DO NOT SHOUT
(usipige kelele)
Sehemu ya......................23
Mtunzi: Saul David
Tel: +255756862047
Email: saulstewarty@gmail.com
ILIPOISHIA....
Sasa ilikuwa ni saa mbili na dakika 15, zikiwa zimesalia dakika 45 pekee ufike muda uliopangwa kukutana ARENA hotel.
Caren alikuwa chumbani kwake akimalizia kujiandaa, alivaa track suti nyeusi iliyouchora mwili wake vizuri, koti refu jeusi, miwani,kofia na gloves nyeusi pia.
Alipiga hatua akasimama mbele ya kioo akajitazama kisha akaachia tabasamu.
SASA ENDELEA....
Saa moja jioni Sophia alikuwa amejifungia chumbani kwake kwa zaidi ya masaa manne mfurulizo,
Hakutamani kula wala kunywa chochote hakuna kitu kilichokuwa kikimnyima raha na kumkosesha furaha zaidi ya penzi lake kwa kijana Yusto.
Alimpenda mno kijana huyo lakini upendo wake unaingia dosari na kujikuta anavunjika moyo baada ya kushuhudia Yusto akiwa na ukaribu mkubwa na binti mwingine mgeni chuoni hapo Caren.
Sophia hakutaka kukubali kushindwa, alijikuta akiingiwa na wivu mkubwa dhidi ya Caren moyo wake ukipata msukumo wa kufanya lolote ilimradi tu ammiliki Yusto.
Sophia alitoka chumbani kwake, taratibu akapandisha ghorofa ya juu akiwa na nia ya kuelekea chumba anachokaa Caren.
Alitembea kwa tahadhali huku mkono wake wa kushoto akiwa ameshikiria kisu kidogo mno cha kumenyea matunda.
Kiufupi hata yeye mwenyewe hakuelewa ni nini anataka kufanya lakini moyo wake wenye hasira ulimsukuma kufanya hivo.
Akiwa ndo kwanza anakikaribia chumba cha Caren, mara mlango wa chumba hicho ulifunguliwa, haraka Sophia alirudi nyuma na kujibana kwenye Kona moja. Akawa anachungulia.
Alimuona mtu alievalia mavazi meusi kanzia juu mpaka chini yaani kofia miwani koti,suruali hadi gloves akitoka chumbani kwa Caren.
"Ni yeye" alisema Sophia baada ya kumtazama mtu huyo kwa makini na kung'amua kuwa alikuwa ni Caren mwenyewe.
Baada ya kuhakikisha ameufunga mlango wa chumba chake vizuri Caren alitembea haraka haraka akapita karibu na pale alipokuwepo Sophia lakini hakumuona.
Sophia alianza kumfuata nyuma taratibu wakateremsha ngazi kuelekea ghorofa za chini.
Alipofika karibu na chumba chake Sophia aliingia upesi nae akavaa koti lake refu jeupe kisha kofia aina ya kapelo na miwani akatoka upesi akaendelea kumfuata nyuma Caren.
***
Caren alitembea haraka haraka hadi alipotoka nje ya chuo mbele yake akaona gari ambalo lilikuja kumchukua likiwa limeegeshwa pembeni ya barabara.
Akiwa analikaribia gari hilo caren alichukua simu yake nyingine ndogo akatuma ujumbe kwa namba isiyojulikana.
"""Kuna mtu ananifuatilia""""
Caren aliingia kwenye lile gari na bila hata kuuliza dereva alianza safari kwa mwendo wa taratibu.
""Ni Sophia"""
Meseji iliingia kwenye simu ya Caren.
""Okay muacheni"""
Alijibu huku safari ikiendelea kuelekea ARENA HOTEL.
Sophia nae baada ya kutoka nje ya chuo alimuona Caren wakati akiingia kwenye lile gari.
Haraka na yeye akasimamisha bajaji, akapanda.
"Ongeza mwendo hakikisha hawakuachi mbali"alisema Sophia pasipo kujua Caren alishamuona kitambo sana tangu walipokuwa ghorofani hostel.
****
Kikosi maalum cha takribani watu 22 kutoka wa bosi Mark moon tayari kilishawasili ARENA HOTEL kikiongozwa na jasusi Simigo.
Wakiwa wamevalia mavazi ya kawaida kabisa walifika na kujichanganya na watu waliokuwa wakitoka na kuingia ndani ya hotel hiyo maarufu.
Simigo, Brandina, Frank na Yusto wao walikuwa ndani ya noah moja iliyokuwa imepaki hatua kadhaa kutoka hotelini hapo.
Gari hiyo ndiyo ilikuwa kama chungu cha oparesheni hiyo madhubuti ya kumkamata Caren na wenzake. Gari ilikuwa na mitambo mingi sana ndani yake.
Punde alifikia jasusi mpili akiwa amevalia mavazi ya wahudumu wa hotel ile, akaingia ndani ya gari.
"Tayari nimeshatega vinasa sauti kwenye meza zote mle ndani, lakini Caren bado hajafika" alisema jasusi Mpili
"Sawa kazi nzuri nafikiri ndo huyo kafika" alisema Simigo baada ya gari moja kupita pembeni yao likasimama na baada ya sekunde kadhaa kweli akashuka Caren.
Sasa ilikuwa ni saa mbili na dakika 58 Usiku.
Moyo wa Yusto ulikuwa ukimuenda mbio sana hadi dakika hiyo hakuwa akiamini kabisa kama Caren anaweza kuwa kama vile wanavyodhani wao kwa namna alivyokuwa amemzoea mpenzi wake huyo ilikuwa ni ngumu kwake kukubaliana na hisia hizo.
"Natamani usiwe wewe Caren, ubaki Caren yule ninaemjua mimi"
Aliwaza Yusto huku akimsindikiza Caren kwa macho wakati akiingia ndani ya ile hotel, ARENA HOTEL.
Brandina nae alikuwa akimuangalia Yusto kila wakati akawa anashuhudia namna kijana huyo anavyoteseka. Akajikuta anatabasamu
"Mapenzi kitu cha ajabu sana kwa nini usingenipenda mimi Yusto" aliwaza Brandina huku akimuangalia Yusto, mara Yusto akageuka wakagonganisha macho.
"Mmh vipi" aliuliza Yusto
"Vipi nini"
"Umenisemesha"
"Nani Mimi"
"Ndiyo nani mwingine Sasa"
"Akuu nipo bize na kazi mimi" alisema Brandina huku akigeuka upande mwingine akawa anaangalia jinsi Simigo anavyohangaika na mitambo.
****
"Caren anaingia Caren anaingia"
Alisema Simigo huku sauti hiyo ikifika moja kwa moja kwenye vifaa maalum ambavyo vijana wake wote walikuwa wamevivaa sikioni.
Kimya kilitawala kwa dakika kadhaa.
Huku wale vijana waliokuwa mlendani wakamfuatilia Caren kwa kila hatua.
"Kona namba tano, meza ya nne wako wawili Caren ni wa tatu" sauti ya kijana mmoja ilisikika akitoa maelezo kwa wote.
Haraka Simigo ilibinya binya mitambo yao akazima vinasa sauti vyote walivyotega kwenye meza mle ndani ikabaki meza aliyokuwepo Caren na hao watu wengine wawili kama ilivyo elezwa.
"Everybody in position"(kila mtu kwenye nafasi) Simigo alitoa maelezo na hapo kila mtu alikaa kwenye sehemu aliyotakiwa kuwepo.
Frank na Yusto nao waliziweka sawa bastola zao kisha wakavaa vile vifaa vya mawasiliano masikioni wakashuka kwenye gari kisha wakaingia ndani ya hotel hiyo.
Kwa namna walivyokuwa wamevaa haikuwa rahisi kuwatambua. Walijua namna ya kupishana na watu huku wakiwa wameinamisha nyuso zao zilizofichwa na kofia zao saawia.
"Najua sio wewe Caren najua huwezi kufanya hivyo mpenzi" Yusto alijifariji hali akitetemeka mwili na roho.
****
Sophia nae tayari alishawasili ARENA HOTEL kwa tahadhali kubwa aliingia na kuketi meza ya pembeni karibu na alipokuwepo Caren na wenzake. Akaa na kuwapa mgongo Kisha akaagiza kinywaji akiamini hakuna aliyemuona wala kumshtukia, akajifanya ni mteja wa kawaida hotelini hapo.
***
Yusto, Frank, majasusi pamoja na vijana wengine kwenye oparesheni hiyo walitulia kimya kusikiliza maongezi yatakayo kuwa yakiendelea kutoka meza aliyokaa Caren na wenzake.
Je nini kitafuata...!
ITAENDELEA......
TUKUTANE TENA JUMAMOSI
Jipatie simulizi yote kwa pamoja (1-80), softcopy (PDF), kwa Tsh 1500 tu visa bado ni vingi na burudani inaendelea....
0756862047