Mkuu kupanda mlima Kilimanjaro, Hali yake ya hewa, inabadilika mara nyingi kidogo.Kutokana na ile ya baridi kali sidhani kama nyoka au mnyama mwingine anaweza kukaa kwenye mazingira yale,labda awe yule mnyama anayekaa kaskazini mwa Canada kule Greenland!
Sent using Jamii Forums mobile app
Beef Lasagna kheri ya mwaka mpya sis.Umenipa hamasa ya kupanda huu mlima.
Vipi haukufika Kileleni Uhuru?Au nimemiss bandiko lingine.
Sent using Jamii Forums mobile app
Na wewe piaBeef Lasagna kheri ya mwaka mpya sis.
Utapanda lini mlima?Au wewe tayari?
Mkuu, mlima Kilimanjaro unapandika kipindi chote cha Mwaka, sema bado kuna miezi mizuri.Wakuu naomba maelezo kidogo ,wadau wanasema kipindi kizuri kupanda huo Mlima ni kuanzia Julai .
Hiyo Julai huku kwetu bonde la Kilombero ndiyo kuna baridi kali usiku.
Sasa huko kwenye uwanda wa juu si unalifuata hukohuko ?
Kiwatengu na Wazoefu wengine , ni kwanini hicho kipindi Julai hadi Desemba ni kizuri?
Nashukuru,Na wewe pia
Mimi na milima changanya baridi hapana ukipanda wewe inatosha 😅😅😅😅😅😅😅 Acha niwasome wenzangu hapa nishafika kileleni mwenzio tayari kwa simulizi hii 😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Khaaaa.....MKUU umeuliza maswali ya msingi sana. Najua Heaven on Earth atakuja kujibu hapa, lakini kwa uelewa wangu, ile hali ya kule juu haiwezi kufanana na nchi yeyote kwa sababu moja kubwa. Hali ya mwinuko juu ya usawa wa bahari. Hiyo peke yake, inafanya kiwango cha Oxygen kuwa kidogo na kuleta hali ya kupumua kwa shida. Baridi la kule maji yana mnayobeba mgongoni yanaganda, inafika wakati ni nyuzi hasi 15 na kushuka chini Zaidi. Kuna nchi zinaweza kuwa na hali ya baridi Zaidi kuliko huko Uhuru Peak lakini mwinuko wake hauleti shida kwenye mfumo wa upumuaji. Hiyo ndio tofauti kubwa.
Kumbuka mnafika mahali ambapo mvua ikinyesha haiwahusu, inashughulika na walio chini yenu, nyie mpo juu yake.
Mengine wataongezea wataalam na mainjinia watakapokuja kusoma hii unayotaka kusikia hii hahahahahahaaa.
Mkuu, mlima Kilimanjaro unapandika kipindi chote cha Mwaka, sema bado kuna miezi mizuri.
Binafsi huwa napenda sana mtu apande kuanzia May, June, July, August na September...huwa mvua sio nyingi sana.
Mfano mwaka Jana 2018, mwezi wa 10 na 11...haikuwa mizuri kabisa.
Iliondoka na watu kadhaa, hasa maporter, wakipigwa mvua nyingi, huwa wanapata shida sana.
Sitasahau siku nimepanda kupitia Machame, mvua haikukatika ndani ya siku 2 full sasa unakuta hakuna namna, mnaenda tu.
Kama kuna mvua, ni hatari kuliko upepo.
Bahati nzuri mvua huwa zinanyesha huku chini chini....
Maeneo kama ya Kibo hut au Barafu camp, hayana mvua kabisa kwa sababu ni jangwani.
Si lazima lakini ni muhimu.Khaaaa.....
Kupanda huu mlima sasa inakuwa kama vita vya kagera??
Yani hii shughuli inasababisha nia yako inabadirikabadirika kila wakati. Baada ya simulizi nimefuatilia videos kibao, kila mmoja ana lalamika ingawa tena wanafurahia...nini hiki?
Yani safari ya huu mlima ni jasho, kamasi, mikojo mate...ukifanya mchezo na damu. Yani kqma kusomea ukomandoo....hatari sana.
Safari yote ni roho mkononi kama umepanda helicopter...yani muda wote ni hatari hatari hatari tu. Ukifurahia hatari, ukipanda mzuka hatari, yani hatari mwanzo-mwisho.
Kila mmoja analia kivyake...hivi ni lazima??
Sent using Jamii Forums mobile app
Khaa!nikajua na ww ulikua kati ya msafara wa kupanda naye😂😂😂 jaman kuna watu mnahitaji ushauri wa Dk kbs😂😂...
Hahahaha huh u huh 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂Unafanyiwa checkup ya mammbo mengi sana kuona kama utahimili hali ya hewa inayobadilika badilika kadri mnavyosogea juu.
Cha kushangaza, watoto wadogo wa umri kati ya 12-14 wanapanda bila kupata dhoruba kama ilivyo kwa watu wazima,...
Dhambi nazo zinatuongezea mizigo hahahahahahhaha
Tujaribu bwanaaaaa...Na wewe pia
Mimi na milima changanya baridi hapana ukipanda wewe inatosha [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Acha niwasome wenzangu hapa nishafika kileleni mwenzio tayari kwa simulizi hii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu hao madaktari wamepungukiwa kazi hadi kunishauri mimi!!! Kweli? Hakika wakimalizana na mimi watarudi kwako wakushauri kuwa mimi client wako sikustahiri ushauri...
Anyway, comment yangu ililenga kuonesha how impressive is HOE's story, kupanda mlima ni jambo moja na kuelezea kwa mtiririko mzuri wa visa na matukio kwa ufanisi ni jambo jingine linalostahiri pongezi za dhati. Kwangu mimi HOE amefanikiwa kunipandisha huo mlima kitaswira. Namuona kama mtu anayeweza kuwa useful kwenye taasisi muhimu za utalii ama hata kuwa msemaji wa taasisi nyeti za serikali. Bahati mbaya watanzania hatujui namna ya kutumiana in a resourceful manner... The only credit we can offer her ni "kugonga like", haitoshi.
Kama hujanielewa bado, basi fikiria tena vizuri ni nani anamuhitaji daktari kwa ushauri.
Yaani umenikera nimekuwa mwekundu story hujaimalizia hadi mwisho.niko kama mwanamke ambaye kakatishiwa utamu kati,hizo hasira zake ni bora umalizie tu kuandika
"... When a woman loves, she loves for real..."Bonge moja ya Story nimetamani isiishe kwa mara ya kwanza nimeweza kusoma nukta kwa nukta mpaka mwisho
"Nikiwa na Fred.. He is such a nice guy sijapata kuona.. Mtu mwema sana"
Dah Fred angefaa kutunikiwa basi tena ndio hivyo haiwezekani
Sent using Jamii Forums mobile app
Itakuwa ametoa comment kabla hajafika mwishombona nimemaliza mpaka uhuru Peak mkuu... Imebakia tu ya kushuka mlima lol
ila namalizia kuandika.. nimetingwa tu hapa