DO NOT SHOUT
(usipige kelele).
Sehemu ya.........10
ILIPOISHIA...
baada ya kupiga tu hatua kadhaa uso kwa uso wanakutana na Sophia akiwa na Jonh wanaingia chuoni huku wameshikana mikono.
Wote walitoa macho kwa mshangao si Caren si John, si Sophia wala si Yusto, hakuna aliyetegemea....
ENDELEA...
Jonh alimtazama Caren kwa sekunde kadhaa kisha macho yake yakahamia kwa Yusto ambae haswa alikuwa ndiye adui yake mkubwa.
Haikuwa rahisi kwake kuamini kwamba kwa kipindi kifupi tayari Yusto na Caren walikuwa wamezoeana kiasi Cha kutoka out wakiwa pamoja.
Alimjua vizuri Caren alikuwa mgumu tena mgumu haswa, haikuwa rahisi mtu kumzoea hasa jinsia tofauti, lakini mambo yalionekana kuwa ni tofauti kabisa kwa Yusto.
Jonh alijikuta anatengeneza chuki ya aina yake, akamchukia Yusto zaidi na zaidi.
Hali ilikuwa hivyo kwa Yusto pia, hakuwa akimpenda John kwani ndiye mwanaume aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuuvunja moyo wa rafiki na mdogo wake kipenzi Sophia. Lakini hakuelewa ni vipi Sophia ameweza kutoka akiwa ameongozana na John.
Sophia nae alimtazama Yusto pasipo kupata majibu ni lini kivipi Yusto amekuwa na mazoea na Caren. Alimjua vizuri Yusto kuwa hakuwa mtu wa kuzoeana na wanawake hovyo hovyo lakini leo anashangaa kumuona akiwa na Caren tena wakiwa tayari kutoka usiku huo.
Wakati Yusto aliendelea kufikiri ndopo aliikumbuka sms kutoka kwa Sophia aliyotumiwa mda mfupi ulopita akiwa chumbani kwa Caren.
Yusto kwa ajili yako nitapoteza heshima yangu, kwa ajili yako nitafanya lolote liwe baya au zuri ili nikutoe akilini, naomba usiniulize wala kunijali kwa chochote niacheee, mpaka pale utakapo heshimu na kukubali hisia zangu kwako'
Maneno haya yaliyobeba hisia kali yalijirudia rudia kichwani kwa Yusto ndipo akatambua lengo hasa la Sophia kukubali kutoka na John hali anamchukia. Nafsi ikawa inamsuta Yusto kwani alikuwa anamjali sana Sophia kuliko kitu kingine.
"Jamani wa kutoka atoke wa kuingia aingie nataka kufunga geti" mlinzi alifoka baada ya kuona watu hao wamebaki wanatazama kwa muda mrefu.
Mwisho kila mtu aliendelea na safari yake wakapishana bila hata kusalimia kila mtu akiwa na dukuduku lake moyoni.
Wakati wanapisha John na Yusto walitazamana kwa macho makali, kila mmoja akidhilisha chuki aliyokuwa nayo dhidi ya mwenzake.
Ukweli ni kwamba Sophia alikuwa amejikaza vya kutosha kwani baada ya kupiga hatua kazaa alianza kukimbia huku akiangua kilio, jambo aliloliona lilikuwa limemuumiza kupita kiasi.
Haikuwa rahisi kwake kuvumilia kwani alimpenda mno Yusto na kwa kuwa Yusto hakuwa mtu wa kupenda penda wanawake, aliamini ipo siku atamuelewa, lakini leo ameshuhudia jambo ambalo hakuwahi kuwaza lingetokea, moyo wake ulivyunjika na kumuuma mno.
"Sophia, Sophia..." Jonh liita huku akikimbia kumfuata, alipomfikia akamshika mkono.
"Nini wewe niachee" Sophia alifoka huku akiutoa mkono wake kwa nguvu kutoka kwenye mikono ya Jonh
"Hebu nisikilize kwanza sophy"
"Nisikilize nini Jonh unataka kusema nini"
"Sasa si tulikuwa wote, kwa nini unakimbia unaniacha"
"Kazi yako imesha isha nilikuomba unisindikize club haya tumesharudi nenda zako Jonh"
"Ni hilo tuu.."
"Kwa hiyo kingine nini, unataka nini, alafu mbona unaoneka kujali tangu lini wewe ukanijali Mimi zaidi ya kuniumiza, fyuuuuh" Sophia aliongea kwa hasira kisha akaondoka kuelekea bwenini kwao.
John alibaki amesimama huku akimsindikiza Sophia kwa macho.
"Haya sasa huyo Yusto wako uliyekuwa unamwamini leo yuko wapi kaishia kukuumiza, pambana na hali yako" John aliongea kwa sauti ya chini kisha na yeye akawa anaelekea chumbani kwake.
Tukio aliloliona halikumtoka kichwani. John alionekana kumpenda mno Caren hakuwa tayari kuona mlimbwende huyo mgeni chuoni kwao anamilikiwa na mwanaume mwingine zaidi yake, akawaza ni naman gani ataweza kukabiliana na Yusto kijana ambaye ameonekana kuwa mwiba mchungu kwake.
Akiwa anatembea bado hajafika chumbani kwake alichukua simu yake na kupiga mahali, simu iliita na mwisho ikapokelewa.
"Ndio John hapa naongea, kesho saa tisa tukutane maskani, kunakazi nataka kuwapa njoo na vijana wako....powa powa" aliongea Jonh na kukata simu.
Akatulia kwa muda kisha akatabasamu....
" Yusto, Yusto... Mwanakulitafuta mwanakulipata"
Aliongea John akafungua mlango wa chumba chake na kuingia ndani.
⭐⭐⭐
Dakika 15 baadae Yusto na Caren walionekana wanashuka kwenye taksi nje ya club moja maarufu jijini hapa.
"Yusto" Caren aliita
"Yes tell me"
" Uko sawa"
"Mmh yah, kwanini umeuliza"
"Nakuona tu hauko sawa, tangu tulipokutana na John unaonekana hauna furaha kabisa, tumepanda taksi hadi hapa uko kimya tu..."
"ooh no niko poa, Caren usijali" John aliongea huku akililazimisha tabasamu.
Akanyoosha mkono wake na kumshika Caren, wakawa wanatembea kuingia ndani.
Hakika walionekana kupendeza mno kwa namna walivyokuwa wanatembea hali wameshikana mikono.
Wakati huo ilikuwa ni usiku sana, hakukuwa na watu wengi sana mle ndani, kulikuwako familia moja ya watu kama 7 hivi wakisherehekea happy birthday ya kijana wao mdogo yapata miaka nane, kijana huyo alikuwa ni mlemavu wa ngozi(albino).
Yusto na Caren Waliingia ndani wakachagua meza moja tulivu wakaagiza vinywaji na kuanza kutumia taratibu huku kila mmoja akimtazama mwenzake kwa macho ya kuibia ibia.
"Mmh tunaweza kucheza" alisema Yusto huku akisimama na kunyoosha mkono.
Bila hiyana Caren aliupokea mkono wa Yusto akasimama, wakaanza kucheza mziki laini ulokuwa unapigwa eneo hilo.
Yusto aliweka glass ya kinywaji mezani akazunguusha mikono yake miwili nyuma ya kiona laini cha Caren na kumsogeza karibu. Caren nae akaweka mikono yake juu ya mabega ya Yusto Wakawa wanacheza hali wakizunguuka zunguuka, kila mmoja akimtazama mwenzake usoni na kutabasamu.
Walizidi kukumbatiana huku kila mmoja mapigo ya moyo wake yakianza kubadilika kadri muda ulivyokuwa ukienda.
Yusto alimvuta Caren karibu zaidi wakawa wanatazamana vizuri kwa macho yaliyolegea,
na mwisho, Yusto akasogeza mdomo wake karibu kabisa na mdomo wa Caren.
Caren alielewa ni kinaendelea alifumba macho tayari kulipokea busu kutoka kwa Yusto...
ITAENDELEA....
DO NOT SHOUT
(usipige kelele)
Sehemu ya..........11
Mtunzi: Saul David
ILIPOISHIA....
Yusto akasogeza mdomo wake karibu kabisa na mdomo wa Caren.
Caren alielewa ni kinaendelea alifumba macho tayari kulipokea busu kutoka kwa Yusto...
SONGA NAYO...
Caren alihisi msisimko wa ajabu mara tu baada ya kugusanisha ilimi wake na ulimi wa Yusto, lilikuwa ni tukio geni sana kwake.
Walimwagiana mabusu moto Moto mfurulizo huku Caren akijikuta anazidi kumkumbatia Yusto kwa nguvu.
Yusto nae hakuacha kuuchezesha ulimi wake ndani ya kinywa cha Caren kiasi cha kumfanya mwanadada huyo kuregea na kuanza kuishiwa nguvu kabisa.
Yusto aliligundua hilo, haraka aliacha kufanya kile anachokifanya na kumtazama Caren usoni.
Macho ya Caren yalionekana kuregea mno, wakawa wanatazamana na kisha wakatabasamu kwa pamoja.
Mara ghafula kishindo kikubwa kilisikika mlangoni, wanaume 7 waliofunika nyuso zao kwa vitambaa waliingia kwa kasi huku baadhi yao wakiwa na siraha za moto mkononi na wengine wakiwa na mapanga.
"Lala chini, wote lala chini, nimesema chini, alafu kimya" sauti ya mwanaume mmoja ilisikika ikiamrisha.
Ile familia waliyokuwa wakifanya sherehe ya happy birthday kwa mtoto wao albino walipiga kelele na kulala chini kwa hofu.
Wakati huo tayari club yote ilikuwa imezingirwa na wale watu ambao walionekana kuwa makini na kazi iliyowaleta.
"Nyinyi hamjaelewa, nimesema chini" alifoka yule mwanaume huku akiwatazama Caren na Yusto ambao bado walikuwa wamepigwa na butwaa.
Yusto alimshika mkono Caren kisha kwa pamoja wakachuchuma chini.
Wale majambazi walisogea hadi walipokuwa ile familia, wakafika na kumnyanyua yule mtoto albino juu juu, kisha wakamlaza juu ya meza moja.
"Sisi shida yetu ni kiganja chake cha mkono basi, tunamkata alafu tutamwacha mkamtibu, au tumbebe moja kwa moja tukamuuwe huko, hahahahah"
Aliongea jambazi mmoja kwa dharau huku akiwa analiandaa panga lake vizuri.
Mama mzazi wa mtoto huyo aliangua kilio na hazikuzidi sekunde tatu akatulia kimya akiwa amepoteza fahamu.
Si Yusto wala si Caren hakuna aliyekuwa tayari kuona tukio hilo linafanyika mbele yao, lakini tatizo kila mtu alitaka kuilinda siri yake dhidi ya mwenzake. Caren alikuwa uwezo mzuri sana wa kuwakabili wale watu lakini alihofu kuwa Yusto angemshtukia na huenda angeharibu kazi iliyomleta pale chuoni, vivyo hivyo kwa upande wa Yusto nae aliogopa kushtukiwa.
Sasa ilikuwa ni wakati wa kumkata yule mtoto albino mkono, ambae alikuwa anapiga kelele kwa hofu kubwa aliyokuwa nae.
Lakini kelele hiyo haikufika kokote kwani walichokifanya majambazi hao ni kuongeza sauti ya mziki wa ile club.
Uvumilivu ulimshinda baba wa mtoto akasimama huku akiwaomba wale majambazi wamchukue yeye badala ya mtoto wake.
Kofi zito lilitua kwenye paji la uso wa yule baba, akaanguka chini huku damu ikimtoka puani na mdomoni.
"Caren nini" Yusto alimuliza Caren baada ya kuona anataka kusimama mara baada ya yule baba kupigwa kibao kizito.
"Yusto watamuuwa yule mtoto kwa hiyo tutaendelea kushangaa tu" alihoji Caren.
"Sasa unataka kufanya nini" Yusto aliuliza hali akishangazwa na ujasiri alokuwanao Caren, alivyoongea vilikuwa haviendani kabisa na sura yake, alitegemea wakati huo Caren angekuwa amejikunyata anatetemeka kwa hofu lakini haikuwa hivo, macho ya Caren yalikuwa makavu kabisa.
"Nyinyi mnaongea nini hapo" alisema jambazi mmoja huku akisogea pale walipo kuwa Yusto na Caren ambao walitulia kimya wakawa wanamtazama wakati anakuja.
Alifika na kuanza kuwaangalia kwa zamu. Macho yake yakaganda kwenye sura ya msichana mrembo Caren.
"Wewe binti hebu simama, simama juu" alisema yule jambazi huku akionyesha kabisa kumtamani Caren.
Caren alisimama bila ubishi wowote kisha yule jambazi akawa anamzunguuka akimtazama.
"Walah Mungu ni fundi jamani, cheki, yani toto toto kweli" alisema yule jamaa kauli iliyowafanya wenzake kuangua kicheko.
Wakati huo wote Yusto alikuwa ametulia pale chini hali akiichunguza kwa makini ile bastola aliyoshika yule jambazi, hapo akagundua kuwa haikuwa bastola bali ni Toy yaani feki.
"Washenzi hawa" alisema Yusto kwa sauti ya chini, huku akiaanza kukunja shati lake taratibu
Yule jamaa aliendelea kumkagua Caren na safari hii alinyoosha mkono wake akitaka kumshika matiti.
Kabla mkono wake haujagusa mwili wa Caren, Caren alizunguuka kwa staili ya ajabu huku akiwa amemshika yule jambazi mkono, kufumba na kufumbua alijikuta yuko chini huku akilalamika kwa maumivu makali katika bega lake la kulia.
Kitendo hicho kiliwashangaza wengine na wawili kati yao walikimbia kwa kasi wakitaka kwenda kumvaa Caren.
Lakini walirudisha na kuangushwa chini na Yusto ambae aliwavaa kwa ghafula bila wao kutegemea.
Yusto alisimama pembeni ya Caren, huku tayari wakiwa wanazunguukwa na majambazi hao ambao waliongezeka na kuwa wengi baada ya waliokuwa nje kuingia ndani.
"Baby" aliita Caren
"Yes baby"
"You are here"
"Yes am here darling" alijibu Yusto huku walitazama na Caren usoni.
Sasa hakukuwa na sababu ya kujificha tena ilikuwa ni wakati wa kila mtu kutumia uwezo wake kujiokoa na kuokoa maisha ya yule mtoto albino.
Caren aliinama na kuchana sketi yake ndefu ilokuwa ikimbana, akachana mpasuo ulofika hadi kwenye kiuno chake, paja lake moja likawa nje na kufanya nguo yake ya ndani kuonekana, wala hakujali.
Majambazi nao walizidi kumiminika na Sasa walikuwa Kama 14 hivi wote walikuwa tayari kupambana, na taratibu walianza kuwasogelea Caren na Yusto.
Wimbo ulokuwa ukiimba uliisha na sasa Amapiano ya diamond - IYO, ilianza kuimba.
Caren na Yusto walitazamana kwa mara nyingine kisha kila mmoja akatoa ishara kuwa yuko tayari.
⭐⭐⭐
SIMULIZI HII INAPATIKATA YOTE 1-80 (MWISHO)
HARD-COPY (KITABU) = Tsh 10,000
SOFT-COPY (PDF/WORD) = Tsh 2,500
WhatsApp: 0756862047
Email:
saulstewarty@gmail.com
KARIBU
ITAENDELEA.....