NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR
Mono no aware.
SEHEMU YA 652.
Rufi licha ya kwamba alijuwa uwepo wa Xiao Xiao ndani ya jiji la Dar lakini bado hakuamini kama angeweza kukutana nae katika eneo kama hilo la Kawe Beach.
Upande wa Xiao Xiao ukweli ni kwamba haikuwa mara ya kwanza kumuona Rufi, mara ya kwanza alivyomuona hakuamini kama anaweza kuwa Rufi lakini siku hio mara baada ya kumuona kwa mara nyingine hakutaka kudharau hisia zake na aliweza kuthibitisha ni yeye kweli.
Ilimshangaza kumuona Rufi nchini Tanzania mara baada ya miaka mingi ya kutoroka kutoka katika ulimwengu wa kijini.
Rufi licha ya kukamatika hakutaka kabisa kuongea na Xiao na palepale alikimbia kurudi ndani ya mgahawa na Xiao Xiao na yeye alimkimbilia kumfuata.
Roma mara baada ya kumuona msichana huyo wa kichina alikumbuka alivyokutaka nae mara ya mwisho mpaka kuja maeneo hayo hayo na kuachana .
Alikumbuka namna mrembo huyo alivyokuwa akimsumbua kwa kumtumia jumbe za meseji za kumtaka kimapenzi ambazo alidharau na kutomjibu mpaka akajikatia tamaa.
“Nini kinaendelea , kwanini Rufi anakimbiiana na yule mdada?”Aliuliza Amina ambaye alikuwa kwenye mshangao kama Roma .
Muda huo huo kabla Roma hajajibu Rufi alishawafikia na Roma alisimama mbele ya Rufi akimkinga na Xiao Xiao.
Mrembo yule wa kichina mara baada ya kumuona Roma alijikuta akijawa na mshangao kwani ni kama hakutegemea kumuona katika maeneo hayo.
“Hata wewe pia upo hapa , aisee kweli kilichopangwa hakikwepeki nadhani imepangwa tuoanane kwa mara nyingine”Aliongea Xiao Xiao akimwangalia Roma kwa furaha.
“Ndio nipo hapa pia , lakini kwanini unamfukuza Rufi?”
“Rufi!!?Oh.. nafahamiana nae ni shemeji yangu kwa kaka yangu”
“Huyo kaka yako ndio anaefahamika kwa jina la Xiao Hang?”Aliuliza Roma na kumfanya Xiao kutoa macho.
“Umejuaje jina la kaka yangu , au Rufi kakuambia kila kitu?”Aliuliza huku akiwa na mshangao , ingekuwa ngumu kwa Roma kujua jina la kaka yake kwani alikuwa akiishi huko katika jamii ya majini.
Roma hakujibu swali lake na palepale alimshika mkono yule mchina na kisha alianza kumvuta kumtoa nje ya mgahawa huo na ndani ya dakika chache tu walionekana wakiingia upande wa kushoto kwenye vyoo na mabafu ya kubadilishia nguo kwa watu wanaoenda kuogelea.
Amina yeye alikuwa kwenye mshangao kuona Roma amempeleka yule mchina kwenye mabafu .
Upande wa Lanlan hakushangaa kile kilichokuwa kikiendelea na alisimama na kwenda kuchukua kifurushi cha mishikaki na kurudi juu ya meza na kuendelea kula.
Upande wa yule mchina Xiao Xiao hakuelewa Roma anataka kumfanya nini na namna ambavyo alimshika mkono hakuwahi kufanyiwa hivyo na mwanaume na alijikuta mapigo yake ya moyo yakienda spidi spidi.
Pengine alijua labda Roma kadhamiria kwenda kufanya nae bafuni ndio maana anamwingiza huko.
Alikuwa mwekundu kama yai la kisasa kutokana na uzungu wake na aliishia kujiuliza ni kipi ambacho anapaswa kufanya ,ijapokuwa alikuwa akitamani kuonana na Roma kwa mara nyingine na kufanya nae mapenzi ili kuweza kumtumia kupanda levo lakini katika hali kama hio ya kushitukiza alijiona ni kama hakuwa tayari.
Upande wa wanaume ambao walikuwa kwenye mgahawa huo waliishia kumwangalia Roma kwa mshangao na wivu , ukweli ni kama walimdhania Roma na mchina huyo ni wapenzi kwani Xiao Xiao hakuleta ukinzani wakati wa kuvutwa na Roma mpaka kuingiziwa ndani ya mabafu.
Roma hakujali sana macho ya wengi yaliokuwa yakimwangalia , kwani mara baada ya kumfikisha Rufi kwenye bafu ambalo hutumiwa na wanaume aliwapa ishara vijana wadogo waliokuwa wakibadilisha mavazi kuondoka na walifanya hivyo haraka haraka na kisha wakakimbilia nje lakini mmoja wapo ambaye alikuwa mkubwa kidogo aligoma.
“Wewe kama nani mpaka kutuamrisha tuondoke?”Aliongea
Roma alikuwa na hasira na palepale alipiga ngumi ukuta kiasi cha kutengeneza ufa na jambo lile lilimuongopesha yule wmanaume na palepale alikimbia kuelekea nje akiwa kwenye mshangao.
Upande wa Xiao Xiao alikuwa akimwangalia Roma na macho ya aibu , huku akishindwa kuzuia kulegea kutokana na macho yake pamoja na uso ambao ulikuwa umetakata na kumfanya kumuona mtanashati.
Yeah Roma alikuwa amebadilika uso sana tofauti na mwanzo ambapo alikuwa mbeba mizigo , kipindi hicho alionekana kuwa Handsome sana , pengine ni kutokana na kupanda levo, kilichokuwa kikimpunguzia pointi ni aina ya uvaaji wake tu.
Roma alimshika na kumsukumia Xiao kwenye chumba kilichokuwa pembeni kushoto kwake na kisha akafunga mlango na palepale alikwenda kumkandamiza ukutani huku akimwangalia usoni kwa macho yasiokuwa yakielezeka.
Xiao alikwepesha macho kwa aibu huku akiwa na msisimko wa aina yake na alikuwa akisubiria kwa hamu hatua ya pili ambayo Roma anakwenda kufanya.
Ijapokuwa Roma alionekana kuwa siriasi hali ile ya ki uwanaume ilimfanya kuvutiwa zaidi na aliona kitakacho fanyika hapo ni yale mapenzi ya vurugu na hio ndio ilikuwa ‘Fantasy’ yake.
“Kufanyia hapa sio vizuri , kama vipi tufanye haraka haraka tuondoke…”Aliongea huku akionyesha hali ya aibu za kike na kumfanya kuzidi kupendeza..
Wanawake wa rangi nyeupe ni tofauti kidogo na wanawake wa kiafrika hususani katika swala la mahusiano , ni wawazi sana likija swala la mahusiano na anaweza akaruhusu ngono kufanyika hata na mtu ambaye hamjui vizuri.
Upande wa Roma mawazo yake yalikuwa mengine kabisa muda huo alikuwa akijiuliza ni kipi anapaswa kumfanyia , aliogopa kwamba kama ataenda kusema huko kwenye ulimwengu wao kama Rufi yupo Tanzania basi ingekuwa tatizo.
Roma hakutaka matatizo kwa wakati huo kwani nguvu zake za kijini hakuwa na uwezo wa kuzitumia kwa wakati huo na asingeweza kumlinda Rufi kama atakamatwa.
Mbaya zaidi kama itajulikana alikuwa na mahusiano na Rufi ndio ingekuwa tiketi ya majini hayo kuja kumvamia na kutaka kumuua maana alijua tabia yao namna moja ni kutopenda kudharaulika.
“Unataka nifumbe macho kwanza kabla hujaanza kunikiss… najihisi sipo tayari lakini unaonekana una hamu, hivyo sijali kama unataka tufanye , isitoshe nilikuwa nikikufikiria sana”Aliongea Xiao huku akiona pengine Roma alikuwa akiona aibu ndio maana alikuwa akimwangalia tu bila kuchukua hatua yoyote.
Xiao Xiao alikuwa ni mzuri haswa wa sura ijapokuwa alikuwa na rangi ya kichina lakini macho yake yalikuwa tofauti kidogo na wachina wa kawaida , kitu pekee ambacho hakuwa nacho ni umbo tu.
Roma alijiwazia alikuwa ameua watu wengi ambao pengine kati yao hawakuwa na hatia hivyo kujiongezea dhambi kwa kuua na mwanamke mrembo kama Xiao lisingekuwa tatizo.
Alijiambia kama mwanamke huyo ataendelea kuwepo hai basi siri ya uwepo wa Rufi nchini Tanzani itafichuka na ili kuficha siri hio kwa wakati huo hatua ya kwanza ni kumuua.
Baada ya kuwaza kwa muda palepale akili yake ilifanya maamuzi na shetani mtoa roho alimvaa na sura yake iligeuka na kuwa ile ya kikatili na palepale alipeleka mkono kwenye shingo yake.
Xiao alijua Roma alikuwa akitaka kuinua kidevu chake , hio pia ni moja wapo ya staili ambayo alipenda kufanyiwa na mwanaume , kunyanyuliwa kidevu na kuangaliwa usoni na mwanaume mwenye uchu kabla ya kubusiwa.
“Xiao Xiao kama utakuwa na kinyongo na mimi kwa kukuua leo hii basi naomba ukiwa kuzimu roho yako initafute na ulipize kisasi, hili halina uhusiano wowote na Rufi hivyo usije kumchukia”Aliongea Roma.
“Unamaanisha nini?”Xiao Xioa alijikuta akiwa katika mshangao huku akichanua macho yake lakini palepale aliweza kugndua kwamba Roma hakuwa akipanga kufanya nae mapenzi bafuni.
Roma hakutaka kuchelewesha muda na palepale alimshikilia shingo kwa nguvu kumkaba na Xiao Xiao alijihisi kuanza kukosa pumzi.
“No .. usinifanyie hivi..”Aliongea lakini Roma kabla hajakaza mkono mlango palepale mlango ulisukumwa kwa nguvu na aliingia Rufi ambaye alionekana kuhema kwa nguvu.
“Hubby usifanye hivyo , tafadhari naomba umuache ,, huyo sio tishio kwetu”Aliongea Rufi kwa kubembeleza.
Wakari Rufi na Amina wakimuona Roma akimwingiza Xiao kwenye bafu palepale waliangaliana na kisha wakapeana ishara ya kwenda kuchungulia nini kinafanyika.
Baada ya kusikia Roma alikuwa akipanga kumuua Xiao Xiao palepale alisukuma mlango kumuokoa.
Xiao Xiao mara baada ya kujua Roma alikuwa akitaka kumuua na sio kufanya nae mapenzi machozi yalianza kumtoka palepale.
“Uli.. ulikuwa ukitaka kuniua?”Aliuliza huku akionyesha mshangao na uso wake wa kirembo ulibadilika na kuwa mwekundu , pengine angekuwa na nguvu za kijini katika levo ya nafsi basi moja kwa moja angekuwa ashampiga Roma.
“Rufi huyu anatokea katika ulimwengu wa kijini , ukoo uliolazimishwa kuolewa nao , kama ataenda kutoa taarifa ..”
“Najua ...”Rufi alijikuta akimeza mate huku akionyesha huruma.
“Najua ni hatari lakiki sitaki kukuona ukimuua mtu ambaye hana hatia .. pengine hujui hili lakini wakati nilipochumbiwa kwenye ukoo wao walinidharau sana na kuniona kama kiumbe cha ajabu lakini ni Xiao Xiao pekee ambaye hakuoneysha kunidharau, sio mtu mbaya na hawezi kufanya kitu ambacho kitaniathiri”
Roma alimwangalia Rufi na kuona anapaswa kutii kile anachomwambia kwani asingefanya hivyo angeziumiza hisia zake.
“Okey fine”Aliongea Roma na kisha akamwachia Xiao Xio
Xiao Xiao alijikuta akichuchumaa na kuanza kulia kilio cha kwikwi huku akiwaangalia wote na kuangalia mkono wake ambao ushavimba kutokana na kushikiliwa kwa nguvu.
“Umenikatali sana , mimi sio kama baba yangu wala kaka yangu , kama yeye mwenyewe hataki kurudi kwanini aende , kwanini umeshindwa kuongea na mimi vizuri tu”Aliongea na kisha palepale akasimama.
“Kama hunipendi si ungesema tu kwamba hunipendi , kwanini ya kutaka kuniua , nilipatwa na furaha baada ya kukuona kwa mara nyingine kutokana na kukuwazia muda wote tokea mara ya mwisho tuonane kwanini unapenda kucheza na hisia zangu hiv, nakuchukia sana , sitaki kukuona tena kwenye maisha yangu”Aliongea awamu hio kwa Kichina kabisa na kisha alitoka nje kwa kukimbia huku akitoa machozi .
“Hubby asante kwa kunisikiliza”Aliongea Rufi akivuta pumzi ya ahueni.
“Natumaini maamuzi yako ni sahihi na hakuna kibaya ambacho kitatokea”Aliongea Roma.
“Kama mambo yatabadilika nitaondoka kuelekea Mediyerranian kuishi na Sister Rose , nadhani hawawezi kuvuka mpaka kuja mpaka kule”Aliongea
“Rufi unarahisisha mambo , kama watataka wanaweza kwenda mahali popoate hata kama ni kwa kupigana na miungu hawatojali , mwili wako ni hazina kubwa kwao kukupoteza kirahisi , isitoshe majiini ni viumbe ambavyo havipendi kushindwa kirahisi”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kutoa machozi.
“Jamani tumekuja hapa kwa ajili ya kumsindikiza Lanlan kucheza hebu tuachane na hayo kwasasa , Nasra ,Dorisi na Lanlan wanatusubiria”Aliongea Amina kwa kingereza huku akitangulia.
“Hubby nimefurahi , tulijua ulitaka kufanya nae kwasababu alikuwa mrembo lakini kumbe ulitaka kumuua kwa ajili yangu , namuoea huruma Xiao Xiao lakini nimefurahi kuona unanijali , Thanks a lot love”Aliongea.
“Nyie warembo siku moja mtaniua”Aliongea Roma huku akimfinya mashavu huku akitoa tabasamu.
Baada ya chakula Lanlan alienelea kucheza michezo akiungana na Nasra na Dorisi na walijikuta wakifurahi sana siku hio.
Ilifikia hatua mpaka Nasra akajiuliza imekuwaje Edna akamuacha mtoto mzuri kama Lanlan kwani uwepo wake tu ulikuwa ukileta furaha.
Roma wakati huo hakuacha kumkumbuka Edna na alijiaribu kupiga simu nyumbani kumuulizia Edna kama amerudi lakini Bi Wema alimwambia bado hajarejea.
“Pengine atarudi jumatatu kwani ndio siku ambayo inatarajiwa kuwa na kikao cha kutangaza mabadiliko ya kampuni ya Vexto”Aliongea Nasra mara baada ya kumuona Roma amekuwa mnyonge.
“Mimi sitaki hata kujisumbua na maswala yake mengine , ninachotaka ni kuongea nae na kuweka mambo sawa tu basi , nimefikiria sana katika hizi siku na nimegundua kuna kitu alikuwa akinificha”Aliongea Roma na Nasra alimshika begani kumtuliza huku akimwangalia kwa kumuonea huruma.
Muda wa jioni wote walirudi nyumbani kwao wakimuacha Amina anapoishi na Roma alichukuana na Lanlan kueleka nyumbani kwa Nasra
Wakati wanaingia getini walishangazwa na uwepo wa magari matatu ambayo hawakuwa wakiyajua, mawili yalikuwa ni Aud rangi nyeusi na moja wapo ilikuwa ni gari aina ya Maserati ya rangi nyekundu.
“Ineonekana tuna ugeni hapa”Aliongea Rom.
“Naona hivyo pia”Alijibu Nasra aliemshika Lanlan mkono.
“Nasra wewe ondoka na Lanlan moja kwa moja kwenda juu akapumzike mimi nitaonana nao”Aliongea Roma na Nasra alitingisha kichwa kumwelewa na kisha alitumia mlango wa nyuma wakati Roma akielekea eneo la seubuleni.
Mtu pekee amaye aliachwa nyumbani alikuwa ni Qiang na mara baada ya kuingia ndani Roma aliweza kumuona mwanadada huyo ambavyo amekosa utulivu kwani alikuwa akizunguka zunguka huko na huko , lakini alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kumuona Roma.
SEHEMU YA 653.
Roma mara baada ya kuingia ndani aliweza kuona sura anazozifahamu , mmoja wapo alikuwa ni Afande Jamali na mwingine alikuwa ni mwanamke kutoka familia ya Sharif.
Alikuwa amevalia suti nyeusi na viatu rangi nyekundu aina ya skuna, nywele zake alikuwa amezifunga kurudi nyuma na kumfanya kuwana mwoneknao wa kujiamini pamoja na wa kuvutia kwa wakati mmoja.
Alikuwa ni mwanadada mrembo Maimuna Sharif ambaye alionekana kama vile ni ofisa kutoka benki kwa muonekano wake kiasi ambacho kama wewe ni mwanaume wa kawaida ingekufanya kukosa hali ya kujiamini mbele yake.
Afande Jamali mara baada ya kumuona Roma palepale alisimama kwa heshima.
“Mr Roma naomba unipe ruhusa yako kukutambulisha , huyu ni Miss Maimuna Sharif Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bale Group na mtoto wa kwanza kutoka kwa mzee Hafidh Sharif”Aliongea Jamali.
“Tunakutana tena Mr Roma”Aliongea Maimuma huku akionyesha tabasamu na kunyoosha mkono wake kumpatia Roma.
Roma aijiuliza mwanamke huyu anafanya nini , alikuwa akikumbuka alimuona siku ya jana yake mkoani Kilimanjaro , lakini licha ya kutoelewa nia ya ujio wake hakuwa akimuogopa hivyo alinyoosha mkono wake kumsalimia.
Roma mara baada ya kugusana na mkono wa mrembo huyo alijikuta akijiambia alikuwa na mkono mlaini mno ijapokuwa haikuwa mlaini kama wa Rufi lakini bado ulikuwa mlaini wa kumpagawisha mwanaume yoyote rijali.
Roma kwa kumwangalia ru Maimuna alijua kabisa sio mwanamke wa kawaida , ilionekana kabisa alikuwa na mafunzo ya kimapigano na alijiambia hakika alikuwa akijua kujijali.
Moja ya mbinu ya kupima kama mtu ana mafunzo ya kimapigano ni kupitia pumzi yake, watu ambao wana mafunzo ya kimapigano hususani ya Kung fu mara nyingi upumuaji wao ni wa tofauti na watu kawaida wanapumua kama vile wanahesamu pumzi inayvoingia na kutoka, kitu kingine pia katika utembeaji wao au pale wanapokuwa wamesimama hii huwatofautisha sana.
Kwa mfano wakati wa kutembea ni kama vile kuna mstari anaofuatisha kwani hatua zake hazipindishiki huku mikono yake yote ikiwa usawa wa mwili , mtu wa kawaida tembea yake inateneza mstari wa Zigzag huku vidole vya miguu yake vinatengeneza angle
Sasa sifa hizo zote alikuwa nazo huyu mwanadada Maimuna ambaye alikuwa mbele ya Roma na kujikuta akimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida na kujiambia alikuwa na urembo wa mwili na ngozi yake ni laini mno , pia ni mkurugezi wa kampuni ya Bale lakini pia wakati huo huo alikuwa na mafunzo ya mapigano.
Ilikuwa ngumu sana kumkutana mwanamke mwenye mafunzo ya mapigano kuwa na ngozi laini hususani ya mikono.
Wakati wakiwa wameshikana mkono Roma alijikuta akihisi mtekenyo kwenye kiganja chake na palepale aligundua Maimuna alikuwa amemtekenya kwa kutumia ukucha wa kidole cha mwisho.
Jambo lile lilimshangaza na kumfanya Roma ajulize mwanamke huyo anafanya nini , au yupo hapo kwa ajili ya kumtega.
Baada ya kuachiana wote watatu waliweza kuketi chini huku Qiang akiandaa juisi.
“Afande Jamali nadhani hujamleta hapa kwa ajili ya kunisalimia tu”Aliongea Roma akitaka maongezi yaende moja kwa moja katika topiki ambayo imewalata.
“Ndio Mr Roma , sitozunguka zunguka , nipo hapa kama mwakilishi wa wizara ya ulinzi?”Aliongea.
“Mzee Hashim Tozo ndio kakuagiza?”Aliogea Roma akimaanisha waziri wa ulinzi ambaye alikuwa ni ndugu yake Afande Tozo, Roma alishawahi kukutana nae mara kadhaa nyumbani kwa Afande Kweka na alikuwa amezoeana nae japo sio sana,
“Ndio Mr Roma , nipo hapa kufikisha ujumbe kutoka serikalini , serikali ya Tanzania inaheshimu familia yako pamoja na familia ya Mzee Sharif kwani mchango wenu kwa taifa ni mkubwa , Mstaafu jenerali ametoa taarifa yake kwamba familia yake haihusiki na swala lolote lililotokea siku ya jana na kusema unapaswa kuwajibika kwa kila kitu binafsi, hivyo ndio maana tupo hapa kwa ajili ya maongezi”Aliongea.
“Nenda moja kwa moja kwenye pointi”
“Ngoja niseme mimi… Mr Roma nipo hapa kwa ajili ya kutafuta haki ya familia yangu”Aliongea Maimuna
“Haki ya familia yako?”
“Ndio , nimekuja hapa kwa ajili ya kukutaka urudishe hazina yetu , kisha ujenge upya jengo la ibada na baada ya hapo usujudie roho za miungu wetu mara nne”Aliongea Maimuna huku akiwa na uso wenye urafiki.
“Kwanza nikueleze kwamba hio hazina sijui nini maana mimi sina , pili mmefikiria nini kudhania kwamba ninaweza kwenda kusujudia miungu yenu ilihali mimi ndio niliochoma moto jengo lenu la ibada”
“Mr Roma watu waliokukosea ni Salihi naibu waziri wa elimu pamoja na Asha na kama ni kisasi ulitakiwa kuwalipiza wao , kwanini ukahusisha familia nzima katika kisasi chako kwa kuchoma jengo letu la ibada pamoja na kuiba hazina yetu huku ukiharibu makazi yetu , mpaka kuja kwangu hapa ni kwamba familia yetu imekaa chini na viongozi wa kiserikali na kukubali jambo hili kuisha kwa amani na kusahaulika kama utatii matakwa yetu , urudishe hazina yetu na kisha usujudie miungu yetu kuiomba msamaha”
“Kama hiki ndio ambacho kimewaleta mnaweza kuondoka”aliongea Roma akisimama na kisha kunyoosha kidole kuelekea mlango wa kutokea nje.
Maimuna wala hakuonyesha kuathirika , yaani alikuwa akiongea kirahisi mno na palepale alisimama na kisha akamsogelea Roma karibu zaidi kimadaha na kufanya marashi yake makali ya bei ghali kuathiri pua za Roma.
“Mr Roma , siku ya jumatatu jioni nimeandaa sherehe ndani ya hoteli ya Wache Kigamboni, wageni wangu ni wabia wa kibiashara ambao wanashirikiana kwa ukaribu zaidi na kampuni yetu ya Bale Group , unaonaje ukishiriki na wewe?”Aliongea huku akiwa na tabasamu la kiuchokozi.
“Kwanini nihudhurie?”
“Kwasababu nitakupa sababu ambayo itakufanya ushindwe kukataa kuhudhuria , nina uhakika utaweza kukubaliana na matakwa yetu baada ya hio hafla”
“Vipi kama nisipo hudhuria?”Aliuliza Roma na kumfanya Maimuna kutingisha mabega.
“Nina uhakika mwanaume jasiri kama wewe hutopenda kuonekana Muoga mbele ya familia ya Sharif .. Besides I’ m just a frail woman .. alright that is settled, nitakuja kukuchukua mwenyewe hio siku”Aliongea huku akimkonyeza na kisha alimpita kimadaha na kuelekea nje huku akitingisha makalio yake ya wastani kwa fujo kama zote.
Roma aliishia kushika kiuno na kujiambia hakika ameweza kuamsha shauku yake.
“Vipi mmeshawazuia kutumia njia ya fujo katika kulipiza kisasi?”Aliuliza Roma akimwangalia afande Jamali.
“Hata mimi mwenyewe sijui na nafuata tu maagizo ninayopewa na wakuu wangu , lakini nakushauri Mr Roma hii familia haiwezi kuliacha hili lipite hivi hivi kuna nguvu kubwa ambayo ipo nyuma yao , lakini inaonekana hawataki kufanya fujo kudai haki yao , unapaswa kufikiria mara mbili ili kulimaliza kimya kimya”Aliongea Afande Jamali
“Babu alisema kwasababu mimi ndio msababishaji nitawajibika mwenyewe na hakuna mtu wangu wa karibu ambaye ataguswa “
“Inaonekana kuwa hivyo , isitoshe wanawake wako wote sio raia wa kawaida , serikali haitaki hili swala kuingiliana usalama wa raia … maagizo yashatoka kama famili ya Sharif itafanya jambo lolote la kutaka kudhuru familia yako basi tutaingilia”Aliongea Jamali.
“Nimefarijika kusikia hivyo , isitoshe adui yao ni mimi hivyo nipo tayari kuona nini wananniandalia, ninashauku ya kutaka kujua mchezo wao utazaa nini”Aliongea Roma na kumfanya Afande Jamali kushindwa kumuelewa Roma kabisa kwani alionyesha kutokuwa na hofu kabisa.
Baada ya wageni kuondoka na walinzi wao, Roma alikaa hapo sebuleni kwa muda mpaka Nasra aliposhuka na kukaa pembeni yake.
“Hii familia ya Sharif ina nguvu sana?”Aliuliza Nasra.
“Inaonekana , ila kwa sasa nahitaji kufanya maandalizi”
“Unahitaji msaada wangu?”
“Ndio”
“Nini nikusaidie?”Aliongea Nasra akionyesha shauku.
“Simu yangu imeisha chaji , nichajie na kisha niletee laptop yako hapa , kuna mtu nahitaji kuwasiliana nae kwa njia ya online”Aliongea Roma.
Nasra alijikuta furaha yake ya kutaka kumsaidia Roma ikipotea, na kujiambia alijawa na shauku ya bure.
Ukweli ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kutohitaji msaada wowote kutoka kwao iliwafanya kuwa na shauku kama atataka msaada.
Licha ya kuchukia alichukua simu ya Roma na kwenda nayo juu kuichomokea chaji na kisha alishuka na Mackbook Pro na kumpatia na Roma aliunganisha na internet palepale na aliingia mtandaoni na kulipia VPN na kisha akapakua kivinjari cha Tor na kisha akaingia mtandaoni.
“Naweza kuangalia unachofanya?”Aliuliza Nasra akiwa makini na kumfanya Roma kumwangalia na kutabasam.
“Unaweza ndio kuangalia wewe ni mwanamke wangu”Aliongea
Roma hakuona haja ya kumficha Nasra kile ambacho alikuwa akipanga kufanya , mpango wake ni kutaka kuomba msaada kutoka nje ya nchi kufika Tanzania kwa ajili ya kumsaidia jambo lake.
Roma baada ya kuingia kwenye mtandao wa Deep Web palepale aliandika link ambayo alikuwa ameikariri na dakika hio hio yaliweza kuonekana mawasiliano ya watu mbalimbali na ajabu kila mtu ambaye Roma alikuwa akiwasiliana nae ilimhuhiaji kwanza kuingiza Passcode.
Licha ya kukaa na kuangalia lakini Nasra hakuelewa chochote kwani Roma alikuwa akiwasiliana na watu kwa kutumia lugha tofauti tofauti.
Kitu pekee ambacho aliweza kugundua ni kwamba kila mtu ambaye aliwasiliana nae alionekana kumuheshmu sana Roma
Ilimchukua nusu saa Roma mpaka kumaliza .
“Babe you were so cool”Aliongea Nasra huku akijikumbatisha kwenye kifua cha Roma.
“Umeelewa chochote nilichokuwa nikiongea?”
“Sijaelewa lakini , ulivyokuwa ukiongea inapendeza sana”Aliongea akirembua na kumfanya Roma mzuka kumpanda.
“Lanlan ashalala?”Aliuliza Roma.
“Ndio na anakoroma huyo”Aliongea na kumfanya Roma kutoa tabasamu na kuingiza mkono kwenye kifua cha mrembo Nasra na kuchoropoa embe dodo.
“Kama kashalala unaonaje tukifanyia hapa hapa kwenye sofa na kisha tukaoge wote”Aliongea Roma lakini hakusubiri jibu kwani paleplae alimnyanyua na kisha akamlalia kwa juu na kilichoendelea masofa yatahadithia.
Siku ilofuata ilikuwani jumapili na Roma hakuwa na mpango wa kumpeleka Lanlan kucheza tena.
Siku hio aliona kitu pekee ni kuangalia maendelo yake katika kujifunza mbinu ya Andiko la urejesho, maana aliona Lanlan ni mwendo wa kula bata tu tokea arudi ulimwengu wa majini pepo.
Kutokana na Roma kutokuwa na nguvu za kijini hakuweza kumwangalia Lanlan amefikia levo ya ngapi hivyo kitu pekee ambacho alitaka kujua ni kumchukua na kisha wakaenda hadi msituni na wakati huo akiwa na matofali ya zege.
Baada ya kuyapangilia chini kwa mstali maalumu mawili mwili matatu mtatau na manne nne alimwambia Lanlan aanze kuyapasua kutoka mwanzo mpaka mwisho kwa kutumia ngumi.
Lanlan misuri ya mwili wake ilianza kutuna kama vile ni puto na palepale alianza kuyapasua kwa kasi na ndani ya dakika yote alikuwa ameyapiga na pigo moja moja mpaka kupasuka.
Roma alijikuta akiridhika na alijiambia kutokana na nguvu aliotumia pengine atakuwa katika levo ya Uchoyo au wanaita levo ya kujijali mwenyewe na muda wowote angeingia katika levo ya Takdiri au Hatima kwa lugha nyingine.
Hii ni levo muhimu sana katika mafunzo ya kijini lakini ukiachana katika mafunzo ya kijini lakini pia katika maisha ya binadamu ni moja wapo ya hatua ambayo ni muhimu kwa mafannikio ya binadamu yoyote , ni binadamu wachache sana ambao wanajua Takdiri yao nini katika ulimwengu huu na hao ambao wamebahatika kuijua mafanikio yao ni ya juu sana kuliko wale ambao hawaijui Takdiri yao ni nini.
Kila binadamu huzaliwa na kuwepo katika uso wa dunia kwa kusudi maalumu na ndio maana katika hatua za kujitafuta ili kujua wewe ni nani tofauti na jina lako hutakiwi kuuliza maswali mtu wa nje bali unatakiwa kujiuliza wewe mwenyewe maswali na kutafuta majibu na hapa ndipo utaweza kujua nini Takdiri yako.
Maendeleo ya Lanlan yalimshangaza sana Roma , ijapokuwa yeye wakati wa kujifunza hakutumia vidonge vyvoyote kujibust lakini kwa Lanlan spidi yake ilikuwa ya juu na alikuwa na shauku ya kutaka kujua kitamtokea nini mpaka kupita levo ya kifo na uhai halafu kuzaliwa upya.
Roma alijikuta akimsifia Lanlan kwa kazi nzuri huku akimwahidi mambo mengi lakini Lanlan alitaka kupaishwa juu angani lakini Roma uwezo huo hakuwa nao na alijikuta ile hali ya kutaka kurudisha uwezo wake na kumuondoa mdudu aliekuwa akimtawala kumvaa.
Roma aliona kwamba haijalishi Lanlan uwezo wake unaongezeka kwa spidi namna gani lakini bado tu alikuwa akipaswa kumlinda.
Roma mara baada ya kurudi na kumaucha Lanlan mojakwa moja alielekea katika maabara ya Clark eneo la Makongo juu , maabara ambayo ilikuwa urithi kutoka kwa Profesa Shelukindo.
Roma mara baada ya kufika aliweza kugundua pia Rufi yupo na wote walikuwa bize kupitia baadhi ya vitabu.
“Kuna chochote ambacho mmepata?”Aliuliza Roma akiwaangalia warembo hao namna ambavyo wapo bize.
Clark alikuwa amevalia simple huku nywele zake alikuwa amezifunga na lastick kwa nyuma, muda wote mwanamke huyo alionekana kuwa bize.
“Kulingana na maarifa ya Rufi kuhusu roho mnyama wa maafa , hakuna aina yoyote ya nguvu ya kiroho ambayo inaweza kushindana nayo kwasababu ni mnyama aliewahi kuwepo katika kipindi cha dunia kuwa katika hali ya ukiwa na machafuko , inawezekana alikuwa ni mnyama mwenye nguvu kubwa duniani”
“Dear nipo hapa kwa taarifa nzuri lakini kwanini unaongea kuniogopesha?”
“Mimi ni mwanasayansi na sio motivation speaker , ninachokuambia ni fact , mambo hayapo mazuri sana kwa upande wetu”
“Hubby huna haja ya kujali sana kuhusu alichoongea Clark , ijapokuwa sina wazo namna ya kuishinda lakini tunaweza kushinda kutokana na hasira yake”
“Hasira yake?”
“Ndio”
“Hio ni roho ya mnyama mkali sana ambaye sifa yake kubwa ni kukasirika na kutokuwa na huruma , hivyo tunapaswa kutafuta roho nyingine ambayo ni ya mnyama lakini mpole ili tu kuiamsha ndani yako , ijapokua roho hio inaweza kuwa na nguvu kidogo kushindana na Chaos, hivyo kabla ya jaribio hilo tunapaswa kuanza na nguvu zako za kijini , tunapaswa kuibadili nguvu yako ya kijini na kuiweka katika kitu ambacho kitakandamiza roho yake ya ukali”Yalikuwa ni maelezo mengi ambayo Roma alishindwa kuyaelewa.
“Umeongea vitu vingi , je una mpango wowote?”
“Tuna mawazo tofauti , nilikuwa nikiwaza vipi kama utaombewa kanisani au kusomewa swala msikitini , watu wa dini wana upako wa kutosha, ninachojua nguvu iliopo ndani yako ni ya kipepo hivyo inaweza kusafishwa na nguvu ya kiroho ya nuru ya kidini ambayo ni safi”
“Clark tangu lini wewe kama mwanasayansi ukaanza kuamini katika maombezi”Aliongea Roma kwani siku zote Clark kila mama yake alipokuwa akimlazimisha kwenda kanisani alimwambia hakuna Mungu kwasababu hakuna uthibitisho wa kisayansi.
“Mimi najua mambo mengi kuliko unavyodhania , ijapokuwa sijawahi kuamini katika imani yoyote lakini kuna nguvu ya kiroho ambayo sio ya kawaida katika misikiti pamoja na kanisani ndio maana watu wana imani kali, nimeamini baada ya kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi”Aliongea na Roma alitingisha kichwa kwani hata yeye alikuwa akikubalaina nae.
“Vipi kuhusu wewe Rufi?”
“Mimi nimeona labda ujaribu kusali kibudha au kihindu, kuna Monk ambao wana uwezo mkubwa wa kufanya ‘Exorcism’ lakini kazi kubwa ni kuwapata na kuwa na utayari kufanya hio kazi, nimeshindwa kujua ni aina gani ya nguvu ya kiroho ambayo inaweza kushindana na nguvu ya Chaos”
“Kwahio mwishowe tuna uelekeo lakini mpango hatuna”
“Sio kabisa , kama tutashindwa kukusaidia kwa njia za maombezi au Exorcisim basi angalau tunapaswa kupata Dhana za kijini za kiwango cha juu kabisa ambazo zina uwezo wa kushindana na roho ya mnyama wa maafa”
Baada ya Rufi kuongea vile mawazo ya Roma yalimkumbusha kitu kimoja ambacho aliiba katika madhabahu ya Mzee Sharif.
“Nimekuja hapa kwa kitu kingine pia , hebu ngoja niwaonyesheni muone..”Aliongea Roma na kisha palepale alitoa ile Kokoto iliokuwa na jina la Hazina na kisha akampatia Rufi.
“Unaijua hii maana yake?”
Write Note:Exorcism ni kama vile wanavyofanya waganga wa kienyejji katika kufukuza mapepo , sasa katika imani ya Kibudha na Kihindu hufanya hicho kitendo pia kwa muumini mwenye mapepo.
SEHEMU YA 654.
Rufi na Clark walikuwa wameshangazwa sana na neno Hazina na palepale walijikuta wakifungua kile kijiboksi kuangalia kilichopo ndani.
Lakini mara baada ya kuona kitu chenyewe walijikuta wakikosa yale matamannio yao, walijiuliza kokoto inaweza vipi kuwa hazina.
“Ndio nini hiki , ndio Hazina uliokuwa ukisemea , mbona inaonekana kama pande la mkaa lakini uzito wake ni mkubwa kuliko wa mkaa , au ni jiwe?”Aliuliza Rufi.
Clark hakuonyesna kukupurukuka na aliishia kuangalia kwa umakini kujaribu kukagua na kulipatia maana yake kwani palepale aliliweka katika Darubini na kuanza kulikagua kisayansi na ndani ya dakika tano tu alionekana kupata majibu kadhaa.
“Linaonekana kama vile ni ‘Carbide’, kuna aina ya madini ndani yake lakini ajabu pia kuna protini , au ni Fossi , asili mara nyingi inakuwaga na vitu ambavyo vinaonekana kama vimekufa lakini bado vipo hai , hata hivyo vitu vya aina hio sio vingi lakini sio adimu pia”(Fossil ni mabaki ya kale)
Roma alijikuta pia na yeye kuchukia na kujiambia hio takataka kwanini iwe ndio Hazina , lakini kwa wakati mmoja alijiambia familia ya Sharif ni matajiri na hata kiboksi kilichotumika kuihifadhia ni cha madini ya Dhahabu, alijiuliza au ni kumbukumbu.
Roma mara baada ya kuona hakuna majibu ya haraka haraka alificha hazina yake alioona kama takataka na kisha akawaambia waondoke pamoja kwa ajili ya chakula cha mchana
Roma wakati akiwa njiani kurejea nyumbani aliweza kupokea simu kutoka kwa Sophia na kumweleza kwamba yupo Afrika ya kusini anashoot matangazo ya Promosheni ya filamu na angerejea Tanzania hivii karibuni kwa ajili ya Show ya siku ya usiku wa Christmas na Roma alimuahidi kwamba atahudhuria show yake.
Roma mara kutoka nje ya gari aliweza kumkuta Lanlan ambaye alikuwa amelalia tumbo kwenye kibaraza huku makaratasi mengi na penseli za kuchotea zikiwa zimezagaa huku pembeni yake akiwa amesimama Qiang Xi.
Muda huo ilikuwa ni jioni na Nasra alikuwa ameenda Supermarket kwa ajili ya kununua vitu vya kupika usiku.
Roma alimsogelea Lanlan na kisha aliinua karatasi ambazo alikuwa amemaliza kuchora na kisha aliona sura ya Superman na chini yake kuna jina la Daddy.
“Lanlan mimi ndio Superman?”Aliuliza Roma huku Lanlan akiwa bize kukoleza rangi ya mti aliochora na alimgeukia Roma na kutingisha kichwa kukubali kwamba ndio yeye.
“Na huyu mwanamke na msichana ni nani ?”
“Huyo msichana mdogo ni Lanlan na msichana mkubwa ni mama yake Lanlan , Mama ana nwele ndefuu mpaka shingoni”
“Umekosea, Lanlan wetu ni kibonge lakini huyu hapa ni mwembamba”
“Lakini Lanlan hapo amekonda kwasababu amemmisi mama yake”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu.
“Umekonda vipi wakati ulikuwa ukila chakula chote ambacho Aunt Nasra anakuandalia , hujakonda bwana”
“Lakini Lanlan atasikia njaa asipokula , ila anammisi mama yake”Aliongea huku akiwa kama vile anaona aibu kuumbuliwa na kumfanya Roma kutoa cheko.
“Aunt yako Nasra atakasirika , yaani amekupikia chakula kitamu lakini hujamchora?”
“Kwasababu mama simuoni na nammiss ndio maana nimemchora”Aliongea na kumfanya Roma kukaa kimya.
Sio kwa Lanlan ambaye tu alikuwa amemmisi Edna bali hata yeye mwenyewe alikuwa amemkubuka sana .
“Daddy ,Je Mama hatutaki tena?”Aliuliza huku akitia huruma na kumfanya Roma kushangaa.
“Lanlan , unapaswa kukumbuka kwamba mama yako anakupenda na kwasasa hana furaha ndio maana , kila kitu kitakuwa sawa muda si mrefu”
“Nina uhakika Mama ananipenda kwasasabu yeye ndio amenizaa”Aliongea Lanlan akiwa na uhakika na Roma hakuelewa ujasiri wake unatokana na nini.
Ilimfanya kuingiwa na majonzi kwa kuona pengine Lanlan ameshindwa kumtofautisha mama yake mzazi na Edna, Roma alishindwa kujizuia na kumkumbatia.
Qiang ambaye alikuwa akisikiliza maongezi hayo alijikuta akitokwa na machozi tu na kuishia kuyafuta kwa siri.
Hakuna ambaye angeweza kuamini kwamba Lanlan alikuwa ameficha kile anachojisikia na kujitahidi kuonekana ni mwenye furaha muda wote.
Usiku wa jumapili uliweza kuisha vizuri na Roma mara baada ya kuamka alijua ndio siku ambayo Edna atakuwa amerudi na ataenda kazini kama alivyosema Nasra.
Kuhusu hafla ambayo Maimuna aliongea hakutaka sana kuwazia maana ingemfanya tu kuwa na wasiwasi.
Roma alitaka kumsubiri Edna atakaporudi ndio aongee nae lakini alijiambia anapaswa kuchukua hatua yeye kwanza kama mwanaume , alijiambia pengine Edna anasubiria yeye aanze.
Hivyo mara baada ya wazo hilo kumuingia alienda moja kwa moja mpaka nyumbani na aliweza kukutana na Bi Wema ambaye alimwambia Edna alirudi lakini ameelekea kazini.
Roma palepale alifanya maamuzi ya kuelekea huko huko kazini kuonana nae.
Roma mara baada ya kufika ndani ya jengo la makao makuu ya kampui ya Vexto moja kwa moja alienda mpaka Floor ambayo ndio rasmi ofisi ya Mwenyekiti wa kampuni inapatikana , ni ofisini ileile ya Edna lakini ilikuwa imebadilsihwa tu hadhi.
Ijapokuwa Ernest ndio alikuwa CEO lakini hakuwa akitumia ofisi ya Edna ya mwanzo.
Roma mara baada ya kutoka kwenye lift moja kwa moja alitembea mpaka kwenye mlango wa kuingilia ofisni huku akipata burudiko la kiyoyozi na harufu ya kuvutia na kisha aligonga mlango lakini hakuweza kupata mrejesho.
Dakika ileile mlango wa ofisi ya Sekretari ulifunguliwa na aliweza kutoka msichana mrembo kiasi alievalia kinadhifu.
“Wewe ni Mr Roma?”Aliuliza.
“Ndio , wewe ni nani?”
“Mimi ni Sekretari mpya , naitwa Yulia , naamini hunifahamu , upo hapa kwa ajili ya kuonana na Mwenyekiti”Aliongea kwa namna ya heshima.
Ilionekana alikuwa na taarifa zote kuhusu Roma ni nani , ni kama kawaida mfanyakazi mpya lazima ajue Hidden rules za mazingira ya kazi ili kuepuka kufanya makosa na kuwa upande mbaya na watu wakubwa.
Roma aliishia kutabasamu kumuondolea woga , alijua atakuwa ni mbadala wa Recho ambaye alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa idara.
“Ndio yupo wapi?”
“Yupo kwenye kikao na Bodi ya wakurugenzi , wapo chumba namba tatu cha mikutano”
Kama ilivyotarajiwa , mwanamke mchapakazi ambaye hana mpango wa kuacha.
Roma hakuwa mgeni hivyo alijua chumba namba tatu cha mikutano kipo upande upi na mara baada ya kufika aliweza kuona viti vyote vilikuwa vimejaa na wafanyakazi wa juu wa makampuni pamoja na wanahisa , wote wakiwa na sura za kitaaluma.
Edna alikuwa amekaa mbele kabisa kawenye kiti cha kibosi akiwa kauzu kama kawaida yake , hakukuwa na ishara zozote kama alikuwa na mawazo na ilikuwa ni kama ukauzu wake uliongezeka zaidi na zaidi.
Kila mfanyakazi aliekuwa ndani ya hilo eneo alikuwa akimhofia Edna huku wengine wakionyesha heshima zao , ilikuwa ni kama mawaziri wanavyomheshimu mheshimiwa Raisi.
Baada ya Roma kufungua mlango na kuingia macho yote yalimgeukia huku baadhi ya Sura zikimwonyeshea tabasamu , akiwemo Ernest Komwe na Monika.
Upande wa Dorisi na Nasra walishangazwa na ujio wake kwani hawakutegemea kama angeweza kuja hapo mapema hivyo.
Roma aliwaonyeshea tu tabasamu na ksiha akageuza uso wake kwa Edna na kumwangalia kwa namna isiokuwa ikielezeka.
Kama sio jasiri usingeweza kuingia ndani ya chumba kama hicho ambacho kilikuwa na zaidi ya watu therathini.
Edna alionekana kukunja sura tu mara baada ya kumuona Roma lakini hakukuwa na mabadiliko makubwa , yaani alimwangalia kwa sekunde tu na kisha akampotezea kama hamjui.
Baadhi ya watu tayari walishagundua mabadiliko hayo na kuishia kuwaangalia kwa namna siokuwa ya kawaida.
Roma baada ya kuona namna Edna alivyomwangalia alijikuta akikosa furaha na aliishia kushika kidevu chake na kufunga mlago na kisha akaegamia ukuta kama bodigadi.
Ijapokuwa alitamani kuongea na Edna lakini hakuona haja ya kumsumbua akiwa katika kazi kama hivyo.
“Recho , please continue with your presentation”Aliongea Edna akimwashilia kwa kunyanyua karamu.
Kampuni hio ilikuwa ikitumia mara nyingi lugha ya kingereza katika vikao vyote na mara nyingi hata wafanyakazi wakifanyiwa usaili wanapimwa uwezo wao wa kuongea kingereza kwa ufasaha na kukielewa pia. Isitoshe lazima iwe hivyo kwani kulikuwa na wafanyakazi na baadhi ya wanahisa ambao ni wazungu wasiokuwa wakijua lugha ya kiswahili , akiwemo Rich pamoja na Ernest mwenyewe.
Recho alionekana kukosa utulivu mara baada ya kumuona Roma lakini alijakaza na kisha aligeukia Projector.
“Kutokana na kuundwa kwa Vexto group kimataifa , itahitajika kugawa majukumu kwa wafanyakazi wakubwa wa kampuni kwenda kufanya kazi katika matawi Tanzu ambayo yapo nje ya nchi ili kurahisisha mwenendo mzuri wa kampuni pamoja na kugundua fursa nyingine za kibiashara, Mwenyekiti wetu wa bodi anaamini sisi wafanyakazi wa ngazi ya juu tunapaswa kuwa mfano katika kutoa mchango wa maendelo katika kampuni hivyo , Mwenyekiti amependekeza Dorisi kupandishwa cheo kuwa sawa na Nasra na watapaswa kuondoka nchini kwenda kufanya kazi katika matawi yafuatayo , Dorisi ataelekea Cape Town Afrika ya kusini na Nasra ataelekea Buenos Aires Argentina, watakuwa ndio Wakurugenzi wa makampuni haya yote mawili ambayo yameanzishwa rasmi na kazi zao ni kujenga msingi wa kibiasara katika masoko hayo mapya.
SEHEMU YA 655.
Dorisi na Nasra ni kama vile hawakuwa wamesikia vizuri , hata Roma ambaye alikuwa amesimama vilevile ni kama hajasikia vizuri.
Afrika ya Kusini , Argentina?!!
Roma hakushangaa sana uwezo wa Edna kuchanja mbuga kimataifa hususani kutokana na mtaji waliokuwa nao , hivyo sio jambo la kushangaza kampuni ya Edna kuanzisha tawi jipya Argentina na Afrika ya kusini lakini alijiuliza kwanini anataka kuwatuma Dorisi na Nasra.
Bila shaka kama wataenda huko ilimaanisha kwamba madaraka yao pamoja na malipo yangekuwa makubwa zaidi lakini kuwaagiza wanawake hao wawili kwenda nje ya nchi ni sawa na kuwafukuza tu ndani ya Tanzania.
Dorisi na Nasra waliweza kuhisi kitu na waliishia kumwangalia Edna kwa macho yasiokuwa ya kawaida lakini Edna hakuwaangalia hata kidogo.
“Mwenyekiti , sote sisi tunajua michango mikubwa na uwezo wao mkubwa katika maendeleo ya kampuni na ni sahihi kuwa wakurugenzi wa kampuni tanzu lakini nadhani wangeweza kufanya kazi nzuri zaidi kama wangebakia hapa makao makuu kutokana na uzoefu wao”Aliongea Ernest Komwe akitoa mchango wake.
“Wanapaswa kuongoza kampuni kama ishara ya kutoa mfano kwa wengine watakaochukua nafasi zao , sitojisikia vizuri kama nikituma mtu ambaye sio mdhoefu na biashara zetu , isitoshe kwenda huko kutawafanya kupata uzoefu wa kimazingira , CEO Ernest vipi unataka kwenda wewe?”Swali hilo lilimfanya Ernest kufunga bakuli lake.
Monika ambaye alishawahi kufanya kazi kama msaidizi wa Edna alikuwa akijua tabia yake hivyo alimwangalia mume wake na kumpa ishara ya kutulia.
Kila mmoja alijua kama Dorisi na Nasra wataenda huko watafanya kazi nzuri sana lakini isingekuwa rahisi kwao kwani walikuwa wakienda kukutana na mazingira mapya.
Roma aliekuwa amesimama kwenye kona ya mlango alijikuta akikunja ngumi na kujiambia je anafanya hayo yote kwa ajili ya kumlipizia.
Alijiambia sio tu kwamba wakati huo alikuwa akimpotezea lakini ameenda mbali na kuanza kuwaondoa wanawake wake karibu na kuwatuma nchi ya mbali.
Bila shaka , kama kiongozi mkuu wa kampuni Edn alisifika kwa kutopenda kupingwa akiamua jambo lake , kwa jinsi ambavyo alimwagiza Recho kusoma mapendekezo yake ilikuwa ikimaanisha kwamba alishafanya maamuzi tayari.
“If there is no objection from the vice presidents , we can proceed with the voting process , raise your hand if you approve of this proposal”Aliongea akimaanisha kama hakuna pingamizi kutoka kwa watendaji wasaidizi wa kampuni basi anaekubaliana na pendekezo lake anyooshe mkono kupiga kura.
Kati ya wakurugenzi ambao walikuwepo ni Mzee Alex mmiliki wa zamani wa kampuni ya Jr ambaye ipo chini ya Edna kama mwanahisa mkuu na wote kwa pamoja waliangaliana na kisha walionekana hakuna ambaye alikuwa akipinga kwani walinyoosha mikono kupiga kura ya ndio.
Yaani kwa jinsi wanahisa hao walivyonyoosha wote pasipo ya yoyote kutopinga ni kama vile walikuwa washajiandaa,
Recho alisimama kwa ajili ya kuhesabu kura hizo lakini Edna alimzuia.
“Hakuna haja ya kuhesabu , tayari tuna asilimia hamsini ya kura zote wanaokubali kabla sijatoa kura yangu , inaonyesha wengi wenu mmekubaliana na pendekezo langu , Miss Dorisi na Miss Nasra matawi yote mawili hayajamaliza hata miezi sita tokea yafunguliwe hivyo tunategemea kazi kubwa yenye mchango chanya kutoka kwenu”
Dorisi aliishia kuwa kimya huku macho yake yakiwa tayari ni makundu , ni kama vile muda wowote angetoa machozi , upande wa Nasra alionyesha hasira na wasiwasi kwa wakati mmoja.
“Edna kuna haja ya kwenda mbali hivi , inaonyesha hapa kabisa ulishaongea na Shareholders kupiga kura ya ndio ili sisi kwenda nje ya nchi mbali na Tanzania , umefurahi sasa?”Alisimama Nasra na kubwata huku akimwangalia Edna kwa macho makavu.
Watu wote kimya , hakuna ambaye alikuwa tayari kuongea lolote , ni kama walikuwa wakitarajia dhoruba kuamka muda wowote.
Ilionekana kwa watu hao ni kama kweli Edna alikuwa akifanya makusudi kabisa na hakujisumbua hata kuficha dhamira yake na ilionekana ni kama kuwadhalilisha mbele ya kila mtu.
Lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alikuwa tayari kupinga maamuzi ya Edna , licha ya kwamba maamuzi yake yalionekana kuwa na ukakasi.
Mtu pekee ambaye hakupiga kura ya ndio au hapana alikuwa ni Mzungu Richie peke yake , alikuwa amefumba macho kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza.
“Sijaelewa unachotaka kumaanisha”Aliongea Edna akimwangalia Nasra.
“Edna acha maigizo , unakasirisha ujue”Aliongea Nasra akiwa amepaniki hatari.
“Kama hukubaliani na maamuzi ya bodi , tunakukaribisha muda wowote kuleta barua yako ya kujiuzulu”
“Unadhani nnitashindwa kufanya hivyo?”
“Sidhanii hivyo , najua zipo kampuni nyingi ambazo zinakuhitaji”Aliongea Edna bila ya kuonyesha hisia zozote ni kama vile hakuwa akimjua Nasra,
“Benadetha utadili na hili swala , kama Mkurugenzi Mtendaji Nasra akitaka kujiuzlru nipo tayari kununua hisa zake zote kwa thamani mara mbili iliopo sokoni”Aliongea na Benadetha ambaye alikuwa kimya muda wote aliishia kutingicha kichwa tu.
“Edna unafikiri nimesema haya kwasababu ninajali sana kuhusu hisa zangu , unafikiri nitakuwa na furaha kama utanipa hela?”
“Furaha yako hainihusu , asante kwa mchango wako uliotoa kwa kampuni , sitokutendea vibaya kama utaamua kujiuzulu”Aliongea na kumfanya Nasra kujibwaga kwenye kiti huku akimuona kama Edna sio yule ambaye alikuwa akimjua.
“Nasra huna haja ya kuwa hivi , Mwenyekiti wa bodi ashafanya maamuzi lakini ni kweli hatuwezi kwenda nchi za mbali hivyo kwa ajili tu ya kazi hivyo chaguo lililobaki ni kujiuzulu”Aliongea Dorisi.,
“Dorisi unamaanisha nini kwamba hatuwezi , tatizo hapa sio kwenda mbali hivyo , shida ni kwamba hajaongea na sisi kabla , anatuchukulia sisi kama takataka kututupa kila mahali anapoona panafaa , nimeamua kufanya kazi hapa sio kwasababu sina sehemu nyingine ya kwenda kufanya kazi , sijali sana kuhusu nafasi yangu wala mshahara ninaopata wala hisa ninazomiliki, lakini mimi pia kama mfanyakazi wa hii kampuni nina kanuni zangu na utu wangu ambao unapaswa kuheshimiwa”
Dorisi aliishia kukunja sura , alikuwa akijua Nasra alikuwa sahihi lakini ilionekana haiwezekani kuweka mstari kati ya maswala ya kazi pamoja na mambo binafsi.
Dorisi mara baada ya kuwaza hivyo alijikuta akimgeukia Roma na kumpiga jicho na aliweza kugundua alikuwa kwenye mawazo pia kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza , kwani alikuwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Edna tokea siku ambayo nilijiunga na kampuni hii , sijawahi kuwaza kama nitapata chochote , , bibi yako na mama yako ndio watu ambao wamenifanya kuwa Nasra wa leo hii kwa kila kitu nilichokuwa nacho na siku zote nitaendelea kuwa mwenye shukrani , kama shukrani zingeweza kupimwa katika kipimio cha hela basi ningesema faida ambayo nimeingiza kwenye hii kampuni imepita deni ambalo mama yako ananidai , kama sio wewe kuongoza hii kampuni nisingejisumbua kufanya kazi ndani ya kampuni moja kwa miaka yote hio , sikuacha kufuata ndoto zangu na kufanya bidii kwa ajili ya mafanikio ya hii kampni kwa ajili ya mtu yoyote bali nimefanya yote hayo kwa ajili yako , Edna najua ni kweli kabisa nimekukosea wewe binafsi lakini kwanini unataka kunidhalilisha kazini , sijui wengine watanionanje lakini mimi kama mwanamke mwenzio nimekudharau”
Roma alijikuta akiinua uso wake na kumwangalia Nasra ambaye hakutaka kuonekana mnyonge mbele ya Edna , hali yake ya kujiamini na ujasiri wake ilimkumbusha na kumuona kama mwanajeshi.
Edna muonekano wake haukuadilika kabisa , ni kama vile hajamsikia kwa chochote kile alichoongea .
“Kama Miss Nasra na Miss Dorisi watachukua maamuzi ya kujiuzuru , majukumu yao ambayo walikuwa wakiyafanyia kazi kwasasa yatakuwa chini ya Recho , Benadetha pamoja na Rich , nitapenda kuona kila mmoja wenu kuanza kufikiria ni nani ambaye anafaa kurithi kazi zao kabla ya kikao kingine au vinginevyo nitafanya hio kazi mwenyewe”Aliongea kwa kujiamini kabisa.
Ukauzu wake na hali ya kujiamini na kutoathirika iliwaanya wafanyazi kumhofia na kujiuliza inakuwaje akawa haathiriki kwa chochote kutokana na kubweka kwa Nasra.
Nasra alijikuta akimpiga jicho la chuki Edna na palepale alikusanya kila kilichokuwa chake na kisha aliondoka akiwa wa kwanza, ilikuwa ni kama vile alikuwa amepoteza muda mwingi wa kufanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto.
Ni Dorisi peke yake ambaye alijitahidi kuzuia hisia zake zisimvae na palepale na yeye alikusanya vitu vyake na kumsogelea Roma na kumpa ishara ya kumfuata.
“Bado tu unataka kubakia hapa?”Aliuliza Dorisi na Roma alijikuta moyo wake ukijinyonga, katika mazingita kama hayo kama angeonyesha kusita sita ingewafanya kujisikia vibaya zaidi hivyo aliuvaa ujasiri na kisha akawashika mkono na kuondoka nao.
“Tutaenda kwenye hoteli yoyote, na nitawaruhusu mywe bia hadi mlewe mpunguze mawazo , mnaonaje?”Aliongea Roma na wote walitingisha kichwa na kuondoka.
Roma alifanya kama alivyowaambia na aliwapeleka katikati ya jiji na kisha akawaagizia chakula pamoja na vilevi na siku hio Dorisi na Nasra walikichafua haswa kiasi kwamba walilewa chakali.
Baada ya kuelwa wote hakuna ambaye alitaka kuondoka na Nasra na Dorisi wote walitaka kulala hotelini na Roma licha ya kwamba ilikuwa mchana bado.
Roma mara baada ya kujifikiria kidogo aliona awape kile walichotaka na palepale alienda kuchukua chumba na kisha aliwabeba wote kwa pamoja na ulevi wao na kuwabwaga kitandani na kupiga Treesome ya nguvu kwa muda mrefu na mpaka anakuja kumaliza wote walionekana kutosheka na bakora za kimkakati na waliishia kukumbatiana na kisha wakapitiwa na usingizi.
Roma alijikuta akitingisha kichwa na palepale aliangalia saa na kuona ni saa kumi na moja kuelekea saa kumi na mbili.
Ijapokuwa Edna alionekana alikuwa amebadilika nje kabisa ya mategemeo yake lakini hakutaka kupitisha hio siku bila ya kuongea nae , hivyo aliingia bafuni na kuoga na kisha akavaa na kuwaacha.
Kwa spidi aliotumia kuendesha ilimchukua dakika chache tu kufika Ununio na ile anaingia katika barabara ya Ununio Road aliweza kuona gari ya Edna kwa mbele akionekana ndio anarudi kazini.
Dakika chache tu gari iliweza kuruhusiwa kuingia ndani ya geti tena kilichomshangaza zaidi Roma ni kwamba ijapokuwa geti lilikuwa likijifungua lenyewe lakini lilifunguliwa ‘Manual’ tena aliefungua ni Lanlan ambaye pembeni yake alikuwa amesimama Bi Wema.
Roma hakujisumbua kuingiza gari ndani kwani alitoka palepale na kukimbilia ndani,.
“Edna subiri”Aliongea Roma mara baada ya Edna kutoka nje ya gari baada ya kuliegesha lakini ni kama hajamsikia Roma.
Lanlan ambaye alikuwa ndio anamalizia kufunga geti alijikuta akitoa tabasamu la furaha na kuanza kumkimbilia mama yake kwa shangwe huku akimwita Mama.. Mamaaa..
Edna mara baada ya kuitwa vile alisimama na ksiha akamgeukia Lanlan na kumwangali kama vile hamjui.
“Umemuita Mama mtu asiesahihi , mimi sio mama yako”Aliongea kwa Kingereza huku akimtoa Lanlan mikono ambayo imemshikilia.
Kitendo cha Edna kumwambia Lanlan vile kilimfanya kumwangalia kwa macho ya kutia huruma na palepale aliishia kuchuchumaa na kuanza kudondosha machozi chini.
Roma alietaka kuongea tena alijikuta mdomo wake ukiishia hewani na hasira zilimpanda mara baada ya kumuona binti yake akilia.
Lanlan alikuwa na furaha ya kumuona mama yake kwa mara nyingine na hata ujio wake hapo ni kutokana na kujua huo ndio muda wa kurudi kazini lakini jibu la Edna lilimnyong’onyesha , alikuwa ni kama vile amemwagiwa ndoo ya maji ya baridi.
Roma alikubali Edna kumchukia yeye lakini alijiuliza kwanini anamfanyia hivyo na Lanlan ambaye anamchukulia kama mama, uvumilivu palepale ulianza kumpotea.
“Edna naona sasa unavuka mpaka”Aliongea Roma kwa namna ya kufoka huku akimpakata Lanlan na kumfanya machozi yake yaloanishe kifua chake
“Mommy doesn’t want Lanlan again …Mommy doesn’t like me anymore..”Aliongea Lanlan akilia akisema kwamba mama hamtaki tena na mama yake hampendi.
Kilio cha Lanlan kiligusa moyo wa Bi Wema na alijikuta akimsogelea Edna na kumwangalia usoni.
“Edna unafanya nini , huwezi kutolea hasira zako kwa mtoto kisa tu mna ugomvi”Aliongea Bi Wema na palepale alimsogelea Lanlan kwa jaili ya kumtuliza lakini ilikuwa ngumu kutulia.
Lanlani alikuwa na kumbbukumbu za kuachwa na mama yake kwa mara ya kwanza hivyo hicho kinachotokea ni kama alikifananisha na kumbukumbu zake mbaya zilizopita ndio maana kilio hakikiwa cha kawaida.
“Bi Wema mimi sitaki kuhusika nao tena , huyo ni mtoto wake na sisi tumeachana, ni kwamba tu hatujasainishiana maswala ya talaka kwani kuna taratibu za kuchukua”Aliongea
Roma alikuwa akitetemeka kwa hasira mno kutokana na kilio cha Lanlan na alijihisi ni kama ule uchizi wake wa siku nyingi unaanza kumvaa.
“Edna ,,, unaweza kunichukia utakavyo na sitolaumu lakini umemuumiza binti yangu kihisia ,, na hii ni sababu ambayo inanifanya nitake kukua sasa hivi..”