edna , Edna unanisikiliza , Babe unanifanya nakosa amani”Aliongea Roma lakini hakukuwa na majibu kabisa na Roma alihisi kuna tatizo huenda limemtokea Edna na hataka sana alitoka kwenye ofisi ya Benadetha na hakutumia lift bali alitumia ngazi na alitembea mara mbili tu alipotea na kuja kutokezea kwenye floor ya ofisi ya Edna.

Na ile anafika alikutana na Monica pia ambaye alikuwa akitaka kuingia kwenye ofisi ya Edna na kabla hawajasalimian Roma alishampita na kuingia ndani ya ofisi ya Edna.

Roma ile anazama ndani alichokishudia kilishitua mapigo yake ya moyo , Edna alionekana kupoteza fahamu akiwa amedondoka kwenye kapeti chini mbele ya meza yake huku akiwa ameshikilia simu.

Upande wa Monica na yeye alifika na alijikuta akipatwa na mshituko mara baada ya kushuhhudia Edna amelala hajitambui.

Roma kwanza alijituliza na kisha akachuchumaa na kumshika Edna mkono na akafumba macho , alikuwa akijaribu kuhamisha nishati kutoka kwenye mwili wake Kwenda kwa Edna wakati huo huo akijaribu kupima mapigo ya moyo kujua ni nini kimempata Edna na ndani ya dakika moja tu aliweza kugundua mwili wa Edna una sumu ndani yake , kwa maana ya kwamba inawezekana kuna kitu cha sumu amekula , alijikuta hasira zikimjaa mara moja, na Roma kwa jinsi alivyogundua aliamini kama sumu hio itaedelea kubakia mwilini basi itamsababishia Edna Saratani ya ini

“Nini kimemtokea jamani Boss..”Aliongea kwa wasiwasi Monica lakini Roma hakumjali , alitumiwa uwezo wake wa kijini kuhamisha nguvu ambavyo ingemuweka Edna sawa kwa muda na kisha akamgeukia Monica.

“Vipi Edna kuna kitu chochote amekula ndani ya madakika haya?”

“Hapana , ila nilimtengea kahawa muda si mrefu”Aliongea kwa wasiwasi

“Umetengeneza wewe mwenywe au kuna mtu mweingine kategeneneza?”

“Hapana Director , sijamuwekea sumu , hii ni kawada ambayo mara nyingi nilikuwa nikimtegenezea kutokana na kuipenda sana”Alijibu na kumfanya Roma kufikiria kidogo.

“Nitamuagiza mtu kuja kufanya uchunguzi kwenye ofisi yako na utampa ushirikiano kwa kila kitu , lakini pia utampatia kikombe cha kahawa ambacho Edna alitumia , kama mtu yoyote atauliza Edna yuko wapi utawaambia kwamba ameondoka na hajisikii vizuri , unaweza kwenda kuendelea na majukumu yako”Aliongea Roma

Zamani Monica alikuwa akimdharau Roma , lakini siku hizi za karibuni alikuwa akimuogopa kama Edna tu , hivyo alitingisha kichwa na kisha akatoka huku akiwa na machozi.

Roma alimbeba Edna kama mtoto na kisha akatoka nae , alitumia ngazi kushuka mpaka eneo la maegesho ya magari pasipo ya kuonekana na mfanyakazi yoyote wa kampuni na baada ya kumuingiza Edna kwenye gari aliliondoka kuelekea hospitalini.

Wakati akiwa njiani , aliwasiliana na Diego na kumuagiza kwamba aagize watu Kwenda ofisini kwa Edna kufanya uchunguzi na kuchukua ushaihidi wa sumu , huku pia akimuelezea Diego kuendelea na kutafuta taarifa zinazohusina na Ernest Komwe , kwanzia wazazi wake na kila kitu kinachomuhusu , lakini wakati huo huo akimpa maagizo ya kuendelea kumfatilia bwana huyo kwa kila nachofanya kuanzia watu anaokutana nao na sehemu alipo kwa muda huo.

Dakika chache tu aliweza kufika hospitalini na alimtoa Edna na kumuingiza ndani na madaktari walipotaka kumhudumia aliwakataza na kuwaambia anataka chumba cha VIP tu na matibabu anayajua yeye mwenyewe , Roma hakutaka kabisa kuwaamini madaktari kutokana na hali ya Edna , hivyo aliona kazi yote afanye yeye mwenyewe.

Baada ya kukabidhiwa wodi , na kumlaza Edna kitandani alianza kukusanya uwezo wake wote wa kijini , Roma hakuona haja ya kutumia damu yake kumponyesha Edna , kwani sumu iliokuwa mwilini ilikuwa ya kawaida hivyo alitumia kutibu kwa kutamka maneno kwa lugha anayoelewa yeye alikuwa kama waumini wanao nena kwa lugha na kila alivyokuwa akiongea mikono yake ilitoa moshi mfani hivi mweupe kama wingu ambao uliingia moja kwa moja kwenye mkono wa Edna , alifanya kitendo hicho kwa kurudia rudia , kuanzia tumboni mpaka kwenye masikio na ile anamaliza alimuinamisha Edna sakafuni na palepale akatema damu huku akiwa hajitambui vilevile , ilionekana ni kama alitegemea hivyo alimfuta na kisha akamlaza chini na kisha akaunganisha lipsi zake za mdomo na za Edna na akaanza kufosi hewa ya oksijeni kuingia ndani ya mwili wake kwa taktibani dakika tano mpaka alipomalizza na kisha kuketi huku akimwangalia Edna.

Roma alijiambia usalama wa Edna ni muhimu Zaidi kuliko kampuni , hivyo kumtoa kule ilikuwa ni kumsaidia.

Dakika tano nyingine Edna alionekana kurejewa na fahamu na alianza kumwangalia Roma na kuangalia mazingira na alitambua alikuwa hospitalini na alianza pia kukumbuka kilichomtokea.

“Kampuni… , Kwenye kampuni kunaendelea nini?”Aliuliza Edna kwa wasiwasi.

“Huna kitu kingine cha kufikiria Zaidi ya kampuni , hujui kufikiria afya yako kwanza kwanini upo hapa na nini kimetokea, Edna hii tabia yako sio taaluma bali ni upumbavu” Lakini Edna hakujibu.

“Kama ningejua ungeuliza kampuni mara baada ya kuamka , nisingekusaidia kabisa kukuamsha , ningeacha kwamba kampuni ifilisike ndio nikuamshe , huenda pia ingesaidia ukawa mama wa nyumbani na sio muda wote kufanya kazi zako pasipo ya kujali muda , umeolewa lakini unafanya kazi mchana na usiku , watu hata wakisikia tabia yako watadhani labda nyumbani na tunakunyanyasa , Unajua kwamba ulikuwa umewekewa sumu wewe , kama nisingekuwa karibu huenda mwili wako ungepata Cancerr, unajua hilo?”Roma aliona amfokee kwanza mgonjwa ili akili imkae sawa na kweli Roma alikuwa amekasirika kwani maneno yake hayakuwa na utani hata kidogo na aliendelea kufoka atakavyo , alitema nyongo kwa muda , lakini Edna aliekuwa akimwangalia aliishia kutabasamu

“Unatabasamu , unaona haya yanayokutokea mazuri sio, ngoja nikuambie haijalishi unanichukuliaje lakini mimi sijali mtu yoyote kwenye kampuni , hata kama kampuni ifilisike siamini kama Maisha yao hayawezi kuendelea bila wewe kiasi kwamba muda wote uwafikirie”

“Benadetha yupo polisi na wewe upo hapa unanifokea hufikirii saivi anahali gani , hauna wasiwasi juu yake”

“Nina wasiwasi ndio lakini unatakiwa kujua kila mtu ana vipaumbele vyake “

“Okey nishakuwa sawa , nataka nirudi kazini”Aliongea Edna na kumfanya Roma kukunja sura.

“Edna , Edna hivi unajua nilikuwa na wasiwasi kiasi gani juu yako , nimeacha kila kitu kwa ajili yako ili nifanikishe kutoa sumu kwenye mwili wako , kama yakutokea yashatokea tayari na sio kwamba kuwepo kwako kwa kampuni kunaweza kufanikisha kila kitu mara moja , Hivi unataka nitoe moyo wangu nje uone ninachojisikia muda huu Eh?”Roma alionekana leo kuwa sio wa kawaida kabisa mbele ya mke wake.
 
SEHEMU YA 364.

Harufu iliofifia ya ‘Sanitizer’ ndani ya wodi hio ilifurahisha pua zao kwa kiasi fulani , huku ukimya pia ukitawala, Edna alikuwa akifikiria maneno aliongea Roma ya juu ya kunyofoa moyo wake na kumuonyesha jinsi anavyojisikia .

“Hakuna maneno mazuri Zaidi ya kuongea mpaka useme unataka kunyofoa moyo wako?”

“Unafikiri hata nikitumia maneno mzuri zaidi unaweza kunisikiliza na kunielewa , chukua maji na sukutua kidogo, ijapokuwa ndio umeamka lakini mwili wako uko sawa kwa sasa, lakini unapaswa kupumzika”Aliongea Roma huku akimkabidhi Edna maji kwenye chupa na aliipokea na kushuka kitandani.

“Roma siwezi kuendelea kukaa hapa , kuna mambo mengi napaswa kuyafanyia maamuzi , nitajiweka sawa na kurudi kazini”Aliongea na kumfanya Roma kupumua huku akiwa ameshika kiuno.

“Nilijua tu huwezi kunisikiliza”Aliongea huku Edna akiingia maliwatoni kujisafisha.

Roma alivyokuja hapo hospitali aliweka simu yake silence ili asipate usumbufu , hivyo ilibidi aitoe na kuangalia watu waliompigia , na alijiikuta akishangaa kwani kulikuwa na Missed call 11 za Nasra ,Tano za Monica , kumi na tatu za Dorisi , mbili za Diego na sita zikiwa ni za Amina.

Roma aliona aanze na Diego, lakini kabla hata hajaanza kupiga simu yake ilianza kuita na mpigaji alikuwa ni Nasra.

“Ooh! Hatimae umepokea simu , Roma Edna upo nae hospitalini , anaendeleaje , amepona , uko hospitali gani , nitakufa na mawazo mimi”

“Yuko sawa punguza wasiwasi , muda si mrefu nitamleta kazini , mbona umenipigia mara kibao ni kwa ajili ya hali ya Edna tu au kuna lingine?”

“Nipo kwenye wakati mgumu muda huu , waandishi wa habari wamejazana nje ya kampuni wakiuliza maswali na muda huu tena kuna mtu kavujisha habari Edna kapoteza fahamu na kupelekwa hospitalini , kila mfanyakazi anachanganyikiwa , Edna kama yuko sawa mrudishe kwenye kampuni ili kupoza hii hali , ikiendelea hivi Jumatatu tunaweza kufilisika”

“Naona bado hawajaridhika na matokeo na wanatusaka mpaka mwisho”Aliongea Roma , lakini simu haikujibiwa na ni makelele tu yaliosikika.

“Roma nitakupigia”Aliongea Nasra na kukata simu.

Roma baada ya kumaliza kuongea na Nasra alimpigia Diego ili kujua kile ambacho kinaendelea .

“Diego how is analysis and investigation that I made you do?”Aliuliza akimaanisha kwamba vipi kuhusu uchunguzi pamoja na majaribio aliompatia afanye.

“Your Majesty Pluto, I’m very sorry. Ernest Komwe background is slightly too complicated. I can’t compile anything of substance just yet. I need a bit more time. But as for the two things that you asked us to analyze, we’ve already gotten the result.”

“Mfalme Pluto , niwie radhi, Ernest Komwe ubini wake kidogo unaonekana kuwa na mkanganyiko , siwezi kuelezea chochote kwa sasa , nahitaji muda kidogo lakini kuhusu vitu viwili ulivyoniambia nivifanyie kazi nishapata majibu”

Roma alijikuta akishangaa kidogo mnara baada ya kusikia neno mkanganyiko kwenye maneno ya Diego, Roma anachojua ni kwamba Ernest Komwe alikuwa moja ya wafanyakazi wa Vexto, kampuni ya Yamakuza ndio ilimpendekeza Ernest Komwe kuja Tanzania kuwa CEO msaidizi swala ambalo lilikubaliwa na Edna.

“Diego kwanini taarifa yake ziwe za mkanganyiko , Ernest ni mfanyakazi wa kawaida tu ndani ya Vexto anashikilia cheo cha CEO msaidizi , kwanini taarifa zake ziwe ngumu kupatikana?”

“Mfalme Pluto hata mimi nilifikiria hivyo hivyo , lakini kwa namna tulivyoweza kutafuta taarifa tumegundua Ernest Komwe sio jina lake halisi na kabla ya kufanya kazi katika tawi la Vexto Kenya ashawahi kufanya kazi kwenye kampuni ya Yamakuza tawi la HongKong, CV yake pia inaonekana haipo sawa kabisa na taarifa zake nyingi zinaonekana kufanyiwa sana marekesbisho , ndio maana kuna mkanganyiko, Mfalme Pluto naomba unipe muda kidogo nifuatilie hili”Aliongea Diego

Roma hakutegemea swala la Ernest Komwe kuchukua muda kiasi hicho , kwani tokea jana Diego alikuwa akitafuta Habari za Ernest komwe , lakini hata hivyo aliona ampe muda Diego afanye kazi yake.

“Vipi kuhusu Ushahidi niliowaambia mkauchukue kwenye kampuni , majibu yakoje?”

“We’ve already gotten the results. There is poison in that coffee indeed. It is a substance similar to ‘tannin’ that can be found in tea leaves. When this kind of acid is combined with a certain extract from animal protein, for example a substance in the proteins of dogs, it will produce a type of carcinogen that destroys humans’ internal organs.”

“Tushapata majibu, ni kweli kwenye kahawa kulikuwa na sumu inayofanana sana na ‘Tannin’ ambayo inapatikana katika majani ya chai ambayo yana Acid ndani yake , Aina hio ya Acid ikiunganishwa na aina flani ya protini ambazo zinatoka kwa Wanyama , kwa mfano protini ya mbwa inadhalisha aina flani hivi ya chembechembe zinazosababisha ‘Cancer’ ambazo zikiingia kwenye mwili zinaharibu ogani za ndani”Aliongea halafu akaendelea.

“Pia tumegundua kikombe hakina tu hii ‘Tanin’ bali kina aina nyingine ya protini ambayo hatujafahamu ni ya mnyama gani , kwa lugha nyepesi mfalme Pluto ni kwamba kahawa hio ilikuwa ikdhamiria kumuua mnywaji”

“Pia mfalme Pluto sumu ya aina hii kwenye mwili inafanyakazi kwa muda mrefu sana na inatakiwa muhusika kuinywa karibia kila siku ili iweze kuleta madhara , kwa maana hio ninaweza kukadiria kwamba Madam Persephone alianza kuwekewa sumu hii kwenye kahawa wiki iliopita na kwa vyovyote muwekaji wa sumu atakuwa ni mtaalamu sana kwani aliweka kiasi kinachotakiwa na kinacholeta madhara kwa muda husika , ukijumlisha na namna tukio la kuvujinshwa kwa nyaraka lilivyotokea basi malengo yake ilikua ni leo”

Roma baada ya kusikiliza maelezo yote ya Diego , alijikuta ile hamu ambayo alikuwa ni kama ameisahau kwa muda ikianza kumtekenya , hamu ya kuona damu ya mtu ikimwagika, Roma alijiambia kama Edna alikuwa akinywa kahawa yenye sumu muda wote huo basi hawezi kumruhusu Monica kuendelea kuwa sekretari wa Edna kwa namna yoyote ile hata kama hahusiki.

Roma ile anakata simu , Edna alitoka maliwatoni , Edna baada ya kuona Roma alikuwa akiongea na simu ilibidi amuulize kama kuna kilichotokea.

“Vipi kuna dharula imetokea?”

“Kampuni inakuhitaji , waandishi wa Habari wanaonekana kujazana nje ya kampuni , tuondoke kama umemaliza”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa na safari ya kurudi kazini ikaanza.

Roma wakati akiwa kwenye gari alijaribu kumpigia Amina ili kujua alikuwa na shida gani na ilionekana Amina alikuwa na wasiwasi tu ndio maana alipiga simu na Roma alijaribu kumtuliza.

“Ushajua nani kahusika na kuibiwa kwa nyaraka ndani ya ofisi ya Benadetha?”

“Muhusika anaonekana alijipanga kwa muda mrefu sana na anafanya mambo yake kwa umakini na muda wote anatuchora tu tunavyojihangaisha”

“Unamaanisha nini?”

“Hakuna kitu chochote kilichoibiwa kwenye ofisi ya Benadetha , bali aliiba sehemu nyingine , wakati huo huo akitufanya tuone ameiba ndani ya ofisi yake”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangaa.

“Tokea jana macho yetu yote yalikuwa kwenye sanduku la usalama ambalo lipo kwenye ofisi ya Benadetha na hio ni kwasababu kila mmoja anajua kulikuwa na kopi mbili tu na ni rahisi kuona kwamba wewe huwezi kunufaika kwa chochote kama nyaraka hizo utazivujisha , kwahio kila mmnoja wetu tukaamini upande mmoja tu , na hata tukafikiria labda kuna Camera ambazo zimefungwa ndani ya ofisi ya Benadetha pasipo kujua, hivyo ukiachana na kisanduku , akili zetu zilikuwa zikimtamfuta mtu ambaye anaweza kuingia ndani ya ofisi ya Benadetha na kuiba nyaraka hizo “Aliongea Roma

“Lakini si ndio ilivyo , kama sio kutoka kwenye ofisi ya Benadetha ni wapi , nina uhakika kabisa hazikuvuja kupitia ofisi yangu , ukiachana na Monica hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuingia kwenye ofisi yangu nikiwa sipo lakini pia sehemu yote karibu na sanduku hakuna aina yoyote ya Camera”

“Ngoja nimalize kukuelezea …. Ukweli hata mimi mwenywe niliingia kwenye mtego wa mwizi . alionekana kujipanga , na alionekana alikuwa akinifahamu mimi sana kabla hata hajaanza mpango wake au unaweza kusema amefanya vitu vingi kutuchanganya kabla ya tukio , muhusika alionekana kwanza siku kadhaa zilizopita alikuwa akitembelea sana ofisi ya Benadetha mara kwa mara bila hata ya kuwa na sababu za msingi na alihakikisha kila mtu anafahamu anatembelea ofisi ya Edna sio wafanyakazi tu hata kwa mimi mwenyewe”

“Mke wangu usiniambie haujamfahamu mtu mwenyewe ni nani mpaka hapo, nafikiri hata wewe pia umemshuku ndio alievujisha nyaraka na nadhani ndio maana hukuita polisi kufanya uchunguzi na ukaniacha mimi nifanye uchunguzi si ndio?”

“Unamzungumzia Ernest , maana ndio aliekuwa akitembelea ofisi ya Benadetha, pia alionekana kuwa na ukaribu nae mara nyingi na hili linajulikana kwa wafanyakazi wengi wa kampuni, ijapokuwa hata mimi nilikuwa nikimshuku lakini sikuweza kulitaja jina lake kwani hakuna ushihidi wowote kama amehusika”Aliongea

“Hakika hakuna ushahidi , hata nilivyoenda kuangalia rekodi za kamera na nikapiga mahesabu muda ambao angetumia kufungua sanduku na kuiba nyaraka havikuwa vikishabihiana kabisa , alichokuwa akikifanya ni kutufanya tufikirie wote nyaraka zimeibiwa kutoka ofisi ya Benadetha , wakati huo hakuwa na mpango wa kuiba kutoka kwenye ofisi yake”

“Kwahio unamaanisha kwamba yote aliokuwa akiyafanya ni mtego wa kutuchanganya , lakini hata hivyo amewezaje?”

“Hata mimi nilikuwa nikifiria vilevile , lakini nilichogundua sio binadamu alietusaliti bali ni mashine ya kutolea kopi ndani ya ofisi ya Monica”

“Mashine ya kutolea kopi! , unamaanisha kwamba Monica alitengeneza kopi nyingine? , hilo haliwezekani , nishakuambia nilisimamia mwenye kazi hio”

“Sikulaumu kwa kutolifahamu hili mapema , lakini sasa hivi mashine zote za photocopy zinakuja na ‘Internal Harddisk’ au ‘Solid state disk’(Kifaa kama memori ya simu), ukishamaliza kutoa kopi kuna taarifa zinahifadhiwa humo kama akiba, kwa mtaalamu wa komputa anchokifanya ni kutoa hio Hardisk na kisha kuchomeka kwenye tarakishi na baada ya hapo atatumia dakika kadhaa tu kupata taarifa zote , mambo kama haya yanatokea sana kwenye ulimwengu wa kijasusi watu kuiba taarifa kupitia mashine za kutolea kopi, ndio maana idara nyingi mashine nyingi zinazotumika hulindwa sana na wanabadilisha hizi hardisk kila baada ya muda au kuziharibu kabisa”

Edna alijikuta akipatwa na mshangao kupitia maneno ya Roma , hata hivyo ilikuwa sawa tu kwani mrembo huyo alisomea maswala ya biashara , hivyo yeye likija vifaa vya kieletroniki anachojua ni matumizi tu na sio vinavyofanya kazi.

“Lakini bado kuna swali moja , kama kweli ameiba kupitia ofisi ya Monica , ninachojua mimi chumba kinachohifadhia mashine kinafungwa mara baada ya Monica kutoka kazini”Aliongea Edna na Roma alitabasamu , aliona Edna hamfahamu vizuri sekretari wake.

“Mke wangu , kampuni yetu imejaaliwa warembo wengi , lakini katika wanawake wote warembo Ernest akaamua kutoka kimapenzi na Monica , amefanya hivyo ili kwanza Monica kuweza kumuamini”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangaa kwani Habari hio ilikuwa mpya kwake.

“Unamaanisha Monica na Ernest ni wapenzi?” Roma alitabasamu na kisha akamwangalia mke wake.

“Kwenye mashindano ya Kizazi nyota niliwaona wote wakiwa wameshikana kimahaba kwa Zaidi ya mara mbili , mara moja nilidhani labda walikutana njiani lakini walivyokuja kwenye fainali wakiwa pamoja ndio nilifahamu ni wapenzi , huwa nina tabia ya kuangalia watu wanaonizunguka kwa kila wanachofanya , hususani mahusiano ya mmoja na mwingine , hii inanisadia sana kwenye baadhi ya nyakati”

“Muwindaji kwenye ubota wako , eti inanisaidia kila wakati kwanini usiende moja kwa moja?”Aliongea Edna.

“Unamaanisha nini?”








SEHEMU YA 366.

Nasra alionekana kuulizia ni kipi afanye , kwani alikuwa akishindwa kufanya baadhi ya maamuzi kutokana na kwamba yalikuwa yakimtaka CEO mwenyewe na ndio maana akapiga simu , lakini Edna alimjibu kwamba yupo eneo la maegesho hivyo anapandisha juu na Nasra alionekana kupata ahueni.

“Roma unaruhusa yangu kumtoa Benadetha polisi , nataka arudi kazini anisaidie baadhi ya kazi zinazohusiana na idara yake”Aliongea Edna.

“Okey mke wangu, wewe kapambanie kampuni mengine niachie mimi lakini pia upunguze wasiwasi”Aliongea Roma.

“Wewe ndio wa kupunguza wasiwasi, kwani haitotokea siku nikashindwa kujihudumia kimatumizi kama nitafilisika , hivyo usiogope sana na kinachoendelea kwenye kampuni”Aliongea Edna na kisha alifungua mlango na kutoka na kumuacha Roma akimwangalia kwa nyuma na kujiambia kuna muda ni vizuri mwanamke kuweza kujitegemea , lakini muda mwingine mwanamke akijitegemea kwa kila kitu sio jambo zuri.

Roma wakati akigeuza gari alikuwa akiwaza baadhi ya mambo , kwa mfano aliwaza wanawake wake wote walikuwa wakiweza kujitegemea na hakuwahi hata kuwaza kutoa hata mia yake mfukoni kwa ajili ya kuwasaidia ijapokuwa sio kama hakuwa na uwezo wa kuwasaidia pesa, lakini kwa upande mwingine alijiona kuwa na bahati, ndio hata hivyo wanaume wengi hawapendi kuombwa pesa lakini wakati huo huo hawataki wanawake wakiwazidi wanaume kimapato ki ufupi sio mwanamke tu ambaye haeleweki bali hata wanaume muda mwingine hawaeleweki ni vile tu wanawake wanaongoza kwa kutokueleweka.

Dakika kadhaa tu alifika kituo husika cha magogoni , ambacho ndio sehemu ambayo Benadetha alikuwa amezuiliwa na kwakua hakupenda sana kudili na polisi ilibidi ampigie Mage simu na Mage alimuunganisha na polisi wa hapo atakaemuongoza.

Alivyotoka kwenye gari na kuingia kituoni aliweza kumuona Benadetha akiwa eneo la mapokezi na alionekana alikuwa akimsubiri kwnai alimpungia mkono huku akitoa tabasamu hafifu.

“Mr Roma unaweza kuondoka na Miss Benadetha asharuhusiwa tayari kwa maagizo ya Miss Edna”Aliongea moja ya polisi ambaye aliagizwa na Mage kumpa ushirikiano Roma na alishangaa kidogo , kwani aliamini kungekuwa kidogo na hatua za kufuata kabla ya kuondoka nae , lakini anakuta kila kitu kishakamilika.

Roma alimchukua Benadetha , hakupenda sana kukaa kituo cha polisi , alikuwa kama watanzania wengi wasiopenda kuonekana maeneo ya vituo vya polisi.

“Roma Boss Edna anaendeleaje , nasikia alipatwa na shida kiafya amepona?”Aliongea Benadetha akiwa ni mwenye wasiwasi na Roma alitabasamu.

Utofauti wa Benadetha na wafanyakazi wengine , pengine kama utamfananisha kati ya Nasra na Dorisi, Benadetha alikuwa ni mtu siriasi kwa kila anachokifanya na ukitaka umjue Benadetha tabia yake ni namna anavyoongea , hakuwa muongeaji sana lakini pia hakuwa mkimya sana ,alikuwa akipenda utani wakati mwingine lakini hata katika utani , maneno yake anakuwa ameyachuja sana , ni rahisi kusema kwamba alikuwa amebarikiwa na hekima kwani maneno yake yamejaa upole sana.

“Haumkasirikii boss wako kukulaza polisi mpaka muda huu, kwanin hata unajali afya yake?”Aliuliza Roma huku akimfungulia mlango wa gari kuingia na Benadetha alitabasamu kidogo.

“Siwezi kumkasirikia boss Edna, kwani amejaariwa roho nzuri , ijapokuwa amenileta kituoni jana lakini bado aliendelea kunijali”

“Umejuaje anakujali wakati amekulaza kituoni?”

“Wakati nakuja polisi nilikuwa na wasiwasi sana , lakini huwezi kuamini nimelala kama nipo hotelini tu licha ya kukosa uhuru , nililazwa kwenye chumba cha watuhumiwa VIP na jana Boss Edna alinipigia simu na kuniambia nivumilie walau usiku mmoja atafute muhusika, na mimi nilimuelewa anachomaanisha . nilipata chakula kizuri pia hata kuoga”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma kushangaa kidogo , hakuamini ubabe wote ule wa mke wake wa siku ya jana , ulikuwa wa maigizo tu , kumbe alienda mbali mpaka kuhakikisha Maisha ya Benadetha kituoni sio magumu.

“Hata hivyo ni haki yako , tokea nifike kwenye kampuni , unaeonekana kuwa siriasi na kile unachokifanya mchango wako ni mkubwa na Edna anapaswa kukulinda kama mfanyakazi wake”Aliongea Roma na kuwasha gari na kulitoa mdogo mdogo , huku Benadetha akimwangalia usoni.

“Hongera pia kwa kuwa na mke mzuri kama Edna, ambaye ana kila kigezo”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma kutabasamu.

“Hahaha.. Edna ni mwanamke mzuri ndio , lakini haimaanishi kama amekamilika kwa kila kitu , upendo wangu kwake unayafunika madhaifu yake yote na yeye hunivumilia”

“Hio sehemu ya mwisho ndio ninasisitizia”Aliongea Beenadetha.

“Ipi?”

“Kukuvumilia Roma”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma kushangaa kidog.

“Wote tunajua unamichepuko mingi , Dorisi , Nasra, yule sekretarri wako , lakini Boss bado anakupenda hivyo hivyo, siamini ingekuwa mimi nipo kwenye nafasi yake ningejisikiaje”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma na yeye kujiona mwenye hatia.

“Benadetha baba yako amenipigia?”Aliongea Roma na kumfanya Benadetha kushangaa .

“Amekupigia! , amepata wapi namba yako?”

“Nikuulize wewe , amenipiga mkwala huku akiniambia wewe ni mpenzi wangu kitu ambacho sio kweli”Aliongea Roma na kumfanya Benadetha kushangaa na kuona aibu kwa wakati mmoja.

“Baba sijui alikufahamu vipi , ila miezi miwili iliopita alivyokuja kututembelea hapa Dar alianza kuuliza kuhusu Habari zako , huku akiniambia ahakikishe unakuwa mkwe wake na alikuwa akiomba sana namba zako ila sikumpatia na nilimueleza sina mahusiano na umfanyakazi mwenzangu tu , lakini hakutaka kunikubalia , aliendelea kunisisitizia kwamba anahitaji akuite mkwe kila siku anavyonipigia simu”Aliognea Benadetha kwa sauti ndogo sana na kumfanya Roma kushangaa , lakini kwa Benadetha kuona aibu.

Roma alifikiria kwanza maneno ya Benadetha na kuona inawezekana Mzee Nguluma ni kweli anamfahamu yeye , ukizingatia kwamba alishawahi kujihusisha sana na maswala ya kibiasahara katika ulimwengu wa wahalifu , wakati akimsaidia Rose kudili na baba yake , hivyo aliamini huenda alimfahamu kupitia huko.

“Umesema baba yako anakuja kuwatembelea na kukupigia mara kwa mara?”

“Ndio baba aliachana na mama yangu wakati nikiwa kidato cha kwanza , ijapokuwa hawakuwahi kuoana kwa ndoa lakini walitambulika kama wanandoa , baba baada ya kuhamia Shinyanga ndipo mama alivyojua kuwa baba ana mwanamke mwingine huko Kahama na amezaa nae pia , ndio ugomvi ulipoanzia mpaka wakaachana , baba aliendelea kunilea kwa kutuma matumizi tu na mahitaji mengine”Aliongea Benadetha na sasa kumfanya Roma kuelewa , kwa jinsi Benadetha anvyoongea Roma aliona huenda hajui kama baba yake anajihusisha na madawa ya kulevya pamoja na kuwa na ushirikiano na makundi ya kigaidi huko Congo.

“Kwahio mama yako pia ameolewa hapa Dar?”

“Hajaolewa , mama licha ameachana na baba lakini bado anampenda na baba kila akija Dar analala nyumbani kwetu , lakini mama ukimuuliza atasema wameachana ,nikimuuliza kwanini analala kwetu kama wameachana anashindwa kujitetea”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma kutabasamu.

“Unavyofanya kazi kwa juhudi nikajua una majukumu mengi kumbe baba yako anajiweza kiuchumi, au Benadetha kuna mwanaume unamlea nini?”Aliongea Roma kiutani na kumfanya Benadetha kucheka.

“Sina mwanaume mimi , kuweka juhudi kwa kila ninachokifanya ni kupigania ndoto zangu na sehemu pekee ambayo naona naweza kufanikisha ni kwenye kampuni ya Vexto”

“Unaamini vipi Vexto inaweza kuwa msaada mkubwa wa kutimiza ndoto zako?”

“Boss Edna amejipambanua mara nyigi sana juu ya ndoto zake za kuifanya kampuni ya Vexto kuwa kubwa kimataifa , ndoto zake haziwezi kutimia pasipo ya kuwa na msaada kutoka wetu , kampuni ya Vexto msingi wake kwanzia mwanzo ulijengwa na mwanamke na mpaka sasa kampuni inawafanyakazi asilimia themanini wote wakiwa ni wanawake , chochote kitakachokamilishwa na Vexto siwezi kukosekana ,ndoto yangu kubwa ni kuwa sehemu ya historia ya Vexto , kuwa sehemu ya wanawake waliofanikisa kampuni kuwa kubwa kimataifa”Aliongea Benadetha na Roma alitingisha kichwa kukubaliana nae.

Lakini wakati huo huo akimuona kweli Edna alikuwa kiongozi , kwani ukimwangalia Dorisi hana mpango wa kuondoka Vexto kabisa ,licha ya kwamba alikuwa na uwezo wa kufungua kampuni yake mwenyewe , ukimwangalia Nasra na yeye anaonyesha dalili ya kuendelea kudumu ndani ya kampuni ya Vexto kwa muda mrefu licha ya kwamba alikuwa na uwezo wa kuanzisha kampuni yake , kwa urahisi ni kusema kwamba Edna aliweza kuishinda mioyo ya wafanyakazi wake wote licha ya ukauzu wake.

Roma hakutaka sana kuingizia maswala ya mapenzi na Benadetha kabisa, alikuwa akijifahamu mwenyewe kwamba hakuna mwanamke ambaye alikuwa na uwezo wa kujizuia kwake kutokana na yeye mwenyewe alivyo.

Roma wakati akiwa chini ya mafunzo ya Master Chi kwenye jangwa la Gobi , alikuwa akikumbuka baadhi ya maneno ambayo alielezewa na Master wake na kubwa Zaidi ilikuw ni kumpa tahadhari Roma juu ya wanawake.

“Hii mbinu inahusina na namna ambavyo utaweza kuvuna nishati inayohusiana na Yang , kadri itakavyokuwa inatawala mwili wako ndio utakapokuwa unavutia Zaidi nishati ya Yin”Aliongea Master Chi huku kijana mdogo alievalia kitamaduni akiwa amekaa chini akifanya tahajudi kwa kuangalia jua linalozama upande wa magharibi”

“Master unamaanisha nini kusema nitavutia Zaidi Yin Energy?”

“Ijapokuwa Yang Energy inasimama kwenye maana ya vitu vingi lakini ukija katika ubinadamu inasimama kama nguvu ya kiume na Yin Energy inasimamam kama nishati inayozalishwa na mwanamke , siku zote nishati hizi mbili zinatofautiana lakini ni zenye kuvutana, ukikutana na mwanamke mwenye nishati Yin dhaifu na nishati yako ya Yang utammeza kihisia”Aliongea na kumfanya kijana kufumbua macho na kumwangalia Master wake kwa mshangao , lakini alijikuta akipigwa na kigongo cha mgongo.

“Sijakuambia ufumbue macho kabla ya giza , endelea kunyonya nguvu ya Yang inayozalishwa na jua linalozama “Aliongea kwa kufoka na kumfanya kijana mdogo kuendelea kufumba macho huku akiwa kama anasali .

Alichokuwa akijaribu kuelezewa ni kwamba kadri atakavyokuwa anazidi kunyonya nishati ya Yang na kadri itakavyojaa kwenye mwili wake, ndio itamfanya wanawake wenye nishati ndogo ya Yin kutomkataa kimapenzi katika maneno yake ya kumeza kihisia , hio ndio pointi yake.

Kila mtu anazaliwa na hii nishati ambayo wachina wameipa jina la Yang kwa upande wa wanaume , lakini pia Yin kwa upande wa mwanamke , nishati hizo kila mtu anazaliwa nazo lakini zinatofautiana mtu na mtu , wengine wanazaliwa zikiwa nyingi sana kwenye miili yao , kiasi kwamba aina ya watu hawa kwenye jamii unaweza kuwatambua kutokana na mvuto wao.

Lazima yupo mwanamke anaependwa sana kwenye jamii licha ya kuwa na tabia mbovu mbovu kwenye jamii yako , hio yote ni kutokana na kwamba amezaliwa na kiwango kikubwa sana cha hii nguvu asili ya Yin, hivyo akikutana na mwanaume ambaye ana nguvu hafifu za Yang ni lazima uingie kwenye mtego wake kwa namna yoyote ile na wewe mwanaume ambaye una nguvu chache za Yang huwezi kupindua.

Hivyo hivyo kwa wanaume kuna wale ambao wanazaliwa na nishati za Yang kwa kiwango kikubwa na hawa wanaume unaweza kuwatambua tu kwa jinsi walivyokuwa na mvuto kwenye mambo mengi , unaweza ukamkuta mwanaume yupo yupo tu , hana hela, hana mwonekano , hana kingine cha ziada kukushinda wewe unaejitahidi kujipuliza unyunyu na kuramba midomo, lakini likija swala la warembo anakuacha mbali na unaishia kusema tu huyu jamaa ana kamzizi kumbe siri ni nishati ya Yang.

Hao ndio watu waliozaliwa na hii nishati asili ya Yang , kwa maana kwamba mwanaume wa aina hio kila atakapokutana na mwanamke ambaye ana nguvu ndogo ya Yin basi mwanamke huyo atajishtukia tu yupo kitandani na kesho asubuhi unakuta analalamika amemsaliti mume wake au sababu zinginezo ambazo hazijui kwanini zimemfikisha kwenye kitanda cha mwanaume, lakini vile vile kwa mwanaume utakuta anajilaumu kuwa dhaifu mbele ya mwanamke Fulani na kujishutikia kufanya nae uzinzi yote hayo ni kuwa na nguvu dhaifu za Yang kwa mwanaume au Yin kwa mwanamke.

Sasa ili Maisha yako kuwa bora Zaidi aidha kwa mwanamke au kwa mwanaume ni kwa kuzinyonya hizi nguvu katika mazingira , kwani zipo kila mahali , japo inasemekeana sana Yang inapatikana kwa wingi kwenye jua linalochomoza na linalozama, utaweza kuipata kwa njia tofauti tofauti lakini sio kuota jua licha ya kwamba inasaidia wakati mwingine.

Ieleweke tunaposema Yang Au Ying ni nishati tu na haimaanishi siku zote imebeba upande wa mwanamke na mwanaume bali ni maneno hayo ndio yanayoashiria tu kwamba kuna aina hizo za nishati kwenye mazingira, kwa mfano ukija katika tafiti rasmi wanabailojia walienda mbali kwa kusema Yang And Yang ni sawa na kusema ‘Pheromones’?(hapa nenda google).

Hata hivyo ili uweze kupata mafanikio mazuri kwenye Maisha ni kuweza kubalansi hizi nguvu zote mbili hapo ndipo utaona zikikuletea faida.

Naam ilikuwa ni siku nyingine kabisa yaani jumapili , siku hii Edna alishindwa kabisa Kwenda kutembelea Watoto kutokana na kile kinachoendelea kwenye kampuni, ijapokuwa alirudi nyumbani lakini aliendelea kufanya kazi , upande wa Roma aliacha kwanza Kundi lake la the Eagles kuendelea na uchunguzi wao unaohusiana na taarifa za Ernest Komwe.

Macho ya kila mfanyakazi wa Vexto ilikuwa ni Jumatatu wakati soko la hisa litakapofunguliwa , kila mmoja alikuwa na wasiwasi na kile mabacho kitatokea, kwa upande wa Edna siku ya jumapili hakuwa na chakufanya, kwani bado hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja kusema nani kavujisha siri za kampuni , hivyo maamuzi namna ya kuokoa kampuni ilitakiwa kufanyika siku ya jumatatu, hali itakavyokuwa sokoni ndio atakavyoweza kufanya maamuzi , alishapokea simu za vitisho kutoka kwa wawekezaji wengi na washirika wa kibaisahra juu ya kuvunja mkataba na kampuni yake , lakini aliwahakikisha kwamba anafanya kila liwezekanalo kuirudisha kampuni kwenye ubora wake.

Ikiwa ni muda wa jioni kabla giza la saa moja halijafunika anga la jiji la Dar es salaam , Roma aliweza kupokea simu kutoka kwa Diego.

“Vipi umepata chochote?”

“Mfalme Pluto niseme kwamba hata mimi nimeshangazwa , taarifa zake zinachanganya sana tofauti na nilivyofikiria? Ijapokuwa taarifa tuliokuwa nayo haijathibitishika bado , lakini tumegundua kuna uwezekano madam Persephone na Ernest wakawa ndugu kwa upande wa Mama”Aliongea Diego na kumfanya Roma kushangaa kidogo.

“Unasema kweli?”

“Ndio mfalme Pluto , siwezi kukuelezea kila kitu , ila nitakutumia faili kwa njia ya Email usome”.

“Kama ni hivyo fanya haraka”Aliongea Roma na wakakamilisha maongezi na dakika hio hio faili liliweza kuingia kwenye simu yake kubwa kupitia email.

Roma alieketi kwenye masofa kwenye sebule ya juu , alijikuta uso wake ukibadilika badilika kadri alivyokuwa akisoma faili ambalo limetunwa na Diego , kuna muda alikuwa akishangaa , kuna muda alikuwa na wasiwasi na kuna muda alirudi kwenye mshangao , alitumia dakika kama kumi na moja tu kupitia faili lote na kwa hasira aliweka simu yake pembeni na kuendelea kuangalia runinga.

Ilikuwa ni siku nyingine kabisa , saa kumi kamili za asubuhi ndani ya kampuni ya Vexto Edna na wafanyakazi wengine walikuwa washafika kwa ajili ya kuanzisha mapambano ya kuokoa kampuni.

Soko lilikuwa lishafunguliwa masaa kadhaa yaliopita na kwa maelezo ya Nasra ni kwamba hali ilikuwa mbaya Zaidi kuliko livyotegemewa , kwani hisa zilikuwa zikishuka mno thamani na wawekezaji wengi walikuwa wakizutoa sokoni.

“Edna , if this goes on, within less than half an hour our stocks would plummet through the twenty-percent baseline!”

“Edna kama hali itaendelea hivi ndani ya nusu saa ijayo hisa zitashuka thamani kwa asilimia ishirini Zaidi”Aliongea Nasra wakiwa ndani ya chumba cha idara ya masoko wote wakiwa wamesimama wakikodolea macho tarakishi ambazo zinaonyesha namba namba tu , kama hujasomea uchumi kinachoonyeshwa hapo ndani utaona nyota nyota tu , lakini kwao kila kitu kilikuwa kikijieleza kwa lugha ya kiuchumi Zaidi.

Edna aliesimama , akiwa na uso wake wa kupendeza aliendelea kuangalia soko , huku akisoma kila namba inayoonekana kwenye skrini huku karamu yake ikiwa imegusa lipsi za mdomo , licha ya kwamba alionekana kuwa na wasiwasi , lakini alionekana alikuwa akifikiria.

Kulikuwa na wafanyakazi Zaidi ya saba ndani ya ofisi hio ambao wote walikuwa ndani ya ofisi moja na Edna , huku upande wa idara nyingine wafanyakazi walikuwa washafika kazini muda mrefu tu , tena kuna wengine hawakuondoka kabisa kurejea nyumbani hususani idara ya Finance ambayo ilikuwa ikisimamiwa na mwanamama aliefahamika kwa jina la Elizabeth Mlowe.

“Miss Eliza , pass a message to the financial management department. When our share price falls to fifteen percent, purchase two to five thousand units using separate accounts. Repeat the purchase every ten to fifteen minutes. Alternate these purchases via at least a hundred accounts.”

“Miss Eliza , toa maagizo wa idara ya udhibiti wa feza , hisa zetu zitakaposhuka thamani kufikia asilimia kumi na tano, zinunuliwe hisa kwa mafungu yenye thamani elfu tano kwa kutumia akaunti tofauti tofauti , warudie mchakato huo kila baada ya dakika kumi na tano , hayo mafungu ya manunuzi angalau yawe katika akaunti mia moja”Aliongea Edna , hapa kwa wale ambao wanaelimu ya uchumi watakuwa wameelewa.

Anachomaanisha ni kwamba kuwe na akaunti mia moja ambazo kila akaunti inatakiwa kununua hisa katika fungu la thamani ya dola elfu moja au milioni mbili za kitanzania na zoezi hilo lifanyike kila baada ya dakika kumi na tano katika akaunti angalau mia moja, anachojaribu kufanya Edna ni kujaribu kuzinununa hisa kwa kutumia hela ya kampuni ili zisizidi kuporomoka thamani.

“Madam unasema?”Aliongea Eliza kionyesha kutokuelewa.

“Vipi tena , unataka nirudie?”aliongea Edna.

“Boss Edna , the problem is if we do that, it wouldn’t do any good for our current situation. There are tons of investors getting rid of our shares in the hundreds of thousands. We would hardly be doing anything to help the downward trend.”

“Boss Edna , tatizo tukifanya hivyo , haileti maana kutokana na hali ilivyo , kuna wawekezaji wengi ambao wanaziuza hisa zetu kwa mamia maelfu , , tutashindwa kushindana na soko linaloshuka thamani”

“Ninachokuambia ni kufanya kama nilivyokuagiza na sija kuomba unitolee maelezo”Aliongea Edna

“Edna najua una wasiwasi lakini alichokisema mkuu wa idara ya usimamizi wa Feza ni sahihi , hakuna sababu ya kufanya hivyo”

Hapa usichanganyikiwe, Nasra ni mhasibu mkuu wa kampuni na Eliza yeye alikuwa akisimamia idara ya fedha , tofauti ilipo kati ya hawa wawili ni kwamba idara ya fedha yenyewe inahhusika na maswala ya mipango na uelekezwaji wa miamala yote ya kampuni , wakati huo ofisi ya mhasibu inahifadhi na kutoa ripoti zote zinazohusiana na hio miamala , kwa mfano mtu wa finance atafanya miamala yote ya kampuni kutoa hela benki na kuziingiza , wakati huo huo mhasibu yeye kazi yake itakuwa ni kutunza kumbukumbu ya ile miamala pamoja kuitolea ripoti na mengineyo, katika baadhi ya taasisi idara ya fedha na uhasibu zinaweza kuwa sehemu moja au ofisi moja katika idara moja , lakini baadhi ya taasisi nyingine ni idara mbili tofauti hio yote ni kurahisisha kazi,lakini pia naweza kusema kwamba mtu wa ‘Fedha’ anaweza kuwa na majukumu mengi Zaidi kuliko mtu wa ‘mhasibu kwasababu mhasibu yeye anadili na namba tu pamoja na kumbukumbu wakati huo mtu wa fedha anakuwa na vitu vingi vya kuzingatia katika idara yake kuanzia kufanya tafiti juu ya taarifa zinazoendana na mipango ya kampuni na mengineyo.

“Ninafanya hapa linalowezekana kuhakikisha tunaidhibiti hii hali wakati huo huo tukisubiria kile ambacho Mungu ametupangia kuweza kukipitia siku ya leo, Nasra ninataka uwasiliane na watendaji wakuu wa benki zote ili kuhakikisha fedha zetu zinapatikana kwa wakati na katika mfumo wa taslimu”Aliongea Edna.

“Okey boss lakini kwanini tusiingize kiasi cha pesa Kwenda Athena , huenda wakatusaidia katika hili?”Aliuliza Nasra.

“Hatuwezi kuwatemegea ‘Traders’ kwenye swala kama hili , unaona kabisa hata wawekezaji ambao walinunua hisa zetu sikiwa na thamani ya juu wanaziuza kwa thamani ndogo , hii ni kwasababu wanajua wakiendelea kubaki nazo watapata hasara Zaidi , hivyo hata Athena hawawezi kushindana na mitazamo ya watu wengi kwenye soko la hisa ,wataishia kupoeza hela ya kampuni tu, I will discuss with the others to modify the issues of acquisition and allocation. We can do this”

Nasra ilibidi akubaliane na Edna , kwani hakuwa na pendekezo lingine zuri Zaidi kudili na hali.

Katika vyombo vya Habari vingi vilikuwa vikioanisha kwamba hasara Zaidi itatokea ndani ya kampuni ya Vexto baada ya matawi yote kufungua siku hio ya jumatatu, kampuni pekee ambayo ilikuwa ikitegemewa kutoathirika sana ni kampuni ambayo inaongozwa na Roma , Vexto entartaiment, hio ni kwamba bado kuna makubwa Zaidi yaliokuwa yakitegemeewa kupitia kampuni hio kutokana na kipaji ambacho alikuwa nacho Sophia , wananchi wengi walikuwa wakiegemea wimbo wa kwanza atakaoachia Sophia kwa kupitia Vexto Media , hivyo raia walikuwa wakiamini mauzo yatakuwa juu, sasa kampini nyingine za mavazi , ujenzi , uchakataji wa mazao na mafuta ulionekan kwend akuathirika sana.

Washindani wa kampuni ya Vexto wakati Edna akihangaika kuikoa kampuni wao walikuwa kwenye mahoteli wakinywa mvinyo mwekundu kwa kujipongeza kwa kile kinachoendelea, kila mmoja alikuwa akiamini Vexto inakwenda kufa kifo cha mende.

Upande mwingine wakati hayo yakiendelea , upande wa Bagamoyo kwenye moja ya Jumba la kifahari kinachoendelea ni ni srori nyingine kabisa.
 
SEHEMU YA 367

Ni mbele kidogo na shule ya sekondari ya bweni ya St Trust upande wa kushoto mwa barabara inayoelekea Msata , kuna jumba moja ambalo lipo maeneo hayo , jumba hili lilikuwa ni moja ya jumba kubwa ambalo linaonekana kwa kupitia barabarani , kama ukiwa kwenye basi au kwenye daradala basi ni rahisi kuona geti lajumba hili baada ya kupita la shule.

Sasa ndani ya jumba hili ambalo ndani yake kuna ulinzi mkubwa wa baadhi ya wanaume waliovalia suti wakiwa wameshika mitutu ya bunduki kama wanalinda benki vile , wakiranda randa kulia na kushoto kuhakikisha ulinzi unakuwa wa kuaminika kwa yoyote aliokuwa ndani ya jumba hilo.

Ndani yake kabissa katika eneo la sebuleni anaonekana Ernest Komwe akiwa kifua wazi , akiwa ameketi kwenye masofa ya bei ghali huku mkononi akiwa ameshilkilia glasi ambayo ndani yake ilikuwa na kimiminika chekundu kama damu, akiwa akishushia taratatibu taratibu huku macho yake yakiwa kwenye runinga ambayo inaonyesha namba namba za soko la hisa za kampuni ya Vexto , alionekana kufurahia kwa chochote kile kinachoendelea kwenye soko hilo la hisa.

Pembeni yake anaonekana pia mwanamke aliejilaza kivivu kwenye sofa , akiwa na uso uliopauka kwa wasiwasi , akiwa usingizini , mwanamke mwenywe alikuwa ni Monica na alionekana alikuwa amechoka sana kwa chochote kila kinachoedelea hapo ndani, Ernest ghafla tu aliweza kushuhudia hisa za Vexto zikianza kupanda kidogo kidogo.

“Wow! Naona Edna anajaribu kununua hisa zake mwenywe ili kuwaingiza mtegoni wanunuzi wa hisa wadogo wadogo, Mh anaona ni kipi sasa ataweza kufanya kwenye hali kama hio, Edna wewe ni mjinga tu, Monica amka umuone Boss wako unaemuona amekamilika kila idara , nishakuambia ni mwanamke tu wa kawaida kama wengine”Aliongea huku akimtingisha Monica aliekuwa kwenye usingizi, alionekana kuwa na furaha kweli, muda huu ni pale Edna alivyowaambia watu wa idara ya fedha kununua hisa za kampuni kwa mafungu elfu moja moja.

“Ernest una nini wewe , kufilisika kwa kampuni ya Vexto kutakusaidia nini?”Aliongea Monica ambaye alikuwa akitia huruma kwa muonekano wake wa nywele.

“Hakuna sehemu niliposema nataka kampuni ya Vexto ifilisike kabisa , ninachotaka ni Edna kufilisika na kukosa kigezo cha kuendelea kuwa CEO , baada ya mpango uliopangwa Kwenda kama tunavyotgemea , Edna ataondoshwa na nitarudi kwenye kampuni kuikoa kama CEO mpya”Aliongea

“Na ukishaipata hio nafasi utafaidika nini?”

“Hujui hata ninachomaanisha , kampuni ya Vexto ni ndogo sana kukidhi matamanio yangu , ninachokifanya hapa ni kuhakikisha napata kilichohalali yangu”Aliongea.

“Ernest wewe ni chizi , mimi naondoka na nakuacha hapa hapa , ninaenda kumsaidai Boss Edna”Aliongea huku akijinyanyua na kuanza kupiga hatua kuelekea mlangoni , lakini kabla hajafungua Ernest alikuwa ashamfikia na alimkumbatia kwa nyuma, Monica alijaribu kufurukuta , lakini alishindwa kutoka kwenye kumbatio la Ernest.

“Unataka kuondoka , inamaana haunipendi tena?, Hupendi kuniona mimi nikiongoza kampuni ya Vexto tofauti na Edna?”

“Ernest naomba uniachie niondoke, acha ukichaa wako tafadhari”Aliongea huku akianza kutoa machozi, Monica na ubabe wake wote mbele ya Ernest alionekana mdhaifu sana.

“Ernest sipendi kukulinganisha na Edna boss wangu , wewe ni mwanaume wangu na nakupenda na sitaki uendele kufanya mambo kama haya yasio na msingi”

“Monica usinipandishe hasira nimekuchukua na kuja na wewe hapa , sio kwamba una umuhimu sana kwangu”Aliongea huku akianza kukasirika , lakini alijikuta akizishusha hasira zake mara baada ya Monica kukaa chini huku akianza kulia kama mtoto na alijikuta akimuonea huruma.

“Monica ijapokuwa nilikuwa nikikutumia kwenye mipango yangu , lakini haimaanishi sikujali , kama nitakuja kuwa CEO wa Vexto na kuwa Tajiri , utakuwa mke wangu na hautaendelea kuwa msaidizi tena wa Edna bali nitakupa cheo kikubwa ndani ya kampuni”Aliongea na kumfanya Monica kukaa vilevile kwenye kapeti huku akionekana kuwaza.

“Asante kwa kunielezea mpango wako … lakini Ernest sijali ni ukichaa namna gani unaweza kukupata , sijali ni mangapi mabaya utafanya , lakini nitaendelea kukupenda”AliongeaMonica

“Unamaanisha umekubali”

“Sorry! Ernest siwezi kuendelea kukaa hapa napaswa kurudi kwenye kampuni kumsaidia boss Edna .nafasi yangu kwenye kampuni ni ndogo ndio , lakini nilikuwa nikiridhika nayo , nimefanya kazi kwa muda mrefu ndani ya kampuni hivyo siwezi kuiona ikididimia”

“Kwahio unamaanisha unampenda sana Edna kuliko mimi , kwanini unaacha kunijali miimi mwanaume ninaepanga kukufanyia makubwa?”Aliuliza kwa hasira , lakini Monica aliishia kutabasamu kwa uchungu.

“Ni kwasababu nina mimba yako Ernest , sitaki mtoto atakae zaliwa kuwa na baba mtenda maovu kukamilisha ndoto zake”Aliongea Monica na kumfanya Ernest kushangazwa na kauli hio , na alijikuta akichanganyikiwa kwa wakati mmoja, alikuwa kama mtu ambaye hakuwa amemsikia vizuri.

Upande mwingine nchini Rwanda siku ya jumamosi alionekana Mheshimiwa Jeremy akiingia kwenye chumba chake cha kujisomea ndani ya ikulu upande wa nyumbani , mara baada tu ya kukaa kwenye kiti chake aliwasha runinga na moja kwa moja Kwenda upande wa taarifa za habari za kiuchumi kimataifa, na habari iliomtia wasiwasi Zaidi ni inayohusiana na kampuni ya Edna , baada ya kuangalia hali bado si shwari , alichukua simu yake iliokuwa kwenye Briefcase na kisha akatafuta namba ya raisi Senga.

“Senior nilikuwa nikitegemea simu yako”Aliongea Mheshimiwa Senga upande wa pili wa simu.

“Ndio Senga kwa hali inayoendelea ndani ya kampuni ya Edna , nilikuwa nikivuta muda tu kukupigia”Aliongea.

“Ndio Senior nimeona kinachoendelea”

“Senga Edna anatokaje kwenye hili linaloendelea?”

“Senior niseme kwamba kinachoendelea kwa sasa siwezi kufahamu anaweza kuchukua maamuzi gani ila serikali yangu ipo tayari kutoa msaada usio wa upendeleo kwenye hali kama hii”

“Senga unamaanisha nini usio wa upendeleo, kwa Edna ningetegemea uweke juhudi ya kumsaidia kuiokoa kampuni?”

“Ni kweli , lakini ya wizara ya uwekezaji na biashara wanashauri tusitoe upendeleo kwani kutaibuka migogoro na kuua ushindani na usawa wa biashara nchini jambo ambalohata mimi nimeunga mkono”Aliongea Senga upande wa pili na kumfanya Raisi Jeremy kuvuta pumzi na kuzishusha.

“Naelewa pointi yako lakini hata hivyo tunapaswa kumsaidia , msaada sio lazima uwe wa moja kwa moja , ninachotaka ni benki za Tanzania kuzingatia maombi yake akiomba mkopo”.

“Sawa Senior nitawapa vijana wangu kazi ya kushughulikia hilo swala kwani pia linagusa uchumi wa taifa kwa ujumla , lakini siwezi kukuahidi chochote kutokana na hali yenyewe , tutaangalia maamuzi ambayo Edna atafanya kuikoa kampuni ,ndio nitaangalia namna nzuri ya kumsaidia”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kuvuta pumzi ya ahueni.

“Nitashukuru sana kwa msaada wowote utakao msaidia , naamini Edna atatoka kwenye hio changamoto”Aliongea na kisha wakaagana na akakata simu, lakini wakati huo huo kuna mtu aligonga mlango mara mbili na kisha akasukuma, alikuwa ni mke wake Kizwe alieingia akiwa ameshikilia kikombe.

“Mume wangu nimekuona siku nzima ya sabato leo haupo vizuri . nimekuja kukuangalia kama uko sawa na kukuletea supu ya mzizi wa Ginseng kutoka Marekani , yatakusaidia kurudisha mudi yako wakati ukiendelea kujisomea”Aliongea Kizwe ambaye amevalia suruali nyeusi chini , huku juu akiwa amevalia shati la kitenge , alikuwa amependeza haswa.

Raisi Jeremy alipokea kikombe kile kutoka kwa mke wake na kunywa kidogo na kisha akamwangalia.

“Vipi huyu Desmond kaenda tena Tanzania?”

“Ndio , awamu hii amesema anaenda kuhakikiha anamleta mkwe nyumbani”Aliongea kwa kingereza na kumfanya Raisi Jeremy kushangaa kidogo.

“Unasema ashapata mchumba kutoka Tanzania?”

“Ndio, tena mume wangu nikikuonyesha mwanamke mwenyewe hutoamini , najua unataka Desmond aoe mwanmke wa kirwanda , lakini sidhani kama huyu mwanamke utamkataa kwani ana mafanikio makubwa na anamfaa sana Desmond”Aliongea Kizwe na kisha alitoa simu yake kwenye mfuko wa suruali na kisha akaenda upande wa kuhifadhia picha na akagusa picha iliokuwa ikimuonyesha Edna na Desmond.

Hii ni picha ambayo alipiga Ernest Komwe miezi kadhaa iliopita picha hio ilikuwa ni Desmond akiwa amepiga magoti , huku upande wa Edna akiwa amesimama akipokea burungutu la maua akikabidhiwa na Desmond.

Raisi Jeremy baada ya kuangalia picha ile kutoka kwenye simu ya mke wake alijikuta akitoa jicho kama kabanwa na mlango.

“Vipi hata wewe naona umeshangaa mume wangu , mimi pia nilivyoiona nilipatwa na mshangao , sasa hivi mtoto wetu yupo Tanzania kwa ajili ya kumsaida mchumba wake na shida ya biashara iliompata”

“Mke wangu unamaanisha Desmond, ana… ana mahusiano ya kimapenzi na Edna!!!!?”

“Ndio mume wangu , si ndio maana Desmond yupo nchini Tanzania mara nyingi , ni kwasababu ya penzi lake kwa Edna”

“Hapana haiwezekani huyu Edna ameshaolewa, hata wewe juzi uliona akiweka hilo wazi kupitia mashindano yaliosimamiwa na kampuni yake”

“Mume wangu unaonekana kumjua sana Edna, hata hivyo Edna hawezi kutofautiana na tabia za wanawake wengine huenda anatoka kimapenzi na Desmond kwa siri na ni swala la muda kuweka mahusiano yao wazi”Aliongea huku akiweka tabasamu la kinafiki.

Ukweli huyu Kizwe alikuwa akitaka kumhenyesha mume wake kwa kumueleza Desmond anatoka na Edna , alijua swala hili lingemchanganya sana Jeremy , kwani hakuwahi kuielezea familia yake kama Edna ni mtoto wake na Raheli.

Jeremy hakuwa akifahamu kama mke wake alikuwa akiijua siri yake alioitunza kwa miaka mingi ,siri iliokuwa ikihusiana na mapenzi yaliokuwepo kati ya Raheli pamoja na yeye , mpaka kuchangia kuzaa mapacha.

“Kizwe hili haturuhusu litokee, sitoruhusu Desmond kuwa na mahusiano na Edna”Aliongea huku hasira zikianza kujitengeneza.

“Kwanini mume wangu?”

“Kizwe akili yako sikuhizi imekuwa ndogo , wewe huoni Edna kashaolewa, unafikiri nini kitatokea kama taarifa zikisambaa, mbona umekuwa na akili ndogo namna hii, hata hivyo siamini kama Edna anaweza kumsaliti mume wake”Aliongea Raisi Jeremy na Kizwe alitoa taasamu la kifedhuli.

“Kama mama yake aliweza kutembea na mume wa mtu , Edna anashindajwe kumsaliti mume wake, The Apple doesn’t fall far from the tree”Aliongea kwa kumalizia na usemi kwamba tunda la tufaa halidondoki mbali na mti wake.

“Kizwe unajaribu kuongea nini…?”Aliongea huku mikono ilioshika kikombe ikitetema.

“Jeremy ijapokuwa sijawahi kukuuliza , usijifanye sijui kama ulitembea na rafiki yangu Raheli , niliacha tu kuliongela hili swala kwani uliendelea kunionyeshea mapenzi ninayoyataka na tulikuwa na furaha”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kushangaa na kuwa na wasiwasi kwa wakati mmoja.

“Ulikuwa ukiyajua yote hayo na hukujaribu kuongea chochote?”

“Nishakujibu tayari , sikutaka ndoa yetu iingie doa kwasababu ya Raheli , najua mliachana baada ya yeye kuolewa na kumzalia Adebayo mtoto”Aliongea Kizwe na kumfanya Jeremy kuvuta pumzi mpaka hapo alishukuru kitu kimoja, aliamini Kizwe hakujua kama Edna ni mtoto wake.

“Mke wangu naomb….”

“Shshiii…Jeremy hayo mambo yalishapita na nilishakusamehe muda mrefu tu ndio maana nikakaa kimya huna haja ya kuomba msamaha”Aliongea Kizwe na kumfanya Jeremy kuvuta pumzi.

“Asante sana mke wangu.. kwa kuvumilia kukengeuka kwangu , hakika wewe ni mke mwema sana”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu.

“Usijali Jeremy…. Muda mwingine watu hufanya makosa na nilishukuru sana baada ya kuona mapenzi yenu yaliisha baada ya Raheli kuolewa”Aliongea huku akimsogelea karibu.

“Yeah Mke wangu , najua kipindi kile zilikuwa tamaa tu , lakini niliachana nae kabisa”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu na kisha kugeukia runinga iliokuwa ikitangaza hali mbaya ya kampuni ya Vexto.

“Mume wangu kesho natarajia Kwenda Tanzania kibiashara unaonaje nikitumia safari hio angalau kumsaidia Edna , Raheli alikuwa ni rafiki yangu licha ya kunisaliti , lakini kutokana na historia yangu sidhani kama nitajisikia vizuri kuona kampuni alioipigania kufilisika,nitajaribu kumuunganisha na meneja mmoja wa benki kumsaidia mkopo, Unaonaje mume wangu au tusiingilie?”Aliongea Kizwe na kumfanya Jeremy kumwangalia mke wake usoni kumsoma maneno yake kama yana ukweli ndani yake na hakuona dalili yoyote ya unafiki kwenye macho ya mke wake.

“Uko siriasi?”

“Mume wangu , ulifikiri nitamchukia Edna kwasababu ya historia yenu na Raheli , yule mtoto yeye hana kosa lolote “Aliongea na kumfanya Jeremy kutabasamu na kisha akamsogelea mke wake na kumshika mkono.

“Ni miaka mingi sasa imepita , tumepitia milima na mabonde , nashukuru sana mke wangu kwa kuendelea kuwepo kwenye Maisha yangu , sasa hivi najikuta kuwa mwenye hatia kwa jinsi ulivyonivumilia, Mke wangu naomba unisamehe kwenye siku zote ambazo sikukufanyia vyema kama mume wako, kama kuna namna yoyote ya kumsaidia Edna nakuruhusu ufanye hivyo”Aliongea Jeremy.

“Usijali mume wangu , ninachokifanya ni kukusapoti wewe kwa kila kitu”Aliongea na baada ya dakika kadhaa tu alitoka kwenye chumba hicho akimuacha Jeremy.

Kizwe mara baada ya kutoka nje alitabasamu kinafiki huku akigeukia mlango wa chumba cha kujisomea na kisha aliendeleza safari yake , tabasamu lake ni kama lilikuwa likimwambia Jeremy kwamba utanikoma.

Upande wa Raisi Jeremy baada ya mke wake kutoka alimpigia simu Linda na kumpa maelekezo ya Kwenda Tanzania na kumrudisha Desmond nyumbani, Raisi Jeremy licha ya kwamba aliamini hakuna mahusiano yoyote ya Edna na Desmond lakini aliamini huenda Desmond akawa na harakati za kumtongoza Edna , hivyo alitaka kuepusha hali ya Kaka kumtongoza dada yake.
 
SEHEMU YA 368.

Siku ya jumatatu mchana hali iliendelea kuwa mbaya kwani licha ya kwamba Edna alitoa maagizo ya hisa za kampuni kununuliwa mafungu mafungu , lakini bado hali haikutengemaa kutoka na mwelekeo wa chini wa soko, lakini mbinu hio waiendelea nayo , idara ya fedha ilihakikisha wananunua hisa za kampuni kila baada ya dakika kumi na tano kwa mafungu ya tahamni ya dola elfu moja kwa akaunti mia moja na upande wa idara ya ‘public relation’ inayoongozwa na Benadetha walikuwa wakiwasiliana na wawekezaji kutoendelea kujiondoa kwenye kamupuni huku wakiwahakikishia kwamba mambo yatakuwa mazuri , kwani kampuni inafanya kila linalowezekana.

Muda wa mchana wafanyakazi baadhi wa ngazi za juu walikuwa kwenye ukumbi wa mikutano wakiendelea kuangalia namba zilizokuwa zikionekana kwenye skrini , Edna ndio aliekuwa kiongozi wao.

Wakati wakiendelea kukodolea macho yao kwenye skrini, mlango ulifunguliwa na kuwafanya wote kugeuka kuangalia nani anaingia na alikuwa ni Roma, na wote walimwangalia kwenye mikono yake , kwani harufu nzuri ya vyakula ilisambaa mara tu baada ya kuingia hapo ndani , sasa ukizingatia wengi wao walikuwa na njaa kutokana na ubize kutowaruhusu kula siku hio walijikuta wakimezea mate harufu.

Edna alimwangalia Roma kwa namna isioelezeka , huku wafanyakazi wengine pia wakimwangalia , ijapokuwa Roma kaingia bila kugonga lakini hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kuongea nae chochote , kwani walikuwa wakifahamu ni mume wa boss wao.

“Hahaha… kwa jinsi mnavyoniangalia naamini hamjakula kabisa chakula”Aliongea huku akisogea na mifuko yake mingi na kisha kuweka juu ya meza kwa kila mfanyakazi.

“Mr Roma umetuletea nini?”

“Nimewaletea chakula cha mchana”Aliongea Roma huku akiendelea na kazi yake ya kugawa na baada ya wafanyakazi kugundua Roma kaleta chakula wote walifungua ndani na kukutana ni kuku wa KFC.

Kila mmoja alionekana kuwa na njaa lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kuanza kula na wote walimwangalia Edna , ni kama walikuwa wakiomba ruhusa.

“Msiniangalie mnaweza kula”Aliongea Edna na wafanyakazi wote kwa furaha kila mmoja alichukua kifurushi cha kwake.

“Babe na wewe cha kwako hiki?”Aliongea Roma akimkabidhi Edna.

“Mbona cha Benadetha kifungashio chake ni kikubwa kuliko changu?”Aliongea Edna na kumfanya Benadetha kukagua shea yake aliopewa na kugundua ni kwei yeye kifungashio chake kilikuwa kimetuna sana kuliko vya wengine na alijikuta akiona aibu huku akimwangalia Roma.

“Benadetha mwenzio ana baba na amenipigia simu nimuangalie mtoto wake kwa ukaribu na ndio ninachofanya , hata akikosa kazi hapa kwenye kampuni bado ana baba wa kumjali, kuhusu wewe upo na mimi mumeo tu , ikitokea kampuni imefilisika tutarudi mbagala tukaambizane kubeba mizigo, kuna muda tunaweza akukosa chakula pia, hivyo nakuzoesha mapema”Aliongea Roma huku akitabasamu lakini alijikuta akimfanya Edna kuona aibu utani wa Roma kwani kulikuwa na wafanyakazi wenzake.

“Kama ni hivyo bora nisile kabisa”

“Kama hutaki kula basi nitampa Dorisi akusaidie, nimepata tabu kukuleta chakula lakini hutaki kula”Aliongea Roma huku akichukua chakula cha Edna.

“Wewe usikiondoe , sijala na mimi chakula cha mchana”Aliongea Edna huku akimpokonya Roma na kukiweka mezani na kumfanya Roma kutabasamu,, sasa baada ya kumaliza kuwapa watu wote ,vyakula vilionekana kubaki na alisogea mpaka sehemu alipokaa mke wake nakuweka vifuruhi vitatu chini, halafu akawaangalia wafanyakazi walivyokuwa wakifurahia mapaja ya kuku ya KFC huku wakiongea.

“Natoa tangazo mapema , hakuna mtu anaruhusiwa kuchukua tena hivi vilivyobaki , vyote ni vya mke wangu , atakaegusa nitahakikisha namtupia nje ya jengo”Aliongea kwa sauti na kufanya wafanyakazi wote kumwangalia kwa mshangao lakini waliitikia wote kwa pamoja, huku wengine wakiishia kutabasamu.

Roma aliekuwa amesimama karibu na Edna alijishtukia akipigwa na kisigino cha kiatu kwenye mguu na alipangalia ni mke wake aliempiga kisirisiri , Edna alikuwa mwekundu kama nyanya huku akiona aibu.

Roma alichukua baadhi ya mifuko mingine aliokuja nayo ambayo pia ilionekana kuwa na kuku wa KFC kwa kuanza safari ya kuondoka.

“Unaenda ofisini kwa Nasra?”

“Mke wangu unaonekana kuwa na akili , nampelekea na yeye chakula”Aliongea Roma.

“Mh! Unaonekana kumjali?”

“Nitafanyaje sasa, mumeo ni mtu bize sana baada ya hapa nampelekea Amina, ndio alienipa hili wazo la kuwaletea chakula ili mshibe muendeleze mapambano”Aliongea Roma.

“Okey unaweza Kwenda”Aliongea Edna huku akigeuzia macho yake kwenye chakula na Roma alitoka na baadhi ya mifuko yake huku akimfanya Dorisi na Benadetha kumwangalia Edna na kisha wakaishia kutabasamu.

Baada kama ya lisaa la wafanyakazi kushiba chakula kilicholetwa na mume wa Edna, kikao kiliendelea.

“Boss Edna kesho mnada wa majengo mradi wa hoteli ya kampuni ya Adani utafanyika, naulizia kama tutaendelea kuhusika katika mnada huo kutokana na maelekzo uliotoa wiki iliopita?”Aliuliza moja ya mfanyakazi wa kiume alievalia suti ya bluu.

“Hela niliotenga kwa ajili ya ununuzi uendelee kama kawaida na hakikisheni tunaweza kushinda kwenye mnada huo wewe na timu yako , malengo ya kupata mradi huo sio majengo bali ni ardhi inayozunguka miradi yote”Aliongea Edna akijibu huku akiangalia kishkwambi chake.

“Boss Edna kwa hali inayoendelea sasa hivi , kwanini hela zote tusizielekeze kwenye kuokoa kampuni , kuliko kutupa hela zote kwenye miradi ya Adani?”Alishauri moja ya mfanyakazi wa kike.

“Boss Edna naunga mkono hoja, hatuwezi kuendelea na mradi huu kwani hakuna faida tena kama kampiuni itaendeleakuwa kwenye matatizo”Aliongea mwingine.

“Naelewa hofu yenu , lakini huu ndio mradi ambao tulipanga kuanza nao kwenye mwanzo wa mwaka 2023, hatuwezi kughairisha na tukifanya hivyo ni kuwatangazia maadui zetu kwamba tumeshindwa tayari, hata wafanyakazi wetu wanaopambana pamoja na sisi watakosa Imani ya kuendelea”Aliongea na wote walionekana kumuelewa.

Muda huo huo aliingia mfanyakazi wa kike ambaye alionekana kuwa na wasiwasi kwa kumwangalia tu na kufanya wafanyakazi wote wa juu hao wa kampuni kumwangalia.

“Boss Edna , devastating news. A few of our major shareholders are threatening to change the CEO, or they’ll sell their shares at filthy-low prices!”

“Boss Edna , Habari ya kutisha , baadhi ya wanahisa wakubwa wa kampuni wanatishia kuhitaji mabadiliko ya CEO au watauza hisa zao zote sokoni kwa bei ya hasara”Aliongea mwanadada huyo na kufanya watu wote kuashangaa huku zogo likiamka.

Unachotaka kujua hapa ni kwamba Edna baada ya kuuza hisa Zaidi ya asilimia arobaini zote, zilinunuliwa na baadhi ya wafanyabiashara wengine ,kwa maana ya kwamba asilimia arobaini ya hisa za kampuni zilikuwa zikimilikiwa na mtu mmoja mmoja huku asilimia kumi inayobaki ikimilikiwa na wachuuzi wadogo wadogo wa hisa.

Sasa hawa wamiliki wa hisa wenye asilimia arobaini wanyohaki ya kumchagua CEO wanaemtaka ndani ya kampuni kwa kupiga kura , lakini kwasababu Edna anamiliki asilimia hamsini inamaanisha kwamba akikataa basi wanahisa hao wote watalazimika kuuza hisa zao kwasababu hawana Imani na CEO na kama wataziuza zote sokoni ni kwamba soko litazidi kushuka thamani.

Sasa kwasababu kampuni ya Vexto imeoridheshwa kwenye soko la hisa la kimaataifa la Marekani ,NASDAQ, kama thamani ya soko ikivuka vigezo vya kuendelea kubakia sokoni kwa taratibu za Nasdaq inakuwa ‘Delisted’(Ondolewa katika orodha) kwa maana kwamba inatangazwa rasmi kufilisika.

Sasa swali je Edna atakubali kuachia ngazi kama CEO na kuacha wanahisa wasiuze hisa zao , au ataendelea kushikilia hisa zake na kampuni iondolewe katika soko la kimataifa na kutangazwa rasmi imefilisika?”

SEHEMU YA 369

Wafanyakazi wote waliokuwa ndani ya ukumbi wa mikutano walizubaa na kushangaa kwa wakati mmoja , walijiuliza kwa wakati mbaya kama huyo nani angeweza kufikiria kubadilisha CEO wa kampuni?.

“Nadhani ni jambo la kawaida , wamenunua hisa zetu kwa mamilioni ya pesa na sasa hisa zimeshuka thamani kwa Zaidi ya asilimia therathini ni haki kwa upande wao kupatwa na wasiwasi”Aliongea mfanyakazi mmoja.

“Waambie kama wanataka kuuza hisa zao wafanye hivyo , siwezi kuwazuia kufanya watakavyo na siwezi kutoka kwenye nafasi yangu”Aliongea Edna kibabe akimwagiza yule mfanyakazi aliekuja kutoa taarifa.

“Boss Edna , unamaanisha tunashindana nao moja kwa moja , naona kama sio jambo zuri”Aliongea mmoja wapo na Edna alimwangalia.

“Kwahio unataka niachie nafasi yangu?”Aliuliza

“Boss Edna unaonaje ukaniruhusu mimi niongee nao , kama wataziuza kweli hisa zote asilimia arobaini tutafilisika kweli”

“Hapana waache wafanye wanachotaka , wamenunua hisa zetu kwa thamani kubwa unafikiri ni wajinga kuziuza zote kwa wakati mmoja wapate hasara”Aliongea Edna na kufanya wafanyakazi wote kuvuta pumzi ya kukata tamaa , licha ya kwamba hawakuridhika na maamuzi ya Edna lakini hawakuwa na uwezo wa kumpinga kwani kama kampuni itaingia hasara atakae filisika ni Edna na maamuzi yake ni pesa zake, kwani alikuwa akimiliki Zaidi ya asilimia hamsini ya hisa zote za kampuni.

Upande mwingine mara baada ya Ernest kufahamu kama Monica ni mjamzito , ni kama mapenzi yake yaliibuka upya kwa mwanamke huyo , kwani alianza kumjali na kumbembeleza asiondoke , lakini hata hivyo Monica alitaka tu kuondoka muda wote, lakini kwakua hakuwa na nafasi ya kuchoropoka kwenye mikono ya Ernest , basi aliendelea kubaki hapo hapo mpaka alipokuja kupitiwa na usingizi na alipokuja kuamka ilikuwa ni jioni.

Alijishtukia akiwa kitandani tofauti na sehemu aliopotelea usingizini kwenye sofa , kwani mara ya mwisho alikuwa eneo la sebuleni akiwa na Ernest mpaka kupitiwa na usingizi , dakika chache tu akiwa ndio anajiandaa kushuka kitandani mlango wa chumbani ulifunguliwa na Ernest aliingia huku akiwa na bakuli ambalo ndani yake ilionekana kuna uji wa lishe.

“Monica naomba unywe huu uji japo kidogo tu , hujakula tokea asubuhi na tumboni unakiumbe kinachokuwa”Aliongea huku akimuwekea karibu.

“Sitaki kunywa wala kula chochote nataka uniachie niondoke Ernest”

“Monica huwezi kuodoka , sasa hivi najua washajua kama mimi ndio nimevujisha nyaraka zile na nikikuachia lazima utawaambia nilipo , hivyo nakuahidi kila kitu kikitulia nitakuachia uondoke , ila kwa sasa naomba unywe huu uji kidogo upate nguvu”Aliongea kwa upole huku akimsogezea Monica alimwangalia Ernest usoni kwa sekunde na kisha akapokea kivivu.

“Usijisumbue sana ,ngoja nikunyweshe”Aliongea huku akiweka pembeni lile bakuli , jamaa alionekana kumjali mno Monica , huenda ni kwasababu ya ujauzito wake.

Upande wa mita kadhaa kutoka , kwenye hoteli maarufu iliokuwa ikiangaliana na jumba hilo , ndani ya chumba cha hadhi ya raisi, Adeline na Fanny walikuwa wameweka Darubini zao kuelekea upande wa jumba analoishi Ernest, kwa jinsi walivyoseti mitambo utadhani wanaangalia nyota angani , kila baada ya dakika walikuwa wakiangalia kupitia darubini hizo , kutokana na jengo walilokuwepo kuwa refu basi iliwawezesha kuona kila kinachoendelea ndani , ijapokuwa hawakuweza kumuona Ernest , lakini waliamini bado yupo ndani ya jumba hilo na walichokuwa wakusbiria ni ruhusa ya mfalme Pluto tu kuchukua nafasi yake.

Roma alishawapa maelezo kwamba wasifanye chochote kile, aliwaambia kwamba lazima Ernest kuna watu anashirikiana nae hivyo lazima wangefika hapo mafichoni , hivyo alitaka kumkamata kila mmoja na ndio maana hakuchukua hatua yoyote.

Upande wa kampuni ya Edna mapambano ya kuokoa kampuni yaliendelea , jambo moja ambalo waliweza kufanikiwa ni kulifanya soko kutoshuka wala kupanda yaani , chati yake ilikuwa ikienda mlalo ikimaanisha kwamba thamani ya hisa ilikuwa iki ‘ Consolidate’, wafanyakazi wote walisubiri mpaka muda ambao soko linafungwa na ndio kila mmoja sasa akapata nafasi ya kurudi nyumbani , Edna akiwa bado hajaanza safari ya kurudi nyumbani alipigiwa simu na Roma kwamba amsubiri anakuja kumchukua na Edna alitii na ndani ya madakika kadhaa tu Roma aliweza kufika ndani ya kampuni na kumchukua Edna kwa ajili ya kumrejesha nyumbani , muda huu ilikuwa ni saa kumi na mbili inakwenda saa moja.

Edna alionekana kuchoka kweli , kwani baada ya kukaa tu kwenye gari usingizi ulimpitia na hata anatoka kwenye gari baada ya kufika nyumbani alikuwa na usingizi kutokana na tembea yake.

Blandina baada ya kumuona Edna alivyochoka alijikuta akimuonea huruma na sio yeye tu hata Bi Wema pia alimuonea huruma.

“Jamanii , jamanii ,,, muangalie alivyochoka Edna najua changamoto zipo lakini afya yako lazima iwe kipaumbele , kwa staili hii unaweza kuzimia kazini”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kutabasamu kwa jinsi mama yake alivyokuwa na wasiwasi , alijiambia alifanya vizuri sana kutowaambia kilichomtokea Edna siku ya jumamosi, juu ya kuwekewa sumu wangekuwa na wasiwasi zaidi.

“Mama na Bi Wema msiwe na wasiwasi , nipo sawa ni uchomvu tu”Aliongea Edna lakini wote walionekana kutoridhika.

“Roma mshike mkono umpeleke juu akalale, angalia asije akadondoka kwenye ngazi”Aliongea Blandina.

“Mama usijali nitamsindikiza , napanga pia kumuogesha”Aliongea Roma na kumfanya Blandina kumfinya kwenye mkono, Lakini Roma jicho alililopigwa na Edna lilitosha kumuacha kutoendelea kuongea.

“Mpeleke mwenzio akampumzike , sio muda wa utani huu”Aliongea na Roma alimchukua Edna na kumpeleka mpaka ndani ya chumba chao, ukumbuke Roma alikuwa akilala na Edna kwa siku kadhaa licha ya kwamba hawakuwa wakifanya chochote na walikubaliana wataanza kufanya mapenzi siku ambayo watafunga ndoa ya pete, yaani wabatilishe ile ya mkataba na wafunge ndoa upya ya kanisani,ijapokuwa ilikuwa ngumu kwa Roma kuweza kumvumilia mwanamke mrembo kama Edna kulala nae kitanda kimoja pasipo kumgusa , lakini aliruhusu upendo wake kuchukua nafasi ,kwamba hawezi kumfanyia Edna kitu ambacho hayupo tayari, lakini upande mwingine Roma aligundua kulala chumba chake mwenyewe ilikuwa vyema sana kuliko kulala na mke wake na alijiambia hata kama awe anapewa kitumbua na Edna kulala nae itakuwa changamoto, kwani hatakuwa akipata nafasi ya kulala na wanawake wengine, lakini usiku mmoja alipokuwa amelala na Edna akifikiria swala hilo alijikuta kuna mbinu ilimjia akilini mwake na kumfanya atabasamu kifedhuli.

“Mama Lanlan yuko wapi?”Aliuliza Edna mara baada ya kupiga hatua kadhaa Kwenda juu.

“Kalala huyo baada ya kucheza gemu na kuchoka, mwakani inabidi umfanye utaratibu umuanzishie masomo”Aliongea Blandina.

“Ndio mama napanga tutalijadili hilo , kuangalia ni shule gani inamfaa”Aliongea Edna na Blandina aliitikia kuunga mkono.

“Niache sasa nipumzike”Aliongea Edna mara baada ya kukaa kitandani , lakini Roma alimsogelea na kumshika mkono huku akimpa ishara ya kutulia kimya, na Edna alijikuta akihisi mkono wake kuwa wa moto na baada ya dakika chache tu alijikuta mwili wake ukipata msisimko wa ajabu, ni hisia flani hivi kama damu za moto zilikuwa zikiingizwa kwenye mwili wake na ndani ya dakika kama tano tu , mwili wake ulitoka uchomvu wote na kumfanya kushangaa..

Edna alkumbuka hata juzi yake Roma alivyoweza kumponyesha sumu iliokuwa kwenye mwili wake , ijapokuwa siku ile hakuuliza ameponaje , lakini aliamini Roma ndio kafanya kazi yote , si alikuwa anajua bwana mume wake sio kiumbe cha kawaida ,ndio maana hakupenda sana kuuliza maswali.

“Kumbe una mbinu zako kuniponyesha uchomvu kwanini usingenifanyia hivi kule kule ofisini?”

“Kama ningekufanyia hivi kulekule ofisini usingerudi nyumbani,”

“Kwa hali ile inayoendelea kwenye kampuni ulifikiri napenda hata kukaa masaa mengi hapa nyumbani, nilighairisha baadhi ya mambo muhimu kwasababu nilichoka na nilihitaji kupumzika”

“Hata kama ulitakiwa kurudi nyumbani kwanza wanafamilia wakuone, Lanlan ni mtoto na hawezi kukaa muda mrefu pasipo ya kukuona, labda uwe umesafiri”Aliongea Roma na kumfanya sasa Edna apatwe na hamu ya kumuona Lanlan.

“Ninaenda kumwangalia Lanlan mara moja na nitarejea ofisini kuendelea na kazi”Aliongea.

“Unataka kurudi kweli?”

“Ndio nilirudi kupumzika kwasababu nimechoka na sasa ushanipatia dawa yako ya mazingaombwe inabidi nirudi”

“Okey! Basi nitakurudisha kama unataka kurudi”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa na kisha alitoka na Kwenda kwenye chumba cha Qiang anacholala na Lanlan.

Baada ya kufungua mlango kuingia , Qiang Xi na yeye alioenakna kuwa usingizini huku Lanlan akiwa amemuwekea mguu kwenye shingo akiwa hana habari , alikuwa amelala fofofo.

Edna baada ya kuona Lanlan anamuumiza mlezi wake alimuweka sawa kwa kumnyoosha vizuri na kisha alimpiga busu na kutoka kwenye chumba hiko na wakaungana na Roma na kushuka tena chini sebuleni kuaga.

Sasa Blandina na Bi Wema mara baada ya kumuona Edna anashuka akiwa mpya walishangaa na hata walipoaga wanaondoka tena walishindwa kuwazuia na kuwauliza pia imekuwaje usingizi ukaisha ghafla.

Edna alimwangalia Roma aliekuwa akiendesha gari na kujikuta akijisikia vizuri , kwenye wakati mgumu kama huo ilikuwa ni vyema sana kuwa na mtu wa kumtegemea na hivyo ndio kilimfanya kuwa na amani juu ya uwepo wa Roma.

“Mbona kama hunipeleki kazini , kwa ninavyokujua kitendo cha kuniponyesha uchomvu usingekifanya kama ungekuwa na madhumuni ya kuniacha nipumzike”Aliongea Edna wakati wakiwa barabara ya Haile selasie..

“Hilo halina umuhimu kwa sasa ,ninachokifanya muda huu ni kukuonyesha nadharia yangu juu ya watu kwenye kampuni yako ambayo hawana nia njema kwako”Aliongea Roma na kumfanya Roma kushangaa kidogo.

“Mbona unachukua muelekeo wa huko?”Aliuliza Edna baada ya Roma kukunja kulia akiachana na Tunisia Road akichukua barabara ya Bagamoyo kwenda Mwenge na Roma alimwambia atulie kuna kitu anataka kumuonyesha.

Dakika kama kumi tu hivi wakati wanafikia karibu na jengo la hoteli ya Kebbys ghafla ilitokea gari mbele yao ikija kwa spidi sana ikiwa mwelekeo tofauti na wa kwao , yaani kwamba wao wakiwa upande wa kushoto mwa barabara upande wa jengo la hoteli yenyewe ilikuwa katikati ya barabara ambayo bado ilikuwa chini ya ujenzi, ilikuwa ni gari kubwa hizi za ujenzi(Concrete Mixer Truck) ambazo zinatembea na bodi kama pipa muundo wa yai juu hivi ambalo linazunguka , sasa hata watu waliokuwa karibu na hayo maeneo ya Sayansi walijikuta akishangazwa kwani gari ilikuwa na spidi.

Upande wa Roma hio gari alikuwa ameiona muda mrefu tu , wakati yeye akikucnja kuingia Bagamoryo Road gari hio ilimuovertake na kumpita kwa spidi, kwa tafsiri nyepesi ni kwamba hio gari ilienda kugeuza. Muda huo magari mengi yalipungua sana barabarani na mengi yalikuwa ni daladala hivyo ile gari bara baada ya kufikia usawa wa gari yao ilipiga msele kuisogelea gari hii ya Edna ,Mercedenz Benz ambayo muda huo ilikuwa ikiendeshwa na Roma.

Edna mwenyewe aliona gari hio na moyo wake ulipiga kite lakini alikuja kupagawa mara baada ya kuiona gari hio ikiwalenga na ile inawakaribia kwa minajili wa kuwagonga ubavuni upande wa kulia alijikuta akiifumba macho yake na kuinama chini asione kinachokwenda kutokea.

Roma alikuwa mtaalamu kweli , alikuwa ni kama aliitegemea hio gari kwani ile inamkaribia kwa spidi kwa nusu mita tu alipitisha gari yake kwa spidi kubwa kama risasi na kisha akakanyaga breki na Edna alipokuja kufumbua macho walikuwa hai , aijikuta akiangalia nyuma na kuona ile gari imepitiliza upande wa pili wa barabara na Kwenda kuvamia ukuta, ilionekana dereva hakutegemea , hivyo akashindwa kuiongoza na kuvaa ukuta na kilichoonekana ilikuwa ni vumbi tu na moshi uliokuwa ukitoka kwenye lile gari.

Edna baada ya kupona kwenye mshitiko alijikuta akimwangalia Roma kwa wasiwasi sana.

“Ulifahamu kuna mtu alikuwa akinifuatilia si ndio?”Aliuliza Edna huku akihema kwa nguvu kiasi kwamba pumzi zake Roma aliweza kuzisikia

“Hili sio tu kukudhuru wewe bali hata mimi pia nililengwa , walishindwa kukuua kwa sumu hivyo niliamini lazima kuna mtego mwingine ambao unaandaliwa kwa ajili yako na niliamini kwa vyovyote hauwezi kufanyikia ndani ya kampuni ili kuzima Ushahidi bali nje ndio maana nikakuambia nakuja kukuchukua kukurudisha nyumbani”.

“Wakati nakurudisha nyumbani kuna gari iliokuwa inatufatilia nyuma na hata tulivyoanza safari tena ya kurudi ilikuwa mita kadhaa kutoka getini kwetu, ndio maana nilipofika hapa nilikatisha upande huu , nilitaka kupeleka gari sehemu salama Zaidi ambayo haina watu , lakini naona wamekosa uvumilivu na kutaka kufanyia ajali hapa katikati ya jiji”Aliongea tena na kumfanya Edna kushangaa Zaidi.

“Nilidhani Ernest ananitaka mimi tu kwenye mipango yake ili ikamilike, kwanini na wewe akataka kifo chako?”

“Babe usisahau mimi ni mume wako kihalali, ikitokea unaumwa au kupatwa na shida yoyote unadhani nani anaweza kurithi kampuni yako , ilihali wewe mwenyewe ndio ulianza kunifanya niongoze kampuni ya Vexto Media?”Alliongea Roma na kumfanya Edna kweli aone ni pointi, ni kweli kwamba mpaka muda huo hakuna mrithi wa kampuni na chochote kikimtokea basi ni dhahiri Roma angekuwa kwenye nafasi yake.

“Babe au hujaandika wosia bado , kama hujafanya hivyo uanze mchakato mapema na uandike jina langu , Roma Ramoni”Aliongea Roma kiutani.

“Muda kama huu unapata wapi ujasiri wa kuongea utani wakati tumepona kwenye kifo, hata niandike wosia siweki jina lako, halafu ungepata hasara gani kama ungenielezea huu mpango tokea kule kwenye kampuni?”

“Babe wangu Edna , nadhani mpaka hapa sasa unamchukia Ernest sasa kiasi cha kutaka kumuua?”Aliongea Roma huku akiendelea na safari akiacha watu walioanza kuzunguka gari lile.

“Simchukii kwa kufikia levo ya kutaka kumuua hata hivyo mpaka sasa nashindwa kujua ni sababu gani ipo nyuma yake ya kutaka kuona nikianguka kibiashara”

“Amejaribu kukuua Zaidi ya mara mbili , lakini haumchukii kwa kiwango cha kumuua , mimi upande wangu naona kifo ndio adhabu inayomfaa”

“Najua una wasiwasi sana na Maisha yangu , lakini kwa upande wangu bado msimamo wangu upo kwenye sheria za nchi kufuata mkondo wake , kama tumtamuua tu bila kuzingatia chochote si inatufanya na sisi pia kufanana nae , wote tutakuwa wauaji kama yeye tu”

“Kwanini unapenda kuzungumzia mambo ya sheria za nchi wakatu huyo mjinga anataka kukuua kwa nafasi yoyote ambayo ataipata?”Aliuliza Roma.

“Mimi sio kama wewe , ninao uwezo wa kuangalia washindani wangu wa kibiashara wanapoteza wananishindwa na kupoteza hela zao au kufilisika kabisa , lakini kuwaua ni jambo ambalo siwezi kufanya , I am just businesswoman , I can’t soak my hands in blood, I know I sound just all sappy right now , and you can be impatient with me but I can’t just do it”Aliongea Edna huku akimalizia kwa kingereza akimaanisha kwamba hawezi kuloanisha mikono yake na damu , ijapokuwa anaongea kinyonge muda huo na yeye Roma anaweza kukosa Subira juu yake , lakini hawezi kuua mtu.

Unafikiri Edna kweli hawezi kuua mtu , ngoja tuone msimamo wake.
 
SEHEMU YA 370.

Roma alijikuta akitabasamu kwa uchungu kutokana na maneno ya Edna , aliamini wanawake wengi wako hivyo kuwa na moyo mwepesi sana , hivyo kuua kwao ni jambo gumu sana kufanyika kwa upande wao.

“Wanawake wote mko hivyo lakini kama angekuwa Rose ingekuwa Habari nyingine , angetuma watu wake wamletee kichwa tu, kwenye sinia”

“Wewe subuthuu., usimtumie Rose kuniamsha nakuambia , Siwezi kuwa kama yeye,harafu hujaniambia Ernest yuko wapi , si ulisema vijana wako wanamfatilia?”

“Kama bado anaishi hilo sio jambo la kuwazia kuhusu kuwa nyuma ya nondo sasa hivi, ninachokifanya sasa hivi nikumuwekea mtego mhusika mkuu , usiwe na waasiwasi , usalama wako ni wajibu wangu”Aliongea Roma na Edna alitingisha kichwa na kukawa na kimya cha muda mfupi mpaka walipokuja kusimamisha gari pembeni ya mgahawa mmoja maarufu uliofunguliwa hivi karibu na shule ya Makongo.

“Nisubiri kwenye gari nitachukua ‘Take away’ na utakula huku tunaelekea kwenye kampuni”Aliongea Roma huku akifungua mkanda wa gari na kabla Edna hajajibu Roma alishatoka na ndani ya madakika kama kumi na tano Roma alirudi na vyakula vya Edna, sasa kitendo cha Roma kwenda kuhangaika kununua chakula akiwa yeye amekaa tu kwenye gari ni kama kilimfanya kujisikia vibaya kama mke.

“Roma nadhani unaniona kama mwanamke ambaye sina vigezo vya kuwa mke .nimekaa hapa ila wewe ni wa kuhangaika tu kwa ajili yangu na kukupa maagizo kama vile bosi kwako?”Aliongea Edna kwa kulalamika.

“Acha kufikiria mbali , kama unao uwezo wa kunivumilia mumeo na michepuko yangu niweze kusema nini juu ya hili dogo , hata hivyo kwa namna yoyote ulivyo nakukubali kama mke wangu , si ndio maana ya ndoa, kuchukuliana madhaifu yetu?”Aliongea Roma na kumfanya Edna kutabasamu na kisha akatingisha kichwa kukubaliana nae.

Upande mwingine siku hio hio mchana ndani ya jiji hili la Dar es salaam , alionekana First Lady akiingia ndani ya jengo moja refu lililokuwa mtaa wa posta ya Zamani , yaani kivukoni akiwa ametangulizana na mwanadada mmoja ambaye alionekana kuwa ni msaidizi wake , alievalia suti nyeusi iliomkaa vyema mwilini , kwa upande wa First Lady pia alikuwa amevaa suti ya rangi nyeupe ambayo ilimkaa vyema sana ukijumlisha na urefu wake.

Alikuja kuingia kwenye moja ya chumba ambacho kilionekana kuwa ni cha mikutano ndani ya jengo hili baada ya kutoka kwenye lift , na hio ni kutokana na kwamba ndani yake kulikuwa na wanaume kwa wanawake , jumla wakiwa kumi wakiwa wamevalia kinadhifu kabisa, ambao wana sura za kibosi.

Watu hao wote walikuwa ni wafanyakazi wa benki,matawi ndani ya Tanzania , haikueleweka aliwezaje kuandaa kikao hicho ndaji ya jiji la Dar e salaam , lakini watu hao walionekana kumheshimu mara baada ya yeye kuingia hapo ndani kwani walisimama wote kwa pamoja kwa ajili ya kumpa heshima yake.

Sasa jambo moja ambalo unatakiwa kulifahamu hapa ni kwamba gavana wa benki ya Tanzania ambaye ni mchepuko wa Matilda alikuwa ni ndugu yake Kizwe anaeishi hapa Tanzania na ni kwakutumia koneksheni zake ndio maana aliweza kumfanya kuwa gavana wa benki , sasa hata Matilda aliweza kukutana na First Lady kupitia gavana wa benki huyo.

Sasa tunaweza kuona kwamba inawezekana kikao hicho cha wakuu wa benki kiliandaliwa kwa msaada wa gavana mkuu wa benki za biashara ndani ya Dar Es salaam.

“How are things going regarding the incident at Vexto International?”

“Mambo yanakwendaje ndani ya kampuni ya Vexto mpaka sasa?”Aliuliza mara tu ya kuketi.

“Asante madam kwa kuuliza , hisa za kampuni ya Vexto zimeshuka thamani kwa Zaidi ya asilimia therathini na tano mpaka sasa hali yao sio nzuri kwao, kuvuja kwa nyaraka za siri imekuwa msumari wa jeneza kwa kampuni yao”Aliongea mwanaume mmoja mzeee hivi.

“Kwa uwepo wenu hapa ,wafanyakazi wa juu ambao mna ujuzi wa kutosha katika maswala ya uchumi , nataka kujua kama kuna uwezekano wa kampuni ya Vexto kushinda hali hio?”

“Ashaukumu sio matusi madam, kwa hali inayoendelea ndani ya kampuni mpaka sasa mtu yoyote mwenye ujuzi wowote wa maswala ya hisa ataona kwamba zitashuka Zaidi ya asilimia hamsini, ni Mungu pekee ambaye anaweza kubadilisha hali yao , labda tu kama watakuwa na Zaidi ya dola bilioni tano za akiba na kuwa na ujasiri wa kuziingiza zote kwenye biashara ya hisa, ndio njia pekee ya kuweza kutoka kwenye hali waliokuwa nayo , lakini naamini hawana hicho kiasi kwani wangekuwa nacho wangeshakiingiza sokoni”Aliongea mmoja wao na wengine wote walikubaliana nae.

“Kama ni hivyo basi niende moja kwa moja kwenye dhumuni la kutaka kuonana na ninyi wote hapa , sitaki kwa kila mmoja wenu kuisaidia kampuni ya Vexto kwa aina yoyote ya mkopo”Aliongea kwa kujiamini na kufanya watu wote kushangaa huku wakiangaliana

“Tulidhani umetuitia kwa ajili y a kuongea namna ya kuisaidia kampuni ya Vexto , kwani ndio namna taarifa zilizotufikia Madam”Aliongea mmoja wao.

“Nadhani wote mnafahamu ni kwa namna gani mume wangu amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye upanuaji wa biashara zenu za miamala hapa nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla na wote nyie mpo kwenye nafasi zenu kutokana na juhudi za serikali ya Rwanda, ninachowaambia hapa sio kwamba mnatenda makosa kisheria , kwani hata hivyo kampuni ya Vexto ndio hivyo inaelekea ukingoni fuateni maagizo yangu na kama kuna shida yoyote itatokea nitawajibika”Aliongea.

“Kwasababu Madam ndio umeongea na unamuwakilisha mkuu wa nchi ambaye ametupa sapoti miaka kwa miaka , basi tunaungana kwa pamoja kutotoa msaada wa aina yoyote kwa kampuni ya Vexto na tutaliweka hilo hadharani kabla ya kesho mchana”Aliongea bwana mmoja ambaye alionekana kuwa na usemi kwa wenzake wote .

“Well! Once again thank you all for coming , the duration of my visit here is limited so I will have to skip the lunch event , But I ensure you all that my next visit will be with the president and the drinks and food will be on us”

“Niseme tena asanteni kwa kuitikia wito , uwepo wangu hapa nchini ni wa muda mfupu sana , hivyo sitohudhuria utaratibu wa chakula cha mchana , lakini nawahakikisha wote kwamba siku nikija nitakuwa na raisi na vyakula na vinywaji vitakuwa juu yetu”Aliongea Madam Kizwe na wote kwa pamoja walisimama na kumpa heshima yake na kisha yeye na msaidizi wake wakaondoka.

Kizwe mara baada ya kuingia kwenye lift alijikuta akitabasamu kinafiki na kisha akamgeukia msaidizi wake.

“About the thing I told you to prepare is it ready?”

“Jambo ambalo nimekuambia uandae lipo tayari?”

“Yes maam it is ready and the information is all organized it shall be deliverrd to the hands of Edna up on your request”

“Ndio , Tayari na taarifa zote zipo katika mpangilio na zinaweza kumfikia Edna muda wowote kwa maagizo yako”

“And the file?”

“Vipi kuhusu faili?”

“Also included Maam”

“Limeunganishwa pia”Alijibu kiheshima.

“Vipi kuhusu yule mpuuzi , bado yupo upande wetu?”

“Ndio Maam , yupo kwenye lile jumba Bagamoyo na mwanamke ambaye alimtumia ndani ya kampuni”Alijibu na kumfanya Kizwe kutabasamu.

“This is final leg. Make sure all arrangements including the ones abroad are in place , Just to be safe , the back up plan must not go wrong as well”

“Hii ni hatua ya mwisho , hakikisha mpangilio wote ukijumlisha na ule wa nje ya nchi upo kwenye mkao , ili kuwa salama Zaidi , mpango mbadala usije kuenda kombo pia kama huu utafeli”Aliagiza.

“Yes! Maam”

Muda huo huo na lift iliwafikisha chini na Kizwe alitoa tabasamu la ushindi kisha akatoka na kutembea kwa madaha kabisa kuelekea upande wa maegesho ya gari.Hio ilikuwa ni mchana, turudi muda wa jioni wa siku hio hio.

Ndani ya jumba la kifahari anaonekana Ernest akiwa kifua wazi akiongea na simu, na kwa jinsi ambavyo sura yake ilikuwa ikionekana ni dhahiri kuna jambo limemkasirisha muda huo wa jioni.

“Uliniambia mpango ulikuwa umekamilika na hauna dosari na sasa unapata uthubutu wa kuniambia umefeli , wao ni miungu mpaka kuweza kupona kila mtego tunaowawekea?”Aliongea kwa hasira kwa kutumia lugha ya kingereza.

“Naomba utuwie radhi sana , ni miezi mingi sasa tumeweza kudili na huyu Roma , lakini anaonekana kutokuwa mtu wa kawaida kabisa, leo tumeweka mtego lakini baaada ya kuukwepa hakujisumbua Zaidi ya kuendelea na safari yake , jambo ambalo linatutia wasiwasi kutokana na tunavyomfahamu”

“Nilijua mnajiita Black Mamba kutokana na uwezo wenu , ila sio shida kwasababu mmefeli , msifanye chochote kingine kwasasa”Aliongea.

“Asante sana kwa kutuelewa”Aliongea , lakini sasa kumbe nyuma yake Monica alikuwa akisikia kila kitu juu ya mazungumzo yake na baada ya kumaliza tu Monica alikimbilia nje akinuia kuondoka lakini alizuiwa na walinzi waliokuwa na siraha na kusukumiwa ndani kibabe.

“Monica mbona hutaki kunielewa ,unataka kuondoka ili niweze kukamatwa?, wewe sasa ni mama wa mtoto wangu alie tumboni nitahakikisha nakujali kwa uwezo wangu , lakini hapa ndani huwezi kuondoka mpaka hali itulie”

“Nimechoshwa na sababu zako za kipuuzi Ernest , unapata wapi ujasiri wakupanga mauji ya Edna na mume wake , siwezi kukuruhusu kuendelea nakuhakikishia nikipata mwanya nitamwambia”

“Monica acha kuwa mjinga kufikiria kwamba mpaka sasa hawajui kama nahusika kuwatengenezea mtego wa kupata ajali , wanajua kila kitu , lakini kwasasa haijalishi kama wataishi au watakufa , kampuni ya Vexto ikishafilisika Edna atatoka kwenye nafasi yake kama CEO kwa ndoano au kwa hila na kampuni itakuwa kwenye mikono yangu”

“Haiwezekani , huna namna yoyote ya kuwa CEO ,kwani wewe ni mtu wa nje ya familia”

“Mtu wa nje ya familia!!, Hahahaha.. , Wakati huo utakuwa wakati wangu wa kuweka wazi mimi ni nani haswa, Edna ni mtoto aliezaliwa nje ya ndoa na ashukuru kuwa katika nafasi hio kwa muda huu tu … Monica nitakuonyesha wazi Edna mwanamke unaemfahamu ni nani haswa” Aliongea na kumfanya Monica kuanza kupatwa na wasiwasi.

“Monica sitaki kukuona mwenye hasira kwa sasa kwasababu ni mjamzito , nitakupeleka juu kwa ajili ya kupumzika , nimeandaa mtu kwa ajili ya kukuandalia chakula mke wangu”Aliongea na kisha akamlazimisha Kwenda vyumba vya juu na baada ya kuhakikisha kaingia ndani ya chumba cha kulalia , alirudi chini sebuleni.

Lakini alijikuta akijawa na mshangao , mara baada ya kuona sura ambayo hakuwa ameitegemea , alikuwa ni Kizwe aliefika hapo ndani bila ya taarifa.

“Boss, umekuja mpaka huku kufanya nini?”Aliongea kwa kubabaika.

“Naamini kukaa hapa , unajisikia kuwa salama Zaidi na huru kuliko huko nje?”

“Madam asante sana kwa kunihakikishia usalama wangu”

“Kama kweli unanishukuru , hakikisha kila kitu kinaenda sawa kama kilivyopangwa ,nimekufundisha vitu vingi na umesoma na kuwa na elimu kubwa , ndio maana nikakuamini , nadhani unajua ninachomaanisha?”

“Madam Boss , nitahakikisha kila kitu kinaenda sawa , tokea zamani niliiishi kwa kumchukia Edna Maisha yangu yote”Aliongea lakini Kizwe alionekana kutoridhishwa na maneno hayo kutokana na mwonekano wake.

“Unajua ni kitu gani nakupendea Ernest?”aliuliza. na Ernest alitingishwa kichwa kwamba hajui.

“Nakupendea unafiki wako, unafikiri sijui kama unanichukia , naamini siku utakayopata nafasi hata ya siraha utanidhuru, But do you know your best attribute is ? You have a strong perspective toward superficial achievements and you would risk everything to obtain those , Your Morality means nothing in front of money and power , isn’t that right?”Aliongea na kumfanya Ernest kukunja sura na kufosi tabasamu kwa wakati mmoja.Alichokuwa akimaansiha hapo ni kwamba Ernest anamtazamo imara sana kwenye mafanikio ambayo hajayafanyia kazi na atahatarisha jambo lolote lile kuyapata huku akiendelea kumwambia kwamba yeye tabia yake mbele ya pesa na madaraka haizingatii kabisa maadili.

“You are absolutely right”

“Hakika uko sawa”Alijibu Ernest.

“Hahahha.. ni vyema unajifahamu , Haya niambie nini kinaendelea ndani ya Vexto kwasasa?”Alicheka kishambenga huku akikaa kwenye sofa na kuuliza swali

“Edna anaonekana kujiamini bado mpaka wakati huu kama kampuni inaweza kurudi kwenye mstari , kwani mpaka sasa inaonekana kampuni yake inaendelea na mpango uliokuwepo wa kuhusika kwenye mnada wa miradi ya Adani ambayo inahitaji pesa licha ya kwamba mbinu zao zote zipo mitandaoni , lakini vyombo vingi vya Habari duniani wametoa wasiwasi wao kwamba Edna anajichimbia kaburi , soko la hisa litakapofunguliwa tena asubuhi ni hakika kwamba itakuwa mwisho wao”Aliongea na Kizwe aliridhika kwa maelezo.

“Vipi kuhsu mpango wa mauji , wenyewe umeendaje?”

“Madam Roma anaonekana kuwa mtu ambaye haeleweki kabisa kwani na huu pia umefeli”Aliongea na kumfanya Kizwe kuonyesha sura ya kutoridhika.

“Mpaka sasa nimeshindwa kujua kinagaubaga kuhusu Maisha yote yanayomuhusu Roma , lakini najua kwamba familia ya Afande Kweka inamjali sana na wapo nae karibu kwa kila kinachoendelea na sio kwao tu mpaka kwa jeshi, napatwa na muwasha washa wa huyu mtu ni wapi aliishi kwani alijitokeza juzi tu na anaonekana kufelisha mipango yetu”

“Lakini kwa ninavvyo..”

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi kama kampuni itafilisika , waliokuwa karibu yake wengi watamkimbia , kuhusu wewe kupitia sapoti yangu na ya serikali tutaendelea kumdidimiza na kwa vigezo vyako utakuwa ni mwenye nafasi kubwa ya kumrithi , ukifanya mabadiliko madogo ndani ya kampuni , Vexto itarudi kwenye ubora wake ndani ya miaka miwili ijayo”

“I will give my all Madam”Aliongea huku akitoa tabasamu pana , lakini Kizwe alimwangalia kwa namna ya dharau.

“Just little treat got you this excited , what pathetic excuse of human being”

“Ka ofa kadogo tu hako kanakupagawisha ,ni kisingizio gani cha kusikitisha kinachotolewa na binadamu”Aliongea huku akitabasamu kwa kejeli huku akiendelea kuongea

“Kumtoa kwenye nafasi aliopewa kama zawadi ni hatua ya kwanza , Edna mtoto wa Raheli yapo mengi yanakuja Zaidi”Aliongea huku akitabasamu kifedhuli.

******

Ni siku nyingine ya asubuhi bada ya soko kufunguliwa , hali ilionekana kuwa mbaya Zaidi kuliko ilivyotegemewa , kwani hisa zilianza kutoka kwenye mstali mlalo na sasa zilianza kushuka kwa kasi mno na kuwafanya wafanyakazi wote akiwemo Roma kushangaa mno.

“Boss kwa staili hii tunafilisika , wahisani wakubwa wanaonekana kutupa hisa zetu sokoni kama walivyosema”Aliongea Nasra kwa wasiwasi sana huku akimwangalia Edna.

“Ni kwasababu ya taarifa ya hawa wapuuzi kutangaza kwamba hawapo tayari kutoa msaada wowote wa kifedha kwa kampuni yetu , ndio maana haya yanatokea”Aliongea mmoja wao huku akiangalia kishikwambi chake ambacho kilionyesha mkuu wa muungano wa benki kubwa ndani ya Tanzania akitangazia uma msimamo wao juu ya kampuni ya Vexto wakati akihojiwa na waandishi wa Habari.

Katika taarifa hio mkuu huyo flani anasema kwamba kwamba ni msimamo wa mabenki kutoisaiidia kampuni ya Vexto, kwani hata kama wafanye hivyo hakuna namna ya kampuni hio kurudi tena sokoni , hivyo wanajitoa rasmi.sasa hapo kinachoonekana ni matokeo ya Kizwe kuandaa kikao na wakuu hao, ilionekana alikuwa akifanya hivyo ili hisa za kampuni zilizokuwa kwenye Consolidation kushuka Zaidi thamani

Edna mwenyewe aliweza kuiona hio Habari , lakini wakati wenzake wakiwa na wasiwasi na kuchanganyikiwa yeye alionekana kuwa kimya muda wote.

Roma aliekuwa nyuma alikuwa pembeni tu akiangalia kile kinachoendelea , hakutaka kuingilia tena alikuwa akisinzia , aliona aache kila kitu afanye Edna mwenywe na kama atahitaji msaada wake ataongea.

“Boss Edna ongea chochote , soko likivuka asilimia hamsinni tutakua nje ya NASDAQ?”Waliongea wote kwa pamoja huku wakitaka Edna afanye maamuzi yoyote kuokoa hali.

Ikiwa imebakia dakika kama tano tu thamani ya soko kufunga chini ya asilimia hamsini ya thamani ya kampuni , Edna alitoa simu haraka na kisha aliweka sikioni.

*“Start now”*Aliongea kwa kutumia simu.
 
SEHEMU YA 367

Ni mbele kidogo na shule ya sekondari ya bweni ya St Trust upande wa kushoto mwa barabara inayoelekea Msata , kuna jumba moja ambalo lipo maeneo hayo , jumba hili lilikuwa ni moja ya jumba kubwa ambalo linaonekana kwa kupitia barabarani , kama ukiwa kwenye basi au kwenye daradala basi ni rahisi kuona geti lajumba hili baada ya kupita la shule.

Sasa ndani ya jumba hili ambalo ndani yake kuna ulinzi mkubwa wa baadhi ya wanaume waliovalia suti wakiwa wameshika mitutu ya bunduki kama wanalinda benki vile , wakiranda randa kulia na kushoto kuhakikisha ulinzi unakuwa wa kuaminika kwa yoyote aliokuwa ndani ya jumba hilo.

Ndani yake kabissa katika eneo la sebuleni anaonekana Ernest Komwe akiwa kifua wazi , akiwa ameketi kwenye masofa ya bei ghali huku mkononi akiwa ameshilkilia glasi ambayo ndani yake ilikuwa na kimiminika chekundu kama damu, akiwa akishushia taratatibu taratibu huku macho yake yakiwa kwenye runinga ambayo inaonyesha namba namba za soko la hisa za kampuni ya Vexto , alionekana kufurahia kwa chochote kile kinachoendelea kwenye soko hilo la hisa.

Pembeni yake anaonekana pia mwanamke aliejilaza kivivu kwenye sofa , akiwa na uso uliopauka kwa wasiwasi , akiwa usingizini , mwanamke mwenywe alikuwa ni Monica na alionekana alikuwa amechoka sana kwa chochote kila kinachoedelea hapo ndani, Ernest ghafla tu aliweza kushuhudia hisa za Vexto zikianza kupanda kidogo kidogo.

“Wow! Naona Edna anajaribu kununua hisa zake mwenywe ili kuwaingiza mtegoni wanunuzi wa hisa wadogo wadogo, Mh anaona ni kipi sasa ataweza kufanya kwenye hali kama hio, Edna wewe ni mjinga tu, Monica amka umuone Boss wako unaemuona amekamilika kila idara , nishakuambia ni mwanamke tu wa kawaida kama wengine”Aliongea huku akimtingisha Monica aliekuwa kwenye usingizi, alionekana kuwa na furaha kweli, muda huu ni pale Edna alivyowaambia watu wa idara ya fedha kununua hisa za kampuni kwa mafungu elfu moja moja.

“Ernest una nini wewe , kufilisika kwa kampuni ya Vexto kutakusaidia nini?”Aliongea Monica ambaye alikuwa akitia huruma kwa muonekano wake wa nywele.

“Hakuna sehemu niliposema nataka kampuni ya Vexto ifilisike kabisa , ninachotaka ni Edna kufilisika na kukosa kigezo cha kuendelea kuwa CEO , baada ya mpango uliopangwa Kwenda kama tunavyotgemea , Edna ataondoshwa na nitarudi kwenye kampuni kuikoa kama CEO mpya”Aliongea

“Na ukishaipata hio nafasi utafaidika nini?”

“Hujui hata ninachomaanisha , kampuni ya Vexto ni ndogo sana kukidhi matamanio yangu , ninachokifanya hapa ni kuhakikisha napata kilichohalali yangu”Aliongea.

“Ernest wewe ni chizi , mimi naondoka na nakuacha hapa hapa , ninaenda kumsaidai Boss Edna”Aliongea huku akijinyanyua na kuanza kupiga hatua kuelekea mlangoni , lakini kabla hajafungua Ernest alikuwa ashamfikia na alimkumbatia kwa nyuma, Monica alijaribu kufurukuta , lakini alishindwa kutoka kwenye kumbatio la Ernest.

“Unataka kuondoka , inamaana haunipendi tena?, Hupendi kuniona mimi nikiongoza kampuni ya Vexto tofauti na Edna?”

“Ernest naomba uniachie niondoke, acha ukichaa wako tafadhari”Aliongea huku akianza kutoa machozi, Monica na ubabe wake wote mbele ya Ernest alionekana mdhaifu sana.

“Ernest sipendi kukulinganisha na Edna boss wangu , wewe ni mwanaume wangu na nakupenda na sitaki uendele kufanya mambo kama haya yasio na msingi”

“Monica usinipandishe hasira nimekuchukua na kuja na wewe hapa , sio kwamba una umuhimu sana kwangu”Aliongea huku akianza kukasirika , lakini alijikuta akizishusha hasira zake mara baada ya Monica kukaa chini huku akianza kulia kama mtoto na alijikuta akimuonea huruma.

“Monica ijapokuwa nilikuwa nikikutumia kwenye mipango yangu , lakini haimaanishi sikujali , kama nitakuja kuwa CEO wa Vexto na kuwa Tajiri , utakuwa mke wangu na hautaendelea kuwa msaidizi tena wa Edna bali nitakupa cheo kikubwa ndani ya kampuni”Aliongea na kumfanya Monica kukaa vilevile kwenye kapeti huku akionekana kuwaza.

“Asante kwa kunielezea mpango wako … lakini Ernest sijali ni ukichaa namna gani unaweza kukupata , sijali ni mangapi mabaya utafanya , lakini nitaendelea kukupenda”AliongeaMonica

“Unamaanisha umekubali”

“Sorry! Ernest siwezi kuendelea kukaa hapa napaswa kurudi kwenye kampuni kumsaidia boss Edna .nafasi yangu kwenye kampuni ni ndogo ndio , lakini nilikuwa nikiridhika nayo , nimefanya kazi kwa muda mrefu ndani ya kampuni hivyo siwezi kuiona ikididimia”

“Kwahio unamaanisha unampenda sana Edna kuliko mimi , kwanini unaacha kunijali miimi mwanaume ninaepanga kukufanyia makubwa?”Aliuliza kwa hasira , lakini Monica aliishia kutabasamu kwa uchungu.

“Ni kwasababu nina mimba yako Ernest , sitaki mtoto atakae zaliwa kuwa na baba mtenda maovu kukamilisha ndoto zake”Aliongea Monica na kumfanya Ernest kushangazwa na kauli hio , na alijikuta akichanganyikiwa kwa wakati mmoja, alikuwa kama mtu ambaye hakuwa amemsikia vizuri.

Upande mwingine nchini Rwanda siku ya jumamosi alionekana Mheshimiwa Jeremy akiingia kwenye chumba chake cha kujisomea ndani ya ikulu upande wa nyumbani , mara baada tu ya kukaa kwenye kiti chake aliwasha runinga na moja kwa moja Kwenda upande wa taarifa za habari za kiuchumi kimataifa, na habari iliomtia wasiwasi Zaidi ni inayohusiana na kampuni ya Edna , baada ya kuangalia hali bado si shwari , alichukua simu yake iliokuwa kwenye Briefcase na kisha akatafuta namba ya raisi Senga.

“Senior nilikuwa nikitegemea simu yako”Aliongea Mheshimiwa Senga upande wa pili wa simu.

“Ndio Senga kwa hali inayoendelea ndani ya kampuni ya Edna , nilikuwa nikivuta muda tu kukupigia”Aliongea.

“Ndio Senior nimeona kinachoendelea”

“Senga Edna anatokaje kwenye hili linaloendelea?”

“Senior niseme kwamba kinachoendelea kwa sasa siwezi kufahamu anaweza kuchukua maamuzi gani ila serikali yangu ipo tayari kutoa msaada usio wa upendeleo kwenye hali kama hii”

“Senga unamaanisha nini usio wa upendeleo, kwa Edna ningetegemea uweke juhudi ya kumsaidia kuiokoa kampuni?”

“Ni kweli , lakini ya wizara ya uwekezaji na biashara wanashauri tusitoe upendeleo kwani kutaibuka migogoro na kuua ushindani na usawa wa biashara nchini jambo ambalohata mimi nimeunga mkono”Aliongea Senga upande wa pili na kumfanya Raisi Jeremy kuvuta pumzi na kuzishusha.

“Naelewa pointi yako lakini hata hivyo tunapaswa kumsaidia , msaada sio lazima uwe wa moja kwa moja , ninachotaka ni benki za Tanzania kuzingatia maombi yake akiomba mkopo”.

“Sawa Senior nitawapa vijana wangu kazi ya kushughulikia hilo swala kwani pia linagusa uchumi wa taifa kwa ujumla , lakini siwezi kukuahidi chochote kutokana na hali yenyewe , tutaangalia maamuzi ambayo Edna atafanya kuikoa kampuni ,ndio nitaangalia namna nzuri ya kumsaidia”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kuvuta pumzi ya ahueni.

“Nitashukuru sana kwa msaada wowote utakao msaidia , naamini Edna atatoka kwenye hio changamoto”Aliongea na kisha wakaagana na akakata simu, lakini wakati huo huo kuna mtu aligonga mlango mara mbili na kisha akasukuma, alikuwa ni mke wake Kizwe alieingia akiwa ameshikilia kikombe.

“Mume wangu nimekuona siku nzima ya sabato leo haupo vizuri . nimekuja kukuangalia kama uko sawa na kukuletea supu ya mzizi wa Ginseng kutoka Marekani , yatakusaidia kurudisha mudi yako wakati ukiendelea kujisomea”Aliongea Kizwe ambaye amevalia suruali nyeusi chini , huku juu akiwa amevalia shati la kitenge , alikuwa amependeza haswa.

Raisi Jeremy alipokea kikombe kile kutoka kwa mke wake na kunywa kidogo na kisha akamwangalia.

“Vipi huyu Desmond kaenda tena Tanzania?”

“Ndio , awamu hii amesema anaenda kuhakikiha anamleta mkwe nyumbani”Aliongea kwa kingereza na kumfanya Raisi Jeremy kushangaa kidogo.

“Unasema ashapata mchumba kutoka Tanzania?”

“Ndio, tena mume wangu nikikuonyesha mwanamke mwenyewe hutoamini , najua unataka Desmond aoe mwanmke wa kirwanda , lakini sidhani kama huyu mwanamke utamkataa kwani ana mafanikio makubwa na anamfaa sana Desmond”Aliongea Kizwe na kisha alitoa simu yake kwenye mfuko wa suruali na kisha akaenda upande wa kuhifadhia picha na akagusa picha iliokuwa ikimuonyesha Edna na Desmond.

Hii ni picha ambayo alipiga Ernest Komwe miezi kadhaa iliopita picha hio ilikuwa ni Desmond akiwa amepiga magoti , huku upande wa Edna akiwa amesimama akipokea burungutu la maua akikabidhiwa na Desmond.

Raisi Jeremy baada ya kuangalia picha ile kutoka kwenye simu ya mke wake alijikuta akitoa jicho kama kabanwa na mlango.

“Vipi hata wewe naona umeshangaa mume wangu , mimi pia nilivyoiona nilipatwa na mshangao , sasa hivi mtoto wetu yupo Tanzania kwa ajili ya kumsaida mchumba wake na shida ya biashara iliompata”

“Mke wangu unamaanisha Desmond, ana… ana mahusiano ya kimapenzi na Edna!!!!?”

“Ndio mume wangu , si ndio maana Desmond yupo nchini Tanzania mara nyingi , ni kwasababu ya penzi lake kwa Edna”

“Hapana haiwezekani huyu Edna ameshaolewa, hata wewe juzi uliona akiweka hilo wazi kupitia mashindano yaliosimamiwa na kampuni yake”

“Mume wangu unaonekana kumjua sana Edna, hata hivyo Edna hawezi kutofautiana na tabia za wanawake wengine huenda anatoka kimapenzi na Desmond kwa siri na ni swala la muda kuweka mahusiano yao wazi”Aliongea huku akiweka tabasamu la kinafiki.

Ukweli huyu Kizwe alikuwa akitaka kumhenyesha mume wake kwa kumueleza Desmond anatoka na Edna , alijua swala hili lingemchanganya sana Jeremy , kwani hakuwahi kuielezea familia yake kama Edna ni mtoto wake na Raheli.

Jeremy hakuwa akifahamu kama mke wake alikuwa akiijua siri yake alioitunza kwa miaka mingi ,siri iliokuwa ikihusiana na mapenzi yaliokuwepo kati ya Raheli pamoja na yeye , mpaka kuchangia kuzaa mapacha.

“Kizwe hili haturuhusu litokee, sitoruhusu Desmond kuwa na mahusiano na Edna”Aliongea huku hasira zikianza kujitengeneza.

“Kwanini mume wangu?”

“Kizwe akili yako sikuhizi imekuwa ndogo , wewe huoni Edna kashaolewa, unafikiri nini kitatokea kama taarifa zikisambaa, mbona umekuwa na akili ndogo namna hii, hata hivyo siamini kama Edna anaweza kumsaliti mume wake”Aliongea Raisi Jeremy na Kizwe alitoa taasamu la kifedhuli.

“Kama mama yake aliweza kutembea na mume wa mtu , Edna anashindajwe kumsaliti mume wake, The Apple doesn’t fall far from the tree”Aliongea kwa kumalizia na usemi kwamba tunda la tufaa halidondoki mbali na mti wake.

“Kizwe unajaribu kuongea nini…?”Aliongea huku mikono ilioshika kikombe ikitetema.

“Jeremy ijapokuwa sijawahi kukuuliza , usijifanye sijui kama ulitembea na rafiki yangu Raheli , niliacha tu kuliongela hili swala kwani uliendelea kunionyeshea mapenzi ninayoyataka na tulikuwa na furaha”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kushangaa na kuwa na wasiwasi kwa wakati mmoja.

“Ulikuwa ukiyajua yote hayo na hukujaribu kuongea chochote?”

“Nishakujibu tayari , sikutaka ndoa yetu iingie doa kwasababu ya Raheli , najua mliachana baada ya yeye kuolewa na kumzalia Adebayo mtoto”Aliongea Kizwe na kumfanya Jeremy kuvuta pumzi mpaka hapo alishukuru kitu kimoja, aliamini Kizwe hakujua kama Edna ni mtoto wake.

“Mke wangu naomb….”

“Shshiii…Jeremy hayo mambo yalishapita na nilishakusamehe muda mrefu tu ndio maana nikakaa kimya huna haja ya kuomba msamaha”Aliongea Kizwe na kumfanya Jeremy kuvuta pumzi.

“Asante sana mke wangu.. kwa kuvumilia kukengeuka kwangu , hakika wewe ni mke mwema sana”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu.

“Usijali Jeremy…. Muda mwingine watu hufanya makosa na nilishukuru sana baada ya kuona mapenzi yenu yaliisha baada ya Raheli kuolewa”Aliongea huku akimsogelea karibu.

“Yeah Mke wangu , najua kipindi kile zilikuwa tamaa tu , lakini niliachana nae kabisa”Aliongea na kumfanya Kizwe kutabasamu na kisha kugeukia runinga iliokuwa ikitangaza hali mbaya ya kampuni ya Vexto.

“Mume wangu kesho natarajia Kwenda Tanzania kibiashara unaonaje nikitumia safari hio angalau kumsaidia Edna , Raheli alikuwa ni rafiki yangu licha ya kunisaliti , lakini kutokana na historia yangu sidhani kama nitajisikia vizuri kuona kampuni alioipigania kufilisika,nitajaribu kumuunganisha na meneja mmoja wa benki kumsaidia mkopo, Unaonaje mume wangu au tusiingilie?”Aliongea Kizwe na kumfanya Jeremy kumwangalia mke wake usoni kumsoma maneno yake kama yana ukweli ndani yake na hakuona dalili yoyote ya unafiki kwenye macho ya mke wake.

“Uko siriasi?”

“Mume wangu , ulifikiri nitamchukia Edna kwasababu ya historia yenu na Raheli , yule mtoto yeye hana kosa lolote “Aliongea na kumfanya Jeremy kutabasamu na kisha akamsogelea mke wake na kumshika mkono.

“Ni miaka mingi sasa imepita , tumepitia milima na mabonde , nashukuru sana mke wangu kwa kuendelea kuwepo kwenye Maisha yangu , sasa hivi najikuta kuwa mwenye hatia kwa jinsi ulivyonivumilia, Mke wangu naomba unisamehe kwenye siku zote ambazo sikukufanyia vyema kama mume wako, kama kuna namna yoyote ya kumsaidia Edna nakuruhusu ufanye hivyo”Aliongea Jeremy.

“Usijali mume wangu , ninachokifanya ni kukusapoti wewe kwa kila kitu”Aliongea na baada ya dakika kadhaa tu alitoka kwenye chumba hicho akimuacha Jeremy.

Kizwe mara baada ya kutoka nje alitabasamu kinafiki huku akigeukia mlango wa chumba cha kujisomea na kisha aliendeleza safari yake , tabasamu lake ni kama lilikuwa likimwambia Jeremy kwamba utanikoma.

Upande wa Raisi Jeremy baada ya mke wake kutoka alimpigia simu Linda na kumpa maelekezo ya Kwenda Tanzania na kumrudisha Desmond nyumbani, Raisi Jeremy licha ya kwamba aliamini hakuna mahusiano yoyote ya Edna na Desmond lakini aliamini huenda Desmond akawa na harakati za kumtongoza Edna , hivyo alitaka kuepusha hali ya Kaka kumtongoza dada yake.
Ohooooooo
 
kazi nzuri...ila kama unataka kutupa mkono majemedari wako wa toka mwanzo.Yaani kutoka j4, alhamis na jmosi sasa imekiwa siku yoyote mkuu?
Mkuu Hades Singanojr...aka Roma Romani.
 
Back
Top Bottom