PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi :Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293
SEHEMU YA SIBA-07
Lakini kabla kijana Zabroni hajawafikia wazee hao,machale yalimcheza. Bila kuchelewa alijibadilisha akawa katika sura yake ya kawaida kisha akapotea maeneo hayo ambapo mzee Ngurumo na mwenyekiti walipo fika eneo lile alilopotelea Zabroni kamwe hawakuweza kumuona,zaidi walijikuta wakihisi joto ambalo nalo hawakuweza kulitilia maanani kwani walikuwa na haraka za kwenda kutazama nyumba ya nani inaungua. Mwenyekiti alipo kuta nyumba yake ipo salama alifurahi sana lakini pia hakusita kutoa pole kwa jirani yake aliyechomewa nyumba,wakati huo huo mzee Baluguza naye alionekana kuinamisha uso wake chini akitafakari jambo fulani. Lakini punde si punde mzee huyo alitoka kwenye dimbwi la tafakari baada kuguswa bega na mwenyekiti,Baluguza aligeuka akakutana na uso wa Mwenyekiti. "Kulikoni mwenzetu naona umetukimbia kimaajabu" Alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Baluguza, kwa sauti ya unyonge huku akiutazama ule moto unaolanda kwenye nyumba alisema "Hii ni kawaida yangu mzee mwenzangu,naona hakuna muda wa kupoteza. Kesho naomba uitishe mkutano wa kijiji ili nimuumbue mbaya wenu " alisema mzee Baluguza.
Kesho yake palipo pambazuka mbiyu ya kijiji ililia, taarifa zikagonga masikioni mwa wanakijiji kwamba kutakuwa na mkutano wa wakijiji siku hiyo. Hivyo haitakiwa mwanakijiji yeyote akose kuhudhulia. Mbiyu hiyo aliisikia na kijana Zabroni ,akiwa kitandani kwake. Akajiuliza "Wanamikakati gani mbweha hawa?..ni lazima na mimi nihudhulie ili nijue wanamikakati gani ",alisema Zabroni huku akisimama kutoka kwenye kitanda chake,alichukuwa bukta yake iliyokuwa imekatwa miguu kwa kuzidiana kisha akaelekea mahili yalipo makaburi ya wazazi wake. Hapo Zabroni alienda kwa niaba ya kuyasafisha kabla muda wa mkutano haujawadia, na pindi kijana huyo akifanya hicho kitendo upande wa pili kijiji kilionekana kuzizima majonzi. Wanakijiji walikuwa wakisikitika kuwapoteza wanakijiji wenzao waliokufa usiku wa jana kwa ajari ya moto,hali hiyo ikawafanya kuwa na shauku kila mmoja kufika mkutano ni. Hali hiyo ilimpelekea mazishi kufanyika mapema sana ili watu wawahi,haikuwepo haja tena ya kukaa msibani mpaka jioni kwani hali iliyokuwepo sasa ilitisha kila familia haikuwa na amani nyumbani kwake,wazee kwa vijana wote walianza kuogopa. Hivyo siku hiyo waliposikia mbiyu wakaamini kuwa huwenda mbiyu hiyo ikawa na jambo la heri katika kijiji chao.
Na hatimae Muda uliwadia sasa,watu walianza kukusanyika mkutanoni. Kwa muda wa nusu saa wanakijiji wote walikuwa wamefika ingawa si wote kwani kuna baadhi walikuwa bado wanajiandaa kuanza safari,ilihari wengine tayari walikuwa wameanza. Vile vile Upande mwingine Zabron naye alianza safari ya kujongea kwenye mkutano huo,nia na madhumuni kutaka kusikiliza mikakati gani inayo endelea kijiji hapo. Na wakati Zabroni alipokuwa akitembea njiani,Ghafla mbele yake akaona kamba. Alipoiona kamba hiyo akajipapasa kwenye mfuko wa bukta yake akakuta kibiriti. Aliachia tabasamu baada kujihakikishia kwamba kibiriti anacho upesi akaichukuwa kamba hiyo akaenda nayo mpaka kwenye nyumba moja ambayo ya mzee Ngurumo. Alipo fika hapo alitazana kulia na kushoto kuangalia usalama wake akagundua hakuna mtu yoyote mahali hapo. Pasipo kupoteza muda aliifunga kamba kwenye fito ya nyumba kisha akailaza hatua mbili za mtu mzima kutoka mahali ilipo nyumba. Kwa mara nyingine tena akarudia kutazama kila pande, alitazama kulia na kushoto pia nyuma yake hakuona mtu,haraka sana akachukuwa nyasi kavu akizisambaza kidogo juu ya kamba ile kisha akafyatua njiti, nayo ikaripua moto akaishusha kwenye zile nyasi nazo zikanasa moto ambao pole pole ulitembea kwenye ile kamba ya kitambaa. Kamba ambayo pia ilikuwa pana na ndefu kwa kiasi chake. "Mchezo umekwisha", alijisemea ndani ya nafsi kisha akaondoka kuelekea kwenye mkutano wakati huo huo huo mzee Baluguza alionekana kutoka ndani ya nyumba ya Mwenyekiti huku mkononi akiwa na jungu ambalo lilikuwa na makorokoro mengi ndani yake, wanakijiji walitulia kimya mpaka mzee huyo anafika kwenye umati wa wanakijiji. Alipo fika alisimama akitaka kusema jambo,lakini kabla hajasema akamuona Zabroni naye akijisogeza kwenye mkutano. Mzee Baluguza alimkazia macho ila mwishowe akajifanya kupotezea ili mtukutu Zabroni asijishuku. Zabroni alifika mkutanoni akaungana na wenzake alitulia chini akisubiri kujua kipi kinacho taraji kutokea. Muda huo huo Baluguza akamnong'oneza Mwenyekiti, akamwambia "Nenda kanichukulie nyayo za yule kijana"
"Kijana yupi? .."alihoji Mwenyekiti huku akiwa makini kumsikiliza mtalamu Baluguza.
"Kijana yule tuliyepisha naye juzi jioni wakati ulipokuja kunipokea", mwemyekiti alivuta kumbukumbu kwa muda wa sekunde kadhaa mwishowe akakumbuka kuwa mtu mwenyewe ni Zabroni mtoto wa mzee Ndalo. "Sawa nitazijuaje hizo nyayo?..", kwa mara nyingine tena aliuliza Mwenyekiti. Mzee Baluguza alikaa kimya kidogo huku akichukuwa kipande cha kitambaa ambacho kilionekana cheusi kisha akamkabidhi Mwenyekiti halafu akamwambia "Kavaa saganyoka,hivyo ni rahisi sana kuzigundua. Nenda haraka chukua mchanga kudogo hapo alipo kanyaga kisha niletee hapa nimalize kazi", alijibu mzee Baluguza. Mwenyekiti akiwa na wasiwasi kwa kijana Zabroni alifanya kama alivyo ambiwa kisha haraka sana akarudi wakati huo mzee Fungafunga akiwa kama mmoja ya baraza la wazee kwenye mkutano huo yeye alikuwa akiwaongelesha huku mzee Baluguza akifanya yake. Mara baada kumaliza ndipo huyo mzee alipo simama na kisha kusema "Habari zenu wanakijiji, jina langu naitwa Baluguza nadhani wapo wanaonifahamu na wasio nifahamu. Nimekuja hapa kutokomeza hili janga linalo endelea hapa katika kijiji chenu. Haya mauwaji yakinyama, yanatisha lakini leo ndio siku kuu ambayo mtu huyu mshenzi na mjinga atagundurika. ", aliongea kwa kujiamini kabisa Baluguza punde akaendelea kusema." Rafiki yako ndio huyo huyo adui yako, kwa maana hiyo basi kikulacho kinguoni mwako. Mtu anayefanya vitendo hivi wala hatoki nje ya kijiji hiki ila mpo naye humu humu" alisema Baluguza, akameza mate halafu akaendelea kusema. "Kwa maana hiyo basi leo lazima agundulike huyu mtu anaye uwa watu wasiokuwa na hatia, na akishagundulika ndipo kijiji kitaamua mtu huyu afanywe kitu gani. Je, mpo tayari?.." Sauti za wanakijiji zilipasa zikisema "Tupo tayariiiiii!" Lakini wakati wanakijiji hao wanapasa sauti zao kutaka kumfahamu kirusi wa kijiji mara ghafla ule moto uliokuwa ukitambaa kwenye kamba hatimae ilifika kwenye nyumba,nyumba ya mzee Ngurumo ikaanza kuteketea ikiwa mchomaji yupo hapo hapo kwenye mkutano wakati huo mzee Baluguza akitaraji kumuumbua mchomaji huyo mbele ya wanakijiji.
ITAKUAJE HAPO tukutane sehemu ijayo!
Sent using
Jamii Forums mobile app