Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 20
“Kama wewe unafanya nao kazi kwanini wawe na haja ya kumtafuta mdogo wako?”
“Kwa sababu mtu huyu huwa anawaendesha watu kupitia udhaifu wao, udhaifu wa mwanaume ni familia yake au mtu wake wa karibu sana ambaye anampenda sana na ndivyo inavyokuwa. Watu wengi sana wanamtumikia sio kwamba kila mtu anapenda hapana bali unakuwa hauna namna kwani zinakuwa zinatishiwa familia na watu ambao wanakuzunguka hivyo unajikuta kwamba hauna chaguo lingine zaidi ya kumtii yeye na njia hii imemfanya kuwa na watu wengi sana ambao wanamuabudu ili kuzilinda familia zao. Hata hili kovu ambalo unaliona kwenye uso wangu ni yeye mwenyewe aliwahi kunichana na kisu baada ya kuhisi kwamba namsaliti halafu baadae akaja kugundua kwamba sikuwa mimi lakini tayari alikuwa amesha nifanyia ukatili kama huu”

“Sasa kama ulikuwa hautaki kwanini haukuwahi kuondoka na kwenda kuishi mbali ukaachana na huu udhalimu?”
“Kwa sababu kama ningekimbia ningeongeza kasi kubwa sana ya wao kumtafuta mdogo wangu na lazima wangekuja kumpata ila kama nikifa kwenye mikono yake hatakuwa na wasiwasi kwamba nina mtu yeyote yule ambaye bado yupo upande wangu mpaka sasa japo huwa wana wasiwasi sana kwamba nina ndugu ila hilo hawajalitilia manani sana kwa sababu nilikuwa mtiifu sana kwao”

“Ni sababu ipi ambayo imekufanya useme kwamba siwezi kutoka hapa na kwanini hakuna watu leo?”
“Kulikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba eneo hili linaweza kuvamiwa kutokana na amri ya raisi kupishana na bosi hivyo aliamua kuwapa taarifa wateja wake kwamba hili eneo limefungwa mpaka atakapo tangaza kwa mara nyingine tena na kuwapa taarifa. Baada ya hilo jambo kufanyika wakawa wameletwa wanaume wengine ambao ni hatari hata zaidi yangu na ndio wapo ndani ya hili jengo leo hivyo una nafasi ngumu sana ya kutoka ukiwa hai ndugu yangu”

“Hilo ndilo nililokuwa nalihitaji, nilitaka niwakute hawa watu wote, wewe kaa hapo nakuja kukutoa ukiwa hai ili uende kwa mdogo wako” Max aliongea akiwa anataka kunyanyuka lakini mwanaume huyo ambaye alikuwa amejitambulisha kama Siza alimdaka mkono wake.

“Mimi siwezi kuishi tena kwa sababu hata ukiniacha hapa bado wataniua tu ila naomba uniahidi nilicho kuomba kwamba utamlinda mdogo wangu kwa maisha yako yaliyo bakia kisha mimi nitakupa majina mawili ya watu wa karibu ambao wanafanya kazi na Denis Kijazo”
“Sawa nitajie watu hao haraka sana”
“Hapana, mpaka uniahidi kwanza na kunihakikishia kwamba mdogo wangu atakuwa salama”

“Nakuahidi nitamlinda kama ndugu yangu wa damu” mwanaume huyo alitabasamu baada ya Max kutamka hivyo kisha akatikisa kichwa kama ishara ya kuweza kukataa jambo, aliinua uso wake na kutamka.
“Hapana, Muoe uishi naye kama mkeo” Max alizidi kumshangaa mwanaume huyo maana alikuwa anaongea bila hata wasiwasi.
“Nakuahidi nitalitimiza hilo jambo kwa moyo wangu wote” kuhusu kumuoa mwanamke huyo ambaye hata hakuwa akimfahamu aliitikia tu kama kumridhisha ila hakumaanisha kweli na alishangaa sana kwamba mwanaume huyo alikuwa anamaanisha nini mpaka alitamka hivyo.

“Msafiri Kigoti huyu ni gavana wa benki kuu lakini mtu wa pili ni Madilu Mpagazi na huyu ni mfanya biashara mkubwa sana ndani ya nchi. Hawa ni watu ambao mara kadhaa amekuwa akionekana nao maeneo ya siri sana na inaonekana kwamba kwake ni watu wake wa mhimu sana hivyo kama ukifanikiwa kumpata mmoja kati yao unaweza kuwa na mwanzo mzuri sana maana hawa wanajua kila kitu kuhusu mtu huyo japo itakuwa ni ngumu sana kukupa taarifa zake maana wanamuogopa sana” Max alibaki anasikitika tu

“Una uhakika na hiyo taarifa yako?”
“Nimefanya kazi kwa huyu mtu kwa muda mrefu sana hivyo nilikuwa nimeanza kujua mambo yake mengi sana ambayo dunia ya huko nje haiyajui kabisa”
“Asante sana kwa kulisaidia taifa lako taarifa nyeti kama hizi ndugu yangu”
“Kuna taarifa nyingine ambayo inaweza kuwa mhimu sana kwako na kwa watu ambao unafanya nao kazi”
“Ipi hiyo?”
“Ni kuhusu mheshimiwa Laurent Mande”
“Alishakufa huyo gavana wa benki kuu aliyepita”
“Una uhakika gani kwamba alikufa?”
“Mhhhh taarifa zilikuwa zinasema hivyo”
“Hapana huyo mtu yupo hai”
“Inawezekana vipi hili jambo likawa la kweli?”

“Nimekwambia kwamba mtu huyu anacheza michezo ya akili sana na mara nyingi huwa anautumia udhaifu wa watu kuwaendesha. Huyu mtu ni mzima kabisa na amehifadhiwa huko Morogoro ila sijui ni wapi hivyo ukiwabana hao watu wake wanaweza wakawa na taarifa za kukupatia zaidi. Kabla sijapoteza maisha naomba nikuone japo sura yako tu” Max alitoa kitambaa chake usoni mwanaume huyo akafanikiwa kumuona kijna mdogo tu mbele yake lakini akiwa anaendelea kumwangalia kwa umakini hapo damu zilimrukia Max kwenye mwili wake ndipo alishtuka kwamba Siza alikuwa amepigwa risasi ya kichwa. Hakutaka kuzubaa alijirusha mbali na shoka lake mkononi kisha akaifunika sura yake na kujibanza sehemu ambayo ilikuwa na ukuta mzito sana, mwanaume ambaye alipiga risasi hiyo kwa Siza alipiga risasi nyingi sana kwenye ule uelekeo ambao alikuwa amejificha Max akiwa anamuona Siza anamwanga damu pale chini kichwa chake kikiwa kimetobolewa vibaya sana.

Max aliangalia kwenye mkono wake, shilingi yale alikuwa nayo ambapo aliiokota pale chini wakati ule anamsogelea Siza kwa mara ya kwanza. Aliizungusha kwa nguvu sana kuielekezea ilipokuwepo taa ambayo ilikuwa inatoa mwanga hafifu sehemu hiyo, iliipasua taa hiyo jambo ambalo lilikuwa la ghafla sana hivyo yule mwanaume ambaye alikuwa anashambulia alishtuka na kuangalia upande huo wakati taa hiyo inazimika na hilo lilikuwa ni kosa lake ambalo lilimuwahisha kaburini. Ile nafasi ambayo yeye aliitumia kuzubaa kushangaa kilichokuwa kinaendelea pale ndio muda ambao Max alijitoa pale alipokuwa amejibanza na kuchomoka kwa kasi sana kuelekea kwa mwanaume yule.

Alihisi kama kuna kitu kinakuja upande wake hivyo akakoki silaha na kugeuka haraka sana ila alikuwa amechelewa mno kwani Max alikuwa amepita na shingo yake, shingo ilikatwa vibaya sana na kisu hali ambayo ilimfanya abakie ameishika shingo hiyo huku akitapa tapa. Max hakuhangaika hata kugeuka nyuma maana hesabu zake zilikuwa zimeisha, hivyo aliokota shilingi yake,alitembea kwa kasi sana maana alikuwa ana ramani nzima ya jengo hilo kubwa, kila sehemu ambayo alikuwa anapita malango yalikuwa yapo wazi kabisa kumaanisha kwamba mgeni yeyote alikuwa anakaribishwa kuingia humo ndani.

Alitokezea sehemu ambayo ilikuwa na ulingo wa mapigano, sehemu hiyo ya ulingo ilikuwa na taa safi kabisa ambayo ilikuwa inawaka vyema na katikati ya ulingo huo kulikuwa na damu ambayo ilionekana kuwa mbichi kabisa kama ishara kwamba kuna mtu aliuawa muda mfupi tu ambao ulikuwa umepita. Pembezoni mwa ulingo huo kulikuwa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa amekaa pembeni akiwa kifua wazi na upanga pembeni huku akiwa anavuta sigara bila wasiwasi akionekana kuwa mbali sana kimawazo lakini aligundua kwamba hiyo sehemu mwanaume huyo hakuwa mwenyewe bali kulikuwa na wanaume wengine.

Hilo aliligundua baada ya kuangalia kwenye siti za watazamaji na kuona pande tatu tofauti kuna mwanaume mmoja mmoja akiwa amesimama bila wasiwasi kila mtu akiwa anavuta sigara yake. Mwanaume aliyekuwa pale ulingoni alirusha pingu mbele ya Max huku akinyanyuka
“Bwana mdogo unaweza ukajifunga hizo pingu ukamsikilize bosi kwa hiari au kama ukitaka kutumia njia nyingine ambayo inakufaa basi unaweza kutuua sisi wanne ambao unatuona humu ndani kisha ukaondoka zao maana tulikuwa sita tu na mpaka umefika hapa maana yake wawili umeshafanikiwa kuwaua” mwanaume huyo aliongea akiwa anaimalizia sigara yake ambayo aliishia kuizimia kwenye kifua chake ambacho kilituna sana.

Max alimwagalia mwanaume huyo kwa umakini sana kisha akasogea karibu kabisa na zilipokuwepo kamba ambazo zilizungushiwa kwenye ulingo huo kwenye mkono wake akiwa na shoka lake kama kawaida.
“Hivi ndivyo ambavyo huwa unamwambia kila mtu ambaye unakutana naye?”
“Acha taarabu bwana mdogo, fuata nilicho kuagiza au kama hautaki basi unakaribishwa ulingoni hapa tuweze kupimana nguvu ili uende huko ukiwa hauna baadhi ya viungo kwenye mwili wako” hiyo kwake ilikuwa ni kama dharau kubwa, aliruka na kutua kwenye kamba ambapo alijigeuza kwa sarakasi kali sna na kutua ndani ya ulingo hali ambayo ilifanya buti lake litue kwa nguvu sana kwenye damu ya mtu ambaye alikuwa ameuawa, damu hiyo ilimrukia mwanaume ambaye alikuwa humo ulingoni kifuani, aliigusa kwa kidole chake na kuiramba kisha aliukanyaga upanga wake kwa nguvu kwenye kishikio, ukajirusha juu kisha akaudaka kwa mkono wake mmoja na kuanza safari ya kumsogelea Max kwa nguvu mwili wake ukiwa unaitikia kwa namna ulivyokuwa umekazwa vyema.

Mwanaume huyo alikuwa anazungusha upanga huo kwa nguvu sana lakini aliishia kuikata kata kamba ambayo ilikuwa juu kabisa ya ulingo huo. Aliteleza kwenye damu akiwa anauzungusha upanga wake kwa nguvu lakini alisimama ghafla akiwa na hofu baada ya kukoswa na shoka ambalo lilitua chini na kumkosa kidogo kwenye uso wake. Alielewa kwamba hakutakiwa kufanya utani maana alikuwa anayaweka maisha yake hatarini sana hata wale wenzake ni kama kilichokuwa kinatokea kilikuwa nje kabisa na matarajio yao kwani pambano hilo walijua lingeisha haraka sana ila kuchelewa kwake kuisha kuliwafanya wasogee karibu ili nao waweze kulifaidi kwa uzuri kabisa.

Mwanaume huyo alinyanyuka kwa sarakasi kali sana lakini aliishia kupigwa buti kali la kichwa ambalo lilimpeleka kwenye kamba za pembeni ambazo zilimpotezeshea mwelekeo akawa anarudi bila mpangilio, shoka lilitua kwenye kifua chake na kukipasua vibaya sana hali ambayo ilipelekea kudondokea kichwa ambacho kilipasuka vibaya mno na habari yake ikawa imeishia hapo hapo. Jambo hilo liliwashtua wenzake ambao wote walichomoa mapanga yao na kuja kwa kasi sana eneo la ulingoni wakiwa ndani ya mavazi mazito sana.

Ujio wao wa kasi ulimchanganya sana Max ambapo alifanikiwa kuyapangua mateke ya wanaume wawili lakini mwanaume mmoja alizamisha upanga wake kwenye ubavu wake na kumkutanisha na buti kali la shingo ambalo lilimpelekea pembeni kabisa mwa ulingo huo na kama sio kudaka kamba basi angetoka kabisa nje ya ulingo. Watu hao walikuwa wanakuja kwa kasi mno wawili wakiwa wanazunguka chini huku mmoja akiwa anakuja kwa sarakasi kali sana ya juu. Alidunda kwenye kamba akiwa bado ana maumivu na ubavu wake ambao ulikuwa unatoa damu, hali hiyo ilimfanya kuwakwepa wale wanaume wa chini hivyo akakutana na wa juu ambaye alimruhusu ampige na ngumi kali lakini na yeye lengo lake lilitimia baada ya kuzamisha kisu chake kidogo kwenye shingo ya mwanaume huyo na kuichana vibaya sana kisha akatua kwa mbele na wakati anatua alirusha shoka lake ambalo lilitua kwenye kiuno cha mwanaume mmoja ambaye alikuwa anajiandaa kugeuka akabaki anagala gala chini kwa kilio kizito sana maana kuanzia wakati huo kwenye maisha yake yote asingeweza kutembea tena.

20 inafika mwisho.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 21
Mmoja ambaye alikuwa amebakia ni kama hakuwa akiamini kilichokuwa kinaendelea, yeye na hao wenzake watatu ambapo wawili walikuwa wamekufa tayari na mmoja alikuwa kwenye hali mbaya sana na ni yeye tu pekee ambaye alibaki amesimama akiwa vizuri kabisa, wasiwasi ni kama ulianza kumuingia kwenye nafsi yake kama watatu waliuawa basi pekeyake ilikuwa ni ngumu sana kumkabili adui yake japo hakutakiwa kuuonyesha huo udhaifu hapo.

Lakini kwa upande wa adui yake Max alikuwa anatokwa na damu kwenye ubavu wake na mdomoni maana sehemu hiyo upanga uliingia, alichana sehemu ndogo ya koti lake pembezoni kwenye zipu akazungushia kwenye jeraha hilo kwa kugundika na gundi ambayo aliitoa kwenye mfuko wake akiwa amesimama anaangaliana na mwenzake ambaye alikuwa amebaki mwenyewe. Wakati wanaume hao wakiwa wanapigiana mahesabu mmoja akiwa an upanga mkali sana kwenye mwili wake na mwingine akiwa na shoka la chuma kwenye mkono wake, nje ya jengo hilo ulisikika mlio wa gari zikiwa zinaingia hapo kwa kasi sana. Zilikuwa ni gari tatu ambazo zilipiga breki za ghafla sana na watu ambao alikuwa ndani ya gari hizo walitoka kwa kasi sana huku kwenye kila gari moja akitoka mwanaume mmoja na kupotelea kwenye kiza ambacho kilizingira eneo hilo hususani baada ya Max kuipasua taa ambayo ilikuwa inatoa mwanga ndani ya eneo hilo.

Max aliangalia saa yake kwa umakini sana huku akionekana kama mtu ambaye alikuwa anapiga hesabu zake kulingana na dakika ambazo alikuwa anakaa humo ndani. Mwanaume ambaye alikuwa mbele yake alihesabu vyema hatua zake akiwa anamjia Max lakini alikosea kidogo kwenye mahesabu yake baada ya kuja kwa kasi lakini mwanaume aligusa kwenye kiuno chake na kutoa bastola kwa kasi ambapo alimtandika risasi mbili mwanaume huyo kwenye magoti yake na kumfanya adondoke vibaya sana kwenye sakafu nzito ambayo ilikuwa ulingoni hapo kwani ulikuwa ni ulingo wa tofauti sana, haukuwa umejengwa kwa plastiki bali simenti yenyewe kabisa hivyo mtu akidondoka hapo alikuwa anakutana na simenti moja kwa moja.

Alimsogelea mwanaume huyo na kulishusha shoka lake kwenye mkono wa huyo mwanaume ambaye aliishia kupiga kelele lakini alitulizwa na shoka hilo pia baada ya kukatwa mguu wa kulia na kuambiwa atulie vinginevyo angeendelea kukatwa kila sehemu ya mwili wake.
“Mmejinadi sana wakati naingia hapa, nadhani mlihisi kwamba nimefika hapa kwa bahati mbaya ila ni jambo ambalo hamkuwa sawa hata kidogo, sijui lakini huenda mimi naenda kuwa mtu hatari sana ndani ya nchi hii kwa sababu kazi ambayo ipo mbele yangu inanifanya kuua iwe kazi yangu rasmi ambayo huenda nitaifanya kwa miaka mingi sana ambayo inakuja huko mbele mpaka pale ambapo nitakuwa nakufa”
“Wewe ni nani?”

“Kunijua haina umuhimu wowote ule ila nina swali dogo sana kwako, unaweza ukachagua kufa kama shujaa wa taifa au unaweza ukachagua kufa kifala kama jambazi la taifa. Unaweza ukaniambia kwamba kuna mambo gani ya siri ambayo wewe unayajua kuhusu jumba hili na hawa watu ambao wanalimiliki hili jumba?”

“F**k you” mwanaume huyo aliongea akiwa anamuonyesha Max dole la kati, mwanaume alimwangalia sana mwanaume huyo kisha akasimama na kulishika shoka lake vyema, alilishusha shoka hilo na kuisambaratisha shingo ya mwanaume huyo ambapo kichwa kilijitenga kabisa na kiwili wili.

Lakini wakati Max anatekeleza unyama huo ambao alikuwa anaufanya hapo ulingoni, kuna wanaume watatu mmoja akiwa ndani ya suti kali sana na wengine wawili wakiwa kwenye mavazi meusi walikuwa wanafika hapo na kushuhudia mwanaume mwenzao akitolewa shingo kikatili mno. Max aligundua kwamba kulikuwa na ugeni mwingine ndani ya hilo eneo.

“Ohhhh shiiiiiit” alitamka kwa hasira akiwa anaangalia saa yake kwa umakini sana. Haikueleweka sababu ya msingi ya yeye kutaka kwenda na muda sana maana alichukia sana watu hao kufika hapo kwani wangempotezea muda na muda wake wa kukaa hapo ndani ulionekana kwamba ulikuwa umeisha. Baada ya tukio hilo aliruka kutoka kwenye ulingo akiwa amemlenga mwanaume mwenye suti ambaye alikuwa mbele na shoka lake. Mwanaume huyo hakuwa mwingine bali Bilali ambaye alikuwa amekuja sehemu hiyo kuwateketeza watu ambao walikuwa hapo lakini alikuwa amechelewa kwani wakati wanafika walikuta kuna mtu mwingine ambaye alikuwa anaifanya kazi hiyo kwa niaba yao.

Baada ya kukoswa na shoka hilo Bilali akiwa anageuka haraka sana sehemu ambayo mwanaume yule alitua hakumuona, alifanikiwa kuona tu koti likiishia ukutani sehemu ambayo ilikuwa inaelekea kwenye geti la kutokea. Walishangazwa na tukio hilo ambapo mwanaume mmoja alisogea karibu na ule mlango ambapo mtu yule aliishia na hapo ndipo alisikia akitukana.

“Oooooh Fu**ck, kuna bomu tukimbie haraka” alitoa sauti kali sana baada ya kusikia alamu ya bomu ikilia kwa nguvu sana, hali hiyo iliwafanya wakimbie kwa nguvu sana baada ya kuelewa sababu ambayo ilimfanya mwanaume yule kukimbia kwa nguvu sana kutoka nje, ina maana alikuwa anajua kile ambacho alikifanya. Wakati wanafika getini ndio muda ambao jengo lilikuwa linalipuka kwa nguvu na kushuka chini. Mlipuko ulikuwa ni mkubwa sana kiasi kwamba uliwarusha mbali mno huku mwanaume ambaye alifanya tukio hilo akiwa hajulikani kwamba ni wapi alikuwepo wakati huo.

DRAGON BOYS walinyanyuka baada ya kama dakika tatu kupita huku wote wakiwa wamechakaa sana kwani moto ambao uliwarusha huko ulichoma choma nguo zao.
“Tuondoke haraka sana” Bilali aliwapa amri hao vijana wake ambapo kila mtu aliingia kwenye gari yake na kutoka hapo haraka sana huku wakiwa wanalishuhudia jengo hilo kubwa ambalo lilijengwa kwa pesa nyingi sana likiwa linateketea lote. Kwa mbali kidogo sehemu ambayo ilipandwa miti mirefu ya kisasa pakiwa na bembea alionekana Max akiwa anaangalia kwa mbali namna jengo hilo lilivyokuwa linateketea kama utani. Wakati anaingia sehemu ile ambayo ilikuwa ina ulingo ni wakati ambao alikuwa ametega bomu kubwa sana karibu na ile sehemu ikiwa ni maagizo kutoka kwa mkubwa wa nchi kwani watu ambao walikuwa wanalimiliki jengo hilo walimuudhi pakubwa sana baada ya kumuua mkuu wa jeshi la nchi ya Tanzania hivyo alikuwa anahitaji kuwalipa kwa yale ambayo walikuwa wameyafanya. Max baada ya kuhakikisha kwamba jengo hilo limeshuka lote hakuwa na muda wa kupoteza tena aliondoka eneo hilo mwili wake ukiwa mzito sana kwani alikuwa amepoteza damu kiasi cha kutosha na tayari alikuwa amejeruhiwa vibaya kwenye mbavu yake.

Maeneo ya Mikocheni karibu na lilipo shirika la msalaba mwekundu ndiyo sehemu ambayo ilikuwa makao makuu ya wanaume hao watatu DRAGON BOYS. Yalikuwa ni makazi yao ya siri sana ambayo yalikuwa yanatumika kuwahifadhi pale wanapokuwa na kazi zao za dharura sana basi ungewakuta hapo wakiwa wanaipanga mipango yao mikali sana, kitu ambacho kilitokea siku hiyo hakikuwa cha kawaida ndiyo maana wote waliongozana moja kwa moja mpaka ndani ya eneo hilo ili kuweza kujaduili kwa urefu juu ya kile ambacho kilifanyika.

Wanaume hao wote baada ya kuingiza gari zao kwenye jengo hilo la kifahari, waliingia ndani na kufunga milango yote kisha wakaingia kwenye chumba kimoja ambapo baada ya kubonyeza rimoti kiliachia katikati zikatokea ngazi na wanaume hao wakashuka huko chini kisha pakajifunga tena kwa mara nyingine. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na skirini nyingi kubwa sana, waliziwasha haraka sana na kusogea hapo ili kuona kama kulikuwa na kitu ambacho wangeweza kukiona huku wakiwa kimya sana, hakuna hata mmoja wao ambaye alikuwa anaongea jambo lolote lile.

Lengo la kukaa hapo ni kwamba walihitaji kuona kamera zote za jiji ili kuweza kujua kama mhusika ambaye walimkuta kule alikuwa ni nani na baada ya pale alielekea wapi ili waweze kumtafuta. Ziliwashwa kamera za jiji zima huku wakiwa wanatafuta haraka sana kila sehemu kuanzia nje ya lile jengo ambalo lililipuka. Wakati wanaondoka pale walimuona mwanaume huyo kwa mbali akiwa anawaangalia bila wasiwasi kisha akaondoka ndani ya hilo eneo, kwenye mkono wake alikuwa na simu mfano wa rimoti ambapo aliiminya mara kadhaa na umeme ukakata maeneo yote ambayo yalikuwa yanazunguka hapo.

Kuzima kwa umeme kulienda sambamba na uzimwaji wa kamera ambazo zilikuwa zinaonekana mbele yao, kamera zilipokuja kurudi kwenye hali yake ya kawaida hawakuona mtu yeyote yule. Walijaribu kupekua kila sehemu ya jiji lakini kilichokuwa kinaonekana ni watu tu wakiendelea na harakati zao za maisha ya kawaida hususani kwa wale ambao walikuwa wanakesha wakifanya kazi ili kuupigania mkate wao kwa namna yoyote ile.

Bilali alibaki anacheka huku akiwa anasikitika sana, aliinua na kucheka kwa nguvu mno kwa sababu jambo kama hilo halikuwahi kumtokea kwenye maisha yake ya kawaida na siku hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza yeye kuchezewa michezo kwenye mipango yake kama hiyo.
“Hatimaye nimempata”
“Nani?”
“Mtu ambaye ananizidi uwezo”
“Unamaamisha nini kusema hivyo?”

“Huyu ndiye mtu ambaye sisi tulikuwa tunamtafuta, nina imani ananizidi kwa kila kitu na leo amedhihirisha hilo kwa kunifanya mimi kama mtoto mdogo”

“Kwamba huyu ndiye mtu wa mhimu zaidi wa huyo mzee ambaye tunatakiwa kumuua?”
“Hapana huyu ndiye ambaye sisi tunatakiwa kumlinda na ndiye mtu wa mhimu sana kwenye kulifanikisha hili jambo kama bosi alivyo agiza wakati ananipa maagizo yake ya mwisho”

“Umejuaje na una uhakika gani na hili jambo?”
“Kwani sisi tulienda kufanya nini pale?”
“Kuliteketeza lile jengo”
“Na yule mtu amefanyaje?”
“Kaliteketeza jengo”
“Safi, nadhani sasa mumeelewa na ni lazima yule mtu ametumwa na raisi mwenyewe na si vingine”
“Lakini alitaka kutuuua yule mtu”

21 inafika mwisho.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 22
“Kwenye mazingira kama yale ulitaka aanze kukuamini na hakujui? Fikiria mara mbili juu ya hilo, ukifika wakati kama ule unatakiwa kwanza kuyawaza maisha yako kuliko jambo lolote lile kwa sababu hata sisi tungekaa kijinga pale tungelipuka na lile jengo halafu unahisi kwamba ingekuwaje au ungemlaumu yeye ukiwa ndani ya mchanga? Jibu ni hapana hivyo alitumia nadhania ya bwana Charles Darwin “SURVIVAL FOR THE FITTEST”
“Kwahiyo unashauri nini?”

“Huyu tunahitajika kumpata haraka sana lakini pia tunatakiwa kukutana na mheshimiwa raisi ili tujue ni hatua gani ambayo tunatakiwa kuipiga kwa sasa. Kwa jambo ambalo limefanyika leo wahusika sidhani kama watakuwa na uvumilivu sana maana watahitaji kuweza kulipiza juu ya kuteketezwa kwa jambo lao, kwahiyo sisi tunatakiwa kuwa hatua moja mbele zaidi yao ili wanapofanya maamuzi tuwe tunajua kwamba sisi tunawakamatia wapi ila jambo la msingi huyu mtu tunatakiwa kumpata mapema sana kwani ndiye atakuwa msaada wetu mkubwa sana. Hakuna mtu wa kawaida ambaye anaweza kuingia kwa kujiamini sehemu kama ile namna ile halafu akatoka akiwa salama bila shida yoyote ile, nimeishi sana ndani ya ule ukumbi, nimepigana sana ndani ya ule ukumbi na nimecheza sana Kamari ndani ya ule ukumbi hivyo naweza kuwa miongoni mwa watu wachache sana ambao wanaujua ule ukumbi kiundani zaidi. Mle huwa wanalinda watu wenye uwezo mkubwa sana kwenye tasnia ya mapigano, kama mtu yule ametoka salama pale basi sio mtu wa kawaida kwenye mapigano hivyo akiwa upande wetu tutakuwa tumeongeza mtu wa maana sana ambaye tunamhitaji mno” alikamilisha maelekezo yake kwa vijana wake ambayo pia yalikuwa kama maagizo juu ya kumpata mwanaume huyo ambaye waliona kwamba ingekuwa ni vizuri sana kama angekuwa upande wao.

Kulipuka kwa jengo maarufu zaidi ndani ya nchi, kulipuka kwa ukumbi mkubwa zaidi ambao matajiri walikuwa wanakula raha kwa namna ambavyo walikuwa wakijisikia wao, ukumbi ambao habari zake maskini waliishia kusimuliwa tu na baadhi ya watu ambao walibahatika kuuishi usiku hata mmoja huko ndiyo ilikuwa habari kubwa zaidi ambayo ilikuwa inaliendesha jiji hususani kwenye mitandao ya kijamii. Usiku huo huo wa tukio habari zilianza kuzagaa kila sehemu, watu walikuwa wanapigwa na butwaa juu ya kulipuka kwa jengo hilo huku wengine wakitaka kujua usalama wa watu ambao walikuwa ndani ya jengo hilo.

Baadhi ya maskini walijifariji kwamba kuna muda kutokuwa na pesa kwao lilikuwa jambo bora zaidi maana wale ambao walikuwa wanajivunia kuwa na pesa nyingi sana huenda walifia ndani ya jengo hilo, ila kiuhalisia ilikuwa ni kujifariji ujinga tu maana dakika chache tu mbele ungewaona watu hao hao walaulaani sana umaskini baada ya njaa kali kuweza kuwazidia huku wakiwa hawana la kufanya. Taarifa hizo zilikuwa zinasambaa kwa kasi kubwa sana kiasi kwamba zilianza kuvuka hadi nje ya mipaka ya nchi huku watu wengi sana wakiwa wanahoji kwamba ni kitu gani hasa ambacho kilikuwa kimesababisha jengo hilo kubwa kuweza kulipuka.

Wakati huo ambao habari hizo zilikuwa zinasambaa kila sehemu, taarifa ilifika moja kwa moja kwa mhusika mkuu wa jengo hilo. Denis kijazo usiku wa manane huo alikuwa amelala na mkewe, ilimuamsha simu ambayo ilikuwa inaita kwa fujo sana, aliinuka na kuipokea simu hiyo huku akimlaani sana aliyekuwa ameipiga ila aliipokea kwa sababu usiku kama huo lazima ilikuwa ni taarifa nyeti sana ambayo ilifanya mpaka atafutwe.

Baada ya kupokea simu hiyo mtu ambaye alikuwa amempigia alimtaka kiongozi huyo aweze kutoka ndani ya nyumba yake akiwa amevaa kisha kuna sehemu alihitaji kumpeleka. Alikuwa mlinzi wake mkuu ndiye ambaye alimpa bosi wake taarifa hiyo, licha ya kuwa na hasira za kusumbuliwa usiku ila alisisitizwa kwamba jambo hilo lilikuwa la mhimu sana na yeye ndiye pekee ambaye alikuwa anatakiwa kulifanyia maamuzi hivyo alitakiwa kuwepo.

“Kipi kinakufanya unisumbue na usiku wa manane wote huu ambao nimepumzika na mke wangu?” aliuliza kwa ghadhabu baada ya kutoka nje ya chumba chake.
“Naomba twende kule ukumbini mheshimiwa, kuna dharura ya ghafla sana ambayo inakuhitaji wewe ufanye maamuzi”

“Huwezi ukaniambia hapa?”
“Hapana, nahitaji uone kwa macho yako” mheshimiwa kuna kitu kilipiga kwenye moyo wake kwa nguvu sana kwani aliona kabisa kwamba sehemu hiyo haikuwa na usalama wowote ule ila aliamua kukubali na kuingia kwenye gari ambapo msafara wake uliondoka nyumbani kwake na kuelekea lilikokuwa liapatikana jengo hilo. Barabarani walikuwa wanapishana na polisi ambao walionekna kuwa kwenye haraka kubwa sana.

Walivyokaribia kufika kwenye hilo eneo dereva alisimamisha gari na mheshimiwa akaambiwa hapo anaweza kushuka, alitembea hatua kadhaa na kukaa chini. Ule mwanga wa gari nyingi za polisi na wa zimamoto ulikuwa unamulika vizuri sana lile eneo, hakukuonekana kuwa na jengo lolote lile zaidi ya vifusi ambavyo vilikuwa vimejirundika sehemu tofauti tofauti. Aliishiwa nguvu kwani sehemu hiyo kulikuwa na jengo kubwa sana na la bei ghali mno ila kilichokuwa kinaonekana mbele yake lilikuwa ni jambo ambalo alihisi kwamba analiona ndotoni.

“Nini kinaendelea?” hakujibiwa bali mlinzi wake huyo alimpa simu ili aweze kuangalia taarifa ya habari juu ya jambo ambalo lilikuwa limetokea hapo. Alisikitika sana na kuipasua simu hiyo ambayo ilikuwa kwenye mkono wake.

“Wewe malaya nitakupasua vipande vipande kwenye mwili wako na hiyo sehemu yako ya siri nitaichomoa niibanike kisha nitaila” aliongea kwa jaziba sana huku akinyanyuka na kutoa amri kwamba watu wote watolewe hilo eneo na hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa anatakiwa kuendelea kurekodi kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea ndani ya hiyo sehemu.
“Bosi nadhani itakuwa vyema kama utaondoka hili eneo ukapumzike kwa sababu tayari umepaona, sisi tunasubiri amri yako”
“Vijana ambao waliwekwa kwa ajili ya kulinda hapa wameangukiwa na jengo?”

“Ndiyo bosi lakini kwa taarifa za polisi kwa miili ambayo tayari wameipata ni kwamba watu hao waliuawa kabla ya kuanguka kwa jengo kwa sbaabu kuna alama ambazo ni za mapanga au shoka ndizo ziliyatoa maisha yao huku wawili wakikutwa na risasi ambapo mmoja amepigwa risasi ya kichwa ambaye alikuwa mlinzi wa getini lakini na mguu wake mmoja umetolewa huku mwingine akiwa amepigwa kwenye magoti na huyu amekutwa ulingoni”

“Maana yake aliwatuma watu kuifanya hii kazi sio?”

“Sio watu mkuu ni mtu, kwa aina ya mauaji ambayo yametokea inaonekana muuaji alikuwa mmoja tu”
“Mmoja?”

“Ndiyo, kwa sababu kama wauaji wangekuwa tofauti basi hata aina ya mauaji ilitakiwa kuwa tofauti”
“Inawezekanaje na huyo mtu atakuwa amempata wapi?”

“Nadhani huenda atakuwa na watu wengi wa siri ambao ndio wanampa ujasiri wa kuyafanya haya yote ambayo anayafanya ndiyo maana alikuwa na jeuri mpaka ya kumtuma mtu kuja kukutia hasara kubwa namna hii”

“Hivi yule kijana mwingine ambaye alidaiwa kubakia Ikulu wakati Dax amekuja nyumbani, jana alipatikana?”
“Hapana, kwa taarifa zilizopo ni kwamba mpaka sasa hajulikani alipo”
“Namtaka huyu kijana apatikane haraka sana na kama akipatikana basi achunguzwe kwa umakini sana ili niwe na uhakika kama ni yeye ndiye amehusika kwenye jambo hili basi nitamfanyia jambo ambali atakufa akiwa analiogopa sana jina langu”

“Sawa mkuu”
“Halafu piga simu Ikulu waambie kwamba nataka kuonana na huyo changudoa”
“Taarifa ambayo ipo Ikulu ni kwamba hakuna mtu ambaye anatakiwa kufika pale wala kutoka kwa sasa mpaka raisi atakapotoa amri na vitambulisho vyako vyote pale vimefungiwa kwa sasa hauruhusiwi kufika pale na imetolewa amri kwamba kama ukiingia pale utakuwa kama msaliti hivyo raisi atakutafuta mwenyewe atakapokuwa na mazungumzo na wewe”

“Mhhhhhh hiyo amri kaitoa Teo mwenyewe?”
“Ndiyo mkuu”
“Huyu malaya atakuwa na siku chache sana za kuweza kuishi Ikulu”
“Kuna kingine ambacho unakitaka kwa sasa mkuu?”
“Kesho wapigie simu washirika wangu wote waambie kwamba kuna kikao cha dharura na kila mtu afike haraka sana hivyo maamuzi yatabadilika kutoka kwenye kumchunguza huyu mwanamke na kwa sasa tunaenda kumuua”
“Bosi”
“Fanya nilicho kuagiza kwa sababu ukijifanya unataka kunishauri muda huu basi nakuua” ilikuwa ni kauli ya msisitizo sana ambayo mlinzi hakuwa na namna ya kuipinga zaidi ya kuweza kuitii kama bosi wake alivyokuwa anahitaji iwe.

Nyakati hizo ambazo mambo yote hayo yalikuwa yanaendelea, raisi Teodensia Mpanzi alikuwa ameketi na watu wasio pungua watano ambao walikuwa wamefungwa mbele yake kila mtu kwenye kiti chake. Hao watu ndio wale ambao Brandina alipewa amri ya kwenda kuwatia mbavuni kwa sababu wanne ndio ambao walikuwa wanasambaza sana taarifa za kudai kwamba yeye alikuwa ni changudoa na hakustahili kuwepo kwenye hiyo nafasi huku mmoja wao ambaye alijulikana kama Mama Tana akiwa ndiye mmiliki wa danguro ambalo ndilo lilimfanya yeye kukutana na raisi Denis Kijazo. Mama huyo ndiye ambaye alikuwa chanzo cha watu hao kuzipata taarifa zake nyingi sana kwa sababu aliishia naye kwa muda na ndiye ambaye alimuuza kwa raisi.

Mwanamke huyo alikuwa akitemeka sana kwani licha ya yeye kuwa ndiye ambaye alimuuza mwanamama huyo kwa raisi lakini huyo mbele yake hakuwa changudoa tena bali raisi wa nchi.
“Nilikuwamini sana mama Tana ndiyo maana sikutaka hata kuja kukuingilia kwenye biashara yako kwa sababu nilikuwa naheshimu sana muda ambao tulifanya kazi pamoja licha ya kujua kwamba biashara hiyo ni haramu kwa nchi yetu. Sasa ni kipi ambacho kimekufanya uanze kuwapa watu taarifa zangu? Ina maana unaoa wivu sana mimi kukaa hapa, ina maana hautaki mimi kuwa raisi wako bali unatamani niendelee kuwa changudoa kwenye danguro lako kisha uniuze kama ulivyokuwa unanitumikisha kwa wanaume wakati ule sio?”

22 inafika mwisho.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 23
“Hapana mheshimiwa sina maana hiyo”
“Maana yako ni ipi?”
“Ni kwa sababu ya pesa tu”

“Kuniuza kwa yule fedhuli ulilipwa kiasi kikubwa sana cha pesa kwahiyo ukaona kabisa hazitoshi mpaka ukaamua kutaka kuniteketeza kabisa?”
“Nisamehe sana hili halitajirudia tena, naapa”

“Nawachukia sana wanadamu ambao huwa wanafanya makosa wakiwa wana uelewa wao halafu wanategemea kulitumia neno samahani ili kujiweka kwenye mstari wa kutia huruma. Hivi unahisi mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwenye msamaha labda?” aliongea kwa sauti akiwa anaweka mkono wake karibu na sehemu ambayo alikuwepo Brandina, Brandina alitoa bastola haraka sana na kumkabidhi mheshimiwa huyo ambapo aliichukua na kuwapiga vijana wawili na risasi kwenye vichwa vyao hali ambayo ilimfanya mama Tana kuzidi kutetemeka sana na wale vijana wengine wawili ambao walikuwa wamebakia wakiwa pembeni wasiamini kile ambacho walikuwa wanakiona mbele yao.

“Naweza kufanya lolote lile ambalo unalitaka wewe mheshimiwa ila naomba sana usiniue”
“Kazi nyako ni rahisi sana hapa. Nakurekodi video uongee ukiwa kawaida tu bila kuonyesha wasiwasi kisha ueleze ukweli wa mtu ambaye amekupa hii kazi ambaye bila shaka ni Denis mwenyewe na utengue kauli yako kwa kuniomba msamaha na baada ya hapo nitafikiria kama naweza kukusamehe au vipi”

“Asante sana mheshimiwa” mwanamke huyo hilo kwake alilihesabia kama msamaha ulikuwa umetoka tayari. Hakuwa na namna zaidi ya kuongea kila kitu ambacho aliambiwa akizungumze lakini hata baada ya kumaliza kufanya hivyo aliuawa na wenzake kwani hao ndio ambao wangeanza kutafutwa sana na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vinahitaji kupata ukweli wa taarifa ambayo ilikuwa imesambaa sana ikimhusu raisi wa nchi ya Tanzania Teodensia Mpanzi.
“Sijawahi kumwamini mtu muongo hata siku moja” aliongea huku akitoka ndani ya chumba hicho na kumrushia bastola Brandina kama ilivyokuwa mwanzo.

Kulikucha asubuhi na mapema sana, asubuhi ambayo ilikuwa na habari motomoto huku wenye peji zao za udaku wakiwa wanajinasibu kwamba walikuwa na habari motomoto kuwafikishia raia sehemu mbali mbali. Ni asubuhi hiyo ambayo walikutana wanaume ambao sura zao hazikuwa na furaha hata kidogo, walikutana watu ambao mioyo yao ilikuwa na hasira mno kwa sababu walikuwa wameguswa sehemu mbaya sana ambayo ilikuwa inagusa maslahi yao moja kwa moja.

“Kiongozi tumekuja hapa na tunakuheshimu sana lakini tunashangaa unafanya nini mpaka mambo kama haya yanatokea tena chini ya mwanamke? Unamaanisha kwamba umeshindwa kutuongoza na unahitaji tuchague mtu mwingine wa kusimama hapo kwenye nafasi yako?” alifoka mwanaume mmoja ambaye alikuwa na kichwa kikubwa sana na tumbo kubwa ambalo liliashiria ulafi wa kula aliokuwa nao na alionekana kuwa moja kati ya watu ambao walikuwa na utajiri mkubwa kwa jinsi alivyokuwa anajiamini.

“Kuja kwetu hapa tunahitaji kujua kwamba ni hatua gani inafuata na maamuzi gani umeyachukua ili kuweza kuokoa mali zetu, tunataka kujua nini mwafaka wetu baada ya hili maana inaonekana kwamba huu ni mwanzo tu na mambo mengi sana mabaya ambayo yanaenda kutokea kitu ambacho kitafanya tupewe hata kesi za uhujumu uchumi mwisho wa siku tuchukuliwe mali zetu zote, aisee mimi sipo tayari kuweza kurudi Karume kuuza mitumba”

“Kwangu mimi nadhani hapa tunapaswa kumuua huyo mwanamke kwa sababu jinsi tunavyompa muda zaidi anazidi kuhisi kwamba anatumudu na huenda atapiga hatua nyingi sana ambazo sisi tutakuwa tunajifanya wajanja kumzuga ila huenda yeye katuzidi na anatuona sisi kama mafala”

“Kama mmekosa watu wa kufanya hii kazi, tuna watu wengi sana ambao tunaweza kuwaagiza kutoka nje ya nchi wakaja kuifanya na tusijulikane kwamba sisi ndio wahusika ila kusema kamba huyu malaya aendelee kuliongoza taifa hapana mimi siungi mkono hii hoja kabisa, anatakiwa kutolewa tena ikiwezekana aletwe mbele yetu na anayeweza am-bake kabisa na kurekodiwa ili iwe funzo kwa mjinga mwingine ambaye atatamani kuja kuanza kutuzunguka kwa hapo baadae” zilikuwa ni kauli tofauti tofauti za wadau ambao walikuwa wamefika kwenye mkutano na Denis Kijazo kama alivyokuwa ameagiza huku akiwa anawasikiliza kwa makini sana na kukaa kimya kama ni mtu ambaye hakuwepo hapo. Baada ya watu hao kubishana kwa muda mrefu sana bila kufikia mwafaka, alisimama mzee mmoja wa makamo kidogo na kuguna ambapo wote walikaa kimya akaanza kuongea

“Miaka mitano nyuma tuliwahi kuwa na kikao kizito kingine kama hiki huku tukiwa tunawaza nani wa kumkabidhi nchi ambaye atalinda maslahi yetu kwa pamoja. Kutokana na mimi kuwa miongoni mwa watu ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana sisi kuwepo hapa kwenye umoja huu ikapendekezwa kwamba mwanangu ndiye apewe nchi kitu ambacho kilikubaliwa na kila mtu kisha baada hapo mtoto wa kiongozi Kijazo angekuwa raisi anayefuata baada ya mwanangu lakini hata kama angeanza mtoto wa Kijazo kisha akafuata mwanangu bado ingekuwa sawa tu. Lakini jambo la ajabu ambalo lilitokea akaamua kumpatia changudoa nchi jambo ambalo lilitukera na kutuchukiza sana wote kwa sababu halikuwa kwenye makubaliano ila tuliamua kuheshimu maamuzi yake kama kiongozi wetu ambaye ametutoa mbali sana baada ya kutuhakikishia kwamba huyo malaya angekaa pale tu kama kivuli ila nchi angekuwa anaiendesha yeye lakini jambo la ajabu hivi tunavyo ongea hata yeye amezuiliwa kwenda Ikulu bila sababu maalumu mana yake ni kwamba hata yeye Ikulu kwa sasa hapamhusu. Hivyo tunataka kupata majibu ya haraka sana na tunaamini mpaka umetuita muda huu basi ushawaza nini cha kufanya na kwamba ni hatua gani kali ambayo unaichukua dhidi ya jambo hili. Jengo ambalo limelipuka ni jengo ambalo tumewekeza mabilioni yetu, ni jengo ambalo tulilijenga kwa maumivu makali sana hata kama wengine shea zetu ni ndogo lakini zinapswa kuheshimiwa, sasa ni hatua gani ambayo unaichukua na inaweza kurudisha hasara ambayo imetokea” mzee huyo alitoa maelezo ambayo yalipigiwa kelele na kila mtu ambaye alikuwa ndani humo wengi wakionekana kukubaliana naye.

Denis Kijazo baada ya kumskiliza mzee huyo ambaye ni kama alikuwa anamsubiri yeye amalize kisha na yeye ndipo aongee, alisimama na kuiwasha sigara yake kisha akawazunguka watu wote humo ndani akiwa anaivuta sigara yake na kurudi kukaa huku akiwa anatoa kidonge kimoja na kumeza kwa kutumia pombe. Alijikohoza kidogo na kukifungua kinywa chake;

“Ni wangapi kati yenu humu ndani wamefika hapa leo kwa juhudi zao?” ndilo lilikuwa swali lake kwenda kwa hao watu huku akiwa anaendelea kuivuta sigara yake kwa fujo sana. Wote walikuwa wapo kimya, hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa anaongea jambo lolote hata wale ambao walikuwa wanachangia kwa uchungu sana. Alicheka kwa sauti mno na kutikisa kichwa chake.

“Kuna muda natamani bora ningefuga mbwa kuliko kuwa na watu wapumbavu kama nyie kwenye upande wangu, natamani mngekuwa mmekufa wote wapuuzi wakubwa nyie. Nani anastahili kunipigia kelele hapo kati yenu? Nani ambaye ana uchungu na hizi mali kuliko mimi ambaye ndiye nilizipigania pale Ikulu nikiwa kama raisi? Niliwaokota sehemu tofauti tofauti na kuwapa maisha, wengine mlikuwa mmekata hata tamaa ya kuishi halafu leo mnakuja kunibwekea kwa eti mna uchungu na mali zenu? Mali zipi hizo? Kwa mtu ambaye hana mpango na mimi na anajihisi anastahili kudai haki yake kwangu nampa sekunde thelathini atoke humu ndani na kuondoka kabla sijabadili maamuzi vinginevyo wote mnatakiwa kukaa kimya na kunisikiliza, sijawaita hapa ili muanze kunitambia jinsi mlivyo umia bali nimewaita hapa kuwapa maagizo juu ya nini cha kufanya” baada ya mheshimiwa kuweza kuongea kwa ukali sana, watu wote ambao walikuwa humo ndani walikaa kimya sana kwa sababu angefanya maamuzi ya kutisha sana kama kuna mtu angeendelea kuwa na misimamo ya kuweza kumpinga, baada ya kuona watu wote wamekaa kimya na kuamua kumsikiliza yeye ndipo aliizima sigara yake na kwenda kukaa kwenye kiti chake tena.

“Kwa sasa watu wote ambao mpo humu ndani mnatakiwa kusimamisha biashara zenu zote ambazo mnahisi zina mashaka au kasoro zozote, nazungumzia biashara zote ambazo sio za halali, nazungumzia biashara ambazo mnahisi kwamba zinaweza kuwa na athari kwenu kama mkikamatwa. Sijajua ni kwa kina kirefu kiasi gani huyu mwaamke amefika maana mpaka ananisaliti mimi lazima amejipanga vya kutosha hivyo sitaki kukurupuka kufanya maamuzi kabla ya kujua kwamba ana nani na nani pembeni yake lakini nataka kuhakikisha kama je hana watu wengine miongoni mwetu ambao huenda wanampatia taarifa za kila tunacho kifanya! Na baada ya hapo nitawapa jibu kwamba ni kipi nimeamua kukifanya juu yake ila kwa sasa kila mtu ajifanye kama vile hayupo, tucheze kama tumekufa halafu mtasikia ni kipi kinacho endelea ila hili jambo litakuwa la muda mfupi sana baada ya hapo litakuwa limeisha na tutajua kwamba tunarudisha vipi hii hasara kubwa ambayo tumepata. Mnaweza kwenda” aliamua kufupisha maelezo baada ya kuona kuna malumbano badala ya maelewano huku kila mtu akionekana kujali zaidi maslahi yake hivyo wote walitakiwa kuondoka na kwenda kuyafanyia kazi maagizo yake huku wakiwa wanasubiri kuona kile ambacho kitafuata baada ya hapo.

Baada ya watu hao kuondoka, aliitoa simu yake na kumpigia Philipo Tibaigana. Simu hiyo ilimkutia ofisini kwake, baada ya kupokea simu hiyo mazungumzo yalianza akiwa anamsikiliza kiongozi huyo kwa umakini sana.

“Najua kwa sasa kuna mambo mengi sana yatatokea hapa katikati kwa sababu hata mimi nilikuwa kwenye hicho kiti cha uraisi. Kwa sasa lazima atakuwa anafanya uchunguzi mkali sana wa kuweza kujua nani yupo upande wake na nani hayupo kwenye upande wake ambapo miongoni mwa watu ambao anaweza kuanza nao ni wewe hapo. Huenda mpaka sasa ameshaanza kukuhisi juu ya wewe kutokuwa mtu wake na swali la msingi linatakiwa kuwa kama ameshakutambua ni kwanini asitafute mtu mwingine wa kuweza kukaa kwenye nafasi yako? Hivyo kuna mawili kwamba anakujua wewe uhalisia wako kabisa au anakufanyia uchunguzi ili kuweza kujiridhisha”

“Kwahiyo ni kipi ambacho natakiwa kukifanya mheshimiwa”
“Wewe unatakiwa kuwa mtiifu kwake hata kama atakuwa ana mashaka sana na wewe, jifanye huelewi kile ambacho kinaendelea na hauhusiki kwa lolote lile”

“Sasa kama ameshanijua huoni kama anaweza kuniua muda wowote?”
“Kama amekujua na alitaka kukuua ungekufa muda mrefu tu, yule ni raisi hata kama kuna watu wengi sana wanamsaliti ila bado kuna watu ambao wanamtii vile vile na kama angetoa amri basi hakukuwa na namna ya wewe kukiepuka kifo. Kitu cha msingi sana kwa sasa sio kwamba anakujua au hakujui bado ila ni kwamba nani anakuchunguza wewe? Hilo ndilo jambo ambalo unatakiwa kulifanyia kazi haraka sana na kuweza kulidhibiti kwani inaweza kuja kutuletea shida sana kwa baadae na mambo yako mengi inabidi uyafanye kwa umakini mkubwa sana”

23 inafika mwisho.

Tchao.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 24
“Sawa kiongozi nimekuelewa”
“Utanipa ripoti nzima baada ya kila kitu kwenda sawa”
“Nimekuelewa mkuu” simu hiyo ilikatwa haraka sana baada ya mazungumzo kuweza kuisha.

Asubuhi na mapema sana Max alikuwa amewahi ofisini ili kwenda kupeleka ripoti kwa mkubwa wake wa kazi ambaye alikuwa ni raisi. Tangu jana yake asubuhi alikuwa amepotea na wakati huo ndio ambao alikuwa anarudi Ikulu.
“Nipe habari nzuri Max”
“Nimemaliza kazi bosi”

“Safi, kuna jambo lolote lingine au kuna changamoto yoyote?”
“Ndiyo bosi”
“Nakusikiliza”
“Wakati nafika ndani ya lile eneo sikukuta watu ambao kila siku huwa wanaenda kupata starehe pale zaidi ya walinzi ambao walikuwa wanalilinda jengo lile”
“How?”

“Inaonekana kwamba walikuwa wanajua kwamba kuna mtu anaweza kuvamia pale hivyo wakawa wameweka watu kwa ajili ya kuweza kumuua au kumkamata ndiyo maana hata kulifunga walilifunga kwa usiri mkubwa sana”
“Kwahiyo kipi kimetokea?”

“Nimekutana na wanaume sita ambapo nimewaua wote lakini mlinzi wa getini wakati naingia nilipambana naye na kumkata mguu kisha nikamtaka anipe sababu ya kukosekana kwa watu pale lakini ni mtu ambaye alionekana kunisikitikia sana na kusema kwamba nilikuwa na nafasi ndogo sana ya kutoka pale nikiwa salama kabisa nikashangaa sana”

“Ndipo akaniambia kwamba walikuwepo wanaume hatari sana ndani ya lile eneo kitu ambacho kilikuwa cha kweli lakini nilimhakikishia kwamba pale hakuna ambaye angetoka akiwa mzima na hapo akanipa stori ya maisha yake kwamba hakuwa pale kwa kupenda bali mtu huyo alikuwa anamlazimisha kufanya kazi hizo za hatari. Nikataka kujua kwa ufupi kwamba shida nini? Ndipo akasema kwanza niahidi kumlinda mdogo wake asije kuuawa ndipo atakuwa tayari kuniambia sababu na mambo ambayo alionekana kuyajua” raisi alizidisha umakini na kumsogelea mwanaume huyo ili amuelewe vizuri.

“Baada ya mimi kuahidi kumsaidia akawa amenipa majina mawili ya watu ambao wapo karibu sana na mheshimiwa Denis Kijazo ambao ndiyo kama mkono wake wa kulia” mwanaume aliongea akiwa anazidi kumsogelea mheshimiwa akionyesha kabisa kwamba taarifa hizo hazikutakiwa kufika sehemu nyingine zaidi ya hapo ambapo walikuwepo wao.
“Nani na nani?”

“Madilu mpagazi na Msafiri Kigoti ambaye ni gavana wa benki kuu. Hawa ndio watu ambao wana ushirika mkubwa sana na Denis Kijazo na ndio ambao huwa wanampa kiburi kufanya jambo lolote lile akijua wapo kwa ajili yake” mheshimiwa alichoka, hao mmoja alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana ndani ya nchi lakini mwingine alikuwa ni kiongozi mkuu wa benki ya taifa.

“How?” aliuliza akiwa kama bado haamini ukweli juu ya maelezo hayo.
“Kuna lingine tena mheshimiwa”
“Whaaaaat?”
“Unamkumbuka Laurent Mande?”
“Unamzungumzia gavana ambaye alipoteza maisha?”
“Yupo hai”
“No”

“Ndiyo mheshimiwa, mtu huyo amenihakikishia kwamba amefichwa kwa taarifa zinavyodai japo hata yeye hajui ni wapi kwa eneo husika”
“Umemwamini huyo mtu”
“Ndiyo mkuu”
“Why”

“Ni komando wa zamani wa nchi hii. Ameomba mwenyewe kuniambia ukweli kwa sababu hakutaka kufa kama msaliti wa nchi lakini pia alikuwa anataka kumlinda dada yake hivyo kama angedanganya alikuwa anajua madhara ambayo yangefuatia baada ya pale ndiyo maana nina uhakika kwamba alikuwa ananiambia ni ukweli” mheshimiwa alikaa kwenye sofa kwanza maana mambo ambayo alikuwa anaambiwa yalikuwa yanakizidi kichwa chake uwezo na alihisi kabisa kwamba kichwa chake huenda kingepasuka bure wakati huo.

“Amekwambia ni sababu gani ambayo ilimfanya yeye kuifanya hiyo kazi kwa ajili ya kumlinda dada yake?”
“Ndiyo, Denisi Kijazo mara nyingi ni mtu ambaye anatumia udhaifu wa mtu ili kumuendesha. Licha ya mwanaume huyo ambaye jina lake ni Siza kumficha sana ndugu yake na kuamua kumuacha aishi maisha ya upweke kama hakuwa na ndugu lakini watu hao walikuwa na taarifa kwamba anaye ndugu ila hawajawahi kujua kwamba huyo ndugu yake yuko wapi na anafanya nini hivyo wakati anamshawishi kijana huyo kufanya kazi kwake alipewa sharti kwamba kama akikubali kufanya kazi na watu hao basi hawatakuwa na haja hata ya kumtafuta mdogo wake aliko ila kama akigoma basi lazima wangemtafuta na anajua kabisa wangempata tu. Hivyo kwa ajili ya kulinda maisha ya mdogo wake akaikubali hiyo kazi”

“Hata ungekuwa wewe ungefanya hivyo Max?”
“Ndiyo bosi, familia ndicho kitu bora zaidi hapa duniani hivyo ukiwa na familia tena ndogo unakuwa tayari kufanya jambo lolote ili kuilinda” maneno hayo yalikuwa mazito sana na yalimkumbusha raisi mbali sana kipindi akiwa na mimba huko Kyela huenda naye angekuwa na familia ila kwa bahati mbaya sana mimba iliharibika hivyo hakutaka kuendelea kuongelea habari hizo.

“Kila mtu ni msaliti kwangu, nifanye nini Max. niwaue wote hao ambao umenitajia?”
“Hapana mheshimiwa, hawa tunaweza kuwatumia kwa faida nyingi sana hapo baadae”
“Are you sure about this Max?”
“Ndiyo bosi, hatutakiwi kukurupuka, tunatakiwa kuwa watulivu sana kwa sababu kukurupuka kwetu tutakuwa tunawapa ushindi wa mezani kirahisi sana. Tunatakiwa kujifanya kama tunaucheza mziki wao huku tukiwa tunamalizana na mmoja mmoja na siku ambayo watakuja kushtuka watakuwa wamechelewa sana”

“Nakutegemea sana katika fanya kila namna kuhakikisha tunaenda kuyamaliza mambo haya kabla hayajafika sehemu mbaya zaidi ya hapa”
“Sawa bosi”
“Huyu mtu ambaye ulisema kwamba utamlinda mdogo wake, una uhakika kweli unataka kulifanya jambo hilo?”

“Ndiyo mheshimiwa”
“Huyo mwanamke unamfahamu?”
“Hapana, ila amenipa maelekezo yote namna ya kuweza kumpata”
“Ukimpata utanikutanisha naye”
“Sawa mheshimiwa”

“Unaweza kwenda” hakutaka kuendelea kusikia mambo mengine, kwa siku hiyo aliamini aliyo yapata yalitosha huku akiwa ana uhakika kwamba hiyo ndiyo taarifa pekee ambayo kijana wake alitakiwa kumpatia lakini Max alijikohoza tena kidogo na kuuinua uso wake kwa mara nyingine.

“Kuna jambo lingine mheshimiwa” raisi aliinua uso wake vizuri na kujiweka kwenye mkao wa kuyapokea mambo mengine hayo.
“Wakati nimemaliza kazi nahitaji kuondoka lile eneo kuna watu wengine waliingia ambao walikuwa watatu”
“Unawafahamu?”
“Hapana, ila hawakuwa pale kwa sababu yangu”
“Kwanini?”
“Wanaonekana ni watu tofauti kabisa, kwa kuwatazama tu nao ni wauaji hatari sana kwa namna macho yao yanavyo angalia kwa haraka sana lakini hata wao wameonekana kwamba walikuwa wameenda kuifanya kazi ambayo mimi nimeifanya”

“Umewaua?”
“Hapana muda ulikuwa umeisha kwa sababu wakati naingia pale nilitega bomu hivyo kama ningeendelea kukaa pale lazima tungekufa wote hivyo nilitafuta upenyo nikakimbia”
“Wao wamebaki ndani?”

“Hapana hata wao wamefanikiwa kutoka eneo lile salama maana baada ya kutoka nilienda kukaa sehemu na kuangalia jengo lile likidondoka ila wao walikuwa wametoka na kutoweka na gari yao pale” mheshimiwa raisi alihema kwa nguvu sana huku tabasamu likionekana kwa mbali kwenye uso wake.
“Mheshimiwa unawafahamu?”
“Hapana Max ila asante sana kwa kazi nzuri, unaweza kwenda nadhani nikikuhitaji nitakuita tena”
“Sawa mheshimiwa” alijibu na kutoa heshima kwa kiongozi wake kisha akatoka ndani ya ofisi kuu ya raisi.

24 inafika mwisho.
Tchao.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 25
Mwanaume huyo wakati anatoka alikutana na Dax ambaye alikuwa anamshangaa sana mwenzake, alimvuta na kwenda naye mpaka nje sehemu ambayo haikuwa na kamera na zilikuwa zinawashwa kwa muda maalumu tu sehemu hiyo kwa sababu ilikuwa kwa ajili ya kufanyia mawasiliano hasa ya simu kwa wale watu ambao walitaka uhuru wa maongezi hasa wanapokuwa wanaongea na wenzi wao.

“Ulikuwa wapi jana?”
“Kwanini unaniuliza swali kama hilo?”
“Kwa sababu mheshimiwa alinipa kazi ya kukutafuta na kukupeleka kwake maana jana alikuwa anakuhitaji sana”

“Nilipewa majukumu mengine na mheshimiwa raisi”
“Mjukumu mengine ndiyo yalikufanya upotee siku nzima?”
“Mbona una wasiwasi sana kuhusu mimi? Unaweza kwenda kumuuliza raisi mwenyewe kama unataka kujua kwamba alinipa majukumu yapi maana una wasiwasi utadhani kuna kitu nimekuibia ndugu yangu”

“Mkurugenzi anakuhitaji na yupo nje ya Ikulu anakusubiri”
“Huu ni muda wa kazi unahisi naweza kutoka saivi?”
“Mimi nitabaki kwenye nafasi yako kafanye naye mazungumzo kisha utarudi maana itakuwa ni hatari sana kwa kazi yako kama akijua umegoma kuwasiliana naye” Max alimwangalia sana kwa umakini mwenzake huyo maana aliambiwa kabisa kwamba awe naye makini sana kwa sababu huyo alikuwa ni nyoka.

Mkurugenzi wa shirika la kijasusi alikuwa ametulia kwenye gari yake akiwa anamsubiria kijana wake huyo aweze kufika nje ya Ikulu, mwanaume alikuwa kwenye suti yake taratibu akiwa anaelekea sehemu ambapo ilikuwepo gari hiyo kisha akaimgia ndani.
“Heshima yako kiongozi”
“Ulikuwa wapi siku ya jana?”

“Nilikuwa kwenye majukumu ambayo nilipewa na mheshimiwa raisi”
“Majukumu yapi?”
“Ni jambo ambalo alihitaji liwe kati yangu mimi na yeye hivyo siwezi kukwambia kiongozi”

“Leo umeanza kufanya mambo yako ya siri kwa kunizunguka mimi halafu unaniambia kirahisi sana kwamba huwezi kunipatia taarifa zako?”

“Hakuna jambo ambalo nakuficha kiongozi ila hili nafanya kwa ajili ya kiongozi wetu wa nchi”
“Unajua hilo ni kosa kubwa sana ambalo linaweza kukuleta matatizo makubwa sana?”
“Ndiyo kiongozi najua”
“Kwahiyo upo tayari kuyabeba matokeao yake?”

“Ndiyo kiogozi” mzee huyo alichukia sana maana kijana wake alionyesha wazi kabisa kwamba hakuwa tayari kuweza kumpatia taarifa ambazo yeye alikuwa anazitaka kutoka kwake wakati huo,
“Ni wewe ulilipua lile jengo siku ya jana?”

“Hapana kiongozi, nimeona tu kwenye vyombo vya habari wala sijui ni nani aliyekuwa amehusika”
“Jana umepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, unarudi jengo hilo limelipuliwa halafu leo unasema kwamba haujui chochote kuhusu tukio hilo?”
“Ndiyo kiongozi”

“N kwanini raisi hajaniita juu ya jambo hilo ambalo limetokea? Hilo ni jambo ambalo linahatarisha amani ya nchi, hilo ni jambo ambalo linapaswa kujibiwa kwa wananchi sasa kivipi raisi asionyeshe hata mshtuko wa juu ya kile ambacho kimefanyika? Tukio limefanyika usiku mpaka sasa hakuna taarifa yoyote huku akiwa amezuia hata jeshi la polisi kutoa taarifa yoyote ile na hakuna mtu ambaye amemtafuta kuhitaji majibu yote. Unaweza ukaniambia kwamba raisi ana ajenda gani?”

“Sina ambalo nalifahamu kiongozi, kwa nafasi yangu sidhani kama mimi ni mtu ambaye raisi anaweza kunishirikisha mambo makubwa sana kama hayo ila hiyo ni nafasi yako wewe kuweza kushughulikia mambo kama hayo”
“Max are you playing me?”
“No, sir.”
“Who are you”

“You have all my details sir” mzee huyo alibaki anamwangalia kwa hasira sana kijana huyo.
“Kuanzia sasa nakusimamisha kazi mpoka nitakapokupatia taarifa nyingine tena ya wewe kurejeshwa kazini” aliongea akiwa anamtaka kijana wake atoke haraka sana.

“Yes, sir” Max hata hakushtuka wala kuuliza jambo lolote lile zaidi ya kutoa heshima na kushuka ndani ya gari ili kuelekea ndani kuripoti kisha kubeba kila kilicho chake ili aweze kutoka maana alikuwa amesimamishwa kazi.

“Kwanini namwachisha kazi hata hashtuki wala kuhoji sababu ya msingi ya mimi kumsimamisha kazi? Lazima kuna jambo la hatari linaendelea hapa katikati baina ya huyu bwana mdogo na raisi hivyo mpango wangu unatakiwa kuanza leo leo bila kupoteza muda, hili jambo linaelekea pabaya sana na sio muda nisipo angalia naweza kujikuta kwenye nafasi mbaya sana maana naona kama huu ni mchezo wa kuweza kuviziana” mkurugenzi huyo alihisi mawazo yake yalikuwa sahihi kabisa kwani haikuwa kawaida mtu anaachishwa kazi kwa kosa dogo kama hilo ambalo hakulifanya makusudi alikuwa kwenye majukumu makubwa ya raisi na anakubali bila hata kuhoji, nafsi yake haikukubaliana kabisa na hilo jambo. Aliitoa simu yake mfukoni na kumpigia Dax

“Njoo haraka sana” mwanaume huyo alitoka haraka kwenda mpaka nje ambako mkurugenzi huyo alikuwa amekaa ndani ya gari.
“Umegundua chochote?”
“Ndiyo kiongozi”
“Nambie”

“Ni yeye ambaye amelipua lile jengo na kuwaua wale walinzi ambao walikuwa kule”
“Una uhakika?”
“Ndiyo kiongozi wakati wanafanya mazungumzo nilikuwa mlangoni nawasikiliza mazungumzo yao”
“Yapi?”
“Alikuwa anamueleza raisi kwamba alifanikiwa kufika kule ambapo aliwaua watu wote ambao aliwakuta lakini hata yeye alionekana kushangazwa sana kwani watu wote hawakuwepo zaidi tu ya walinzi. Kwa maelezo yake ni kwamba alikutana na walinzi sita ambao aliwaua wote na kulidondosha jengo hilo lakini kati ya hao walinzi kuna mlinzi mmoja alimuomba kitu kwa ahadi ya kumpatia siri ambazo alikuwa nazo”
“Enhe ni kitu gani hicho?”
“Mtu huyo anadai kwamba alikuwa na mdogo wake ambaye alikuwa anamtaka Max aweze kumlinda”
“Whaaat?”
“Ndiyo na mtu huyo alimuomba hilo kwa kumpa siri ambazo nimeshindwa kabisa kuzisikia ila yanaonekana ni mambo nyeti sana ambayo walikuwa wanazungumza wakati ule maana alionekana kunong’ona kwa sauti ya chini kiasi kwamba hata kinasa sauti changu ambacho nilikiweka pale chini kwenye tundu dogo la hewa mlangoni kilishindwa kabisa kunasa”

“Oooh shit kuna mipango ya siri sana lazima wameipanga wapuuzi hawa, nahitaji hii kazi uifanye haraka sana tena kwa weledi mkubwa mno. Fuatilia kwa umakini ujue wanaongea nini, kuhusu nani na ni watu gani ambao wapo nyuma ya hili, maana huenda tunachelewa kukielewa chungu ambacho kitatumika kuja kutupika weneywe”

“Nimekuelewa mkuu”
“Kuna kitu kingine unataka kuniambia?”
“Ndiyo mkuu”
“Nakusikiliza”

“Kwenye moja ya kauli zake ambazo sina uhakika ndiyo maana sijakwambia moja kwa moja ila ni kama alisema kwamba yule mlinzi ambaye alimuomba amlindie mdogo wake alimpa taarifa kwamba kuna watu wa karibu sana wa bosi ambao alikuwa anawajua na aliamini kwamba wangemsaidia Max ndipo akampa sharti la kumlinda dada yake kwanza”
“Mbona hujanambia kuhusu hili?”

“Sina uhakika sana na nilicho kisikia maana ilikuwa kwa mbali mno wakati anazidi kusogea mbali sana na mlango ndiyo maana sikutaka kukupa taarifa nusu nusu”
“Unajua ni nani na nani?”
“Hapana mheshimiwa”
“Huyu mtoto anajikuta nani hasa? Dax usije ukanifelisha katika hili maana nitakufanyia kitu kibaya sana, nahitaji ufanye kazi kwa umakini sana na kujua kila ambacho kinaendelea hapa Ikulu na kwa huyu kijana Max”

“Sawa bosi”
“Unaweza kwenda” mheshimiwa alimaliza maongezi hayo akiwa anamwangalia sana kijana wake huyo akiwa anaishia, ishara mbaya sana zilianza kujitokeza mapema na kilichokuwa kinahitajika ni umakini wa hali ya juu sana vinginevyo yangewakuta mambo mabaya sana. Aliliondoa gari lake kwa kasi sana akiwa anaendesha mwenyewe akionekana kabisa kwamba kuna mahali alikuwa anawahi wakati huo pia aliona kuna umuhimu wa kumtaarifu Denis Kijazo juu ya taarifa hizo ili kama anaweza afanye jambo.

25 inafika mwisho.

Tchao
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 26
BRANDINA.
Historia ya maisha ya Brandina inaanzia huko ndani ya visiwa vya Ukerewe, sehemu ambako ndiko alizaliwa na alikuwa anaweza kupaita nyumbani. Brandina hakubahatika kuwa na baba zaidi ya mama ambaye alikuwa anauza chakula pembezoni mwa ziwa ili aweze kuyaendesha maisha yake pamoja na mwanae wa pekee ambaye ndiye alikuwa Brandina mwenyewe.

Brandina licha ya kuzaliwa ndani ya ardhi ya Tanzania lakini mama yake mzazi hakuwa mtanzania kama yeye bali yeye alikuwa ni raia kutoka ndani ya nchi ya Ethiopia. Mhebeshi huyo ambaye alikuwa mrembo sana wa kuvutia kwa rangi lakini pia hata umbo lake lilisadiki hilo alifanikiwa kuingia ndani ya nchi ya Tanzania kupitia shirika la wakimbizi na baada ya kufika hakuwahi kufikiria kuja kuondoka tena mpaka pale yalipokuja kumkuta mazito ambayo hakuwahi kuyafikiria kabla.

Mama yake Brandina alikuwa ni mwanamke ambaye alizaliwa kwenye familia yenye ukwasi mkubwa sana wa pesa na kumfanya kuishi maisha mazuri sana kwani ndiye alikuwa mtoto wa kipekee kwenye familia hali ambayo ilimfanya kupata elimu iliyokuwa bora sana utotoni kwake lakini mambo yalikuja kuharibika baada ya wazazi wake kuweza kufariki. Wazazi wake walikufa kwenye ajali ya gari ambayo baadae zilikuja kusambaa habari kwamba ilikuwa imetengenezwa na watu ambao walidaiwa kuwa ndugu wa karibu wa mzee huyo ili waweze kurithi mali zake.

Tukio hilo lilitokea mtoto wao akiwa shule na wakati anarudi nyumbani alikutana na msiba huo ambao ulimfanya kuzimia lakini kuzimia kwake haikuwa sababu ya kuukataa ukweli ambao ulikuwa mbele yake. Baada ya msiba kuweza kutokea ndugu zake walitishia kumuua na kumpa nafasi akimbie na asije kufuatilia mali hizo maana wasingeweza kumuacha akiwa hai zaidi ya kumuua huku wakidai kwamba wao ndio walikuwa ndugu halali wa baba yake hivyo mali zilikuwa zao na huo ukawa mwanzo wake wa kuweza kuishi maisha magumu sana mtaani akikosa msaada.

Baada ya maisha yake kuwa magumu sana aliamua kujiunga na shirika la wakimbizi ambako alikuja kusikia habari nzuri za kuvutia kuhusu nchi ya Tanzania kwa jinsi ilivyo na amani pamoja na ukarimu wa watu wake hivyo kupitia shirika hilo alifanikiwa kupata nafasi ya kuweza kuitembelea nchi ya Tanzania ambako aliamini kwamba anaweza kuyaanza maisha mapya huku akiendelea kujifunza lugha adhimu kabisa ya Kiswahili.

Baada ya kufika ndani ya ardhi ya watu wa amani aliishi kwa muda mrefu na kuizoea hali ya nchi huku maisha yake yakiwa ni ya kubangaiza ambapo alijituma sana kufanya kazi lakini alikuwa anakatishwa ndoto zake kwa kukutana na wanaume mafisi ambao walikuwa wanampa kazi lakini baadae wanaanza kumtamani kimapenzi kitu ambacho hakuwa tayari na siku moja alifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni moja kubwa sana kuwa kama katibu wa bosi wa kampuni hiyo.

Bosi wa kampuni hiyo alionyesha kabisa nia ya kumtaka mwanamke huyo kwa namna alivyokuwa mrembo sana lakini hakuna kitu ambacho alifanikiwa kukibadilisha kwenye kichwa cha huyo mrembo ambaye mapenzi hayakuwa jambo la mhimu sana kwake maana alikuwa anajua kile ambacho kilitokea kwenye maisha yake huko nyuma hivyo alitakiwa kupigana sana kuhakikisha anayaweka mazingira kwenye hali ya usawa kwanza kabla ya mambo yote.

Siku moja akiwa kwenye dawati lake anabonyeza komputa yake, alihisi kama kuna mtu alikuwa amesimama mbele yake tena mtu huyo alionekana kusimama kwa muda kidogo. Alishtuka na kujichekesha huku akimkarimu mgeni kwa kumkaribisha maana alionyesha uzembe mkubwa sana kazini lakini mwanaume huyo mrefu maji ya kunde ambaye alikuwa mbele yake hakuonyesha hasira zaidi ya tabasamu ambalo lilikuwa kwenye uso wake huku akiwa ndani ya suti.

Mwanaume huyo alijitambulisha kama Elkana na alikuwa hapo kwa ajili ya kuripoti kazini hivyo alitakiwa kuonana na bosi moja kwa moja. Haikuwa shida sana mwanamke huyo alimtaka huyo bwana aweze kuandika jina lake kwenye daftari ambalo lilikuwa hapo pamoja na mawasiliano yake ili iwe rahisi kwenye marejeo na mwanaume huyo alifanya hivyo ambapo baada ya muda mfupi alitoka ndani ya ofisi hiyo na kuaga kisha akapotelea kwenye malango ya gharama sana ambayo yalikuwa ofisini pale.

Baadae wakati mrembo huyo anajiandaa kuondoka aligundua kwamba kuna picha ilikuwa ipo chini, alivyo jaribu kuiangalia, ilikuwa ni ya mwanamke wa makamo na nyuma ilindikwa my mom kisha kukawa na kopa la upendo. Alitabsamu akiwa anaiangalia picha hiyo ambayo ilizizoa hisia zake na kumpeleka mbali sana miaka hiyo akiwa na mama yake mzazi mpaka alijikuta machozi yanaanza kumtoka.

Aliichukua namba ya mwanaume huyo kwenye daftari ya marejeo kisha akampigia simu ili kujua alipo akimpa maelekezo ya kwamba alikuwa na mzigo wake na kama ingempendeza amuelekeze alipo ili aweze kumpelekea na mwanaume huyo hakuwa na shida alifanya hivyo na huo ndio ukawa mwanzo wa penzi ambalo lilihalalisha kupatikana kwa Brandina.

Aliyesema kwamba penzi ni kama kikohozi hakuwahi kukosea, waungwana hao wawili walianza kukohoa hadharani kiasi kwamba penzi lao lilikuwa maarufu sana kila sehemu, kila mtu alijua kuhusu wao na hata kazini kila mtu alilitambua na kuwafurahia sana isipokuwa mtu mmoja tu ndiye hakulifurahia kabisa jambo hilo. Bosi wa kampuni hiyo alichukizwa sana kwa sababu mwanamke huyo alikuwa anampa ahadi tu halafu kirahisi anakuja kumfuata mfanyakazi wake na kumkubalia tena kutangazana hadharani? Hakukubali hilo jambo ukawa mwanzo wake wa kumfuata mwanamke huyo na kumtisha.

Aliambiwa kwamba kama akiendelea kumkataa bosi huyo basi mwanaume wake angepoteza kazi lakini pia angeweza kuuawa ili amkose aone namna inavyouma kumkosa mtu ambaye nafsi inakuwa inamhitaji. Kwa kuogopa kumpoteza mpenzi wa maisha yake aliamua kukubali kufanya jambo la hatari ambapo alimkubalia pia bosi huyo na ukawa mwanzo wa yeye kuwachanganya wanaume wawili kitu ambacho hakuwahi kukifikiria kwenye maisha yake yote ila asili ilimuamulia nini cha kufanya na namna ya kuishi na hakuwa na namna zaidi ya kulipokea hilo kwa mikono miwili.

Aliamua kumzawadia mpenzi wake bikra yake kisha ndipo akaanza kuchepuka ambapo alikuwa anawachanganya wanaume hao wawili kwa nyakati tofauti. Walipendana sana na Elkana kiasi kwamba waliamua kuambizana ukweli wa maisha yao ya nyuma huko ambapo Elkana alimwambia mwanamke huyo kwamba yeye alikuwa ni mzaliwa wa kanda ya ziwa huko na muda wake mwingi aliutumia ndani ya taifa la Ujerumani kuweza kusoma ila kwa bahati mbaya sana akiwa huko familia yake ilipata ajali kwenye meli wakiwa wanasafiri wote kwenda kwenye mapumziko hali ambayo ilifanya kubaki pekeyake bila mtu wa kumuangalia na baada ya kumpata mwanamke huyo alihisi kwamba amepata familia.

Maneno yalimuuma sana mwanamke huyo na kujihisi hatia kubwa sana kwa mwanaume huyo kwani kumsaliti aliona kabisa hamtendei haki hivyo aliamua kumwambia ukweli kuhusu yeye na bosi wake kitu ambacho alihisi kingeweza kusaidia bila kujua kwamba alikuwa anatengeneza majonzi mengine kwenye maisha yake. Mwnaume huyo alichukia sana baada ya kutambua kwamba bosi wake anaitumia nafasi yake kuweza kumvua nguo mwanamke ambaye alimpenda sana na kumheshimu kama mkewe ajae.

Kama ilivyo kawaida ya watu wa kanda ya ziwa hawakuwa wakitaka kufanyiwa dharau za kitoto kama hizo hivyo mwanaume huyo alibeba panga ili akamkate kate bosi wake kwenye ofisi yake lakini kwa bahati mbaya sana wakati anafika kwenye ofisi hiyo bosi wake alimuwahi na bastola na kumpiga risasi hali ambayo ilimfanya mwanamke huyo kushtuka sana maana dawati lake halikuwa mbali na ofisi hiyo hivyo alikimbilia humo ndani kuweza kujua nini kilikuwa kimetokea lakini baada ya kufika alichoka kwa kile ambacho alikiona.

Mwanaume ambaye yeye alimpenda sana na kumuona kama mumewe alikuwa amelala chini kwenye dimbwi la damu nafsi ikiwa imeacha mwili. Alilia sana na kuhisi alifanya ujinga sana kuweza kumwambia ukweli bora hilo jambo angelimaliza kwa namna nyingine ila kwa bahati mbaya sana majuto yaligeuka kuwa mjukuu kwake maana hakuwa na kitu cha kuweza kukibadilisha kwa wakati huo. Mwanaumke huyo akiwa kwenye hasira alimuona bosi wake akiwa anacheka kwa furaha sana akijinadi kwamba ilikuwa nafasi yao kuweza kuyafurahia mapenzi ila mwanamke huyo aliahidi kwamba ni lazima angehakikisha kwamba anamfunga.

Aliifikisha kesi mahakamani lakini hakuna aliye msikiliza, watu wenye pesa walikuwa wameiweka mahakama kwenye mifuko yao walidanganya kwamba mwanaume huyo alikuwa ni kibaka tu ambaye alikuwa anataka kumuua bosi wake baada ya kufukuzwa kazi kwa tabia zake mbaya zisizo vumilika ambazo alionywa mara kadhaa na hakusikia hivyo bosi huyo kumuua alikuwa anajilinda tu mwenywe. Mwanamke huyo aliumia sana na kuapa kwamba angelipa kisasi hivyo akamkubali bosi wake na kudai kwamba ameshamsahau mwanaume wake kitu ambacho kilimpa bosi huyo kiburi na furaha kubwa sana lakini hakujua mwenzake alikuwa ana lengo gani.

Siku moja wakiwa kitandani wanayafurahia mapenzi, alimtaka bosi huyo ayafumbe macho kuna zawadi alitaka kumpa, naye bila kuwaza lifanya hivyo bila kujua lengo la mwanamke huyo. mrembo huyo alichomoa kisu kikali sana chini ya kitanda na kukilengesha sehemu ya moyo ya mwanaume huyo na wakati anamwambia kwamba afumbue macho yake alikizamisha kisu sehemu hiyo ambapo mwanaume huyo hakuchukua muda mrefu akawa amepoteza maisha na huo ukawa mwanzo wake wa kutafutwa sana na ndugu wa bosi huyo wakiahidi kama wangemkamata mwanamke huyo basi wangemfanyia kitu kibaya sana na ndio ukawa mwanzo wake wa kuishi mafichoni.

Kwenye kujihami na kesi hiyo mwanamke huyo alianza kuishi kwa kujificha sana lakini kwa bahati mbaya sana ndugu wa bosi wake wa kiume waliweza kumpata, baada ya kumpata hawakumpeleka polisi bali walienda kumfungia sehemu na kuanza kumbaka, walikuwa wanambaka zamu kwa zamu kulingana na namna alivyokuwa mwanamke mrembo sana hali ambayo ilimuacha kwenye sonona kubwa mno mwanamke huyo.

Wakati anapitia mambo yote hayo hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba alikuwa mjamzito, alikuwa na mimba ambayo ilikuwa ya mwanaume wake ambaye alimpenda sana. Baada ya kufanyiwa ukatili kwa siku kadhaa mwanamke huyo alifanikiwa kutoroka na baada ya kufanikisha hilo alihitaji kwenda sehemu ambayo hakuna mtu anamfahamu, alihitaji kwenda mbali sana kujificha kwani nchi ambayo aliahidiwa kwamba ilikuwa na utajiri mkubwa sana wa amani ndiyo ambayo ilikuwa inamuadhibu kwa wakati huo.

Akiwa na mwanaume wake ambaye alikuwa anatokea kanda ya ziwa, aliwahi kuzisikia hadithi nyingi sana mbaya na za kuvutia kuhusu huko, aliwahi kusikia namna watu wanavyo yaendesha maisha yao lakini pia jinsi watu wanavyo ishi kwa kuzitumia nguvu zao. Kati ya hadithi zote ambazo alizisikia hadithi ya kisiwa cha Ukerewe ndiyo ambayo ilimvutia zaidi hivyo akaona sehemu hiyo itamfaa sana yeye kuweza kuanzisha makazi yake mpya huko na ndio ukawa mwanzo wake wa kwenda kukaa huko kwa mara ya kwanza kabisa kwenye maisha yake.

26 inafika mwisho.

Tchao.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 27
Alifika huko akiwa hajui kwamba angeenda kufanya nini, alianza kufanya kazi ya kukaanga samaki na kuuza chakula huku uzuri wake ndio ukiwa mdhamana wake mkubwa wa kupata mtaji kutoka kwa wanaume mafisi ambao walikuwa wanavua samaki. Baadae alibahatika kufungua kimgahawa chake kidogo na haukupita muda sana akawa amejifungua mtoto wa kike ambaye jina lake alimuita Brandina na baba yake jina lake alikuwa anaitwa Elkana hivyo akaamua kumpatia jina halisi kabisa la baba yake.

Maisha kwake hayakuwa mazuri sana wala mabaya sana lakini alimshukuru Mungu kwani alifanikiwa kumlea vizuri sana mwanae huyo mpaka binti yake alipo anza kujitambua wote wakiwa wanasaidiana kazi ya mgahawa pale ambapo mwanae angetoka shule ambayo alikuwa anasoma. Mwanamama huyo alianza kuumwa na hali yake haikuwa nzuri kwa sababu kasi ya ugonjwa ambao alikuwa nao ulionekana kuwa na nguvu kulizidi tumaini ambalo alikuwa nalo na hakuchukua siku nyingi sana akawa amepoteza maisha huku akiwa amemwachia mwanae diary yake ambayo ilikuwa na taarifa zote za maisha yake.

Taarifa zilikuwa zinaelezea uhalisia wa maisha ambayo mama yake aliyaishi, maisha ambayo alikutana nayo wakati anaendelea wa kuishi lakini vitu vya kutisha ambavyo alifanyiwa akiwa anaishi mpaka siku anakufa. Brandina alidondosha chozi kwa huruma kubwa sana kwa sababu alihisi kwamba mama yake alikufa tu hivi hivi lakini aligundua kwamba mama yake alikufa kwa homa ya ini, homa ambayo aliandika kwamba aliambukizwa na wale watu ambao walimbaka ambao walikuwa ndugu wa yule bosi wake.

Mama yake alimsisitiza mwanae kwamba baba yake mzazi aliuawa na wanafamilia hao, mama yake alimkumbusha kwamba hiyo ndiyo familia ambayo ilimfanya yeye aishi maisha magumu sana kwani kama sio hao basi angezaliwa kwenye maisha ambayo yalikuwa mazuri lakini alimtaka mwanae asije kusahau kwamba wanafamilia hao ndio ambao walifanya mama yake mzazi kuweza kupoteza maisha hivyo lilikuwa ni jukumu lake na uamuzi wake kama alikuwa anahitaji kuwasamehe au asiwasamehe.

Brandina wakati anaisoma hiyo diary alikuwa ni binti ambaye alikuwa anakua kwa kasi sana, binti ambaye aliichukua sura na rangi ya mama yake ambayo ilimfanya kuwa mwanamke mrembo sana zaidi hata ya mama yake mzazi. Uzuri wake ulifanya akawa kivutio kikubwa sana kwa watu ambao walikuwa wanaenda kisiwani hapo, urembo wake ulikuwa habari ambayo ilikuwa inaenea mithili ya upepo uvumao kwa nguvu. Mgahawa wake ambao aliachiwa na mama yake ulizidi kupata wateja wengi kila siku huku kila mtu akiwa anatamani sana kuweza kuhudumiwa na mwanamke huyo ambaye alikuwa akitabasamu watu wengi walikuwa wanafurahia sana kuwa karibu naye.

Licha ya kuwa kwenye hali ambayo ilifanya biashara yake kuweza kukua kila siku, tangu alipo isoma diary ya mama yake, moyoni mwake alishindwa kabisa kupata amani, alishindwa kabisa kufanya maamuzi ya kuweza kuwasamehe watu wale ambao walimletea maumivu makali sana namna hiyo hivyo akajikuta anapatwa na kasi kubwa sana ya kisasi ndani yake, alitamani kuweza kuwaadhibu watu hao kwa namna ambayo angeona kwamba ingemfaa yeye ili wazazi wake waweze kupumzika kwa amani. Sasa angeweza vipi kuwalipizia watu hao ambao kwanza alisikia kwamba walikuwa wanaishi ndani ya jiji la Dar es salaam ambako hakuwahi kufika? Kichwani kwake alikuwa na wazo moja tu pekee ambalo aliona ndiyo itakuwa nafasi yake ya kuweza kulikamilisha hilo, wazo hilo lilikuwa ni kuweza kuutumia urembo wake, aliamini kwamba uzuri wake ungempatia kila alichokuwa anakihitaji kwenye maisha yake lakini alikuwa miongoni mwa wale wanawake wachache sana ambao walikuwa wanaamini kwamba nguvu ya mwanamke inapatikana katikati ya mapaja yake.

Akiwa anaendelea na biashara yake alimtafuta mwanamke mmoja ambaye alikuwa kungwi maarufu na mkubwa sana ambaye hakuna mwanafunzi wake hata mmoja aliwahi kuachika kwenye ndoa yake baada ya kupata mafunzo kwake. Alihitaji mwanamke huyo amfundishe namna nzuri ya kuweza kumkamata mwanaume yeyote yule, alihitaji kuwa gwiji wa mapenzi, alihitaji kuishika akili ya mwanaume yeyote yule kupitia zawadi ambayo ilikuwa katikati ya miguu yake. Ukawa mwanzo wake mzuri wa kujifunza kuhusu mapenzi.

Alijifunza kwa bidii sana kwa sababu hakuna kitu ambacho alikuwa anakijua kuhusu mapenzi na siku ya mwisho iliyokuwa inautimiza mwezi wa sita tangu aanze kufundishwa, alipewa mwanaume ambaye alikuwa kijana wa kungwi huyo kwa ajili ya kumfundisha mwanamke huyo kwa vitendo zaidi. Hiyo ndiyo ilikuwa siku yake ya kwanza kabisa kujihusisha na mapenzi, hakuyafaidi sana ila hakujutia kwani mwanaume huyo alikuwa fundi haswa na ilibaki kidogo tu aweze kumpenda ila moyo wake ulimuonya kwamba alikuwa anayafanya hayo kwa ajili ya kazi maalumu na sio kumpenda mtu. Mazoezi yalienda kwa wiki nzima mpaka pale alipofanikiwa kuiva kwa vitendo kabisa sasa akawa anawaza sehemu ambayo alitakiwa kuanzia kutimiza lile takwa lake ambalo alikuwa analitaka.

Ilikuwa ni siku ambayo ilidaiwa kwamba mkuu wa mkoa wa jiji la Mwanza alikuwa anatembelea kwenye kisiwa hicho akiwa na waziri wa uvuvi hivyo alifanya maandalizi makubwa sana kwenye mgahawa wake akiwa na imani kwamba kwa sababu huo ndio ulikuwa mgahawa maarufu zaidi ndani ya sehemu hiyo basi lazima wageni hao wangefikia hapo na hakutaka kufanya kosa lolote lile juu ya jambo hilo kwa sababu aliamini kwamba safari yake ya kulipa kisasi ilikuwa inaanzia siku hiyo.

Mchana wa jua kali kweli viongozi hao walipita ndani ya eneo hilo na kwa sababu wanasiasa walikuwa wanapenda sana mambo ya picha ili kuwadanganya raia wajinga jinsi wanavyo wajali raia wao, baada ya kufika kwenye mgahawa huo walianza kufanya hivyo na kumwaga sifa huku wasisitiza vijana kupiga kazi maana binti mdogo kama huyo alikuwa na biashara ambayo ilikuwa inafanya vizuri sana. Brandina alikuwa amevaa nguo za kuvutia sana na hesabu zake zilikuwa kwa mkuu wa mkoa ambaye jina lake alifahamika kama Philipo Tibaigana kwa sababu mwanaume huyo alizipata sifa zake kwa namna alivyokuwa anapenda wanawake hususani mabinti warembo hivyo akaamini kwamba akifanikiwa kumtia kwenye mkono wake huyo basi itakuwa ni hatua kubwa sana kwa upande wake.

Baada ya kumaliza shughuli zote ambazo ziliwapeleka huko kiongozi huyo alifanikiwa kuyapata mawasiliano ya mwanamke huyo ambaye naye alionekana kumhitaji, kwa urembo ambao alikuwa nao Brandina kiongozi huyo nafsi yake ilijiwekea nadhiri kwamba kama angemkosa mwanamke huyo basi hakuwa na maana yoyote ile kuwa hai au kuendelea kuishi ni bora angekufa tu.

Ukawa mwanzo mzuri wa hadithi ya mapenzi ya uongo kati ya watu hao wawili ambapo penzi lao lilishamiri sana mpaka siku moja ambapo Brandina aliamua kumuomba kiongozi huyo kama anaweza amsaidie kumuingiza ndani ya jeshi. Haikuwa kazi sana kwa sababu kabla ya kuwa mkuu wa mkoa aliwahi kuwa ruteni wa jeshi na ndiyo sababu kubwa ambayo ilimfanya Brandina kutaka kuwa naye karibu kwa sababu alikuwa ameipitia historia ya mtu huyo.

Penzi ambalo alikuwa anampatia kiongozi huyo lilimfanya asiwe na chaguo lingine zaidi ya kukubali kila kitu ambacho mwanamke huyo alikuwa anakitaka. Japo alitamani sana kuweza kujua sababu ya mwanamke huyo kutaka kwenda jeshi lakini jibu alilopewa ni kwamba aliacha shule baada ya mama yake kufariki na alikuwa anapenda sana jeshi hivyo nafasi hiyo aliona kama ilikuwa ya dhahabu sana kwake, basi akapata nafasi kiwepesi sana kuingia huko.

Safari yake ilikuwa nzuri hususani baada ya Philipo Tibaigana kuteuliwa kuwa waziri wa ulinzi, Brandina alizidi kupata nafasi kubwa sana huku akiwa kama mwanamke rasmi wa Philipo Tibaigana na baada ya muda mrefu kupita Philipo Tibaigana alifanikiwa kuipata nafasi ya kuwa mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania. Baada ya kuingia huko alifanikiwa kumchukua mrembo Brandina ambaye alikuwa ni moja kati ya wanajeshi hodari sana na kumfanya kuwa jasusi ndani shirika lake ili awe naye karibu zaidi.

Brandina baada ya kuona kwamba alikuwa na nafasi kubwa sana kwenye maisha yake na mali alikuwa nazo aliamua kuweza wazi ukweli wake kwa Philipo Tibaigana kwamba alifanya yale yote kwenye maisha yake ili kuweza kulipa kizazi kwa watu ambao walimuulia wazazi wake, alihitaji kuifuta ile familia kwenye uso wa dunia waungane na wazazi wake ambao aliamini kwamba walionewa na hawakustahili kuuawa bali kuishi. Mambo hayo yalimshtua sana mkurugenzi kwani lilikuwa ni jambo geni sana kwake lakini kwa mapenzi ambayo alikuwa nayo kwa mrembo huyo alimpa nafasi ya kufanya hilo tukio kwa msaada wa majasusi wengine na kisha angefuta ushahidi wote kwa sababu suala la usalama wa taifa lilikuwa lipo chini yake.

Mpango wa Brandina ulitimia kirahisi sana kwa sababu ya kuitumia fahari iliyopo katikati ya mapaja yake kama alivyokuwa anamini kwamba hapo ndipo ilipo nguvu ya kufanya jambo lolote duniani hata akitaka kuuendesha ulimwengu basi akiitumia sehemu hiyo vizuri kwake inakuwa kazi nyepesi sana. Baada ya kufanikisha hilo jambo kwa kuiua kikatili sana familia ile ambayo ilimfanya aishi kama yatima, Brandina hakuwa yule mwanamke tena ambaye alikuwa na roho ya huruma, hakuwa tena mwanamke ambaye alikuwa na roho ya kike bali kwa wakati huo alikuwa ni mwanamke mkatili sana, alikuwa ni mwanamke ambaye aliamini kwamba duniani anaweza kufanya jambo lolote lile na likafanikiwa.

Kilichokuwa kinampa jeuri kubwa ni kuwa karibu na mkurugenzi wa shirika la kijasusi huku akiamini kwamba hakuna mtu ambaye alikuwa anaweza kumgusa hivyo kwa wakati huo akawa ana hamu kubwa sana ya mafanikio makubwa, alitamani jina lake lije libaki kwenye kumbukumbu za maisha ya watu na lijulikane kila sehemu ili kuwaenzi wazazi wake. Akawa anatamani kupata nafasi kubwa ambapo aliahidiwa na Philipo Tibaigana kwamba siku moja angekuja kumuingiza mwanamke huyo kwenye siasa na kutokana na nguvu aliyokuwa nayo kwake lingekuwa suala dogo tu na miaka kadhaa huko mbele mwanamke huyo angejikuta kwenye vitengo vikubwa sana serikalini.

Kwa kumuonyesha mfano, Philipo yeye ndiye ambaye alimpenyeza na kufanikiwa kumuweka kwenye nafasi kubwa sana ya kuwa mlinzi mkuu wa raisi. Mwanamke huyo alifanikiwa kuipata nafasi hiyo kutoka kwa mwanaume ambaye alikuwa anamvulia nguo ikiwa ni kama malipo ya ufundi ambao alikuwa anampa kitandani.

Huyu ndiye Brandina ambaye kulipa kwake kisasi kulimfanya muda mwingi awe pembeni ya mtu mkubwa zaidi wa usalama ndani ya taifa la Tanzania, huyu ndiye Brandina ambaye moyo wake uliwaka moto na kuzihitaji nafasi kubwa sana akiamini kwamba siku moja jina lake litaimbwa kutoka kila sehemu na kila pande ya dunia. Huyu ndiye Brandina ambaye alitakiwa kutumika kukamilisha mpango wa Denis Kijazo wa kuweza kumteketeza mheshimiwa raisi wa taifa la Tanzania Teodensia Mpanzi na huyu ndiye Brandina ambaye ilikuwa ni karata ya mhimu sana kuusambaratisha umoja wa watu ambao walikuwa wapo kinyume na mwalimu wa mipango Denis Kijazo. Jina lake lilitakiwa kutumika vipi kuwamaliza na kukamilisha kazi zote hizo kwa wakati mmoja?

Usiku wa manane ilikuwa inasikika sauti ya mgugumio kitandani, sauti ya mwanaume ambaye alikuwa kwenye furaha kubwa sana ya kulifurahia penzi kuliko ilivyokuwa kwa mwanamke. Mwanamke hakuonekana kulifurahia sana penzi hilo bali kwa mwanaume ilikuwa ni tofauti sana maana alikuwa anahisi kama dunia yote ipo kwenye mkono wake. Kwenye hicho kitanda walikuwepo watu wawili Philipo Tibaigana na mrembo Brandina Elkana ambaye alikuwa ndiye mlinzi mkuu wa mheshimiwa raisi.

27 inafika mwisho.

Tchao.
 
Jibariki na hii PASAKA kwa 2000 tu nikupe mwendelezo kwa 2000 kwa leo tu.

0621567672 (WhatsApp).... HALO-PESA

0745982347.... M-PESA

0714581046.... TIGO-PESA

FEBIANI BABUYA
 
[emoji91][emoji91][emoji91]
 
We're waiting for 28,
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 28
“Leo rasmi ndiyo siku ambayo unatakiwa uanze kuifanya kazi ya kunisaliti” mheshimiwa aliongea akiwa anasimama na kuiwasha sigara yake na kuivuta kwa hisia sana kama mtu ambaye ameridhika vya kutosha na ngono zembe ambayo alikuwa anaifanya muda mfupi hapo

“Unahisi anaweza kuingia kwenye mtego kirahisi namna hii kwa sababu ya huku chini?” hakuongea jambo akamvamia mwanamke huyo na kufanya naye mapenzi kwa fujo sana kwa dakika kadhaa kisha akamrushia kitandani naye akakaa kwenye kiti akiwa anahema sana mwilini mwake akiwa uchi.

“Hakuna kitu duniani kina nguvu kama hiyo mali ambayo unayo katikati ya mapaja yako. Hiyo sehemu ndiyo ambayo imekufanya wewe kufika hapa leo, hiyo ndiyo imekufanikishia wewe ndoto zako na kuwa karibu na watu wakubwa kama mimi sasa unahisi kwamba ni kitu gani ambacho kinaweza kikakushinda kwa bwana mdogo kama yule ambaye anaonekana kabisa sio mtu wa wanawake? Yule akionja mara moja tu basi atakuwa mtumwa wako hivyo ukihitaji kujua jambo lolote kutoka kwake inakuwa ni rahisi sana kikubwa hakikisha anakuamini na asije akakuona na mwanaume mwingine yeyote yule kwa kipindi ambacho utakuwa naye na muigizie kama unampenda sana kiasi kwamba akija kushtuka awe ameshachelewa tayari” mwanamke huyo alitembea kwa maringo sana huku nyuma akitikisa maungo yake na kusogea kwenye kioo akiwa anajingalia namna alivyokuwa mrembo sana.

“Baada ya hili kukamilika unaniahidi nafasi gani?”
“Nitakupatia nafasi yoyote ile ambayo unaihitaji kwa sababu ukifanikiwa kujua kila kitu kwake basi utakuwa ni wakati ambao tutahitajika kumuua raisi na kijana huyo ndiye atapewa kesi kisha naye tutamuua”
“Whaaat?”

“Lazima afe akishabebeshwa kesi kwa sababu duniani hakuna kitu ambacho huwa kina siri ya muda mrefu labda mpaka mwenye hiyo siri anapokuwa hayupo milele ila vinginevyo litakuwa ni suala la muda tu hivyo ili kuhakikisha oparesheni yetu imeenda vizuri basi hatutakiwi kubakisha ushahidi wowote ule”

“Hapana hii sio sawa, sidhani kama kijana asiye na hatia kama yule anatakiwa kufanyiwa yote hayo kwa sababu kumpa tu hiyo kesi inatosha na sio kumuua, hili jambo halipo kwenye mpango”
“Tangu lini umeanza kuwa na huruma wewe wakati nafsi yako inajiwazia yenyewe tu?”
“Sio kuwa na huruma lakini huyu hakuna kitu ambacho ametukosea au amenikosea mimi”
“Unampenda?”
“Hapana”

“Sasa kwanini una wasiwasi sana kuhusu huyo kijana ambaye hata hauna undugu naye?”
“Sio wasiwasi mimi nilikuwa naongea tu”

“Katika makosa ambayo hutakiwa kuyafanya kwenye kazi yako ni kumpenda huyo mwanaume. Narudia tena hautakiwi kumpenda kamwe zaidi ya kumuigizia na kumpatia mwili wako pale ambapo anakuwa anakuhitaji wewe na usije ukampa sababu yoyote ile ya kumfanya atafute mwanamke mwingine. Umfanye akuwaze wewe kila wakati, hata ukiwa chooni unapopata nafasi ya kumpa mapenzi we mpe hata kama hajaomba hili ji jambo ambalo huwa linatuchanganya sana wanaume hivyo kila akiwaza ngono sura yako itakuwa ndiyo pekee inakuja kwenye kichwa chake na hilo jambo litamfanya akuamini na kukupenda sana hivyo akifikia hatua hiyo ndio muda ambao unatakiwa kujua kila kitu chake, unatakiwa kujua kila mpango wake na kuja kuripoti kwangu”

“Nimekuelewa mpenzi nitalifanyia kazi hilo haraka sana ila punguza wivu”
“Kwamba mimi nina wivu na wewe hapo au?”
“Ndiyo”

“Hahaha hahaa binti utakuwa haupo sawa, mimi sijawahi kumpenda mtu kiasi kwamba naweza kumuonea wivu ila huwa napenda tu kufanya mapenzi na wanawake warembo kama wewe japo nina sharti langu moja kama nalala na wewe basi siwezi kuruhusu ulale na mwanaume mwingine maana inakuwa ni kama dharau kubwa sana kwangu ila kusema nakupenda kama ulijua hilo unajidanganya sana”

“Kama haunipendi kwanini mpaka sasa umenifanya kuwa mwanamke wako kwa miaka yote hii?”
“Kwa sababu napenda sana kufanya mapenzi na wewe ndiyo maana nakuweka karibu yangu ili nisije nikalikosa hili penzi”

“Hivi umewahi kuwaza baada ya haya maisha ambayo tunaishi kitafuata nini?”
“Huwa sijali kabisa kuhusu maisha ya siku zinazokuja zaidi ya kuizingatia siku ambayo naiishi kwa kwa wakati huo”

“Kwahiyo hata nafasi yako hiyo kubwa huwa hauiwazii?”
“Unamaanisha nini?”
“Kila siku utakuwa mtu wa kutumwa tumwa mpaka lini?”
“Unamaanisha kwamba nimsaliti Denis Kijazo”
“Nashukuru una kichwa chepesi”

“Usije ukathubutu tena kuwaza huo ujinga na usije ukaongea hiyo kali kwa mtu mwingine yeyote yule kwa sababu utakufa siku hiyo hiyo. Yule sio mtu wa kawaida kama ambavyo huwa unamuona anatabasamu, ni mtu ambaye ana watu wa kila aina ndani na nje ya nchi na ndiye mtu ambaye aliniweka hapa leo. Ni mtu ambaye akizihitaji taarifa za maisha yako yote anazipata kwa masaa ishirini na manne tu sasa unahisi mtu wa hivyo unaanzia wapi kumsaliti, ni nani ambaye utampelekea hilo wazo asimfikishie taarifa zako? Naona ushaanza kuwaza ujinga ondoka ukaianze kazi haraka sana” alimpa somo kuhusu mtu huyo kisha akamtaka aondoke na kuanza kuifanya kazi ya kumuweka Max kwenye kumi na nane zao huku wakiamini mapenzi ndiyo ilikuwa silaha pekee ya kuweza kujua ni kipi ambacho raisi alikuwa amekipanga na ni watu gani walikuwa wamemzunguka na kumpa nguvu kupitia Max.

Kutokana na kusimamishwa kazi na kuiongozi wake Max alikusanya kila kilicho chake bila hata kumuaga mheshimiwa raisi na kutoweka eneo lake la kazi maana hiyo ilikuwa ni amri. Siku nzima inakatika mwanaume huyo akiwa yupo nyumbani kwake sehemu ambayo alikuwa ana nyumba ya kuishi eneo la Kinondoni Biafra. Usiku alikuwa ndani akiwa anaendelea na kazi zake za kufanya tafiti mbalimbali juu ya majukumu ambayo yalikuwa yanamkabili ila alisikia mlio wa mtu akipiga kengele getini, aliwasha kamera ya nje ili kuweza kujua kwamba alikuwa ni nani huyo, alishangaa kumuona mwanamke na alipo muangalia vizuri alishtuka maana alikuwa ni Brandina.

Alijiuliza maswali mengi sana juu ya kile ambacho kilikuwa kimemleta mwanamke huyo na ukizingatia hakuwahi kuwa na ukaribu naye hata siku moja wala kufikia mazoea ya kuweza kutembeleana na kwa kumbukumbu zake hakukumbuka kama aliwahi hata siku moja kuweza kumueleza ni wapi alikuwa akiishi na ndiyo sababu alikuwa kwenye mshangao wa kujiuliza hayo mambo yalikuwa yanatokeaje. Aliangalia saa yake ulikuwa ni usiku sana na hakuwa na shaka kwamba mwanamke huyo alikuwa ametoka kazini muda mrefu tu ila hakuwa na namna alifungua geti hilo na mrembo huyo akaingia ndani ya gari na kuingia nayo ndani kisha geti likajifunga tena. Max alitoka mpaka nje kwenda kumpokea mwanamke huyo.

“Brandina, kitu gani kimekuleta hapa muda huu na umejuaje kama mimi naishi hapa?”
“Hivyo ndivyo unavyo wakaribisha wageni wanapofika kwako Max?”

“Ooh samahani, karibu ndani” hakuwa na namna zaidi ya kumkaribisha ndani na kumpatia juisi kama ambavyo mrembo huyo aliagiza
“Hapa unaishi mwenyewe”
“Ndiyo, kwanini?”

“Nilikuwa naogopa kwamba huenda umeoa”
“Kama nimeoa wewe unaogopa nini?” mwanamke huyo hakuweza kujibu chochote zaidi ya kutabasamu akiwa anamwangalia Max kwa macho ya mitego sana.

“Brandina unaweza ukaniambia kwamba ni kipi kimekuleta hapa?”
“Wewe hapo”
“Unasema?”

“Nimezunguka sana sehemu nyingi kwenye maisha yangu ila sikuwahi kupata bahati ya kumpata mtu ambaye naweza kumkabidhi moyo wangu kwa sababu sikuwahi kuridhika na tabia za wanaume ambao nawaona huko nje ila nahisi kwa sasa nimekupata wewe”
“Umelewa eeh?”

“Bahati mbaya sana mimi sio mtumiaji wa vilevi” Max aliinuka na kumshika Brandina akitaka kumtoa hapo kwake maana aliona kama mwanamke huyo alikuwa analeta mazoea ambayo hakuwa anayataka kwa wakati huo lakini zoezi lake lilifeli maana mwanamke huyo alimkumbatia kwa nguvu sana huku akiwa anatoa machozi na kuongea kwa hisia sana.

“Max hata kama haunipendi kwa sasa ila unaweza ukajipa muda na mwisho ukaja kunipenda taratibu tu, nimejipa muda wa kutafakari juu ya hili na naona wewe ndiye mwanaume pekee ambaye mimi naweza kumuamini, nakupenda na nahitaji uwe mwanaume wa mwisho mimi kumpenda kwenye maisha yangu tafadhali”

“Brandina, kazi yetu hairuhusu kabisa sisi kupendana wala kupenda na ni jambo ambalo haliwezekani”
“Hakuna kitu ambacho hakiwezekani na hakuna sehemu ambapo imeandikwa kwamba kwa kazi yetu sisi hatutakiwi kupendana ni maamuzi binafsi ya mtu, kuwa kwenye hii kazi haimaanishi sisi ni maroboti, sisi ni wanadamu kama wanadamu wengine na sisi tuna mioyo kama watu wengine na najua hata kwako ipo hivyo. Naamini hata moyo wako unaamini kwenye mapenzi ni kwa vile tu unaogopa Max” mvuto wa urembo aliokuwa nao, sauti yake ya kudeka akiwa inalalamika karibu na sikio la mwanaume na ukijumlisha na ile harufu nzuri ya marashi ambayo ilikuwa kwenye mwili wake, Max alijikuta anakosa misimamo na kuanza kuhema kwa nguvu sana.

28 inafika tamati.

Tchao
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 29
Brandina aliliachia koti ambalo lilikuwa kwenye mwili wake kisha akakivua haraka kigauni kifupi ambacho kilikuwa kwenye mwili wake na ndani hakuvaa hata chupi. Mwili ulikuwa kama mwanamke huyo alivyozaliwa huku akiwa anaangalia kwa macho ya kuchombeza, alisogea nyuma hatua moja na kugeuka kwa kuzunguka huku akitulia na kumwangalia mwanaume ambaye alikuwa mbele yake. Alikuwa mrembo zaidi akiwa uchi, Max alijaribu kuvumilia lakini uzalendo ulikuwa unamshinda kuweza kuvikwepa hivyo vishawishi wakati huo.

“I love you M….” Brandina hakumalizia sentesi yake mwanaume alimvamia na kuanza kumpa juisi ambayo ilikuwa kweny mdomo wake, walibebana mpaka chumbani ambako walipeana penzi kali mno na walikuja kuachiana baada ya saa moja na nusu huku wakiwa wapo hoi kila mtu akiwa ameifurahia sana kampani ya mwenzake. Penzi ambalo Max alipewa lilimfanya nafsi yake kujutia kutomfahamu mwanamke huyo mapema, akajikuta taratibu anaanza kumuingiza kwenye moyo wake kwa kasi sana hata yeye alishindwa kuelewa kwamba ni kipi ambacho alikuwa anatakiwa kukifanya hivyo wakawa wameyazalisha mapenzi ambayo yalianza kuchipua kwa kasi ya ajabu sana.

Alfajiri na mapema wakati wapenzi hao wapya wakiwa wanapeana burudani kitandani simu ya Max ilianza kuita kwa fujo sana, alinyanyuka na kuweza kuiangalia, aliyakuwa anapiga alikuwa ni mkurugenzi.
“Ndiyo kiongozi”

“Yes, sir” alijibu mara mbili tu kisha simu ikakatwa. Alirudi na kukaa kitandani
“Nani anapiga?”
“Bosi”
“Anasemaje”
“Nirudi kazini”

“Kuna sababu gani ambayo ilifanya akakusimamisha kazi ghafla halafu tena anakurudisha ghafla sana namna hii?”
“Hata mimi sijui”
“Nadhani tunatakiwa kwenda muda huu”

“Mimi niliomba ruhusa ya kwenda kufanyiwa vipimo hivyo nakuja baadae maana mheshimiwa raisi leo hana ratiba yoyote ya kutoka hivyo kwa sasa nataka nilale kidogo kisha baadae nitakuja” Max alimwangalia kwa umakini sana mwanamke huyo maana ni kama alikuwa anataka kuanza kujimilikisha hadi hapo kwake lakini alishindwa cha kufanya ikamlazimu kujiandaa haraka sana na kwenda kazini ambapo alikuwa ameitwa moja kwa moja na mheshimiwa raisi.

“Max kuna nini mpaka uliondoka kimya kimya bila kuaga”
“Samahani mheshimiwa ilikuwa ni amri ya bosi wangu hivyo sikuwa na namna ya kuweza kuipinga”
“Nilikuwa nakuhitaji baada ya Brandina leo kuwa na ratiba ya hospitali sasa nimeshangaa wananiambia kwamba uliondoka tangu jana. Unaweza ukaniambia kwamba ulisimamishwa kwa sababu ipi maana mimi nimeshangaa sana na nilipo mpigia simu mkurugenzi akaniambia kwamba unakuja sasa hivi alikusimamisha kwa utovu wa nidhamu”
“Alikuwa anataka kujua usiku wa jana nilikuwa wapi lakini pia alikuwa anataka kujua mambo mengine mawili. Alitaka kujua kwamba kama mimi ndiye ambaye nilihusika kulipua lile jengo na sababu ya kwanini wewe haujachukua hatua yoyote juu ya haya yote ambayo yanaendelea kutokea”

“Mhhhh ulimpa jibu gani?”
“Nilimwambia kwamba sijui lolote wala sio mimi ambaye nahusika na kama alikuwa anataka kuuliza hayo mambo alitakiwa kukuuliza wewe kwani yalikuwa juu ya uwezo wangu na hapo ndipo ambapo alichukia sana na kuniambia kwamba ananisimamisha kazi”

“Unaweza kwenda ila kuwa makini sana maana hawa watu wamefikia hatua mbaya sana”
“Sawa mheshimiwa” Teo alisimama dirishani kwa muda kidogo akiwa anayaangalia madhari ya bahari, alisikitika sana juu ya mambo yote ambayo yalikuwa yanatokea kwa wakati huo.

“Sikuwahi kufikiria hata siku moja kama nitakuja kuwa sehemu kama hii ambayo maisha ya watu yanategemea kauli yangu na busara zangu, hili ni jambo ambalo napaswa sana kujivunia na kwa kumuenzi Francis Mboye hawa watu lazima niweze kuwateketeza wote” aliongea mwenyewe akiwa anajipa moyo huku akiitoa simu yake kwenye mfuko wa koti, aliitafuta namba ambayo alikuwa anaitaka na kuipiga.

“Nakuhitaji ofisini kwangu”
“Sawa bosi” upande wa pili uliitikia na simu hiyo ikawa imekatwa wakati huo huo.
“Bosi, umenihitaji”

“Ndiyo. Nilitaka kujua sababu za msingi za wewe kumsimamisha kazi kijana zilikuwa ni zipi?”
“Kushindwa kuniheshimu kiongozi wake, namuuliza maswali ananijibu kwa dharau na kuanza kunificha anacho kifanya wakati jambo ambalo alikuwa analifanya lilikuwa linahatarisha sana usalama wa taifa na sheria inaruhusu mimi kumuadhibu kijana yeyote yule anapokwenda kinyume na sera za shirika letu”

“Ulikuwa unataka kujua kazi ambayo mimi nilimpa ndiyo maana ukamsimamisha? Kwahiyo kwa sasa unamaanisha kwamba upo hapo kuchunguza kila ambacho mimi nakifanya?”
“Hapana mheshimiwa nadhani utakuwa umenielewa vibaya”
“Unataka nikuelewa vipi?”

“Nilikuwa nafanya kwa ajili ya usalama wa nchi yetu maana jengo limelipuka lakini haujatoa tamko lolote lile wala kunipa utaratibu wa nini cha kukifanya baada ya hilo maana wananchi wanahoji na mitandao ya kijamii inatumika kuzua mjadala ambayo kila mwananchi anaanza kujitengenezea maelezo yake ambayo anaona kwamba yanamfaa kwenye hilo”

“Unamaanisha mimi ndiye natakiwa kukufundisha wewe namna ya kuifanya kazi yako? Limetokea tatizo kulifanyia kazi ni mpaka mimi nikuite mezani na kukuelekeza? Unamaanisha kwamba haujui kwamba mimi nilitakiwa kusubiria ripoti yako tu ofisini?”

“Nisamehe sana mheshimiwa”
“Philipo, napaswa kuwa na wasiwasi na wewe?”
“Mheshimiwa unamaanisha nini?”
“Naweza kukuamini?”

“Ndiyo mheshimiwa, ndiyo mimi nipo hapa kwa ajili yako”
“Kweli”
“Ndiyo”

“Naomba historia yote ya shirika letu la kijasusi, usiacha hata sentensi moja nataka kulijua tangu siku ambayo lilianzishwa, mpaka siku ya leo lilipofikia”

“Sawa bosi, nakuletea taarifa zote ndani ya muda mfupi sana” mkurugenzi alitoa heshima na kutoka humo ndani akiwa anashangaa sana, haikuwa kawaida raisi kutaka taarifa za watu hao tena ghafla sana namna hiyo. Alisimama na kugeuka kuiangalia ofisi ya mwanamke huyo kwa muda kidogo akiwa ni kama mtu ambaye alikuwa anayawaza mengi sana yaihusuyo ofisi hiyo.

“Unaenda kuishia pabaya sana na kuwa raisi ambaye amekaa ofisini kwa siku chache sana” aliongea mwenyewe huku akiwa anatoka kwenda kuzichukua taarifa ambazo zilikuwa zinalihusu shirika hilo la kijasusi.

THE WINGS OF TANZANIA INTELLIGENCE SERVICES (WTIS)
Shirika la kijasusi la taifa la Tanzania. Ni shirika ambalo lilianzishwa mnao mwaka 1970 chini ya raisi wa kwanza John Mahanji ambaye alimteua Lenus Maziku kuwa mkurugenzi wa kwanza wa shirika hilo. Sababu za msingi za kuanzishwa kwa shirika hilo zilikuwa ni baada ya magaidi kuweza kuvamia nchi na kuua raia mia-mbili huku wakifanikiwa pia kutoka na shehena kubwa sana ya madini lakini magaidi hao waliacha ujumbe pia kwamba walifanikisha jambo hilo kwa msaada mkubwa sana wa baadhi ya viongozi ambao walikuwa ndani ya serikali.

Ni jambo ambalo lililiacha taifa kwenye mshtuko mkubwa sana kwani hawakuwa na uhakika kama ni kweli magaidi hao walikuwa wamesaidiwa na viongozi au walifanya hivyo ili kuwagombanisha wenyewe kwa wenyewe kuwapunguza nguvu ya kuendelea kufanya maendeleo kwa taifa lao. Kupitia matukio hayo ndipo raisi huyo aliona umuhimu mkubwa wa kuwa na shirika hilo ambalo lilipewa kazi ya kwanza kuweza kuwachunguza magaidi ambao walikuwa wamefanikiwa kuua raia na kutoka na madini lakini pia kufanya uchunguzi wa siri sana ndani ya serikali ili kujua kama kweli kulikuwa na wasaliti au yalikuwa ni maneno ya kichonganishi tu.

Jambo hilo mheshimiwa raisi alilifanya kwa siri sana na ni watu wachache sana ambao walijua kama alifanya maamuzi ya kuanzisha shirika hilo maana wengi waliambiwa kwamba jeshi la polisi pamoja na jeshi la wananchi ndilo pekee ambalo lingefanya kazi hiyo. Alimteua rafiki yake wa karibu ambaye alikuwa mkuu wa majeshi kwa kipindi hicho na kumtaka awachambue makamanda wake ambao alikuwa akiwaamini sana kwa ajili ya kufanya kazi hiyo. Kikosi kiliundwa na rasmi wanaume hao wakaingia kufanya uchunguzi wa chini kwa chini.

29 inafika mwisho.

Tchao
 
Back
Top Bottom