Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

Unaweza kuimalizia yote mpaka mwisho kwa 2500 tu.

2500 yako tu nakutumia pdf yote.

Lipia kwa namba

0621567672 ( WhatsApp)

0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA

Muwe na asubuhi njema.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
JIJI LA KAMALI ( GAMBLING CITY)

INTRO...........
Usiku wa kiza kinene ambacho kilikuwa kinasindikizwa na mvua ambazo hazikuwa na mpaka wa kuweza kuzielezea vyema, alionekana mwanaume mmoja akiwa ndani ya nguo zake nyeusi tii na begi jeusi usiku huo huku mwili wake ukiwa umefunikwa na koti kubwa jeusi pia ambalo lilikuwa refu kiasi kwamba lilivuka mpaka magotini.

Mikono yake ilifunikwa na gloves nzito nyeusi pia ambapo mkono wake wa kulia ndio ambao alikuwa ameutumia kuweza kushika begi lake mkononi akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka sana huku akiwa makini mno kuonyesha wazi kwamba alikuwa anatakiwa kulifikisha begi hilo salama kabisa sehemu ambapo lilikuwa linahitajika kuweza kufika.

Akiwa kwenye mwendo wake huo wa haraka, wakati amefika katikati ya barabara ndogo ambayo ilikuwa imezungukwa na majengo marefu sana na pembeni yake kukiwa na vichochoro vingi, alihisi kwamba eneo hilo ni kama lilikuwa na mtu au watu wengine ukiacha yeye hivyo alizidisha hali ya umakini sana kwa hapo ambapo alikuwa amesimama.

Masikio yake yalimtekenya vizuri mithili ya funguo zinapokuwa zinazamishwa kwenye kufuli na kumpa taarifa hiyo, alikuwa ni mtu wa kuutumia sana mlango wake wa sita wa fahamu huo wa hisia hivyo alikuwa na uhakika kwamba hisia zake zisingeweza kumsaliti kamwe kwani alikuwa akijiamini sana kwenye jambo hilo hivyo akawa na uhakika kwamba kulikuwa na ugeni ndani ya hilo eneo.

Alisimama na kutulia ili kuweza kujua kwamba huyo mgeni alikuwa anatokea upande upi huku akiwa ameyafumba macho yake kuweza kujipa hali ya utulivu zaidi kwenye masikio yake. Akiwa bado amesimama hapo alihisi kama kuna kitu kilikuwa kinakuja kwa kasi sana sehemu ambayo alikuwa amesimama hivyo aliinama kwa kasi mno mithili ya radi ya mvua.

Wakati anainama alipishana na shoka ambalo lilienda kukita kwenye ukuta mmoja wa jengo la pembeni. Aligeuka haraka sana ila wakati anageuka alitumia muda mrefu ambao ulimpa nafasi mtu ambaye alikuwa ameingia hapo kufanya kile ambacho alikuwa anakitaka.

Alihisi kifua kinamuwasha mithili ya mtu aliye tafuna pilipili kichaa maana spidi ambayo mvamizi aliitumia kumkita hapo kifuani haikuwa ya binadamu mwenye mifupa ya kawaida bali alikuwa ni mashine haswa kama namna umeme unavyo safari kwenye zile njia zake. Alipokea mishindo ya haraka na mabuti makali na kumfanya begi kumtoka mkononi huku ikionekana wazi kwamba mabuti hayo yalitokea kwa mtu ambaye alidhamiria kabisa kumuua ndiyo maana hakumpa hata nafasi ya kuweza kumtazama maana mvamizi huyo uso wake ulifunikwa kwa kitambaa cheusi na hata mvamiwaji hakupata hiyo nafasi ya kumtazama kwa ukaribu.

Mwanaume huyo licha ya kurushwa mbali na mabuti hayo hali ambayo ingemfanya auvunje mgongo wake kwa kujibamiza kwenye kuta za mawe mazito za majengo ambayo yalikuwa pembeni, hakuwa fala kufa kijinga namna hiyo. Mkono wake ndio ambao aliutumia kukita kwenye kuta hizo na sio mgongo ambao ulitua ukutani kwa nguvu sana.

Kasi ambayo alitua nayo kwa mkono wake ililifanya koti lake kujivuta kidogo na kwenye mkono wake ikaonekana alama ya tatoo (tatuu) ambayo ilisomeka kama 001. Baada ya kujichomoa hapo ndipo aligeuka na kumuangalia mtu ambaye alionekana alihitaji kumuua, mtu huyo alikuwa kwenye mavazi meusi kama yeye na koti kama lake, yaani kiufupi wote walikuwa wamevaa sawa ila utofauti wao ni kwamba mvamiwaji alivaa kofia aina ya pama kichwani ila mvamiaji alikuwa amejifunika tu kitambaa kwenye uso wake hivyo sura yake haikuwa ikionekana kabisa.

Baada ya hapo ulipigwa mkono wa hatari mno mpaka umeme ulipo katika ghafla sana ndipo mvamiwaji alitulia akiwa makini sana maana hakuwa akimuona mtu ambaye alitakiwa kumshambulia huku akiwa amepigwa vibaya sana na umeme huo kukatika alishukuru sana japo ilikuwa ni hatari maana angeweza kuuawa bila kujua mhusika yuko wapi ila aliamini kwamba angepata dakika chache za kupumzika maana bila hivyo ni lazima angekufa.

Akiwa anaangaza kwa umakini huku na huko umeme ulirudi tena ghafla sana na ndipo alipo gundua kwamba ndani ya eneo hilo hapakuwa na mtu mwingine zaidi yake, mvamizi alikuwa ameondoka muda mrefu sana ila chini palikuwa na karatasi nyeupe ambayo ilikuwa imesainiwa kwa damu huku ikiendelea kunyeshewa na mvua.

Aligeuka na kuangalia pale ambapo begi lilikuwa limedondokea ili kujua usalama wake ila kwa bahati mbaya sana begi halikuwepo kabisa eneo hilo, alishtuka sana akionyesha hofu ya wazi moyoni na kwenye uso wake hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuisogelea ile karatasi ili aweze kusoma kile ambacho kilikuwa kimeandikwa.

“KAMALI YANGU YA MWISHO, NDIYO KAMALI YAKO YA KWANZA” hayo ndiyo maneno ambayo yalikuwa yameandikwa hapo. Aliogopa sana baada ya kuisoma huku akionekana wazi kwamba mikono yake ilikuwa inatetemeka wakati huo. Hiyo ilikuwa ni kauli ambayo alikuwa anaitumia mwanaume mmoja ambaye alimuua yeye mwenyewe kwa mkono wake miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita huko nyuma, huku begi ambalo lilionekana kuwa na nyaraka mhimu mno likiwa limepotea kizembe sana.

Inawezekanaje mwanaume ambaye alimuua kwa mkono wake mwenyewe bado awe hai? Hilo begi lina nini mpaka mtu ambaye alisemekana kwamba alikufa aweze kupotea nalo? Nini maana halisi ya JIJI LA KAMALI na jiji hilo lina mambo yapi na siri zipi labda?

Unategemea kukutana na nini humu ndani? Mimi nashika kalamu yangu sasa nakaa mezani, kazi yako wewe ni kuhakikisha unaenda nayo nukta kwa nukta ili uweze kuifunua kila kurasa kuweza kuzisoma serikali tatu kwa wakati mmoja ndani ya JIJI LA KAMALI.

Simulizi hii inasomwa kwenye group la WhatsApp tu pekee na haitapostiwa mahali pengine popote hivyo nicheki haraka nikuunge kwenye group langu la WhatsApp uanze kusoma simulizi hatari sana ya watu wenye jiji lao la KAMALI (ni hatari sana).

Kujiunga bei yake ni shilingi 3000 tu, yaani ukilipia 3000 nakuunga kwenye group haraka sana.

Usikae kinyonge wakati naingia kujifungia ili ufurahi na kwenda kuisherehekea vyema likizo yako ndefu. Maandishi yapo yanakusubiri wewe tu, usijibane ukataka kukosa simulizi hii bora ya kusisimua eti kisa 3000 tu.

Lipia kupitia namba

0621567672 ( WhatsApp)

0745982347

Zote FEBIANI BABUYA

Nataka watu 30 tu wa mwanzo nianze nao haraka sana, unaweza kuwahi kabla nafasi hazijajaa ili usije ukaikosa[emoji996]

Niwatakieni asubuhi njema.

Kalamu ni yangu mwenyewe;

FEBIANI BABUYA.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Boom.....kesho inaanza kwa group [emoji736]
Gambling%20City2.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
I want to die judge,innocent killer,gereza la hazwa, ulimwengu wa watu wabaya.Hizi riwaya zote nimesoma mpaka mwisho.Hii Riwaya Document number 72 ikimbize basi mkuu ili na yenyewe tuinunue huko mbele ! FEBIANI BABUYA
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 27:
Baada ya kuzipata habari, mheshimiwa raisi hakutaka kukaa tena Ikulu, alihitaji haraka sana kusogea mpaka ilipo kambi hiyo ndogo ya kijeshi iliyokuwepo huko Kawe kwa siri sana, alihitaji mwenyewe kuweza kumhoji waziri huyo wa ardhi ili kujiaminisha kwa masikio yake kama kijana huyo ambaye yeye ndiye aliyempa hiyo nafasi anahusika kweli na hilo tukio la kutisha sana lililo iacha dunia mdomo wazi?.

Msafara wake ulichukua muda mfupi sana kuweza kufika huko Kawe, alishuka kwenye gari akiwa na haraka isiyokuwa ya kawaida. Alikuwa ana hamu kubwa mno kufika alihisi kama alikuwa anachelewa sana kukutana na mwanaume huyo. Mtu aliyekuwa amefika kumpokea alikuwa ni waziri wa ulinzi mwenyewe akiwa sambamba na mkuu wa majeshi, watu hao wawili walimpa heshima ya juu kiongozi wao wa nchi ambapo aliwahitaji wamuonyeshe alipo mwanaume huyo ambaye anampa wakati mgumu sana kuwaeleza wananchi kile ambacho hakika kilitokea.

"Ni kweli wewe ndiye uliyefanya hili tukio?" Aliuliza kwa sauti nzito mno baada ya kupelekwa sehemu alipokuwa amefungwa waziri wa ardhi huku akiwa anaikunja shati ya kwenye mkono wake, waziri huyo alibaki anamwangalia mheshimiwa asiwe na cha kujibu. Alipigwa na kibao kizito kwenye shavu lake mpaka chozi lilimtoka, ni kibao ambacho kilikuwa kinawasha isivyokuwa kawaida, alitamani angepata nafasi ya kukuna kwenye shavu hilo ila kwa bahati iliyokuwa mbaya hakuna mtu aliyeweza kumpa hiyo nafasi.
"Unajua mimi ni nani?"
"Wewe ni raisi wa nchi yangu"
"Kwahiyo unaona mimi naweza kuongea na wewe ukanikalia kimya?"
"Hapana mheshimiwa"
"Sitarudia tena kukuuliza"
"Ndiyo mheshimiwa ni mimi ndiye niliyefanya hili tukio"
"Whaaaaaat?"
"Utanisamehe mheshimiwa"
"Kwamba ni kweli ni wewe?"
"Ndiyo"
"Ooooh.....shiiiiit! Wailes. Umewezaje kufanya jambo la kipuuzi namna hii? Umeamua kunivua nguo namna hii? Unataka kunifanya nionekane raisi wa hovyo kwa kuwapa nafasi watu wasio faa kwenye nchi hii?"
"Nilifanya hivi ili kulinda heshima yako mheshimiwa kwa maana sikutaka kabisa jambo hili lijulikane, niliona kwamba linaweza kukuharibia ila kwa bahati iliyokuwa mbaya wakati nalitekeleza ndipo nikakutana na hili jambo lililo nifanya nikakamatwa"
"Kipi kilikufanya ukaamua kuutenda ukatili wa namna hii?"
"Ni kesi nzito sana ambazo zilikuwa mbele yangu"
"Sipendi kuuliza mara mbili mbili, nipe maelezo yanayo jitosheleza"
"Kuna kipindi wale wabunge waliwahi kunishtaki mimi kwa kesi ya ubakaji ila kwa baadae nikaja kushinda na bunge likaja kunilipa kama fidia ya kunichafua, ika ukweli ni kwamba hawakunionea bali nilihusika kweli na hilo jambo. Yule mbunge Isaya Ndango alikuwa na ushahidi juu ya hilo, akikuwa ana ushahidi wa mimi nikiwa nawalawiti watoto wadogo pamoja na mkataba wa kandarasi ya ujenzi ambapo nilifanya ubadhilifu wa zile bilioni mianane. Hivyo siku ile alikuwa anahitaji kuliweka bunge wazi pamoja na wananchi na wale viongozi ambao walikuwa wapo pale walikuwa wapo tayari kumuunga mkono kwa gharama yoyote ile hivyo niliona njia sahihi ya kuzima kila kilichokuwa kinaendelea ni kuweza kuwaua wote ambao wanahusika" maneno hayo yalimfanya mheshimiwa raisi amwangalie sana waziri huyo ambaye alikuwa ameinamisha kichwa chake chini.

Hakuhitaji kuendelea kuongea lolote tena zaidi ya kutoka humo ndani akiwa mwingi wa hasira sana ila kabla ya kutoka humo ndani kuna kauli ambayo ilimtamkia
"Kama ukipona kwenye hili basi mimi nitakubali kujihudhulu kwenye hii nafasi yangu na kurudi kule niliko tokea wakati ule sina kitu chochote kile kwenye maisha yangu"

Wakati anatoka pale ndio wakati ambao alikuwa amemtumia mkurugenzi wa shirika la kijasusi taarifa ya kupatikana kwa mhusika wa hilo tukio ambalo aliahidi kwamba kesho yake alikuwa anaenda kuliweka wazi suala hilo na kiongozi huyo alitakiwa kuwepo, huku yeye na vijana wake wakiwa wamebaki midomo wazi wasiwe na neno lolote lile la kuweza kuongeza juu ya hilo jambo.

Habari hizo zilivujishwa kwa makusudi ili watu waanze kuzipata usiku huo huo ambao mambo hayo yalianza kutokea. Watu wengi kwenye mitandao walianza kusambaziana habari kwamba asubuhi mheshimiwa angekuwa anatoa taarifa juu ya yule mhusika wa tukio hilo la kigaidi hivyo watu walitakiwa kuwa macho ili wamjue mbaya wao ni nani huku watu wakisisitiza kwamba kama akikamatwa mhusika wa hilo tukio hakutakiwa kuachwa kabisa kwa gharama yoyote ile, alitakiwa kufanywa kitu ambacho kingekuwa somo na kwa wengine wenye tabia mbovu kama yake ya kuleta majonzi kwenye nchi yao.

Usiku wa deni huwa hauchelewi kuisha na ndivyo ilivyokuwa, wananchi walikuwa wamehwahi mapema sana kwenye runinga zao asubuhi hiyo ya mapema ili kuweza kumjua mhusika wao. Ilifika saa mbili na dakika hamsini kwa saa za Tanzania, ndio muda ambao mheshima raisi wa Tanzania alikuwa anapanda kwenye sehemu ambayo alitakiwa kufanyia hotuba hiyo fupi.

"Ndugu zangu watanzania, ni matumaini yangu mu wazima wa afya kabisa kwenye hii siku nyingine ambayo MUNGU katupa nafasi nyingine ya kuendelea kuhema. Leo ndiyo ile siku rasmi ambayo yale majivu ya mashujaa wetu yanaenda kufukiwa baada ya kumpata yule binadamu ambaye alileta majonzi mazito sana kwenye taifa hili japo nahitaji sana utulivu wenu mpaka nitakapokuwa namaliza hotuba hii mwa maana kuna mtu mwingine atakuja kututhibitishia uhusika wa mhusika wetu kwa maana ndiye mtu wake wa karibu zaidi"

"Kwanza niwahakikishie kama nilivyokuwa nimewaahidi tangu mwanzo, ya kwamba mhusika wa hili tukio atakuwa wa mfano na kwa wale wengine wote ambao wana mipango kama yake, ila kabla ya kuweza kupata hukumu yake ni lazima kwanza atutajie kwamba ni nani na nani ambao alikuwa ameshirikiana nao kwenye hili tukio ambalo amelifanya ila hapa hataongea kwa lolote zaidi mtamsikia mahakamani atakavyokuwa anakiri makosa yake mwenyewe kwa maelezo yake ambayo amenipatia kwamba anajutia kwa huu udhalimu wake ambao ameufanya"

"Ndugu wananchi niweze kuwaomba msamaha sana kwa mtu huyu ambaye amelidhalilisha taifa kwa sababu ni miongoni mwa watu ambao hata mimi mwenyewe niliwahi kuwaamini sana mpaka nikaja kumpatia nafasi kubwa sana ndani ya nchi hii"

"Mhusika wa hili tukio ni moja kati ya mawaziri wangu ndani ya wizara, ambaye ni mheshimiwa Wailes Mkwavinyika, waziri wa nyumba, ardhi na makazi. Huyu ni miongoni mwa watu ambao walikuwa makini sana na kazi tangu zamani akiwa mbunge kitu kilichofanya nipendezewe naye na kumpatia hiyo nafasi ambayo nilikuwa nina imani kwamba angeitendea haki lakini cha ajabu yeye alienda kufanya yale ambayo alihisi yanamfaa kwa upande wake yeye mwisho wa siku nikaishia kumuweka mtoto wa rafiki yangu kwenye hatari kubwa"

"Huyu ni mtu ambaye kwa sababu niliwahi kuona ni mchapakazi nikawa nimemuweka karibu na mtoto wa mheshimiwa waziri mkuu ili amfundishe kazi ila cha ajabu ndiye huyu ambaye kamuua waziri mkuu na nadhani alikuwa ana mipango ya hatari sana juu ya mtoto wake pia"

"Wailes Mkwavinyika, anahusika na matukio ya ubakaji, kulawiti watoto wa kike, lakini pia anahusika kwenye ubadhilifu wa mali za serikali zaidi ya bilioni mianane, hivyo kuna mali zake ambazo zitataifishwa lakini sio zote. Sio zote kwa sababu huyu bwana ana mke na watoto wawili na kitu cha ajabu alitaka kuwaua hata watoto wake mwenyewe pamoja na mkewe kwa sababu za kibinafsi ambazo alikuwa nazo yeye mwenyewe"

"Bwana huyu baada ya mkewe kuujua mpango ambao alikuwa nao, aliamua kuhitaji kwenda kuripoti kituo cha polisi baada ya kuhakikishiwa kwamba lazima afungwe kwa yale matukio yake ambayo aliyafanya na hakukuwa na namna ya yeye kuweza kupona. Alicho kifanya ni kumteka mkewe pamoja na watoto ambao walikombolewa jana na jeshi kwa kazi kubwa ambayo ilifanywa na waziri wa ulinzi na vijana wake ambao bila shaka wanastahili sifa za pekee kabisa"

"Hivyo mali zake zote ambazo alizichuma kihalali hazitaguswa kabisa, zitabaki kuwa chini ya mkewe ili ziweze kutumika kuwalelea watoto wake ambao hawana hatia kabisa. Nadhani kwa mimi sina lingine la kuongeza zaidi ya kumkaribisha mkewe ili aje kuthibitisha hili jambo ambalo limetokea." Mheshimiwa alimaliza hotuba yake ambayo iliwaacha watu wote midomo wazi huku akimpandisha mke wa waziri huyo ambaye alienda kuthibitisha kwamba huyo mumewe ni kweli anahusika na kila kitu ambacho kilitokea na yeye wakati anahitaji kwenda kuripoti ndipo mtu huyo akamteka yeye na wanae huku akiwa anamtishia kumuua.

"Uliwezaje kumpandikiza sumu mke wangu mpaka akawa tayari kudanganya mbele ya watu zaidi ya milioni hamsini?" Waziri wa ardhi akiwa ndani ya chumba alichokuwa amehifadhiwa, taarifa hiyo ikuwa anaiangalia kwenye runinga huku pembeni yake akiwepo yule kiongozi wa ulinzi na usalama Ikulu wakiwa wanaangalia wote.
"Njia ni ile ile tu kama niliyo itumia kwako, achague kukataa kisha watoto wafe wote au akubali kuongea kisha yeye na watoto wabaki wanaishi maisha mazuri"
"Una uhakika utatimiza ahadi yako?"
"Ahadi yangu imeanza kutekezwa baada tu ya mkeo kukubali kupanda pale na kuongea, hivyo familia yako hakuna mtu atakuja kuigusa hata kwa kidole chake"
"Nina maombi mengine mawili ya mwisho, kwa sababu najua kwa sasa hatutaonana tena kwa maana siku chache tu zijazo mimi naenda kunyongwa baada ya kufikishwa mahakamani"
"Nakusikiliza"
"Kwanza naomba usimame kama baba wa wale watoto na uwalee kama wanao kwa gharama yoyote ile, hiyo itawafanya wawe na uhakika wa usalama zaidi"
"Na jambo la pili ni lipi?"
"Naomba sana wanangu usiwaingize kwenye hii michezo ya siasa wala kwenye mambo ya usalama haya. Walee kama watoto wengine wa kawaida ila tu wakikua basi unaweza ukawafungulia biashara" baada ya kuongea maneno hayo mwanaume huyo alimpa mkono kumaanisha kwamba makubaliano yalikuwa yamekwenda vizuri kisha akatoka humo ndani na kumwacha waziri huyo akiwa anasubiria kitanzi.

Nini kinaenda kujiri? Episode ya 27 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 28:
Nchi nzima iliingia kwenye taharuki kubwa isivyokuwa kawaida kusikia kwamba mheshimiwa waziri wa ardhi ndiye aliyekuwa nyuma ya hiyo mipango yote. Kabla ya tukio hilo kuweza kutokea mwanaume huyo alikuwa ni miongoni mwa viongozi bora sana ambao nchi ilikuwa ikijivunia sana kuwa nao, sasa kivipi tena iwe ndiye yeye anayehusika na hayo mambo? Watu hawakuwa na namna kwa sababu walijua kwamba wanasiasa sio watu wa kuwaamini sana huwa wanabadilika kila sekunde moja iendayo wakijawa na maneno mengi sana mdomoni.

Hali ilikuwa hivyo pia hata kwa mrembo Sarafina, mtoto wa waziri mkuu. Alikumbuka vyema sana kwamba mwanaume huyo ndiye ambaye baba yake alimkutanisha naye na kuanza kufanya naye kazi yeye akiwa kama mkandarasi wa taifa, huyo ni miongoni mwa mawaziri ambao alikuwa akifanya nao kazi kwa ukaribu sana akiwepo pia na waziri wa ujenzi, hivyo alishangazwa sana na hizo habari ambazo aliweza kuzisikia. Aliamua kuifunga safari na kwenda mpaka nyumbani kwa waziri huyo ili kwenda kuzipata taarifa sahihi za nini kilitokea.

Alifanikiwa kufika nyumbani kwa waziri huyo lakini kitu cha ajabu ambacho alikutana nacho ni walinzi waliokuwa wengi sana ndani ya lile eneo, hakuamini baada ya kuambiwa kwamba familia hiyo imehamishwa kwa siri mpaka pale mambo yatakapo tulia ili isije kupata madhara ina maana kama baba wa familia alikuwa ni gaidi huenda kuna wengine ambao walikuwa naye wanaweza kuidhuru familia hiyo hivyo kwa usalama wao wameamua kuwahamisha ili mambo yakitulia iweze kurudishwa tena. Basi hakuwa na namna zaidi ya kuondoka.

Calvinjr, majira ya asubuhi na mapema baada ya kuisikiliza taarifa kutoka kwa mheshimiwa raisi aliwahi nyumbani kwa dada yake ambaye alikuwa bado anauguza kidonda chake tumboni baada ya kupigwa na kisu ndani ya jiji la DOGMA TULIPO. Mwanaume huyo alifika na kuingia mpaka ndani ambapo dada yake alikuwa amekaa sebuleni akionekana kuangalia runinga.

“Nilimshangaa sana huyo mwanaume ambaye alikuwa na jeuri ya kumgusa dada yangu na kufanikiwa kukizamisha kisu kwenye tumbo lake, kama ningefanikiwa kukutana naye basi huenda ningemfanyia kitu kibaya sana ambacho asingesahau kamwe kwenye maisha yake” aliongea akiwa anasogea kwenye friji na kuchukua maziwa kama ilivyokuwa kawaidea yake.
“Wewe ndo mwanaume kwenye familia na unakuwa goi goi namna hiyo utaweza kutulinda wewe kweli? Ilibaki kidogo tu ungempoteza dada yako?”
“Mhhhh dada hivi una uhakika kwamba mimi ni goi goi au wewe ndiye hunijui mimi vizuri?”
“Kwenda zako huko, unataka kuniambia kwamba mimi simjui mdogo wangu niliye muachia ziwa? Haya niambie ni kipi kimekuleta na asubuhi yote hii kwangu?”
“Hivi kinacho endelea wewe unakiamini sis?”
“Hapana kwanini unauliza?”
“Ukimwangalia vizuri Yule mke wa waziri wakati anaongea pale unajua kabisa kwamba ni mtu ambaye amelishwa maneno ya kuzungumza tena akiwa na hofu kubwa sana”
“Kwahiyo unataka kusemaje?”
“Inatakiwa nimtafute Yule mwanamke niongee naye”
“Calvinjr”
“Usijali sana mimi nitaongea naye mwenyewe”
“Hautakiwi kuongea naye kwa sasa?”
“Kwanini?”
“Muda huu zinahitajika akili zaidi kuliko haraka, inatakiwa kwanza tujue kama je waziri naye alikuwa ana uhusika kwenye haya matukio au kauziwa tu kesi, na kama anahusika kweli ni lazima basi tujue kwamba je yeye ndiye alikuwa kiongozi wa haya yote au katolewa tu sadaka?. Hapo ndipo tunaweza kujua kwamba tunatakiwa kuanzia wapi ila sio kwenda kwenda tu, tunaweza kuleta madhara ambayo siyo.”
“Una uhakika na unacho kisema?”
“Ndiyo, kwa sasa tunatakiwa tukae kwanza pembeni tuangalie ni kipi kinaendelea ili tujue kama kuna dalili za jambo lolote lile kutokea”
“Mhhhhh, sidhani kama hilo ni wazo zuri, adui ukimpa muda mrefu zaidi wa kujipanga, atakuwa na nguvu kubwa sana ya kuweza kukudhibiti wewe ila kama ukimtafuta akiwa naye anaendelea kujipanga inakuwa ni rahisi sana kukabiliana naye, tunavyo endelea kusubiri sana hili jambo litakuwa na madhara makubwa sana. Kama mambo yangekuwa kama unavyosema wewe hivyo ; haujiulizi inakuwaje mpaka kila mpango ambao tunaupanga wa siri watu hao wanakuwa wanajua hatua zetu? Wanajuaje? Unahisi ni waziri tu ndiye ambaye alikuwa anaweza kulifanya hili? Waziri hana hayo mamlaka ya kuweza kuzichuja taarifa za mamlaka za usalama angalau hata kama angekuwa waziri wa ulinzi ingeniingia akilini”

“Calvin kuna muda kumpa adui nafasi ya kuona ameshinda mchezo huwa ni njia rahisi sana ya kuweza kumshinda kwani atahisi kwamba amefanikiwa kuwafanya watu wote waonekane hawana akili hivyo anakuwa anajihisi yupo huru kila sehemu. Hiki walicho kifanya mimi sina imani nacho sana ila nahisi kama wanaigiza basi wamechukulia kwamba nchi nzima ina watu wapumbavu wasiokuwa waelewa hivyo wanaweza kuwafanya kila wanacho jisikia wao na muda wanao taka wao. Kama kuna chochote huu ndio utakuwa muda wetu mzuri zaidi wa kujua tunaanzia wapi”
“Okay” Calvin aliondoka kishingo upande kwa sababu maneno ya dada yake hayakumuingia sana ila hakuwa akipenda kubishana na dada yake huyo hivyo akaamua kuondoka.

Baada ya siku kadhaa kuweza kupita, mheshimiwa waziri aliweza kufikishwa mahakamani na kusomewa mashataka yake ambayo alikiri kuhusika na tukio hilo huku akimuomba msamaha mheshimiwa raisi kwa kuweza kumuangusha kwenye nafasi aliyoweza kumpa pamoja na kuwaomba wananchi wa Tanzania msamaha kwa kuweza kushindwa kukitimiza kile kiapo ambacho aliweza kukiapa. Waziri huyo alinyongwa mpaka kufa huku serikali ikiahidi kuwatafuta wale wote ambao alishirikiana nao kwa maana wengi walikuwa ni vijana wake na walikuwa wanajuliakana kwamba ni wapi wapo.

Kifo cha mheshimiwa huyo kilirejesha amani na furaha kwa wananchi kwa asilimia nyingi sana, watu walirejea kwenye majukumu yao ya kila siku huku wakiendelea kuyapambania maisha yao kama ilivyokuwa mwanzo kwani jambo hilo lilileta taharuki kubwa sana nchini. Ila kwa upande wa Calvinjr hakuwa tayari kuliacha hilo jambo lipite kwa maana kitu kilichokuwa kimetokea kilikuwa ni kikubwa sana na alishangaa mno baada ya kuona kinaisha kirahisi sana namna hiyo, hivyo aliandaa mpango wa pekeyake kuweza kuwatafuta watu wote ambao alihisi kwamba huenda ndio walikuwa ndani ya mpango huo pamoja na huyo waziri ambaye alikuwa amenyongwa.

Jioni moja baada yamiezi kadhaa kupita alienda kukutana na mkurugenzi wake wa shirika la kijasusi, alikuwa ana mazungumzo naye ya mhimu sana ambayo aliona yanaweza kuwa msaada mkubwa sana kwake.
“Kipi kimekufanya tukutane jioni hii ya leo?”
“Mkuu kuna jambo nataka nikuulize lakini pia nahitaji sana msaada wako”
“Lipi hilo?”
“Hivi haya mambo yote yaliyo tokea unayaamini na umeamua kuyaacha yapite?”
“Vipi kuna kitu umekihisi labda?”
“Hapana mkuu”

“Calvinjr nisikilize vizuri sana, hii nchi inaongozwa kwa miongozo maalumu, sio kwamba unaweza kujipangia namna ya kuyafanya mambo kwa sababu umeamua tu na kujisikia. Kila kitu ambacho kinafanyika kwenye nchi hii kinatoka kwenye kimywa cha mheshimiwa raisi kwa sababu yeye ndiye mtu mwenye kauli ya mwisho kabisa. Hata mimi nilikuwa nina mashaka sana na haya mambo, mimi nimeanza kufanya kazi kabla hata wewe haujazaliwa hivyo najua namna michezo ya siasa inavyokuwa inafanyika”

“Nina uhakika Yule waziri hana hatia ila kuna watu wapo pembeni wamejua tu kuzichanga karata zao vyema na kwa wakati huu wameshinda mchezo japo wametumia mbinu ya kitoto sana ila ndio washindi. Mimi nilimfuata mheshimiwa raisi ili kumweleza haya kwamba huenda kwa nyuma kuna michezo ambayo inaendelea lakini sijui hawa watu wamemuingiaje mheshimiwa raisi mpaka naye akawaamini, nahisi ni kwa sababu yeye alikuwa amechanganyikiwa na hajui atawaambia nini wananchi hivyo alivyopata wazo ambalo aliona litamtoa yeye kwenye lawama hakuwaza mara mbili akaamua kulipokea”

“Watu ambao wanaonekana wapo nyuma ya hili jambo wanaonekaan kuwa ni watu wenye nguvu mno, kumfanya waziri kama Yule akubaliane na wewe lazima nyuma yake kunakuwa kuna nguvu kubwa sana au kuna kitu kikubwa ambacho kinatumika kumfanya mtu akubali kila kitu ambacho anakuwa anakisiliza. Mheshimiwa raisi aliniambia kwamba niachane na haya mambo kwani yameisha salama tusije tukazusha mengine yakamharibia madaraka yake, kama mhusika kakubali kuhusika basi hakuna namna zaidi ya kuyateketeza magenge yake yote na hiyo ndiyo kazi ambayo inafanyika kwa sasa” mkurugenzi Gulamu Leopard alimweleza kijana wake yale ambayo hakuwa akiyajua kwamba hata yeye hakuwa na uhakika kabisa na hayo mambo ila hakuwa na cha kufanya.

“Kwahiyo mheshimiwa yeye anacho kiangalia ni nafasi yake tu?”
“Hivyo ndivyo siasa ilivyo bwana mdogo”
“Sasa kwanini ulikubaliana nae kirahisi sana hivyomkuu?”

“Mimi sijakubaliana naye kirahisi, ndani ya nchi hakuna mtu mwenye huo uwezo wa kukubaliana na raisi kwa sababu sisi tunaishi kwa kufuata amri yake hivyo anacho kiongea sio makubaliano bali ni amri ambayo utake usitake ni lazima uifuate na hii ni nchi yake, anafanya anacho kitaka yeye mpaka muda wake uishe”
“Kwahiyo hata kama anakosea mahali hatakiwi kurekebishwa?”

“Ngoja nikukumbushe kitu bwanamdogo, kwenye nchi hii wamewahi kutokea wazalendo ambao ulikuwa ukiikata miili yao tu inatoka damu yenye rangi ya bendera ya nchi hii. Wale watu ulikuwa ni mfano mzuri sana na kama alama nyingine ya ushindi wa taifa hili, walipigana pale ilipo wabidi, walipambana na kila namna ya udhalimu ili tu kuiweka nchi kwenye hali ya usalama ila walikosea sehemu moja tu pekee. Walikosea kuanza kuwagusa viongozi wakubwa, kwenye siasa tunaamini kwamba raisi hakosei bali huwa anapitiwa tu au kutingwa na majukumu ambayo yanamfanya achanganye baadhi ya mambo ambayo yanakuwa hayaendi sawa na hata mkitaka ayabadilishe mnatakiwa kwenda kumuomba na sio kufanya makubaliano”

“Kitu ambacho unatakiwa kukiweka akilini ni kwamba Yule ndiye amiri jeshi mkuu wan chi hii, yeye ndiye mtu anaye sikilizwa na kila mtu haijalishi wewe una cheo gani, yeye ndiye anaye toa amri kwa watu wote ndani ya nchi. Kwenda naye kinyume ni kwamba umeiasi nchi,anaweza kukufuta kazi muda huo huo na kukupatia kesi nzito na akatoa mwenyewe amri ya hukumu unayotakiwa kuipata, je unahisi bado unaweza kupingana na maamuzi yake? Raisi hata kama akiwa mtu wa hovyo, akiwa mtu ambaye anakurupuka kufanya maamuzi, akiwa ni mtu asiye na maono ya mbali, kitu pekee ambacho unatakiwa kukiweka akilini ni kwamba; Yule amechaguliwa na wananchi kukaa IKULU na hao hao wananchi ndio wana uwezo wa kumtoa IKULU na sio wewe pekeyako, nadhani sasa unanielewa vyema”

“Ndiyo mkuu, nimekuelewa ila mimi sikuhitaji tumhusishe raisi katika hili?”

“Whaaaat?”
“Hili jambo nahitaji nilifanye pekeyangu, hata dada yangu sijue kabisa”
“Una mpango gani?”
“Nina uhakika kwa asilimia miamoja kwamba huyu waziri hahusiki kwa lolote”
“Kipi kimekufanya uamini hivyo?”
“Nilimwangalia sana kwa makini mkewe akiwa anaongea mbele ya vyombo vya habari, alionekana kuongea kwa simanzi sana, inamaana hakupenda alichokuwa anakifanya, sasa kwanini asikipende? Huenda anajua anaongea uongo wa kumpeleka mumewe sehemu mbaya na hata yale maneno yake anaonekana kabisa kwamba amelishwa na mtu aweze kuyaongea. Jambo lingine nimekuja kugundua siku ile namuona mumewe akiwa anaongea mahakamani, ni mtu ambaye alikiri kuhusika lakini ukiangalia uso wake ulikuwa unaonyesha kabisa kwamba unapingana na yale maelezo ambayo alikuwa anayatoa hivyo naye alidanganya kama mkewe”

“Kwahiyo unataka kusemaje?”
“Yule mtu hahusiki kabisa na hili tukio”
“Kipi kimekufanya uhisi upo sahihi?”
“Unakumbuka uliwahi kunifundisha kwamba udhaifu wa mtu upo kwenye kile kitu ambacho anakipenda sana”
“Ndiyo, sasa hilo linahusikaje hapa”
“Familia ya waziri iko wapi?”
“Unataka kusema kwamba huenda wametumia familia yake kumfanya akubali kila kitu?”
“Ndiyo mkuu”
“Ooooh shiiit!” mkurugenzi aliongea akiwa anatabasamu na kumpiga piga Calvinjr mgongoni, alimtengeneza mtu ambaye alikuwa anawaza mbali sana.
“Kwahiyo unahitaji nini?”

“Najua wewe hakuna taarifa ambayo hauna ndani ya nchi hii, naomba unipe location ya sehemu ilipo hiyo familia”Calvinjr aliongea kwa kumaanisha sana akiwa ana imani kwamba huko angeenda kuupata ukweli wa kutosha ambao utawafanya wapate majibu ya maswali yao.

“Hakikisha haukamatwi huko unako enda na kama ikitokea umeamua kuua, usiache alama kabisa huko kwa maana mtu ambaye alikuwa ana uwezo wa kuua kama wewe aliwahi kuuawa miaka ya nyuma huko hivyo kama ukifanya hivyo utazua taharuki mpya na vyombo vingi vya usalama vitaanza kuweka jicho la umakini sana, fanya mauaji ya kawaida tu usiache alama yoyote ile” Mzee huyo alikubali kumpa location ya eneo ambalo ilikuwepo familia hiyo huku akimsisitiza kijana wake huyo asiende kufanya mauaji ya kikatili huko ambako alitakiwa kwenda kuichukua familia hiyo kwa maana ilikuwa chini ya ulinzi wa jeshi hivyo kuipata kwake ilitakiwa kutumia mabavu na kuondoka na familia hiyo ambapo wangeitumia kuweza kuupata ukweli.
“Asante sana bosi”

Kichaa kapewa rungu na kiongozi wake, nini anaenda kukifanya? Kumbuka huyu hajulikani kabisa, alikuwa ni jasusi wa siri sana hivyo eneo lolote ambalo angepatikana ingekuwa ni hatari sana kwake alitakiwa kujilinda mno.

Unahisi ni kwanini kiongozi wake alimsisitiza kutofanya mauaji ya kikatili, kuna nini nyuma ya huyu kijana? Na huyo anayesema kwamba aliwahi kufanya mauaji ya kikatili huko nyuma ni nani? Episode ya 28 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kuimalizia yote mpaka mwisho kwa 2500 tu.

2500 yako tu nakutumia pdf yote.

Lipia kwa namba

0621567672 ( WhatsApp)

0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA

Muwe na asubuhi njema.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 29:
Ilikuwa imepita miezi sita tangu mheshimiwa waziri aweze kuhusika na tukio la kulipuliwa kwa bunge pamoja na kunyongwa kwake na ndio muda ambao Calvinjr aliamua kulivalia njuga suala hilo kwani ulipita ukimya mkubwa sana.

Mwanaume baada ya kupewa anuani ya sehemu ambayo alitakiwa kwenda kuichukua familia ya mheshimiwa waziri wa ardhi, hakutaka kabisa kumshirikisha dada yake, alihitaji jambo hilo alifuatilie yeye mwenyewe huku aliyekuwa na taarifa juu ya jambo hilo ni bosi wake tu. Familia hiyo ilikuwa imehifadhiwa ndani ya mji wa Morogoro, huko ilikuwa inalindwa kwa siri sana isivyokuwa kawaida kwani walimuahidi mheshimiwa waziri kwamba watailinda familia hiyo ndiyo maana akakubali kuibeba kesi isiyokuwa yak wake.

Watu hao walienda kuiacha familia hiyo huko kwa sababu walijua kwamba kama wangeiacha ndani ya jiji la Dar es salaam ingetumika kufanyia uchunguzi huenda mambo yao yangekuja kujulikana siku moja hivyo waziri wa ulinzi alikuwa anahakikisha familia hiyo ipo salama ndani ya mji huo wa Morogoro kwa siri kubwa mno ili isije ikaingia kwenye hatari lakini haikuwa hatari kama walivyokuwa wamelifikisha jambo hilo kwa mheshimiwa raisi bali kuna mambo ambayo watu hao walikuwa wanajaribu kuyaficha yasije kujulikana kupitia familia hiyo.

Mwanaume siku hiyo alikuwa na gari yake kuelekea ndani ya mkoa unao sifika kuwa na vipaji vingi sana vya mpira. Eneo ambalo alikuwa ameelekezwa halikuwa mbali sana kutoka ilipo stendi kuu ya Msamvu hivyo alilazimika kupita hiyo sehemu na kwenda kuihifadhi gari yake mbali kidogo na stendi hiyo eneo ambalo halikuwa na mwingiliano wa watu wengi. Alishuka kwenye gari hiyo akiwa akiwa ndani ya koti jeusi, mikononi alikuwa na gloves,kichwani kofia nyeusi na barakoa ambayo iliuficha uso wake.

Nyumba ambayo alitajiwa alikuwa anaiona mbele yake mita kama miambili hivi, ni nyumba ambayo ilikuwa imejitenga kidogo na nyumba zingine na ilikuwa ni nyumba ya kifahari sana. Alijigusa kiunoni, alikuwa na bastola moja tu pekee na upande wa pili alikuwa ana kisu kidogo tu, alitabasamu na kuanza kusogea ndani ya hilo eneo. Alivyo karibia kufika sehemu hiyo, aliitoa simu yake na kuzima kamera zote ambazo zilikuwa ndani ya nyumba hiyo ili kitakacho fanyika hapo kibaki kuwa siri ya mambo yote ambayo atayafanya.

Alisogea mpaka getini na kugonga, hakuna mtu hata mmoja ambaye alionekana kuwa ndani kwa maana palitulia sana, mwanaume aligonga tena lakini geti halikufunguliwa, aligonga kwa mara ya tatu, ndipo alisikia kama kuna mtu anakuja uelekeo wa geti hilo kwa hatua nzito za buti ambalo bila shaka lilikuwa kwenye mwili wake. Alifungua geti kisha akasogea pembeni, ni kama naye alihisi kitu hivyo hakukurupuka kutoka nje, ila alishangazwa baada ya kuona hata mgongaji naye hajitokezi kuingia ndani, akaamua kutoa kichwa chake ili kuchungulia kama ni mtu yupi alikuwa amefika hapo.

Hilo ndilo kosa ambalo alilifanya, alipigwa ngumi ya kichwa ambayo ilimfanya ajibamize kwenye geti hilo zito vibaya na kutoa mlio wa maumivu kwa maana kichwa chake kilikuwa kimepasuka, kelele zake ni kama zilikuwa za kumpa nafasi ya kusikilizia maumivu yake tu kwani kisu kilizamishwa kwa nguvu, akajipiga piga kidogo na mikono kifuani na kuoteza maisha. Calvinjr hakuwa na muda wa kukaa hapo,alichungulia ndani hakuona mtu pale nje hivyo akaingia kwa tahadhari sana maana alielewa kwamba huenda waliopo humo ndani hawakuwa watu wa kawaida kama alivyokuwa yeye.

Ukimya ulikuwa mzito sana ambao hata yeye ulianza kumtisha, aliona mlango ukiwa umefungwa ila akasikia mchakacho kwa upande wa nyuma ya nyumba hiyo hivyo akajua kwamba kuna mtu yupo upande huo akaanza kusogea taratibu ili aweze kukutana naye. Pande la mtu lilikuwa upande wa nyuma wa nyumba hiyo likiwa linavuta sigara taratibu, Calvinjr alijitokeza akiwa ameiweka silaha yake juu kwa kunyoosha mikono yake kama mtu aliye salimu amri. Mwanaume huyo ambaye alikuwa mbele yake alikuwa ndani ya kombati ya jeshi juu akiwa na tisheti ya kawaida tu sigara ikiwa kama kiburudisho kwake, aliitoa bastola kwa kasi kwenye kiuno chake ila alitulizwa na maneno.

“Ningeamua kukushambulia kwa hii bastola ningekuwa nimekuua kwa muda mrefu sana ila sijataka kufanya hivyo kwa sababu naona kabisa wewe unaweweza kunifaa kunipima kasi yangu ya jasho la mwili usiku huu” Mwanaume aliongea kwa kujiamini huku akiwa anaitupa chini bastola hiyo kwa madaha na kumfanya mwanaume Yule ambaye alikuwa mbele yake acheke kwa dharau mno.

“Sijawahi kukutana na mtu akanitamkia maneno ya dharau namna hayo leo ndiyo mara ya kwanza kwenye maisha yangu nakutana na mtu ambaye anataka pambano na mimi kwa maana wengi huwa wananikimbia”

“Mhhh mpo wangapi kwani? Maana kama inakufaa ungewaita wenzako waje kukusaidia kwa sababu hayo maneno hautakuwa na nafasi ya kuyatamka tena?”
“Wewe ni nani kwanza ambaye unakuja eneo kama hili na kuanza kuleta maneno ya tambo? Unajua upo wapi hapa?”
“Yes, najua nipo wapi na nafanya nini. Naomba nipatie huyo mwanamke na watoto wake niondoke kistaarabu kama hutaki ofa ya pambano na mimi ambayo nimekupa kwa maana unaonekana muoga sana”
“Hahahahaha, hivi una wazo lolote juu ya hicho kitu unacho kiongea?”

“Nimekuuliza mpo wangapi hapa, ili uwaite wenzio waje kukusaidia?” Calvinjr alitamka kitu ambacho kilimfanya mwenzake amuone kama ana dharau sana. Mwanaume huyo aliiachia bastola yake na kuirushia pembeni, kama mgeni huyo akikuwa ameomba pambano naye alihitaji kumonyesha namna ulimwengu wao unavyokuwa.

Aliuchota mchanga chini kwa kiatu chake na kuurushia pale alipokuwepo Calvinjr, wakati anauzuia mchanga huo, alipigwa na kitu kizito kwenye msuli wa mkono, hiyo ilikuwa ngumi ya jitu hilo lilillokuwa limejazia sawa sawa kabisa kisha akabingwa buti ambalo lilimfanya ayumbe yumbe mpaka kwenye ukuta wa nyumba hiyo kisha akakaa sawa.hakupewa nafasi ya kumfanya apumzike kwa muda mrefu ni baada ya kuhisi mvumo wa kitu kizito kuonekana kikiwa kinakuja pale alipokuwepo, aliianama na kupishana na ngumi ambayo ilikita kwenye ukuta wa jumba hilo na kuifanya hiyo sehemu itikisike kwa nguvu hata hivyo aliishia kupigwa teke la kifua ambalo lilimrushia mbali na kumfanya atake kudondokea chini ya ardhi, hata hivyo alitanguliza mkono wake chini akajirusha na kutua vyema akiwa amesimama kwa mara nyingine.

Calvinjr alitikisa vizuri buti lake la mguuni na kumsubiria mtu huyo aje,mwanaume huyo aliyekuwa ana nguvu za mikono na miguu alisogea tena na kurusha ngumi mfululizo ila alirudi nyuma hatua kadhaa baada ya kupokea ngumi nzito ya usoni ambayo ilimfanya arudi nyuma hatua kadhaa akiwa anatikisa kichwa chake kwani alihisi kama anasikia kizunguzungu na alipewa hiyo nafasi mpaka alipokaa sawa kwa mara nyingine tena. Kwa sasa alianza kusogea kwa tahadhari ambapo alijirusha na kujigeuza na teke hewani ili atue nalo kwenye kifua cha Calvinjr ila kwa bahati mbaya hakupewa hiyo nafasi kwani akiwa hajamfikia, Calvinjr aliruka naye huko huko juu na kumkita teke zito la mbavu mwanaume huyo alijigongesha vibaya ukutani.

Calvinjr aliangalia saa yake, dakika kumi zilikuwa zimepita akiwa bado yupo na mtu huyo, jambo hilo aliona kwamba ni la hatari sana kupoteza muda namna hiyo, alikitoa kisu kidogo kwenye mkono wake. Mwanaume Yule alijinyanyua akiwa anajinyoosha kwa hasira kitu ambacho kilifanya amfuate Calvinjr kwa jazba sana na kuanza kurusha ngumi kwa nguvu. Kitu alifanywa ni kuchanwa chanwa na kisu kama nyama ya buchani kisha mwanaume akazamisha kisu hicho kwenye moyo wa mwanaume huyo ambaye aliishia kuyatoa macho kama vile alitamani kuomba msamaha ila muda ulikuwa umeisha.

Calvinjr aliusogelea mlango huo wa ndani na kuusukuma, ulifunguka bila shida ambapo sebuleni alimuona mwanaume mmoja ndani ya kombati akiwa yupo busy na simu yake ya mkononi, alikuwa upande wa nyuma yake hivyo aliona kila kitu. Mwanaume huyo alikuwa anaangalia video za ngono huku mikono yake ikiwa ndani ya suruali yake akiendelea kujichua. Mwanaume alisikitika kwa kitendo ya kipuuzi ambacho alikuwa anakifanya mwanaume huyo, alimmiminia risasi nne kichwani ambazo zilileta taharuki humo ndani na kumfanya mwanaume mmoja ambaye alionekana kutokea jikoni kurusha kisu kwa nguvu ambacho kilikuwa kwenye mikono yake.

Kisu hicho Calvinjr alikikwepa kwa kuinama, huku mwanaume huyo akiwa anakimbia kwa nguvu sana kumuwahi Calvinjr kabla hajaruhusu risasi nyingine kutoka kwenye bastola. Calvinjr alilipiga sofa ambalo lilikuwa mbele yake na mguu kwa nguvu ambapo mwanaume Yule aliyekuwa anamkimbilia, alijigongesha na kudondoka chini vibaya, alivyotaka kunyanyuka tu risasi moja ilizama kwenye goti lake akabaki anapiga kekele za maumivu akiwa anagalagala hapo chini.
“Mpo wangapi humu ndani?”
“Tupo wanne”
“Una uhakika”
“Naomba usiniue tafadhali, mimi ni mpishi tu humu ndani sihusiki kwa lolote”
“Kwani mimi nimesema unahusika na lolote?”
“Hapana kiongozi mimi sijui lolote kweli” mwanaume huyo alikuwa anaomba msamaha baada ya kuona mwenzake kapigwa risasi vibaya za kichwa ambazo ziliyachukua maisha yake hata yeye mwenyewe alikuwa amepokea risasi ya goti mpaka wakati huo. Kitu kimoja kwake lafudhi yake haikuwa ya kitanzania.
“Unaitwa nani?”
“Naitwa Paul Amza”
“Kwenu wapi?”
“Rwanda”
“Ulifikaje huku?”
“Kuna mtu alinipa kazi ya kuja kuwapikia watu hawa?”
“Whaaat!”
“Ndiyo kiongozi, mimi sijui lolote naomba uniache tafadhali”
“Aliyekupa hii kazi anaitwa nani?”
“Blaise Norbert”
“Ni nani huyo mtu?”
“Ni dakitari mkubwa sana ndani ya nchi ya Rwanda”
“Daktari wa Rwanda anahusikaje na Tanzania?”
“Sijui kiongozi mimi alinipa tu kazi ya kuja kuifanya huku, naomba uniache niende nakuahidi sitarudi tena kwenye hii kazi”
“Mama na watoto wake mlio wahifadhi huku wapo wapi?”
“Sijui unacho kiongea” jibu lake lilimfanya Calvinjr kumnyooshe bastola mtu huyo kuelekea kwenye kichwa chake.
“Wapo juu, wapo juu, usiniue tafadhali”
“Unajua kabisa nikikuacha hai nitakuwa nimefanya kosa eeh?”
“Nakuahidi sitamwambia yeyote juu ya hili”
“Sijawahi kumwamini binadamu” Calvinjr alitamka na kukifumua kichwa cha mwanaume huyo ambaye aliionekana kuwa bado kijana tu. Tukio hilo kuna mwanamke alikuwa amejibanza kwenye kona ya juu akiwa analishuhudia. Alishangaa namna mwanaume huyo alivyokuwa na roho ya kikatili kwa kuweza kuwaua watu hao bila huruma wala kujiuliza mara mbili, alikimbia kwa hofu huku akiubamiza mlango kwa nguvu kubwa ya uoga, Calvinjr aligeuza macho yake na kuangalia eneo hilo ambalo alihisi kuna mtu alikuwa pale.

Unadhani kinafuata nini? Episode ya 29 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 30
Calvinjr aliamua kupandisha juu ya ile sehemu ambayo alikuwa ana uhakika kwamba familia hiyo ilikuwepo. Alifika na kukuta mlango wa hapo ndani umesukumwa tu na haukufungwa huenda ni kwa sababu ya hofu kubwa ambayo alikuwa nayo aliyekuwa anaufunga huo mlango ndiyo maana hakukumbuka hata kuweka komeo. Mwanaume aliusukuma na kuweza kuingia ndani ya chumba hicho ambapo aligundua kwamba kilikuwa chumba cha kulala kwa namna kilivyokuwa.

Pembeni ya kona moja ya chumba hicho, alikuwa anaonekana mama ambaye alikuwa amewakumbatia wanae, bila shaka alikuwa ni mke wa waziri wa ardhi, mwanamke huyo alikuwa anatetemeka sana kwani mtu aliyekuwa anamuona mbele yake, muda mchache tu uliokuwa umepita alitoka kumshuhudia akiwa anafanya mauaji ya kikatili isivyokuwa kawaida.

"Naomba usiwafanye chochote wanangu tafadhali, hawana hatia yoyote ile" kauli ya mwanamke huyo akiwa kwenye majonzi ndiyo iliyo mfanya Calvinjr agundue kwamba ile bastola ambayo alikuwa nayo kwenye mkono wake ndiyo ambayo ilikuwa inamtisha mwanamke huyo, hivyo akaamua kuihifadhi kiunoni na kukaa kwenye kiti ambacho kilikuwa karibu na mlango.

"Dada yangu pole sana kama nimekushtua kwa ulicho kiona pale chini, mimi sijaja hapa ili kukudhuru wewe na watoto wako bali nimekuja hapa ili kukupa msaada"
"Wewe ni nani mpaka useme unataka kunipa msaada? Unanipa msaada wa nini wakati naishi kwa furaha na wanangu, nakuomba sana uondoke hapa" mwanamke huyo aliongea kwa jazba sana akimhitaji mtu huyo aondoke mbele yake.
"Mimi kukutajia utambulisho wangu siwezi ila najua kwamba wewe hauishi kwa furaha kama unavyo niambia hapa bali unaogopa"

"Nini!. Nimwogope nani?" Mke wa waziri aliongea kwa kuonyesha kwamba hakuna mtu ambaye anamuogopa ila kiuhalisia alikuwa anatetemeka sana.
"Unawaogopa watu ambao wamemuua mumeo" kauli ya Calvinjr ilimfanya mwanamke huyo anyanyuke mwa hasira na kuanza kumpiga makofi Calvinjr huku akiwa analia, mpaka pale alipochoka, akajikunyata konani akiwa anapiga makelele ya uchungu.
"Ondoka kwenye maisha yangu, niache mimi na wanangu. Unataka kuniletea matatizo kwenye maisha yangu. Acha niishi maisha ya furaha na wanangu"
"Hivyo ndivyo walivyo kudanganya kwamba utaishi maisha ya furaha? Nisikilize vizuri dada yangu, wewe kuwa na hawa watu haupo salama hata kidogo. Mipango yao ikikaa vizuri hawatakuwa na uhitaji na wewe tena hivyo lazima watakuua tu wewe na wanao ili kuendelea kuilinda siri yao na mipango yao kwa ujumla"
"Wameniahidi kunilinda maisha yangu yote mimi pamoja na wanangu" aliongea kwa jazba sana mwanamke huyo.
"Hivyo ndivyo wanasiasa walivyo pale wanapokuwa wanahitaji kukamilisha mambo yao, watakulaghai kwa maneno matamu sana ili waiibe akili yako ila pale wanapokuwa wamekamilisha mipango yao, hawatakukumbuka tena, habari yako inaweza kuishia hapo hapo"
"Wewe haya mambo umeyajulia wapi?"
"Mimi nipo kwenye mfumo japo sio mwanasiasa"
"Kwahiyo wewe ni nani?"
"Siwezi kukwambia uhalisia wangu kwa sababu kama nikifanya hivyo nitayaweka maisha yako hatari zaidi hivyo inatakiwa usinijue kabisa"
"Kwangu unataka nini?"
"Nahitaji kukusaidia wewe na watoto wako msafirishwe kwenda nje ya nchi mahali ambapo mtakuwa salama wakati sisi tunashughulika na wahusika wote ambao walikuwa nyuma ya huu mpango na kuamua kumsingizia mumeo ili kuwapumbaza wananchi ila kabla ya kufanya hivyo kuna kitu kimoja ambacho unatakiwa kunisaidia"
"Kitu gani?"
"Nahitaji uniambie kila ambacho kilitokea na namna ulivyoweza kuthibitisha kuhusu mumeo kuhusika na kulipua bunge pamoja na kuhisika na mauaji ya watu wengi namna ile. Na je ni kweli alihusika? Na kama hakuhusika, kwanini uliongea vile? Huo utakuwa ushahidi mkubwa sana ambao utakuja kutusaidia kwa baadae"
"Hapana, siwezi kufanya hivyo kamwe"
"Najua unahofia usalama wa watoto wako ila hii ndiyo njia ambayo itakuja kukuweka salama wewe na wanao, kwa sababu hawa watu mwisho wao unakuja"
"Unahisi kwanini natakiwa kukuamini wewe na kukwambia ukweli?"
"Kwa sababu ndiyo njia pekee kwa maana hauna njia nyingine, kwani unajua waliokuwa walinzi wa mumeo wako wapi?"
"Hapana sijui"
"Wote wameuawa ili kulinda siri kwani wanahisi walikuwa wanajua ukweli kwamba kiongozi wao hakuwa akihusika kwa lolote hivyo wanaweza kuja kuropoka hapo baadae"
"Hapana, hapana, kwanini wawaue watu ambao hawana hatia?"
"Kwani mumeo alikuwa na hatia?"
"Hapana, ndiyo aaah MUNGU wangu!" Mwanamke huyo alikuwa anajichanganya mwenyewe na kuanza kuropoka ukweli.

"Ningeamua kukuua ningeshakuua muda mrefu sana ila hawa watu wamekuja kukuficha huku ili watu wasipate nafasi ya kukuhoji kuhusu ukweli, hususani watu wa usalama ndiyo sababu wakaamua kukuweka chini ya jeshi kwa maana taasisi hizi haziingiliani kwenye majukumu ila kama tungekuwa tumekupata muda mrefu basi ukweli tungekuwa tumeupata"

"Kwahiyo wewe ni mtu wa usalama?" Calvinjr aliitikia kwa kutingisha kichwa chake.
"Nitakwambia kila kitu ila naomba sana uhakika wa usalama wa wanangu, hata kama mimi nitakufa lakini sitaki lolote liweze kuwapata wanangu, tafadhali sana"

"Mmekuwa salama baada tu ya mimi kuingia ndani ya hili eneo na kwa sasa mtatolewa kabisa kwenye nchi hii na hakuna mtu atajua mliko enda hivyo huko mtaenda kuyaanza maisha mapya ambapo tutahakikisha mnaishi maisha mazuri wewe na wanao"

"Ilikuwa siku moja jioni ambapo kuna watu walikuja nyumbani na mwanaume mmoja ambaye mimi sikuwahi kumuona ila ni kama walitoka Ikulu kwa maana gari zao zilikuwa na namba za Ikulu, mwanaume yule alisema kwamba ana mazungumzo na mume wangu. Baada ya yale mazungumzo mume wangu alikuwa mtu mwenye mawazo sana ila aligoma kabisa kuniambia kama kuna tatizo lolote, muda wote alikuwa ananiambia kwamba kila kitu kipo sawa"

"Kesho yake walikuja wanajeshi pale ndani na kuwaweka walinzi chini ya ulinzi na kudai kwamba mume wangu ni gaidi, ulitokea mvutano mpaka pale mume wangu alipo jitokeza na kudai kwamba alikuwa tayari kuongozana nao ila kuna maneno ambayo aliniambia kabla ya kuondoka huku akisisitiza kwamba natakiwa kuishi nikijua kwamba mume wangu hana hatia ila kafanya yale kwa ajili ya familia. Alisisitiza kwamba hata wanangu natakiwa kuja kuwaambia kwamba yeye hana hatia kabisa kuhusu lile tukio ambalo ameambiwa alifanye"

"Sasa mimi sikuelewa kwamba kama hajahusika ni kwanini anakamatwa yeye? Nilikuja kuelewa mpaka siku nyingine ambayo nilitembelewa na mwanaume yule yule wa Ikulu ambaye alikuja siku ya kwanza kuonana na mume wangu. Mwanaume yule alinitaka nikathibitishe kwamba mume wangu ni gaidi kweli na niliwahi kuijua mipango yake tangu mwanzo na kuahidi kumripoti kwenye mamlaka za usalama ila akawahi na kuniteka mimi pamoja na wanangu. Hilo ni jambo ambalo lilikuwa linatosha kabisa kumkuta na hatia moja kwa moja kwani watu wangeamini kama mtu alikuwa tayari kuidhuru familia yake mwenyewe basi hakuna kitu atashindwa kukifanya"

"Niligoma sana kuhusu hilo jambo, nisingeweza kufanya hivyo kwa mwanaume ambaye ninampenda sana. Watoto wangenionaje labda? Na vipi kama baadae wakija kujua kwamba baba yao hakuwa na hatia ila mimi niliamua kumsingizia tu? Nilikataa kabisa na kuhaihidi kwamba nitaipigania haki ya mume wangu na kuithibitishia nchi kwamba mume wangu hana hatia, ila nilipewa mtihani ambao ulinifanya niwe na chaguo lile tu pekee"

"Chaguo ambalo nilibakiwa nalo ni kuchagua kati ya mume na mtoto, alidai kwamba kama nikikubali kuongea, basi mimi na wanangu tutalindwa na kupewa kila kitu ila kama nikigoma kuongea basi wanangu watauawa mbele yangu kisha mimi nitaachwa niishi maisha ya kikatili sana ambayo sijawahi kuyaona. Hiyo ndiyo sababu ambayo ilipelekea mimi kuwa msaliti kwa mume wangu, ni kitu ambacho sidhani hata kama mbingu zitanisamehe kabisa kwa ujinga ambao niliufanya" wakiwa wametoka nje ya chumba hicho ili watoto wasiweze kusikia lolote lile, mwanamke huyo alitapika ukweli wote wa mambo na namna watu hao walivyokuwa wamemuweka kwenye mtego ambao hakuwa na namna ya kuuepuka.

"Hapana hauna haja ya kujilaumu sana, umefanya kitu kikubwa sana ili kuweza kuilinda familia yako, kama mumeo alijitoa kwa ajili ya ulinzi wa familia basi kama ungeenda tofauti ndipo ungeonekana kwamba umemsaliti mumeo ila kwa hapo umeonyesha ushujaa na kuwa mama bora sana. Hayo ndiyo maisha ya watu ambao waliandikiwa kuwa majasiri" Calvinjr alimpa moyo huku akiwa anaisevu hiyo video ambayo alikuwa ameirekodi kwenye simu yake mama huyo akiwa anautoa ushidi.
"Naomba sana wanangu wawe salama"
"Usijali tunaondoka muda huu pamoja" Calvinjr baada ya kumaliza tu kujibu, simu yake iliita, hakuchukua muda akawa ameipokea haraka sana.
"Pakeji ninayo kwenye mkono wangu. Andaa safari ya hii pakeji leo leo usiku na usimwambie hata mheshimiwa raisi mkuu"
"Sawa mkuu" Calvinjr aliikata simu hiyo ambayo alionekana kuongea na mkubwa wake wa kazi kisha akamtaka mwanamke huyo awachukue watoto waweze kuondoka ndani ya eneo hilo akiwa ana ukweli wote kama alivyokuwa anahisi, sasa kilichokuwa kinafuata ni kujua ni hatua ipi ambayo walitakiwa kuicheza.

Episode 30, inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HAYA TUPITE NA OFA YA DERBY LEO. NA HII MVUA UNAPATA KINYWAJI CHAKO CHA MOTO HUKU UNAGUSA EPISODES HIZI WAKATI UNASUBIRI MMOJA ANYOLEWE LEO BAADAE.

IMALIZIE KWA 2000 tu kama OFA YA WABABE WA KARIAKOO.

Lipia 2000 kwa namba

0621567672 ( WhatsApp)

0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA.

Nakupa pdf nzima kwa hiyo ofa


UKIPASUKA LUPASO LEO SIMULIZI ITAKULIWAZA[emoji41]

GOOD LUCK
FB_IMG_1699167018540.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 30
Calvinjr aliamua kupandisha juu ya ile sehemu ambayo alikuwa ana uhakika kwamba familia hiyo ilikuwepo. Alifika na kukuta mlango wa hapo ndani umesukumwa tu na haukufungwa huenda ni kwa sababu ya hofu kubwa ambayo alikuwa nayo aliyekuwa anaufunga huo mlango ndiyo maana hakukumbuka hata kuweka komeo. Mwanaume aliusukuma na kuweza kuingia ndani ya chumba hicho ambapo aligundua kwamba kilikuwa chumba cha kulala kwa namna kilivyokuwa.

Pembeni ya kona moja ya chumba hicho, alikuwa anaonekana mama ambaye alikuwa amewakumbatia wanae, bila shaka alikuwa ni mke wa waziri wa ardhi, mwanamke huyo alikuwa anatetemeka sana kwani mtu aliyekuwa anamuona mbele yake, muda mchache tu uliokuwa umepita alitoka kumshuhudia akiwa anafanya mauaji ya kikatili isivyokuwa kawaida.

"Naomba usiwafanye chochote wanangu tafadhali, hawana hatia yoyote ile" kauli ya mwanamke huyo akiwa kwenye majonzi ndiyo iliyo mfanya Calvinjr agundue kwamba ile bastola ambayo alikuwa nayo kwenye mkono wake ndiyo ambayo ilikuwa inamtisha mwanamke huyo, hivyo akaamua kuihifadhi kiunoni na kukaa kwenye kiti ambacho kilikuwa karibu na mlango.

"Dada yangu pole sana kama nimekushtua kwa ulicho kiona pale chini, mimi sijaja hapa ili kukudhuru wewe na watoto wako bali nimekuja hapa ili kukupa msaada"
"Wewe ni nani mpaka useme unataka kunipa msaada? Unanipa msaada wa nini wakati naishi kwa furaha na wanangu, nakuomba sana uondoke hapa" mwanamke huyo aliongea kwa jazba sana akimhitaji mtu huyo aondoke mbele yake.
"Mimi kukutajia utambulisho wangu siwezi ila najua kwamba wewe hauishi kwa furaha kama unavyo niambia hapa bali unaogopa"

"Nini!. Nimwogope nani?" Mke wa waziri aliongea kwa kuonyesha kwamba hakuna mtu ambaye anamuogopa ila kiuhalisia alikuwa anatetemeka sana.
"Unawaogopa watu ambao wamemuua mumeo" kauli ya Calvinjr ilimfanya mwanamke huyo anyanyuke mwa hasira na kuanza kumpiga makofi Calvinjr huku akiwa analia, mpaka pale alipochoka, akajikunyata konani akiwa anapiga makelele ya uchungu.
"Ondoka kwenye maisha yangu, niache mimi na wanangu. Unataka kuniletea matatizo kwenye maisha yangu. Acha niishi maisha ya furaha na wanangu"
"Hivyo ndivyo walivyo kudanganya kwamba utaishi maisha ya furaha? Nisikilize vizuri dada yangu, wewe kuwa na hawa watu haupo salama hata kidogo. Mipango yao ikikaa vizuri hawatakuwa na uhitaji na wewe tena hivyo lazima watakuua tu wewe na wanao ili kuendelea kuilinda siri yao na mipango yao kwa ujumla"
"Wameniahidi kunilinda maisha yangu yote mimi pamoja na wanangu" aliongea kwa jazba sana mwanamke huyo.
"Hivyo ndivyo wanasiasa walivyo pale wanapokuwa wanahitaji kukamilisha mambo yao, watakulaghai kwa maneno matamu sana ili waiibe akili yako ila pale wanapokuwa wamekamilisha mipango yao, hawatakukumbuka tena, habari yako inaweza kuishia hapo hapo"
"Wewe haya mambo umeyajulia wapi?"
"Mimi nipo kwenye mfumo japo sio mwanasiasa"
"Kwahiyo wewe ni nani?"
"Siwezi kukwambia uhalisia wangu kwa sababu kama nikifanya hivyo nitayaweka maisha yako hatari zaidi hivyo inatakiwa usinijue kabisa"
"Kwangu unataka nini?"
"Nahitaji kukusaidia wewe na watoto wako msafirishwe kwenda nje ya nchi mahali ambapo mtakuwa salama wakati sisi tunashughulika na wahusika wote ambao walikuwa nyuma ya huu mpango na kuamua kumsingizia mumeo ili kuwapumbaza wananchi ila kabla ya kufanya hivyo kuna kitu kimoja ambacho unatakiwa kunisaidia"
"Kitu gani?"
"Nahitaji uniambie kila ambacho kilitokea na namna ulivyoweza kuthibitisha kuhusu mumeo kuhusika na kulipua bunge pamoja na kuhisika na mauaji ya watu wengi namna ile. Na je ni kweli alihusika? Na kama hakuhusika, kwanini uliongea vile? Huo utakuwa ushahidi mkubwa sana ambao utakuja kutusaidia kwa baadae"
"Hapana, siwezi kufanya hivyo kamwe"
"Najua unahofia usalama wa watoto wako ila hii ndiyo njia ambayo itakuja kukuweka salama wewe na wanao, kwa sababu hawa watu mwisho wao unakuja"
"Unahisi kwanini natakiwa kukuamini wewe na kukwambia ukweli?"
"Kwa sababu ndiyo njia pekee kwa maana hauna njia nyingine, kwani unajua waliokuwa walinzi wa mumeo wako wapi?"
"Hapana sijui"
"Wote wameuawa ili kulinda siri kwani wanahisi walikuwa wanajua ukweli kwamba kiongozi wao hakuwa akihusika kwa lolote hivyo wanaweza kuja kuropoka hapo baadae"
"Hapana, hapana, kwanini wawaue watu ambao hawana hatia?"
"Kwani mumeo alikuwa na hatia?"
"Hapana, ndiyo aaah MUNGU wangu!" Mwanamke huyo alikuwa anajichanganya mwenyewe na kuanza kuropoka ukweli.

"Ningeamua kukuua ningeshakuua muda mrefu sana ila hawa watu wamekuja kukuficha huku ili watu wasipate nafasi ya kukuhoji kuhusu ukweli, hususani watu wa usalama ndiyo sababu wakaamua kukuweka chini ya jeshi kwa maana taasisi hizi haziingiliani kwenye majukumu ila kama tungekuwa tumekupata muda mrefu basi ukweli tungekuwa tumeupata"

"Kwahiyo wewe ni mtu wa usalama?" Calvinjr aliitikia kwa kutingisha kichwa chake.
"Nitakwambia kila kitu ila naomba sana uhakika wa usalama wa wanangu, hata kama mimi nitakufa lakini sitaki lolote liweze kuwapata wanangu, tafadhali sana"

"Mmekuwa salama baada tu ya mimi kuingia ndani ya hili eneo na kwa sasa mtatolewa kabisa kwenye nchi hii na hakuna mtu atajua mliko enda hivyo huko mtaenda kuyaanza maisha mapya ambapo tutahakikisha mnaishi maisha mazuri wewe na wanao"

"Ilikuwa siku moja jioni ambapo kuna watu walikuja nyumbani na mwanaume mmoja ambaye mimi sikuwahi kumuona ila ni kama walitoka Ikulu kwa maana gari zao zilikuwa na namba za Ikulu, mwanaume yule alisema kwamba ana mazungumzo na mume wangu. Baada ya yale mazungumzo mume wangu alikuwa mtu mwenye mawazo sana ila aligoma kabisa kuniambia kama kuna tatizo lolote, muda wote alikuwa ananiambia kwamba kila kitu kipo sawa"

"Kesho yake walikuja wanajeshi pale ndani na kuwaweka walinzi chini ya ulinzi na kudai kwamba mume wangu ni gaidi, ulitokea mvutano mpaka pale mume wangu alipo jitokeza na kudai kwamba alikuwa tayari kuongozana nao ila kuna maneno ambayo aliniambia kabla ya kuondoka huku akisisitiza kwamba natakiwa kuishi nikijua kwamba mume wangu hana hatia ila kafanya yale kwa ajili ya familia. Alisisitiza kwamba hata wanangu natakiwa kuja kuwaambia kwamba yeye hana hatia kabisa kuhusu lile tukio ambalo ameambiwa alifanye"

"Sasa mimi sikuelewa kwamba kama hajahusika ni kwanini anakamatwa yeye? Nilikuja kuelewa mpaka siku nyingine ambayo nilitembelewa na mwanaume yule yule wa Ikulu ambaye alikuja siku ya kwanza kuonana na mume wangu. Mwanaume yule alinitaka nikathibitishe kwamba mume wangu ni gaidi kweli na niliwahi kuijua mipango yake tangu mwanzo na kuahidi kumripoti kwenye mamlaka za usalama ila akawahi na kuniteka mimi pamoja na wanangu. Hilo ni jambo ambalo lilikuwa linatosha kabisa kumkuta na hatia moja kwa moja kwani watu wangeamini kama mtu alikuwa tayari kuidhuru familia yake mwenyewe basi hakuna kitu atashindwa kukifanya"

"Niligoma sana kuhusu hilo jambo, nisingeweza kufanya hivyo kwa mwanaume ambaye ninampenda sana. Watoto wangenionaje labda? Na vipi kama baadae wakija kujua kwamba baba yao hakuwa na hatia ila mimi niliamua kumsingizia tu? Nilikataa kabisa na kuhaihidi kwamba nitaipigania haki ya mume wangu na kuithibitishia nchi kwamba mume wangu hana hatia, ila nilipewa mtihani ambao ulinifanya niwe na chaguo lile tu pekee"

"Chaguo ambalo nilibakiwa nalo ni kuchagua kati ya mume na mtoto, alidai kwamba kama nikikubali kuongea, basi mimi na wanangu tutalindwa na kupewa kila kitu ila kama nikigoma kuongea basi wanangu watauawa mbele yangu kisha mimi nitaachwa niishi maisha ya kikatili sana ambayo sijawahi kuyaona. Hiyo ndiyo sababu ambayo ilipelekea mimi kuwa msaliti kwa mume wangu, ni kitu ambacho sidhani hata kama mbingu zitanisamehe kabisa kwa ujinga ambao niliufanya" wakiwa wametoka nje ya chumba hicho ili watoto wasiweze kusikia lolote lile, mwanamke huyo alitapika ukweli wote wa mambo na namna watu hao walivyokuwa wamemuweka kwenye mtego ambao hakuwa na namna ya kuuepuka.

"Hapana hauna haja ya kujilaumu sana, umefanya kitu kikubwa sana ili kuweza kuilinda familia yako, kama mumeo alijitoa kwa ajili ya ulinzi wa familia basi kama ungeenda tofauti ndipo ungeonekana kwamba umemsaliti mumeo ila kwa hapo umeonyesha ushujaa na kuwa mama bora sana. Hayo ndiyo maisha ya watu ambao waliandikiwa kuwa majasiri" Calvinjr alimpa moyo huku akiwa anaisevu hiyo video ambayo alikuwa ameirekodi kwenye simu yake mama huyo akiwa anautoa ushidi.
"Naomba sana wanangu wawe salama"
"Usijali tunaondoka muda huu pamoja" Calvinjr baada ya kumaliza tu kujibu, simu yake iliita, hakuchukua muda akawa ameipokea haraka sana.
"Pakeji ninayo kwenye mkono wangu. Andaa safari ya hii pakeji leo leo usiku na usimwambie hata mheshimiwa raisi mkuu"
"Sawa mkuu" Calvinjr aliikata simu hiyo ambayo alionekana kuongea na mkubwa wake wa kazi kisha akamtaka mwanamke huyo awachukue watoto waweze kuondoka ndani ya eneo hilo akiwa ana ukweli wote kama alivyokuwa anahisi, sasa kilichokuwa kinafuata ni kujua ni hatua ipi ambayo walitakiwa kuicheza.

Episode 30, inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu imeisha nianze kupita nayo?maana ni mwoga wa alosto[emoji1666]
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 34

Ndani ya jengo kubwa ambalo lilikuwa na ofisi za watu walionekana kuwa wazito sana kama sio vigogo wakubwa, ndizo zile ofisi ambazo kwa mara ya mwisho mwanaume aliye julikana kama Derick, mwanaume aliyekuwa na kipara king'aacho haswa pamoja na mwili ambao ulikuwa mkubwa mithili ya nyumba. Alionekana tena akiwa anaelekea kwenye ofisi ya kiongozi wake ambapo bila shaka alikuwa anaenda kumuona mtu ambaye alikuwa anampa jeuri ya kuishi mjini maisha ayatakayo mwenyewe.

"Heshima yako kiongozi"
"Nipe ripoti yote Derick"
"Bosi mambo yanaenda kama tulivyo yapanga. Baada ya lile tukio kuna uzembe mdogo ulifanyika wale vijana saba wakakamatwa hivyo tulimuagiza kijana mmoja aweze kuwaua na kweli alifanikisha hilo"
"Huyo kijana yuko wapi Derick?"
"Nilihisi kwamba anaweza kuja kutoa baadhi ya siri kama angebanwa hivyo alivyotoka tu pale nilimuua mwenyewe"
"Safi, napenda sana ufanyaji wako wa kazi, upo makini sana. Enhe nini kiliendelea?"
"Tuligundua mambo kama mawili, kwanza mke wa yule mbunge, tulihisi kwamba anaweza kuwa na taarifa nyingi sana kwani kwa muda mwingi mno alionekana kuwa karibu sana na mumewe hivyo hivyo nikatuma vijana ambao walifanikiwa kumuua ila kuna tatizo dogo lilijitokeza kule bosi"
"Lipi hilo?"
"Vijana ambao niliwatuma kule ni watatu ila walio fanikiwa kurudi ni wawili tu"
"Kwamba huyo mmoja yuko wapi?"
"Alikutwa akiwa amejiua mwenyewe"
"Ina maana kuna mtu alikuwa akitaka kumlazimisha kusema ukweli?"
"Ndiyo bosi, halafu mwilini mwake alikuwa na majeraha makubwa sana kwa ndani, sijui yule mtu alimfanyaje au alimpiga vipi ila alionekana ni mtu mwenye uwezo mkubwa"
"Ina maana kuna watu wanalifuatilia hili jambo kwa ukaribu sana?"
"Ilikuwa hivyo ila kwa sasa hakuna kitakacho patikana tena kwao"
"Una maanisha nini kusema hivyo?"
"Mtu pekee ambaye walitakiwa kumpata alibakia yule mbunge ambaye alikuwa rafiki wa Isaya Ndango, yeye anaitwa James Lewanyika, tulimuwahi na kumuua kabla hajafikiwa na mtu yeyote yule"
"Una uhakika ushahidi wote umeuzika, au wewe ndo unahisi?"
"Bosi nina uhakika kabisa juu ya hilo"
"Na vipi kuhusu familia ya waziri Wailes Mkwavinyika?"
"Hiyo ipo chini ya ulinzi huko Morogoro na hakuna kitu ambacho wanaweza kukifanya kwa sababu mama yule anaogopa kuwapoteza wanae hivyo maisha yake yote ataishi kwa kufuata kile anacho ambiwa na hatakuja kuufungua mdomo wake popote pale kwani anajua wazi kwamba ndio utakuwa mwisho wa kuwaona watoto wake anao wapenda mno"
"Una uhakika Derick?"
"Ndiyo bosi" Derick alikuwa akijiamiki mno, majibu yake hayo yalimfanya huyo bosi wake aweze kumkazia macho usoni kwake ila bosi wake huyo alishtushwa na mlio wa simu ambao ulimtoa kwenye huo umakini wa kufanya mazungumzo na Derick.
"Ooooh shiiit! Bosi anapiga" yeye alikuwa ni bosi ila pia nae alionekana kuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa ni bosi wake. Kwenye kioo cha simu yake jina liliandikwa Mr Black na huyo ndiye ambaye alikuwa akimpigia simu hiyo. Alimgeukia Derick na kumwangalia kwa umakini sana kisha akamuuliza.
"Are you sure?"
"Ndiyo bosi" jibu la Derick lilimfanya aipokee simu yake kwa wasiwasi.
"Hello bosi"
"We mpuuzi unaweza ukanipa sababu za wewe kutumia pesa zangu nyingi kiasi hicho halafu unafanya upumbavu wa kitoto sana namna hii?"
"Mbona kila kitu kipo vizuri bosi"
"Una uhakika wa unacho kisema?"
"Ndiyo bosi, watu wote ambao walikuwa wanahisiwa kuwa na ushahidi hata kidogo tumemalizana nao tayari"
"Na huyo mke wa waziri?"
"Yupo chini ya ulinzi huko Morogoro"
"Una uhakika?"
"Ndiyo bosi" mtu huyo upande wa pili ambaye alionekana kwamba alikuwa anaogopwa sana alitulia kwa muda mfupi na kuna ujumbe ukaingia kwenye simu ya mtu huyo ambayo ilikuwa ni video ikiwa inaonyesha namna eneo hilo la morogoro kwenye nymba aliyokuwa amehifadhiwa mwanamke huyo ilivyokuwa kimya huku ikionekana miili ya walinzi wakiwa wameuliwa kikatili. Macho yake ya kwanza aliyanyanyua na kumwangalia Derick kwa hasira sana.

"Unaweza ukanipa jibu kwamba mwanamke huyo yuko wapi na ni nani ambaye kamchukua hilo eneo?"
"Naomba nipe muda nitalishughulikia kwa sasa"
"Nisikilize wewe mjinga, pesa zangu unazitumia halafu kazi unaifanya kwa mapozi. Kwa sasa nakupa nafasi moja, nafasi ambayo unatakiwa kuitelekeza leo leo"
"Nipo tayari bosi"
"Wewe na kijana wako huyo bwana mdogo leo hii mnatakiwa kuondoka nchini. Nendeni huko Rwanda mpaka nitakapo waambia ni muda mwafaka wa kurudi huku. Mmesababisha madhara makubwa sana kwa sababu hata kama mwanamke yule hamjui mhusika ambaye alihusika kwenye like tukio ila akikiri tu kwamba yale maneno alilishwa basi italeta taharuki na mnaweza kuanza kufuatiliwa kwa ukaribu kitu ambacho kitakuwa cha hatari sana endapo hizi habari zikianza kusambaa."
"Kwa upumbavu ambao umeufanya ilitakiwa nikuue ila nakuacha kwa sasa kwa sababu nina kazi na wewe kwa hapo baadae ila kama ukiichezea nafasi hii ambayo nimekupa basi wewe na mdogo wako nitawaua wote"
"Asante sana bosi" aliitikia kwa unyenyekevu kwa huyo mwanaume ambaye alionekana kumuogopa sana, mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kuyachukua maisha yake muda wowote ambao angeuhitaji yeye hivyo nafasi pekee ambayo alikuwa amepewa ni kuikimbia nchi yake kwa muda usio julikana mpaka pale ambapo angepewa taarifa mpya.
"Unaona ulivyo nidhalilisha leo mjinga wewe, mpaka mdogo wangu anaanza kutishiwa maisha. Jiangalie sana nisije nikakuua kwa mikono yangu mwenyewe. Mpigie simu dogo aje haraka sana hii kampuni atabaki anaiendesha mwenyewe, kwa sasa mimi na wewe na vijana wengine tunaenda nchini Rwanda"
"Sawa bosi" Derick aliitikia huku akitoka nje haraka sana kuanza kutekeza majukumu ambayo alipewa ili asije akapoteza kibarua ambacho kilikuwa kinampa jeuri ya kutumia pesa atakavyo anapokuwa ndani ya jiji.

Mahali patakatifu kama alivyowahi kupaita mwanafalsafa mmoja kutoka ndani ya nchi ya Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, aliwahi kupaita mahali patakatifu kwa sababu ndiyo sehemu ya mhimu zaidi ndani ya nchi. Ndiyo sehemu ambayo anaishi mtu ambaye maamuzi yake ndiyo yanayo amua hatima ya nchi pamoja na wananchi wa nchi hiyo kwa ujumla.

Ikulu, majira ya asubuhi ya mapema kabisa, palikuwa na nuru, nuru iliyo onyesha utulivu na ubora wa mazingira pamoja na watu ambao walikuwa ndani hake. Akiwa ameshikilia gazeti la siku hiyo kwenye mkono wake huku kwenye mkono wake mwingine akiwa ameishika simu ambayo bila shaka alitoka kuitumia muda sio mrefu sana kuweza kuwasiliana na mtu wake kama sio watu wake. Mheshimiwa raisi alipitia gazeti hilo ambalo lilikuwa linaangazia kutimia kwa miezi sita tangu lile tukio la kutisha kutokea ndani ya jiji la DOGMA TULIPO.

Yeye kama raisi alikuwa amesifiwa sana kwa ukomavu wake mkubwa pamoja na moyo wake wa kupambana na wananchi pamoja lakini pia kwa moyo wake mkunjufu wa kukubali kuzisaidia familia za wale wote wahanga wa tukio hivyo watu walikuwa wakimtakia maisha marefu mno raisi wao ambaye waliamini kwamba atawafikisha kwenye nchi ya ahadi, jambo hilo lilimfanya atabasamu huku akiiangalia kwa umakini mkubwa sana simu ambayo ilikuwa kwenye mkono wake mwingine.

Mheshimiwa alitamka
"Maisha ni zaidi ya ule mzingo ambao unazunguka, kwa sababu ule mzingo unazunguka tu pasina kuyatambua mambo vyema ila maisha yanakuzungusha kila pande huku yakikupa somo na funzo kubwa sana ambalo halina ulazima sana wa wewe kulichukua ila ni la mhimu sana kama utalihifadhi kwenye moyo wako"

"Leo naitwa shujaa, leo kila mtu anatamani kupiga picha na mimi, huku wengine wakiangua kilio kila wanionapo wakijiona wenye bahati kubwa pale wanapo jibiwa salamu zao na mimi. Haya ndiyo maisha ambayo tunaambiwa tusidharau sana watu kwani kesho imebeba mengi sana ya siri ambayo yanauhitaji ujasiri ili kuyakabili. Leo nipo sehemu ya mhimu zaidi ndani ya nchi, nikisikilizwa na kila mtu, mimi ndiye mwenye kauli ya mwisho kwenye kila jambo, mimi ndiye ninaye amua nataka nchi yangu iwe vipi na hakuna mwenye uwezo wa kunipinga kwa sababu akifanya hivyo basi anakuwa ameiasi nchi na anakuwa gaidi muda huo huo"

"Ila haya ni matokeo ya maumivu mazito sana ambayo yapo nyuma yangu. Maumivu ambayo hakuna mwanadamu anaweza kuyasimulia zaidi yangu mimi mwenyewe ndiye nayajua, kwa sasa kila mwanamke ananitaka na kunipenda huku wengine wakitamani hata kunibebea tu watoto, hahahahaha. Kweli maisha yanabadilika sana, maisha yanaenda kasi sana, stori ya maisha yangu inasikitisha na kuhuzunisha mno kwa maana imejaa manyanyaso ya watu wengi, imejaa roho mbaya za watu wengi ila hao leo ndoo wanao nipigia magoti na kufanya lolote lile ambalo mimi nahitaji walifanye. Mimi ndiye Mr president mwenyewe"

Mheshimiwa raisi kuna kitu gani anataka kutuambia mpaka kaanza kutupa ABC ya maisha yake?

Episode ya 34 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom