DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)
Sehemu ya..............20
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Email: saulstewarty@gmail.com.
ILIPOISHIA...
Majasusi wanafanikiwa kuidukua simu ya Caren ikiwa ni katika harakati za kumpeleleza ili kujua kama ni kweli Caren ndiye agent anaehusika na matukio kadhaa yaliyotokea chuoni.
Yusto nae akiwa na pamoja na majasusi hao anaradhimika kuifanya zaki yake lakini moyoni akiwa bado anampenda Caren.
Je, nini kitafuata?
SASA ENDELEA...
Jasusi Simigo na Brandina waliendelea kusubiri huku wakiwa wameelekeza macho na masikio yao kwenye compyuta kufuatilia kila kitakachoendelea kwenye simu ya Caren.
***
Caren akiwa chumbani kwake alionekana kukosa raha kabisa, matukio kadhaa yaliyotokea siku hiyo yalimuondolea mudi kabisa.
Kwanza alikutana na John kijana anaelazimisha kuwa na mahusiano nae, na mara kadhaa amekuwa akimpa vitisho kuwa atamfanyia kitu kibaya Yusto kama tu ataendelea kuwa nae.
Pili amekutana na Sophia ambae anaonyesha kumpenda sana Yusto na yuko tayari kufanya chochote ili ampate, hali inayopelekea wao kuwa kama maadui.
Tatu na kubwa zaidi ni suala lake la mahusiano na Yusto. Kwa taratibu na sheria za kazi anayoifanya Caren hakuwa akiruhusiwa kuwa na mahusiano na mwanaume yoyote, lakini tayari Caren alishavunja sheria hiyo na kujikuta anaangukia penzini na kijana Yusto. Anashindwa kujizuia kabisa kutokana na msukumo wa sihia dhidi ya kijana huyo zinazotoka ndani kabisa ya moyo wake. Pasipo kujua kuwa Yusto alikuwa ni mlinzi wa Siri wa chuo hicho na hii ilikuwa ni hatari kwake kama Yusto atagundua.
Caren anatiwa upofu na mapenzi.
Wakati akiwa bado kwenye dimbwi la mawazo mara simu yake iliita na haraka Caren akaipokea, ilikuwa ni namba ya rafiki yake ambae pia ni agent wanaefanya kazi moja ya kuangusha biashara za bosi Mark moon.
Wakati Caren akiipokea simu, Simigo na Brandina nao tayari walinasa mawasiliano haraka wakavaa headphone kubwa masikioni wakakaa wa kutulia ili kufuatilia mawasiliano hayo kati ya Caren na namba iliyompigia
"Hallo best"
"Yes Caren habari"
"Ni nzuri kiasi ndugu yangu vipi huko"
"Huku kwema, vipi kuna tatizo"
"Ndiyo rafiki angu, mwenzako nimenasa huku"
"Umenasa kivipi, au umeharibu kazi"
"Aah hapana ila nimejikuta tu nampenda mtoto wa mtu huku, nimeshindwa kabisa kujizuia rafiki yangu, nimeshindwa"
"Wee Caren wewe, huoni kama ni hatari"
"Ntafanyaje sasa rafiki angu hebu nishauri nafanyajee." Alisema Caren huku akiangalia sms iliyoingia kwenye simu yake ilikuwa sms kutoka kwa Yusto akimtaarifu kuwa amefika yupo mlangoni.
"Best naomba nikupigie baadae" alisema Caren kisha akakata simu.
Alijiweka sawa kisha akasogea mlangoni akafungua.
"Wow, karibu Yusto" alisema Caren huku wakitazama na Yusto wakatabasamu, Yusto akaingia ndani.
*****
Jasusi Simigo na Brandina walimaliza kusikiliza mawasiliano kati ya Caren na rafiki yake.
"Vipi kuna kitu chochote umekipata" aliuliza Simigo huku akimtazama Brandina ambae alitikisa kichwa kuashiria hajapata chochote katika maongezi hayo.
"Hapana kipo Brandina hebu fikiria, kwanza kauliza kama Caren kaharibu kazi kazi gani hiyo, lakini pili kwa nini huyu mwanamke kasema ni hatari kitendo cha Caren kupenda, kwanini iwe hatari" aliuliza Simigo huku akiendelea kumtazama Brandina usoni, lakini Brandina alionekana yuko mbali kimawazo huku akiwa amekodolea macho kwenye compyuta.
Simigo alishangazwa na hali hiyo akageuka kutazama ni nini alichokuwa akikiangalia Brandina.
Aliona ule ujumbe wa Yusto alioutuma kwa Caren mda mfupi uliopita.
"""Nimefika Caren niko hapa nje mlangoni kwako"""
Simigo aliusoma ujumbe huo kisha akageuka na kumtazama Brandina kwa sekunde kadhaa.
Ilionyesha wazi ujumbe huo haukuwa umemfurahisha Brandina hata kidogo. Kitendo cha Yusto kwenda chumbani kwa Caren, kilimuumiza.
"Brandina"
Kimyaa...
"BRANDINAAA....."
"Eeh..aah umesemaje" Brandina alikurupuka kwenye dimbwi la mawazo baada ya Simigo kumuita mara ya pili kwa nguvu.
",Hivi unashida gani siku hizi, unawivu, Yusto kwenda kwa Caren imekuumiza, haya umeshajua kama hawa wawili ni wapenzi potezea sasa fanya kazi uzembe uzembe sitaki" alifoka Simigo.
Brandina alimtazama Simigo kwa macho fulani ya kebehi.
"Aliyekwambia nimempenda Yusto nani"
"Hebu acha kujishau bana hata mtoto mdogo anaweza kujua kama umempenda"
"Achana na Mimi, nambie nini kinafuata, tukamkamate Caren au" aliuliza Brandina huku akijaribu kupotezea mada.
***
John maarufu kama Master Joo kijana aliyekuwa anatikisa chuo kizima akionena kuwa na pesa kuliko wengine wote anajikuta kwenye mtihani mzito baada ya kushindwa kulipata penzi la binti mrembo Caren.
Mwanzo alifikiri mambo yatakuwa ni rahisi kwani hakuna alichokitaka akakikosa kutokana na jinsi alivyokuwa akiishi na kuogopeka chuoni pale lakini anakutana na Caren mwanamke mwenye misimamo yake, anakataa wazi wazi huku kikwazo kikubwa akiwa ni Yusto.
Pamoja na kumtishia Yusto mara kadhaa akiamini labda Yusto ataachana na Caren kwa kumuogopa lakini Yusto hayuko tayari kufanya hivyo.
Mwisho Jonh akiwa na chuki nzito dhidi ya Caren anaamua kuingia rasmi katika jukumu la kutaka kumuadabisha kijana huyo ambae amekuwa mwiba mchungu kwake.
***
John alionekana akiwa anaendesha pikipiki moja ya kisasa. Alikatiza mitaa kadhaa na mwisho alifika kwenye jengo moja kubwa nje kidogo na jiji la Dar es salaam. Alifika na kusimama nje ya geti baada ya walinzi waliokuwa wamevalia suti nyeusi kumzuia asiingie.
John alivua helmet yake kichwani, hapo wale walinzi waliinamisha vichwa vyao chini ikiwa ni kumpa Jonh heshima aliyostahili.
John alishuka kwenye pikipiki yake, kwa dharau akamrushia helmet mmoja wa wale walinzi pale nje kisha akaanza kupiga hatua kuingia ndani ya jengo hilo kubwa la kisasa.
Ilionekana ni jengo lililokuwa kama kiwanda cha kutengeneza bidhaa fulani, kulikuwa watu wengi mle ndani na kila mmoja alionekana kuwa bize na kazi yake.
Kila alipopita kijana John watu waliinamisha vichwa chini kama ishara ya kumuheshimu.
Jonh alitembea mwendo wa dharau majigambo na kujiamini bila kujali alikutana na nani mzee au kijana.
Kwa ufupi John alikuwa ni mtoto wa pekee wa mama mmoja tajiri, maarufu kama Madam Jane ambae alitajwa kuwa mmoja wa wanaweke matajiri afrika.
Madam Jane, alibahatika kuwa na mtoto mmoja ambae ni Jonh na hili jengo lilikuwa ni moja ya kati ya viwanda vyake vya kibiashara.
***
Jonh alitembea na mwisho aliingia ndani ya chumba kimoja kikubwa ndani akawakuwa watu wengi kila mmoja akiwa bize na kompyuta yake.
Chumba kilikuwa na mitambo mingi na screen kibao zikizokuwa ukutani kuzunguuka chumba hicho.
Jonh alipiga hatua mwisho akasimama mbele ya mtu mmoja aliyekuwa bize na compyuta yake.
"Aah master Joo siku nyingi, naona leo umekuja kututembelea" alisema yule bwana huku akijitahidi kumchangamkia Jonh.
John aliingiza mkono kwenye mfuko wa koti lake akatoa picha moja na kuiweka meza, ilikuwa ni picha ya Yusto.
"Nataka kujua kila kitu kumuhusu huyu mtu, ni nani kutoka wapi, maisha yake ya nyuma na sasa kila kitu nataka kujua" alisema John.
Hii ndio njia pekee aliyoona bora kuitumia ili kukabiliana na Yusto,
"Ukitaka kumpigia vizuri adui yako tafuta udhaifu wake" aliwaza John huku akitabasamu.
Je, nini kinafuata...
Vipi kuhusu Caren na Yusto?
Brandina na Simigo?
Sophia na Frank?
ENDELEA KUFUATILIA MKASA HUU.
Jipatie simulizi hii mwanzo hadi mwisho kwa Tsh
1500 tu. USIACHE pia kufuatilia simulizi yangu mpya
THE MODERN WAR(Vita ya kisasa).
0756862047