Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 7
“Sijajua ulifanikiwa vipi kuwa raisi wa taifa hili hilo unalijua wewe na njia ulizopita kwani siasa ni michezo ya kijinga tu ambayo kuna muda wajinga ndiyo wanakuwa washindi huku wananchi wakipumbazwa kwamba kuna haki, sijui demokrasi na ujinga mwingine lakini kichwa chako hakikufaa kabisa uwe kwenye nafasi kubwa kama hizo maana uwezo wako ni mdogo sana kichwani. Wakati unamuinua huyo changudoa na kumpa hiyo nafasi kubwa ambayo umempa ulisahau kitu kimoja Denis”

“Kipi hicho?”

“Ulisahau kwamba madaraka huwa yanawabadilisha watu, umesahau kwamba madaraka huwa yanawafanya watu wajihisi kwamba wana nguvu kubwa sana sehemu yoyote ile ambayo wanakuwa wanaenda ndiyo sababu wakisha yapata huwa hawakumbuki tena kuhusu nyuma walikotoka wala watu ambao wamewatoa huko. Wewe hapo ulishikwa mkono na watu wengi sana ambao wamekufikisha hapo ulipo leo lakini si unakumbuka ulichokuja kuwafanya kwa baadae? Ulihisi kama watakuwa tishio kwako ukaamua kuwaua wote ili utawale kila kitu, je wewe uliwahi kuwaza hili kwa mtu ambaye ulikuwa unampa nafasi kwamba anaweza kuwa kama wewe? Kosa kubwa ambalo umelifanya ni kumchukulia kwa udogo huyo mwanamke na huenda kama ungemchukulia kwa ukubwa zaidi usingekuja kunililia hapa nikupe ushauri”

“Mhhh mze nadhani bado haujanielewa vizuri, sijaja hapa kwa ajili ya kutaka unipe shule kwamba nimeshindwa kumdhibiti huyu mwanamke au kanishinda hapana, hapa nipo nahitaji ushauri mmoja tu wa ndiyo au hapana basi, hivyo ulitakiwa kulisikiliza swali langu kwanza kabla ya kuanza kunisomea risala yako hapa”

“Unataka kumuua?” mzee huyo ni kama alielewa mapema sana dhamira ya mtu huyo licha ya kujifanya kwamba alikuwa anazunguka nayo sana.

“Ndiyo, nimekuja hapa ili unishauri kama kumuua mapema hivi itakuwa ni sawa? Maana kama nikiendelea kumpa muda anaweza kuniharibia mambo mengi sana kwa sababu hivi ninavyo zungumza nikiwa njiani kuja huku tayari kuna akaunti zangu za benki zimezuiliwa yaani haziruhusiwi kufanya miamala kitu ambacho kimenichukiza sana kufanyiwa jambo la kijinga na mwanafunzi wangu mwenyewe nadhani natakiwa kulifanyia maamuzi haraka sana”

“Hilo ndilo litakuwa kosa lako kubwa zaidi kuwahi kulifanya kwenye maisha yako”

“Una maanisha?”

“Najua kwa sasa una watu wengi sana kwa upande wako ambao wanakusikiliza na kukutii kwa lolote na wapo tayari hata kufa kwa ajili yako pia na natambua kwamba kwa sasa huenda una mengi ambayo umejifunza ila umeniacha mimi hai kwa ajili ya kuendelea kukupa maarifa ila hivi umewaza kwamba ni kwa sababu gani labda mwanamke huyo ameamua kubadilika haraka sana namna hiyo wakati anakujua kabisa kwamba wewe ni binadamu mkatili sana?”

“Nadhani bado hajanijua vizuri ndiyo maana anahisi anaweza kunimudu”

“Najua kwamba huwa unaigiza kwa tabasamu lako mbele za watu ndilo linalo wafanya watu wahisi kwamba wewe ni mtu muungwana sana ila hawajui binadamu aliyepo nyuma ya hilo tabasamu, huenda ni kweli umeishi hivyo hata kwake pia kwa kumuigizia kwamba wewe ni mtu mwepesi tofauti na ulivyo wewe lakini unatakiwa kujiuliza kwamba kwa muda wote huo ambao huyo binti alikuwa na wewe unahisi hakuutambua udhaifu wako hata kidogo? Unahisi hajui baadhi ya mambo yako ya siri ambayo unahisi hayajui? Unadhani nini kinampa jeuri ya kuanza kukugeuka tena unasema ameanza mapema kabisa hivi?”

“Unanishauri nini?”

“Nitakuelekeza kwa mfano halisi. Biashara ya kuuza miili kwa wanawake imeandikwa tangu miaka na miaka huko kabla hata sisi hatupo kwenye dunia hii kama ambavyo vitabu vitakatifu vinaeleza hivyo ni biashara endelevu ya vizazi na vizazi kama ambavyo sisi tunaendelea kuzaliwa. Kwahiyo hii inaonyesha kwamba hii biashaara haiwezi kuja kuisha hapa duniani ni mpaka siku ya mwisho iweze kufika kama ambavyo tumeahidiwa kwenye vitabu vya dini. Kuna baadhi ya viongozi waliwahi kujaribu sana kuiua biashara hii hata kabla ya vita vya kwanza vya dunia kufanyika lakini walishindwa na hata dunia ya sasa kwa miaka takribani hamsini viongozi wa dini wanajitahidi sana kukemea hii biashara iishe kwani inahatarisha sana mmomonyoko wa maadili na kuleta tamaduni mbaya za kutoka magharibi ambazo zinafanya tamaduni zetu kufa lakini wameshindwa licha ya mamlaka zenye nguvu kuingilia na kupinga kwa nguvu lakini bado imeshindikana. Unahisi ni kwanini jambo hilo limeshindikana kabisa kuisha?

“Ni kwa sababu ni biashara ambayo ina manufaa makubwa sana duniani kwa sasa na watu ambao wanaihitaji ni wengi zaidi ya wale ambao wanahitaji ipotee kwenye mifumo”

“Umejibu sahihi lakini hiyo ni sababu nyepesi sana ambayo haiwezi kuwa na mashiko ya kuifanya isipotee au washindwe kuipoteza kabisa. Uhalisia ni kwamba kwa makusudi au kwa bahati mbaya hawa ambao wanataka hii biashara ifungwe wameshindwa kabisa kujua chanzo chake hasa ni nini wanaishia kukomaa na matokeo yake tu, huwezi kulikomesha jambo kwa kupambana na matokeo yake kwa sababu hata kama utayamaliza yale matokeo ilimradi hicho kitu bado kipo basi kitaendelea kuleta matokeo mengine kila kuitwapo leo na ndiyo maana biashara hiyo haiwezi kuja kuisha kamwe. Kuna wanawake wanafanya hiyo biashara kwa sababu maisha ni magumu sana na kuna watu wengi sana ambao wanawategemea nyuma yao hivyo inafika mahali wanakuwa hawana namna tena zaidi ya kuifanya tu ili wajikwamue kimaisha lakini kuna wengine wanaifanya kwa sababu watu mnaokabidhiwa nafasi kubwa ndani ya nchi hamjali lolote, mnajaza ndugu zenu ambao ni wapumbavu kupitiliza kwenye mifumo ya ajira huku vijana ambao wanastahili mkiwanyima ajira halafu kila siku mnaanza kuwatukana na kuwadhihaki kwamba wanauza miili yao, mara wanawake wote ni Malaya tu, hivi ulishawahi kukaa chini ukajiuliza haya maswali kama kiongozi? Nakuhakikishia hii biashara haiwezi kuisha kamwe kama vyanzo vyake havijajulikana, kuna wanawake wanafanya hivyo kwa sababu ya msukumo wa maisha mazuri ambayo wanayaona kwa wenzao lakini kuna wengine wanafanya ikiwa ni madhara mabaya ya utumiaji wa mitandao ya kijamii bila kusahau msukumo wa marafiki na baadhi ya mambo mengi sana ambayo najua unayafahamu kwenye kichwa chako. Umenielewa nilicho maanisha kutokana na jambo lako ambalo ulikuwa unahitaji msaada?” Denis Kijazo alibaki anacheka tu akiwa anamwangalia mzee huyo, alikuwa ni mzee mwenye akili sana kwa sababu hata elimu yake ilikuwa ni kubwa mno ndiyo maana aliaminiwa mpaka kuwa gavana wa benki kuu ya taifa la Tanzania.

“Moja kati ya ushindi mkubwa ambao niliupatia mezani ni kukuacha wewe hai, kuna muda nawaza kama ningekuua mapema basi ningekuwa nakosa maamuzi ya busara kwenye mambo yangu mengi sana ambayo huenda kwa baadae yangekuja kunileta madhara makubwa sana. Huyu mwanamke natakiwa kujua kwanza ni kitu gani kinampa sana kiburi lakini pia huenda kuna watu ambao wanampa kiburi na kama ulivyosema kwamba nilimchukulia kwa udogo huenda aliitumia nafasi hiyo kutengeneza watu wake ambao alijua hata kukiwa na matatizo wanaweza kumlinda na ndiyo maana anajiamini sana” mzee huyo alitikisa kichwa kuonyesha kukubaliana na jambo hilo kwamba alitakiwa kwanza kujua chanzo na sababu ya mwanamke huyo kubadilika ghafla sana ilikuwa ni nini na ni nani na nani ambao walikuwa wanamzunguka kiasi kwamba wakampa hiyo nguvu ya kuweza kujiamini sana kiasi hicho.

“Ukishindwa kuzimudu hisia zako ambazo zinakuletea mihemko kwenye mwili wako basi duniani mtu yeyote anaweza kukuendesha. Nimemaliza kukueleza ulicho kijia naomba sana niione familia yangu japo kwa picha tu” alipogusia jambo la familia yake aliongea kwa kutia huruma sana na mwanaume ambaye alikuwa mbele yake aliitoa simu yake na kumuonyesha mzee huyo picha ambayo ilimtoa sana machozi. Alikuwa anawaona watu wanne kwenye picha moja ambapo alikuwa ni mkewe, mtoto wake wa kwanza wa kike pamoja na mapacha wawili wa kiume ambao ndio walikuwa ni watoto wake wa mwisho.

“Usijali familia yako ipo salama na inaishi kwa furaha kabisa na kesho ni siku ya kuzaliwa ya hao mapacha. Wote wanajua kwamba wewe ulishakufa tayari wameanza kukusahau kwa sasa zaidi ya kuzikumbuka picha zako tu, moja kati ya makosa ambayo uliwahi kuyafanya kwenya maisha yako ni kuamua kupingana na kile ambacho mimi nilikuwa nakitaka kama ambavyo huyu mwanamke naye ameamua kufanya, huenda yeye atakuwa na majuto makali zaidi hata ya wewe. Kwaheri Professor Mande” alitamka huku akiwa ananyanyuka na kutoka ndani ya chumba hicho ambacho baada ya yeye kutoka tu kiliweza kujifunga chenyewe, aliingia humo akiwa na hasira sana lakini alitoka akiwa mwepesi na akiwa anajua ni wapi ambapo alitakiwa kuanzia ili kuweza kutimiza jambo hilo kwa usahihi pasipo kujulikana kwamba alikuwa anahusika na lolote lile huku professor Mande akibaki kwenye majozi makubwa sana kwani ulipita muda mrefu sana bila kuweza kuiona familia yake huku familia hiyo ikiwa inajua kwamba yeye alishakufa muda mrefu sana.


Chumba kilikuwa kina kiza kila sehemu kasoro katikati tu ya chumba hicho ndipo palikuwa na mwanga ambapo wanaume wanne walikuwa wamemzunguka mwanaume mmoja wote wakiwa vifua wazi bila mashati. Mmoja alizunguka kwa sarakasi huku akijipinda ya kuyatuma mateke yake kwa mwanaume ambaye alikuwa katikati yao lakini mahesabu yake hayakwenda sawa baada ya ngumi nzito kutua kwenye bega lake na kumfanya adondoke vibaya chini lakini alifanikiwa kutanguliza mkono mmoja ambao ulifanikiwa kuupa balansi mwili wake usiweze kwenda wote kabisa chini ila kwa bahati mbaya wakati anatua na mkono huo ulipigwa na teke lenye kilo nyingi na kuvunjika ambapo alipiga kelele sana ila alitulia baada ya teke kutua kwenye uso wake na kumpeleka ukutani ambako kulikuwa na kiza.

Tukio lilikuwa la sekunde ishirini tu wakati mwanaume huyo ambaye alikuwa pekeyake akiyakwepa mateke na ngumi za wanaume wengine watatu, alipigwa ngumi ya mbavu na mwanaume mmoja ambapo baada ya kugeuka kwa hasira alimkita na viganja mwanaume mmoja kwenye masikio yake mpaka masikio yakaziba kabisa akawa hasikii kile ambacho kilikuwa kinaendelea hapo, alipigwa ngumi nyingi za kifua ambapo alibaki anatetemeka huku akiwa anashuka chini taratibu na mdomoni akiwa na damu nyingi sana. Wawili walikuwa wanamshangaa mwenzo alivyokuwa anashuka kama utani, walikwenda kwa pamoja mmoja akiwa chini na mwingine akilenga upande wa juu. Mwanaume huyo alijigeuza haraka sana ambapo alimkwepa wa chini ambaye alishika sakafu na kuyazungusha mateke yake kwa kasi ya ajabu hivyo aliyakwepa kwa sarakasi kisha akakutana na wa juu ambaye alimpiga double kick mbili za haraka haraka ambazo zilimzoa mpaka ukutani ambako kilisikika kishindo kikali sana na sauti ya mtu mara moja tu ikiwa inapiga kelele kisha kukawa kimya ghafla sana.

Wakati anatua chini yule mmoja alikuwa amezungusha mateke mengine lakini yeye alitua nyuma kidogo kwa hatua moja hivyo mateke hayakumpata lakini wakati yule ambaye alikuwa chini ananyanyuka alikuwa ameshika kisu mkononi ambacho bila shaka alikificha kwenye kiuno kwake maana kwenye buti isingewezekana kwa sababu wote walikuwa miguu mitupu bila viatu. Hivyo alikizungusha kisu chake ambacho kilimkosa mwenzake shingoni mkono ukawa umepitiliza. Wakati anahitaji kuurudisha mkono huo ukiwa na kisu shingoni kwa mwanaume huyo, alikuwa ameukwepa na kufanikiwa kuudaka ambapo aliubinya kwa nguvu mshipa mmoja wa mkono wa mwanaume aliyekuwa amekishika kisu hicho akaishia kupiga kelele kwa maumivu hali ambayo ilipelekea kisu hicho kumponyoka kwenye mkono wake na kutua kwenye mkono wa mwanaume ambaye alikuwa anakabiliana naye.

Mwanaume huyo baada ya kukidaka kisu hicho alijizungusha kwa kasi kwenye mkono wa mwenzake na kukizamisha kisu hicho juu ya bega kwa nguvu kisha akakichomoa kwa nguvu na kuuchana chana vibaya sana mkono. Mwanaume huyo alipokea maumivu makali sana, upigaji wake wa kelele ulifanya apokee ngumi nzito ya shingo ambayo ilimfanya apoteze fahamu na kudondokea chini. Dakika moja tu pekee na sekunde chache sana zilifanya mwanaume huyo aimalize kazi. Ulisika mlio wa makofi mtu akiwa anapongea kile kilichokuwa kimefanyika hapo na baada ya muda mfupi taa iliwashwa humo ndani akawa anaonena mheshimiwa raisi Teodensia Mpanzi ndiye ambaye alikuwa anapiga makofi hayo kumpongeza kijana wake.

Episode 7 nasema bye.

Tchao

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
BADO NINAISHI.

Inamhusu mwanaume mmoja ambaye alikuwa ni kiongozi wa genge la kihalifu ambalo lilikuwa linaitwa SARAFU KUMI NA TANO.

Mwanaume huyo alikuwa anasakamwa na mamlaka za usalama ndani ya taifa la TANZANIA kwa miaka kumi bila mafanikio. Ndipo alitumika mwanamke mrembo ANELIA BATON ambaye alimwingiza mwanaume huyo kwenye HONEY TRAP kwa kupitia kikosi hatari kutoka ndani ya shirika la kijasusi kiitwacho HOLY TRINITY, walifanikiwa kumpata mwanaume huyo.


Alihukumiwa kifungo cha miaka sitini gerezani na baada ya hapo angenyongwa. Alipelekwa ndani ya gereza hatari la DOMINIC, huko alikutana na tajiri mmoja ambaye alikuwa amejificha ili kuyalinda maisha ya mwanae ambaye alitekwa.

Tajiri huyo alikutana na mwanaume huyo aliye itwa REMMY CLAUDE na kumuomba akamuokoe mwanae yeye anyemsaidia kumtorosha gerezani. Walifikia makubaliano mwanaume akatoroshwa gerezani.


Huko uraiani alienda kumtafuta mtoto wa kiongozi huyo lakini wakati anafanikisha hilo tajiri huyo alikuja kupata habari kwamba mfungwa huyo aliye Mtorosha gerezani hakufungwa kwa bahati mbaya bali ilikuwa ni mipango yake yeye ili akutane na tajiri huyo.

Alishangaa sana ilikuwaje mtu ajitoe kafara kufungwa gerezani kwa sababu yake? Ndipo akaja kugundua kwamba Remmy alikuwa anautafuta umoja wa watu ambao hawakuwa wakifahamika na tajiri huyo ndiye mtu pekee ambaye angemsaidia kuwajua wote ndani ya umoja huo.

Anakuja kushtuka akiwa amechelewa, mwanaume huyo alikuwa amempata mwanae tayari na kupotea naye hali ambayo ilileta maafa makubwa sana na kulilazimu shirika la kijasusi kuanza na moja kumtafuta.


SARAFU KUMI NA TANO halikuwa pambo bali ilikuwa idadi ya wanafamilia ambao waliuawa kikatili takribani miaka ishirini iliyokuwa imepita ila kwa bahati mbaya mtu mmoja alifanikiwa kuishi.

Sitaki nikumalizie uhondo. Unataka kujua huyo Remy ni nani? Kwanini alijitoa sadaka kwenda gerezani? Huo umoja una nini hasa ndani yake na unaongozwa na nani?

Nini hatima ya maisha ya Remy Claude?

Hili ni moja kati ya andiko ambalo litakufanya ujivunie sana kuyasoma maandishi.

Sasa RASMI IMEACHIWA NA UNAWEZA KUIPATA KWA PESA ZA KITANZANIA SHILINGI 5000 TU.

5000 yako unapewa andiko lote mpaka mwisho.

Unaweza kufanya malipo kwa namba hizi hapa [emoji116]

0621567672.... HALO-PESA

0745982347..... M-PESA

0714581046..... TIGO-PESA

Zote jina FEBIANI BABUYA.

Ni wakati sasa..... KARIBU INBOX.


ASHRAFU NDILO JINA LANGU
FB_IMG_1707902862253.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 8
Aliyekuwa akipambana na hao watu alikuwa ni Donald Daniel, waweza kumuita Donny au 001. Huo ulikuwa ni mtihani ambao alikuwa amepewa na raisi ili aweze kukubali kumpa kazi yeye na mwenzake Dax ili kuweza kumlinda ikiwa ni kama maagizo kutoka kwa mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania.

“Kwa sasa rasmi nyie mtakuwa walinzi wangu” alitamka kwa furaha sana kwani kwake kupata kijana hatari kama huyo tena wakiwa wawili ilikuwa ina maana kubwa sana kwa sababu alijua mbele yake alikuwa na kazi ngumu sana ambayo ingeyahatarisha maisha yake kwa kiwango kikubwa hivyo angewatumia hao kuweza kujipa ulinzi na kuwatumia kwenye kazi zake. Baada ya kumaliza kuwapongeza vijana wake hao kwa uwezo mkubwa ambao walionekana kuwa nao, alienda moja kwa moja mpaka ndani ya chumba chake ambacho alikuwa anakitumia kulala. Baada ya kufika ndani cha chumba hicho alifungua begi lake na kutoa simu moja ndogo ambayo ilikuwa ni mpya tu, akaweka laini mpya pia kisha akafunga begi na kuelekea chooni huku milango yote ikiwa imefungwa vyema sana ndani ya chumba hicho.

Baada ya kufika huko aliiweka ile laini ambayo ndani yake ilikuwa na namba moja tu ambayo ilionekana kuwa binafsi, aliliweka koo lake sawa simu ikiwa inaita kuonyesha kwamba aliyekuwa anataka kuongea naye alikuwa ni mtu mhimu sana kwa upande wake.

“Hello mzee” aliongea na kutulia ili kusikilizia upande wa pili utasema nini lakini kulikuwa na ukimya kama wa dakika moja hivi ndipo akasikika mtu upande wa pili akiwa anakohoa kwa mbali kama ishara ya kumjibu aliyekuwa amempigia kwamba alikuwa amemsikia na alikuwa tayari kwa mazungumzo.
“Hello, heshima yako kiongozi wangu. Sijapata kabisa nafasi ya kukupongeza tangu utangazwe kuwa mshindi hivyo hii inaweza kuwa nafasi nzuri zaidi mimi kukupa mkono wangu wa pongezi”

“Nadhani bila wewe hili lisingewezekana hivyo nikushukuru wewe ambaye ndiye umefanya kila jambo liwezekane. Nikwambie tu kwamba nimeanza kulifanyia kazi lile jambo haraka sana maana niliona kwamba kama tukiendelea kusubiri sana huenda nitazidi kuingia kwenye mikono yake na tusije tukapata nafasi ya kukamilisha hili jambo mapema”
“Hii simu ni salama?”

“Hii ni salama ndiyo maana nimekupigia ili tuongee kwa undani”

“Vizuri maana kwa sasa umeingia kwenye vita na mtu hatari sana hivyo unatakiwa kuchukua tahadhari kwenye kila jambo lako ambalo unakuwa unalifanya”

“Hilo nalielewa mzee nashukuru sana kwa kunijali”
“Nimeona taarifa yako ya baraza jipya la mawaziri kama tulivyo kubaliana lakini nadhani ulifanya kwa hasira sana wakati ulitakiwa kutulia kwanza hata siku nne zipite ndipo utangaze”

“Nilifanya vile kwa sababu alituma mtu na listi yake ambayo alitaka mimi niitangaze tena haraka sana hivyo niliona kwamba kama nikichelewa yanaweza kutokea mengine”
“Hata hivyo ulipaswa kutulia kwanza, yule ni mtu hatari mno ambaye ana watu kila sehemu, anajulikana nchi nyingi sana duniani na ana watu sana huko hivyo hizi Kamari anajua sana namna za kuzicheza ndiyo maana hatutakiwi kabisa kucheza vibaya hata kwa hatua moja biashara itaishia hapo”

“Kwahiyo unanishauri nifanye nini mzee?”

“Kwa sababu umeshatangaza naye vita tayari basi hakuna namna hapo zaidi ya kuingia nae ulingoni moja kwa moja hivyo nataka unisikilize kwa umakini mkubwa sana, unatakiwa kufanya yafuatayo;”

“Nakusikiliza mzee”

“Kwa sasa nguvu yake kubwa ipo kwenye ule ukumbi wake wa ALEXIOS, unatakiwa kuufungia haraka sana kabla hajaanza kujibu mashambulizi”

“Sijakuelewa mzee, kwani ule ukumbu unahusika nini yeye kujibu mashambulizi japo ni kweli nipo kwenye mpango wa kuufunga?”

“Nguvu kubwa aliyo nayo ukiacha pesa nyingi ambazo amejibinafsishia kwenye taifa hili ni watu, ana watu kila idara ya serikali na kila sehemu nyeti pia ya serikali hivyo nataka ufanye hilo ili kuweza kuwajua watu wake ambao wapo kwenye nafasi za juu zaidi serikalini”

“Mzee sijakuelewa bado hilo linahusika vipi na kuwajua watu wake? Kwanini nisingeingiza vijana tu moja kwa moja waanze kufanya upelelezi?”

“Shida sio kuwaingiza vijana kwenda kufanya huo upelelezi ambao wewe unausema, shida unamtuma nani na unamwamini nani? Huyo mtu ana watu kila sehemu na wanamtii kuliko kitu chochote kile kwa sababu amewahakikishia mifumo ya upigaji kila sehemu sasa unaweza kutaka kuwatumia watu hao halafu wakaharibu mpango mapema sana. Kumbuka ikijulikana mapema mimi na wewe ndo basi tena tunakufa kizembe sana, mimi siogopi kufa ila nataka nife nikiwa nimehakikisha kwamba hili limekamilika kwanza hivyo nisikilize kwa umakini utanielewa maana hii nchi naijua kuliko mtu yeyote yule ambaye yupo hai mpaka sasa”
“Nakusikiliza mzee”

“Ukiufungia huo ukumbi wake utakuwa umewaathiri watu wengi sana hususani wawekezaji wenzake na wateja wake wakubwa. Wakikereka lazima wataanza majungu na lawama za hapa na pale iwe ni moja kwa moja au kwenye mitandao kwani sio kila mtu anaweza kuhimili mihemko na kukaa nayo moyoni lazima kuna hata mmoja atakuja kuropoka na kukukosoa hadharani tu awe ni kiongozi wa chama chako au chama pinzani hivyo sisi tutaitumia hiyo mihemko yao kuweza kuwajua hao ambao wapo pembeni yake ambao hawajulikani ili wakati wa kumdondosha tujue kabisa tunamdondosha na watu gani ili tusije tukaleta madhara makubwa maana hawa watu wake wa pembeni ndio ambao wanampa kiburi sana. Umenielewa?”

“Nakuelewa mzee ila sijaona bado mtu wa kumkabidhi hiyo kazi ya kuanza kuwatafuta watu hao kama ikitokea tukapata mwanga na sehemu ya kuanzia”
“Kila kitu kipo kwenye mpango sijakurupuka, wakati hayo yanaendelea kwa sababu yeye huwa ni mtu wa hii michezo sana anaweza akajikausha kabisa kama hayupo huku akiwa anaangalia namna sahihi ya kuweza kukuangusha hivyo mimi kuna kijana ambaye nitamtumia kuhusu hilo ondoa shaka”
“Unamwamini?”

“Ndiyo namwamini kama nafsi yangu na hii kazi ataifanya kwa uwezo mkubwa sana”

“Anaitwa nani”

“Anaitwa Bilali. Ni kijana wangu wa siku nyingi sana ambaye ananitii mimi kuliko binadamu yeyote yule ila kwa sasa ni moja kati ya wacheza Kamari maarufu sana ndani ya hili jiji na hata kwenye huo ulingo huwa anaenda kwa siri sana kuweza kupigana na mimi huwa napenda kwenda kwa siri pia kutazama mapambano yake”
“Mzee mcheza Kamari ndo unataka tumwanini na kumpa nafasi kubwa namna hii? Hawa watu wakiona pesa tu huwa wanabadilika ndani ya dakika tu nadhani tunaweza kuuingiza huu mpango kwenye sehemu ya hatari zaidi hafai, kumtumia huyo”

“Ulitakiwa kwanza kujua sababu ya yeye kucheza Kamari. Ni komando kutoka ndani ya jeshi ambaye ana miaka kadhaa tangu atoke kwenye kazi hiyo na alistaafishwa kwa sababu maalumu na kwa sababu alikuwa ni mtu wa daraja la juu sana hajulikani kwa watu wengi ila kwa sasa ameishia kuwa mcheza Kamari na mtu wa kufanya mapigano ya kulipwa lakini pia ni muuaji wa kukodiwa na huyu ndiye ambaye ataifanya hii kazi kwa weledi mkubwa na kutupatia majibu ya kile ambacho sisi tunakitaka bila kushtukiwa na mtu yeyote yule”
“Mzee la…….”

“Mpaka nakwambia hivi ujue ninamjua kwa kila kitu, hii nchi nimeijua kabla hata wewe haujazaliwa hivyo hautakiwa kuwa na hofu juu yangu na huyu kijana ila kwa upande wako wewe unatakiwa kuwa makini sana na hautakiwi kumuamini mtu yeyote yule wa karibu yako kwa sababu hapo ulipo umezungukwa na watu wengi ambao unahisi ni watu wako ila huenda hakuna hata mmoja ambaye ni mtu wako. Nimesikia umeletewa vijana wawili hapo na Filipo Tibaigana ni kweli?”
“Ndiyo mzee, umejuaje?”

“Najua kila kitu ambacho kinaendelea kwenye nchi hii ila hili jambo sio la mhimu sana kwa sasa, unatakiwa kuwa makini sana na hao vijana wawili na unatakiwa kuandaa mtu ambaye utamwamini aweze kuwapeleleza mmoja mmoja kwa kila kitu, hatua ambazo anazipiga, watu ambao anaongea nao kwa siku mpaka anapolala na kuamka ili kuwa na uhakika zaidi maana kuna namna nahisi hao watu watakuwa wamekuja hapo kwa lengo maalumu bila wewe kujua”
“Kwahiyo natakiwa kuwafukuza kazi ili niwe salama zaidi?”

“Hapana, mtaji wa akili huwa ni mhimu sana kwenye kufanya maamuzi magumu, kuna mmoja kati yao anaweza kuwa wa mhimu sana hapo baadae hivyo unatakiwa kuwachunguza kwa ukaribu sana utakapo jiridhisha basi ambaye atakuwa msafi zaidi ya mwenzake huyo tutamtumia kumchunguza mkurugenzi wa usalama wa taifa, simwamini sana na haupaswi pia kumwamini sana yule mtu mpaka tutakapokuwa na majibu kamili kuhusu yeye”

“Asante sana mzee ndiyo maana kila kitu kwenye huu mpango nakutegemea wewe kwa sababu haya yote nisingeyafikiria”
“Kumbuka tu ulipo toka na kiapo ambacho ulikula mbele yangu kuhusu kulilinda hili taifa, mimi kabla ya kufa nitakupatia kila kitu hivyo hakikisha hawa watu wote wanateketea lakini tekeleza hilo nililokwambia kisha mpango wa kwanza uanze kazi haraka sana”

“Shukrani mzee, nimesahau na kuuliza kuhusu hali yako”
“SIiku nyingine tutaongea kwa urefu kwa leo nadhani tuishie hapa inaweza kuwa hatari zaidi kuongea kwa muda mrefu” mzee huyo alimaliza kuongea kisha akaikata simu hiyo ambapo haraka sana raisi huyo aliitoa laini kwenye simu hiyo na kuivunja vunja kisha akaidumbukiza kwenye choo pamoja na simu yake baada ya kuivunja vunja kwenye chumba kisha akaflash maji na kuweza kutoka huko akiwa kama sio yeye na kwenda kulala huku kichwani kwake akiwa na mambo mengi sana maana alikuwa kwenye wakati mgumu wa kufanya maamuzi ambayo bila shaka yalikuwa yanayaweka maisha yake kwenye mstari wa hatari mno.

Mheshimiwa Denis Kijazo baada ya kurudi ndani ya jiji la Dar es salaam, alikuwa na kikao cha dharura na mwanaume mmoja ambaye alifika sehemu ya tukio akiwa amefunikwa na shuka kubwa sana kwenye mwili wake huku akiwa amezungukwa na walinzi wa kutosha. Mwanaume huyo alikuwa kwenye hiyo hali ikiwa ni ishara ya kutotaka kujulikana majira hayo ya usiku wa mapema ambao alikuwa anakutana na mheshimiwa.
“Heshima yako kiongozi” mwanaume huyo alisalimia kwa heshima akiwa anasogea kukaa kwenye kiti ambacho kilikuwa mbele ya meza ambayo alihitajika kuketi kwa ajili ya mazungumzo, lakini hakujibiwa kitu chochote zaidi ya kumuona mheshimiwa huyo akiwa amemmkazia macho tu. Aliyekuwa amefika hapo, alikuwa ni Philipo Tibaigana mkurugenzi wa shirika lakijasusi la nchi ya Tanzania.
“Wakati nakukabidhi hicho kiti unakumbuka vitu ambavyo nilikusisitiza uweze kuvifanya?”

“Ndiyo mheshimiwa na nimefanya hivyo kwa miaka yangu yote ambayo nimekaa hapa”

“Sijasema kwamba haujafanya nilicho kitaka ufanye lakini kuna muda ukiona kwenye maisha yako usiku unaanza kuonekana mfupi sana basi ujue umekua sana na majukumu yako yamekuwa ni mengi. Mimi sikukuweka hapo ili upendeze sana au uwe maridadi kwenye nafasi yako ila nilikuweka hapo kwa ajili ya wewe kuweza kulinda maslahi yangu si unakumbuka?”
“Ndiyo mheshimiwa”

“Nahitaji unitajie watu ambao unahisi kwamba hawapo pamoja na mimi kwa muda ambao upo kwenye hiyo nafasi yako, najua wewe una taarifa za watu wengi sana ndani ya taifa hili hususani wakubwa hivyo nahitaji hizo taarifa haraka sana niweze kuzifanyia kazi”

Epidode ya 8 inafika mwisho.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 9
“Meja jenerali Francis Mboye”
“Mhhhhh hapana huyo ni moja kati ya watu ambao nimekulia kwenye mikono yao sasa kivipi unaniambia kwamba yupo kinyume na mimi?”

“Huyo ndiye mtu pekee ambaye mimi nina wasiwasi naye sana mheshimiwa katika kundi kubwa la watu ambao wanakuzunguka na huenda ni kweli mbele ya mtu huyo haupo salama kabisa na unaweza kuja kushtuka wakati umesha chelewa sana”

“Kipi kinakufanya uamini hilo jambo?”

“Wakati upo kwenye madaraka sio kila mtu alikipenda kile ambacho ulikuwa unakifanya, sio kila mtu alikuwa anavutiwa na namna ulivyokuwa unaiendesha siasa yako hivyo wakati unatengeneza watu wako wengi sana ila pia ulitengeneza maadui wengi sana akiwepo huyu mzee ambaye alichukizwa sana baada ya wewe kuanza kuyapambania maslahi yako badala ya kulipambania taifa”
“Nakuamini vipi juu ya hili jambo?”

“Huyu mzee ndani ya jeshi ana kikosi chake cha siri ndani ya jeshi ambacho kinaitwa THE DRAGON BOYS. Wapo vijana watatu tu ambao wanakiunda hiki kikosi ila ni watu hatari sana. Nimefanikiwa tu kulijua hilo ila sijui wanaishi wapi na ni nani na nani ambao ndio wanakiunda hiki kikosi ila ni makomando ambao wamefuzu ngazi za juu sana za mafunzo hivyo kwenye moja ya mipango ambayo nahisi ameiandaa kwa ajili ya kukupoteza wewe hawa vijana ndio ambao wanaaminika zaidi kuweza kutumiwa kwenye hiyo kazi na kwa ripoti nilizo nazo kama kweli hawa wakipewa maagizo ya kuingia kazini basi huenda utakuwa na masaa ya kuhesabu tu wewe kutiwa hasara ambazo huenda zitakufanya mawazo yakuue”

“Mhhhhhhhhhh mhhhhhhhhh ulikuwa wapi kunipa hizi taarifa mapema?”

“Umewahi kuniambia kwamba nisiwe nakupa habari nusunusu hivyo sikutaka kukupa kitu ambacho sikuwa na uhakika nacho ila kwa sababu imelazimu basi nakwambia mtu huyo mchukulie kwa uzito mkubwa na ikiwezekana anza kumfuatilia kwa umakini kuanzia sasa huenda ukathibitisha hili na kama utafanikiwa kuwajua hawa vijana wake basi unaweza ukaanza kuicheza karata yako ya kwanza kwa ushindi?”

“Kwanini awe yeye wakati huu?” mkurugenzi huyo aliguna kwa muda kisha akasogeza kichwa chake karibu na alipokuwa ametulia kiongozi wake ili watu ambao walikuwa pembeni wasije wakasikia kama heshima kwa kiongozi wake ambaye wakati yupo madarakani ndiye ambaye alimpa hiyo nafasi aliyokuwa nayo mpaka wakati huo.

“Kwa sababu ndiye ambaye anasemekana kwamba yupo nyuma ya raisi Teo ambaye wewe ulimpa madaraka ukiamini kwamba atakutii kwa kila kitu” mheshimiwa alibaki ametulia kwanza kwa muda akiwa kama anayavutia kasi hayo maelezo ambayo alikuwa amepewa wakati huo kwani ni kama alikuwa haamini bado kwa kile ambacho alikuwa anakisikia.

“Una maanisha huyu mzee ananizunguka mimi?”
“Sitaki kukuhakikishia kwa sababu nahisi ni mtu ambaye ulikuwa unamuamini kama ndiye baba yako kwenye maisha ya siasa na maisha ya dunia yetu hii hivyo unatakiwa kufanya maamuzi baada ya wewe mwenyewe kujiridhisha ila huyo mzee hapendezwi na mambo unayo yafanya hivyo anaweza kuwa ndiyo mwanzo wa anguko lako kiongozi” Denis Kijazo alipigiza kwenye meza kwa hasira sana huku akiwa anang’ata meno yake kwa uchungu tabasamu likiwa la kutosha kwenye uso wake.

“Una lolote la kunishauri?”

“Ndiyo kiongozi”

“Nakusikiliza”

“Kwa sasa unatakiwa kufanya kama haujui lolote linalo endelea yaani uwe kama mtu mfu”
“Hilo haliwezekani kwa sababu sio muda wanaanza kuniteketezea mali zangu ikiwemo ule ukumbi wangu jambo ambalo siwezi kuruhusu lifanyike”

“Mpaka sasa licha ya wewe kuwa na watu wengi sana upande wako ila kiuhalisia ni kwamba kuna watu ambao ni watiifu sana kwa yule mzee na inasemekana kwamba kuna watu alishawapandikiza kwako pia hivyo wakati unawazunguka watu kila sehemu kuna watu pia wamekuzunguka wewe bila wewe mwenyewe kujua hivyo unatakiwa kwanza kupitisha msako wa kimya kimya kuwapoteza mapandikizi wote ambao wapo kwako ila wanafanya kazi kwa mzee huyo kisha hapo utakuwa unaweza kupanga mipango yako upya na kufanya yale ambayo unaona ni sahihi ila ukisema kwa sasa ndo ufanye maamuzi basi unaweza ukajiingiza kwenye matatizo na kujimaliza mwenyewe”

“Na kuhusu biashara zangu ambazo zinaenda kupotea? Hivi unajua nitapoteza shingapi? Unajua mpaka sasa kuna akaunti zangu ngapi yule malaya amezifunga?”

“Mkuu hilo najua vizuri sana lakini usikurupuke kama mtu ambaye ndo anaingia kwenye hii kazi wakati sisi wote tunajifunza kwako, hizo mali zako zitarudi tu pale ambapo utatumia akili badala ya mihemko kufanya maamuzi. Kwa sasa mfanye ajione kwamba yeye ndiye bosi wa nchi kama anavyotaka, mfanye ajihisi kwamba ushindi upo kwenye upande wake kwa sababu mwanadamu akifikia hiyo hatua huwa anahisi kwamba anaweza kufanya lolote lile ambalo analitaka na kujisikia na hiyo ndiyo hatua ambayo watu wengi huwa wanapoteza umakini na misimamo. Sasa wakati huo vijana ambao wapo maeneo yote ya mhimu watakuwa wanafanya kazi ya kutaka kujua kama kuna mtu mwingine ambaye labda wamemuweka kama mtego ili uingie kichwa kichwa wapiti na wewe na baada ya kuhakikisha kwamba tumeshazipata taarifa zote basi tutaingiza mpango wa kwanza kwenye utekelezaji na huo ndio ambao utakuwa mwisho wake”

“Nimeupenda mpango wako ila naona kama haujitoshelezi sana”
“Upo sahihi mkuu, kuna wale vijana wawili ambao nimewapeleka kule kama walinzi, mmoja nimempa kazi kabisa na anajua ni kipi ambacho anatakiwa kukifanya na kwa sababu atakuwa muda wote yupo karibu na raisi basi atatusaidia sana kutupatia taarifa zote za kila ambacho kitaendelea kuanzia wakati ambao raisi atakuwa anaamka na kwenda kulala huku tukiwapandikiza watu wengine kwenye idara zake zote ambazo anazitegemea. Lakini yule kijana mwingine Max yeye ni mzalendo sana na ameenda pale akiwa hajui kazi ambayo anaifanya kwa sababu asingekubali kuifanya kama ningemwambia ukweli hivyo yeye nimempa maagizo ya kuripoti kwangu kila ambacho kinaendelea na kupitia hilo nitakuwa napata taarifa kwake bila yeye kujua hivyo kwa kule Ikulu sehemu ya mhimu tayari tushaiweka mkononi mwako”

“Safi, nadhani hili lifanyike haraka sana ili huyu malaya nimfundishe namna ambavyo huwa nawafanyia watu wasaliti ambao wanashindwa kutambua kwamba mimi ni nani hasa kwenye taifa hili. Halafu huyo kijana huoni kama anaweza kuwa tatizo kwa hapo baadae kama mambo yakienda vibaya?”
“Hayo mahesabu nimeyafanya vizuri sana mkuu na hilo nalitambua kwamba huyo ndiye ambaye anaweza kuka kikwazo kikubwa sana kuweza kutimiza majukumu yetu kwa usahihi”

“Sasa kama ulikuwa unalijua hilo kwanini umempa hiyo nafasi yeye?”

“Kwa sababu huyu tutakuwa na kazi naye kubwa sana kwa hapo baadae na ndiye ambaye atatumika kukamilisha mpango wetu bila mtu yeyote yule kuweza kushtukia mchezo”
“Una maanisha kwamba?”

“Baada ya kukamilisha kila kitu huyu bwana mdogo atabebeshwa msala mzima wa kuhusika na mauaji ya raisi wa nchi hivyo sisi tutabakia upande salama kabisa yeye akipata kesi ya usaliti wa taifa lake kwa kuhusika na mauaji ya raisi wake”

“Hahahaha hahahaha hahaha kuna muda nafurahi sana kufanya kazi na watu wenye akili kubwa kama wewe, unaweza kwenda na huku kunako bakia nitaendeleza mimi mwenyewe” mwanaume huyo aliinama tena kutoa heshima kwa bosi wake kisha akalivaa tena shuka lake na kutoka humo ndani ili asije akajulikana hata kwa walinzi wa mheshimiwa Denis Kijazo maana hakuna mtu hata mmoja ambaye walikuwa wanamwamini sana kwa wakati huo ambao walikuwa wanahisi kwamba kulikuwa na mapandikizi ambayo yangekuwa hatari sana kwao.



“Tanzania Tanzania”
“Nakupenda kwa moyo wote”
“Nchi yangu Tanzania”
“Jina lako ni tamu sana”

Ni mistari ya wimbo wa taifa wa nchi ya Tanzania ambayo ilikuwa inaimbwa kizalendo sana na mwanaume mmoja ambaye alikuwa kwenye hali ya kilevi hata sauti yake iliweza kusadiki hilo jambo. Ni maeneo ya Ukonga nyakati za kiza kinene ambapo mwanaume mmoja ambaye alikuwa kwenye magwanda yake akiwa ameshika kifurushi mkononi ambacho alikuwa anakitumia kuhifadhia pombe alipokuwa anakatisha kwenye mitaa usiku huo huku watu wengine wakiwa wamelala muda mrefu sana majumbani mwao. Mwa mwonekano wa haraka haraka mwanaume huyo usingesita kumuita kichaa kwa namna alivyokuwa kwani mwilini alikuwa na mavazi ambayo yalishonwa kwa magunia na kwenye miguu yake alikuwa na maviatu ambayo yalifungwa vitambaa vingi sana ili yasiweze kuachia ili kuendelea kumsitiri na hali ya jiji ambayo ilikuwa inachafuliwa sana na mvua ambazo zilikuwa zinanyesha mara nyingi.

Akiwa kwenye uimbaji wake mzito ambao ulikuwa unamfanya aendelee kujivunia kuwa mtanzania, mwili wake ulisisimka sana kiasi kwamba hata kifurushi chake ambacho kilikuwa na pombe akawa amekifunga kwa nyuma kwenye gwanda lake ambalo lilikuwa mwilini huku akiwa kama ananesa nesa mithili ya mtu ambaye alikuwa amelewa. Kusisimka kwake mwili sana alielewa kwamba hilo eneo halikuwa rafiki tena bali alikuwa ametembelewa usiku huo tulivu, alitoa tabasamu hafifu kwenye uso wake kisha akasogea kwenye nguzo moja ya umeme na kujiegamiza hapo.

Alikimbia kwa kasi kusogea mbele, alipishana na ngumi kali sana ambayo ilitua kwenye hiyo nguzo ambayo ilitikisika kwa nguvu. Alisimama kwa mbele ya hiyo nguzo ambapo alibendi kidogo baada ya mtu ambaye alikuwa nyuma yake kumkosa na buti la bega, aliruka sarakasi tano mfululizo kwa spidi kali kiasi kwamba kilikuwa kinaokena kivuli tu pekee kisha akaenda kutua mbele ambapo alichotwa na mtama mkali mno kisha akashindiliwa na mateke matatu kifuani kwake ambayo yalimzoea mpaka kwenye ile nguzo ambayo alikuwa amesimama kwa mara ya kwanza baada ya kuhisi kwamba kulikuwa na ugeni hapo.

Alikuwa anadondokea uso kwenye nguzo hiyo ila mkono wake mmoja aliugusisha chini ambapo alidunda kwa nguvu na kugeuka kwa miguu yake ambayo ilitua kwenye hiyo nguzo ila alimanusura kifurushi chake cha pombe kimponyoke, alikidaka kwa mguu mmoja na kukirusha juu kwa nguvu akanywa funda moja na kukifunga tena vizuri akiinyosha shingo yake na kujishika tumboni maana alipigwa na mabuti makali mno. Wanaume watatu tu ndiyo ambayo walikuwa mbele yake kuweza kuifanya hiyo kazi ya kuweza kumpeleka chini, alikimbia kwa zigzaga kuelekea pale walipokuwepo ambapo alitishia kwenda kwa mmoja hivyo nao wakajipanga lakini hakufanya hivyo alidunda chini kwa mguu mmoja na kujiviringisha kwa sarakasi tatu za juu akatua nyuma yao hali ambayo iliwalazimu wa kugeuka haraka sana ili kuweza kukabiliana naye.

Episode ya 9 inafika mwisho.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 10
Aliyekuwa mbele alipigwa kwenye shingo na kiganja alikata moto hapo hapo hakuweza kuongea tena alidondoka chini, buti la mwanaume wa pili lilikuwa linakuja kwenye shingo yake alibendi kwa nyuma huku visigino vyake pekee ndivyo vilikuwa chini. Kwa namna alivyo jizungusha ilikuwa ni ngumu kwa mtu wa kawaida kubaki amesimama zaidi ya kudondoka vibaya lakini kwa mwanaume huyo lilikuwa zoezi rahisi sana wakati anasimama vyema alirudi na ngumi mbili ambazo zilitua kwa mwanaume mmoja lakini na yeye pia alipokea mateke ya mbavu mawili kutoka kwa mwanaume mmoja ambaye alitokea pembeni akateleza chini kwa miguu yake na kusimama kisha na yule mwanaume ambaye alikuwa amedondokea mbele yake akiwa ananyanyuka na kudondoka tena kwa ngumi ambazo zilikuwa zimetua kwenye kifua chake lakini alifanikiwa kusimama vyema.

Mwanaume huyo baada ya kuona watu hao wanazidi kumchukulia muda wake alijiviringisha kwa chini na kuinukia pale walipokuwepo huku kwenye mkono wake akiwa na cheni ambayo ilikuwa imeandikwa B13 na cheni hiyo alikuwa akiikunjua kinakuwa kisu kikali sana hivyo wakati anasimama hapo mguu wa mwanaume mmoja ambaye alikuwa anahitaji kumtwisha nao hapo alipokuwepo aliudaka na kuzamisha cheni hiyo ambayo ilitoboa toboa vibaya sana hilo buti hali ambayo ilimfanya mwanaume huyo ajivute nyuma ili asije akapata madhara ya cheni hiyo lakini kurudi kwake nyuma kulimfanya mwanaume ambaye alikuwa kwenye hayo manguo ya magunia kuinamia kwa mbele kisha akampiga mwanaume mwenzake vibaya sana na kisigino cha mdomoni ambacho kilimtoa damu nyingi sana na kumfanya arudi nyuma akiwa anaguna kwa maumivu.

Mwenzake alikuwa anakuja kwa haraka sana lakini hatua zake hazikuendana na mtu ambaye alikuwa anashindana naye mpaka aliposhtukia cheni ipo kwenye shingo yake, mwanaume huyo alihitaji kuifungua cheni hiyo ili kuipoteza shingo ya mtu huyo ila alighairisha zoezi lake baada ya kusikia mlio wa gari ukifika hilo eneo kwa kasi sana.
“Stop” ni sauti ambayo ilisikika kutoka kwa mzee ambaye alikuwa anashuka ndani ya gari hiyo ambapo mwanaume huyo alimzunguka mwenzake kwa nguvu na kumpiga mtama mkali kisha akamkita na goti kwenye kifua chake ambapo alienda kudondokea kwenye miguu ya yule mze ambaye alikuwa ameshuka akiwa na walinzi wawili.

“Bosi?” mwanaume huyo ambaye alikuwa amevamiwa hilo eneo akiwa kwenye hayo manguo yake aliita kwa mshangao huku akiwa anainama kutoa heshima kwa kiongozi wake huyo.
“Ni vizuri haujamuua hata mmoja maana kama ningechelewa kidogo ningewapoteza vijana hawa ambao hawana hatia yoyote ile”
“Sikujua kama ni wewe uliwatuma hapa ila washukuru sijataka kuwaua haraka maana nilitaka niwajue kwanza kwamba ni akina nani ila bila hivyo ningewaua muda mrefu sana”

“Panda kwenye gari” mzee huyo alitoa amri moja tu kisha gari hiyo ikatolewa hapo kwa kasi sana huku wale wanaume watatu ambao walikuwa wamevamia hapo wakikokotana na kutoweka haraka sana hilo eneo kwani maagizo ambayo walikuwa wamepewa na kiongozi wao walikuwa wameyatakeleza vizuri. Gari hiyo ilienda kusimamishwa maeneo ya mzambarauni pembezoni mwa reli ya treni na mzee huyo akawataka walinzi wake wawili watoke ndani ya hiyo gari alihitaji kubaki na kijana wake tu pekee na taa zote zikazimwa pakawa kimya sana ndani ya hilo eneo.

“Bilali nadhani unatakiwa kuwa makini sana, usipende sana kuitoa toa cheni yako hiyo kwa sababu ina utambulisho wa kifupisho cha jina lako, kuna watu ambao ni wataalamu sana wa kuunganisha doti hivyo inaweza kupelekea wewe ukajulikana haraka sana sehemu ambayo unakuwa upo mwisho wa siku ukaja kupotea kizembe sana. Kwenye kikosi cha DRAGON BOYS kumbuka wenzako wawili wanakutazama wewe hapo hivyo hautakiwi kufanya ujinga wowote ule ambao unaweza ukafanya wenzako wakaingia kwenye hatari”
“Nimekuelewa bosi, naomba unisamehe sana kwa hilo”
“Hayo yameisha nipe ripoti kamili”
“Hawa watu nimewafuatilia kwa umakini sana lakini kiufupi ni kwamba mheshimiwa raisi yupo kwenye hatari kubwa sana ya kuweza kuuawa”
“Hilo nalijua, nahitaji unipe taarifa kamili kwamba ni nani yupo upande wetu na ni nani hayupo upande wetu na nahitaji kujua sana kwamba ni akina nani ambao Denis anawaamini sana na kuwatumia sana kwenye hizi kazi zake”
“Watu wengi ambao wapo kwenye mfumo wa serikali ni wake na wanamtii yeye, kuanzia jaji mkuu wa serikali, mwanasheria mkuu wa serikali, spika wa bunge, waziri mkuu ambaye mpaka sasa hajatolewa, makamu wa raisi ambaye amemaliza naye utawala na watu wengi sana Ikulu wapo upande wake lakini jambo la hatari zaidi hata mkurugenzi wa shirika letu la kijasusi ni mtu wake wa karibu sana na kila habari nyeti huwa anampatia”
“Whaaaat?”
“Ndiyo bosi iko hivyo lakini pia kuna watu wachache sana ambao hawapo upande wake”
“Ni akina nani hao?”
“Kuna kiongozi mmoja wa upinzani lakini kwa wale ambao wapo ndani ya chama chake kuna DCI na IGP, hawa tunaweza kuwatumia kama silaha kwetu”
“Kwa namna ipi?”

“Kwa sasa mheshimiwa raisi anatakiwa kumteua waziri mkuu ambaye anamwamini sana kwa sababu tutamhitaji sana hapo baadae lakini pia anatakiwa kumpata makamu wa raisi ambaye ataweza kumuamini sana ndiye ampe hii nafasi na kwenye baadhi ya vitengo vikubwa tuwapenyeze wapelelezi wetu wa kuaminika ambao watakuwa wanakusanya taarifa za watu hao na kutupatia na hapa inatakiwa tuwapate watu ambao wapo nje ya mfumo ndio itakuwa rahisi zaidi kuweza kuwamudu kwenye kuwaendesha ila asimtoea mkurugenzi wa taasisi ya kijasusi”
“Kwanini asitolewe?”
“Huyu atatusaidia sana kwenye ukamilisho wa kuzipata taarifa za ndani sana za watu hao”
“Mtu ambaye hayupo upande wetu anatupaje taarifa za watu hao?”
“Nadhani unajua kuhusu yeye kumpa mheshimiwa raisi wale walinzi wawili na unajua kabisa kwamba wamelekwa pale kwa kazi maalumu?”
“Hilo nalijua, endelea”

“Sasa kwa wale vijana wawili ambao wamepewa ile kazi kuna walakini kwamba mmoja ni mzalendo na mwingine ni mtu wao ambaye wamemtuma kwa kazi maalumu pale Ikulu ndiyo maana nasema kwamba maisha ya raisi yapo hatarini muda wote kwa sababu muuaji yupo naye anamlinda muda wote vipi kama akipewa maagizo ya kuweza kumuua? Ni suala la dakika moja tu kutekeleza amri ya kiongozi wake ila sisi tutaitumia hii nafasi kuwaingiza wao kwenye shimo” mwanaume huyo ambaye alijulikaan kama Bilali alikohoa kidogo kujiweka sawa ili ampe mheshimiwa mpango mzima juu ya kile ambacho walitakiwa kukifanya hapo kuwatia watu hao kwenye mifuko yao.

“Nimefuatilia kwa undani sana taarifa za wale vijana tangu wanaanza kupatiwa mafunzo hapa Tanzania mpaka wanafikia hatua ya kumlinda mheshimiwa raisi ila mmoja wao kuna tatizo kidogo kwenye rekodi zake ndiyo maana ndiye ambaye naweza kusema kwamba ni msaliti na anafanya kazi zao wale watu. Anaitwa Karistus Dickson ni mzaliwa wa jiji la Mwanza huko, huyu kwenye rekodi zake alikuwa ni mtu ambaye kila baada ya siku kadhaa alikuwa akipotea kwenye kambi na baada ya muda kama wa dakika kumi angeonekana anarudi na kujumuika na wenzake na kwa huo muda ambao aluikuwa anapotea inaonekana alikuwa anafanya mawasiliano kwenye simu na baadhi ya watu jambo ambalo kiitifaki halikutakiwa kufanyika hivyo hilo limeleta uwalakini kwamba lazima alikuwa anaendelea kufanya kazi yake hata akiwa mafunzoni ya kuripoti kila ambacho kilikuwa kinaendelea kwa viongozi wake hivyo huyu ndiye hatari kubwa zaidi ambayo ipo kwa upande wa raisi na haitakiwi huu mpango ubadilike haraka sana namna hii maana inaweza kuwa hatari huyu anatakiwa kuendelea kuwepo pale ili kutimiza kazi yetu kwa usahihi”

“Lakini huyu mwingine ambaye anaitwa Donald Daniel, yeye ni kijana ambaye sina uhakika ila anaonekana ni mzalendo sana na ndiye ambaye tunatakiwa kumpata haraka sana kwa namna yoyote ile maana jina lake ni safi zaidi hata ya Obama kwa sababu hana historia yoyote ile mbaya wala kukutwa na tatizo au dosari yoyote ile kwenye maisha yake hata alipokuwa huko kwenye mafunzo lakini pia ni mwanaume wa shoka sana. Rekodi zake zinaonyesha kwamba alikuwa amepata alama za juu sana za mapigano na upelelezi kwenye kila sehemu ambayo alikuwa amepita hivyo naweza kusema anatufaa moja kwa moja”

“Na huyo kijana tunampataje?” mzee huyo aliingilia meongezi hayo baada ya kuonekana kwamba alikuwa amemuelewa sana kijana wake.
“Mtu pekee ambaye anatakiwa kufanya naye haya mazungumzo ni mheshimiwa raisi bosi”
“Hilo ni jambo gumu sana, tunaweza kujiingiza kwenye shimo sisi wenyewe, vipi kama akimmwagia hizo siri halafu akawa tofauti na unavyo mdhania huoni kama raisi atakuwa amejiteketeza yeye mwenyewe?”
“Bosi hii ndiyo njia ngumu lakini ndiyo njia pekee. Nina uhakika na taarifa zangu hivyo kwa asilimia sabini nina imani nipo sahihi na kama sipo sahihi basi ni kwa asilimia thelathini tu ambazo haziwezi kuathiri mpango wetu na kama tukimpata huyu tayari tutakuwa na mtu wa mhimu wa kumwamini kwenye mkono wetu ambaye anaweza kutusaidia sana kutekeleza majukumu haya ya mhimu”
“Na baada ya kumpata mpango wako ni upi?”

“Huyu atatusaidia kumchunguza kwa ukaribu sana mkurugenzi wa taasisi ya kijasusi kwa sababu yeye anaweza kukutana naye muda wowote ule hivyo kupitia yeye tutaweza kupata taarifa nyingi na kumbuka ukimtoa raisi yule ndiye mtu mhimu zaidi ndani ya taifa kwa sababu ana taarifa za siri ambazo zinaweza kuliteketeza taifa au kulikomboa taifa”
“Mpango wako mwingine ni upi?”

“Wakati kazi hiyo inafanyika ndio muda ambao raisi anatakiwa kuufungia ukumbi ule kama tulivyokuwa tumekubaliana mwanzo na muda huo mimi nitakuwa nimeingia kwenye upelelezi ili kuweza kuwajuia washirika wake wengine wa siri ambao huenda wanampa nguvu kuliko hawa wanasiasa maana lazima kuna wawekezaji wakubwa ambao wapo nyuma yake sasa tunatakiwa kuwapata hao na kama tutafanikiwa kuwapoteza ndipo tunaweza kumfuata yeye moja kwa moja itakuwa kazi sio ngumu sana kuliko kumfuata yeye bila kuwajua ambao wapo nyuma yake hapo hakuna jambo la maana ambalo tutakuwa tumelifanya zaidi ya kupoteza muda tu”

“Good, umefanya kazi nzuri sana lakini kuna jambo lingine ambalo ulisema kwamba ulikuwa unahitaji sana kuniambia kwa haraka mno”
“Ndiyo bosi ndiyo maana nikataka tuonane moja kwa moja”
“Lipi hilo”
“Unamkumbuka Laurenti Mande?”
“Ndiyo, aliwahi kuwa rafiki yangu kwa kipindi fulani, huyo si gavana ambaye alipoteaga kwenye mazingira ya kutatanisha na mpaka sasa inaaminika kwamba alifia baharini?”

Naweka nukta sehemu ya 10 panapo majaaliwa tukutane tena wakati ujao.

Tchao.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 11
“Ndiyo bosi, huyo mtu yupo hai”
“Hapana hilo haliwezekani kabisa”
“Iko hivyo mheshimiwa kwa sababu kwa taarifa ambazo nimezipata ndani ya ule ulingo wa mapambano kutoka kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wanabishana mle ndani ni kwamba bado yupo hai na amehifadhiwa mahali”

“F**k you Denis. Amemhifadhi wapi?”
“Bado sijajua ila inasemekana kwamba ni nje ya mji, nilishindwa kutambua maana hata wale watu walionekana kubishana tu kiasi kwamba hakuna ambaye alikuwa an uhakika na jambo hilo ila kwa maelezo yao ni kwamba yupo hai na wakati ule baada ya kiasi kikubwa sana cha pesa kupotea ndani ya benki kuu huyu ndiye ambaye alifanikisha hilo na ni Denis Kijazo akiwa raisi ndiye ambaye alimtumia mzee huyo kukipoteza kiwango hicho cha fedha. Hivyo nilikuwa nahitaji amri yako kama niingie na kwenye hili au tumalize hili la kumuweka salama kwanza raisi juu ya hawa watu kwa haya majukumu mazito ambayo yapo mbele yake?”

“Hiyo kazi achana nayo kwanza nitakupa taarifa muda wa kuanza kuifanyia, kwa sasa tumalize hili kwanza na hakikisha unakuwa makini sana kwani huenda kuna watu wanakutazama namna unavyo ishi bila wewe kuweza kutambua na kumbuka tu wewe ndiye kete yangu ya dhahabu ambayo naitegemea kuweza kukamilisha hii kazi hivyo kwa namna yoyote ile wewe unatakiwa kuishi”
“Nimekuelewa bosi na nitahakikisha jambo hili nalitekeleza kwa umakini mkubwa sana”

“Bilali mimi maisha yangu yapo hatarini sana kwa sababu yule mtu akipata tu taarifa zangu basi anaweza kunipoteza haraka sana kwani ana watu kila eneo. Mimi hakuna namna naweza kukikwepa kifo kwenye hili lazima tu nitakufa hivyo kama ikitokea nimepata tatizo lolote lile usije ukawa mwisho wa kazi hii kwa sababu nina imani kwamba nimeiacha kazi kwenye mikono salama. Na kama nikifa kabla hatujakutana tena basi utahitajika kukutana na mheshimiwa raisi ambapo utajitambulisha kwa maelezo ambayo utayakuta ndani ya frashi ambayo nakupatia saivi hapa. Hili jambo lazima likomeshwe na nchi lazima irudi kwenye hali ya usalama hata kama itahitajika kuyatoa misha ya watu wengi kiasi gani” mzee huyo alitulia huku akiwa anamkabidhi kijana huyo Frash kwenye mkono wake licha ya kiza kuwepo eneo hilo bado mazungumzo yao yalifanya atambue mkao wa kijana wake ndiyo maana ilikuwa ni rahis tu kwake kumkabidhi.

“Kazi yako ya kwanza kwa sasa ni kumlinda mheshimiwa raisi kwa namna yoyote ile na kazi ya pili ni kutekeleza mpango huu na ili mpango uweze kukamilika ni lazima raisi na wewe muwe hai hata kama maisha yangu yatapotea. Kama ulivyokula kiapo kunilinda na kunitumikia basi na kwa Teo utatakiwa kufanya hivyo hivyo lakini pia nikitoka hapa naenda kukutaa na Teo aweze kuongea na huyo kijana na kisha baada ya hapo mtafute huyo kijana wewe mwenyewe ukae naye chini japo inaweza kuwa ngumu sana kukuelewa ila hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuweza kufanya hivyo ili kazi isije ikaharibika. Ndani ya hiyo frashi kuna taarifa za mhimu sana za kukuongoza juu ya nini cha kufanya hata kama nisipokuwepo mimi, kuna taarifa nyingi sana za akaunti za benki ambazo watu hao wamehifadhia pesa ambazo wameziiba serikalini lakini pia kuna nyaraka za mikataba yao mingi sana ya ubadhilifu mkubwa ambao wanaufanya.” Alitulia mzee huyo na kumeza mate kisha akaendelea.

“Humo ndani pia kuna taarifa za nini cha kukifanya kama ikitokea raisi ataingia matatizoni au mpango huu ukiharibika. Ila pia humo ndani kuna taarifa zote za umiliki wa mali zangu na na baadhi ya watu ambao ikitokea sipo utatakiwa kuwatafuta na wanaweza kukupa msaada na kukupa muongozo juu ya nini cha kufanya kwa sababu ni watu ambao nipo nao kwenye mbio hizi za kuweza kuukomesha huu udhalimu ambao unaendelea kwenye nchi yetu. Nakutegemea sana kijana wangu fanya hivyo kama kuenzi uwepo wangu na mchango wangu kwenye kuliokoa hili taifa lisije likadumaa kama lilivyo dumazwa kwa hii miaka mingi na nakuacha wewe kama mtoto wangu kwa sababu sikubahatika kupata mtoto kwenye maisha yangu yote.” aliongea kwa uchungu sana mzee huyo huku akiwasha taa za ndani ya gari hiyo chozi likimtoka kwenye uso wake na ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kijana wake kumuona bosi wake akiwa anatoa machozi mbele yake.

“Nilikula kiapo mbele yako na nipo tayari kukilinda kiapo hicho mpaka siku ambayo nitafikia mwisho wa kuivuta pumzi yangu ya mwisho” mwanaume aliongea kwa msisitizo huku akiwa anampigia saluti bosi wake ambaye alikuwa anaongea kama mtu ambaye alikuwa anamuaga maana ni kama vile alikuwa amekiona kifo mbele yake. Alimkumbatia kijana wake huyo na kumpiga piga mgongoni

“Good luck son. Go” alimtakia bahati njema na kumtaka aende. Mwanaume huyo alitoka nje ya gari hiyo na kusimama kwa heshima kisha akapiga saluti mpaka gari hiyo ilipotoweka, hata yeye alishusha chozi kwenye uso wake kwa sababu kama kiongozi mkubwa kama huyo alikuwa anamuaga na kuhakikisha kwamba hawezi kupona basi hilo lilikuwa ni jambo siriasi sana, licha ya kuwa mwanaume wa kutisha mno ila bado alijua kwamba alikuwa mwanadamu wa kawaida na ipo siku angekufa tu.


Ilikuwa ni asubuhi nyingine ambayo ilikuwa njema sana kwa upande wa raisi kwani aliamka akiwa mwepesi sana baada ya usiku wa jana yake kukamilisha baadhi ya majukumu ya kuweza kuteua na kujaza nafasi nyingi sana selikalini kwa kuwapatia watu ambao kwa upande wake yeye alihisi kwamba wanamfaa hivyo siku hiyo alikuwa amepanga kwamba angeitumia kuweza kupumzika na kuweza kukipumzisha kichwa chake sawa ili hali yake iweze kutulia akiwa anawaza kujaza nafasi kubwa za juu za selikali kama waziri mkuu na makamu wa raisi bila kusahau kuangalia kama kulikuwa na haja ya kubadilisha nafasi ya jaji mkuu wa selikali au kama angemuacha yule yule.

Hizo nafasi za juu kabisa hakutaka kukurupuka kuweza kuteua watu haraka kwani alihitaji kuwapata watu ambao angewaamini kwa sababu alijua hao ndio watu ambao wangemsaidia kwenye hiyo vita yake kubwa ambayo alikuwa ameianza na bosi wake aliyempatia ugali na kumpa maisha kwenye siasa. Lakini wakati anaamka asubuhi hiyo alikutana na imeili (email) ikiwa inamtaka afungue haraka sana faili ambalo lilikuwa ndani ya email hiyo.

Moyo wake ulianza kumdunda kwa haraka haraka sana kwa sababu alihisi huenda lilikuwa ni jambo la hatari sana ukizingatia namba hiyo ilikuwa ni binafsi na alikuwa akiitumia kwa ajili ya mambo ya mhimu tu pekee. Baada kufungua file hilo ambalo lilikuwa kwa mfumo wa nyaraka alikutana na listi ya majina ya watu ambao walikuwa ni wasaliti kwake na kumtii kwa ukaribu sana Deusi Kijazo akiwepo jaji mkuu, mwanasheria mkuu, spika wa bunge na waziri mkuu ambaye muda wake ulikuwa umeisha ila alikuwa bado ofisini akisubiri kama ataendelea au atatolewa kwenye hiyo nafasi.

Hilo ni jambo ambalo lilimshtua sana maana hakutarajia kukutana na jambo kama hilo na watu hao ni moja kati ya watu ambao alikuwa akiwaamini sana. Akiwa anaendelea kusoma taarifa hizo pia kwa chini yake kulikuwa na majina ya watu ambao walikuwa waaminifu sana na ndio watu ambao alikuwa anatakiwa kuwa nao karibu kwani wangemlinda sana pale ambapo mambo yangeenda vibaya. Aliyekuwa amemtumia hizo taarifa ndiye mzee ambaye yeye alikuwa akifanya naye mawasiliano kwa siri sana hivyo alikuwa anamuamini kuliko kitu chochote kile na ndiye ambaye alimtafuta yeye ili aweze kuifanya hiyo kazi wakati huo na alikuwa anafanya hayo yote kama heshima kwa mzee huyo.

Kwenye listi ya majina ambayo yalikuwa yamewekwa hapo alikutana na majina mawili ambayo alishauriwa kwamba lilikuwa jambo la busara kama watu hao angewapa nafasi za juu zaidi kuliko zile walizopo ili wawe na nguvu kubwa ya kuweza kumsaidia kwani hao wangeweza kuwa watiifu kwake kama angefanikiwa kuwatumia vyema. Kasiani Ndepo, huyu alikuwa ni IGP ndani ya taifa la Tanzania ila alitakiwa kumteua kuwa makamu wake, jina la pili lilikuwa ni Justin Mtadei, huyu alikuwa ni DCI na kwa wakati huo alikuwa anatakiwa kumteua kuwa waziri mkuu wa nchi kwa sababu hao ndio watu ambao walikuwa kwenye nafasi za juu na walikuwa wasafi wa kutokujihusisha na mtandao mchafu wa Denis Kijazo.

Mheshimiwa alikaa kwa muda mrefu sana akiwa anahema kwa ngumu kwa namna mambo yalivyokuwa yanaenda kwa kasi sana, ilifika hatua hata yeye mwenyewe akawa kama anaiogopa sana nafasi ambayo alikuwepo kwa wakati huo kwani alizungukwa na maadui wengi sana ambao muda wowote ule walikuwa wanayahatarisha maisha yake. Alihisi kwamba taarifa hiyo iliishia hapo lakini alikutana na maelezo ambayo yalikuwa yanaendelea chini yake, taarifa ambazo zilimshtua sana mheshimiwa raisi.

Taarifa hiyo ilikuwa imetoka kwa meja jenerali Francis Mboye ambaye alikuwa ni mkuu wa jeshi la nchi ya Tanzania, huyo ndiye mzee ambaye alikuwa anwasiliana kwa siri sana na mheshimiwa raisi Teodensia Mpanzi. Mzee huyo ndiye ambaye alikuwa anaishi kwenye dunia ya siri sana ya kuweza kulisafisha taifa lake kutoka kwa maharamia ambao waliamua kuligeuza taifa kuwa sehemu yao ya burudani na kufanya ufedhuli wao ambao walikuwa wanaona unawafaa na unawaletea maslahi mazuri wao na familia zao pamoja na matumbo yao kwa ujumla.

Ndani ya taarifa hiyo mzee huyo aliandika kwamba raisi alikuwa anatakiwa kumteua mtu mwingine kwenye hiyo nafasi yake ambayo yeye alikuwepo haraka sana kwani alikuwa na muda mchache sana wa kuweza kuishi ila kabla ya kusema kwamba ni kipi kilikuwa kinamfanya aweze kusema maneno kama hayo alimtaka raisi kwanza asome kwa umakini kitu ambacho ndicho kilikuwa kimekusudiwa mpaka yeye kumtumia taarifa hiyo ya siri kwenye hiyo namba yake binafsi.

Alimsisitiza kwamba yeye anakufa kwa kujitoa kwa ajili ya taifa lakini watu hao wanatakiwa kuendeleza pale ambapo yeye atakuwa ameishia ili hata asipokuwepo basi huko ambako atakuwepo kwa wakati huo atakuwa na amani kwa kuamini kwamba aliwaacha watu sahihi kwenye hizo nafasi ili watekeleze lile jambo kwa weledi. Alimsisitiza sana raisi kwamba kwa wakati huo watu wengi hawakuwa upande wake ila mtu ambaye angekuwa kete yake ya mhimu ni kijana wake Bilali ambaye baada ya kifo chake atamtafuta raisi na kujitambulisha kwake na kijana wake huyo ndiye ambaye angempa raisi mpango mzima wa wapi wanaanza na wapi watakuja kuishia na kipi kitakuja kuendelea baada ya hapo.

Alidai kwamba alifanya hivyo kwa sababu za kiusalama kwani kama angetuma vitu hivyo kwa raisi huenda kuna watu wangeweza kuvikamata kwa mitambo maalumu hivyo ni bora kijana huyo aje amletee mwenyewe. Alimtambulisha kijana huyo kama kiongozi wa kikosi chake cha siri cha hatari cha DRAGON BOYS ambao wote walijuwa ni makomando ambao aliwastaafisha yeye jeshini ili wazifanye kazi za siri za kulilinda taifa bila kujulikana kwa mtu yeyote yule na huyo Bilali ndiye alikuwa kiongozi wao na ndiye ambaye angeweza kumkutanisha na hao wenzake wawili ambao hakuna aliyekuwa anajua kwamba wanapatikana wapi mpaka wakati huo. Alimwelekeza kwamba mwanaume huyo akishajitambulisha amkague kwenye kwapa yake upande wa kulia ana alama ya mnyama Dragon hivyo asipo iona alama basi ajue huyo siyo yeye maana anaweza akaingizwa mtu mwingine hapo katikati akachanganya kwa kuhisi ni yule ambaye yeye anamdhania halafu akajiingiza kwenye mtego mbaya sana.

Mzee huyo alimpa taarifa nyeti sana kwa kumwambia kwamba hatua zote ambazo zilikuwa zinatakiwa kufuatwa zilikuwa ndani ya frash ambayo alimpatia Bilali hivyo bilali siku ambayo ataifungua frashi hiyo atajua kila kitu na baadhi ya siri ambazo mzee huyo aliamua kuzificha. Kuna kitu ambacho alidai kwamba yeye alikificha kwa muda mrefu sana na ni watu wachache sana ambao wanakijua ila alikuwa anataka raisi huyo aweze kukitambua kwa wakati huo, ni kwamba alikuwa ana familia kabisa na zile taarifa za kusema kwamba hana familia ni yeye alizitengeneza wakati anaingia rasmi kwenye mambo ya siasa kwa sababu alikuwa anajua namna siasa inavyofanya kazi na familia yake ingekuwa udhaifu wake mkubwa sana ambayo ingemfanya ashindwe kutimiza majukumu yake kwa usahihi zaidi na huenda angeweza kuiingiza kwenye matatizo makubwa sana kwa uzalendo wake mwenyewe hivyo akaamua jambo hilo kubakia siri nzito kwenye nafasi yake ambapo aliapa kwamba jambo hilo angekufa nalo mwenyewe kwenye moyo wake.

11 inafika mwisho.

Tchao.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 12
Kuhusu eneo ilipokuwa familia hiyo Bilali ndiye ambaye ataweza kujua baada ya kuifungua ile frashi na kusoma kile kilichopo ndani yake hivyo ndiye ambaye atakuja kumpa hizo taarifa. Meja jenerali aliamua kutoa jibu la kwanini hakuwa na imani kama alikuwa na maisha marefu ni baada ya kuweza kupigiwa simu na raisi mstaafu Denis Kijazo na kumtaka mzee huyo akakutane naye kwa haraka sana hivyo alijua kwamba hakuna namna ya kuweza kuishi na mzee huyo alitishiwa kwamba kama asingeenda basi siku hiyo hiyo raisi angeuawa hivyo alienda huko kwa sababu ya kumlinda mheshimiwa raisi ili aweze kuukamilisha mpango wake kwani yeye siku hiyo ya kufa alikuwa anaisubiri kwa muda mrefu sana na aliamini kwamba ilikuwa imefika hivyo hakuwa na namna ya kuikimbia tena.

Jambo la mwisho na la mhimu sana ni kwamba mheshimiwa alikuwa anatakiwa kukaa na kijana wake Donald Daniel, Donny waweza kumuita 001 na kumpa mpango mzima ili kijana huyo asaidiane na Bilali kuweza kulikamilisha jambo hilo. Aliweka wazi kwamba kijana huyo ndiye ambaye alikuwa msaada mkubwa sana kwa hapo baadae kwani kwa mahesabu yake alikuwa anajua wazi kwamba Bilali lazima atakufa tu kwa namna yoyote ile na wakati ambao atakufa atakuwa amefanya kazi kubwa sana hivyo atahitajika mtu wa kuweza kuimalizia kazi hiyo na kwa hesabu ambazo alikuwa ana uhakika nazo kwa asilimia mia moja ni kwamba kijana wake huyo ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mlinzi wake ndiye mtu ambaye alikuwa anatakiwa kuimaliza kazi hiyo kwa maana hiyo mpaka wakati huo ndiye ambaye alikuwa mtu wa mhimu zaidi ya wote kwenye huo mpango hivyo alitakiwa kuwa hai.

Alimsisitiza sana kwamba anatakiwa kukutana na kijana huyo kwa siri sana ili asije akajua mtu yeyote hata yule mwenzake Dax ambaye alitoa taarifa kwamba alikuwa msaliti lakini hakutakiwa kumfuta kazi na hakutakiwa kujua kabisa kuhusu yeye kukutana kwa siri na Max. kama akifanikiwa kumshawishi huyo kijana akawa upande wake basi wangekuwa wamepiga hatua kubwa sana kwenye hizo harakati zao na kwa wakati huo wasingekuwa na kitu chochote cha kusubiri mpango ulitakiwa kuendelea kama ulivyokuwa mwanzo.

Mzee huyo alimtakia bahati njema na kuweza kumuomba kwamba kama siku hayo mambo yakija kuisha raisi huyo akiwa hai basi hata mara moja moja awe anaikumbuka familia yake pale ambapo Bilali atampa ukweli kuhusu ilipo familia hiyo ila jambo lingine la siri ni kwamba Bilali angekuja kumpa taarifa nyeti sana ambayo watatakiwa kuifanyia kazi haraka sana.

Teodensia Mpanzi mpaka anamaliza kulisoma faili hilo machozi yalikuwa yanashuka kwenye mashavu yake kwa uchungu mkubwa sana kwa sababu mtu ambaye yeye aliamini kwamba ndio ulikuwa mkono wake wa kulia, alikuwa kwenye hatua za mwisho za maisha yake na yeye hakutakiwa kufanya lolote juu ya hilo kwa sababu angeharibu kazi nzima. Hivyo aliachiwa majukumu mazito sana kwenye mkono wake ambayo hakuelewa angeweza vipi kuyamaliza kwani kila kitu alikuwa anaitegemea akili ya mzee huyo ila aliambiwa kwamba kuna kijana ambaye muda sio mrefu mzee huyo atakapokuwa amekufa angemtafuta na huyo ndiye yeye alipaswa kumtumia kwa usahihi sana kuweza kutimiza lile ambalo walikuwa wamelianza kwa pamoja.

Jambo lingine ambalo lilibaki linamuumiza kwenye akili yake ni kuhusu huyo kijana mpya ambaye alikuwa ni mlinzi wake na hakuwahi kumjua kabla ya hapo na aliambiwa kwamba huyo ndiye ambaye alikuwa mtu wa mhimu zaidi kwenye hiyo Kamari ambayo walikuwa wanaicheza wao hivyo alitakiwa kumkalisha chini na kumpa mpango mzima na kijana huyo na kwa namna yoyote ile alikuwa anatakiwa kuishi na kuwa hai hata kama ingetokea nini. Hakuishia hapo tu kuwaza alishangaa sana kwamba ni mahesabu yapi hayo ambayo mzee huyo alikuwa ameyapiga mpaka akajua kwamba huyo kijana wake Bilali ni lazima afe? Hayo ni maswali ambayo ilikuwa ni ngumu sana kwa upande wake kuweza kuyapatia majibu kirahisi kwani hakuwa na mtu wa kumjibu. Aliichukua simu yake haraka sana na kupiga namba ambayo alikuwa anaitumia kuwasiliana na mzee huyo, aliambiwa kwamba namba hiyo haikuwahi kuwepo kabisa kumaanisha kwamba mtumiaji alikuwa amesha iharibu ili kuua ushahidi.

Kitu pekee ambacho alibaki anakifanya kwa wakati huo ni kutoa machozi na kuendelea kushangaa namna nchi ilivyokuwa imejaa wasaliti kiasi kwamba hata kiongozi wa usalama wa shirika la kijasusi alikuwa anamsaliti pia. Teodensia Mpanzi alisogea kwenye droo yake moja na kutoa picha yake moja akiwa bado ni binti akiwa kwenye ubora wake, alikuwa kwenye huzuni kubwa sana lakini aliitoa picha nyinyine ambayo aliipiga miaka mingi baadae baada ya ile ya kwanza, hiyo ya pili alikuwa kwenye tabasamu tofauti na ya mwanzo. Hizo picha zilimkumbusha mbali sana, zilimrudishia kumbukumbu za maisha yake ambayo alikuwa anayaishi huko nyuma kabla ya kuweza kufika hapo ambapo alikuwepo kwa wakati huo.

MIAKA 40 NYUMA.
Ndani ya boda ya Kasumulu ambayo ipo mpakani mwa wilaya ya Kyela na nchi ya Malawi, kulikuwa na mtoto wa kike ambaye alikuwa anajulikana kama Annet Msekwa. Mtoto huyo mdogo ni mtoto ambaye hakuwa na makazi maalumu ndani ya hilo eneo kwa sababu ya kutokuwa na wazazi ambao wangehakikisha kwamba wanamsimamia kwenye ukuaji wake pamoja na kumhudumia hivyo kutokana na kuwakosa wazazi hao akajikuta akiwa bado mtoto mdogo sana akiwa anaranda randa mtaani tu asiwe na kwakwenda wala cha kufanya.

Baba yake alidaiwa kuwa ni mfanya biashara mdogo ambaye alikuwa anakuja mara kadhaa ndani ya hilo eneo kuja kujumua sukari ambazo zilikuwa zimevushwa kimagendo kutoka ndani ya nchi ya Malawi kuja Tanzania na ndani ya eneo hilo kulikuwa na mama ntilie ambaye alidaiwa kwamba alikuwa ni Mmalawi na aliingia ndani ya nchi ya Tanzania bila vibali ila rushwa ya ngono ilikuwa inamuwekea dhamana pale ambapo mamlaka zingetaka kuanza kufuatilia uhalali wake wa kuweza kuishi ndani ya Tanzania hivyo urembo wake ndiyo ilikuwa dhamana ya maisha yake.

Wakati akiwa anaendelea na maisha ya hapo kwenye hiyo boda ndipo alipotokea mwanaume mmoja ambaye alikuwa anafanya biashara ya sukari na kuangukia kwenye penzi zito sana na mwanamke huyo hali ambayo ilipelekea mtu huyo kumpatia mimba huyo mwanamke kwa baadae lakini baada ya tukio hilo mwanaume huyo hakuwahi kuonekana tena mpaka mwanamke huyo anajifungua binti wa kike ambaye alikuwa mrembo sana. Hakuwa amesoma kusema kwamba angeenda kuomba kazi nzuri sehemu ambazo angalau zingechangia kwa kiasi kikubwa kuweza kumuongezea kipato kikubwa hivyo aliamua kupambana mwenyewe na mtoto wake japo maisha yalikuwa magumu sana.

Mtoto wake akiwa ana miaka mitatu tu mwanamke huyo aliugua vibaya sana baada ya kuumwa na mbwa ambaye alikuwa ana kichaa. Maisha yalikuwa ni magumu sana upande wake hivyo alishindwa kuweza kujihudumia mwenyewe hali ambayo ilipelekea kifo chake mbele ya mtoto wake wa miaka mitatu na nusu huku raia wengine wakiwa wanapita tu kama vile hawakuwa wakiona wakati mama huyo anahitaji msaada kutoka kwao.

Jina la Annet Msekwa mwanae alimuita tu ili mtoto huyo aweze kupata jina la ubini na hakumuita jina lingine linalo husiana na yeye kwa sababu hakutaka mwanae aje kujulikana na mtu yeyote yule maana huenda mazingira mabaya ya mama yake yangekuja kumtesa hata mtoto kwa baadae kama watu wakijua kwamba yeye ndiye yule ambaye mama yake alikuwa anauza mwili ili kuweza kuishi. Kufa kwa mama yake akiwa bado mdogo sana ilikuwa safari yake mpya ya kuanza kutanga tanga ambapo leo angekuwa hapa na kesho pale kwa watu ambao walikuwa wanajitolea kuishi naye lakini wengi hawakuweza kudumu naye kwa kisingizio cha kudai kwamba walikuwa na mzigo mzito sana wa kulea familia zao na kipato kilikuwa kidogo sana kwa upande wao hivyo wisingeingia hasara kwa starehe ambayo aliifanya mtu mwingine.

Hali hiyo ilimfanya kuwa binti wa kutanga tanga sana kitu ambacho kilimfanya aijue michezo ya ngono akiwa bado binti mdogo sana wa miaka kumi na tatu tu pekee, baada ya kuanza kupevuka huku ule urembo mkali ambao alikuwa nao mama yake ukianza kushamiri kwa ukubwa sana ndani yake hivyo akawa kivutio kwa watu wengi sana na wanaume wengi wakawa wanatamani sana kuwa naye na hakuwa na namna ya kuweza kuwakataa kwani walikuwa wanampa pesa ambazo zilikuwa zinamsaidia kujikimu na mahitaji madogo madogo.

Baada ya kufikisha miaka kumi na mitano kuna mwanaume ambaye alitokea kuwa mwema sana kwake, mwanaume huyo alikuwa tofauti na wengine kwani kila akija lile eneo alikuwa anamsaidia sana lakini hakuwahi kuomba ngono kwake hata siku moja hali ambayo ilifanya amuone mwanaume huyo wa mhimu sana kwake. Baada ya muda kupita walizoeana sana na wakakubaliana kuoana vizuri na kweli ikawa hivyo akiwa na miaka kumi na sita tu mwanaume huyo alimuoa na kwenda naye sehemu ambayo alikuwa amejenga.

Mwanaume huyo alikuwa ni mzaliwa wa Kyela upande wa Ngekye njia ya kuelekea ufukweni Matema. Baada ya kwenda walikuwa wanaishi kwa furaha sana maana mwanaume huyo alikuwa amejijenga vyema kwenye maisha yake na alikuwa kijana tu na huyo ndiye alikuwa mke wake wa kwanza kwenye maisha yake. Baada ya muda mwanaume huyo ambaye alikuwa anafanya biashara ya kusambaza dagaa maeneo mbali mbali, akiwa ameenda kusimamia wavuvi wake baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa karibu na ziwa Nyasa, kwa bahati mbaya sana alikwamba ndani ya maji sehemu ambayo ilikuwa na mamba wakali sana ambao walimuua huko huko na hawakupata kitu chochote zaidi tu ya taarifa ambazo familia ilizipokea kwa mashuhuda kwamba ameliwa na mamba na wakati huo Annet alikuwa na mimba kubwa tu ambayo muda wowote ule alikuwa anajifungua.

Taarifa ya kufa kwa mumewe kipenzi ilimtia simanzi nzito sana kiasi kwamba akawa mtu wa mawazo sana hali ambayo ilipelekea mimba yake kuweza kuharibika. Kuharibika kwa mimba yake ukawa mwanzo wa familia kumfukuza kwa kudai kwamba alikuwa anataka kula mali za ndugu yao wakati hana hata mtoto hivyo maisha yakawa mtihani mpya kama zamani tena kwake, akajihisi hakuwa na bahati Anneth. Kwa namna maisha yalivyokuwa hakuona namna ya yeye kuishi kule, hata kurudi tena kule boda ya Kasumulu hakutaka kabisa maana alikuwa na kumbukumbu mbaya sana juu ya sehemu ile hivyo akaamua kusafiri, kusafiri kwenda mbali kwenye jiji ambalo alikuwa amezipata sifa zake nyingi sana, jiji la Dar es salaam akiwa binti mrembo sana Anneth.

Baada ya kufika kwenye jiji maarufu zaidi nchini Tanzania hakuwa na nafasi nyingine ya maisha zaidi ya kuutumia vizuri mwili wake ili kuweza kupata nafasi ya kuishi kwa mara nyingine tena japo hakuipenda biashara hiyo kwa sababu kwake ilionekana kuwa kama laana maana alihisi huenda ndiyo ilifanya mama yake akafa lakini angekuwa na lipi Anneth la kuweza kulifanya ili kujikwamua na hiyo hali? Hakuwa na elimu ya kumsaidia wala ndugu mwenye uwezo mkubwa wa kumsaidia hivyo akawa hana namna nyingine ya kufanya, hiyo ndiyo ambayo ilikuwa njia yake pekee ya kuweza kujitoa kwenye huo msala ambao ulikuwa mbele yake.

Kwenye kujiuza kwake alikuja kukutana na mwanamke mmoja ambaye alikuwa maarufu sana ndani ya jiji kwa biashara ya kuuza wanawake hususani kuwauzia watu maarufu kama viongozi wakubwa pamoja na wasanii maarufu ambao hawakuwa wakitaka kuonekana hadharani basi walikuwa wanawasiliana na mwanamama huyo ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwapelekea watu hao kwa siri kisha wanamlipa pesa nyingi sana. Lengo la Anneth kumtafuta mwanamama huyo lilikuwa ni kutaka kukutana na watu wakubwa ambao aliamini kwamba kwa uzoefu wake mkubwa kwenye ngono ungempa nafasi ya kuweza kumtengenezea maisha mapya kabisa na safi ambayo yasingemrudisha kule ambako alikuwa ametoka mwanzo.

Kutokana na urembo wake na namna alivyokuwa binti wa kuvutia alimshawishi yule mama ambaye aliweka dau kubwa sana na kuanza kuwapa taarifa wateja wake wakubwa. Jambo hilo lilifanikiwa baada ya miaka mingi kidogo kupita na wakati huo Anneth alikuwa ana umri wa miaka thelathini baada ya muda mrefu sana wa kuhangaika ndipo alifanikiwa kupata nafasi kwenye danguro la mama huyo. kwa namna alivyokuwa mrembo bado alikuwa anaonekana ni kigoli kabisa kwa wakati huo hivyo mama huyo akalisambaza jina hilo kwa watu wake wa mhimu huku akianza na aliyekuwa raisi wa wakati huo ambaye alikuwa ndo anaingia madarakani Denis Kijazo kwa sababu mama huyo alikuwa anamjua sana kiongozi huyo maana tangu akiwa waziri alikuwa ananunua warembo sana kwake na alikuwa amempa hiyo kazi kama angepata mrembo mzuri sana basi yeye ndiye alikuwa anatakiwa kuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa hiyo.

12 naiweka kalamu pembeni, niseme bye.

Tchao.
 
BADO NINAISHI.

Je umeisoma dunia ya kutisha ya REMY CLAUDE? Kama jibu ni hapana basi leo nakusogezea ofa ya mwisho ya mwezi ambapo unaisoma kwa 4000 tu badala ya 5000.

4000 yako tu leo inakufanya unalisoma moja kati ya andiko bora sana la kijasusi kuwahi kuandikwa.

Muda ni wako sasa, lipia 4000 kwa hizi namba

0621567672 .....HALO-PESA

0745982347...... M-PESA

0714581046..... TIGO-PESA

Zote jina FEBIANI BABUYA.


ASHRAFU NDILO JINA LANGU..... usilikose hili andiko kwa namna yoyote ile.
FB_IMG_1709203161279.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 13
Wakati huo Anneth alikuwa amebadilisha kabisa jina lake ili asije kujulikana sehemu yoyote ile ambayo alikuwa amewahi kuishi kwani kwa sura alikuwa amebadilika sana baada ya muda mrefu mno kupita na watu wake wa zamani wasingeweza kabisa kumtambua kwani hata yeye mwenyewe alikuwa amebadilika sana mwonenako wake. Aliamua kujiita Teodensia Mpanzi huku jina la mwanzo akijiita kwa sababu ni jina ambalo alitamani sana kuweza kuja kumuita mtoto wake wa kike ila kwa bahati mbaya sana hakupata nafasi hiyo ya kuweza kufanikiwa kupata mtoto kama ilivyokuwa ndoto yake tangu mwanzo.

Raisi huyo baada ya kukutanishwa na mwanamke huyo ambaye kwake alikuwa bado ni mgeni sana kwa upande wake alichanganyikiwa na kujikuta akifanya naye mapenzi mara kwa mara huku akitoa amri kwamba mwanamke yule hakutakiwa kuguswa na mwanaume mwingine yeyote yule hali ambayo ilifanya Teo kuwa kwa ajili yake tu pekee. Penzi ambalo alikuwa anapewa na mwanamke huyo lilikuwa ni penzi ambalo nafsi yake ilikiri kwamba hakuwahi kulipata sehemu yoyote ile hivyo hakuwa tayari kabisa kuweza kulipoteza ndiyo sababu alitaka awe analipata yeye tu.

Skendo za raisi kuweza kupata mwanamke kwenda danguro zilianza kusambaa kiutani utani ila baadae jambo hilo lilishika hatamu huku watu wengi wakiwa wanasimuliwa tu ila hawakujua kama ni kweli na ni mwanamke gani ambaye alikuwa anazungumziwa maana Teo kuonekana kwake kusema watu wamfahamu ilikuwa ni adimu sana hivyo ikabakia kuwa kama stori za udaku tu kwa watu ambao walikuwa wanataka kumchafua raisi huyo na yeye mwnyewe alisimamia msimamo wake hapo kwamba hao walikuwa ni watu ambao hawakutakiwa kusikilizwa kwani walikuwa wanataka kuigawa nchi kwa wakati ambao walikuwa ni wamoja.

Lakini wakati jambo hilo likiwa linafurahiwa sana kuna mtu ambaye alilichukulia kwa nafasi ya tofauti sana, hakuwa mwingine bali meja jenerali Francis Mboye ambaye Denis Kijazo alimteua kuwa mkuu wa jeshi la nchi kwa sababu mtu huyo ndiye ambaye alimpatia nafasi kubwa sana yeye jeshini lakini pia ndiye mtu ambaye alimfundisha siasa na kumkutanisha na watu wengi sana ambao kwa baadae walikuja kumfanya akawa raisi mpaka wakati huo ambao alikuwa ndani ya mwaka wake wa kwanza wa uongozi.

Denis hakuwa akifurahiwa sana na mzee huyo licha ya kwamba alimpa nafasi kubwa sana mzee huyo ndiyo maana kwa mzee huyo hizo taarifa zilikuwa nyeti sana na hakutaka kabisa kuweza kuzichukulia kirahisi kama wengine walivyokuwa wanaziona kwa macho yao ya juu juu. Jambo ambalo lilimkera sana mzee huyo ni baada ya raisi huyo kuweza kuwaua watu wote ambao alikuwa amemkutanisha nao wakamfanya kuwa raisi.

Aliwaua wote kwa kudai kwamba watu hao walianza kumtishia na kumpangia cha kufanya kitu ambacho kingekuwa ni hatari sana kwenye uongozi wake wakati ambao yeye alikuwa anatakiwa kuliongoza taifa wao walianza kuonyesha dalili za kumsaliti. Mzee huyo aliona kabisa kijana madaraka yalianza kumpeleka pabaya sana na huenda kingeweza kuja kuwa kirusi kikubwa na kibaya sana ndani ya taifa kwa baadae kama angeendelea kuongea kwa namna hiyo hivyo aliamua kujitolea ili kuweza kupambana naye kwa siri sana huku hadharani akitaka kuendelea kumtii kama bosi wake ili mtu huyo asije akaja kumshtukia maana alionekana kuwa na ajenda za hatari sana na kama asingetumia akili kubwa kupambana naye basi angepoteza maisha kweupe kabisa akiwa hajapiga hatua yoyote ile kwenye hizo harakati zake za kumzuia asije akafanya ujinga taifa likaelekea sehemu mbaya sana.

Sasa muda wote ambao alikuwa anawaza kumtuliza kiongozi huyo mkubwa wa serikali alikuwa anatafuta sehemu ambayo angeanzia ila hakuwa anaiona. Hivyo siku ambayo alipata taarifa kwamba mtu huyo alikuwa anatembea na changudoa ambaye alimuokota kwenye danguro aliona kabisa kwamba huo ungekuwa mwanzo wake wa kutekeleza kile ambacho alikuwa amekipanga kwenye kichwa chake.

Kwanza alitakiwa kuifuatilia historia ya maisha ya mwanamke huyo amjue ndani nje kisha baada ya hapo ndipo akae nae chini akiwa anajua ataanzia wapi na kumshikia wapi kwani kupitia huyo angejua vitu vingi sana ambavyo kwa baadae ungekuja kuwa msaada mkubwa sana kwenye hizo harakati zake ambazo alikuwa amezianza wakati huo. Akiwa bado yupo jeshini kama luteni alikuwa na vijana wake ambao alikuwa anawaamini sana na vijana hao walipikwa kwenye mikono yake ila baadae kwa ushauri wake walipelekwa na serikali nje ya nchi kupata mafunzo ya kikomando na wakati huo walikuwa wanafanya kazi chini yake kwani yeye ndiye ambaye walikuwa wanamuamini sana.

Baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa jeshi alipata nafasi ya kuwa nao karibu zaidi kwa sababu walikuwa chini yake kwa kila kitu ambapo yeye ndiye alikuwa anaweza kutoa ruhusa ya kuwatumia sehemu au asiwatumie na makomando wakubwa sana namna hiyo huwa sio rahisi kila mtu kuwajua hivyo kupitia hao makomando watatu aliunda kikosi chake cha siri ambacho aliamua kukipa jina la DRAGON BOYS akiwa na maana kwamba ni vijana ambao hawazuiliki kwa sababu ya kuwa hatari mithili ya ule moto ambao huwa anautoa ndege aina ya Dragon.

Sasa wakati ambao alikuwa anahitaji kuzikusanya taarifa za mwanamke huyo aliamua kumtumia moja kati ya vijana wake kutoka ndani ya kundi lake hilo la siri na kutokana na umuhimu wa tukio husika aliamua kumtumia kiongozi wa kundi hilo ambaye alikuwa anaitwa Bilali. Mwanaume huyo alitakiwa kwa gharama yoyote ile kuweka ukaribu na mwanamke huyo ikiwezekana hata kufanya naye mapenzi ili kuweza kumvuta karibu yake zaidi kwa siri sana bila raisi kujua maana ilisemekana kwamba huyo mwanamke alikuwa kwa ajili yake tu na ilikuwa ni ngumu sana kuweza kumshawishi mwanamke huyo kutoa penzi sehemu nyingine huku akijua kwamba raisi anamfuatilia na anamlipa pesa nyingi sana lakini pia ingekuwa hatari sana kama angekuja kujua kwamba kuna mtu mwingine anamvua chupi mwanamke ambaye alikuwa amejimilikisha kama ni wake wa pekeyake tena hakutaka kabisa mtu mwingine yeyote aje ajitokeze katikati yao.

Bilali alitakiwa kuicheza hiyo Kamari kwa weledi na ubora wa hali ya juu sana maana pia ilikuwa ni hatari kwa usalama wake mwenyewe ila hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kuingia ulingoni na kuifanya kazi hiyo. Kulingana na kuwa mali ya raisi mwanamke huyo alihamishwa na kuanza kukaa sehemu za gharama sana ambapo alitafutiwa apatimenti Upanga na kumfanya kuwa mwanamke ambaye alikuwa anaishi maisha ya gharama sana ndani ya taifa la Tanzania.

Kuwa sehemu yenye pesa akiwa na ulinzi mkali kulimfanya kuanza kwenda sehemu za starehe na za gharama kubwa sana kwa sababu pesa haikuwa tatizo tena kwa upande wake hivyo alikuwa anafanya shopping za gharama sana maana kila kitu kilikuwa kinalipwa na mheshimiwa raisi. Ila wakati mambo yote hayo yanaendelea, Teo hakuwa ameshtukia jambo moja kwamba kila hatua ambayo alikuwa anaipiga alikuwa anafuatiliwa kwa ukaribu sana.

Mtu ambaye alikuwa anamfuatilia kila hatua ambayo alikuwa anaipiga alikuwa ni Bilali ila hakuwa akijulikana kabisa kwamba alikuwa analifanya jambo hilo la kumfuatilia mwanamke huyo kwa huo ukaribu. Kitu ambacho Teo kilimfanya aanze kutamani kila wakati kutoka kwenda kufanya shopping kwenye duka moja kubwa ambalo lilikuwa linapatikana Mliman City kila alipokuwa akienda alikuwa akimkuta kijana mtanashati ambaye alikuwa anamuuzia vitu. Alikuwa kijana ambaye alikuwa anavutia sana na alionekana kumpenda sana mwanamke huyo maana kwa namna walivyokuwa wanaangaliana ni wazi kabisa kwamba macho yao yalikuwa yanazungumza kwa hisia nzito sana za mapenzi ambazo zilikuwa ndani yao wote wawili.

Jambo hilo lilimfanya ajikute anamuwaza sana kijana huyo kila mara ambapo alikuwa mwenyewe maana kukutana na raisi ilikuwa ni mpaka apate muda wa ziada hivyo akajikuta anaanza kumpenda sana yule kijana na kutamani kuwa naye karibu jambo ambalo alienda kumwambia kijana huyo kwa mdomo wake mwenyewe akiwa ameenda kufanya manununzi walinzi wake wakiwa nje. Kijana huyo alisita sana lakini mwanamke huyo alimsisitiza sana kwamba alikuwa anampenda kwa muda tu tangu aanze kuja maeneo hayo kwa mwezi mmoja tu pekee ambao ulikuwa umepita hivyo mahusiano yakazaliwa kwa mitego tu ambayo mwanamke huyo alikuwa anawekewa na kwa vile muda mwingi alikuwa anakuwa mpweke sana aliona hiyo kwake ilikuwa ni fursa kubwa sana ya kuweza kuwa karibu zaidi na huyo mwanaume asijue kwamba alikuwa amewekwa kwenye mtego mkali mno na komando ambaye yeye alidhania kwamba ni kijana tu anaye yatafuta maisha ndani ya hilo eneo.

Usiku wakati anarudi kutoka kwenye mizunguko yake, walinzi walibakia nje huku Teo yeye akiingia kwenye apartment yake ya gharama sana. Baada ya kuingia ndani alishangaa kumkuta mtu yupo sebuleni kwake akiwa amevaa boxer tu pekee mwili wake ukiwa kama alivyo zaliwa na kwa namna mwili huo ulivyokuwa umekata kata kila sehemu, alitamani kuanza kumlaumu kwa kuingia humo ndani bila taarifa huku akitamani kumuuliza kwamba aliingiaje lakini hakuweza kwani aliishia kumeza tu mate hasa baada ya kuona sehemu ya siri ya mwanaume huyo imetuna sana baada ya yeye kusimama akiwa anamwangalia mwanamke huyo machoni ambapo Teo alijikuta anamkimbilia mwanaume huyo na kwenda kumkumbatia kwa nguo wakajikuta wanahamia kitandani na kulifaidi penzi zito sana ambalo lilimtoa mpaka machozi mwanamke huyo na alikiri wazi kwamba hakuwahi kulipata sehemu yoyote ile na siku hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kuridhika kitandani hivyo alimtaka mwanaume huyo awe wake rasmi na yeye akamuahidi kwamba alimpenda mwanamke huyo mara ya kwanza kabisa tu walipokutana kwahiyo angekuwa wake.

Mwanamke huyo alimtaka mwanaume aweze kumpa maelekezo kwamba alifanikiwa vipi kuingia hapo ila aligoma na kusema ilikuwa siri yake na alifanya hayo kwa sababu ya upendo mkubwa ambao alikuwa nao juu yake. Mapenzi yao yakawa yameanza hapo rasmi ambapo mwanamke huyo alijikuta anapoteza kabisa muda mwingi kwa raisi ila alilazimika kufanya hayo yote kwa sababu tu ya pesa na kwa mapenzi mazito ambayo alikuwa nayo kwa kijana mtanashati ambaye kwake alijitambulisha kama Piusi alilazimika kumpa stori nzima ya maisha yake ili atengeneze uaminifu mwanaume huyo asije akachukia baadae akijua historia ya kweli ya maisha yake hivyo kilaini sana Bilali akawa amezipata taarifa zote za mwanamke huyo kwenye mkono wake.

Baada ya hilo jambo kukamilika taarifa zilifika kwa mheshimiwa meja jenerali Francis Mboye ambaye aliamua kutengeneza mazingira ya kukutana na mwanamke huyo haraka sana iwezekanavyo kwa sababu alikuwa anaujua udhaifu wake, uimara wake na historia nzima ya maisha yake. Asubuhi na mapema sana Teo alikuwa amekwenda kwenye lile duka ambalo alikuwa amezoea kununua vitu vyake ambalo lilikuwa ni duka la meja jenerali mwenyewe huku akiutumia umiliki wa mtu mwingine kabisa ambaye alifanya yeye asitambulike hata kidogo.

Baada ya kufika kwenye lile duka hakumuona mwanaume ambaye alikuwa amemhifadhi kwenye moyo wake na haikuwa kawaida yeye kwenda pale halafu akamkosa mwanaume huyo hivyo hilo jambo lilimshtua pakubwa sana na mshtuko huo ulijionyesha wazi kabisa kwenye macho yake akalazimika kuuliza kuhusu alipo huyo kijana lakini taarifa ambazo alipewa zilimfaya ashindwe kuyazuia machozi yake hadharani hapo hali ambayo ilimfanya mhudumu wa kike kumpa kitambaa kisafi na kumvutia pembeni ili kumpeleka sehemu ambayo walikuwa wanaitumia kubadilishia nguo ili alie huko mpaka pale ambapo angekuwa sawa ndipo atoke maana haikuwa sawa kwa mwanamke mrembo kama huyo kudhalilika hadharani namna hiyo wakati sehemu ya siri kabisa ilikuwepo.

13 nawek kalamu chini, bye-bye.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 14
Taarifa ambayo alipewa mahali hapo ni juu ya kifo cha ghafla sana cha kijana Piusi baada ya kudaiwa kwamba alikutwa akiwa ameuawa sehemu ambayo alikuwa amepanga na familia yake haikutaka jambo hilo lifike mikononi mwa polisi hivyo waliamua kuondoka na mwili wa ndugu yao kwenda kumzika mkoani kwao. Aliuliza kama wanawajua watu hao lakini wafanyakazi wa hiyo sehemu walidai kwamba Piusi alikuja mwenyewe ndani ya jiji hilo na hata hao ndugu walionekana tu baada ya mtu huyo kuweza kuuawa hivyo hawakuacha hata mawasiliano ya kusema kwamba yangewasaidia kujulikana kwamba wao walikuwa ni akina nani haswa.

Aliingia kwenye chumba ambacho kilikuwa kinatumika kubadilishia nguo na kutulia kwenye kioo akiwa anamwaga machozi kwa uchungu sana huku akijihisi kama yeye alikuwa ni mwanamke mwenye laana kubwa sana kwani mume wake wa kwanza alikufa na huyo mpenzi ambaye alikuwa amempenda sana naye alipotea tena kwenye mazingira ya ajabu tu kama yale yale ya mume wake wa kwanza. Ila akiwa anaendelea kujifuta vizuri alihisi kama kuna mtu alikuwa anaufunga mlango wa hicho chumba, alishtuka sana na kuweza kugeuka haraka maana alionekana kuwa mwanaume wakati sehemu hiyo ilikuwa ya wanawake tu.

“Shiiiiiiii, hauna haja ya kupiga kelele maana nimeitafuta sana hii nafasi ya kuweza kukutana na wewe tuongee wawili tu kwa muda mrefu lakini sikukupata kabisa hivyo nina imani kwamba kwa leo tutakuwa na mazungumzo marefu na mazuri sana” mwanaume huyo wa makamo aliongea akiwa anamtaka mwanamke huyo akae lakini hakuwa na amani akabaki anatetemeka tu.

“Wewe ni nani?”
“Ni baada ya kusikia mwanaume ambaye ulikuwa unachepuka naye ameuawa, taarifa hizo zimenishtua sana ndiyo maana nimekuja hapa ili tuongee”

“Mimi sijamuua na sijui kilicho tokea hivyo hakuna lolote ninalo lijua” aliongea huku akiwa analazimisha kutoka hiyo sehemu maana hakuona kama alikuwa salama mbele ya mtu ambaye hakuwa anamfahamu kabisa na hakuwa na kumbukumbu yoyote kama kwenye maisha yao waliwahi kukutana hata siku moja.

“Tumia akili acha mihemko hivi unaona ni kawaida kijana wa watu kuanza tu kufanya mapenzi na wewe anakufa? Huoni kama kutakuwa kuna tatizo kubwa sana mahali ambalo unatakiwa kulifahamu? Umeniuliza mimi ni nani hivyo kaa chini ili tufahamiane halafu utakuwa huru kama utataka tuongee au kama utakuwa na haraka sana basi nitakuacha uende ila hii nafasi ni moja tu na haitakuja kutokea tena kwenye maisha yetu mpaka tunakufa. Kazi ni kwako ukitaka kunisikiliza kaa na kama hutaki unaweza kuondoka” aliongea akiwa anampisha mwanamke huyo kama anataka kwenda aende tu maana yeye hakufika hapo kumlazimisha au kumfanya kitu kibaya bali alitaka wafanye mazungumzo ya amani tu. Kwa wasiwasi mkubwa sana Teo alijikuta anakosa msimamo na kuamua kurudi kuketi maana hakuwa na chaguo lingine zaidi ya hilo.

“Unajua kwamba ni nani ambaye amemuua?” mwanamke huyo aliuliza swali hilo akiwa anajifuta machozi ambayo yalikuwa yameanza kushuka upya kwenye uso wake.
“Ndiyo”
“Ni nani huyo?”
“Hilo jambo sio la mhimu sana na wala usiwe na haraka nalo hivyo kuwa mpole na unisikilize kwa umakini kwa sababu nimekuja hapa kwa shida ya mhimu sana ambayo inatakiwa kuanzia leo wewe ndiye unaweza ukawa mtu wa mhimu zaidi kuweza kuitatua shida hiyo”
“Nakusikiliza mheshimiwa”
“Umeniuliza mimi ni nani sio?”
“Ndiyo”
“Najua kwamba wewe sio mtu ambaye unavutiwa sana na siasa baada ya kuyajua maisha yako ndiyo maana mimi huenda haunifahamu kwani kwako kitu pekee ambacho unakipa kipaumbele zaidi ni pesa tu na hilo sio kosa lako kwa sababu kwa maisha ambayo umeyaishi unastahili kuwa hivyo. Mimi naitwa meja jenerali Francis Mboye ambaye ni mkuu wa jeshi la nchi ya Tanzania” utambulisho wake ulimshtua sana Teo kwani hakutegemea kama kuna siku angeweza kuonana na mtu huyo hadharani na wakafanya mazungumzo ambayo hakujua lengo lake hasa lilikuwa ni lipi. Alijikuta akianza kutetemeka kwani habari za mtu huyo alikuwa nazo na namna alivyokuwa anamiliki watu wenye mabavu ndani yake hivyo uwepo wake haukushiria amani kwa upande wake akajikuta anajiona kama mkosaji mbele yake. Mzee huyo alitulia kwanza akiwa anamwangalia mwanamke huyo akiwa anatetemeka kwa nguvu kiasi kwamba hakuweza tena kukaa akajikuta anataka kusimama.

“Usiogope mimi kuja hapa, sijaja kukudhuru au kukukamata kwamba una kosa hapana ila nahitaji msaada wako mkubwa sana” aliongea na kuhema hali ambayo ilimshtua sana Teo kwani mtu huyo alikuwa anaweza kutumia mabavu tu kumtaka afanye kile ambacho angekitaka na ukizingatia yeye alikuwa changudoa tu sasa suala la kuanza kuombwa lilimshtua kidogo na kumshushia presha ambayo alikuwa nayo hivyo akaketi lakini hata mzee huyo alisogeza kiti na kuketi mbele yake wakabaki waangaliana tu.
“Mheshimiwa mimi ni raia wa kawaida tu sasa ni kipi ambacho unahisi kwamba naweza kukifanya mpaka inafikia hatua unaanza kuniomba mimi msaada?”
“Kwa upande wako upo sahihi kusema kwamba wewe ni raia wa kawaida tu ila kwa sasa taifa hili linakutegemea wewe, maisha ya kizazi kijacho yanategemea maamuzi yako ya muda huu hapa kwa asilimia nyingi sana na nina imani kwamba hautawaangusha katika hilo”
“Mheshimiwa mbona sikuelewi unataka nini kwangu?”
“Unamfahamu Denis Kijazo?”
“Ndiyo, si unaamanisha raisi?”
“Upo sahihi huyo huyo mwanaume ambaye huwa anavua nguo ukiwa naye kitandani” hakumkwepesha mwanamke huyo ikabidi amchane ukweli ambao ulimfanya ameze mate maana hakuwa na la kujitetea juu ya hilo.
“Ndiyo”
“Huyo nataka unisaidie kumteketeza”
“Nini?”
“Nadhani umenisikia sina haja ya kurudia hayo maneno”
“Unataka kumsaliti raisi wa nchi?”
“Unaijua kazi yangu?”
“Ndiyo wewe unatakia kuilinda hii nchi kwa namna yoyote ile”
“Safi, nataka kuilinda nchi hii kutoka kwa huyo mtu wako kwa sababu yeye ndiye sababu kubwa ya taifa hili kushindwa kuendelea, yeye ndiye sababu ya umaskini ambao kila siku unaongezeka nchini lakini yeye ndiye yupo nyuma ya matatizo yote ambayo yanaikumba nchi hii ikiwemo mauaji ya watu hivyo nahitaji apotee kabisa duniani lakini nataka tuanze kwanza kujua mizizi ambayo imemzunguka na kumpa nguvu, nahitaji kujua kwamba anafanya kazi na nani na nani. Nataka kujua uimara wake upo wapi na udhaifu ake upo wapi ili yeye aje kuwa wa mwisho baada ya kuzimaliza sehemu zote ambazo zinaweza kuja kumpa msaada hapo baadae” alikuwa anaongea vitu ambavyo masikio ya Teo yalikuwa yanahisi kama mtu huyo alikuwa mlevi kwani hakuona sababu ya yeye kuhusika kwenye hayo mambo.

“Unataka nimsaliti mwanaume ambaye amenifanya niwe na maisha mazuri, unataka nimsaliti mwanaume ambaye ni mtu mkubwa zaidi ndani ya nchi? Unataka nife nikiwa najiona kijinga namna hii? Hapana sijui ulitaka nini kwangu lakini siwezi kufanya jambo la kipuuzi sana namna hiyo”

“Nimekuja kukuomba kistaarabu ila kama utahitaji nitumie nguvu katika hili basi sitakuwa na namna. Najua utaanza kutishia kwamba utamwambia ukweli kwamba mimi namsaliti yeye ila kabla ya kufanya hilo jambo la kijinga kuna vitu ambavyo unatakiwa kujiuliza kwanza, ni nani amemuua mwanaume ambaye ulikuwa umeanza kumpenda sana, je mke wa raisi akijua kwamba wewe ndiye ambaye unatoka na raisi atakufanya nini? Ukiacha mke vipi kama nikithibitisha kwamba wewe ni hawala wa raisi tena changudoa unadhani shirika la kijasusi la nchi hii litakuacha hai? Ukiacha hayo vipi kama mimi mwenyewe nikiamua kukupoteza nani atajua kwenye taifa hili?” Teo alibaki ametoa macho kwa hasira sana maana maeneo ambayo alikuwa amebanwa hakuwa na namna angeweza kutoka zaidi ya kuwa mpole na kusikiliza kile ambacho angeambiwa.

“Unadhani unanifahamu mimi? Mimi natoka na mheshimiwa raisi kimapenzi na ananijua na kunipenda sana. Unahisi nikimwambia kwamba umenidhalilisha atakuacha kwenye hiyo nafasi yako?”
“Bibie usifanye mambo kuwa magumu, nina taarifa zako zote tangu wakati mama yako anautumia mwili wake ili kuishi huko Kyela, najua maisha ambayo uliyaishi mpaka ukaja kuishia kwenye danguro ambalo limekufanya ukakutana na Denis Kijazo hivyo unatakiwa kuniikiliza kwa umakini sana kabla sijafanya maamuzi mabaya juu yako. Hili ni taifa na ni nchi ambayo kuna watoto wa kike wanateseka kama wewe, kuna watoto wa kike wanabakwa kila siku na kuitumia miili yao kama kinga dhidi yao ili waendelee kuwa hai kama alivyokuwa anafanya mama yako na wewe mwenyewe huku msababishaji mkuu akiwa anatumia pesa ambazo zilitakiwa kutatua hizo changamoto kuhonga wanawake kibao ambao wengine wewe huwajui ukihisi wewe ndiye hawala wake pekee lakini mtu huyo anatumia hizo pesa kuishi maisha ya ufisadi mkubwa ambapo anatumia pesa za nchi kuwekeza huko nje”

“Je unataka ufe kijinga dunia ije kuliimba jina lako kama changudoa ambaye alikufa kijinga duniani na ukashindwa hata cha kujitetea mbele za Mungu au unataka uache historia kama mwanamke shujaa ambaye alifanya makubwa sana kwa taifa lake na wananchi wakaliimba jina lako mpaka kwenye mashairi wanafunzi wakajifunza? Fikiria kisha nipe jibu maana naona unanipotezea muda wangu”
“Nani amemuua Pius?”
“Denis Kijazo”
“Kwanini?”
“Alihisi kwamba huenda unatoka naye baada ya kukuona kila mara ukija hapa dukani”
“Kwahiyo mimi ndiye chanzo cha kifo chake?” aliongea akiwa anaanza kulia tena.
“Hilo halina umuhimu kwa sasa hivyo unaweza ukafanya jambo la kumfanya huko aliko aweze kupumzka kwa amani”
“Unataka nifanye nini?” aliongea kwa hasira sana akionekana wazi kwamba alikuwa na hasira sana na Denis Kijazo baada ya kugundua kamba ndiye ambaye alikuwa nyuma ya kila ambacho kilikuwa kimetokea.
“Unatakiwa uendelee kuishi naye kama kawaida na unatakiwa uzidishe mapenzi kwake na usije ukaonyesha ishara yoyote ila ya kumsaliti yaani usije ukalala au kuwa na ukaribu na mwanaume yeyote yule kiasi kwamba ukampa wasiwasi. Baada ya kufanikisha hilo atakuamini sana na wakati huo utatakiwa akutafutie namna uwe msomi, yule hawezi kushindwa hata kwa kulazimisha hivyo uhakikishe unakuwa na vyeti vya elimu kwa gharama yoyote ile. Tafuta watu wa kukufunza kusoma vizuri, tafuta watu wa lugha wakati yeye akiwa anakutafutia hizo nafasi za kuonekana kwamba wewe ni msomi”

14 natua kalamu chini.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 15
“Baada ya miaka mitano utakuwa umeiva sana baada ya hapo unaweza kumshawishi aanze kukupa nafasi na kukufanya uwe na ushawishi mkubwa sana ndani ya chama na mimi nitakuwa karibu sana kuweza kumshamishi aweze kukufanya kuwa mwanamke mwenye nguvu sana ndani ya taifa hili kwani wewe ndiye ambaye utamsaidia kuyalinda maslahi yake huku nikiwachafua kila watu ambao watatakiwa kuwa kwenye nafasi ambayo nataka wewe uje uwepo hapo baadae. Lakini wakati huo utakuwa unaendelea na hizo taarifa ambazo nataka uweze kunipatia kila hatua ambayo mtu huyo atakuwa anaipiga halafu kwa baadae nitakujulisha kwamba ni jambo gani ambalo litakuwa linafuata na ni kipi ambacho utatakiwa kukifanya kwa wakati huo”

“Unaonekana unamfahamu sana na anaonekana kuwa mtu wako wa karibu sana, sasa kwanini unataka kuyafanya haya na kipi kimekufanya uniamini mimi kama naweza kushika nafasi kubwa kama hizo wakati unaona kabisa mimi ni changudoa tu?”

“Duniani viongozi wengi wakubwa ni wale ambao huwa wanatokea sehemu ambazo hazieleweki, yaani unalala na kuamka unashangaa fulani ndiye mkuu wa nchi mpaka unaanza kujiuliza kwani imekuwaje lakini inakuwa imeshatokea. Hao watu wanafanikiwa sana kwa sababu anakuwa hajulikani kabisa hivyo hata presha ya ufanyaji wake kazi inakuwa ndogo kwani hakuna mtu ambaye anakuwa anamfahamu. Hivyo hata wa kumzingatia sana anakuwa hayupo kitu ambacho kinamfanya kuwa salama na kuyafanya mambo yake kwa amani hivyo wakati wenzake baadae wanakuja kushtuka wanakuwa wamesha chelewa kwani mpaka wamchunguze kiundani basi anachukua kiti kiwepesi sana sehemu yoyote ile ambayo anataka kukaa. Na wewe nataka uwe hivyo, kwa sasa unatakiwa kuishi kama tu changudoa ambaye raisi kwa upumbavu wake kaamua kukupenda na mpe kila kitu ambacho unahisi wanawake wengine huwa hawampi kitu ambacho kitamfanya akili yake yote iwe kwako na hapo ndipo ushindi utaanzia. Hayo mengine utayafanya kwa siri sana kiasi kwamba uma usijue lolote ila yatakuja kuwa mhimu pale uma utakapo anza kuhoji uhalali wako wa kuingia kwenye siasa na haya mazingira ambayo nimekwambia kwamba unatakiwa kuyatengeneza yatakuja kuwafunga midomo wote”

“Kingine kuhusu mimi na yeye kuwa marafiki, ni kweli kwa sababu yule ni kijana wangu ambaye nimemfua mwenyewe kwenye mikono yangu lakini baada ya kupata madaraka akaamua kunisaliti na kutusaliti wote ambao tulimfanya kukaa pale alipo leo. Licha ya kunipa hiki cheo lakini bado nina ndoto za kumtoa kwenye ile nafasi ambayo yupo na kumpoteza kabisa kwa sababu najua yeye kuwa hai inamaanisha taifa linazidi kuwa kwenye hatari kubwa sana na huenda huu mfumo utaenda kwa miaka mingi. Kupotea kwake kutaokoa maisha ya watu wengi sana lakini pia kutaokoa raslimali nyingi sana za taifa hili kwahiyo naomba sana ushirikiane na mimi kwa dhati kabisa tuweze kumteketeza huyu mtu”

“Sasa tutammalizaje wakati yeye ni raisi na ana ulinzi mkali sana, hata ikija kutokea akafa huoni kama itazua taharuki na hatari kubwa sana kwa taifa?”
“Hatumuui kwa sasa”
“Una maanisha nini?”
“Kwa sasa hatuwezi kumuua kwa sababu ametuzidi kila kitu kuanzia watu, nguvu ya pesa lakini yeye ndiye yupo pale juu hivyo inatakiwa muda wa kuweza kujipanga vyema kisha baada ya hapo ndipo tutatekeleza hilo. Suala la kumuua ni baada ya yeye kuondoka madarakani kwani akitoka na akaendelea kuwa hai bado hii nchi itaendelea kuwa kwenye mateso makubwa mno hivyo mpango wangu ni wa hii miaka kumi yaani nataka anavyotoka ndiyo iwe safari yake ya mwisho atoke moja kwa moja na ndio utakuwa muda sahihi wa kuweza kumuua”

“Sawa mheshimiwa, mimi nimekubali kuifanya hii kazi ila naomba unihakikishie kwamba kama litatokea tatizo lolote lile basi utanilinda au kunitoa nje ya nchi”
“Usijali kuhusu hilo ila hakikisha kwamba hakuna mtu ambaye anashtukia juu ya hili jambo. Mimi nitakuwa nakutafuta mwenyewe nikiwa nahitaji kuwasiliana na wewe kwani najua namna ya kukupata. Kingine usiwaamini kabisa wale walinzi wako maana kila ambacho unakifanya huwa wanakifikisha kwake muda wote hivyo ukiwa nao usiwaonyeshe utofauti wowote”

“Asante kwa kunifanya moja kati ya watu ambao watakumbukwa kama mashujaa wa taifa hili” Teo aliongea akiwa na furaha ya tumaini jipya kwenye maisha yake wakati mzee huyo akigeuza kioo kimoja ambacho kilikuwa ukutani na usingeamini kwamba nyuma yake kulikuwa na mlango, alipotelea huko. Teo alikuwa anawaza mengi sana akiwa ameketi hapo kwani hiyo ilikuwa ni kama ndoto kwake, hakuwa na uhakika kabisa na hiyo kazi ambayo alikuwa amepewa na hakujua kwamba hayo mambo yangekuja kuishia wapi ila alitakiwa kukifanya kile ambacho alikuwa ameambiwa na mambo mengine yangejulikana mbele japo alikuwa anaogopa sana. Alisikia sauti za watu wakigonga mlango kwa nguvu sana huku wakiwa wanaita kwa nguvu, hawakuwa wengine bali walinzi wake ambao walipatwa na mashaka kwamba huenda mwanamke huyo akawa kwenye matatizo ndiyo maana alichukua muda mrefu kutoka, hiyo ingekuwa ni kesi kubwa sana kwa mheshimiwa raisi hivyo akatoka kuungana nao tena.

Hizo zilikuwa ni kumbukumbu za raisi Teodensia Mpanzi akiwa anakumbuka namna alivyoweza kukutana na kiongozi huyo mkuu wa jeshi mpaka kufanikiwa kuja kuingia Ikulu kwa sababu ya mipango thabiti ya mzee huyo. Alikuwa anashusha machozi kwenye uso wake kwa sababu simu ambayo alipigiwa na mzee huyo huenda ndiyo ilikuwa simu ya mwisho na alikuwa anamuaga huku akimtaka kuhakikisha kwamba mpango wao unafanikiwa kama walivyokuwa wamepanga na kumuomba asije akamuangusha katika hilo naye aliapa kwa namna yoyote ile alikuwa anatakiwa kulikamilisha jambo hilo hata kama lina hatari kiasi gani kwenye maisha yake.


Meja jenerali Francis Mboye alifika na gari yake kwenye jumba la kifahari la Denis Kijazo akiwa kwenye suti yake nyeusi akiwa ameongozana na mlinzi wake mmoja ambaye ndiye alikuwa dereva wake. Baada ya kushuka kwenye gari yake alisimama getini na kuangalia dunia kila upande kwani alijua kabisa kwamba huo ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake. Akiwa amesimama hapo mlinzi wake ambaye pia ndiye alikuwa dereva wake alimsogelea pale alipokuwepo na kuanza kumsachi kama hakuwa na silaha kwenye mwili wake.

Alitabasamu sana ila kwa uchungu mkubwa kiasi kwamba chozi lilimtoka, huyo kijana kwake alikuwa ni zaidi ya mwanae wa kumzaa kwa namna alivyokuwa anamtunza na kumlea ila wakati anafika hapo ndipo aligundua kwamba hata huyo alikuwa ni moja ya vijana watiifu sana wa Denis Kijazo ndiyo maana yeye ndiye ambaye akichukua hilo jukumu la kuweza kumdhalilisha bosi wake bila hata aibu.

“Hii siku utaikumbuka sana siku unaingia kaburini Herman. Nimeishi na wewe zaidi hata ya mtoto wangu wa damu lakini leo unakuja kunitenda hivi bwana mdogo? Kwanini? Ulikosa nini mpaka ukafanya haya?” aliuliza kwa uchungu sana wakati huo geti lilikuwa linafunguliwa ili aweze kuingia ndani.
“Niligundua kwamba hata wewe ni mbwa tu ambaye unatumwa mzee, sikuwa na uhakika kwamba siku ukitolewa kwenye hiyo nafasi kama naweza kupata nafasi kubwa zaidi ya hii niliyo nayo kwako. Mimi sipendi kuishia kuwa mlinzi tu pekee bali nataka kuwa mtu mkubwa sana kwa hapo baadae na hilo jambo niliona nitalipata upande wa pili ambao ndio upande wenye nguvu, ambao ndio upande wenye pesa nyingi na ndio upande ambao unaweza ukanipa kila ninacho kitaka kwenye maisha yangu. Mimi ndiye ambaye nilikuwa nakuchunguza kwa ukaribu sana mpaka nikafanikiwa kujua kwamba una ajenda zako za siri na raisi kwa sababu licha ya bosi kukuamini sana wewe bado alikuwa na wasiwasi kwani haukuwahi kumpinga hata siku moja na kwa nafasi yako kuna baadhi ya mambo ulitakiwa kuwa unampinga maana hayakuwa na maslahi kwenye taifa lakini wewe kila ambacho alikuwa anakifanya ulikuwa unamuunga mkono hilo likampa wasiwasi sana kwani anajua vyema kwamba ukiona kuna mahali mtu kawa mtiifu sana na ana nafasi ya kufanya jambo siku zote hapo kuna hatari mno. Hatuna muda wa kupiga stori saivi hivyo haya mambo nenda ukamwambie mwenyewe atakusikiliza” mwanaume huyo aliongea kijasiri sana akiwa anamsukuma bosi wake huyo mbele kwenda kwa bosi wake mwingine ambaye alidai kwamba aliona huyo ndiye anaweza kumfanikishia ndoto zake ambazo alikuwa anaziota kila siku na kila wakati. Francis Mboye meja jenerali huyo aliishia kutabasamu tu kwenye uso wake kwa uchungu sana, duniani hakupaswa kumuamini mtu yeyote yule maana hata wale ambao walikuwa wanamzunguka kwa ukaribu sana walikuwa wanamdharau hadharani namna hiyo, hilo lilikuwa ni jambo la hatari sana kwa upande wake yeye.

Waliongoza mpaka sehemu ambayo ilikuwa inatumika kuchezea mpira wa kikapu, hapo walimkuta kiongozi huyo akiwa na watu kadhaa ambao walionekana kuwa wageni wake na bila shaka walikuwa kwenye kikao naye cha siri sana maana palikuwa na vyakula na kila kitu.

“Kwenye maisha yangu yote tangu niweze kukujua nimekuwa nikikuchukulia kama baba kwangu, nimekuwa nikikuchukulia kama mfano bora kwangu lakini zaidi nilikufanya kuwa mshauri wa karibu sana kwangu hivyo nikakuamini sana huenda kuliko hata ninavyo jiamini mimi mwenyewe kwa kuamini kwamba hata wewe ulikuwa unaniona kama mwanao kabisa na ulikuwa ukinitakia mema kwenye maisha yangu lakini jambo la ajabu ni kwamba wewe tena ukawa unataka kuniangamiza mimi kwa kunizunguka nyuma bila mimi kujua? Ulishindwa nini kuja kuniambia mimi mwenyewe moja kwa moja mpaka ukaamua kufanya hivi?” Denis Kijazo aliongea kwa sauti yake ya taratibu na tabasamu juu kama ilivyokuwa kawaida yake huku akiwa anamenya tunda na kisu wakati ambao mzee huyo alikuwa amefikishwa na mlinzi wake ambaye alitoa ishara ya heshima na kusogea pembeni kidogo.

“Nilitamani kuwa hivyo lakini kuna wakati nafsi yangu iligoma kabisa kwa sababu kuna muda nilitamani kabisa kukuua maana nilizalisha mtu wa hovyo sana ambaye baadae amekuja kuwa kirusi kwenye taifa huku familia yake ikiwa salama lakini maskini wengine wakiwa wanateseka mtaani. Haina maana mimi kujivunia kuwa na mtu kama huyo wakati lengo la kulisaidia taifa limeshindikana hivyo nilitamani kukuua kwa mkono wangu mwenyewe ni kwa sababu tu sikuwahi kuipata hiyo nafasi”

“Natamani sana kama haya maneno ungeweza kuyatamka huko nyuma ila kwa bahati mbaya umekuja kuyatamka jioni sana ukiwa hauna namna nyingine ya kuweza kuishi hivyo sitataka unipotezee muda wangu. Yule malaya ambaye nilimuokota kwenye danguro tena kwa ushauri wako mwenyewe ukanishauri nimpe nafasi kubwa na nikafanya hivyo kumbe alikuwa malaya wako na mlikuwa mmelipanga hili kwa muda mrefu ili kuniteketeza lakini ulishindwa kuelewa jambo moja kamba mimi nipo kila sehemu na kuna watu ambao wananiabudu hata hivi nashangaa uliishije miaka yote hii kwenye hiki kivuli nikashindwa kukujua? Kwa hilo nakupa sana hongera. Nitawaua wote ambao wanahusika kwenye hili ila kwa sasa nahitaji kwanza uniambie kipi kinaendelea kwako na ni watu gani ambao wapo nyuma yako mpaka ukapata ujasiri wa kuweza kunisaliti mimi?”

“Mimi najua siwezi kuishi, nimekuja hapa kukipokea kifo changu lakini nakuhakikishia hata wewe hapo siku zako zinahesabika na hivi karibuni utaishia pabaya na kufa kifo cha aibu sana” mzee huyo aliongea akiwa anasogea na kuketi kwenye kiti ambacho kilikuwa kipo karibu na Denis Kijazo.

“Hahaha hahaha ni jambo la ajabu na aibu kubwa sana leo napata vitisho kutoka kwa mtu ambaye yeye ndiye amenitengeneza mimi kuweza kufika hapa nilipo. Wakati nakupa nafasi ya kuwa mkuu wa jeshi la taifa hili kwa mara nyingine niliamini kwamba ungekuwa mtu mtiifu sana kwangu, niliamini kwamba wewe ungekuwa kama mshauri bora sana kwa upande wangu kwa sababu ni mtu ambaye niliamini tupo kwenye safari moja lakini umekuja kunisaliti na kuisaliti imani yangu kwako. Nataka kujua ni kwa sababu yule mwanamke alikuwa nakupanulia miguu hata wewe kilicho katikati yake kikakuchanganya au kuna jambo lingine ambalo mimi silijui”

15 niseme basi.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 16
“Denis hilo halina umuhimu kwa sasa kwa sababu haya yote ambayo unayafanya yana mwisho wake na mwisho wako unakuja”

“Hilo nalijua kwamba kuna siku nitakufa ila sio kufa kwa watu wapumbavu kama wewe hapo hivyo ninacho kuuliza kwangu kina maana kubwa sana ndiyo maana nataka kujua kila kitu”
“Unavyo niona unahisi mimi ni ni wa kutembea na makahaba kama ulivyo wewe?”

“Mhhhh unaanza kunikosea heshima”
“Huo ndio ukweli, mimi nimefanya haya yote kuweza kuisaidia nchi yangu, unaweza kusameheka kama ukiwahi kwenda kutubu kwa sasa ila kwa unavyozidi kuchelewa unazidi kupoteza muda wako wa thamani wa kuishi”

“Ni bora nisingejua kwamba ulikuwa ukishirikiana na yule malaya kwa sababu nitamfanyia kitu kibaya sana. Jambo moja ambalo unahisi mimi silijui ila lipo kwenye kichwa changu ni kuhusu familia yako, najua kwamba familia yako ipo ila kuna mahali umeificha japo kwa bahati iliyokuwa nzuri sijui umeificha wapi ila kama ukiniambia nacho kuuliza basi sitahangaika hata kuweza kuitafuta ila kama itakuwa ngumu kwako basi mimi nitaitafuta na unajua kabisa nitaipata mapema tu hivyo chaguo ni lako” maneno ya Denis Kijazo yalimshtua sana mzee huyo japo hakutaka kuonyesha mshtuko moja kwa moja maana angeonyesha udhaifu mkubwa sana.

“Utakuta nakusubiri mshenzi mkubwa wewe. Yakumbuke maneno yangu UTAKUFA VIBAYA SANA” mzee huyo alitamka kauli hiyo kijasiri sana kisha akatoa kidonge ambacho kilikuwa kwenye mfuko wake mdogo wa koti, alikimeza na kuanza kutoa povu mdomoni.

“Ohhh shiiiit!” Denis alitamka kwa ghadhabu huku akiwa anamsogelea na kutaka kuzuia hilo jambo lakini alikuwa amechelewa, aliamini kwamba angeweza kupata mambo mengi sana kwa mtu huyo kabla ya kumuua lakini zoezi lake liliweza kufeli kwa sababu mhusika mwenyewe aliyatoa maisha mapema sana akionekana wazi kwamba hakuwa tayari kumpa ushirikiano mtu huyo.

Akiwa na hasira kali ambazo zilimfanya kuchomoa bastola yake na kupiga risasi nyingi sana kwa juu huku akiwa na tabasamu kwenye uso wake, alifika mlinzi wake mmoja na kumpa taarifa kwamba kulikuwa na ugeni wake nje ya jumba lake hilo. Alimpa amri mlinzi huyo kuhakikisha watu hao wamefanyiwa ukaguzi wa kutosha kabla ya kupelekwa sehemu ambayo alikuwa anatakiwa kwenda kufanya nao mkutano wakati huo akawa anaagana na wageni ambao alikuwa nao hapo mezani na kutoweka.

Watu ambao walikuwa wamefika ndani ya hilo eneo walikuwa ni Madilu Mpagazi ambaye alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana ndani ya jiji la Dar es salaam pamoja na Msafiri Kigoti ambaye alikuwa ni gavana wa benki kuu. Hawa walikuwa ni wanahisa ndani ya ukumbi wa Denis Kijazo lakini pia walikuwa ni watu wake wa karibu sana ambao miradi mingi ya biashara na ubadhilifu wa pesa walikuwa wakishiriki kwa ukaribu sana.

“Mheshimiwa tangu siku ile hatujapata nafasi ya kuweza kukutana lakini kuna jambo ambalo mpaka sasa tumeshindwa kulielewa. Siku ile ulituambia kwamba kila kitu kipo chini ya usimamizi mzuri lakini mbona mambo yameenda tofauti sana na hali halisi ambayo inatokea?”

“Najua hilo na mpaka sasa hata mimi nimeweza kushtushwa sana na jambo hilo kwani nimeanza kunusa usaliti mkubwa sana kwa watu ambao wananizunguka hata hivi mkuu wa jeshi amekufa dakika chache ambazo zimepita maana naye alikuwa msaliti kwangu ila kwa sasa naona huyo malaya ndiye anafuata na kama kuna mmoja wenu atakuwa anafanya hili basi aje kuniambia mapema naweza kumsamehe ila kama nikimkamata mwenyewe nitamfanyia jambo baya sana yeye na familia yake” alikuwa siriasi sana kiasi kwamba walianza kupata wasiwasi mno hivyo iliwalazimu kuwa wapole maana hakuonekana kuwa sawa kabisa kwa wakati huo.

“Mheshimiwa sisi ni washirika wako kwa kila kitu na hii miradi inatunufaisha sana hivyo hakuna sababu yoyote ile ya sisi kuweza kwenda kinyume na wewe kwani hayo yatakuwa mambo ya hovyo sana. Tulichojia hapa ni kutaka kujua kwamba je ni kipi kinaenda kufanyika baada ya hali hii kuweza kujitokeza?”

“Kwa sasa hatutakiwi kufanya jambo lolote la hovyo hivyo tutakuwa kama hatupo”

“Sijakuelewa unamaanisha kwamba tunatakiwa kushuhudia tukiingia hasara na huyo changudoa apate ushindi kirahisi sana namna hii?”

“Ndiyo”

“Umerukwa na akili sio” gavana wa benki kuu aliongea kwa sauti kwa kuropoka kiasi kwamba hata yeye mwenyewe alijishtukia.

“Samahani sana mheshimiwa nimevuka mipaka” alijiongelesha baada ya kukumbuka kwamba mtu ambaye alikuwa anaongea naye hapo ndiye alikuwa amemfikisha hapo alipo.
“Sio wewe tu hata wenzako walianza hivyo hivyo baada ya kufika pale ambapo walipataka, wakati una maisha magumu ulikuwa mnyenyekevu sana ila kwa sasa una kila kitu unahisi unaweza kunipandishia sauti hadi mimi sio? Nashukuru umeanza kunionyesha rangi yako mapema lakini si unayajua madhara yake?”

“Ndiyo mheshimiwa naomba unisamehe sana”

“Kwa sasa sitaki mtu hapa kwangu mnaweza kwenda kuendelea na shughuli zenu kisha mimi nitajua cha kufanya baada ya hapo nitawapa taarifa” watu hao walionekana walihitaji kujua mambo mengi sana lakini hawakuwa na namna ya kufanya zaidi ya kumtii mtu huyo kwani kuendelea kubishana naye ingekuwa changamoto kubwa sana ambayo ingewaletea matatizo kama sio vifo maana walikuwa wanamjua vizuri sana.


Mheshimiwa raisi akiwa bado kwenye msongo mzito wa mawazo asubuhi na mapema aliamka akiwa na mambo kadhaa kwenye kichwa chake. Jambo la kwanza aliamua kutangaza hadharani kuwateua watu wawili ambao wangekuwa wasaidizi wake wa karibu na mwingine angekuwa mtendaji mkuu wa shughuli zote za kiserikali kwa niaba yake. Kasian Ndepo ambaye alikuwa IGP alimteua kuwa makamu wa raisi na siku hiyo hiyo alitakiwa kuapishwa na kuanza rasmi kuifanya kazi yake lakini pia alimteua Justin Mtadei ambaye alikuwa DCI kuwa waziri mkuu wa nchi ya Tanzania.

Hizo ni habari ambazo zilishika kurasa nyingi sana za mitandao maana raisi huyo alikuwa anafanya teuzi za ghafla sana ambazo watu wengi hawakuwa wamezitegemea lakini wengi walikuwa wanampongeza sana kwa kutoliteua lile kundi la wapigaji ambao walikuwa wanajulikana lakini baadhi ya viongozi wa huko nyuma walikuwa wanaendelea kulilinda na kuwaweka watu wao ndani ya mifumo ya uongozi wa serikali. Lakini jambo ambalo lililishtua zaidi taifa kwa wakati huo ni baada ya raisi kutangaza kwamba mkuu wa majeshi meja jenerali Francis Mboye alikuwa amefariki baada ya kupata mshtuko wa ghafla na moyo wake ukaacha kufanya kazi.

Taarifa za tukio hilo zilikuwa chache sana kiasi kwamba watu wakaanza kuhoji kuhusu hali halisi ambayo ilikuwa inaendelea kwenye ngazi za juu. Kuna watu ambao walikuwa wanaamini kwamba watu hao walikuwa wanauana wenyewe kwa sababu za kimaslahi huku wengine wakijinasibu kwamba walikuwa na taarifa kamili kwamba taifa lilikuwa linaelekea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kwani wakubwa walikuwa wameanza kuleteana usaliti ndani yao wenyewe kwa wenyewe. Taarifa za kifo cha kiongozi huyo alithibitisha baada ya kupokea taarifa kwamba mwili wa mkuu wa majeshi ulikuwa ndani ya hospitali ya taifa ambako aliwatuma watu wake waweze kuhakiki na baada ya kumpa taarifa iliyokuwa kamili ndipo alipata ujasiri wa kuweza kulitangaza jambo hilo kwenye vyombo vya habari.

Raisi huyo wakati akiwa anawasubiria watu wake hao ambao alikuwa amewateua waweze kuja haraka sana waanze kazi, aliingia mlinzi wake wa kike ofisini kwake ambaye alikuwa naye tangu siku ya kwanza anaingia kazini na huyo ndiye alikuwa mlinzi wake mkuu kabla ya kuletwa kwa Max na Dax.

“Bosi samahani sana, kuna kundi kubwa la watu ambalo linasambaza taarifa hizi mitandaoni naona kama zinaweza kuwa na madhara makubwa sana kwa hapo baadae” mwanamke huyo aliongea akiwa anampatia mheshimiwa simu ili aweze kuona na kumpa maelekezo ya nini ambacho kilitakiwa kufanyika. Taarifa hizo hazikuwa nzuri na kwa nafasi yake zilikuwa mbaya sana tena zaidi ya sana kwa sababu zilikuwa zinaenda kumuondolea imani kubwa ambayo alikuwa ameanza kuitengeneza kwa wananchi wake. Zilikuwa ni taarifa za baadhi ya watu ambao walikuwa wanajinadi na kudai kwamba wao walikuwa wanamjua sana mwanamke huyo na ushahidi walikuwa nao tena wengine wakidai kwamba walikuwa tayari kutoa ushirikiano wa kutoa uozo wa raisi huyo hadharani huku wakidai kwamba huyo alikuwa ni changudoa ambaye aliboboea sana kwenye madanguro hivyo hakuwa na sifa yoyote ya kuweza kuendesha taifa na alitakiwa kuondolewa kwenye nafasi yake haraka mno.

“Unawajua hawa watu?” aliuliza kwa hasira sana akiwa anamwangalia mlinzi wake usoni

“Ndiyo bosi, baadhi yao inawezekana kabisa kuwapata na hata huyu mama mwenye hili danguro anaonekana kuhusika maana moja kati ya vijana ambao wameonekana wakikazia sana kuhusu hili jambo kamera zimemnasa mara kadhaa akiingia kwenye hili danguro hivyo mmiliki wake ndiye atakua anahusika kuanza kusambaza hizi taarifa” Brandina ambaye ndiye alikuwa mlinzi wake mkuu aliongea akiwa anaigeuza simu kwa mara nyingine na kumuonyesha tena bosi wake.

“Denis, Denis, Denis nakuahidi utalipa kwa hili” aliongea akiwa anabamiza mikono yake kwenye meza na kuvisambaratisha vitu hovyo hovyo humo ndani.

“Bosi unataka nifanye nini?”

“Nawataka hawa wote kwenye mkono wangu haraka sana, nawahitaji wakiwa hai. Ukitoka nje niitie Dax kuna kazi nataka aweze kuifanya wakati huu. Fanya haraka” alitoa maagizo na kuongea kwa ghadhabu ambapo mlinzi wake aliondoka kwa wasiwasi huku akitoa heshima akimwacha kiongozi wake akiwa anacheka kwa hasira sana tena kile kicheko chenye tabasamu la kinafiki. Ndani ya dakika moja tu Dax alikuwa amefika tena akiingia kwa kukimbia kwenda kumsikiliza bosi wake.

“Shika hii bahasha, nenda kwa Denis Kijazo raisi ambaye alikuwa amepita kisha mpatie hii na umsisitizie ahakikishe kwamba anaisoma kwa namna yoyote ile”

“Nimtaarifu kabla ya kwenda?”

“We mpuuzi nini ningetaka kumtaarifu kulikuwa na haja gani ya kukutuma wewe. Haujui kazi yako sio?”

“Hapana mheshimiwa naomba unisamehe sana”

“Potea hapa na umwambie mwenzako aingie naye nina maongezi naye muda huu”

“Sawa bosi” aliondoka kwa haraka sana maana kiongozi wake alionekana kutokuwa sawa na angeweza kufanya jambo lolote lile baya. Kwa muda wa nusu saa mwanaume huyo alikuwa kwenye spidi kali sana kuweza kuwahi huko alikokuwa ameelekezwa kwenda kupeleka bahasha hiyo, alifika na kukaguliwa kisha akaruhusiwa kuingia ndani ambapo aliambiwa asubiri kisha akutane na bosi mwenyewe, alipewa hiyo nafasi baada ya kuwaambia kwamba alikuwa ana maagizo ya raisi kutoka Ikulu moja kwa moja.

16 niseme baaaasi.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 17
“Bila shaka mkurugenzi wako alikupa majukumu ya kufanya ukiwa Ikulu na unajua nini cha kufanya?” Denis Kijazo aliuliza baada ya kufika hiyo sehemu ambayo kijana huyo alikuwa anamsubiri.
“Ndiyo mheshimiwa, najua kila kitu”
“Safi, enhe! Nambie kilichokuleta kutoka Ikulu” hakuwa na namna zaidi ya kuitoa bahasha ambayo alipewa na raisi na kumkabidhi kiongozi huyo, alimpa mlinzi wake kabla ya kuifungua akaikagua na baada ya kuridhika kwamba iko sawa akamrudishia tena bosi wake ambaye aliifungua ili kuweza kuisoma.

“YOU ARE A COWARD” Ndiyo maneno machache tu yaliyokuwa yameandikwa humo ndani akimaanisha kwamba yeye ni muoga. Alituliza kichwa chake kwa umakini kwamba kama ni hivyo mbona alikuwa anaweza kumtumia kwa meseji tu na sio kumtuma kijana huyo hivyo kumtuma kijana huyo kwake ilikuwa ni tafsiri kwamba alikuwa amejua kila kitu kuhusu huyo kijana wake na kumtoa kwake ilikuwa ni njia ya yeye kuweza kufanya mambo yake pasipo mtu yeyote yule kujua.
“Si huwa mpo wawili?”
“Tupo watatu kiongozi”
“Wenzako wako wapi?”
“Brandina kuna majukumu amepewa ambayo mimi siyajui ila mwenzangu wakati naondoka alikuwa ameitwa ofisini hivyo sijui alipo kwa sasa ila nahisi huenda atakuwa Ikulu bado”
“F***k you Teo” mheshimiwa aliongea kwa sauti kali akiwa anazunguka zunguka hiyo sehemu ambayo walikuwepo.
“Kuna tatizo mheshimiwa?”
“Kukuagiza huku alikuwa anataka kukutoa pale bila wewe kushtuka huenda kuna jambo linaendelea kati ya yeye na mwenzako ambalo hakutaka wewe ulijue. Sasa unatakiwa kurudi Ikulu haraka sana na kwenda kuchunguza kila kitu ambacho ameongea na mwenzako ili kujua kama kuna kitu chochote kinaendelea au kama kuna majukumu ya siri ambayo amempa mwenzako na kuanzia leo kuwa makini sana na huyo mwenzako, hakikisha kila anacho kifanya, kila anacho ongea naye unanipatia taarifa haraka sana. Umenielewa?”
“Ndiyo mheshimiwa”
“Nenda haraka sana” mwanaume aliondoka hapo akiwa anakimbia maana alikuwa amepokea maelekezo kutoka kwa mtu mkubwa sana na alitakiwa kuyafanyia kazi haraka kwani ndiye ambaye alikuwa anawafanya waishi vizuri.

Baada ya Dax kutoweka hiyo sehemu, Denis Kijazo aliitoa simu yake na kumpigia simu mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania Philipo Tibaigana. Simu hiyo iliita kwa muda mfupi sana ikapokelewa.
“Uko wapi?”
“Nipo ofisini mheshimiwa”
“Ni kitu gani ambacho kinaendelea huko na sijui?”
“Hakuna jambo lolote mheshimiwa”
“Raisi ana mpango gani na huyo kijana wako Max?”
“Sina taarifa yoyote ile kiongozi”
“We mpuuzi hivi pesa zangu unahisi naokota na kukulipa ili unenepeshe kitambi chako sio? Huyo malaya amemtuma kijana huyu ambaye anatusaidia kazi pale kwangu kuleta bahasha yenye maneno ambayo alikuwa anaweza kunitumia kwa simu maana yake alikuwa anataka kumtoa pale na hata yule binti ambaye ni mlinzi wake mkuu nasikia naye kamtoa na kubakia na huyo kijana mmoja. Sasa nataka kujua kwamba huyo binti ameenda wapi na kufanya kazi gani lakini na huyo ambaye amebaki Ikulu mtafute uongee naye ujue alikuwa wapi na kufanya kazi gani, kuna mchezo huyu changudoa anataka kuufanya na sitaki litokee tatizo lolote lile hivyo hili jambo limalize haraka sana na unipe majibu ambayo yanaeleweka” alitoa amri na kukata simu kitu ambacho kilimuacha mkurugenzi huyo kwenye mshangao mkubwa sana.

Mkurugenzi huyo aliitafuta namba ya huyo kijana wake ili kumtaka aweze kufika kwenye ofisi yake maana kulikuwa na dharura lakini hakumpata kabisa hewani hivyo alimtafuta Dax na kumpa taarifa ya kuweza kumtafuta mwenzake lakini hata yeye baada ya kufika Ikulu alitoa taarifa za kutokuwepo kwa Max na mheshimiwa raisi hakuwepo ofisini na baadhi ya walinzi walidai kwamba sehemu ambayo alikuwepo ilikuwa ni siri kutokana na amri yake hivyo hakuna ambaye alikuwa anatakiwa kuulizia ulizia lakini pia haikutakiwa taarifa kutoka kuhusu sehemu ambayo alikuepo. Mheshimiwa huyo alitoa maagizo kwa hasira sana kwa kudai kwamba kijana huyo atakapo onekana basi alitakiwa kuripoti haraka sana kwake.

Baada ya Brandina na Dax kuondoka kutekeleza majukumu ambayo walikuwa wamepewa na mheshimiwa raisi, Max au waweza kumuita Donald Daniel ambalo ndilo lilikuwa jina lake halisi la kuzaliwa aliingia ndani ya ofisi hiyo na kutoa heshima kwa kiongozi wake huyo mkubwa wa nchi.
“Una miaka mingapi kwa mara nyingine” alimuuliza akiwa anamtaka aka echini
“23 mheshimiwa”
“Unaelewa nini maana ya uzalendo?”
“Ni kuwa tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili maslahi ya nchi yangu hata kama nitayatoa maisha yangu kwa ajili ya hilo”
“Unapenda siasa?”
“Hapana mheshimiwa”
“Kwanini?”
“Kwa sababu sijawahi kupata nafasi ya kuwa huko lakini huwa naona watu wengi sana wakilalamika kuhusu siasa na mambo ambayo wanafanyiwa na wanasiasa ila kwa wewe nakuona kuwa kiongozi wa tofauti sana na nina imani taifa litajivunia sana kuwa na raisi kama wewe”
“Vizuri kwa kuwa muwazi na hujataka kuwa mnafiki juu ya hilo, kama hupendi kwanini haujachukua hatua yoyote ile kubadilisha kila ambacho hakipo sawa”
“Kazi yangu mimi ni kufuata amri mheshimiwa kuhusu hayo mengine sihusiki kabisa”
“Hata kama ni kuua mtu asiye na hatia?”
“Ndiyo mheshimiwa, kuwa na hatia au kutokuwa na hatia kwa mtu sio biashara yangu mimi kwenye kazi yangu maana amri ndicho kitu pekee ambacho mimi nakiangalia”
“Unajisikiaje pale ambapo unamuua mtu asiye na hatia?”
“Nitajisikia vibaya kama kifo chake hakina msaada mkubwa kwa taifa ila kama kifo chake kitaokoa vingi basi naweza kujisikia vizuri kwani maisha ya watu wengi yana thamani kuliko maisha ya mtu mmoja”

“Safi, kuna kazi ambayo nataka nikupe ila ni kazi ya hatari sana lakini naamini wewe ndiye unaweza kuwa mtu sahihi zaidi kwenye hii kazi ila nataka kabla ya kukupa hii kazi ule kiapo mbele yangu kama raisi wa nchi yako kwamba hautafanya jambo lolote lile la kijinga wala kuonyesha ngozi ya usaliti na kama utafanya hivyo basi utakuwa tayari kufa kwa muda huo huo”

“Mimi nimeapa kukulinda wewe kwa namna yoyote ile mheshimiwa hivyo kauli yako kwangu ni zaidi ya wimbo wa taifa au sauti ya risasi. Mimi nitakutii wewe na kufuata amri yako mpaka siku ambayo nitakuwa naingia kaburini” mwanaume alipa mbele ya mheshimiwa raisi akiwa amepiga magoti.

“Kuna mambo magumu sana ambayo yanaendelea nyuma ya pazia, kuna watu ambao wanataka mimi nife kwa lazima kwa sababu nimegusa maslahi yao. Kiongozi wa hawa watu ambaye anataka mimi nife ni mtu ambaye ndiye ameniweka hapa na ni mtu mwenye nguvu kubwa sana na kila sehemu ana watu wake ambao wanamtii yeye hivyo hata kupambana naye japo najua ni jambo la hatari sana ndiyo maana nimekwambia ni kazi hatari mno. Lakini huyu mtu tunatakiwa kuwadondosha watu wake wote kisha na yeye auawe”

“Suala la kuweza kumuua halijaanza leo, ni suala ambalo lipo kwa miaka kumi sasa ila tulisubiri awe sehemu ambayo haitaleta utata mkubwa sana kuhusu namna ya kumuua na kifo chake kwa ujumla. Sio jambo rahisi kuweza kumuangusha yeye na watu wake lakini ni lazima iwe hivi kwa sababu hakuna namna nyingine zaidi ya hii na kwenye huu mpango kuna uwezekano hata mimi pia naweza kufa lakini hata kama nikifa basi ujue kwamba wewe ndiye utakuwa kila kitu kuweza kulimaliza hili genge ambalo limefanya nchi hii idumae kwa maendeleo, limefanya nchi kuwa uwanja wa mauaji lakini limefanya nchi imekuwa ya mtu mmoja na yeye anahisi ndiye ambaye anatakiwa kufanya maamuzi ya namna gani nchi hii inatakiwa kuendeshwa” maelezo ya mheshimiwa yaliufanya moyo wake uanze kwenda mbio sana maana alihisi kwamba alikuwa anapewa ni majukumu ya kawaida tu ila aligundua kwamba mambo hayo hayakuwa ya kawaida bali ilikuwa ni Kamari moja ya hatari sana kuicheza.

Raisi hakuwa na namna zaidi ya kuamua kumuamini kijana huyo kama bosi wake Francis Mboye alivyokuwa amemwelekeza kwani ndilo tumaini pekee ambalo walikuwa wamebaki nalo hivyo alitakiwa kumuamini kwa lazima huyo kijana maana hakuwa na namna nyingine ya kufanya kutokana na kuzungukwa na kundi kubwa la watu ambao walikuwa ni wasaliti isivyo kawaida. Alimpa stori nzima juu ya kila kitu ambacho kilikuwa kinatakiwa kufanyika na wapi walikuwa wametoka kuanzia siku wanauandaa mpango huo mpaka hatua ambayo alikuwa amefikia siku hiyo ambayo alikuwa anaongea naye. Wakati anamaliza maelezo hayo raisi, Max alikuwa anatetemeka akiwa bado amepiga goti pale chini ambapo alikuwa anakula kiapo.
“Mheshimiwa naweza kujua kwamba huyo mtu ambaye anatakiwa kufa ni nani”
“Denis Kijazo”
“Unamaanisha raisi mstaafu?”
“Ndiyo”
“Kwamba huyu ndiye mtu ambaye huwa anasababisha haya mambo yote kutokea nchini?”

“Ndiyo kijana wangu, hapa nakuomba na sio kukupa amri kwa sababu hili jambo linahitaji uzalendo kwanza kabla ya kutumia nguvu. Yafikirie mamilioni ya maisha ya watanzania yatakavyokuwa na maisha ya amani pindi huyu fedhuli akifa, yafirikie maisha ya watoto ambao hawawezi kupata elimu bora, ambao hawaweze kupata maji safi, ambao hawapati huduma bora za afya kwa sababu pesa ambazo zinatakiwa kwenda huko watu hawa wanaziweka kwenye mifuko yao. Lifikirie kundi la vijana wenzako ambao wamesoma sana na hawapewi ajira kwa sababu ajira zilizopo hawa watu wanawapa watoto zao na ndugu zao tu. Kujitoa kwako na kufanya maamuzi yaliyo sahihi leo hii yataokoa maisha ya watanzania wengi sana ambao hawakujui lakini kupitia wewe watakuwa na tumaini jipya la maisha ambayo yatakuwa na usawa. Hili ni jambo nyeti na la siri sana ndiyo maana hata watu ambao wanahusika ni wachache mno lakini nimekwambia wewe kwa sababu mkuu wa majeshi kabla ya kufa ndiye alinipa ushauri kwamba wewe ndiye mtu pekee ambaye naweza kukuamini baada ya kukufanyia uchunguzi kwa muda mrefu hivyo uamuzi wako leo utaokoa maisha ya watanzania” mwanamke huyo ambaye ndiye alikuwa raisi aliongea akiwa anatokwa na machozi usoni maana lilionekana kuwa jambo nyeti sana kwake.

17 bye-bye.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 18
“Naapa kwa jina la nchi yangu, nitalitumikia taifa langu wakati wowote ule ambao mimi nitahitajika na nitaifuata amri yako mpaka siku naenda kaburini. Naomba uniambie ni kitu gani ambacho natakiwa kukifanya mheshimiwa” jibu la Max lilichanua tabasamu upya kwenye uso wa raisi huyo kwani alipata tumaini lingine ambalo lingempa nguvu ya kupambana na watu hao ambao alikuwa amekula kiapo cha kula nao sahani moja.

“Ule ukumbi ambao nimekwambia kwamba unamilikiwa na mtu huyo inatakiwa leo usiku ufungwe lakini sitaki ufungwe hivi hivi nataka walinzi wa lile eneo wote waweze kufa ili apate ujumbe kwamba mimi simuogiopi na baada ya hapo wataanza kufanya mambo yao kama kunitishia hiyo itatusaidia kumkamata mmoja mmoja na baada ya hao wenzake kuisha tutamaliza na yeye mwenyewe. Kwahiyo nataka watu hao wote uweze kuwaua usiku wa leo kisha utarudi hapa asubuhi kama kawaida kama siku zingine ila kwa leo ondoka muda huu na mtu yeyote asije akakupata hewani wala kujua uko wapi mpaka pale utakapo maliza kazi. Kuhusu maongezi yangu na wewe fanya kama hii siku haijawahi kutokea na hatujawahi kuongea lolote na kukutaka kwetu kuongea haya mambo itakuwa kwa siri sana kwa sababu tumezungukwa kila sehemu na watu wao mpaka pale ambapo mambo yatakaa sawa ila kwa sasa hakuna sehemu ambayo ni salama kabisa”

“Sawa mheshimiwa ila naona kama ingekuwa ni busara kuweza kumshirikisha mkurugenzi anaweza kuwa msaada sana katika hili”
“Unajua kwanini nimekupa hii kazi wewe na sio Philipo Tibaigana?”
“Hapana sijui”
“Kwa sababu naye ni mmoja wao” maneno hayo yalimuacha mdomo wazi mwanaume akiwa haelewi kama kweli mkubwa wake wa kazi naye alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanasaidia kuliteketeza taifa.
“Hili linawezekanaje mheshimiwa?”

“Usiwaamini sana wanadamu, jambo la msingi usimuonyeshe kama umejua lolote lile ambalo linaendelea kwake hivyo endelea kumtii kama mwanzo maana yeye ndiye amewapenyeza watu wake wengi hapa ambao wanaangalia kila kinacho endelea na hata huyo mwenzako ambaye mmekuja naye ni kijana ambaye anafanya kazi hiyo ya kutuchunguza hivyo kuwa makini sana na maisha yako kwa sababu wewe unatakiwa kuwa hai kwa namna yoyote ile, kuna siku nitakwambia kwanini wewe unatakiwa kuwa hai hata kama mimi nitakufa” aliambiwa mambo mazito sana lakini hakuwa na namna ya kuweza kuyakataa kwa sababu yalitoka kwa mtu ambaye alikuwa ni bosi wake hivyo alitakiwa kufanya kila ambacho alikuwa anaelekezwa huku kichwani kwake akiwa bado ana maswali mengi sana.

USIKU
Usiku wa kiza kinene ambao ulikuwa unasindikizwa na taa nyingi ambazo zilikuwa zinalizungukia jiji la Dar es salaam zikiendelea kulifanya jiji hilo kuwa la kuvutia sana isivyo kawaida huku likiwaruhusu wapenda starehe kuendelea kuufurahi uzuri na umaridadi wa jiji hilo lakini ilikuwa tofauti kwa mwanaume mmoja. Usiku huo yanapo patikana makaburi maeneo ya Sinza Makaburini mwanaume mmoja alifika hapo akiwa ndani ya suti moja safi sana huku akishuka kwenye gari moja ya gharama mno. Baada ya kushuka hakusimama hapo bali alianza kuingia katikati kabisa ya makaburi hayo ambapo alifuatwa na mwanaume mmoja ambaye alidai kwamba yeye alikuwa mlinzi wa eneo hilo na hakuna mtu ambaye alikuwa anatakiwa kuingia makaburini usiku kama huo hata hivyo mwanaume huyo hakuongea lolote zaidi ya kutoa waleti kwenye mfuko wake na kutoa noti kadhaa na kumpatia mlinzi huyo ambaye hakuongea jambo zaidi ya kuondoka kimya kama sio yeye ambaye alikuwa anadai hakuna mtu anaruhusiwa kuwa hapo kwa mara ya kwanza.

Mwanaume huyo alitembea haraka haraka mpaka yalipokuwa makaburi manne ambayo yalikuwa yameongozana na kuwa na rangi moja, alikaa kwenye kaburi moja na kuinama chini huku akionekana kuwa mtu mwenye simanzi nzito sana kwenye nafasi yake.

“Mama leo nimefanikiwa kumjua mtu ambaye alihusika kuyateketeza maisha yenu, leo nimemjua mtu ambaye ndiye alinifanya mimi nikabaki kuwa mkiwa kwenye haya maisha bila uwepo wenu nyie na ndugu zangu wawili ambao mpaka leo wangekuwa wakubwa sana mama. Ni mtu ambaye nimemtafuta kwenye maisha yangu yote nikitamani siku nikimpata niweze kumuua kwa mkono wangu kwa yale ambayo alinifanyia lakini siwezi kufanya hivyo mama, siwezi tena kwa sababu mtu huyo tayari amekufa” mwanaume huyo aliongea akiwa na hasira sana huku usoni kwake machozi alikuwa yanamtoka baada ya kuionyesha sura yake vizuri.

Hakuwa mwingine bali alikuwa ni Bilali ambaye alikuwa kijana wa kutegemewa sana na meja jenerali Francis Mboye. Huyo ndiye mwanaume ambaye alikuwa amefika eneo hilo la Sinza Makaburini ambapo walikuwa wamezikwa ndugu zake na wazazi wake na ilikuwa ni kawaida kila baada ya muda angefika eneo hilo akiamini kwamba walikuwa wanamuona na kumsikia vizuri hivyo kwenda eneo hilo alikuwa anajihisi amani kubwa sana na kila anapo ingia ndani ya eneo hilo alikuwa anahakikisha kwamba anakuwa msafi isivyo kawaida ikiwa ni kama asili ya mama yake ambaye alimlea hivyo tangu akiwa mdogo kabisa.

“Siku ile natamani sana kama ningekufa na nyie kwenye ule moto kwa sababu huenda mpaka leo nisingekuwa nayapitia haya maumivu ila kuishi kwangu najiona kabisa sina thamani yoyote ile maana hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kujali tena uwepo wangu mama kama wewe ulivyokuwa unafanya kwangu lakini naumia sana mama kwa sababu mtu ambaye nilimuamini sana yeye ndiye chanzo cha haya yote ambayo yanatokea hivyo moyo wangu unauma sana”

“Amenitoa mbali sana, amenilea kama mwanae, amenikuza na kunifanya kuwa miongoni mwa makomando wa kutegemewa sana ndani ya taifa hili lakini kama haitoshi ameamua kuniachia urithi wa mali zake karibia zote. Na huyo ndiye mtu ambaye mimi nimemtafuta kwa miaka yangu yote mpaka nafika hapa ili nimuue kwa mkono wangu ila kwa bahati mbaya sana yeye ndiye alikuwa bosi wangu kwa miaka yangu yote ambayo nilikuwa hai, yeye ndiye mtu ambaye mimi binafsi nilikuwa namuamini sana kuliko mtu yeyote yule na ndiye mtu pekee ambaye mimi nilikuwa namsikiliza kuliko mtu yeyote yule. Mama sijui nifanye nini, nipo njiapanda sielewi kuna nini kinaenda kutokea kwa sababu nipo kwenye njiapanda ya kuamua kuyafanya majukumu ambayo ameniachia lakini kulingana na alicho kifanya nafsi yangu inakuwa nzito sana kuyafanya haya majukumu na kinacho niuma sana ni kwanini hakuniambia akiwa bado yupo hai? Kwanini asubiri mpaka amekufa ndipo mimi nijue” akiwa anaongea kwa uchungu lakini alihisi kama kuna upepo unapita sehemu aliyokuwepo, alibaki ametulia tu kimya huku akiwa anaamini kwamba huenda alikuwa ni mama yake mzazi alikuwa anaongea naye na kumjibu kile ambacho alikuwa anakiongelea hapo kwa wakati huo. Imani yake ilikuwa inamtuma hivyo akiamini kwamba mama yake muda wote alikuwa bega kwa bega na yeye na alikuwa akimsikiliza mwanae na kumsaidia kufanya maamuzi yake kwenye jambo lolote ambalo alikuwa analifanya.

Akiwa amekaa hapo eneo hilo walionekana wanaume wawili wakiwa wanasogea taratibu sana mmoja akiwa anazungusha saa ya chuma ambayo ilikuwa ya mviringo na haikuwa na mikanda badala yake sehemu ambazo inatakiwa kukaa mikanda, kulikuwa kumewekwa vitu vyenya ncha kali ambavyo vilikuwa vinaingia kwa ndani akiibonyeza na akiamua kuvitoa ilikuwa ni sekunde moja tu pekee. Wanaume hao walikuwa wamevaa nguo nyeusi huku miguu yao ikiwa na mabuti mazito sana, baada ya kufika ndani ya sehemu hiyo wote wawili waliinama chini kama ishara ya kutoa heshima kwa mtu huyo ambaye alikuwa mbele yao.

“Mmechelewa sana kufika hapa, nilikuwa na dakika chache sana za kukaa hapa na baada ya hapo msingeweza kunikuta”
“Tusamehe sana kiongozi, tulihitaji uweze kupata muda wa kutosha na familia yako” Alijibu mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa kijana tu ila mmoja umri wake ulikuwa mkubwa.
“Nashukuru kwa kujali hilo. Nadhani mnapata taarifa kwamba bosi amekufa!”
“Ndiyo sababu tupo hapa bosi amekufaje kizembe hivi halafu raisi anatangaza kiwepsi kabisa namna ile. Tunahitaji kujua ni kipi ambacho kimetokea?”
“Kiongozi ameuawa”
“Na nani?”
“Na raisi mstaafu Denis Kijazo”
“Mshenzi sana yule mzee, atajutia kuzaliwa kwenye hii dunia”
“Msifanye jambo lolote la kipumbavu”
“Kwahiyo bosi amekufa tukae tunashangilia?”
“Angalia sana huo mdomo wako unapokuwa unaongea mbele yangu, umesahau mimi ni nani kwako sio?”

“Nisamehe sana kiongozi lakini tunataka kujua kwanini hautaki aliye sababisha alipie kwa hili?”
“Kuna maagizo ambaye mzee aliniachia kabla ya kufa”
“Unataka kutuambiak kwamba mzee alijua kwamba atakufa? Na wewe ulijua na haujafanya chochote”
“Ndiyo”
“Kwanini?”
“Ndiyo yalikuwa maagizo yake na kama ningenda tofauti basi ningeharibu kazi yote”
“Kivipi?”

“Ilikuwa ni kumuokoa yeye asife au kuhakikisha tunatatua jambo kubwa ambalo lipo mbele yetu. Yeye aliamua kuyatoa sadaka maisha yake ili hili jambo lifanikiwe maana ni mhimu sana kwa upande wa taifa” Bilali ambaye alikuwa kiongozi wa wanaume hao wawili ambao kwa pamoja walikuwa wanaunda kundi hatari la DRAGON BOYS aliamua kuwapa uhalisia wa mambo yote ulivyo na kile ambacho walikuwa wanatakiwa kukifanya baada ya hapo.

“Shiiiit!”
“Kuhusu kifo cha bosi tutalipa kisasi ila hatutakiwi kukurupuka kwa sababu hata hivi nafasi ya sisi kuishi ni ndogo sana, kuna uwezekano mkubwa sisi wote watatu tukafa”

“Kiongozi sijakuelewa unamaanisha nini?”
“Huyo mtu ni mtu mzito sana kuliko hata ambavyo unamjua wewe, ana watu kila sehemu, anatoa amri kila sehemu kwa sababu hata raisi mwenyewe maisha yake yapo hatarini sana mpaka wakati huu na raisi ndiye mtu ambaye anatakiwa kutusaidia katika hili kwa sababu ndiye ambaye bosi alimuweka pale ili aweze kumaliza haya mambo ila kwa bahati mbaya amekufa akiwa hajatimiza ndoto yake lakini katuacha sisi ambao tunatakiwa kuikamilisha ndoto yake kwa namna yoyote ile hivyo tunatakiwa kumpa sapoti kubwa sana mheshimiwa raisi hata kama tutahatarisha maisha yetu”
“Unamaanisha kwamba maisha yetu yapo kwenye hatari kubwa?”

“Ndiyo tena sana ila kitu pekee ambacho kinafanya mpaka sasa tuwe salama ni kwa sababu hatujulikani ila siku ambayo tutajulikana basi kuna uwezekano tutaanza kupotea mmoja mmoja na tusipo jiangalia tunaweza kuisha wote kwa pamoja”

18 inafika mwisho hapa.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom