Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #81
SEHEMU YA 75
kuwapumbaza watazamaji hao. Baada ya hapo ndipo alipofanya hila kukorofisha mtambo huo. Katika kipindi hicho cha kutoonekana aliondoka na kupenyapenya kwa hila katika viochochoro hadi nyumbani kwa Moole ambako alibisha mlango na kufunguliwa na Moole mwenyewe. Alipoomba mzigo wake Moole alikanusha kabisa kwamba hakuwa amechukua mzigo wa mtu kama huyo. Lakini ngumi mbili tatu zilimfanya amwongoze ghalani ambako Joram alimvamia na kumfunga mikono na miguu, kisha akaufungua na kuchukua vile vitu muhimu tu. Akarudi haraka hadi chumbani kwake ambako, akisaidiwa na Nuru alipekuapekua na kupata ramani walizoziandaa, pesa na vitu vingine. Ni wakati Joram alipomaliza kujivisha ngozi hizo zilizomfanya aonekane kama alivyo sasa, alipoingia yule kachero wa kwanza. Hila aliyoitumia Nuru ya kujifanya kuwa alikuwa akipambana na mzungu aliyetaka kumnajisi ilimsaidia sana. Ndipo kachero huyo alipopata kile alichostahili kupata. Nao akafanya haraka kumsaidia Nuru kuvaa “Uzungu” wake na alipokamilika walivichukua vilivyokuwa muhimu na kuingia mitaani.
Wakiwa wameikariri ramani hiyo kikamilifu, kazi waliyoifanya mitaani humo ilikuwa kufuata yale majengo waliyokusudia na kutega vile vigololi vilivyopatikana kwa Chonde na kuvitegesha katika kipindi cha saa tatu kamili. Walifanya kazi hiyo kwa ukamilifu kuliko walivyotegemea. Watu wachache ambao walilazimika kupoteza maisha ni wale walioshuku jambo au kujaribu kuwazuia kufanya kazi yao. Wakiwa hawajui kuwa wanapambana na nani watu hao walikufa kwa utulivu kabisa, isipokuwa yule ambaye kifo kilimtetemesha hata akaamua kuruka dirishani kutoka ghorofa ya nne akiwa na kisu kifuani.
Sasa kazi ya kutega vigololi ikiwa imekwisha, Joram alimtazama Nuru na kumnong’oneza, “Awamu iliyobaki ni yangu peke yangu. Ni lazima niingie katika mtambo wao na kuulipua. Nikiweza kuulipua kabla ya madhara tuliyoandaa katika jiji hili kutokea litakuwa jambo jema sana. Nikishindwa, mioto itakapoanza nenda pale ambapo nimekuonyesha katika ramani ukanisubiri.”
“Hatuwezi kwenda wote?”.
“Haiwezekani. Tumelijadili hilo mara nyingi sana.”
Wakakubaliana.
Kisha Joram akajiingiza miongoni mwa watu waliokuwa wakipita katika mitaa hiyo, akielekea ilikomwelekeza ramani yake. Mwendo wake ulikuwa wa haraka na uhakika, ingawa alifahamu kikamilifu ulinzi mkali uliozunguka mtambo huo. Matumaini ya kurudi yalikuwa ndoto isiyo na hakika. Hakujali. Asingejali kufa, endapo tu kifo hicho kingetokea baada ya kufanikiwa kutega mabomu yake katika mtambo huo. Aliamini kuwa Nuru asingeshindwa kurudi Tanzania katika msukosuko mkubwa utakaoutokea mji huu, saa mbili na nusu baadaye.
Nuru alimwacha Joram na kuondoka kwa hatua chache. Mara tu alipoamini kuwa asingegeuka tena kumtazama, alianza kumfuata. Hakujua kuwa yeye pia alifuatwa na watu wanne wenye silaha kali mkononi na mioyo yenye hofu na hasira dhidi yake.
MKOBA wake wenye silaha zake zote ukiwa umetulia mkononi, kwa utulivu na uhakika kama mzigo wowote ambao haukuchukua chochote cha haja, Joram alipiga hatua moja baada ya nyingine katika mitaa ya mji mkuu wa Afrika Kusini. Alipishana na wengi akiandamana na wengi wenye misafara yao.
Kitu fulani katika damu yake kilimnong’oneza kuwa anafuatwa. Hilo halikumshangaza. Tangu alipoachana na Nuru alifahamu fika kuwa angepinga ushauri wake wa kumsubiri pale alipomwelekeza hadi atakapoimaliza awamu hii ya mwisho ambayo ilikuwa ya hatari mno. Akiwa ameshangazwa na ushujaa wa msichana huyu, jinsi alivyokuwa tayari kuihatarisha roho yake kwa hiari, aliamini kabisa kuwa asingekubali kuikosa fursa hii ya mwisho, fursa ambayo endapo ingefanikiwa isingefutika katika kurasa za matukio muhimu ya kihistoria duniani.
ITAENDELEA