NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR
Mono no aware.
SEHEMU YA 704.
Katika ulimwengu wa kijini wakati wa kufunguka kwa jicho la Anga wanaita ni kipindi cha mavuno makuu ,ni kipindi muhimu sana katika huo ulimwengu kama ilivyokuwa katika ulimwengu wa majini pepo kupambania kuingia katika mnara ili kupata mimea na hazina ndio ilivyokwa ulimwengu wa majini wa kawaida.
Ni hatari sana kuingia kwenye ulimwengu wa Jicho la Anga hivyo wanaoenda huko ni majini ambao wapo katika levo za juu sana ili kuweza kushindana na majini ambao washageuka na kuwa pepo(ghost).
Ndio majini wanakufa pia na wenyewe wanaamini roho za majini hukimbilia katika ulimwengu wa Jicho la Anga.
Sasa Roma mara baada ya kupata habari hio anajikuta akipatwa na hamu ya kwenda kujionea , aliwaza labda anaweza kupata siraha ya kimaajabu katika huo ulimwengu lakini kwa bahati mbaya njia ya kuingilia katika ulimwengu huo ipo chini ya miliki za kijini , lakini pia aliona hata kama akiingia inaweza kuwa shida kwake kurudi.
Yaani kwa kifupi ni kwamba mshindi wa kuingia huko akishapata nafasi koo zingine hulinda jicho hilo ili kuhakikisha hakuna anaevamia kinyemela na kuingia.
“Tukiachana na hayo , nini kimekuleta hapa Bro XiaoCheni?”Aliuliza Zomu na kumfanya Roma kusita kidogo kuongea , ni kama vile ni jambo la aibu.
“Kuna kitu ambacho nahitaji unisaidie lakini nahisi kama haitowezekana..”
“Ongea tu Braza , mimi kama rafiki yako lakini pia kama jini ambaye nimepokea ukarimu mwingi kutoka kwako , kwanini nikatae kukusaidia?”
Roma palepale alianza kumwambia kuhusu Feilo kukutana nae nyakati za usiku kwa ajili ya kujifunza pamoja .
“Feilo amesema uende kwenye makazi yake saa nne usiku kwa ajili ya kukusubiri hivyo…”
“Ah… kumbe ni jambo hilo , niliamwangalia Feilo namna alivyokuwa akitumia ngumi yake kukushambulia na ile ngurumo yake ya Simba vilinivutia mno ,nilikuwa nikitamani pia kukutana nae , hivyo nipo tayari usiku wa saa nne nitamtafuta”
“Asante sana Bro Zomu kwa msada wako , lakini natumaini hutoenda na Zato , Feilo ni muumini wa Kibuddha na hapendi wanawake wake kabisa”Aliongea Roma akicheza na maneno vizuri kabisa ili kukamilisha jambo lake.
“Usijali hata Zato mwenyewe hapendelei sana kuwa karibu na wanaume , hivyo nitamuacha, naamini kwa muda huo atakuwa amelala pia”Aliongea Zato huku akionyesha kidogo hali ya kusikitika akimuonea huruma dada yake kwa uvivu wa kujifunza.
Sasa Roma alikuwa tayari amekamilisha mpango wa kuhakikisha Zomu anakaa mbali na Zato nyakati za usiku , haikueleweka alikuwa akipanga nini lakini alikuwa akifanya kitu kilekile ambacho ameagizwa na Zilha.
Hivyo usiku Zomu angeenda katika eneo ambalo Feilo anajifunzia kwa ajili ya kushirikiana na kujaribu kupambana na huku nyuma Zato angekuwa peke yake.
Roma mara baada ya kuachana na Zomu hakutaka kuzembea na yeye alianza kujifunza mbinu za kutumia siraha za kijini kama vile mapanga n.k.
Njia rahisi pia ya kujifunza mbinu za anga ni kutumia kujifunza mapigano asilia kwa kutumia upanga au njia za kawaida , hivyo majini wengi walikuwa wakitumia mbinu hio hii ni kwasababu mtu au jini linapokuwa katika mafunzo ya kisiraha akili yake inapata umakini zaidi na zaidi lakini pia ina upa ubongo hali ya utulivu.
Hatimae ile saa ikawa imetimia , Roma makusudi kabisa alihakikisha hakuna majini ambao wapo karibu wenye uwezo wa juu zaidi ili kuhakikisha mpango wake unaenda sawia.
Baada ya kuona eneo lipo shwari palepale alitoka anapoishi na kwenda katika makazi wanayoishi Zato na Zomu wakati huo akiwa na uhakika Zomu tayari ashaondoka.
Kwa kutumia Dhana yake ya Jani la Upofu aliamini hakuna jini lolote ambalo lina uwezo wa juu kunasa kile anachokifanya kwa usahihi.
Roma mara baada ya kufika nyuma ya nyumba ya Zomu na Zato alijificha na kisha palepale aliruhusu nguvu za kijini kujifahamisha mazingira ya eneo hilo yalivyo.
Jini Zilha uwezo wake ulikuwa mdogo sana kuliko wa Roma hivyo hata kama akihisi msisimko wa nguvu za Roma asingeweza kugundua chochote.
Roma mara baada ya kuangalia aliona ni kama alivyotegemea Zato alikuwa yupo peke yake akiwa usingizini kama alivyosema Zomu.
Majini pia wenyewe wanalala na hio yote ni kutokana na kuwa na miili ya kibinadamu kabisa ambayo inatoa damu, lakini hata hivyo wanaweza kutokulala kwa muda mrefu sana bila ya kupata shida yoyote, wao kulala ni kama ibada.
Zilipita dakika tano tu wakati Roma akiwa amejibanza nyuma ya nyumba hatimae Zilha aliweza kufika ndani ya makazi hayo , alianza kukagua mazingira kwa wasiwasi kuhakiki kama hakuna kiumbe chochote kinachomuangalia na baada ya dakika moja hatimae alifungua mlango taratibu.
Roma palepale alifutika alipokuwa amejificha na ile anaibuka alikuwa nyuma ya Zilha.
Zilha alikuwa akimwangalia Zato aliekuwa amelala kwa macho ya uchu kweli , kiuno chake , manyonyo na sura yake ya kirembo ilimfanya kupagawa kabisa na udenda kumtoka.
Zilha alimpenda Zato kutokana na kuwa msichana ambaye amekaa ki’sassy zaidi na mkali mno hasa anapoangaliwa na mwanaume na hali hio ilimtia shauku angeonekana vipi mara baada ya kumwingizia bakora yake na ndio maana alitumia shida yao ya vidonge ili kuwabakisha ndani ya himaya yao ili kukamilisha shauku yake.
Alikuwa akimpangia mpango muda mrefu sana hata kabla ya Roma kuja ulimwengu wa kijini , ukweli ni kwamba ashafanya mipango ya aina hio hio mara nyingi na ikafanikiwa hivyo aliamini na kwa Zato anakwenda kufanikiwa.
Mara nyingi akishakamilisha mpango wake palepale kwasababu majini hao wa kike wanakuwaga na uwezo wa chini basi atawabembeleza kwa vidonge na tuvizawadi na kuwatishia kidogo na baada ya hapo watakuwa wanajileta wenyewe.
“Kama ungekuwa na akili usingefikiria njia za kihuni namna hii kucheza na hawa wanawake”Aliwaza Roma kwenye akili yake akiwa nyuma ya Zilha na palepale aliachia mkandamizo wa nguvu za kijini na kumsomba Zilha kimzobemzobe na kutoweka mbele ya makazi ya Zato na Zomu.
Zilha alijikuta akipiga Yowe mara baada ya kufanyiwa shambulio hilo la kushitukiza na jini mwenye nguvu zaidi yake.
Bahati nzuri ni kwamba walishafika kwenye msitu mbali na makazi ya majini hivyo sauti yake haikuweza kwenda mbali.
“Wewe … wewe ni nani?”Zilha jasho lilianza kumtoka huku akitetemeka kwa woga bara baada ya kudondoka chini.
Roma palepale aliondoa ule mkandamizo wa nguvu zake za kijini na kisha akaupamba uso wake na tabasamu bandia.
“Kwanzia sasa mimi ndio nitakuwa nauliza swali na wewe ndio unajibu”
Zilha alimeza mate mengi alishindwa kabisa kuona levo ya Roma lakini aliweza kuamini kwamba hakuwa katika levo ya Nafsi ,haikuwa kwake tu ambaye amedanganywa lakini majini wote walidanganywa na Xiao Cheni jini aliejifanyisha kuomba hifadhi.
Lakini katika hali kama hio hakutaka sana kufikiria Roma ni nani haswa na aliishia kutingisha kichwa kukubaliana na Roma.
“Vizuri”Roma alitabasamu huku akimwangalia jini Zilha kwa macho yaliojaa umakini.
“Una mdogo sijui binamu wako afahamikae kwa jina la Rufi ndio au sio?”
“Huyo M*lay umemjuaje ….!!?”Zilha alijikuta akishangaa huku akitamka tusi na kumfanya Roma kumwangalia kwa macho makali.
“Pumbavu zako, mwite tena hivyo uone kama sitokuua hapa hapa”
“Ndio namjua na sitomwita tena hivyo …. Rufi ni mtoto wa mjomba?”
“Je yupo hapa Kekexili?”
“Kwanini unaulizia kuhusu yeye kwanza?”Aliuliza Zilha kwa kuchanganyikiwa.
“Acha upumbavu , jibu swali langu”Aliongea huku akimchapa kibao na kumfanya Zilha kutoa mguno wa maumivu.
“Sijui mahali alipo lakini nina uhakika hayupo hapa Kekexil … alitorokea kwenda ulimwengu wa kawaida kuepuka ndoa na ni juzi tu familia yetu ilipokea taarifa kwamba wameweza kumpata huko duniani lakini sina uhakika kama walishaenda kumchukua kumrudisha au lah… Mjomba yeye amesema Rufi ni msaliti wa familia na miliki yote ya majini hivyo hana nia ya kumtambua kama binti yake tena, hivyo hata kama akirudi lazima atakuwa katika miliki ya Xia”
“Kama ni hivyo kwanini ulikuwa kwenye Jumbe jeupe leo hii , sio kwasababbu kuna majini ambao hufungiwa ndani ya jengo lile?”
“Ndio kuna wafungwa lakini sio Rufi , kuna majini ambao wapo kinyume na familia yetu ndani ya miliki na pia ambao wametusaliti ndio wamefungiwa”
“Sasa kama ni hivyo kwanini ulienda kuwatembelea?, Yaani unaona furaha kutembelea wasaliti , unaniona mimi mjinga?”Aliongea Roma kwa hasira na kumfanya Zilha kushindwa hata kumwangalia usoni.
“Ni kijakazi wetu afahamikae kwa jina la Sui ambaye alimsaidia Rufi kutoroka kipindi cha nyuma , familia yetu ilitaka kumuua mara baada ya tukio hilo ila nilimuona anatia sana huruma na nikamuomba babu yangu kumfunga gerezani”Aliongea.
Roma hapo hapo alikumbuka Rufi kumtaja jini ambaye alimsaidia kurorokea kwenye ulimwengu wa kawaida , inaonekana tokea kumtorosha Rufi alikuwa ni mfungwa ndani ya jumba hilo jeupe.
Kwa muonekano wa Zilha hata mjinga anaweza kujua nini ambacho anamfanyia Sui , ilionekana alikuwa akitumika kama chombo cha Zilha kupunguzia genye.
“Sio kwamba ulitaka kumuokoa bali ulikuwa ukipanga kumtumia kingono”
“Ndio nilimuokoa lakini niliona ni vyema pia nikijilipa kidogo kidogo”
Roma alijikuta akijizuia kutokumuua na mpaka hapo alikuwa tayari kumuokoa Sui vinginevyo kama habari hizo zingemfikiria Rufi basi angeteseka sana na mawazo maana alikuwa ni mlezi wake.
“Nimesikia kuna njia ya moja kwa moja ya siri kwa wanafamilia kuingia katika Jumba Jeupe , niambie njia hio ikoje?”
“Hapana , siwezi kusema , Jumba Jeupe ndio fahari ya miliki yetu na lipo chini ya familia , kama nitakuambia njia hio baba yangu na babu yangu wataniua , nipo tayari kukupatia vidonge, Dhahabu na hazina zote nilizo nazo ”
“Kama ni hivyo chagua mambo mawili , aidha kufa sasa hivi au kuwa hai?”Aliongea Roma kwa usiriasi mkubwa.
Jini Zilha alijikuta akihisi msisimko wa roho ya kimauaji kutoka kwa Roma , ilikuwa ni kama kifo kipo kwenye masikio yake na katika maisha yake hakuwahi kuhisi nguvu ya kimauaji inayomtoka Roma kama hio.
“Nitaongea …!”
Hakutaka kufa hivyo aliamua kumwambia Roma kila kitu namna ya kuvunja mfumo wa kimiujiza ambao unalinda jengo hilo
Ni mfumo kama wa nywira lakini ilihitajika kutumia nguvu za kijini ili kufungua wakati huo huo ukitumia njia ambazo amelekeza Zilha.
Ilikuwa rahisi kwa Roma kujifunza na kuelewa hekima ya mababu wa kijini ambao walitengeneza mfumo huo ,ilikuwa ni njia ya kipekee sana na Roma aliishia kutoa mshangao na kujiambia kweli majini wa Zamani walikuwa ni viumbe wenye akili sana na ilimfanya kuwa na huzuni vizazi vipya walikuwa ni majini ambao hawana thamani kabisa na ambao hawafikirii nje ya boksi kama Zilha.
Roma aliona pengine ndio maana maisha yao yalionekana kizamani zamani.
Majini wanasifika katika kutii sheria kuliko hata binadamu na sheria ambazo zimewekwa na waasisi wao na wanafuata mpaka wakati huo bila kubadili chochote , yaani mawazo ambayo yamewekwa na mababu zao ndio ambao wanaishi nayo katika wakati huo na hili liliwafanya kutopiga hatua ya kimaendeleao na kitu pekee ambacho wanawaza ni kuvuna nishati tu na kupanda levo.
Upande wao Material things ni vitu ambavyo havina thamani kubwa kama ilivyo kwa binadamu kupenda vitu kama vile madini na pesa.
Sio kwamba hawana akili , akili wanazo tena zaidi ya mara kumi ya binadamu wa kawaida lakini akili zao hawazitumii katika Miundombinu kama ilivyo kwa binadamu bali wao akili zao huzitumia katika kuelewa siri za kiroho juu ya yale ambao wameyasahau na yale ambayo hawajui.
“Wewe kama mtoto mkubwa ndani ya familia yenu, je kuna hatua zozote zinazohitajika katika kuingia katika Jumba jeupe?, kwa mfano labda kuomba ruhusa kwa babu yako na kadhalika?”Aliuliza Roma na kumfanya Zilha kumwangalia kwa huzuni.
“Mwanafamilia yoyote anaweza kuingia muda wowote atakao”
“Je kama ukiambiwa kumtoa Sui nje muda wowote , inawezekana?”
“Ndio , Sui yupo chini yangu , ikimaanisha kwamba ni mtumwa wangu , ninao uwezo wa kumfungia na kumfanya awe huru muda wowote , wazee na walinzi wa Jumba hawawezi kunizuia kwa chochote , naomba uniachie nikamtoe Sui sasa hivi”Aliongea na kumfanya Roma kutoa tabasamu la kejeli.
“Vua nguo zako”
“Nini!?”
“Nimesema Vua nguo zako , shati , suruali na viatu kila kitu”Aliongea huku akimwangalia kwanzia chini mpaka juu.
“Unakwenda kunifanyia vile mnavyofanyiana binadamu?”
“Acha ujinga , unajua kila kinachoendelea ulimwengu wa kawaida licha ya kukaa huku”Aliongea Roma na kumpiga teke.
Zilha hakuwa na jinsi na palepale alianza kusaula nguo moja baada ya nyingine huku akijiambia baada ya hapa ni kwenda kumwambia babu yangu na baba na watamshikisha huyu mpuuzi adabu.
Roma aliona pete ambao Zilha amevaa kwenye kidole chake , baada ya kumaliza kuvua nguo alimwambia aivue na yenyewe ampatie.
Zilha alionyesha uso wenye uchungu lakini maisha yake yalikuwa muhimu kwa wakati huo hivyo alifanya kama alivyoambiwa.
“Inatosha sasa maana sihitaji nguo yako ya ndani”
“Kwahio naweza kuondoka?”
“Ndio lakini sio kurudi kwenye familia yako”
“Kwahio niende wapi?”
“Kuzimu”
Aliongea Roma na palepale kitenesi cha mwanga wa bluu kilijitokeza katika mkono wake wa kushoto.
Mwanga wake ulianza kufanya mazingira kuwa angavu na kufanya wadudu kuanza kuamka.
Lakini upande wa Zilha alihisi nguvu ya ajabu ambayo inatoka katika kitufe kile na alitaka kukimbia .
Hio ni mbinu mpya Roma ambayo alikuwa ameigundua kwa kuunganisha moto wa kiroho na maji ya kiroho ndio kukatokea siraha ya namna hio , ilikuwa ni kama moto wa rangi ya bluu lakini haukuwa moto.
Haikuwa na haja ya Roma kutumia siraha hio ya kimaajabu ya juu kabisa kumuua nayo Zilha lakini alifikiria mateso aliokuwa akipitia Sui mlezi wa Rufi na aliona pengine hata chungu chake kingejisikia kichefuchefu kumeza huyo mpuuzi.
“Hapana… sitaki kufa”Alibweka mara baada ya kugundua nini ambacho kinakwenda kumtokea na kuanza kukimbia lakini spidi ya Roma ilikuwa kubwa kuliko ya kwake na palepale kwa kuunganisha nishati ya mbingu na ardhi alimshusha chini ardhini.
“Bang!!!”
Roma alimtupia kile kitufe cha rangi ya bluu eneo la moyo wake na palepale mwili wake ulianza kuyeyuka kwa kasi mno.
“Arghhh…!!”
Zilha aliishia kutoa ukulele wa maumivu na ndani ya dakika hio hio alikuwa tayari ameshapoteza uhai na palepale upepo ulianza kuongezeka na kupeperusha chembechembe za mwili wake.
Roma wala hakujisikia vibaya kwa kile alichokifanya hata kama alikuwa ni mtoto mkubwa wa familia ambaye anatarajiwa kuwa mrithi hapo baadae , alikuwa ni njia kwake ya kuweza kumpata Rufi.
Roma palepale alivaa mavazi ya Zilha na kisha ka kutumia Dhana ya Jani la Upofu alichukua muonekano wake na kubadilisha levo yake ya kijini na sasa kwa asilimia mia moja alifanana na Zilha.
Kuhusu ubini wake alijitambulisha ndani ya familia hio kama Xiao Cheni hakuwa na haja nao tena na alijiambia hata kama ikija kutokea familai hio kumtafuta Xiao Cheni na kutokumona wasingehangaika sana kwani hana thamani kubwa kwao.
Roma palepale aliona ingekuwa vibaya kama angeenda kumuokoa Sui moja kwa moja wakati wa usiku hivyo alijiambia labda anapaswa kwenda kesho yake kwani kama ni Zilha halisi alishakufa na yeye ndio Zilha.
Akiwa njiani alijaribu kuangalia katika hifadhi ya pete ya Zilha kuona kama kuna chochote cha maana lakini aliona hakuna kwani kulikuwa na vidonge vya daraja la chini na baadhi ya mimea ambayo aliona ni takataka kwake.
Roma mara baada ha kufika katika makazi ya familia ya Zilha ambao ndio wakuu wa miliki ya Kekexil aligundua hakuwa akijua ni upande upi ambao Zilha alikuwa akiishi., alichokumbuka ni kwamba familia hio yote ilikuwa ikiishi katika eneo moja.
Bila kujali Roma alitua ardhini ndani ya eneo hilo na kujifanyisha anatembea tembea kwa namna ya kukagua mazingira.
Ile anataka kupita nyumba moja ambayo ilikuwa imejengwa kwa staili ya kipekee alianza kuhisi harufu ya marashi makali ikiongezeka na kufumba na kufumbua alikuwa ameshikiliwa shingo na mwanamke mrembo.
SEHEMU YA 705.
“Wewe mkorofi mbona unachungulia vyumba vya wanawake usiku usiku au ndio unatafuta kitoweo?”
Sauti nyororo ilisikika kwenye masikio ya Roma na palepale alipokea busu la shavu ambalo lilimletea msisimko wa aina yake na Roma alijiambia mabusu ya jini ni tofauti na ya binadamu.
Mwanamke huyo hakuwa mwingine , alikuwa ni Jini Manyani binamu yake Zilha na alikuwa amevalia gauni ambalo lilifanya umbo lake la rangi nyeupe kuonekana, ni vazi ambalo lilikaa kimitego zaidi.
“Kwanini unanishangaa, hujawahi kuwa hivi au nimekuwa mrembo sana leo?”Manyani aliongea baada ya kuona Roma ameduwaa.
Roma alijikuta akimeza mate huku pua zake zikisumbuliwa na marashi ya yanayofanana na mmea wa Orchid uliokaushwa na kushusha shingo yake na kuanza kumkagua jini Manyani.
Roma licha ya kujua Zilha alikuwa muhuni lakini hakutegemea kama alikuwa akitembea na binamu yake na alijiuliza kumbe hata ulimwengu huo ulikuwa umeharibika tu kama ulimwengu wa kawaida
Kwa wakati huo Roma hakujua namna ya kuendelea na hali hio lakini alijua kwasababu alikuwa akijifanyisha ndio Zilha basi hawezi kumkatalia.
Yalikuwa ni mawazo ya sekunde moja tu na palepale Roma alibadili muonekano wake na kuweka ule wa kihuni na kumfanya kufanana na Zilha kabisa.
“Nimeshindwa kulala na kuanza kutafuta kitoweo na wewe ndio umejileta mwenyewe, Kabebi kangu mwaah…!!”Aliongea Roma huku akishika shavu la Manyani , aliona kwa namna yoyote ile anapaswa kuwa romantic.
“Nilijua ulienda kucheza na mdogo wake Zomu ,nadhani jitihada zangu zimekufanya kunikumbuka”Baada ya kuongea hivyo alimsogelea Roma na kuanza kumbusu kwenye midomo yake na kutumbukiza ulimi kwenye mdomo wa Roma.
Roma hakutegemea Manyani kuwa mpana namna hio kwa kwenda moja kwa moja kwenye hitajio lake licha ya kwamba wapo eneo la wazi , huenda alikuwa amecheza michezo ya namna hio na Zilha mara nyingi.
Kulingana na uzoefu wa Roma aligundua huyu jini atakuwa amecheza na majini wengine wa kiume sana.
Roma alikumbuka wakati anatoka na Feilo kwenye jumba jeupe alimtahadharisha kwamba katika familia hio ya kifalme anapaswa kuwa makini na Jini Zilha pamoja na Lilsi kwani wanapenda kuwatumikisha kingono sana binadamu na majini wa kiume.
Roma alijiambia mama na mwana hakika wanafanana
Licha ya kwamba alikuwa amechezewa sana lakini umbo lake bado lilikuwa zuri na alikuwa akivutia mno kulinganisha na wanawake makahaba ambao alikuwa akitumia kabla ya kukutana na Edna.
Roma kwa muda huo hakutaka sana kujali , isitoshe alikuwa amecheza sana na wanawake hivyo kumshughulikia jini kama huyo hakuona tatizo , kama aliweza kulala na Lilith Vampire anashindaje kulala na jini Manyani ili kulinda misheni yake.
Roma mara baada ya kujishawishi kupitia matendo yake machafu ya nyuma palepale alianza kumshambulia jini Manyani na kumfanya kuanza kuzidiwa.
“Twende ndani ya chumba vangu , ijapokuwa hakuna mtu hapa anaetuona lakini sio pazuri”Aliongea na Roma hakuchelewesha na palepale aliruka na mrembo huyo kupitia dirishaji na kwenda kutua kwenye chumba chake.
Kabla ya kuanza mchezo Manyani alimzuia Roma kuendelea na kisha palepale kama anapunga upepo aliachia nguvu ya kijini ambayo iliwasha kitu kama mshumaa katikati ya chumba na ndani ya dakika chache tu harufu nzuri ilianza kusambaa,
“Unafanya nini?”Aliuliza Roma asielewe nini kinaendelea na Manyani alionyesha uso wa kuomba msamaha na kuanza kulamba kifua cha Roma kimahaba.
“Kaka Zilha usikasirike , sijasema kwamba huwezi kufanya , si unakumbuka mara ya mwisho tulitumia harufu ya Mandala na ukafanikiwa kusimamia shoo kwa masaa mawili?”
Roma palepale kwa siri sana alipumua kwa ahueni , ilionekana alikuwa akimsaidia Zilha kudumu muda mrefu kwenye tendo, lakini Roma kwake aliona hilo halina maana lakini kudili na jini hilo Roma aliona anapaswa kuwa makini ili kuhakikisha anakuwa anajisikia vizuri.
Dakika ileile alimbeba juu juu na kupandisha gauni lake na kisha akamlamba vibao vitatu vya makalio.
“Slap! Slap! Slap!”
Upande wa jini Manyani alifurahishwa na kitendo kile kana kwamba alikuwa akihitaji Roma kuendelea kufanya hivyo na kumfanya Roma kuona kweli huyu ni malaya wa kijini aliekubuhu.
Roma hakutaka hata kujisumbua kumwandaa kwani alimchukulia kama changudoa wa kijini hivyo alivua nguo zake kuanza kazi.
“Broo ,, ime.. ime , kwanini imekuwa kubwa hivyo!!?”
Roma palepale alikumbuka kiungo chake hakikubadilika ukubwa na kufanana na Zilha , lakini hata hivyo angejuaje saizi yake kwani hakumwangalia.
“Mwanamke mjinga , hujui inaweza kubadilika muda wowote kwa kumeza vidonge?”:
“Ah!,Ndio umetumia vile Vidonge vya Tinya ambavyo vinavumishwa kuongeza ukubwa?”Aliuliza kwa mshangao lakini Roma hakutaka kujisumbua kujibu , alijiambia anachokifanya hapo ni sehemu ya misheni yake na mambo ya Tinya Tinya watajua wenyewe.
Roma alimpa bakora za kimkakati jini Manyani na kwa mwanamke huyo alijihisi ni kama vile amevamiwa na mnyama na alijiuliza imekuwaje kaka yake akawa na nguvu namna hio siku hio, lakini hakutaka kujiuliza zaidi alijiambia huenda ni vidonge vya Tinya.
Ukweli ufanisi wa Dhana ya jani la upofu ilikuwa ni juu mno na Manyani hakuona utofauti wowote.
Manyani alikuwa ni jini mwenye uwezo wa nafsi na alikuwa na uwezo wa kuhimili mikiki ya namna hio lakini hakutaka kutumia uwezo wa kijini bali alijifanyisha kama binadamu wa kawaida ili kukolewa na surubu.
Dakika chache mbele aliweza kuhiisi ni kama mwili wake upande wa chini umekuwa wazi mara baada ya nyoka kuchoropoka pangoni na alihisi ubaridi ukiingia.
Dakika hio hio wakati akijishanga shangaa alishikwa shingo na Roma na kumfanya aachame na kabla hajajua kinachomtokea Dragoni tayari alishaingizwa kwenye mdomo wake na kuishia kuguna.
Roma alikuwa amemisi sana mambo hayo wakati alipokuwa Ulaya lakini hakutaka kuyafanya kwa wanawake zake kwasababu alikuwa akiwapenda , lakini kwasababu alimchukulia jini Manyani kama kahaba aliona ateme uchafu wote ndani ya mdomo wake ili kuweka rekodi sawa.
“Naona unapenda kuchezewa Rafu sio”
“Ndio napenda sana rafu kaka yangu , nakupenda sana kaka lala leo hapa hapa maana nitakumisi kuanzia kesho ukiondoka”
“Kesho nikiondoka!!!”
Roma machale yalimcheza palepale huku jasho likianza kutiririka mgongoni , ilionekana kesho Zilha kuna sehemu alikuwa akienda na ilikuwa bahati nzuri kwamba alikutana na huyo jini kahaba la sivyo angekamatika.
“Nadhani sina haja ya kwenda , nataka kukufaidi wewe mrembo”
“Mh! ,unawezaje? Mjomba anakupeleka kutembelea matawi ya miliki yetu hivyo hupaswi kukataa kwani unapaswa kupata sapoti kutoka kwao kama unataka kumrithi , Kaka una uwezo mdogo sana wa kijini kama hutotumia nafasi hii vizuri na baba yangu akipata mtoto wa kiume mwenye vigezo au babu akipata jini anaefaaa huwezi kurithi tena na itakuwa ni usumbufu”
Roma palepale alijua sasa safari hio inahusiana nini kumbe ilikuwa ni kwenda kutembelea koo zingine ambazo zipo chini ya miliki ya Kekexil. “Nilijua tu kuna zaidi ya koo moja ndani ya uimwengu wa kijini”aliwaza Roma.
Ukweli hata yeye alishangazwa kama kweli Kekexil ilikuwa na nguvu kama alivyosema Rufi kwanini alipofikia hakuna majini wengi , kumbe majini wote hawaishi sehemu moja.
Ukweli ni kwamba Kekexil ni jina la miliki lakini koo ya Mo ilikuwa na nguvu sana katika ulimwengu huo hivyo kuweza kutwaa koo zingine na kuunda miliki moja inayofahamika kwa jina la Kekexil , hivyo ni sawa na kusema ndani ya miliki ya Kekexil familia yenye nguvu zaidi ni ya Mo ambayo ndio ya baba yake Yezi.
Ilionekana Zilha alikuwa na presha kubwa kwani familia nyingi za kijinni ndani ya miliki hio zilikuwa na majini wa rika lake ambao walikuwa juu sana kinguvu , hivyo kwake ingekuwa ngumu kupata nafasi ya kurithi bila ya kuwa na koneksheni.
Lakini kwa wakati huo haikuwa na maana tena kwani tayari amekwisha kufa na Roma sasa ilipaswa kutembelea hizo familia nyingine za kijini kwa niaba yake.
Roma hakuwa na chaguo lingine kwa wakati huo na aliona kwanza asubirishe mpango wa kumuokoa Jini Sui, hata hivyo alijua wasingekaa huko muda mrefu kwani huyo Master Shagoni ambaye alitegemewa kuja kwenye ukoo huo kutoa mafunzo angekuja katikati ya mwezi hivyo lazima Mkuu namba tatu wa majini , Mohi lazima angerudi wakati ambao Shagoni anafika.
“Tatizo nini, hata kama nnikiondoka najua utafuata wanaume wengine na kucheza nao”
“Kaka kwahio una wivu na mimi? , nikuambie tu sijacheza na hao wanaume kwa muda mrefu , hao majini ni watumwa kwa familia yetu na ni kama midoli tu ya kucheza nao , unapaswa kujua mimi nakupenda zaidi wewe”Roma alijihisi ubaridi wa mgongoni kwa kuona kinachoendelea kati ya ndugu na ndugu.
“Kuwa makini huko uendako , mashindano ya kuingia Jicho la Anga yataanza mwaka huu na hao watoto wa koo nyingine wanachowaza ni kukuondoa kwenye orodha..”Aliongea mara baada ya kukosa jibu analitarajia kutoka kwa Zilha na Roma alitingisha tu kichwa kukubaliana nae.
*******
Asubuhi baba yake Zilha alikuwa ashajiandaa kuanza safari na wazee wengine na alimpa maagizo Mkuu wa Chemba jini Ganyo kwenda kumwita lakini muda uleule alisitisha baada ya kumuona mtoto wake akifanya mazoezi nje ya ukumbi.
Mohi na wasaidizi wake walisimama na kuanza kushangaa na kujiuliza ni lini Zilha akaanza kujifua kimazoezi kwa hiari yake.
Roma alijifanyiha kuona aibu kuangaliwa na baba yake feki na palepale alitoka alipokuwa anafanya na kupaa na kwenda kutua mbele ya baba yake.
Jini mkuu namba tatu alijikuta akishangazwa na mtoto wake mara baada ya kugundua tayari ameingia katika levo ya kutawala moto wa rangi ya njano jambo ambalo hakutegemea na palepale hatia ilianza kumvaa na kujiambia kumbe alikuwa akimfokea bure mtoto wake na alikuwa akijifunza kwa siri.
Siku zote alimchukulia Zilha kama mtukutu ambaye hajali kujifunza mbinu za anga na mara nyingi kupenda kutoroka ulimwengu wa kijini na kwenda duniani kulala na wanawake wa kibinadamu lakini maendeleo yake hayo yalimfanya kuona alikuwa akimfokea bure.
Baada ya Roma kupokea sifa pale kwa jina la Zilha hatimae safari ilianza na alielewa kwamba ingewachukua siku kumi na tano kwenda na kurudi.
Roma aliishia kufuata nyuma nyuma akiendelea kusikiliza maongezi yao na alianza sasa kuelewa namna ulimwengu huo ulivyo na mahusiano ya familia hio na koo zingine yalivyo.
Roma alifanya makusudi kabisa kupandisha kidogo uwezo wake ili kumfanya Zilha kuonekana yupo siriasi kumfurahisha baba yake ili hata akiuliza maswali ajibiwe.
Roma katika kusikiliza maneno hayo alikuja kugundua kuna majini wengi sana ambao wamesambaa katika familia mbalimbali na familia zote hizo ilionekana zilikuwa na uwezo wa kushika wadhifa waliokuwa nao familia ya Mo.
Yaani kwamba familia hizo kama zitaweza kuzidi familia ya Mohi kinguvu basi hawana namna zaidi ya kukubali kushindwa na kuachia madaraka kwa familia nyingine , hivyo safari hio ilikuwa ni kuhakikisha kwamba wanakuwa na ushirikiano wa ukaribu na familia hizo ili kuwasapoti.
Kitu kingine ambacho Roma alijifunza ni kwamba kila familia inakuwa na Mkuu wao ambao ananguvu zaidi ya familia nzima , yaani ilikuwa kama kwa ukoo wa Zaola kupambania mzee wao kuingia levo nyigine ndio ilivyokuwa kwa familia nyingine walikuwa na wakuu wao ambao wote walikuwa levo za juu kabisa za kuivuka Dhiki.
Kitu kingine ambacho Roma alikuja kujua ni kwamba familia ya Xia ndio ambayo ina nguvu kubwa sana kuliko hata ya Kekexil na hio yote ni kutokana na kwamba wanao masters wengi wa kijini ambao wamepita Dhiki kitambo.
Roma alikuja kujua pia yule Bibi kizee aliefahamika kwa jina la jini Tigola ambaye kazi yake ni kulinda geti la mlango wa kuingilia kwenye Jumba jeupe ni sehemu ya Master ambao Rufi alikuwa akizungumzia
Mpaka wakati huo Roma alikuwa ashafahamu Master watatu , wa kwanza ni babu yake Zilha ambaye ndio mkuu namba moja wa majini katika miliki ya Kekexil na wa pili alikuwa ni Master Shagoni ambaye alitarajiwa kufika kufundisha na watatu ni yule Ajuza.
Roma aliuliza maswali mengi wakati wakiwa njiani na kwasababu wazee hao wakijini walianza kumchuklia yupo siriasi basi walimjibu kila kitu , isitoshe walijua hakuwa akijua chochote kuhusu msingi wa miliki yao hivyo walimweleza kwa furaha kwani walitarajia angekuja kuwa mrithi.
Kadri Roma alivyokuwa akisikiliza maelezo yake ndio jinsi woga ulivyomwingia na kugundua eneo hilo ni hatari zaidi nje ya alifyofikiria kwa yeye kuendelea kubaki hivyo aliona anapaswa kuwa makini zaidi na zaidi na kukamilisha misheni yake na kuondoka kimya kimya.
Kulikuwa na vitu vingi sana ambavyo Rufi hakumwambia , pengine ni kwasababu hakuvijua na ndio sasa Roma aliweza kuvijua.
Roma hakutaka kupumzika hata kidogo mpango wake sasa ulikuwa ni kwanza kumuokoa jini Sui ambaye alikuwa mlezi wa Rufi na kisha angehamia kwenda miliki ya Xia kwa ajili ya kumuokoa Rufi.
Roma alijua kama atachokoza maveterani wa huko itamfanya kuwa na hatari na atashindwa kuwaokoa Rufi na Sui lakini vilevile na yeye angekuwa hatarini.
Hatimae waliweza kufika katika koo ya kwanza na kulingana na maelezo yao koo hio ndio ndogo kati ya koo kumi na nne ambazo zipo chini ya miliki ya Kekexil.
Ijapokuwa walikuwa ni koo tanzu ya miliki ya Kekexil lakini walikuwa wakifanana sana na kilichomfanya Roma kuzima shauku yake ni kwamba kati ya majinni ambao aliona kulikuwa na watu weusi, lakini kilichompa shida ni kwamba alishindwa kutofautisha yupi ni binadamu wa kawaida mwenye nguvu za kijini na yupi alikuwa ni jini kamili kwani kwa maelezo ya Feilo ni kwamba asilimia kubwa ya majini ambao wapo ndani ya miliki hio wametokea Hongmeng na binadamu wa kawaida waliojigeuza kuwa majini.
Unatakiwa kukumbuka Hongmeng ndio chanzo cha uwepo wa binadamu katika ulimwengu wa kijini kutokana na kwamba ndio wasimamizi wakuu wa mkataba kati ya majini na miungu na vilevile ndio majini ambao wanajihusisha ana kwa ana na ulimwengu wa kawaida kupitia China, majini wengine hawana kabisa habari na binadamu au ulimwengu wa kawaida.
Jambo pekee ambalo Roma aliona ni kwamba asilimia kubwa ya watu waliokuwepo ndani ya ulimwengu huo ni wa bara la Asia , waarabu walikuwa wachache sana na sura nyingi ambazo aliona ni wajapani , wachina na Wathailland.
Kwa namna moja ama nyingine Roma aliona labda kuna muunganniko mkubwa wa nguvu za kijini na wasalia Budhha ndio maana.
Unachopaswa kujua kuna muunganiko mkubwa kati ya Buddha na majini kuliko dini yoyote ile na ukitaka kuthibitisha hili angalia namna dini hio ilivyoanza haikuletwa na mitume kama ilivyo kwa ukristo na Uislamu.
Ijapokuwa watu wa ngozi nyeusi walikuwepo lakini walikuwa ni wa kuhesabu sana jambo alingine ambalo lilimshangaza ni kwamba majini wengine ilikuwa ngumu kuwajumuisha katika makundi kulingana na jamii za dunia , kwa mfano wengine hawakuonyesha kuwa na sura ambazo zinafanana na kabila lolore au jamii yoyote katika dunia ya kawaida ,yaani sura zao zilikuwa za kipekee lakini kitu kimoja tu ni kwamba wote walaikuwa weupe ambao wana nywele ndefu sana ambazo wamezifunga kwenda mgongoni.
Kingine pia hakukuwa na mabadiliko ya kimiundombinu kama ulivyo dunniani , asilimia kubwa ya maeneo yote yalikuwa yametawaliwa na miti na bustani za maua ya kuvutia mno ambayo huwezi kukuta duniani.
Koo jumla zote zilikuwa ni kumi na nne na katika kila koo walilala siku moja hivyo mpaka wanakuja kufikia siku ya kumi na nne walikuwa washatembelea koo zote na ilikuwa imebakia koo moja tu.
Katika siku hizo Roma alijifunza vitu vingi sana na kilichomshangaza licha ya kwamba majini walikuwa na tamaduni zinazofanana lakini kila koo ilikuwa na tamaduni za kipekee mno.
Familia ya mwisho kabisa kutembelea ilikuwa ni familia ya pili kwa ukubwa na hio familia ilikuwa ni koo moja na familia ya Mohena , familia hio ndio ambayo baba yake Rufi ndio alikuwa akiish.
Jambo hilo lilimshangaza Roma kwani mwanzoni alijua baba yake Rufi alikuwa akiishi makao makuu ya miliki lakini iligeuka Rufi alikuwa akiishi upande mwingine kabisa nje ya makao makuu na kule makao maku alikuwa akishi Mohi na familia yake.
Yaani Mohena baba yake Rufi alikuwa na familia yake mbali na ndugu zake na familia yake ilikuwa kubwa na ya pili ukichana na ya Mohi kaka yake.
Roma sasa kwasababu hakuwahi kumuona baba yake Rufi alijikuta akijawa na shauku ya kuona ni aina gani ya jinni ambaye alimchezea Bi Wema hisia zake na kisha kutoroka na binti yake.
Kila familia ambayo walikuwa wakifika walikuwa wakisubiriwa nje na mara baada ya kutua sasa palepale aliweza kumuona mwanaume ambaye alikuwa amemchanganya Bi Wema kimapenzi , alikuwa ni mwanaume mwembaba aliekuwa amevalia joho la rangi ya bluu alikuwa na sura mabayo ni ngumu kusema ni mchina au mwarabu yaani alikuwa mchanganyiko.
Kjwa muonekano wake ni ngumu kabisa kusema labda ni jini alikuwa wa tofauti kabisa na hapa sasa Roma aliamini kwanini Bi Wema alikubali kirahisi, bwana huyo alionekana mpole sana kimuonekano lakini upole wake ulionekana kuficha mengi.
Unachopaswa kuelewa pia majini hawafanani sura kama vile binadamu wanavyonana kutokana na kuwa ndugu , hio ni kutokana sura zao hazitokani na kijenetiki bali wenyewe wanazipata baada ya kufika kiwango flani cha nguvu za kijini mara baada ya kuzaliwa na ukishapata mwili basi huwezi kupata mwili tena na huo ndio unazeeka nao mpaka kufa.
Wanaorithi sura sasa ni wale ambao wamezaliwa na nusu jini na nusu binadamu kama ilivyo kwa Rufi na XiaoXiao,.
Roma aliona pengine ndio maana urembo wa Rufi ulikuwa wa kipekee hasa kwenye ngozi yake , ilionekana baba yake alikuwa mtanashati mno.
Majini hawakuwa kama miungu ambao wao hutumia uungu wao kuhama kutoka kwa mwili mmoja kwenda mwingine mara baada ya wanaotumia kuzeeka.
Kiitu kimoja ambacho kilimfanya kuona baba yake Rufi hakuwa wa kawaida ni kutokana na levo yake , kwa haraka haraka alikuwa katika levo ya juu mno , ijapokuwa hakuwa ameficha uwezo wake lakini Roma alijua alishaipita dhiki na sasa alikuwa levo ya juu zaidi kiasi cha kulingana na yeye , utofauti tu ni kwamba mbinu ya Roma na majini hao ilikuwa ikitofautiana hivyo ndio maana alikuwa na faida kubwa lakini baba yake Rufi alikuwa juu zaidi kumkaribia kaka yake.
Roma hapo alichokuwa akitega ni kujua tu kama mzee huyo angemzungumzia Rufi hata kidogo lakini habari ambazo zilikuwa zikiongelewa hapo ni za majigambo tu kuringishiana uwezo mpya ambao kila mmoja amepata , stori ambazo Roma kwake hakuwa akipendezwa nazo hata kwani aliona walikuwa wakipoteza muda na yeye alikuwa na haraka ya kumaliza misheni yake na kurudi kwa familia yake.
Waliendelea kubadili stori huku wakinywa kinywaji flani kama dawa lakini wao waliita mvinyo , katika safari hio Roma alipata uzoefu , kwa mfano kuna majini ambao alikutana nao katika familia zingine hawatumii kabisa pombe wala mvinyo na walipewa aina ya kinywaji ambacho kilikuwa kichungu mno lakini wao walikifurahia.
Roma alifuatisha maongezi yao kwa muda mrefu na alikuwa wakiongelea zaidi kuhusu mashindano ya kuingia kwenye jicho la Anga huku wakienda mbali kupeana tahadhari ya namna ya awamu hio kushinda katika mashindano hayo na kutowaruhusu koo zingine kuwashinda.
Kilichomvutia Roma ni kwamba aliweza kusikia katika koo ambazo zingeshiriki katika mashindano hayo hata Panasi wapo na alichokuja kujua ni kwamba Hongmeng ni jamii ambayo haikuwa ikiogopeka kabisa , jamii ambayo wengi wanaiogopa n Panasi halafu inakuja ya Xia na ndio inafuatia ya Kekexil hivo ndio alijifunza Roma na Hongmeng ndio wa mwisho kabisa.
“Mohena … nimesikia miliki ya Xia wamefannikiwa kumrudisha Rufi mara baada ya kumkamata?, je ni kweli?”Aliuliza jini mkuu namba mbili, huyu ni kaka yake jini mkuu namba moja
Sasa mazungumzo ambayo Roma alikuwa akitaka kuyasikia yalikuwa ndio hayo na alitega sikio vizuri apate kusikia.
SEHEMU YA 706.
Wote familia nzima ilimwangalia Mohena jibu lake akiwemo baba yake Zilha ambaye alinyanyua kikombe cha mvinyo na kunywa kidogo.
“Ni taarifa mpya ambayo mimi pia nimeipata , sijajua ni kwa namna gani wameweza kumpata huko duniani lakini Mkuu wa miliki Kiku alimtuma Mzee Lao na Lahani kwenda kumkamata”
“Hii ni bahari nzuri , miliki hio imekuwa na kinyongo na sisi kwa muda mrefu na kuona ndio tulimtorosha , wapo mpaka watu wetu walipigana katika safu za milima ya barafu kwa ajili ya swala hili , hii koo tokea muda mrefu inaona labda tulifanya njama kwa kufanya nao dili feki”
“Mjomba sikuwahi kutegemea huyu mwanamke angesababishia miliki yetu matatizo namna ile , kaka niseme kwamba huku mfunza vizuri binti yako , ijapokuwa alizaliwa katika ulimwengu wa kawaida lakini bado ana damu ya kijini ndani yake ya familia yetu , kama watoto wetu wangekuwa kama Rufi sidhani kungekuwa na amani”
“Kaka upo sahihi lakini kwasasa sio mwanafamilia wetu tena , na anabahati sijakutana nae ningempa adhabu kali sana”
“Alitusababishia hasara bila sababu na kutogombanisha na Xia , hivi unajua kipindi kile baba alivyokuwa na hasira , kama nisingekusaidia ungefungwa katika Jumba jeupe wewe”Aliongea Mohi.
Waliendelea kubishana wao kwa wao wakimuongelea vibaya Rufi , hakuna ambaye alionyesha kumjali kabisa hata baba yake alionekana hana chembe ya mapenzi kwa Rufi kabisa na haikueleweka kwanini hakumuacha duniani na Bi Wema kuendelea kuelelewa kama hampendi.
Roma alikasirishwa sana na maneno yao na alitamani kuua mmoja baada ya mwingine lakini alijiuzuia kwani walikuwa wengi ambao wapo levo za juu za kuipita dhiki lakini pia alikuwa na mpango wa kumuokoa Sui kabla ya kushitukiwa ni Zilha feki.
Moheni baba yake Rufi alikuwa na mtoto mkubwa tu wa kiume na ndio anafuatia Manyani ambaye anaishi katika makao makuu ya miliki ndio anakuja sasa Rufi ambaye ndio wa mwisho.
Baada ya kuongea kwa muda hatimae topiki nyingine iliibuka ambayo ilikuja kumfanya Roma na mtoto mkubwa wa baba yake Rufi kupigana ili kuonyeshana uwezo.
Lakini baba yake Zilha alikataa kutokana na kwamba Subiani alikuwa levo ya juu kuliko Zilha na aliona pengine mdogo wake anataka Subiani kupambana na Zilha ili kumuua na kisha aseme ni bahati mbaya na hapo ndio amfanye mtoto wake kuwa mrithi.
Mabishano yaliibuka kati yao na kusema kwamba mashindano ambayo yanafanyika sio ya kuuana bali ni kuonyeshana ujuzi wa kutumia siraha na mwishowe baada ya Roma kuona mtafaruku hio alitoka mbele ya baba yake Zilha na kumwambia atapambana.
Roma aliamini angejifanyisha tu kupigana bila ya kushinda na kama Subiani angekuwa na hila juu yake basi angetumia mbinu yoyote ile kuhakikisha anamkwepa.
Subiani alifurahi Zilha kujitokeza mwenyewe kwa ajili ya kupambana nae , alitaka kuchukua naasi hio kuonyesha wazee wa ukoo ni namna gani Zilha alikuwa hafai kuwa mrithi na yeye ndio anafaa kwani ni mwenye juhudi kwenye ukoo.
Mohi alikuwa na wasiwasi kweli kuona mapambano hayo, upande wa Roma licha ya kwamba hakuwa akimuogopa Subiani lakini alikuwa na wasiwasi kwamba anaweza kuzidiwa na kuonyesha uwezo wake na mwishowe kugundulika na alijua kama atagunulika ndani ya majini hao saba ambao wana uwezo wa juu ingekuwa kasheshe kwenye kudili nao hivyo alipanga kuwa makini.
Bahati ilikuwa upande wa Roma jini Subiani hakuonekana kuwa na hila yoyote wala njama zidi ya Roma na alipambana kama alivyoahidi kwamba asingetumia uwezo wake wa juu kupambana na Zilha na mwisho wa siku Roma alitumia nafasi hio kuonyesha mbinu mpya za kutumia siraha mbele ya baba yake Zilha.
Alimua kumfanya jini huyo kuwa na furaha mwisho mwisho zidi ya mtoto wake kabla hajajua kwamba tayari ashakufa muda mrefu.
Mpaka mwisho wa mapambano Roma alikuwa ameonyesha uwezo wa juu zaidi katika kutumia siraha , ijapokuwa mshindi alikuwa ni Subianni lakini Roma alifanya kitu kikubwa zaidi katika kupangua mapigo mbalimbali ya Subiani lakini vilevile katika kubuni mbinu za kushambulia.
Roma alitumia uwezo wake aliojifunza katika Temple za China kum’chalenge; Subianni na mwisho wa siku mpaka pambano linaisha Zilha alionekana kusifiwa sana na jambo hilo lilimfanya Mohena baba yake Rufi kutokuwa na furaha kwani mpango ulikuwa ni kumdhalilisha Zilha mbele ya wazee wa ukoo ili kumpa mtoto wake nafasi ya kuchaguliwa kama mkuu namba nne wa ukoo na kuanza maandalizi ya kushindana katika pambano la kuingia katika jicho la Anga.
Baada ya maongezi ya kifamilia kuisha hatimae Roma na wazee wote walianza safari ya kurudi makao makuu ya Kekexil.
Baada ya kufika Roma ambaye alikuwa ni jini Zilha aliitwa ma jini mkuu namba tatu Mohi katika ukumbi kwa ajili ya maongezi.
“Zilha mimi kama baba yako sijui ni lini au kwa namna gani umeweza kujifunza zile mbinu lakini nikuambie nimefurahi sana kuona una maendeleo mazuri , lakini hata hivyo spidi yako bado ni ndogo , tafadhari jitahidi kufika katika mwishoni mwa levo ya moto wa njano ili uweze kuwakilisha miliki katika mashindano ya kuingia kwenye jicho la anga”
Roma mara baada ya kusikia kauli hio alijiambia vyovyote vile anachopanga hapo ni kundoka mapema sana kabla ya mashindano hayo , lakini kwasababu alikuwa akimwigizia Zilha alitingisha kichwa kwa utii.
“Mjomba wako yule ni mtu wa njama sana anadhani hatujui ana mipango nyuma ya pazia na yule kizee … ni bahat nzuri babu yako yupo upande wetu”Aliongea akimaanisha mkuu namba mbili wa miliki ya Kekexil kuwa na mipango na Mohena mjomba wake jini Zilha.
“Baba kuna kitu wamefanya?”Aliuliza Roma akijifanyisha kushangaa.
“Mwanzoni nilidhani unachojua ni kucheza na wanawake , lakini unaonekana sio mjjinga na angalau umeanza kufikiria ki utu uzima , hivyo sioni mbaya kukuambia , ukweli ni kwamba mjomba wako Moheni ana biashara za siri na mjomba wako mkuu namba mbili kupitia koo ya majini roho kutokea Kaskazini kwa kuwatuma binadamu kama sehemu ya masharti ya kuwapa utajiri ili kukusanya mimea na damu ya kafara ili kutengenza vidonge, babu yako Mkuu namba moja ameamua kukaa kimya ili kuepusha mgogoro , hatujui hii mimea binadamu wamepata vipi lakini si umeona familia yao ilivyo na vijana ambao wapo levo za juu wanatumia vidonge vyenye mchanganyiko wa damu na mimea kutoka kwa majini Roho”
Roma hakujua hata majini Roho waliokuwa wakizungumziwa ni kutokea wapi lakini kwa haraka haraka alijua Zilha atakuwa anajua hivyo hakutaka kuuliza lakini kwa namna moja aliona mkuu namba moja jini Menui alikuwa na uvumilivu wa kutosha , maana mtoto wake na mdogo wake walikuwa wakimsaliti kwa kukiuka sheria.
“Baba , hiii si inachangia uwezo wao , vipi kama huko mbeleni wakitushambulia na kutaka kututoa katika nafasi zetu”
“Kipi cha kuogopa sasa, haijalishi wanajikusanyia nguvu vipi lakini babu yako ana nguvu kuliko mkuu namba mbili”
Mkuu namba mbili ni mdogo wake jini Menui ambaye ndio mkuu wa miliki yote ya Kekexili hivyo kwa upande wa Zilha ni babu yake upande wa wajomba.
Moheni ambaye ni baba yake Yezi yeye ni mkuu namba nne , ijapokuwa anao uwezo mkubwa kuliko kaka yake lakini bado anabakia katika nafasi ya nne kutokana na kwamba alikuwa ni mdogo , sasa alikuwa akipanga njama za kumfanya mtoto wake jini Subiani kurithi nafasi ya juu katika miliki ya Kekexil.
Sasa katika safari hio Roma alijua kwamba Menui mkuu namba moja , mdogo wake mkuu namba mbili , Ajuza mlinzi wa geti na Master Shagoni kutoka familia ya Lilsi ni sehemu ya Master wakuu wa miliki ya Kekexil , Roma alikuwa amekariri kwani alijua chochogte ambacho kitatokea lazima awe na taarifa sahihi.
Sasa ilionekana Mkuu namba mbili anamuunga mkono baba yake Rufi, lakini jambo ambalo lilimshangaza Roma ni kwamba jini Lilsi upande wao wana Master ambae ni Shagoni sasa Roma alijiuliza kwasababu Lilsi ni mke wa Moheni yaani mama yake wa kambo wa Rufi kwanini asimsapoti mume wake na kumsapoti Shemeji yake.
Kitu kingine amabcho alijifunza na kushangaa ni kwamba huyo jini Lilsi katika familia yao ndio anahesabika jini mkuu mwanamke namba mbili ambao kicheo kwa lugha yao ni Lufiali , sasa Roma aalijiuliza kama Lilsi sio mwanamke namba mbili je mwanamke namba moja ni nani na kuna siri gani inaendelea.
Baada ya Roma kufikiria sana alijikuta akiona hio miliki ni rahisi kuangushwa kwani ina migogoro ya ndani mno tena mikubwa zaidi , kwa mfano Manyani badala ya kumsapoti kaka yake Subiani yeye anamsapoti Zilha kwasababu ni mpenzi wake.
Roma mara baada ya kumaliza kuongea na baba yake Zilha alienda moja kwa moja mpaka kwa Zomu na Zato kuwasalimia.
Sio kwamba alitaka kuwaaga hapana , alijua kwasababu alishapotea kama msingi wa makubaliano mwanzo ya kupata vidonge basi wasingepewa tena.
Hivyo aliona atumie sura ya Zilha kuwapatia vidonge vyake ambavyo ametegneneza yeye mwenyewe kama shukrani ya kuwa rafiki yao.
Kwa kipindi cha zaidi ya siku kumi na tano Zomu na Zato pamoja na Feilo walimsaka sana Xiao Cheni bila mafanikio lakini walishindwa kuelewa inakuwaje binadamu kupotea katika ulimwengu wa kijni ghafla tu.
Wakati huo Zomu na Feilo tayari walishakuwa marafiki mara baada ya kukutanishwa na Roma siku aliomuua Zilha hivyo Roma aliwakuta wote watatu wakiwa pamoja.
Mara baada ya kumuona ni Zilha anaewasogelea wote walisimama kiheshima na kumpigia saluti huku wakionyesa wasiwasi.
Roma hakuongea ujinga tena kwani alikuwa ni Zilha kwa wakati huo hivyo alichokifanya aliandaa vidonge set mbili na kila set aliweza kimoja cha daraja la juu na vitatu vya daraja la kati na kumi na mbili vya daraja la chini na kisha akawapatia kama zawadi yake ya kuagana nao.
Feilo na Zomu waliogopa sana mara baada ya kupokea vidonge hivyo kutoka kwa Roma kwani walijua wanapokea kutoka kwa Zilha.
“Nimewapatia hivi vidonge bila ya baba yangu na babu kujua kwasababu nimeona jitihada zenu hakikisheni mnafanya siri kwani ikigundulika mna hivi vidonge basi mtakufa”Aliongea Roma kwa sauti ya Zilha.
Wote waliguswa na ukarimu wake kwani walijua vidonge hivyo sio tu kwamba vitasaidia familia yao lakini pia wao wenyewe vinawatosheleza katika mafunzo.
Wakati Roma anataka kuondoka Feilo alichukulia hio kama fursa ya kutaka kumuuliza Zilha kuhusu wapi Xiao Cheni alipo.
“Master , unajua ni wapi Xiao cheni alipo yaani kapotea hivi tu ndani ya wiki mbili zilizopita , tuna wasiwasi juu yake”
Aliongea kwa wasiwasi na kumfanya Roma kuwa na hatia isitoshe ilikuwa ni ngumu kwa majini kusubiri kwa muda mrefu juu ya rafiki yao aliepotea
“Najuaje jambo dogo kama hilo , pengine ameenda kujificha mahali anafanya mafunzo , vipi mnadhani naweza kumfatilia mtu kama yule mimi , jaribuni kudili na mambo yenu msije kupoteza nguvu zangu za kuwapa vidonge”
“Ndio Master , tutakuwa mtiifu kwako milele na miliki yote ya Kekexil”
Roma hakujali zaidi na palepale safari yake ni kuelekea katika Jumba jeupe kuanza misheni namba moja ya kumuokoa Jini Sui.
Mara baadca ya kufika aliweza kumkuta yule Ajuza bado yupo pale nje akilinda geti akiwa vilevile na hakumshuku kwa chochote na alimruhusu kupita.
Roma alijikuta akihema kwa ahueni mara baada ya kuingia kwenye jengo hilo , na alishukuru kwa kuwa na muonekano wa Zilha na sasa anaweza kuingia popote , mwanzoni alikuwa na hofu pengine Zilha alimdanganya baadhi ya maelezo.
Kwasababu alikuwa akienda floo za juu hakutumia njia ya kawaida kwenda juu , isitoshe kwa maelezo ya Feilo floor za juu hupitii kwa ngazi bali unapaa kwa nje na kisha unavunja formation ya safu ya mwanga wa kijini na kuingia ndani.
Hivyo Roma mara baada ya kufikia ile Formation ya kijini alitumia maelekezo yaleyale aliopewa na Zilha na kuivunja vizuri tu na ikaondoka na akaingia ndani bila ya kushitukiwa.
Roma alitamani kupitia katika floor zingine ili kujua nini kipo huko lakini kwasababu kulikuwa na walinzi hivyo aliona hatua ya kwanza ni kumuokoa jini Sui kwanza.
Baada ya kuingia ndani ya floor hio palepale aliweza kutembea katika kordo na hatimae kwa juu yake aliweza kuona gereza.
Hakupinga mjenzi wa jengo hilo hakika alikuwa amefanya kazi ya kueleweka , mpaka Roma kuhisi pengine hata mapiramidi kule Misri ndio walihusika, muundo wake ulikuwa ni mgumu sana kuona katika mazingira ya dunia , kitu kingine ambacho kilimfanya kushangazwa na muundo ni kwamba mawe yaliojengea yalionekan akuwa mazito mno.
Floor za tatu zote ambazo zilikuwa zikilindwa na safu ya formation ya nguvu za kijini zilikuwa ni gereza na hio ndio ilifanya wafungwa kushindwa kabisa kutoka katika jengo hilo kwani ili uwezo kutoroka lazima kwanza uvunje hio safu.
Ni floor ya mia na tatu kwenda juu na ilikuwa ni eneo ambalo lina ubaridi wa aina yake , ilikuwa ni barafu tupu na kama kukiwekwa kipimo pengine ni zaidi ya nyuzi hasi hamsini.
Ni kwasababu walikuwa majini ndio maana hawakufariki kirahisi lakini binadamu hapo hakai hata sekunde atakuwa amekauka na kugeuka barafu.
Kila gereza katika floor lilijengwa na vyuma vizito mno ambavyo vimeungannishwa na nguvu za kichawi, jini mwenye levo ya kupita Dhiki hapo hawezi kupita kwa namna yoyote.
Roma alitumia nguvu ya kijini kuanza kutafuta sura ya jini mwanamke ndani ya hilo eneo na ndani ya sekunde chache tu aliweza kumuona na alipotea aliposimama na kwenda kuibukia nje ya selo yake ya gereza la barafu.
“Sui!!!”Aliita Roma huku akimwangalia mwanamke ambaye anatetemeka kwenye kona ya selo , akiwa na nywele ambazo zimechanguka na nguo ambazo hazitamaniki alikuwa akitia huruma mno.
Baada ya kusikia sauti ya kuitwa mwanamke yule jinni ambaye alikuwa ameinamisha kichwa chake kwenye mapaja aliinua kichwa chake na kuonyesha uso wake , alikuwa ni mrembo mno na kwa haraka haraka Roma aliona akipata matunzo anaweza kumfikia Aoiline wa ulimwengu wa majini pepo.
Alionyesha uso uliojaa chuki na alimpiga jicho kali Roma na kisha alishusha macho yake chini vilevile.
Roma alishangaa lakini palepale alikumbuka alikuwa na sura ya adui yake hivyo
alijikuta akipatwa na ahueni.
Kwa muonekano wake ilionekana Zilha amefanya vitu vibaya sana kwake , pengine hata nguo zake zilichanika kutokana na kulazimishwa kubakwa.
“Sui mimi sio Zilha , angalia …”Aliongea Roma na palepale aliondoa athari ya Dhana ya jani la Upofu na kurudisha sauti yake vizuri na sasa sura yake ya Kiafrika ilionekana.
Jini Sui palepale alimwangalia Roma kwa macho ya mshangao mno akiwa na hali ya kuchanyikiwa.
“ Wewe.. wewe ni nani!!?”Aliongea kwa tabu na kumfanya Roma kuangalia kulia na kushoto na kuona hakuna jini lolote linalomwangalia.
“Mimi ni binadamu , jina langu ni Roma Ramoni na Rufi ni mpenzi wangu , najua wewe ni mlezi wake na ndio ulimsaidia kutoroka katika ulimwengu huu wa majini , ni wakati wa mimi kukuokoa na wewe pia ndio maana nipo hapa”Aliongea Roma na palepale Sui alifutika alipokuwa amechuchumaa na kwenda kujipigiza kwenye nondo kwa hamaki na kilihoonekana ni cheche za kugusana kwa nguvu za kijini na zile nondo.
SEHEMU YA 707.
Sui alishituka kweli aliposikia jina la Rufi , ni kama vile alikuwa akisubiria kusikia jina hilo kwa muda mrefu ndio maana alipaniki na kwenda kujigonga kwenye nondo ya gereza katika selo yake lakini hakuumia maana ni jini.
“Rufi! Unamaanisha Miss Rufi Moheni, anaendeleaje , yupo wapi sasa hivi , wewe ndio boyfriend wake….!!!?”Aliuliza mfululizo huku akigonga gonga nondo kama vile anataka kubomoa selo yake.
Roma aliguswa na matendo yake katika wakati kama huo huyo mwanamke alichokuwa akijali ni Rufi wakati baba yake mzazi anamuombea kifo.
“Tulia kidogo , nitakuambia kila kitu”Aliongea Roma akijitahidi kumtuliza na palepale alimpa ishara ya kurudi nyuma na akaita moto wa rangi ya bluu na palepale sehemu ya komeo ilianza kuyeyuka taratibu kama vile ni plasiti ilioshika moto.
“Moto wa bluu!!! , inawezakanaje !!!, ni mbinu gani ya mafunzo ya kijini unatumia , kwanini umeweza kutengeneza moto wa bluu?”
Kama jini ambaye amekulia katika mazingira ya kujifunza kupanda levo kila kitu kwake kilikuwa mshangao , alikuwa kwenye levo ya nafsi na alikuwa na uelewa na moto wa bluu.
Ukweli ni kwamba moto wa bluu majini wengi waliishia kuuona katika vitabu tu na hawana uelewa namna ya kuutengeneza na ni ndoto ya kila jini.
Roma aliishia kutoa kicheko , haikuwa mara ya kwanza kuona Jinni akishangazwa na moto wake wa bluu.
Roma mara baada ya kuingia ndani ya gereza hilo aliyeyua barafu lote kwa kutumia moto wa njano na palepale selo ilipata joto mpaka alipomuona Sui amerudi katika hali yake ya kawaida ndio alianza kumwelezea kila kitu namna alivyokutana na Rufi mpaka akaja kutekwa tena katika ulimwengu wa kijini na yeye ndio yupo hapo kwa ajili ya kumuokoa,
Sui mara baada ya kusikia Rufi yupo mikononi mwa familia ya Xia alijikuta akikunja ndita kwa wasiwasi.
“Mimi ndio napaswa kuwajibika katika hili , kama utanilaumu kwa kilichotokea siwezi kujitetea lakini nakuhakikisha nitamuokoa”
“Kwasababu umekuja huku ulimwengu wa majini wewe mwenyewe inaonyesha Rufi hakufanya makosa kukuchagua , wewe ni mwanaume tegemezi , ninaweza kuwa jini kijakazi katika miliki ya Kekexil lakini mimi sio mjinga , ninashukuru kwa wewe kuja kuniokoa na siwezi kukulaumua isitoshe kuna majini wenye uwezo mkubwa ndani ya miliki ya Xia ukijumlisha hao wazee ambao hawajawahi kuonekana kwa macho, licha ya kuzingatia hayo yote umehatarisha maisha yako na kuja kumukoa , nimeguswa , Roma.. kama hutojali naomba nikuite mr Roma..”Aliongea na Roma alitingisha kihcwa.
“Mr Roma kwasababu Zilha amekwisha kufa siwezi kuteseka tena zaidi ya kupambana na baridi , kama utaniokoa hapa nitakuongezea mzigo , vipi kama wakikushuku na mwishowe wakatuzuia , itakuwa ni usumbufu tu”
“Hutakiwi kufikiria hivyo , kama siwezi kukuokoa wewe nnitawezaje kumuokoa Rufi”
“Lakini ni hatari mno kuliko unavyofikiria , Zilha alinifungia hapa mara baada ya kupata ruhusa kutoka kwa babu yake na huwezi kunitoa bila ruhusa ya babu yake , ukilazimisha lazima walinzi watatuzuia”
“Kwahio unamaanisha siwezi kukutoa hata kama mimi ni Zilha?”Aliuliza Roma.
“Hapana , miliki ya majini sehemu zote wanatiii sheria mno hususani zile kubwa isingekuwa hivyo huu ulimwengu usingekuwepo leo hii”
Roma alijikuta akikunja ndita na kuona kuna hatari mbele yake , alijiambia bado tu hajakutana na Mzee wa ukoo huo wa Kekexil atawezaje kumtafuta na kumuomba ruhusa bila ya kumshitukia.
“Mr Roma usiwe na wasiwasi , nimefurahi umekuja mpaka hapa kuniona lakini kwasasa kipaumbele chako kiwe kumuokoa Rufi , tokea yule mshenzi Zilha alivyonileta hapa sijawahi kuwaza kuondoka , kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa kuliko wa kwangu aliishia kunidhalilisha na kwasasa mimi ni mchafu … na kama sio kuwa na wasiwasi juu ya Rufi ningeshajiua muda mrefu , sasa nishajua Rufi yupo hai nimefurahi sina hitajio lingine hata nikifa sas hivi , nimeisubiri kwa hamu hii siku asante kwa kuja kuniona”Aliongea kwa sauti ndogo.
Huyo jinni mwanamke alikuwa akitia huruma mno lakini kwa wakati mmoja maneno yake yalimgusa mno Roma , upendo wake kwa Rufi ulikuwa ni ule wa mzazi kabisa kama ilivyokuwa kwa Bi Wema,
Rufi alikuwa sahihi mtu pekee ambaye alimpenda kwenye ulimwengu huo wa kijini alikuwa ni Sui peke yake mlezi wake.
Sui alikuwa amepitia mateso makubwa sana kwa kuchezewa na Zilha , pengine kwake kifo ilikuwa afadhali kuliko kuishi.
Lakini Roma hakutaka kufikiria Sui alikuwa jini mchafu , kama ilivyo kwa wanawake wa kibinadamu ambao walikuwa wakijiuza , upande wa Sui yeye sio kama alichagua kufanyiwa hivyo , haikuwa hatima yake hivyo hakuwa mchafu na ilimfanya zaidi kumheshimu.
Baada ya kuwaza alijiambia kwa namna yoyote lazima amtoroshe kwenye ulimwengu huo wa kijini hata ni kuhatarisha misheni yake.
“Sui wewe ndio uliemtoa Rufi kwenye ulimwengu huu mara ya mwisho hivyo naamini utakuwa unaijua njia ya mkato ya haraka”
“Ndio , kama utapenda kujua nitakuambia kwa maelezo ya kutosheleza”
“Okey! Hili ni swali lingine , kama nitataka kuchukua mimea ya dawa katika floor za chini nikiwa na sura ya Zilha je hao wazee wanaotengeneza vidonge watanizuia?”Aliuliza Roma na alimfanya Sui kuduwaa.
“Hio mimea wanapewa hao wazee kwa ajili ya kutengeneza vidonge , kama unaitaka itakuwa ngumu labda kama unataka kuchukua kdiogo tu”
“Vipi kama nataka kuchukua yote?”Aliongea Roma huku macho yake yakiwa yamejaa ujanja ndani yake.
“Mr Roma unataka kuiba hio mimea? , lakini hao wazee wote angalau wote wapo juu ya levo ya kuipita dhiki katika moto wa njano , kuna kumi ambao wanalinda hili jengo kwa mwaka mzma na wote wapo juu ya levo ya kuipita dhiki katika Maji ya barafu”
Kuna levo tatu za maji , maji ya kawaida , maji ya barafu yaani kugeuza maji kuwa barafu na maji ya kiroho, unaweza kufikia vyote kwa wakati mmoja yaani unaweza kuwa na uwezo wa maji ya barafu ila ukawa huna uwezo wa moto wa rangi nyeupe na unaweza kupata ufunuo wa maji ya kiroho lakini ukakosa ufunuo wa moto wa bluu au mweupe.
Ukweli ni kwamba ukishaipita dhiki unakuwa na uwanja mpana na unaweza kubahatika kupata ufunuo wowote bila mpangilio.
Roma sasa ashakwisha kupita levo ya maji ya kiroho na sasa alikuwa katika ufunuo wa kuunganisha maji ya kiroho na moto wa kiroho na kutengeneza siraha ya kijini ya tufe la bluu.
“Mr Roma nakushauri uondoke hapa mapema , ni muhimu zaidi kumuokoa Rufi kuliko kuchukua hio mimea, isitoshe huwezi kutengenza vidonge”
“Nani kasema siwezi kutengeneza vidonge , ninaweza , ni kwamba tu sio staili yangu kuacha vitu vya thamani nyuma , sina mpango wa kurudi tena hapa nikishaondoka hivo nataka niwatie hasara ya kutosha”Aliongea Roma na kumfanya Sui kutoa macho na kupanua mdomo kwa mshangao akijiuliza au hajamsikia vizuri.
“Sui unaelewa hili jengo lilivyo , je nikipigana na hao majini wa levo ya juu ya dhiki yule mwanamke kule nje anaweza kuhisi?”
“Siwezi kuongea kwa uhakika kwasababu kuna safu ya formation ya mwanga wa kijini ambayo hutumika kama ulinzi , ile formation inazuia nguvu zote ndani ya jengo hili kutotoka nnje ili kuruhusu utengenezaji wa vidonge kuwa mzuri , nadhani majini ambao wapo nje ya hili jengo hawawezi kuhisia chochote labda uliharibu”
Roma alitingisha kichwa na kuridhika na jibu lake na palepale alifungua hifadhi yake ya anga kwa kutumia pete na kisha alianza kutoa nguo za kike na kumpatia Sui.
“Vaa hizi , ijapokuwa wewe ni mkubwa kwangu lakini sioni ni vizuri kuwa nusu uchi mbele yangu”Aliongea Roma na kumfanya Sui sasa kuelewa kumbe alikuwa uchi kwani manyonyo yalikuwa nje na mapaja yote.
Roma nguo hizo zilinunuliwa na Edna kipindi walipokuwa Korea na kwasababu Edna hakutaka kubeba begi walizitupia kwenye hifadhi ya pete na hawakukumbuka kuzitoa , kulikuwa na nguo nyingi sana lakini kwa bahati nzuri zimepata matumizi kwa wakati huo,
Sui alishikilia fasheni yenye katuni mbele yake pamoja na skeri fupi na aliona ni nguo za kushangaza , pengine ni kwasabu ni wa ulimwengu huo lakini hakufikirai sana.
Wakati anabadilisha Roma alimpa mgongo na baada ya kubadili alishindwa kumwangalia Roma usoni na kutoa kicheko cha aibu na Roma alijiambia kumbe majini ni kama bindamu tu.
Edna alikuwa mrefu kuliko Sui hivyo shati lilionyesha kitambi lakini hakuwa na muda wa kufikiria angalau kwa muda huo amejisitiri.
“Sui nnitakutorosha kwenye huu ulimwengu na kupeleka ulimwengu wa kawaida sehemu ninayoishi mimi, je upo tayari?”
“Mr Roma naweza kuishi ulimwegnu wa kawaida!!!”Aliuliza kwa mshangao.
“Ndio unaweza , ijapokuwa huyo mwanamke hapo nje ana nguvu kubwa ya kijini lakini hawezi kunizuia yeye peke yake”
Roma hakuwa akidanganya Ajuza mlinda geti alikuwa na levo ya juu sana , alikuwa juu ya levo ya kupita dhiki katika kudhibiti maji ya barafu.
“Basi nitakusikiliza kwa utakachokuwa unaniambia na kukifanya”Aliongea
“Huna haja ya kufanya chochote , wewe kaa nyuma yangu na tukishatoka kwenye hili jengo nitakushikilia ili tuweze kukimbia kwa spidi”
Baada ya kukubaliana Roma alijibadilisha na kuwa Zilha palepale na kisha akamchukua Sui na kuanza kushuka nae kuja chini
Baada ya kufika katika floor ya chini ambayo huhifadhia mimea Roma alichunguza na uwezo wake na aliweza kugundua kuna wazee wawili ambao wapo levo ya kutengeneza moto wa rangi nyekundu na mmoja akiwa na uwezo wa kutengeneza moto wa njano.
Walikuwa wakipangilia mimea kuligana na kanuni na ilionekana ndio ilikuwa imefika na walishangaa mara baada ya kumuona Zilha na Sui,
“Master mdogo , inafanya nini hapa?”Aliongea jini yule ambaye ana uwezo wa moto wa njano na wote kwa pamoja walimsogelea Roma kumpa heshima , hawakuelewa kama ni feki na Roma aliona hio ndio nafasi adhimu kwani palepale aliita chungu na kikatokea nyuma yao bila ya kutoa mkandamizo na ndani ya dakika chache kilianza kupanuka saizi ya kuweza kumeza wote wawili na walijikuta wote wakigeuka na Roma aliishia kutoa tabasamu la kishetani.
“Master,,, wewe.. Zilha!!”
Wote walijikuta wakipagawwa na palepale walianza kuvutwa kuelekea ndani ya kile chungu.
Roma palepale aliachia uwezo wake wa juu wa mapigo mzunguko tisini na tisa ya radi ambayo majini wenyewe wanaita Radi ya kitai na palepale aliunganisha na nguvu ya andiko la urejesho na kabla hata hawajapambana wote walitumbukia
“Nyam!! , Nyam!!’
Roma aliweza kuona kivuli cha mmyama wa maafa akitafuna kama vile Mamba mkubwa na ndani ya sekunde nguvu yao yote ilifyonzwa na chungu cha maafa na nguvu nyingine ilienda kwa Roma.
Ijapokuwa walikuwa levo ya kuipita dhiki lakini nguvu yao ilikuwa kidogo tu kwa Roma lakini haikuwa mbaya sana , Roma alikuwa amepitia mapigo tisini na tisa ya radi na hao wazee waliikuwa wamepitia awamu moja tu ya radi.
Roma mara baada ya kugeuka nyuma alimuona Sui alikuwa akitetemeka kwa hofu huku akiangalia lichungu linaloelea na kufuka moshi ambalo limemeza watu kwa mshituko mkubwa.
“Usiogope , hii ni Dhana yangu , kwanzia sasa nitafagia kila floor na kubeba kila kitu , wakija kushtuka hamna kitu”Baada ya kuongea palepale aliingia kazini na kuanza kukusanya mimea na kutupia kwenye shimo lake na hakusahau kutoa pete za wale wazee na kuangalia kama kuna chochote lakini Roma alikunja sura baada ya kuona kumbe walikuwa masikini tu maana hamna chochote.
Kwasababu yule Ajuza hajahisi chochote Roma alipumua kwa ahueni na kuelekea floor inayofuata.
Awamu hio alikumbana na jini ambalo lilikuwa bize kutengengeza vidonge na ilionekana halikutaka bughuza ndio maana limejitenga , lilikuwa kwenye levo ya kupita dhiki na alikuwa amewasha moto wa rangi nyekundu.
Kumbuka nikisema moto wa njano ni ule moto wa kawaida unaoona , moto wa bluu ni kama ule unaoona kwenye gesi na rangi nyingine , sasa moto wa rangi nyekundu ni aina ya moto wa kijini ambao unafanana na rangi ya volkano ile lava yake inayoruka.
Moto wa rangi ya njano wa kijini sio wa kawaida una uwezo wa kuyeyusha chuma cha kawaida, ki ufupi kila rangi ya moto sio ya kawaida kama moto unaonekana kwa macho ya kawaida ni moto wa kimaajabu lakini unafuata kanuni za rangi ya ‘flames’ za moto.
Roma mara baada ya kuona huyo mzee akiwa bize alitabasasmu kwa dharau maana mzee yupo bize kama vile anatengeneza vidonge vya maana kumbe daraja la kwanza , alichoshukuru Roma ni kwamba yupo peke yake hivyo kudili nae haikuwa tatizo.
Roma bila hata ya kuongea neno alipotea aliposimama na kutokezea mbele yake , alikuwa amempa mgongo hivyo hakuona ujio wa Roma na palepale alizalisha donge la maji ya kiroho na kumpiga nalo utosini na palepale mzee yule bila hata ya kushtuka alianza kuyeyuka kwa haraka sana , hakuweza hata kutamka neno.
Maji ya kiroho mara nyingi ni kama tindikali au Acid tena zaidi ya Acidi maana inayeyusha mpaka mifupa.
Sekunde chache tu yule jini mzee alikuwa ashayeyuka na kilichosalia ilikuwa ni nguvu yake ya kijini Roma aligeuza kichwa chake kuangalia roho ya mnyama iliokuwa ndani yake na mara baada ya kukutanisha na macho ya Roma ilijificha eti, lakini Roma aliruhusu chungu kile kiifyonza maana haikuwa na ubora mzuri.
Roma mara baada ya kumaliza aliangalia chungu ambacho kilikuwa kikitumiwa na lile jini kutengengezea vidonge , kilikua ni kidogo mno kuliko cha kwake.
Roma alipatwa na tamaa kutaka kubeba kile chungu lakini aliona tayari anacho tena cha kwake kikiwa na roho ya mnyama ambaye hafi hivyo palepale aliita moto ambao ulikuwa katika rangi ya Zambarau , huo moto ulitokana na yale mapigo ya radi na Roma alifanikisha kuutengeneza mara baada ya kuunganisha shoti za radi na moto wa bluu.
Kile chungu ilichukua dakika chache tu kilishayeyuka na kuacha ujiuji chini ambao ulianza kupeperushwa na upepo na hakukubakia na ushahidi wa aina yoyote.
Jini Sui aliekuwa akiangalia hayo yote alijiuliza Roma ni nani , yaani ameua jini wa levo ya maji ya barafu na pigo moja tu na kisha akayeyusha Cauldron ndani ya sekunde , aliishia kumwangalia Roma kwa hofu na uwezo wake angalau sasa ulimpa ile hali ya kujiamini kwamba anaweza kurotoka katika eneo hilo bila shida.
Roma alikitanguliza chungu awamu hio bila hata ya kufika katika floor na kilimeza kila kiumbe kilichokuta , majini wengi ambao wapo levo ya nafsi na mwanzoni mwa levo ya kuipita dhiki walimezwa.
Wengi wao hawakujua hata nani katuma chungu hicho kwani kiliwameza tu bila ya taarifa na Roma alifika kazi imeisha.
Roma mara baada ya kupiga chabo kuangalia hifadhi yake ilivyojaa mimea alijikuta mwili ukimsimka.
Ni hivyo tu alikosa kitu kama tunda la damu ya finiksi kutengengeza vidonge vya daraja la juu sana vya kihistoria.
Kilichomfurahisha Roma zaidi ni mara baada ya kupata Dhana kibao za daraja la kati na la chini , ijapokuwa zilikuwa za uwezo mdogo lakini alikumbuka ana warembo na akiwapa zingewasaidia sana.
Upande wa Sui aliishia kumeza mate mengi , wakati akimwangalia Roma akichagua Dhana hizo kama vile ni takataka.
Katika ulimwengu wa kijini ondoa madini , aondoa hela na utajiri wowote hivyo kwao ni material thing , kitu cha thamani kwa majini ni Dhana halafu inafuatia vidonge.
Kuna majini yana zaidi ya miaka mia mbili hayajawahi kugusa kabisa Dhana sembuse Sui ambaye alikuwa kijakazi tu, ndio maana alimwangalia Roma kwa mshangao.
Mpaka Roma anafika chini alimaliza majini yote kama hamsini hivi , yaani kama ni hasara ni hasara ya maana na hakuishia kuiba dhana tu alibeba mpaka vitabu, ijapokuwa vimejaa mbinu za kichawi lakini aliona kama watependa kujifunza basi asingewazuia.
Roma mara baada ya kufika sasa floor ya chini sasa akiwa amekwisha kuridhika kuwatia hasara Kekexil alimpa ishara Sui kusogea karibu yake wakati wakielekea getini.
Baada ya geti kufunguliwa Sui machozi yalimtoka , kwa miaka saba hatimae amevuta hewa ya oksijeni safi na kuona mazingira ya nje kwani lile gereza ilikuwa ni giza tupu,
“Simameni hapo hapo!!”
Sauti ya yule bibi ilisikika huku mkandamizo wa hewa ukiongezeka kwa kasi na ilikuwa ni kama vile milima inaporoka au wingu linashuka chini.
Ajuza ambaye alikuwa akilinda geti hilo kwa muda mrefu sana hatimae Roma aliweza kuisikia sauti yake na kufumbua macho na kumwangalia Roma kwa macho makali mno.
“Bibi namtoa huyu m*laya nje nina shughuli nae”Aliongea Roma akiigiza tabia ya Zilha.
“Sijapokea maagizo yoyote kutoka kwa Menui mkuu namba moja wa miliki , huwezi kumtoa mfungwa nje”Aliongea kwa sauti kali kweli ya kuumiza masikio kama vile sio mzee.
“Bibi huyu hawezi kukimbia maana nampeleka nyumbani , , naomba uniruhusu”
“Zilha Mohi, hebu niambie tarehe yako ya kuzaliwa na siku?”Aliongea yule kizee na kumfanya Roma kushangaa,
“Bibi unamaanisha nini kusema hivyo!?”Roma alijiuliza mbona maigizo yake yalikuwa vizuri tu kwanini amemshuku.
“Unaniuliza namaanisha nini? , ngoja nikuambie Zilha hajawahi kuongea bila heshima mbele yangu wala kuniomba , umetoa wapi uthubutu wa kuongea kijeuri mbele yangu tena unaenda mbali na kuomba wewe ni Zilha kweli!?”
Roma alitukana ndani kwa ndani ashajua ni wapi amebugi , kumbe yule mpuuzi alikuwa akimheshimu huyo Ajuza.
“Wewe ni nani?”Swali lilimtoka Ajuza huku mkandamizo wa nguvu ya kijini ukimtoka na palepale sasa Roma aliweza kujua ni levo gani , alikuwa levo ya maji ya kiroho na kwasababu alionekana kuwa mzee nguvu yake ya kijini ilikuwa ni ya kutisha mno.
Mkandamizo ule wa nguvu ya kiroho ulimfanya hata Sui kutema damu chini maana sio ya kawaida na Roma palepale alichia nguvu zake za kijini na kumlinda.
Unafikiri Roma atachoropoka hapo.
ITAENDELEA JUMAPILI.