Jiwe la kubusu ni hivi, ili kutoka pale barango kwenda karanga lazima mpite mlimani, na mkiwa pale barango mlima unauona uleeeee, mkifika pale mlimani njia ni nyembamba sana, sasa kuna sehemu kuna jiwe kubwa ili kupita hapo lazima ulikumbatie hilo jiwe na unapita upande upande lakini mbaya zaidi chini kuna korongo so ukikosea step kidogo tu unaweza kujikuta uko korongoni, so mnapita mmoja mmoja na kwa uangalifu mkubwa. Nakumbuka kundi letu tulikuwa zaidi ya watu 30 tulitumia almost 2hrs kuvuka hapo....na slogan ya mlimani ni Pole Pole....no hurry
Sent using
Jamii Forums mobile app