DO NOT SHOUT
(usipige kelele)
Sehemu ya..............17
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Email: saulstewarty@gmail.com.
ILIPOISHIA ...
Kwa mbali alionekana Brandina anaenda zake mabweni ya wanaume kwa ajili ya kwenda kuzungumza na Yusto lakini alisimama ghafula baada ya kumuona Caren kwa mbali, haikuwa sura ngeni kwake kwani tayari alikuwa na picha zake. akatamani kujua anafanya nini wakati huo, akaanza kuwasogerea pale waliposimama na Sophia.
SASA ENDELEA ...
Caren na Sophia walikuwa wanatazamana huku kila mmoja akiukumbuka ule usiku walipokutana Caren akiwa na Yusto na Sophia akiwa na John.
"Habari" Caren alivunja ukimya
"Si nzuri Caren, nina shida na wewe ndio maana niko hapa" alisema Sophia huku akimsogelea Caren kwa ukaribu zaidi kisha akaanza kuzungumza
"Caren Mimi kama mwanamke mwenzio niko hapa kwa ajili ya kukuomba unisaidie jambo moja, ni kuhusu Yusto. Sijui ni nini kinaendelea kati yako wewe na Yusto lakini nataka nikwambie kuwa Yusto ni mwanaume wangu, ndoto zangu zote nimezielekeza kwake, Mimi na yeye tumetoka mbali mno tumekuwa tukiishi kama marafiki lakini ukweli tunapenda sana. Yusto hajawahi kuwa na hisia za kimapenzi na mimi lakini kama mwanamke nimekuwa nikipambana kumfanya anipende hivi karibuni jitihada zangu zilianza kuzaa matunda Yusto alianza kuzielewa na kuziheshimu hisia zangu kwake. lakini ghafula umekuja wewe Caren, ujio wako umevuruga kila kitu, yaani kila kitu. tulikuwa tumepiga hatua tatu mbele lakini wewe umeturudisha hatua kumi nyuma. Caren nakwambia yote haya ili unionee huruma mimi kama mwanamke mwenzako, bila Yusto mimi si chochote, nakuomba nakuomba sana Caren niachie Yusto wangu"
Sophia alikuwa akiongea kwa uchungu mkubwa mno kiasi cha kumfanya Caren amatazame kwa jicho la pekee.
Ni kweli Sophia alimaanisha kile alichokisema, lakini ilikuwa ni ngumu sana kwa Caren kufanya hivyo, tayari moyo wake ulishaanza kuota mizizi kwa penzi la Yusto, kumtoa ghafula tena haikuwa ni kazi rahisi hata kidogo.
Ni kweli Sophia alionekana kuhitaji msaada lakini angefanya nini sasa ilihali na yeye pia anampenda Yusto.
Caren alijikuta katika hali ya kujiuma uma asijue atamjibu nini Sophia. Sophia nae aliendelea kumtazama Caren usoni akihisi ni lazima atasema neno lolote angalau kumfariji.
Caren hakuwa na la kusema kabisa, alishindwa hata kumuangalia Sophia usoni. Akawa anawaza na kujijibu mwenyewe.
'''
_hapana Caren usimuonee huruma, usikubali kumuacha Yusto, ni mwanaume wako tena anakupenda""
Aliwaza Caren.
Mwisho akamua kuondoka bila kujibu chochote. Hakufika mbali Sophia alimkimbilia na kumshika begani akamzuia asitembee.
"Inamaana hujanisikia Caren, inamaana nilichoongea umeona ni upuuzi Caren kweli" alisema Sophia safari hii chozi likamdondoka,
Caren alimtazama usoni kwa masikitiko huku roho yake ikimuuma pia, hakutaka aendelee kujiumiza zaidi.
Akaanza tena kuondoka huku akiutoa mkono wa Sophia begani kwake lakini Sophia alimng'ang'ania kwa nguvu kiasi cha kufanya aichane nguo yake.
Caren alipigwa na butwaa baada ya kuona nguo yake imechanwa kiasi cha kufanya bra aliyovaa ndani ionekane, aligeuka haraka na kumsukuma Sophia kwa nguvu akadondoka chini.
Kilikuwa ni kitendo ambacho Caren hakuwa ametarajia kukifanya ilitokea tu ghafula, Sophia alianguka chini vibaya mno akaumia mguu wake.
"Hey hey hey ninyi vipi" mara sauti ya mwanamke ilisikika nyuma ya Caren
Caren akageuka kuangalia ni nani, hakuwa mwingine bali Brandina jasusi mkenya aliyekuwa chuoni hapo kwa kazi maalum. Kwa muonekano wake wala usingezani anafanya kazi hiyo hatari na ngumu. Brandina alikuwa mrembo haswa na alijua kutunza urembo wake.
"Wewe, ni nini kumsukuma mwenzako hivyo bila hata haya, vipi kama ukimuumiza" alisema Brandina huku akimsogelea Caren.
Caren alibaki kimya bila kuzungumza chochote akawa anamtazama Brandina akizidi kumsogelea na mwisho akafika karibu kabisa wakawa wanatazamana uso kwa uso.
"Nakuliza unaniangalia nini" alisema Brandina huku akilini mwake akijua ni nini anafanya jasusi huyu.
"Don't try me, better to ask before judging" (usinijaribu, ni vema kuuliza kabla ya kuhukumu).
Caren aliongea kwa kiburi kisha akampisha Brandina na kuondoka zake.
Hali akitabasamu Brandina alimsindikiza Caren kwa macho hadi alipopotelea jengo la hostel (bweni).
"She is smart" (yuko vizuri)
Alisema Brandina akiwa tayari amepata jibu la alichokuwa anakitafuta kwa Caren. Hii ilikuwa ni moja ya mbinu za kijasuji kusoma saikolojia ya mtu.
Brandina aligeuka na kumtazama Sophia pale chini, akamsogelea na kuchuchumaa pembeni yako.
"Pole mpenzi umeumia" alisema Brandina.
"Asante dada, mguu kidogo umeshtuka, watu wengine bwana, nasema atalipa kwa hili, lazima alipe" Sophia aliongea kwa hasira kiasi.
Brandina aliyekuwa pembeni yake alijikuta anatabasamu.
""
Wewe ndo utakuwa kete yangu ya kumpata Yusto,,, oooh mwanaume anabahati huyu inakuwaje tukampenda wote watatu"""
aliwaza Brandina huku akitabasamu akawa anamsaidia Sophia kunyanyuka pale chini.
"Naitwa Brandina, ni mpishi wenu mpya hapa chuoni"
" Ooh kumbe, wageni wengi hapa chuoni na ulivyo ulivyo nikajua wewe mwanafunzi mwaka wa kwanza"
"Noo, mimi ni mpishi tu bana,"
"Karibu sana eti"
"Asante dia"
Alisema Brandina hali wakiwa wameshikana mikono na Sophia.
ITAENDELEA...
==>Mambo yanazidi kukolea
==>Mapenzi bado ni changamoto kwa vijana hawa watano Caren, Sophia, Brandina, Yusto na John
==>Nani ni nani na nani ataibuka mshindi?
===>John/brandina atafanya nini?
===>Vipi sekeseke lililopo kati ya Frank, Yusto na majasusi dhidi ya Caren.
ENDELEA KUFUATILIA MKASA HUU WA KUSISIMUA....
Njoo Whatsapp kujipatia simulizi hii hadi mwisho ( ep 80) kwa Tsh 2000 tu.
0756862047