Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro


Kubeba pombe inaruhusiwa mkuu!?
 
hiyo hapo mzee baba,watu wanajipanga sio wanakurupuka tu na kuvunja record
 

I never knew am such a good story teller before.. Nimejua baada ya hii thread
I am overwhelmed na muitikio wa watu wengi na namna walivyofuatiliana na mimi
mwanzo mwisho.. it gave me the strength to keep on writing. Asanteni pia kwa meseji zenu

It gives me so much happiness to know I inspired a lot of people kupitia simulizi yangu.
 

Hi Heaven

Your story is trully Inspiration to anyone

I saw the sense of accomplishment that you get after climbing, the feeling of achievement, appreciation for the journey, and the chance to be outdoors.

I hope you aweken a lot of giants here.

Pia ninaweza kuwadanganya watu kua nimeshapanda mlima kwa refference yako na namna ulivyoelezea na kuweka hizo picha. ninaweza kusimulia watu kila kitu mpaka aina ya vyoo kila kituo
 
Ila Mimi hutonidanganya hahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Heaven on Earth

Before, am pretty sure that you didn't realise the accomplishment of your desire to climb the mountain.

Lakini hebu angalia impact inayojitokeza hapa baada ya wewe kusimulia?? Mwanzoni ulichukulia poa tu, lakini huwezi amini umenifanya kwa hizi siku 2 nisome sana khs kupanda huo mlima kuliko hata kula na kunywa.

Usishangae TANAPA siku moja wakakutangaza kuwa ni Barozi bora kabisa kuwahi kutokea tena kwa kujitolea kuliko hata huyo Kiba aliyeishia kukatika tu mauno.

Kama kuna makusudio hupangwa na Mungu, basi safari yako ilipangwa ili kuwanufaisha wengi.

Naamini hujutii na tena zaidi unahisi hukukusanya taarifa za kutosha.

Tupo tunakufuatilia.....utakoma kulianzisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tena watu tupo visu Kweli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

..Asante. umenielewa 100%.

..Natarajia Heaven on Earth atanijibu maswali yangu.

..nia yangu ni kuona kama TRAINING/MAANDALIZI ya kupanda mlima yanaweza kuboreshwa zaidi.

..Kwa haraka nimeona challenges tatu kubwa ;physical challenge, wembamba wa hewa, ubaridi mkali unaoambatana na upepo.

..Pia nimeona kuwa dada yetu alifanya maandalizi yake maeneo ya Dsm na Morogoro ambako kuna joto na altitude ndogo.

..Swali ninalojiuliza ni: what if kabla ya kupanda mlima "angejifua" maeneo ya Mbulu ambako kuna baridi kali na hewa nyembamba, au Iringa ambako kuna baridi kali?

..Pia kama angekuwa ameishi ktk nchi ambayo ina majira ya winter makali labda ingemsaidia zaidi kujiandaa kimavazi. Labda angekuwa na advantage kidogo na baridi ingemsumbua lakini siyo kama ilivyomsumbua ktk safari yake ya kupanda mlima.
 
Safi sana.mimi nimepanda huo mlima zaidi ya mara 10 na nimepita njia zote ila njia ngumu kidogo ni umbwe na machame.Ukipita hizo njia kuna sehemu inaitwa baranco,sasa hapo kuna huo mwinuko unaitwa baranco wall wenyewe wapagazi wanapaita brekfast,hapo ni shida. Ila Safi sana mrembo kwa icho ulichofanya mana Kupanda huo mlima ni bonge la adventure.Next time kapande na Mount meru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali langu huko Mlimani hakuna wanyama wakali au nyoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa juu kabisa ila kabla hujafikia ukanda wa jangwa na ukanda wa barafu kuna aina moja tu ya ndege wanaopatikana huko ambao huitwa Alpine chat.
nyoka na wanyama wakali nazan wapo tu ukanda wa chini ambao ume contain msitu.
Mmasai ame sambaa kila mahali lakini kule kashindwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ule Mlima hautabiriki kabisa MKUU. Kuna mtu anaweza kupanda vizuri safari hii lakini mara nyingine akashindwa kabisa.
Ushauri wako unatija, kuna kitu wanaita acclimatization (kuwekwa kwenye mazingira yanayoendana kidogo na hali ya hewa ya mlimani), tulikaa Moshi mjini kama wiki moja kabla ya kupanda mlima. Walizingatia tumetoka Dar ambapo ni joto kwa hiyo yale mabadiliko ya ghafla yangeweza kufanya watu wengi wajisikie vibaya Zaidi na kushindwa kufika summit.

Jambo lingine la muhimu ni kampuni inayowaongoza, uzoefu wao unasaidia sana kufanikisha lengo la kufika juu. Ukifuata maelekezo yao, Maisha ni mepesi sana. Pia kuna tatizo la ki saikolojia, inafika kipindi unakua na mood bila hata kujua inatoka wapi. Nakumbuka kuna kipindi nilikua najiuliza kitu gani kimenifanya nije kupanda huu mlima? Uzuri, ni jambo ambalo nilikua nimejiwekea kwamba lazima nipande. Ilifika mahali wenzangu wakachoka wakaketi kujadiliana kwamba waishie njiani, nilipowafikia sikutaka kukaa nao, tungefarijiana kutokumaliza. Nilipita kama siwaoni, baadae na wenyewe walijivuta tukamalizia safari.

Unaweza kuwa unafanya mazoezi sana na bado ukakata pumzi, kinachotakiwa ni kuwa fit kiafya. Haihitaji nguvu sana au mazoezi mazito. Kuna jamaa wa Afrika ya kusini alikuwa mwanamichezo hodari sana, alipofika huko juu akaongeza mbwembwe anataka aongeze mwendo akimbie kimbie, alifia huko huko (2016). Hizo habari zilitufikia wakati sie ndio tunapanda tulikua kama siku ya tau au ya nne kufika kileleni.

Swali ambalo bado sijawahi kujibiwa ni ile gas huwa inatoka na watu mnakua wagonjwa au kuwa na hali mbaya wote, wanasema mlima unapumua, ina maana lile shimo la Volcano ndio linatoa gas au ni kitu gani? Na si tunaambiwa ile ni Volcano mfu? Haupumui kila siku, ila ikitokea mpo juu ukapumua mtakua na hali ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…