Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Ni kweli sio lazima ila ni good experience kama ya kung'oa jino bovu. Unafurahi likishatoka na ukipona. Ila kabla ukiwazia process unaweza kukubali uendelee na maumivu.

I was just in deep feelings, trying to understand the best part of it. Unfortunately most of the stories up there filled with hesitations and regrets. Life and Death...

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro.
Don't Try to give up...
 
SUMMIT NIGHT.


KUELEKEA GILMAS POINT

824dbcf3bbf8f2526bbd3ae7b07acce4.jpg



Mlima Kilimanjaro haupandwi mchana wala asubuhi ni mnapanda usiku.. yaani ile Mid night ndio safari ya kupanda inaanza. Mimi nakumbuka tulihimizwa kula haraka na kwenda kulala mapema. By Saa 5 sharp tunaamshwa... yaani nilijiona hata sijalala hata kidogo then muda huo.

Hapa unashauriwa kupanda Mlima na clean clothes kuanzia chupi hadi socks.. sijajua ni kwanini. Wakati naamka yule mzungu alielala chini ya kitanda changu wao ndio walikua wanaondoka. So naamka kivivu naanza kubadili nguo kuna baridi so nilikua naona kama mateso fulani cos inabidi nichojoe nguo zooote. Sim yangu ilikua full charged na nilikua na power bank maana nilitaka kupiga as many pictures as possible.

Katika group yetu mtu mmoja anashindwa kupanda Mlima.. Yeye aliishia Kibo hata alivyopimwa ikaonekana oxygen kwake itakua shida so bora abaki.. Na huko juu ndio kuna mgandamizo mkubwa wa hewa. Nikamuonea huruma. Huyu ni yule aliebebwa pia hadi kufika Kibo maana alishindwa kutembea.

Saa 7 kamili ndio tunaanza safari...Hii ni kosa kubwa tulifanya la kuchelewa kuondoka nadhani tulikua group kubwa la watu wengi kuchelea kutoka. lazima uwe na head tochi hio inakusaidia kuona usiku cos kuna mawe saana.. Chupa ya hot water..tulipangwa katika msururu mmoja.. Tukasisitizwa kutembea katika line bila kuachana wala kutoka katika mstari.. Wale ma Guide ndio walikua pembeni. Tukapiga sala ya pamoja pale then safari ikaanza.


Taratibu ule mstari ukaanza kuachia.. wengine wakaanza kubaki nyuma.. wengine katikati.. wengine mbele.. Mimi hapo mwanzo nilikua fresh.. yaani mambo mswano naona Uhuru ile inafikika fasta tu... Wale porters wanaimba nyimbo za kutuhamasisha kupanda Mlima.. Yaani wale jamaa wanafanya kazi kubwa saana. Mimi ile hali niliyokua nayo hata kunyanyua mdomo nilikua siwezi..


Kwa mbali unaziona tochi tu kwa juu yako.. I’m like I wish mimi ndio ningekua kule juu ama yatokee maajabu nipae hadi kule juu lakini ilikua haiwezekani ni lazima upande wewe mwenyewe.. Njia ya kuelekea Gilmans ni zig zag yaani mnakua mnazunguka na hii inachangia pia kuchoka na kutumia muda mwingiiii... kuna mawe mengi na makubwa pia so walikua wanasisitiza kuwa makini.

Nikaanza kuchoka.. Speed yangu ikawa ndoogo.. Nahema kwa shida kama mbwa alietoka kukimbia mbio ndefu halafu vile anakua anatoa ulimi wake nje kuhema ndio nilikua mimi... Muda mwingine ilinibidi kufungua mdomo ili kuweza kutoa na kuingiza hewa. There is very thin layer huko juu.... Mtu mwingine hali yake inabadilika inabidi arudishwe chini haraka sana. Na kunakua na team kazi yao ni kurudisha watu.. Akaanza kulia hataki kurudi.. She is like I came all the way then nirudie hapa SIRUDI.. nyie niacheni niendeelee.... wakifanya vipimo vyao wanaona hii ngoma ikipanda zaidi ya hapo ni atarudishwa akiwa mahututi ama kifo.. walitumuia Muda kum convince ndio akakubali. Wale ma Guide pia hawataki kuchukua risk za namna hiyo..Uruhusu mtu aende juu then akafie huko..... Kwenye 21 tukabaki 19

Nilikua sizungumzi na mtu ni macho tu ndio yanaongea. Yaani ukinitizama usoni unaweza kujua hata nini kinaendelea katika mind yangu... nikawa nawashangaa hata wale wengine wanapata wapi nguvu za kuimba... Tunatembea then kidogo mnasimama kupumzika.. Nilikua nakasirika tukipumzika kidogo hao tunaambiwa tunyanyuke tuendelee na safari. Kwasababu Mimi katika group ya watu 8 let say nakuwa mwishoni wenyewe wako mbeleni so wakati wao washapumzika mimi ndio nafika...Muda wa kupumzika unakua hautoshi.

Nilikua na usingizi wa kufa mtu yaani pamoja na lile baridi nilikua nikifumba macho huku tunatembea naona kabisa usingizii huo unanipitia... Guides walitusisitiza tujitahidi tusifumbe macho.. The thing is unaweza kupitiwa na usingizi then ikawa moja kwa moja. Kwa mara ya kwanza katika maisha niliona usiku ni mrefu... yaani hakukuchi kufike asubuhi

Kuna muda nikasimama nikaangalia chini nilikotoka naona Taa zinamulika yaani unaona kabisa mjini.. Nikaanza kujiuliza hivi mimi why did I come here?? Ili iweje?? Sasa hivi si ningekua nimelala sehem nzuri badala yake niko mlimani huku.. ningekua nakula vizuri badala yake nimekuja huku. Nikaanza kumuonea wivu yule tulimuacha KIBO. Nikaona si bora ningebakia zangu kibo nipumzike.. nilale weeee. Nikaona yeye kubaki was the best decision ever.


Kwenda Gilmans sio mchezo jamani.. na mnatembea usiku kwa usiku kuanzia saa 7.. ngoma ikagonga saa 10 mtu unatembea tu na haujui unafika saa ngapi..unaambiwa in one hour utakua Gilmans.. lisaa linapita hufiki..Naanza kukata tamaa... Nguvu ya ku Give up ikawa inakuja..Nikaona to hell with all these.. Ngoja tu nipoteze pambano nirudi zangu Kibo.. Then upande mwingine nafikiria hivi mimi I came all the way nije kukata tamaa hapa what if ni kipande kichache kimebakia then nitakua nimefika..


Asubuhi kunakucha na kupambazuka hatujafika Gilmas.. Fred mwanzoni nilikua nae lakini baadae kuna mtu katika group akawa hali yake sio nzuro ikabidi nimuache nae ili aje nae juu taratibu..

Kisa cha Bangi

Tukiwa njian tunaenda kuna hao wazungu tulikua nao sambamba.. Kuna sehem wakafika katika mawe makubwa kupumzika wakawa wanavuta sasa kaka mmoja (Alex nimpe hilo jina) tulikua nae group yetu wakamwambia you wanna try.. It helps a-lot.. Alex kihere here akajoin bila kujua hao wazungu ni wazoefu wa hizo mambo.... sisi hao tukaendelea mdogo mdogo.. Baada ya muda tukawaona hao wanakuja na wapo mwendo mkali kidogo zaidi ya wakwetu.. Na Alex alikua nao so akatuacha sisi akawajoin hao wazungu..


Nakumbuka kimoyo moyo nikasema ningejua ningejaribu hata puff moja mbona jamaa yetu kawa na nguvu.. So wakatupita.. Muda si muda nikashangaa Alex anarudishwa chini mzobe mzobe kabebelewa hali imekua tete hajiwezi.. Tukashtuka labda tushampoteza huko tukaambiwa he is okay ila he cant breathe well wanamrudisha huko chini akatafutiwa stretcher likamshusha. Baadae alivyokuka kutuhadithia nilicheka sana kumbe wenzake ni wazoefu wa zile mambo anasema alichungulia mlango wa kifo

Mida ya saa mbili kasoro nadhani ndio naingia Gilmas.. Sisi tumefika Gilmans kuna group nyingine walikua washafika Uhuru peak wanarudi chini.. Tulichelewa sana kufika Sikuamini aisee Nikawa naona kama muujiza fulani.. Tulivyofika tu wakatuwahi na maji moto. Jua liko vizuri ila the thing is baridi unaisikia hadi katika mifupa.




Sent from my iPhone using JamiiForums

Nikiwa Gilmans

29ebfa60118c2c475ae9132664cd7062.jpg


Japo sim yangu ilikua full charge ukiwa juu ikazima kabisa kwamba battery empty. the last picture I took with my phone


40c7062c34b9a820756b5e9342e2d9c6.jpg


Tulikua tunatembea namna hiyo

10d184e1216887a442a07b5e2fe05ea5.jpg


Hapa ukiwa maeneo umya Juu Gilmas ukiangalia tulikotoka kule chini

4c00e27f62e7db0468d8e1ff7db5dc6d.jpg


3c45e6688ea9cb7a5b206c08aed9e104.jpg



Sent from my iPhone using JamiiForums
Dahhhh yaan ulifika juu ukakaaa dakika moja tu.....? AISEE ulikosea sana atleast mngekaa for ten minutes mkarud.. mkaenda Mpk kwenye lile shimo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja niongeze bidii ya kuwafaham wana JF nje ya humu!! Wewe nimeona kwenye thread fulani chimbo lako... Kuna siku ntapita hapo kimyakimya nijionee na kuunga mkono juhudi zako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kipindi cha nyuma kuonana ilikuwa kawaida
Ila kwa sasa ni changamoto
Refer threads zinazoletwa baada ya watu kujuana huko nje!!
 
Although funny may be a bit challenging, bado hofu ya kufa premature ni kubwa aisee japo nimezaliwa na kukulia Rombo ila hali aliyoielezea sijawahi kuipata. Inatisha kidogo japo inafurahisha na kutia moyo. Pia nimejifunza huruhusiwi kukaa zaidi ya dakika 5 kileleni. Cha kujiuliza je wanaopanda Everest mrefu kuliko huu inakuaje kwenye suala la hewa?. Ukiichukulia kama adventure ni nzuri ila ukweli ni kama kuingia theater nusu kubaki hai nusu kufa aisee.
Mkuu niliwahi kwenda Uhuru peak na nikakaa zaidi ya dakika kumi, mara nyingi huwa inategemea sana na hali ya hewa ya kipindi hicho.
 
Kwa story nlizozikuta kwa tour guider wetu jamaa hakutoboa na hakuanzia chini alipanda kwa helicopter mpk kibo then ndo akaanza safari ya kwenda uhuru na alikua na walinzi wake si chini ya wa5 na wasaidizi wabongo so kipindi wanapanda wale wasaidizi wake wabongo ndo walimwona kua hali yake siyo nzuri ndo ikabidi wamzuie kuendelea akashushwa chapchap then akarudi UK baada ya muda hawa wasaidizi wabongo ikabidi awaite UK walikaa wiki moja akawashukuru kwa kuokoa maisha yake akawapa na mpunga then wakarudi bongo sasa cjui ilikua story tu au ni kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Helicopter haifiki Kibo kabisa...inaishia mita kadhaa kabla ya kibo.
Kumbuka mwinuko wa kibo hut ni 4700m.
 
SAFARI YA KUSHUKA MLIMA..

71e42ea7ef4312fde77d882c8c3243de.jpg


Kule juu hatukuchukua muda tulianza kurudi kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.. Nilikua nimechoka saaaaana. Tukatembea weee hadi tukafika Gilmans. Uzuri wa kushuka ni unaenda straight hakuna mambo ya kusema upite zig zag mle mle katika njia unapita tu.

Nilivyofika Gilmans nikaanza kushindwa kutembea miguu ikagoma kabisa..nikitembea dakika moja nyingi naishiwa nguvu nasimama au nakaa. Huo muda Fred alikua ameshashuka chini kwani yule mwenzetu niliemuacha nae aliishia Stella so alimrudisha chini. This time nikawa ma guide mmoja mtu mzima anaitwa Moses no comment on him but... Nikamkumbukaje Fred hapa angekua ananibembeleza [emoji23]

Nikaanza kulia.. kushuka ni rahisi ila mimi nilikua nimeishiwa nguvu. Kuna muda nilikua nakuangali kule juu najiuliza hivi mimi niliwezaje kupanda juu halafu hapo najisemea hata unipe bilion moja hunirudishi huko juu mimi...

mzee Moses ananisisitiza nijitahidi nishuke ananiambia Kibo ni pale tunafika sasa hivi wewe jitahidi..Na kweli naona vibanda vilee najipa moyo mwenyewe nanyamaza then naendelea kutembea.. Nikitembea kidogo nachoka nakaa tena naanza kulia. It was a mixed feeling... halafu pia nilikua nimeikumbuka familia yangu.... Tukipishana na watu wananipa pole kama zote.... Nikaishiwa nguvu siwezi kutembea mwenyewe so akawa ananishikilia ndio naweza kutembea.... Tumeshikizana wee Kufika sehem I couldn’t walk at all yaani hata kusimama mwenyewe nikawa siwezi... Hata nikijaribu vipi nashindwa.... ilikuja stretcher kunibeba na kunirudisha Kibo.

Wakati tunaelekea Kibo nilishangaa porters wengi wanapanda kuelekea mlimani. Nikawa najiuliza hawa jua lote hili ndio wanaenda kupanda Mlima nikauliza akanambia wanaenda kupokea watu wanaotoka mlimani. Wengine ndio hao wanarudi na hali kama ya kwangu.

Ukifika Kibo yaani wanakuhudumia vizuri hapo.. Nikapewa chai.. mara soup ya moto.. Tukaambiwa tupumzike kidogo tukiamka tunaanza safari ya Horombo. Ngoma hailali. Nikamuwazia yule mzungu aliefariki.. Nikasema silali wala nini nitakaa macho hadi hiyo time ya kurudi Horombo.. Nisije kufia usingizini. Ila Chezea usingizi na uchovu nilikuja kushtuka naamshwa nikale.. I wish niweke picha moja niliyopigwa wakati nimelala... I was half dead.. chakaram.

ku pack vitu was a headache.. Na ilitupasa tufanye haraka maana hizo domitories kuna wageni wengine walikua wamefika so inabidi waingie.. Saa 8/9 tunaaza safari ya kurudi Horombo.. Usingizi ulinisaidia sana huku nilikua poa njiani tunapiga story kwa saaana na wala sikua na uchovu mkubwa sana.. Rohoni kwangu najisikia safiii. Horombo nawahi kufika mapema kushinda hata wale wengine..Kuna baadhi ya watu walienda kuoga mimi sikuoga wala nini.. Nilisema hadi nifike mjini.. I want hot shower nikae hata lisaa bafuni.

Horombo tunalala then kesho asubuhi inaanza safari ya kurudi Marangu getini. Kabla hatujaondoka hapo Horombo tuliimbiwa nyimbo nadhani kama ni utamaduni fulani.. Nili enjoy saana zile nyimbo.. tukacheza pale.. Mimi na wenzangu 3 tulirudi Marangu getini na ambulance. Asubuhi ile Guide kama kuna mtu katika watu wake hayuko vizuri kuna gari linakuwepo for emergency kuwarudisha getini.. So wengine wanatangulia kwa miguu sisi tunabakia kusubiri gari...

Katika Ambulance kuna waarabu fulani ambao niliwakumbuka vizuri wakati wa kupanda kuanzia Mandara tulikua wote benet.. nao wanarudi kwa ambulance na mchina mmoja. Wale waarabu wa 4 they told us kwamba only 1 of them was able to reach the peak.. huyo mwanaume wale wadada hawakufika.... Mmoja wao alikua anatapika saana... alikua analalamika kuumwa... walituambia wametokea UAE.. Kurudi na gari was another experience..

Ile asubuh tulipoamka Horombo ndio tulianza kushangaana sura zetu [emoji23][emoji23] ni pua zimebabuka... ngozi haiko sawa.. ukimuangalia mwenzako unaweza kujiona wewe una afadhali na mwenzako nae akikuangalia anajiona yeye ana afadhali.. Sisi ndio tunakua wa kwanza kufika tunasubiria wenzetu waliokuja.

Final Goodbye na Porters

Tunapata wasaa wa kuagana na crew ya Origin pale Marangu getini maana baada ya hapo tulikua tunaenda hotelini na wengi wao wasingeweza kuja kule.. It was very sad. Its only few days we stayed in Kili but the bond we had shared with those people was so strong... Watu walilia saana...

Tip tulichangishana tangu mwanzo elfu 75 each.. na mwanzo tulipanga kila mtu achangie laki wengine wakaona laki nyingi tufanye 75... Maana tayari tulishalipia fedha.... ila baada ya kupanda mlima na kuona kazi wale watu wamefanya we all thought kwama 75 haikua pesa.. It was nothing compared na service walitotupatia kule juu. Ile pesa waligawana katika group. Sisi hatukutaka kila mtu ampe tip mtu mkononi kivyake.. maana kuna mtu wa jikoni yeye humuoni unashangaa tu chakula mezani.. kuna mtu anaebeba bag yako humuoni ila muda wote ukifika point fulani unaletewa bag liko salama. So kuna wengine hatu interact nao ila tunapata service yao. Wao wenyewe walijua waligawana vipi ile pesa.

Nilichukua mawasiliano na Fred.. Alinambia hataweza kuja hotelini.. na mpaka kesho kutwa huwa tunawasiliana ingawa most of the time anakua hapatikaniki yuko mlimani.. Nilimpatia tip yake personal tofauti na ile ya group na pia vifaa vingi nilivyonunua kwa ajili ya kupanda mlima nilimuachia.. Alishukuru sana. Pia alinambia ataenda kusomea mambo ya u guide kuna chuo huko.. Kwasababu yeye ni porter na ili uwe guide inabidi upate cheti... So kitu ambacho nimepanga ni kumsaidia part ndogo ya ada.. Mimi sio tajiri maisha yangu ya kuunga unga but what he did kwangu ni wema na utu wa hali ya juu. He was extremely caring. Very understanding.... Maybe that is the only way I can repay him.. Mara kibao huwa namwambia yeye ni mtu poa saana.

Tunarudi Hotelini.. Hiyo ndio siku kulikula misosi tunayopendelea.. It was a celebration evening.. Hiyo siku nilitumia karibu saa nzima kuoga.. maji ya motoooo... I was so relieved... Jioni tukagawiwa certificates wenye kunywa bia ndio walizinywa hapo na pia nilipata nafasi ya kuonana na kiwatengu kwa mara ya kwanza na nitumie nafasi hii kumshukuru kwa ushauri wake na moyo wa kunisaidia mpaka nikafanikisha safari yangu Kilimanjaro.

Wengi wetu tulipata na ganzi katika mikono siku zile za mwanzoni lakini baadae iliishia taratibu.

We came back to DSM safely with a lot of great memories. Climbing Mt Kilimanjaro to the peak is something that I will hold close into my heart. My trip was very eventful and joyous, I met new people who were very generous and down to earth like Fred.. they took care of me as if I were their own child/sister, I came across various obstacles, I strived for the best and most importantly I achieved my goal. It’s unreal how we became so attached with guides/porters in such a short period of time. I journeyed through pain, laughter, suffering, dirtiness and Mr Peters famous porridge and soup.(ambayo ilikua huwezi kukwepa kunywa)

I had the greatest moments and created incredible memories which will remain in my mind and heart forever. As they say nothing comes easy and it’s true, It wasn’t easy at all but I did it... One thing I learned is to appreciate everything this life offers.

I thank God for protecting me all the time, My Mother for her support.. My group mate who not only made the trip funny but also easy,.....Mr Emmanuel & Origin Team for for this wonderful journey[emoji92]

My family & Friends made this for Us..

80a1aea0e82016378de52fa15f5dd06e.jpg


The Team behind our success

28135f6fadaf143b68a13658755970bf.jpg


Going back to Horombo

8c6fd52e073b6e6758d8a5cbbf46ecb0.jpg


Last picture @ Kibo

bd15f5493f3ad6121c40f423cd68be42.jpg


I bought so many things pale Marangu Getini. Hii na i dedicate kwa wote ambao wanasema hawawezi kupanda Mlima

6ea49fb4301c3a3c19cbfaa139eae9f8.jpg




THE END


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ntakutafuta..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom