Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 11.

Calvin baada ya kutoka kuonana na bosi wake, alitakiwa kuweka mambo sawa kwenye kampuni yake kabla ya kuelekea huko lindi mchana wa siku hiyo hiyo. Lakini kabla ya kufanya hayo yote alipaswa kwenda kumtazama kwanza mgonjwa wake ili aweze kujua kwa wakati huo alikuwa kwenye hali gani.

Hivyo ilimlazimu kupitia hospitali kwanza ndipo aendelee na majukumu yake, alisogea mpaka lilipo wodi la mwanamke yule lakini palikuwa na walinzi wa mama wa mwanamke huyo hivyo aliamua kuto sogea hilo eneo akaanza kuondoka ila kabla hajafika mbali simu yake iliita.

Aliyekuwa anapiga ndiye ambaye alikuwa ndani ya wodi aliyokuwa ameipa mgongo na kuamua kuondoka.

"Nasikia umekuja halafu unataka kuondoka bila kujua hata hali ya mgonjwa wako? Nimewaambia wakuruhusu uweze kuingia ndani angalau unipe pole" aliisikia kwamba mbali sauti iliyokuwa kwenye majonzi mazito sana, mwanamke huyo alionekana kuwa kwenye maumivu makali ambayo isingekuwa rahisi kuelezeka kwa njia ya kawaida waliyo izoea wengi.

Calvinjr alijongea mpaka mlangoni ambapo kabla ya kuingia alisikia watu wakiongea kwa ndani huku mmoja akiwa kama anataka kujua jambo fulani.

"Huyo unaye ongea naye ni nani?" ilisikika sauti ya mama akiwa anamlisha mwanae
"Huyo ndiye ambaye amenileta hapa?"
"Namjua huyo mtu?"
"Sidhani mama"
"Sasa mbona ofisini wanasema hukuwepo? Huyo mtu umekutana naye wapi?"

"Mama nilikuwa kwenye biashara ndipo nikapokea hizi habari, sikujua kilicho endelea mpaka nilipofika hapa hospitalini, hivyo unatakiwa kumshukuru maana huenda leo ungepoteza watu wako wawili wa mhimu" kabla mama huyo hajajibu walikatishwa na sauti ya hodi ya mtu ambaye bila shaka alitegemea kuingia ndani muda mchache uliokuwa unafuata.

"Mama shikamoo" Calvinjr alisalimia huku akiwa anakaa kwenye kiti ambacho kilikuwa pembeni ya kitanda.

"Marahaba mwanangu, asante sana kwa kumleta mwanangu hapa maana nasikia huenda kama sio msaada wako angekuwa kwenye hali mbaya zaidi. Ninaye huyu huyu mmoja tu pekee naomba kama utapendezwa unaweza ukasema kwamba unahitaji nini ili niweze kukulipa kwa wema wako"

"Mama wala usijali, kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzangu ni wajibu wangu ukizingatia huyu ni mtu mkubwa nchini na mfanya biashara mwenzangu pia hivyo ni langu jukumu kumlinda, japo nina swali moja kama hamtojali" Calvinjr alisita huku akiwa anawaangalia kwa umakini sana watu hao.

"Sijajua ni kipi kilitokea maana niliona tu taarifa ikikatika kutoka bungeni na ghafla naye mrs William anadondoka chini, hivyo niliogopa kwamba huenda ni ofisi yetu imehusika labda kulingana na hali ya hewa kuwa mbaya. Nimeogopa sana ndiyo maana nilihitaji kujua ili nione kama kuna sehemu naweza kusaidia" maneno yake ni kama alikuwa anataka wasimhisi kwa lolote lile wala kumjua.

Watu hao wote wawili walishusha machozi kwa pamoja na kujifuta ambapo mama huyo alimgeukia Calvinjr na kumuuliza;
"Mimi unanifahamu?"

"Ndiyo mama, wewe ni mke wa kiongozi mkubwa sana ndani ya nchi hii hivyo kukufahamu ni lazima"
"Na huyu binti uliye msaidia ulikuwa unamjuaje?"

"Huyu mimi namjua kama mkandarasi mkuu wa serikali lakini pia ni mwanamke mwenye mafanikio makubwa sana kibiashara ambaye huwa ananivutia sana na natamani siku moja nije kuyafikia mafanikio yake"

"Basi huyo hapo ni mtoto wa damu wa mume wangu ambaye ndiye alikuwa waziri mkuu wa hii nchi. Kwa bahati iliyokuwa mbaya aliniaga kwamba anaenda kwenye mkutano wa bunge ambako ndiko huko mlipuko ulio tokea,umeenda na maisha yake. Hivyo huyo alishtuka kwa ule mlipuko kwa sababu alijua mle ndani kuna baba yake mzazi"

"MUNGU wangu!!!!! Naombeni mnisamehe sana kwa kuuliza hilo jambo maana sikujua lolote, poleni sana. Hakika huu utakuwa msiba mkubwa sana kwa taifa letu kufiwa na waziri mkuu? Ohhhhh shiiiit! Pole sana mrs William" aliongea akiwa kama anawaonea sana huruma huku akimsogelea mrembo huyo na kumpiga piga mgongoni ili kumpa pole yake ila alikuwa tayari amesha mjua kwa muda mrefu tu maana alitoka kuambiwa.

"Sijui baba yangu kawakosea nini mpaka wakaamua kumchukua mapema sana kiasi hiki" mrembo huyo aliongea kwa uchungu sana akiwa anamkumbatia Calvinjr.

"Mama samahani, haujapigiwa hata simu labda na watu kukupa taarifa kuhusu chanzo cha mlipuko huo ni nini?" Calvinjr aliuliza kwa makusudi kabisa.

"Hapana hakuna taarifa yoyote ile ambayo imetolewa zaidi ya hizo ambazo zinasambaa mitandaoni. Vyombo vya usalama vimenipa taarifa kwamba niwe mvumilivu taarifa zikikamilika wataniletea na nitazipata"

"Sawa mama basi mimi ngoja nikaweke mambo sawa ofisini kisha nitakuja kuungana na mgonjwa wangu pamoja na kumpa sapoti yangu msibani" Calvinjr aliongea akiwa ananyanyuka akimwangalia Sarafina mwa masikitiko sana japo naye alionyesha kwamba hamjui kabisa mwanamke huyo kuundani.

"Tunashukuru sana, kama unakuja tena basi uje nyumbani kwa maana hapa tumeruhusiwa kutoka saivi, ukifika nyumbani piga simu yake ili usisumbuliwe na walinzi"

"Sawa mama" mwanaume alitoka ila baada ya hilo tatizo kuisha alikuwa ana maswali kwa mwanamke huyo, inawezekanaje ni mtoto wa waziri mkuu na hataki kujulikana?.

Theobald Mnyika, mwanaume aliyekuwa na mamlaka ya juu zaidi ndani ya nchi ya Tanzania. Huyu ndiye alikuwa raisi mwenyewe, majira hayo muda mfupi baada ya tukio hilo kubwa na baya ambalo lilionekana kuwa la kigaidi kutokea ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo ambao ndio ulikuwa na bunge la nchi yaani DOGMA TULIPO.

Alikuwa amechanganyikiwa mzee huyo akiwa mwingi wa wasi, hakuelewa jambo lolote ambalo lilikuwa linaendelea ndiyo maana alihitaji ripoti ambayo inaeleweka na kutoa maagizo yake pamoja na kauli yake kwa maana wananchi walikuwa wanasubiri kuona raisi wao atasema nini juu ya jambo hilo.

Sehemu ya kupata taarifa kwa haraka ilikuwa ni moja tu, kwa mkurugenzi wa shirika la kujasusi wa nchi yake, yaani Gulamu Leopard. Alikuwa amempa maagizo kijana wake huyo kwa kazi aweze kufika Ikulu ili ajue kipi kinaendelea na ni mpango gani ambao upo mezani.

Alikuwa yupo kwenye korido yake ambayo mara nyingi sana alikuwa akiitumia kwa ajili ya kupumzikia huku akiwa amevaa pajama pekee kwenye mwili wake kwa maana muda mchache uliokuwa umetoka kupita alikuwa kuogelea kwenye maji ya baridi ili kuupa mwili hali ya uchangamfu lakini aliona kama anautesa mwili hivyo akaamua kwenda kulala ila kwa bahati ambayo ilikuwa mbaya sana hata kitanda hakikulalika kabisa.

Hivyo aliamua kuagiza kahawa ambayo ilikuwa ya moto lakini aliishia kuzunguka nayo hilo eneo mpaka ikapoa. Aliangalia saa yake na kuona muda unakwenda, aliagiza msaidia wake amletee simu haraka sana aweze kumpigia kijana wake wake wa kazi huyo japo kiumri walikuwa hawajapisha sana ila kikazi alikuwa ni mdogo kwake.

Kabla hajafanya hivyo aliletewa taarifa ya kwamba mkurugenzi huyo alikuwa amefika hivyo aliamuru moja kwa moja aletwe hapo hapo mbele yake, hawakuwa na haja ya kwenda ofisini, wangeupoteza muda bure.

"Nipe taarifa zote zinazo endelea mpaka mlipo ishia kwa wakati huu na kipi kinaendelea mpaka unavyofika hapa kwangu?" Mzee huyo alimuuliza mkurugenzi huyo kwa kasi hata kabla hawajapeana salamu.
Gulamu alimeza mate kwanza, kwa sababu maelezo yake ndiyo ilikuwa pona pona ya kazi yake vinginevyo kwa ule uzembe ambao ulikuwa umetokea alitakiwa kufukuzwa kazi muda huo huo.

"Mkuu mpaka sasa tupo tunafuatilia ila tumeshapiga hatua kadhaa ambazo zinatupa mwanga"
"Kuwa siriasi na maelezo yako, sio unaanza kuongea na mimi kama unatafuta mfanyakazi wa kumuajiri kwenye shirika lako hilo. Nimekuita hapa ili unipe sababu kwanini sitakiwi kukufuta kazi muda huu na kumuweka mtu mwingine kwenye hiyo nafasi yako?" raisi aliongea kwa jazba macho yake yakiwa mekundu sana.

"Jinsi tukio lilivyo tokea hakuna mwananchi wa kawaida au mfanyakazi wa kawaida ambaye anaweza kuingia na bomu lenye uwezo mkubwa kiasi kile. Pale tuliweka ulinzi kila sehemu mpaka kwenye mashine zisizo onekana lakini cha kushangaza kuna watu wameweza kufanikisha hilo hivyo imetupa mwanga kwamba kuna mhusika ndani yetu ambaye tunafanya naye kazi ndo kahusika"

"Kwahiyo hayo ndiyo maelezo ambayo unataka mimi nikawape wananchi na unategemea watanielewa? hivi kichwa chako kinafanya kazi sawa sawa? Usifanye nijute kukuweka kwenye hiyo nafasi!" Mheshimiwa raisi aliendelea kufoka mbele ya mzee mwenzake kwani jambo la kujibia hayo yote lilikuwa kwenye mkono wake yeye ndiyo maana alikuwa ana hasira isivyo kawaida.

"Kuna kiongozi ndiye amefanya hili tukio" kauli hii ya mkurugenzi ilimshtua na kumfanya amgeukia mwanaume huyo akiwa amemkazia macho.
"Ndiyo ni kiongozi ndiye amefanya huu mlipuko"
"Haiwezekani"

"Kwenye lile eneo watu wote ambao wanapita huwa wanakaguliwa kila sehemu mpaka mabegi yao kama yapo salama lakini hilo jambo huwa halifanywi kwa viongozi wakubwa tu pekee. Maana yake ni kwamba bomu liliingizwa kwenye moja ya begi la kiongozi mkubwa wa serikali ambaye gari yake na begi lake haliwezi kukaguliwa"

"Kwanini unahisi natakiwa kuyaamini maneno yako bwana Gulamu?" raisi aliuliza kwa mshangao.
"Unatakiwa kuniamini kwa sababu ya yule mwanasiasa Isaya Ndango"
"Huyo mbunge wa kawaida sana, sasa anahusikaje kwenye haya?"

"Yule bwana mdogo alikuwa na ushawishi mkubwa sana na inasemekana kwamba kuna baadhi ya viongozi wakubwa ambao alitaka kuwaumbua kwa mambo yao ya nyuma ya pazia ambayo wananchi walipaswa kuyajua. Sasa inasemekana kwamba alikuwa amewashawishi wanasiasa kadhaa ili wamuunge mkono ikiwemo waziri mkuu ambaye alikuwa tayari kumsapoti kuhakikisha waovu wanafichuliwa"

"Sasa leo ndiyo siku ambayo alitakiwa kuwasilisha majina ya watu hao pamoja na kuyazungumza yale waliyo yatenda mbele ya uma na ndipo tukio hilo lilipoweza kufanyika. Mpaka hapo hauwezi ukanipa imani yako mkuu kunisikiliza?" Maneno ya mkurugenzi, yalilikuna sikio la mheshimiwa raisi, aliomba wakae chini ili wayazungumze kinaga ubaga ili wajue, je yule panya aliye mfunga paka kengele alipona? Kama hakupona yuko wapi?

Episode 11 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 12.

"Kwahiyo unataka kuniambia kwamba?" Mheshimiwa raisi aliuliza wakiwa sasa wameketi chini.
"Mhusika ni kiongozi wa serikali, ndiyo maana nimekwambia kuna hatua tumepiga mkuu. Sio rahisi sana kuanza kumchunguza kiongozi yeyote wa serikali ila hapa tunahitaji msaada wako"

"Msaada upi unao uhitaji kwangu?"

"Naomba unipe hiyo ruhusa ya kufanya uchunguzi wangu hata kwa baadhi ya viongozi ambao nitawahisi kwamba wanahusika, ili hata siku wakigundua kwamba wanafuatiliwa wasije wakaanza kupiga kelele maana watajua ilikuwa ni ruhusa yako"

"Kwahiyo unataka kuniingiza kwenye ugomvi na viongozi wangu?"
"Hapana kiongozi"
"Ila maana yako ni ipi sasa?"
"Huenda ndiyo njia sahihi zaidi ya kuwapata hawa watu"

"Vipi kama ukimhisi mtu, ukamchunguza akagundua na baadae ukakuta sio yeye? Hiyo aibu mfaifichia wapi? Si mtaonekana kama shirika lenu ni la kubahatisha?"

"Na vipi kama tukifanya hivyo halafu tukakuta kweli wanahusika? Utatupa baraka zako kuwaadhibu?" Mkurugenzi alimbana mheshimiwa ambaye alibaki anamwangalia tu usoni, akakazia zaidi.

"Mheshimiwa najua hii siyo rahisi ila kuna muda kwa ajili ya amani ya nchi huwa yanahitajika kufanyika maamuzi magumu, na miongoni mwake ndiyo haya. Ni lazima baadhi ya watu wafanyiwe uchunguzi hususani wale ambao tutapata taarifa za awali kwamba wanahusika na haya mambo. Hapa nikutoe wasiwasi kwenye kitu kimoja, huwa hatumfuati kila mtu kwa sababu tumemhisi kwa macho, hapana."

"Tunacho kifanya, kuna vijana ambao ni mashuhuri sana kwa hizi kazi, ninawatuma kwenye maeneo husika ambapo wanaanza kazi mara moja. Kwenye hayo maeneo ambayo wanakuwepo ndiko ambako huwa tunazipata taarifa za awali, taarifa hizo ndizo ambazo tunazifanyia kazi na tukishakuwa na uhakika nazo ndipo tunaanza kuzichukulia hatua na ndiyo mpango uliopo kwa viongozi pia"

"Majina ambayo yataingia kwenye mkono wetu basi tutaanza kuyachunguza siku hiyo hiyo" raisi aliwekewa mpango uliopo mezani, sasa kazi ilibaki kwake kutoa ruhusa tu wanaume waingizwe kazini kuwasaka mpaka viongozi ambao kama wanahusika basi hawatakuwa na sehemu ya kuponea.

Alifikiria kwa muda kidogo kwa maana alikuwa anawajua watu hao kwa umakini wanapo amua kumfuatilia mtu hakuna sehemu ataweza kupona kama kweli anahusika vinginevyo awe ni mtu mwenye akili ambazo sio za kawaida.

Hata hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuruhusu hilo jambo lifanyike haraka iwezekanavyo.

"Na huyo mbunge kesi yake imeishia wapi?"

"Huyu nataka kwanza nifanye mpango wa kuipata familia yake, najua kama kuna siri alikuwa nazo basi lazima mkewe atakuwa na hizo taarifa kuhusu jambo hilo. Nina imani kama nikimpata mkewe basi atanisaidia sana, hivyo kesho nitatuma vijana ambao wataenda kuweka ulinzi huko kisha waweze kuja naye nimhoji mwenyewe" raisi alikuwa makini sana kumsikiliza ili naye ajue anaanzia wapi na hilo jambo.

"Huyo mbunge kwake ni wapi?"

"Alikuwa ni mbunge wa Lindi huko akiwa analiongoza jimbo la DAMU INAYO ISHI, hivyo hata familia yake inaishi huko"

"Basi hakikisha kila hatua ambayo mnafikia naipata taarifa haraka sana"
"Sawa kiongozi hilo halina shaka"

"Halafu kuna kitu hapa nataka kifanyike saivi"

"Nakusikiliza bosi"

"Andaa msafara nataka niende huko DOGMA TULIPO muda huu na Helikopta"
"Saivi?"
"Ndiyo"
"Mkuu hapana hiyo haiwezekani"
"Kwahiyo siku hizi una mpaka jeuri ya kuipinga amri yangu?"

"Hapana kiongozi, sina mamlaka ya kukupinga kwa lolote ndani ya nchi yako mwenyewe ila wewe hapo ni raisi wa nchi hii ambayo inayategemea maamuzi yako ili kuweza kusonga mbele. Ile sehemu imeshambuliwa muda sio mrefu, vijana wapo kazini ili kuhakikisha kwamba hakuna hatari yoyote inafanyika"

"Hatujui kama kuna tatizo lingine linaweza kutokea kule, bado hali ya usalama haijawa sawa, sasa kivipi raisi wa nchi uende kirahisi namna hiyo? Itakuwaje kama tageti ya mhusika wa hilo tukio ni wewe? Mimi moja ya kazi yangu kubwa ambayo niliapa kuifanya ni kukulinda wewe kabla kitu chochote hakijatokea pamoja na wananchi wako hivyo siwezi kuruhusu uingie kwenye hatari kirahisi sana namna hii kiongozi"

"Basi ulipaswa kulilinda bunge kwanza kabla ya kuniwazia mimi hapa. Nakupa nusu saa tu pekee nataka safari iwe tayari, nataka nikaongee na watu wangu nikiwa huko huko eneo la tukio hivyo andaa na vyombo vya habari vya Ikulu vitaripoti moja kwa moja kile ambacho nahitaji kukiwasilisha huko"

"Sawa mkuu" Gulamu Leopard hakuw na uwezo wa kubishana na kiongozi wake, licha ya kujua hatari kubwa ambayo ilikuwa huko alilazimika kufuata amri kwani kazi yake kubwa ilikuwa ni utekelezaji tu na kuhakikisha usalama wa kiongozi huyo mkubwa wa nchi ambaye hakuonekana kujali kabisa zaidi ya kuhitaji kuongea na wananchi wake siku hiyo ya uchungu sana kwenye maisha ya watanzania wengi.

Ndani ya jiji la DOGMA TULIPO ambapo pia ndio ulikuwa mji mkuu wa nchi ya Tanzania, watu walipewa taarifa kuwa mbali na hilo eneo kwani kiongozi mkuu wa nchi alikuwa anafika wakati wowote kuanzia muda huo. Vyombo vya ulinzi na usalama vilisafisha njia kwa muda mfupi na kuhakikisha ulinzi wa hali ya juu kila sehemu.

Raisi wa nchi alikuwa anaingia ndani ya eneo hilo, hicho ni kitu ambacho kiliongeza kelele nyingi sana kwa wananchi ambao walikuwa wanaripotiwa habari hizo moja kwa moja kutoka kwa waaandishi wa habari mbali mbali ambao waliruhusiwa kufika hapo kwa ruhusa maalumu.

Kwa mara ya kwanza kabisa, raisi Theobald Mnyika, alikuwa ameongozana na mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Tanzania. Kiongozi huyo wa usalama alikuwa anajulikana kwa watu wachache tu kwani hata uapisho wake ulikuwa ni wa siri kubwa, jambo hilo lilimpa raisi furaha kwa maana aliamini kwamba kuwa karibu na mtu huyo basi anakuwa ana uhakika na usalama zaidi kwa vile vijana wake wote wanakuwa wapo karibu na hilo eneo.

Mheshimiwa raisi alishuka baada ya helikopta hizo kutua chini umbali kidogo na lilipotokea shambulio hilo ndani ya uwanja mkubwa wa bunge. Alizingirwa na walinzi wengi mno huku akiwa anasikia kelele za nguvu za wananchi wakiwa wanamtaka kiongozi wao mkuu awape neno ili wajue ni kipi kilicho fanyika. Kabla hajapiga hatua hata moja alimgeukia mkurugenzi wa usalama na kumuuliza.

"Unahisi kipi napaswa kuwaambia?"
"Waambie kwamba hili sio shambulizi la kigaidi, kwa sababu hapa ndipo ilipo hofu yao kubwa. Wakishajua sio magaidi waliofanya hivi utarudisha amani kwa asilimia hamsini, hizo hamsini zinazo baki ndizo ambazo tunazifanyia kazi saivi"

"Una maanisha nini kuhusu hizo asilimia hamsini zinazo bakia"

"Mpaka sasa kuna watu saba wamekamatwa kwa kuhisiwa kuhusika na hili jambo, watu hao hawajaeleweka sana kwa maana wameonekana kwamba walikuwa karibu na hili eneo wakati mlipuko unatokea na hawajulikani walikuwa wanafanya nini hapa"

"Mhhhh haya mambo ya mhimu ulipaswa kunipa taarifa zake mapema sana"
"Nimepewa hizo taarifa na moja ya vijana wangu saivi mkuu"

"Wapo wapi kwa sasa?"

"Tumewahifadhi ndani ya ile nyumba ya MEMA YATAKUJA ambayo ulitujengea kwa ajili ya kuweka kambi ndogo ya siri ya shirika letu hapa DOGMA TULIPO"

"Safi sana, nahitaji kupata taarifa haraka baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi wangu na kama kuna mpuuzi akijulikana kahusika, nahitaji aletwe kwangu nimhoji mwenyewe, nitamfanya kitu kibaya sana" mheshimiwa alifurahia mwa namna kiongozi huyo wa usalama alivyokuwa makini lakini pia alionekana kuongea kwa jazba sana kuhusu hao wahusika ambao ilisemekana kwamba wamekamatwa kwa kuhusika na hayo mambo.

"Sawa kiongozi"

Baada ya kuwa na uhakika na cha kukizungumza, alianza kupiga hatua kuelekea sehemu ambayo ndipo mlipuko ulitokea. Alipewa gloves za kuvaa mikononi pamoja na miwani maalumu ili hata kama kuna chembe chembe za bomu zilibakia zisije kumuathiri kiongozi huyo mkubwa. Kila kilichokuwa kinafanyika hapo kilikuwa kinaonekana moja mwa moja nchi nzima, watu walikuwa wanasubiri kwa hamu sana kiongozi mkuu atoe neno lake.

Raisi alishangazwa na namna watu hao walivyo ifanyia hiyo sehemu ukatili mkubwa kiasi hicho kiasi kwamba palibaki tambalale kama uwanja wa mpira huku baadhi ya sehemu kukiwa na mashimo ambapo bila shaka mabomu ndimo yalitegwa. Aliinama na kuyachota majivu ya hiyo sehemu na kuyaweka kwenye kimfuko cheupe kwa mkono wake mwenyewe.

"Yamelipuka mabovu matatu kutoka sehemu ambazo zinaonekana kuwa na mashimo. Mhusika ambaye alitega mabomu haya alionekana kwamba alidhamiria sana kile ambacho alikuwa anakifanya ili kama ikitokea bomu moja halijalipuka basi mengine yanayo bakia yanamaliza kazi na kama likilipuka la kwanza ina maana yote yanalipuka na mlipuko unakuwa ni mkubwa zaidi.

Hii ndiyo sababu kubwa ambayo imefanya eneo hili kupata madhara zaidi ya vile ilivyotakiwa kuwa, mabomu matatu ndiyo yamehusika kuteketeza hili eneo" mkurugenzi Gulamu Leopard alielezea kuhusu uwepo wa mashimo hayo baada ya kuona kiuongozi wake amemkazia macho kama kuuliza hiki nini sasa mbona sielewi.

"Okay waambie waandae sehemu ya mimi kutolea hotuba fupi kisha tunaenda Ikulu ya hapa hapa sitaki kurudi Dar es salaam kwa sasa mpaka nipate mwafaka wa hili jambo"
"Sawa kiongozi"

Ndani ya dakika chache kila kitu kilikuwa kimeandaliwa vyema, mheshimiwa alipanda kwenye jukwaa dogo akiwa na walinzi wake, wanaume ambao walikuwa na sura za kazi haswa ila hakuwa mbali pia na Gulamu Leopard, huyu angekuwa na msaada mkubwa sana kwenye maelezo ambayo yangekosekana.

Mheshimiwa alikuwa tayari kwa ajili ya kuongea na watu wake kuhusu kile ambacho kilitokea, je unahisi anataka kuwaambia nini?

Episode ya 12 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 13.

"Ndugu wananchi wa nchi yangu pendwa. Nchi ambayo nimezaliwa, nchi ambayo imenikuza na kunilea, nchi ambayo imeniweka kwenye hii nafasi ambayo leo ninayo, nchi yenye wananchi wakarimu na wapenda amani zaidi duniani"

"Siwezi kuuliza kuhusu hali zenu, kama tu hali ya mimi raisi wenu ni mbaya kiasi hiki, naelewa hata nyie hamuwezi kuwa na hali nzuri kwa namna yoyote ile huko mliko ukizingatia tupo kwenye majonzi makubwa sana ambayo yanaandika historia nyingine mbaya sana ya nchi hii"

"Hapa mbele yenu nasimama na kuongea kama raisi ila pia kuna muda mwingine naongea kama ndugu na raia wa nchi hii kwa uchungu mkubwa sana ambao umenifanya nitumie masaa mengi sana kuwaomboleza ndugu zetu wapendwa mpaka nikaamua kuja huku mwenyewe licha ya watu wangu wa usalama kugoma kabisa kutokana na hali ya usalama wangu nimewaambia kitu kimoja tu"

"Kama watanzania hawana uhakika na usalama wa maisha yao maana yake haina faida ya mimi kuwa salama tena, nilichaguliwa kuwaongoza watanzania, niliingia Ikulu kuwalinda watanzania, mali zao pamoja na maslahi yao. Sasa kuna faida ipi ya mimi kubaki Ikulu kuangalia namna tausi wanavyo vutia huku watu wangu wakiwa kwenye kilio? Nikaona kabisa kwamba hii sio sawa, acha niongee na watu wangu, nilie nao pamoja lakini niwape japo neno la tumaini ambalo litafanya tuwapumzishe wenzetu kwa amani mbele za mwenyezi MUNGU" mheshimi akiwa mbele ya maiki kulihutubia taifa lake, alitulia kwanza kuvuta pumzi baada ya kuwapa wananchi maneno ya utangulizi. Akaendelea;

"Nchi hii haijawahi kushuhudia tukio la kutisha kama hili tangu ijipatie uhuru wake hivyo najiona raisi mwenye hatia nyingi sana tukio kama hili kutokea kwenye kipindi changu. Haimaanishi kwamba naombea lingetokea kwenye awamu nyingine? Lahasha! Maisha ya watanzania ni mhimu sana wakati wote ila imenifanya nijisikie kama sijatimiza ahadi yangu kubwa ya kuwalinda watu wangu ambao nawapenda sana kwa maisha yangu yote"

"Kitu ambacho natakiwa kuwaambia watanzania ni kwamba, natoa pole zangu za dhati sana, kwanza kwa familia za wapendwa wetu ambao wametangulia mbele ya haki. Najua wengi walikuwa na watu ambao walikuwa wanawategemea kuendesha maisha yao kwa namna moja ama nyingine. Hivyo nataka kwanza niwatoe hofu watu hao kwa maana kila familia ambayo mtu wao alikuwepo hapa ndani atapatiwa msaada wa kina na serikali ili kuhakikisha kwamba kupotea kwa wapendwa wetu sio sababu ya kubomoa familia ambazo wamezijenga kwa damu na jasho" alitulia tena kidogo kuvuta pumzi kabla ya kuendelea.

"Lakini pili nawapa pole wananchi wangu wa Tanzania kwa ujumla kwa kushuhudia moja ya vitu ambavyo sio bora mbele ya macho yanu, ila niwahakikishie tu kwamba vyombo vyetu vya usalama vinafanya kazi kwa umakini mkubwa sana ila kuna kosa moja dogo sana lilifanyika mahali" kauli yake ilimfanya mpaka mkurugenzi ashtuke, kiongozi huyo alianza kuongea mambo ambayo hawatakiwi wananchi kuambiwa kabisa. Kila mwananchi alibaki anasikiliza kwa umakini, kwa maana hiyo ilionekana kuwa sehemu ya muhimu sana kuweza kujua kwamba kosa lilikuwa ni nini hasa mpaka liyachukue maisha ya watu wengi kiasi hicho.

"Jambo la mhimu zaidi ambalo mnatakiwa kulifahamu ni kwamba, hili shambulio sio la kigaidi kama watu wengi wanavyo zisambaza hizi habari na kuanza kuwatishia wananchi ambao wanahisi nchi imeruhusu magaidi kuingia. Nawathibitishia kama raisi wa nchi kwamba nchi hii hakuna gaidi ambaye anaweza kuingia na kufanya jambo lolote, vyombo vya ulinzi vipo makini sana muda wota na....." mheshimiwa kabla ya kuendelea kuongea kuna mtu aliingilia maongezi hayo.

"Mheshimiwa mara ya kwanza umesema kwamba kuna kosa limefanyika mahali na wala sio magaidi basi wananchi wako wangetamani sana kujua ni kosa lipi hilo?" mwandishi wa habari mmoja ambaye alikuwa mita kadhaa na vifaa vyake aliropoka kwa kutumia kipaza chake bila kuruhusiwa. Kiitifaki alikuwa amefanya makosa makubwa sana mawili, kwanza kuongea mbele ya raisi bila kuruhusiwa lakini pili ni kuingilia mazungumzo ya mheshimiwa akiwa bado anaendelea kuongea.

Mheshimiwa aligeuka na kumwangalia kijana huyo kwa umakini kisha akatabasamu kwa mbali sana kiasi kwamba hicho kitu walikiona watu wa karibu sana kwani kwa kilicho tokea walijua huenda angepandwa na hasira sana.

"Kosa lililo fanyika ni kwamba kuna msaliti ndani yetu sisi wenyewe" kauli yake ilizalisha minong'ono kila mahali, kuanzia wale waandishi wa habari waliokuwa eneo lile, wananchi ambao walikuwa umbali mdogo na hilo eneo lakini pia hata wananchi ambao walikuwa wanashuhudia jambo hilo moja kwa moja kwenye runinga.

"Hii sehemu ina ulinzi mkubwa sana ambao hakuna kitu kinaweza kuingia humu ndani bila ruhusa kwa wakaguzi, kuna ulinzi mkali wa vifaa vya kisasa ila tatizo ni moja kwamba viongozi wakubwa wa serikali huwa hawakaguliwi wanavyo ingia hu....."

"Mzee tafadhali, haya mambo hayatakiwi kujulikana kwa wananchi, sio kila jambo lazima walijue mkuu" Gulamu Leopard alimsogelea bosi wake na kumpa huo ushauri maana alikuwa anavuka mipaka na kuanza kutoa siri zisizo takikana kwa wananchi.

"Hii ndiyo njia pekee" aliongea kwa hasira na kumfanya mwanaume huyo kurudi nyuma maana asingeweza kupingana na bosi wake.

"Hivyo majibu ya haraka haraka ni kwamba mhusika wa hili jambo ni kiongozi wa serikali hii hii ambayo naiongoza mimi. Nimechukizwa sana na jambo hili baada ya kugundua kuna viongozi wanawaza kuiteketeza nchi yangu ambayo silali nakesha kuipambania. Naahidi mbele yenu kwamba hayatazidi masaa sabini na mawili huyu mpuuzi atakuwa amepatikana na ataletwa hadharani ili aelekeze ni kwanini alifanya upuuzi mkubwa sana namna hii"

"Kwa nchi hii ambayo hairuhusu upuuzi kama huu hata mimi siwezi kukubaliana nao, mhusika au wahusika wa hili jambo nawahakikishieni kwamba watapata mateso makali sana hadharani mpaka wanakufa iwe kama mfano, na wale wote wenye magenge magenge yasiyo eleweka mtaani, wanaanza kukamatwa hivi ninavyo ongea, makundi kundi yasiyo eleweka muda huu polisi fanyeni kazi haraka sana. Lakini jambo la mhimu zaidi ni kwa mkuu wa majeshi na kanali wake, hakikisheni wananchi wangu wanakuwa salama kwa asilimia miamoja pamoja na mali zao"

"Kwa kumaliza, ndugu zangu watanzania, nawaombeni sana muwe wapole kwa kipindi hiki kigumu ambacho tunakipitia ili tuwapumzishe wenzetu salama"

"Namwaga majivu haya kama ishara ya heshima na kuwaaga mashujaa wetu ambao walikuwa tayari kuipigania ardhi hii kwa jasho na damu hivyo ili kuweka alama ya kumbumumbu bora ya taifa hili, majivu yote ya wapendwa wetu yatazikwa sehemu moja na kutengenezewa kaburi la kihistoria. Na haya yote yatatekelezwa na jeshi la wananchi hivyo familia za wahusika wakae tu nyumbani kwa ajili ya usalama wao nasi tutawafikia"

"Ahsanteni sana ndugu zangu,"
"MUNGU IBARIKI TANZANIA" alimaliza kwa kumwaga yale majivu ambayo alikuwa ameyaweka kwenye kile kimfuko cheupe na kuanza kuondoka hiyo sehemu baada ya kumaliza kile ambacho kilikuwa kimemleta hapo.

Hotuba yake fupi iliacha majonzi kwa watanzania wengi kila sehemu, kuna watu walimpa sifa kiongozi huyo kwa hotuba ya kuwapa tumaini wananchi wake huku wengine wakienda mbali sana na kudai kwamba kama itakuwa vyema basi hao wahusika wa hilo tukio wakamatwe haraka sana na waletwe mbele ya wananchi ili waeleze ni sababu zipi zimewafanya waliletee maafa makubwa kiasi hicho taifa lao wenyewe ambalo ndilo hasa limewakuza na kuwalea? Walitakiwa kutoa majibu, hata nyazifa zao kubwa walizokuwa nazo serikalini ilikuwa ni kwa ajili ya wananchi ambao ndio waliwaweka hapo.

LAZIMA YATARUDI
Pembezoni mwa mto mmoja ambao ulikuwa unaitenganisha morogoro na Dar es salaam, mto uliokuwa unaitwa LAZIMA YATARUDI, alikuwa anaishi mzee mmoja ambaye alikuwa ni mganga wa kienyeji eneo hilo. Mzee huyo licha ya umri wake kumtupa mkono lakini hakuwa anapitwa na maendeleo ya ukuaji wa teknolojia.

Alikuwa na kilinge chake ambacho alikuwa anakitumia kufanyia kazi zake za uganga lakini ndani ya nyumba yake kubwa ambayo iliezekwa kwa bati lililo choka, alikuwa amekaa na kijana wake ambaye ndiye alikuwa msaidizi wake kwenye hayo mambo yake ya uganga. Walitulia kuangalia taarifa hiyo kutoka kwa mheshimiwa raisi kwani siku hiyo hawakupata wateja kabisa kutokana na ile hali ambayo ilitokea.

Watu walikuwa wanaogopa hata kutembea wakiamini kwamba nchi yao imeweza kuvamiwa na magaidi ambao wanaweza kuwaingiza kwenye hali ya hatari sana. Alikohoa kidogo baada ya hotuba hiyo kuisha.

"Hii ni moja ya sababu ambayo imenifanya niichukie sana siasa kwenye maisha yangu na kuamua kuja kujificha huku mbali nisiwe karibu na huo ulimwengu wa watu wa namna hiyo"
"Mzee unamaanisha nini kusema hivyo?"

"Umekiona alicho kiongea raisi wako?"
"Ndiyo, si tulikuwa wote hapa"
"Umeyaamini maneno yake kwa asilimia ngapi?"
"Kwa utendaji wake wa kazi naweza kusema ni miamoja"
"Na hapo ndipo wananchi huwa mnafeli"
"Unamaanisha nini mzee?"

"Mwanasiasa akizungumza maneno kumi, basi ya kweli ni mawili. Hili jambo halijatokea kwa bahati mbaya, hiyo nina uhakika kabisa kwamba haiwezekani ikawa bahati mbaya. Lazima kuna maslahi ya watu wazito hapa yaliguswa na mmoja wa wale ambao walikuwepo mle ndani na sio bure, ila watakacho kifanya hapa ni kutafuta mtu wa kumrushia fuko la lawama baada ya hapo watamchafua sana na kwa vile wananchi huwa wanafungwa kiini macho wataamini kila kitu, hii inanisikitisha sana"
"Mzee wewe haya mambo umeyajulia wapi?"

"Mimi nimezaliwa zamani sana, hata kabla ya mimba ya baba yako kutungwa mimi nilikuwa na familia tayari, najua mambo mengi ambayo wewe mpaka usimuliwe. Tumia akili yako tu ndogo bunge lina wabunge wasio pungua miatatu tisini na pointi kadhaa, sasa kwanini bunge la leo walikuwepo wabunge wasio zidi hata miambili bila hata sababu maalumu?"

"Kuna mambo ambayo yalitokea miaka mingi sana iliyoweza kupita, kuna kila dalili yanaweza kujirudia tena kwa mara nyingine. Jina la huo mto mimi ndiye nililiasisi kwa kuamini kwamba mambo yale YATARUDI TENA na kweli naona yanaenda kutokea, nchi itakuwa kwenye wakati mgumu sana" Mzee huyo alimuachia mafumbo kijana wake huyo atumie akili yake kuweza kuyafumbua na kama akili yake haifanyi kazi kirahisi basi atajijua mwenyewe.

Yeye alienda kupumzika akidai kwamba mifupa yake inamuua isivyokuwa kawaida huenda ni uzee ulikuwa unamuandama sana namna hiyo.

Episode ya 13 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 13.

"Ndugu wananchi wa nchi yangu pendwa. Nchi ambayo nimezaliwa, nchi ambayo imenikuza na kunilea, nchi ambayo imeniweka kwenye hii nafasi ambayo leo ninayo, nchi yenye wananchi wakarimu na wapenda amani zaidi duniani"

"Siwezi kuuliza kuhusu hali zenu, kama tu hali ya mimi raisi wenu ni mbaya kiasi hiki, naelewa hata nyie hamuwezi kuwa na hali nzuri kwa namna yoyote ile huko mliko ukizingatia tupo kwenye majonzi makubwa sana ambayo yanaandika historia nyingine mbaya sana ya nchi hii"

"Hapa mbele yenu nasimama na kuongea kama raisi ila pia kuna muda mwingine naongea kama ndugu na raia wa nchi hii kwa uchungu mkubwa sana ambao umenifanya nitumie masaa mengi sana kuwaomboleza ndugu zetu wapendwa mpaka nikaamua kuja huku mwenyewe licha ya watu wangu wa usalama kugoma kabisa kutokana na hali ya usalama wangu nimewaambia kitu kimoja tu"

"Kama watanzania hawana uhakika na usalama wa maisha yao maana yake haina faida ya mimi kuwa salama tena, nilichaguliwa kuwaongoza watanzania, niliingia Ikulu kuwalinda watanzania, mali zao pamoja na maslahi yao. Sasa kuna faida ipi ya mimi kubaki Ikulu kuangalia namna tausi wanavyo vutia huku watu wangu wakiwa kwenye kilio? Nikaona kabisa kwamba hii sio sawa, acha niongee na watu wangu, nilie nao pamoja lakini niwape japo neno la tumaini ambalo litafanya tuwapumzishe wenzetu kwa amani mbele za mwenyezi MUNGU" mheshimi akiwa mbele ya maiki kulihutubia taifa lake, alitulia kwanza kuvuta pumzi baada ya kuwapa wananchi maneno ya utangulizi. Akaendelea;

"Nchi hii haijawahi kushuhudia tukio la kutisha kama hili tangu ijipatie uhuru wake hivyo najiona raisi mwenye hatia nyingi sana tukio kama hili kutokea kwenye kipindi changu. Haimaanishi kwamba naombea lingetokea kwenye awamu nyingine? Lahasha! Maisha ya watanzania ni mhimu sana wakati wote ila imenifanya nijisikie kama sijatimiza ahadi yangu kubwa ya kuwalinda watu wangu ambao nawapenda sana kwa maisha yangu yote"

"Kitu ambacho natakiwa kuwaambia watanzania ni kwamba, natoa pole zangu za dhati sana, kwanza kwa familia za wapendwa wetu ambao wametangulia mbele ya haki. Najua wengi walikuwa na watu ambao walikuwa wanawategemea kuendesha maisha yao kwa namna moja ama nyingine. Hivyo nataka kwanza niwatoe hofu watu hao kwa maana kila familia ambayo mtu wao alikuwepo hapa ndani atapatiwa msaada wa kina na serikali ili kuhakikisha kwamba kupotea kwa wapendwa wetu sio sababu ya kubomoa familia ambazo wamezijenga kwa damu na jasho" alitulia tena kidogo kuvuta pumzi kabla ya kuendelea.

"Lakini pili nawapa pole wananchi wangu wa Tanzania kwa ujumla kwa kushuhudia moja ya vitu ambavyo sio bora mbele ya macho yanu, ila niwahakikishie tu kwamba vyombo vyetu vya usalama vinafanya kazi kwa umakini mkubwa sana ila kuna kosa moja dogo sana lilifanyika mahali" kauli yake ilimfanya mpaka mkurugenzi ashtuke, kiongozi huyo alianza kuongea mambo ambayo hawatakiwi wananchi kuambiwa kabisa. Kila mwananchi alibaki anasikiliza kwa umakini, kwa maana hiyo ilionekana kuwa sehemu ya muhimu sana kuweza kujua kwamba kosa lilikuwa ni nini hasa mpaka liyachukue maisha ya watu wengi kiasi hicho.

"Jambo la mhimu zaidi ambalo mnatakiwa kulifahamu ni kwamba, hili shambulio sio la kigaidi kama watu wengi wanavyo zisambaza hizi habari na kuanza kuwatishia wananchi ambao wanahisi nchi imeruhusu magaidi kuingia. Nawathibitishia kama raisi wa nchi kwamba nchi hii hakuna gaidi ambaye anaweza kuingia na kufanya jambo lolote, vyombo vya ulinzi vipo makini sana muda wota na....." mheshimiwa kabla ya kuendelea kuongea kuna mtu aliingilia maongezi hayo.

"Mheshimiwa mara ya kwanza umesema kwamba kuna kosa limefanyika mahali na wala sio magaidi basi wananchi wako wangetamani sana kujua ni kosa lipi hilo?" mwandishi wa habari mmoja ambaye alikuwa mita kadhaa na vifaa vyake aliropoka kwa kutumia kipaza chake bila kuruhusiwa. Kiitifaki alikuwa amefanya makosa makubwa sana mawili, kwanza kuongea mbele ya raisi bila kuruhusiwa lakini pili ni kuingilia mazungumzo ya mheshimiwa akiwa bado anaendelea kuongea.

Mheshimiwa aligeuka na kumwangalia kijana huyo kwa umakini kisha akatabasamu kwa mbali sana kiasi kwamba hicho kitu walikiona watu wa karibu sana kwani kwa kilicho tokea walijua huenda angepandwa na hasira sana.

"Kosa lililo fanyika ni kwamba kuna msaliti ndani yetu sisi wenyewe" kauli yake ilizalisha minong'ono kila mahali, kuanzia wale waandishi wa habari waliokuwa eneo lile, wananchi ambao walikuwa umbali mdogo na hilo eneo lakini pia hata wananchi ambao walikuwa wanashuhudia jambo hilo moja kwa moja kwenye runinga.

"Hii sehemu ina ulinzi mkubwa sana ambao hakuna kitu kinaweza kuingia humu ndani bila ruhusa kwa wakaguzi, kuna ulinzi mkali wa vifaa vya kisasa ila tatizo ni moja kwamba viongozi wakubwa wa serikali huwa hawakaguliwi wanavyo ingia hu....."

"Mzee tafadhali, haya mambo hayatakiwi kujulikana kwa wananchi, sio kila jambo lazima walijue mkuu" Gulamu Leopard alimsogelea bosi wake na kumpa huo ushauri maana alikuwa anavuka mipaka na kuanza kutoa siri zisizo takikana kwa wananchi.

"Hii ndiyo njia pekee" aliongea kwa hasira na kumfanya mwanaume huyo kurudi nyuma maana asingeweza kupingana na bosi wake.

"Hivyo majibu ya haraka haraka ni kwamba mhusika wa hili jambo ni kiongozi wa serikali hii hii ambayo naiongoza mimi. Nimechukizwa sana na jambo hili baada ya kugundua kuna viongozi wanawaza kuiteketeza nchi yangu ambayo silali nakesha kuipambania. Naahidi mbele yenu kwamba hayatazidi masaa sabini na mawili huyu mpuuzi atakuwa amepatikana na ataletwa hadharani ili aelekeze ni kwanini alifanya upuuzi mkubwa sana namna hii"

"Kwa nchi hii ambayo hairuhusu upuuzi kama huu hata mimi siwezi kukubaliana nao, mhusika au wahusika wa hili jambo nawahakikishieni kwamba watapata mateso makali sana hadharani mpaka wanakufa iwe kama mfano, na wale wote wenye magenge magenge yasiyo eleweka mtaani, wanaanza kukamatwa hivi ninavyo ongea, makundi kundi yasiyo eleweka muda huu polisi fanyeni kazi haraka sana. Lakini jambo la mhimu zaidi ni kwa mkuu wa majeshi na kanali wake, hakikisheni wananchi wangu wanakuwa salama kwa asilimia miamoja pamoja na mali zao"

"Kwa kumaliza, ndugu zangu watanzania, nawaombeni sana muwe wapole kwa kipindi hiki kigumu ambacho tunakipitia ili tuwapumzishe wenzetu salama"

"Namwaga majivu haya kama ishara ya heshima na kuwaaga mashujaa wetu ambao walikuwa tayari kuipigania ardhi hii kwa jasho na damu hivyo ili kuweka alama ya kumbumumbu bora ya taifa hili, majivu yote ya wapendwa wetu yatazikwa sehemu moja na kutengenezewa kaburi la kihistoria. Na haya yote yatatekelezwa na jeshi la wananchi hivyo familia za wahusika wakae tu nyumbani kwa ajili ya usalama wao nasi tutawafikia"

"Ahsanteni sana ndugu zangu,"

"MUNGU IBARIKI TANZANIA" alimaliza kwa kumwaga yale majivu ambayo alikuwa ameyaweka kwenye kile kimfuko cheupe na kuanza kuondoka hiyo sehemu baada ya kumaliza kile ambacho kilikuwa kimemleta hapo.

Hotuba yake fupi iliacha majonzi kwa watanzania wengi kila sehemu, kuna watu walimpa sifa kiongozi huyo kwa hotuba ya kuwapa tumaini wananchi wake huku wengine wakienda mbali sana na kudai kwamba kama itakuwa vyema basi hao wahusika wa hilo tukio wakamatwe haraka sana na waletwe mbele ya wananchi ili waeleze ni sababu zipi zimewafanya waliletee maafa makubwa kiasi hicho taifa lao wenyewe ambalo ndilo hasa limewakuza na kuwalea? Walitakiwa kutoa majibu, hata nyazifa zao kubwa walizokuwa nazo serikalini ilikuwa ni kwa ajili ya wananchi ambao ndio waliwaweka hapo.

LAZIMA YATARUDI
Pembezoni mwa mto mmoja ambao ulikuwa unaitenganisha morogoro na Dar es salaam, mto uliokuwa unaitwa LAZIMA YATARUDI, alikuwa anaishi mzee mmoja ambaye alikuwa ni mganga wa kienyeji eneo hilo. Mzee huyo licha ya umri wake kumtupa mkono lakini hakuwa anapitwa na maendeleo ya ukuaji wa teknolojia.

Alikuwa na kilinge chake ambacho alikuwa anakitumia kufanyia kazi zake za uganga lakini ndani ya nyumba yake kubwa ambayo iliezekwa kwa bati lililo choka, alikuwa amekaa na kijana wake ambaye ndiye alikuwa msaidizi wake kwenye hayo mambo yake ya uganga. Walitulia kuangalia taarifa hiyo kutoka kwa mheshimiwa raisi kwani siku hiyo hawakupata wateja kabisa kutokana na ile hali ambayo ilitokea.

Watu walikuwa wanaogopa hata kutembea wakiamini kwamba nchi yao imeweza kuvamiwa na magaidi ambao wanaweza kuwaingiza kwenye hali ya hatari sana. Alikohoa kidogo baada ya hotuba hiyo kuisha.
"Hii ni moja ya sababu ambayo imenifanya niichukie sana siasa kwenye maisha yangu na kuamua kuja kujificha huku mbali nisiwe karibu na huo ulimwengu wa watu wa namna hiyo"

"Mzee unamaanisha nini kusema hivyo?"
"Umekiona alicho kiongea raisi wako?"
"Ndiyo, si tulikuwa wote hapa"
"Umeyaamini maneno yake kwa asilimia ngapi?"
"Kwa utendaji wake wa kazi naweza kusema ni miamoja"
"Na hapo ndipo wananchi huwa mnafeli"
"Unamaanisha nini mzee?"

"Mwanasiasa akizungumza maneno kumi, basi ya kweli ni mawili. Hili jambo halijatokea kwa bahati mbaya, hiyo nina uhakika kabisa kwamba haiwezekani ikawa bahati mbaya. Lazima kuna maslahi ya watu wazito hapa yaliguswa na mmoja wa wale ambao walikuwepo mle ndani na sio bure, ila watakacho kifanya hapa ni kutafuta mtu wa kumrushia fuko la lawama baada ya hapo watamchafua sana na kwa vile wananchi huwa wanafungwa kiini macho wataamini kila kitu, hii inanisikitisha sana"

"Mzee wewe haya mambo umeyajulia wapi?"

"Mimi nimezaliwa zamani sana, hata kabla ya mimba ya baba yako kutungwa mimi nilikuwa na familia tayari, najua mambo mengi ambayo wewe mpaka usimuliwe. Tumia akili yako tu ndogo bunge lina wabunge wasio pungua miatatu tisini na pointi kadhaa, sasa kwanini bunge la leo walikuwepo wabunge wasio zidi hata miambili bila hata sababu maalumu?"

"Kuna mambo ambayo yalitokea miaka mingi sana iliyoweza kupita, kuna kila dalili yanaweza kujirudia tena kwa mara nyingine. Jina la huo mto mimi ndiye nililiasisi kwa kuamini kwamba mambo yale YATARUDI TENA na kweli naona yanaenda kutokea, nchi itakuwa kwenye wakati mgumu sana" Mzee huyo alimuachia mafumbo kijana wake huyo atumie akili yake kuweza kuyafumbua na kama akili yake haifanyi kazi kirahisi basi atajijua mwenyewe.

Yeye alienda kupumzika akidai kwamba mifupa yake inamuua isivyokuwa kawaida huenda ni uzee ulikuwa unamuandama sana namna hiyo.

Episode ya 13 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 14.

Tina, mwanadada ambaye alikuwa maarufu sana hususani kwa wale wanawake warembo kwa sababu ya kumiliki duka kubwa la vipodozi pale Mlimani City, huku wadada hao warembo wakimuamini sana kwa upatikanaji wa vipodozi vyenye uhakika kabisa kutoka kwenye duka lake, sisi tulikuwa tunamfahamu kama jasusi ndani ya shirika la kijasusi la Tanzania yaani TBSIS.

Siku hiyo majira ya asubuhi baada ya kupewa amri na kiongozi wake kwamba aelekee ndani ya jiji la DOGMA TULIPO kuweza kuchunguza kile ambacho kilikuwa kimetokea huko, hakuwa na namna zaidi ya kuchukua ndege ili aweze kuwahi.

Ndani ya saa moja tu pekee alikuwa amefika ndani ya jiji hilo ambalo lilikuwa linakua kwa kasi sana kutokana na ule uwekezaji mkubwa ambao serikali ilikuwa inaufanya kwa wakati huo ndani ya hilo eneo. Mwanamke huyo alitua ndani ya eneo hilo akiwa kama mwandishi wa habari ambaye alikuwa na vielelezo vyote vya kumuonyesha kuwa bingwa wa kazi hiyo.

Kitu pekee ambacho alihisi kwamba anakikosa ni usafiri hivyo akalazimika kwenda kwenye moja ya yadi kubwa za magari ili apate nafasi ya kukodi gari ambayo angeweza kuitumia kwenye hiyo mizunguko yake ya ukusanyaji wa habari mbalimbali. Suruali nyeusi iliyokuwa imezichora nyama safi za umbo lake halikuwaacha salama wanaume mafisi wenye tamaa kwa kila wakionacho. Buti lililo utosha mwili lilikuwa sawa na mguu wake.

Juu shati nyeupe ilikuwa imetulia ndani ya mwili lakini kizibao kisafi kikawa kinapunguza maswali mengi kwani kilionyesha wazi kwamba wanamke huyo alikuwa ni mwandishi wa habari bila shaka, kizibao hicho kwa juu kilizibwa na skafu ambayo ilizungushiwa shingoni.

Macho yalifunikwa na miwani midogo myeupe huku kichwani kukiwa na kofia yenye rangi sawa na suruali, mkononi akiwa na kimkoba kidogo bila kusahau kamera kubwa ambayo aliivaa kwenye mabega yake.

Aliulizia sehemu ambayo aliona kwamba anaweza kupata usafiri wa kukodi, zikitumika dakika kumi tu akawa amefikishwa eneo ambalo alitakiwa kuacha vielelezo vyake rasmi kisha akawa amepewa gari ambayo alidai angeitumia kwa wiki nzima. Baada ya kuipata gari hiyo, aliweka vitu vyake ndani na kuanza kuelekea eneo lilipo bunge.

Akiwa umbali wa kutosha kufika hilo eneo, alizima gari na kutulia kwanza akiwa anawaza kwamba ni wapi ambapo anatakiwa kuanzia baada ya kufika eneo hilo. Akiwa ametulia hapo, kwa mbele kidogo kulikuwa na mgahawa wa kisasa ambao haukuwa na watu wengi kwa wakati huo, aliona kuna mwanaume anashuka kwenye boda boda akiwa na koti na kofia kichwani vyote vikiwa vyeusi.

Akajikuta anavutiwa kuendelea kutazama kitu ambacho alikuwa anakifanya mwanaume huyo ambaye alifika mapokezi na kununua kitu, kisha akabeba tishu nyingi na kuzitumia kujifutia kisha akatumia tishu hizo kuingiza mkono mfukoni akiwa amezizuzungusha kwenye mkono wake, alitoa kitu ambacho Tina hakukiona kwa maana kilikuwa kimezungushiwa tishu, kisha akakitupia kwenye dustbin.

Alivyofika nje aligeuka huku na huko kuona kama kuna mtu alikuwa amemuona, alivyo jiridhisha hakuna aliye muona akaigusa kofia yake kidogo hapo ndipo Tina akagundua mwanaume huyo alikuwa amejifunika barakoa ambayo ilikuwa nyeusi kama kofia yake. Mwanaume huyo alionekana kutoa simu yake mfukoni akionekana kutaka kuipiga mahali sehemu ambayo Tina hakuijua.

Taratibu Tina alichomoa kisu kwenye begi lake na kukichomeka kwenye buti lake kisha akatoka ndani ya ile gari yake na kuanza kuelekea ile sehemu ambayo alielekea yule mwanaume. Baada ya kuzunguka mpaka nyuma ya ule mgahawa, aligundua kwamba kulikuwa kuja njia ambayo iliendelea kushuka chini hivyo akawa anaifuata kwa kukimbia maana aliona kama anampoteza huyo mtu wake.

Mita miamoja mbele aliona kuna mtu anaruka ukuta mahali na kuingia ndani, alikimbia kwa kasi na kudunda juu ya ukuta huo akatua ndani kwa sarakasi bila kutoa sauti mithili ya paka. Mwanaume aliyekuwa ameingia humo alikuwa anakaribia kuufungua mlango ambao ulikuwa mbele yake ila alihisi kama kwa nyuma yake kuna mtu hivyo akageuka haraka sana akiwa na kisu kikali na kirefu sana kwenye mkono wake.

Wakati anaingia hapo Tina kuna kosa hakutaka kulifanya, aliitoa miwani yake usoni na kujifunika kitambaa cheusi, anaelewa kwamba maeneo kama hayo huwa yanakuwa na kamera nyingi maeneo mengi hivyo kupita hivi hivi ingekuja kumletea madhara kwa baadae japo alikuwa anahisi kwamba kama mtu huyo ni mhalifu basi hawezi kuwa na kamera hapo ila kwake thadhari ilikuwa ni mhimu sana.

"Jieleze wewe ni nani kabla sijafanya maamuzi ya kukubaka hapa saivi" mwanaume huyo aliongea kwa sauti ya mamlaka akiwa ndani ya barakoa, aliyesimama mbele yake licha ya kujifunika usoni ila bado alikuwa anaonyesha kabisa kwamba ni mwanamke. Tina badala ya kumjibu mtu huyo alimuonyeshea kidole cha kati kumtusi.

Mwanaume huyo aliona kama huyo dada alikuwa hamjui, alimsogelea kwa nguvu na kisu chake mkononi ili amzamishie tumboni ila haikuwa rahisi sana kama yeye alivyokuwa anahisi, Tina alijivuta nyuma kidogo kisu kikapita na hewa, mwanaume huyo alizunguka na teke kwa hasira.

Tina aligeuka na kudunda chini kwa mkono wake mmoja, alivyojivuta na kusimama alijibinua kwa mguu wake wa kushoto ambao ulitua kwenye bega la mwanaume huyo, akayapokea maumivu na kuhitaji kurudisha kwa hasira ila alichelewa ule mkono wake ambao ulikuwa na kisu wakati anaurusha Tina akainama akiwa anakwepa kisu hicho huku akichomoa cha kwake ambacho alikizamisha kwenye kifundo cha mkono cha mwanaume huyo.

Alihitaji kupiga kelele, lakini alishtukia anapigwa buti zito la kwenye koromeo akawa hana uwezo wa kutoa sauti zaidi ya kuhema kwa nguvu macho akiwa kayatoa na kisu chenyewe kikiwa kimemponyoka. Tina alijua humo ndani huenda kuna wengine hivyo alitakiwa kuwaangalia kwanza kabla hajaingia kwenye matatizo.

Alimpiga mwanaume huyo ngumi nzito ya shingo, akapoteza fahamu, akamtoa barakoa usoni, sura hiyo hakuwa anaifahamu kabisa, ilikuwa ngeni kwake. Alimsachi kwenye mfuko wake, akakutana na kikaratasi kidogo na simu, hakuwa na muda wa kuviangalia zaidi ya kuviweka na kivihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae. Aliitoa simu yake na kutuma meseji kuhitaji msaada na location ya eneo ambalo alikuwepo kwa wakati huo kwani kuna washukiwa ambao walikuwa wanahisiwa kuhusika na huo mlipuko alikuwa amewakamata.

Alipo hakikisha ujumbe umefika alipokuwa ameutuma, sasa taratibu akawa anasogea ndani baada ya kugundua kwamba mlango huo haukufungwa. Sebuleni palikuwa na watu wawili ambao walikuwa wanafanya mapenzi kwa fujo sana. Alicho kifanya ni kutoa gesi kwenye mfuko na kuipulizia sebuleni hapo kisha yeye akajibanza Konani, haikupita hata dakika moja watu hao wakaanza kukohoa na kuomba msaada kwa makelele ila hawakufanikiwa kwani walidondoka na kuzimia hapo hapo.

Zile kelele ziliwaamsha wenzao ambao walikuwa chumba kingine, wanaume wanne walifika hapo huku wakiwashangaa wenzao wakiwa uchi yaani wa kike mmoja na wa kiume mmoja. Hawakujua shida nini mpaka walipokuja kushtuka kwamba hapo sebuleni palikuwa na gesi, walishtuka baada ya hewa kuwa nzito na kuanza kukohoa ila huenda walikumbuka hayo wakiwa wamechelewa sana kwani hakuna hata mmoja ambaye alifanikiwa kukimbia wote wakadondoka chini na kupoteza fahamu hivyo watu saba wakawa kwenye mkono wa Tina kirahisi sana.

Tina alikuwa amejifunika vyema sana hivyo gesi hiyo haikumdhuru kabisa yeye, alicho kifanya alianza kukagua chumba kwa chumba ndani ya hiyo nyumba. Aligundua kwamba watu hao walikuwa wakiishi hapo kwa muda kidogo na huenda mipango yao mingi ilikuwa inafanyika ndani humo humo. Alitafuta kwenye vyumba vyote mpaka alipofika kwenye chumba ambacho kilionekana kuwa cha mkutano wa watu hao.

Kitu cha ajabu ambacho mpaka wakati huo kilimpa maswali ambayo hayakuwa na majibu ni kwamba hakuona dalili yoyote ya simu sehemu zote zaidi ya ile ambayo aliipata kule nje kwa mtu mmoja ambaye alimzimisha. Ndani ya chumba hicho palikuwa na ubao ambao ulikuwa umechorwa ramani ya bunge la nchi ya Tanzania na muda ambao bunge hilo lilitakiwa kulipuliwa, aligeuka kuangalia kwenye meza kubwa pembeni palikuwa na ramani nzima ya hilo jengo la bunge.

Aliduwaaa sana ila alicho kifanya alikifanya ni kuibeba ramani hiyo na kuizamisha kwenye kifua chake halafu akaenda kufuta kila kitu kwenye ule ubao, kabla hajamaliza kufuta alisoma maneno ambayo hakuelewa maana yake "HIM DID IT ALONE (OFFICIAL WITH THE SUITCASE)" alihakikisha ameyakariri hayo maneno kwenye kichwa chake ambayo yalikuwa ni kama ishara kwa mhusika wa tukio hilo.

Akikagua kila sehemu kuhakikisha haachi ushahidi wowote ule wa maandishi maana hizo siri hazikuwa nzuri sana kufika kwenye mikono ya kila mtu hivyo akafuta kila kitu. Hakuwa na wasiwasi kabisa kuhusu kamera za humo ndani alijua mipango ya hatari kama hiyo watu hao wasingeweza kuifanya wakiwa wanarekodi kwa maana ingekuja kula kwao wao wenyewe kwa baadae.

Akiwa anaangalia baadhi ya vitu humo ndani, alisikia vishindo vya magari nje ya nyumba hiyo ndiyo akakumbuka kuangalia simu yake kwani aliomba msaada wa watu kuja kuwabeba washukiwa wa tukio hilo. Alikutana na jibu kutoka mwenye namba ambayo aliiomba msaada huo likiwa limeandikwa "NOTED" akajua basi hapo nje ni wavaa suti walikuwa wamefika.

Yeye hakutakiwa kabisa kukutwa na hao watu kwani alikuwa ni undercover (mpelelezi wa siri) ambaye hakuwa akijulikana hivyo kama watu hao wangemkuta hapo basi naye angejumuishwa kwenye huo msala moja kwa moja. Alifungua dirisha ambalo lililiwa linatokezea upande wa pili na kurukia nje kisha akalifunga vyema na kutowekea upande huo wa nyuma wa nyumba hiyo, mbele wanaume wa kazi wakiwa wamefika.

Safari yake Tina iliishia kwenye ule mgahawa ambapo alienda na kununua maji akiwa ameshatoa kitambaa usoni na kuwa kama mteja wa kawaida tu, alichukua tishu ambazo alijifanya kwamba anataka kuzitumia kufutia maji yake mkononi. Alizirushia zile tishu kwenye dustbin lakini alifanya makusudi kwa kuirushia na simu yake.

Alifanya hivyo ili kama kuna mtu anamfuatilia asiweze kuhisi chochote, alikuwa makini sana mwanamke huyo. Baada ya kuhakikisha hilo alizamisha mkono kuchukua simu yake ila alitoka na vitu viwili kwenye mkono wake, simu pamoja na rimoti ndogo ambavyo vyote aliviingiza mkononi japo alishtuka sana kuona rimoti ya aina hiyo eneo kama hilo kwani ilikuwa ni hatari mno.

Unahisi ni kipi kipo kwenye hiyo rimoti? Nini safari yetu humu ndani?

Episode ya 14 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 15.
Tina alihakikisha hakuna ambaye anazisoma alama zake za nyakati kabisa kwa kile ambacho alikuwa anakifanya pale, alijongea taratibu kwa mwendo wake wa madaha mpaka alipofika kwenye gari yake, aliingia kwa mapozi sio kwamba alikuwa anauza sura bali kama kuna mtu alikuwa anaangalia hapo asiweze kuhisi chochote kwake zaidi ya kumuona kama mwanamke wa kawaida tu asiye na maajabu yoyote yale kwenye hiyo dunia zake zaidi ya kuhadaika na urembo wake usoni.

Baada ya kutulia kwenye gari, aliinamana na kuchomoa kisu chake kwenye buti lake la mguuni
"Oooh shiiit!" alitamka baada ya kugundua kwamba buti hilo kwa ndani lilikuwa na damu, hapo ndipo alikumbuka kwamba alimjeruhi mtu ndani ya ile nyumba ambako ametoka na hakusafisha kabisa kisu hicho hivyo akawa amekiweka kwenye buti moja kwa moja ndiyo maana aliweza kuchafuka damu namna hiyo japo zilikuwa hazionekani kwa nje, basi akajisafisha na kuanza kutoa kitu kimoja kimoja kwenye mifuko yake.

Kwanza alianza na ile rimoti ambayo aliipata kwenye ule mgahawa, alivyo iangalia kwa umakini aligundua kwamba ni rimoti ambayo inatumika kuruhusu bomu kulipuka au kulifanya lisilipuke kabisa. Alijikuta anashika moyo wake kwa maana hiyo huyo ndiye mtu ambaye amelipua sehemu ile kwa kuitumia hiyo rimoti, akawa amepata jibu kwamba huenda mwanaume huyo wakati anafanya tukio lake alivaa gloves na kuzivua baada ya kuiweka rimoti hiyo mfukoni lakini pia wakati anataka kuitoa hakutaka kuacha alama za vidole ndiyo maana aliamua kutumia tishu kuitoa mfukoni.

Kuhusu hiyo rimoti jibu alikuwa amelipata sasa vipi kuhusu simu na kile kikaratasi ambacho alikikuta kwenye mfuko wa yule bwana? Alikitoa haraka sana pamoja na simu. Aliifungua simu, akakutana na nywila ambazo alitakiwa kuziingiza ili awe na uwezo wa kuitumia. Kwake hilo lilikuwa ni tatizo dogo sana ambalo halikuhitaji hata kuumiza kichwa chake.

Aliichukua laptop yake kwenye siti ya nyuma ya gari hiyo, akaiunganisha na simu hiyo ambapo ilimchukua dakika tano tu pekee akawa ameifungua. Kitu cha ajabu kwenye simu nzima alikutana na namba moja tu pekee, alishtuka na kuiangalia simu vizuri hapo akagundua kwamba simu hiyo ilikuwa ni mpya kabisa na huenda hiyo ilikuwa siku ya kwanza kabisa kuweza kutumika.

Aliingiza namba hiyo kwenye mifumo yao ya kijasusi ili aweze kuitambua kwamba inatokea wapi au mmiliki wa hiyo namba ni nani, alishangazwa baada ya kuona namba kama hiyo haijawahi kutumika popote pale wala haipo kwenye mifumo ya usajili bado, maana yake alikuwa anapoteza muda wake tu. Alichoka, hapo sasa ndipo akakumbuka kwamba kuna kikaratasi kingine ambacho kilikuwa kwenye mfuko wake.

Alikitoa ili kuweza kusoma kile ambacho kilikuwa kimemeandikwa.
"THE BLUE OPERATION REACHING RWANDA. THE TEN IMAGINARY LIFE TIME. ACCOMPLISHED " Hayo ndiyo maneno ambayo yalikuwa yameandikwa ndani ya karatasi hiyo, licha ya mwanamke huyo kuwa maridadi sana kwenye hiyo kazi yake ila kwenye hayo maneno hakuambulia chochote kile akawa anayarudia kila sekunde kuona kama anaweza kupata mwangaza wowote ule lakini hakutoka na kitu chochote kile.

Swali lake kilibakia ni kwamba kama yule ndiye ambaye alikuwa amelipua ile sehemu, muda wote huo alikuwa anatafuta nini kwenye lile eneo? Au alikuwa anaangalia kama kuna masalia ya ushahidi? Kidogo hii ilimuingia akilini, alihisi huenda mtu huyo alikuwa anahitaji kuhakikisha kwamba hakuna ushahidi ambao unabakia ndani ya hilo eneo.

Aliichukua simu kwa ajili ya kuweza kumpigia kiongozi wake Gulamu Leopard, aliitafuta namba yake na kupiga, wakati anampigia kiongozi wake huyo, yeye alikuwa njiani kuelekea Ikulu ambako aliitwa na mheshimiwa raisi, aliipokea simu hiyo.
"Nakusikiliza"
"Mkuu nimeweza kuwakamata vijana ambao nimekuomba msaasa na nashukuru umewatuma vijana wamefika kuwabeba wale watu"
"Unataka kuniambia wamekuona?"
"Hapana mkuu siwezi kuruhusu jambo kama hilo litokee"
"Safi na hungera kwa kazi nzuri, kuna msaada wowote ambao una uhitaji?"
"Ndiyo mkuu lakini pia kuna jambo la mhimu sana ambalo nataka kukwambia"
"Nakusikiliza" Tina aliyaangalia sana maandishi ya kwenye lile karatasi, alitaka kuyatamka ila akasita sana na kugeuzia macho eneo ambalo lilikuwa na rimoti ile.

"Nimeipata rimoti ambayo ndiyo imehusika kulilipua hilo jengo" nadhani hata Mr Gulamu alipatwa na mshangao, dakika nzima alikuwa yupo kimya hajajibu lolote lile kutoka kwenye hayo maelezo ambayo alikuwa ameambiwa.
"Una uhakika na unacho kisema?"
"Ndiyo mkuu"
"Hiyo rimoti unayo wewe?"
"Ndiyo bosi"
"Basi hakikisha unaitunza kwa umakini mkubwa bila mtu yeyote kujua mpaka tukikutana usiku nikifika huko"
"Sawa mkuu"
"Ni msaada upi unauhitaji?"
"Nahitaji video za marejeo kabla bunge halijalipuka"
"Ni hilo tu?"
"Ndiyo mkuu"
"OK nakutumia saivi, sijapata muda wa kutulia na kuzitazama"
"Nashukuru mkuu" alikata simu baada ya kuwa na uhakika wa kuzipata video hizo kwani alihitaji kujua kipi kiliendelea kabla ya hiyo tukio ndani ya hilo eneo la bunge.

Akiwa kwenye mawazo mazito, ujumbe uliingia kwenye simu yake, basi ikamlazimu kuufungua, hapo ndipo akakutana na mfululizo wa matukio ambayo yalitokea ndani ya bunge kabla ya bunge kuanza. Aliweka video ya dakika thelathini kabla ya bunge hilo kuanza hapo ndipo angepata chochote ambacho kilifanyika.

"They are very smart (wapo smati sana)" aliongea hapo kumaanisha wale wahusika wa lile tukio ambalo lilikuwa limetokea kwani hakuona dalili yoyote ile ya kuwepo kwa kitu chochote cha kufanya apate lolote lile. Zilikuwa zinaonekana shughuli za video za shughuli za kawaida tu ambazo zilikuwa zinaendelea ndani ya hilo eneo.

Aliamua kuangalia video za sehemu zingine ikiwa ni kama kuupa muda nafasi ya kukimbia kwa kasi, video hizo zilikuwa zinaonyesha maeneo ambayo walikuwa wanayatumia wabunge kupumzikia. Aliwaona wabunge wawili wakiingia sehemu moja na kukaa huko kwa muda kidogo ila kati ya wabunge hao alimuona Isaya Ndango ambaye alikuwa ni mbunge pendwa zaidi ndani ya nchi ya Tanzania.

Aliona ni mazungumzo ya kawaida tu ila aliikuza hiyo sura ya mwanasiana huyo na kuimechisha na jina lake, habari zake zote zikajitokeza kwa maandishi hivyo akawa anasoma soma kuhusu mwanasiasa huyo ambaye alionekana kuwa na mtazamo chanya sana juu ya maisha ya nchi na kizazi kijacho kwa ujumla.

Akiwa anajiandaa kuachana na hiyo habari, alishtuka kidogo baada ya kumuona William Ivan Msoka ambaye alikuwa ni waziri mkuu wa nchi yake akiingia ndani ya hilo eneo. Haikuwa kawaida sana waziri mkuu kuingia maeneo ya faragha kama hayo na kufanya majadiliano ya siri na ilikuwa ni kinyume na sheria, sasa kwanini waziri huyo aende huko?

Inamaana kuna mambo ya siri ambayo walipaswa kuyaongea watu hao watatu, hapo palimfanya kuwa makini sana na alichokuwa anakiangalia hapo kwa macho yake. Dakika kama tano tu aliona waziri mkuu huyo akiwa anatoka humo ndani akiwa na tabasamu tele kwenye uso wake. Dakika mbili zilizo fuatia pia mbunge Isaya Ndango alitoka akiwa na tabasamu tele usoni kwake ila yule mwenzao mmoja alikuwa hajatoka mpaka wakati huo.

Tina alishangaa inawezekana vipi wamuache mwenyewe? Alitamani sana angeona kilichokuwa ndani ila kwa bahati mbaya sana ndani hakukuwa na kamera kabisa ili kulinda faragha za watu. Hivyo njia pekee ambayo ilikuwa imebakia hapo ni kuweza kuangalia kamera za nyuma ya jengo ambalo watu hao watatu walikuwep.

Ni kweli kwenye kamera hizo aliweza kumuona mbunge huyo akitoka, yeye uso wake ulikuwa ni tofauti sana na wenzake maana alikuwa na sura yenye majonzi isiyo na furaha kabisa. Baada ya kufika nje, aliliangalia jengo la bunge kwa masikitiko makubwa akishika njia ya sehemu ya kupaki magari bila shaka alikuwa anataka kutoka nje kabisa ya jengo hilo.

"Ooooh no! Oooo! My God! kwamba huyu alijua kinacho tokea? Kama hakujua ni kwanini yeye aondoke tena akiwa kwenye sura kama hii? Kipi kimemfanya aliangalie jengo hili kwa masikitiko huku akitoka hapo na baadae kidogo jengo linalipuka? Maana yake huyu anajua kitu, huyu anajua nini kinaendelea"

"Nina hakika amepona huyu hajafa, kama kapona atakuwa wapi saivi? Huyu atanisaidia sana kunipa majibu yangu ila kuna kazi moja ndiyo ambayo natakiwa kuifanya, huyu natakiwa kumpata kwanza kabla ya mtu yeyote mwingine hajajua kwamba yupo hai naweza nisimpate tena"

Mwanamke huyo alifurahi sana, alikuwa ameingia kwa muda mchache ndani ya hilo eneo na alikuwa ameshapata mwangaza wa kueleweka juu ya hiyo kesi yake. Alirudisha macho yake kwenye simu hiyo na kupeleka mbele matukio mpaka wakati ambao bunge lilikuwa linaanza, mbunge Isaya Ndango wakati anasimama ili aanze kutoa maoni yake alikonyezana na mheshimiwa waziri mkuu.

"Yes, it's them" Tina aliongea kwa furaha mno, akiwa na uhakika wa mwanzo mzuri wa safari yake ya muwachunguza watu hao na majira ya usiku wakati wa kukutana na kiongozi wake alikuwa na taarifa za kutosha za kumpatia na aliamini kwamba mhusika angepatikana muda mfupi sana uliokuwa unakuja.

Je ni kweli kuhusu hayo ambayo anayafikiria Tina, watampata huyo mtu kirahisi sana hivyo?

Episode 15 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mtu akiitaka kwa ajili ya Muvie unatoa ruksa
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 2.

Tina alibaki amejiinamia akiwa anayatoa machozi ambayo ni kama alikuwa anayatoa baharini kwa maana hakuna kitu cha maana chochote ambacho yangemsaidia. Nafsi yake ilikuwa inamuuma sana, watu hao ukatili ambao walikuwa wanamfanyia ulikuwa umevuka mipaka, licha ya kuwa mpelelezi mahiri lakini kifo alikiogopa mno kwa maana naye alijiona kuwa mwanadamu wa kawaida kama vile walivyokuwa wengine.

Aligeuzwa kuwa chombo cha starehe kwa wanaume hao ambao hata hakujua kuhusu afya zao, ila kilicho kuwa kinamuumiza zaidi ni yeye kuwa kama dala dala ambayo abiria wangepanda hapa na kushuka pale asielewe mwisho wa kituo chake ni wapi.

Kumbukumbu zake zilishindwa kumkumbusha kabisa kwamba alikuwa yupo ndani ya eneo gani mpaka wakati huo, alichokuwa anakumbuka ni kwamba mara ya mwisho alikuwa na mwanaume mmoja kitandani wakifanya mapenzi. Hakuwa na nguvu za kumzuia yule mwanaume kumfanya kile ambacho alikuwa ameazimia kukifanya kwa maana mwili wake haukuwa na nguvu kabisa zaidi ya mwili huo kuzidiwa na hamu ya mapenzi ambayo hata yeye ilimshangaza sana kwamba ilitoka wapi.

Hakujua kwamba ni kipi kiliendelea mpaka pale alipokuja kushtuka akiwa ndani ya hicho chumba, sasa maswali mengi yalikuwa yanapita kwenye kichwa chake kwamba alikuwa wapi ila alikata tamaa kwa maana swali hilo alikuwa amejiuliza mara nyingi sana na hakuwa na jibu wala mtu wa kumpa hilo jibu.

Mara ya kwanza aliwahi kuchukulia mambo kawaida sana hivyo akataka kujaribu kutoroka ndani ya jengo hilo ambapo alifanikiwa kufungua mlango tu, baada ya kutoka nje ya mlango wa chumba alicho kuwepo, alikutana na mwaaume mmoja ambaye alikuwa kwenye vazi la bukta huku kifua chake kikiwa wazi.

Alihisi anaweza kumdhibiti huyo mtu kisha angetoka lakini kilicho mkuta, alitaka kupoteza jicho lake ambalo lingeharibu urembo wake wote ambao alikuwa nao. Mwanaume huyo alimpiga vibaya bila kujali kwamba huyo alikuwa ni mtoto wa kike na ndiyo hiyo siku ambayo alipangiwa ratiba ya kulala na wanaume watano kila baada ya siku mbili kwa ukaidi ambao alikuwa ameufanya.

Alibakwa kwa nguvu sana siku ile na hicho ni kitu ambacho kwenye maisha yake hawezi kukisahau kabisa hata kama angeamshwa ndotoni, maana maumivu ambayo alikuwa anayapitia kwenye moyo wake yalimfanya ahisi kwamba yeye siyo mwandamu wa kawaida akaishia kumlaumu sana MUNGU.

Siku ile ambayo alikamatwa akihitaji kutoroka, alishuhudia mwenzake mmoja akipigwa kisu cha moyo mbele yake baada ya kubakwa, kisha watu hao wakakipasua kichwa cha mwanamke huyo kwa risasi nyingi ikiwa ni kama onyo kwake kwamba kama akija kujaribu tena kufanya huo ujinga wake basi angefanywa kile kile ambacho mwenzake alifanywa japo yeye hatauawa ila angepitia mateso ambayo angetamani yeye mwenyewe kutafuta nafasi ya kujiua.

"Uko wapi kaka?!" aliongea kwa sauti ya kichovu ambayo imekosa furaha na nuru kwenye uso wake. Alitamani mtu ambaye alikuwa akimuita kaka angekuwa karibu yake wakati huo ambao yeye hakuwa na tumaini lolote lile la kuwa salama. Kumbukumbu zilimbeba na kumrejesha mbali sana akiwa na huyo ndugu yake wa kiume.

"Dada bado unayo nafasi ya kufanya maamuzi yako upya, kwa sasa unatakiwa uwe na familia yako utulie na kulea watoto wako, haya mambo ebu kaa nayo mbali dada yangu, maisha ya huku siyo ya kawaida halafu wewe ni mtoto wa kike" mdogo mtu alikuwa anamshauri dada yake aweze kuacha kile ambacho alikiamua ili akatengeneze familia yenye furaha siku zote.

"Calvinjr unajua kwanini niliichagua hii kazi?"
"Hapana"
"Basi unatakiwa kujua kitu kimoja, dada yako ni mwanamke jasiri sana ambaye anaipenda sana nchi yake, mimi sijaja kwenye hii kazi kwa kubahatisha bali nimeamua kukabiliana na watu ambao wanaikosesha nchi yetu amani. Watoto wa kike wananyanyaswa sana lakini hakuna hatua kubwa zinazo chukuliwa, kuna watu kwa maslahi yai wanaifilisi hii nchi na sioni watu wakiwa na uchungu kwenye haya mambo mdogo wangu"

"Nadhani una ujua kwa ukubwa uwezo wa dada yako, mimi sio yule mwanmke wa kushinda na vipodozi mezani bali mimi ni yule mwanamke ambaye nimejitoa kulipambania taifa langu. Kama MUNGU akijaalia basi familia nitakuwa nayo wakati ujao, maana hata mama huwa ananisimbua sana kwa hilo" dada mtu ambaye alikuwa anafanya kazi ya upelelezi alionyesha msimamo kwa mdogo wake kwamba hayupo tayari kuachana na hiyo kazi bali alitaka kuwafichua wote ambao walikuwa wanayafanya maovu.

"Sister please naomba usiende huko, tumezaliwa wawili tu unaendaje pekeyako kwenye nchi ambayo haujawahi hata kuishi? Haujui watu wake wanaishi vipi? Na mama unamuaga unaenda wapi? Vipi kama ukipatwa na tatizo huko unahisi nani atakusaidia? Nipo tayari kubadili plani nzima nikaenda mwenyewe" Calvinjr hakuwa tayari kumuacha dada yake aende huko pekeyake, alikuwa na hofu sana kuhusu maisha ya dada yake wa pekee huyo.

Tina alimsogelea mdogo wake na kwenda kumkumbatia akiwa na tabasamu, alijua ni kwa namna gani yeye na ndugu yake walikuwa wakipendana sana ndiyo sababu hakuwa tayari kumruhusu kwenda ndani ya nchi hiyo tena akiwa hana mtu wa kumpa msaada.

"Kaka, kweye maisha yako usitumie sana hisia kufanya maamuzi mahali ambapo inahitajika akili zaidi, haitajalisha kwamba hisia zitakuumiza ila kuna muda unapaswa kufanya maamuzi magumu ili kupata matokeo ambayo yapo sahihi. Mimi kwenda Rwanda sio mpango wangu tu, ni kiongozi amefanya hayo maamuzi kwa sababu anajua mazingira ya kazi yalivyo"

"Kule inatakiwa niende mimi mwenyewe maana kama tukienda wote itakuwa ni rahisi sana kufuatiliwa na kujulikana kitu ambacho kitafanya tupoteze kila kitu ambacho tumekianza hivyo natakiwa kwenda kwanza halafu baadae kama kutakuwa na ulazima wa nyie kunifuata itakuwa sawa"

"Kumbuka Calvinjr, wameuliwa viongozi wengi sana, nchi imechafuka saivi, raia wanailaumu serikali kwa uzembe wake mkubwa ambao imeufanya mpaka kuruhusu idadi ya wanasiasa wengi kufa namna hiyo kwa siku moja. Hatutakiwi kulala kabisa na huu ndio muda ambao inabidi tuhakikishe tunafanya jambo lolote lile ili kuwapata hawa watu ambao wamehusika na hili jambo"

"Tukitanguliza hofu ya kuogopa kupoteza maisha basi jua kwamba kazi haitafanyika na ni kitu ambacho kitakuwa ni hatari sana kwa usalama wa taifa letu. Kumbuka tu ni jambo la hatari sana pale inapotokea wananchi wanaacha kuiamini serikali yao, hilo huenda ndilo jambo la hatari zaidi ndani ya nchi kwa maana kuna watu wanaweza kuutumia mwanya huo kufanya yale ambayo wanayataka wao"

"Mimi nakwenda Rwanda kuanza kazi ya kuwatafuta hawa watu kwa namna yoyote ile ila kila nikiwa huko nitakuwa na amani kwa kitu kimoja tu, kwamba bado ninaye wewe hapo, wewe ndiye mtu ambaye ninakutagemea sana kwenye hii kazi. Huenda mimi naanza ila nitahitaji sana msaada wako hapo baadae"
"Pale nitakapokuwa sipo, usinitafute kabisa mpaka pale nitakapo kutafuta mimi, na hakikisha unamtunza mama, maana ndicho kitu cha pekee cha thamani ambacho MUNGU ametupatia kwenye haya maisha yetu"

"Kumbuka tu kwamba dada yako nakupenda sana". Tina alilia kwa kwikwi na sauti ya chini baada ya kukumbuka maongezi ya mwisho mwisho akiwa anahitaji kuianza safari yake ya kwenda Rwanda ambako kulimfanya akaishia ndani ya hicho chumba alicho kuwepo.

Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuweza kutafuta ushahidi wa hayo mauaji ambayo yalihusisha vifo vya wanasiasa wengi sana ndani ya Tanzania ila ni kama alikuwa na bahati mbaya baada ya kukamatwa na sasa alikuwa analipa kwa mateso makali mno.

Aliinua uso wake kutazama kila kona ya hicho chumba na kuishia kusonya kwa fadhaiko la kukata tamaa, hakuwa na imani ya kuendelea kuishi zaidi ya kumuomba MUNGU aweze kumchukua haraka sana. Hakuona mahali pa kuupatia msaada wowote wala mtu wa kujali kuteseka Kwake hivyo kupambana na hali yake ndio ulikuwa msingi wa kila kitu kwa huo wakati.

Alijaribu bahati yake kwa mwanamke yule wa Kirwanda lakini hakusikilizwa, aliona kabisa kwamba mwanamke yule angeweza kumsaida kwa namna moja ama nyingine ya kumjulisha hata tu lile eneo ambalo alikuwepo ila kwa bahati iliyokuwa mbaya mwanamke huyo alimkataa kabisa kwa kumtaka apambane na maisha yake mwenyewe! Kwa maisha yapi? alibaki anajicheka mwenyewe huku chumba kikimzomea kwa kile ambacho alikuwa anakipitia.

Akiwa analia huku anacheka kama mtu aliye changanyikiwa, mlango wa chumba hicho ulifunguliwa tena lakini hakuona mtu akiingia zaidi ya kusikia kishindo cha sauti kama vile kuna mzigo umetupwa humo ndani. Taa iliwaka ghafla sana na kumfanya afumbe macho yake ili yasiumie, lakini baada ya kuyafumbua hakuona mtu yeyote akiwa amesimama mbele yake.

Baada ya kuona hivyo akaamua kuinamisha macho chini ili kuona ile sehemu ambayo alihisi kwamba kuna mzigo ukitupwa kuna nini, alicho kiona kilimtisha kiasi kwamba alishindwa kuvumilia, akawa anatokwa na jasho jingi huku akihema kwa nguvu na kwa taabu kubwa. Alipiga kelele mara moja tu na kutulia. Haikueleweka kama alipoteza maisha au alikuwa amezimia kwa ule mshtuko mkubwa ambao aliupata kwa kipe ambacho alikuwa anakishuhudia pale.

Unahisi aliona nini mbele yake cha kumshtua sana kiasi hicho? Je huko Rwanda kilimpata nini kwenye harakati zake hizo za upelelezi? Na alikuwa anampeleleza nani mpaka aangukie kwa hao watu? Ni wanasiasa wapi hao wa Tanzania ambao walidaiwa zaidi ya 100 waliuliwa na kwanini wauliwe?

Twende sawa ndani ya DOCUMENT namba 72 taratibu tutayapata majibu yetu. Episode 2, inafika mwisho.

Kalamu ni yangu mwenyewe.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 16.
Calvinjr alikuwa kwenye kasi kubwa sana ndani ya gari ambayo aliitumia kusafiri nayo kwenda huko Lindi. Akiwa barabarani aliweza kuiona vyema habari ya kiongozi mkuu wa nchi, alishangazwa mno na namna mzee huyo alivyokuwa anaongea mambo ya siri hadharani sana namna hiyo, ikamlazimu kumpigia simu kiongozi wake wa kazi ili kujua kama labda hawajampa kitu cha maana cha kuongea raisi huyo.

"Bosi mna maana gani kuruhusu hayo yote kutokea?" aliongea huku akiwa anaendesha
"Una maanisha alicho kiongea mheshimiwa raisi"
"Yes"
"Huyo ndiye kiongozi wa juu zaidi ndani ya nchi hii, huyo ndiye mtu mwenye mamlaka zaidi ndani ya hii ardhi, kama ukimshauri jambo na hataki kuelewa utafanyaje? utamalazimisha raisi wa nchi? Nchi ni ya kwake acha afanye anacho hisi kinamfaa mwenyewe"

"Lakini huoni kama anatupa mtihani mgumu sana, ni kama anawapa tahadhari maadui waweze kujificha, kazi yetu inaenda kuwa ngumu zaidi ya ambavyo ilitakiwa kuwa kwa maana haya mambo yalitakikana kuisha kimya kimya wakiwa wamejisahau tungewapata kirahisi. Sijui mheshimiwa anawaza nini ila kafanya makosa makubwa sana"

"Tina kuna watu amewakamata tunaenda kuanza nao hivyo wewe hakikisha unampata huyo mwanamke kisha unaondoka naye bila mtu kukushtukia, nina imani leo jioni utakuwa umefika huko na usiku unaweza ukaianza safari ya kurudi kesho tuonane"

"Sawa mkuu" alijibu tu ila alikuwa amechukia sana, uzembe ambao alikuwa ameufanya mheshimiwa raisi ulikuwa unawarudisha nyuma hatua nyingi mno. Ni rahisi sana kumshika na kumfuatilia adui akiwa hajui kama umeyaelekezea macho yako kwake ila ni rahisi sana kwa adui kukukimbia au kukabiliana na wewe akiwa anajua kabisa kwamba adui yake ni mtu fulani.

Kwa bahati iliyokuwa mbaya hakuwa na cha kufanya kwa maana aliyekuwa amefanya hilo kosa ndiye aliyekuwa kiongozi mkubwa zaidi ndani ya nchi ya Tanzania, hivyo alitakiwa kuwa mpole tu japo alilaani mno kitendo hicho.

Safari ya kuelekea Lindi ndani ya jimbo la DAMU INAYO ISHI ndicho kilikuwa kitu cha mhimu zaidi kwa wakati huo na ilitakiwa akikamilishe mara moja ndipo mambo mengine yangefuatia. Hiyo ilimfanya aongeze zaidi kasi ya hiyo gari kwa maana kama angechelewa huenda usalama wa mke wa mbunge Isaya Ndango ungekuwa mdogo.

Majira ya usiku wa mapema sana alikuwa anaingia ndani ya mkoa huo kwenye jimbo ambalo ndilo alilienga kufika. Alifikia mwenye senta moja ambayo ilikuwa imechangamka isivyokuwa kawaida, hapo alishuka na kuhitaji kuuliza wapi palikuwa nyumbani kwa mbunge huyo. Kwenye kuzunguka kwake kwa dakika kadhaa ndani ya eneo hilo ili kupima usalama aligundua kwamba kila sehemu watu walikuwa wanaongelea kifo cha mbunge huyo mashuhuri huku watu wengine wakiwa wanadai kwamba wanaenda kutoa pole kwa mbunge wao ambaye walimpenda sana.

Sasa aligundua kwamba hana hata haja ya kuanza kuuliza, kujichanganya na watu hao ingekuwa rahisi sana kufika huko. Kuna kundi kubwa la watu ambao walikuwa wanaelekea sehemu hiyo ambayo aligundua kwamba haikuwa mbali sana kutoka pale japo mbunge huyo alijenga pembeni kidogo ya hako kamji. Alivyo ona wanakaribia kwa ishara ya uwepo wa watu wengi, alianza kutembea taratibu mpaka alipobakia mwenyewe.

Mwilini hakuwa na suti kwa sababu hilo lilikuwa eneo la kazi maalumu, mguuni buti ambayo ingehimili hali yoyote ngumu ilimtosha vizuri kabisa, jeans ya bei ilikaa kwenye mwili wake bila kusahau tisheti na kofia kichwani, vilimfanya aonekane kijana wa kawaida na maridadi ambaye anajipenda kwa namna mwili wake ulivyokuwa umekaa vyema.

Kilicho mfanya mpaka akapunguza mwendo alitaka kuona namna watu walivyokuwa wakiingia na kutoka hiyo sehemu hivyo akawa kama anabinya binya simu yake ajue namna mazingira yalivyo. Alihitimisha ya kwamba usalama wa eneo hilo ulikuwa ni asilimia sifuri kabisa, kwa maana hiyo alitakiwa kuwahi kukutana na mke wa mbunge huyo.

Alimwita mtu mmoja ambaye alikuwa anapita karibu na hilo eneo huku akiwa anamwangalia kwa umakini na kumuuliza ni kwa namna gani anaweza kukutana na mama mwenye nyumba ili aweze kutoa pole yake. Kijana huyo alimwambia amsubiri hapo hapo ngoja akamuite mdogo wa kiume wa mke wa mbunge Isaya Ndango ndiye ambaye angemkutanisha na dada yake kiwepesi zaidi.

Zilipita dakika tano tu kijana huyo alirudi akiwa na kijana mmoja ambaye alitaka kujua shida yake ilikuwa ni ipi hasa, Calvinjr alijieleza kwamba yeye ni moja wa watumishi wa bunge hivyo amekuja hapo kuwawakilisha wafanyakazi wenzake kutoa pole kwa mbunge huyo ndiyo maana alihitaji kukutana na mwanamke huyo. Basi kijana huyo alimchukua na kumpeleka mpaka ndani ya nyumba kubwa sehemu ambayo alikuwepo dada yake, alimwambia Calvinjr asubiri kwenye kiti yeye anaenda kumuita dada yake.

Ndani ya dakika moja tu kijana huyo alitoka akiwa anahema, huku akieleza kwamba dada yake kuna watu walikuwa wamekuja hapo na kudai kwamba ni watu wa usalama wa taifa walihitaji kuzungumza naye, hivyo alitoka nje kuweza kuongea nao.
"Oooooh f*****k. Ni kwa muda gani wanadai kwamba walitoka naye?"
"Dakika thelathini na tano zilizo pita"
"Wakeelekea wapi kwa maelezo yao?"
"Wanadai wametokea mlango wa nyuma huko ambako huwa hakuna mwingiliano wa watu kwa sababu tunatumia kufugia mifugo na kulima bustani"

"Nipeleke haraka sana" Calvinjr aliongea kwa sauti ya ukali akiwa amemkazia macho kijana huyo anbaye alikuwa amejawa na hofu tayari. Alinyoosha njia hiyo ambayo ndiyo walitakiwa kuwahi muda huo. Calvinjr akiwa ameongozana na kijana huyo alimuona mwanaume mmoja akiwa ndani ya suti na miwani amejichanganya sehemu walipokuwa wamekaa wanaume wakiota moto na kupiga soga. Aliwaza majira ya usiku mtu gani anavaa miwani kiasi hicho? Mwanaume huyo aligeukia upande wa pili akiwa kama anasoma kitu kwa umakini kwenye simu yake na kunyanyuka kupokea simu yake ambayo ni wazi hakutaka mtu yeyote asikie.

Calvinjr mtu yule alimpa maswali mengi ila alitakiwa kuwahi kwanza huko nyuma ya sehemu hiyo za kufugia na kulimia bustani. Banda la mbwa lilikuwa kimya mbwa wote wakionyesha kwamba walikuwa wamelala, ni wazi walitiliwa sumu. Calvinjr kichwa kikawa kimepata moto. Hawakupiga hatua hata kumi wakakutana na mwili umelala chini, kijana huyo alianza kupiga makelele kwa uoga ila Calvinjr alimzuia kufanya hivyo akabaki analia kimyakimya.

Calvinjr alivaa gloves laini kwenye mkono wake mmoja, alimgusa mwanamke huyo puani hakuwa akihema, alimgusa kwenye eneo la shingo, alikuwa ameanza kuwa wa baridi. Watu wasio julikana walikuwa wameyabeba maisha yake.

"Shiiit!!!" Alitamka kwa hasira sana akiwa anamkumbuka yule mwanaume ambaye alimuona ananyanyuka na kupokea simu yake, alikimbia kuelekea lile eneo akimuacha kijana aliyekuwa naye akipiga makelele ya kuomba msaada dada dada yake alikuwa chini kalala.

Calvinjr alifika lile eneo hakumuona yule mtu, huku watu waliwa wamechanganywa na makelele ambayo waliyasikia mtu akihitaji msaada, Calvinjr alimdaka mwanaume mmoja kati ya wale waliokuwa wamekaa pale akiwa anahitaji amuelekeze kwamba ni wapi mwanaume yule mwenye suti alikokuwa ameleekea, mwanaume huyo alimuonyesha tu njia aliyokuwa amepita.

Njia hiyo ilikuwa na miti mingi aina ya milingoti, Calvinjr alikimbia kwa kasi kuelekea hiyo sehemu. Kwa mbali alimuona mtu akitamka neno.
"Job done sir! (Kazi imeisha mheshimiwa)" kisha baada ya kumaliza kuongea na simu hiyo aliipasua kwa kuigawanyisha vipande viwili kwa mkono wake akaitupa pamoja na gloves za mkononi, bila kusahau koti la suti, alionekana kuwa mtu aliyekuwa akiifanya kazi yake kwa ufasaha sana.

Licha ya Calvinjr kuwa na maswali ya kwamba mbona kama watu hao aliambiwa kwamba hakuwa mmoja, wenzake wako wapi? Hakuona umuhimu wa hilo jambo kwa huo wakati bali huyo alipaswa kutapika ukweli wote ambao alikuwa anaujua.

Alikimbia kumsogelea mwanaume yule ambaye alikuwa anakaribia kuimaliza ile milingoti atokezee upande wa barabara ambayo walikuwa wanapita watu ila hakupewa hiyo nafasi kabisa. Calvinjr alijirusha kwa teke moja mbele ambalo lilifanya mwanaume huyo ahisi kuna mvumo unakuja eneo alilo kuwepo hivyo akainama tele hilo likaishia kwenye mlingoti na kuyabandua magome ya mti huo.

Aligeuka kwa nguvu na kurusha ngumi zake mbili ambazo zilimpata Calvinjr kwenye mbavu zake akateleza kidogo na kusimama wakawa wanaangaliana sasa. Jamaa aliona kama atapotezewa muda wake alijigeuza na mateke mawili ambayo Calvinjr aliyaona na kuyakwepa ila baada ya kuyakwepa mateke hayo mwanaume yule aligeuka na kutua chini kwa mkono wake mmoja wa kulia kisha mguu wa kushoto ukacheza na bega la Calvinjr ambalo lilipata maumivu kiasi na kumfanya adondoke chini.

Yule jamaa akaamua kuchomoa kisu kwenye kiuno chake kurahisisha kazi yake ambayo hakujua uzito wake unakuwaje, aliurusha mkono wa kushoto kwa kasi, Calvinjr aliukwepa ila alipishana na kisu ambacho kilimkosa kidogo kilichokuwa kimerushwa kwa kutumia mkono wa kulia wa mwanaume huyo. Alijivuta na kujisogeza mbele kidogo ambapo alitishiwa kama anapigwa ngumi wakati anarudi nyuma kukwepa alipigwa na mtama wa haja.

Aliyumba na kutaka kusimama vyema aliongezwa mwingine, akawa anaenda chini ila hiyo nafasi ya kuenjoy hata hakupewa alikutanishwa na buti la kifua ambapo alienda kujibamiza kwenye mlingoti ambao ulikuwa upo karibu kabisa na hilo eneo ambalo walikuwa wanalitumia kupigania. Alidondoka chini kwa maumivu, kichwa chake kilipigwa kama kitenesi akajigongesha tena kwenye mti kiasi kwamba paji lake la uso likawa limechanika.

Calvinjr alimsogelea na kumuuliza
"Nani amekutuma uje ufanye haya?" Ila swali lake halikujibiwa na mwanaume huyo zaidi ya kubaki anamcheka tu
"Unahisi unaweza kuzuia lolote? Hahahahahahah wewe bado naona ni mtoto sana, kama kuna mtu kakutuma uje kufuatilia haya mambo utakufa kabla ya umri wako. Hapa tupo wengi hivyo hata mimi kufa haibadilishi chochote kile maana kila atakaye ingia kwenye hii njia atakufa kifo kibaya kama yule mnoko alivyokufa" mwanaume huyo aliongea kwa dharau huku akijing'ata kwenye ulimi wake na kuanza kutoa povu

"Nani kakutuma? Hey hey nambie nani kakutuma?" Calvinjr aliongea kwa nguvu huku akiwa anamvuta vuta mtu huyo lakini haikusaidia kitu kwani alitulia kabisa na kupoteza maisha yake. Alimkagua mdomoni akagundua kwamba mwanaume huyo alikuwa na kidonge ambacho alikimeza cha sumu na ndicho kilichoweza kuondoka na maisha yake.

Akiwa amechuchumaa hapo, aliitoa simu mfukoni mwake na kumpigia kiongozi wake ;
"Negative boss"
"Kwanini?"
" mission failed. Nimechelewa kwa dakika thelathini tu, nimekuta tayari wamemuua na kuna mhusika mmoja nilikuwa nimemuweka kwenye mikono yangu tayari ila kameza kidonge ambacho nadhani kilikuwa mdomoni bila mimi kujua ila kanihakikishia kwamba hili jambo ni kubwa kuliko tunavyo fikiri na kila atakaye ingia katikati yake ni moja kwa moja lazima afe"

"Ondoka hilo eneo haraka sana na usimhoji mtu yeyote tena nadhani hawa watu huenda wapo miongoni mwa hao hao wenye maisha ya kawaida hivyo wanajua kila kinacho endelea. Kama ukiwa karibu na mtu mwingine tutasikia msiba mwingine haraka sana hivyo ondoka hapo" Mr Gulamu alimjibu kifupi sana tena akisisitiza aondoke huko, kitu ambacho Calvinjr kilimshangaza.

"Bosi, hili jambo kuna mtu mwingine alikuwa anajua kabla yet....." akiwa anahitaji kuuliza aligundua kwamba simu hiyo ilikuwa imekatwa muda mrefu sana hivyo akawa hana namna zaidi ya kutoweka ndani ya eneo hilo baada ya kusikia milio ya gari za polisi.

Unadhani hawa watu ni akina nani ambao wanahitaji kuificha hii siri isiyo julikana chanzo chake ni kipi? Twende sawa.

Episode ya 16 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom