Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

[emoji2923][emoji2923][emoji2923][emoji2923][emoji373][emoji1635][emoji120]
 
Muda wa nin mzee jumapili ikitajwa Kwa huyu mwamba ujue ni ya kirumi.
Jamaa anazingua sana.Maadam aliahidi watu mlioko whatsap mngeirusha humu manake alishaahidi labda majukumu yamemzidi!
 
Singano wateja wako wa kesho wanalalamika jitahidi kuangalia ratiba yako kwanza kabla ya kuahidi. Leo tunasoma bure lakini kesho tutanunua. Kumbuka uaminifu hupimwa kwa vitu vidogo kama hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANO JR

SEHEMU YA 609..
Hayakuwa mauaji bali ilikuwa ni uchinjaji wa aina yake , Bwana mwenye chunusi nyeupe licha ya kupitia mafunzo katika sehemu nyingi za dunia lakini hakuwahi kuona mtu katili kama Edna, namna ambavyo amewaua watu wake ilimtisha na kumshangaza kwa wakati mmoja lakini hata hivyo mshangao wake haukudumu kwani mbele ya Edna ilimaanisha kifo kama asiingejaribu kujiokoa.
Hawakutaka kuchelewa kwani palepale na wenyewe walitumia wepesi wao kurudi nyuma kukimbia huku wakimrushia Edna risasi lakini ilikuwa kama vile Edna alikuwa akijua risasi ikitoka kwenye bunduki ‘Trajectory’ yake itakuwa wapi kwani alikwepa kwa sarakasi murua kabisa.
Bahati mbaya mtu mwenye chuusi upande aliochagua kukimbilia ulikuwa hauna mlango na kabla hata hajajua nini cha kufanya alishindwa kukwepa upanga uliorushwa kwake na palepale ulimchoma kifuani karibu na shingo na kutoboa.
“How…..”
Neno ‘How’ ndio kauli yake ya mwisho kuongea kwani alidondoka chini na kuanza kuupambania uhai wake.
Jambazi mwingine baada ya kuona Edna kaelekeza umakini wake kuelekea kwa Bwana mwenye chunusi hakutaka kupoteza nafasi kwani palepale alikimbilia upande wa mlangoni.
“Boom!!”
Ulikuwa mlio wa risasi uliopitia katika eneo la kisogo katika kichwa chake na aliishia kutoa macho tu na kudondoka chini na hakuchukua muda mrefu akakata roho.
Edna mara baada ya kuona amemaliza kazi alitupia pembeni ile bunduki na kumkimbilia Lanlan na kumkumbatia.
Lanlan muda huo licha ya kupigika alikuwa bado na nguvu zake na aliweza kushuhudia kila kitu alichokifanya mama yake na alikuwa akitoa macho ya mshangao akiwa na furaha juu.
“Mommy you are so strong , the bad guys are all dead”Aliongea Lanlan kwa furaha akimaanisha kwamba mama yake ana nguvu kubwa na watu wabaya wote wamekufa.
“Nisamehe, Nisamehe .. Lanlan mama hajakulinda vizuri na ni makosa yangu naomba unisamehe”Aliongea Edna muda huo hakuwa na furaha hata kidogo kwenye macho yake na aliishia kulia kilio cha kwikwi.
Lanlan kutokana na uwezo wake licha ya kupata michupuko lakini hakuwa na maumivu makali na aliishia kutoa tabasamu la kitoto na kusogezea mdomo mashavu ya mama yake na kuyabusu.
Edna tabasamu palepale lilimvaa lakini ilikuwa ni kwa sekunde tu kwani palepale alianza kujihisi uchomvu usiiokuwa wa kawaida huku macho yakianza kubadilika na kuwa na ukungu na ndani ya dakika hio hio alidondoka chini na kupoteza fahamu.
******
Nusu saa mbele nchini Rwanda ndani ya makazi ya raisi Jeremy alionekana Master 4 akiwa ameketi eneo la sebuleni akiwa na Raisi Jeremy aliekuwa amekaa mbele yake upande wa kushoto huku juu ya meza kukiwa na glass za mvinyo.
Muonekano wa Raisi Jeremy haukuwa ule uliozoelekea ni kama alikuwa katika hali ya kutokuamini jambo na hata sauti yake wakati wa kuongea ilisikika ikiwa sio ya kuelezeka.
Mbele yao upande wa kuingilia mlangoni alikuwa amesimama bwana moja mrefu mweusi ambaye alikuwa sehemu ya wanausalama wa raisi Jeremy na alionekana alikuwa akitoa ripoti ambayo ndio hio ilimfanya Raisi Jeremy kutokuamini.
“Una uhakika ni Edna ambaye amewaua hao wajinga?”
“Ndio mheshimiwa , Risasi na visu vilivyokutwa vina alama zake za vidole , Lanlan pia amethibitisha kwa kusema Bi Edna ndio aliehusika kuwaua wote mara baada ya kuhojiwa na Brigedia Tobwe wakati wa kuwaokoa”
“Upuuzi !! Edna hajawahi kujifunza mahali popote mapigano anawezaje kuwaua wanajeshi wa kitengo cha Special forces?”Aliongea kwa kufoka na kumfanya yule bwana mtoa taarifa kuonyesha wasiwasi.
“Mheshimiwa Taarifa ni za uhakika , bado sielewi imekuwaje wakafa lakini ushahidi unaonyesha kila kitu Bi Edna ndio kahusika, pengine kama kuna mtu ambaye anajaribu kuficha ukweli na akaamua kumshikisha Bi Edna siraha ili aonekane ni yeye”
“Unaweza kuondoka”Aliongea huku akiinua mkono wake na bwana yule alitingicha kichwa chake kwa heshima na kisha akageuka na kutoka eneo hilo.
“Master 4 nimefeli kukamilisha kazi .. inaonekana nahitaji muda zaidi kuweza kupata mbinu ya Roma ya mafunzo ya kijini”Aliongea Raisi Jeremy huku akiwa na uso uliosawajika.
“Jeremy umerahisisha mambo , wale wanajeshi wa Kamanda Razaq ni wepesi kuwatawala kutokana na chuki yao zidi ya Roma lakini hawana uwezo mkubwa .. mtoto wako wa nje ya ndoa ana siri nyingi ambazo wewe mwenyewe huzijui, bado tu hujafahamu kuhusu hili?”Aliongea Master 4 akiwa katika muonekano wa kawaida.
“Master bado nashindwa kuamini kama ni kweli ndio kahusika kuwaua , kuna uwezekano kuna mtu amebadilisha ukweli”Aliongea na kumfanya Master 4 kutoa tabasamu.
“Lanlan ni mtoto tu kwanini adanganye , fanya uchunguzi wa kina kupitia wanausalama wako uliowapandikiza na umjue binti yako vizuri au uanze kufikiria mara ya pili kumrudisha katika familia la sivyo itakuwa ni sawa na kujipiga risasi mguuni”
“Niamini Master , nitahakikisha nafanya uchunguzi wa kina kumjua vizuri binti yangu”
“Unatakiwa pia kutumia akili Jeremy , kwasasa haifahamiki Roma Ramoini yupo wapi na itakuwa ngumu kukamilisha mipango yetu akirudi , hivyo usije kupoteza hii fursa”Aliongea na kumfanya Jeremy kutingisha kichwa kukubali.
Kwa jinsi ambavyo alikuwa akipewa maelekezo ni kama vile hakuwa yule ambaye alikuwa raisi mwenye kujiamini , lakini nyuma ya pazia kuna watu ambao waliokuwa wakimwendesha kwa siri.
*******
Upande mwingine nchini Tanzania katika mkoa wa Iringa ndani ya jumba la Afande Kweka, Edna aliweza kufumbua macho yake taratibu na mbele yake ilionekana sura ya kitoto iliokuwa ikimwangalia kwa ukaribu.
Edna alijikuta akitoa tabasamu hafifu na kupandisha uso wake kama vile yupo kwenye ndoto na kumgusa Lanlan shavuni lakini mara baada ya kuona kila kitu ni uhalisia palepale alifumbua macho yake yote na wasiwasi ulimwingia kwa mara nyingine.
“Lanlan tupo wapi..?”
“Umeamka?”Sauti nzito ya mikwaruzo kutoka kwa Afande Kweka iliweza kusikika upande wake wa kulia.
Ni muda huo huo Edna aliweza kugundua kwamba walikuwa nyumbani na palepale aliinuka haraka haraka na kukaa kitako huku akimuweka Lanlan pembeni yake na aliweza kuona sura za wanafamilia wote zilikuwa zikimwangalia.
Ukiachana na wanafamilia watu wengine waliokuwepo hapo alikuwa ni Afande Tobwe aliekuwa kwenye gwanda za kijeshi pamoja na wanajeshi wake baadhi na RCO wa mkoa wa Iringa.
Na Edna kwa kuangalia tu aliweza kuona kuna hali ya wasiwasi katika macho yao.
“Mjomba wewe ndio umetuokoa ?”Aliuliza Edna akimlenga Afande Tobwe , alikuwa akimwita mjomba tokea akiwa mdogo na alikuwa amezoea hivyo.
Afande Tobwe alijikuta akiangaliana na wanajeshi wake huku wakionyesha hali ya kuchanganyikiwa na swali la Edna.
“Edna hukumbuki kilichotokea ?”
“Nini..sikumbuki..”Aliongea kwa kutingicha kichwa lakini lanlan palepale Lanlan alisimama na kuingilia maongezi , ilikuwa ni kama alikuwa akielewa mama yake alikuwa akiulizwa nini.
“Mommy you were so strong , you killed all of the bad guys ! Swoosh Swoosh Swoosh , The all died so Quikly”
“Mama ulikuwa na nguvu , uliwaua wale watu wabaya wote , Swoosh Swoosh Swoosh , na wote tayari wamekufaha kwa haraka sana”Edna alikuwa ni mwenye kuchanganyikiwa wakati akisikiliza maelezo ya Lanlan ambaye alikuwa akielezea kwa vitendo kwa kuruka juu na chini akionyesha namna ambavyo mama yake aliwaua wale watu wabaya.
Afande Tobwe na wengine hawakuwa wakikataa kuhusu jambo hilo pia, walikuwa wanaamini kile ambacho Lanlan anaongea na isitoshe uchunguzi uliofanyika ulibaini alama za vidole katika siraha zilizokuwa katika eneo.
Afande Tobwe na Afande Kweka waliangaliana , wote walionekana kuwa na wasiwasi juu ya kile kilichotokea na namna Edna ambavyo hakumbuki chochote.
“Edna mwanangu ni sawa tu kama hukumbuki chochote ili mradi tu upo sawa”Aliongea Blandina ambaye alikuw ana wasiwasi na afya ya Edna muda wote.
Baadaya Damasi kuondoka na kurejea Dar es salaam yeye alibakia hapo Iringa kwa ajili ya kukaa karibu na Edna kwa kipindi ambacho Roma hayupo.
“Edna ni sawa tu kama hukumbuki chochote hili tukio sio la kawaida lakini vilevile ulikuwa ukijifunza mbinu za kuvuna nishati kwa kipindi kirefu kidogo hivyo inaeleweka unaweza ukawa umefanya wewe , lakini kwanzia kesho na kuendelea utakuwa ukitembea na walinzi, sitaki kuona mpo hatarini tena kabla ya Roma kurudi”
Edna aliishia kutngisha kichwa kwasababu hata hivyo hakuwa akikumbuka chochote lakini bado moyo wake haukuwa katika amani kutokana na kutokuwepo kwa taarifa yoyote kuhusu Roma.
Baada ya kuwa na wasiwasi juu yao Blandina aliandaa haraka haraka chakula kwa kusaidiana na wafanyakazi ili waweze kupumzika mapema.
Ijapokuwa alikuwa akijua wamerudi wakiwa salama lakini kwa upande wake alikuwa na mawazo kama Edna tu juu ya kupotea kwa Roma na nyumba yote ilionekana kukosa ile furaha iliozoeleka.
Muda ulikuwa umeenda kwani ilikuwa ni usiku wa saa mbili kuelekea saa tatu lakini Afande Tobwe bado hakuwa ameondoka .
Alikuwa akijali sana maswala ya familia ya Afande Kweka kutokana na watoto wake kuwa na mahusiano na Roma.
Afande Kweka alikuwa ameketi huku akiangalia baadhi ya picha ambazo zimepigwa kutoka eneo la tukio , namna ambavyo watu walivyokutwa wamekufa na kilichoonekana katika uso wake ni ndita pekee kujikunja.
“Marshall nimefatilia kuhusu hawa watu na nimegundua ni wanajeshi waliofanya uasi chini ya Afande Razaq , wote walikuwa ni makomandoo wa wakihudumu katika kitengo cha special forces, kuhusu hawa wengine ni raia wa kichina na tumeshafanya mawasiliano na ubalozi ili kuweza kuwatambua”
“Haya yote yametokea nje ya uelewa wetu nadhani kuna mtu atakuwa amesaidia katika hili na isitoshe taarifa ya kupotea Roma tulihakikisha ni siri , nina uhakika kuna mtu ambaye aliwasaidia mwenye muunganiko wa kishushu ndani ya taifa”Aliongea RCO wa mkoa wa Iringa.
“Sidhani kama haya yote yanafanyika kutokana na visasi vyao juu yetu, kama ni hivyo wangemuua Edna na Lanlan lakini walichokifanya ni kutaka kuiba mbinu ya mafunzo ya Roma”Aliongea ijapokuwa kauli yake ya mafunzo na mambo kama hayo haikuwelekea kwa mkuu wa polisi lakini hakuuliza.
“Hata mimi nimewaza hivyo lakini kama nitakua sahihi mtu ambaye anaweza kwenda mbali hivyo labda upande wa Rwanda maana ujasusi wao ndani ya Tanzania umekuwa kero sana kwa usalama wa taifa letu, lakini kwa wakati mmoja sidhani kama Raisi Jeremy anaweza akafanya kitu kama hiki”Aliongea Afande Tobwe.
“Jeremy hawezi kujali kushukiwa katika hili , sasa hivi atakuwa hana cha kuogopa kwasababu Roma hayupo, hata kama angejulikana kama mhusika bado hatuna cha kumfanya , isitoshe hata kama tukisema ni yeye anazo sababu za mashiko za kukataa”Aliongea na kisha Afande Tobwe alimgeukia bwana mwingine aliekuwa amembatana nae.
“Muelezee Marshal kuhusu uchambuzi wetu wa tukio”Aliongea na bwana aliefahamika kwa jina la Jecha alianza kuelezea.
“Kutokana na viashiria ambavyo tumeweza kupata katika eneo la tukio lakini pia sababu za vifo vyao , tuliweza kugundua kwamba kama itakuwa ni kweli Bi Edna ndio kahusika, uwezo wake ni wa viwango vya juu sana , Daktari wa maswala ya kiuchunguzi ameweza kuthibitisha watu wote wamekufa ndani ya sekunde therathini jambo ambalo linamaanisha kila mtu alikufa katika ‘interval’ ya dakika tatu , hata wale maninja wa hali ya juu hawawezi kuwa na uwezo huo tukizingatia uwezo wa wanajeshi pamoja na siraha walizokuwaa nazo .
Bi Edna atakuwa na ufahamu mkubwa na bastora walizokuwa wameshikilia na siraha zingine kwani aliweza kutarajia mashambulizi yao na kuweza kushambulia bila ya yeye kudhulika , kwa taarifa tulizokuwa nazo watu wa uwezo huu ni maninja wa hali ya juu duniani wanaofahamika kwa jina la ZERO,Mr Roma Ramoni ni mmoja ya maninja hao lakini ni ngumu kuweza kumpata kama yeye”Aliongea na Afande Kweka uso wake haukuwa katika mabadiliko na aliendelea kuangalia damu zilizokuwa katika picha hizo.
“Tujuavyo Edna ni kweli anajifunza mbinu za mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi lakini kwa levo yake haiwezekanni kuua watu zaidi ya kumi tena ambao ni wanajeshi , kama kweli ndio kahusika basi naweza kusema kuna kitu anaficha na sisi hatukijui”Aliongea Afande Tobwe
“Afande samahani kama nitakuwa naongea kimakosa , lakini kama kuna mtu mwenye uwezo wa aina hii lazima awe amepitia mafunzo ya hali ya juu ya kininja tena kwa ajili ya kuua na mara nyingi ni zaidi ya miaka mitano ya mafunzo makali sana pamoja na uzoefu , lakini kuhusu Bi Edna nadhani kila mmoja wetu hapa tunayajua maisha yake tokea akiwa mdogo”Aliongea Kapteni Jecha.
Eneo lote liligeuka kuwa kimya walijua kabisa Kapteni Jecha alikuwa sahihi , kulikuwana taarifa za kujitosheleza kuhusu Edna tokea anazaliwa mpaka akiwa mkubwa.
“Tukiachana na hayo yote kwasasa nadhani Afande Tobwe uhakikishe wanajeshi hao wanafanyiwa utaratibu wa kimaziko na hao wa wachina endelea kuwasiliana na ubalozi ili tujue ni wakina nani , nitaandaa wanajeshi wa kitengo maalumu kutoka kambi ya Lugalo kuendelea kufanya uchunguzi wa chini chini ili tuweze kujua siri ya Edna ni ipi”Aliongea Afande Kweka.
Ukweli alikuwa na wasiwasi sana huenda kuliko watu wote waliokuwa hapo ndani kwani ni yeye pekee ambaye alikuwa akijua siri nyingi sana kuhusu Edna na yale yote ambayo alikwisha kuyafanya yakiihusisha familia yake.
Yupo Lanlan katika maisha ya Edna mtoto ambaye alikuwa akijua kabisa ni wa Seventeen lakini ghafla tu Edna anakuwa na ujuzi wa juu wa kininja unaofanana na wa kundi la Zero, hisia zake hazikuwa zikieleweka kwa muda huo na alipotezea kila mawazo mabaya ambayo yalikuwa yakiingia katika kichwa chake na kuamua kudili na yale ambayo yalikuwa yakielekeweka na kujiambia Roma akirudi atadili na mke wake maana ndio anamjua vizuri.









SEHEMU YA 610.
Ni ndani ya ulimwengu wa majini pepo katika jumba la kimalkia , alionekana Sophia akiwa ameketi katika kiti kwenye kibaraza cha jumba hilo akikodolea macho mandhari ya nje.
Zilipita siku sita tokea aingie kwenye jumba hilo akiwa amefungiwa bila kutoka lakini Aoiline alikuwa akimtendea vizuri kwani aliwapanga hadi vijakazi ambao walikuwa wakimhudumia kwa zamu kwa kila alichotaka..
Licha ya hivyo haikumletea furaha kwasababu tu hakuweza kutoka nje ya chumba , aliweza kupata taarifa kupitia vijakazi na kufahamu Aoiline alikuwa amemfungia Roma katika gereza la ardhini bila sababu yoyote.
“Unafikiria nini?Au unamfikiria mpenzi wako?”Sauti nyororo iliweza kusikia nyuma yake na Sophia aligeuza shingo haraka haraka na aliweza kumuona Aoiline akiwa anamwangalia kwa macho ya kipole.
Licha ya yeye mwenyewe kuwa mwanamke mrembo lakini hakuwa ameuzoea uzuri na urembo wa Aoiline.
“Hatimae umeweza kujitokeza , unapanga kutufanyia nini?”Aliuliza na kumfanya Aoiline kuziweka nywele zake vizuri zilizokuwa zikipeperushwa na upepo..
“Nimeamua kuja kukuona muda huu kwasababu kama ningekuja mapema ungeonyesha hasira zako tu , ni jambo la kawaida kwa mimi kumtembelea mgeni wangu hususani muda ambao ametulia , kuhusu nia yangu ni rahisi nahitaji nyie watu kubakia hapa kama wageni wangu”
“Mimi sio mjinga, kama umetualika hapa kama wageni wako kwanini umemfungia Roma gerezani?”AliongeaSophia huku akianza kuonyesha kukasirika.
“Nadhani wewe mwenyewe ndio humjui ni mwanaume mwenye kiburi na hata kama ningemuambia abakie hapa angalau kwa miaka kadhaa asingekubali hivyo nikaamua kumfungia kwa lazima”
“Unaongea nini , miaka kadhaa!?, unapanga kumfungia kwa miaka kadhaa?”Aliuliza Sophia kwa mshangao lakini wakati huo sauti yake ikiwa juu.
“Kwanini unashangaa , unadhani naweza kuwaruhusu muondoke na kwenda kupigwa na radi kwenye mnara?”
“Sio hivyo lakini..”Sophia alijikuta akishindwa kuendelea kuongea.
“Kwahio unasema ukweli , Bro Roma anaweza kufa kama ataingia kwenye mnara?”Aliuliza na kumfanya Aoiline kumwangalia Sophia na macho ya kiuchokozi.
“Umekuwa ukimuulizia Roma tokea nimeingia kwenye hiki chimba tofauti na kuuliza kama naweza kukuruhusu kutoka au ni kipi naenda kukufanyia.. inaonekana unamjali zaidi unavyojijali mwenyewe , Dada Sophia ndio kwamba unampenda sana?”
Sophia alijikuta akishitushwa na swali lake na alitingicha kichwa haraka haraka kukataa lakini uso wake uliokuwa ushaanza kutawaliwa na homoni za aibu haukufichika.
“Sio kama nampenda , Bro Roma ni shemeji yangu kwanini nimpende?”Aliongea na kumfahya Aoiline kushangaa kidogo.
“Umesema ni shemeji yako , mbona sio kawaida , kwanini mashemeji wote kwa pamoja mkaja ndani ya ulimwengu huu mkiwa pamoja ? au ndio ulikuwa ukimsaliti dada yako?”
“Wew.. unanisingiuzia , tulikuwa tukishambuliwa na gaidi na ndio ilivyotokea tukavutwa kuja kwenye huu ulimwengu kama ajali , hatukujua chochote kuhusu huu ulimwengu na hakuna kilichotokea baina yetu”
Sophia aliongea hivyo kujitetea lakini muda huo masikio yake yalikuwa ya moto, kila akikumbuka tukio la Roma kipindi kile akiwa hana nguo mapigo yake ya moyo yalisonga kwa kasi sana.
“Hivi unajisikia wewe mwenyewe , tokea tukutane ulikuwa ukimwita Kaka badala ya shemeji hii inamaanisha una hisia za kimapenzi na yeye , isitoshe Roma mwenyewe ameweza kuja na wewe licha ya kwamba unaonekana kama mzigo kwake , inaonyesha anakujali sana hivyo hakuna haja ya kukataa”Aliongea na kumfanya Sophia kuishiwa na maneno.
Mawazo yasiokuwa na idadi yalikuwa yakipiga katika kichwa chake huku akijiuliza maswali mengi.
Ni kweli Roma ananijali kwa kiasi kikubwa? , ni kweli ananithamini? , anahisia sawa na za kwangu? , maswali hayo katika mawazo yake yalimfanya kujionea aibu.
“Ameoa lakini bado mna ukaribu , naamini sio mtu mzuri , wewe ni mwanamke mjinga tu ambaye umetokea kufa na kuoza kwa ajili yake”Aliongea Aoiline huku akitoa tabasamu la kejeli.
“Sio kweli , Roma ni mtu mzuri kwa kila mtu sio kwangu tu..”Sophia alichukua nafasi ya kumtetea Roma.
“Kwahio unasema kwamba kuna wanawake wengine anao wajali si ndio , kama ni hivyo mke wake si atakuwa anatia huruma?”Aliongea huku akikunja ndita,
Sophia alitaka kukataa maneno yake lakini aliishia kati kwani yalikuwa ni ya kweli.
“Unaongea kwa staili ya kufanya kama kuna kinachoendelea kati yetu lakini ukweli mahusiano yangu na yeye ni ya kishemeji , isitoshe ni chaguo la Sister kuendelea kuwa nae licha ya kuwa na wanawake wengine”
“Mh ,, hili halimaanishi kwamba hakuna kitu ambacho hakitotokea hapo baadae , pengine anasubiria muda muafaka wa kukula na wewe”Aliongea huku akitoa tabasamu la kiuchokozi na kuanza kumkagua Sophia kuanzia juu mpaka chini kwa macho ya kijini.
“Nimeweza kuona mpaka sasa wewe ni bikta , kama ni hivyo basi jitahidi kukadhana na mafunzo ya kijini kuliko kuruhusu wanaume wakudanganye”
Sophia hakujibu chochote kama vile alikuwa na hasira kwa Aoiline kumsema vibaya Roma.
“Nakuambia haya kwasababu unaonekana kuwa mtu mwenye moyo mwepesi na wa kikarimu na ndio maana sijakufanya chochote kwa siku zote , kama huniamini tunaweza kumuuliza Roma mwenyewe akufafanulie jinsi ulivyo”
“Unamaanisha nini ..?”Aliongea akionekana kuchanganyikiwa kidogo lakini Aoiline hakumjali kabisa na alimsogelea Sophia na kumbeba juu juu na kutoka nae nje ya chumba.
******
Upande wa mashariki wa ulimwengu huo wa majini pepo kulikuwa na milima ya Volkano mingi mno mingine ikiwa inalipuka mingine ikiwa ni ile Tuli.
Ndani ndani upande wa pili wa milima hio ndio kuna ukoo wa kijini wenye nguvu zaidi , ulikuwa ni ukoo wa kijini ambao ulikuwa umejitenga kabisa na majini wengine katika Korongo la Joka .
Yaani hao ndio majini pekee ambao hawakutaka jamii nyingine ziwaingilie, ni kama vile huku duniani uchukulie mfano wa nchi ya Korea Kaskazini ambao wananchi wao wamefungiwa na kuuziliwa kutoka.
Hii ndio miliki ambayo kuna Majoka wale wakubwa na hata ukiianza kuingia katika Korongo hilo kuna mifupa mbalimbali ya Majoka kila mahali.
Kulikuwa na jengo kubwa sana kama ngome lililojengwa kwa mawe makubwa juu ya kilele cha mlima , usanifu wa jengo hilo ulikuwa ni wa tofauti sana na ule wa jumba la kimalkia la jini Aoiline.
Ni usanifu ambao umejengwa kwa ajili ya kuruhusu Dragoni kutoka na kuingia katika jumba hilo bila shida yoyote.
Dakika hio hio lilionekana Joka kubwa lenye mabawa angani likiiamba ambaa kuelekea upande wa jengo hilo na baada ya kuupigisha mkia wake kulia na kushoto palepale kufumba na kufumbua lilikuwa lishaingia ndani ya jumba hilo.
Dakika hio hio Mara baada ya Joka lile kuingia ndani ya jumba hilo ulitokea mwanga wa kijani ukitoka chini na kugonga paaa na palepale lile Joka lilibadilika na kuwa mwanaume ‘Handsome’ sana , alikuwa ni mrefu alievalia mavazi ya kitamaduni ya rangi ya kijani.
Uso wake ulikuwa ni ule wa utulivu na kujiamini akionyesha ishara ya kumsalimia mwanaume mwingine ambaye alikuwa amekaa eneo la juu kabisa katika jiwe kubwa la madini ya rubi lenye kukaliwa na kiti cha Dhababu cha kifalme.
“Ewe Mfalme nimempata Joka mjumbe wa barafu lakini amejeruhiwa , kutembea kwake kunaingiliana na maumivu hivyo atafika muda si mrefu baadae”Aliongea yule mtu ambaye sura yake haikuwa ikielezeka ilikuwa ni kama vile kila sifa ya kabila hapa duniani alikuwa nayo.
Mwanaume alieitwa mfalme ni wa makamo alieketi katika kiti cha kifalme ambacho ni kama kingo zake zilikuwa mifupa ya mnyama au ndege .
Uso wake ulikuwa ni ule wenye usiriasi mkubwa na mtu yoyote anweza kuhisi hofu kutokana na msisimko aliokuwa akitoa.
Huyo mwanaume ndio mtawala wa Majini Joka katika eneo lote la Korongo la Joka, alikuwa akifahamika kwa jina la Mfalme Wuja.
“Joka Mjumbe wa upepo umekuwa nje ya makazi ya kifalme kwa muda , je Joka mjumbe wa barafu aliingia matatizoni?”Aliongea kwa sauti yake nzito huku akiwa na uso ule usiokuwa na hisia za aina yoyote , haikueleweka alikuwa katika furaha , huzuni au majuto.
“Ewe mfalme, Joka mjumbe wa barafu alienda kufanya doria ili kuweza kutafuta malighafi ulizohitaji lakini alipata ukinzani kutoka kwa Bashe na Yawaragi , wanajeshi wa miliki ya Mbweha wa Jade , kulitokea mpambano mkali kati yao “Alijibu Joka mjumbe wa upepo.
“Nadhani huyo Mbweha aliweza kuhisia kitu na ndio akatuma watu kwa ajili ya kumchunguza lakini licha ya uwezo wake hawezi kulinda kila mtu ndani ya miliki yake , lakini Je Joka mjumbe wa barafu ameweza kukamilisha misheni yake?”
Joka mjumbe wa upepo alitaka kuongea lakini aliingiliwa na sauti kutoka nyuma yake
“Ewe Mfalme , Joka Mjumbe wa barafu amefika”Baada ya sauti ile kutoka kwa kijakazi ghafla tu lilionekana Joka kubwa la rangi ya bluu lenye mabawa huku likiwa na kichwa ambacho kilikuwa kama vile kimezingirwa na barafu.
Baada ya kujibadilisha kutoka katika muonekano wa Joka aligeuka na kuwa binadamu wa kawaida ambaye alikuwa ni mzee kama wa miaka sitini hivi mwenye ndevu nyeupe na alievalia joho la rangi nyeupe ambalo limefungwa na mshipi wa rangi ya bluu kiunoni, kwa muonekano wake alikuwa ni wa kawaida kabisa.
“Ewe mfalme , niwie radhi kwa kuchelewa kwangu nimeweza kukamilisha misheni”Aliongea na palepale alitoa kijiboksi cha mbao kidogo na kukiweka hewani na palepale kilisafiri mpaka kumfikia Mfalme Wuja.
Baada ya mfalme Wuja kupoktea kiboksi kile alikifungua ndani na palepale zilionekana chupa mbili kama vibuyu za madini ya Jade .
Ijapokuwa chupa hizo zilikuwa zimefungwa kwa juu lakini hazikuweza kuzuia harufu ya damu iliokuwa ikitoka ndani yake.
Mfalme wa Majoka bwana Wuja macho yake yalichanua kwa msisimko mkubwa wa furaha na palepale alisimama na kuanza kutoa cheko kubwa ambalo lilisababisha mwangwi na dakika hio hio na ngurumo za Majoka ziliweza kusikika kila kona kwa kupokezana kusindikiza furaha ya mfalme.
Kwa mtu wa kawaida angeweza kutishika kwelikweli lakini kama utazoea na kuelewa huo ni wakati wa mfalme kuwa na furaha basi usingeweza kuogopa.
“Haha.. umenishangaza sana , nilikuwagiza kwenda kupata damu ya majini pepo ya levo ya anga na mashetani wa anga lakini wewe umeweza kuniletea damu ya majini pepo anga saba na mashetani ya anga sita , hebu nielezee kwa haraka umewezaje kufanya haya yote kuzidi matarajio yangu , Joka mjumbe wa upepo amesema pia ulijeruhiwa , je mejeraha yako ni makubwa zaidi ?”Aliuliza Mfalme Wuja huku akimwangalia Joka mjumbe wa barafu.
Joka mjumbe wa upepo mwenyewe alikuwa katika mshangao , alijua mwenzake aliweza kutimiza misheni lakini hakuwa na taarifa kama aliweza kwenda zaidi ya kile alichoagizwa na kuua zaidi ya majini kumi na tatu wa mashetani wa anga kutoka msitu wa Mianzi Zambarau pamoja na Majini pepo wa anga kutoka utawala wa Mbweha.
“Ewe mfalme haya yametimilika kutokana na rehema zako, nilikuwa kwenye hatari kubwa wakati nilipokuwa nikipambana na Bashe na Yawaragi katika mpaka wa mlima wa Theluji wa Joka jekundu na Msitu wa Kiza , nilidhani ninakwenda kushindwa kukamilisha misheni lakini mgeni wa kibindamu mwenye uwezo usio wa kawaida aliweza kunisaidia na kuwashinda”
“Mgeni!!? Binadamu mwenye uwezo usiokuwa wa kawaida?”Aliongea Mfalme Wuja huku akionekana katika mshitoko wa taarifa ile.
“Nimeweza kupewa taarifa kuna binadamu mwenye mafunzo ya kijini katika jiji la Jiwe Jeupe , je ndio unaemzungumzia?”
“Nadhani atakuwa ni huyo , uwezo wake wa kijini ni wakutisha , mkubwa kuliko wa kwangu , aliniona wakati ambao nilikuwa nikizidiwa nguvu hivyo akachukulia hio kama nafasi na kumuua Bashe na Yawaragi na tukaweza kupata damu yao , alikuwa akitafuta Mnara wa kuweza kutoka katika huu ulimwengu na nikamdanganya kwamba nitamuogoza , kupitia safari nzima nilichagua njia ambazyo zinalindwa na majini pepo anga na kwa msaada wake tuliweza kuua majini anga wengi ambao walitaka kutuzuia , tuliweza kuagana mara baada ya kufika katika mpaka wa Msitu wa Kiza na ndipo nilipomuelekeza kuelekea katika jiji la Jiwe Jeupe na ndipo nilipofanya safari ya kwenda katika bonde la Ziwa kupata damu ya kutosha kutoka kwa mashetani wa anga lakini nilifanikiwa kuyashinda sita tu na ndipo nilipoanza kupungukiwa na nguvu zangu , kwasababu ya hilo walianza kunifukuza na kupatwa na jeraha na ndipo Joka Mjumbe wa pepo alipotokeza na kunisaidia”
Wuja alibadilisha uelekeo wa macho yake na kumwangalia Joka mjumbe wa pepo kwa namna ya kiulizo.
“Ewe Mfalme , niliweza kumkuta Joka mjumbe wa barafu katika mpaka wa bonde la Ziwa na Korongo la Joka , Mkuu wa mashetani Anga bwana Zao alikuwa amejificha muda wote katika Msitu wa mianzi Zambarau, baadhi ya Shetani wa anga wamekuwa dhaifu kuliko mwanzo pengne ndio maana Joka mjumbe wa barafu ameweza kuwaua”
“Nyie watu mnafikiria sana , Joka Mjumbe wa barafu ameyahatarisha maisha yake kwa ajili ya kuniletea damu , siwezi kumshuku hata kidogo, Joka Mjumbe wa upepo msindikize Joka Mjumbe wa Barafu kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu na kupona , kwasasa hupaswi kufanya misheni yoyote mpaka siku ya mashindano”
“Mfalme je damu hio inatosha?”Aliuliza Joka mjumbe wa barafu.
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , Joka Mjumbe wa barafu umefanya kazi nzuri , unaweza kuondoka sasa”
Joka Mjumbe wa barafu alisita kidogo na kisha akamgeukia mfalme Wuja akionekana na swali
“Ewe mfalme je naweza kujua nani ambaye anakwenda kutuwakilisha katika mashindano yanayokwenda kuanza ndani ya wiki mbili?”
“Kwanini unauliza ?”
“Sijawahi kushiriki hata mara moja na natamani nishiriki, nataka nidumishe mfululizo wa ushindi wetu”
“Nitafikiria juu ya hilo , unaweza kuondoka sasa”
Joka Mjumbe wa pepo alionekana kusita sita lakini alikubali na kuondoka na baada ya kutoka nje aliweza kurudi katika hali ya U’Joka na kuondoka katika ngome ya kifalme.
Upande Mfalme Wuja aliangalia Majoka mawili yakipaa hewani kupitia dirisha na kisha akageuza macho yake kwenye vile vibuyu viwili vya damu huku akiwa na uso usiokuwa ukielezeka.







SEHEMU YA 611..
Roma alikuwa amepoteza hata hesabu ya muda kutokana na kufungiwa gerezani kwa muda mrefu.
Mwanzoni alikuwa amehukia sana na alikuwa na hasira kuja katika ulimwengu huo na kujikuta gerezani lakini kadri muda ulivyokuwa ukisogea alijikatia tamaa huku majonzi yakianza kumvaa na aliona ni kama vile karne moja imepita tokea aingizwe hapo ndani.
Kitaalamu Roma hakupaswa kuwa na wasiwasi au kuathirika kwa kufungiiwa sehemu kama hio lakini aliweza kuona hakuwa na chochote cha kufanya ndio kilichomfanya kuingiwa na majonzi.
Mawazo yake hayakutoka mbali na usalama wa mke wake , Binti yake, warembo wake na Sophia ambaye hakuweza kumuona tokea waingizwe hapo ndani.
Alijiambia ni kipi kitatokea kama ataendelea kubakia hapo kwa muda mrefu .
Kila wazo baya likimjia Roma alijikuta akipambana na ukuta akidhamiria kuharibu hilo gereza kwa kupitia nguvu zake ambazo zishamrudia lakini licha ya kujaribu hivi na vile hakukuwa na matokeo chanya na kuishia kujikalia chini kwa huzuni.
Haikujalisha ni marangapi amejaribu lakini nguvu zake zilikuwa zikimwishia tu huku yeye akishindwa kuwasiliana na elementi za mbingu na ardhi.
Alishindwa kuelewa kwanini Aoiline hakumuua mwanzoni wakati alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, pia Roma hakuweza kuwa na uhakika kama akifa hapo uungu wake unaweza kutoka katika ulimwengu huo na akazaliwa katika mwili mwingine
Muda ulisonga bila ya yeye kuelewa na hatimae ufa wa mwanga uliweza kuonekana juu yake, kitendo cha mwanga kuingia ndani Roma hakutaka kuchelewa na kuhitaji kuondoka katika hilo gereza.
Lakini kabla hata hajatoka mtu mwingine alidondoka chini na palepale mlango wa gereza ukajifunga.
Roma kwa kutumia macho yake ya kichawi aliweza kumuona ni Sophia na palepale hakutaka kujiuliza mara mbilimbili na alimsogelea na kumkumbatia.
Sophia alionekana kupoteza fahamu lakini kwa haraka haraka mara baada ya kumkagua alionekana alikuwa hana tatizo lolote na hata uso wake wa kirembo ulionekana wa moto , hivyo moja kwa moja aliona alikuwa akiishi vizuri.
Wakati Roma akipumua kwa ahueni mwenyewe kwa kuwa na wasiwasi mkubwa , Sophia aliweza kuamka.
“Bro Roma …”Aliita Sophia huku akimwangalia Roma katika giza.
“Una macho makali kweli , umeshanijua ni mimi?”Aliuliza Roma.
“Ni kwasababu naijua harufu yako”Aliongea kwa kumnong’oneza huku akiona aibu za kike.
Roma alijikuta akikosa cha kuongea katika hali hio isiokuwa ya kawaida na aliishia kumuweka Sophia chini kwani alikuwa mikononi mwake amempakata.
“Kwanini upo hapa , Aoiline kuna kitu chochote ambacho amekufanyia?”Aliuliza Roma akibadilisha topiki haraka.
Sophia alijisogeza karibu kabisa na Roma kama kujikumbatisha kana kwamba anaogopa kutenganishwa nae tena huku akitingicha kichwa kukataa.
“Alikuwa mzuri kwangu na alisema ni kwasababu mimi ni mpole na mkarimu..”Aliongea na kumfanya Roma kucheka.
“Inaonekana tayari ukarimu wako umekwisha kulipwa , hivi ananichukia kwasababu tu sikutaka kuondoka nae akiwa katika sura tofauti?”Aliuliza lakini Sophia hakujibu swali lake na alinyoosha mkono wake kujaribu kushika uso wa Roma.
Joto la vidole vyake lilimfanya Roma kutulia , kwa jinsi Sophia alivyokuwa akimshika Roma usoni ilikuwa ni kama vile anashika kitu cha thamani kubwa ambacho hataki kiharibike.
“Sophia unafanya nini?”Roma alitaka kutoa uso wake usiguswe lakini alishindwa kufanya hivyo zaidi ya kumwangalia tu.
“Sikuioni vizuri kwasababu ya giza , nilitaka kukugsa nione kama umekonda?”
“Acha ujinga, na uwezo wangu wa kijini sina haja ya kula chochote , kwanini nikonde , ukiachana na hayo kwanini amekungiza humu na wewe pia?”Sophia alijikuta aking’ata lips zake na kisha akapeleka sura yake chini.
“Nilitaka kuwa karibu yako , nitakaa na wewe hapa kwasababu hataki kukutoa”Aliongea na kumfanya Roma kukunja ndita .
“Kwanini unakuwa mjinga, huwezi kunisaidia chochote hapa , kwanini umekuja kwa ajili ya kupitia mateso wakati ulikuwa ukiendelea vizuri huko juu , wewe sio mimi na nguvu zako bado hazijafikia hata levo ya Nafsi , hutoweza kuchukua muda mrefu na aina hii ya chuma”
“Kwanini nisiweze , ni chaguo langu kwenda popote ninapotaka , Roma kama ulikuwa ukipanga kuongazana na mtu mzigo kama mimi kuelekea katika ziwa la Mbingu , kwanini nishindwe kukaa na wewe katika gereza hili la chini ya ardhi?”
“Ni tofauti “Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la uchungu.
“Tofauti yake ni nini ,, nimetaka tu kuwa karibu yako, sikuweza kuwa karibu yako katika ulimwengu wa kawaida kwasababu ya dada yangu , je lazima nijizuie hapa na kukaa mbali na wewe licha ya kwamba sina uhakika kama tunaweza kutoka unajua ni kwa kiasi gani nilikuwa na wasiwasi juu yako wakati wote ambao ulikuwa hapa mwenyewe , unajua ni kwa kiasi gani nilikumisi na ni kwa kiwango cha namna gani nimeweza kujichukia kwa kutoweza kukusaidia kwa chochote ?”Aliongea huku akianza kulia kwa kwiki na kumfanya Roma kumwangalia namna anavyotoa machozi , ukiachana na mara ya kwanza ambayo Roma alikutana nae kule Japani, Sophia wa muda huo alionekana mwenye kupendeka.
“Sophia ,, nisamehe ,, hicho sio nilichokuwa nikijaribu kumaanisha”Aliongea Roma huku moyo wake ukifurukuta na Sophia alitingicha kichwa kwa masikitiko.
“Haishangazi ndio maana watu wanasema sehemu ya mbali zaidi katika ulimwengu ni kusimama mbele ya mtu unaempenda lakini haelewi chochote kuhusu hisia zako , licha ya kwamba nakupenda sana lakini siwezi kusema nakupenda , Roma sitaki kuwa mtu mzuri tena wala kuwa dada mzuri kwa Edna , moyo wangu umechoka , mimi bado mdogo na nataka kuwa mbinafsi pia , je unaweza kunikubalia msichana mbaya kama mimi niwe mpenzi wako?”Sophia alifunguka.
Hewa ya humo ndani ni kama ilikuwa haitembei wakati akimwangalia Sophia , ijapokuwa alihisi aibu na wasiwasi lakini moyo wake ulikuwa ukilia kwa ajili yake .
Kwa kipindi chote alikuwa akijitahidi kuubadilisha upendo wake na kumuona kama ndugu yake , ijapokuwa Sophia alionyesha hisia zake waziwazi lakini Roma hakutaka kuvuka mstari.
Alikuwa akihofia ni maamuzi gani ambayo Edna atachukua , ijapokuwa alikuwa amemuumiza kwa mara nyingi kwasababu ya wanawake wengine lakini Sophia alikuwa ni wa kipekee.
Licha ya kwamba Sophia na Edna hawakuwa na undugu wadamu lakini bado alimchukulia kama mdogo wake Edna.
Edna asingeweza kumchukulia Sophia kama wanawake wengine kutokana na kwamba jina lake lilikuwa na muunganiko mkubwa na familia ya Sophia.
Zamani Sophia alikuwa akijizuia kutokuonyesha hisia zake waziwazi kwa kuogopa kugundulika mbele ya dada yake na hata kuamua kwenda kujichimbia katika matemple ya wachina, lakini katika mazingira kama hayo katika ulimwengu mwingine hakutaka kujizuia , ilikuwa ni kama ile minyororo isiokuwa imemfunga ilikuwa imemuachia na sasa alikuwa huru kuwa karibu na mwanaume anaempenda.
“Sophia .. siwe.,.”
Roma alikuwa akijaribu kumkatalia lakini kabla hata hajamaliza sentensi yake lipsi za midomo yake zilivamiwa.
Sophia hakuwa na mchezo alimsogelea Roma nakupitisha mikono yake kwenye shingo yake na kuanza kumbusu kwenye mdomo na haikuwa kugusanisha tu Lips kwani palepale alipanua mdomo wake na kutoa ulimi nje na kuutumbukiza katika mdomo wa Roma.
Roma alikuwa akiweza kabisa kunusa harufu ya ubikra ya Sophia kupitia ulimi wake.
Sophia kwa namna ambavyo alikuwa akimbusu Roma ilikuwa ni kama vile maisha yake yote anayakabidhi kwake kupitia busu hilo , ni busu ambalo liliwakilisha uvumilivu , hamu na kila kitu kuhusu yeye.
Roma alikuwa hahisi chochote mwanzoni kuhusu busu hilo ,pengine ni kwasababu ya mstari ambao alikuwa ameuweka kati yake na Sophia lakini kadri Sophia alivyyokuwa akichezesha ulimi wake katika midomo yake pumzi yake ilianza kubadilika na kuwa nzito huku akili yake ikianza kuyumba
Bila kujielewa Roma alijikuta akianza kumsugua sugua Sophia katika mgongo wake akionekana ashaanza kukolea.
Sophia licha ya kuwa mzuri wa sura lakini hakuwa na shepu kubwa kuliko wengine lakini bado mwili wake ulivutia sana kimapenzi.
Roma pumzi zake zilizidi kuwa nzito na moyo wake ulizidi kuongeza kasi ya kusukuma damu na mwili uliomkumbatia ulikuwa ndio dawa pekee ya ugonjwa unaoanza kuonyesha dalili.
Mwanamke aliekuwa na hisia nae ameweza kumwelezea hisia zake katika ulimwengu mwingine na alijiambia huenda ni stori nzuri ya kimapenzi wanaitengeneza.
Roma alianza kujidharau yeye mwenyewe kwa kuwa muoga, hakuweza hata kuzielezea hisia zake kama Sophia alivyofanya.
Viungo vya mwili wake vilikuwa vikimuumbua na unafiki wake.
Mkono wa Roma ulikuwa ushatoka na kuingia ndani ya nguo yake na kuanza kuminya minya embe dodo zilizokuwa zinamchoma kiufan..
“Nakupenda sana Sophia ..”Aliongea lakini wakati sauti hio ilipomtoka mdomoni Sophia alimsukuma na kurudi nyuma akijitoa kwake.
Roma alimwangalia kwa macho ya mshangao lakini palepale aliweza kumuona Sophia akimwangalia na tabasamu la dharau .
Mikono yake bado ilikuwa hewani na alijikuta akimeza mate mengi mara baada ya kugundua kuna kitu hakipo sawa.
Tabasamu la dharau lilizidi kuonekana waziwazi mbele yake na kufanya moyo wake kuanza kutoa kilio.
“Wewe ni… wewe ni Aoiline na sio Sophia ?”
Jasho lilimtoka mwanaume huku akiongea kwa sauti na kumfanya Sophia kutoa cheko kubwa na ni kama anga linachezeshwa na palepale Sophia alibadilika na kuwa Aoiline.
Roma alitamani kutoa kilio , alichezewa akili kwa kiasi kikubwa sana, alijiambia ndio maana ilishangaza Sophia aliweza kumtongoza vizuri sana licha ya kwamba bado alikuwa bikra , kumbe alikuwa ni jini mzoefu Mbweha wa mikia tisa.
“Wewe mkorofi kwanini unaangalia chini mara baada ya kuchezewa na mimi”Aliongea Aoiline kwa kumtania.
Roma alijikuta akiona aibu kwa kuweza kudanganywa , lakini katika hali kama hio aliweza kulaumu uwezo wake wa kijini , mbinu yake ya kujibadilisha muonekano wake na kuficha uwezo wake ilikuwa ni ya kutisha.
Sasa mara baada ya kujua huyo alikuwa ni Aoiline je Sophia yupo wapi?.
“Sophia yupo wapi na umemfanya nini?”
“Vipi , ndio unaanza sasa kumuwazia si ndio, unahisi naweza kumdhuru?”Aliongea huku akizungusha nywele zake kimapozi.
“Kama utathubutu kumdhuru basi lazima nilipize kisasi hata kama siwezi kukushinda”Aliongea Roma kwa hasira huku sauti yake ikiwa nzito.
“Hebu muone sasa , kama wewe sijakuuwa kwanini nimuue msichana mdogo kama yeye , kumwaga damu yake hakuna thamani kwangu”
Roma alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kusikia maneno hayo lakini bado hakuweza kuacha kujiona mjinga kwa kuweza kudanganywa na kuchezewa na huyo mwanamke kama mdoli, aliumia kwasababu ilikuwa mara yake ya kwanza kufanyiwa hivyo na mwanamke.
“Vipi , bado tu hujatosheka na unataka kufanya kale kamchezo hapa hapa gerezani?”Aliongea akimwangalia kwa macho ya utani.
“Hehe.. kama utakuwa tayari mimi sina tatizo , nishafanya ngono na wanawake wengi lakini bado sijawahi kumuonja Mbweha wa mikia tisa”Aliongea huku akitoa tabasamu la hasira.
Aouline hakuweza kujali maneno yake ya kiuchokozi , alikuwa na uwezo wa kudhibiti hasira zake kwa kuishi miaka mingi .
“Sina muda wa kupoteza hapa, nimefanya haya yote ili kumfumbua macho Sophia namna rangi yako halisi ilivyo , nilitaka kumuonyesha kwamba shemeji yake Roma Ramoni ni Casanova ambaye anawaza kumla”
Roma alijikuta akishangazwa na maeneno yake na hata ile hasira iliokuwa ndani yake ilipotea ghafla .
“Unaongea nini wewe , kwahio unamaanisha Sophia anajua hiki kilichotokea?”
“Haha..unaniona mimi mjinga eti , unadhani siwezi kuweka Kamera za kiunlizi hapa?”Aliongea na palepale alipiga mwanga wa rangi ya bluu kwenye ukuta kama vile ni Projector na ndani ya dakika tu eneo la nje katika makazi ya kifahari ya mrembo Aoiline yaliweza kuonekana
Ilikuwa ni eneo la ukumbi ndani ya jumba hilo la kimalkia na Sophia alikuwa amesimama kwenye kioo huku uso wake ukiwa mwekundu na wa aibu.
“Hizi chuma sio za kawaida ndio maana nilikwambia zimetokea chini ya bahari isio na mwisho, zinaweza kuonyesha kila kinachoendelea hapa kupitia kioo kwa teknolojia nje ya fikra za kibinadamu , hivyo Sophia kaona kila kitu “Aliongea Aoiline kwa kujivunia.
Miguu ya Roma ni kama ilikuwa ikimlegea , hali hio tatanishi ilimletea kwa kiasi kikubwa hali ya hatia , lakini kwa bahati nzuri ni kwamba Roma hakuwa na aibu , sasa kila kitu kipo wazi aliamua kumsalimia Sophia kwa kujifanyisha hakuna kilichotokea.
“Sophia ni makosa yangu kwa kukufanya uwe hivyo , sitokaa mbali na wewe tena hata kama tukiweza kutoka katika huu ulimwengu”Aliongea Roma , hakujua cha kufanya kwani aliweza kuonyesha hisia zake wasiwasi kwa Sophia feki na siri yake kuwa wazi.


SEHEMU YA 512
Sophia alifurahishwa na maneno ya Roma lakini kwa wakati mmoja alishikwa na aibu, ni machozi pekee alioweza kuyatoa akishindwa kuzuia furaha yake, ile hali ya kumngojea kwa muda mrefu hatimae imeondoka na kila kitu kipo katika wakati uliopo , kila kitu cha kuufanya ulimwengu wake uwe na furaha kipo mbele yak.
Aoiline baada ya kuona namna ambavyo mwanaume Roma Ramoni asivyokuwa na aibu palepale alifunga kioo na kumfanya Roma asiendelee kuwasiliana na Sophia.
“Hivi wewe mkorofi kwanini bado unaigiza kuwa kama Casanova ilihali tayari umeoa , ndio kwamba unajjivunia kwasababu Sophia amekufa na kuoza juu yako?”
“Mimi ni mwanaharamu tu lakini bado sijawahi kutotimiza wajibu wangu , nitawajali kama nawapenda na hakuna mtu ambaye anaweza kuzuia hisia , ninchoweza kufanya ni kuwalinda wanawake wangu mbali na hatari , sifanyi kazi kikamilifu lakini nafanya kila linalowezekana kutimiza haja zao”
“Hakika wewe ni jasiri”Aliongea kwa kumtania.
“Kwanini niwe muoga ilihali dhamira yangu ni ya wazi , mwanaume mwingine ana mwanamke mmoja lakini hakidhi haja zake zote , mimi sio mwaminifu kwa mke wangu lakini ninampenda kiasi cha kutoa uhai wangu kwa ajili yake , licha ya yote yanayotokea naamini ataendelea kunielewa”
“Hakika huna aibu kwa kusema hayo ukiwa na uso usio kuwa na hatia hata kidogo”
“Nadhani sifanyi kosa ilimradi uovu wangu siufichi , mimi ndio mimi na tabia zangu zipo wazi”Aliongea na kumfanya Aoiline kumwangalia kwa macho yasiokuwa na hisia kabla ya kuanza kutoa kicheko.
“Kama yule mtu angekuwa kama wewe , mkweli wa hisia zake..”
“Yule mtu , unamzungumzia nani?”Aliuliza Roma kwa mshangao mara baada ya kumuona Aoiline kaishi njiani.
“Ni wapi ulijifunza mbinu ya Andiko la nguvu ya Urejesho isio na kikomo?”Aliuliza na kumfanya Roma kuwa katika mshangao ,alijiambia anajua mbinu yake kama alivyotarajia.
“Nilikutana na Master mwenye asili kutoka milima ya China, ndio alienielekeza “
“Master wa asili ya kichina..?, niseme kwamba hakika unakipaji kikubwa, hio mbinu ndio kubwa sana dunia nzima na ni ngumu mno , unaweza kukutana na yule mtu kama utaweza kufika levo za juu kabisa za kuhimili mapigo ya radi”Aliongea na kumfanya Roma kuzidi kujiuliza huyo mtu mwenye mbinu kama ya kwake ni nani kwanini hataki kumtaja jina.
“Basi sawa , wewe mkorofi nina kazi nataka kukupatia?”
“Kazi gani?”
“Ushasahau tayari kuhusu shindano la kuingia kwenye mnara , siwezi kushiriki mimi”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.
“Kwahio unasema kwamba mimi ndio napaswa kukuwakilisha katika mashindano hayo?”
“Ni kazi ambayo ni kama nakusaidia , bingwa wa hayo mashindano ataweza kupata madawa mengi na Hazina ambazo zipo ndani ya mnara, isitoshe nimekusaidia kuweka hisia zako wazi na kujipatia mpenzi mwingine , unapaswa kuwa na shukrani”
“Mimi sina shida ya kushiriki isitoshe ndio ulikuwa mpango wangu , lakini je una uhakika ninaweza kshinda?”
“Haiwezi kuwa tatizo kwako mshindani mkubwa ambaye unaweza kukutana nae ni Joka Mjumbe wa barafu kutoka miliki ya Korongo la Joka , sidhani kama anaweza kukushinda kutokana na uwezo wako , watu wangu mashindano yaliopita waliweza kushindwa lakini haimaanishi wana uwezo mkubwa”
“Kwahio ulitaka nibakie hapa ukiwa na nia ya kunifanya mimi ndio nikakuwakilishe , huogopi kwamba ninaweza kupotea moja kwa moja kwenye mnara mara baada ya kupigwa na radi tisini na tisa?”
“Wewe mkorofi hakika una mawazo mengi ya kufikirika, kwanza huwezi kumuacha Sophia nyuma na pili hata kama utaingia kwenye mnara lazima uingie katika floor ya kwanza ukiwa na mimi hivyo siwezi kukuruhusu”
Aliongea na kumfanya Roma kuona ni kweli yupo sahihi , hawezi kuondoka katika huo ulimwengu na kumuacha Sophia nyuma.
Baada ya kukubaliana Roma alitolewa katika gereza hilo na kuingizwa sasa ndani ndani kabisa kwenye jumba hilo la kimalkia ambalo liliwakilisha ufahali wake katika jamii ya majini pepo.
Sophia alijikuta mapigo ya moyo wake yakiongezeka mara baada ya kumuona Roma , ijapokuwa alikuwa na aibu lakini kitendo cha kumsubiria kwa muda mrefu kumfungukia kilimfanya kujawa na hamu ya kumsogelea na kumkumbatia.
“Punguza presha , au na wewe unataka nikufanyie kama nilivyomfanyia Mbweha?”Aliongea Roma mara baada ya kumpa Sophia Kumbatiao lakini alionekana kuwa na wasiwasi sana kiasi cha Roma kusikia mapigo ya moyo wake yakienda kasi kasi.
“Sio hivyo..”Aliongea Sophia huku akijitoa na kumwangalia kwa wasiwasi Aoiliine akiogpa Roma anaweza kumkasirisha tena na kuishia kurudishwa katika gereza la chuma.
Aoiline hakujali sana kuhusu wao na alisogea na kukaa katika kiti chake cha kimalkia na kama kawaida yake aliangalia katika lile tundu linalopitisha mwanga na aliingia katika mawazo kana kwamba kuna kitu ambacho anakisubiria kwa hamu lakini hana uhakika kama kitatokea.
Dakika hio hio mwanga wa kijani uliweza kuingia katika hilo eneo kwa spidi kali na ndani ya sekunde tu alitokezea mwanaume kijana.
Kutokana na spidi aliongia nayo ilimshangaza Roma hususani katika eneo hilo ambalo hakua na spidi kutokana na kikwazo cha anga.
Alikuwa ni mwanaume wa rika la Baiju na alikuwa kwenye levo sawa na yeye ya daraja la nane lakini spidi yake pengine ni kubwa kuliko ya Baiju.
“Bwana wangu nina taarifa kwako ya dharula”Aliongea huku akionyesha kutomjali Roma na Sophia waliokuwa hapo ndani.
“Iluwa je kuna kitu chochote kimetokea katika mpaka wetu tena?”
“Ndio, Bashe na Yarawagi waliokuwa wakilinda mpaka kati ya Msitu wa Giza na mlima wa Joka jekundu kudumisha maagizo yako waliweza kuendelea na kazi zao kama kawaida lakini jana wakati natembelea kufanya dolia niliweza kugundua …”Alishia njiani.
“Umegundua nini , unaweza kusema?”
“Bashe na Yawaragi hawakuweza kuonekana katika nafasi zao , hakuna viashiria vyvoyote vya Aura zao pia , Huji na wenzake waliweza kupatikana lakini katika eneo ambalo kuna kila alama za mapigano , hivyo ninaamni watakuwa wameuliwa”
“Ukiburi…!!!”
Aliongea kwa sauti huku akisimama na palepale aliachia mkandamizo wa hewa wa kijini usiokuwa wa kawaida na kufanya vijakazi na wahudumu wote kuinamisha vichwa vyao chini kusujudu wakiomba huruma , Iluwa na yeye alikuwa amesujudu hivyo hivyo akiwa kama wengine tu.
Roma alikuwa tayari ashamkinga Sophia wakati akijaribu kushindana na hasira za Mbweha wa mikia tisa , alikuwa akiogopa na alijiambia siku ya jana hakuonyesha uwezo wake wote lakini hapo ilikuwa ni zaidi ya jana yake , aliona kabisa nguvu zake ni kubwa mno na zisizo za kutabirika.
Alijiuliza kama alikuwa na nguvu hizo katika mazingira haya yenye vikwazo vipi siku ambayo atatoka nje.
Roma mwenyewe alikuwa katika levo zaidi ya daraja la sita kama atahesabiwa kwa namna yao lakini bado tu alishindwa kuona uwezo halisi wa Aoiline, alijiuliza au ni zaidi ya daraja la tisa.
“Pumbavu zako wewe Mfalme Wuja , mara ya mwisho umetuma watu wako na kuumiza watu wangu lakini nikaamua kupotezea lakini awamu hii ukaamua kuvuka mpaka na kunichokoza ten.”Aliongea kwa hasira.
“Bwana wangu una mpango gani au ni wewe mwenyewe unaenda kuwaadhibu?”
“Niende mimi? Wanayo hata hio thamani ya jitihada zangu?”
“Bila shaka hawana”Aliongea huku jasho likimtoka katika paji la uso.
Aoiline anaweza kuwa mtu mcheshi muda mwingine lakini anapochokozwa anakuwa ni mtu mwingine kabisa .
“Unaweza kuondoka sasa , kuhusu mipaka hupaswi kufanya lolote , agiza majini pepo wa anga kurudi katika mamlaka zao na wape maelekezo walio chini yao kuchukua nafasi zao”Aliongea na Iluwa akikubali agizo lakini bado alionekana kusita kuondoka.
“Bwana wangu bado nimechanganyikiwa kuhusu jambo moja”
“Ongea”
“Waliochini ya Mfalme Wuja , Majoka matano wapo katika levo ya daraja la nane na sisi majini pepo wa anga tunaweza tusifanikiwe kuwashiinda kwa mapigano ya ana kwa ana lakini kama Bashe na Yarawagi walipigana wakiwa pamoja wasingeweza kufa kirahisi,, labda tu kama kuna mtu mwingine ambaye aliingilia”Aliongea akiwa ameikunja ndita na Aoiline alimuona ana hoja lakini mara baada ya kumwangalia Roma alipumua.
“Unaweza kuondoka nina mango wangu kichwani”Aliongea na kumfanya Iluwa kuchangayikiwa lakini alikubali kuondoka kufumba na kufumbua.
“Nadhani umeweza kusikia majini wa Korongo la Majoka wamekuwa ni wenye viburi , nilikuwa ni mwenye uvivu kulipiza kisasi lakini wameenda mbali wakati huu hivyo nataka ukawape fundisho”
“Mim!?, si ni muda mfupi tu ulikuwa ukiniambia nijandae kwa ajili ya mashindano, lakini sasa hivi unataka tena niende kwenye Korongo la Majoka , vipi kama nitakutana na mfalme wao , ninaweza kufa”
“Unaogopa nini? Unadhani Mfalme Wuja yuko huru mpaka mkutane , hawezi kukufanya chochote ilimradi tu huingi ndani ndani katika mamlaka yake , nataka ukaue baadhi ya Majoka ambao wapo katika levo ya Anga na utakuwa sawa”Aliongea na kumfanya Roma kutoa cheko na kufanya hata wale vijakazi kushangaa maana ni yeye pekee ambaye alikuwa akioongea kwa kjisikia mbele ya Aoiline.
“Je hayo yote ni kwasababu ya kulinda hadhi yako tu , unaniambia hawezi kusadia chochote hata kama watu wake watakuwa wanakufa ndio jinsi mnavyoongoza?”
“Ni sheria ya msituni , kuishi ni kwa mwenye nguvu zaidi , kama unasema tunapaswa kusaidia waliodhaifu kwanini nyie binadamu mnawinda wanyam atofauti na kuwasaidia?”
“Binadamu tunasaidia binadamu , isitoshe nyie wote ni majini, si ndio?”
“Wewe ni mjinga , sijawahi kusema sisi wote ni wa ukoo mmoja, isitoshe nguvu ndio kila kitu , walio chini yangu wananitegemea kwa ajili ya kuishi maisha yasio na usumbufu , wana deni kwangu lakini wao hawanidai hivyo sio jukumu langu la kuwalinda , sijali kuhusu vifo vyao najali kuhusu hadhi yangu , ninachomaanisha kama nyama ya mnyama uliemla leo ana nguvu kuliko wewe je kwanini umle?,Hata kama nyie wawili mngekuwa ni viumbe tofauti mnaweza kuishi kwa amani , hivyo ni ujinga wao kufa ila mimi najali kurudisha hadhi yangu ,sifanyi hivi kulipiza nafanya hivi kulinda hadhi yangu”
Roma alijiambia huyu ni ‘Psycho’ kitu kinachoharibu urembo wake lakini kwa asilimia fulani maneno yake kidogo yalileta maana.
“Sitaki kupingana na wewe , lakini nitakusaidia kama utaniambia nini sababu ya hii migongano, Sidhani kama ni jambo linalohusisha hasira zenu pekee”Aliongea na kumfanya Aoiline kushangazwa na swali lake.
“Sijui chochote na pia sitaki kujua ni mpango gani anao mfalme Wuja , hivyo kwangu siwezi kupoteza muda kuwazia , huenda mpango wake ni kutaka kunishinda au kutoka katika huu ulimwengu , sina matamanio ya kujua mipango yake”
“Kama ni hivyo basi angalau unipe zawadi kwa kukusaidia”
“Kutokumuua mpenzi wako ndio zawadi yangu kubwa kwako”Aliongea huku akimwangalia Sophia kikauzu.
Roma alijiambia hana chochote cha kufanya mbele ya mwanamke huyo na kitu pekee cha kufanya ni kutii maagizo yake.
“Unapaswa kuondoka mapema , kwa spidi yako angalau unaweza kutumia siku sita mpaka saba kwenda na kurudi , utarudi ndani ya muda muafaka wa mashindano”Aliongea na kisha palepale alimrushia Roma Karatasi iliokunjwa kunjwa(Scroll).
Roma aliichukua na kisha aliifungua ndani na kusoma kilichoandikwa na alijikuta akipagawa mara baada ya kugundua ni maandiko yaliopo katika Code maalumu , aliweza kusoma kutokana na kujua baadhi ya historia muhimu.
“Kumbukumbu za utengenezaji wa vidonge vya kijini kutoka kwa Malkia Tushani”Ndio Roma alivyoweza kutafsiri andiko hilo.
Inasemekena Roho ya malkia Tushani ilihusishwa na nafsi ya Mbweha wa mikia tisa kama mlinzi mkuu , yaani mlinzi wa nafsi tokea kufa kwake.
Sasa kusemekana huko kulionekana ni kweli mara baada ya Roma kuona Aoiline kuwa na kumbukumbu ya Andiko lake.
“Ukoo wangu ulikuwa na mahusiano mazuri na binadamu wa kawaida tokea ustaarabu wa kibinadamu ulipoanza , tunazo mbinu ambazo hazihesabiki zinazohusiana na utengenezaji wa vidonge lakini bado hatuna ujuzi wa kutengeneza , hata hivyo hatukuhitaji vidonge kwa ajili ya uwezo wetu , nimekuona una dhana ya tanuru la maafa na unaweza kudhalisha moto wa rangi ya njano na nyeupe kwasababu ya nguvu ya andiko , naamini utakuwa ushajifunza namna ya kutengeneza vidonge, ondoka na hilo andiko la kikanuni, unaweza ukajitengenezea vidonge hivyo mbele ya safari kwani malighafi zake zinapatikna katika ulimwengu huu peke”Aliongea na kumfanya Roma kuguswa.
“Kwanini unanisaidia?”
“Unawakilisha miliki yangu katika mashindano , kwa uwezo wako ulionao ni dhiafu mno , hivyo napaswa kukusaidia”
Roma aliweka andiko lile katika anga la pete ya Sumeru na kumshukuru sana kwa kumpatia kanuni hizo.
“Huna haja ya kunishukuru na nenda katafute na ujue ni nani anamsaidia Mfalme wa Majoka kunidhalilisha, najua kuna unachofikiria lakini sitaki kukuuliza hivyo ondoka uende kama huna swali lingine la kuuliza , nitamlinda mpenzi wako mpaka utakaporudi”
Aliongea na kumfanya Roma kuvuta pumzi , mwanamke huyo alikuwa akimsoma mawazo yake kama vile ni kitabu.
Roma alikuwa akiwaza pengine ni Lekcha ambaye anasababisha hayo yote baada ya kuvutwa na yeye ndani ya ulimwengu huu.
Lekcha uwezo wake ulikuwa ukiimalika kwa kuweza kutumia miili ya wengine , kama atakuwa ameingia ndani ya ulimwengu huo na kuanza kuyatumia Majini hayo kwa faida zake basi angeweza kupata uwezo wa hali juu sana , isitoshe nguvu zake za ant-matter hazikuwa na kikwazo cha kimazingira.
Roma alikuwa na wasiwasi kwani kama atakutana nae inamaanisha siraha yake kubwa ingekuwa ni Cauldron pekee.
Hakutaka kupoteza muda na palepale aliondoka kwa ajili ya kutimiza maagizo ya Aoiline kwenda katika miliki ya Majoka kutoa fundisho.
 
Thanks bro singanojr pia usisahau ahadi

Najua sitonunua simulizi sababu bado mapambano na maisha ila angalau ni shabiki yako
 
Inaonekana siku Roma akitoka huku atakuwa hayar sana
Ndo hivyo mkuu we si unaona Sophia mwenyewe amepanda level na saa hivi anapaa ka tai jike. Ujuzi atakaoupata kutoka kwa malikia mbweha ili aweze kumwakilisha vyema kwenye pambano ukiongezea na vile vidonge itakuwa ni balaa. Lakini tusisahau akiweza kupona mapigo 99 ya radi atapanda level na uwezo kuongezeka kama ilivyofanyika kwa yale mapigo 9 ya hapo awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila Singano(kongole kwake) anaonekana ana story tamu sana akiifikisha hii mpaka mwisho itabidi ninunue story zake nyingine alizonazo ili nisome kwa muda wangu na spidi ninayoitaka. Kiukweli sipendi na ninaudhika na watunzi wasiofikisha story zao mpaka mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwamba anajua kutunga aisee
 
Back
Top Bottom