Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

majini-watu majini-pepo majini majini majini maniji 😬 😬 😬 😬 😬 😬 😬 bikira ukahaba illuminant freemason VEXTO amina edna yezi doris rose lanlan visiwa vya wafu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣hongmeng kekexil panas wema recho . . . .benadetha ernest najma monica maimuna rufi lekcha aoiline desmond sharif kweka zhenzhei pluto Persephone Diego zero Omari Poseidon . . . .

NJOONI MMALIZIE MAJINA MAANA NI MENGIII . . . .

Hata hivyo, mwamba SINGANO ameupiga wa ukweliiii
 
Visiwa vya malidives,seventeen, jeremy, desmond,blandina,bibi wema,the don,mr wadudu,mfalume wuja,mr Kuo, rufi etc.
ila ep moja imenifanya niirudie zaidi ya mara tatu ile inayoelezea kumbe roma yuko mikononi mwa shirika fulani na ndo linamuongoza bila mwenyewe kujua, na kumbe kifo cha seventeen ni feki, na kumbe ili wajue wako huru wakaruhusu walipue maabala ya shirika aisee hii dunia ina mengi. sasa atakuwa wapi huyu seventeen au ndo edina mwenyewe au ndo yule dada aliyebaki ulimwengu gani sijui ule unaomeza watu kupitia mnala maana roma kafichwa vitu vingi hata master wake alijificha wakati anakutana nae mara kwa mara akiwa na lanlan.

Hii simulizi ni ndefu sana hii na ya kuvutia haichoshi hata kidogo.uzuri na mwandishi yuko vema anatupia mapande kadhaa raia tukimaliza tunabaki bila kiu hadi wakati mwingine.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 704.
Katika ulimwengu wa kijini wakati wa kufunguka kwa jicho la Anga wanaita ni kipindi cha mavuno makuu ,ni kipindi muhimu sana katika huo ulimwengu kama ilivyokuwa katika ulimwengu wa majini pepo kupambania kuingia katika mnara ili kupata mimea na hazina ndio ilivyokwa ulimwengu wa majini wa kawaida.
Ni hatari sana kuingia kwenye ulimwengu wa Jicho la Anga hivyo wanaoenda huko ni majini ambao wapo katika levo za juu sana ili kuweza kushindana na majini ambao washageuka na kuwa pepo(ghost).
Ndio majini wanakufa pia na wenyewe wanaamini roho za majini hukimbilia katika ulimwengu wa Jicho la Anga.
Sasa Roma mara baada ya kupata habari hio anajikuta akipatwa na hamu ya kwenda kujionea , aliwaza labda anaweza kupata siraha ya kimaajabu katika huo ulimwengu lakini kwa bahati mbaya njia ya kuingilia katika ulimwengu huo ipo chini ya miliki za kijini , lakini pia aliona hata kama akiingia inaweza kuwa shida kwake kurudi.
Yaani kwa kifupi ni kwamba mshindi wa kuingia huko akishapata nafasi koo zingine hulinda jicho hilo ili kuhakikisha hakuna anaevamia kinyemela na kuingia.
“Tukiachana na hayo , nini kimekuleta hapa Bro XiaoCheni?”Aliuliza Zomu na kumfanya Roma kusita kidogo kuongea , ni kama vile ni jambo la aibu.
“Kuna kitu ambacho nahitaji unisaidie lakini nahisi kama haitowezekana..”
“Ongea tu Braza , mimi kama rafiki yako lakini pia kama jini ambaye nimepokea ukarimu mwingi kutoka kwako , kwanini nikatae kukusaidia?”
Roma palepale alianza kumwambia kuhusu Feilo kukutana nae nyakati za usiku kwa ajili ya kujifunza pamoja .
“Feilo amesema uende kwenye makazi yake saa nne usiku kwa ajili ya kukusubiri hivyo…”
“Ah… kumbe ni jambo hilo , niliamwangalia Feilo namna alivyokuwa akitumia ngumi yake kukushambulia na ile ngurumo yake ya Simba vilinivutia mno ,nilikuwa nikitamani pia kukutana nae , hivyo nipo tayari usiku wa saa nne nitamtafuta”
“Asante sana Bro Zomu kwa msada wako , lakini natumaini hutoenda na Zato , Feilo ni muumini wa Kibuddha na hapendi wanawake wake kabisa”Aliongea Roma akicheza na maneno vizuri kabisa ili kukamilisha jambo lake.
“Usijali hata Zato mwenyewe hapendelei sana kuwa karibu na wanaume , hivyo nitamuacha, naamini kwa muda huo atakuwa amelala pia”Aliongea Zato huku akionyesha kidogo hali ya kusikitika akimuonea huruma dada yake kwa uvivu wa kujifunza.
Sasa Roma alikuwa tayari amekamilisha mpango wa kuhakikisha Zomu anakaa mbali na Zato nyakati za usiku , haikueleweka alikuwa akipanga nini lakini alikuwa akifanya kitu kilekile ambacho ameagizwa na Zilha.
Hivyo usiku Zomu angeenda katika eneo ambalo Feilo anajifunzia kwa ajili ya kushirikiana na kujaribu kupambana na huku nyuma Zato angekuwa peke yake.
Roma mara baada ya kuachana na Zomu hakutaka kuzembea na yeye alianza kujifunza mbinu za kutumia siraha za kijini kama vile mapanga n.k.
Njia rahisi pia ya kujifunza mbinu za anga ni kutumia kujifunza mapigano asilia kwa kutumia upanga au njia za kawaida , hivyo majini wengi walikuwa wakitumia mbinu hio hii ni kwasababu mtu au jini linapokuwa katika mafunzo ya kisiraha akili yake inapata umakini zaidi na zaidi lakini pia ina upa ubongo hali ya utulivu.
Hatimae ile saa ikawa imetimia , Roma makusudi kabisa alihakikisha hakuna majini ambao wapo karibu wenye uwezo wa juu zaidi ili kuhakikisha mpango wake unaenda sawia.
Baada ya kuona eneo lipo shwari palepale alitoka anapoishi na kwenda katika makazi wanayoishi Zato na Zomu wakati huo akiwa na uhakika Zomu tayari ashaondoka.
Kwa kutumia Dhana yake ya Jani la Upofu aliamini hakuna jini lolote ambalo lina uwezo wa juu kunasa kile anachokifanya kwa usahihi.
Roma mara baada ya kufika nyuma ya nyumba ya Zomu na Zato alijificha na kisha palepale aliruhusu nguvu za kijini kujifahamisha mazingira ya eneo hilo yalivyo.
Jini Zilha uwezo wake ulikuwa mdogo sana kuliko wa Roma hivyo hata kama akihisi msisimko wa nguvu za Roma asingeweza kugundua chochote.
Roma mara baada ya kuangalia aliona ni kama alivyotegemea Zato alikuwa yupo peke yake akiwa usingizini kama alivyosema Zomu.
Majini pia wenyewe wanalala na hio yote ni kutokana na kuwa na miili ya kibinadamu kabisa ambayo inatoa damu, lakini hata hivyo wanaweza kutokulala kwa muda mrefu sana bila ya kupata shida yoyote, wao kulala ni kama ibada.
Zilipita dakika tano tu wakati Roma akiwa amejibanza nyuma ya nyumba hatimae Zilha aliweza kufika ndani ya makazi hayo , alianza kukagua mazingira kwa wasiwasi kuhakiki kama hakuna kiumbe chochote kinachomuangalia na baada ya dakika moja hatimae alifungua mlango taratibu.
Roma palepale alifutika alipokuwa amejificha na ile anaibuka alikuwa nyuma ya Zilha.
Zilha alikuwa akimwangalia Zato aliekuwa amelala kwa macho ya uchu kweli , kiuno chake , manyonyo na sura yake ya kirembo ilimfanya kupagawa kabisa na udenda kumtoka.
Zilha alimpenda Zato kutokana na kuwa msichana ambaye amekaa ki’sassy zaidi na mkali mno hasa anapoangaliwa na mwanaume na hali hio ilimtia shauku angeonekana vipi mara baada ya kumwingizia bakora yake na ndio maana alitumia shida yao ya vidonge ili kuwabakisha ndani ya himaya yao ili kukamilisha shauku yake.
Alikuwa akimpangia mpango muda mrefu sana hata kabla ya Roma kuja ulimwengu wa kijini , ukweli ni kwamba ashafanya mipango ya aina hio hio mara nyingi na ikafanikiwa hivyo aliamini na kwa Zato anakwenda kufanikiwa.
Mara nyingi akishakamilisha mpango wake palepale kwasababu majini hao wa kike wanakuwaga na uwezo wa chini basi atawabembeleza kwa vidonge na tuvizawadi na kuwatishia kidogo na baada ya hapo watakuwa wanajileta wenyewe.
“Kama ungekuwa na akili usingefikiria njia za kihuni namna hii kucheza na hawa wanawake”Aliwaza Roma kwenye akili yake akiwa nyuma ya Zilha na palepale aliachia mkandamizo wa nguvu za kijini na kumsomba Zilha kimzobemzobe na kutoweka mbele ya makazi ya Zato na Zomu.
Zilha alijikuta akipiga Yowe mara baada ya kufanyiwa shambulio hilo la kushitukiza na jini mwenye nguvu zaidi yake.
Bahati nzuri ni kwamba walishafika kwenye msitu mbali na makazi ya majini hivyo sauti yake haikuweza kwenda mbali.
“Wewe … wewe ni nani?”Zilha jasho lilianza kumtoka huku akitetemeka kwa woga bara baada ya kudondoka chini.
Roma palepale aliondoa ule mkandamizo wa nguvu zake za kijini na kisha akaupamba uso wake na tabasamu bandia.
“Kwanzia sasa mimi ndio nitakuwa nauliza swali na wewe ndio unajibu”
Zilha alimeza mate mengi alishindwa kabisa kuona levo ya Roma lakini aliweza kuamini kwamba hakuwa katika levo ya Nafsi ,haikuwa kwake tu ambaye amedanganywa lakini majini wote walidanganywa na Xiao Cheni jini aliejifanyisha kuomba hifadhi.
Lakini katika hali kama hio hakutaka sana kufikiria Roma ni nani haswa na aliishia kutingisha kichwa kukubaliana na Roma.
“Vizuri”Roma alitabasamu huku akimwangalia jini Zilha kwa macho yaliojaa umakini.
“Una mdogo sijui binamu wako afahamikae kwa jina la Rufi ndio au sio?”
“Huyo M*lay umemjuaje ….!!?”Zilha alijikuta akishangaa huku akitamka tusi na kumfanya Roma kumwangalia kwa macho makali.
“Pumbavu zako, mwite tena hivyo uone kama sitokuua hapa hapa”
“Ndio namjua na sitomwita tena hivyo …. Rufi ni mtoto wa mjomba?”
“Je yupo hapa Kekexili?”
“Kwanini unaulizia kuhusu yeye kwanza?”Aliuliza Zilha kwa kuchanganyikiwa.
“Acha upumbavu , jibu swali langu”Aliongea huku akimchapa kibao na kumfanya Zilha kutoa mguno wa maumivu.
“Sijui mahali alipo lakini nina uhakika hayupo hapa Kekexil … alitorokea kwenda ulimwengu wa kawaida kuepuka ndoa na ni juzi tu familia yetu ilipokea taarifa kwamba wameweza kumpata huko duniani lakini sina uhakika kama walishaenda kumchukua kumrudisha au lah… Mjomba yeye amesema Rufi ni msaliti wa familia na miliki yote ya majini hivyo hana nia ya kumtambua kama binti yake tena, hivyo hata kama akirudi lazima atakuwa katika miliki ya Xia”
“Kama ni hivyo kwanini ulikuwa kwenye Jumbe jeupe leo hii , sio kwasababbu kuna majini ambao hufungiwa ndani ya jengo lile?”
“Ndio kuna wafungwa lakini sio Rufi , kuna majini ambao wapo kinyume na familia yetu ndani ya miliki na pia ambao wametusaliti ndio wamefungiwa”
“Sasa kama ni hivyo kwanini ulienda kuwatembelea?, Yaani unaona furaha kutembelea wasaliti , unaniona mimi mjinga?”Aliongea Roma kwa hasira na kumfanya Zilha kushindwa hata kumwangalia usoni.
“Ni kijakazi wetu afahamikae kwa jina la Sui ambaye alimsaidia Rufi kutoroka kipindi cha nyuma , familia yetu ilitaka kumuua mara baada ya tukio hilo ila nilimuona anatia sana huruma na nikamuomba babu yangu kumfunga gerezani”Aliongea.
Roma hapo hapo alikumbuka Rufi kumtaja jini ambaye alimsaidia kurorokea kwenye ulimwengu wa kawaida , inaonekana tokea kumtorosha Rufi alikuwa ni mfungwa ndani ya jumba hilo jeupe.
Kwa muonekano wa Zilha hata mjinga anaweza kujua nini ambacho anamfanyia Sui , ilionekana alikuwa akitumika kama chombo cha Zilha kupunguzia genye.
“Sio kwamba ulitaka kumuokoa bali ulikuwa ukipanga kumtumia kingono”
“Ndio nilimuokoa lakini niliona ni vyema pia nikijilipa kidogo kidogo”
Roma alijikuta akijizuia kutokumuua na mpaka hapo alikuwa tayari kumuokoa Sui vinginevyo kama habari hizo zingemfikiria Rufi basi angeteseka sana na mawazo maana alikuwa ni mlezi wake.
“Nimesikia kuna njia ya moja kwa moja ya siri kwa wanafamilia kuingia katika Jumba Jeupe , niambie njia hio ikoje?”
“Hapana , siwezi kusema , Jumba Jeupe ndio fahari ya miliki yetu na lipo chini ya familia , kama nitakuambia njia hio baba yangu na babu yangu wataniua , nipo tayari kukupatia vidonge, Dhahabu na hazina zote nilizo nazo ”
“Kama ni hivyo chagua mambo mawili , aidha kufa sasa hivi au kuwa hai?”Aliongea Roma kwa usiriasi mkubwa.
Jini Zilha alijikuta akihisi msisimko wa roho ya kimauaji kutoka kwa Roma , ilikuwa ni kama kifo kipo kwenye masikio yake na katika maisha yake hakuwahi kuhisi nguvu ya kimauaji inayomtoka Roma kama hio.
“Nitaongea …!”
Hakutaka kufa hivyo aliamua kumwambia Roma kila kitu namna ya kuvunja mfumo wa kimiujiza ambao unalinda jengo hilo
Ni mfumo kama wa nywira lakini ilihitajika kutumia nguvu za kijini ili kufungua wakati huo huo ukitumia njia ambazo amelekeza Zilha.
Ilikuwa rahisi kwa Roma kujifunza na kuelewa hekima ya mababu wa kijini ambao walitengeneza mfumo huo ,ilikuwa ni njia ya kipekee sana na Roma aliishia kutoa mshangao na kujiambia kweli majini wa Zamani walikuwa ni viumbe wenye akili sana na ilimfanya kuwa na huzuni vizazi vipya walikuwa ni majini ambao hawana thamani kabisa na ambao hawafikirii nje ya boksi kama Zilha.
Roma aliona pengine ndio maana maisha yao yalionekana kizamani zamani.
Majini wanasifika katika kutii sheria kuliko hata binadamu na sheria ambazo zimewekwa na waasisi wao na wanafuata mpaka wakati huo bila kubadili chochote , yaani mawazo ambayo yamewekwa na mababu zao ndio ambao wanaishi nayo katika wakati huo na hili liliwafanya kutopiga hatua ya kimaendeleao na kitu pekee ambacho wanawaza ni kuvuna nishati tu na kupanda levo.
Upande wao Material things ni vitu ambavyo havina thamani kubwa kama ilivyo kwa binadamu kupenda vitu kama vile madini na pesa.
Sio kwamba hawana akili , akili wanazo tena zaidi ya mara kumi ya binadamu wa kawaida lakini akili zao hawazitumii katika Miundombinu kama ilivyo kwa binadamu bali wao akili zao huzitumia katika kuelewa siri za kiroho juu ya yale ambao wameyasahau na yale ambayo hawajui.
“Wewe kama mtoto mkubwa ndani ya familia yenu, je kuna hatua zozote zinazohitajika katika kuingia katika Jumba jeupe?, kwa mfano labda kuomba ruhusa kwa babu yako na kadhalika?”Aliuliza Roma na kumfanya Zilha kumwangalia kwa huzuni.
“Mwanafamilia yoyote anaweza kuingia muda wowote atakao”
“Je kama ukiambiwa kumtoa Sui nje muda wowote , inawezekana?”
“Ndio , Sui yupo chini yangu , ikimaanisha kwamba ni mtumwa wangu , ninao uwezo wa kumfungia na kumfanya awe huru muda wowote , wazee na walinzi wa Jumba hawawezi kunizuia kwa chochote , naomba uniachie nikamtoe Sui sasa hivi”Aliongea na kumfanya Roma kutoa tabasamu la kejeli.
“Vua nguo zako”
“Nini!?”
“Nimesema Vua nguo zako , shati , suruali na viatu kila kitu”Aliongea huku akimwangalia kwanzia chini mpaka juu.
“Unakwenda kunifanyia vile mnavyofanyiana binadamu?”
“Acha ujinga , unajua kila kinachoendelea ulimwengu wa kawaida licha ya kukaa huku”Aliongea Roma na kumpiga teke.
Zilha hakuwa na jinsi na palepale alianza kusaula nguo moja baada ya nyingine huku akijiambia baada ya hapa ni kwenda kumwambia babu yangu na baba na watamshikisha huyu mpuuzi adabu.
Roma aliona pete ambao Zilha amevaa kwenye kidole chake , baada ya kumaliza kuvua nguo alimwambia aivue na yenyewe ampatie.
Zilha alionyesha uso wenye uchungu lakini maisha yake yalikuwa muhimu kwa wakati huo hivyo alifanya kama alivyoambiwa.
“Inatosha sasa maana sihitaji nguo yako ya ndani”
“Kwahio naweza kuondoka?”
“Ndio lakini sio kurudi kwenye familia yako”
“Kwahio niende wapi?”
“Kuzimu”
Aliongea Roma na palepale kitenesi cha mwanga wa bluu kilijitokeza katika mkono wake wa kushoto.
Mwanga wake ulianza kufanya mazingira kuwa angavu na kufanya wadudu kuanza kuamka.
Lakini upande wa Zilha alihisi nguvu ya ajabu ambayo inatoka katika kitufe kile na alitaka kukimbia .
Hio ni mbinu mpya Roma ambayo alikuwa ameigundua kwa kuunganisha moto wa kiroho na maji ya kiroho ndio kukatokea siraha ya namna hio , ilikuwa ni kama moto wa rangi ya bluu lakini haukuwa moto.
Haikuwa na haja ya Roma kutumia siraha hio ya kimaajabu ya juu kabisa kumuua nayo Zilha lakini alifikiria mateso aliokuwa akipitia Sui mlezi wa Rufi na aliona pengine hata chungu chake kingejisikia kichefuchefu kumeza huyo mpuuzi.
“Hapana… sitaki kufa”Alibweka mara baada ya kugundua nini ambacho kinakwenda kumtokea na kuanza kukimbia lakini spidi ya Roma ilikuwa kubwa kuliko ya kwake na palepale kwa kuunganisha nishati ya mbingu na ardhi alimshusha chini ardhini.
“Bang!!!”
Roma alimtupia kile kitufe cha rangi ya bluu eneo la moyo wake na palepale mwili wake ulianza kuyeyuka kwa kasi mno.
“Arghhh…!!”
Zilha aliishia kutoa ukulele wa maumivu na ndani ya dakika hio hio alikuwa tayari ameshapoteza uhai na palepale upepo ulianza kuongezeka na kupeperusha chembechembe za mwili wake.
Roma wala hakujisikia vibaya kwa kile alichokifanya hata kama alikuwa ni mtoto mkubwa wa familia ambaye anatarajiwa kuwa mrithi hapo baadae , alikuwa ni njia kwake ya kuweza kumpata Rufi.
Roma palepale alivaa mavazi ya Zilha na kisha ka kutumia Dhana ya Jani la Upofu alichukua muonekano wake na kubadilisha levo yake ya kijini na sasa kwa asilimia mia moja alifanana na Zilha.
Kuhusu ubini wake alijitambulisha ndani ya familia hio kama Xiao Cheni hakuwa na haja nao tena na alijiambia hata kama ikija kutokea familai hio kumtafuta Xiao Cheni na kutokumona wasingehangaika sana kwani hana thamani kubwa kwao.
Roma palepale aliona ingekuwa vibaya kama angeenda kumuokoa Sui moja kwa moja wakati wa usiku hivyo alijiambia labda anapaswa kwenda kesho yake kwani kama ni Zilha halisi alishakufa na yeye ndio Zilha.
Akiwa njiani alijaribu kuangalia katika hifadhi ya pete ya Zilha kuona kama kuna chochote cha maana lakini aliona hakuna kwani kulikuwa na vidonge vya daraja la chini na baadhi ya mimea ambayo aliona ni takataka kwake.
Roma mara baada ha kufika katika makazi ya familia ya Zilha ambao ndio wakuu wa miliki ya Kekexil aligundua hakuwa akijua ni upande upi ambao Zilha alikuwa akiishi., alichokumbuka ni kwamba familia hio yote ilikuwa ikiishi katika eneo moja.
Bila kujali Roma alitua ardhini ndani ya eneo hilo na kujifanyisha anatembea tembea kwa namna ya kukagua mazingira.
Ile anataka kupita nyumba moja ambayo ilikuwa imejengwa kwa staili ya kipekee alianza kuhisi harufu ya marashi makali ikiongezeka na kufumba na kufumbua alikuwa ameshikiliwa shingo na mwanamke mrembo.

SEHEMU YA 705.
“Wewe mkorofi mbona unachungulia vyumba vya wanawake usiku usiku au ndio unatafuta kitoweo?”
Sauti nyororo ilisikika kwenye masikio ya Roma na palepale alipokea busu la shavu ambalo lilimletea msisimko wa aina yake na Roma alijiambia mabusu ya jini ni tofauti na ya binadamu.
Mwanamke huyo hakuwa mwingine , alikuwa ni Jini Manyani binamu yake Zilha na alikuwa amevalia gauni ambalo lilifanya umbo lake la rangi nyeupe kuonekana, ni vazi ambalo lilikaa kimitego zaidi.
“Kwanini unanishangaa, hujawahi kuwa hivi au nimekuwa mrembo sana leo?”Manyani aliongea baada ya kuona Roma ameduwaa.
Roma alijikuta akimeza mate huku pua zake zikisumbuliwa na marashi ya yanayofanana na mmea wa Orchid uliokaushwa na kushusha shingo yake na kuanza kumkagua jini Manyani.
Roma licha ya kujua Zilha alikuwa muhuni lakini hakutegemea kama alikuwa akitembea na binamu yake na alijiuliza kumbe hata ulimwengu huo ulikuwa umeharibika tu kama ulimwengu wa kawaida
Kwa wakati huo Roma hakujua namna ya kuendelea na hali hio lakini alijua kwasababu alikuwa akijifanyisha ndio Zilha basi hawezi kumkatalia.
Yalikuwa ni mawazo ya sekunde moja tu na palepale Roma alibadili muonekano wake na kuweka ule wa kihuni na kumfanya kufanana na Zilha kabisa.
“Nimeshindwa kulala na kuanza kutafuta kitoweo na wewe ndio umejileta mwenyewe, Kabebi kangu mwaah…!!”Aliongea Roma huku akishika shavu la Manyani , aliona kwa namna yoyote ile anapaswa kuwa romantic.
“Nilijua ulienda kucheza na mdogo wake Zomu ,nadhani jitihada zangu zimekufanya kunikumbuka”Baada ya kuongea hivyo alimsogelea Roma na kuanza kumbusu kwenye midomo yake na kutumbukiza ulimi kwenye mdomo wa Roma.
Roma hakutegemea Manyani kuwa mpana namna hio kwa kwenda moja kwa moja kwenye hitajio lake licha ya kwamba wapo eneo la wazi , huenda alikuwa amecheza michezo ya namna hio na Zilha mara nyingi.
Kulingana na uzoefu wa Roma aligundua huyu jini atakuwa amecheza na majini wengine wa kiume sana.
Roma alikumbuka wakati anatoka na Feilo kwenye jumba jeupe alimtahadharisha kwamba katika familia hio ya kifalme anapaswa kuwa makini na Jini Zilha pamoja na Lilsi kwani wanapenda kuwatumikisha kingono sana binadamu na majini wa kiume.
Roma alijiambia mama na mwana hakika wanafanana
Licha ya kwamba alikuwa amechezewa sana lakini umbo lake bado lilikuwa zuri na alikuwa akivutia mno kulinganisha na wanawake makahaba ambao alikuwa akitumia kabla ya kukutana na Edna.
Roma kwa muda huo hakutaka sana kujali , isitoshe alikuwa amecheza sana na wanawake hivyo kumshughulikia jini kama huyo hakuona tatizo , kama aliweza kulala na Lilith Vampire anashindaje kulala na jini Manyani ili kulinda misheni yake.
Roma mara baada ya kujishawishi kupitia matendo yake machafu ya nyuma palepale alianza kumshambulia jini Manyani na kumfanya kuanza kuzidiwa.
“Twende ndani ya chumba vangu , ijapokuwa hakuna mtu hapa anaetuona lakini sio pazuri”Aliongea na Roma hakuchelewesha na palepale aliruka na mrembo huyo kupitia dirishaji na kwenda kutua kwenye chumba chake.
Kabla ya kuanza mchezo Manyani alimzuia Roma kuendelea na kisha palepale kama anapunga upepo aliachia nguvu ya kijini ambayo iliwasha kitu kama mshumaa katikati ya chumba na ndani ya dakika chache tu harufu nzuri ilianza kusambaa,
“Unafanya nini?”Aliuliza Roma asielewe nini kinaendelea na Manyani alionyesha uso wa kuomba msamaha na kuanza kulamba kifua cha Roma kimahaba.
“Kaka Zilha usikasirike , sijasema kwamba huwezi kufanya , si unakumbuka mara ya mwisho tulitumia harufu ya Mandala na ukafanikiwa kusimamia shoo kwa masaa mawili?”
Roma palepale kwa siri sana alipumua kwa ahueni , ilionekana alikuwa akimsaidia Zilha kudumu muda mrefu kwenye tendo, lakini Roma kwake aliona hilo halina maana lakini kudili na jini hilo Roma aliona anapaswa kuwa makini ili kuhakikisha anakuwa anajisikia vizuri.
Dakika ileile alimbeba juu juu na kupandisha gauni lake na kisha akamlamba vibao vitatu vya makalio.
“Slap! Slap! Slap!”
Upande wa jini Manyani alifurahishwa na kitendo kile kana kwamba alikuwa akihitaji Roma kuendelea kufanya hivyo na kumfanya Roma kuona kweli huyu ni malaya wa kijini aliekubuhu.
Roma hakutaka hata kujisumbua kumwandaa kwani alimchukulia kama changudoa wa kijini hivyo alivua nguo zake kuanza kazi.
“Broo ,, ime.. ime , kwanini imekuwa kubwa hivyo!!?”
Roma palepale alikumbuka kiungo chake hakikubadilika ukubwa na kufanana na Zilha , lakini hata hivyo angejuaje saizi yake kwani hakumwangalia.
“Mwanamke mjinga , hujui inaweza kubadilika muda wowote kwa kumeza vidonge?”:
“Ah!,Ndio umetumia vile Vidonge vya Tinya ambavyo vinavumishwa kuongeza ukubwa?”Aliuliza kwa mshangao lakini Roma hakutaka kujisumbua kujibu , alijiambia anachokifanya hapo ni sehemu ya misheni yake na mambo ya Tinya Tinya watajua wenyewe.
Roma alimpa bakora za kimkakati jini Manyani na kwa mwanamke huyo alijihisi ni kama vile amevamiwa na mnyama na alijiuliza imekuwaje kaka yake akawa na nguvu namna hio siku hio, lakini hakutaka kujiuliza zaidi alijiambia huenda ni vidonge vya Tinya.
Ukweli ufanisi wa Dhana ya jani la upofu ilikuwa ni juu mno na Manyani hakuona utofauti wowote.
Manyani alikuwa ni jini mwenye uwezo wa nafsi na alikuwa na uwezo wa kuhimili mikiki ya namna hio lakini hakutaka kutumia uwezo wa kijini bali alijifanyisha kama binadamu wa kawaida ili kukolewa na surubu.
Dakika chache mbele aliweza kuhiisi ni kama mwili wake upande wa chini umekuwa wazi mara baada ya nyoka kuchoropoka pangoni na alihisi ubaridi ukiingia.
Dakika hio hio wakati akijishanga shangaa alishikwa shingo na Roma na kumfanya aachame na kabla hajajua kinachomtokea Dragoni tayari alishaingizwa kwenye mdomo wake na kuishia kuguna.
Roma alikuwa amemisi sana mambo hayo wakati alipokuwa Ulaya lakini hakutaka kuyafanya kwa wanawake zake kwasababu alikuwa akiwapenda , lakini kwasababu alimchukulia jini Manyani kama kahaba aliona ateme uchafu wote ndani ya mdomo wake ili kuweka rekodi sawa.
“Naona unapenda kuchezewa Rafu sio”
“Ndio napenda sana rafu kaka yangu , nakupenda sana kaka lala leo hapa hapa maana nitakumisi kuanzia kesho ukiondoka”
“Kesho nikiondoka!!!”
Roma machale yalimcheza palepale huku jasho likianza kutiririka mgongoni , ilionekana kesho Zilha kuna sehemu alikuwa akienda na ilikuwa bahati nzuri kwamba alikutana na huyo jini kahaba la sivyo angekamatika.
“Nadhani sina haja ya kwenda , nataka kukufaidi wewe mrembo”
“Mh! ,unawezaje? Mjomba anakupeleka kutembelea matawi ya miliki yetu hivyo hupaswi kukataa kwani unapaswa kupata sapoti kutoka kwao kama unataka kumrithi , Kaka una uwezo mdogo sana wa kijini kama hutotumia nafasi hii vizuri na baba yangu akipata mtoto wa kiume mwenye vigezo au babu akipata jini anaefaaa huwezi kurithi tena na itakuwa ni usumbufu”
Roma palepale alijua sasa safari hio inahusiana nini kumbe ilikuwa ni kwenda kutembelea koo zingine ambazo zipo chini ya miliki ya Kekexil. “Nilijua tu kuna zaidi ya koo moja ndani ya uimwengu wa kijini”aliwaza Roma.
Ukweli hata yeye alishangazwa kama kweli Kekexil ilikuwa na nguvu kama alivyosema Rufi kwanini alipofikia hakuna majini wengi , kumbe majini wote hawaishi sehemu moja.
Ukweli ni kwamba Kekexil ni jina la miliki lakini koo ya Mo ilikuwa na nguvu sana katika ulimwengu huo hivyo kuweza kutwaa koo zingine na kuunda miliki moja inayofahamika kwa jina la Kekexil , hivyo ni sawa na kusema ndani ya miliki ya Kekexil familia yenye nguvu zaidi ni ya Mo ambayo ndio ya baba yake Yezi.
Ilionekana Zilha alikuwa na presha kubwa kwani familia nyingi za kijinni ndani ya miliki hio zilikuwa na majini wa rika lake ambao walikuwa juu sana kinguvu , hivyo kwake ingekuwa ngumu kupata nafasi ya kurithi bila ya kuwa na koneksheni.
Lakini kwa wakati huo haikuwa na maana tena kwani tayari amekwisha kufa na Roma sasa ilipaswa kutembelea hizo familia nyingine za kijini kwa niaba yake.
Roma hakuwa na chaguo lingine kwa wakati huo na aliona kwanza asubirishe mpango wa kumuokoa Jini Sui, hata hivyo alijua wasingekaa huko muda mrefu kwani huyo Master Shagoni ambaye alitegemewa kuja kwenye ukoo huo kutoa mafunzo angekuja katikati ya mwezi hivyo lazima Mkuu namba tatu wa majini , Mohi lazima angerudi wakati ambao Shagoni anafika.
“Tatizo nini, hata kama nnikiondoka najua utafuata wanaume wengine na kucheza nao”
“Kaka kwahio una wivu na mimi? , nikuambie tu sijacheza na hao wanaume kwa muda mrefu , hao majini ni watumwa kwa familia yetu na ni kama midoli tu ya kucheza nao , unapaswa kujua mimi nakupenda zaidi wewe”Roma alijihisi ubaridi wa mgongoni kwa kuona kinachoendelea kati ya ndugu na ndugu.
“Kuwa makini huko uendako , mashindano ya kuingia Jicho la Anga yataanza mwaka huu na hao watoto wa koo nyingine wanachowaza ni kukuondoa kwenye orodha..”Aliongea mara baada ya kukosa jibu analitarajia kutoka kwa Zilha na Roma alitingisha tu kichwa kukubaliana nae.
*******
Asubuhi baba yake Zilha alikuwa ashajiandaa kuanza safari na wazee wengine na alimpa maagizo Mkuu wa Chemba jini Ganyo kwenda kumwita lakini muda uleule alisitisha baada ya kumuona mtoto wake akifanya mazoezi nje ya ukumbi.
Mohi na wasaidizi wake walisimama na kuanza kushangaa na kujiuliza ni lini Zilha akaanza kujifua kimazoezi kwa hiari yake.
Roma alijifanyiha kuona aibu kuangaliwa na baba yake feki na palepale alitoka alipokuwa anafanya na kupaa na kwenda kutua mbele ya baba yake.
Jini mkuu namba tatu alijikuta akishangazwa na mtoto wake mara baada ya kugundua tayari ameingia katika levo ya kutawala moto wa rangi ya njano jambo ambalo hakutegemea na palepale hatia ilianza kumvaa na kujiambia kumbe alikuwa akimfokea bure mtoto wake na alikuwa akijifunza kwa siri.
Siku zote alimchukulia Zilha kama mtukutu ambaye hajali kujifunza mbinu za anga na mara nyingi kupenda kutoroka ulimwengu wa kijini na kwenda duniani kulala na wanawake wa kibinadamu lakini maendeleo yake hayo yalimfanya kuona alikuwa akimfokea bure.
Baada ya Roma kupokea sifa pale kwa jina la Zilha hatimae safari ilianza na alielewa kwamba ingewachukua siku kumi na tano kwenda na kurudi.
Roma aliishia kufuata nyuma nyuma akiendelea kusikiliza maongezi yao na alianza sasa kuelewa namna ulimwengu huo ulivyo na mahusiano ya familia hio na koo zingine yalivyo.
Roma alifanya makusudi kabisa kupandisha kidogo uwezo wake ili kumfanya Zilha kuonekana yupo siriasi kumfurahisha baba yake ili hata akiuliza maswali ajibiwe.
Roma katika kusikiliza maneno hayo alikuja kugundua kuna majini wengi sana ambao wamesambaa katika familia mbalimbali na familia zote hizo ilionekana zilikuwa na uwezo wa kushika wadhifa waliokuwa nao familia ya Mo.
Yaani kwamba familia hizo kama zitaweza kuzidi familia ya Mohi kinguvu basi hawana namna zaidi ya kukubali kushindwa na kuachia madaraka kwa familia nyingine , hivyo safari hio ilikuwa ni kuhakikisha kwamba wanakuwa na ushirikiano wa ukaribu na familia hizo ili kuwasapoti.
Kitu kingine ambacho Roma alijifunza ni kwamba kila familia inakuwa na Mkuu wao ambao ananguvu zaidi ya familia nzima , yaani ilikuwa kama kwa ukoo wa Zaola kupambania mzee wao kuingia levo nyigine ndio ilivyokuwa kwa familia nyingine walikuwa na wakuu wao ambao wote walikuwa levo za juu kabisa za kuivuka Dhiki.
Kitu kingine ambacho Roma alikuja kujua ni kwamba familia ya Xia ndio ambayo ina nguvu kubwa sana kuliko hata ya Kekexil na hio yote ni kutokana na kwamba wanao masters wengi wa kijini ambao wamepita Dhiki kitambo.
Roma alikuja kujua pia yule Bibi kizee aliefahamika kwa jina la jini Tigola ambaye kazi yake ni kulinda geti la mlango wa kuingilia kwenye Jumba jeupe ni sehemu ya Master ambao Rufi alikuwa akizungumzia
Mpaka wakati huo Roma alikuwa ashafahamu Master watatu , wa kwanza ni babu yake Zilha ambaye ndio mkuu namba moja wa majini katika miliki ya Kekexil na wa pili alikuwa ni Master Shagoni ambaye alitarajiwa kufika kufundisha na watatu ni yule Ajuza.
Roma aliuliza maswali mengi wakati wakiwa njiani na kwasababu wazee hao wakijini walianza kumchuklia yupo siriasi basi walimjibu kila kitu , isitoshe walijua hakuwa akijua chochote kuhusu msingi wa miliki yao hivyo walimweleza kwa furaha kwani walitarajia angekuja kuwa mrithi.
Kadri Roma alivyokuwa akisikiliza maelezo yake ndio jinsi woga ulivyomwingia na kugundua eneo hilo ni hatari zaidi nje ya alifyofikiria kwa yeye kuendelea kubaki hivyo aliona anapaswa kuwa makini zaidi na zaidi na kukamilisha misheni yake na kuondoka kimya kimya.
Kulikuwa na vitu vingi sana ambavyo Rufi hakumwambia , pengine ni kwasababu hakuvijua na ndio sasa Roma aliweza kuvijua.
Roma hakutaka kupumzika hata kidogo mpango wake sasa ulikuwa ni kwanza kumuokoa jini Sui ambaye alikuwa mlezi wa Rufi na kisha angehamia kwenda miliki ya Xia kwa ajili ya kumuokoa Rufi.
Roma alijua kama atachokoza maveterani wa huko itamfanya kuwa na hatari na atashindwa kuwaokoa Rufi na Sui lakini vilevile na yeye angekuwa hatarini.
Hatimae waliweza kufika katika koo ya kwanza na kulingana na maelezo yao koo hio ndio ndogo kati ya koo kumi na nne ambazo zipo chini ya miliki ya Kekexil.
Ijapokuwa walikuwa ni koo tanzu ya miliki ya Kekexil lakini walikuwa wakifanana sana na kilichomfanya Roma kuzima shauku yake ni kwamba kati ya majinni ambao aliona kulikuwa na watu weusi, lakini kilichompa shida ni kwamba alishindwa kutofautisha yupi ni binadamu wa kawaida mwenye nguvu za kijini na yupi alikuwa ni jini kamili kwani kwa maelezo ya Feilo ni kwamba asilimia kubwa ya majini ambao wapo ndani ya miliki hio wametokea Hongmeng na binadamu wa kawaida waliojigeuza kuwa majini.
Unatakiwa kukumbuka Hongmeng ndio chanzo cha uwepo wa binadamu katika ulimwengu wa kijini kutokana na kwamba ndio wasimamizi wakuu wa mkataba kati ya majini na miungu na vilevile ndio majini ambao wanajihusisha ana kwa ana na ulimwengu wa kawaida kupitia China, majini wengine hawana kabisa habari na binadamu au ulimwengu wa kawaida.
Jambo pekee ambalo Roma aliona ni kwamba asilimia kubwa ya watu waliokuwepo ndani ya ulimwengu huo ni wa bara la Asia , waarabu walikuwa wachache sana na sura nyingi ambazo aliona ni wajapani , wachina na Wathailland.
Kwa namna moja ama nyingine Roma aliona labda kuna muunganniko mkubwa wa nguvu za kijini na wasalia Budhha ndio maana.
Unachopaswa kujua kuna muunganiko mkubwa kati ya Buddha na majini kuliko dini yoyote ile na ukitaka kuthibitisha hili angalia namna dini hio ilivyoanza haikuletwa na mitume kama ilivyo kwa ukristo na Uislamu.
Ijapokuwa watu wa ngozi nyeusi walikuwepo lakini walikuwa ni wa kuhesabu sana jambo alingine ambalo lilimshangaza ni kwamba majini wengine ilikuwa ngumu kuwajumuisha katika makundi kulingana na jamii za dunia , kwa mfano wengine hawakuonyesha kuwa na sura ambazo zinafanana na kabila lolore au jamii yoyote katika dunia ya kawaida ,yaani sura zao zilikuwa za kipekee lakini kitu kimoja tu ni kwamba wote walaikuwa weupe ambao wana nywele ndefu sana ambazo wamezifunga kwenda mgongoni.
Kingine pia hakukuwa na mabadiliko ya kimiundombinu kama ulivyo dunniani , asilimia kubwa ya maeneo yote yalikuwa yametawaliwa na miti na bustani za maua ya kuvutia mno ambayo huwezi kukuta duniani.
Koo jumla zote zilikuwa ni kumi na nne na katika kila koo walilala siku moja hivyo mpaka wanakuja kufikia siku ya kumi na nne walikuwa washatembelea koo zote na ilikuwa imebakia koo moja tu.
Katika siku hizo Roma alijifunza vitu vingi sana na kilichomshangaza licha ya kwamba majini walikuwa na tamaduni zinazofanana lakini kila koo ilikuwa na tamaduni za kipekee mno.
Familia ya mwisho kabisa kutembelea ilikuwa ni familia ya pili kwa ukubwa na hio familia ilikuwa ni koo moja na familia ya Mohena , familia hio ndio ambayo baba yake Rufi ndio alikuwa akiish.
Jambo hilo lilimshangaza Roma kwani mwanzoni alijua baba yake Rufi alikuwa akiishi makao makuu ya miliki lakini iligeuka Rufi alikuwa akiishi upande mwingine kabisa nje ya makao makuu na kule makao maku alikuwa akishi Mohi na familia yake.
Yaani Mohena baba yake Rufi alikuwa na familia yake mbali na ndugu zake na familia yake ilikuwa kubwa na ya pili ukichana na ya Mohi kaka yake.
Roma sasa kwasababu hakuwahi kumuona baba yake Rufi alijikuta akijawa na shauku ya kuona ni aina gani ya jinni ambaye alimchezea Bi Wema hisia zake na kisha kutoroka na binti yake.
Kila familia ambayo walikuwa wakifika walikuwa wakisubiriwa nje na mara baada ya kutua sasa palepale aliweza kumuona mwanaume ambaye alikuwa amemchanganya Bi Wema kimapenzi , alikuwa ni mwanaume mwembaba aliekuwa amevalia joho la rangi ya bluu alikuwa na sura mabayo ni ngumu kusema ni mchina au mwarabu yaani alikuwa mchanganyiko.
Kjwa muonekano wake ni ngumu kabisa kusema labda ni jini alikuwa wa tofauti kabisa na hapa sasa Roma aliamini kwanini Bi Wema alikubali kirahisi, bwana huyo alionekana mpole sana kimuonekano lakini upole wake ulionekana kuficha mengi.
Unachopaswa kuelewa pia majini hawafanani sura kama vile binadamu wanavyonana kutokana na kuwa ndugu , hio ni kutokana sura zao hazitokani na kijenetiki bali wenyewe wanazipata baada ya kufika kiwango flani cha nguvu za kijini mara baada ya kuzaliwa na ukishapata mwili basi huwezi kupata mwili tena na huo ndio unazeeka nao mpaka kufa.
Wanaorithi sura sasa ni wale ambao wamezaliwa na nusu jini na nusu binadamu kama ilivyo kwa Rufi na XiaoXiao,.
Roma aliona pengine ndio maana urembo wa Rufi ulikuwa wa kipekee hasa kwenye ngozi yake , ilionekana baba yake alikuwa mtanashati mno.
Majini hawakuwa kama miungu ambao wao hutumia uungu wao kuhama kutoka kwa mwili mmoja kwenda mwingine mara baada ya wanaotumia kuzeeka.
Kiitu kimoja ambacho kilimfanya kuona baba yake Rufi hakuwa wa kawaida ni kutokana na levo yake , kwa haraka haraka alikuwa katika levo ya juu mno , ijapokuwa hakuwa ameficha uwezo wake lakini Roma alijua alishaipita dhiki na sasa alikuwa levo ya juu zaidi kiasi cha kulingana na yeye , utofauti tu ni kwamba mbinu ya Roma na majini hao ilikuwa ikitofautiana hivyo ndio maana alikuwa na faida kubwa lakini baba yake Rufi alikuwa juu zaidi kumkaribia kaka yake.
Roma hapo alichokuwa akitega ni kujua tu kama mzee huyo angemzungumzia Rufi hata kidogo lakini habari ambazo zilikuwa zikiongelewa hapo ni za majigambo tu kuringishiana uwezo mpya ambao kila mmoja amepata , stori ambazo Roma kwake hakuwa akipendezwa nazo hata kwani aliona walikuwa wakipoteza muda na yeye alikuwa na haraka ya kumaliza misheni yake na kurudi kwa familia yake.
Waliendelea kubadili stori huku wakinywa kinywaji flani kama dawa lakini wao waliita mvinyo , katika safari hio Roma alipata uzoefu , kwa mfano kuna majini ambao alikutana nao katika familia zingine hawatumii kabisa pombe wala mvinyo na walipewa aina ya kinywaji ambacho kilikuwa kichungu mno lakini wao walikifurahia.
Roma alifuatisha maongezi yao kwa muda mrefu na alikuwa wakiongelea zaidi kuhusu mashindano ya kuingia kwenye jicho la Anga huku wakienda mbali kupeana tahadhari ya namna ya awamu hio kushinda katika mashindano hayo na kutowaruhusu koo zingine kuwashinda.
Kilichomvutia Roma ni kwamba aliweza kusikia katika koo ambazo zingeshiriki katika mashindano hayo hata Panasi wapo na alichokuja kujua ni kwamba Hongmeng ni jamii ambayo haikuwa ikiogopeka kabisa , jamii ambayo wengi wanaiogopa n Panasi halafu inakuja ya Xia na ndio inafuatia ya Kekexil hivo ndio alijifunza Roma na Hongmeng ndio wa mwisho kabisa.
“Mohena … nimesikia miliki ya Xia wamefannikiwa kumrudisha Rufi mara baada ya kumkamata?, je ni kweli?”Aliuliza jini mkuu namba mbili, huyu ni kaka yake jini mkuu namba moja
Sasa mazungumzo ambayo Roma alikuwa akitaka kuyasikia yalikuwa ndio hayo na alitega sikio vizuri apate kusikia.

SEHEMU YA 706.
Wote familia nzima ilimwangalia Mohena jibu lake akiwemo baba yake Zilha ambaye alinyanyua kikombe cha mvinyo na kunywa kidogo.
“Ni taarifa mpya ambayo mimi pia nimeipata , sijajua ni kwa namna gani wameweza kumpata huko duniani lakini Mkuu wa miliki Kiku alimtuma Mzee Lao na Lahani kwenda kumkamata”
“Hii ni bahari nzuri , miliki hio imekuwa na kinyongo na sisi kwa muda mrefu na kuona ndio tulimtorosha , wapo mpaka watu wetu walipigana katika safu za milima ya barafu kwa ajili ya swala hili , hii koo tokea muda mrefu inaona labda tulifanya njama kwa kufanya nao dili feki”
“Mjomba sikuwahi kutegemea huyu mwanamke angesababishia miliki yetu matatizo namna ile , kaka niseme kwamba huku mfunza vizuri binti yako , ijapokuwa alizaliwa katika ulimwengu wa kawaida lakini bado ana damu ya kijini ndani yake ya familia yetu , kama watoto wetu wangekuwa kama Rufi sidhani kungekuwa na amani”
“Kaka upo sahihi lakini kwasasa sio mwanafamilia wetu tena , na anabahati sijakutana nae ningempa adhabu kali sana”
“Alitusababishia hasara bila sababu na kutogombanisha na Xia , hivi unajua kipindi kile baba alivyokuwa na hasira , kama nisingekusaidia ungefungwa katika Jumba jeupe wewe”Aliongea Mohi.
Waliendelea kubishana wao kwa wao wakimuongelea vibaya Rufi , hakuna ambaye alionyesha kumjali kabisa hata baba yake alionekana hana chembe ya mapenzi kwa Rufi kabisa na haikueleweka kwanini hakumuacha duniani na Bi Wema kuendelea kuelelewa kama hampendi.
Roma alikasirishwa sana na maneno yao na alitamani kuua mmoja baada ya mwingine lakini alijiuzuia kwani walikuwa wengi ambao wapo levo za juu za kuipita dhiki lakini pia alikuwa na mpango wa kumuokoa Sui kabla ya kushitukiwa ni Zilha feki.
Moheni baba yake Rufi alikuwa na mtoto mkubwa tu wa kiume na ndio anafuatia Manyani ambaye anaishi katika makao makuu ya miliki ndio anakuja sasa Rufi ambaye ndio wa mwisho.
Baada ya kuongea kwa muda hatimae topiki nyingine iliibuka ambayo ilikuja kumfanya Roma na mtoto mkubwa wa baba yake Rufi kupigana ili kuonyeshana uwezo.
Lakini baba yake Zilha alikataa kutokana na kwamba Subiani alikuwa levo ya juu kuliko Zilha na aliona pengine mdogo wake anataka Subiani kupambana na Zilha ili kumuua na kisha aseme ni bahati mbaya na hapo ndio amfanye mtoto wake kuwa mrithi.
Mabishano yaliibuka kati yao na kusema kwamba mashindano ambayo yanafanyika sio ya kuuana bali ni kuonyeshana ujuzi wa kutumia siraha na mwishowe baada ya Roma kuona mtafaruku hio alitoka mbele ya baba yake Zilha na kumwambia atapambana.
Roma aliamini angejifanyisha tu kupigana bila ya kushinda na kama Subiani angekuwa na hila juu yake basi angetumia mbinu yoyote ile kuhakikisha anamkwepa.
Subiani alifurahi Zilha kujitokeza mwenyewe kwa ajili ya kupambana nae , alitaka kuchukua naasi hio kuonyesha wazee wa ukoo ni namna gani Zilha alikuwa hafai kuwa mrithi na yeye ndio anafaa kwani ni mwenye juhudi kwenye ukoo.
Mohi alikuwa na wasiwasi kweli kuona mapambano hayo, upande wa Roma licha ya kwamba hakuwa akimuogopa Subiani lakini alikuwa na wasiwasi kwamba anaweza kuzidiwa na kuonyesha uwezo wake na mwishowe kugundulika na alijua kama atagunulika ndani ya majini hao saba ambao wana uwezo wa juu ingekuwa kasheshe kwenye kudili nao hivyo alipanga kuwa makini.
Bahati ilikuwa upande wa Roma jini Subiani hakuonekana kuwa na hila yoyote wala njama zidi ya Roma na alipambana kama alivyoahidi kwamba asingetumia uwezo wake wa juu kupambana na Zilha na mwisho wa siku Roma alitumia nafasi hio kuonyesha mbinu mpya za kutumia siraha mbele ya baba yake Zilha.
Alimua kumfanya jini huyo kuwa na furaha mwisho mwisho zidi ya mtoto wake kabla hajajua kwamba tayari ashakufa muda mrefu.
Mpaka mwisho wa mapambano Roma alikuwa ameonyesha uwezo wa juu zaidi katika kutumia siraha , ijapokuwa mshindi alikuwa ni Subianni lakini Roma alifanya kitu kikubwa zaidi katika kupangua mapigo mbalimbali ya Subiani lakini vilevile katika kubuni mbinu za kushambulia.
Roma alitumia uwezo wake aliojifunza katika Temple za China kum’chalenge; Subianni na mwisho wa siku mpaka pambano linaisha Zilha alionekana kusifiwa sana na jambo hilo lilimfanya Mohena baba yake Rufi kutokuwa na furaha kwani mpango ulikuwa ni kumdhalilisha Zilha mbele ya wazee wa ukoo ili kumpa mtoto wake nafasi ya kuchaguliwa kama mkuu namba nne wa ukoo na kuanza maandalizi ya kushindana katika pambano la kuingia katika jicho la Anga.
Baada ya maongezi ya kifamilia kuisha hatimae Roma na wazee wote walianza safari ya kurudi makao makuu ya Kekexil.
Baada ya kufika Roma ambaye alikuwa ni jini Zilha aliitwa ma jini mkuu namba tatu Mohi katika ukumbi kwa ajili ya maongezi.
“Zilha mimi kama baba yako sijui ni lini au kwa namna gani umeweza kujifunza zile mbinu lakini nikuambie nimefurahi sana kuona una maendeleo mazuri , lakini hata hivyo spidi yako bado ni ndogo , tafadhari jitahidi kufika katika mwishoni mwa levo ya moto wa njano ili uweze kuwakilisha miliki katika mashindano ya kuingia kwenye jicho la anga”
Roma mara baada ya kusikia kauli hio alijiambia vyovyote vile anachopanga hapo ni kundoka mapema sana kabla ya mashindano hayo , lakini kwasababu alikuwa akimwigizia Zilha alitingisha kichwa kwa utii.
“Mjomba wako yule ni mtu wa njama sana anadhani hatujui ana mipango nyuma ya pazia na yule kizee … ni bahat nzuri babu yako yupo upande wetu”Aliongea akimaanisha mkuu namba mbili wa miliki ya Kekexil kuwa na mipango na Mohena mjomba wake jini Zilha.
“Baba kuna kitu wamefanya?”Aliuliza Roma akijifanyisha kushangaa.
“Mwanzoni nilidhani unachojua ni kucheza na wanawake , lakini unaonekana sio mjjinga na angalau umeanza kufikiria ki utu uzima , hivyo sioni mbaya kukuambia , ukweli ni kwamba mjomba wako Moheni ana biashara za siri na mjomba wako mkuu namba mbili kupitia koo ya majini roho kutokea Kaskazini kwa kuwatuma binadamu kama sehemu ya masharti ya kuwapa utajiri ili kukusanya mimea na damu ya kafara ili kutengenza vidonge, babu yako Mkuu namba moja ameamua kukaa kimya ili kuepusha mgogoro , hatujui hii mimea binadamu wamepata vipi lakini si umeona familia yao ilivyo na vijana ambao wapo levo za juu wanatumia vidonge vyenye mchanganyiko wa damu na mimea kutoka kwa majini Roho”
Roma hakujua hata majini Roho waliokuwa wakizungumziwa ni kutokea wapi lakini kwa haraka haraka alijua Zilha atakuwa anajua hivyo hakutaka kuuliza lakini kwa namna moja aliona mkuu namba moja jini Menui alikuwa na uvumilivu wa kutosha , maana mtoto wake na mdogo wake walikuwa wakimsaliti kwa kukiuka sheria.
“Baba , hiii si inachangia uwezo wao , vipi kama huko mbeleni wakitushambulia na kutaka kututoa katika nafasi zetu”
“Kipi cha kuogopa sasa, haijalishi wanajikusanyia nguvu vipi lakini babu yako ana nguvu kuliko mkuu namba mbili”
Mkuu namba mbili ni mdogo wake jini Menui ambaye ndio mkuu wa miliki yote ya Kekexili hivyo kwa upande wa Zilha ni babu yake upande wa wajomba.
Moheni ambaye ni baba yake Yezi yeye ni mkuu namba nne , ijapokuwa anao uwezo mkubwa kuliko kaka yake lakini bado anabakia katika nafasi ya nne kutokana na kwamba alikuwa ni mdogo , sasa alikuwa akipanga njama za kumfanya mtoto wake jini Subiani kurithi nafasi ya juu katika miliki ya Kekexil.
Sasa katika safari hio Roma alijua kwamba Menui mkuu namba moja , mdogo wake mkuu namba mbili , Ajuza mlinzi wa geti na Master Shagoni kutoka familia ya Lilsi ni sehemu ya Master wakuu wa miliki ya Kekexil , Roma alikuwa amekariri kwani alijua chochogte ambacho kitatokea lazima awe na taarifa sahihi.
Sasa ilionekana Mkuu namba mbili anamuunga mkono baba yake Rufi, lakini jambo ambalo lilimshangaza Roma ni kwamba jini Lilsi upande wao wana Master ambae ni Shagoni sasa Roma alijiuliza kwasababu Lilsi ni mke wa Moheni yaani mama yake wa kambo wa Rufi kwanini asimsapoti mume wake na kumsapoti Shemeji yake.
Kitu kingine amabcho alijifunza na kushangaa ni kwamba huyo jini Lilsi katika familia yao ndio anahesabika jini mkuu mwanamke namba mbili ambao kicheo kwa lugha yao ni Lufiali , sasa Roma aalijiuliza kama Lilsi sio mwanamke namba mbili je mwanamke namba moja ni nani na kuna siri gani inaendelea.
Baada ya Roma kufikiria sana alijikuta akiona hio miliki ni rahisi kuangushwa kwani ina migogoro ya ndani mno tena mikubwa zaidi , kwa mfano Manyani badala ya kumsapoti kaka yake Subiani yeye anamsapoti Zilha kwasababu ni mpenzi wake.
Roma mara baada ya kumaliza kuongea na baba yake Zilha alienda moja kwa moja mpaka kwa Zomu na Zato kuwasalimia.
Sio kwamba alitaka kuwaaga hapana , alijua kwasababu alishapotea kama msingi wa makubaliano mwanzo ya kupata vidonge basi wasingepewa tena.
Hivyo aliona atumie sura ya Zilha kuwapatia vidonge vyake ambavyo ametegneneza yeye mwenyewe kama shukrani ya kuwa rafiki yao.
Kwa kipindi cha zaidi ya siku kumi na tano Zomu na Zato pamoja na Feilo walimsaka sana Xiao Cheni bila mafanikio lakini walishindwa kuelewa inakuwaje binadamu kupotea katika ulimwengu wa kijni ghafla tu.
Wakati huo Zomu na Feilo tayari walishakuwa marafiki mara baada ya kukutanishwa na Roma siku aliomuua Zilha hivyo Roma aliwakuta wote watatu wakiwa pamoja.
Mara baada ya kumuona ni Zilha anaewasogelea wote walisimama kiheshima na kumpigia saluti huku wakionyesa wasiwasi.
Roma hakuongea ujinga tena kwani alikuwa ni Zilha kwa wakati huo hivyo alichokifanya aliandaa vidonge set mbili na kila set aliweza kimoja cha daraja la juu na vitatu vya daraja la kati na kumi na mbili vya daraja la chini na kisha akawapatia kama zawadi yake ya kuagana nao.
Feilo na Zomu waliogopa sana mara baada ya kupokea vidonge hivyo kutoka kwa Roma kwani walijua wanapokea kutoka kwa Zilha.
“Nimewapatia hivi vidonge bila ya baba yangu na babu kujua kwasababu nimeona jitihada zenu hakikisheni mnafanya siri kwani ikigundulika mna hivi vidonge basi mtakufa”Aliongea Roma kwa sauti ya Zilha.
Wote waliguswa na ukarimu wake kwani walijua vidonge hivyo sio tu kwamba vitasaidia familia yao lakini pia wao wenyewe vinawatosheleza katika mafunzo.
Wakati Roma anataka kuondoka Feilo alichukulia hio kama fursa ya kutaka kumuuliza Zilha kuhusu wapi Xiao Cheni alipo.
“Master , unajua ni wapi Xiao cheni alipo yaani kapotea hivi tu ndani ya wiki mbili zilizopita , tuna wasiwasi juu yake”
Aliongea kwa wasiwasi na kumfanya Roma kuwa na hatia isitoshe ilikuwa ni ngumu kwa majini kusubiri kwa muda mrefu juu ya rafiki yao aliepotea
“Najuaje jambo dogo kama hilo , pengine ameenda kujificha mahali anafanya mafunzo , vipi mnadhani naweza kumfatilia mtu kama yule mimi , jaribuni kudili na mambo yenu msije kupoteza nguvu zangu za kuwapa vidonge”
“Ndio Master , tutakuwa mtiifu kwako milele na miliki yote ya Kekexil”
Roma hakujali zaidi na palepale safari yake ni kuelekea katika Jumba jeupe kuanza misheni namba moja ya kumuokoa Jini Sui.
Mara baadca ya kufika aliweza kumkuta yule Ajuza bado yupo pale nje akilinda geti akiwa vilevile na hakumshuku kwa chochote na alimruhusu kupita.
Roma alijikuta akihema kwa ahueni mara baada ya kuingia kwenye jengo hilo , na alishukuru kwa kuwa na muonekano wa Zilha na sasa anaweza kuingia popote , mwanzoni alikuwa na hofu pengine Zilha alimdanganya baadhi ya maelezo.
Kwasababu alikuwa akienda floo za juu hakutumia njia ya kawaida kwenda juu , isitoshe kwa maelezo ya Feilo floor za juu hupitii kwa ngazi bali unapaa kwa nje na kisha unavunja formation ya safu ya mwanga wa kijini na kuingia ndani.
Hivyo Roma mara baada ya kufikia ile Formation ya kijini alitumia maelekezo yaleyale aliopewa na Zilha na kuivunja vizuri tu na ikaondoka na akaingia ndani bila ya kushitukiwa.
Roma alitamani kupitia katika floor zingine ili kujua nini kipo huko lakini kwasababu kulikuwa na walinzi hivyo aliona hatua ya kwanza ni kumuokoa jini Sui kwanza.
Baada ya kuingia ndani ya floor hio palepale aliweza kutembea katika kordo na hatimae kwa juu yake aliweza kuona gereza.
Hakupinga mjenzi wa jengo hilo hakika alikuwa amefanya kazi ya kueleweka , mpaka Roma kuhisi pengine hata mapiramidi kule Misri ndio walihusika, muundo wake ulikuwa ni mgumu sana kuona katika mazingira ya dunia , kitu kingine ambacho kilimfanya kushangazwa na muundo ni kwamba mawe yaliojengea yalionekan akuwa mazito mno.
Floor za tatu zote ambazo zilikuwa zikilindwa na safu ya formation ya nguvu za kijini zilikuwa ni gereza na hio ndio ilifanya wafungwa kushindwa kabisa kutoka katika jengo hilo kwani ili uwezo kutoroka lazima kwanza uvunje hio safu.
Ni floor ya mia na tatu kwenda juu na ilikuwa ni eneo ambalo lina ubaridi wa aina yake , ilikuwa ni barafu tupu na kama kukiwekwa kipimo pengine ni zaidi ya nyuzi hasi hamsini.
Ni kwasababu walikuwa majini ndio maana hawakufariki kirahisi lakini binadamu hapo hakai hata sekunde atakuwa amekauka na kugeuka barafu.
Kila gereza katika floor lilijengwa na vyuma vizito mno ambavyo vimeungannishwa na nguvu za kichawi, jini mwenye levo ya kupita Dhiki hapo hawezi kupita kwa namna yoyote.
Roma alitumia nguvu ya kijini kuanza kutafuta sura ya jini mwanamke ndani ya hilo eneo na ndani ya sekunde chache tu aliweza kumuona na alipotea aliposimama na kwenda kuibukia nje ya selo yake ya gereza la barafu.
“Sui!!!”Aliita Roma huku akimwangalia mwanamke ambaye anatetemeka kwenye kona ya selo , akiwa na nywele ambazo zimechanguka na nguo ambazo hazitamaniki alikuwa akitia huruma mno.
Baada ya kusikia sauti ya kuitwa mwanamke yule jinni ambaye alikuwa ameinamisha kichwa chake kwenye mapaja aliinua kichwa chake na kuonyesha uso wake , alikuwa ni mrembo mno na kwa haraka haraka Roma aliona akipata matunzo anaweza kumfikia Aoiline wa ulimwengu wa majini pepo.
Alionyesha uso uliojaa chuki na alimpiga jicho kali Roma na kisha alishusha macho yake chini vilevile.
Roma alishangaa lakini palepale alikumbuka alikuwa na sura ya adui yake hivyo
alijikuta akipatwa na ahueni.
Kwa muonekano wake ilionekana Zilha amefanya vitu vibaya sana kwake , pengine hata nguo zake zilichanika kutokana na kulazimishwa kubakwa.
“Sui mimi sio Zilha , angalia …”Aliongea Roma na palepale aliondoa athari ya Dhana ya jani la Upofu na kurudisha sauti yake vizuri na sasa sura yake ya Kiafrika ilionekana.
Jini Sui palepale alimwangalia Roma kwa macho ya mshangao mno akiwa na hali ya kuchanyikiwa.
“ Wewe.. wewe ni nani!!?”Aliongea kwa tabu na kumfanya Roma kuangalia kulia na kushoto na kuona hakuna jini lolote linalomwangalia.
“Mimi ni binadamu , jina langu ni Roma Ramoni na Rufi ni mpenzi wangu , najua wewe ni mlezi wake na ndio ulimsaidia kutoroka katika ulimwengu huu wa majini , ni wakati wa mimi kukuokoa na wewe pia ndio maana nipo hapa”Aliongea Roma na palepale Sui alifutika alipokuwa amechuchumaa na kwenda kujipigiza kwenye nondo kwa hamaki na kilihoonekana ni cheche za kugusana kwa nguvu za kijini na zile nondo.

SEHEMU YA 707.
Sui alishituka kweli aliposikia jina la Rufi , ni kama vile alikuwa akisubiria kusikia jina hilo kwa muda mrefu ndio maana alipaniki na kwenda kujigonga kwenye nondo ya gereza katika selo yake lakini hakuumia maana ni jini.
“Rufi! Unamaanisha Miss Rufi Moheni, anaendeleaje , yupo wapi sasa hivi , wewe ndio boyfriend wake….!!!?”Aliuliza mfululizo huku akigonga gonga nondo kama vile anataka kubomoa selo yake.
Roma aliguswa na matendo yake katika wakati kama huo huyo mwanamke alichokuwa akijali ni Rufi wakati baba yake mzazi anamuombea kifo.
“Tulia kidogo , nitakuambia kila kitu”Aliongea Roma akijitahidi kumtuliza na palepale alimpa ishara ya kurudi nyuma na akaita moto wa rangi ya bluu na palepale sehemu ya komeo ilianza kuyeyuka taratibu kama vile ni plasiti ilioshika moto.
“Moto wa bluu!!! , inawezakanaje !!!, ni mbinu gani ya mafunzo ya kijini unatumia , kwanini umeweza kutengeneza moto wa bluu?”
Kama jini ambaye amekulia katika mazingira ya kujifunza kupanda levo kila kitu kwake kilikuwa mshangao , alikuwa kwenye levo ya nafsi na alikuwa na uelewa na moto wa bluu.
Ukweli ni kwamba moto wa bluu majini wengi waliishia kuuona katika vitabu tu na hawana uelewa namna ya kuutengeneza na ni ndoto ya kila jini.
Roma aliishia kutoa kicheko , haikuwa mara ya kwanza kuona Jinni akishangazwa na moto wake wa bluu.
Roma mara baada ya kuingia ndani ya gereza hilo aliyeyua barafu lote kwa kutumia moto wa njano na palepale selo ilipata joto mpaka alipomuona Sui amerudi katika hali yake ya kawaida ndio alianza kumwelezea kila kitu namna alivyokutana na Rufi mpaka akaja kutekwa tena katika ulimwengu wa kijini na yeye ndio yupo hapo kwa ajili ya kumuokoa,
Sui mara baada ya kusikia Rufi yupo mikononi mwa familia ya Xia alijikuta akikunja ndita kwa wasiwasi.
“Mimi ndio napaswa kuwajibika katika hili , kama utanilaumu kwa kilichotokea siwezi kujitetea lakini nakuhakikisha nitamuokoa”
“Kwasababu umekuja huku ulimwengu wa majini wewe mwenyewe inaonyesha Rufi hakufanya makosa kukuchagua , wewe ni mwanaume tegemezi , ninaweza kuwa jini kijakazi katika miliki ya Kekexil lakini mimi sio mjinga , ninashukuru kwa wewe kuja kuniokoa na siwezi kukulaumua isitoshe kuna majini wenye uwezo mkubwa ndani ya miliki ya Xia ukijumlisha hao wazee ambao hawajawahi kuonekana kwa macho, licha ya kuzingatia hayo yote umehatarisha maisha yako na kuja kumukoa , nimeguswa , Roma.. kama hutojali naomba nikuite mr Roma..”Aliongea na Roma alitingisha kihcwa.
“Mr Roma kwasababu Zilha amekwisha kufa siwezi kuteseka tena zaidi ya kupambana na baridi , kama utaniokoa hapa nitakuongezea mzigo , vipi kama wakikushuku na mwishowe wakatuzuia , itakuwa ni usumbufu tu”
“Hutakiwi kufikiria hivyo , kama siwezi kukuokoa wewe nnitawezaje kumuokoa Rufi”
“Lakini ni hatari mno kuliko unavyofikiria , Zilha alinifungia hapa mara baada ya kupata ruhusa kutoka kwa babu yake na huwezi kunitoa bila ruhusa ya babu yake , ukilazimisha lazima walinzi watatuzuia”
“Kwahio unamaanisha siwezi kukutoa hata kama mimi ni Zilha?”Aliuliza Roma.
“Hapana , miliki ya majini sehemu zote wanatiii sheria mno hususani zile kubwa isingekuwa hivyo huu ulimwengu usingekuwepo leo hii”
Roma alijikuta akikunja ndita na kuona kuna hatari mbele yake , alijiambia bado tu hajakutana na Mzee wa ukoo huo wa Kekexil atawezaje kumtafuta na kumuomba ruhusa bila ya kumshitukia.
“Mr Roma usiwe na wasiwasi , nimefurahi umekuja mpaka hapa kuniona lakini kwasasa kipaumbele chako kiwe kumuokoa Rufi , tokea yule mshenzi Zilha alivyonileta hapa sijawahi kuwaza kuondoka , kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa kuliko wa kwangu aliishia kunidhalilisha na kwasasa mimi ni mchafu … na kama sio kuwa na wasiwasi juu ya Rufi ningeshajiua muda mrefu , sasa nishajua Rufi yupo hai nimefurahi sina hitajio lingine hata nikifa sas hivi , nimeisubiri kwa hamu hii siku asante kwa kuja kuniona”Aliongea kwa sauti ndogo.
Huyo jinni mwanamke alikuwa akitia huruma mno lakini kwa wakati mmoja maneno yake yalimgusa mno Roma , upendo wake kwa Rufi ulikuwa ni ule wa mzazi kabisa kama ilivyokuwa kwa Bi Wema,
Rufi alikuwa sahihi mtu pekee ambaye alimpenda kwenye ulimwengu huo wa kijini alikuwa ni Sui peke yake mlezi wake.
Sui alikuwa amepitia mateso makubwa sana kwa kuchezewa na Zilha , pengine kwake kifo ilikuwa afadhali kuliko kuishi.
Lakini Roma hakutaka kufikiria Sui alikuwa jini mchafu , kama ilivyo kwa wanawake wa kibinadamu ambao walikuwa wakijiuza , upande wa Sui yeye sio kama alichagua kufanyiwa hivyo , haikuwa hatima yake hivyo hakuwa mchafu na ilimfanya zaidi kumheshimu.
Baada ya kuwaza alijiambia kwa namna yoyote lazima amtoroshe kwenye ulimwengu huo wa kijini hata ni kuhatarisha misheni yake.
“Sui wewe ndio uliemtoa Rufi kwenye ulimwengu huu mara ya mwisho hivyo naamini utakuwa unaijua njia ya mkato ya haraka”
“Ndio , kama utapenda kujua nitakuambia kwa maelezo ya kutosheleza”
“Okey! Hili ni swali lingine , kama nitataka kuchukua mimea ya dawa katika floor za chini nikiwa na sura ya Zilha je hao wazee wanaotengeneza vidonge watanizuia?”Aliuliza Roma na alimfanya Sui kuduwaa.
“Hio mimea wanapewa hao wazee kwa ajili ya kutengeneza vidonge , kama unaitaka itakuwa ngumu labda kama unataka kuchukua kdiogo tu”
“Vipi kama nataka kuchukua yote?”Aliongea Roma huku macho yake yakiwa yamejaa ujanja ndani yake.
“Mr Roma unataka kuiba hio mimea? , lakini hao wazee wote angalau wote wapo juu ya levo ya kuipita dhiki katika moto wa njano , kuna kumi ambao wanalinda hili jengo kwa mwaka mzma na wote wapo juu ya levo ya kuipita dhiki katika Maji ya barafu”
Kuna levo tatu za maji , maji ya kawaida , maji ya barafu yaani kugeuza maji kuwa barafu na maji ya kiroho, unaweza kufikia vyote kwa wakati mmoja yaani unaweza kuwa na uwezo wa maji ya barafu ila ukawa huna uwezo wa moto wa rangi nyeupe na unaweza kupata ufunuo wa maji ya kiroho lakini ukakosa ufunuo wa moto wa bluu au mweupe.
Ukweli ni kwamba ukishaipita dhiki unakuwa na uwanja mpana na unaweza kubahatika kupata ufunuo wowote bila mpangilio.
Roma sasa ashakwisha kupita levo ya maji ya kiroho na sasa alikuwa katika ufunuo wa kuunganisha maji ya kiroho na moto wa kiroho na kutengeneza siraha ya kijini ya tufe la bluu.
“Mr Roma nakushauri uondoke hapa mapema , ni muhimu zaidi kumuokoa Rufi kuliko kuchukua hio mimea, isitoshe huwezi kutengenza vidonge”
“Nani kasema siwezi kutengeneza vidonge , ninaweza , ni kwamba tu sio staili yangu kuacha vitu vya thamani nyuma , sina mpango wa kurudi tena hapa nikishaondoka hivo nataka niwatie hasara ya kutosha”Aliongea Roma na kumfanya Sui kutoa macho na kupanua mdomo kwa mshangao akijiuliza au hajamsikia vizuri.
“Sui unaelewa hili jengo lilivyo , je nikipigana na hao majini wa levo ya juu ya dhiki yule mwanamke kule nje anaweza kuhisi?”
“Siwezi kuongea kwa uhakika kwasababu kuna safu ya formation ya mwanga wa kijini ambayo hutumika kama ulinzi , ile formation inazuia nguvu zote ndani ya jengo hili kutotoka nnje ili kuruhusu utengenezaji wa vidonge kuwa mzuri , nadhani majini ambao wapo nje ya hili jengo hawawezi kuhisia chochote labda uliharibu”
Roma alitingisha kichwa na kuridhika na jibu lake na palepale alifungua hifadhi yake ya anga kwa kutumia pete na kisha alianza kutoa nguo za kike na kumpatia Sui.
“Vaa hizi , ijapokuwa wewe ni mkubwa kwangu lakini sioni ni vizuri kuwa nusu uchi mbele yangu”Aliongea Roma na kumfanya Sui sasa kuelewa kumbe alikuwa uchi kwani manyonyo yalikuwa nje na mapaja yote.
Roma nguo hizo zilinunuliwa na Edna kipindi walipokuwa Korea na kwasababu Edna hakutaka kubeba begi walizitupia kwenye hifadhi ya pete na hawakukumbuka kuzitoa , kulikuwa na nguo nyingi sana lakini kwa bahati nzuri zimepata matumizi kwa wakati huo,
Sui alishikilia fasheni yenye katuni mbele yake pamoja na skeri fupi na aliona ni nguo za kushangaza , pengine ni kwasabu ni wa ulimwengu huo lakini hakufikirai sana.
Wakati anabadilisha Roma alimpa mgongo na baada ya kubadili alishindwa kumwangalia Roma usoni na kutoa kicheko cha aibu na Roma alijiambia kumbe majini ni kama bindamu tu.
Edna alikuwa mrefu kuliko Sui hivyo shati lilionyesha kitambi lakini hakuwa na muda wa kufikiria angalau kwa muda huo amejisitiri.
“Sui nnitakutorosha kwenye huu ulimwengu na kupeleka ulimwengu wa kawaida sehemu ninayoishi mimi, je upo tayari?”
“Mr Roma naweza kuishi ulimwegnu wa kawaida!!!”Aliuliza kwa mshangao.
“Ndio unaweza , ijapokuwa huyo mwanamke hapo nje ana nguvu kubwa ya kijini lakini hawezi kunizuia yeye peke yake”
Roma hakuwa akidanganya Ajuza mlinda geti alikuwa na levo ya juu sana , alikuwa juu ya levo ya kupita dhiki katika kudhibiti maji ya barafu.
“Basi nitakusikiliza kwa utakachokuwa unaniambia na kukifanya”Aliongea
“Huna haja ya kufanya chochote , wewe kaa nyuma yangu na tukishatoka kwenye hili jengo nitakushikilia ili tuweze kukimbia kwa spidi”
Baada ya kukubaliana Roma alijibadilisha na kuwa Zilha palepale na kisha akamchukua Sui na kuanza kushuka nae kuja chini
Baada ya kufika katika floor ya chini ambayo huhifadhia mimea Roma alichunguza na uwezo wake na aliweza kugundua kuna wazee wawili ambao wapo levo ya kutengeneza moto wa rangi nyekundu na mmoja akiwa na uwezo wa kutengeneza moto wa njano.
Walikuwa wakipangilia mimea kuligana na kanuni na ilionekana ndio ilikuwa imefika na walishangaa mara baada ya kumuona Zilha na Sui,
“Master mdogo , inafanya nini hapa?”Aliongea jini yule ambaye ana uwezo wa moto wa njano na wote kwa pamoja walimsogelea Roma kumpa heshima , hawakuelewa kama ni feki na Roma aliona hio ndio nafasi adhimu kwani palepale aliita chungu na kikatokea nyuma yao bila ya kutoa mkandamizo na ndani ya dakika chache kilianza kupanuka saizi ya kuweza kumeza wote wawili na walijikuta wote wakigeuka na Roma aliishia kutoa tabasamu la kishetani.
“Master,,, wewe.. Zilha!!”
Wote walijikuta wakipagawwa na palepale walianza kuvutwa kuelekea ndani ya kile chungu.
Roma palepale aliachia uwezo wake wa juu wa mapigo mzunguko tisini na tisa ya radi ambayo majini wenyewe wanaita Radi ya kitai na palepale aliunganisha na nguvu ya andiko la urejesho na kabla hata hawajapambana wote walitumbukia
“Nyam!! , Nyam!!’
Roma aliweza kuona kivuli cha mmyama wa maafa akitafuna kama vile Mamba mkubwa na ndani ya sekunde nguvu yao yote ilifyonzwa na chungu cha maafa na nguvu nyingine ilienda kwa Roma.
Ijapokuwa walikuwa levo ya kuipita dhiki lakini nguvu yao ilikuwa kidogo tu kwa Roma lakini haikuwa mbaya sana , Roma alikuwa amepitia mapigo tisini na tisa ya radi na hao wazee waliikuwa wamepitia awamu moja tu ya radi.
Roma mara baada ya kugeuka nyuma alimuona Sui alikuwa akitetemeka kwa hofu huku akiangalia lichungu linaloelea na kufuka moshi ambalo limemeza watu kwa mshituko mkubwa.
“Usiogope , hii ni Dhana yangu , kwanzia sasa nitafagia kila floor na kubeba kila kitu , wakija kushtuka hamna kitu”Baada ya kuongea palepale aliingia kazini na kuanza kukusanya mimea na kutupia kwenye shimo lake na hakusahau kutoa pete za wale wazee na kuangalia kama kuna chochote lakini Roma alikunja sura baada ya kuona kumbe walikuwa masikini tu maana hamna chochote.
Kwasababu yule Ajuza hajahisi chochote Roma alipumua kwa ahueni na kuelekea floor inayofuata.
Awamu hio alikumbana na jini ambalo lilikuwa bize kutengengeza vidonge na ilionekana halikutaka bughuza ndio maana limejitenga , lilikuwa kwenye levo ya kupita dhiki na alikuwa amewasha moto wa rangi nyekundu.
Kumbuka nikisema moto wa njano ni ule moto wa kawaida unaoona , moto wa bluu ni kama ule unaoona kwenye gesi na rangi nyingine , sasa moto wa rangi nyekundu ni aina ya moto wa kijini ambao unafanana na rangi ya volkano ile lava yake inayoruka.
Moto wa rangi ya njano wa kijini sio wa kawaida una uwezo wa kuyeyusha chuma cha kawaida, ki ufupi kila rangi ya moto sio ya kawaida kama moto unaonekana kwa macho ya kawaida ni moto wa kimaajabu lakini unafuata kanuni za rangi ya ‘flames’ za moto.
Roma mara baada ya kuona huyo mzee akiwa bize alitabasasmu kwa dharau maana mzee yupo bize kama vile anatengeneza vidonge vya maana kumbe daraja la kwanza , alichoshukuru Roma ni kwamba yupo peke yake hivyo kudili nae haikuwa tatizo.
Roma bila hata ya kuongea neno alipotea aliposimama na kutokezea mbele yake , alikuwa amempa mgongo hivyo hakuona ujio wa Roma na palepale alizalisha donge la maji ya kiroho na kumpiga nalo utosini na palepale mzee yule bila hata ya kushtuka alianza kuyeyuka kwa haraka sana , hakuweza hata kutamka neno.
Maji ya kiroho mara nyingi ni kama tindikali au Acid tena zaidi ya Acidi maana inayeyusha mpaka mifupa.
Sekunde chache tu yule jini mzee alikuwa ashayeyuka na kilichosalia ilikuwa ni nguvu yake ya kijini Roma aligeuza kichwa chake kuangalia roho ya mnyama iliokuwa ndani yake na mara baada ya kukutanisha na macho ya Roma ilijificha eti, lakini Roma aliruhusu chungu kile kiifyonza maana haikuwa na ubora mzuri.
Roma mara baada ya kumaliza aliangalia chungu ambacho kilikuwa kikitumiwa na lile jini kutengengezea vidonge , kilikua ni kidogo mno kuliko cha kwake.
Roma alipatwa na tamaa kutaka kubeba kile chungu lakini aliona tayari anacho tena cha kwake kikiwa na roho ya mnyama ambaye hafi hivyo palepale aliita moto ambao ulikuwa katika rangi ya Zambarau , huo moto ulitokana na yale mapigo ya radi na Roma alifanikisha kuutengeneza mara baada ya kuunganisha shoti za radi na moto wa bluu.
Kile chungu ilichukua dakika chache tu kilishayeyuka na kuacha ujiuji chini ambao ulianza kupeperushwa na upepo na hakukubakia na ushahidi wa aina yoyote.
Jini Sui aliekuwa akiangalia hayo yote alijiuliza Roma ni nani , yaani ameua jini wa levo ya maji ya barafu na pigo moja tu na kisha akayeyusha Cauldron ndani ya sekunde , aliishia kumwangalia Roma kwa hofu na uwezo wake angalau sasa ulimpa ile hali ya kujiamini kwamba anaweza kurotoka katika eneo hilo bila shida.
Roma alikitanguliza chungu awamu hio bila hata ya kufika katika floor na kilimeza kila kiumbe kilichokuta , majini wengi ambao wapo levo ya nafsi na mwanzoni mwa levo ya kuipita dhiki walimezwa.
Wengi wao hawakujua hata nani katuma chungu hicho kwani kiliwameza tu bila ya taarifa na Roma alifika kazi imeisha.
Roma mara baada ya kupiga chabo kuangalia hifadhi yake ilivyojaa mimea alijikuta mwili ukimsimka.
Ni hivyo tu alikosa kitu kama tunda la damu ya finiksi kutengengeza vidonge vya daraja la juu sana vya kihistoria.
Kilichomfurahisha Roma zaidi ni mara baada ya kupata Dhana kibao za daraja la kati na la chini , ijapokuwa zilikuwa za uwezo mdogo lakini alikumbuka ana warembo na akiwapa zingewasaidia sana.
Upande wa Sui aliishia kumeza mate mengi , wakati akimwangalia Roma akichagua Dhana hizo kama vile ni takataka.
Katika ulimwengu wa kijini ondoa madini , aondoa hela na utajiri wowote hivyo kwao ni material thing , kitu cha thamani kwa majini ni Dhana halafu inafuatia vidonge.
Kuna majini yana zaidi ya miaka mia mbili hayajawahi kugusa kabisa Dhana sembuse Sui ambaye alikuwa kijakazi tu, ndio maana alimwangalia Roma kwa mshangao.
Mpaka Roma anafika chini alimaliza majini yote kama hamsini hivi , yaani kama ni hasara ni hasara ya maana na hakuishia kuiba dhana tu alibeba mpaka vitabu, ijapokuwa vimejaa mbinu za kichawi lakini aliona kama watependa kujifunza basi asingewazuia.
Roma mara baada ya kufika sasa floor ya chini sasa akiwa amekwisha kuridhika kuwatia hasara Kekexil alimpa ishara Sui kusogea karibu yake wakati wakielekea getini.
Baada ya geti kufunguliwa Sui machozi yalimtoka , kwa miaka saba hatimae amevuta hewa ya oksijeni safi na kuona mazingira ya nje kwani lile gereza ilikuwa ni giza tupu,
“Simameni hapo hapo!!”
Sauti ya yule bibi ilisikika huku mkandamizo wa hewa ukiongezeka kwa kasi na ilikuwa ni kama vile milima inaporoka au wingu linashuka chini.
Ajuza ambaye alikuwa akilinda geti hilo kwa muda mrefu sana hatimae Roma aliweza kuisikia sauti yake na kufumbua macho na kumwangalia Roma kwa macho makali mno.
“Bibi namtoa huyu m*laya nje nina shughuli nae”Aliongea Roma akiigiza tabia ya Zilha.
“Sijapokea maagizo yoyote kutoka kwa Menui mkuu namba moja wa miliki , huwezi kumtoa mfungwa nje”Aliongea kwa sauti kali kweli ya kuumiza masikio kama vile sio mzee.
“Bibi huyu hawezi kukimbia maana nampeleka nyumbani , , naomba uniruhusu”
“Zilha Mohi, hebu niambie tarehe yako ya kuzaliwa na siku?”Aliongea yule kizee na kumfanya Roma kushangaa,
“Bibi unamaanisha nini kusema hivyo!?”Roma alijiuliza mbona maigizo yake yalikuwa vizuri tu kwanini amemshuku.
“Unaniuliza namaanisha nini? , ngoja nikuambie Zilha hajawahi kuongea bila heshima mbele yangu wala kuniomba , umetoa wapi uthubutu wa kuongea kijeuri mbele yangu tena unaenda mbali na kuomba wewe ni Zilha kweli!?”
Roma alitukana ndani kwa ndani ashajua ni wapi amebugi , kumbe yule mpuuzi alikuwa akimheshimu huyo Ajuza.
“Wewe ni nani?”Swali lilimtoka Ajuza huku mkandamizo wa nguvu ya kijini ukimtoka na palepale sasa Roma aliweza kujua ni levo gani , alikuwa levo ya maji ya kiroho na kwasababu alionekana kuwa mzee nguvu yake ya kijini ilikuwa ni ya kutisha mno.
Mkandamizo ule wa nguvu ya kiroho ulimfanya hata Sui kutema damu chini maana sio ya kawaida na Roma palepale alichia nguvu zake za kijini na kumlinda.
Unafikiri Roma atachoropoka hapo.
ITAENDELEA JUMAPILI.
Ok
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

BY SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 725.
Tulipoishia Roma anaingia katika mtego wa Jini Anjiu na kumfanya afanikishe kupitia mapigo ya radi kwa kutumia Chungu chake na baada ya tukio hilo anajigamba kwa kumwambia Roma kwamba amemshindwa na hamuwezi tena kutokana na uwezo wake.
Roma alijua palepale alichokuwa akifanya Anjiu ni mashambulizi ya kimaneno ili kumfanya asijiamini , Roma alijua uwezo wake ulikuwa umeongezeka sana hivyo haikumaanisha moja kwa moja alikuwa amepoteza pambano.
Lakini sasa baada ya kuona namna ambavyo amechezewa akili na Anjiu alishindwa kujizuia na kuonyesha hasira waziwazi.
“Nani kapoteza?, sio kwa namna unavyofikiri , ingawa umeweza kuivuka Dhiki, kwa upande wangu nimefaidika sana na huna uwezo wa kushindana na ukubwa wa nguvu yangu ya ukweli ya nishati za mbingu na ardhi….Kwamba ndio nini sasa kama umweza kupita levo ya Dhiki ya radi .je unao uwezo wa kutengeneza siraha za kimaajabu ninazo tengeneza mimi?, hio mbinu yako unayojivunia nayo ya moto wa ndege na radi yako ya Zambarau haviwezi kuniua zaidi ya kunisababishia maumivu tu au unataka kuonja radha ya moto wangu mweusi?”
Anjiu uso wake ulijikunja baada ya kushangazwa kidogo na namna ambavyo Roma hakuingia kwenye mtego wake wa maneno ili kumfanya asijiamini.
Jini huyo alijua licha ya kwamba alikuwa na uwezo mkubwa katika kujifunza mbingu za nishati ya mbingu na ardhi alijua Roma angepatwa na hofu kutokana na maneno yake.
Alionekana kutokujua kitu kimoja kuhusu Roma, malezi yake yalikuwa ya tofauti kabisa na binadamu wa kawaida , katika maisha ya Roma maisha yake yote ni kupambania maisha yake na hicho ndio alichokuwa akielewa na siku zote aliamini kushindwa maana yake ni kifo hivyo ni ngumu sana kukubali kushindwa kirahisi.
Hata Athena ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kumfanya kuwa na adabu hakuwahi kukubali kushindwa na Athena na alijua siku moja tu lazima na yeye amshikishe adabu.
Sasa kama hamuogopi Athena anamuogopaje jini Anjiu ambaye ndio kwanza ameonja radha halisi ya mapigo ya radi jambo ambalo yeye alipitia miezi mingi iliopita.
Likija swala la vita hata Anjiu mwenyewe hamfikii Roma hata kidogo kwa uzoefu.
Baada ya kuona namna ambavyo Roma alikuwa hana wasiwasi Rufi aljikuta akipatwa na ahueni vinginevyo angekuwa na wasiwasi na kuona kwamba hawawezi kushinda katika vita hio.
“Sawa tu , kwasababu unajikuta kujiamini sana nitakuonyesha utofauti uliopo kati yako na mimi”
“Askari wa kipepo ungana na mimi!!!”
Dakika ileile ambayo aliongea lile pepo ambalo lilikuwa limejigawa kutoka kwenye mwili wake lilimrudia kama kivuli na kuwa mtu mmoja.
Ghafla tu mkandamizo wa nguvu za mbingu na ardhi wa Jini Anjiu uliongezeka kwa kiasi kikubwa sana kwa zaidi ya asilimia therathini.
Ijapokuwa Roma alikuwa na utulivu lakini alishangazwa na namna ambavyo uwezo wa Anjiu ulivyoongezeka kwa sekunde.
“Uwezo wangu wa kijini kama nilivyokwisha kukueleza nilikuwa nimeupunguza na kuuhifadhi katika Askari pepo wangu , kwa sasa nishapitia Dhiki hivyo sina hofu ya kumiliki uwezo wangu wote, halafu bado tu unajiona unao uwezo wa kunishinda?”
Roma aliishia kutoa tabasamu la kejeli na bila ya kuongea neno lolote alitumia Chungu cha maafa ambacho kilikuwa kikizunguka angani ili kumshikilia Anjjiu mwili wake.
“Hakuna utofauti wowote wa namna ulivyokuwa na nguvu , kadri unavyokuwa na nguvu ndio vizuri zaidi kwangu kwani nitakuua na kutumia nguvu zako kama virutubisho”Aliwaza Roma.
Anjiu alikuwa katika kiwewe , alijua kwa kuunganisha uwezo wake wote ingemfanya Roma kuogopa na kuacha vita na yeye lakini Roma hakuwa na dalili ya kuacha kabisa vita hio.
Kitu ambacho hakuwa akikijua Anjiu ni kwamba mbinu yake ya kutumia pepo kama namna ya kukuza uwezo wake wa kijini Roma alikuwa anaijua sana hio mbinu kwani alibahatika kuingia katika ulimwengu wa majini pepo.
Ulimwengu ambao majini huvuna nishati kwa ajili ya kuamsha mapeppo yao ya ndani tofauti na kuyamaliza kama ilivyokuwa kwenye ulimwengu wa majini watu.
Ijapokuwa uwezo wa pepo lake ulikuwa na nguvu lakini ukweli ni kwamba faida ya kutumia pepo ni katika kujiimarisha katika utimamu wa kimwili tu na sio katika kufanya mashambulizi.
Ndio mara nyingi faida kubwa ya majini ambao wanatumia mbinu ya kuamsha mapepo yao ya ndani ni kwamba wanakuwa na miili yenye nguvu mno.
Hivyo Roma alijua Askari pepo huyo alikuwa akimtumia tu kama vile ni Dhana ya kuhifadhia nishati mbingu zake lakini pia kumuwezesha kupitia levo ya Dhiki.
Kitu kingine ni kwamba licha ya Anjiu kuwa na uwezo wa kutumia pepo lake lakini msingi wake wa nguvu za kijini sio ule wa majini pepo , yeye alitumia sehemu ya nguvu zake za kijini katika kuamsha pepo lake lakini majini pepo wenyewe hawatumii sehemu ya nguvu zao katika kuvuna nishati bali uwezo wao huongozwa na pepo kikamilifu.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Anjiu yeye pepo lake alilitumia kama Dhana ya kumsaidia katika mashambulizi lakini majini pepo wao pepo ndio uhalisia wao.
Chungu cha maafa kilikuwa kimeongezeka uwezo wake maradufu tofauti na ilivyokuwa mwanzo kabla ya kumeza nishati ya radi.
Kutokana na asili ya chungu hicho kuwa na nguvu ya giza kiliweza kumuona Anjiu kama chakula bora kabisa kula hivyo kilianza kuonyesha makali yake na kutaka kummeza.
“Shit!!”
Anjjiu mara baada ya kuhisi mvuto mkubwa kutoka kwa chungu hicho aliishia kutoa tusi na palepale alijitahidi kujitoa katika eneo hilo ili kuondoka katika mvutano huo kwa kutumia uwezo wake lakini ilionekana kuwa ngumu.
“Alama ya mkono ya Daloshoo..!!!!”
Anjiu aliinua mkono wake mmoja juu angani mara baada ya kutamka kauli hio na palepale alama za kimaandishi za michoro(runes) zilichomoza zikiwa na mwanga wa kustaajabisha hewani na sekunde ileile zote zilijikusanya pamoja na kutengeneza umbo la Alama ya mkono(handprint).
Vidole vya mkono ule vililikuwa vimetawalia na elementi zote tano na nguvu ya mbingu na ardhi ilitoka kwenye vidole vile kama vile mlango wa bwawa la maji umefunguliwa.
Chungu cha maafa palepale kilisogelea kwa kasi alama ile ya vidole na kwenda kupigana na ile nguvu lakini kilishindwa kufika kwani alama ile ya vidole vya Daloshoo vilikuwa na nguvu kubwa ya msukumo.
Kutokana na chungu kushindana na nguvu ile ya alama Anjiu palepale alitumia fursa ile kujichomoa katika ile kani ya mvutano na kuanza kumshambulia Roma.
Kutokana na Roma kumshikilia Rufi na mkono mmoja hakutaka kumsogelea Anjiu karibu hivyo palepale alitengeneza moto wa rangi ya Zambarau na kuanza kumshambulia nao.
Mara baada ya mashambulizi yao yote kukutana kati ulitokea mlipuko ambao uliangaza eneo lote lakini muda ulule Roma aliongeza mashambulizi ya kasi zaidi na kitendo cha Anjiu kuchelewa kwa sekunde tu mashambulizi ya Roma yalimfikia na kutokana na kasi yake alishindwa kutoa shambulizi la kupangua na aliishia kuruka na kukwepa shambbulizi lile.
“Scorching sun and fire rain!!!”(Jua la kuchoma na Mvua ya moto).
Dakika ileile mwili wa Jini Anjiu uligeuka kwa mara nyingine na kuonekana kama vile ni malaika wa moto wa jua na palepale mwili wake ni kama vile nguo ilioloana inayokun’gutwa kwani matone ya moto yalimtoka na kwenda kumvaa Roma kama vile ni matone ya mvua.
Mvua hio ya moto ambayo imetokana na mbinu ya Golden Crow ilikuwa na spidi kubwa mno tofauti na Roma alivyofikiri, katika spidi ya kupepesa jicho walikuwa washafikiwa na moto ule na kufunikwa.
Licha ya Roma kutengeneza ngao ya moto wa Zambarau lakini moto ule uliweza kupita lakini Roma hakutaka kuumia kizembe hivyo alitengeneza maji ya Kiroho kushindana na moto ule lakini wakati huo akijua hio sio nia kamilifu ya kuweza kushindana na moto huo hivyo bahati nzuri ni kwamba Chungu hakikuwa na matumizi hivyo alikipa maelekezo kupitia fahamu zake na kumshambulia Anjiu.
Anjiu ni kama alikuwa amejiandaa kwani wakati Chugnu kinaanza kumsogelea alituma shambulizi la moto kwenda kukipiga na alionekana kufanikiwa kumaliza kasi yake ya kumsogelea kwa muda na aliishia kutoa sauti ya chini ya kuzomea na ngurumo kama vile alikuwa amechangayikiwa.
Mara baada ya kupita dhiki ya radi tisa uwezo wa mbinu yake ya Ndege wa Dhahabu na yenyewe ilikuwa imeimarika mno.
Roma alishikwa na huzuni ya ghafla na kujiambia kama angekuwa na uwezo wa kudhibiti radi kama siraha angekuwa ashamaliza pambano hilo muda tu.
Ijapokuwa aliweza kupata mashambulizi matatu ya radi lakini bado hakuwa na uelewa wa namna ya kuidhibiti radi na kuitumia kama siraha na alijua kama mashambulizi ya namna hio yataendelea atashindwa kumlinda Rufi na atashindwa kutoka hapo akiwa hai.
“Daloshoo safu ya elementi tano!!”
Ghafla tu safu tano za mwanga wa vidoti doti zilitokeza katika pande zote na mara baada ya kumfikia Roma zilimzingira na kutengeza umbo la nyota kwa staili ya kumuweka katikati.
Roma alijikuta akishngazwa na jambo lile na kujiuliza ni mbingu gani hio , inakuwaje jini huyu kuwa na safu nyingi za siri namna hio.
Roma kabla hata hajajua kinachoendelea lile umbo la nyota lilianza kutengeneza rangi za ajabu na kuanza kuzunguka kwa spidi kubwa na kuanza kutengeneza kimbunga cha rangi na kumfanya ashindwe kuona kinachoendelea kwa nje..
Roma alishangazwa na jambo lile na kugundua uhatari wa mbinu hio na hakutaka kufanya ujinga na palepale aliita chungu ili kuanza kuanza kunyonya nguvu ile
Kimbunga kile kilipunguza spidi na Roma alitumia nafasi hio kutengeneza moto wa rangi ya Zambarau na kupiga umbo lile la nyota. Na hatimae alifanikiwa kutoka katika kimbunga kile ambacho kilikuwa kimemznigira kwa kumuweka kati.
“Ndege wa Dhahabu , Mkuki wa kiuungu!!!”:
Ilikuwa ni kama vile Anjiu alitegema Roma kitu ambacho atafanya na alikuwa akisubiria nafasi hio na palepale moto wake uligeuka na kutengeneza umbo la mkuki na kutokana na Roma kuchelewa na kutotegemea shambulizi lile hakuwa na muda wa kukwepa na aliishia kumshika Rufi na kugeuka ili kuruhusu mkuki ule kumchoma mgongoni wakati huo mwili wake akiuzingira na nguvu ya kiroho.
“Boom!!!”
Mkuki ule ulilipuka lakini cheche zake ziliweza kupita katika ngao ya Roma na kufikia mwili wake kwa nguvu ya kutosha , kama mwili wa Roma usingekuwa timamu basi palepale angegeuzwa kifusi cha nyama.
“Hubby!!!”
Rufi masikio yake yalikuwa yakigonga kengele na aliishia kutoa kilio kuliita jina la mpenzi wake tu.
Lakini aliishia kutemewa damu nyingi usoni na Roma, Maumivu alioyaskia katika mgongo wake iikuwa ni kama vile viungo vya ndani ya mwili vimegeuzwa mshikaki , ngozi yake iliungua katika kiwango ambacho hakuwa akihisi maumivu tena.
Akili yake ilimpotea kwa sekunde kadhaa , ilikuwa ni kipindi kirefu kidogo kupitia maumivu kama hayo na Roma hakuwa ameyazoea kabisa na palepale alijua kabisa mtu ambaye anaweza kumpatia shambulizi hilo basi anao uwezo wa kumuua pia.
“Duuh bado upo hai tu , hakika mbinu yako ya andiko sio ya kawaida”Jini Anjiu kwa mara yingine alijikuta akionyesha mshangao wake waziwazi.
“Ungeachana na huyo mwanamke pangine ungekuwa na uwezo wa kushindana na mimi lakini nikuambie tu huna uwezo wa kunishinda ukiwa utaendelea kumlinda”
Roma akiwa katika hasira aligeuka kwa spidi akiwa na moto wake wa rangi ya samawati na kumrushia anjiu na Anjiu hakuwa mzembe kwani kwa kupigisha kiganja chake hewani tu moto wake wa ndege wa Dhahabu uliweza kuzimisha shambulizi lile.
“Hata kama umeweza kunyonya nishati ya radi bado hunniwezi , nina mbinu ya moto wa Ndege wa Dhahabu licha y moto wako huo wa kimbingu na wa kiroho haileti tofauti yoyote na mashambulizi yako hayawezi kuwa na madhara kwangu na ninazo mbinu nyingi za kukushinda , ijapokuwa Cauldron uwezo wake ni mkubwa lakini bado uwezo wake ni wa kati , kitendo cha kupitia mapigo ya radi kimeleta mshituko katika ulimwengu wote wa majini na wazee wakubwa watafika hapa muda sio mrefu kujua nini kinaendelea na muda huo huotokuwa na nafasi ya kujiokoa tena nakushauri nipatie andiko la urejesho na mimi kama mkuu wa miliki ya Xia nitakuachia huru wewe na mwanamke wako kuondoka”
Licha ya maumivu ya Roma kupona kwa kasi lakini maneno ya Anjiu yalimshitua kidogo na aliishia kutoa tabasamu na kutoa meno yake ambayo yamechafuka na damu.
“Ushapitia mapigo ya radi lakini bado unahitaji mbinu yangu?”
“Hakuna ambaye anaweza kukataa mbinu nzuri ya mafunzo , tunataka kujua ni kwanini mwili wako ni imara namna hio?”
Ukiachana na uwezo wa Roma kupona haraka kutokana na mbinu ya andiko, majini hao wanajua utimamu wa mwili wa Roma umetokana na nguvu za kijini, wasichokijua ni historia kamili ya Roma.
Roma ni sehemu ya matokeo ya projekti LADO na ndio iliomfanya kuwa na mwili wa namna hio , hata kama hatumii mbinu hio ya andiko virusi ambavyo vipo katika mwili wake vikiamshwa uwezo wake wa kupona unakuwa mkubwa.
“Kama haya yataendelea nafasi yangu ya kushinda itazidi kushuka , leo nilifanya makosa , sikutegemea Anjiu kuwa na hila namna hii , nimekuja hapa kumuokoa Rufi na nilichotaka ni kumlipia kisasi lakini nadhani kwasasa bado mpaka nitakapoweza kudhibiti radi”Aliwaza Roma huku akiwa katika hali ya kimaamuzi ya kutaka kuondoka na kuachana na maswala ya kupambana.
Lakini sasa dakika ambayo alikuwa akijiandaa kukimbia aliweza kuhisi nguvu za aina sita za mbingu na ardhi kubwa zikisogelea eneo hilo kutoka pande zote , ni nguvu za majini ambao wapo katikati mwa levo za maji ya upako na mwishoni.
“Kwanini ndio unataka kuondoka ilihali ndio wazee wetu sita wamekwisha kufika, unadhani unaweza kuondoka kirahisi hivyo?”
Roma uso wake ulizidi kuwa mweusi na Rufi aliishia kumwangalia Roma kwa wasiwasi na alishiia kujilaumu kwa kuwa mzigo kwake na Roma ni kama alishajua Rufi alichokuwa akiwaza na alimwangalia kwa tabasamu.
“Usiwe na wasiwasi nilishakuambia nitakulinda kwa namna yoyote ile”
“Hehe … mnao muda tu wa kuonyesheana mapenzi ?”Aliongea Anjiu kwa kejeli.
Kwa jinsi nguvu za majini wengine wakubwa waliokuwa wakisogea hilo eneo ni kama wanatengeneza duara kwa kila mtu kuwa na uwezo wa kulinda kilomita kadhaa za eneo lake , ilikuwa ni kama vile wanafanya ushirikiao kwa kuhakikisha hakuna kitu kinachowapita.
Kufumba na kufumbua hatimae Roma aliweza kuona sura za wanaume watatu majini wa makamo , wazee wawili na mwanamke mmoja wa makamo.
Mwanamke pamoja na Mzee alievalia joho rangi nyeusi kwa pamoja uwezo wao ilikuwa mwishoni mwa levo ya maji ya kiroho kama ilivyo kwa Anjiu na ilionyesha muda wowote wangeweza kupitia Dhiki ya radi.
Majini wengine wanne wote waalikuwa na uwezo sawa na wa Ajuza Tigola wa miliki ya Kekexi.
Ukubwa wa miliki ya Xia hatimae ulikuwa wazi na Roma alijua ongezeko la hawa majini ni tishio kwake.
Majini wa miliki ya Xia walishia kutoa shangwe za utukufu mara baada ya ujio wa wazee hao wa miliki.
Yaani ukisikia baraza la wazee ambalo ndio uchangua nani awe kiongozi wa miliki basi huundwa na hao majini ambao wote wapo katika levo ya maji ya upako.
Majini wale wote mara baada ya kumwangalia Roma kwa macho yaliojaa utukufu waligeuza sura zao na kuangalia lijichungu ambalo lilikuwa likizunguka hewani kwa maringo na walionyesha mshangao wa waziwazi na palepale waligeuza sura zao na kumwangalia Anjiu.
“Anjiu umefanikiwa kuingia levo ya Dhiki ya radi ya mapigo tisa?”Mzee ambaye alikuwa mwishoni mwa levo ya maji ya upako aliongea.
“Ndio babu nimeweza kupata Epifania muda mfupi uliopita na kuweza kushinda jaribio”
Ilionekana huyo mzee alikuwa ndio babu yake Anjiu , kwa umri wa Anjiu ungeshangaa kuwa na babu lakini majini umri wao ulikuwa ni mkubwa mno kuliko binadamu.
Roma alikumbuka kauli ya jini Sui kwamba ndio huyo mzee ambaye aliweza kuchukua nafasi ya baba yake Laofi kuwa mkuu wa miliki.
Huyo mzee jina lake halisi ni Senji na ndio ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa Anjiu kuwa na nafasi aliokuwa nao wakati huo.
“Siamini kama umeweza kulipita jaribio , nadhani kwasasa hatuna thamani tena”Mwanamke ambaye alikuwa katika muonekano wa ukauzu aliongea.
“Bibi Sena umeniona nikikua na wewe ni msingi wa miliki yetu, nimepata bahati tu na kila kitu nilichokuwa nacho leo hii ni kutokana na maelekezo yenu tokea nikiwa mdogo.”
Ijapokuwa Anjiu hakuwa kijana lakini alijishusha na kuwa kama mtoto mbele ya wazee hao na kauli yake ilimfanya Sena kujisikia vizuri.
“Ni nani huyu mtoto, uwezo wake wa kijini ni mkuu mno na hilo Jungu lake , Usiniambie ndio chungu ambacho tuliweza kusoma tu katika hadithi?”
“Inaonekana ni chungu cha maafa ndio , huyu binadamu anaonekana kuwa mtoto mdogo lakini ameweza kufikia uwezo huo wa nishati za mbingu na ardhi na hebu angalia mwanamke ambaye amembeba anakiwango kikubwa cha nishati ya Yin , mwili mzuri wa kufanyia majaribio ya vidonge, Anjiu hebu tuelezee hii hali?”Aliongea Senji.
Ilikuwa ni haki yao kuwa katika mshangao wa hali ilivyo kwani hawakuwa katika makao makuu ya miliki kwa miaka mingi na hawajui ambacho kilikuwa kikiendelea.
Anjiu mkuu wa miliki alielezea tukio zima kwa kusema Roma ni binadamu mwizi ambaye amevamia miliki yao na kumuua Lao mtumishi na mzee Laofi na kundi la majini wa levo ya maji ya meupe na barafu na hakuishia hapo tu alielezea na kilichotokea miliki ya Kekexil.
Malezo hayo yote yaliwafanya wale wazee kupatwa na hasira ya kutaka kumchuna ngozi Roma.
“Haha… Panas na Xia hatujawahi kukwaruzana , nimekuwa mbali na miliki kwa miaka hamsini hadi sasa lakini miliki yetu imevamiwa na mtoto mdogo tena binadamu , Anjiu hii ndio namna ambavyo unaongoza hii miliki?”Aliongea Senji.
“Huyu mwanaharamu uwezo wake ni wa ajabu, sio tu kwamba mwili wake sio wa kawaida lakini pia anao uwezo wa kutengeneza maji ya kiroho , moto wa kiroho na moto wa bluu siraha ambazo mashambulizi yake ni makubwa mno kuliko za kwetu , sio mwepesi kudili nae”
Baada ya kusikia maelezo hayo wazee hao walijikuta wakishangazwa lakini kwa wakati mmoja tamaa zilianza kujitengeneza katika nyuso zao.
“Imetosha kwa huu ujinga , kamata huyu mtoto na chukua mbinu yake , mlazmishe pia kutueleza namna ambavyo amefanikiwa kujifunza kwa muda mfupi , huyo mwanamke pia chukua na awe ni kifaa rasmi cha majaribio , kulingana na hadithi katika kumbukumbu zetu Chungu cha Maafa ndio kilitumika kumfungia mnyama wa machafuzi aliewahi kuwepo , ni Dhana ya kikale ya mababbu zetu , hazina ambayo inazidi Dhana zote , tukiwa nayo haitokuwa ngumu kuunganisha miliki zote na kuwa chini yetu kama Anjiu utatumia uwezo wako kuiendesha”Aliongea moja wapo ya wale wazee.
“Umeongea pointi, angalau kwa wakati huu tumepata kitu cha thamani”Aliongea Sena kwa tabasamu la furaha.
“Huyu mtoto uwezo wake sio wa kuchukulia poa lakini pia kushindana na chungu cha maafa sio rahisi , kwanini tusishambulie wote kwa pamoja na kumfanya asiwe na nguvu?”
Wale wazee wote waliangaliana na kisha wakatingishiana vichwa kuonyesha ishara ya makubaliano na ilionekana washaamua na kuona hio ndio mbinu rahisi ya kumdhibiti Roma.
Wakati huo walikuwa wakiendeshwa na tamaa, kwanza kupata mbinu ya Roma ya mafunzo , pili kumkamata Rufi ili kuwa kifaa cha majaribio na tatu kubwa kuliko yote kupata Dhana ya kilijendi ya Chungu au Sufuria la maafa.

SEHEMU YA 726.
Roma mara baada ya kusikiliza maneno yao aliishia kushikwa na hasira na aliona kabisa hao wazee wa kijini hawakuwa kabisa na aibu, yaani licha ya kuwa na umri zaidi ya miaka elfu mbili kama utawaunanisha wote lakini bado wanapanga kushambuliana na yeye ambae ana miaka ishirini kupanda.
Ukweli ni kwamba kwasababu ya wazee hao kuishi muda mrefu , hawakujali kabisa maneno ya wengine , kwao aibu sio kitu na wakati huo malengo yao ni kupata kitu cha thamani kilichokuwa mbele yao.
“Mimi na Sena tutashambulia , nyie wanne zungukeni hilo Jungu la maafa na muanze utarafibu wa kulikamata , Anjiu wewe ungana na sisi tumalize hili swala haraka iwezekanavyo”Aliongea Senji ki amri.
“Umeeleweka”
Sena alikuwa tayari katika mkao wa kumshambulia Roma na alitoa nguvu kubwa ya kijini ya andiko la Roshinisutra.
“Joka la sanaa ya wino - Jozi Majoka katika dansi moja!!”
Palepale ghafla tu Kizingia(vortex) cheusi kilianza kumtoka , ilikuwa ni kitu kinachofanana na wiuo wa karamu kama maji maji mazito hivi ambayo yamebeba Aura ambayo sio ya kawaida . ni aura ambayo inafanana nae kabisa.
Sekunde tu wino ule mwingi uligeuka na kuwa nyoka mfano wa Cobra na kuanza kucheza cheza.
Yaani kilichokuwa kikionekana ni kama wale watu wanaocheza na mijoka ikiwa imewazingira mwili, sasa jini Sena alikuwa amezingirwa na majoka mawili meusi kama wino yaliokuwa yamekaa kulia na kushoto yakichezesha vichwa vyao , yalikuwa makubwa mno na ya kuogofya.
Roma hakutaka kuzembea na palepale aligeuza nguvu zake za nishati ya mbingu na ardhi na kuwa moto wa bluu unaofanana na nyoka pia wa rangi ya bluu ili kupambana na zile nyoka za wino.
Sena alikuwa mwepesi mno na palepale yale majoka yake yaliongezeka urefu na kufyatuka kuelekea kwa Roma lakini Roma na yeye alifyatua nyoka zake ambazo zilikuwa katika moto wa bluu na kwenda kupambana.
Kitendo cha nyoka wale wa bluu kugusana na wale wa wino palepale walisambaratishwa na nguvu zao zilizobakia zilimsogelea Sena kwa kasi lakini alikuwa mwepesi mno kwani palepale alitoaDhana iliokuwa ikifanana na mkuki lakini ambayo imemgawanyo katikati kama vile ni Uma ya Tuni(Tuning fork).
“Onja Dhana yangu ya ‘Kilio pepo’”
Jini Sena alikuwa tayari ashafanya miujiza yake na kuifyatua siraha yake ya Kilio cha pepo na kutengeneza wimbi kali la nguvu za kijini.
Roma palepale alizuia shambulizi lile na nguvu zake za kijini lakini shambulizi lile lilikuwa limeambatana na sauti kali za kuchafua akili , ilikuwa ni sauti kali mno za vilio.
“Arghh…!!”
Rufi aliweza kusikia sauti zile pia na alijikuta akitoa yowe na damu kuanza kumtoka midomoni.
Muonekano huo ulimfanya Roma kupatwa na ukichaa , hio siraha ya ‘Kilio Pepo ‘ ilikuwa ni shambulizi la sauti(Sonic attack) ukijumlisha na aura yake iliendana na jina lake.
Roma alijua kama ni hivyo asingeweza kuizuia na alijua ni vizuri kuikwepa kwani kama atakumbana nayo moja kwa moja basi inaweza kuharibu masikio ya Rufi.
Lakini sasa kabla hata hajachukua maamuzi nguvu kubwa ya kijini ilimsogelea kwa kasi na kwa mara moja tu aliweza kuona mamia ya nguvu za kijini ambazo zipo katika rangi , ilikuwa ni kama vile ni nyota katika mstari kutoka angani zinamdondokea.
“Mkondo Nyota …Anguko la ngurumo!!!”
Ulikuwa ni uchawi uliotoka kwa Senji huku macho yake yalikuwa yakiwaka waka kama vile yanaungua na moto na kitendo kile cha kutingisha mkono tu vitu ambvyo vilikuwa katika umbo la nyora vilianza kumdondokea Roma
Roma aliishia kutoa mlio wa sauti huku akigeuza nguvu yake ya kijini na kuwa moto wa Zambarau na kuzingira mwili wake na palepale akituma mashambulizi kushambulia zile nyota na zilisambaratishwa palepale na ni muda huo huo aliita Jungu lake na kwenda kumvaa Sena ambaye alikuwa karibu yake.,
“Unatoa wapi ujeuri huo?”
Sena alishikwa na hasira na ile siraha yake ya Kilio pepo ilianza kuzunguka na kutengeneza mchoro wa kuvutia macho na palepale alianza kuongea kwa sauti kubwa kama wale wachungaji wanaokemea pepo.
“Joka sanaa ya wino –Wino mzito!!!”
Palepale ulifyatuka ujiuji wa wino kama kamba na kwenda kukifunga kile chungu na kuanza kukivutia mbali ili kukipunguza nguvu na alitumia fursa hio kujiondoa katika kani mvutano wake.
Hakuishia kujitoa tu bali aliendelea kuipigisha hewani ile siraha yake na kufyatua mawimbi ya sauti na kumfanya Roma kuyakwepa haraka, ijapokuwa alikuwa na uwezo wa kupambana nayo lakini alifanya hivyo ili kuepusha madhara kwa Rufi,
Anjiu mara baada ya kuona Pambano ndio linaelekea ukingoni kutokana na Roma kuzidiwa na mashambulizi alitoa tabasamu la kejeli na palepale aligeuka na kuwa kama jua.
“Ndege wa Dhahabu wa miguu mitatu , Kusanyiko la ndege elfu moja”
Makundi ya ndege katika mamia mamia yalianza kumsogelea Roma kwa kasi lakini Roma hakuwa akidili na yeye tu , hali ilikuwa inazidi kumuia vigumu zaidi na zaidi.
Huku alikuwa akipambana na mkondo wa nyota , huku anapambana na majoka wino na sauti na kumfanya akose muda wa kukipa chungu maagizo.
Wakati huo sasa Roma ngao yake ilianza kukosa nguvu na ilionekana muda wowote ingeangushwa na mashambulizi ya ndege wale wa moto.
Ilikuwa ni vita ya pata shika kwani majini watatu wa nguvu za juu walikuwa wakimshambulia na kwa mtu yoyote mwenye akili timamu lazima angeona Roma hachomoki kwa namna yoyote ile.
Majini wa miliki hio waliokuwa wakiangalia mapambano hayo kwa mbali walikuwa katika furaha lakini kwa namna moja walimkubali Roma kutokana na namna ambavyo alikuwa akijilinda na mashambulizi bila kusahahu alikuwa na mwanamke amemshikilia na mkono mmoja.
Xiao ambaye alikuwa akiangalia aliishia kushika gauni ake kwa nguvu kama anataka kulichana vile huku michirizi ya machozi ikiwa imepamba uso wake , alionekana alikuwa akimlilia Roma lakini kwa wakati huo hakuwa na cha kufanya kabisa.
“Kwanini nipo hivi , kwanini naumia , si alitaka kuniua , sielewei kadri anavyoshambuliwa naumia mimi?”
Mrembo huyo nusu jini alikuwa katika hali ya maswali mazito akipambana na hisia zake za mapenzi kwenda kwa mwamba Hades.
Roma sasa alianza kuona nguvu zake za mbingu na ardhi zinaenda kombo kwani upande maadui ulikuwa na nguvu kubwa ambazo ni zaidi ya za kwake.
Ingekuwa sio kwa mwili wake kuwa na uwezo usiokuwa wa kawaida basi angekufa.
Haikuwa habari nzuri kwa Roma hio, ijapokuwa alikuwa akipigaina nao kwa maji ya kiroho na moto wa bluu lakini licha ya kutumia Chungu chake matokeo hayakuwa mazuri.
Na alijua akiendelea hivyo anaweza kufanya kosa na kupoteza uwezo wake wa kijini wote au kuishiwa nguvu.
Kilichomsumbua Roma sana wakait huo alijua majini hao bado hawakutumia hata nusu yote ya uwezo wao na hata kama asingekuwa amemshikilia Rufi na kumlinda wakitumia asilimia zote za uwezo wao basi hatokuwa na nafasi tena ya kuwa hai.
“Napaswa kufanya nini?”
Swali liliibuka katika kichwa chake na palepale Roma alikiona kifo chake kikikaribia.
******
Wakati huo huo upande mwingine kusini magharibi mwa miliki hio hio ya Xia alionekana Mkuu wa miliki ya Panas yaani Gefu akiwa amesimama juu ya msitu maili mia moja mbali na pambano linapoendelea.
Alikuwa na muonekano usioelezeka na alikuwa kimya akionekana kuwa katika subira ya jambo flani.
Hakuwa peke yake , nyuma yake walikuwa ni majini wazee Chotara ambao wamevalia kanzu wote kimya wakiwa katika hali ya subira pia.
Majini hao wawili walikuwa ni wanaume na wawili walikuwa ni wanawake wakitengeneza jumla ya majini wanne na mkuu huyo alikuwa ni wa tano.
Ukiachana na majini hao ambao wapo eneo moja nusu kilomita kutoka waliposimama kulikuwa na majini wengine makundi kwa makundi ambao wote wapo katika levo ya maji ya barafu na meupe wakiwa katika hali ya wasiwasi.
Yaani walionekana kama vile wapo katika hali ya tahadhari ya kuingia vitani muda wowote.
Dakika chache mbele alionekana jini ambaye yupo katika levo ya maji meupe akipaa kuwasogelea kutoka chini kuja juu na aliinamisha kichwa mbele ya Mkuu huyo mara baada ya kumkaribia.
Jini huyo alikuwa ni shushu ambaye alikuwa ameingizwa katika miliki ya Xia kwa ajili ya kutoa taarifa ya kila kinachoendelea.
Kutokana na wingi wa majini ambao walikuwa na ruhusa ya kufanya watakvyo katika miliki ya Xia ingekuwa ngumu kukosekana kwa mashushu.
“Kwanini umecheleawa , hali ipoje , nini kimetokea?”Aliuliza Gefu,
“Niwie radhi namba moja , nimechelewa kwasababu hali ilivyo ni ya kushitusha sana , Anjiu ameweza kupita Dhiki ya radi”Aliongea yule shushu katika sauti iliojaa kitetemeshi.
Sekunde ambayo maneno hayo yanatoka mdomoni majini wote waliosikia walijikuta wakishikwa na sura mpauko.
“Roma hali yake ikoje?”
“Hali yake haionekani kuwa nzuri , sidhani kama atadumu kwa muda mrefu , Wazee wote sita wa miliki ya Xia wamefika na kuna uwepo wa Sena jini maarufu wa miaka ile pamoja na Senji mkuu wa miliki aliepita , wazee wngine wote ni wataalamu ambao walipata umaarufu miaka mia moja iliopita ,Roma kamshindwa Anjiu ataweza kupambana nao wote saba? , ijapokuwa anajitahidi lakini ni swala la muda tu kabla hajauliwa au kukamatwa”Aliongea na kumfanya Gefu kuonyesha wasiwasi kiasi lakini alijituliza.
“Nimekuelewa rudi Xia na hakikisha hukamatwi”
“Sawa”
Dakika ileile yule shushu jini aliondoka katika hilo eneo na Gefu aliinua uso wake juu angani akionekana kufikiria jambo.
“Wazee radhi zangu kwenu , inaonekana wote mmekuja hapa bure tu”
“Hatuja poteza muda wetu kuja hapa , kwasababu tushajua mafanikio ya Anjiu hili linamaanisha hata sisi pia tunayo nafasi , lakini elewa baadae nguvu ya miliki ya Xia itakuwa kubwa zaidi hivyo unapaswa kuwa nao makini”
“Sio mbaya , licha ya mipango yetu mikubwa inayoendelea katika ulimwengu wa binadamu lakini pia nguvu za nishati ya mbingu na ardhi ni muhimu pia ili kuimarisha eneo letu , Gefu unapaswa kujifunza kutoka kwa Rozu , tunafikiri huyu msichana ndio tumaini letu kubwa kwasasa katika vijana ambao wataweza kushindana na Anjiu”
“Asante kwa ukumbusho wenu wazee wangu , sitosahau busara zenu”
Wazee hao wanne walinzi wakuu wa miliki ya Panas hawakuongea neno lingine , mpango wao ulikuwa ni kumsaidia Roma lakini mara baada ya kusikia Anjiu ameweza kuvuka Dhiki ya radi uwezo huo wa kumsaidia hamna na Roma anakwenda kufa.,
Hivyo hawakutaka kusikia neno lingine kutoka kwa Gefu hivyo waliamua kuondoka katika spidi ya kupepesa macho na kutokomea.
“Kwahio tunaachana na misheni yetu”
Jini ambaye alikuwa katika levo ya maji ya barafu alisogea na kuongea na Gefu.
“Tukiendelea ni sawa na kujitoa kafara tu , kwanini tuhatarishe maisha yetu kwa kutaka kumsaidiia Roma? , ni muda wa kurudi Panas”
Baada ya kauli hio Gefu aliongoza njia na kupaa kuelekea mbali kurudi katika miliki yao.
Ilionekana walikuwa hapo kwa ajili ya kumpa sapoti Roma ili awapatie mbinu ya Andiko kutokana na msaada wao lakini hatari waliiona hivyo waliamua kuufyata mkia na kukimbia.

SEHEMU YA 727.
Roma akiwa katika wasiwasi wa kupotea maisha akiwa na Rufi mawazo yalikataa kabisa kushindwa mara baada ya kumkumbuka Lanlana na wanawake wake wanaomsubiri nyumbani.
Licha ya ukinzani wake katika kuzuia mashambulizi lakini alikuwa akipoteza nguvu sana katika kukusanya nishati ya mbingu na ardhi.
Roma alikuwa akisikia mapigo yake ya moyo na pumzi wake lakini kwa wakati mmoja aliweza kuhisi hali ya Rufi imekuwa dhaifu sana kutokana na mashambulizi ya sauti.
Chungu kilijitahidi katika kushambulia na kuwalinda lakini haikutosha kabisa kwani maadui walikuwa wengi na Roma aliishia kuimarisha uzio wake tu bila kufanya shambulizi..
Licha ya kwamba Cauldon ilikuwa na uwezo lakini ilikuwa ni swala la muda tu kushindwa, wakati huo mashambulizi ya ndege wa moto , Majoka ya wino na Mkondo wa nyota vilimfanya ashindwe hata kuona hata wale majini walikuwa wakifanya nini wala kupanga.
Yaani ki ufupi ni kwamba Roma alikuwa amezingirwa pande zote na alikuwa ni kama vile amefunikwa na mashabulizi na hakuwa akishambulia bali alikuwa akijilinda tu kama vile anasubiri mtu kuja kumuokoa.
Lakini sasa akiwa hajui ni kipi anapaswa afanye ufahamu mwingine uliibuka katika akili yake na kuanza kuongea na ufahamu wake, ilikuwa ni kama vile yupo ndotoni bila ya kufumba macho.
“Heheee…!!!”
Ilikuwa ni sauti ambayo Roma alikuwa akiitambua , sauti ambayo ilikuwa katika hali ya kuchokoza kama vile inamcheka kwa kile anachopita.
Jambo lile lilimshangaza Roma , uwezo wake wa kiuungu palepale ulisisimka kwa dakika na ndani ya akili yake aliishia kutamka maneno’chaos’ yaani Roho ya mnyama wa maafa.
Katika ufahamu wake Roma kama vile anaota hatimae aliweza kuona sura yake iliokuwa ikimwangalia kwa muonekano wa kichokozi.
“Ni muda mrefu hatujaonana Dogo”Roho ya mnyama iliokuwa katika sura ya Roma iliongea kwa dharau.
“Ina,,,inawezekana..!!” Roma aliishia kuonyesha mshangao huku bila ya kujielewa akiendelea kuzuia mashambulizi katika uhalisia.
“Naona unashangaa na kujiuliza kwanini bado nipo hai kwenye ufahamu wako … hehe ulidhani ulinizimisha kwa kujimezesha lile lijikifaa la Kibuddha. Hakika wewe ni binadamu kilaza, Mimi ndio Mnyama wa Kiuungu, mkuu wa Enzi na Enzi nisiekufa niliezaliwa kabla hata ya uwepo wa majini na binadamu , hicho mlichokiita moyo wa kibuddha ni kakifaa kakipuuzi tu kalikotengenezwa na bindamu kichaa wa karne zile , binadamu ambaye naweza kummeza hata akiungana na wenzake mia moja, halafu eti umejikaza mwenyewe na kujimezesha bila hata ya kujishtukia”Mnyama wa kimaafa alikuwa akiongea na ufahamu wa Roma kwa vichambo.
Roma palepale alijua nini kinachoendelea na alijikuta akiwa kwenye hamani.
“Ulifanya makusudi sio?”
“Hahaa… umechelewa kugundua mpango wangu , kama nisingejifanyisha kumalizwa na wewe nisingepata fursa ya kuendelea kumeza majini na kurudisha uwezo wangu kimya kimya kwasababu ulikataa knnipatia uwezo wako”
Roma alijikuta akijidharau kwa ujinga wake sio tu kwamba alidanganywa na Anjiu lakini hata roho ya mnyama imemdanganya na kuingia mtegoni.
Chaos ni Jini mharibifu aliekuwa katika umbo la mnyama ambaye aliwahi kuwepo na mara baada ya kuuliwa roho yake na nafsi vilifungwa katika Cauldron na akaweza kuishi kwa maeflu au mamilioni ya miaka, hivyo licha ya kuwa katika umbo la mnyama uwezo wake wa akili ni mkubwa sana kuliko wa binadamu.
Ni sawa ufanananishe majini Joka na Chaos wote ni majini ambao maumbo yao ni ya mnyama lakini fahamu zao ni kubwa na zenye akili.
Sasa mara baada ya kuona Roma yupo hatarini ndio roho hio ikajitokeza ndani ya Roma.
Sasa hapa unaweza ukashangaa lakini ukweli ni kwamba Chungu ni Chungu na Roho ni roho , kitendo cha Roma kumiliki Chungu inamaana alimiliki Roho sasa mara baada ya kumeza ule moyo wa Kibudha Roma aliamini ile nguvu ya kiroho ameweza kuidhibiti na kuishikilia katika Chungu lakini haikuwa hivyo Roho hio ilijifanyisha kuwa chini ya Roma na kuendelea kujifanyisha kuwa ndani ya Chungu ili kuendelea kumeza majini kujijengea uwezo kimya kimya.
“Kama ni hivyo kwanini ndio umejitokeza sasa hivi?”
“Hivi unafikiri unaweza kuidhibiti hii hali ya hatari uliopo kama nisingejitokeza? , ungekuwa na uwezo wa kudhibiti Radi ungekipa nguvu kubwa Cauldron na kuweza kumeza mashambulizi yao lakini kwasasa uwezo wako ni wa chini sana na hutoweza kuishi kama utaendelea”
“Siamini , huna uwezo wa kushambulia kwasababu ya uwezo wangu mdogo au kwasababu unafanya yote haya makusudi , hukuonyesha kujali mara baada ya kumeza radi na kila kinachoendelea lazima ni mpango wako”
“Huna haja ya kukasirika dogo , kwangu wewe ni kama kajimdoli tu nisingejisumbua hata kujiileta kwako kama sio mwili wako imara ambao unanifaa sana , ndio nikiamua kupambana mimi mwenyewe mambo sijui ya radi na upuuzi mwingine haviwezi kunitisha , ninao uwezo wa kumeza kila aina ya radi lakini kwanini nikusaidie kama mimi mwenyewe sifaidiki, hata hivyo nimekusaidia katika vingi mpaka sasa hivi?”
“Hujanisaidia kwa chochote unachofanya ni kutimiza mipango yako ya baadae tu kwa kunitumia”Ufahamu wa Roma uliongea.
“Hahaha… ndio unatakaje sasa kama nakutumi ,kila sekunde ambayo nimemeza na kutafuna majini au kusharabu nishati ya radi nakugawia kiasi cha nguvu hio ili kukufanya uwezo wako uongezeke na mwili wako pia kuimarika . ingawa nafanya haya yote ili kuhakikisha mwili wako unakuwa katika hali nzuri kwa ajili ya kuutumia baadae lakini huwezi kukataa ukweli kwamba nilikusaidia sana”
Ukichaa ulianza kumshika Roma palepale , ilikuwa ni kama vile yeye analelewa na roho hio ya mnyama kwasababu tu ilikuwa ikihitaji kutumia mwili wake.
Kitendo cha ufahamu wake kushikiliwa ilimfanya Roma kupandwa na Jazba na ukichaa kwa wakati mmoja lakini roho ya mnyama haikujisumbua na ukinzani wa Roma.
“Ushauri wangu kwako ni kupunguza jazba, kama unakili unapaswa kuelewa huna uwezo wa kushindana na hawa majini , kama unatamani kuondoka hapa pamoja na mchumba wako bila madhara niazimishe mwili wako kwa muda nikusaidie”
Roma aliishia kuwa katika bumbuwazi , ijapokuwa katika uhalisia akili yake ilikuwa ikifanya kazi lakini upande mwingine alikuwa akijibishana na roho hio katika akili.
Roma alimwangalia Rufi namna ambavyo midomo yake ilivyopauka na alijihisi moyo wake kuumia.
“Hubby unaendeleaje…Koho,,,koho…”Rufi alitaka kujua hali ya Roma lakini aliishia kukohoa na kutoa damu nyingi mdomoni ikionyesha Dhahiri alikuwa amepata majeraha ya ndani.
Maongezi ya Roma na roho ya mnyama hakuna jini yoyote ambaye alikuwa akijua wala kuhisi.
Dakika hio Roma alijisi maumivu katika moyo wake , ilikuwa ni kama vile moyo wake unapasuka.
“Ndio kama nitaendelea na huu ukiburi wangu Rufi atafia mikononi mwangu , hata kama hatokufa atapitia mateso makali mno pia hakuna namna hawa majini wakawaacha na wanawake wangu waliopo nyumbani kuishi kwa amani”Roma aliwaza.
Roho ya mnyama ni kama ilikuwa ikipiga chabo Roma anafikiria nini na palepale ilipigilia msumari katika ushawishi wake.
“Zingatia watu wako unaotaka kuwalinda lakini pia jali juhudi zao kwako , unataka kuona maisha yao yakiamuliwa na wengine , kama utaniacha nitumie mwili wako naapia kwa damu ya ukuu wangu wa kitakatifu wa wanyama wote nitakulipa kwa kuwalinda wanawake wako wote na familia yako kwa ujumla , nitammeza kila adui ambaye atataka kuwadhuru … vilevile hawa majini hapa nitawafyeka wote bila kuacha ushahidi wa mifupa yao nyuma , unaonaje ofa yangu?”
Roma hakutaka kuthubutu kuamini maneno yake , kama ilikuwa ikijua kutii ahadi isingeitwa Roho ya mnyama wa maafa.
Roho hio haikuwa na haraka kutaka majibu kutoka kwa Roma na iliishia kutoa tabasamu katika sura ya Roma katika hali ya utulivu kabisa.
Ijapokuwa ilikuwa na uwezo wa kushindana na ufahamu wa Roma lakini ingekupambana na ukinzani na kushindwa kutimiza mpango wake hivyo moja kwa moja ilitumia kanuni ya ushawishi ya kutokuwa na papara ili Roma kujileta mwenyewe.
Roma na yeye alikuwa akifurukuta na kushindwa kuchukua maamuzi ya haraka juu ya hali aliokuwa nayo.
Upande wa majjini hao wa miliki waliokuwa wakimshambulia walikuwa wakikosa subira na walikuwa wakipanga kutumia uwezo wao wote ku,maliza Roma haraka iwezekanayo.
“Mhmh..!! Hiki Chungu cha maafa hakika kinaendana na sifa zake , ni Dhana ipitayo Dhana zote , sijaamini kitakuwa na uwezo wa kuhimili mashambulizi muda mrefu hivi ?”Aliongea Sena huku akionyesha hali ya kuchanganyikiwa kidogo.
“Nafikiri ashafikia mwishoni mwa uwezo wake na hana njia ya kujiokoa tena , mnaonaje sisi wote saba tukishambulia kwa shambulizi moja la wakati mmoja?”Alishauri Senji,
Baada ya kuthibitisha Roma hakuwa na uwezo wa kujiokoa tena wote walikusanya nguvu zao za kiiijini katika kiwango cha juu kabisa.
Anjiu hakuwa na maoni juu ya pendekezo hilo ijapokuwa alijua wakipiga shambulizi moja watamuua Roma moja kwa moja na kukosa mbinu ya andiko lakini hakutaka kupinga.
Ghafla tu Roma aliweza kuhisi ongezeko kubwa la nguvu za kijini ambazo zinajiandaa kumvamia kwa nje , Roma palepale alijuliza majini hao ndio kwamba wana usongo wa kumuua kiasi hicho?.
“Sina jinsi napaswa kucheza kamari ya pata potea”Aliongea Roma na kisha alimwangalia Rufi aliekuwa akitia huruma kwenye mikono yake.
“Rufi sina jinsi nitabetia roho ya mnyama wa maafa , I am sorry”
Rufi alijikuta akikosa neno baada ya kusikia maneno yake na dakika ileile mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu kumzingira Roma alishajua anamaanisha nini.
“Hubby .. umeamua ..”Rufi alishindwa hata kumalizia sentensi yake na machozi palepale yaliupamba uso wake baada ya kujua Roma tayari amekwisha kufanya maamuzi na kuruhusu roho ya mnyama kutawala mwili wake.
Hata kauli yake aliotoa haikuweza kusikiwa tena na Roma kwani alishapotea kwa wakati huo na mmiliki wa mwili wake ni Chaos.
Hatimae Roho ya mnyama Chaos ilifurahi mara baada ya kupata hatimiliki ya mwili wa Roma na ilionekana kweli ilikuwa ikijikusanyia nguvu za kijini kwa kipindi kirefu kimya kimya kwani mara baada ya umiliki wa mwili huo uwezo wake ulipaa kileleni kwa sekunde tu.
Ingawa uwezo wake haukuwa mkubwa kama ilivyokuwa hapo mwanzo lakini majini hayo yasingekuwa na uwezo wa kushinda mbele yake, kumiliki mwili wa Roma ilikuwa ni hatua nzuri sana kwake ya kurudisha utukufu wake uliopotea.
Upande wa majini kila mmoja alikuwa amekusanya nguvu kubwa kwa ajili ya mashambulizi na kutokana na wote kuwa profesheno kwenye mbinu yao ya miliki ya Roshinisutra , waliamini mashambulizi hayo Roma hawezi kupona hata iweje kwani ingekuwa ni mara mbili ya bomu la nyuklia.
“Ni muda wa kumuua kwa shambulizi moja sasa”Aliongea kwa nguvu Senji na ndani ya sekunde iliofata nguvu zao za kijini ilikuwa ni kama Tsunami ambayo inaelekea kumfunika Roma.
“BOOM!!!
Mwanga ulitokana na mlipuko huo ulikuwa mkubwa kiasi cha kufanya miliki yote ya Xia kuwa angavu kama vile ni wakati wa mchana.
Mtikisiko wa muunganisho wa mshambulizi hayo ya majini saba wa levo za juu ni kama vile unataka kudondosha ulimwengu wote wa kijini.
Wakati huo walikuwa washajua Roma yupo mwishoni mwa uwezo wake na shambulizi lao hilo ni hukumu yake ya kifo kwa kujifanya mjuaji kuja ulimwengu wa kijini na kuwachokoza, katika akili zao walikua wakiamini kabisa hapo hachomoki.
Mlipuko na mwanga mpaka unakuja kuisha na kupotea ile sehemu ya mlipuko Roma na Rufi hawakuoekana tena , yaani palikuwa peupe .
Wakati huo huo jungu la maafa lilikuwa likizunguka juu angani na nguvu yake ilionekana kufifia.
“Its over”(Imekwisha).”Aliongea Sena.
“Ilipaswa kuisha muda mrefu”Alijibu Senji.
Majini wa miliki hio waliokuwa wakiangalia kwa mbali walipiga yowe la shangwe mara baada ya kuona mafanikio hayo na ile hali ya kujiamini ilikuwa imerudi.
Lakini sasa dakika ileile Anjiu sura yake ilijikunja huku macho yake yakisinyaa na palepale aligeuza kichwa chake na kuangalia angani upande wa mbali kama vile anaangalia jua.
“Imewe,,, imewezakana vipi !!!”
Mshituko wake uliwashutia na wale wazee wengine na wote kwa pamoja waliangalia juu angani na kila mmoja alijikuta akishikwa na butwaa kiasi cha kushindwa kuvuta hewa.
Kulikuwa na kivuli kilichokuwa kimesimama mamia ya kilomita kutoka kilipo chungu cha maafa.
Upepo wa baridi ulikuwa ukimpuliza Roma ambaye alikuwa ameshikilia Rufi kwa mkono mmoja huku mwingine ukiparaza paraza mashavu yake kimahaba.
Kiini cha macho ya Roma kilikuwa ni rangi nyekundu tii na muonekano wake licha ya umbo kuwa la kawaida lakini hakuonyesha ishara yoyote ya kuwa na ubinadamu ndani yake.
Alionekana kuzingirwa na ukungu uliokuwa ukimtoka katika mwili wake kama vile ni mvuke ambao ulitoa msisimko ambao ni kuogofya na wa kikale.
“Haiwezekani… amewezaje kuokoka , hata kujua hatujui lakini ameweza kukwepa shambulizi letu , kivipi nauliza!!?”Sena alikuwa katika bumbuwazi na hamaki ya karne.
Katika Anga mtu ambaye aliitwa ‘Roma Ramoni’ alishusha macho yake ya rangi ya balbu nyekundu na kuwaangalia watu hao kwa tabasamu la uovu , huku akilamba lipsi zake akionyesha ishara kamili ya tamaa kama Simba ambaye ameona swala.
Roma huyu hakuwa katika umbo la mnyama kwasababu virusi ambavo walikuwa wakifanya kazi ya kupanua mwili wake wamelala kutokana na nguvu ya kijini lakini wale waliohusika kumtengeneza, yaani Zeros kwa kumwangalia Roma wangeweza kujua alikuwa katika kiwango cha juu mno cha uhatari kutokana na macho yake tu.
 
Shukhran mkuu ubarikiwe
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 708.
Tulipoishia Roma anashitukiwa na Jini Tigola mara baada ya kutoka akiwa ameambatana na Jini Sui mlezi wake Yezi katika harakati za kutaka kumtorosha kutoka ulimwengu wa kijini ,Roma ambae yupo katika sura ya Jini Zilha anaulizwa ataje siku aliozaliwa na mwaka na hapo ndio anashitukiwa sasa na Ajuza mlinda geti wa Jumba Jeupe.
Kimahesabu ni kwamba Ajuza uwezo wake wa kijini ni wa chini kulinganisha na wa Roma lakini alikuwa ameishi kwa karne na amekuwa katika levo ya maji ya kiroho kwa muda mrefu hivyo nguvu yake ya kijini ilikuwa kubwa mno.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba alikuwa na uzoefu wa hali ya juu zaidi tofauti na Roma ambaye ni majuzi tu ndio alijua kutumia nguvu za kijini.
Upande wa yule bibi pia alijua ijapokuwa hakuwa akiona uwezo halisi wa Roma lakini nguvu yake ya kijini ilikuwa ya chini hivyo aliona anammudu.
“Haha..haha… hahah… unaonekana kuwa binadamu ambaye una kipaji kikubwa lakini unajidanganya kuona kwamba unaweza kumtorosha huyo mfungwa nje ya miliki ya Kekexil”Aliongea huku kicheko chake kikiwa kikubwa mno kama filimbi na palepale alipaa kwenda angani na alifunga kiganja chake na kukifungua na zilitoka shoti za nguvu ya kijini.
“Nakuita pepo Aoki Sutra!!” Aliongea kwa nguvu.
Roma alikuwa akijua miliki ya Kekexil mbinu yao kubwa ya kuheshimiwa ni hio iliopewa jina la Aoki , mapigo mengi yaliokuwa kwenye mwanga wa kijani yalimsogelea Roma kwa namna ya kutaka kummeza
Roma hakutaka kuzubaa na palepale aliita nguvu ya andiko la urejesho na kisha akaunganisha na nishati ya mbingu na ardhi na akamzingira nayo Sui.
Hakuwa na mpango wa kukimbia katika eneo hilo na aliishia kujikinga na bila ya kufanya shambulizi kwani alikuwa akimlinda Sui asidhurike na nguvu hio ya kijini.
Eneo lore lilikuwa likivuma upepo kama vile ni kimbunga na ingekuwa kuna nyumba hakika paa zake zingezolewa palepale.
“Chaos Cauldron!!”
Roma aliita chungu chake , hakutaka kujizuia tena kutumia Dhana hio kushambuliana na mtu ambaye anamfikia ki uwezo.
Chungu kile kilitengeneza kani mvutano kwa kuzingira mzingo wa kilomita moja ili kuvuta kile kiumbe ambacho kipo ndani ya duara lake.
“Nini!! Chaos Cauldron!!! “
Bibi yule hakushindwa kuonyesha mshangao wake kwani ulikuwa umejiandika katika uso wake wote.
Chungu kilianza kupiga makelele kama vile ni tanuru la moto linalochochewa kuni huku pale katikati kukionekana macho ya kivuli cha mnyama.
Lakini licha ya nguvu yake yule bibi hakuwa mwepesi kuruhusu kushindwa na chungu hicho tofauti na majini wengine , yeye alikuwa na uzoefu wa kupigana vita vingi vya majini bila kusahau uwezo wake wa kijini ulivyokuwa mkubwa.
Alianza kuchezesha vidole vyake kwa haraka sana na palepale ni kama anatengeneza mapovu ya rangi ya kijani ambayo yalianza kusogelea kile chungu kwa kasi mno.
“Nafsi pepo Aoki Nenda!”Aliongea kwa nguvu.
Na palepale lilitokea pepo jeusi kama shetani hivi ambalo lipo katika hali ya moshi kutokana na kukosa mwili , ni pepo ambalo lilikuwa likifanana na mtu mzee sana lakini nguvu ambayo lilikuwa limebeba haikuw aya kawaida hata kidogo.
Nafsi pepo wa nguvu ya Aoki alienda kukumbana na roho ya mnyama wa maafa na kuzuia ile kani mvutano kumvuta yule bibi lakini ilichukua dakika chache tu yule pepo alimezwa na kile chungu paepale na kugeuka kuwa nguvu ya ki Aoki ndani ya chungu.
Lakini yule bibi hakuishia pale tu alianza kuachia nguvu yake iliojaa roho wa Aoki kushambuliana na kile chungu na dakika tu ilikuwa ni kama anga lote limegeuka na kutengeneza utando wa buibui na Roma alijua Ajuza ana mzuia kutokukimbia., akionyesha kwamba yupo tayari kupambana mpaka mwisho.
“Kama hadithi zilivyosema juu ya Chaos Cauldron , ijapokuwa sijui wewe ni nani lakini uwezo wako wa kijini hautoshi kumfanya huyo roho mnyama kuonyesha nguvu yake yote , hivyo huna uwezo wa kunishinda”aliongea yule bibi kwa kejeli..
Roma aliishia kulaani ndani kwa ndani na kujiambia hana muda wa kutosha kupambana na huyo Ajuza na kama majini wengine wakigundua kinachoendelea master wote watajikusanya na kuanza kumshambulia.
Jini Tigola pia ulikuwa mpango wake na alimwangalia Roma kwa macho ya dharau.
“Mr Roma tukimbie kuelekea upande wa Kusini Magharibi ndio njia ya mkato kutoka katika hii dimension , tuondoke sasa hivi”Aliongea Jini Sui huku akiwa ana tetemeka kwa woga.
Roma pia alijua kama majini wengi watafika ndani ya hilo eneo itakuwa ngumu kumtorosha hivyo bila ya kujishauri alikiongezea nguvu chungu ili kuendelea kumshabulia Ajuza na akatumia mkono wa kushoto na kutengeneza shoti kama radi rangi ya zambarau na kushambulia ule utando kama buibui uliofunika anga na palepale tundu kubwa lilionekana
“Pepo Aoki zuia”Aliita pepo wake kwa mara nyingine mara baada ya kuona shoti ya kutisha kutoka kwa Roma ikiharibu ngao yake ya utando wa buibui.
“Wewe ajuza tutapambana siku nyingine nina haraka”Aliongea Roma na palepale alikificha chungu chake na kumshikilia Sui ili kukimbia .
Lakini sasa dakika ileile anataka kukimbia alijihisi vinyweleo vya mwili kumsisimka kwa nguvu huku macho yake yakiangalia upande wa mbele yake na mshale uliokuwa ukitembea kwa kasi kubwa huku ukitoa mng’ao wa rangi nyeupe kama vile ni kimondo ulimsogelea kwa kasi kwa ajili ya kumzuru.
Roma palepale ufahamu wake ulielewa kinachoendelea , ni jini mwingine ambaye yupo kwenye levo ya maji ya kiroho na jambo hilo lilimshangaza.
Yaani kile kitu ambacho alikuwa akihofia hatimae kimetokea , hakuwa akiogopa kupambana na jini Tigola kwani alikuwa na uwezo wa kumshinda , ukweli ni kwamba kama angeamua kutumia uwezo wake wote jini huyo asingechukua hata dakika ashammaliza.
Kipaumbele chake ni kumlinda jini Sui kwani alikuwa kwenye levo ya nafsi na uwezo wake ni mdogo kujilinda na msukumo wa mawimbi ya nguvu ya kijini ya levo za juu.
Kingine pia alikuwa na wasiwasi kama majini wengine ambao wapo katika levo sawa na ya Tigola kuja kumpa msaada hatokuwa na uwezo wa kumlinda Sui kwa asilimia mia moja.
Sasa Roma mara baada ya kuona mshale unamsogelea kama vile ni Kombora la nyuklia hakuwa na muda tena wa kukimbia na palepale alimrusha nyuma yake jini Sui na akaita siraha yake ya Tufe la bluu na mara baada ya kukutana na ule mshale ulitokea mlipuko mkubwa kama vile nguvu zote mbili zimekataana, ilionekana kama vile mafataki yanaruka hewani na kulipuka.
Ule mlipuko wa nguvu zote mbili ulifanya eneo la chini kupatwa na mtetemeko wa ardhi na hatimae majini wote walishajua nini kinaendelea na kila aliekuwa karibu na eneo hilo aliangalia hewani.
Dakika ileile ya mlipuko mwanaume mwingine jini alijitokeza , alikuwa na nywele ndefu mno ambazo hazijafungwa na zilikuwa zikipeperushwa na upepo huku uso wake ukiwa na hali ya mshangao kiasi flani lakini haikuwa na hasira yaani kwa kumwangalia tu ungejua kwamba ni jini hatari.
Mara baada ya mwanga ule kupotea ile siraha ya mshale ili mrudia mkononi mwake kwa mbwembwe zote ikimlaki master wake.
“Shagoni bora umekuja ndani ya muda muafaka , hebu nisaidie kumuua huyu mwizi”Aliongea yule bibi kizee wa kijini.
Jini huyo hakuwa mwingine bali alikuwa ni Master Shagoni mwenyewe , mmoja ya majini wenye uwezo wa juu sana ndani ya ‘dimension’ hio ya majini watu , alikuwa akitarajiwa kufika makao makuu ya miliki ya Kekexil kwa ajili ya kufundisha vijana ambao wangeenda kushiriki mashindano ya mavuno makuu katika kuingia kwenye Jicho la Anga.
Master Shagoni jini mwenye nguvu alimwangalia jini mwenzake bibi kizee jini Tigola kwa namna flani hivi kama hana muda wa kumsikiliza porojo zake na palepale aliachana nae na kugeuzia macho yake kwa Roma ambaye kwenye kiganja chake cha mkono kulikuwa na moto ambao unacheza cheza wa rangi ya bluu pamoja na lichungu likubwa ambalo lipo juu ya kichwa chake.
Roma alijikuta macho yake yakijifumba mara baada ya kuhisi majini kuongezeka ndani ya eneo hio , sasa kwasababu mambo yashafikia hatua hio hakukuwa na haja ya kujifanyisha ni Zilha tena na alichopaswa ni kutengeneza njia kwa kuua baadhi ya majini na kisha kukimbia.
Kwa kuchezesha mkono tu Chaos Cauldron ilitoka katika kichwa chake na kurudi nyuma na kwenda kusimama juu ya kichwa cha jini Sui na palepale boriti za mwanga zilichomoza ndani yake na kwenda kumvaa jini Sui na alivutwa pale kuingizwa ndani ya chungu.
“Sui nitakulinda na Cauldron , kaa humo ndani na usisogee”Aliongea Roma kwa sauti nzito huku Sui akiwa anaonekana ndani ya chungu kile.
Ijapokuwa nguvu ya Dhana hio ya Chaos Cauldron haikuwa na uwezo wake wote kama inavyosemekana katika hadithi mbalimbali lakini ilikuwa na uwezo wa kumlinda jini Sui akiwa ndani yake na hakuna jini lolote ambalo lina uwezo wa kumdhuru akiwa ndani ni kama vile walivyofanya wakati wanachoropoka kwenye ulimwengu wa majini pepo.
“Mr Roma kuwa makini na hio siraha ya Master Shagoni inayoweza kupaa , ni Dhana ya daraja la juu kabisa na nguvu yake inaweza kushindana na jini hata kilomita kadhaa bila hata yeye mwenyewe kuwepo , ni hatari sana”Sauti ya Jini ilisafirishwa kutoka kwenye Cauldron na kumfikia Roma.
Roma mwenyewe alishaona nguvu ya Dhana hio na alikuwa kwa namna flani amejiandaa kupambana nayo.
Kwa jinni wa levo yake ilikuwa ikileta maana kumiliki Dhana ya aina hio kama ilivyokuwa yeye kumiliki Dhana ya Chungu.
“Uwezo wako wa nishati ya mbingu na ardhi ni mkubwa mno na wa kushangaza kiasi cha kuweza kupangua siraha yangu , nadhani nimehisi nguvu ya levo ya maji ya barafu kutoka kwako , mimi Shagoni sijawahi kupambana na mtu asie na jina , niambie jina lako na tupambane”Aliongea Shagoni huku akiwa na macho yaliochanua kwa mchecheto wa kuingia ulingoni.
Mwanzonni alikuwa amefika hapo kwa ajili ya kutii wito wa miliki ya Kekexil kwasababu tu dada yake jini Lilsi kamuomba , hakuwa akijali sana kuhusu mashindano ya miliki za kijini kupambana katika uwanja kwa ajili ya kuingia kwenye jicho la Anga.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba Lilsi sio jini ambaye yupo ndani ya miliki ya Kekexil, majini mfumo wao wa kimaisha ni ule wa kizamani yaani wa kifalme na jini Lilsi ameozeshwa tu kwa miliki ya Kekexil lakini jamii yake ya kijini ni tofauti sana.
Sasa Master Shagoni hakutegemea kama angekuja kukutana mapambano ya majini waliokatika levo ya maji ya kiroho na zaidi sana kukutana na mshindani mwenye uwezo mkubwa , kwa dakika hio alikuwa na hamu zote kupambana kwani alikuwa akitafuta mtu mwenye uwezo mkubwa kujipima.
“Shagoni acha kuongea upuuzi na mshambulie”Aliongea yule Ajuza kwa hasira.
“Wewe kizee , sitaki kubishana na wewe kwani una umri mkubwa kuliko mimi lakini nikwambie tu mimi sio mtumwa wa miliki ya Kekexil , endelea kuniongelesha kwa sauti yako ya amri uone , nitakuua hapa hapa kabla sijaanza pambano”Aliongea kwa hasira huku akimkodolea macho.
“Wewe mwanaharamu usie na shukrani sitaki kujibishana na wewe”Jinni Tigola alikuwa na hasira mno kujibishwa na Master Shagoni na alijua huo sio muda wa kubishana nae na palepale aligeuza sura yake na kumwangalia Roma.
“Wewe kibaka , huwezi kukimbia kutoka hapa , ndani ya muda mfupi tu majini wote wenye uwezo wa juu watakusanyika , ndugu zangu watakapofika utaenda kuonana na aliekuumba”
Roma alikuwa anahisi uwepo wa kundi la majini ambao wanasogelea kutoka mbali , baadhi yao wapo levo ya maji ya barafu huku wengi wakiwa maji ya meupe na moto wa rangi nyekundu na njano lakini hawakuwa tishio kwake.
Hivyo hivyo hao majini walijua hawana uwezo wa kuingilia mapambano hayo hivyo ilionekana walisimama mbali kuangalia kinachoendelea.
Lakini kwa Roma alijua pambano hilo litachukua sura mpya kama majini ambao wapo levo ya maji ya kiroho wangefika hapo kabla hajaondoka.
“Kwasababu unakitaka kifo chako basi sina budi kukitekeleza”Aliongea Roma , alikuwa na hasira mno hivyo hakutaka kuzuia tena hasira zake na alijiambia ngoja aje atajaribu kupigana na jini ambaye yupo levo ya maji ya kiroho bila hata ya kutumia chungu.
Dakika ileile Roma alifutika alipokuwa amesimama na ile anatokea alikuwa tayari yupo mbele ya jini Tigola na ngumi yake iliofunikwa na mwanga wa rangi ya bluu ilimsogelea kumlenga eneo la kichwani.
Tofauti na Dhana za kijini Roma mwili wake ulikuwa mgumu mno mbali zaidi ya Dhana.
Upande wa Tigola alikuwa ni majigambo tu na alijua ndani ya moyo wake kabisa hawezi kumshinda Roma na alikuwa akivuta muda ili msaada kumfikia hivyo alijitahidi kuwa makini na kujilinda mara baada ya kuona Roma anamshambbulia.
Shambbulizi la Roma palepale kwa spidi kubwa alilipunguza nguvu yake kwa kutumia nguvu ya pepo Aoki lakini hata hivyo Roma alikuwa ametegemea kwani palepale ulitokea mlipuko wa nguvu ya kijini iliokuwa kama radi ya rangi ya zambarau na kuharibu nguvu ya kijini ya Aoki na kuzidi kumsogelea.
Jinni Tigola baada ya kuona Roma ameweza kuhimili nguvu yake alirudi nyuma lakini spidi yake ilikuwa ndogo na kadri Roma alivyokuwa akimsogela alihisi nguvu ya ajabu inamsogelea pia ambayo inatokana na maji ya kiroho ambayo kwa majini ni kama tindikali ya kuyeyusha.
“Kama kizuizi changu akikivunja nitajeruhiwa sana kama sio kufa kabisa”Wazo hilo lilimwingia yule kizee huku akionyesha hali ya kupaniki.
Roma alizidi kumsogelea huku akijitahidi kushikilia kizuizi chake lakini kilivunjwa vunjwa na moto wa njano uliokuwa kama vinyoka vyoka pamoja na umeme kama radi wa rangi ya zambarau na palepale alijikuta mwili wake ukikakamaa na kujutia kwanini kaamua kupambana nae kichwa kichwa , angevuta muda na sio kumchokoza.
Kilichomfanya kuchanganyikiwa zaidi Master Shagoni hakuwa akichukua hatua yoyote na alikuwa akiangalia tu.
Jini Mohi mkuu namba tatu wa majini wa Kekexil aliweza kuona kila kinachoendelea kutokea mbali na aliweza kugundua aliekuwa ni mtoto wake Zilha alikuwa ni feki na mara baada ya kuchukua muda mrefu kujituliza sasa alirudiwa na ufahamu na kumwagiza mkuu wa Chemba jini Ganyo kutuma majini ambao wameipita Dhiki kumsaidia Ajuza.
Yeye mwenyewe licha ya kuwa na uwezo bado aliogopa kusogelea pambano hilo kwa kuogopa kama kibaya kitatokea basi milikii ngeyumba.
Master Ganyo hakuchelewa na palepale alichukua oda ya mkuu wake na kisha alichagua majini ambao wapo katila levo ya maji ya barafu, moto na maji ya meupe kwenda kumsaidia jini Tigola huku yeye mwenyewe hakuthubutu kwenda.
Wote walikuwa katike levo ya kuipita dhiki lakini msuguano wa nguvu ya ardhi na mbingu uliokuwa ukitolewa na Roma ulikuwa ni wa kutisha hivyo hakutaka kujipeleka kizembe.
Asilimia kubwa ya majini aliochagua ni wale ambao wameomba hifadhi katika miliki ya Kekexil na sasa kwasababu wametumwa kwenda kupambana hawakuwa na chaguo lingine zaidi ya kutii licha ya kujua wanajitafutia vifo.
Kufumba na kufumbua mashambulizi yalirushwa kuelekea alipo Roma kila upande , walikuwa wakijaribu kuunganisha nguvu zao ili kumshusha chini.
Haikujalisha uwezo wa Roma ulikuwa mkubwa vipi lakini alikuwa akipambana peke yake na pengine angeathirika na mapigo yao kutokana na kwamba ni mashambulizi ya pamoja.
Roma upande wake alikuwa akihisi kabisa uwezo wao wa kijini pamoja na Dhana ambazo wamezielekezea kwake , na alijua mpango wao ni kumshusha chini na alijikuta akitoa kicheko cha hasira.
“Nyie watumwa hamna uwezo wa kumuokoa mtu ambaye anakufa”Aliongea Roma.
Alishajua kwamba ni ngumu kuzuia mashambulizi yote yanaotokea kila upande hivyo aliachana na kujilinda na palepale mara baada ya kuinua mkono wake kulionekana puto la maji ya kiroho ambalo liliendelea kuwa kubwa zaidi na zaidi kadri alivyokuwa akiliongezea nguvu kama vile linapulizwa huku ndani yake likiwa na maji
“Ni maji ya kitoho!!”
Jinni Tigola alimaka lakini hakupewa hata muda wa kuvuta pumzi kwani ilikuwa ameshachelewa kukimbia.
“Nenda kuzimu”
Aliongea Roma na palepale lile puto alilirusha juu na kisha akalipiga na mshale wa nguvu za kijini na likapasuka , kwasababu lilikuwa kubwa sana lilivyopasuka lilitengeneza mvua ya maji ya kiroho kuelekea pande zote akilenga wale majini wengine waliokuwa karibu yake kumshambulia.
Dakika ilile mashambbulizi yao ya Dhana na nguvu ya kijini yalitua kwenye mwili wa Roma , milio ya milipuko ya nguvu za kijini ilisikika ikiwa imemzingira Roma ashindwe kumsogelea yule Ajuza tena.

SEHEMU YA 709.
Mkuu namba tatu wa majini watu . Mohi na wengine wote waliokuwa wakiangalia kwa mbali walijikuta wakifurahishwa na jambo lile akiwemo jini Tigola ambaye alikuwa akijiandaa kupokea shambulizi la Roma.
Kwao jini lolote ambalo lingepokea mashambulizi ya wakati mmoja kama yale lazima kufa hivyo walisuiria kwa hamu zote kuona Roma akiwa maiti.
Lakini sasa kundi la wale majini walijikuta wakitoa vilio vya kusaga meno na kuanza kuporomoka kutoka angani , uwezo wao wa kijini ulikuwa mdogo kuhimili nguvu maji ya kiroho ambayo ni kama tindikali inayoyeyusha mwili na tone moja tu lilitosha kuharibu mwili na nafsi.
Dakika ileile wote walijikuta roho zao zikimezwa na yale maji na kusafishwa kabisa na kufanya nafsi zao zote kupotea kabisa na hazikupewa hata nafasi ya kutoka kwenye miili yao na kuwa ghost kwenda ulimwengu mwingine kama wanavyoamini.
Miliki ya Kekexil baada ya kuona tukio lile walijikuta wakiomboleza kwa hasara ya majinni wale , walikuwa wametumia nguvu kubwa na vidonge kwa ajilil ya kuwafua lakini walikuwa wamekufa kwa shambulizi moja tu la Roma,
Bila ya kutegemea kitu cha kushitukisha kilitokea mara baada ya mlipuko ule kuisha , mtu alitoka katika mlipuko ule, alikuwa ni Roma, ijapokuwa alionekana kuchanguka lakini nguvu yake ya kijini haikuwa imepungua.
Jini Sui amaye alikuwa akiangalia kwa pembeni ndani ya chungu cha kijini alijikuta akimaka na kuwa na furaha mara baada ya kumuona Roma akiwa hajapata majeraha.
Upande wa Roma shambulizi lile la milipuko ya nguvu za kijini pamoja na Dhana halikumletea athari ya aina yoyote kutokana na utimamu wa mwili wake lakini vilevile nguvu ya andiko ambayo kazi yake ni kumponyesha.
“Haijalishi ni majini wangapi mtawatuma kunishambulia nitawaua wote na hakuna ambaye anaweza kuwasaidia tena, naanza na wewe Nenda kuzimu”Aliongea Roma mara sasa baada ya kumfikia Jini Tigola yule kizee ambae alikuwa akishangaa shangaa.
Macho ya jini Tigola yalionyesha njama na kejeli na palepale alitoka alipokuwa amesimama na kusogelea kile chungu cha kijini akiwa na nia ya kumtoa Jini Sui ili kumfanya mateka na Roma baada ya kuona hila yake hakutaka kumchelewesha na alikiruhusu kile chungu kumvuta ili kumeza na ilimfanya kushindwa kuwa na muda wa kujilinda na palepale alitoa bangiri ambayo alikuwa amevaa mkononi na kuitupia kwenye kile chungu kutegeneza ngao .
Ilikuwa ni Dhana ya juu ya ki ulinzi , isitoshe sio majini wote ambao wanaweza kumiliki Dhana lakini hata hivyo jini Tigola hakuonyesha kunufaika na Dhana ile katika kutengeneza ngao kwani nguvu ya mvuto wa chungu iliiboboa palepale na kuifanya ile bangiri yenyewe kukatika vipande vipande.
Ilionekana ni Dhana nzuri lakini ni kama kifaa ambacho hakikuwa na ugumu wowote mbele ya nguvu kubwa ya Cauldron.
Jini Tigola palepale alichokuwa akitaka ni kumvuta nje Jini Sui akiacha kuomboleza Dhana yake ilioharibiwa , lakini Roma hakutaka kumpa hio nafasi kwani palepale alimsogelea akiwa na donge la maji ya upako na kutokana na mvuto wa chungu alishindwa kukwepa shambulizi la Roma mapema.
“Argghhh…!!!”
Alijikuta akipiga yowe wakati maji yale yakianza kuiharibu roho yake pamoja na mwili. Alijitahidi kuzuia nguvu ya yale maji kwa kutumia nguvu yake ya kijini ili kuondoa athari yake lakini ilishindakana kabisa kwani spidi ya yale maji katika kuharibu mwili ilikuwa kubwa mno.
“Shagoni unafanya nini, naomba unisaidie?”Aliongea kwa nguvu Jini Tigola.
Master Shagoni ambaye alikuwa akiangalia pambano hilo hatimae alisogea huku siraha yake ikitoa msisimko wa ajabu mno na kumsogelea Roma kwa kasi ili kumpa msaada Tigola .
“Huwa sipendelei pambano la two in one ila kwasababu ushamuweza ni zamu yangu sasa”Aliongea Master Shagoni kwa mchecheto.
Lakini upande wa Roma hakumjali kabisa , alitaka kummaliza kabisa jini Tigola kwasababu alikuwa amemjeruhi pakubwa alijua akimwacha anahema anaweza kujiponyesha.
Roma hakuwa na muda wa kuzuia ile siraha ya Shagoni na hakutaka kujisumbua na palepale alituma moto wa bluu kuelekea alipo jini Tigola.
Ile siraha ilimpiga mgongoni na kumrusha kama mpira lakini upande mwingine shambulizi lake kwenda kwa jini Tigola lilifanikiwa na lilimyeyusha palepale.
Jini Tigola mwisho wake ukawa mbaya sana kwani alipiga yowe na kilio cha kusaga meno huku mwili wake ukiteketea na mara baada ya kuhimili maumivu kwa sekunde kadhaa hatimae alikosa mhimili na kudondoka kutoka angani lakini hata chini kwenywe hakufika kwani aliyeyuka na kupotea nio ikawa mwisho wake.
“Ma am!!!”
“Bibi!!”
“Ajjuza!!”
Majini yote yakiongozwa na jini mkuu namba tatu , walipiga ukulele wakishuhudia kifo cha moja wa majini wa kuogopeka ambae yupo katika kitengo cha ulinzi kinachofahamika kwa jina la Taisha, ndio hivyo kakutana na mbabe na anakufa mbele yao tena bila hata ya maiti yake kubaki , wote kwa macho ya chuki walimwangalia Master Shagoni kwa kutokumsaidia Tigola ndani ya muda muafaka.
Waliamini kama angepambana na yeye kwa wakati mmoja na Tigola hayo yasingetokea ndio maana walikumbwa na simanzi na hasira zidi yake.
Upande wa Roma aliona huyo bibi alijitakia mwenyewe , hakuwa na mpango wa kupigana nae licha ya kuona kwamba anamuweza lakini akaleta ujeuri, tena mbaya zaidi kutaka kumtumia Sui kama mateka.
Upande wa Master Shagoni hakujali sana kuhusu chuki za za wanamiliki ya Kekexil na alikuwa akimwangalia Roma kwa mshangao kwa kufanikisha kummaliza Tigola kiwepesi namna ile lakini kwa wakati mmoja siraha yake ambayo amemshambulia nayo Roma mgongoni kutoleta madhara ya namna yoyote kwake.
“Inawezekana vipi hili , kwanini siraha yangu haijakudhuru hata kidogo?”Aliongea akiwa katika mshangao akimwangalia Roma ambaye alikuwa akijiweka sawa angani mara baada ya kufyatuliwa na lile shambulizi na alipeleka mkono wake mgongoni na kuona hajaumia na alitoa tabasamu.
Kwa Shagoni kulingana na uzoefu wake ilikuwa ngumu kwa binadamu ambaye ana uwezo wa kijini kutodhulika na siraha yake, hakuamini kabisa kwani ni mara ya kwanza lakini hata hivyo hakuonyesha huzuni bali alifurahi.
“Haha.. hakika unashangaza sana , kwasababu nguvu ya kawaida ya siraha yangu haina athari kwako , ngoja tuone nguvu ya roho therathini na sita za nyangumi zisipovunja ulinzi wako”
Baada ya kuongea hivyo siraha yake ile iliokaa kama kichwa cha samaki ilianza kusambaza nguvu kubwa ya kijini , kubwa sana kuliko mwanzo , msisimko wa siraha, ni aina ya ufunuo ambao alipata lakini alishindwa kuupatia jina hivyo aliishia kuitwa ‘Msisimko wa Dhana’.
Likija swala la kutumia siraha kama panga na mikuki , Roma alikuwa na uwezo huo kutokana na kupitia mafunzo mengi ya kininja lakini kwa Master Shagoni ni habari nyingine kabisa , alikuwa ni jini ambaye alipanda levo kwa kujifua katika mapigano ya siraha za mapanga na mikuki kwa miaka mingi sana na akapata mafanikio makubwa.
“Roho 36 za nyangumi kichaa…!!!”
Baada ya kuongea ile kauli ile siraha yake ilianza kubadilika umbo na kuwa kama samaki mkubwa aina ya nyangumi ambaye yupo katika mfumo wa roho na kumsogelea Roma kwa kasi.
Roma mara baada ya kuona aliebakia ni huyo Shagoni aliona kabisa hana muda wa kupambana na anapaswa kuondoka kwa haraka eneo hilo , aliona kama ataendelea kupambana anaweza asiondoke kabisa.
Palepale alikiruhusu chungu kushambuliana na Roho Nyangumi kichaa wakati huo akiwa ashamtoa tayari jini Sui na kuanza kukimbia bila ya Shagoni kumuona.
Chungu kile kilianza kuvutana na roho ile ya Nyangumi kwa kusumbuana nayo na palapale ilipunguzwa nguvu.
“Njoo!”Aliongea Roma akiwa mbali.
Master Shagoni ambaye alikuwa katika kufurahi kupambana na kile chungu aligundua kuna kitu hakipo sawa , kwanii baada ya roho wa nyangumi wake kushindwa na Cauldron palepale roho wa mnyama na chungu vyote vilipotea katika upeo wake wa macho..
Alijiua Roma ataendelea kupambana lakini alikuja kujua aliwekewa mtego wa kumpa Roma nafasi ya kukimbia kwani alipokuwa makini kupambana na chungu Roma ashasepa na alipofika mbali akakiita.
“Wewe mwanaharamu usiwe na aibu ndio unakimbia bila ya kupambana hata kidogo”Aliongea kwa hasira huku sauti yake ikiwa imeunganishwa na nguvu ya kijini na kufanya itembee kilomita nyingi.
Upande wa Roma ambaye alikuwa kwenye mbio kukimbia alishia kutoa tusi na kujiambia kama sio kuwa na Sui asingeogopa kuzingirwa na majini na kupambana nao wote kisha kuwaua.
“Pumbavu kabisa unadhani nakuogopa , ningekuua kama nilivyomuua ajuza mwenzako”Aliwaza Roma huku aking’ata meno kwa hasira katika maisha yake hajawahi kukimbia pambano lakini kwa hali aliokuwa nayo busara ilikuwa ni kukimbia.
Roma hakutaka kupambana na Shagonni kwa sababu moja , hakuingilia mpambano wake na Jini Tigola hivyo moja kwa moja alijua ana nguvu kubwa , kama angepambana nae basi ingemchukua muda mrefu sana na mwisho wa siku majini yenye uwezo mkubwa zaii ya Shagoni yangefika.
Roma aliishia kujiambia ngoja amsamehe Shagoni kwa siku hio ila atamtafuta akiwa hana mtu wa kulinda.
Miliki yote ya Kekexil hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kumzuia Roma kuondoka na hata baadhi yao walimpisha huku akipotea machoni kwao kwa spidi ya mwanga.
Ndio hivyo ilikuwa sahihi kwao kuwa katika kiwewe kwani jini ambaye yupo ndani ya kitengo cha Taisha alikuwa ameuliwa kiwepesi na binadamu mweusi ambaye haijulikani ametokea wapi , ilikuwa ikiogopesha kama yupo mtu ambaye anaweza kumuua jini lenye uwezo kama Tigola ambaye ameishi Karne nyingi na miliki yote kumuogopa.
Taisha ni kitengo amacho kinaundwa na majini wenye nguvu ambao kazi yao ni kujitokeza pale tu ulimwengu wao unapovamiwa , umoja huu haukutegemea kabisa miliki, yaani ni kama hapa duniani itokee kiumbe kutoka sayari nyingine kikashambulia basi kitengo maalumu ambacho kinajumuisha wanajeshi kutoka kila nchi watashiriki kuilinda dunia.
Sasa jini Tigola ambaye yupo chini ya kitengo cha Taisha alikuwa ameuliwa kwa shambulizi moja tu , hivyo iliwafanya majini wote kumuogopa Roma kama ukoma.
Mkuu namba tatu wa miliki ya Kekexil alikusanya majini wote na kisha wakamzingira Master Shagoni na kumwangalia kwa macho ya kumlaani.
“Shagoni, ulikuwa ukifikiria nini , kwanini ulikaa kizembe na ukapotezea mwanachama mwenzako wakati akiomba msaada , je familia yako ndio imeanza uhaini zidi ya Kekexil?”
Jini Mohi alikuwa na hasira mno , Kekexil ilikuwa tayari ni dhaifu mbele ya miliki ya Xia na Panasi lakini bado wamepoteza komandoo wao Ajuza Tigola.
Master Shagoni aliishia kugeuka na kisha akaiita siraha yake yenye roho ya nyangumi therathini na sita.
“Kwahio kukasirika kwako ndio tuseme unataka kupambana na mimi”Aliongea
“Wewe…!!”Jini Mohi alijikuta akipaliwa kutokana na hasira.
“Nachukia sana mapambano ya kumchangia mtu mmoja , kifo sio jambo kubwa kati ya wabobezi wawili wanaopambana , huwezi kupanda levo bila ya kuji’challenge’ ukiwa peke yako, nyie wajinga hamuwezi kuelewa ninachoongea hapa , hata hivyo sijaja kukamata mwizi wenu aliewaibia , muda wangu ni wa thamani mno na nipo hapa kwa sababu ya mdogo wangu Lilsi , kauli yangu moja tu miliki ya Panasi na Xia watanifunga kamba kunivutia kila upande wakihitaji huduma yangu, wewe ni nani wa kuniambia cha kufanya?”
Mkuu namba tatu kutokana na hasira alishindwa kujizuia kutokutetemeka, jini Lilsi hakutaka kuendelea kuangalia na aliingilia.
“Usiwe na hasira , sisi wote ni familia moja na miliki moja, kama kuna wa kulaumiwa hapa basi ni yule mwizi ambaye alivaa uhusika wa Zilha na kutuletea hasara nyumbani kwetu”
Kauli hio ilimfanya Shagonni kupunguza jazba na palepale alirudisha siraha yake katika hifadhi ya pete.
Sasa baada ya kauli ya Lilisi kubadili maongezi , majini hao walianza kuongea wao kwa wao wakizungumzia kilichotokea , wengi wao wakianza kujiuliza huyu mwizi mwenye uwezo wa ajabu ni nani.
Upande mwingine Jini Manyani alikuwa mwekundu na akichemka kwa hasira na kujidharau na alijiambia ndio maana alimpelekea moto usiku ule , kumbe hakuwa Zilha bwana.
“Kwahio inamaannisha kitumbua changu kimechezewa na kibaka?”Aliwaza huku akijilaumu kwa hasira , kwani ndio hivyo kibaka Roma Ramoni amekula mbususu na kisha akaiba na kusepa, alijiamia siri hio ataenda nayo kaburini.
Dakika hio hio nguvu ya kijini iliongezeka juu ya makao makuu ya miliki hio ya Kekexil ikiwasogelea.
Kufumba na kufumbua lilionekana Jini mtu ambaye amevalia joho la rangi ya Zambarau akiwa na nywele nyeupe mno ambazo zimechanwa viuri kurudi nyuma na kupepea na kumfanya aonekane kama malaika.
“Baba!”
Jini Mohi alikuwa katka hali ya furaha mara baada ya kumuona baba yake lakini dakika ileile hisia zake zilitawaliwa na hatia pamoja na simanzi.
“Heshima kwako Mkuu Namba Moja!!!!”
Majini wote waliongea kwa nguvu wakionyesha heshima mbele ya jini Menui ambaye ndio mkuu namba moja wa miliki ya Kekexil.
Upande wa Master Shagoni alimwangalia Mkuu namba moja mara moja tu bila ya kuongea chochote.
Jini Menui ndio mkuu wa miliki ya majini watu ya Kekexil na huyu hakupenda sana kukaa makao makuu kwani anapenda kujificha akiendelea kujifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi na dakika ambayo alitoka huko alipokuwepo aliweza kuhisi msuguano wa nguvu za kijini katika miliki yake na kuja kwa haraka lakini alishachelewa.
“Mohi , nini kimetokea?”
Aliongea na sauti yake ilikuwa kali mno kama ngurumo ya radi mara baada ya kushindwa kuhisi uwepo wa jini Tigola.
Jini Mohi alimwelezea baba yake kila kitu kilichotokea katika miliki hio mwanzo mwisho na muda huo huo jini Manyani alitumwa pia kwenda kuangalia kilichotokea katika Jumba jeupe na kurudisha jibu kwamba hakuna kitu jengo limesafishwa lote.
Jini Menui alijikuta akibadilika mara baada ya kusikia kwamba hakuna mimea yoyote iliobakia kwani imeibiwa yote pamoja na vifo vya majini tegemezi, mshipa wa damu katika uso wake ulichomoza huku ukionekana kupitisha damu kwa kasi mno na nguvu za kijini zilimtoka na kusababisha upepo mkali sana kuvuma.
“Nilikuwa nikijifunza kwa zaidi ya miezi mwili tu lakini tafrani imeikumba miliki yetu , umefanya kazi gani kama kaimu wa nafasi yangu?”Alifoka.
Jini Mohi alijikuta akitetemeka kwa woga huku kichwa chake akiwa amekiinamisha chini bila ya kushindwa kuongea , sio alishindwa kuongea ni kwmaba hakuthubutu kuongea.
“Kwanzia leo na kuendelea kila jini ndani ya miliki hii anapaswa kuwa macho , hakikisha hampitwi na ishara yoyote ya uvamizi , sitokuwamna huruma kwa jini yoyote ambaye atafanya uzembe na kupelekea hasara zaidi kwa miliki yetu”
“Yes!!!!”
Majini wote waliitikia kwa pamoja lakini walijua ingekuwa kazi kubwa kwa miliki hio kuweza kuhimili hasara walioweza kupata na kurudi katika utukufu wao.
Jini mkuu namba moja aliwatawanyisha majini wote na kutuma wengine kwenda kufanya usafi ndani ya jumba jeupe huku akikusanya wakuu wote kuelekea ukumbini katika baraza kuu la umiliki wa Kekexil.
Hakuongea neno lolote na Master Shagoni akionyesha ni kwa namna gani hajaridhishwa nae.
Shagoni hakujali kabisa na alifuata nyuma nyuma kuelekea kwenye baraza la mikutano la mkuu namba moja wa miliki kama vile alikuwa akipenda kusikiliza kile ambacho wanaenda kujadiliana.
Wazee wote wa ukoo walikusanyika kuanza kuzungumza juu ya jambo lilitokea , yaani mwizi kuvamia miliki yao.
“Natangaza kwanzia leo huyu binadamu ni adui yetu namba moja , ninaamini amemuua Zilha”Aliongea Menui akiwa na uso usiosomeka anawaza nini
Jini Mohhi uso ulimshuka ijapokuwa Zilha alikuwa mzembe lakini alikuwa ni mtoto wake wa pekee wa kiume.
Na sasa alijua Zilha ambaye alionekana mtiifu alikuwa feki na hasira zilimpanda zaidi na zaidi akiwa na nia ya kwenda kumchuna Roma ngozi.
“Tuma majasusi wetu kutafuka katika pande zote za ulimwengu wa kijini, pia tuma wengine ambao wataenda kutahadharisha miliki nyingine zote juu ya uvamizi huu , kama Dhana yake ni Chaos Cauldron basi lazima kuna jini ambaye ashawahi kuiona ikitumika , lazima kuwe na taarifa , tukishamjua ni nani na wapii alipo hata kama ni duniani lazima alipie, jicho kwa jicho , jino kwa jino”Aliongea Jini Menui.
“Mkishampata mniambie , nataka pambano la kueleweka zidi yake”Aliongea Master Shagoni wakati akiwa ameegamia mlango kivivu.
Majini wote walimwangalia huku wakionyesha kabisa walikuwa na hasira nae .
“Kama Tigola amemshindwa wewe utakuwa unakitafuta kifo kwa kufanya hivyo , usije kukurupuka na ungana na kitengo chetu cha Taisha katika kupambana na adui na utaweza kuwa hai”
“Hakuna mwanachama mwingine wa kitengo cha Taisha hapa lakini bado unawategemea”.
Menui alikuwa na uso wa kusawajika , hata yeye ni wa kulaumiwa kwa kile kilichotokea , wanachama wa kitengo cha Taisha hawakuwa wakikaa ndani ya miliki , wapo mbali sana na ni mpaka awaite.
Alijilaumu kwani yeye ndio alipaswa kutoa ulinzi katika miliki yake lakini alikuwa amejitenga akijifunza , ukweli ni kwamba aliamini hakuna ambaye anaweza kudhuru miliki yake ikiwa Bibi Tigola yupo.
Ndio hivyo hawezi kuongea kwa sauti la sivyo lawama zingeangushiwa kwake.
Lakini hata hivyo alikuwa ashajiandaa kuwaita wana kitengo wa Taisha ili kupambana na adui ili kurudisha heshima ya miliki yao.
Majini wana visasi sana hivyo ilieleweka.
******
Upande mwingine Roma alijikuta akivuta pumzi mara baada ya kutokea dunia ya kawaida kupitia bahari , ilikuwa ajabu kweli kwani njia hio ya mkato ilikuwa nyepesi mno lakini hakuamini kama chini ya bahari kulikuwa na njia ya mkato.
Ilikuwa maajabu mno kwani hakujua hata imetokea vipi bali alijikuta tu yeye na Sui wapo ndani ya bahari na kuja kuibukia juu.
Roma hakutaka kuchelewa chelewa tena kwani alibadilisha mavazi na kisha akamchukua Jini Sui na kumpeleka katika miliki yake ya visiwa vya wafu.
Hakuwa amemaliza bado , ilikuwa ni hatua ya kwanza kumuokoa Sui hivyo alipaswa kurejea tena kwa ajili ya kumuokoa Rufi.

SEHEMU YA 710.
Mediterranian ndio sehemu ambayo aliona ni salama zaidi kwani asingekuwa na wasiwasi na majini kuja kumtafuta huko.
Roma mara baada ya kutoka kwenye ulimwengu huo alihisi uungu wake ukiwa umeimarika kwa kiasi kikubwa mno kutokana na hatua za ufufuo wa moyo wa Gaia, na kama angetumia kanuni za anga uwezo wake ungelingana na wa Poseidon wakati anapambana nae.
Kuona Roma ameimarika hivyo ki ufahamu aliamini hata miungu wengine watakuwa wameimarika zaidi na zaidi , aliamini Apollo, Artemis na Hermes kuwa katika viwango vya juu na majini ambao wapo levo ya maji ya upako wasingekuwa tishio kwao tena.
Roma hakuelewa ni kwa kiasi gani nguvu yake ya kiuungu ingeongezeka na wala hakuelewa ni kwa namna gani uwezo wake wa akili ungebadilika lakini alijua kitu kimoja nguvu hio ingemsaidia sana katika vita yake na majini.
Unatakiwa kuelewa uwezo wa miungu ulishuka kutokana na kuhama hama kutoka mwili mmoja kwenda mwili mwingine, mazingira ya dunia hayaendani na uwezo wao hivyo tokea walivyotua duniani uwezo wao wa kufikiri ulikuwa ukishuka kwa viwango.
Kufufuka kwa moyo wa Gaia inamaanisha kwamba Athena anajaribu kuyabadili mazingira ya dunia kuendana na yale yalivyokuwa katika sayari yao , wakati huo huo mazingira yakibadiika ingekuwa rahisi zile roho za ndugu zao zilizopotea kuamka.
Unaweza ukashangaa hapa sasa lakini hii inamaanisha kwamba hata kama binadamu wa enzi hizo ndio walitawaliwa roho zao na kufa nazo zingeamka kwa namna moja ama nyingine hata kama ni kutokea makaburini.
Kuna mambo mengi sana kuhusuiana na moyo wa Gaia kwani ni kitu ambacho kimevumbuliwa na watu ambao wana uwezo mkubwa sana wa akili mara kumi ya binadamu.
Roma hakuwa na mpango wa kutumia kanuni za anga kwenye kupambana, kama utalinganisha uwezo wake wa anga na wa kijini basi uwezo wa kijini ulikuwa mkubwa mno.
Kitu kingine alikuwa akikumbuka maneno ya Hades wa zamani kupewa uungu wake ilikuwa ni kwa ajili ya kuelewa viumbe hao kutoka sayari nyingine ,yaani kwa kauli nyingine ni kama Roma alipewa ufunguo wa kuelewa viumbe hao wanafikiria vipi, ijapokuwa hakujua sababu lakini moja kwa moja lazima Hades alimpa nafasi Roma ya kuelewa udhaifu wao na nguvu zao ili kuja kuwashinda kwa kutumia nguvu za kijini.
Muda ambao Jini Sui alipofika katika mazingira ya bahari ya Mediterraniani macho yake yalichanua , isitoshe maisha yake yote hakubahatika kutoka katika ulimwengu wa kijini.
Alishangazwa na mazingira ya fukwe na bahari , ijapokuwa asilimia kubwa ya ulimwengu wa kijini kuna mazingira yanayofanana na ulimwengu wa kawaida lakini bado ilikuwa ni tofauti.
Dakika ileile baada ya kufika juu ya ngome ya kifalme ya mfalme Pluto viumbe wawili waliovalia rangi ya zambarau na njano walitokeza mbele yao.
“Hubby!!!”
Walikuwa ni Rose na Magdalena walikuwa na furaha lakini pia na mshangao wa kuwaona , lakini zaidi sana walishangaa kumuona Roma alikuwa na mwanamke mrembo alievalia sketi fupi , wote walijiuliza Roma kamtoa wapi huyo mwanamke ambaye muonekano wake ni wa kipekee.
Roma alielewa mshangao wao palepale na aliongea haraka hraka kujitetea.
“Msifikirie sana huyu ni mlezi wa Rufi kutoka miliki ya Kekexil , ndio ambae amemlea kwa makuzi yake yote jina lake ni Sui”
“Mlezi wa Rufi !!!, unamaanisha ni jini mtu?”Aliuliza Magdalena kwa mshangao lakini kwa wakati mmoja walishangaa na kujiuliza kwanini Roma amemleta mlezi wake na sio Rufi.
“Twendeni chini kwanza , nitaelezea kila kitu”Aliongea Roma na kisha walikubaliana wote na kuingia ndani ya ngome.
Ilikuwa ni mchana tayari muda wa chakula na warembo wake wote walikuwepo wakiwa katika mavazi mbalimbali ya kupendeza.
Kwa mtu wa nje ambaye ungeona kinachoendelea ndani ya ngome hio hususani muda huo warembo hao walivyokusanyika katika nyumba moja ungesema Roma ashaionja pepo kabla ya kifo.
Kutokana na kujifunza mbinu za anga na ardhi walikuwa warembo marafudu zaidi , ngozi zao zilikuwa nyororo na macho yao yalikuwa ni kama vile wanalia kutokana na nguvu ya kijini lakini pia kupitia hatua ya ‘purification’ , ki ufupi walikuwa na mvuto na kila mmoja alikuwa na uzuri usiofanana na mwingine , ukitaka mrembo mwembamba Yezi alikuwepo , ukitaka mwenye mwili wa kutamanisha kingono Amina alikuwepo , akitaka shugamami Neema alikuwepo nakuendelea.
Mrembo Amina ndio aliekuwa wa kwanza kumkimbilia Roma na kujirusha kwenye mikono yake na kumbusu.
“Hubby kwanini umerudi mwenyewe , Rufi yupo wapi?”Amina alideka mikononi mwa Roma.
Marehemu Fayezi mtoto wa tajiri Khalifa angekuwepo hai na kumuona Amina alivyobadilika angepatwa na ukichaa mara kumi na sita.
Roma alikuwa na nguvu na alimshikilia na mkono mmoja Amina kwenye kiuno chake , huku akiwa na furaha kuona yupo katika levo ya mzunguko kamili.
“Bado bado , nimerudi kwasababu kuna kitu napaswa kushughulikia lakini pia kuangalia maendeleo yenu , Darling naona upo karibu kuifikia levo ya nafsi, kazi nzuri”
“Its not just me!,the others have great improvement too”Aliongea Amina, ukumbuke Amina hajui kiswahili kama ilivyo kwa Lanlan na Rufi tu.
Roma baada ya kukagua aliweza kuona kuna mabadiliko makubwa wakati ambao hakuwepo , alikuwa ameondoka kwa takribani wiki mbili.
Kwa mfano Rose na Magdalena walikuwa mwishoni mwa levo ya nafsi na Roma alikuwa na hamu ya kuona ni Dhiki gani wangepitia.
“Nasra , Dorisi , Mage , Neema na Yezi ambaye ameanza kwa kuchelewa wote walikuwa kwenye levo ya mzunguko kamili .
Kutokana na vidonge uwezo wao ulikuwa umeongezeka kwa kasi mno , Roma alitaka wapande levo kwa haraka sio kwa ajili ya kumsaidia katika mapambano yake lakini waweze kujilinda wao wenyewe lakini pia kuwa na maisha marefu.
“Edna yupo wapi , mbona simuoni hapa”Aliongea Roma mara baada ya kutokumuona Lanlan na Edna.
“Ametoka na Lanlan asubuhi , ndio tunapanga kuwatafuta maana Lanlan atakuwa na njaa”Aliongea Nasra ambaye alikuwa amevaa Apron .
Tokea siku ambayo wameanza kuishi pamoja walikuwa na muda wa kuburudika na ukiachana na kuongea na wanavisiwa pamoja na kuvuna nishati, ili kupoteza muda walikuwa wakifanya vile vitu ambavyo wana hobi navyo , kwa mfano Nasra na Dorisi walikuwa bize kwenye maswala ya upishi.
Ron hakutaka wasumbuke na alitaka kuajiri mpishi lakini walikataa na kusema wangejipikia wenyewe.
Roma aliridhika na jibu la mrembo Nasra na kisha palepale alimtambulisha Sui kuwa ni Jini mtu ambaye alikuwa ni mlezi wa Rufi.
Sui sasa ndio anagundua mahusiano yaliopo kati ya Roma na hao wanawake na alijikuta akishangaa na kujiambia Rufi amependa mwanaume kicheche..
Lakini licha ya hivyo hakumchukulia Roma vibaya kwani yupo tayari kumuokoa Rufi kutoka ulimwengu wa majini watu , alijiambia hakuna mtu ambaye amekamilika , Roma ni afadhali kulinganisha na hao majini ambao wanafanya mambo yao kwa siri.
Roma hakuelezea zaidi na alimzuia Magdalena ambaye alikuwa akitaka kwenda kumtafuta Edna na kumwambia ataenda yeye kuwalera
Warembo hao hawakuwa na pingamizi kwani walijua Roma ana mazungumzo na mama na mtoto pembeni.
Roma mara baada ya kutumia uwezo wake wa utambuzi palepale alipotea na kuja kuibukia juu ya mlima , ilikuwa ni eneo ambalo linavutia sana likiwa na maua mbalimbali.
Ni eneo ambalo kuna kaburi la Seventeen , sehemu ambayo Roma alimleta Edna wakati walipofika kusherehekea harusi..
Edna aliekuwa amevalia gauni la rangi nyeupe alikuwa amesimama pembeni ya kabuli hilo bila ya kuongea chochote akionekana kuwa ni mwenye mawazo, unyororo wa ngozi pamoja na nywele ndefu zinazopeperushwa na upepo , ilirandana na haiba yake ya utulivu pamoja na mazingira kikamilifu na mtu yoyote angeshikilia pumzi kutokana na urembo wake na kuishia kumwangalia tu kwa mbali.
Upande wa Lanlan alikuwa amechuchumaa akichezea maua na mara baada ya kugeuka ndio aliekuwa wa kwanza kumuona baba yake na macho yake yalichanua kwa mshangao.
“Dadiiii…!!”
Kama upepo alikimbia na kuruka na kwenda kumkumbatia na palepale Edna alishituka katika hali ya kimawazo na kumwangalia Roma akiwa na macho yaliojaa furaha pamoja na mshangao.
Roma alifurahi sana huku akimbeba juu juu binti yake na kumbusu shavuni kizungu kabisa na kumfanya Lanlan kucheka na kuficha sura yake kwenye shingo yake.
“Zimepita wiki mbili tu lakini uzito umeongezeka , ulikuwa ukilishwa nini?”Aliongea Roma kwa kingereza huku akishika tumbo la Lanlan akiwa na wasiwasi atakuwa bonge muda si mrefu.
Lakini hata hivyo hakuwa na wasiwasi sana , alijua akishapanda levo kwenye mafunzo basi itakuwa rahisi kwake kuondoa mafuta mwilini , hivyo ubonge wake ni wa muda tu.
Roma alimwangalia kwa macho ya kijini na palepale alijua nguvu yake ya kijini ilikuwa imeongezeka na aligundua Lanlan yupo tayari levo ya tano ya mbinu ya andiko la urejesho wa azimio na muda si mrefu ataweza kuingia levo ya nusu mzunguko.
Njia ya Lanlan ni ile ndefu na kadri ambavyo anajifunza ndio ambavyo nguvu yake inaongezeka , yaani yale maneno ambayo yapo katika andiko ni kwamba yanajiandika kimatendo ndani ya mwili wake na hio ndio maana ya Andiko la urejesho wa azimio.
Ni kama ilivyo kwa vitabu vya dini , ukiachana na mafundisho yake ambayo ni kama sheria kwa muumini nguvu yake ipo katika kuyageuza yale maneno na kuwa nguvu halisi, huo ni uzoefu ambao watu wengi wanye kumuamini Mungu wana ushahidi nao.
Sasa Lanlan alikuwa na uwezo ambao ulimfanya kufanikisha kuisharabu nguvu ya lile andiko mpaka kufikia levo ya tano kwa umri wake mdogo, haikuwa kwasababu tu ya kipaji chake lakini pia vidonge ambavyo Roma amempatia vilimsaidia, lakini Roma alijua akishapita hapo uwezo wake hakuna ambaye ataufikia kwani Lanlan msingi wake ni mbinu ya andiko.
Upande wa wengine Roma alikuwa akiwafundisha mbinu ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi njia ya mkato ambayo ameiboresha zaidi na sio njia ndefu kama ya Lanlan na yeye pia.
Kuhusu Lanlan kuendelea juu zaidi mpaka kumfikia Roma au kumpita Roma hakujihanganisha kwani ni mambo ambayo yapo nje ya ufahamu wake lakini hata hivyo alitamani kuona mtoto wa Seventeen kumpita hata yeye.
“Its because I’m growing up . I’ m not fat”Aliongea Lanlan akimaanisha kwamba ni mzito kwasababu anakua na sio ubonge.
“Acha kutoa visingizio , unakuwa mzito lakini hurefuki , sio mbaya , kwasababu unajitahidi kwenye mafunzo kula upendavyo hata sahani kumi”Aliongea na kumfanya Lanlan kufurahi.
“Umeniletea zawadi?”
Kama kawaida Lanlan alikuwa ni mtoto ambaye anadhani baba yake amesafiri kibiashara na sasa ndio anarudi na angemletea zawadi kama alivyomzoesha.
Roma alifikiria kidogo na alikumbuka Dhana alizoiba katika lile Jumba jeupe na palepale aliitoa moja inayong’aa na kisha kumpatia , ilikuwa ina maandishi na ilikuwa ikipendeza kwa macho.
Ilikuwa ni Dhana ambayo ina uwezo wa kukamata jini lolote lile ambalo lipo chini ya levo ya kuipita Dhiki na kwasababu aliona haina matumizi kwake sio mbaya Lanlan kuitumia kama kifaa cha kuchezea.
Lanlan ijapokuwa hakuipenda kwasababu sio chakula lakini alikuwa amefurahi kuona baingiri hio ya Dhahabu.
Edna alisimama tu pembeni akiangalia mambo ya baba na mwana na alishindwa kuzuia tabasamu kwenye uso wake na kumfanya kupendeza zaidi.
Alimsogelea Roma na kisha alishika mkono wa Lanlan na kuangalia bingiri ambayo Lanlan ashaitumbikiza kwenye mkono wake.
“Hii si Dhana , naona ni hasara kumpatia kama kifaa cha kuchezea”Aliongea na kumfanya Roma kucheka.
“Kwanini iwe ni hasra wakati ni zawadi kwa binti yangu , ninazo nyingi tu nimezichukua huko ujinini na sizihitaji maana ni za daraja la kati na la chini nilikuwa nikipanga kuwapatia , babe kwasababu wewe ndio mke wangu kipenzi na Komandoo wa moyo wangu ngoja nikupe nafasi ya kuchagua kwanza “
“Nichukue , Mhmh..!! nina uhakika umeua na kisha ukaziiba , hawawezi wakakupatia Dhana zao kwa hiari , vipi umefanikiwa kumuokoa Rufi , nini kimetokea huko?”
Roma aliangalia uelekeo wa ngome na kisha akamgeukia.
“Nitakuambia tukiwa njiani “
Mkono mmoja alimpakata Lanlan na mkono mwingine alimshikilia Edna mkono na walianza kutembea kurudi chini ya mlima , kutoka eneo hilo na ngomeni umbali ulikuwa mfupi sana na Roma alitembea taratibu ili kupata muda kidogo wa kuwa na mke wake na binti yake.
Hususani katika wakati kama huo ambao alikuwa amepitia hatari nyingi katika ulimwengu wa kijini na mapambano ya kutisha , Roma aliona ashukuru kila dakika na saa anayokuwa na wapendwa wake.
Wakati wakiwa wanatembea alimwambia Edna kila kilichotokea katika ulimwengu huo , ijapokuwa maelezo aliona ni ya hatari na kumuogopesha Edna lakini alielezea kila kitu.
Kama kawaida Edna aliishia kutingisha kichwa tu bila ya kuuliza swali.
Wakiwa njiani watu wa visiwa hivyo kila walipomuona walisimama na kuonyesha heshima na Roma aliwapungia tu mkono na kupita.
Alisalimiana pia na baadhi ya wanajeshi ambao waliokuwa chini ya ngome hio kwa muda kabla ya kuelekea ndani.
“Oh vizuri.. , hivi kwanini umefikriia kumpeleka Lanlan kwenye kaburi la mama yake , haujisikii vibaya?”Aliuliza Roma ukweli alikuwa na shauku ya kutaka kujua ni sababu gani Edna amemkuta mbele ya kaburi la Seventeen.
Unadhani atatoa jibu gani?
Ok
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGAQNOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 711.
Tulipoishia:
Roma amefanikiwa kumuokoa Jinni Sui mlezi wake Rufi kutoka ulimwengu wa majini watu na kumpeleka Visiwa vya wafu.
Roma mara baada ya kurudi Visiwa vya wafu anamkuta Edna akiwa katika kaburi la Seventeen akiwa na Lanlan , Roma anamuuliza Edna imekuwaje akampeleka Lanlan katika kaburi la mama yake , je hajisikii vibaya?
Endelea nayo sasa:
Ukweli ni kwamba Roma alitamani kulizika kabisa jina la Seventeen katika moyo wake na asingependa tena kulitaja mbele ya Edna , sio kwamba hakuwa na ujasiri wa kulitaja lakini ukweli ni kwamba hakutaka kugombana na mke wake tena.
Uhusiano wao kwa wakati huo ulikuwa umeimarika hivyo aliona yaliopita si ndwele na wagange yajayo.
Edna akiwa ameinamisha kichwa chake alishia kutoa tabasamu hafifu na kisha kujibu swali la mume wake.
“Alikuwa ni mama yake Lanlan hivyo niliona nimruhusu Lanlan kukaa pale kwa muda hata kama hakuzikwa pale , nimefanya hivyo ili kumfanya Lanlan kumtambua mama yake mzazi”
“Haujisikii vibaya ?”
“Hapana , haijalishi ilikuwaje lakini kwasasa mimi ndio mtu ambaye nipo na wewe , mimi ndio mshinda si ndio?”
Roma aliishia kugeuza macho yake na kumwangalia Lanlan ambaye alikuwa haelewi kinachoendelea kwa muda.
“Lanlan mama yako ni mtu muungwana na mkarimu dunia nzima , unapaswa kumjali sana ukishakua mtu mzima , sawa?”
“I’m a good kid”Alijibu Lanlan akimaanisha kwamba yeye ni mtoto mwema.
“Nashangaa kuna mtu aliniambia anataka kuniua mbele ya mtoto”Aliongea Edna na kumfanya Roma kuingiwa na ubaridi.
“Haha… kwanini unakumbushia yaliopita , niliongea vile kwasababu ulinifanya mjinga , kama usingeniigizia nisingeongea vile”Aliongea na kumfanya Edna kubetua mdomo huku akikwepesha macho yake.
“Babe hupaswi kuyaweka moyoni yale maneno , kuna muda siwezi kuzuia hisia zangu ijapokuwa ninaweza kujizuia kufanya baadhi ya vitu kutokana na nguvu zangu lakini sina uhakika asilimia mia , hebu fikiria wewe mwenyewe mimi nakupenda sana na hata ukiniua sitoweza kukujeruhi kwa namna yoyote ile’
Bila ya kueleweka nini kimemkuta, Edna mikono yake ilianza kutetemeka kutokana na kauli ile na alionyesha kuwa na wasiwasi.
Roma na yeye palepale aliona Edna muonekano wake umebadilika kabisa alimuona ni kama vile alikuwa akipitia maumivu moyoni.
“Edna nini tatizo?”Aliuliza Roma akiwa na wasiwasi.
Edna aligeuka na kumwangalia Roma , muonekano wake ulikuwa umegubikwa na hisia ambazo hazikueleweka.
“Unasema hata… hata kama nikikuua huwezi kunizuia?”Aliuliza kwa sauti iliojaa kitetemeshi.
Swali hilo lilimshangaza Roma , hisia zake zilibadilika palepale lakini alijitahidi kuficha na kutoa tabasamu.
“Ndio nilivyosema na siwezi kwenda kinyume na maneno yangu , wewe ni mke wangu mama wa mtoto wangu , nitawezaje kukuumiza , siwezi kukuona unapata jeraha lolote lile hata kama itanigharimu kifo changu”
Macho yao yalikutana baada ya ile kauli na kila mmoja alikaa kimya bila ya kuongea neno , hatimae Roma aligeuza macho yake na kuangalia ngome yao .
“Lanlan atakuwa na njaa , tutaongea baada ya chakula cha mchana”Roma alivunja ule ukimya.
Edna aliishia kutingisha kichwa na kumfuata Roma kwa nyuma kuingia katika ngome hio ya kifalme.
Katika eneo kubwa la ukumbi wa chakula ndani ya makazi hayo ya mfalme Pluto , wanawake walikuwa wamekaa katika meza mduara huku wakiongea kujaribu kumchangamsha Sui , huku mara kwa mara wakimuuliza kile ambacho kilitokea huko ujinini.
Baada ya Roma kuingia akiwa na Edna waliungana nao katika meza na kuendelea kupata chakula.
Baada ya chakula cha mchana Roma alielezea kwa ufupi kile kilichotokea lakini pia alielezewa kilichotokea kwa kipindi ambacho hakuwepo hapo visiwani.
Wanawake wake walikuwa washazoea mazingira ya kisiwa hicho na baadhi yao pia hawakuwa wakiishi hapo.
Kutokana na Clark kuwa mwanafamilia wa jumba la kifalme kutoka Wales na alikuwa na wanafunzi dunia nzima aliondoka kwenda kudili na maswala yake ya kitafiti na kufundisha baada ya kuingia katika levo ya Nafsi, ijapokuwa alikuwa na nguvu za kijini lakini ‘passion’ yake ilikuwa kwenye maswala ya sayansi na teknolojia.
Kuhusu Sophia umaarufu wake uliendelea kupaa juu kileleni na kwa wakati huo alikuwa kwenye Tour nchini Marekani na kuendelea kufanya Collabo na wasanii wakubwa wa taifa hilo.
Ki ufupi ni kwamba alikuwa akiyafurahia maisha yake ya muunganiko wa mziki ambayo ni kazi yake na kuvuna nishati za mbingu na ardhi, ijapokuwa alikuwa bize lakini mara kwa mara alikuwa akitembelea visiwa hivyo.
Upande wa Najma alikuwa bize na maswala ya kisiasa , hatua ya kwanza ilikuwa ni kusaidiwa kuingia katika ulingo wa siasa na kwanzia hapo alihitaji kufanya juhudi yeye mwenyewe ili kuweza kuonekana, ki ufupi alikuwa akifurahia kazi yake ya usemaji ndani ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki.
Sasa Roma mara baada ya kuona kila mmoja ameridhika na alikuwa na chakufanya alipata utulivu wa akili , lakini hata hivyo hakutaka kupumzika kazi kubwa iliokuwa mbele yake ni kumuokoa Rufi.
Katika wakati huo alikuwa ashasababisha machafuko katika ulimwengu wa kijini hivyo mpango wake wa kurudi alipaswa kuuandaa kimakini sana, lakini aliona kwasababu alikuwa amemuokoa Sui na kuja nae nje basi angeweza kupata taarifa za kutosha kuhusu ulimwengu huo.
Mchana yote baada ya chakula walimsikiliza Sui akielezea taarifa zote zinazohusiana na ulimwengu wa majini watu hususani katika miliki ya Xia.
Katika maelezo yake walikuja kushangaa baada ya kgundua alikuwa na miaka sitini na alishawahi kuolewa lakini mume wake alikufa katika vita na miliki ya Panas.
Kitendo cha Zilha kumchezea mwanamke ambaye ni mkiubwa kwake kwa zaidi ya miaka ishirini Roma aliona pengine hata kifo haikuwa adhabu ya kumtosha.
“Miliki ya Xia ina majini wengi ambao wapo levo ya maji ya upako , hata mkuu wao Jinni Anjiu ndio ambaye ana nguvu za kijini kubwa zaidi katika miliki, uwezo wake ni mkubwa sana mwishoni kabisa mwa levo ya maji ya upako , hapatani kabisa na mdogo wake Zianji, mwanzoni alikuwa na uwezo mkubwa kuliko Anjiu lakini alimtega wakati alipokuwa akipitia Dhiki ya mbingu , kidogo tu afariki lakini kwa bahati nzuri aliweza kurudiwa na uwezo wake wa kijini na sasa yupo mwanzoni mwa maji ya kiroho , Guru wa miaka mingi katika ukoo huo anafahamika kwa jina la Master Laofi, yeye yupo katikati mwa levo ya maji ya upako na hana mahusiano mazuri na Anjiu na Zianji kwasababu baba yake ndio alipaswa kuwa Mkuu wa miliki , kulingana na umri wa Anjiu na mdogo wake uwezekano wa wazazi wao kuwa hai ni mkubwa na inawezekana wapo chini ya kitengo cha Taisha au jumuia yoyote”
Roma moyo wake ulikuwa katika kiwewe , alipata wakati mgumu sana katika kupambana na jini Tigola ambaye yupo katikati mwa levo ya maji ya upako, kama atakutana na majini watatu ambao wote wapo levo ya upako na kupatiwa mashambulizi mengi basi kuna hatihati ya kufa.
“Nimesikia mbinu ya kijini katika miliki ya Xia ni nzuri zaidi kuliko koo zote , je unaweza kuelezea?”
“Koo zote tatu ukiachana na Hongmeng mbinu zao za juu hufunzwa wale warithi tu wa miliki , nadhani umeweza kuona mbinu ya Kekexil ya Aoki , ni mbinu ambayo imejikita katika elementi za miti kwa njia zote za mashambulizi na kujilinda , Panas mbinu yao ya mafunzo inafahamika kwa jina la Tailiba neno ambalo tafsiri yao ni ‘Jinini True force’, ni mbinu ya kijini ambayo ni ya hatari sana kwani inachukua elementi za madini na chuma , inasemekana ni mbinu ambayo wameirithi kwa jini aliewahi kuwa na nguvu kubwa wa enzi hizo aliefahamika kwa jina la Baidi yaani Joka Kuu jeupe kutoka Magharibi, kuhusu koo ya Xia mbinu yao inafahamika kwa jina la RoshiniSutra , ni mbinu ambayo inaimarisha mara mbili nishati ya mbingu na ardhi , ukiachana na uwezo wake wa uharibifu lakini ina uwezo wa kufanya ‘manipulation’ ya elementi zote tano , kwasasa ni Anjiu ambaye ameweza kufanikisha kuitumia yote kwa silimia zabini , anao uwezo wa kuiga mbinu ya jini mwingine kwa asilimia sabini kwa kuangalia mara moja tu”
“Huo utakuwa usumbufu sasa , kama nitakuwa sahihi basi huyu Jinni Anjiu atakuwa ananijua vizuri nje ndani , kama nitaenda moja kwa moja basi atanijua mara moja, nadhani napaswa kujua wapi Rufi alipo kwanza kuliko kwenda kumtafuta kila mahali , oh tena hebu niambie vipi makao makuu yao ni makubwa kuliko ya Kekexil?”
“Ndio ni miliki kubwa sana kuliko miliki zote ina maelfu ya raia ambao wanaishi makao makuu , ni miliki ambayo tamaduni zao zinafanana kwa kiasi kikubwa na Hongmeng na wanatumia madini ya Jedi nyeupe katika ujenzi wao wa nyumba , huku majengo yote yakiwa na safu za mwanga wa kijini kwa ajili ya ulinzi , ndio sehemu ngumu kuzamia kati ya miliki zote za kijini. Wakati wa kumtorosha Rufi sikuweza kutembea tembea hivyo sijui mengi”Aliongea kwa huzuni lakini Roma alimtoa hofu.
Baada ya kufikiria kidogo Roma alikumbuka jambo na alimgeukia Magdalena.
“Magdalena mtoto wa Master wako , Wang Shu si ni sehemu ya koo ya kijini ya Wang , hii koo si ina uhusiano na miliki ya Xia, vipi bado yupo katika dhehebu la Tang?”
“Master aliniambia nisikueleze ukweli , lakini kwasababu umeuliza sina haja ya kukuficha , ukweli ni kwamba Wang Shu alipotea”
“Alipotea!!?”
“Ndio , siku mbili mara baada ya kuondoka katika ngome ya Tang alipotea , Master yeye pia hajui ni wapi ameelekea na alimtafuta bila mafanikio , Master alikuwa katika huzuni na aliniambia juzi tu hapa na hakutaka nikuambie kutokana na matatizo uliokuwa nayo”
Roma alishangazwa na jambo hilo alitumia mbinu yake ya andiko kumpata mtoto wake Tang Luyi lakini mara baada ya siku chache tu akapotea , aliona kwa mwanamke yoyote mwenye roho nyepesi angekosa uvumilivu.
Ukweli Roma aliona pengine kwasababu koo ya Xia ina utamaduni mwingi unaofanana na wa kichina basi angetumia matawi yake kuzamia , lakini kupotea kwa Wang Shu ilimaanisha asingekuwa na taarifa hivyo ingekuwa ngumu kuzamia.
“Mr Roma haina haja ya kuwa na wasiwasi namna hio , ijapokuwa wanaweza wakawa wamemteka Rufi lakini hawawezi kumfanyia kitu kibaya , isitoshe wanauhitaji mwili wake kwa ajili ya majaribio ya dawa , kibaya ambacho atakipata ni mateso ya kimwili tu”
Roma alona Sui alikuwa na pointi, kutokana na majini kutokuwa na uwezo wa kutumia kanuni ya andiko la urejesho basi wasingemwingilia Rufi kimwili kwani wanaogopa mwili wake ambao una sumu.
“Okey hubby punguza wasiwasi , kwasasa unapaswa kupumzisha akili kabla ya kurudi , tulitamani kukusaidia kama uwezo wetu ungekuwa unakidhi”Aliongea Rose.
“Usiwe na wasiwasi nipo ngangari , nitapumzika leo na kesho nitarudi , nina mpango kichwani namna ya kukabiliana na hali nitakayokutana nayo”
Baada ya kuongea hivyo hakuna ambaye aliuliza swali , walijua swala la Rufi kuokolewa lilikuwa ni la muhimu na sio la kuchelewesha hivyo haikuwa na haja ya kumuomba akae nao kwa muda kidogo.
Kwasababu alikuwa na usiku mmoja tu wa kukaa ndani ya kisiwa hicho basi alitoa zile mbinu na baadhi ya Dhana alizoiba katika ulimwengu wa kijini na kuzigawanya kwa kila mmoja.
Kwa Rose na Magdalena walikuwa na uwezo wa kujifunza mbingu nyingine zaidi za mafunzo wakati wengine wakitafuta kuingia katika levo ya nafsi.
Levo ya nafsi ndio kama mafanikio kwa jini au binadamu, ukishaingia katika levo ya nafsi inamaana umeweza kuvukwa vikwazo vyote na sasa upo nje ya duara na akili yako inafanya kazi tofauti na binadamu , ni kama vile unakuwa nusu jini na nusu binadamu , levo ya nafsi inamaanisha sasa kuanza kuona siri za ulimwengu,inamaanisha kuona dunia katika mtazamo tofauti.
Baada ya chakula cha usiku Roma alienda katika ‘basement’ yake kwa ajili ya kuendelza kazi ya kutengeneza vidonge.
Wakati huo alikuwa na mimea mingi hivyo aliamini angeweza kutengeneza vidonge vingi sana , spidi ya Roma katika utengenezaji wa vidonge ilikuwa ni tofauti na majini , yeye alikuwa na chungu chenye nguvu na uwezo wake wa kijini ulikuwa mkubwa lakini vilevile alikuwa na andiko la malkia wa Tushani alilopewa na Aoiline hivyo kazi yake ilikuwa nyepesi sana.
Mpaka inakuja kufika saa sita usiku alikuwa ametengeneza vidonge vingi sana na aliweza kuvipangilia kutokana na ubora wake na kisha akaondoka katika chumba hicho
Roma mara baada ya kutoka aliangalia vyumba ambavyo vilikuwa katika floor ya pili , ngome hio ilikuwa kubwa mno hivyo vyumba vyake vilikuwa vikubwa pia , katika kila mlango kulikuwa na jina kuonyesha ni chumba cha nani.
Kwa jinsi majina hayo yalivyokuwa yanasomeka ilikuwa ni kama vile shetani anamtawala ili kujiingiza katika starehe.
Kama asingekuwa na mawazo juu ya Rufi basi angejichekea kwa baraka alizokuwa nazo hapo ndani .
Ni chumba kimoja tu ambacho hakikukuwa na jina na hiko kilikuwa ni cha Edna na kilikuwa katika floor ya tatu kikiwa na sebule yake.
Kwasababu alikuwa na usiku mmoja tu aliona mtu pekee wa kulala nae ni mke wake hivyo alienda moja kwa moja mpaka floor ya tatu.
Dakika ambayo anafungua mlango uso ulimshuka , Edna alikuwa amelala akiwa amekumbatiana na Lanlan ambaye mdomo ulikuwa wazi.
Roma alijiuliza kwanini Lanlan kalala na mama yake tena , palepale alijiambia anapaswa kumwandalia chuma chake cha hadhi ya mtoto wa mfalme katika floor hio hio karibu na mama yake ili aweze kupata uhuru na mke wake.
Baada ya kuwafunika vizuri na shuka alitoka nje na kufunga mlango na kushuka floor ya pili akiwa hajui aibukie chumba cha nani.
Alitumia uwezo wake wa utambuzi kuona kama kuna mrembo yoyote ambaye hajalala na aligundua wote wapo usingizini kasoro Amina peke yake na alijiona kuwa na hatia kwani ni muda mrefu sana hajakuwa nae karibu hivyo hakujiuliza mara mbilimbili na kuelekea kwenye chumba chake.,
Roma mara baada ya kufika aligundua Amina alikuwa akifanya tahajudi kujifunza mbinu za anga , chumba chake kilikuwa kikinukia mno na kilikuwa kimepambwa kwa kila kitu kwa rangi ya pink.
Roma ilibidi akae kimya kimya pembeni yake akimwangalia kwa muda mpaka atakapomaliza.
Nusu saa mele Amina alifungua macho yake mara baada ya kuhisi pumzi ya mtu mwingine ndani ya chumba na alishanga mara baada ya kuona ni Roma.
“Hubby , kwanini upo hapa , ushamaliza kutengeneza vidonge?”
“Ndio”Aliongea Roma na kisha palepale alimkumbatia na kumbusu kwenye paji la uso.
“Babe , una juhudi sana , muda huu wenzio wote wamelala lakini wewe upo kwenye mafunzo?”
“Sina jinsi , mimi sina akili kama wengine wote , kila mmoja ana kipaji kikubwa kuliko mimi hivyo kupelekea uwezo wangu kupanda kidogo kidogo sana , siwezi kupigana pia na naogopa nitakuja kuwa mzigo kama kila mmoja atafanikiwa kuingia katika levo ya nafsi, ndio kwanza nimeingia levo ya mzunguko kamili, nitakuwa tofauti na wenzangu ..”Aliongea huku akitia huruma.
“Hey! Unaongea ujinga gani , kwanini uwe tofauti , sichagui wanawake kwasababu ya levo zao, utakuwa kipenzi changu milele..”Aliongea Roma huku akijifanyisha kukasirika.
“Hubby mimi nakuamini, lakini ujue wewe sio mtu wa kawaida na tuna wasiwasi unaenda katika ulimwengu wa majini peke yako , ni sehemu ya hatari lakini hatuwezi kufanya chochote kwasababu uwezo wetu ni mdogo , lakini haimaanishi itabakia hivyo milele , Rose , Magdalena na hata Sophia na Clark wote wapo mwishoni mwa levo ya nafsi na wataingia levo ya Dhiki muda wowote na watakuwa na uwezo wa kukusaidia ,Mage na Nasra wapo fasta sana kuliko mimi na pia washaanza kujua namna ya kupambana kijeshi , Da’ Neema na Dorisi ijapokuwa uwezo wao unaweza usiwe mkubwa lakini nguvu zao za kijini ni kubwa mno kuliko za kwangu , hata Yezi ambaye ameanza kwa kuchelewa sasa hivi ananikaribia , mimi ndio kilaza tu na naogopa mwishoni nitakuwa mzigo na nitajisikia vibaya ikiwa hivyo”
Roma alijisikia vibaya kutokana na maneno yake , ilionekana alikuwa na uchungu kutokana na kuwa nyuma nyuma kuliko wengine wote.
“Hey Babe , kwanini umekosa kujiamini , Amina ninaemjua mimi siku zote alikuwa ni mwenye kujiamini , nakumbuka aliweza hata kunitega kwa ajili tu ya kutimiza haja zake , kama utaendelea kuwa mtu ambaye hujiamini na kuanza kujionea huruma sitokupenda , umenielewa?”Aliongea akiwa siriasi na kumfanya Amina kumwangalia Roma kimahaba na dakika ileile alishindwa kujizuia tena na kuanza kupeana busu nyevu.
Roma aliijikuta akiwa katika ulimwengu mwingine , Amina likija swala la sita kwa sita alikuwa mtundu kuliko wanawake zake wote, ijapokuwa alimkuta bikra mwanzoni alishindwa kuelewa ni kwa namna gani ameimarika kwa kiasi hicho.
Walizungushana kwenye chumba hicho kwa muda mrefu sana wakifanya Romance dakika therathini mbele Amina alikuwa chapachapa huku macho yakiwa yamemlegea na Roma hakutaka kumchelewesha kwani alionyesha kuteseka.
Kiuno cha kwanza , cha pili , cha tatu ,….. cha kumi, Roma alijikuta akihisi hisia ambazo hazikuwa za kawaida kila alipokuwa akipanda ni kama kuna nguvu ambayo sio ya kawaida inamvuta ndani na kupelekea vinyweleo ya mwili kusisimka kwa kiwango kikubwa , ajabu ni kwamba ndani ya dakika kumi tu alishindwa kuendelea na kushusha mzigo , alijitahidi kujizuia kujikontrol lakini ilishindikana.
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupanda juu ya mwanamke na kushuka ndani ya dakika kumi tu, upande wa Amina na yeye aliweza kufika kileleni muda sawa na wa Roma na kuanza kukakamaa mwili huku kiini chake cha macho kikiwa kama kinapotea na kurudi kama saa mbovu.
Ilikuwa ni kama vile Roma ameshikiliwa na vinyuzi nyuzi vya msisimko ambavyo vilitoka katika mwili wa Amina na kuingia katika mwili wake na kushikilia katika chanzo cha nguvu zake za kijini.
Hali hio ilishawahi kumtokea wakati akiwa na Dorisi lakini awamu hio ilikuwa ya tofauti sana kwani ilikuwa ni kama vile kuna nyaya za umeme zimeunganishwa kati yake na Amina kusafirisha nishati ya mbingu na ardhi kutoka katika mwili wake na mwili wa Amina.

SEHEMU YA 712.
Katika hali ambayo Roma alikuwa akipitia alitaka kumuuliza Amina kama anasikia utofauti kama ambao anausikia yeye lakini alipomuangalia Amina macho yake kile kiini cha jicho kilikuwa kikibadilika badilika rangi na kwenda kijani na kupotea kama vile ni saa
Amina hakuwa akijielewa yeye alikuwa akihisi raha za ajabu, ijapokuwa Roma alikuwa ameacha kupeleka moto kutokana na kufika kileleni lakini mwichi wake ambao umemuingia ulimpa msisimko ambao haukuwa wa kawada lakini alishangaa kuona Roma anamwangalia kwa macho ya mshangao.
“Babe kwanini unaniangalia hivyo?”
“Kuna kitu chochote ambacho sio cha kawaida unajisikia?”
“Najihisi ni kama vile damu yangu inachemka na inaleta raha flani hivi?”
“Vinazidi kuongezeka , Mpenzi unaniingizia nini?”
“Mimi mwenyewe sijui kinachotokea?”
Amina aliishia kufumba macho huku akitoa tabasamu, wakati Roma akijihisi ni kama mwili wake umaungana na Amina huku akishindwa kutoa dudu yake nje upande wa Amina alijihisi ni kama vile ametumia madawa ya kulevya.
Roma aliweza kugundua sasa kinachotokea, ukweli ni kwamba alishasikia kuna mbinu ya kijini ambayo inaweza kumuwezesha mwanamke kupanda levo kupitia mwanaume au mwanaume kupanda levo kupitia mwanamke.
Mawazo yake yalikuwa sahihi kabisa , kama unakumbuka yule msichana jini kutoka China afahamikae kwa jina la XiaoXiao alitaka kumfanya Roma kuwa mpenzi wake na kumtumia katika kupanda levo, hii haitokei tu mara nyingi inatokea pale kati ya mwenza kuwa na hisia nyingi sana zidi ya mwenzake , ukishakuwa na hisia nyingi zidi ya mwenza wako mara nyingi wewe ndio unafaidika na ndio ambacho kilikuwa kikimtokea Amina , alikuwa na hisia nyingi zidi ya Roma hivyo alikuwa akifaidika na uwezo wake.
Upande wa Roma hata kama mbinu hio ipo lakini kwanini ni kama vile amenasa ndani ya mwili wa Amina na kushindwa kutoa naniliu yake , ukweli sio kwamba alikuwa akishindwa bali kuna nguvu ambayo ilikuwa ikiasili fahamu zake na kumfanya aendelee kuitumbukiza.
Katika hali ya kushangaza Amina nguvu zake zilianza kuongezeka kwa kasi mno na mara tu aliweza kufikia katila mwishoni mwa levo ya mzunguko kamili na Roma bila ya kujielewa alianza kuchezesha kiuno kushuka na kupanda na kumfanya Amina kuanza kujipinda pinda kama nyoka na kadri Roma alivyokuwa akiendelea ndio nguvu ya Amina ilivyokuwa ikiongezeka , hakika hali hio ilimshangaza.
Roma kuona hali hio aliendelea kuzidisha kasi alikuwa akijisikia vizuri sana , ijapokuwa uwezo wake ulikuwa haupungui wala kuongezeka lakini fahamu zake ni kama zimeunganishwa na Za Amina.
Lisaa limoja mbele Amina alijikuta akiingia levo ya Nafsi na hatimae alijikuta akifumbua macho yake na kuyakutanisha na Roma na alihisi mwili wake ukiwa na hisia ambazo sio za kawaida huku macho yake ni kama vile yanapulizwa na upepo wa baridi kali kiasi cha kumfanya machozi kumtoka mwenyewe bila ya kujielewa.
“Hubbby..nimewe”
“Ndio umeweza , upo mwanzoni mwa levo ya nafsi sasa , ijapokuwa sijui ni nini kimetokea lakini naamini sio jambo baya, muda si mrefu utaweza kupata ufunuo wako”Aliongea Roma na sasa Amina alionekana kuwa mwanamke mtu mzima zaidi kuliko alivyokuwa mwanzo.
*******
Miliki ya Panas ipo kusini kabisa mwa ulimwengu wa kijini, miliki hii ipo mbali sana kutoka miliki nyingine, inasemekana ni rahisi kusafiri kuingia katika miliki ya Panas ukiwa duniani kuliko ukisafiri kutoka Kekexil katika ulimwengu wa kijini kwenda Panas.
Haikueleweka ni kwanini lakini njia ya mkato na rahisi zaidi ni kupita duniani, lakini hata hivyo kutokana na sheria za majini katika ulimwengu wa kawaida hawakutumia njia ya duniani kwani ni ya hatari zaidi kulinganisha na ya ulimwengu wao.
Tofauti kubwa ya Panas na jamii nyingine za majini ni ustaarabu wao kuendana kwa asilimia nyingi sana na binadamu wa kawaida , miliki ya Panas jamii yake hata hivyo haikuwa kama ilivyo kwa jamii ziingine , hii ni jamii ambayo huundwa na majini Chotara.
Katika hisrotia inasemakana kwamba hapo mwanzo kabisa kabla ya kuwepo kwa jamii ya Panas jini mwanamke aliefahamika kwa jila la Zildali aliasi kutoka katika familia yao kwa kukiuka sheria na kutembea na binadamu mpaka kumpelekea kupata ujauzito.
Kitendo hicho kiliikasirisha sana familia yake na kutaka kumuua kulingana na sheria lakini Zildali alifanikiwa kutoroka na kukimbilia katika ulimwengu wa kawaida kwa ajili ya kuendelea kuishi na mpenzi wake.
Kitendo cha Zildali kutoroka kilizidi kuwakasirisha majini na kupelekea kutumwa kwa wajumbe ulimwengu wa kawaida kumtafuta Zildali popote pale na kwa bahati nzuri waliweza kumpata yeye mwenyewe na mpenzi wake binadamu na katika harakati za kumkamata Zildali mpenzi wake binadamu alifariki kwa kuuliwa na majini lakini Zildali akafanikiwa kuondoka kwa namna ambavyo majini waliotumwa kumkamata walishindwa kuelewa amepotea vipi kwenye upeo wao kwani Zildali uwezo wake ulikuwa ni wa kawaida tu kuliko wa kwao.
Kitendo cha kupotea kwa Zildali kiliwafanya kurudi ujinini na kutoa taarifa kupotea kwake na hapo ndio ikawa mwisho wa jina la Zildali kutajwa katika miliki yake.
Zildali upande wake hakufariki bali alivutwa na kani ambayo haikuelezeka na alipokuja kushituka alikuwa katika ulimwengu wa kijini katika eneo ambalo hakuelewa ni wapi , lakini kutokana na mazingira kufanana na ulimwengu wa kijini alielewa alikuwa katika ulimwengu wa kijini wa peke yake.
Zildali kwanzia hapo ndio aliona hio ni sehemu sahihi ya kujificha huku akimuomboleza mpenzi wake binadamu pamoja na kulea ujauzito.
Miezi ya kujifungua mara baada ya kutimia aliweza kujifungua kawaida kabisa kama binadamu na kupata mtoto wa kiume ambaye alimpatia jina la Panas na eneo lake la mafichoni kwanzia siku hio pakaitwa Panas.
Zildali alijaribu mara nyingi kutoka katika ulimwengu huo kurudi ujinini lakini alishindwa kabisa kwani kila alivyokuwa akisafiri ni kama anazunguka na kurejeshwa katika eneo lilelile , hali hio ilimpa hisia mchanganyiko , hisia za furaha pamoja na za huzuni kwa wakati mmoja , alipatwa na huzuni kwa kuona mtoto wake Panas amezaliwa katika ulimwengu ambao hauna muunganiko na miliki zingine za kijini na furaha yake ilitokana na kwamba aliona hilo ni eneo zuri na salama la kuanzisha maisha.
Katika harakati za kuendeleza kizazi alimtoa Panasi mtoto wake na kwenda kuoa mwanamke kutoka jamii nyingine ya kijini na hapo ndio uzao wao ulipoanza kuongezeka , lakini haikuishia hapo tu watoto wa Panas waliweza pia kutembea na binadamu na kupata watoto na kurudi nao katika ulimwengu wa kijini na miliki yao iliongezeka zaidi na zaidi na kuwa na majini mchanganyiko ambao asilimia themanini ni majini na asilimia ishirini ni binadamu.
Haikueleweka kwa undani mbinu yao ya kijini ya mafunzo waliipata vipi lakini walianza kujifunza mbinu za anga na kuendelea kuwa miliki yenye nguvu mpaka ikafikikia kipindi wakagundua sasa namna ya kutoroka katika miliki yao kwenda miliki nyingine.
Hivyo hio ndio miliki ya Panas ilivyoanza na kuwa na tamaduni za kipekee kabisa tofauti na jamii nyingine za kijinni, walitwa majini chotara kutokana na mchanganyiko wao wa kibinadamu na kutokana na hilo wakawa na tabia zinazofanana na binadamu na ndio maana mpaka leo hii kwanzia muundo wa majengo yao unafanana kwa asilimia mia moja na binadamu wa kawaida.
Ni rahisi kukuta ghorofa la vioo katika miliki ya Panas lakini huwezi kukuta ghorofa hilo katika miliki a Hongmeng au Kekexil.
Ndani ya miliki ya Panas kulikuwa na usanifu wa kila namna kuanzia maghorofa yalioenda hewani mpaka majumba ya kimakazi ambayo yamejengwa kwa mawe na matofali pamoja na vyuma na madini ya kila namna.
Sasa katikati ya makao makuu ya miliki ya Panas katikati kulikuwa na jengo refu la ghorofa kama arobaini hivi ambalo limepakana na majengo mengi yaliokuwa yameachana umbali mrefu.
Katika jengo hilo ndani yake anaonekana mwanaume jini alievalia mavazi ya suti akiwa amekaa katika ofisi kubwa ambayo ilikuwa juu kabisa ya Floor ya jengo hilo.
Amevalia blazer rangi nyeusi na jeans ya kubana na alionekana kuwa mrefu kwa sentimita kama 170 hivi , mbele ya meza yake wamesimama wanaume wawili ambao mmoja amevalia mavazi ya kanzu , jini huyo hakuwa mwingine bali ni Master Namba nne aliekuwa mlinzi wa muda wa raisi Jeremy.
Mwanaume mwingine alikuwa ni mweusi na mrefu na alikuwa amevalia suti kutoka juu mpaka chini.
“Kaka mkubwa , miliki ya Kekexil ipo kwenye machafuko na inatafuta taarifa zinazohusiana na Roma Ramoni katika ulimwengu wote wa kijini , je tuendeleze hatua ya pili ya mpango wetu?”Aliongea Master Namba nne ambaye jina lake halisi ni Gegu.
Mwanaume ambaye alikuwa amekaa mbele ya kiti alieitwa kwa jina la Kaka mkubwa anafahamika kwa jina la Gefe na ndio mkuu wa miliki ya kijini ya Panas.
“Una uhakika Tigola amekufa?”
“Ndio amekufa na maiti yake kuyeyuka , mbinu ya Roma ya andiko la urejesho hakika inatisha sana”Aliongea Gegu.
“Kaka naona kama tunakosa umakini kumchokoza Roma Ramoni , maana namuona kama kichaa na ana mbinu nyingi mno za hila , inasemekana ameweza hata kuigiza sura ya Zilha na kumuua Tigola”
“Haha.. kama hatuwezi kufanya chochote , Xia watatuzidi hatua moja mbele , ijapokuwa Tigola alikuwa katika levo ya maji ya upako lakini ni katikati na amepambana na Roma akiwa peke yake , haijalishi Roma uwezo wake ni mkubwa kiasi gani lakini uwezo wake una mipaka , muda si mrefu atakuja kugundua kwamba hawezi kufanya kila kitu akiwa peke yake na hapa ndio wakati wa kunufaika sasa”Aliongea Gefu.
“Mpango mzuri , na sasa tunachopaswa kufanya ni kutoa taarifa inayohusiana na Roma Ramoni kwenda Kekexil na watawakusanya wale vichaa wao kutoka mafichoni na ikishatokea moja kwa moja Roma lazima atahitaji msaada wetu ili kulinda familia yake”Aliogea Gegu huku akitoa tabasamu la ushindi.
“Hatukutegemea angeenda kuleta fujo katika miliki ya Kekexil , tulitegemea angeenda kupunguza nguvu katika miliki ya Xia na kutupa nafasi nzuri”
“Kaka Mkubwa usiwe na wasiwasi , miliki ya Xia ndio ambao wamemkamata Rufi , muda si mrefu Roma ataanzisha vita zidi yao , isitoshe faida kubwa Kekexil wakishapata taarifa za Roma katika ulimwengu wa kawaida lazima wataanzisha vita, na Roma hatoweza kupambana na miliki zote mbili kwa wakati mmoja hivyo tutamtuma Jeremy kwenda kufanya nae dili atupatie mbinu ya andiko la urejesho na namna linavyotafsirika , tukifanikisha hivyo tutakuwa na wanajeshi ambao wamepitia mapigo ya radi na tutakuwa na nafasi kubwa ya kwenda kuwaweka Xia chini yetu , Ijapokuwa Anjiu kwasasa anaweza kumzidi Dada wa tatu lakini tukipata andiko hilo la azimio moja kwa moja wewe utaweza kuhimili mapigo ya radi pamoja na dada na hapo ndio uwezo wenu utakuwa mkubwa zaidi na zaidi na baada ya hapo tutaenda kuzima miliki zote na kubakiza jina moja tu la Panas , Hongmeng tutawapokonya ushawishi wao ndani ya China na haitochukua muda dunia ya kawaida na ulimwengu wa kijini utakuwa chini ya ushawishi wetu”Kaui yake ilimfanya Gefu kutoa tabasamu.
“Gagu je Dada wa tatu amemaliza mazoezi yake ya kujitenga?”Aliongea akimuuliza yule bwana mweusi ambaye sasa tunamjua anaitwa Gagu.
“Hapana ,amesema hana uhakika ni lini mazoezi yake yatakamilika na atatokea wakati akiona muda ni sahihi”
“Basi sawa , hata hivyo hatuna haja nae kwasasa , Kaka namba nne nadhani unaweza kufanikisha hili swala , kuwa makini Kekexil wasijue tunahusika , sitaki wajue kama sisi ndio tulitoa taarifa ya Rufi kuwepo Tanzania na kumfanya Roma kuvamia miliki yao , kama ukifanikisha hili vizuri basi utakuwa na zawadi yako”
“Nimeelewa , kuwa na amani hili limeisha”Aliongea Kaka namba nne bwana Gefu.
Katika miliki ya Panas hakuna mkuu bali wao vyeo vyao wanaitana kaka au dada kulingana na uwezo wake , Gefu yeye ndio Kaka namba moja , halafu kuna dada namba tatu halafu ndio anakuja kaka namba nne abaye ndio huyo master Namba nne sasa jini Gegu.

SEHEMU YA 713.
HOLLAND(UHOLANZI)
Ni ndani ya jiji la The Hague lililopo kusini mwa nchi ya Uholanzi kulikuwa na kikao katika moja ya jengo la umoja wa mataifa.
Ukweli ni kwamba jengo hili linamilikiwa na Zeros organisation lakini kwa nje linaonekana kumilikiwa na UN.
Jengo hili ukiachana na ofisi mara nyingi hutumika kama ukumbi wa mikutano ya siri sana ya daraja la juu, ukumbi huu haukuwa ukipatikana juu ya jengo bali ni chini ya ardhi na ulinzi wake ni ngumu sana kwa taarifa ya vikao hivyo kuvuja kwa namna yoyote ile.
Katika meza kubwa ya duara kulikuwa na sura za watu tofauti tofauti waliovalia mavazi ya suti na kwa haraka harka ilionekana kuna kikao cha siri ambacho kinaendelea.
Katikati ya meza hio kulikuwa na alama kubwa ya nembo ya herufi sifuri kama chata maalumu la umoja wa Zeros organisation , hivyo moja kwa moja inaonyesha kikao hicho kimekutanisha viongozi wakuwa wa zeros organisaiton.
Kati ya watu waliokuwepo ndani hapo ni moja wapo ya mzee alieonekana kuwa na nywele nyeupe ikimaanisha kwamba amekula chumvi nyingi , huyu ni raisi mstaafu wa taifa kubwa duniani ambaye ashawahi kuwa maarufu sana katika kipindi cha utawala wake.
Katika mfumo wa majina wa Zeros alifahamika kwa jina la Code la The First Black , ndio ambaye alikuwa katibu mkuu wa umoja wa Zeros na hata ndani ya eneo hilo ndio alikuwa mwenyekiti katika kikao hicho.
Ijapokuwa alionekana kula chumvi nyingi lakini afya yake ya ubongo ilionekana kuwa imara.
Wengine wote waliokuwa wamezingira meza hio walikuwa ni viongozi wakubwa ambao ni wanachama wa Zeros organisation ambao wote walishawahi kufanya ujasusi katika idara kubwa duniani kama vile CIA , M16, KGB, Mossad n.k
Pembani ya The First Black alionekana mwanamke mrembo , pengine ndio mwanamke pekee kati ya watatu waliokuwa hapo ndani kuonekana kuwa na umri mdogo , huyu mwanadada hakuwa mwingine bali ni Clellia Allisanto mkuu wa Umoja wa mataifa.
“Japo nipo hapa kama mwenyekiti wa kikao lakini alieitisha kikao hichi cha 110 tokea kuundwa kwa umoja wetu , mimi nipo kama mjumbe tu na Clellia Allisanto ndio muwakilishi wa kiongozi mkuu wa Hegemony, hivyo ndio amebeba jukumu la kutuelezea ajenda ya kikao chetu cha 110,karibu Clellia”Aliongea kwa lugha ya kingereza.
“Ajenda ya kikao ni maendeleo ya Projekti Utopia , kuanzia hatua inayofuatia na mambo ambayo yamekwisha kufanya kabla ya hatua namba tatu haijaanza kuchukua nafasi”Aliongea , haikuwa na haja ya kusalimiana kwani alishafanya hivyo wakati wa kukaribishana.
Eneo lilikuwa tulivu mno na kwa namna moja ama nyingine kila mwanakikao alionekana kuwa na sura yenye shauku.
“Kwa niaba ya mkuu wetu wa Zeros organisation , The First Black nikupe pongezi zako kwa kuweza kuibeba jumuia ya wanachama wa Illuminat na kuwa kitengo endeshi ndani ya Zeros kama ilivyo kwa idara nyingine kama vile Freemasons, Skull and Bones , Bilderberg group ,Priory of sion , The Hermetic Order na wengine wote naomba wote tutoe sauti ya mlio wa pongezi kwenda kwa the First black kwa mchango wake”Aliongea na wote kama vile ni wanakwaya walianza kutoa sauti za kimpangilio , ni kama vile wanaguna lakini sauti zao zinaendana sana.
“Mpaka sasa Zeros organisation imeweza kuunganisha jumuia zote za siri kuu duniani na kuwa sehemu ya idara za utendaji shawishi dunia nzima kuelekea mpango Utopia na kwa niaba ya mkuu wetu nitoe tena pongezi kwenu wakuu wa Idara”Aliongea na wote walitoa sauti.
“Mwisho kabisa Mkuu anatoa pongezi kwa kila idara kufanyia maelekezo kwa utii mkubwa katika kufanikisha mpango wa Projekti Utopia na leo hii nimekuja na taarifa za mkuu wetu kuweza kuiunganisha Ant- Illuminat na Zeros organisation”Aliongea na wote walitoa macho ya mshangao.
“Clellia unamaanisha nini kuinganisha Ant- Illuminat na Zeros , tunajua jumuia hii ipo kinyume na tamaduni zetu pamoja na mpango Utopia?”Aliuliza mmoja wapo.
“Haya ni maagizo ambayo nimepokea kutoka kwa mkuu na nipo hapa kutoa taarifa hii , kwanzia leo hii Ant-Illuminat ipo chini ya Zeros organisation , ijapokuwa taasisi hii haitakuwa endeshi kwa kufuata miiko ya kanuni za Zeros lakini utendaji wake wa kazi utaendana na maagizo ya kiongozi wetu , mtawala wa Hegemony na msingi wa mageuzi ya dunia, mwisho kabisa nitoe taarifa kwamba Dunia ishaingia katika mabadiliko na kama maagizo yalivyotolewa katika kikao cha 100 tunapaswa kuandaa akili zetu kwa ajili ya Dunia mpya katika utimilifu wa Project Utopia , katika hatua kama hii tunaaswa umoja katika kudumisha utulivu wa raia dunia nzima”
Aliongea na palepale sauti za mlio wa Vocal zilianza kusikika kwa kila mwanachama.
*******
Upande mwingine wa kaskazini mashariki katika ulimwengu wa majini ndio makao makuu ya miliki ya Xia.
Katika miliki hio jengo moja kubwa ambalo limepewa jina la Jumba la Jade lilionekana kubadilika badilika rangi kutokana na mwanga wa jua.
Miundo mbinu ya miliki ya Xia ilidhihirisha utajiri , ijapokuwa makazi yao yalikuwa ni ya kitamaduni zaidi lakini utajiri iliokuwa ndani ya utamaduni huo ni wa kutisha.
Katika ulimwengu wa maijini madini ya Jade ni ya thamani mno kuliko madini ya Dhahabu kutokana na sababu moja tu kwamba madini ya jade yanasharabu zaidi nishati tofauti na Dhahabu ambayo mara zote huakisi mwanga.
Hivyo ni sawa na kusema madini ya Jade yana muunganiko zaidi na majini kuliko ilivyo kwa Dhahabu ijapokuwa Dhahabu pia hupendelewa na majini kwa kiasi kikubwa na kuwa na thamani kwani ndio hutumika zaidi katika kutengenezea Dhana.
Zipo sababu nyingi fungamanishi kufanya Jade kuwa na Thamani zaidi lakini katika miliki nyingine Dhahabu ndio yenye thamani zaidi.
Uzuri wa miliki ya Xia ilikuwa ni ile ya kipekee sana kwani ukiangalia kwa juu nyumba zao ni kama zinabadilika badlika rangi kutokana na madini ya Jade kusharabu mwanga.
Wanasema popote penye uzuri na ubaya pia upo na ndio kilichokuwa kikiendelea katika chumba kimoja ndani ya miliki hio..
Katika chumba ndani ya jengo, kulikuwa na chumba ambacho kimejengwa kwa mawe makubwa ambayo yana ubaridi wa hali ya juu, ni tundu pekee ambalo ndio chanzo cha mwanga unaopita kuingia ndani hapo.
Ndani ya chumba hicho kilikuwa hakina madawa kuonyesha kwamba ilikuwa ni sehemu ya kutengenezea vidonge lakini haikumaanisha kwamba kilikuwa kitupu.
Mlango wa jiwe wa chumba hicho ulifunguliwa na alionekana mwanaume handsome alievalia mavazi meusi huku akiwa na nywele ambazo zimeifunika shingo yake ambaye aliiingia katika chumba hicho.,huyu hakuwa mwingine bali ni Jinii Lahani.
Katika sakafu ya chumba hicho kulikuwa na mtu ambaye amelala akiwa hana tumaini chini ya tundu ambalo linapitisha mwanga katika kona.
Kitendo cha kuingia kwa Lahani katika chumba hicho kulifanya sauti za minyororo kusikika zikisuguana na sakafu.
Alikuwa ni mwanamke ambaye miguu yake yote imefungwa na minyororo, huku akiwa na nguo zilizochafuka na nywele kitimtimu , hata kwa nyayo zake zilikuwa nyeusi kama vile zimekanyaga oili chafu , viatu ambavyo vilikuwa amevivalia msichana huyo havikueleweka vilikuwa wapi tena.
“My, My , My …. una tatizo gani wewe , mchumba wangu , kwanini unaogopa kuniona?”Aliongea Lahani.
Rufi aliishia kujikunyata huku akiwa amezika kichwa chake kwenye mapaja ya miguu yake , ukiachana na ukimya wake mwili mzima ulikuwa ukimtetemeka kutokana na woga.
Hakuwa tena yule mrembo Rufi mwenye ngozi nyororo , hapo alifanana na mateka wa Alshababu.
“Nini… ndio tuseme unaniogopa , lakini kuja kwangu hapa kumenifanya kukataa warembo wawili ili mradi tu nikuone , nyanyua kichwa chako nione sura yako”Rufi aliupiga kimya.
“Eh , kwanini unafanya hivyo , ndio unajilinda sio, lakini tokea mwanzo nishasema sikutamani , wewe ni malaya ambaye ushachezewa tayari na mimi kama Jinni kiasili siwezi kutembea na mwanamke ambaye hana bikra , na isitoshe hakuna mwanaume ambaye anaweza kukutamani au kufanya mapenzi na wewe kwani mwili wako unasumu , hapa ndio mahali ambapo upo salama , wewe unaonaje?”
Baada ya kuona Rufi anaonyesha kiburi kwa kukaa kimya macho yake yalijikunja na palepale alimpiga teke na kumfanya apaae na kwenda kujipigiza kwenye ukuta.
Rufi aliishia kutoa mguno wa maumivu ijapokuwa ni teke ambalo hakuna nguvu ya kijini iliotumika lakini alihisi maumivu makali kwani mwili wake ulikuwa ni kama wa binadamu wa kawaida tu.
Aliishia kupiga magoti huku machozi mengi yakimtoka na kudondokea sakafu.
“Nakuongelesha unanikalia kimya , wewe ni kiziwi?”Aliongea na palepale alimuongezea teke lingine na kumfanya arudi kinyume nyume na kujigonga kwenye ukuta na hapo hapo alitema damu.
Nguo zake zote zilikuwa na damu zilizoganda na mpya , ilionekana alikuwa amechezea kichapo sio kidogo , mwili wake ulikuwa ukiuma huku makovu ya mikanda yakionekana kwenye nguo .
Aliishia kung’ata meno kwa hasira na kisha akainua sura yake juu kumwangalia Lahani na dakika ileile mara baada ya kuiona sura ya mwanaume huyo mjeuri alianza kutoa kicheko kikubwa kama vile ni kichaa huku akitema damu nyingi.
Sasa uso wake muda huo ndio majeraha yalionekana waziwazi , ilikuwa ni kama vile kuna mtu alimkata na wembe kwenye paji la uso kwa kutengeneza X na kuacha kidonda kikubwa, ilikuwa ni bahati macho yake yalikuwa salama.
Kwa mwanamke kama Rufi ambaye mwili wake haukumruhusu kuvuna nishati za mbingu na ardhi , uso wake ulikuwa ndio chanzo cha kujiamini lakini sasa ulikuwa umeharibiwa maumivu yake yalionekana ni yale ya kutokuvumilika.
“Haha….mwanamke mbaya , hebu jione , hata kama ukitupiwa mtaani machokoraa hawawezi kukugusa kabisa , unaonekana kama maiti iliotafunwa na funza , nina tamani sana kuona muonekano wa huyo mwanaharamu wako Roma Ramoni utakavyokuwa akikuona katika hio sura… nina uhakika atakuwa na mshituko , woga , hasira na kichefu , mwanaume yoyote mwenye akili timamu hawezi kuwa na mwanamke kama wewe”
Maneno ya Lahani yalikuwa ni kama kisu ambacho kinapita kwenye moyo wake , haikuwa mara ya kwanza kwa Rufi kutaka kupatwa na ukichaa , kama angekuwa ni yule wa zamani angekuwa ashajipigiza kichwa chake kwenye ukuta lakini mara baada ya kupitia uzoefu wa maana halisi ya mapenzi ni nini , alijishauri na kujiambia alikuwa na tumaini , kwa ajili ya Roma na mama yake anapaswa kuendelea kuishi.
Na macho yake yaliojaa machozi aliinua sura yake na kumwangalia Lahani kwa macho yaliojaa chuki , kama chuki hio ingekuwa nguvu hakika ingemuondoa duniani Jini yule palepale lakini chuki mbele ya Jini kama Lahani ni dua ya kuku kwenda kwa Mwewe.
“Haha.. nini tena , ndio unanichukia , sawa wewe nichukie utakavyo m ninapenda sana ukiniangalia hivyo huku ukishindwa kufaya chochote, haya ndio matokeo yake mara baada ya kunisaliti , mwanamke ambaye nimemchagua hata kama sitolala nae hawezi kuguswa na mwanaume mwingine , wewe ndio mwanamke wa kwanza na wa mwisho kunifanya nijihisi kuwa na chuki namna hii , Rufi mwanaume wako bado tu hajaja kukuokoa , inaonyesha kabisa hana mpango wa kuja ..oh tena sitaki kukuficha nimesikia taarifa kutoka miliki ya Kekexil juu ya binadamu anefanana na Roma kufanya mashambulizi , ameweza hata kupambana na mmoja ya wanachama wa Taisha na kumuua , Mpaka sasa miliki ya Kekexil imemtangaza kama adui yao namba moja na muda wowote atazingirwa na majini wote walio katika levo ya maji ya upako , hawezi kupona na ndio aje kukuokoa hahaha ,,, hahaha… muda wowote atakuwa mateka na kuwekwa gerezani kama ilivyokuwa kwako”
Hali ya kupaniki ilimvaa Yezi palepale , alijua lazima Roma ashafika katika ulimwengu wa majini na kuwakurupusha.
Kama ni hivyo basi ataguswa lakini kwa wakati mmoja alikuwa akitamani asije kabisa
Alijua ni jambo la kutokuwezekana kupambana na majini katika miliki hizo hususani wazee wa kitengo cha Taisha.
Kitu kingine alikuwa na wasiwasi kwamba hata kama Roma akifika yeye atatumiwa kama mateka ili kumkamata.
Rufi alitamani kufa hapo hapo lakini aliogopa kwamba hata kama akifa Roma anaweza kuja na kama ni hivyo basi kifo chake hakitokuwa na maana , baada ya kufikiria jambo hilo aliishia kutoa kilio cha kwikwi.
Hakujali mateso yake katika hatua kama hio bali alijali usalama wa Roma , pengine ni kutokana na sumu kali iliokuwa katika mwili wake , sumu ambayo ilikuwa ni kama vile mwili wake una minyoo ambayo inatoboa nyama ndani kwa ndani , maumivu ambayo alikuwa akiyasikia pengine ndio yaliongeza ukali wa kilio chake.
Tokea saa na dakika ambayo ameletwa ndani ya miliki hio madawa kibao yalishajaribiwa ndnai ya masaa ishirini na nne na alipewa dakika kadhaa tu za kupumzika na badala ya hapo madawa menigne yangesindiliwa katika mwili wake.
Ile sumu ambayo mwanzoni ilikuwa imeondolewa na Roma sasa imerudi upya na ongezeko la sumu ndio ilimsababishia maumivu zaidi na zaidi.
Kutokana na hali yake ya kiafya jamii hio ilijua kabisa Rufi hana muda na angekufa hivyo waliona wajaribishe madawa yao ndani ya muda mfupi kabla ya kifo chake.
Kutokana na ukali wa kilio wa Rufi palepale ilimjulisha Lahani madawa ndio sasa yanafanya kazi mwilini mwake na ilimfanya aweze kujisikia vizuri mno.
Dakika hio hio mlango ulisukumwa na alionekana mzee mmoja alievalia joho la rangi ya zambarau .
“Lahani , hebu muache”Aliongea yule mwanaume kwa sauti ya kibabe na kumfanya Lahani kukunja ndita.
“Mzee , umekuja muda muafaka , nani kakuambia nipo hapa?”Aliongea akionyesha hali ya kutoridhishwa na kauli yake.
Jini huyo mzee alifahamika kwa jina la Laofi na ndio aliekuwa akihusika na maswala yote ya kutengeneza vidonge.
“Rufi ni somo wetu wa kufanyia majaribio na sio mdoli wako wa kuchezea , ushamuharibu tayari na kumpiga na sasa ni nusu mfu na unafanya nini tena sasa hivi?”
“Mzee nipo hapa kuangalia kama bado yupo hai , sifamfanyii chochote”Aliongea.
“Kama ni hivyo hio damu inayomtoka mdomoni inatokea wapi , kama utamuua na kufanya majaribio yetu kufeli jua miliki yote inaathirika na hata baba yako hawezi kukusaidia”Aliongea kwa kufoka na kumfanya Lahani bila ya kupenda kuacha kile alichokuwa amekipanga , hakuwa akimuweza huyo mzee kwani alikuwa kwenye levo ya maji ya upako tayari.
Baada ya kumwangalia Rufi kwa dakika kadhaa aliondoka katika chemba hio ya mawe.
Jini Laofi alimwangalia Rufi kwa dakika na palepale alimsogelea na kumwingizia nguvu ya kijini ili kumuondolea maumivu lakini hakufanya hivyo kutokana na kuwa mwema bali alitaka kuwa na nguvu kidogo kabla ya awamu inayofuata ya majaribio.
Yezi aliishia kujilaza kwenye sakafu hio ya baridi , mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidudnda kwa kasi mno , jasho la ubaridi lilikuwa likimtoka na kumfanya uso wake kufubaa, ilionekana ni kama vile alikuwa akipata shida katika kupumua.
Baada ya dakika kadhaa mlango wa chemba hio ulifunguliwa kwa mara nyingine na kivuli cha mtu kilionekana kikiingia , alikuwa ni mwanamke alievalia gauni huku akiwa amefunga nywele zake kwa kibanio , hakuwa mwingine bali ni XiaoXiao .
Baada ya kumuona Riufi alivyolala kwenye sakafu macho yake yalionyesha hali ya hatia na maumivu na alimkimbilia na kuchuchumaa chini huku mkononi akiwa ameshikilia kidonge..
“Rufi hiki ni kidonge kwa ajili ya kutibu majeraha yako , utajisikia angalau vizuri kidogo baada ya kumeza”
Rufi alijikaza na kunyanyua mkono na kubetua mkono wa Xiao na kufanya kidonge kile kurukia mbali.
“Acha kujifanyisha mwema mbele yangu , kila mtu ndani ya familia yenu ni shetani… nyie ni mashetaniii….”Aliongea huku akimwangalia kwa macho makali.
Xiaoxiao aliishia kung’ata meno yake kwa hasira na palepale aliokota kile kidonge na kisha akamshika Rufi kwa nguvu na kukitumbukiza mdomoni na kuziba pua yake ili ameze.
Haikuwa mara ya kwanza kufanya hivyo na kama sio kwa msaada aliokuwa akitoa kwa Rufi pengine majeraha yake yasingekuwa yamepona lakini licha ya kufanya hivyo kwa mtazamo wa Rufi aliona Xiao ndio aliemuuza na alichokuwa akifanya hapo ni kutaka aendelee kuishi ili kuwa kifaa cha majaribio.
Xiao hakutaka hata kujielezea kwani aliona kabisa Rufi asingemuamini , baada ya kuhakikisha Rufi amemeza kile kidonge alisimama na kuondoka na kabla ya kuondoka aligeuka na kumwangalia.
“Rufi najua unanichukia lakini sikulaumu kwasababu baba yangu na kaka yangu wanakufanyia mabaya sana lakini niamini, sijahusika na wewe kukamatwa , naapia sikuwahi kuwaza kukuumiza”
Baada ya kuongea hivyo alikimbilia nje akiwa na uso uliojawa na huzuni na majuto ndani yake.
Rufi aliishia kwenda kujikunyata kwenye kona akiwa kimya na baada ya miale ya mwanga wa jua kumfikia , makovu yake yalianza kumuwasha na alianza kujikuna kwa kasi.
Dakika ambayo anataka kujikuna na usoni mkono wake uliishia hewani na kuweka chini na aliishia kumungunya maneno.
“Hubby nifanye nini mimi , nataka kufa lakini nimekumisi , naogopa pia kukuona , nifanye nini..hii… hii… hii”Aliongea kwa huzuni kubwa na kuanza kuangau kilio cha kwikwi.

SEHEMU YA 714.
Ilikuwa ni siku nyingine pia katika ulimwengu wa majini watu na Roma alionekana akiwa amesimama juu angani katika safu ya milima ya theruji inayopeperushwa na upepo ndani ya ulimwengu wa majini.
Kulia , kushoro , mbele na nyuma kila kitu ilikuwa ni barafu , hakukuwa hata na dalili yoyote ya miti na kila kitu ilikuwa ni kama vile yupo katika bara la Antarctica.
Hali ya kusita sita ilikuwa imejidhihirisha katika uso wake na kila alipokuwa akipumua mvuke ulikuwa ukionekana na kuganda hewani.
Wakati huo alikuwa katika muonekano wa Xiao Cheni sura ambayo alitumia katika kuvamia miliki ya Kekexil.
Kimahesabu kama angesafiri kuelekea mashariki mbali kabisa angeweza kufika katika ngome ya miliki ya Xia lakini bado hakuwa amepata njia nzuri ya kuzamia katika miliki hio bila ya kushitukiwa.
Alijikuta akikosa chaguzi na alisimama hapo akijaribu bahati yake kama ataweza kukutana na jini lolote ambalo linaelekea upande huo na kisha atumie muonekao wake kuingia katika miliki hio.
Lakini ukweli ni kwamba mpaka kuja kusimama hapo alikuwa amezunguka milima hio ya theruji kwa nusu siku nzima kujaribbu kutafuta jini linalotokea katika miliki ya Xia lakini hakuweza kubahatika kukutana nalo.
Wakati akijifikiria labda aingie hivyo hivyo katika miliki hio hatimae aliweza kunasa msuguano wa nguvu za kijini kilomita kadhaa kutoka aliposimama.
Dakika ileile alitumia Dhana ya jani na kuficha nguvu zake za kijini ili aweze kumuona Jini huyo atakuwa ni nani na je anaweza kumtumia.
Hakuweza kutumia nguvu yake ya utambuzi kwani ilimaanisha angesambaza msisimko hivyo alitegemea hisia zake pekee na kusogea kwa ukaribbu zaidi ili kuona ni nani.
Katika hali ya kutotegemea alishangaa kuona ni Jini mkuu namba tatu kutoka Kekexil , yaani Mohi baba yake na jini Zilha na alionekana akielekea uelekeo wa miliki ya Xia na Roma alijiuliza anaenda kufanya nini.
Licha ya hivyo Roma alijiambia hio ni fursa kwake na palepale alianza kumfatilia kwa nyuma.
Jini Mohi alikuwa peke yake na kwa levo ya nguvu za kijini aliokuwa nazo Roma hakuhisi kabisa alikuwa anafatiliwa.
Baada ya dakika kama kumi hivi Mohi alikunja kushoto na kuanza kuelekea Kaskazini juu ya milima ya safu za barafu akiachana na nijia ya moja kwa moja ya kuelekea miliki ya Xia.
Kitendo hicho kilimshangaza Roma na kujiuliza anaelekea wapi , alijiambia au kuna kambi ya Kekexil uelekeo huo lakini kama ni hivyo kwanini ni karibu na miliki ya Xia?.
Ilikuwa ikishangaza kwani Mohi alikuwa ni kiongozi mkubwa katika miliki ya Kekexil na kitu kingine alikuwa akisafiri bila ya kuwa na walinzi hivyo kwa namna moja ni kama ametoroka na ilionekana alikuwa na shughuli binafsi katika eneo hilo.
Dakika chache mara baada ya kutoka katika milima ya barafu hatimae aliingia katika tambarare eneo ambalo lina msitu mkubwa sana , lilikuwa ni eneo ambalo lina mandhari nzuri kwani nyuma kulikuwa na barafu na mbele kulikuwa ni msitu wenye kijani kizito.
Baada ya kusafiri katika msitu huo hatimae aliweza kutua katika eneo ambalo halikuwa na vichaka wala miti mingi , ni eneo la wazi ambao lipo katikati ya msitu.
Roma aliishia kuchanua macho yake na kwenda kutua upande wa pili wa eneo hilo akijaribu kuangalia nini kinaendelea katika eneo hilo kiasi cha kumfanya Jinni Mohi kutua katika eneo hilo ambalo limezungukwa na misitu kila pande.
Roma ilikuwa bahati kwake kwani upande wa kulia kwake kulikuwa na jiwe kubwa ambalo limetenganisha eneo hilo na aliposimama hivyo ilimpa fursa ya kuweza kuona kinachoendelea katika eneo la katikati na aligeuza uwezo wake wa kijini ili kuonekana kabisa ni binadamu wa kawaida.
Roma alisimama pale kwa dakika kama kumi na tano akimwangalia Mohi ambaye alionekana kama vile kuna mtu anamsubiria na upande wa Roma alianza kuhisi msuguano wa nguvu za kijini ukisogea eneo hilo na kwa haraka sana alijua sio jini mmoja ambaye anafika bali ni wengi.
Na ni kweli kufumba na kufumbua aliona wanaume wawili wakiwa wanakuja eneo wakifuatiwa na majini wengine , huku aliekuwa ametangulia ni wa makamo mrefu ambae amevalia joho la rangi ya zambarau, kichwani alikuwa amevalia kofia inayofanana na taji la madini ya Jade, alikuwa amegubikwa na uso uliojaa maringo.
Nyuma yake alikuwa ni mwanaume pia ambaye alikuwa amevalia joho la rangi ya kahawia kitambaa cha hariri kama kanzu huku kichwani akiwa amevalia pia Taji la rangi ya Dhahabu na wote wawili walikuwa na nywele nyeupe kama theruji.
Nyuma yao kulikuwa na Majini wengine ambao wamevalia kawaida tu kitamaduni ambao wapo katika levo ya kuipita Dhiki katika levo ya maji meupe na moto wa njano.
Kuhusu hao majini wawili waliovalia mataji kichwani yule alievalia taji la madini ya jade alikuwa katika levo ya kati ya maji ya upako na alievalia taji(crown) la Dhahabu alikuwa mwanzoni mwa laevo ya maji ya upako.
Roma alishangaa na kuona kwamba majini hao kulingana na uwezo wao wanaweza kumuua Jinni Mohi kwa mapigo kumi tu na kuokoka ingekuwa ngumu , hivyo alijiuliza kwanini amekuwa jasiri kukutana nao yeye mwenyewe?.
Baada ya majini wale kutua chini Jinni Mohhi alisalimiana nao kwa tabasamu usoni.
“Kaka Laofi , Kaka Zianji salamu kwenu?”
Roma kauli hio aliisikia vizuri na palepale majina yao yaligonga kichwa chake Laofi na Zianji.
Hatimae alikuwa ashawatambua kulingana na maelekezo ya Sui ,Laofi ndio sehemu ya wakuu wa miliki ya Xia na Zianji ni mdogo wake Anjiu mkuu wa miliki, ilikuwa ni kama jini Sui alivyosema, Zianji alikuwa katika levo ya kati ya maji ya upako na Lao alikuwa mwanzoni mwa maji ya upako , lakini swali linaibuka kwanini Mohi mkuu namba tatu kutoka Kekexil kukutana nao.
Roma palepale aliamini kuna kitu anakwenda kugundua na mwenyewe alijihisi kufurahi na alihakikisha anasikia kila neno hivyo aliongezea uwezo wa masikio yake kusikia na nguvu za kijini.
“Hakuna kikubwa ambacho kimebadilika , lakini kaka Mohi kwa kuzingatia wito wako nina uhakika tukio la hivi karibuni limekukalisha katika kiti cha moto”Aliongea Lao akiwa na tabasamu la ajabu kidogo usoni mwake.
“Nadhani mmekwisha kupata taarifa miliki yetu ilivamiwa na sio tu watu wetu wamejeruhiwa na kuuliwa lakini pia tumepoteza kiasi kikubwa cha mimea ya dawa , hivyo naweza kusema miliki imepoteza hazina yetu yote ya utajiri , baba sasa hivi amekasirika sana na ameanza kuwaita wazee wa kitengo cha Taisha mmoja baada ya mwingine, mpango wake ni kutangaza hali ya dharula katika miliki yote na kuwafanya wazee hao kulinda makao makuu , hio sio kubwa lakini mtoto wangu Zilha amekwisha kufa na ndio ambaye nilikuwa nae tu , itakuwa hasara kubwa kwangu mrithi kubadilika na kutokea upande mwingine”
“Oh , kwahio unamaanisha huyo mwizi ambaye alivamia miliki yenu bado tu hamjampata wala kumtambua?”Aliuliza jini Zianji kwa sauti ya chini lakini yenye mikwaruzo.
“Nimetafuta katika kila kona ya ulimwengu huu wa kijini lakini tumeambulia patupu , wasiwasi wetu ni kwamba ashaondoka katika huu ulimwengu wa kijini”
“Kwasababu miliki ya Kekexil ipo katika matatizo kwanini ulihitaji kuonana na sisi wawili kwa haraka hivi , huogopi unaweza ukashitukiwa ndani ya familia yako?”Jini Lao aliuliza,
“Sina jinsi , sasa hivi ndio hivyo Zilha amekwisha kufa na nafasi ya kutafuta jini yoyote mwanamke kunizalia mtoto ndani ya siku chache ni ngumu sana, lakini siwezi kukaa kizembe , mdogo yangu kwa muda mrefu alikuwa ni mwenye kunichukia kwa kuwa wa pili katika kila jambo , nishapata upepo kwamba anae tayari mtoto wa nje ya ndoa lakini sijui ypo wapi na wasiwasi wangu ni kwamba anaweza kuchukulia hii hali kumfanya baba na wazee wa ukoo kumchagua kama mrithi na kama hilo likitokea nitapoteza nguvu yangu ya kimadaraka na sitoweza tena kufanya kazi na nyie , mnapaswa kjua mdogo wangu ni mwenye tamaa sana na itakuwa ngumu sana kudili nae”
Lao na Zianji waliangaliana huku wakionyesha ishara ya kuelewa hali ilivyo.
“Kaka Mohi umekuwa na juhudi kubwa katika kufanya kazi na sisi kwa miaka mingi na uhusiano wetu siku zote umakuwa ni faida pande zote hivyo ni sawa na kusema tupo upande mmoja na wewe na hatuwezi kukaa chini na kuangalia hali hii ikiendelea , sasa tayari tupo katika matatizo kama kuna lolote ambalo unataka tukusaidie Zianji na mimi tupo tayari , wewe ongea na tutaangalia namna”
Jini Mohi macho yake yalichanua na alijiwazia palepale , ‘eti tupo upande mmoja , tunafanya kazi pamoja kwasababu kila mmoja ameshikilia siri ya mwenzake , wote tutapata matatizo kama miliki zetu zitajua tunafanya kazi pamoja’.
“Hakika nyie ni marafiki zangu wa kuaminika. Hivi karibuni majini wengi ndani ya miliki yetu wananiona kama vile nimekosa busara za ki uongozi kutokana na kukosa mrithi , wanaonekana kutoridhishwa na mimi , ninachotaka nyie kutuma baadhi ya majini wenu ambao wapo levo za juu na kufanya vurugu ndani ya miliki na mimi nitajitokeza kama shujaa , baada ya tukio hili kupita tuma baadhi ya mbinu za mafunzo na Dhana na baada ya hapo nitaangalia kama tunaweza kufanya muungano wa kindoa kati ya jamii zote mbili’
“Hakika una visa sana , lakini hatuwezi kukusapoti kwa njia hii kwani likitokea la kutokea sisi pia tutakuwa katika matatizo”Aliongea na ilikuwa ni kama ametegemea na palepale alitoa boksi mbili ndogo katika hifadhi pete yake.
“Hapa kuna vidonge vinne vya daraja la juu kaisa na ishirini vya daraja la kati vyote vikiwa na ubora , nilivitoa katika Jumba jeupe muda sana , chukueni na hakuna ambaye atajua vimetokea wapi?”
Tamaa palepale ziliwavaa wale majini wote wawili , ijapokuwa hawakuwa na uhitaji mkubwa na vidonge lakini kama watawapa watu wao ilimaanisha wangeimarika katika uwezo wao.
Mtu mmoja hawezi kutoa changamoto ya kimadaraka katika miliki , itakuwa ni bora zaidi kukusanya kundi la watu wa kutoa sapoti ili kujiongezea ushawishi hivyo vidonge hivyo vinaweza kutumika kama Rushwa.
Laofi alionekana kuwa mtulivu wakati akipokea viboksi hivyo huku akimpa ishara Zianji kwa namna ya kutingisha kichwa kuonyesha hali ya kuridhika.
“Unajua sana Mohi , hapa kama tusipokusaidia hatutokutendea vizuri , kaa kwa amani kabisa tutahakikisha wewe unakuwa mrithi wa miliki ya Kekexil ili tuweze kunufaika wote , hatuwezi kumruhusu mdogo wako kukuzidi , hatuwezi kumruhusu mtu kama Mohena kuwa kiongozi”
“Upo sahihi Mohena ana sura mbili na ni mtu hatari sana , lazima atakuwa na visasi na kuondoa amani katika huu ulimwengu kama atapewa uongozi”
“Nawaamini sana katika hili , ukweli ni kwamba simuogopi hata kama atataka kumtoa mtoto wake kunipa changamoto lakini yeye mwnyewe haniwezi , zaidi sana nina sapoti yote ndani ya familia yangu , ijapokuwa kamuoa Lilsi kutoka Miliki ya Shela , lakini ameshindwa kuuteka moyo wake”
“Ukiwa na Master Shagoni upande wako , nina uhakika unanafasi kubwa ya kufanikiwa na kupata nafasi ya ukuu namba moja wa miliki , mkuu wetu pia anampenda sana Shagoni , ijapokuwa tabia yake ni mbaya lakini anampenda kutokana na uwezo wake”Baada ya kutaja jina la kaka yake hali flani ilionekana katika uso wake , ilionekana ni kama alikuwa akimdharau lakini kwa wakati mmoja alikuwa akimuogopa.
“Zianji usiwe na wasiwasi , nina uhakika kupitia Damu ya mnyama wa kishetani kutoka katika familia yangu iliokuwepo tokea karne zilizopita , haitochukua muda kumshinda kaka yako na kumuondoa kabisa kwa kile alichokufanyia , baada ya hapo miliki yote ya Xia itakuwa chini yako wewe na Master Lao”
Baada ya kusikia kauli yake hio wote kwa pamoja walitoa kicheko kikubwa sana cha furaha na kumfanya na jini Mohi kuungana nao na kujifanyisha kama vile ni marafiki wakubwa.
Roma ambaye alikuwa akisikiliza yote hayo kutoka mbali alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa , Damu ya mnyama wa kishetan ni nini , ilionekana ni kama kitu ambacho kinaenda kutumika katika kumdhibiti Anjiu mkuu wa miliki ya Xia, sasa Roma alijiuliza hio damu itakuwa na nguvu sana?
Kadri alivyokuwa akiskiliza ndio alivyozidi kukereka , hakuna hata mmoja ambaye alionekana kuwa mwaminifu ndio hivyo aliona ndege wafananao siku zote huruka pamoja.
Malengo yao kila mmoja ilikuwa ni kupanda ki uwezo na madaraka na kuhusu hujuma zao pamoja na usaliti ni jambo ambalo wataanza kulifikiria mara baada ya kutumiza haja zao.
Baada ya Mohi kuhitimisha mazungumzo yake hatimae alijiandaa kuondoka lakini kabla ya hapo alionekana kukumbuka jambo.
“Tukiachana na haya , hivi hamjaweza kupata taarifa ya asili ya yule mwizi , adui namba moja wa miliki yetu , kama mnajua chochote tafadhari niambieni”
Lao na Zianji walitingisha kichwa kuonyesha hawajui na kumfanya Mohi kusikitika kidogo na palepale alipotea katika upeo wao kuelekea juu ya msitu uliiofunikwa na theruji.
Baada ya msisimko wake kupotea jini Lao na Zianji waliangaliana usoni na palepale walianza kuangua kicheko.
“Mzee kama Kekexil itapewa Mohi sidhani kama itakuwa ngumu kwetu kuivamia , ni mjinga sana kama Nyumbu”
Master Lao alifungua kile kiboksi na kangalia vile vidonge na kisha alitoa kicheko.
“Kama angekuwa na akili kama kaka yake . sidhani kama tungepata haya manufaa ya kumtumia “
“Kitu ambacho nashindwa kuelewa wameshindwa vipi kuunganisha dot kumjua huyo mwanaharamu alewaibia , ijapokuwa Kekexil haina ushawishi mkubwa katika ulimwengu wa kawaida lakini mtu huyo amefanya kazi kubwa sana na kuingia hatarini kumuokoa yule kijakazi Sui ambaye yupo levo ya nafsi tu, kila kitu kipo wazi ni swala linalohusiana na Rufi lakini wameshindwa hata kujua na kuanza kutafuta hapa hapa”
“Acha wapambane k na hali zao , wakati ambao watajua ni Roma ambaye amewafanyia vile watatumia nguvu kubwa sana kudili nae , haijalishi nani atashinda au kupoteza , sisi kwetu tutafaidika “Aliongea huku akicheka.
“Kwa ile mbinu anayotumia Roma lazima atakuwa amepitia mapigo tisa ya radi bila shaka , itakuwa vizuri sana kama ataendelea na ukuichaa wake kuwasumbua Kekexil , lakini kama atakuja kwenye miliki yetu basi litakuwa ni tatizo lingine”
“Kwanini unamuogopa? , hata kama litakuwa ni tatizo sisi halituhusu , Anjiu siku zote ni mtu wa majigambo , yeye ndio mkuu na uwezo wake ndio wajuu zaidi katika ulimwengu wote wa majini hivyo bila shaka atakuwa ndio ataongoza katika mapambano , itakuwa vizuri kama atapambana na Roma ili sisi tukae tuangalie pambano na kuvuna faida”Aliongea Zianji na wote kwa pamoja walianza kuangua kicheko cha furaha na dakika chache mbele waliwapa ishara watu wao na kisha wakaondoka katika eneo hilo.
Roma ambaye alikuwa amejificha alitamani hata kutumia chungu chake kuwameza wote lakini alihisi ukinzani ndani kwa ndani , hilo eneo ni karibu sana na miliki ya Xia na hakujua hao majini walikuwa na Dhana zenye nguvu kama Shagoni na kama atashindwa kuwaua kwa pigo moja na wakakimbia basi maisha ya Riufi yatakuwa magumu sana.
Lakini hata hivyo mpaka dakika hio ashapata mpango wake kichwani , kwasababu alishawaona walivyo haitokuwa ngumu kuingia ndani ya makao makuu yao.
Baada ya giza kuingia nyota zilionekana angali zikiwa ziemsambaa na Roma palepale alibadili uwezo wake na kufanana na Masta Laofi na kuanza safari ya kuelekea makao makuu ya Xia.
Roma mara baada ya kukaribia na kuangalia jengo ambalo ni refu lililopo katikati ya mji huo wa majini alishindwakujizuia na kushangazwa pamoja na kugofwa na utajiri wa miliki hio , jengo lote vioo vyake vilkuwa ni vya madini ya Jade tupu , kwa makadirio ya haraka haraka jengo hilo madini yake kama yatakuwa ni katika ulimwengu wa kawaida ingegharimu zaidi ya bilioni moja za kimarekani.
Utajiri wa miliki hio haukuweza kulinganishwa kabisa na matajiri ambao wapo katika ulimwengu wa kawaida , hapo ndio utajiri wenyewe ulipo , kila kona ilinuka utajiri tu lakini upande wa hao majini kwao ilikuwa ni kawaida , pengine katika kipimo cha utajiri ndani ya miliki hio thamani yake ni ndogo kulingannisha na kama utajiri huo utapimwa kwa vipimo vya ulimwengu wa kawaida.
Roma mara baada ya kutembea kwa dakika kadhaa hatimae aliweza kufikia ukuta kuingia ndani , ni kama eneo la getini lakini hakukuwa na geti bali kulikuwa na safu ya ulinzi wa kijini.
Pembeni yake alikuwa amesimama jini mtu mwanaume ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi kama vile ni wale wanajeshi wa Zamani wa tamaduni za kikorea, alikuwa ni jini levo ya nafsi.
“Guru Mkuu!!!”Aliongea yule bwana akimaanisha Mzee mkubwa huku akiwa katika hali ya mshangao na kujiuliz imekuwaje Guru Laofi kuonekana eneo hilo tena usiku akiwa peke yake akitembea kwa miguu.
Roma kama vile mtu ambaye amechoka alisimama akiwa amekunja sura.
“Kwanini unapaniki?”
“Radhi zangu kwako Master, sijategemea kama ungefika muda huu kufanya ukaguzi”Aliongea huku akitetemeka kidogo.;
“Simama , jina lako nani?”
“Naitwa Cheli”
“Una miaka mingapi na umekuwa hapa kwa muda gani?”
“Nina miaka therathii na nimekuwa mlinzi kwa miaka saba”
“Vizuri sana , hakika una utiifu na juhudi ya kazi , hebu nifuate mahali kuna zawadi nataka kukupatia”Aliongea Roma kwa kujiamini.
Jini Cheli mara baada ya kusikia kauli ya Roma ambaye yupo katika sura ya Master Lao alifurahi mno na alishindwa kugundua anaemuona kama Lao ni feki.
Roma aliongoza njia na kuanza kupaa kuelekea upande wa msituni nje kabisa ya mji huo na alisubiri mpaka alipohisi yupo mbali kabisa na makao makuu ya miliki hio na alisimama.
Cheli alishangazwa na kusimama kwa Roma na kujiuliza kwanini amemleta mbali hivyo kwa ajili ya zawadi tu. Lakini hata hivyo hakutana kuongea neno na alifuatisha nyuma nyuma tu ,
“Cheli hivi unajua Lahani amemkamata mwanamke anaefahamika kwa jina la Rufi?”
“Rufi ? kama unamaanisha yule mwanamke kutoka miliki ya Kekexil nishawahi kumsikia lakini mimi ni mlinzi tu hivyo sina taarifa za kutosha”
“Je unajua sasa hivi yupo wapi na hali yake ipoje?”
“Guru Master kwanini unaniuliza swali hilo , hili si swala ambalo jini kama wewe wa kuheshimika unapaswa kujua?”Aliongea na kumfanya Roma kuvuta pumzi na kujiambia huyu jinni hali yake ni ya chini mno kuweza kujua kinachoendelea katika miliki hio.
“Je unaruhusa ya kuingia eneo lolote ndani ya makao makuu?”Aliuliza na kumfanya kushanga.
“Guru Master kwanini unaniuliza hayo maswali , mimi ni mlinzi tu na bila ruhusa kuna sehemu nyingi siwezi kwenda , au unajaribu kuniuliza kama kuna kitu siridhiki nacho , hapana, hapana , najua nafasi yangu , najua ni haki yangu kuingua na kutoka katika ukumbi mkuu na makazi ya Gurus”
Roma alijutia mara baada ya kuona jinni huyo cheo chake kilikuwa kidogo sana lakini aliona atamfaa kwa muda.
“Samahani bro , ni bahati yako mbaya unafanya kazi chini ya miliki ya Xia”Aliongea Roma na palepale alipotea aliposimama na palepale Cheli aliishia kutoa mshangao tu na kuhisi nguvu ya kijini nyuma yake na kabla hata hajajua ni nini kinaendelea alishakufa palepale.
Baada ya Roma kuvua mavazi yake Cheli palepale aliunguza maiti yake vizuri na kisha akajibadilisha katika muonekano wake na kurudisha chini levo yake ya kijini na kurudi makao makuu ya miliki ya Kekexil.
Roma mpango wake sio kuwa mlinzi hivyo alijijaza ujasiri na kuanza kufanya patrol ndani na nje.
Wakati alipokuwa katika miliki ya Kekexil hakujaribu kutumia uwezo wake wa kijini kufanya utambuzi ni wapi Rufi alipo na alifanya hivyo hivyo ndani ya eneo hilo.
Hivyo Roma alitumia jina la Cheli kila alipokutana na baadhi ya majini ambao wapo katika zamu ya ulinzi , alijaribu kwuasogelea na kuwauliza baadhi ya taarifa lakini katika hali ya kusikitisha hao majini kazi yao ni kuzuia wezi tu na hawakuwa wakijua nini kinaendelea ndani makao makuu ya miliki hio.
Muda ambao Roma antaka kufika katikati ya eneo hilo la kifalme sauti nzito iliweza kumuita kutoka nyuma kwa amri.
“Simama hapo hapo”
ITAENDELEA IJUMAA -0687151346 WATSAPP ONLY
Totally good
 
Back
Top Bottom