Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lin mzee baba nyinginDO NOT SHOUT
(usipige kelele)
Sehemu ya......... 9
Mtunzi: Saul David.
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA....
Akiwa bado anacheza Caren aliandika ujumbe kumjibu Yusto huku akitabasamu
'Vp umelal, samahn kw chlew nlikuw bze kdg, mmm hyo zawad nikkuomb utanpa dady[emoji6][emoji6]'
ENDELEA...
Yusto alikuwa bado anaendelea kumshangaa Caren anavyocheza akiwa amevua nguo na kubaki na nguo za ndani pekee, hali hii ilizidi kumuweka Yusto katika wakati mgumu, akajikuta suruali yake inapanda taratibu baada ya mwanajeshi wake kusimama akimkumbusha kuwa yeye ni mwanaume kamili.
"Oooh shit, nini hiki" alisema Yusto huku akijiangalia namna alivyokuwa amesimama imara, wala haikuwa kosa lake hii ingemtokea mwanaume yoyote aliyekamilika kutokana na namna Caren alikuwa ameumbika haswaa.
Yusto alijaribu kubana miguu yake ili mambo yasiharibike zaidi. Wakati akifanya hivyo mara simu yake ilitoa mtetemo baada ya ujumbe mfupi alioutuma Caren kuingia kwenye simu yake. Mtetemo huo ulimshtua Caren aliyekuwa bado anaendelea kucheza mziki, akashtukana na kusimama ghafula, haraka akaenda kuzima redio yake.
Alitulia kimya kwa sekunde kadhaa huku taratibu akiangaza macho yake huku na huku,
"Au nimesikia vibaya" aliwaza Caren huku roho yake ikimwambia hapana kuna jambo mle ndani.
Caren alichukua ile tochi yake akawa ananyata taratibu hadi mlango wa kuingilia bafuni na chooni. Akiwa mlangoni Caren alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu kisha akafunga mlango kwa kasi huku akitanguliza mwanga wa tochi.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Baada ya Frank kuhisi kuwa huenda yule mtu alieyemuona anapotelea gizani alikuwa ndiye haswa aliyesababisha kutoweka kwa umeme chuoni hapo. Kwa kuwa tayari walishahisi kuwa kuna mtu anasababisha matukio hayo ya ajabu ili kuchafua jina la chuo hicho alianza kumfuatilia yule mtu akiamini huyo ndiye muhusika wa matukio yote yanayoendelea hapo chuoni.
Giza lilikuwa ni kubwa mno hali iliyomfanya Frank kutembea kwa tahadhali kufuata uelekeo aliopotelea yule mtu.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Caren alifungua mlango kwa kasi hali akiwa ametanguliza mwanga wa tochi yake, aliangaza huku na huku, bafuni na chooni lakini hakuona chochote.
Mwisho alitoka, akafunga mlango kisha akachukua simu yake kujitupa kitandani akaamini hali ilikuwa shwari.
Aliangalia kama huenda Yusto akawa amejibu sms yake lakini haikuwa hivo, akaitupa simu yake pembeni kisha akachukua mto wake akalala kifudi fudi na kutulia akiwa amefumba macho yake.
Sura ya Yusto haikumtoka akilini, akawa anakumbuka tangu walivyokutana kwa mara ya darasani na mwanaume huyo ambae taratibu alianza kumjaa moyoni.
Caren alijikuta anatabasamu hali akiwa amefumba macho yake, vidipo vidogo vikajitokeza kwenye mashavu yake na kumfanya aonekane mrembo zaidi.
Dakika mbili baada ya Caren kutoka bafuni wakati akikagua, Yusto alionekana akiwa amejishikiza juu kwenye sing board hali akiwa amekanyaga ukuta huku na huku na kutawanya mikono yake. Laiti tu kama Caren akemulika juu angemuona, ama kwa hakika bahati ilikuwa upande wake siku hiyo.
Yusto alishuka kwa ufundi mkubwa bila kutoa sauti au mtikisiko wowote, alionekana ni mtu mwenye mazoezi ya kutosha.
Alikaa chini na kunyosha miguu huku akipiga hesabu afanye nini kutoka mle ndani.
Alipojitazama kwenye suruali bado mwanajeshi wake alikuwa amesimama imara kama awali.
Yusto alijikuta akiachi tabasamu kidogo.
Haraka aliikumbuka simu yake iliyotaka kumuingiza matatizoni, akaiweka 'silence' kisha akafungua kuangalia sms mbili alizotumiwa.
Moja ilitoka kwa Caren nyingine ilikuwa kutoka kwa Sophia.
Yusto aliifungua kwanza sms ya Caren upesi.
Vp umelal, samahn kw chlew nlikuw bze kdg, mmm hyo zawad nikkuomb utanpa dady[emoji6][emoji6]
Yusto alitabasamu kiasi kisha akawa anawaza ajibu nini, wakati huo alirudi kutazama sms ya Sophia.
Yusto kwa ajili yako nitapoteza heshima yangu, kwa ajili yako nitafanya lolote liwe baya au zuri ili nikutoe akilini, naomba usiniulize wala kunijali kwa chochote niacheee, mpaka pale utakapo heshimu na kukubali hisia zangu kwako'
Huu ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Sophia, mwanamke aliyeonyesha kumpenda sana Yusto na tayari moyo wake ulikuwa umejeruhiwa vibaya baada ya kuanzisha mahusiano na John mwanaume ambae hakuchoka kuutesa moyo wake.
Yusto alijikuta anapoteza mudi, akawa anamuwaza Sophia binti mrembo ambae kwake alimchukulia kama rafiki yake kipenzi, hakuwa tayari kumuona anateseka, lakini angefanya nini, ni swali alilojiuliza bila ya kuwa na majibu.
Yusto alionekana mwenye mawazo kibao, alirudi na kuitazama sms ya Caren, kisha akajisikia kumjibu.
'Yap sijalala bado am bored sijapata ucngz'
Caren aliyekuwa ameanza kupitiwa na usingizi alikurupuka ghafula baada ya sms kuingia kwenye simu yake akaamini lazima atakuwa ni Yusto. Ni kweli ilikuwa ni sms kutoka kwa Yusto, akaisoma haraka haraka na kuijibu
hapo wakaanza kuchat, mmoja akiwa kitandani mwingine akiwa bafuni ndani ya chumba kimoja.
Walisahau kabisa majukumu yao, kwani Yusto alikuwa ni kijana aliyeajiriwa kama mlinzi wa Siri wa chuo hicho akijifanya mwanafunzi, wakati huo Caren akiwa ni Agent aliyetumwa chuoni hapo kuja kufanya matukio ya kuchafua sifa ya chuo.
Waliendela kuchat....
'Ooh kama mim tu niko bored pia that's y sijalal yusto'
'Pole nn shida mumy'
Mmh nambie wew kwnz nn shda'
'Teh teh siwez kukwambia nw bna had nikiwa okay'
'Mmh so'
"Kama wot kutok bored bas twend sehem tukarefresh'
'Ooh my God, nw?
Yes now if possible'
Real?
Yap let's go
Okay najianda chap nakuj,'
Fresh utanikuta getin'
Pow dk 0'
Caren alikurupuka kutoka kitandani haraka akaanza kujiandaa, Yusto alirudi tena pale juu akiamini labda Caren angeingia kuoga lakini haikuwa hivo, dakika tano baadae alisikia harufu ya marashi makali na mara mlango ukafunguliwa na kufungwa, tayari Caren alitoka.
Yusto nae alishuka upesi upesi hali akiwa mwenye tahadhali akatoka kwenye chumba cha Caren na kundoka.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Dakika tano baadae Caren alikuwa amesimama kwenye geti la kuingilia chuoni, mara Yusto akatokea nyuma yake huku akikimbia, tayari alikuwa amebadili mavazi yake na kuvaa mavazi ya mtoko.
"Ooh sor nmechelewa"
"Usijal" alisema Caren huku wakitazama usoni kisha wakatabasamu kwa pamoja.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Walianza kutembea kulielekea geti.
Katika chuo hicho hakukua na sheria yoyote inayowazuia wanafunzi kutoka nje wakati wowote, muhimu usikose vipindi vya darasani.
Wakiwa bado hawajafika getini mara walishangaa kuona mlinzi anafungua geti,wakahisi labda amewaona wakiwa mbali lakini haikuwa hivo, baada ya kupiga tu hatua kadhaa uso kwa uso wanakutana na Sophia akiwa na Jonh wanaingia chuoni huku wameshikana mikono.
Wote walitoa macho kwa mshangao si Caren si John, si Sophia wala si Yusto, hakuna aliyetegemea....
Je, nini kitafuata...?
KWA NINI JOHN YUPO NA SOPHIA?
JOHN ATAFANYA NINI HALI ANAMPENDA CAREN?
VIPI KWA YUSTO NA SOPHIA?
Tukutane sehemu ya 10....
Nimecheka kwa sautYusto ni NGOSWE aliyechangamka[emoji16][emoji16][emoji16]
Hahahah!kwamba huyu ni ngoswe wa chuo kikuu, yule alikua wa kijijiniYusto ni NGOSWE aliyechangamka[emoji16][emoji16][emoji16]
Mbna unarudia ileileDO NOT SHOUT
(Usipige kelele)
Sehemu ya.............12
Mtunzi: Saul David
Whatsapp: 0456862047
ILIPOISHIA...
Caren na Yusto wanafunzi wa chuo kimoja maarufu nchini Tanzania wanajikuta wakizama kwenye penzi zito lililoibuka kati yao huku kila mmoja akiwa na kazi yake tofauti iliyomleta chuoni hapo. Caren ni agent wa Siri aliyetumwa kufanya matukio yatakayochafua sifa ya chuo hicho. Wakati huo Yusto yeye ni mlinzi wa Siri aliyeajiriwa na mmiliki wa chuo hicho akiwa kama mwanafunzi.
Usiku, majambazi wanavamia club moja na kutaka kukata kiungo cha mtoto albino, Caren na Yusto wakiwa ni miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya club hiyo hawako tayari kuona tukio hilo linatokea mbele yao...
SASA ENDELEA...
Wimbo ulokuwa ukiimba uliisha na sasa Amapiano ya diamond - IYO, ilianza kuimba.
Caren na Yusto walitazama kwa mara nyingine kisha kila mmoja akatoa ishara kuwa yuko tayari.
Sekunde chache baadae varangati la aina yake lilitokea ndani ya ile club. Caren na Yusto wote walikuwa wamepitia mafunzo ya upambanaji hali iliyopelekea kuweza kuwamudu vizuri wale majambazi. Hakuna aliyeamini kinachoendelea watu 14 walijikuta wanashindwa kufua dafu kwa watu wawili, istoshe mmoja alikuwa mwanamke.
Pamoja na kutumia mapanga walio kuja nayo lakini bado hali ilikuwa ni ngumu kwao kuwakabili mafia hawa wawili.
Kuna wakati walitishia kufyatua risasi lakini haikusaidia kitu kwani tayari Caren na Yusto walishaambizana kuwa siraha hizo zilikuwa ni fake.
Dakika 5 zilikatika bado hali ilikuwa ileile, familia ya yule mtoto albino walijikuta wanashuhudia muujiza huo ambao ama kwa hakika ulileta tumaini la kumnusuru kijana wao albino. tayari walikuwa wamepata nafasi ya kupiga simu polisi.
Dakika 6 baadae ving'ora vya gari za polisi vilianza kusikika jirani kabisa na eneo hilo, baadhi ya majambazi waliokuwa hawajajeruhiwa sana waliinuka na kuanza kukimbia lakini wengi wao walibaki hali wakiugulia kwa maumivu kamali waliyoyapata.
Caren na Yusto walikonyezana kisha nao kwa pamoja wakakimbia na kutoka nje ya club ile, tayari walishatoa msaada uliohitajika hawakutaka tena kuingia kwenye purukushani na polisi, walichukua tax kisha wakarejea chuoni kwao ikiwa ni saa tisa za usiku.
"Huyu ni nani, kajifunza wapi kupambana, ule uwezo hapana sio wa kawaida" haya ni maswali ambayo wote wawili walikuwa wakijiuliza bila majibu wakiwa wamejilaza kitandani muda mfupi baada ya kurejea chuoni.
Caren alishamtilia shaka Yusto vivyo hivyo Yusto alishamtilia shaka Caren. kila mmoja akatamani kumjua mwenzake zaidi kwa ajili ya usalama wa kazi yake. Licha ya kuwaza hayo yote penzi lililoanza kuchipua kati yao ndio lililoonekana kuchukua nafasi zaidi kati ya wawili hao Yusto na Caren.
****
Asubuhi ya siku iliyofuata, Yusto alishtushwa na makelele yaliyokuwa yakipigwa na wanafunzi wa chuo hicho. Alikurupuka usingizini na kutazama saa yake, ilikuwa ni saa nne asubuhi.
Haikuwa kawaida yake kulala kwa kiasi hicho lakini kutokana na shughuli ya usiku alijikuta analala fofofo akiamshwa na makelele ya wanafunzi.
Alijifunga taulo lake akasogea dirishani kisha akachungulia nje kuangalia ni nini kulikuwa kinaendelea.
Alishangaa kuona wanafunzi wengi wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi za chuo hicho huku wakiwa wanapiga kelele na wengine wakiwa wamebeba mabango mkononi.
Wakati akiwa katika hali ya kushangaa asielewe kinachoendelea,
mlango wa chumba chake uligongwa. Haraka akaenda kufunga.
"Frank" aliita Yusto
Frank aliingia bila hata kuzungumza chochote akaenda na kusimama pale dirishani akawa anatazama nje.
" Nini kinaendelea Frank" aliuliza Yusto
"Nikulize wewe, nini kinaendelea" Frank alirudisha swali lake huku akigeuka na kumtazama Yusto kwa hasira, akaendelea kuzungumza.
"Yusto Jana usiku tumepeana majukumu, badala ya kufanya kazi umeondoka na kwenda klabu cha ajabu zaidi umeenda na Caren mtu ambae tunamuhisi kuwa ndo chanzo cha matatizo hapa chuoni. Unajua nini kimetokea Jana eti, unajua? Usiku sio mimi niliekata umeme, Kuna mtu alifanya hivyo kwa makusudi, nilimuona nikamfuatilia bila mafanikio,
na hadi sasa kuna shoti kila mahali hapa chuoni kila wakitengeneza shoti inatokea hatujui tatizo nini, wanafunzi wameandamana kwa sababu wamechoshwa na haya mauza uza kila siku, tunafanyaje Yusto tunafanyaje, bosi akipata hizi taarifa hatuna kazi sisi"
Frank alizungumza kwa machungu mno.
Taarifa hizi zilikuwa ngeni tena zilionekana kumshtua sana Yusto,
hakuwa amewaza kabisa Kama hali ingekuwa Kama ilivyo sasa.
Mbaya zaidi alizima simu yangu jana na usiku alipotoka na Caren hadi dakika hiyo hakuwa ameiwasha.
"Unamahusiano na Caren? " Aliuliza Frank, Yusto akawa kimya.
"Nakuliza unamahusiano na Caren?"
ITAENDELEA.....
SIMULIZI HII INAPATIKATA YOTE , WASILIANA NAMI KUPITIA NAMBA HII,,, (call/Whatsapp)
+255756862047