STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 20.
Asubuhi ya siku mpya kabisa ilimkutia Calvinjr njiani akiwa anaendesha gari yake kwa spidi kali mno ili kuwahi Dar es salaam, alitakiwa kufika mapema ili wakae kikao na kiongozi wake pamoja na dada yake ili waangalie ni sehemu gani ambayo walipaswa kuifanyia kazi kwani mambo yalionekana kuwa magumu tofauti na vile walivyokuwa wanayaona mwanzo na mheshimiwa raisi alikuwa anahitaji ripoti ya kuwasilisha kwa wananchi haraka sana.
Kijana huyo alihisi kichwa chake ni kizito kwani licha ya kuwa na mambo asiyo yajua juu ya uwepo wa wale watu wavaa mavazi meusi, bado hakuelewa ni kivipi haya mambo ya nchi nayo yanatokea. Alitamani sana kuwahusisha wale watu wa yale mashuka meusi kuhusika na haya mambo ila aliona atakuwa anajipoteza tu muda maana hawa wa sasa walikuwa wanavaa suti na sio mashuka tena hivyo akaona kwamba mawazo yake hayapo sahihi. Anajipoteza tu.
Akiwa kwenye msongo huo wa mawazo huku akiwa makini sana na gari yake barabarani, simu yake iliita kwa fujo alitaka kuipotezea ila baada ya kuona jina la Sarafina William ambaye alikuwa mwanamke aliye mpa mchongo mkubwa sana wa pesa za kutosha, hakuona sababu ya kufanya hivyo. Akaamua kusimamisha gari na kutulia kisha akaipokea
"U hali gani mrs William"
"Naomba uniite tu Sarafina kwa sasa"
"Sawa madam, vipi hali yako kwa sasa"
"Namshukuru MUNGU nimekaa sawa japo haiwezi kuwa rahisi sana, aliyekufa ni baba yangu mzazi hivyo nafsi yangu inaniuma sana"
"Kila kilicho andikwa na mwenyezi MUNGU lazima kitatimia, huwa ni suala la muda tu hivyo tunapaswa kumshukuru kwa kila jambo huku tukimuombea mzee apumzike kwa amani"
"Ahsante! Calvin, lakini kwanini ulinidanganya? Unajua mimi sina rafiki wa karibu kwenye maisha yangu zaidi ya baba na mama yangu. Mama kwa sasa hayupo sawa hivyo naye anahitaji faraja, jana nilitegemea sana uwepo wako lakini haikuwa hivyo, siku nzima nimekuwa mpweke sana, sijapenda ulicho kifanya"
"Naomba unisamehe sana, sikufanya kwa ubaya ila nilifanya vile kwa sababu nilijua familia mnahitaji muda wa kuwa pamoja, muda wa kuongea mambo ya mhimu kama familia hivyo sidhani kama ungekuwa ustaarabu na mimi nikavamia ila nilipanga kuja kukuona mkishakuwa mmetulia"
"Nakuhitaji saivi tafadhali Calvin" mwanaume aliangalia saa yake, alibakisha masaa kama matano mpaka aingie mjini, aliwaza kidogo kisha akamjibu.
"Unaweza kunipa masaa matano ili tukae pamoja mpaka jioni? Kwa sasa nimekuja kumsaidia kidogo baadhi ya majukumu mama yangu kwenye biashara zake baada ya huo muda nitakuwa hapo kama hautajali"
"Sawa mimi nitakusubiri, nahitaji na zawadi yangu uliyokuwa umeniahidi"
"Okay" mwanaume alijibu huku akikata simu yake. Aliingia ndani ya gari na kuinamia kwenye usukani
Alimsikitikia sana mwanamke huyo, alikuwa anapitia kipindi kigumu sana. Alielewa hasara za kumkosa mzazi hususani baba kwenye maisha kwa sababu hata yeye maisha yake hakulelewa na baba, aliwasha gari na kuendelea na safari yake.
Tina kwake asubuhi na mapema ya siku ya pili yake ilimkutia kwenye gari ambayo alikuwa ameikodi, hiyo gari ndicho kilikuwa kitanda chake hivyo alilala humo. Asubuhi alikuwa na mawazo mengi ya kuwaza mambo yalivyo tokea kimasihara kabisa mpaka wakawapoteza wale watu saba.
"Eti kuna mtu alitoka Ikulu kirahisi tu namna hii akaingia eneo penye ulinzi kama lile? Haiwezekani. Tufanye kwamba alikuwa na vielelezo vya kutoka Ikulu, sasa alivitoa wapi? na maelezo ya kujua kwamba wale watu wamehifadhiwa pale ndani aliyapata wapi na kwa nani maana haikupita hata siku moja tangu niwakamate wale watu. Hapa kuna kitu ambacho sicho kinaendelea, nadhani hata mimi binafsi natakiwa kuwa makini isivyo kawaida" alijiongelesha mwenyewe akiwa anaangalia angalia picha ya yule mtu kwenye laptop.
"Wait..."Alijiongelesha mwenyewe akiwa anaikuza picha ya mwanaume huyo kwenye monitor.
"Ooooh f****k, ni yeye" aliongea kwa sauti huku akijishika kwenye kichwa chake.
Alirudisha kumbukumbu zake nyuma siku ya jana, akiwa anaingia kwenye jengo la bunge baada ya kuwakamata wanaume wale saba, akiwa kama mwandishi wa habari ili kuweza kupata nafasi ya kuchukua habari wakati mheshimiwa raisi anahutubia nchi, kuna mtu alipishana naye tena mwanaume ambaye alikuwa kwenye koti la leza na kofia kichwani.
Kilicho mfanya mpaka akamkumbuka mwanaume huyo ni kwa sababu ile jana wake waligongana wakiwa wabapishana, mwanaume yule aligeuka kumuangalia Tina, hata yeye pia aligeuka kumuangalia na ndipo walipo kutanisha macho yao.
Hapo sasa akawa amemkumbuka vyema mtu huyo kwamba ndiye huyo ambaye alienda pale kwenye ofiri zao za MEMA YATAKUJA, akafanikiwa kuingia ndani na kuweza kuwaua wanaume saba, alishangaa mno,
"Ina maana kumbe hawa watu wapo kila sehemu? Nadhani ile kauli ya bosi itakuwa ya kweli alivyosema kwamba huenda wengine ni miongoni mwetu watu wa karibu sana" akili yake ilizidi kumwambia yaliyo mengi na kumfanya azidi kupata wasiwasi.
Akiwa kwenye huo mshtuko simu yake ilianza kuita pembeni yake, aligeuka na kuiangalia kwa umakini kwa maana hakuwa hata na mood ya kuweza kuongea na simu kwa wakati huo. Namba ilikuwa ni ngeni kwenye kioo cha zimu yake na hakuwa na kawaida ya kupokea namba ngeni kabisa kwenye simu yake.
Iliita mpaka ikakata, ikawa inaita tena lakini bado hakuipokea hiyo namba mpaka ilipokata kwa mara nyingine tena. Haikukaa sana akasikia mlio wa meseji kwenye simu yake, baada ya kuifungua alishtuka na kuiachia simu hiyo kisha akairudia tena na kuishika vizuri. Kwenye kioo cha hiyo simu palikuwa na picha ya mtu ambaye alikuwa sawa na yule mtu ambaye alikuwa kwenye kioo cha laptop yake yeye ila utofauti na yule wa kwenye simu alikuwa ametapakaa damu shingoni akiwa amefariki.
Aliipiga haraka sana ile namba, iliita kwa sekunde ishirini ndipo ikapokelewa, akaisikia sauti nzito upande wa pili. Alihema kwa nguvu baada ya kujua kwamba ni bosi wake maana mpaka wakati huo alikuwa ana wasiwasi isivyokuwa kawaida.
"Hii namba huwa naitumia kwa mambo ya mhimu, watu wangu wengi hawajui kabisa hivyo hii ndiyo tutakayokuwa tunaitumia na kama kutakuwa na mambo ya mhimu hakikisha unautumia namba hii kuniambia au kutuma taarifa"
"Bosi kwani nini kinaendelea?"
"Huyo bwana mdogo ambaye ameuwa wale watu saba amekutwa amekufa mtaani akiwa amepigwa risasi tatu kwenye shingo yake na mtu ambaye anadhaniwa kuwa mdunguaji hivyo tuneutoa kwanza mwili ili isije kuleta mtafaruko kwa wananchi"
"Kwamba wamemtuma kazi halafu wanamuua wenyewe?"
"Hivyo ndivyo watu wenye akili wanavyofanya ķazi Tina, huwa wanahakikisha hawaachi alama yoyote ile hivyo kama unafanya nao kazi hata uwe mwaminifu vipi ikifikia wakati ambao wanakuwa hawana uhitaji na wewe tena basi ni lazima wakupunguze tu"
"Kwa sasa ni kipi kinafuata bosi?"
"Unatakiwa kuwahi sana kumpata yule Mbunge. Gari yake kwa sasa inasoma kwamba ipo kwenye nyumba ya nje ya mji nadhani atakuwa yupo huko. Nakutumia address muda huu hapa uwahi haraka sana huko kabla mambo hayajaharibika mimi nitakuwa busy kuandaa msafara wa raisi hivyo tutakutana Dar es salaam ukiwa na huyo mtu" Mr Gulamu Leopard alimaliza na kuikata hiyo simu.
Tina alisali kwanza kabla ya kuanza safari ya kuelekea huko kwenye hiyo nyumba ambayo ilisemekana kwamba mbunge huyo alikuwa amejihifadhi kwa siri kwa huo muda bila kueleweka nini sababu ya yeye kujificha kwenye nyumba hiyo ambayo ilisadikika kwamba huenda alikuwa anaimiliki kwa siri pasipo kutambulika kama ilikuwa ipo chini yake.
Tina alisali kwa sababu kila dakiķa moja ilivyokuwa inaenda alikuwa anaona hatari inajisogeza mbele yake, alikuwa anaingia maeneo hatarishi sana licha ya urembo wake ambao huenda angeendelea kuupendezesha kwa vipodozi vyake ambavyo alikuwa akiviuza kwenye duka lake ambalo lilikuwa maeneo ya Mlimani City ila ndiyo hivyo tena alikuwa ameyachagua maisha hayo ya kuishi ukiwa umeishilia roho yako mkononi.
Aliendesha hiyo gari mithili ya mtu aliye na kichaa, alitakiwa kuwahi haraka sana ndani ya hilo eneo kwani hakukuonekana kuwa na usalama wa kutosha baada ya kugundua kwamba yule kijana wa mwanzo alikuwa ameuliwa. Dakika thelathini tu zilizotosha kumfikisha hiyo sehemu, alisimamisha gari umbali wa kama mita miambili na kuufunga uso wake.
Jasusi huyu Tina alikuwa makini sana na kazi yake hivyo hakuwa akihitaji kuacha ushahidi nyuma kwenye kila eneo ambalo anataka kufika au kupita. Alitembea kwa mguu mita kama miambili mpaka alipofika kwenye ile nyumba ya kisasa ambayo haikuwa hata na fensi ila ilikuwa ni nyumba ndogo iliyojengwa kisasa.
Ndani ya nyumba hiyo alisikia mziki ukiwa unapiga kwa sauti ya juu sana, hicho kikamshtua hivyo akawahi kwenye mlango ambao alikuta umefungwa kwa ndani. Kichwa chake kilikuwa kimewaka taa ya hatari hivyo akaamua kuuvunja mlango huo na buti lake ambapo aliingia nao mpaka ndani. Alichokuwa anakifikiria ndicho hicho ambacho alikutana nacho.
Sauti hiyo kubwa ya muziki haikuwekwa kwa bahati mbaya iliwekwa ili hata mtu akiwa anaomba msaada asisikike yeye zaidi ya hiyo sauti kubwa ya mziki ikiwa inapenya vyema kwenye masikioni ya msikilizaji. Mbele yake kuna mwanaume alikuwa anaishambulia shingo ya mbunge James Lewnyika na kisu mithili ya mtu aliye ibiwa mke na mwanaume huyo.
Aliisimamisha shughuli yake hiyo baada ya kuona mtu ameingia tena kwa kuvunja mlango hivyo wakawa wanaangaliana huku kila mtu akiwa anamtamani mwenzake. Tina alitoa gloves zake na kuzivaa kwenye mikono yake, wakati huo huyo mwanaume ambaye alikuwa amevaa kofia kichwani alimsogelea mrembo huyo akiwa na kisu hicho mkononi.
Mwanaume huyo alijibenua kwa teke la upande, alikuwa amemfikia Tina ambapo alijigeuza kwa sarakati huku mateke mawili yakiwa yameachiwa ambayo yalifika kwenye mbavu za Tina ambaye hata hivyo hakutetereka. Mwanaume huyo wakati anahitaji kutua chini alichotwa mtama mkali na kupigwa buti zito la kifua, alitaka kudondoka chini Tina alizunguka na double kick ambayo ilimpata mwanaume huyo kwenye kidevu na kumfanya atoe damu nyingi sana na kwenda kujibamiza kwenye dirisha ambalo alifanya lipasuke huku akidondoka chini kwa maumivu.
Tina alijigusa tumboni alikuwa na damu, ndipo alishtuka kuona ana kisu eneo hilo, mwanaume huyo baada ya kupigwa na hilo buti kali wakati anatua chini alikirusha kishu chake kwa nguvu kikalichana tumbo la mwanamke huyo ambaye aliishia kujitukana kwa kuwa mzembe.
Aliinuka na kuangalia pale dirishani aligundua mtu huyo ametokea hapo dirishani hivyo akaamua kumfuata huko. Kabla hajaruka dirishani hapo akiwa na maumivu makali ya tumbo aligundua kwamba mbunge huyo alikuwa anakoroma kwa mbali hivyo akaghairi kumfuatilia mtu yule na kumsogelea mbunge huyo ili ampe hata neno la mwisho ambalo linaweza kumsaidia.
Akiwa anasogelea kwa umakini sana hapo alipokuwa amelala mbunge huyo, alisikia mlio wa gari za polisi zikija kwa kasi sana eneo hilo.
Nini kinaenda kumkuta Tina, akina nani wanakuwa wanamuwahi kila sehemu hawa? Wanaficha nini mpaka kila anaye onekana kujua anauliwa?
Episode ya 20 inafika mwisho.
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app