Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
auSingano eeh leo tunaenjoy au
Unajua kutuacha na arosto kweli mgoshi,ila big up, utunzi wako ni Habari ingne,nilkua nataka kuitabiri hii riwaya ila acha nikae kimya. Ila umenifurahisha kwa kweli Eti havikawii kuwa dhahabu 😂😂😂SHETANI RUDISHA AKILI ZETU
MTUNZI: SINGANOJR
SEHEMU YA 104.
Hamza hakutaka kumfanya Regina ajisikie vibaya kwa kushindwa kutatua tatizo kama hilo , isitoshe aliona ni kawaida kwake kutojua cha kufanya mara baada ya kuishiwa na mafuta njiani kwa mwanamke ambae hana uzoefu.
Kwasababu sheri haikuwa mbali Hamza alimwambia Regina apande kwenye gari aliokuja nayo na akifika sheri mbele awaambie wamletee mafuta na kisha yeye atangulie nyumbani kwani haina haja ya kurudi nyuma tena.
Regina licha ya kusita sita kidogo lakini alikuwa akijihisi kuchoka mno na alitamani kufika nyumbani na kwenda kulala , isitoshe kuendesha gari kutoka Tanga mpaka Dar es salaamu haikuwa rahisi kwa mtoto wa kike.
Upande wa Regina licha ya kuchoka alijiona mjinga kushindwa kutatua tatizo dogo kama hilo na Hamza ni kama alijua ni nini ambacho anafikiria.
“Regina ni vizuri pia kuwa dhaifu kama unae mtu wa kumtegemea kama mwanamke,vinginevyo si uwepo wangu utaonekana hauna umuhimu?”Aliongea na kumfanya Regina kumwangalia na macho yake ambayo ni kama anataka kulia, hali isioelezeka ilipita katika moyo wake.
Baada ya dakika kadhaa Regina alikubali na kuingia kwenye Maybach na kuondoka.
Hamza licha ya kushukuru kwanini Regina hakuuliza ni nani aliekuwa akiangalia nae filamu lakini kwa namna flani alijiuliza inamaana Regina hakujali au kuna sababu nyingine ndio maana hajauliza.
Nusu saa baadae aliweza kuletewa mafuta na mtu aliekuwa akiendesha pilipiki na baada ya kuweka aliendesha gari kurudi nyumbani.
Usiku huo hata baada ya kurudi hakulala kabisa, alikuwa macho akisoma lile andiko aliliopata kutoka kwa Jagani ambalo lugha yake ilikuwa ni ya Kitamili na ilikuwa ngumu kutafsiri haraka na kuelewa.
Mpaka inafika asubuhi ndio sasa aliweza kuelewa kila kitu na kukariri kisha alichoma ile karatasi maana hakuona kuna haja ya kuendelea kubakia nayo ilihali kla kitu amekielewa, isitoshe aliona kuendelea kubakia nayo ni kama kujiwekea mazingira ya hatari kwa watu kuja kulitafuta na kutaka kuichukua.
Wakati akiwa chumbani kwake aliweza kuskia sauti ya Regina akitoka nje na alijua lazima anaenda kuchukua mazoezi maana ilikuwa tayari ni jumamosi na kama kawaida yake alitumia siku hio kuchukua mazoezi ya mwili.
Hamza hata yeye aliona atumie muda huo kuchukua mazoezi hivyo alitoka nje katika eneo lake la kawaida na kisha alianza kucheza mdundiko.
Regina hakutaka nata kumwangalia maana hakuelewa ni mazoezi gani ambayo Hamza anachukua na ya kutia aibu namna hio.
Mara baada ya kumaliza mazoezi , kwasababu shangazi hakuwepo ilibidi kifungua kinywa waandae wenyewe.
Hamza mara baada ya kumuona Regina anatoa vitu kwenye friji kwa ajili ya kupika alijua ni ule mwendo wa kupika vitu vyeusi hivyo alimzuia.
“Regina unaonaje tukienda kupata kifungua kinywa mgahawani, isitoshe jua sio kali sana leo tunaweza pia kutumia muda huo kupunga upepo, kwanzia jumatatu utakuwa bize na kazi hivyo angalau pata muda wa ku’refresh’ akili”Aliongea Hamza.
Regina mara baada ya kusikia kauli hio kiasi flani aliguswa , isitoshe pia bado alikuwa akiwazia swala la Hamza kwenda kuangalia filamu na mwanamke mwingine japo hakuongea tu , alikuwa akijifikiria muda wote kwanini yeye hataki kutoka nae , hata kama Eliza alimjua kabla yake lakini kisheria ni mume na mke na wanaishi pamoja.
“Sawa basi kwasababu umesema mwenyewe tukatembee tembee”Aliongea Regina bila ya kubadilisha muonekano sana.
Hamza mara baada ya kusikia hivyo alifurahi mno na palepale wawili hao walitoka mpaka kwenye gereji, Regina alijikuta akisita akiwa hajui ni gari gani waendeshe lakini Hamza alisogelea baiskeli yake.
“Unafanya nni?”aliuliza Regina huku akikunja sura.
“Twende na baiskeli itakuwa rahisi zaidi kuliko gari”Aliongea Hamza
“Si utachoka kwenye kuendesha sasa?”
“Regina unadhani mimi ni mwanaume ambae nina matatzo ya kimwili”Aliongea Hamza huku akijionyesha misuli yake.
Muda ule Regina alikumbuka nguvu za Hamza na uwezo wake kwa ujumla na hata Shangazi alisema alikuwa na uwezo ambao ni ngumu kufikiria hivyo alikubali.
“Sawa”Aliongea Regina huku akiona ngoja apate uzoefu mpya.
“Usiguse mikono wewe shikilia kiuno changu tu”Aliongea Hamza mara baada ya Regina kuwa na wasiwasi asijue ni wapi ashikilie.
“Kwani nimesema nakugusa , hebu endesha huko”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka na aliendesha kidogo kisha akashika breki na kumfanya Regina amkumbatie bila kupenda.
Baada ya kuendesha kwenye barabara hio ya fukwe ya bahari alijikuta akijisikia vizuri mno , mwanzoni aliona baiskeli hio hakuwa na thamani kutokana na uchakavu wake lakini mara bada ya kuipanda aliona haikuwa mbaya na ilitembea bila shida yoyote.
Wakati huo pia baada ya mikono yake kushika misuli ya tumbo la Hamza ilitingishka kwani misuli hio ni kama ilikuwa imetengenezwa na chuma.
“Ndio maana ana uwezo wa ajabu , sio kwa misuli hii”Aliwaza Regina
“Huu usafiri wako hauvutii kwa macho lakini angalau unaonekana hauna shida”Aliongea Regina ili kumtoa Hamza kwenye kufikiria kama mikono yake ilikuwa ikichezea misuli ya tumbo lake.
“Haha .. hii baisikeli inaonekana ya muda mrefu lakini nilitumia hela yangu ya kwanza kuipata hapa Tanzania kuinunua”
“Kwanini umenunua iliotumika sasa au ndio ubahili?”Aliongea Regina na muda huo aliangalia mavazi ambayo Hamza amevaa na kukumbuka alieyatengeneza ni Master Alec , sasa baada ya kulinganisha thamnai ya baiskeli na mavazi hayo aliishia kutngisha kichwa kwa masikitiko.
Hamza wakati akiendesha baisikeli hio akipita kwenye nyumba zenye geti ambapo walinzi wake walikuwa nje wakitengeneza bustani waliishia kushangawa na huku wakimuonea wivu,wakijiuliza ndio fasheni siku hizi za kupandishana kwenye baisikeli zilizochakaa.
Kwa namna ambavyo walikuwa wakiangalia ilimfanya Regina kujisikia hali ya kukosa kujiamini kidogo lakini Hamza hakuwa na shida hata kidogo.
“Wife unatamani kula nini , unaonaje Ndizi za kukaanga na maziwa?”Aliuliza Hamza na Regina mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akipatwa na hamu maana ni muda mrefu hajakula ndizi..
“Sawa”
Hamza aliongeza spidi ya kuchanga na dakika ishirni mbele alienda kusimamisha kwenye mgahawa mdogo sana wenye mabenchi pembeni ambapo kuna ndizi zinapikwa hapo na kisha aliagiza na wakaenda kukaa pembeni.
Regina alikuwa amevalia jezi ya rangi ya pink ya Inter Miami na suruali Track ya Gucci, kutokana na kuwa na umbo dogo watu walimfananisha na mwanachuo.
Eneo hilo lilikuwa likipendwa na wanachuo waliopanga maeneo hayo ndio maana ilikuwa rahisi kumfananisha Regina na mwanachuo , licha ya kwamba alikuwa mrembo hakuna aliedhania msichana huyo ni Mkurugenzi wa kampuni kubwa ya Dosam.
Upande wa Regina baada ya kukaa kwenye mabenchi katika eneo hilo kukiwa na baadhi ya watu , alijikuta akiona ni muda mrefu sana kukaa chini kama hivyo akiwa na wepesi wa akili kama mtu wa kawaida tu.
“Regina mbona umeangalia sehemu moja bla kutoa macho, kula tayari nimekuwekea Tomato”Aliongea Hamza mara baada ya kumuona Regina ni kama anashangaa.
“Acha haraka huoni ndizi za moto hizo”Aliongea
“Basi ngoja nizipulize”
“Wewe acha , unataka uzitemee mate?”
“Asa si umesema za moto?”
“Zimepoa”
“Dah!, nyie wanawake kwa ukigeugeu”Aliongea Hamza huku akitingisha kichwa kusikitika.
Wawili hao walitumia zaidi ya lisaa kukaa katika kimgahawa hicho wakitafuna ndizi na kushushia na juisi , baadhi ya wateja waliokuwa hapo walikuwa wakiwageuzia macho mara kwa mara , muonekano wa Regina uliwapagawisha lakini vilevile Hamza alikuwa ni mtanashati(HB) kutokana na kuchanganya kwake rangi na kufanya waonekane walikuwa wakiendana na ndio ilifanya watu kuwaonea wivu.
“Wife baada ya hapa tuelekee wapi?”
“Popote unapotaka wewe”
“Unaonaje tukienda ile barabara ya upande wa Beach , haina magari na tunaweza kushindana kuendesha baiskeli”Aliongea Hamza mara baada ya kufikriia kidogo.
“Tunashindana vip wakati sijui kuendesha”
“Kumbe hujui kuendesha baiskeli?”
“Ni jambo la kushngaza kwani?, wanawake wengi kama mimi hawajui kuendesha”Aliongea Regina na kumfanya Hamza aone ni kweli.
“Bas tufanye hivi tunaenda na nitakufundisha namna ya kuendesha , ukichoka tunaweza kuingia kwenye hoteli pale na kupumzika na pia wanauza Seafood pale muda wa mchana”Aliongea Hamza na pendekeo hilo liliamsha shauku ya Regina
“Nitaweza kuendesha baiskeli leoleo?”
“Kuendesha baiskeli sio kugumu , kunatemgemena tu na wewe mwenyewe”
Regina siku nyingi alitamani pia kuendesha baiskeli lakini hakupata mtu wa kumfunidsha na hivyo baada ya Hamza kusema anaenda kumfundisha alijikuta akipata hamu ya kujua.
“Basi hakuna shida , nitajifunza na nikiweza tunashindana”Kauli hio ilimfanya Hamza kufurahi mno na kujiambia ndio muda wa kujichukulia pointi huo kwa mrembo huyo.
Baada ya kulipa walielekea upande wa barabara ya fukwe na kuingia kwenye hoteli ambayo walikuwa na huduma ya kukodisha baiskeli za kuchukulia mazoezi.
Eneo hilo lilikuwa pia na waendehsa baiskeli na asilimia kubwa walikuwa ni watalii.
Regina aliendesha japo kwa kushikiliwa lakini kila akienda mbele kidogo alikuwa akidondoka kwa kuegamia upande mmoja na mara ya mwisho kudondoka Hamza alimuwahi na kumshika kiuno.
Kama ujuavyo jezi ilikuwa nyepesi na kitendo cha Hamza kumshka kiuno ilimsisimua na kufanya sura yake kuzidi kuwa nyekundu na ilikuwa ngumu kusema alikuwa na aibu au vipi.
“Niachilie basi , mbona unaendelea kunishikilia hivyo naendeshaje sasa?”Alongea Regina mara baada ya kugundua Hamza hakuwa akimwachia.
Hamza macho yake yalikuwa yakikodolea kifua cha Regina na alikuwa akiwaza kama itatokea atakigusa kama Regina atadondoka kwa kuegamia upande wake.
“Hamza jamani!, hujanisikia?”Aliongea Regina kwa mara ya pili huku akionyesha kuchukia , alijua Hamza alikuwa akifanya makusudi kutumia kitendo hicho cha kumfundisha kuendesha baisikeli ili tu afurahie kumshika.
Hamza aliishia kutetema kiasi huku akimwachilia na kuona haya usoni.
Regina muda huo alianza kuendesha kwenda mbele lakini mara baada ya kusogea mita kadhaa alianza kupoteza balansi na alijikuta akipiga kelele mara baada ya kuoan anakwenda kudondoka lakini Hamza alikuwa asharuka kutoka alipo na kwenda kumdaka juu juu.
Baiskeli ilidondoka chini lakini mwili wake ulikuwa umepakatwa na Hamza na kufanya macho yao kukutana katika umbali mfupi sana kama sentimita tatu au nne hivi.
“Unaona sasa bila ya mimi kukushikilia unaweza kujiumiza”
“Ungeniacha nidondoke tu , sijakuomba msaada”Aliongea Regina kwa kiburi.
“Kama ni hivyo sikusaidii tena, nyanyua baisikeli yako mwenyewe”Aliongea Hamza.
“Hio ni juu yako”Aliongea huku akijitoa kwenye mikono ya Hamza na kwenda kusimamisha basikeli yake , hakujua kwanini lakini alijihisi hali baina yao ni kama inazidi kutokueleweka na kufanya mapigo yake ya moyo kwenda kasi mno.
Bila kujua alitumia asubuhi yote kujifunza kuendesha baiskeli mpaka akafanikiwa na hakuweza kuficha furaha yake baada ya kujua kuendesha baisikeli siku hio.
Walirudi mpaka kwenye mgahawa uliokuwa kando ya barabara na kisha waliegesha basikeli zao na kuagiza chakula cha mchana , lakini sasa kabla hata ya kuanza kula walisikia kishindo cha baiskeli zao kudondoka.
Hamza aliishia kukunja sura na kugeza macho yake upande walioweka baskeli zao na palepale ndio aliweza kuona ni gari aina ya BMW Z4 Convertible ndio imeigonga baiskeli yake na kuiharibu.
“Nini kinaendelea?”Aliulia Regina huku akigeuka na yeye na alijikuta akiweka uma chini mara baada ya kuona kilichotokea.
Hamza alisimama na kuelekea upande ule na aliweza kuona mwanamke na mwanaume wakiwa ndani ya gari na walionekana kwasababu gari hio ilikuwa imefunguliwa paa lake.
Hamza mara baada ya kuangalia watu wale palepale macho yake yalisinyaa mara baada ya mwanaume kumfahamu.
“Alex!?”Aliongea Hamza.
Alikuwa ni Alex muuza vyungu , mwanafunzi mwenzake wa chuo cha FEMU, alikuwa na mwanamke ambae Hamza hakumfahamu na ndio aliekuwa akiendesha.
Alex upande wake hakutegemea kumkuta Hamza eneo hilo , ukweli ni kwamba kwa muda mrefu hakumfuatlia sana Hamza tokea tukio la kuagiza watu wakadili nae nyumbani kwake kwa kudhania alikuwa na mahusiano na Frida.
Alex alionekana kushangaa na ni mara baada ya mwanamke mrembo sana kusogelea eneo hilo, ambae hakumjua moja kwa moja kama ni Regina ,ijapokuwa alishawahi kumuona Regina japo kwa kupitia picha kama mwanamke tajiri lakini mazingira hayo yalimfanya asimtambue moja kwa moja na kudhania amemfananisha.
“Hii baisikeli ni ya kwako?”Aliongea yule mwanamke aliekuwa amevalia miwani na Hamza alitingisha kichwa kukubali. Alikuwa ni mwanamke mwenye asili ya Kiarabu , ijapokuwa alikuwa amejaaliwa muonekano wa sura lakini hakuwa na umbo zuri.
“Hamza tunaomba radhi , mpenzi wangu amegonga baiskeli zenu bahati mbaya”Aliongea Alex huku akimwangalia Hamza.
“Babe unamfahamu?”Aliongea yule mwanamke huku akimwangalia Hamza kwa macho ya dharau.
“Ndio ashawahi kuwa kibarua wangu kule kazini”Aliongea Alex na kauli ile Hamza hakunja ndita , ukweli alitaka kusikia Alex akimtambulkisha kama wanasoma wote na kauli hio moja kwa moja aliona Alex ana inferioty juu yake ambayo hakujua inasababishwa na nini lakini ndio anayoionyesha muda huo ila hakujali.
“Hii sehemu ni pembeni kabisa na maegesho haya eneo lake ni kubwa, haya si makusudi umeyafanya kugonga baiskeli yangu?”Aliongea Hamza akimwangalia yule mwanamke.
“Hio nayo unaiita baiskeli , nimeona ni takakata ndio maana nimeigonga, tena angalia uchafu wako umekwaruza rangi ya gari yangu , unaijua thamani yake hii gari?” Aliongea yule mwanamke kwa kejeli kubwa na alichokuwa akifanya ni kama alikuwa akimdhalilkisha Hamza makusudi kutokana na uwepo wa Regina.
Lakini pia kwa wakati mmoja baada ya kusikia Hamza alikuwa kibarua wa Alex aliamini hata mwanamke wake atakuwa ni kapuku tu ndio maana wote wana baiskeli.
“Alex hebu uongea na mpenzi wako aelewe , yeye ndio kagonga baiskeli yangu na kuiharibu, ninachotaka ni fida na sio dharau zake”Aliongea Hamza.
“Hamza achana nae au tuite tu polisi”Aliongea Regina maana hakutaka ugomvi.
“Haina haja ya polisi , wataona ni ku wasumbua tu”Aliongea Hamza huku akimwangalia Alex amtulize mwanamke wake lakini Alex na yeye ni kama alikuwa akimuunga mkono yule mwanamke kutokana na uchakavu wa baiskeli yake.
“Babe , umemsikia huyu fukara , eti anataka fidia , ni kichekesho gani hiki?”Aliongea huku akicheka kwa nguvu na kufanya hata watu ambao walikuwa ndani ya mgahawa huo kugeuza macho upande wao.
“Sumaiya tuachane nao bwana , ngoja nimpatie laki moja ya matengenezo inamtosha”Aliongea Alex.
“Yaani utoe laki moja kwa ajli ya kutengeneza huo mkweche , wao ndio wanatakiwa kulipa fidia hili ni eneo ambao baiskeli za namna hii haziruhusiwi, usitoe hata mia hapa kuna tofauti kubwa ya nani apewe fidia”Aliongea kwa kupayuka na kumfanya Alex kunywea.
“Acha majigambo yako binti sio swala la hela hapa , wewe ndio ambae umeidharau baiskeli yangu na kuigonga makusudi kama vile unataka ugomvi, hivyo unapaswa kulipia”Aliongea Hamza.
“Kwahio unasema unaijua sana sheria , unajua mimi ni nani kwanza?”
“Sijui”
“Mjomba wangu ni Bashite Sweve nadhani ushamfahamu sasa?”Aliongea lakini Hamza bado hakuwa akimfahamu.
“Wife unamjua?”Aliuliza Hamza na Regina aliishia kukunja sura, alikuwa akimjua ndio lakini alikuwa mtu mdogo sana na hata kama anataka kuonana nae inabidi apitie ngazi za chini , yaani kwa ufupi huyo Bashite hana uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na Regina.
“Nishawahi kusikia jina lake ila simjui”Aliongea Regina.
“Acha dharau wewe dada , nani asiemjua mjomba ndani ya jiji hili wakati karibia Tanzania nzima anafahamika”Alex mara baada ya kuona Sumaiya ana utafuta ugomvi na mwanamke yule mrembo aliingilia.
“Hamza haina haja ya kufanya mambo kuwa magumu kwako , fanya hili lipite isitoshe tunafahamiana, tulimalize kishikaji”Aliongea Alex akijaribu kutuliza hali na mara baada ya kuongea hivyo Sumaiya alijisikia kujivunia na alipiga hatua na kwenda kwenye gari na kutoa mkoba kisha akatoa hela za elfu kumi kumi tano na kumtupia Hamza.
“Una bahati nipo kwenye mudi nzuri leo , hicho ndio kiasi kinachokutosha kutengeneza baiskeli yako “Aliongea na kisha alitaka kugeuza kuondoka lakini Hamza alimzuia.
“Kama nilivyosema hapa swala sio hela, na huwezi kunipa hela unavyotaka na kusema ndio fidia hizo ni dharau”Aliongea na kumfanya kugeuka kwa mshangao.
“Hivi wewe ni mjinga eti , yaani unasema elfu arobaini nilizokupatia hazitoshi au ndio ushaona nina hela unataka ujipatie nyingi kwa sababu zisizo na mashiko, nimeacha kumwambia mjomba wangu juu ya hili ili kutokufanya maisha yako kuwa magumu lakini naona unanijaribu”Aliongea.
“Sina haja ya kumuogopa mjomba wako , umeharibu baiskeli yangu sihitaji pesa zako za kejeli nahitaji fidia”Aliongea Hamza na kisha alimsogelea Sumaiya ili kutaka kumshika mkono lakini ilikuwa ni kama Alex alikuwa akisubiria kwani palepale alisogea kwa mbele kumkinga na Hamza hakutaka hata kumjali Alex alikuwa na ukaribu nae chuoni kwani alimshika yeye na kumkunja mkono kwa nyuma na kumfanya aanze kulalamika kuhisi maumivu.
“Ukiomba msamaha kwa kosa ulilolifanya niamuachia mpenzi wako”Aliongea Hamza.
“Unafanya nini wewe mjinga, niambie unataka kiasi gani nitakupa na mwachie Alex”Aliongea.
“Sitaki hela , umeharibu baiskeli yangu makusudi na ukaniletea jeuri yako , hivyo tafuta fundi aitengeneze na ukishamaliza omba msamaha na fundi ndio atatoa makadirio ni kiasi gani unapaswa kufidia”Aliongea Hamza
“Nadhani huna akiili , yaani unataka nikatengeneze huu mchuma wako unaoita baiskeli na nipoteze muda , ingekuwa gari sawa ila sio baiskeli iliochoka kama hio”
“Usipofanya hivyo siwezi kumwachia”Aliongea Hamza huku Alex akijitahidi kutumia nguvu kujitoa lakini alishangaa hakuwa na uwezo hata wa kumsukuma Hamza kurudi nyuma.
Sumaiya mara baada ya kuona Alex anaumia alijikuta akipoa.
“Haya yaishe , ngoja nimpigie fundi aje”Aliongea na Hamza alitabasamu na kumwachia Alex kisha akakaa pembeni.
Matukio hayo yote yalimfanya Regina kuishia kukunja sura tu na kuona ni kama Hamza anayakuza sana kwa baiskeli iliochakaa kama hio.
“Hamza unapoteza tu muda wako , haina haja ya kujibisha na mtu wa namna hio”Aliongea Hamza.
“Kwanini nisidai haki yangu , Wife nishakuambia nina muunganiko wa kiroho na hii baiskeli na siwezi kuiachia kirahisi namna hio, bado haijatmiza malengo yote”Aliongea
“Ni baiskeli tu bwana , nitaakununulia nzuri zaidi ya hii”Aliongea lakini Hamza hakutaka kumsikiliza hata kidogo na Regina aliishia kutingisha kichwa kwa masikikito.
Hamza alikuwa siriasi mno na baiskeli yake na hakutaka waondoke mpaka inatengenezwa hivyo walisubiri mpaka nusu saa baadae na fundi wa baiskeli aliweza kufika
“Naitwa Fundi Simbe nimeambiwa unashida ya matengenezo ya baiskeli”Aliongea mwanaume mmoja hivi alievalia bakrashia na kanzu akijitambulisha kwa Alex na Sumaiya.
“Fundi hubu nenda kaangalie baiskeli yenyewe ni ile pale , ukiharakisha itakuwa vizuri maana nimepoteza muda wangu mwingi hapa, ichunguze kwanza uniambie ni kiasi gani napaswa kulipa kama fidia niondoke”Aliongea huku akimkata jicho Hamza.
Mzee yule alionekana kuwa mstaarabu na muungwa na aliishia kuwatingisha cichwa Hamza na Regina na kisha alienda kuangala ile baiskeli.
Mzee yule mara baada ya kuanza kuikagua ile baiskeli ya Hamza , macho yalianza kumtoka na ni kama kuna kitu ambacho alianza kukitafuta na alizunguka nyuma na mbele kuangalia kwa umakini mkubwa na baada ya kuridhika alirudi sehemu alipokaa Sumaiya huku akihisi kijaso kumtoka.
“Nimekwisha kuiangalia tayari na haya ndio makadirio ya fidia yake pamoja na utengenezaji”Aliongea akiandika tarakimu kwenye kijikaratasi huku akiwa kama hajiamini amini
“Wewe ongea tu , sina haja ya kusoma”
“Kwa jinsi ilivyoharibika na chuma chake makadirio ni Dola elfu arobaini unazotakiwa kulipa..”Aliongea yule Mzee.
“Unasemaje ..?!”
Sumaiya alijikuta akitemtemea juisi aliokunywa mdomoni bla kupenda yule mzee wa watu kwenye kanzu yake mara baada ya kusema anapaswa kulipa zaidi ya milioni mia za Kitanzania.
SEHEMU YA 105
“What the f*ck , Fundi umechanganyikiwa?, hivi unaijua dola elfu arobaini wewe?”Aliongea Alex kwa nguvu akishindwa kabisa kuvumilia.
Regina pia baada ya kusikia kauli hio kutoka kwa fundi huyo aliona atakuwa amechanganyikiwa pia, inakuwaje fidia iwe kubwa hivyo, alijikuta akigeuza shingo yake na kumwangalia Hamza na kumkuta alikuwa amekunja mikono yake akiwa hana wasiwasi kabisa na kengele ya kuumbuka iligonga katika kichwa chake maana ni kama alishajua nini kinaenda kutokea baada ya hapo.
Ubaridi ulianza kumpitia katika uti wa mgongo , kumbukumbu za tukio la Master Alex ni kama lilianza kujichapisha kwenye akili yake.
Alianza kujiuliza maswali na kujiambia au inamaana Hamza hata baiskeli aliokuwa akiendesha ilikuwa na thamani kubwa kuliko alivyokuwa akiwaza.
“Fundi Simbe naomba unisamehe kwa lugha yangu , ni mshituko ulionnipata , hebu ongea vizuri maana nahisi tumekusikia vibaya”Aliongea Alex.
“Mnaweza kuhisii mmenisikia vbaya ila ni kwasababu hamna uelewa juu ya hii baiskeli na mimi ndio mtaalamu wa muda mrefu wa baiskeli najua ninachoongea , nilijua mnajua ndio maana mkanipigia simu nije kuangalia mwenyewe”Aliongea
“Ni baiskeli tu hio tena iliochakaa mno , kwanini fidia yake iwe kubwa namna hio?”Aliuiza Sumaiya.
“Ni ya Zamani ndio maana thamani yake ni kubwa , hii baiskeli imetengenezwa mwaka 1938 kwa ushirikiano kati ya kampuni ya Humber na kampuni ya Dunlop, ndio ilikuwa baiskeli yenye upekee zaidi iliotengenezwa kwa malighafi ghali kuwahi kutokea katika mwaka huo , zilifuatana baiskeli nyingine za muundo huu mpaka mwaka 1953 ndio uzalishaji ukasitishwa , makampuni makubwa ambayo yanauza vitu vya kale kwa mnada, baiskeli ambazo wameweka kipaumbele kwa thamani kubwa kwa atakaepeleka kwao ni hizi za Humber , mimi mwenyewe nimesoma tu lakini niliweza kujua haraka haraka hi basikeli ni yenyewe kutokana na kwamba ukiangalia kwa chini utaona kuna mchoro wa vidole vitano vya kiumbe asie binadamu vilivyofungamana na vidole vitano vya binadamu , kwa juu pia kuna chata la taji ambalo lilimwakilisha Mfalme George wa sita, kwa lugha nyepesi hii ni baiskeli iliotengenezwa na kuendeshwa na mfalme Goerge wa Uingereza , miaka kumi na mbili iliopita ilipigwa mnada na kununuliwa na mtu ambae jina lake halikutajwa kwa Dollar za Kimarekani milioni saba ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni kumi na tano za kitanzania , cha kuzingatia ni kwamba wakati huo baiskeli hii inauzwa ilikuwa katika hali yake nzuri na vitu vya kale kama hivi thamani yake inatokana na historia ya mauzo yake yaliopita katika mnada , nina uhakika kwa hali hiii hata kama haijatengenezwa ikipigwa mnada itauzwa kwa takribaini dollar milioni tatu””Aliongea Mzee huuyo kitaalamu kabisa na alionekana alikuwa mjuvi nje ya muoneano wake.
“Acha porojo fundi , tokea nizaliwe sijawah kusikia kuna baiskeli ghali namna hio , ninavyojua hizi baiskeli ni laki laki ikienda sana ni milioni moja huko lakini sio kufika milioni hamsini kuendelea , sembuse bilioni”Aliongea Sumaiya kwa hasira
“Upo sahihi kwa mtazamo wako kwasabababn pia inaonekana kuwa chakavu sana , lakini hujiulizi kwanini kampuni ya Dunlop ambayo imetengeneza haya mataili yake imetangaza dau kubwa kwa mtu atakae irudisha kwao , kama ingekuwa baiskeli za kawaida kama hizi ambazo zinatengenezwa na kampuni ya Humber ni kweli kabisa gharama yake haizidi hata milioni tatu .. kinachouzwa hapa inavyosemekana sio baisikeli kama baiskeli ni siri na maana ambayo imefichwa juu ya hii baiskeli. Ukweli hata mimi nimeona pekee Vidio ya hii baiskeli ikiwa makumbusho huko Uingereza , lakini sijawahi kuiona ana kwa ana ndio maana nimeshituka sasa hivi kuiona mtu anaiendesha katika mazingira ya kawaida kama hivi, kama hamuamini maneno yangu mnaweza tu kuingia mtandaoni kwenye tovuti ya kampuni ya Dunlop mtaona tangazo na Vidio yake , haijabadilika muonekano kabisa ipo hivi hivi”Aliongea akiwa na uhakika na Hamza alitingisha kichwa kumkubali yule mzee maana hakutegemea fundi atakaekuja angekuwa mwelewa hivyo , hata mpango wake aliokuwa nao mwanzo wa kumkomesha Sumaiya aliachana nayo baada ya kuona mambo yamekuwa mepesi.
Mara baada ya kusikia maelezo ya Mzee Simbe walijikuta wakipagawa , yaani Alex na Sumaiya , macho yaliwatoka na kwa namna mzee huyo alivyokuwa akijiamini haikuwa na uongo hata kidogo .
Palepale Sumaiya alijuta , alijua kugonga baiskeli hio kama ilivyokuwa tabia yake ya kununua ugomvi angeweza kumdhalilisha mtu kwa kiasi kidogo cha pesa lakini hakujua gharama yake itakwenda kuwa sawa na gari yake.
Nani angejua mkweche ambao Hamza anaendesha una thamani zaidi ya bilioni kadhaa za kitanzania na unatafutwa na kampuni kubwa za minada duniani kwa dau kubwa.
Regina hata yeye alikuwa kwenye mshituko mkubwa na mara baada ya akili yake kukaa sawa ilibidi amwangalie Hamza kwa maswali mengi.
“Si ulisema uliinunua wewe kwa mtu au ulinidanganya kuna mtu amekupa?”
“Sijadanganya, kuna mzee alikuwa akiiendesha na aliniambia ameichoka ndio maana nikainunua, mimi sijafikiria sana wakati nainunua nilichotaka ni kumiliki baiskeli kwa ajili ya kurahisisha mishe zangu basi”Aliongea Hamza huku akicheka kinafiki.
“Umefanya makusudi , inawezekana vipi ununue baiskeli ya gharama kubwa hivyo kwa ajili ya kuendesha tu?”Aliuliza Regina.
“Babu alieniuzia hii baiskeli alikuwa haiendeshi na ameihifadhi tu stoo , sasa nikaona kuliko ichakazwe na kutu si bora niinunue niitumie mimi na kuipa uhai , au na wewe unaamini huyo mzee alinipa kama zawadi , pengine alinipenda baada ya kwenda nyumbani kwake kumrekebishia bomba lililokuwa likivujisha maji jikoni ndio maana akaniuzia kwa bei sawa na bure, isitoshe siku hizi wanaoendesha baiskeli pia ni wachache sana, inaweza pia kuwa s sababu”Aliongea Hamza .
“Kama ni hivyo kwanini hukuniambia ni ya thamani sana wakati unajua kila kitu au ulikuwa mpango wako kunifanya nionekane mjinga?”Aliuliza Regina huku akisaga meno na kukumbuka namna ambavyo alimkataza Hamza akautupe huo mkweche.
“Haha.. haikuwa na haja sana , nilijua huwezi kuitupa baada ya kukuambia nina muungano nayo kiroho”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kukosa neno lingine la kuongea na kujiambie ngoja tu avumilie ujinga wake.
“Siwezi kukuamini hata kama umeleta takataka nyumbani kwanzia sasa, hebu malizana nao tuondoke”Aliongea na Hamza aliitikia kwa kichwa na kisha aliwasogelea Sumaiya na Alex.
Alex muda huo alikuwa amechanganyikiwa sana , ukweli ni kwamba alishawahi kumuona Hamza akifika chuo na hio basikeli na siku zote waliishia kumcheka maana ilikuwa chakavu sana , lakini muda huo alikuwa akiumbuka laivu na mpenzi wake Sumaiya.
“Unaonaje sasa namna unavyokwenda kulipa pesa nyingi kutokana na dharau zako?”Aliongea Hamza na kumfanya Sumaiya kuanza kujutia matendo yake.
“Huwezi kunilipisha kiasi chote hicho cha pesa kwa kama fidia , Mjomba wangu ni Meya huwezi kunizurumu kirahisi”Aliongea Sumaiya.
“Kama unahisi mjomba wako anaweza kukusaidia katika hili , mpigie simu , ninachotaka ni fidia hapa sio nani ni nani wako”Aliongea Hamza.
“Sumaiya mpigie simu mjomba wako akusaidia katika hili , hicho kiasi ni kikubwa sana”Aliongea Alex na Sumaiya hakutaka kupoteza muda na kupiga simu palepale na ndani ya dakika chache ikapokelewa.
“Sumaiya kuna nini si tulitoka kuongea asubuhi tu nafanyia kazi swala lako”Sauti upande wa pili ya kiume ilisikika.
“Mjomba nimepatwa na tatizo lingine , niligonga baiskeli ya mtu kwenye maegesho ya magari na sasa hivi anataka fidia ya zaidi ya dolla elfu arobaini”Aliongea akijitetea.
“Nini.. nani huyo mwizi kichaa…”Saut upande wa pili ilifoka.
Upande wa yule fundi mara baada ya kuona kinachoenda kutokea alimsogelea Hamza na kuongea nae kwa sauti ya chini.
“Japo mjomba wake ni meya tu lakini vilevile ana koneksheni kubwa na vigogo wa serikali , nadhani ulimalize tu kwa kiasi kidogo cha pesa nitairekebisha baiskeli yako na kurudi vizuri tu”Aliongea yule bwana.
“Sijali koneksheni yake mimi , hapa ni mpaka nilipwe fidia juu ya dharau alizonionyeshea, watoto kama hawa wanaolelewa vibaya hawawezi kujifunza bila kuwapa fundisho”Aliongea Hamzaa na kumfanya Regina kuona nia ya Hamza ni kumshikisha adabu Sumaiya na sio swala la hela.
“Ngoja nimpigie Mzee Kibatala atajua namna ya kumaliza hili haraka”Aliongea Regina na Hamza alimkumbuka Mzee Kibatala ni mwanasheria Kongwe Tanzania na alimkubalia.
Upande wa Sumaiya mjomba wake alimwambia asubiri atatuma mtu kuja hapo mara moja kudili na huyo mwizi kichaa na wakati anamaliza kuongea na simu ndio na Regina alikuwa anamaliza kuongea na Mzee Kibatala ambae alihakikisha ndani ya dakika atakuwa amelimaliza na Meya.
Wote walisubiri dakika kadhaa huku Sumaiya akijiona mshindi , upande wa Alex yeye haikueleweka alikuwa akifikiria nini ila macho yake yalikuwa hayatoki kwa Hamza na Regina.
Muda huo wakati akiwaza simu ya Sumaiya ilianza kuita na alitabasamu.
“Mjomba ndio maana nampenda , huwa hacheleweshagi maombi yangu’”Aliongea kwa lafudhi yake yake yenye uarabu.
“Sumaiya ushaanza tabia yako ya kutafuta matatizo?”
“Unamaanisha nini mjomba?”
“Mzee Kibatala amenipigia simu juu ya swala la wewe kugonga baiskeli ya watu , inakuwaje unangia katika migorogo na Mkurugenzi wa kampuni kubwa kama ya Dosam , inamaana umeshindwa kumjua Bosi Regina wewe , huangaliagi taarifa ya habari , hujawah kuona picha yake kwenye mitandao”Mjomba alijikuta akifoka na kumfanya Sumaiya kugeuza macho yake haraka na kumwangalia Regina ambae alikuwa ametulia akiwa hana wasiwasi
“Sumaiya aasemaje?”
“Anasema Regina mmiliki wa kampuni ya Dosam…..”Aliongea Sumaiya lakini alikatishwa na sauti ya mjomba wake kwenye simu.
“Sumaiya kama unataka ulichoomba nikukamilishie malizana kwa heshima na bosi wa Dosam na kisha umuombe msamaha , sitaki matatizo kwa kufanya hili swala lisambae kwa wakubwa”Aliongea kwa hasira na palepale simu ikakatwa.
Upande wa Alex muda uleule ni kama sasa akili yake ilikuwa imemtoka usingizini , tokea aje hapo alikuwa akimfananisha Regina lakini alishindwa kumjua fika licha ya urembo wake.
Pumzi zilianza kuwa nzito mara baada ya kugundua hakuwa akimfananisha Regina , alikuwa ndio bosi mwenyewe wa kampuni ya Dosam , mwanamke tajiri lakini sio hivyo tu mwanamke ambae alisababisha kupotea kwa rafiki yake James na baba yake.
Alijikuta akimwangalia Hamza na kisha macho akayarudisha kwa Regina, palepale maswali kibao pamoja na wasiwasi ulimvaa , mara ya kwanza ilikuwa Frida , ikaja Prisila , umiliki wa baiskeli ya bei ghali na sasa Regina.
Ukweli ni kwamba licha ya tokea mwanzo alikuwa akijua familia ya James ilitaka kuingiza nguvu yake katika kampuni ya Dosam , hata kwa kutumia hila lakini licha ya mara nyingi kusikia jina la Hamza likitajwa hakujua ni Hamza anaemjua na alijiona mjinga kwa kutofikiria mbali.
“Kwannini sikumwambia Chriss anionyeshe picha?”Aliwaza Alex akikumbuka siku ambayo Chriss alikuwa akimlaumu James kwa mwanaume anaeitwa Hamza kumchukua na mwanamke wake, alijua mtu huyo alikuwa ni Hamza lakini hakujua ni Hamza huyu.
Hamza mara baada ya kuona wawili hao wanamshangaa , hakutaka kuendelea kupoteza muda , isitoshe muda ulikuwa umeenda na alimsogelea Sumaiya na kisha akamwambia ampatie simu yake.
“Simu yangu ya nini?”Aliuliza huku akiwa mpole lakini Hamza wala hakumjali na palepalepale aliandika akaunti namba yake ya benki
“Ndani ya siku mbili ingiza dola elfu hamsini humo”Aliongea Hamza.
“Nini ,sio tena elfu arobaini?”
“Nishasahau nilisema elfu arobaini hivyo ingiza hamsini ninazokumbuka”Aliongea na Sumaiya aliishia kumwangalia tu Hamza bila ya kuongea neno , alikumbuka namna mjomba wake alivyosikika kwa hasira.
“Sumaiya nitakuchangia nusu , ila hakikisha mjomba wako anakamilisha lile swala”Aliongea Alex akiwa siriasi.
“Lakini Alex nitabakiwa sina hata mia mfukoni na nilitegemea hili dili kwenda Korea kufanya upasuaji”
“Maliza kwanza hili Sumaiya la sivyo utafanya kila tulichopanga kwa mjomba wako kuvurugika , fursa nyingne tajitokeza na utapata hela”Aliongea Alex.
Upande wa Hamza hakujua ni swala gani lakini kwa namna moja ama nyingine alijua lazima ni maswala yake ya kishushushu kama alivyosikia kutoka kwa Frida kwamba Alex alikuwa shushu kutoka Binamu.
Kwasababu Baiskeli iliharibika sana , Fundi alipaswa kuondoka nayo lakini Hamza aliongea nae chini kwa chini akimpa tahadhari wa kuhakikisha baiskeli hio haipotei na wala hakwangui chuma chake na kufanya madini yaliotumika kuitengeneza yaonekane. Mzee huyo pia baada ya kujua Regina ni bosi wa kampuni ya Dosam ile hali ya uaminifu iliongezeka palepale na kuona anaweza kufanywa chochote ikitokea amefanya utapeli.
Sumaya na Alex waliishia kumwangalia Hamza na Regina wakitokomea kwenye macho yao , Sumaiya alikuwa akiwazia hasara ya pesa alioingia lakini wakati huo Alex alikuwa na shauku kubwa ya kumjua Hamza ni nani haswa na kwanini wanawake wenye vyeo vikubwa na warembo wanaonekana kumng’ang’ania , haikuwa hivyo tu tetesi alizoweza kusikia kuhusu kupotea kwa James , Mzee Benjamini na Lamla ilihusishwa na Hamza ambae sasa anamjua ni Hamza aliekuwa akimjua , sasa alijiambia kama Hamza aliweza kuvuruga kila kitu maana yake hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo.
Matukio mbalimbali ambayo yalimhusisha Hamza aliweza kuyakumbuka ikiwemo tukio la Hamza kuuwa mwanajeshi , hofu palepale ilimvaa na kujiambia anapaswa kutokushindana na Hamza na anapaswa pia kumpa tahadhari na ndugu yake Chriss.
Upande wa Regina na Hamza hawakutaka kurudi nyumbani mapema hivyo walirudi eneo lilelile walipokodi baiskeli na kuchukua nyingine na kisha kuendelea kuendesha kwa kushindana awamu hio.
Regina alipenda rangi ya baiskeli mpya Hamza aliokodi na kumpokonya na kisha wakaanza kuendesha, licha na yaliotokea ni kama ashaanza kumzoea Hamza na surprise zake hivyo hata hakumiza kichwa zaidi ya kufurahia uzoefu mpya, lakini alijiambia anapaswa kuzingatia kila anachomiliki Hamza anapaswa kuwa nacho makini maana havikawiii kugeuka dhahabu.
Baada ya kuendesha kwa muda mpaka kuchoka walirudisha baiskeli za watu na kisha walienda kukaa ufukweni.
Regina hakuwahi kuwa na hali tulivu kwa muda mrefu kutokana na kuwa bize mara nyingi na siku hio alijikuta akifarajika kuona watu wengi wapo ufukweni familia kwa familia na wenza kwa wenza wakifurahia maisha na kusahau shida zao.
Alikuwa akijua hata kama mtu amefanikiwa vipi , kila mtu ana shida zake kwenye maisha yake , hivyo kitenDo cha kufurahi huku wakisahau shida ilimfanya kuona pengine na yeye inawezekana kuwa na furaha namna hio.
Wakati akiwa amekodolea macho jua lililokuwa likitokomea magharibi , Hamza alimsogelea kwa nyuma na kisha kumkumbatia kwa kupitisha mikono kwa mbele na kuweka kidevu chake kwenye bega lake.
Regina alitaka kumuondoa Hamza lakini alishndwa na kumuacha kama alivyo na kujikuta akitoa tabasamu hafifu huku akiendelea kuangalia jua, walikaa hivyo kwa muda mrefu huku wakora ndani ya eneo hilo wakimuonea Hamza kwa kuwa na mwanamke mrembo kuzidi wapenzi wao na Hamza alijisikia fahari.
Dakika hio alikumbuka kitu na alitoa simu yake na kumuomba Regina wapige picha ya kukumbuka siku yao ya kwanza kutoka out na Regina alimwamboa hapendelei kupiga picha lakini Hamza alipiga selfie kwa kumlazimisha na mwishowe Regina alijikuta akitabasamu ili picha itoke vizuri.
“Sio mbaya hii picha imetoka vizuri mno , hapa ukiangalia utaona kabisa kijana machachali Hamza Mzee na mwanamke mrembo kuliko wote bongo tunavyoendana , yaani nadhani malaika wanashangilia sasa hivi huko mbinguni”Aliongea Hamza akicheka
“Unafikiria sana ujinga , una machachali gani sasa?”Aliuliza Regina huku akivuta mdomo kiabu.
“Hehe wife ngoja nikutumie kabisa na uiweke kwenye wallpaper ya simu yako , ukiiona mara kwa mara utagundua ni namna gani mimi ni kiijana machachali na utakufa na kuoza kabisa juu yangu”
“Wewe hebu acha kwenda mbali”Aliongea Regina.
“Basi kama hutaki kuiweka , unaonaje ukanisave angalau namba yangu kwa jina zuri zuri, angalau nipate hata faida ya kuitwa mume wako basi”.
“Inatosha sasa , sitaki watu wanione nimegeuka kichaa ghafla”Aliongea Regina na dakika ile aligeuka kichaa kweli na kuanza kukimbia kwenye mchanga wa fuke akipita watu kwa spidi.s
“Regina babe , unaenda wapi sasa , nisubiri basi”Aliongea Hamza na kuanza kumkimbiza Regina kwa nyuma na ilikuwa picha nzuri sana kama vile walikuwa wakitengeneza filamu ya mapenzi.
ITAENDELEA-watsapp: 0687151346
Ahsante mkubwaSHETANI RUDISHA AKILI ZETU

Shukuran sanaSHETANI RUDISHA AKILI ZETU

Mchek tsap ujiunge kwenye group lakeGuys hii story nimeipenda sana lakini sehemu ya 12 hadi 15 sijaziona naweza zipataje?