Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 20.
Asubuhi ya siku mpya kabisa ilimkutia Calvinjr njiani akiwa anaendesha gari yake kwa spidi kali mno ili kuwahi Dar es salaam, alitakiwa kufika mapema ili wakae kikao na kiongozi wake pamoja na dada yake ili waangalie ni sehemu gani ambayo walipaswa kuifanyia kazi kwani mambo yalionekana kuwa magumu tofauti na vile walivyokuwa wanayaona mwanzo na mheshimiwa raisi alikuwa anahitaji ripoti ya kuwasilisha kwa wananchi haraka sana.

Kijana huyo alihisi kichwa chake ni kizito kwani licha ya kuwa na mambo asiyo yajua juu ya uwepo wa wale watu wavaa mavazi meusi, bado hakuelewa ni kivipi haya mambo ya nchi nayo yanatokea. Alitamani sana kuwahusisha wale watu wa yale mashuka meusi kuhusika na haya mambo ila aliona atakuwa anajipoteza tu muda maana hawa wa sasa walikuwa wanavaa suti na sio mashuka tena hivyo akaona kwamba mawazo yake hayapo sahihi. Anajipoteza tu.

Akiwa kwenye msongo huo wa mawazo huku akiwa makini sana na gari yake barabarani, simu yake iliita kwa fujo alitaka kuipotezea ila baada ya kuona jina la Sarafina William ambaye alikuwa mwanamke aliye mpa mchongo mkubwa sana wa pesa za kutosha, hakuona sababu ya kufanya hivyo. Akaamua kusimamisha gari na kutulia kisha akaipokea

"U hali gani mrs William"
"Naomba uniite tu Sarafina kwa sasa"
"Sawa madam, vipi hali yako kwa sasa"
"Namshukuru MUNGU nimekaa sawa japo haiwezi kuwa rahisi sana, aliyekufa ni baba yangu mzazi hivyo nafsi yangu inaniuma sana"
"Kila kilicho andikwa na mwenyezi MUNGU lazima kitatimia, huwa ni suala la muda tu hivyo tunapaswa kumshukuru kwa kila jambo huku tukimuombea mzee apumzike kwa amani"
"Ahsante! Calvin, lakini kwanini ulinidanganya? Unajua mimi sina rafiki wa karibu kwenye maisha yangu zaidi ya baba na mama yangu. Mama kwa sasa hayupo sawa hivyo naye anahitaji faraja, jana nilitegemea sana uwepo wako lakini haikuwa hivyo, siku nzima nimekuwa mpweke sana, sijapenda ulicho kifanya"

"Naomba unisamehe sana, sikufanya kwa ubaya ila nilifanya vile kwa sababu nilijua familia mnahitaji muda wa kuwa pamoja, muda wa kuongea mambo ya mhimu kama familia hivyo sidhani kama ungekuwa ustaarabu na mimi nikavamia ila nilipanga kuja kukuona mkishakuwa mmetulia"
"Nakuhitaji saivi tafadhali Calvin" mwanaume aliangalia saa yake, alibakisha masaa kama matano mpaka aingie mjini, aliwaza kidogo kisha akamjibu.
"Unaweza kunipa masaa matano ili tukae pamoja mpaka jioni? Kwa sasa nimekuja kumsaidia kidogo baadhi ya majukumu mama yangu kwenye biashara zake baada ya huo muda nitakuwa hapo kama hautajali"
"Sawa mimi nitakusubiri, nahitaji na zawadi yangu uliyokuwa umeniahidi"
"Okay" mwanaume alijibu huku akikata simu yake. Aliingia ndani ya gari na kuinamia kwenye usukani

Alimsikitikia sana mwanamke huyo, alikuwa anapitia kipindi kigumu sana. Alielewa hasara za kumkosa mzazi hususani baba kwenye maisha kwa sababu hata yeye maisha yake hakulelewa na baba, aliwasha gari na kuendelea na safari yake.

Tina kwake asubuhi na mapema ya siku ya pili yake ilimkutia kwenye gari ambayo alikuwa ameikodi, hiyo gari ndicho kilikuwa kitanda chake hivyo alilala humo. Asubuhi alikuwa na mawazo mengi ya kuwaza mambo yalivyo tokea kimasihara kabisa mpaka wakawapoteza wale watu saba.
"Eti kuna mtu alitoka Ikulu kirahisi tu namna hii akaingia eneo penye ulinzi kama lile? Haiwezekani. Tufanye kwamba alikuwa na vielelezo vya kutoka Ikulu, sasa alivitoa wapi? na maelezo ya kujua kwamba wale watu wamehifadhiwa pale ndani aliyapata wapi na kwa nani maana haikupita hata siku moja tangu niwakamate wale watu. Hapa kuna kitu ambacho sicho kinaendelea, nadhani hata mimi binafsi natakiwa kuwa makini isivyo kawaida" alijiongelesha mwenyewe akiwa anaangalia angalia picha ya yule mtu kwenye laptop.

"Wait..."Alijiongelesha mwenyewe akiwa anaikuza picha ya mwanaume huyo kwenye monitor.
"Ooooh f****k, ni yeye" aliongea kwa sauti huku akijishika kwenye kichwa chake.

Alirudisha kumbukumbu zake nyuma siku ya jana, akiwa anaingia kwenye jengo la bunge baada ya kuwakamata wanaume wale saba, akiwa kama mwandishi wa habari ili kuweza kupata nafasi ya kuchukua habari wakati mheshimiwa raisi anahutubia nchi, kuna mtu alipishana naye tena mwanaume ambaye alikuwa kwenye koti la leza na kofia kichwani.

Kilicho mfanya mpaka akamkumbuka mwanaume huyo ni kwa sababu ile jana wake waligongana wakiwa wabapishana, mwanaume yule aligeuka kumuangalia Tina, hata yeye pia aligeuka kumuangalia na ndipo walipo kutanisha macho yao.

Hapo sasa akawa amemkumbuka vyema mtu huyo kwamba ndiye huyo ambaye alienda pale kwenye ofiri zao za MEMA YATAKUJA, akafanikiwa kuingia ndani na kuweza kuwaua wanaume saba, alishangaa mno,

"Ina maana kumbe hawa watu wapo kila sehemu? Nadhani ile kauli ya bosi itakuwa ya kweli alivyosema kwamba huenda wengine ni miongoni mwetu watu wa karibu sana" akili yake ilizidi kumwambia yaliyo mengi na kumfanya azidi kupata wasiwasi.

Akiwa kwenye huo mshtuko simu yake ilianza kuita pembeni yake, aligeuka na kuiangalia kwa umakini kwa maana hakuwa hata na mood ya kuweza kuongea na simu kwa wakati huo. Namba ilikuwa ni ngeni kwenye kioo cha zimu yake na hakuwa na kawaida ya kupokea namba ngeni kabisa kwenye simu yake.

Iliita mpaka ikakata, ikawa inaita tena lakini bado hakuipokea hiyo namba mpaka ilipokata kwa mara nyingine tena. Haikukaa sana akasikia mlio wa meseji kwenye simu yake, baada ya kuifungua alishtuka na kuiachia simu hiyo kisha akairudia tena na kuishika vizuri. Kwenye kioo cha hiyo simu palikuwa na picha ya mtu ambaye alikuwa sawa na yule mtu ambaye alikuwa kwenye kioo cha laptop yake yeye ila utofauti na yule wa kwenye simu alikuwa ametapakaa damu shingoni akiwa amefariki.

Aliipiga haraka sana ile namba, iliita kwa sekunde ishirini ndipo ikapokelewa, akaisikia sauti nzito upande wa pili. Alihema kwa nguvu baada ya kujua kwamba ni bosi wake maana mpaka wakati huo alikuwa ana wasiwasi isivyokuwa kawaida.

"Hii namba huwa naitumia kwa mambo ya mhimu, watu wangu wengi hawajui kabisa hivyo hii ndiyo tutakayokuwa tunaitumia na kama kutakuwa na mambo ya mhimu hakikisha unautumia namba hii kuniambia au kutuma taarifa"
"Bosi kwani nini kinaendelea?"
"Huyo bwana mdogo ambaye ameuwa wale watu saba amekutwa amekufa mtaani akiwa amepigwa risasi tatu kwenye shingo yake na mtu ambaye anadhaniwa kuwa mdunguaji hivyo tuneutoa kwanza mwili ili isije kuleta mtafaruko kwa wananchi"
"Kwamba wamemtuma kazi halafu wanamuua wenyewe?"
"Hivyo ndivyo watu wenye akili wanavyofanya ķazi Tina, huwa wanahakikisha hawaachi alama yoyote ile hivyo kama unafanya nao kazi hata uwe mwaminifu vipi ikifikia wakati ambao wanakuwa hawana uhitaji na wewe tena basi ni lazima wakupunguze tu"
"Kwa sasa ni kipi kinafuata bosi?"
"Unatakiwa kuwahi sana kumpata yule Mbunge. Gari yake kwa sasa inasoma kwamba ipo kwenye nyumba ya nje ya mji nadhani atakuwa yupo huko. Nakutumia address muda huu hapa uwahi haraka sana huko kabla mambo hayajaharibika mimi nitakuwa busy kuandaa msafara wa raisi hivyo tutakutana Dar es salaam ukiwa na huyo mtu" Mr Gulamu Leopard alimaliza na kuikata hiyo simu.

Tina alisali kwanza kabla ya kuanza safari ya kuelekea huko kwenye hiyo nyumba ambayo ilisemekana kwamba mbunge huyo alikuwa amejihifadhi kwa siri kwa huo muda bila kueleweka nini sababu ya yeye kujificha kwenye nyumba hiyo ambayo ilisadikika kwamba huenda alikuwa anaimiliki kwa siri pasipo kutambulika kama ilikuwa ipo chini yake.

Tina alisali kwa sababu kila dakiķa moja ilivyokuwa inaenda alikuwa anaona hatari inajisogeza mbele yake, alikuwa anaingia maeneo hatarishi sana licha ya urembo wake ambao huenda angeendelea kuupendezesha kwa vipodozi vyake ambavyo alikuwa akiviuza kwenye duka lake ambalo lilikuwa maeneo ya Mlimani City ila ndiyo hivyo tena alikuwa ameyachagua maisha hayo ya kuishi ukiwa umeishilia roho yako mkononi.
Aliendesha hiyo gari mithili ya mtu aliye na kichaa, alitakiwa kuwahi haraka sana ndani ya hilo eneo kwani hakukuonekana kuwa na usalama wa kutosha baada ya kugundua kwamba yule kijana wa mwanzo alikuwa ameuliwa. Dakika thelathini tu zilizotosha kumfikisha hiyo sehemu, alisimamisha gari umbali wa kama mita miambili na kuufunga uso wake.

Jasusi huyu Tina alikuwa makini sana na kazi yake hivyo hakuwa akihitaji kuacha ushahidi nyuma kwenye kila eneo ambalo anataka kufika au kupita. Alitembea kwa mguu mita kama miambili mpaka alipofika kwenye ile nyumba ya kisasa ambayo haikuwa hata na fensi ila ilikuwa ni nyumba ndogo iliyojengwa kisasa.
Ndani ya nyumba hiyo alisikia mziki ukiwa unapiga kwa sauti ya juu sana, hicho kikamshtua hivyo akawahi kwenye mlango ambao alikuta umefungwa kwa ndani. Kichwa chake kilikuwa kimewaka taa ya hatari hivyo akaamua kuuvunja mlango huo na buti lake ambapo aliingia nao mpaka ndani. Alichokuwa anakifikiria ndicho hicho ambacho alikutana nacho.

Sauti hiyo kubwa ya muziki haikuwekwa kwa bahati mbaya iliwekwa ili hata mtu akiwa anaomba msaada asisikike yeye zaidi ya hiyo sauti kubwa ya mziki ikiwa inapenya vyema kwenye masikioni ya msikilizaji. Mbele yake kuna mwanaume alikuwa anaishambulia shingo ya mbunge James Lewnyika na kisu mithili ya mtu aliye ibiwa mke na mwanaume huyo.
Aliisimamisha shughuli yake hiyo baada ya kuona mtu ameingia tena kwa kuvunja mlango hivyo wakawa wanaangaliana huku kila mtu akiwa anamtamani mwenzake. Tina alitoa gloves zake na kuzivaa kwenye mikono yake, wakati huo huyo mwanaume ambaye alikuwa amevaa kofia kichwani alimsogelea mrembo huyo akiwa na kisu hicho mkononi.

Mwanaume huyo alijibenua kwa teke la upande, alikuwa amemfikia Tina ambapo alijigeuza kwa sarakati huku mateke mawili yakiwa yameachiwa ambayo yalifika kwenye mbavu za Tina ambaye hata hivyo hakutetereka. Mwanaume huyo wakati anahitaji kutua chini alichotwa mtama mkali na kupigwa buti zito la kifua, alitaka kudondoka chini Tina alizunguka na double kick ambayo ilimpata mwanaume huyo kwenye kidevu na kumfanya atoe damu nyingi sana na kwenda kujibamiza kwenye dirisha ambalo alifanya lipasuke huku akidondoka chini kwa maumivu.

Tina alijigusa tumboni alikuwa na damu, ndipo alishtuka kuona ana kisu eneo hilo, mwanaume huyo baada ya kupigwa na hilo buti kali wakati anatua chini alikirusha kishu chake kwa nguvu kikalichana tumbo la mwanamke huyo ambaye aliishia kujitukana kwa kuwa mzembe.

Aliinuka na kuangalia pale dirishani aligundua mtu huyo ametokea hapo dirishani hivyo akaamua kumfuata huko. Kabla hajaruka dirishani hapo akiwa na maumivu makali ya tumbo aligundua kwamba mbunge huyo alikuwa anakoroma kwa mbali hivyo akaghairi kumfuatilia mtu yule na kumsogelea mbunge huyo ili ampe hata neno la mwisho ambalo linaweza kumsaidia.

Akiwa anasogelea kwa umakini sana hapo alipokuwa amelala mbunge huyo, alisikia mlio wa gari za polisi zikija kwa kasi sana eneo hilo.

Nini kinaenda kumkuta Tina, akina nani wanakuwa wanamuwahi kila sehemu hawa? Wanaficha nini mpaka kila anaye onekana kujua anauliwa?

Episode ya 20 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SAKATA LA UCHAGUZI-PESA KWENYE DAMU (ELECTION SAGA-MONEY IN BLOOD)
INTRO...
Miaka mingi sana iliyokuwa imepita ikiwa ni miaka miwili kabla ya uchaguzi, serikali ya nchi ya Tanzania ilipokea taarifa mbaya kutoka kwa magaidi nchini Kongo kwamba raia wa Tanzania waishio huko wametekwa na ili kuwaachia serikali ilitakiwa kupeleka madini ya kutosha.

Sababu hiyo inamuibua waziri wa ulinzi ambaye anagoma kuhusu kupeleka madini hayo, ndipo anakutana na mkuu wa majeshi na wanakubaliana kukituma kikosi cha makomando SITA ambacho kiliitwa 6.0 (SIX POINT ZERO (hiyo zero iliwekwa kwa sababu maalumu, mwanzo ilikuwa ni 7.0). Makomando hao wanafika Kongo na kufanikiwa kuwaokoa mateka wote, wakawapandisha kwenye ndege huku wao wakiwa karibu na ziwa Tanganyika kusubiri usafiri kwani walikuwa wanafuatwa kupewa msaada ili kutoweka haraka kabla hawajashtukiwa.

Lakini huko Kongo kuna mizigo ambayo waliiokoa pamoja na mateka bila kujua ni mizigo ipi, baadae walikuja kugundua kwamba ni madini.Wakiwa wanajiuliza inakuwaje wanarudi na madini tena? Ndipo wanashangazwa na kinacho tokea.

Ndege ya raia wa Tanzania inatunguliwa ikiwa angani na kulipuka yote.....makomando hao wanashangazwa sana na hilo tukio na ndipo wanashtuka kwamba huenda huko walitumwa kufanya oparesheni nyingine na sio kuokoa watu, hapo wanayakumbuka madini ambayo walisisitizwa warudi nayo na kupewa onyo kwamba wasije wakaangalia ni mzigo gani. Wakiwa kwenye mshangao wa raia wao kulipuliwa wote ndipo msaada ambao ulikuwa umewafuata unafika walipo.

Wanaume ambao waliwafuata hapo hawakuwa kwa ajili ya kuwachukua bali kuwaua. Makomando hao wanakuja kushtuka ikiwa ni TOO LATE hivyo wanapigwa risasi vibaya sana miili yao ikibaki inaelea ziwani tu. Wauaji baada ya kuhakikiki kwamba wamemaliza kazi wanayabeba madini na kutoweka kuyapeleka kwa waheshimiwa walio toa amri ya kazi. Waheshimiwa wanatoa taarifa kwamba MAKOMANDO wamelidhalilisha taifa kwani badala ya kuokoa watu wao wameenda kuua raia wote wa Tanzania kisha wametoroka na madini hivyo wanatakiwa kusakwa popote pale duniani (WANAUME WANAUZIWA MSALA)

Kwa bahati mbaya sana mtoto mmoja wa kishua alikuwa ndani ya nchi ya Kongo kufanya utalii.....anafanikiwa kuuona mwili wa mtu ukielea majini hivyo akatoa amri walinzi wake wautoe na ndipo anagundua kwamba mtu huyo kwa mbali bado anahema, anaamua kuondoka naye na kwenda kwao UGIRIKI na mwili wa huyo komando mmoja ambaye anaitumia miaka miwili kitandani na baada ya kuja kuamka MATATIZO YANAANZIA HAPA. Wakubwa wakijua waliua wote lakini kwa bahati mbaya kuna kiumbe kiliishi. UMWAGAJI WA DAMU NDANI YA TAIFA LA TANZANIA UNAANZIA HAPA bila kujali kwamba ni damu za wenye hatia au wasio na hatia, nchi inachafuka na kuna mambo mabaya sana yanakuja kutokea. Hapa ndipo tunaanza kuzifunua kurasa hizi rasmi;

Baada ya miaka kumi na miwili kupita, Tanzania inapitia kwenye kipindi cha uchaguzi ambapo vigogo watatu wanaanza kuiwania nafasi hiyo kwa udi na Uvumba, wa kwanza alikuwa ni raisi mwenyewe (Huyu hakuna mtu aliyekuwa anamjua sura yake hata wananchi ambao alikuwa anawaongoza) utakuwa unajiuliza inakuwaje raisi aliye ongoza miaka 10 wananchi hawamjui?[emoji848]RELAX, wa pili alikuwa ni wa chama kimoja na raisi ambaye alitaka kumchallenge bosi wake na kutaka atoke Ikulu kwa lazima (huyu alikuja kususiwa IKULU, na alipokuja kugundua sababu ya kususiwa IKULU! Alikuwa amechelewa (TOO LATE).

Wa tatu alikuwa ndiye kipenzi cha Watanzania...huyu wananchi wote walihitaji aingie IKULU kwani walimpenda sana lakini siku chache kabla ya uchaguzi huyu anaye pendwa sana, mwanae mdogo anatekwa. Akiwa amepaniki asubuhi anapatiwa maiti ya mwanae ikiwa haina kichwa. ANACHANGANYIKIWA sana ila kabla hajapoa vizuri jioni mwanae mkubwa wa kike naye anapotea kwenye mazingira ya kutatanisha, anapagawa na kuamua kuibeba bastola yake kisha akaondoka nyumbani.

Alihitaji kwenda kuwabana wapinzani wake kwa kuhisi kwamba ndio ambao walihusika lakini aliishia kupigwa risasi nyingi sana na kupata koma na hapo ndipo simu inapigwa mpaka kwenye ardhi ya MALIKIA. Huko alikuwa anasoma mtoto wa kiume wa mzee huyo, lengo la kumpigia ilikuwa ni kumpa taarifa na kumtaka awe karibu na familia asije kuuawa.

Lakini kurudi kwake kunaibua mambo ya kutisha nchini, alidaiwa kuwa moja kati ya watu hatari sana na alikuwa na makubaliano ya kifo na shirika la kijasusi la MI6 Kwa siri sana ambapo alidaiwa kuhusika kukitengeneza kirusi kimoja hatari sana ambacho kiliishia kwenye mikono ya magaidi ikiwa ni siri ambayo aliishi nayo yeye tu maana familia ilimjua kama mtoto wa mama na hata vyombo vya usalama hivyo ujio wake unakuwa mwanzo mpya wa Tanzania nyingine ya kutisha kwa siri sana.

Unataka kujua kwamba kuna nini humu ndani? Basi ungana nami kwenye andiko hili la SAKATA LA UCHAGUZI-PESA KWENYE DAMU.

Simulizi hii ipo yote mpaka mwisho na unaweza kuipata kwa mfumo wa softcopy kwa bei ya shilingi 5000 tu za kitanzania.

5000 yako tu unapata burudani kubwa sana ya kusoma andiko bora sana hili la kipelelezi likiwa limejikita zaidi kwenye kuichambua SIASA na mambo yake ambayo yapo ndani.

Unaweza kufanya malipo kwa namba hizi.

0621567672
0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA.

Kwenye kalamu ni mimi FEBIANI BABUYA.

Chao




Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 21.

Tina hakuwa kwenye hali nzuri ila hakutakiwa kuzubaa pale kwa maana polisi hawakuwa wakijua kuhusu uwepo wake. Mwili wa mbunge James Lewanyika ulikuwa umelala chini, kama ikitokea angekutwa pale basi moja kwa moja yeye ndiye angejulikana kwamba kahusika na mauaji ya mbunge huyo. Mlio wa polisi ulimfanya atokee njia ile ile ambayo yule mhalifu alikuwa ametokea mwanzo.

Alijongea mpaka kwenye gari yake ambayo aliiacha mita kama miambili kutoka pale na hilo ndilo lilimsaidia kwa maana sehemu hiyo ilikuwa na miti kidogo hivyo gari hiyo haikuwa ikionekana kirahisi, alifika mwenye gari na kujimwagia spirit ili kukausha damu. Aliyapata maumivu makali mno ila hakuwa na namna zaidi ya kufanya hilo ambalo lilionekana kuwa bora kwa wakati huo kisha akalioondoa gari hilo hayo maeneo wakati huo polisi wakiwa wameanza kutapakaa lile eneo.

Akiwa njiani, alimtafufa kiongozi wake kwenye simu, simu iliita na kupokelewa na bosi wake ambaye alionekana kuchukizwa.
"Tina nimekwambia tukutane usiku Dar es salaam vipi tena unanisumbua? Saivi naenda kukutana na mheshimiwa raisi"
"Mkuu kuna tatizo"
"Lipi?"
"He is dead"
"Hapana Tina, usiniambie kwamba mbunge James Lewanyika amekufa?"
"Nimechelewa kidogo sana, amekufa"
"Ooooh! God, wewe uko wapi naona unaongea kama una majeraha"
"Nipo kwenye gari, nimejeruhiwa kidogo, ila nimefanikiwa kutoka salama nadhani mhusika wa mauaji baada ya kuona amekamilisha jambo lake alipiga simu polisi mapema ili mtu atakaye kuja wakati yeye ameondoka ndiye akutwe kwenye tukio aonekane kuwa mhusika halisi wa tukio lile"
"Shiiiiit! Kuna msaada wowote wa haraka unauhitaji?"
"Hapana, nadhani ndani ya masaa machache yajayo utanikuta Dar es salaam, hili jambo tunapaswa kukaa upya chini na Calvinjr tujue ni wapi tunaenda kuanzia"
"Ok sio muda nitakuwa njiani na mheshimiwa raisi anahitaji kwenda kutoa pole yake kwa familia ya waziri mkuu hivyo baadae tutaonana. Hakikikisha unajilinda na unakuwa salama, sidhani kama kuna usalama sana na hakikisha hakuna mtu anakuhisi kwa lolote lile.
"Sawa mkuu"

Tina aliendesha gari mpaka eneo ambalo aliona ni salama kwake, alisimamisha na kuingiza mkono kwenye mkoba wake. Alitoa dawa ambayo alikunywa na nyingine akaiweka kwenye kile kidonda kisha alafunga sehemu ya kidonda na kulisafisha gari hilo ambalo alilisafisha vizuri kila sehemu kwa spray kali iliyokuwa inanukia vizuri mno ili kama kuna mtu ataigusa asije akahisi kitu chochote kisicho cha kawaida.

Gulamu Leopard, mkurugenzi huyo wa shirika la kijajusi la TBSIS baada ya kukata hiyo simu ya Tina aliwaza sana, mawazo ambayo yalimuacha njiapanda asijue ni njia gani anapaswa kuifuata kwa wakati huo. Iliwezekana vipi mtu mwingine ajue taarifa ambazo wao wanakuwa wanazifuatilia? Kwamba kuna mtu mwingine anafanya kazi kama ambayo wanaifanya? Sasa mtu huyo hizo alama za kusoma vitu hivyo anazitoa wapi kwa maana wao ndo wana kila kitu na wanatakiwa kuwa watu wa kwanza kujua mambo ya hivyo.

Alihisi kwamba kuna jambo halipo sawa, aliona wazi vijana wake walikuwa kwenye hatari kubwa sana kama wangeweza kujulikana kwamba wanaifanya hiyo kazi. Alikumbuka jinsi wale wanaume saba ambao walikamatwa na Tina walivyouliwa kirahisi sana na mtu aliyedai kwamba anatoka Ikulu, akakumbuka na jinsi mbunge James Lewanyika alivyodaiwa kuuliwa kwa mazungumzo ambayo waliyafanya watu wawili tu, yaani yeye na Tina. Sasa huyo wa tatu alitoka wapi? Vipi kama raisi akijua kwamba kuna uzembe unatokea ndani ya Ikulu ataweza kumsamehe? Kwa maana yeye ndiye anaye husika na usalama wa nchi. Hakujua kwamba ni kipi ambacho anatakiwa kukifanya kwa wakati huo.

Alijongea taratibu kuelekea kwenye chumba cha raisi kwa sababu kulikuwa na mambo mawili ambayo alitakiwa kuyafanya, jambo la kwanza alikuwa amemuahidi kwamba angempatia ripoti kuhusu wale watu saba ambao aliwakamata lakini pia alikuwa anaandaa msafara wa mheshimiwa kuweza kurudi Dar es salaam.
"Habari ya asubuhi kiongozi!"
"Kwema bwana Gulamu, nadhani upo hapa kunipa taarifa njema sana asubuhi hii" raisi huyo alijibu huku akiwa anaifunga tai yake vizuri shingoni.
"Yes, msafara upo tayari hivyo ndani ya dakika arobaini zijazo tutakuwa ndani ya Dar es salaam mkuu"
"Hizo sio taarifa njema, hizo ni taarifa za lazima, nasema taarifa njema kwa sababu unaelewa ni zipi bwana Gulamu"
"Mkuu kuna tatizo limetokea"
"Lipi?"
"Wale watu wameuawa"
"Hahahahah hahaha usiniambie kwamba leo unamfanyia utani raisi wako?"
"Hapana mkuu sitanii"
"Mr Gulamu unataka kuniambia nini labda?"
"Wale watu wote saba wamekufa, hii ndiyo habari mbaya ya asubuhi ya leo"
"Wameuliwa wakiwa wapi?"
"Kwenye kambi yetu"
"Ok nipe jina la huyo mbwa aliyefanya hivyo naenda kumhoji mwenyewe"
"Muuaji hayupo mkuu"
"Una maanisha nini kusema muuaji hayupo"
"Hakukamatwa"
"Sijakuelewa bado, yaani umeniambia kwamba mauaji yalifanyikia kambini kwenu, halafu tena unaniambia kwamba muuaji hajakamatwa? Unataka kuniaminisha nini?" Raisi huyo aliongea kwa ukali sana akiona kama kijana wake huyo hakuwa siriasi na alichokuwa anakisema.
"Mtu huyo alitekeleza hilo tukio na kufanikiwa kuondoka"
"Yaani mtu aingie ndani ya kambi kubwa ya kijasusi kama ile, atekeleze mauaji halafu aondoke"
"Ndiyo mkuu"
"Hahahaha nadhani ninapaswa kuwapa masaa ishirini na manne mniletee hoja za kueleweka hapa vinginevyo kati yenu wote hakuna ambaye ataendelea kuwa na kazi tena" raisi Theobald Mnyika aliongea kwa hasira sana akiwa anamuangalia mtu huyo machoni, aliona kama vile anafanya utani na kile alichokuwa anakisema.
"Mimi nipo tayari kuipokea adhabu yotote ile kutoka kwako kwa sababu wewe ndiye mkubwa wa nchi hii ila kuna jambo ambalo unapaswa ulifahamu kabla ya kunihukumu mimi na vijana wangu"
"Nina dakika mbili za kukusikiliza" kauli ya raisi ilimfanya Mr Gulamu kutoa simu kwenye mfuko wake na kuifungua picha moja kwenye simu hiyo, akaielekeza kwa raisi
"Huyu ndiye kijana ambaye ametekeleza hilo tukio ila hajaingia kwa uzembe wetu kama ulivyo fikria hapo mwanzo. Mtu huyu ameenda pale akiwa na kitambulisho halisi cha Ikulu na kusema kwamba yeye ni mtu wa Ikulu, na utaratibu uliopo ndani ya nchi hii mtu ambaye akithibitishwa kwamba ni wa Ikulu haruhusiwi kukaguliwa wala kuhisiwa vibaya kwenye jambo lolote lile itakuwa ni ukosefu wa nidhamu kwani mtu wa Ikulu anakuwa anasimama mwa niaba yako"

"Sasa huyo alienda kwa vijana wangu akawaambia kwamba wewe ndiye uliyekuwa umemuagiza kule aweze kuongea na wale wafungwa na maagizo yako yalitakiwa kuwa ya siri hivyo kamera za kwenye kile chumba zilizimwa" maelezo ya Mr Gulamu yalimuacha kidogo raisi kwenye hali ya upole, alitakiwa kutulia.
"Nakuamini vipi kwa hayo unayo yaongea?" Mr Gulamu hakujibu neno lolote lile zaidi ya kuitafuta video kwenye simu hiyo ambayo ilikuwa inamuonyesha kijana huyo tangu anaanza kuingia humo ndani mpaka anaondoka, alijikuta anachoka.
"Pumbavu ina maana kuna watu humu ndani ya Ikulu wananisaliti mimi?"
"Ndiyo mkuu hivyo unapaswa kuwa makini na watu unao waajiri. Kijana huyo jina lake alikuwa anaitwa Innocent Mdimbu, ni kijana ambaye alifuzu mafunzo ya hali ya juu sana ya kikomando huko morogoro ambapo aliingizwa ndani ya jeshi la nchi alikofanya kazi kwa miaka mitano. Huko alifanya kazi za hatari kama kuwakomboa wanafunzi waliokuwa wametekwa na Al-shabab, amewahi kwenda kwenye oparesheni ya kuwaondoa m-23, lakini pia alikuwepo kwenye kikosi maalumu kilicho enda kutoa msaada kule nchini Kongo."

"Baada ya kurudi tuliona anatufaa sana kuingizwa huku kwetu kwani hakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu wala utovu wa nidhamu, kazi yake ameifanya kwa weledi na uaminifu mkubwa mpaka jana alipofanya jambo la kijinga kama hilo" Mr Gulamu alimuelezea kijana huyo ambaye bila shaka alikuwa amezichimba habari zake vya kutosha.
"Nahitaji huyo kijana atafutwe haraka sana"
"Hawezi kupatikana mkuu"
"Unamaanisha nini?"
"Amekufa"
"Whaaaat!"
"Baada ya kukamilisha hiyo kazi tu, aliuawa muda mchache baada ya kukamilisha hiyo kazi yake na watu ambao walionekana kuhitaji kuilinda siri hiyo. Ila usijali bosi muda sio mrefu wahusika watakamatwa" Mr Gulamu alitoa maelezo ambayo yalimfanya raisi amuangalie sana.
"Ni vyema niipate hiyo habari ya kumamatwa kwao haraka sana" mheshimiwa alitamka akiwa anatoka ili kwenda ulikokuwa usafiri ili warudi Dar es salaam.

Episode ya 21 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 22.
Calvinjr alikuwa amefika ndani ya jiji la Dar tayari, alikuwa anajiandaa kwenda kukutana na Sarafina William, mtoto wa marehemu waziri mkuu William Msoka. Akiwa njiani kuelekea huko kwa mwanamke huyo, alipokea simu kutoka kwa dada yake, alitabasamu kwa maana alimjua dada yake alivyokuwa, angeanza kumsuta kwanza.
"Nakusikiliza bosi wa mama" Calvinjr aliongea huku akiwa makini kwenye usukani
"Uko wapi Calvinjr?" Sauti ya dada yake ilikuwa ni tofauti na alivyokuwa ameizoea
"Nipo Dar, una tatizo gani sis?"
"Mhhhh mambo naona yamekuwa magumu sana, kila hatua tunayo ipiga kuna watu wanatutangulia hatua moja mbele"
"Unamaanisha nini?"
"Kuna watu ambao mimi niliwakamata ambao moja kwa moja walikuwa wanahusika na lile tukio lakini kitu cha ajabu ni kwamba waliuliwa ndani ya kambi na mtu ambaye alidai anatoka Ikulu kisha naye akauliwa baada ya muda mfupi tu. Lakini cha ajabu mtu mwingine aliyekuwa rafiki wa mbunge Isaya Ndango ambaye alitoroka kwenye lile tukio la jengo kabla ya kulipuka ameuawa"

"Baada ya kufuatilia kwa umakini sana nilijua yule kuna mambo ambayo anayajua kutoka kwenye lile tukio hivyo kumpata yeye ingekuwa ni njia nzuri sana kumtumia yeye huenda angetupeleka kwa mhusika ila cha ajabu wakati naenda kumchukua nimekutana na mtu ambaye alikuwa ameshamchoma choma vibaya sana kiasi kwamba hajachukua muda akawa amekufa. Nimejaribu kumkamata mtu yule ila nimeshindwa akawa amenikimbia" dada yake alihema kwa nguvu baada ya kumuelezea mdogo wake hofu yake ilipokuwa.

"Upo salama sis?"
"Yeah"
"Acha kunidanganya, mimi nakujua wewe kuliko unavyo fikiria, nambie kuna nini kimetokea?"
"Nimepata jeraha dogo tumboni"
"Oooooh f****k, unaweza ukanitajia jina la huyo mpuuzi ambaye amethubutu kumgusa dada yangu?" Aliongea kwa hasira akiwa anabamiza mikono yake kwenye usukani, walizaliwa wawili tu pekee hivyo roho yake yote ilikuwa kwa huyo dada yake hivyo alishangaa sana kuona kuna mtu eti anamjeruhi mwanamke huyo kirahisi sana namna hiyo? Alijawa na hasira sana akasahau kwamba huyo mwanamke alikuwa kwenye kazi ambayo ingeweza hata kuyachukua maisha yake.
"Hey Calvin, nimeumia kidogo tu usijali"
"Sis shida yako wewe ni mbishi sana, nilikwambia kabisa hiyo kazi mimi ndiye nilitakiwa kwenda ukawa unang'ang'ania, kumbuka mimi sina mtu mwingine wa kumuita dad......"

"Hey Calvinjr dada yako anakupenda sana bye" dada mtu aliona lawama zimezidi akaamua kuikata simu yake, Calvinjr alichukia sana ila hakuwa na namna akaamua kumezea ila baadae angeweza kuongea na dada yake huyo.

Alifanikiwa kufika nyumbani kwa waziri mkuu ambapo baada ya kufuata taratibu zote aliweza kupelekwa kwenye chumba ambacho alikuwepo mtoto huyo wa pekee wa waziri mkuu ambaye ndiye alikuwa mkandarasi mkuu wa nchi ya Tanzania. Alifurahi sana kumuona mwanaume huyo ndani ya hicho chumba alichokuwa amewaagiza wasaidizi wake watoke baada ya kusikia kwamba alikuwa na mgeni.

Sara akimkimbilia Calvin na kumkumbatia kwa nguvu huku akimwaga chozi kwenye kifua cha mwanaume huyo. Alideka kadri ya uwezo wake ulipokuwa unaishia mpaka zilipo pita dakika tano ndipo alipo jinasua kifuani hapo akiwa na tabasamu tele kwa maana alijihisi amani sana.

"Zawadi zangu ziko wapi?" Ndilo lilikuwa swali la kwanza Kwenda kwa Calvin. Mwanaume hakuwa na mambo mengi aliingiza mkono kwenye mfuko wa koti jepesi lililokuwa kwenye mwili wake, akatoa ua zuri sana akamkabidhi mwanamke huyo. Sara akiwa kwenye furaha ya kulipokea ua hilo ambalo lilikuwa linanukia sana, Calvinjr alijipapasa kwenye kifua chake na kutoa kitabu.
Alijua kwamba mwanamke huyo anapenda sana kusoma vitabu hivyo alimletea zawadi ya kitabu ambacho jalada lake la nje lilikuwa na picha ya mwanaume mmoja ambaye mwili wake ulikuwa umefungwa kwa minyororo huku kikiwa kimeandikwa GEREZA LA HAZWA, kilichokuwa kimeandikwa na mwandishi FEBIANI BABUYA.

Sarafina akiwa anakishangaa kitabu hicho cha kijasusi kilicho mpa hamu ya kutaka kujua kwamba hilo gereza lilikuwa na nini, Calvinjr alimpa ishara ya kutulia na hapo akaingiza tena mkono kwenye mfuko wake na kutoa kibox ambacho alitaka Sara akifungue. Mwanamke huyo alikifungua akiwa anatamani kujua kwamba kilikuwa na nini ndani, ndani yake kulikuwa na saa ya gharama sana iliyokuwa ni dhahabu tupu, Sara alibaki ameufumba mdomo wake kwa msisimko mkali aliokuwa ameupata.

Calvinjr aliichukua saa hiyo na kumvalisha mwanamke huyo kwenye mkono wake, saa ilimpendeza sana kwenye mkono wake wakaishia kukumbatiana na kuangaliana kwa mahaba isivyokuwa kawaida.
"Asante sana Calvinjr sikutegemea kama ninaweza kuwa na umuhimu mkubwa sana kwako kiasi hiki mpaka nikastahili zawadi bora kama hizi"
"Huenda unastahili zaidi ya hizi maana hata wewe ulinijali sana kunisaidia kuupata mkataba ambao sikuwahi kufikiria kama ninaweza kuupata kwenye maisha yangu hivyo wewe ndiye unayestahili sifa na kila kitu"
"Hahahah kumbe bado haujasahau tu"

"Siwezi kusahau hata kidogo, samahani lakini hivi ni kitu gani ambacho kilikufanya uone kwamba mimi nafaa kuupata mkataba kama ule?" Calvinjr aliuliza kwa maana mkataba ambao alikuwa amepewa ni mkataba ambao hata baadhi ya vigogo serikalini walikuwa wanautolea macho hivyo alishangaa sana kwanini iwe yeye? Sara alisogea kitandani na kukaa akionekana kuwa na mawazo ya mbali sana.

"Vipi Calvinjr ulishawahi kufanya kitu au kuwa tayari kufanya jambo lolote hata kama lina madhara kwako ili kumpa furaha mtu fulani" swali lake ni kama lilikuwa nje ya maada ila mwanaume aliamua kulijibu ili aone kwamba lengo kuu la swali hasa lilikuwa ni nini.

"Yes niliwahi na nipo tayari hata kesho kufanya. Unajua kwenye maisha yangu mimi nina watu wawili tu ambao ndio familia yangu. Nawapenda sana watu hao, sipo tayari kuona wanapata matatizo nikiwa hai na ndio hao nipo tayari kufanya lolote kwa ajili yao hata kama jambo hilo litakuwa na madhara makubwa kwangu na kwenye maisha yangu. Nao ni mama na dada yangu"

"Haujawahi kuwaza kuongeza mtu wa tatu kwenye familia yako ambaye pia utakuwa tayari kufanya kama hivyo unavyoweza kufanya kwa mama na dada yako?"
"Unamaanisha nini kusema hivyo?"
"Namaanisha haujawahi kuwaza familia labda, kuwa na mke na mtoto?"
"Oooohps! yes, nimewahi kuwaza ila naamini kwamba jambo hilo litakuja kwa muda mwafaka utakapofika"
"Unahisi muda mwafaka kwako ni upi usipo utengeneza wewe mwenyewe?"
"Sijakuelewa unamaanisha nini?"

"Mimi nilifanya nilicho kifanya nikijua nafanya kitu sahihi kwa kitu ninacho kipenda sana kwenye maisha yangu, hivyo nikawa tayari kwa matokeo yoyote yale" Calvinjr alielewa kile alichokuwa anamaanisha mwanamke huyo ila hakuwa tayari kuzungumzia hayo mambo kwa huo muda hivyo ilimbidi kubadili maada haraka sana.

"Mrs William kwanini ulikuwa umenificha kwa kipindi chote hiki kwamba wewe ni mtoto wa mheshimiwa?"
"Hilo jambo limekuudhi sana?"
"Hapana nimeuliza tu kwa maana huenda kuna heshima zaidi ya hii nilitakiwa kukupatia"
"Kwahiyo watoto wa viongozi ndio ambao wanapaswa kupewa heshima ya kipekee?"
"Hapana sijamaanisha huko"
"Nisikilize Calvinjr, mimi niliamua kuishi maisha yangu mbali na siasa tangu nikiwa mdogo sana. Niliwahi kumwambia baba yangu kwamba kama ananipenda na anahitaji nimheshimu sana aniweke nje na siasa kabisa na bahati nzuri alikubali hilo jambo. Nilifanya hivyo kwa sababu nilikuwa nasoma stori za siasa, nilikuwa naangalia movie za siasa, nikaona kwamba siasa ni mchezo ambao una mengi sana mabaya, una mambo ya kutisha ambayo yanakufanya kutokuwa na uhakika na maisha yako"

"Siasa ina mambo ambayo hayakubakishi kuwa msafi mbele ya watu hivyo nikaamua kujitengenezea mfumo wangu mwenyewe wa maisha ambao niliona unafaa kuuishi. Nimezaliwa kwenye familia ya siasa ila nimeishi nje kabisa ya siasa na sielewi lolote na sijawahi kutaka kujifunza kabisa. Moja ya madhara ambayo niliwahi kuyaona kwenye siasa ndiyo kama haya ambayo yamemkuta baba yangu kwa sasa"

"Naweza kusema kwamba baba yangu ni moja ya wale baba bora zaidi hapa duniani ila hawezi kunisikiliza tena nikaongea nae lolote, hakunipa hata nafasi ya kutaka nimuage mwanae wa pekee kwa maana alijua siipendi kabisa siasa. Natamani sana ningemjua aliye husika aweze kupata adhabu ambayo anastahili ila huo uwezo mimi sina kwahiyo nitayaacha mambo yakae kama yalivyo"

"Baba yangu kwa sababu alishindwa kabisa kutumia nafasi yake kuninufaisha mimi kitu pekee ambacho yeye alikifanya ni kuacha mimi nifanye kile ambacho nakipenda, na baada ya kumaliza masomo yangu tu ndipo akanitafutia hii nafasi ambayo imeweza kukusaidia hata wewe kuweza kutimiza moja ya ndoto zako. Hakikisha unayafanyia kazi yote ambayo yapo kwenye mkataba haraka sana kwa maana najua kwa sasa nitapata upinzani mkali sana kwa watu ambao watahitaji niondoke kwenye hii nafasi kwa vile sina mtu wa kunilinda tena naweza nisiwe na uwezo wa kuendelea kuwa na nguvu ya kuulinda mkataba wako" mwanamke huyo aliongea kwa uchungu sana. Calvinjr akiwa anajiandaa kumjibu, walisikia mlango huo unagongwa, mfanyakazi wa Sara alitoa maelekezo kwamba anahitajika kwani mheshimiwa raisi alikuwa amefika hapo kutoa pole zake.

Sehemu ya 22 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 23.
Hakukuwa na kingine zaidi ya Sara na Calvinjr kupeana ishara ili kuelekea sebuleni ambako mheshimiwa raisi alikuwa amefika tayari. Walitoka moja kwa moja na kuelekea ambapo Calvinjr alishangaa anamuona bosi wake Gulamu Leopard akiwa na mheshimiwa raisi, alikuwa hajategemea kama atakuwa hapo muda huo ila ilitakiwa wakaushe kama hawajuani kabisa kwani hakuna mtu ambaye alikuwa anajua kwamba hao watu wanajuana.

"Heshima yako kiongozi" Calvinjr alimsalimia mheshimiwa raisi ilivyofika zamu yake, huku raisi huyo aliupokea mkono wa kijana huyo na kumuangalia kwa umakini Sara, alitabasamu sana mheshimiwa raisi.

"Mpywa wangu hata kuniambia umepata mchumba kweli? Hahahahha sema umejua kuchagua bana, ni kijana ambaye bila shaka atakuwa mume bora sana kwako ila nahitaji kuongea naye baada ya hapa niweze kumjua kiundani ili nijue kama upo kwenye mikono salama au natakiwa kuwa makini" mheshimiwa raisi aliongea akiwa anamuangalia Calvinjr kwa umakini mkubwa. Ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kuweza kukutana na kijana huyo hivyo hakuwa na taarifa zake zozote zile.

Maneno yake yalileta mshangao mkubwa kwa kila mtu humo ndani, ila ingekuwa ni kumkosea heshima kama wangeanza kubisha humo ndani ionekane mheshimiwa raisi ameropoka hovyo hivyo iliwalazimu kukubali kila kitu huku Calvinjr na Sarah wakiangaliana kwa mshangazo Calvinjr akiwa na macho ya kuuliza ni nini kile ila kwa Sara alionekana kufurahia sana hali hiyo.

Calvin aliangaliana na bosi wake, walikonyezana tu na kukaushiana kama vile hawakuwahi kuonana sehemu yoyoye ila wala kujuana kabisa. Mheshimiwa raisi alitoa pole zake kwenye ile familia ambayo alidai ilikuwa ni moja ya familia yake hivyo kama wangekuwa wanahitaji chochote walitakiwa kumuona haraka sana, alidai kwamba waziri mkuu alikuwa ni mtu wa mhimu sana kwake ila alipo maliza alihitaji kufanya mazungumzo na Calvin ikiwa ni kama kuhakikisha kwamba mtoto wa rafiki yake yupo kwenye mikono salama au kapuyanga.

"Enhe kijana wangu, jisikie huru. Hapa siongea tu kama raisi wa nchi ila nataka tuongee kama mtoto na mzazi wake, naweza kukujua kwa majina"
"Naitwa Calvinjr"
"Hilo tu ndilo jina lako?"
"Ndiyo mheshimiwa mimi ndivyo huwa naitwa hivyo japo ukitaka kuniita na ukoo wangu huwa natumia wa mama"
"Hapo sasa nimekuelewa, unaweza ukaniambia kwamba kwanini hautumii ukoo wa baba yako?"
"Baba yangu alimtelekeza mama sisi tukiwa wadogo sana, hali iliyo pelekea mama kutulea kwa shida mno hivyo tangu nimekua sijawahi kuhitaji tena kufuatilia historia ya mtu yule" mwanaume alidanganya.
"Aah pole sana, hiyo itakuwa mbaya sana kukukumbushia maisha ambayo ulitakiwa kuyasahau huko nyuma"
"Hata usijali mkuu nimeshazoea hivyo naona kawaida tu"
"Unaweza ukaniambia unajishughulisha na nini?"
"Ninamiliki kampuni yangu inayo jihusisha na mambo ya ujenzi"
"Oooh waoooo, kumbe kijana mdogo una maono makubwa kabisa, unaweza kunitajia jina la kampuni yako"
"Ndiyo mheshimiwa inaitwa Cal-Tina investment"
"Safi nadhani nitavutiwa zaidi kuijua kiundani hiyo kampuni yako ili niweze kujua ni kwa namna gani naweza kukusaidia kwa maana kwa sasa upo na mpwa wangu huyu"
"Nitashukuru sana mheshimiwa kama ikitokea siku hata moja ukifika kwenye kampuni yangu kwani itakuwa heshima ya kipekee sana"
"Kuhusu hilo usijali lazima nitafika, nataka nihakikishe mtoto wa rafiki yangu anakuwa kwenye mazingira yaliyo bora. Ila unaweza ukaniambia kwamba ni kwa namna gani uliweza kukutana na Sara"
"Ndiyo mkuu, mimi na yeye tumejuana kwenye uwanja wa biashara ambapo kuna biashara iliwahi kutukutanisha pamoja tukajikuta tunakuwa karibu zaidi. Siku zilivyozidi kwenda tukajua kwamba wote tulikuwa vijana wenye maono yanayo endana, tukawa tunakutana na kubadilisha mambo mengi sana mpaka pale tulipo gundua kwamba kila mtu alikuwa na upendo usio elezeka kwa mwenzake hivyo tukaziweka hisia zetu wazi na ndio ulikuwa mwanzo wa mapenzi yetu"

"Stori yenu nimeipenda inavutia sana kwa sababu mlikutana kwenye eneo ambalo ni mhimu sana kwenye maisha yenu, unakumbuka ni muda gani tangu mkutane?"
"Ni mwaka mmoja uliopita"
"Kuna kitu chochote ambacho sio cha kawaida umekigundua kwa Sara kwa muda ambao umekuwa naye kwenye mahusiano labda"
"Hapana mkuu hakuna kitu kibaya labda tu nilishtuka baada ya jana kugundua kwamba ni mtoto wa waziri mkuu"
"Oooh kumbe hakuwahi kukwambia?"
"Ndiyo"
"Basi nadhani alikuwa anataka kupata mtu sahihi ambaye atampenda bila kujua nafasi kubwa aliyokuwa nayo"
"Nadhani ni hivyo mheshimiwa"
"Nakuelewa kijana wangu ila hakikisha hauji kumuumiza binti huyo kwani utakuwa umenunua ugomvi na mimi. Hana mtu wa kumpa furaha kwa sasa kwa sababu hata mama yake anahitaji furaha hivyo huenda wewe ndiye ukawa furaha yake, kwa maana hiyo hautakiwi kufanya jambo la kijinga lolote lile. Hicho ndicho kitu ambacho naweza kukifanya kwa sasa kuilinda familia hii" raisi huyo alimaliza kuongea kwenye chumba ambacho walikuwa na mazungumzo yao wawili tu kisha akaanza kutoka ila aligeuka na kumuangalia Calvinjr.

"Jiandaeni siku yoyote naweza nikawaalika Ikulu na itanipendeza zaidi kama utamvisha mwanamke huyo Pete mbele yangu. Hiyo itakuwa ni zawadi bora kwa raisi wa nchi yako" Calvinjr aliitikia kwa kichw kukubali hilo jambo huku akiona kabisa kabanwa mbavuni na hakuona sehemu ya kuchomokea. Baada ya kuhakikisha watu hao wameondoka alimfuata Sara ili waongee, tofauti na alivyokuwa anafikiria yeye alimkuta Sara akiwa mwenye furaha sana.

"Unatakiwa kuongea na mheshimiwa raisi kuhusu hili Sara, nahisi ameelewa vibaya"
"Unamaanisha nini kusema ameelewa vibaya?"
"Ameniuliza mambo mengi sana kuhusu mimi na wewe tulivyokutana mpaka tukawa wapenzi, nimemsimulia kwamba tulikutana kwenye biashara ndipo tukapendana kwa sababu sikujua kama atafika mbali. Kitu cha ajabu anataka mimi nikakuvalishe Pete ya uchumba Ikulu bila kujua kwamba sisi hatuna mahusiano yoyote" Calvinjr aliongea kwa wasiwasi maana halikuwa jambo zuri sana kusema uongo mbele ya raisi. Maneno hayo yalimfanya Sara meno yake yote thelathini na mawili kuonekana vyema kwenye kinywa chake.

"Na unataka mimi nikakwambiaje ili kubadili hilo?"
"Kamwambie kwamba mimi nakupenda sana ila wewe moyo wako upo kwa mtu mwingine ili asije akaona kama mimi nilimdanganya vile bali inatakiwa aamini kwamba mimi nilijua kwamba tupo kwenye mapenzi ila kwa wewe haukuwa kabisa na hizo hisia. Naomba mpigie simu umwambie saivi please" Calvinjr alikuwa anaongea akihitaji hilo jambo lifanyike haraka sana lakini ilikuwa ni tofauti sana kwa Sara.
"Whaaaat!? Calvinjr unasemaje? Kwanini unataka mimi nimwambie sikupendi?"
"Kwa sababu hatujawahi kuwa wapenzi Sara, sisi ni marafiki tu tena kibiashara huoni kama itakuawa ni hatari sana kwangu kama mheshimiwa akigundua kwamba nimemdanganya?"
"Unamaanisha nini kusema hatujawahi kupendana Calvinjr?"
"Whaaaat!"
"Vipi kama mimi nakupenda?"
"Sara sipo kwenye utani, namaanisha hili jambo ambalo nakwambia hapa"
"Hiyo ndiyo sababu haujali hisia zangu Calvinjr? Kila muda unaona kwamba tupo kwenye utani? Kila alicho kifanya mheshimiwa raisi imekuwa kama tiba ya majeraha ya moyo wangu. Mimi nipo tayari kutangazwa hadharani, mimi nipo tayari kwenda Ikulu na kupiga magoti mbele yako ukinivalisha pete...."mwanamke huyo akiwa anaelezea kwa hisia sana alitaka kuendelea lakini calvin alimstopisha
"Unataka kufanya hayo yote kwa sababu ili?"
"Kwa sababu nakupenda Calvinjr"
"Ooooh shiit!" Mwanaume alitamka kwa mshangao mkubwa, hakuwahi kujua wala kufikiria kwamba kumbe muda wote huo mwanamke huyo alikuwa akimpenda sana.
"Kwa muda gani umekuwa hivi Sara?"
"Ni Kwa muda mrefu sana Calvin, nimekupenda tangu tumejuana kwenye ule mradi wa ujenzi wa barabara kule kibaha mwaka jana. Nilifanya kila namna ya kuwa karibu na wewe, nilifanikiwa ila haukunipa nafasi ya kuweza kuonyesha mapenzi yangu kwako, kila muda ulidai kwamba wewe ni mtu ambaye ulikuwa busy na kazi nikawa sina la kufanya"
"Hata ule mkataba ambao umeupata, imekuwa ni ngumu sana kuutoa kwenye kampuni ya kawaida kama ile yako ukifananisha na makampuni makubwa ambayo yalikuwa yanauhitaji mkataba ule ila nilikubali kupigana kwa ajili ya mtu ambaye ninampenda mpaka nikahakikisha ule mkataba unakuwa kwenye mikono yako kwa gharama yoyote ile na kile ndicho kitu pekee ambacho niliona ninaweza kukifanya kwenye maisha yako kama msaada kutoka kwangu."

Calvinjr alichoka, kumbe mwanamke huyo kumpigania kote kule ili amsaidie ilikuwa ni kulipigania penzi lake na kumpigania yule ambaye alikuwa akimpenda sana. Zile tungo rasmi za kuhalalisha nini maana ya upendo leo zilikuwa zinasikika masikioni mwa Calvinjr kutoka kwa mrembo huyo aliye amua kujitosa na kuweka wazi kile ambacho kilikuwa kinausumbua moyo wake hakutaka kufa na maradhi ingali dawa ya maradhi hayo alikuwa akiiona mbele yake, ungekuwa uzembe mkubwa sana kwenye maisha yake.
Sasa aliyekuwa anasubiriwa kutoa tamko, alikuwa ni mtoto wa kiume ambapo hata kama angesema suu tu mwanamke huyo alikuwa tayari hata kuogelea baharini.

Episode ya 23 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 24.
Majira ya usiku kwenye moja ya chumba ambacho kilikuwa kimefunikwa na kiza lakini ndani yake palikuwa na taa ya mafuta ya taa ambayo iliwekwa mezani ili wahusika waweze kuona kile ambacho kilikuwa hapo katikati ya meza. Walikuwa watu watatu humo dani ambapo mwanga wa taa hiyo ulisaidia kuzimulika sura zao kwa mbali na kuwafanya watambulike.

Gulamu Leopard, pamoja na majasusi wake wawili yaani Calvinjr pamoja na Valentina waweza kumuita Tina ambao walikuwa wanafanya kazi kama undercover ndio ambao walikuwepo humo ndani. Baada ya safari zao za DOGMA TULIPO pamoja na huko lindi ndani ya jimbo la DAMU INAYO ISHI, sasa walikutana ili kuweza kujadili mwafaka wa yale ambayo waliyapata huko walikokuwa.

"Unaliwekaje suala lako kwa mheshimiwa raisi?" Mkurugenzi alimuuliza kuhusu suala lake na mrembo Sara.
"Mpaka sasa sielewi nafanyaje kwa maana mwanamke mwenyewe nimejaribu kumwambia aongee na mheshimiwa na kujaribu kumwambia kwamba hanipendi mimi ila kagoma"
"Sasa kulikuwa kuna haja gani ya wewe kumwambia aongee na raisi wakati haya mengine mnaweza kuyamaliza wenyewe"
"Raisi anataka nikamveshe Sara Pete ikulu?"
"Whaaat!"
"Hahahaha kaka usiniambie yule mwanamke ameshakuwa WiFi yangu" dada yake yeye alionekana kufurahia jambo hilo
"Sisiter unaweza kutulia tafadhali ujue jambo hilo sio la utani kama unavyo fikiria wewe"
"Hakuna ubaya ni mwanamke mrembo yule hata mama atampenda tu"
"Tina" ilimlazimu mkurugenzi kuingilia kati kwa maana aliwajua ndugu hao wakianza kubishana hapo kila mtu angetaka kuwa mshindi.
"Kwahiyo Sara kasemaje?"
"Anadai kwamba ananipenda mkuu"
"Ooooh MUNGU wangu, na wewe umemjibu nini?"
"Mkuu nadhani tuachane na hilo jambo nitajua namna ya kulimaliza mwenyewe" alimaliza kuongea huku dada yake akiwa anamkonyeza na kucheka. Basi iliwalazimu kila mtu kuweka mezani kile ambacho alikikusanya huko alikotoka ili waweze kueleweshana kwa pamoja.

"Hili jambo haliwezekani, kivipi mtu awe anajua kila hatua ambayo mnakuwa mnaipiga? Kwani haya mambo mlikuwa mnawashirikisha watu wangapi?" Calvin aliwauliza baada ya kupewa stori ya huko DOGMA TULIPO.
"Hili jambo unalijua wewe, mimi, Tina na mheshimiwa raisi tu"
"Hapana mkuu sio rahisi namna hiyo, hakuna mtu yeyote mwingine mwenye hizi taarifa mbali na sisi wanne ulio tutaja kwenye tukio lolote kati ya hayo ambayo yametokea huko?"
"Mhhhhh, nadhani lile la kutekwa kwa wale watu saba, niliwashirikisha wale vijana wa kule DOGMA TULIPO ambao ndio walienda kuwachukua kule"
"Unawaamini hao vijana?"
"Siwezi kuwajibia kwa sababu walishakula kiapo cha kulinda siri za taasisi"
"Sawa hilo tuliwekee kiulizo kuhusu hiyo sehemu, haya sasa mnaweza kuniambia ni vitu gani ambavyo mlivitpata humo ndani ukiacha kuwakamata hao watu na rimoti?" Sasa hapo ilikuwa ni zamu ya Tina kuweza kutolea ufafanuzi wa kila ambacho alihisi anakijua.

"Kama nilivyo elezea mwanzo, maneno ambayo niliyakuta ubaoni yalikuwa yanaeleweka sana ila yale maneno ambayo yalikuwa kwenye kikaratasi nilicho mkuta nacho mfukoni yule mwanaume sikuyaelewa. Maneno yenyewe ni haya hapa" Tina alitoa ufafanuzi huku akiwa anakiweka kikaratasi chenye hayo maneno ambayo waliamini kwamba huenda Calvinjr atakuwa na uwezo wa kuyatolea tafsiri.

"THE BLUE OPERATION REACHING RWANDA. TEN IMAGINARY LIFETIME. ACCOMPLISHED" Calvinjr alitabasamu baada ya kuyaona hayo maneno
"Aliyekaa chini akauandaa huu mpango hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo alilifanya" maneno yake yaliwafanya Tina na bosi wake wamshangae maana kwake hilo lilionekana kuwa jambo dogo kuliko walivyokuwa wanafikiria.
"Kwamba inamaanisha nini?"
"Kwanza kitu ambacho mnatakiwa kuelewa hapa ni kwamba hii karatasi imeandikwa na watu wawili tofauti kama ukiiangalia kwa umakini japo mtu wa pili alijitahidi sana kukopi mwandiko wa mtu wa kwanza. Ukitaka kuamini kwamba imeandikwa na watu wawili ni kwenye maana zake"

"THE BLUE OPERATION REACHING RWANDA. Ndiyo maneno ambayo yaliandikwa na mtu wa kwanza ambaye bila shaka ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango mzima ambao umefanyika na maneno ya pili yalitakiwa kukamilishwa na mtu ambaye ndiye aliutekeleza huu mpango. Hiyo BLUE inamanisha kwamba tukio lilipangwa kufanyika asubuhi. Asubuhi ndio muda ambao mara nyingi wingu linakuwa la blue hivyo moja kwa moja ndilo lilikoluwa lengo lao na ukiangalia tukio lilifanyika asubuhi bila kujali muda ulikuwa ni saa ngapi"

"OPERATION REACHING RWANDA. Ilikuwa na maana ya kwamba watu hawa wakikamilisha huo mpango wao basi wanaenda huko nchini Rwanda nadhani kwa ajili ya kujiweka mbali kabisa na hatia ya kuhusika na hili tukio, hivyo bila shaka kuna asilimia nyingi sana wahusika wanaelekea ndani ya nchi ya Rwanda."

"Sasa tukija kwenye sentensi ambayo nimesema kwamba hii ilikamilishwa na mtu wa pili aliyekamilisha tukio. TEN IMAGINARY LIFETIME. ACCOMPLISHED. Alijaribu sana kuuficha ila alikuwa anamaanisha kuwafahamisha watu kumi wa kufukirika kwenye haya maisha kwamba mpango umekamilika. Hivyo alikuwa anajibu ni ujumbe wa kwanza kama kuwapa taarifa hiyo kwamba wanaweza kuelekea huko Rwanda kwa maana mpango umekamilika"

"Kwa maana hiyo ni kwamba huenda hao watu kumi ndio viongozi wake?"
"Yes, hilo ndilo jibu sahihi"
"Daaah watu wanatumia akili sana kukamilisha mambo yao" Tina aliwasifia wahusika wa huo mpango.
"Huwezi kupanga mipango mikubwa kiasi hiki kama hauna watu wenye uwezo mkubwa sana kichwani utaishia kudhalilika. Hawa kitu cha kwanza walihakikisha wanatupoteza kabisa sisi kuhusu viashiria ambavyo vinaweza kutupa muongozo, wapo makini sana kwa kila hatu ambayo wanaipiga, hawataki kupoteza pointi hata moja hivyo sisi tunapaswa kuwalazimisha kupoteza pointi yao moja"
"Ndiyo mkuu, sisi kazi yetu kubwa sana kuifanya inatakiwa tumjue mtu mmoja tu kati yao basi mchezo wote utakuwa umeishia hapo"
"Calvinjr are you sure?"
"Ndiyo mkuu na mtu huyu nadhani haitakiwi tumpatie Tanzania"
"Kivipi"
"Kama lengo lao kubwa lilikuwa ni kwenda Rwanda, basi huko lazima tayari wana mazingira ya kufikia na kufanyia mambo yao, sisi inatakiwa tuwafikie huko waliko"
"Unadhani tunawafikiaje kirahisi watu ambao hata hatuwajui?"
"Hapa ndipo tunatakiwa kukaa mezani na kupanga nini cha kukifanya sasa"
"Unataka kuniambia kwamba una mpango mwingine mpya?"
"Ndiyo mkuu"
"Upi huo?"
"Si umesema kwamba kila mtu ambaye anahusika na hili suala wanamtafuta na kumuua kama walivyofanya kwa mke wa Isaya Ndango pamoja na Mbunge James Lewanyika?"
"Ndiyo, sasa hiyo inahusika vipi na mpango wetu?"
"Kama wanafanya hivyo inamaana hata wakisikia kwamba kuna mtu mwingine anahusika na hili jambo watahitaji kumtafuta na kummaliza" Calvinjr alitulia kwanza na kumfanya mkurugenzi atabasamu, alikuwa amemuelewa kijana wake aliwaza nini. Calvinjr alioneka kuwa mbele ya muda sana.
"Unamaanisha tutasambaza uvumi kwamba kuna mtu ambaye anajua habari zao ambapo lazima watatuma watu kumuua na hao watu ndio ambao watatupa njia nzima sio?" Mkuu huyo aliuliza kwa bashasha sana
"Ndiyo mkuu na hiyo sehemu nitatakiwa kuwepo mimi, huyo atakayefika tutamaliza naye mchezo"
"Noooo" Tina alipinga habari ya kusema kwamba mdogo wake ndiye aende kwa watu hao ambao walionekana kuwa hatari na mdogo wake hakuonekana kuwa imara sana kiasi cha kupambana na watu hao kama hakuwa hata na uwezo wa kupambana na dada yake japo kwa dakika tano tu.
"Huenda ni kaka yako na unahisi unamjua sana ila huenda kuna mambo mengi sana ambayo huyajui kuhusu yeye, kama huwezi kumuamini ndugu yako basi niamini mimi. Nitakuruhusu unipige risasi kwenye kichwa changu kama kuna tatizo lolote litampata" maelezo ya mkubwa wao yalimfanya atulie japo alimpiga jicho kali sana Calvinjr, ilikuwa kawaida sana kwa watu hao.

Ujumbe uliingia kwenye simu ya mkurugenzi, ujumbe ulikuwa umetoka kwa mheshimiwa raisi wa nchi. Ujumbe huo ulikuwa ukitoa taarifa ya kwamba mhusika wa mlipuko wa jengo la bunge alikuwa amejulikana na kwa wakati huo alikuwa kwenye mikono ya jeshi na siku ya kesho asubuhi alikuwa anaenda kutangazwa hadharani kwenye vyombo vya habari hivyo kiongozi huyo wa usalama alitakiwa kuwepo eneo hilo.

Mr Gulamu Leopard aliwaonyesha vijana wake ujumbe huo, ujumbe mbao uliwaacha wote kwenye mshangao mkubwa mno. Kivipi mhusika kakamatwa? Kakamatwa na nani? Imekuwaje akamatwe bila shirika la kijasusi kuwa na taarifa hiyo? Yaani mtu ambaye maisha ya watu wengi yanachukuliwa ili asijulikane halafu inatoka taarifa ya kudai kwamba amekamatwa? Walichoka.

Sijui nini kilitokea ila episode ya 24 sina la ziada.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kuimalizia yote mpaka mwisho kwa 2500 tu.


2500 yako tu nakutumia pdf yote.

Lipia kwa namba

0621567672 ( WhatsApp)

0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA

Muwe na asubuhi njema.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 25.
Majira ya usiku wa mapema.
Kabla mheshimiwa raisi hajampatia taarifa mkurugenzi wa shirika la kijajusi Gulamu Leopard. Yalionekana magari matatu yakiwa kwenye msafara ambao ulikuwa na wanajeshi wa kutosha wakiwa kwenye kasi kubwa sana. Safari yao ilikwenda kuishia eneo la Upanga, walisimama kwenye nyumba moja ya kufahari ambayo ilikuwa na uzio mkubwa huku wakiwa na silaha kwenye mikono yao.

Waliingia hapo kwa nguvu na kuwatuliza walinzi wa eneo hilo ambao nao walivaa nguo za kiaskari, walinzi hao walipewa onyo kwamba kama angetokea hata mmoja wao akaenda kinyume basi risasi zilikuwa zinamhusu kama sio kupewa kesi ya ugaidi kwa kulipuuza na kwenda kinyume na matakwa na jeshi la wananchi.

Hata walinzi hao walibaki kwenye mshangao mkubwa wasielewe hao watu walikuwa wanamaanisha nini kwani hiyo nyumba ilikuwa ni nyumba ya waziri wa ardhi,sasa kivipi nyumba ya waziri wa ardhi ivamiwe na jeshi? Kuna kipi hasa ambacho kipo nyuma ya hilo jambo? Hiyo ilisababisha mlinzi mkuu wa waziri huyo kujitokeza na kuwauliza kivipi watu hao wavamie hilo eneo kwani hawajui kama ni nyumbani kwa kiongozi?

"Sidhani kama mnaelewa mpango kazi wa hii nchi, hata wangekuwa usalama hawaruhusiwi kumkamata kiongozi kana kwamba wanamkata ni kibaka mtaani. Hamuoni aibu kama mheshimiwa raisi na waziri wa ulinzi wakipata taarifa mnafanya jambo la kipumbavu kama hili?" Aliuliza mlinzi mkuu wa waziri huyo wa ardhi.

"Nisikilize we bwana, sijapewa amri ya kukukamata ndiyo maana nitakuacha kwa leo ila ni matumaini yangu hata wewe nitakurudia tu. Bosi wake anahusishwa na matukio ya kigaidi na ni matukio ambayo hayaangalii wewe ni nani wala hayahitaji kufuata mpango kazi mtu yeyote yule anakamatwa ili kuiweka nchi kwenye hali ya usalama"
"Utakuwa umechanganyikiwa kamanda, kivipi waziri ahusike na mambo ya kigaidi? Mmeanza kuchanganyikiwa?"
"Sasa kama una uhakika kwamba hahusiki hakikisha unamtafuta mwanasheria wake atakuja kuongea kwa niaba yake" kamanda huyo aliongea akiwa anasogea mbele lakini mlinzi huyo alimuweka chini ya ulinzi kitu kilicho mpelekea kamanda huyo kucheka na kumgeukia.
"Hili ni kosa kubwa sana umelifanya bwana mdogo na litakutokea puani hivi karibuni" wanajeshi wote walikuwa wamemuweka chini ya ulinzi mlinzi huyo. Akiwa hajajibu chochote mheshikiwa waziri wa ardhi wailes Mkwavinyika, mwanaume aliyekuwa anamhusudu sana mtwa mkwawa kama mpaginia uhuru bora wa Tanzania mpaka akaamua kujiita jina lake alijitokeza uso wake ukiwa umekosa nuru. Sura yake ilikuwa yenye simanzi na ndiye aliyefanya wale wote waache kubishana pale nje baada ya yeye kutoka huku familia yake ikiwa nyuma yake ili kuona hapo nje kulikuwa na nini hasa maana waliona walinzi wao wakiwa wanabishana na jeshi.

Alikuwa na mke mzuri sana pamoja na watoto wawili, wakike na wakiume na ndio ambao walikuwa wanaishi kwa kumtegemea waziri huyo.
"Haina haja ya kuanza kugombana, mimi hawa nitaenda nao" alitamka kauli ambayo iliwafanya walinzi wake na familia yake kumshangaa, anaondokaje nao watu ambao wamekuja ghafla namna hiyo? Yeye ni waziri sasa kivipi akamatwe kama raia wengine wa kawaida? Mbona kama anakosewa sana heshima?.

Mlinzi wake bado hakutaka kukubaliana na hilo jambo ila waziri huyo alitikisa kichwa kumpa ishara ya kutulia kijana wake huyo ambaye alikuwa amefanya naye kazi miaka mingi sana kwa uaminifu mkubwa. Kisha akamvuta mkewe pembeni mwanaume huyo na kumpa yale maneno ya kiutu uzima.
"Kwa lolote kitakalo tokea basi usionyeshe masikitiko sana wala mfadhaiko sana kwa sababu watoto wanategemea wewe ndiye uwape tumaini jipya la kuishi mimi nitakapokuwa mbali. Nisikilize vizuri mke wangu, leo naondoka nyumbani na inawezekane nisirudi tena hapa au kupata nafasi ya kuja kuongea na wewe tena kwenye maisha yangu. Kuna kesi nzito sana ambayo inanikabidi mbele yangu ambayo mimi nimeangushiwa mzigo mbovu wa taka ili watu fulani wawe salama ambao hata mimi siwajui"

"Nimeamua kukubali kila kitu ili kukulinda wewe na wanangu ambao nawapenda sana. Kitu ambacho unatakiwa kukijua kuanzia leo ni kwamba mumeo hana kosa wala hatia ila hili jambo unatakiwa kulizika kwenye moyo wako kwa maana kama ukisema kwamba mimi sina hatia basi watoto watauawa. Kwa sasa utakuwa unafuatiliwa kila sehemu hivyo hakikisha unajiweka mbali kabisa na hili jambo na hata akija mtu yeyote ķukuuliza mwambie kwamba hakuna unalo lijua kwa maana mimi nilikuwa nayafanya mambo yangu kwa siri bila familia yangu kujua. Tena kama ikitokea wakahitaji ukathibitishe mahakamani, kaeleze kwamba mimi ni gaidi kweli na nilitishia kuwaua mpaka nyie familia yangu, usipofanya hivyo watakupora mali zote mtaishi maisha magumu sana ila ukikubali kufanya hivyo basi wewe na watoto mtakuwa salama na mtalindwa na serikali"

"Nisamehe sana kwa kukuacha pekeyako ila unatakiwa kuchukulia kama hii siku ya leo haijawahi kutokea. Kadi zote za benki namba ya siri ni mwaka wako wa kuzaliwa na kwenye ile self ya pale ukutani kuna nyaraka zote za mali ambazo nazimiliki hivyo kuanzia sasa kila kitu kitakuwa chini yako na hakikisha unawatunza na kuwalinda hawa watoto kwa gharama yoyote ile. Wakija kuwa wakubwa uje uwaambie ukweli kwamba baba yenu hakuhusika na ile kesi nzito ambayo alipewa, baba yenu alikuwa mtu safi sana. Kwaheri mke wangu nawapenda sana." Mwanaume aliongea maneno ya kuumiza sana, maneno ambayo yalimuacha mkewe kwenye kilio kizito kwa maana mambo yalikuwa yanaenda tofauti kabisa na matarajio tena kwa kasi kubwa isiyokuwa ya kawaida.
Waziri huyo aliondoka hilo eneo bila kuwaaga wala kuwaangalia wanae, alikuwa anaumia mno kuwaacha hao watoto pekeyao na mama yao, aliwaza atawaambia nini wakati wa kuwaaga? Hakuona maneno ya kuwapatia, aliwaza wakimuuliza kwanini watu hao wamkamate kama mhalifu? Hakuwa na jibu la kuwapa, hivyo akaamua kuyafanya maamuzi magumu ya kutoka bila kusema kwaheri wanangu.

Alipanda kwenye gari ambayo walikuja nayo wanajeshi hao na msafara huo wa makamanda hao ukawa umeanza safari ya kutoweka hilo eneo. Wanaume hao walimchukua waziri huyo na kumfunga kitambaa cheusi usoni ambapo hakujua wala kuelewa kwamba walikuwa wakimpeleka wapi. Safari yao ilitumia dakika arobaini tu msafara huo ukawa umesimama ambapo alishusha na kupelekwa eneo ambalo hakujua kwamba ni wapi.

Alifunguliwa kutambaa usoni akiwa kwenye eneo ambalo bila shaka alihisi kwamba yupo chini ya ardhi, alifungwa hapo bila kuambiwa chochote kisha watu hao wakatoka humo ndani na mumuacha pekeyake akiwa na mawazo mengi sana, mawazo ambayo yalizichukua fikra zake na kuzirudisha nyuma ili kumpa kumbukumbu zilizofanya mpaka akaishia hiyo sehemu kwa wakati huo.

Kumbukumbu zake zilirudi mpaka siku ya jana yake, ambapo alikuwa nyumbani kwake kama ilivyokuwa kawaida yake, alikuwa ni mtu ambaye aliipenda sana familia yake hivyo muda mwingi ungemkuta akiwa yupo karibu sana na hiyo familia. Alikuwa anacheza cheza na wanae huku mkewe akiwa anaandaa chakula cha usiku ndipo alipo wapokea wageni ambao hakuwatarajia muda kama huo na hao walikuwa ni watu wa Ikulu wakiwa kwenye suti zao.

Mwanaume ambaye alikuwa amefika na vijana wake kwenye hiyo nyumba ya waziri mkuu ndiye mtu ambaye alikuwa anahakikisha ulinzi wa ikulu upo sawa, kiufupi alikuwa ni mtu mkubwa sana ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ukaribu sana na mheshimiwa raisi pamoja na mkurugenzi wa usalama wa taifa. Waziri huyo alimkaribisha mwanaume huyo mwa heshima kwa sababu alikuwa anamjua vyema sana, alikuwa anaiwakilisha ikulu hivyo alipaswa kuheshimiwa sana.

Walipata chakula pamoja kwa huyo waziri wakiwa wanayaongea mambo ya kawaida tu mpaka pale walipo maliza ndipo mtu huyo akasema kwamba walikuwa na mazungumzo ya siri ambayo walitakiwa kuyafanya na yanatakiwa kuwa baina yao wawili tu hakuna mtu mwingine yeyote yule ambaye anatakiwa kuyasikia. Basi wakazunguka nyuma ya jumba hilo la kifahari, eneo ambalo lilikuwa na bustani ndogo ya kuifanya nyumba hiyo izidi kupendeza.

"Mheshimiwa ni heshima kubwa sana mimi kukarimiwa kiasi hiki pamoja na kupata chakula kutoka kwenye familia ambayo bila shaka inaishi kwa amani na upendo usio elezeka. Ni jambo zuri sana pale ambapo baba unahakikisha familia yako inakuwa salama, ni matumaini ya yangu hakuna hata siku moja utapenda kuona familia yako inaingia kwenye mgongano au kwenye hali itakayo pelekea usalama wake kupotea"

"Mbona sijakuelewa unataka kusema nini? Familia yangu inahusika nini na haya mazungumzo?" Waziri baada ya kutajiwa familia yake aliuliza akiwa anabadilika sura yake. Mwanaume huyo aliangalia upande wa ile nyumba akiwa anatabasamu.
"Nisikilize bwana waziri, wanaume wanapokuwa wanazungumza mambo ya mhimu huwa hawatakiwi kuanza kupaniki kama watoto wa kike, hiyo inaweza kuwa dalili yenye matokeo mabaya sana kwa mbele labda kama moyo wako upo tayari kuyapokea matokeo yoyote yale"
"Unataka nini kwangu?" Mheshimiwa waziri aliuliza uso wake ukiwa umefura kwa hasira, kwa maana aliona kama mtu huyo yupo hapo kwa ajili ya kumtisha.
"Sasa hilo ndilo swali ambalo ulitakiwa kuniuliza mapema wala tusingeanza kubishana bwana waziri. Najua wewe ni mtu ambaye unaipenda sana familia yako, wewe ni ntu ambaye unajaribu kuwa baba bora sana kwani upo tayari kujiweka kwenye hatari kubwa lakini kikubwa familia yako iwe salama sa....." mwanaume huyo akiwa anahitaji kuendelea kuongea kile alicho kikusudia, waziri alimkatisha
"Acha kuitaja taja familia yangu kirahisi sana, nambie unahitaji nini? Kama huwezi kuongea basi naomba uondoke kwenye nyumba yangu" mwanaume huyo alitabasamu.
"Hii ndiyo sababu imenifanya nikufuate wewe hapa. Kwanza nikuweke sawa, nipo hapa kwa niaba ya Ikulu, wewe hapo hauna huo uwezo wa kuniambia mimi niondoke kwani unakuwa kama unamfukuza mheshimiwa raisi. Je nikiondoka bila kuongea utakuwa tayari kuipokea adhabu ya kugoma kuisikiliza Ikulu? Kama hauna huo uwezo basi tulia hapo hapo unisikilize tena unisikilize kwa umakini sana"

"Nafikiri unajua kinacho endelea nchini bwana waziri, unaelewa vizuri sana kwamba bunge limelipuliwa huko DOGMA TULIPO na wahusika wanaendelea kutafutwa na raisi amewaahidi watu kwamba atawatangazia mhusika kwa muda mchache ujao na asipofanya hivyo basi wananchi wataacha kumuamini kabisa, sasa hapa kuna kazi ndogo ambayo unatakiwa kuifanya"
"Kazi gani?" Aliuliza moyo wake ukiwa unaenda mbio sana, alitamani kisiwe kile ambacho alikuwa anakiwazia kichwani.
"Wewe ndiye unayetakiwa kubebeshwa hii kesi yote"
"Nooooooo, hapana hapana siwezi mimi"

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Episode 25 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 26:
Kupinga kwake mheshimiwa waziri hakukumfanya awe amefanya chaguo sahihi zaidi kutoka kwenye hayo maamuzi yake.
"Sijaja hapa ili kukuomba wewe ukubali hiki ninacho kwambia mimi ila chaguo ni la kwako mwenyewe, nadhani ukishindwa kufuata kile ambacho mimi nina kwambia unajua nini kinaenda kutokea" wakati mwanaume huyo anaendelea kuongea macho yake yalikuwa yanatazama ulipo mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ya waziri huyo. Maana fupi ya alichokuwa anamwambia kiongozi huyo ni kwamba kama hakuwa tayari kukubali hilo jambo basi familia yake ilikuwa inauawa, aliogopa sana waziri.

Chozi lilikuwa linamtoka kwa uchungu, huwa sio rahisi kubebeshwa ukatili mbele ya watu kwa jambo ambalo hujalifanya wewe na kila mtu akaamini kwamba wewe ni mtu mbaya. Na kwa bahati iliyo mbaya ikishathibitishwa tu hakuna mtu ambaye atakuja kukuelewa tena, utachukiwa wewe na familia yako yote.
"Kwanini mnanifanyia hivi? Wapi niliwakosea mpaka nastahili adhabu kali namna hii kwenye maisha yangu?"
"Bwana waziri nadhani unaelewa nini maana ya uzalendo, umefundishwa vyema kuwa tayari hata kufa kwa ajili ya nchi yako, sasa kwanini unahisi unaonewa? Hii nchi ina watu zaidi ya milioni hamsini, kujitoa kwako sadaka kutawafanya watu hawa waendelee na maisha ya kawaida wakishajua kwamba mhusika ni wewe na tayari umeshakamatwa ila bila kuwa na uhakika na hili basi wanaweza kufanya hata machafuko ambayo yatafanya tuingie sehemu mbaya sana kama nchi"
"Hili jambo mheshimiwa raisi analijua?"
"Raisi hajui wala hatakiwi kujua kwa sababu yeye anatakiwa kupelekewa taarifa tu kwamba wewe ndiye mhusika na kama akija kukuuliza utatakiwa kukubali kila kitu. Ukiacha nchi pia hili jambo unatakiwa kulifanya ili kumnusuru raisi duniani kwa hii kashfa mbaya ambayo itamkuta kama tu mhusika asipo patikana"
"Ni kitu gani ambacho kimekufanya kati ya watu milioni hamsini uje unichague mimi hapa?"
"Kuna sababu kubwa mbili tu ambazo zilinifanya nione kwamba wewe unafaa kwa majina ambayo nilikuwa nayo mezani. Sababu ya kwanza ni kwamba wewe ni kiongozi. Hii ina faida kubwa zaidi kwenye uhusika wa hili tukio kwani, eneo kama lile raia wa kawaida hawezi kuingia na mzigo na akapenya nao kutokana na ule ulinzi mkubwa uliopo pale hivyo lazima ni kiongozi mkubwa ambaye hakaguliwi ndiye aliingia na mzigo wa hayo mabomu bungeni"

"Na kwenye rekodi zangu, bunge la mwisho kabla ya hili ambalo limeyabeba maisha ya watu wengi ulikuwepo bungeni kuweza kuwasilisha na kusoma bajeti ya ardhi ya mwaka, na siku ile bungeni wakati unaulizwa maswali ulikuwa mtu mwenye hasira sana, hivyo zile hasira tutazitumia kama ushahidi wa kusisitiza ulicho kifanya. Maana yake itaonekana kwamba siku ile ndiyo ambayo ulienda kuyatunza mabomu sehemu ambazo uliona zinafaa mpaka siku ambayo uliamua kuutekeleza mpango wako"

"Lakini sababu ya pili hapa kuna mambo mawili ambayo yanaendana, kwanza kuna kipindi uliwahi kusingiziwa kesi ya ubakaji mahakamani na jopo fulani la wabunge japo kesi ile uliweza kuishinda, hivyo tutatumia sababu hiyo kama kigezo kingine cha wewe kulipiza kwa wale watu pamoja na kesi zingine ambazo tutakuongezea kwa juu. Ila jambo la pili ni kwamba wewe ni moja ya viongozi wenye akili sana na huwa hamkurupuki kuweza kutengeneza hoja zenu. Hivyo hata kwenye lile tukio, ni kwamba alihitajika mtu mwenye uwezo mkubwa kichwani ili kutekeleza lile tukio, nafikiri hapo itakuwa rahisi sana kumaliza mjadala na wananchi wakaamini kila kitu" mwanaume huyo alionekana kwamba hilo jambo alikuwa ameliandaa vilivyo ndio maana kila kona alikuwa anajua ni wapi pa kuingilia na wapi pa kutokea.

"Moja kati ya vitu ambavyo siwezi kuvifanya kwenye maisha yangu, ni kuja kukusamehe wewe kwa kuniingiza mimi kwenye uasi ambao mimi sijaufanya. Kuanzia kesho kurasa za magazeti mengi duniani zinaenda kuniandika kama kiongozi mpuuzi zaidi kuwahi kutokea duniani, watoto watakuja kunisoma mashuleni baadae kama gaidi ambaye niliwahi kujificha kwenye kivuli cha uongozi kwa jambo ambalo hata sijui mwanzo wake ni upi"

"Nisikilize waziri, wewe kunichukia mimi haitakusaidia chochote kile zaidi unatakiwa kuniheshimu sana kwa sababu nimekubali kuilinda familia yako pindi utakapokuwa haupo na familia yako itaishi maisha mazuri sana na wanao watakuja kutafutiwa nafasi kubwa kwa baadae kwa sababu ya maamuzi yako ya busara leo" maneno ya mwanaume huyo yalimfanya waziri aangalie sana upande wa ile nyumba yake.

"Kuna vitu viwili ambavyo nakuomba sana uvitimize pale ambapo mimi nitakuwa sipo au nitakuwa nimekufa"
"Nakusikiliza"
"Kwanza naomba familia yangu itolewe kwenye hii kesi"
"OK, nitafanya hivyo. Kuna lingine?"
"Usinijibu kihuni hivyo. Nahitaji kujua utawatoaje kwenye hii kesi, kwa maana kama wakionekana bado walikuwa na mimi basi hata wao ulimwengu utawachukia sana kwani wataonekana walikuwa pamoja na mimi"
"Haya mambo nimeyapanga muda mrefu sana. Iko hivi vyombo vya habari na uma utajulishwa kwamba, wewe ni mwanaume mbinafsi sana ambapo baada ya kufanya tukio lako la kikatili namna hiyo, mkeo alianza kukuhisi na kuhitaji kukuripoti kutuoni lakini ukaishia kumteka na kumtishia kumuua yeye na watoto ambao hata haukujali kama ni wakwako kutokana na ubinafsi ulio nao. Nadhani umeelewa ni namna gani familia yako itakuwa imewekwa nje na kesi na badala ya kuchukiwa watu watawaonea huruma sana kwa mabaya uliyokuwa unawafanyia hivyo watawapenda sana"
"Kwahiyo unataka hadi wanangu wanichukie kwa kuhisi hata wao nilitaka kuwaua?"
"Hiyo ndiyo njia pekee au una nyingine?"
"Hapana sina"
"Haya nambie hilo jambo la pili, nakusikiliza"
"Jambo la lipi nahitaji familia yangu ilindwe kwa gharama yoyote ile na hakikisha hakuna hata mmoja ambaye anapata tatizo kwenye familia yangu na pale wanangu watakapokuwa wakubwa basi hakikisha unawapatia nafasi kubwa kama ulivyo niahidi hapa"
"Hilo ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wangu hivyo nitafanya kama tulivyo kubaliana hapa"
"Sawa na wananchi watathibitishaje kwamba familia yangu haihusiki?"
"Kesho unakuja kuchukuliwa hapa, kabla hunaondoka hakikisha kwamba unampa mkeo maneno ambayo yatamfanya asiwe na namna zaidi ya kufuata kile ambacho ataambiwa, kwa sababu wakati unatangazwa rasmi kuwa gaidi namba moja nchini naye atatakiwa kupandisha na kutoa maneno kwenye vyombo vya habari na maneno yake ndiyo yataaminiwa zaidi. Kama akiongea kama tunavyotaka basi ahadi nilizo kuahidi kuhusu familia yako, zitaanza kutimizwa muda huo huo ila kama ataenda kinyume basi nadhani unajua nitafanya nini!"
"Sawa nipo tayari kuibeba hiyo kesi"
"Ok, ukiwa unakiri kuhusika na hilo jambo maelezo ambayo utatakiwa kuyatoa ili kuwathibitishia uma kwamba umehusika kulilipua bunge ni haya. Waambie kwamba lile kundi la wabunge pamoja na viongozi wengine ambao waliwahi kutushtaki kwa kesi ile ya ubakaji walikuwa wanajua na wana ushahidi juu ya mambo yako yafuatayo, ubakaji, kulawiti watoto, ikiwemo pia na ubadhilifu wa mali za serikali ambapo ulisaini mkataba wa pesa zaidi ya billion mianane na ukazificha"
"Whaaaat, hizo kesi zote unamaanisha unataka niuawe?"
"Yes ni lazima unyongwe ili hadithi ya hili tukio iishie hapa" ilikuwa ni ngumu sana kuipokea kesi ambayo hata hakujua imetokea wapi, imetekelezwa na nani? Ila kitu cha ajabu ni kwamba alitakiwa kuikubali na kuifanya iwe yake huku akijua kabisa kwamba anaenda kunyongwa. Hakuwa na namna waziri Wailes Mkwavinyika zaidi ya kupeana mikono na mwanaume huyo kutoka Ikulu kumaanisha kwamba mpango wao ulikuwa umepita huku akijua kwamba akifika mahakamani moja kwa moja anaenda kunyongwa kwa aina ya makosa ambayo alikuwa nayo.

Hata hivyo hakujali sana hilo, kwake kuilinda familia yake ndilo lilikuwa jambo la mhimu zaidi. "Wanaume wanajitoa mhanga ili kulinda maslahi ya familia zao, mwanaume sio kuvaa tu suruali, uanaume ni kuyabeba majukumu na kuzivaa changamoto." Hiyo ndiyo kauli ambayo alikuwa anaiishi siku zote kwenye maisha yake. Ni kauli ambayo ilimfanya awe tayari kupigana ili kuiweka salama familia yake na ndicho alicho kifanya.

Hivyo wakati wanaume wale ambao walikuwa kwenye magwanda ya jeshi wakiwa wanafika pale kwake, alikuwa anajua ni kipi kinaenda kutokea na hakutaka hata kupoteza muda kwa sababu jana yake alikuwa ameingia makubaliano na ndivyo hivyo ilivyokuwa mpaka akafanikiwa kuingia kwenye mikono ya hao wanaume.
Mheshimiwa raisi akiwa kwenye ofisi yake, mawazo yakionekana kumzonga kwenye kichwa chake, alikuwa anawaza juu ya hiyo kesi nzito ambayo alikuwa amewaahidi wananchi kwamba wakati mchache ujao alikuwa anawaonyesha yule fedhuli wa nchi aliyewaletea majonzi mazito mno. Alishtuka kutoka kwenye mawazo baada ya simu yake kuanza kuita. Aliangalia jina la mpigaji, alikuwa ni waziri wa ulinzi, aliipokea;
"Hello bosi"
"Nakusikiliza"
"Kuna habari njema kidogo kwa wakati huu wa majonzi"
"Zipi?"
"Tumempata mhuskika wa hili tukio"
"Whaaaaat!"
"Ndiyo bosi"
"Imewezakanaje na mmempata pata vipi na ni nani huyo mtu?"
"Bosi, unajua siku zote sisi tunatakiwa kukusaidia kufanya kazi kwa asilimia miamoja hususani hizi kazi ambazo zinahitaji nguvu kubwa sana. Hivyo wakati umetangaza kumtafuta mhusika mimi niliamua kuwaingiza vijana wangu wa jeshi kazini na ndipo wakamjua mhusika ambaye alikuwa nyuma ya mpango wote"
"Naomba jina lake huyo"
"Wailes Mkwavinyika"
"Unamaanisha waziri wa ardhi?"
"Ndiyo mkuu"
"How?"
"Unaweza kuja kumuona mheshimiwa, tupo Kawe kwenye nyumba ya jeshi hapa ya siri"
"Nakuja hapo sasa hivi"
"Sawa bosi"

Kipi kinaenda kujiri? Episode ya 26 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…