FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #61
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 11.
Calvin baada ya kutoka kuonana na bosi wake, alitakiwa kuweka mambo sawa kwenye kampuni yake kabla ya kuelekea huko lindi mchana wa siku hiyo hiyo. Lakini kabla ya kufanya hayo yote alipaswa kwenda kumtazama kwanza mgonjwa wake ili aweze kujua kwa wakati huo alikuwa kwenye hali gani.
Hivyo ilimlazimu kupitia hospitali kwanza ndipo aendelee na majukumu yake, alisogea mpaka lilipo wodi la mwanamke yule lakini palikuwa na walinzi wa mama wa mwanamke huyo hivyo aliamua kuto sogea hilo eneo akaanza kuondoka ila kabla hajafika mbali simu yake iliita.
Aliyekuwa anapiga ndiye ambaye alikuwa ndani ya wodi aliyokuwa ameipa mgongo na kuamua kuondoka.
"Nasikia umekuja halafu unataka kuondoka bila kujua hata hali ya mgonjwa wako? Nimewaambia wakuruhusu uweze kuingia ndani angalau unipe pole" aliisikia kwamba mbali sauti iliyokuwa kwenye majonzi mazito sana, mwanamke huyo alionekana kuwa kwenye maumivu makali ambayo isingekuwa rahisi kuelezeka kwa njia ya kawaida waliyo izoea wengi.
Calvinjr alijongea mpaka mlangoni ambapo kabla ya kuingia alisikia watu wakiongea kwa ndani huku mmoja akiwa kama anataka kujua jambo fulani.
"Huyo unaye ongea naye ni nani?" ilisikika sauti ya mama akiwa anamlisha mwanae
"Huyo ndiye ambaye amenileta hapa?"
"Namjua huyo mtu?"
"Sidhani mama"
"Sasa mbona ofisini wanasema hukuwepo? Huyo mtu umekutana naye wapi?"
"Mama nilikuwa kwenye biashara ndipo nikapokea hizi habari, sikujua kilicho endelea mpaka nilipofika hapa hospitalini, hivyo unatakiwa kumshukuru maana huenda leo ungepoteza watu wako wawili wa mhimu" kabla mama huyo hajajibu walikatishwa na sauti ya hodi ya mtu ambaye bila shaka alitegemea kuingia ndani muda mchache uliokuwa unafuata.
"Mama shikamoo" Calvinjr alisalimia huku akiwa anakaa kwenye kiti ambacho kilikuwa pembeni ya kitanda.
"Marahaba mwanangu, asante sana kwa kumleta mwanangu hapa maana nasikia huenda kama sio msaada wako angekuwa kwenye hali mbaya zaidi. Ninaye huyu huyu mmoja tu pekee naomba kama utapendezwa unaweza ukasema kwamba unahitaji nini ili niweze kukulipa kwa wema wako"
"Mama wala usijali, kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzangu ni wajibu wangu ukizingatia huyu ni mtu mkubwa nchini na mfanya biashara mwenzangu pia hivyo ni langu jukumu kumlinda, japo nina swali moja kama hamtojali" Calvinjr alisita huku akiwa anawaangalia kwa umakini sana watu hao.
"Sijajua ni kipi kilitokea maana niliona tu taarifa ikikatika kutoka bungeni na ghafla naye mrs William anadondoka chini, hivyo niliogopa kwamba huenda ni ofisi yetu imehusika labda kulingana na hali ya hewa kuwa mbaya. Nimeogopa sana ndiyo maana nilihitaji kujua ili nione kama kuna sehemu naweza kusaidia" maneno yake ni kama alikuwa anataka wasimhisi kwa lolote lile wala kumjua.
Watu hao wote wawili walishusha machozi kwa pamoja na kujifuta ambapo mama huyo alimgeukia Calvinjr na kumuuliza;
"Mimi unanifahamu?"
"Ndiyo mama, wewe ni mke wa kiongozi mkubwa sana ndani ya nchi hii hivyo kukufahamu ni lazima"
"Na huyu binti uliye msaidia ulikuwa unamjuaje?"
"Huyu mimi namjua kama mkandarasi mkuu wa serikali lakini pia ni mwanamke mwenye mafanikio makubwa sana kibiashara ambaye huwa ananivutia sana na natamani siku moja nije kuyafikia mafanikio yake"
"Basi huyo hapo ni mtoto wa damu wa mume wangu ambaye ndiye alikuwa waziri mkuu wa hii nchi. Kwa bahati iliyokuwa mbaya aliniaga kwamba anaenda kwenye mkutano wa bunge ambako ndiko huko mlipuko ulio tokea,umeenda na maisha yake. Hivyo huyo alishtuka kwa ule mlipuko kwa sababu alijua mle ndani kuna baba yake mzazi"
"MUNGU wangu!!!!! Naombeni mnisamehe sana kwa kuuliza hilo jambo maana sikujua lolote, poleni sana. Hakika huu utakuwa msiba mkubwa sana kwa taifa letu kufiwa na waziri mkuu? Ohhhhh shiiiit! Pole sana mrs William" aliongea akiwa kama anawaonea sana huruma huku akimsogelea mrembo huyo na kumpiga piga mgongoni ili kumpa pole yake ila alikuwa tayari amesha mjua kwa muda mrefu tu maana alitoka kuambiwa.
"Sijui baba yangu kawakosea nini mpaka wakaamua kumchukua mapema sana kiasi hiki" mrembo huyo aliongea kwa uchungu sana akiwa anamkumbatia Calvinjr.
"Mama samahani, haujapigiwa hata simu labda na watu kukupa taarifa kuhusu chanzo cha mlipuko huo ni nini?" Calvinjr aliuliza kwa makusudi kabisa.
"Hapana hakuna taarifa yoyote ile ambayo imetolewa zaidi ya hizo ambazo zinasambaa mitandaoni. Vyombo vya usalama vimenipa taarifa kwamba niwe mvumilivu taarifa zikikamilika wataniletea na nitazipata"
"Sawa mama basi mimi ngoja nikaweke mambo sawa ofisini kisha nitakuja kuungana na mgonjwa wangu pamoja na kumpa sapoti yangu msibani" Calvinjr aliongea akiwa ananyanyuka akimwangalia Sarafina mwa masikitiko sana japo naye alionyesha kwamba hamjui kabisa mwanamke huyo kuundani.
"Tunashukuru sana, kama unakuja tena basi uje nyumbani kwa maana hapa tumeruhusiwa kutoka saivi, ukifika nyumbani piga simu yake ili usisumbuliwe na walinzi"
"Sawa mama" mwanaume alitoka ila baada ya hilo tatizo kuisha alikuwa ana maswali kwa mwanamke huyo, inawezekanaje ni mtoto wa waziri mkuu na hataki kujulikana?.
Theobald Mnyika, mwanaume aliyekuwa na mamlaka ya juu zaidi ndani ya nchi ya Tanzania. Huyu ndiye alikuwa raisi mwenyewe, majira hayo muda mfupi baada ya tukio hilo kubwa na baya ambalo lilionekana kuwa la kigaidi kutokea ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo ambao ndio ulikuwa na bunge la nchi yaani DOGMA TULIPO.
Alikuwa amechanganyikiwa mzee huyo akiwa mwingi wa wasi, hakuelewa jambo lolote ambalo lilikuwa linaendelea ndiyo maana alihitaji ripoti ambayo inaeleweka na kutoa maagizo yake pamoja na kauli yake kwa maana wananchi walikuwa wanasubiri kuona raisi wao atasema nini juu ya jambo hilo.
Sehemu ya kupata taarifa kwa haraka ilikuwa ni moja tu, kwa mkurugenzi wa shirika la kujasusi wa nchi yake, yaani Gulamu Leopard. Alikuwa amempa maagizo kijana wake huyo kwa kazi aweze kufika Ikulu ili ajue kipi kinaendelea na ni mpango gani ambao upo mezani.
Alikuwa yupo kwenye korido yake ambayo mara nyingi sana alikuwa akiitumia kwa ajili ya kupumzikia huku akiwa amevaa pajama pekee kwenye mwili wake kwa maana muda mchache uliokuwa umetoka kupita alikuwa kuogelea kwenye maji ya baridi ili kuupa mwili hali ya uchangamfu lakini aliona kama anautesa mwili hivyo akaamua kwenda kulala ila kwa bahati ambayo ilikuwa mbaya sana hata kitanda hakikulalika kabisa.
Hivyo aliamua kuagiza kahawa ambayo ilikuwa ya moto lakini aliishia kuzunguka nayo hilo eneo mpaka ikapoa. Aliangalia saa yake na kuona muda unakwenda, aliagiza msaidia wake amletee simu haraka sana aweze kumpigia kijana wake wake wa kazi huyo japo kiumri walikuwa hawajapisha sana ila kikazi alikuwa ni mdogo kwake.
Kabla hajafanya hivyo aliletewa taarifa ya kwamba mkurugenzi huyo alikuwa amefika hivyo aliamuru moja kwa moja aletwe hapo hapo mbele yake, hawakuwa na haja ya kwenda ofisini, wangeupoteza muda bure.
"Nipe taarifa zote zinazo endelea mpaka mlipo ishia kwa wakati huu na kipi kinaendelea mpaka unavyofika hapa kwangu?" Mzee huyo alimuuliza mkurugenzi huyo kwa kasi hata kabla hawajapeana salamu.
Gulamu alimeza mate kwanza, kwa sababu maelezo yake ndiyo ilikuwa pona pona ya kazi yake vinginevyo kwa ule uzembe ambao ulikuwa umetokea alitakiwa kufukuzwa kazi muda huo huo.
"Mkuu mpaka sasa tupo tunafuatilia ila tumeshapiga hatua kadhaa ambazo zinatupa mwanga"
"Kuwa siriasi na maelezo yako, sio unaanza kuongea na mimi kama unatafuta mfanyakazi wa kumuajiri kwenye shirika lako hilo. Nimekuita hapa ili unipe sababu kwanini sitakiwi kukufuta kazi muda huu na kumuweka mtu mwingine kwenye hiyo nafasi yako?" raisi aliongea kwa jazba macho yake yakiwa mekundu sana.
"Jinsi tukio lilivyo tokea hakuna mwananchi wa kawaida au mfanyakazi wa kawaida ambaye anaweza kuingia na bomu lenye uwezo mkubwa kiasi kile. Pale tuliweka ulinzi kila sehemu mpaka kwenye mashine zisizo onekana lakini cha kushangaza kuna watu wameweza kufanikisha hilo hivyo imetupa mwanga kwamba kuna mhusika ndani yetu ambaye tunafanya naye kazi ndo kahusika"
"Kwahiyo hayo ndiyo maelezo ambayo unataka mimi nikawape wananchi na unategemea watanielewa? hivi kichwa chako kinafanya kazi sawa sawa? Usifanye nijute kukuweka kwenye hiyo nafasi!" Mheshimiwa raisi aliendelea kufoka mbele ya mzee mwenzake kwani jambo la kujibia hayo yote lilikuwa kwenye mkono wake yeye ndiyo maana alikuwa ana hasira isivyo kawaida.
"Kuna kiongozi ndiye amefanya hili tukio" kauli hii ya mkurugenzi ilimshtua na kumfanya amgeukia mwanaume huyo akiwa amemkazia macho.
"Ndiyo ni kiongozi ndiye amefanya huu mlipuko"
"Haiwezekani"
"Kwenye lile eneo watu wote ambao wanapita huwa wanakaguliwa kila sehemu mpaka mabegi yao kama yapo salama lakini hilo jambo huwa halifanywi kwa viongozi wakubwa tu pekee. Maana yake ni kwamba bomu liliingizwa kwenye moja ya begi la kiongozi mkubwa wa serikali ambaye gari yake na begi lake haliwezi kukaguliwa"
"Kwanini unahisi natakiwa kuyaamini maneno yako bwana Gulamu?" raisi aliuliza kwa mshangao.
"Unatakiwa kuniamini kwa sababu ya yule mwanasiasa Isaya Ndango"
"Huyo mbunge wa kawaida sana, sasa anahusikaje kwenye haya?"
"Yule bwana mdogo alikuwa na ushawishi mkubwa sana na inasemekana kwamba kuna baadhi ya viongozi wakubwa ambao alitaka kuwaumbua kwa mambo yao ya nyuma ya pazia ambayo wananchi walipaswa kuyajua. Sasa inasemekana kwamba alikuwa amewashawishi wanasiasa kadhaa ili wamuunge mkono ikiwemo waziri mkuu ambaye alikuwa tayari kumsapoti kuhakikisha waovu wanafichuliwa"
"Sasa leo ndiyo siku ambayo alitakiwa kuwasilisha majina ya watu hao pamoja na kuyazungumza yale waliyo yatenda mbele ya uma na ndipo tukio hilo lilipoweza kufanyika. Mpaka hapo hauwezi ukanipa imani yako mkuu kunisikiliza?" Maneno ya mkurugenzi, yalilikuna sikio la mheshimiwa raisi, aliomba wakae chini ili wayazungumze kinaga ubaga ili wajue, je yule panya aliye mfunga paka kengele alipona? Kama hakupona yuko wapi?
Episode 11 inafika mwisho.
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app