Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Komandi kama unalipia vile eti sasa mbona kimya umemlipa?acheni wenge..Sasa mbona kimya
OkPENZI LA MFUNGWA
Mtunzi : Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293
SEHEMU YA SITA-06
Kwisha kujisemea maneno hayo aliachia tabasamu bashasha huku akimsindikiza kwa macho Zabroni kitendo ambacho kilipelekea mwenyekiti kuingiwa na hofu akajiuliza maswali mengi ambayo aliyakosa majibu yake,ilihali upande wa pili Zabroni o naye aligeuka kumtazama mzee Baluguza ambaye kwa macho yake ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona. Alistuka baada macho yake kugongana na macho ya mzee Baluguza ila hakujali zaidi aliendelea na safari yake kama alivyofanya mzee Baluguza.
"Huyu ni nani?..", ndani ya kichwa chake Zabroni alijiuliza. Upande wa pili mwenyekiti alimkalibisha nyumbani mzee Baluguza kwa furaha huku akimpa tumaini kwamba ajisikie yupo nyumbanin,Baluguza akakaribia kwa bashasha ya hali ya juu. Baada ya maongezi mawili matatu,mwenyekiti akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwa mzee Ngurumo ambaye ndio balozi wa nyumba kumi. Alimkuta. Akamwambia nia na dhumuni ya ujio huo,mzee Ngurumo alimuelewa vema tena akampongeza kwa hatua aliyochukuwa ya kumleta mzee Baluguza mganga mashuhuli aliyefamika kwa huduma yake maridadi isiyokuwa na utapeli.
"Ama kweli wananchi waliokuchagua hakika hawakukosea,kiukwe hili ni tatizo tena sugu. Tusipo chukuwa hatua mapema tutajikuta tukipoteza mpaka familia zetu", aliongea mzee Ngurumo huku akifunga mlango wa nyumba yake. Mwenyekiti alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Ni kweli ,si unajua tusipo ziba ufa tutajenga ukuta? .."
"Kabisa ndugu mwenyekiti"
"Basi hima twende tukazungumze naye tujue hili tatizo atalikomesha vipi" aliongeza kusema mwenyekiti wakati huo tayari wameshatoka nyumbani hapo kwa mzee Ngurumo na sasa walionekana kuanza safari kurudi nyumbani kwa mwenyekiti. Ila kabla hawajafika,Ngurumo akatoa wazo akasema "Unaonaje tukamuone na mzee Fungafunga? Maana hili suala kama linamuhusu na yeye?.."
"Sawa hakuna shida twende ingawa sidhani kama atakuwa karudi kutoka shamba,nasikia ngedere wanasumbua sana shambani. Wami unamsumbua sana"alijibu mwenyekiti.
"Loh. Nikweli lakini tukajaribu"
"Sawa twende"
Mwenyekiti na mzee Ngurumo walielekea kwa mzee Fungafunga, bahati nzuri walimkuta akiwa tayari ametoka shamba alionekana kuchoka sana.
"Hodi! Hodi! Bwana Fungafunga " Ngurumo alisema.
"Anhaa KARIBU bwana,karibu sana. Mama Tina leta vigoda haraka", alijibu mzee Fungafunga kwa tabasamu bashasha ,na punde si punde Mama Tina alileta vigoda. Mzee Ngurumo na mwenyekiti wakapata kuketi kisha soga zikaendelea.
"Naam! mzee mwenzangu,pole sana nasikia ngedere wanamsumbua sana huko", aliongea mzee Ngurumo. Wakati mzee Fungafunga akajitayarisha kumjibu Ngurumo. Upande wa pili kijana Zabroni alionekana kasimama kando kando ya nyumba,alitazama kulia na kushoto hakuona mtu. Giza tayari lilikuwa limeanza kutanda kwa maana hiyo kijiji kilianza kupoa zaidi zilisikika kelele za vijana wa kijiji kijiweni wakibishana mambo mbali mbali,gumzo ilikuwa ni ujio wa mzee Baluguza kijijini hapo. Wapo waliombenza kwamba mzee huyo si chochote si lolote,lakini pia wapo walimnadi ya kwamba huyo mzee ni moto wa kuotea mbali. Hivyo hali hiyo ndiyo iliyoweza kuleta ubishi katika kijiji hicho eneo la kijiweni. Kelele zilipasa kila kona hakuna aliyegusia masuala ya siasa abadani bali wote waliongelea ujio wa Baluguza. Lakini pindi mada hiyo ikiwa imepamba moto, mara ghafla ulionekana mwanga mkali angani ulio ambatana na moshi. Kwa maana hiyo tayari nyumba ya mtu ilikuwa inateketea kwa moto mapema tu saa moja usiku. Taharuki ilizuka, soga la kumnadi mzee Baluguza upesi zilikatishwa ,hima wakakimbia kuelekea kule kunako fuka moshi na moto. Pindi vijana hao walipokuwa wakielekea huko,upande wa pili nyumbani kwa mwenyekiti walionekana mzee Ngurumo,mzee Fungafunga pamoja na mwenyekiti wa kijiji bila kusahau mzee Baluguza. Nao walikuwa wakijadili namna gani ya malipo yatakavyo fanyika pindi mzee Baluguza atakapo kamilisha kazi iliyo mleta, ila makubaliano hayo yaliingia dosari baada mama Tina kupasa sauti ya mayowe alipoona moshi mkali ulioambatana na kipupwe cha moto. "Unaona sasa?..mapema tu leo" alisema mzee Ngurumo huku akinyoosha kidole kule ilipokuwa nyumba inateketea.
"Nadhani hapo mzee mwenzangu utakuwa umeamini kuwa hata zile nyumba za awali sio mimi niliyezichoma moto", alidakia mzee Fungafunga akijitetea mbele ya mwenyekiti ambaye hapo awali baada kuchomwa nyumba tano,Mwenyekiti alimuhisi yeye kwamba ndiyo muhusika kwani aliwahi kung'atwa sikio na mzee huyo kuwa yeye ndiyo aliyechoma nyumba ya mzee Ndalo baba yake Zabroni kwahiyo Mwenyekiti akawa hana imani na mzee Fungafunga lakini siku hiyo alimuamini baada kuona nyumba ikiteketea kwa moto. Wazee hao waliazipiga hatua kuelekea kwenye ajali hiyo,walipo fika waliwakuta vijana wakishughulika kuuzima moto lakini hawakuweza kufanikiwa. Nyumba iliungua yote huku ndani akiwemo mzee Kadili mchongaji nguli wa mipini kijijini hapo,mzee ambaye aliishi yeye peke yake, hakuwa na familia
Kwa mara nyingine tena yanatokea majonzi kijiji hapo,kila mwanakijiji roho juu ilihali huzuni nayo ikitawala mioyoni mwao. Walihofia usalama katika kijiji chao, lakini wakati wanakijiji hao wakiwa katika hali hiyo,mara ghafla mzee Baluguza akamuita kando mwenyekiti kisha akasema "Hivi yule kijana tuliyepishana mude ule yupo hapa? ", Mwenyekiti hakujibu upesi, alikaa kimya huku akijaribu kumkumbuka. Akamkumbuka na ndipo alipo tazama upande ule waliosimama vijana wengi akamuita mmoja wao, naye alitii wito wa mwenyekiti "Zabroni yupo hapa? ..", kijana huyo aliyetii wito wa mwenyekiti aliulizwa.
"Hapana ", alijibu kijana huyo,jibu hilo alilisikia na Mzee Baluguza.Akalizika nalo akatikisa kichwa halafu akamuuliza tena Mwenyekiti "Unapajua anapoishi?..", lakini kabla Mwenyekiti hajamjibu Baluguza, ghafla ilionekana mwanga mkali angani na moshi mwingi. Kiashiria hicho kilimanisha kuwa tayari kuna nyumba nyingine inateketea,Mwenyekiti aligeuka akatazama kule akaona mwanga ule unatokea mahali ilipo nyumba yake. "Lahaulla nyumba yangu", alitaharuki mwenyekiti huku akiweka mikono kichwani alijua fika nyumba yake inateketea. Haraka sana vijana wa kijiji wakajigawa magundi mawili, kundi moja liliendelea kuuzima moto kwenye nyumba hiyo inayoteketea, na kundi lingine lilielekea kule inapoungua nyumba nyingine ambayo mwenyekiti aliamini kuwa ni nyumba yake. Mzee Baluguza aliposikia maneno ya mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti, haraka sana akapotea eneo hilo akaibukia nyumbani kwa Mwenyekiti. Alikuta nyumba ya mwenyekiti ipo salama, ila nyumba nyumba ya jirani yake ndiyo iliyoonekana ikiteketea. Mzee Baluguza akastaajabu kumuona mchomaji akiendelea kufyatua njiti. Mtu huyo hakuwa mwingine ni Zabroni ambaye baada kuchoma nyumba hiyo aliamua kujibadilisha umbile lake akachukuwa umbile la mzee Ngurumo. Hivyo alipokuwa katika umbile hilo la mzee aliendelea kufyatua njiti kuchochea moto wakati mzee Baluguza akimtazama mara mbili mbili mwishowe akakumbuka mtu huyo kamuacha kule alipotoka, aliingiwa na hofu akaona ni mchezo mchafu anachezewa. Aliguna kisha akajisemea "Nimekupata ila siku zako zinahesabika nitakukomsha"., maneno hayo mzee Baluguza alijisemea ndani ya moyo wake huku Zabroni naye akiwa na umbile la mzee Ngurumo alionekana kuishia zake kwenye giza totoro akiacha nyumba ikiteketea vile vile akimuacha mzee Baluguza akiishia kumsindikiza kwa macho tu wakati huo akifahamu fika kijana huyo anauwezo wa ajabu sana. Na pindi Zabroni alipokuwa njiani akitembea kwa kujiamini katika umbile la mzee Ngurumo, mbele yake walionekana wazee wa wawili wakitembea kuelekea kule anakotokea yeye wazee hao ni mwenyekiti wa kijiji sambamba na mzee Ngurumo mwenyewe!
ITAKUAJE HAPO? tukutane sehemu ijayo! Je, Baluguza atauweza moto wa Zabroni?