Simulizi ya ukweli penzi langu

Simulizi ya ukweli penzi langu

SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 05

ILIPOISHIA.......

Suma aliingia chumbani na kuanza kupekua alifunga droo ya kitanda akakuta funguo nyingi akachukua zote na kuanza kufunguka kabati ambalo lilikua kubwa sana akafungua mlango wa kwanza akakutana na nguo za kiume nyingi sana akafungua mlango wapili akakuta viatu vya Kila aina pia vya mwanaume na akaendelea kufunguka milango yote na mwisho kabisa akakutana na kisanduku akakifungua pia na alichokikuta kilimfanya astaajabu sana na kumfanya ashangae sana.

ENDELEA NAYO.......

Suma alivyostaajabu akajikuta anashindwa kufanya maamuzi akafunga lile sanduku na kulirudisha kabatini na kufunga milango yote na kurudisha funguo kwenye droo na kutoka sebleni huku akihaha sana.

Kichwani mwake ikamjia akili ya ghafla akarudi chumbani haraka na kuchukua Tena funguo kisha kufunguka kabati na kufunguka Tena lile sanduku na kuchukua vibunda viwili vya pesa kisha akafunga na kurudisha sehemu yake na kuingia chumba kingine na kuanza kuhesabu zile pesa zilikua nyingi sana kiasi kwamba alihisi kibunda kimoja kitamtosha sana hivyo alirudisha kimoja na kubaki na kimoja kisha akaweka kwenye begi lake na kutoka nnje na kufunga mlango kisha akapanda kwenye gari na kuondoka zake.

Mtakua mnajiuliza gari alikua hawezi kuendesha jamanii ukiishi na mtu mwenye hela na aliyetofauti na wewe lazima na wewe uwe kama yeye hivyo hata Suma pia alikua mjanja sana alionekana mpole na mkarimu lakini mambo yake alikua anafanya kimya kimya.

Alifika Hadi kwenye car wash ambayo alikua anafanya kazi akapiga honi kama kawaida vijana walichangamkia fursa na baada ya kufika Suma alishusha kioo kitu ambacho kiliwashangaza wote pale hasa Juma ndio alikua mkaidi sana kwa Suma siku hiyo akapiga salute.

Walisalimiana na kuanza kupiga story za hapa na pale kisha Suma akawambia
"Nikweli nilipotea ghafla lakini zote ni changamoto tu ndugu zangu na Kuna msemo usemwao Kila kinachotokea hua kimepangwa na kuna sababu malum iliyofanya kitu hiko kitokee hivyo basi nataka kuwambia kua nimepata bahati mwenzenu nimesaidiwa na mama mmoja hivi anapesa sana, mwanzo alinifanya kama mfanya kazi lakini alivyozidi kuona namuheshimu basi ameniamishia ndani"

"Broo kwahiyo unamkula huyo mama?"
Rama aliuliza maana walikua wanashauku sana ya kutaka kujua vingi kuhusu Suma, Suma akawambia.

"Sikilizeni mimi sio kama wengine sawa, kwanza kabisa ngoja nisije kusahau kitu"
alizama mfukoni na kutoa pesa na kuwakabidhi Kila mmoja elfu30 kisha akawambia.

"Mtakunywa soda ila naomba nitoke na Juma kidogo ndugu zangu"

Juma mwenyewe alikubali Kwa haraka tu kisha wakatoka Hadi sehemu waliyoona inafaa kuzungumza wakazungumza vizuri walichotaka kuzungumza Kisha Suma akataka kumrudisha Juma kazini, Juma akamwambia hapana nataka kwenda kwangu, Suma alimpeleka Juma kwake na wakiendelea kusisitiziana kile walichoongea kisha Suma akarudi nyumbani kwa Nadya na kuendele na mambo yake mengine.

Upande wa Aisha simu hiyo walichelewa sana kuamka kutokana na uchovu alipotazama saa ilikua saa4 asubuhi aliamka haraka akafanya usafi na kuandaa kifungua kinywa kisha akamwamsha pia mama yake na kisha baada ya kujiweka sawa walisogea mezani kwaajili ya kupata chakula, lakini kabla ya Aisha hajaanza kula mara alisikika mlio wa simu ukitokea chumbani kwake, haraka aliwahi na baada ya kutazama aliona jina la Suma haraka akatoka chumbani na kumwambia mama yake.

"Mama Suma anapiga"
mama yake alichukua simu na kuipokea.

"Hallow mwanangu unaendeleaje lakini mbona umetususa hivyo?"

"Mama nimeongea na Aisha akanambia uko sawa na sababu ulikua umelala nikamwambia akuache upumzike lakini samahani mama"

"Suma upo wapi baba mbona moyo wangu unaenda mbio mwanangu umefanya kitu kibaya chochote mwanangu Nina wasiwasi sana juu yako"

"mama aa kumbuka ku.... kua hakuna kitu kibaya nilichokifanya ondoa shaka kabisa kuhusu mimi mama"

"Suma usinifiche nieleze Mimi ni mama yako"

Aisha alichukua simu na kumuulizaa Suma Kwa taharuki.
"Suma unanini mbona unamuweka mama kwenye wasiwasi umefanya Nini kibaya?"

"Aah Aisha subiri nitakupigia"
mara Suma alikata simu na kumfanya Aisha aingiwe na uoga na wasiwasi pia kuhusu Suma hivyo hata chakula hakikulika kabisa sio mama yake Wala Aisha wote walikua na mawazo sana.

Upande wa Suma pia ilikua inamuumiza sana sababu alikua anajiuliza mama yake amejuaje kuhusu alichokifanya na mara ghafla mlango ulifunguliwa na akaingia Nadya kitu ambacho kilimshangaza zaidi Suma maana hakuwahi kurudi mapema kiasi hiko Suma akamuuliza.

"Vipi baby Kuna kitu umesahau?"

"Aah ndio kipenzi na nachukua tu kisha narudi ofsini"
Nadya hakua na mengi ya kuzungumza aliingia chumbani na kuchukua ufunguo kwenye droo na kufungua kabati lake kwenye mlango wa mwisho kisha akakifungua kile kisanduku wakati huo Suma alikua anachungulia kupitia tundu la kitasa cha mlango huku jasho likimtoka kwenye mstari wa mgongoni likimtiririka sababu alijua vyema kuwa anaenda kuumbuka hivi karibuni lakini Nadya alikua bize na mambo yake kisha akachukua kiasi alichohitaji na kuhifadhi sehemu husika kisha akatoka sebleni na kumkuta Suma amejilaza akiwa ana mawazo sana maana alishajua kipi anafanya hivyo akishajikatia tamaa kua Chochote kitakachotokea kitokee tu sababu amekipanga.

Basi baada ya Nadya kufika sebleni akamwambia.
"Baby badae ila leo nitachelewa kidogo nivumilie sawa mpenzi eeh"

"Sawa mke wangu nakupenda"
sauti ambayo alikua amezungumza Suma ilikua yenye wasiwasi sana Nadya akasogea karibu na kumuuliza.
"Unanini lakini mume wangu mbona unaniogopesha kiasi hiko?"

"Aah ni vile tu ni ...."
kabla hajamaliza kuzungumza simu ya Nadya iliita na akasimama na kumuaga Suma huku akimdanganya boss wake kua yupo kwenye foleni.

Kuondoka kwa Nadya ndio ilikua nafuu ya Suma alishusha pumzi ndefu kisha akajiuliza.
"Inamaana Nadya hajagundua Chochote? Itabidi nirudishe pesa ya watu kabla ya kugundua nilichokifanya"

Suma alitafuta namba ya Juma na alitaka kuipiga hiyo namba lakini akasita na kuizima simu yake na kuweka Kando, aliendelea na kazi zake kama kawaida na alikua mwenye mawazo sana siku hiyo hadi usiku, tena siku hiyo kabla ya Nadya kurudi alikua ameshalala.

Nadya alivyorudi akamkuta Suma amelala hakutaka kumsumbua kwa Chochote kile alimuacha aendelee kulala.

Zilipita kama wiki mbili Suma aliendelea kumkwepa Nadya siku hiyo Nadya akamtolea uvivu alipomkuta amelala akamwamsha na kumuuliza.

"Suma una matatizo gani sikuizi mbona sikuelewi eeh shida Nini hasa kila siku wewe ni wa kwanza kulala na wa mwisho kuamka shida Nini eeh kama unaumwa unasema mtu anajua anaanzia wapi kama unahisi nimekukosea pia unasema"

"Aah Nadya nisamehe najikuta tu nakua mchovu sana"

"Suma unatembea na mwanamke mwingine nje sio?"

"Nadya mama ni mambo gani ambayo unayazungumza?"

"Sawa kama unajifanya huelewi ila nikija kujua kama una mwanamke mwingine nje ukimuondoa huyo wa kijijini nakuuwa wewe na huyo malaya wako"

Nadya alikua na hasira sana Suma akaona atumie fursa hiyo kumtuliza mtoto apunguze hasira hivyo kama kawaida yake alishajua wapi anampatia basi walifika safari yao mwenyewe Nadya aliomba msamaha kwa Suma Kwa kile alichokisema.

"Baby nisamehe nimezungumza vibaya sana"

"Usijali sana halafu unajua ukiwa unakasirika hivi huaga inakua tamu sana si unaona Leo umeinjoy sana eeh?"

"Ndio baby nakupenda"

"Nakupenda pia mpenzi haya Sasa lala ili kesho uwe na siku nzuri kazini"

"Suma naomba utamu wako usimuonjeshe mtu mwingine yoyote yule zaidi yangu Mimi"

"Na mimi pia Nadya na sasa hivi nimeshasahau kuhusu mwanamke wa kijijini apambane na hali yake wewe na mimi tu utamu wangu ndio utamu wako sawa Nadya wangu?"

"Sawa baby tulale"

Nadya hakuchukua muda mrefu alipitiwa na usingizi lakini upande wa Suma alikua anapanga mipango yake kichwani kwake.

Upande wa Aisha akazungumza
"mama hii wiki ya pili sasa Suma hapigi simu hata kusema Chochote kile hivi hajui kama tunawasiwasi juu yake?"

"Aisha unachojiuliza wewe na mimi najiuliza hiko hiko kwanini Suma amebadilika hivi?"

"Mama unavyosema hivyo unanifanya niingiwe na wivu juu yake"

"Sijamaanisha hivyo, amebadilika mambo yake yaani sio mpigaji wa simu tena na ameshindwa kusema ukweli Nini kinamsumbua inanipa wasiwasi sana"

"Mama twende chumbani ukapumzike Mimi sitalala nitahakikisha namsumbua Hadi atapokea simu yangu."

Aisha alimpeleka mama yake chumbani na kumfunika shuka huku aliendelea kumtafuta Suma Kwa meseji Kwa njia ya kumpigia pia lakini hakua na majibu ya aina yoyote Yale.

Asubuhi mapema Aisha aliamka nakuendelea kumtafuta Suma lakini hakukua na tofauti na usiku wa jana, mara mlango ukagongwa haraka Aisha alifungua na kumuona Dan akamuuliza.

"Dan vipi mbona asubuhi mapema Kuna shida gani?"

"Dada kuna tatizo kubwa sana inasemekana kua wale wafungwa kule wamegudnua kua Bado unaishi wakati walijua umeshakufa hivyo muda wowote ule wanaweza kukuvamia hapa na kukupoteza hivyo Kuna tiketi hapa ya wewe kuondoka haraka iwezekanavyo"

"Dan hizo tiketi naenda wapi Mimi eeh sikiliza Dan Sina popote pa kwenda na ikiwezekana nitapambana Hadi tone langu la damu la mwisho siwogopi Chochote sababu kwanza Sina moyo wa huruma Wala uoga Tena Dan wamenifanya niwe na moyo mgumu kama jiwe la mtumba Sasa utajua kama jiwe lamtunba ni la aina Gani"
Aisha alichukua ile tiketi na kuichana mbele ya Dan, Dan akamwambia.

"Lakini wazazi wako wame..."

"Wazazi wangu wamefariki najua lakini wanataka nilipe kisasi sababu nikiwa nakimbia sitalipa kisasi kwaajili ya wazazi wangu"

"Aisha dada lakini mbona upo hivyo wewe kwani usiwe muelewa tu jamanii?"

"Nitakua muelewa kama utanielewa Nini namaanisha Dan nenda"
Aisha alifunga mlango kwa hasira na kukaa chini akiwa na maumivu sana maana Dan nikama vile alimtonesha kidonda chake ambacho kilianza kupona.

Upande wa Suma baada ya kuagana na Nadya kuelekea kazini alimoigia simu rafiki yake wakaagana kukutana sehemu na wakakutana na Juma alimkabidhi pesa Suma na kumwambia.

"Suma nakuona mbali sana kwa sababu unaakili sana kaka endelea hivyo hivyo"

"Usijali kaka nimekushirikisha wewe sababu wote nataka tuendelee na hata ikiwezekana tuzidi kuifanya car wash iwe yenye ubora na tuwatie na marafiki zetu pia kaka tufanye biashara"

"Sawa Suma hamna shida basi nitakupa taarifa zote"

"Sawa kwaheri"
Suma na Juma waliagana na Kila mmoja kuondoka zake, Suma alipofika tu alirudisha zile pesa Kwenye sehemu husika na kusema.

"Asante Mungu kwa kunilinda na hili jambo bila ya Nadya kushtukia hili"
Akawasha mziki na kuanza kucheza Kwa furaha mara ghafla mlango ulifunguliwa...

ITAENDELEA.......

Kuna nini kinachoendelea kwa upande wa Aisha na pia kwa upande wa Suma? Jina la simulizi PENZI LANGU
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 06

ILIPOISHIA.......

"Asante Mungu kwa kunilinda na hili jambo bila ya Nadya kushtukia hili"
Akawasha mziki na kuanza kucheza Kwa furaha mara ghafla mlango ulifunguliwa.

ENDELEA NAYO....

Nadya ndiye aliyeingia na kumkuta Suma anacheza Kwa furaha alivyogeuka na kumuona Nadya akamsogelea na kumbusu Kwa furaha kisha akamshika kiuno chake na kuendelea kucheza japokua alikua hajui style ya kucheza na mwanamke lakini Nadya ni jambo ambalo kilikua linampa wasiwasi sana kwani Suma awe amebadilika ghafla vile lakini hakutaka kujionesha mbele ya Suma kuwa anamaswali mengi kichwani kwake waliendelea kucheza Hadi nyimbo ilivyoisha Kisha Suma alistop na kumuuliza.

"Umefurahi Kwa mara ya kwanza kucheza na mshamba mmoja kutoka kijijini?"

"Jamanii suma ndio maneno gani hayo baby Mimi sikuchukulii kama mshamba bwana ila tuachane na hayo vipi mbona umekua na furaha sana hivyo?"

"Nadya unanifanya kuwa mwanaume mwenye furaha Kila siku na vile nakupenda najihisi naelekea kuwa chizi kabisa Kwa mapenzi yako"

"Hahaha Suma acha bwana huwezi kua chizi yaani nilikua nimechoka sana sijihisi hata kuchoka Tena na Kwakua umesema una furaha na Mimi pia nafuraha Kwa ulichonifanyia Jana, ukweli Jana ndio nimeusikilizia utamu wako na nikasahau kama kuna kufa Sasa basi baby Leo staki tule nyumbani nataka twende tukale hotelini"

"Ooh halafu hela unatoa wewe au Mimi?"

Nadya alitoa waleti Kwenye begi lake na kumkabidhi Suma na kumwambia.

"Milipanga hili Kwa muda mrefu sana shika hii itakua waleti yako na Kuna kadi ya benki humo na namba ya Siri pia na pesa ambayo utalipia chakula usiku wa leo"

Suma alifungua wallet na kutoa kadi ya benki na kumkabidhi mwenyewe Nadya na kumwambia.
"Nadya sitaki hata kadi ya benki Sina matumizi ya aina yoyote ile Kwa Sasa, kwahiyo Wala hata usiwe na wasiwasi na Mimi"

Nadya ndio alizidi kumhisi vibaya Suma sababu akifikiria dunia ya Sasa nani umpe kadi ya benki na aikatae kirahisi tu Nadya hakutaka kuongea Chochote akaingia chumbani kwake na Moja Kwa Moja akaanza kutafuta sanduku ili aangalie maana alihisi huenda Suma amemuibia pesa zake.

Nawakati Nadya anawaza hivyo upande wa Suma pia alikua anajiamini kwa Chochote sababu mzigo tayari alisharudisha.

Nadya alitazama Kwenye sanduku na kuhesabu kisha akasema niliweka bunda kumi na nimeondoa vinne Bado sita, vipo vile vile kwanini Suma anafuraha hivi huyu ni mwanaume wa aina Gani?

Ni maswali ambayo alikua anajiuliza sana Nadya na baada ya kutoka chumbani akamkuta Suma anaitazama sana ile wallet na baada ya kugeuka na kumuona Nadya haraka alimkumbatia na kumwambia.

"Mke wangu asante sana Kwa zawadi yako nimeipenda sana"

"Hamna shidaa basi twende tukaoge tuondoke baby"

"Nenda kaoge sitaki nikuchoshe haraka nataka tukirudi huko ndio nikutengeneze vizuri"

Nadya aliingia ndani huku akiwaza kiasi Cha kumfanya awe na wasiwasi sana juu ya Suma, aliingia bafuni alioga kisha akamwambia Suma kua yupo tayari na Suma pia alioga na kama kawaida yake Nadya alimtolea nguo na viatu Kwenye kabati na kumpatia, hivyo Suma akamuulizia.

"Nadya hizi nguo ni za nani mbona umekua ukifanya hivi Kila wakati?"

"Suma sijawahi kukwambia kabla lakini nilikua na mpenzi wangu ambae nilimpenda sana lakini alikuja akanisaliti baada ya kwenda kusoma huko nnje ya nchi na mpaka leo hii hajarejea hapa nchini, lakini hivi vitu navyokupatia wewe nikama vile nakuona ni yeye lakini siwezi kukufananisha nae sababu yeye amekua mtu mbaya sana kwangu nakupenda wewe tu pekee Kwa Sasa"

"Ooh pole sana Kwa kilichokutokea"

"Asante halafu pia usiniulize kuhusu mapenzi yangu yaliyopita yananiumiza na kunirudisha nyuma"

"Sawa nisamehe Bure"

Basi walitoka nnje wakiwa na furaha sana japokua Kila mmoja alikua anamuwaza mwenziwe kwani amekua hivyo.

Walifika Kwenye hotel moja yenye viwango flani hivi Kisha wakaagiza chakula na kuanza kula Kwa mahaba yote yaani siku hiyo ndio Nadya alioneshwa mahaba yote na Suma alikua anamdekeza sana Nadya akasahau shida zote na kumuamini Suma kupita maelezo.
walirudi nyumbani na kufikia kulala sababu ya kuchoka sana.

Siku zilienda sana
ilikua siku ya Jumapili ambapo walimaliza kufanya kazi kwa pamoja kisha wakapumzika Kwenye bustani Kwa mikao ya kimahaba, Suma alikua amenyoosha miguu kisha Nadya akalala Kwenye miguu yake huku akichezea nywele zake wakati huo Nadya alikua bize na mitandao ya kijamii, mara simu yake iliingia ujumbe na Nadya haraka aliusoma huo ujumbe ulisomeka.

"Nadya mpenzi narudi baada ya wiki moja nakupenda sana na nimekukumbuka sana, marafiki zangu wengi wamekua wakinitambia na watoto zao na mimi nataka unizalie mtoto mzuri sana kama wewe mwenyewe hakika nitakua na furaha zaidi na zaidi nakupenda sana"

Nadya aliamka pale alipokaa na kuingia ndani akiwa amechanganikiwa sana na hata huo ujumbe hakua ameujibu maana alitoka online Kwa haraka sana.

Suma alitumia fursa hiyo kushika simu yake na ndipo alipoona jumbe nyingi na calls nyingi sana akajiuliza.

"Hee kumbe mbona ni za muda mrefu sana na halafu sikuwahi kuwapigia Wala kuwaambia Chochote mama atakua na wasiwasi sana" haraka alipiga simu, simu iliita bila ya kupokelewa alijaribu kupiga kama mara tatu lakini simu haikupokelewa na yeye alianza kujisikia vibaya sana maana alihisi huenda mama yake amepatwa na jambo baya.

Aliingia ndani akiwa amechanganikiwa pia Nadya alivyomtazama Suma akahisi huenda labda amekasirika baada ya yeye kutoka kwenye bustani bila ya kumwambia Chochote.

Akaamua kumsogelea na kumuuliza.
"Vipi baby mbona umekua hivyo?"

"Sijui Nadya sijui mama yangu amepatwa na nini simu yake inaita tu bila ya kupokelewa"

Nadya akafurahi maana alihisi huwenda Suma amekasirika Kwa yale mambo yake, basi Nadya akasimama na kujisemea moyoni bora Kila mtu apambane na hali yake.

Nadya alikua amechoka sana na hajui Nini afanye maana hakutegemea kile alichoambiwa, alioga na kumuaga Suma kuwa anatoka, Suma Wala hata hakumjali maana nae pia alikua na mawazo yake.

Upande wa Aisha alikua nyumbani kwao na marafiki zake wanaongea mambo mbali mbali huku wakimwambia asiwe anakaa tu ndani siku Moja Moja awe anawatembelea pia Aisha alikubali na kuwaahidi hivyo lakini wakati wanaongea mama yake Suma hakua akipenda kabisa alichukia ujio wao na hata vishawishi vyao Kwa mkwe wake.

Baada ya kuondoka, Aisha akaandaa juisi na kumpelekea mamkwe wake alipokea na kukaa walikunywa pamoja kisha Aisha aliingia chumbani kwake na kushika simu akakuta amepigiwa na Suma mara tatu haraka akampigia Suma hakuchelewa akapokea simu na kabla ya salamu alichiuliza ni kuhusu mama yake.

"Mama yangu Aisha yupo wapi?"

"Suma ndio tabia Gani hujasalimia hata"

"Aisha niambie mama yangu yupo wapi?"

"Sawa mama yuko sebleni Mimi nili..."

"Mpe simu mama yangu tafadhali"

Aisha alimshangaa sana Suma mbona amekuwa hivyo lakini hakua na jinsi alimpelekea simu mama yake wakaongea kisha akakata simu.

Aisha akiwa anasubiria labda yeye ataitwa lakini hata hakuitwa alipotoka tena chumbani kuja sebleni akamuulizia mama yake.

"Mmeelewana mama?"

"Ndio tumeelewana"

"Sawa jambo zuri"

Aisha alichokitegemea labda kuambiwa kua Suma amemmisi au kusalimiwa hakuskia Chochote akahisi tu lazima kutakua na jambo linaendelea,
alichukua simu na kuingia chumbani na kumpigia simu Suma lakini haikupokelewa Aisha aliumia sana na kujisemea.

"Najua sana kua tayari Suma ameshabailika na hawezi kunikumbuka Tena ila leo ndio mwanzo na mwisho wangu wa kumtafuta kama kuishi na mama yake nimeishi nae vizuri tu Sasa nimuda wangu wa kufanya mambo yangu na sio kurudi nyuma kisa mapenzi hapana"
Aisha alikua ana hasira sana na Suma lakini hakutaka kujionesha.

Majira ya usiku Sasa Suma alikua amelala zake sebleni mara akasikia sauti ya kilevi ikiwa inatukana sana na mlango ukafunguliwa Nadya akaingia akiwa amelewa sana kitu ambacho kilimshangaza sana Suma maana alifanya hivyo kabla na aliapa kutorudia na leo karudia Tena anatukana matusi makubwa sana Hadi Suma alikua anajiskia vibaya sababu alijua vyema hakuna miwngine anaetukanwa hapo zaidi ya yeye anaeyaskia hayo matusi.

Aliambeba Nadya na kumpeleka chumbani kisha akamlaza kitandani na yeye akarudi kulala sebleni akiwa anajiuliza kwanini Nadya awe hivyo?


Suma aliamka asubuhi kama kawaida yake na kumuandalia Nadya supu kisha akaenda kumuamsha Nadya aliamka na kuoga kisha akatoka sebleni akiwa amependeza mwenyewe akamuaga Suma kua anaondoka Suma akamuuliza.

"Nadya Kila siku huondoki bila kunywa chai na leo nimekuandalia supu kwaajili ya pombe ulizokunywa Jana"

"Suma sijiskii kula Chochote badae bwana"
Nadya aliondoka zake na kumwachia Suma kwenye mawazo sana akachukua simu yake na kukuta missed calls za Aisha akazifuta na kumpigia rafiki yake Juma wakakutana hapo kwenye duka la vifaa vya magari na akamuuliza.

"Vipi ile hela ambayo nilikuelekeza umefanya kama nilivyokuambia?"

"Yaani Suma mbona Bado kidogo tu kila kitu kinakua sawa"

Basi Suma baada ya kumaliza kuzungumza na Juma alitoka Hadi kwenye matengenezo na kumkuta Kila mtu Yuko bize na kusimamia matengenezo ya sehemu ya kuosha magari.

Wote walimshukuru sana Suma Kwa moto aliokua nao wa kuwainua kutoka pale walipokua, Suma akawambia kua wasijali Kwa Chochote kile.

Suma alirudi nyumbani mapema na kuandaa chakula vizuri na kukihifadhi kwenye hotpot kisha akawa anaangalia movie.

Siku hiyo Nadya alichelewa sana kurudi Suma alilala pale pale Hadi alishtuka baada ya kung'atwa na mbu na baada ya kumtazama saa ilikua saa7 usiku, bado Nadya hajarudi nyumbani ikabidi achukue simu kwaajili ya kutaka kumpigia simu iliita na kukatwa muda huo huo na baada ya muda mfupi Nadya aliingia ndani akiwa amelewa Tena kama siku iliyopita Hali ambayo ilikua inampa mashaka sana Suma.

Alisimama na kwenda kumdaka maana alitaka kuanguka na kuumia vibaya kutokana na viatu virefu alivyokua amevaa.

Suma aliumia sana kutokana na ile Hali, basi alimbeba na kumpeleka chumbani Tena na kumlaza kitandani huku alizungumza
"Nadya hiki unachofanya unanifanya niogope sana na mbona umebadilika ghafla niambie kama nimekukosea nijirekebishe lakini sio kunitenga na kunifanyia haya yote mke wangu kumbuka mimi ni binadamu pia Nina moyo Nadya tafadhali"

Nadya aliziba masikio yake na kugeuka upande wa pili kulala zake kitendo ambacho kilimuumiza zaidi Suma, basi hakua na namna akarudi sebleni pia akalala.

Hiyo ilikua siku ya Jumatatu na ikumbukwe kuwa tayari Nadya alishatumiwa ujumbe na mpenzi wake kua baada ya wiki moja anarudi hivyo hatujui huyo ni mpenzi wake au ndio kama alivyomwambia Suma kuwa alimsaliti.

ITAENDELEA.......

Jina la simulizi ni PENZI LANGU Je! Limefanya nini? Na limemtesa nani? Kuna watu wa 4 (Suma, Nadya, Aisha na huyo aliyetuma sms) ikiwa ni fupi nadhani ushauri wangu unaukumbuka. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 07

ILIPOISHIA.......

Hiyo ilikua siku ya Jumatatu na ikumbukwe kuwa tayari Nadya alishatumiwa ujumbe na mpenzi wake kua baada ya wiki moja anarudi hivyo hatujui huyo ni mpenzi wake au ndio kama alivyomwambia Suma kuwa alimsaliti.

ENDELEA NAYO.......

Upande wa Aisha hakua analala sababu ya mipango yake ya kuhusu kulipa kisasi na kilichokua kinamuwazisha ni nani ayamuamini kufanya nae kazi maana alimuamini sana mpenzi wake Suma lakini amehisi kua amemsaliti lakini hii siri ya Suma kumsaliti Aisha tunaijua Mimi na wewe ndugu msomaji ila Aisha na mama yake wote hawajui isipokua Aisha anahisi kutokana na vijitabia mbalimbali.

"Kama Suma ameweza kunisaliti nani naweza kumuamini Kwa kufanya nae kazi ya kulipa kisasi? na pia najua kua nikazi ngumu haihitaji vijana wavivu na najua pia itatumia pesa nyingi sama lakini sijali kuhusu Hilo nia na malengo yangu ni kulipa kisasi tu na lazima nifanye hivyo"

Aisha alichukua simu yake na kubofya sehemu kadhaa kisha akaweka simu sikioni kwake na simu iliita na kukata yenyewe na baada ya kutazama muda akatabasamu na kusema.

"Eeh kumbe ni usiku wa saa7 mmh aise lazima ndio maana hajapokea itakua amelala"
Kisha nae akavuta shuka na kulala zake.

Asubuhi mapema Aisha aliamka akavaa traki na vest yake na raba akatoka bila ya kumuaga mama yake Suma.

Upande wa Suma aliamka mapema kama kawaida yake kuandaa kifungua kinywa kwaajili ya Nadya, lakini Nadya mwenyewe aliamka na kuoga na kuondoka wakati huo Suma alikua bize na kazi zake nyingine na alivyorudi chumbani kwaajili ya kutaka kumuamsha Nadya hakumkuta na alipojaribu kuangaza kote hakuona hata gari ya Nadya, alikua anajiuliza sana sana na ilizidi kumfanya ajionee sio wathamani Tena hivyo akajisemea.

"Najua sasa nimechoka sana ndio maana haya yote hutokea huyu sio Nadya ambae nimemzoea, siku zote wanasema jiongeze kabla haujaongezwa hivyo hapa akili imo kichwani mwangu Sina muda wa kupoteza Tena."

Alichukua simu yake na kubofya sehemu kadhaa ya keypad yake na kuweka sikioni kwake.

Upande wa Aisha alikua kando ya barabara alikimbia na kufanya mazoezi ya viungo akiwa na hasira sana mara alipita kijana mmoja ambae nae pia alikua anafanya mazoezi akamwambia.

"Usitumie nguvu kufanya mazoezi maana utafanya mwli wako uchoke kupitiliza"

"Ahaa asatne sana kwa ushauri wako"

Mara simu ya Aisha ikaita alifungua zipu ya traki yake na kutoa simu Kisha kupokea bila ya kutazama nani alikua anapiga ikasikika tu sauti.

"Mama shikamoo..!"

"Marahaba Suma lakini Mimi sio mama yako"

"Aisha unathubutu vipi kuitikia Kwa kujiamini hivyo we mjinga sana Yani niambie mama yangu yupo wapi?"

"Aah sasa Suma naona umeota mapembe enewei kama unahitaji kuongea na mama yako basi mpigie kwenye simu yake mjinga mmoja wewe"
Aisha alikata simu na kuiweka kwenye traki yake na kuendele na mazoezi yake na yule kaka akiendelea kumsemesha.

"Kwanini unafanya mazoezi Kwa hasira nahisi Kuna jambo unapanga kufanya kama sikosei"

"Yeah nikweli lakini hayakuhusu"

Yule kaka ilibidi awe kimya Kwa muda kisha kumuacha Aisha akiendelea kukimbia Kwa kwenda mbeke na kurudi nyuma lakini mara ghafla wakati anarudi nyuma kuna gari ilitokea nyuma yake na kumpush Aisha na kumfanya aanguke chini kwa kukosa pumzika kutokana na mazoezi ambayo alikua anayafanya yalikua yana nguvu sana na yeye alikua anatumia nguvu na hasira pia.

Wakati lile jambo limetokea yule kaka ambae alikua anamsemesha Aisha aliona na haraka akawahi kumbeba na kumwambia aliyemgongaa ampeleke hospital na hakua mwingine alikua ni Nadya kutokana na msongo wa mawazo kichwani kwake.

Walifika hospital na baada ya kumfanyia vipimo akagundulika kuwa yupo salama ila alizima kwaajili kukosa hewa mshtuko tu lakini hakua ameumia, Nadya alifurahi sana maana hakuwahi kupata kesi ya kugonga hivyo alikua muoga sana.

Baada ya kupata nafasi ya kumuona Aisha alimuomba msamaha na Aisha akamwambia hana tatizo amemsamehe tayari kisha akalipia gharama za hospital na kuondoka zake.

Aisha alibaki na yule kijana, sasa wakati huo tayari walikua wanatoka hospital wakiwa wanatembea kawaida yule kijana akajitambulisha.

"Naitwa Samuel"

"Naitwa Aisha ila kwanini ulinisaidia wakati nilikujibu vibaya kabla?"

"Aisha tunatakiwa kuwa na moyo wa ubinadamu sawa wewe ulinijibu vibaya lakini Mimi sikutaka kukufanyia ukatili wa kutokusaidia sababu nisingepata faida yoyote kama ungekua umeumia halafu sijakusaidia lakini nimekusaidia nimepata kufahamiana na wewe"

"Ooh nikweli pia nisamehe kwa kukujibu vibaya"

"Usijali kuhusu hilo Aisha lakini nataka kukukaribisha nyumbani kwetu Kuna gym pia unaeza kuja kufanya mazoezi yote unayotaka wewe"

Aisha alitabasamu na kumuuliza.
"Serious unachosema?"

"Ndio karibu sana najua pia itakua nafasi kubwa sana ya kufahamiana kwa ukubwa zaidi"

"Asante saña unaonekana mkarimu sana Samuel.."
Aisha alimtajia namba ya simu Kisha wakaachana kwenye njia panda na Kila mmoja kuelekea nyumbani kwao.

Alirudi nyumbani kwao majira ya saa6 mchana akamkuta mama yake Suma amekua na wasiwasi alimsalimia na kutaka kuingia chumbani kwake mama Suma akamwambia.

"Kwanini unanikwepa Aisha?"

"Mama kwanini nikukwepe mama?"

"Aisha umekua hivyo Kwa muda hata Mimi naliona ndio maana nakuuliza shida Nini?"

"Hakuna shida yoyote mama ni mawazo yako tu hayo"

"Sawa unatoka wapi sasa hivi na hujavaa hata nguo huko juu?"

"Mama nimeanza kufanya mazoezi yangu Sasa na nitakua natoka Kila alfajiri ila bahati mbaya nilipata ajali kidogo ndio maana nimechelewa Leo"

"Ajali Gani Tena mwanangu ona Sasa jamanii"

"Usijali mama ilikua ya gari lakini sijaumia ndio maana nipo hapa"

"Pole sana mwanangu nenda kaoge uje kula"
Aisha aliingia chumbani kwake akajimwagia maji na kujilaza kitandani kwake.

Hatimae siku ya Jumanne ilifika usiku ndipo Aisha aliamka na kumwambia mama yake kua anajiskia vizuri akachukua simu na kumpatia mama yake na kumwambia.

"Suma alipiga akataka kuzungumza na wewe mpigie"
mama yake alichukua simu na Aisha akawa Yuko bize kutengeneza maziwa ya unga kuweka maji ya moto kisha akachukua na mkate akaanza kula huku alijifanya yupo bize na tv.

Mama yake Suma akawa anongea na simu na mwanae.
"Mama uko sawa kweli?"

"Suma nipo Sawa na Aisha ananijali sana kwani shida Nini?"

"Mama nataka kurudi nyumbani mimi maisha ya huku yamenishinda Sasa sitaki tena kuwa huku"

Mama yake baada ya kuskia hivyo akamuita Aisha hadi Aisha alishtuka na kujikuta akimwaga maziwa yake na kumfata mama yake na kumuuliza.

"Shida Nini mama?"

"Suma anataka kwenda kijijini"
Aisha alikata simu na kumwambia mama yake "Mama umeshaharibu najua Suma ameshakusikia tayari aah"

Aisha alichukua simu na kuingia nayo chumbani, kitu ambacho kilimshangaza sanaa mama yake Suma akasogea sebleni na kukuta maziwa yamemwagika akasafisha na kurudisha kikombe kwenye vyombo vichafu.

Upande wa Suma alianza kumtumia ujumbe Aisha kumuuliza kuhusu alichokisema mama yake Aisha hakua amejibu meseji hata moja ya Suma.

Muda ulizidi kwenda Kwa kusubiri ujumbe kutoka Kwa Aisha na Huku akimsubiria pia Nadya.

Siku hiyo alisota sana kusubiri vitu viwili Kwa wakati mmoja Hadi inafika asubuhi hakuna chochote alichokipata.

Suma siku hiyo akachukua karatasi na peni kisha akaandika waraka mzito sana na kisha akachukua nguo zote ambazo alikua amepatiwa na Nadya na kuviweka kitandani kisha akatoka nje na kufunga mlango na kuondoka zake hakuchukua kitu chochote zaidi ya kama vile alivyokua amekuja.

Alifika dukani Kwa Juma na kumwambia.
"Juma rafiki yangu pesa ambayo umekua ukiniwekea kwenye akaunti yangu inatosha sana kuanzia Sasa Kila pesa ambayo itakua unaipata hapa dukani ni yako na pia hili duka ni lako na kule car wash utawachia Rama na wenzie, Mimi wacha nirudi nyumbani kwetu"

"Suma unamaana unarudi Kijijini?"

"Ndio Juma narudi kijijini kwetu"

"Hapana usifanye hivyo Suma mbona tayari umeshaanza kutengeneza pesa nzuri tu jamanii?"

"Usijali Juma kwaheri kama Mungu akipenda tutaonana"

Suma alikua anatembea akiwa anawaza mambo mengi sana kichwani kwake na hasa kuhusu mama yake na Aisha maana hakua amepata jibu sahihi kuhusu wao.

Upande wa Aisha na yeye kama kawaida yake alitoka nyumbani kwake mapema sana alianza na zoezi la kukimbia kabla hajafika mbali simu yake iliita na mpigaji alikua Dan walisalimiani kisha Dan akamuuliza.

"Dada Aisha ulinipigia juzi usiku Jana nilikua bize sana sikuweza kukutafuta lakini leo nipo Sina mzunguko wowote vipi kuna tatizo lolote?"

"Dan mdogo wangu naomba niandalie safari yangu ya kuondoka nchini nadhani nitakupa taarifa siku Gani naondoka lakini Kaa attention Kwa hili jambo"

"Ooh sawa dada Aisha hakuna shida Kwenye Hilo vipi lakini unahitaj Chochote?"

"Hapana Dan we endelea na mambo Yako tu usijali"
Dan alikata simu na kuonekana mwenye matumaini fulani maana alionekana kua na furaha sana mwisho akasema.

"Hatimae sasa nadhani atakua na furaha sana Baada ya kuwaona"

Upande wa Aisha akakumbuka kua siku ya Jana alipata namba ya mtu ambae alimwambia kuhusu gym haraka aligeuka na kurudi nyumbani kwake na kuingia ndani, ilikua tayari saa mbili alimkuta mama Suma amekaa sebleni alimsalimia na kuingia chumbani kwake alitoka akiwa na funguo kichwani kwake akiwa amevalia kofia na Sweta jeusi na raba nzuri sana akamuaga mama Suma.

"Mama naondoka nitachelewa kurudi kidogo hivyo kama utajihisi njaa andaa chakula ule usinisubiri Mimi"

Mama yake Suma alimsogelea na kumshika mkono wake na kuzungumza kwa upole sana.

"Aisha mwanangu mbona umebadilika sana tatizo nini mama?"
Aisha aliutoa mkono wa mama Suma na kumwambia.

"Hilo swali Mimi sio wa kuniuliza mama naondoka zangu sasa hivi"

Aisha alivaa miwani yake na kuondoka zake, na kumwacha mama Suma akiwa Kwenye sintofahamu.

Aisha alifika nnje na kupanda Kwenye gari alichukua simu yake na kumpigia Samuel simu iliita mara kadhaa kisha ikapokelewa.

"Halo Samuel mambo Yako?"

"Poa Aisha vipi unaendeleaje?"

"Niko poa Sasa basi mambo yasiwe mengi naomba unielekeze wapi ulipo nije Kwenye gym yenu"

"Anhaa washa data na kisha zama Kwenye map utaona mahali nilipo"

"Sawa Samuel nimekuelewa"
Aisha alikata simu na kufanya kama alivyomwambia na Samuel, kisha akaona sehemu anayoishi Samuel hapakua mbali na sehemu ambayo anaishi hivyo aliwasha gari na kuondoka zake.

Alikua ameweka headphones kichwani kwake huku anaendesha gari huku anapata mziki mzuri kutoka Kwa wasanii wenye vipaji wa huko marekani.

Mara ghafla akiwa barabarani Kwenye mwendo wa kawaida akampita mtu ambae nikama anamfahamu hivyo ikabidi arudi nyuma ili ajue ninani au amemfananisha.

Aisha alirudisha gari nyuma na kumfikia huyo mtu na kumpigia honi alivyogeuka lahaula hakua mwengine alikua ni Suma Aisha alimshangaa sana akashuka Kwenye gari na kumuuliza.

"Usitake kuniambia kua unaigiza maisha"

"Aisha kwanini uko hapa, hivi ni wewe kweli?"

"Suma kwani Mimi si mkazi wa huku kwanini unataka kujua sababu ya Mimi kua hapa?"

"Aah Aisha mama...."

"Suma kuna sehemu naenda kwa Sasa kwaheri"

Aisha aliingia Kwenye gari na kubamiza mlango wa gari, Kwenye harakati za kuvaa mkanda aweze kuondoka Suma aliufungua mlango wa pili wa Kwenye gari hiyo na kuingia na kukaa kando ya Aisha kitu ambacho kilimshangaza sana Aisha akamuuliza.

"Unataka nini Kwenye gari yangu?"

"Aisha siwezi kukuacha uwende popote pale nahitaji kujua mama yangu Yuko wapi?"
Aisha hakujibu kitu Chochote aliwasha gari akachukua headphone zake kama kawaida na kuzivaa kisha akaendelea na safari yake hadi sehemu husika.

Aliingiza gari ndani ya nyumba yenye geti kisha akampigia simu Samuel na baada ya muda mfupi Samuel alitoka ndani akiwa na kitaulo chake Cha kujifuta jasho na baada ya kumuona Aisha alimkaribisha na kumbatio kisha wakaingia ndani, wakati huo Suma alikua bado yupo Kwenye gari hakutaka shobo sababu alikua fika kua pale sio nyumban kwao na Aisha na kama ingekua pale Aisha angesema Chochote lakini alovyojiwazia akilini mwake ndicho alichokiamua.

Alisubiri Kwa muda kama lisaa1 na nusu Aisha Bado alikua hajarudi garini kitu ambacho kilianza kumfanya awe na wasiwasi sana kuhusu Aisha akasema hatakama nimemsaliti lakini siwezi kuona ujinga unaendelea wakati nipo tu hapa nimekaa.

ITAENDELEA........
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 08

ILIPOISHIA.......

Alisubiri Kwa muda kama lisaa1 na nusu Aisha Bado alikua hajarudi garini kitu ambacho kilianza kumfanya awe na wasiwasi sana kuhusu Aisha akasema hatakama nimemsaliti lakini siwezi kuona ujinga unaendelea wakati nipo tu hapa nimekaa.

ENDELEA NAYO.......

Wakati anataka kufungua mlango wa gari mara akaona mlango umefunguliwa na Aisha alitoka ndani akiwa na taulo pia akijifuta jasho kisha akaingia Kwenye gari na bila ya kuzungumza Chochote na Suma.

Muda wote Suma alikua anamtazama Aisha Kwa shauku ya kutaka kujua Nini kimetokea kule ndani lakini Aisha alikua bize na kuendesha gari huku akiimba nyimbo ambayo alikua anaisikiliza.

Walifika nyumbani kwao Aisha alishuka Kwenye gari na kuchukua vifaa vyake na kuingia ndani akamkuta mama Suma amelala akapitiza Hadi ndani chumbani kwake.

Suma pia aliingia ndani kwa kuchelewa sana kutokana na kutazama ukubwa wa nyumba na mazingira pia, ukweli ilikua mitaa ya kishua sana.

Alipita ndani na kumkuta mama yake amelala Kwenye sofa, haraka alimsogelea Kwa furaha na kumuamsha.

"Mama..! mama ... mama Suma!"
Mama yake alivyoamka na kumuona mwanae alimkumbatia kwa furaha sana akamwambia.

"Nilihisi naota kumbe uko hapa kweli? Mwanangu nilikukumbuka sana Suma wangu tazama Sasa Aisha amenifanyia Kila kitu amekua akinipenda sana sana Hadi amenifanya niwe natembea na Hadi afya yangu imerejea upya kwasababu yake"
Suma alijiskia amani ya moyo lakini alikua na mawazo sana kuhusu alichokifanya.

"Mama Aisha ni Binti mwenye moyo wa kipekee sana na hakuna mwanamke mvumilivu na mwenye upendo kama Aisha na naamini kua sikufanya ubabaifu Kwenye chaguo langu"

"Nikweli kabisa mwanangu lakini mbona umekua hivyo shida Nini wakati tulipokua tunaongea na simu ilikua unaonekana mwenye furaha tatizo Nini?"

"Mama Nina mengi ya kuwasimulia wewe na Aisha Wacha tumsubirie kisha nitawaambia"

"Lakini Aisha ametoka mbona"

"Mama nimerudi na Aisha, Mimi hapa nisingeweza kufikia hapa bila yeye"

"Ooh kumbe, nilikua sijamuona hivo"

"Itakua yupo ndani"

Muda mchache mara Aisha akijitokeza na kupitiliza Hadi jikoni akajiandalia maziwa yake kama kawaida kisha akasogea seblen akawasha tv na kuanza kutazama.

Wakati anaendelea kula chakula na kutazama tv mara simu yake iliita na haraka akapokea na alijikuta akipaliwa na kukimbilia nje kutapika upande wa Suma ilimjengea picha tofauti sana alihisi hata Aisha alikua anamsaliti pia na huko kutapika hakuna kingine zaidi ya mimba, ikabidi amfate Aisha nnje na kumkuta ameacha simu inaongea yeye akiwa anaendelea kutapika, wakati huo Suma amesimama mlangoni akimtazama.

Aisha Baada ya kumaliza kutapika alichukua simu na kuzungumza.
"Dani nimetapika najisikia vibaya sana je leo unaweza kuja kumuona halafu nataka tuzungumze kitu muhimu naomba usichelewe kuja nitaboeka sana"
Aisha alipomaliza kuongea na simu alisimama na kurudi ndani lakini alivyopiga jicho mlangoni akamuona Suma hakutaka kuongea nae chochote alipita mpaka ndani na kumwambia mama yake.

"Mama nipo ndani najisikia homa"

"Sawa mwanangu pumzika"
Aisha aliingia ndani na kuwaacha wenyewe wakizungumza.

Upande wa Suma alitamani sana kuzungumza na Aisha lakini nafsi yake ilikua inamsuta sana Kwa kile alichokifanya yeye pia ilikua inamuumiza sana.

Muda ulizidi kusogea hatimae ilifika jionj ilikua majira ya sa12, Aisha aliamka akaanza kuandaa chakula cha usiku Huku akiwa kimya kabisa ukweli alitamani sana kumuuliza Suma kwanini alikua anamdharau kwenye simu, hapokei simu zake lakini alishindwa kumuuliza sababu hakutaka kujionesha kama ni dhaifu kwake hivyo alikua anasubiria Suma ndio aanze kumuuliza.

Alimaliza kuandaa chakula Kisha akakiweka mezani kwaajili ya kuliwa tayari ilikua saa mbili usiku alichukua sahani yake na kujiwekea chakula chake na kusogea sebleni na kumwambia mama yake.

"Mama ukiwa unajisikia kula chakula kipo tayari pale mezani"

Suma alipoona Aisha anaelekea upande wake akajua moja kwa moja anapelekewa yeye kile chakula alijikalisha vizuri kwaajili ya kukipokea lakini Aisha akasogea mikono pembeni akabadilisha channel na kumuwekea channel ya movie ambayo anapenda mama yake na Suma.

Suma alizidi kujisikia vibaya Kwa kutengwa na Aisha akaamua kumfata Aisha pia na kumshika mkono ule ambao alikua ameshika sahani ya chakula na ile nguvu aliyotumia kumshika Aisha alishindwa kujibalansi na sahani ya chakula ikaanguka chini Aisha alimtandika kofi Suma na kumwambia.

"Usijifanye wewe ni mwenye nguvu pekee Sawa eeh shida yak....!"

Kabla hajazungumza akaanza kutapika Suma alimsogeza chini na kumtazama Kwa jicho la Maumivu sana Hadi alishindwa kujizuia.

Upande wa Nadya kama kawaida yake alirudi usiku sana ila siku hiyo alikua mzima kabisa hakua amelewa na wazo lake lilikua la kuja kumwambia ukweli Suma kuhusu ujio wa mpenzi wake lakini alivyofika akakuta nyumba ipo kimya sana aliingia ndani na kuwasha taa zote na kitu cha kwanza aliingia chunbani kwake maana ukimya huo ulimtia mashaka sana na kuhisi Suma ameshamuibia pesa zake.

Alipoingia chumbani kwake akakuta kitanda kimetandikwa vizuri sana na baadhi ya vutu vikiwa juu ya kitanda akaachana navyo sababu yeye alikua na mawazo na pesa tu Kwa muda huo.

Alifungua kabati lake na kutazama kwenye sanduku akakuta pesa kama zilivyo vile vile akafunga vizuri na kurudi kitandani akakuta nguo zote ambazo alimpatia Suma na Kila kitu kilikuwepo hapo akawa bado anajiuliza kuhusu Suma ni kijana wa aina Gani lakini kwenye harakati flani akaona karatasi nyeupe juu ya dressing table alisogea na kuichukua kisha kuanza kusoma.

"Mpendwa Nadya, nimeamua kuondoka nyumbani kwako kutokana na mambo mabaya ambayo umekua ukinifanyia, mwanzo nilipotezea na kukupa muda zaidi wa kukufanya ujifunze lakini Bado haukuonesha kubadilika nimekua nikifanya Kila kazi ambayo ulitakiwa kufanya kwangu kama mwanamke lakini sikuwahi kukuambia sababu nilijua kua unaishi na mimi kwa nguvu ya pesa zako.

Nadya nilimsaliti mwanamke ambae nampenda sana ambae alinifundisha Mimi mapenzi, mwanamke wa kwanza kwangu kunifanya Mimi kuitwa mwanaume nikamsaliti sababu yako.

Nikweli kwamba mwanzo nilikua sikupendi na nilikuambia ukweli lakini hukujali nilichosema, ukaja ukaniteka na penzi lako lakini nataka ujue Leo kua sikua na wewe kwaajili ya tamaa ya pesa sababu kama ningekua hivyo ningekua nakuibia pesa zako na kuwatumia familia yangu lakini tumekua tunalala na pesa ndani lakini Kijijini kwetu mama yangu anaugua na kushinda na njaa lakini hukuwahi kunisikia kulalamika kwako hata mara moja.

Nadya naumia kuona kuwa hutokuja kupata mwanaume mkarimu na mwenye huruma kama Mimi na usimdharau mtu Kwa umakini wake jali utu, pesa majumba magari ni vya kupita lakini upendo wa kweli unadumu milele na hauwezi kufutika.

Najua umebadilika sababu ya kua mwanaume wako ambae uliesema amekusaliti amekuambia kua anarudi na niliiona hiyo meseji ukiisoma lakini sikutaka kukuuliza chochote sababu tayari nilishajijengea akilini mwangu kuwa maskini Hana kauli Kwa mtu mwenye pesa japokua nilikua naumia mara mbili kwa kumsaliti mpenzi wangu na wewe kunisaliti Kwa kila nilichokifanya kwako Nina mengi ya kuyaeleza ila sitaki kukuchosha nakutakia Maisha mema na yenye furaha na mpenzi wako kwaheri Nadya"

Nadya alipomaliza kusoma huo ujumbe kwenye karatasi na Kila kitu alichokisema Suma kilikua Cha ukweli hivyo ilikua inamuumiza sana maana hata yeye tayari alikua anampenda sana Suma.

Lakini akiwa analia na kuumia moyo wake alikua anarejesha Kila kitu kwenye sehemu yake husika na mara Ghafla mlango ukaanza kugongwa Nadya haraka akatoka sebleni kwaajili ya kufungua mlango na Baada ya kufungua mlango hakuamini macho yake.

Upande wa Suma na Aisha, Suma alikua anatetemeka Kwa hasira na Maumivu mbele ya Aisha akiwa ameinamia chini Suma akaanza kuongea.

"Aisha najua nimekuumiza sana lakini hukuwahi kumtupa mama yangu ulimpenda na kumlinda na kumuheshimu lakini Mimi nilikua mbaya kwako Aisha lakini naomba unisamehe sana kwa nitakacho kueleza Aisha"
Aisha alikua anaumia sana moyoni mwake na alihisi tu kitu kibaya hivyo alimwambia Suma.

"Hapana sitaki kusikia Chochote kutoka kwako Suma usije kuniumiza bure"

"Aisha Mimi kuzungumza na wewe ni kama naondoa kitu kizito moyoni mwangu naomba unisikilize Aisha"

Aisha alikua anaumia sana na kutamani hata kulia sababu walipokua kijijini walikua wanakua wote na kubembelezana pamoja ikitokea tu pale ambapo wamekoseana, lakini Kwa awamu hii Aisha alikua hataki kuonesha udhaifu wake mbele ya Suma.

Suma alizungumza Kila kitu kilichotokea na alichokifanya kitu ambacho kilimuumiza sana Aisha na kuamua kuingia ndani akiwa analia kwa uchungu sana (acheni tu nyie Maumivu ya mapenzi kwa aliekusaliti yanauma sana)

Suma alimkimbilia na kumshika Aisha aweze kumsamehe, Aisha nae alimsimulia Kila kitu kilichotokea kijijini ya kutaka kubakwa na pia kuhusu mwenyekiti wao pia nayo Suma ilizidi kumuumiza na kujutia kumuacha Aisha wake.

Walikua wamekaa kwenye sofa wakati huo wote walikua wamekaa vya kutosha sana mama yao akawambia.

"Najua wote mmepitia nyakati mgumu Kila mmoja Kwa wakati wake lakini Suma ulichokifanya sijakipenda hata kidogo kumsaliti mwenzio lakini naomba sana Aisha umsamehe mwenzio kama kosa tayari amekiri kikubwa ni wewe kumsamehe mwenzio"

Aisha akasema
"Suma Sina kinyongo na wewe nimekusamehe kuwa na amani kuanzia sasa pia karibu sana"

Aisha baada ya kusema hivyo alisimama na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake.

Mama yake Suma akampa ishara mwanae kuwa amfate, Suma alifanya hivyo akamkimbilia Aisha chumbani na wakati anafika mlangoni tayari Aisha alishabamiza mlango wa chumbani.

Suma alimuomba sana Aisha afungue mlango lakini Aisha hakufungua mlango.

Alichukua simu yake na kumpigia Dan na kumwambia afanye mpango wa tiketi ya ndege na kwakua ilikua mapema Dan alimnunulia tiketi haraka kupitia mtandaoni Kisha akamwambia ipo tayari ndege ya sa12 asubuhi Aisha alianza kupanga nguo zake kwenye begi na Kisha akapanda kitandani kulala japokua ilikua ngumu sana kwake kupata usingizi lakini alijilazimisha Hadi akapata usingizi.

Upande wa Nadya pia mpenzi wake alipomuona akamuuliza.
"Vipi mpenzi hujafurahia kuniona? hujanimisi?"

"Aah hapana karibu ndani basi"

Aliingia ndani Nadya akamuuliza
"Nikuandalie Nini ambacho utakula sasa hivi?.."

"Noo baby inamaana umenisahau kabisa Nadya wangu sikia mie nishakula tayari yaani hapo usinizungushe mwenzio nimekumiss sana eti"

Kabla ya Nadya kuongea Chochote tayari alishavamiwa na kumpelekea chumbani mambo yalibamba ipasavyo.

Asubuhi mapema Aisha aliamshwa na mlio wa simu yake alipotizama mpigaji alikua Dan akaamka haraka na kujiandaa kisha akatoka na begi lake bila yoyote kushtuka alipofikia sebleni akamkuta Suma amelala kwenye sofa akamuwekea karatasi karibu yake na kuondoka zake.

Suma aliamka na kukutana na karatasi akaichukua na kuanza kuisoma.

"Mpendwa Suma, natumai ni mzima wa afya kwanza kabla ya yote nisamehe sana kwa kutokufungulia mlango usiku wa Jana najua umejiskia vibaya sana ila sikua na chaguo kingine, tukiachana na hayo Suma nakupenda sana sana nimeamua kuondoka sababu Sina chaguo lingine la kufanya kwasasa nimeamua kujitenga mbali na wewe sababu sitaki kuiona sura yako kwasasa Kila nikikuona nakumbuka maneno mengi yaliyotokea baina yetu hivyo nataka kukaa mbali na wewe Kwa kujipa muda angalau lakini nataka utambue kua nakupenda sana Suma mpenzi wangu mume wangu,
nimeacha funguo za gari chumbani na simu pia ambayo utaitumia na tutakua tunawasiliana kama utahitaji Kila kitu kipo ndani kama utahitaji msaada wowote Kuna namba nimesave Dan utamcheki niagie na mama kwaheri.."

Suma Baada ya kumaliza kusoma ule ujumbe alipandwa na hasira sana na kuanza kupiga kelele za hasira Hadi mama yake akatoka chumbani kutaka kujua Nini kinamsumbua.

Suma alipiga magoti kwenye miguu ya mama yake huku akilia sana kumwambia kua Aisha ameondoka, taarifa zile hata mama yake zilimuuma sana kwanini aondoke.

ITAENDELEA......
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 09

ILIPOISHIA.......

Suma Baada ya kumaliza kusoma ule ujumbe alipandwa na hasira sana na kuanza kupiga kelele za hasira Hadi mama yake akatoka chumbani kutaka kujua Nini kinamsumbua.

Suma alipiga magoti kwenye miguu ya mama yake huku akilia sana kumwambia kua Aisha ameondoka, taarifa zile hata mama yake zilimuuma sana kwanini aondoke.

ENDELEA NAYO......

Nyumba ilipoa sana Baada ya Aisha kuondoka Kila mtu alikua ana mawazo juu ya Aisha atakua wapi na atakua anafanya Nini Suma alikuaa ana mawazo sana mama yake akamwambia.

"Suma mwanangu kwanini tusirudi Kijijini kwenye Maisha yetu ambayo tumezowea kuishi nimechoka kuishi Maisha haya yasiokua na furaha Kila siku Maumivu yasiyoisha"

"Mama usiseme hivyo Aisha ananipenda sana na amefanya hivi ili kuupima tu moyo wangu naomba kuwa na Imani nae atarudi tu mama"

"Mwanangu sasa huna kazi utategemea vitu ambavyo ameacha mwanamke kweli?"

"Mama sio hivyo hata nilipokua nakaa nilikaa Kwa akili na tahadhari pia najua nilifanya kosa la kuchukua pesa pasi na mwenyewe kuniruhusu lakini niliirejesha kama ilivyo Baada ya kufanyia kile nilichohitaji mama na sasa hivi Nina pesa ya kuanzisha kabiashara"

"Ooh kweli mwanangu?"

"Ndio mama"

"Sawa basi usichelewe kuanza kufanya biashara maana huwezi kukaa tu kwenye hii miji ya watu"

"Sawa mama nitaanza kufanya hivyo"

Suma na mama yake walianza kufanya mpango wa kumtafuta sehemu ya kufanyia biashara, huku upande wa Nadya Sasa mambo yalikua moto penzi paja pika pakua na mpenzi wake akamsahau Suma kwa haraka sana.

Siku Moja wakiwa wamekaa kwenye bustani Nadya akiwa amelala kwenye miguu ya mpenzi wake ambae hata jina lake Bado halikua limetumika mara Ghafla alijisikia vibaya alihisi mvurigano wa ajabu na kujihisi anataka kutapika hivyo alisimama na kusogea Kando kwaajili ya kutapika.
mpenzi wake alimfata na kumuuliza.

"Unajisikia vibaya sana mpenzi?"

"Hapana nimejihisi tu tumbo linauma nikajikuta natapika tu"

"Pole sana twende hospital basi"

"Hapana Isaya Niko sawa"

"Basi Sawa hakuna shida"

Isaya alirudi kwenye kimkeka na kukaa huku akichezea simu yake, Nadya alisigea pale alipokaa Isaya na kumkuta anatabasam akamuuliza.

"Mbona unatabasamu hivyo?"

"Aah usijali mambo ya mitandao tu mwenyeewe si unaelewa mpenzi, haya njoo ulale mana napenda sana kushika nywele zako"

Nadya akajiskia Tena ile Hali na haraka akaenda kutapika Tena, Isaya aliingia ndani na kutoka na funguo za gari na kumwambia.

"Tunaenda hospital usitake homa ikuzidie usiku tukaanza kusumbuana siwezi kuamka usiku kukimbizana hospital"

Isaya alimshika mkono Nadya Hadi kwenye gari Kisha akawasha gari na kuelekea hospital.

Baada ya kumfanyia vipimo vyote na majibu yalitoka kuwa Nadya mjamzito wa mwezi mmoja na wiki moja, Isaya alimtazama sana Nadya na kumwambia kwa hasira.

"Nilijua hili kabla Nadya sababu marafiki zangu waliniambia kua wewe ulimiliki mwanaume ndani na ndio maana hata siku ya kwanza wakati tunafanya tendo nilihisi utofauti mkubwa sana sikutaka kukuambia sababu najua wewe ni binadamu pia una hisia zako lakini hili suala la kupata mimba Mimi siafiki hata kidogo mama wee"

Isaya alikuaa ana hasira sana akamshika mkono Nadya na kumuingiza kwenye gari na kurudi nae nyumbani kwake na Kisha akaingia Moja Kwa Moja chumbani kwake na kutoka na begi Kisha akamwambia.

"Nadya kama nilivyosema siwezi kurudia tena, nilikufanyia mpango wa kazi kwenye kampuni ya rafiki yangu na pia nilikupa pesa nyumba na magari matatu hayo hapo nnje lakini hukutaka kunivumilia Sasa basi naondoka zangu na usahau kama ulikua na mwanaume ambae aliitwa Isaya akakuthamini na kukupa Kila kitu kwaheri"

"Isaya naomba nisamehe naweza hata kutoa hii mimba ili ubaki na mimi"

"Unataka kujifanya mauwaji Tena, kama unataka kutoa mimba una nidhihirishia kua unaroho mbaya sana hata Mimi unaweza kuniua pia Wacha niondoke"

Safari hii Isaya alichukua nguo zake na kila kitu chake na kuondoka zake, Nadya alibakia na maumivu yasiyopimika moyoni mwake.

Upande wa Aisha alikua na siku kadhaa huko ulaya lakini pia alipokewa na watu ambao hakuwafahamu na walikua nae Kwa wiki nzima bila ya kumwambia chochote ikabidi awaulize Kwa kutumia lugha ya kingereza sababu alikua amesoma Hadi kufika chuo na matatizo yaliyotokea yakamfanya yeye kuacha chuo.

"Kwanini mmenileta hapa nani amewatuma?"

Mmoja akatoa simu mfukoni na kumuonesha Aisha Aisha alimuona Dan akamuuliza.
"Dan kwanini unanifanyia hivi lakini? Muda wote nipo tu ndani kwahiyo nimeletwa Huku kama mateka au?"

Jibu lilitoka upande mwingine ambapo waliingia mwanamke na mwanaume na kitoto kidogo Cha kiume Aisha alishtuka sana na kusema kwa mshangao mkubwa sana.

"Hii inawezekana vipi mama, baba na Harith...?"

Baba yake akazungumza
"Inawezekana sana mwanangu kwa uwezo wa Mungu"

Aisha alisimama na kuikumbatia familia yake huku akitoa machozi ya furaha sana Kisha akawauliza.

"Mama ilikuaje Yani mpaka mkawa hapa?"

"Aisha mwanangu ni story ndefu Sana ila ni kwa msaada wa Dan pekee"

"Ina maana Dan ndie ambae amewasaidia na wale ni nani ambao wameuwawa?"

"Aisha Binti yangu usiwe na wasiwasi kuhusu sisi okay? sisi tupo salama kama alivyosema mama yako ila Dan ndio msaada wetu mkubwa sana alimteka Harith na kumpeleka mafichoni pia akawateka watu ambao wanafanana na sisi miili na Kisha akawatengenezea sura ambayo zinafanana sura zetu Kisha hao vijana waliomtumia Dan Kwa kumlipa pesa waliwauwa na kwenda kuwafukia mbali sana na wewe hakuweza kukusaidia kutokana na Hilo jambo lilikua la Ghafla sana pia kukuteka wewe alitumwa mtu mwingine"

"Aah mama poleni sana lakini namshukuru sana Mungu kwa miujiza iliyotokea kwenu, mama lakini hata hao waliokufa ni wazazi wa mtu pia na Nina hakika kua Dan atanipa taarifa zote kuhusu hao watu"

"Unataka kufanya nini Binti?"

"Hamna baba kua na amani tu"
basi pale walipiga story nyingi Kisha wakapata chakula Kwa pamoja kama familia Kisha wakaingia ndani kwaajili ya kulala lakini kabla Aisha hajalala mama yake aliingia chumba kwake na kumwambia.

"Binti yangu nani alikuokoa na ilikuaje hasa?"

"Mama waliniwashia moto mkubwa sana kiasi kwamba walitaka kuniuwa Kwa Maumivu na mateso ya ajabu lakini alitokea kijana mmoja na kuniokoa huwezi amin mama, kulikua na watu wengi ambao walikua wanashuhudia msitu ukiungua lakini hakuna aliyesogeea zaidi ya huyo mkaka nikawa naishi kwao nilisahau matatizo yote sababu yake, alikua mkarimu sana yeye na mama yake na nikajikuta nampenda na Baada ya kumuelezea kuhusu hisa zangu hata yeye hakuzipinga akakubali kua na mimi ukweli nampenda sana"

"Sawa nafuraha sana kusikia hivyo lakini mwanangu kwanini tusiishi hapa kuondoa hatari iliyopo maana najua Kila kitu chetu kizuri na kikibwa kipo kule lakini hivyo vitu sio kitu muhimu kama roho zetu"

"Mama nafahamu lakini tayari Niko na familia mpya mama na siwezi kuisahau au kuitelekeza mama"

"Inamaana sie sio familia yako tena?"

"Hapana mama sio hivyo na simaanishi hivyo lakini niliishi na ile familia Kwa upendo sababu niliamini kua nyie tayari hamko duniani mama"

"Lakini tupo Aisha"

"Mama nenda kalale Bado nitakuepo na Kila siku nitakapokua hapa nitapata kuyajua mazingira huku nikiwa nataka kufanya maamuzi yangu basi nitawashirikisha"

Mama yake Aisha alitoka chumbani Kwa Aisha na kumuacha mwenyewe Kisha Aisha alichukua simu yake na kumpigia Dan walipiga story nyingi sana Kisha akamuuliza kuhusu kutafutwa na mtu yoyote lakini akamwambia hajawahi kutafutwa na mtu yoyote, Aisha alikata simu na kumpigia simu Suma na Kwa bahati Suma alikua mtandaoni akaona namba ngeni akapokea ilikua video call akamuona Aisha wake alifurahi sana na haraka akaelekea karibu na mama yake na kuanza kuzungumza nae Kwa furaha.

Aisha alimwambia kua amewakumbuka sana kitu ambacho kiliwarudisha kwenye matumaini mapya kuwa Aisha tayari ameshasahau yote na kutaka kuanza upya Suma akamuuliza.

"Unarudi lini Aisha wangu maana nimekumiss sana mke wangu"

"Suma siwezi kurudi Hadi nione umebadilika"

"Aisha Mimi mbona nimeshabadilika mpenzi wangu angalia tayari nimekonda Kwa kukosa kukuona Kwa zaidi ya wiki sasa"

"Suma acha utani wako"

"Fanya urudi uniponye maradhi yangu Aisha"

"Suma nataka kulala sasa Bai"

"Aisha usikate simu Kuna kitu nataka kukwambia"

"Suma kitu Gani Tena?"

"Nakupenda sana Aisha naomba tuanze upya mke wangu najua nimekukosea lakini nakosa furaha kabisa nisipokua karibu na wewe nielewe mpenzi"

Aisha alijikuta anatamani kupaa na maneno ya Suma yaliyokua matamu ya upole sana hapo ndipo alikua anammaliza sana Aisha, akajikuta anamwambia kua anampenda pia na atarudi siku sio nyingi Suma alipiga kelele za furaha sana na Aisha akakata simu na kuikumbatia Kwa furaha sana.

Maisha yaliendelea kua ya furaha Baada ya kuzungumza kati ya Suma na Aisha.

Upande wa Nadya alikua anapitia mateso sana ya kumkumbuka Suma na Huku Isaya alishafanya maamuzi ya kumuacha Nadya maana hakutaka kutulia na mwanaume mmoja.

Kila siku ilikua ya Maumivu na mateso sana kwake ilifika hatua hata kazini hakua akienda kutokana Hali ya mawazo aliyokua nayo.

Nadya alianza Kwa kuuza magari Yake mawili na kubaki na gari Moja tu.
Siku zilienda na hatimae miezi Tisa ikatimia na Nadya alijifungua mtoto wa kiume mzuri sana ambae alifanana sana na Suma.

Alikua anaishi mwenyewe na mtoto lakini Bado alikua anammiss sana Suma.

Aisha alirudi kutoka ulaya Kwa surprise ya kushtukiza, siku Moja Suma alikua anajiandaa kwaajili ya kwenda kazini kwake lakini alipofungua mlango hakuweza kuamini kumuona Aisha wake alimkimbilia na kumbeba Kwa furaha sana Kisha akamshusha na kumkumbatia na kumwambia.

"Namshukru sana Mungu kua umerudi salama"

"Nafurahi kukuona Tena Suma,lakini unaenda wapi?"

"Nilikua naenda kwenye biashara yangu lakini siendi tena nataka nishinde na wewe tu mke wangu"
Aisha alitabasamu sana akataka kubeba begi lake Suma akamtuliza na kumbeba Hadi kwenye ngazi ya kuingilia ndani Kisha akarudi kuchukua begi la Aisha na kumshika kiuno Aisha wake na kuingiwa nae ndani mama yake alipomuona Aisha alipiga vigelegele vya furaha akamkumbatia Aisha na kumwambia.

"Ni vyema kuwa umerudi mapema maana nilikua nasiku chache nataka kurudi kijijini"

Aisha alimgeukia Suma na kumgeukia mama yake pia Kisha akamuuliza.
"Kwanini urudi kijijini Tena mama?"

"Sikua natarajia kama ungerudi Aisha ulitoka ukiwa umekasirika sana"

"Mama ni hasira tu ambazo Kila aliyeumia huwa nazo lakini tayari tumeyamaliza na nimekuja kuishi na Suma Kama mke na mume"....

ITAENDELEA.......

Aisha amesharudi kuja kuishi na Suma wake, na huku Nadya ameshajifungua mtoto wa Suma. Yajayo yanafurahisha, jina la simulizi ni PENZI LANGU
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA.......

"Sikua natarajia kama ungerudi Aisha ulitoka ukiwa umekasirika sana"

"Mama ni hasira tu ambazo Kila aliyeumia huwa nazo lakini tayari tumeyamaliza na nimekuja kuishi na Suma Kama mke na mume"

ENDELEA NAYO......

Suma na Aisha walikua na furaha sana sababu walikua wanafanya Kila kitu Kwa ushirikiano sana, siku nyingine walikua wanatoka na kwenda Kwenye biashara wakiwa pamoja na watu wengi ambao walikua wanamfahamu Suma Kwa muda mfupi hawakuacha kuwasifia kua wanapendezana sana wakiwa pamoja kitu ambacho kiliwafanya kuzidi kupendana zaidi.

Siku Moja wakiwa wanarudi nyumbani ilikua tayari majira ya usiku sana Aisha akamwambia Suma.

"Halafu baby unajua sahivi nachoka sana kwahiyo sasa hivi sitakua nakuja dukani kwako nitakua nyumbani na mama"

"Aisha mke wangu hua napata Hali flani ya furaha pindi napokua na wewe dukani, au zile bidhaa ndio hua zinakuchosha?"

"Hapana baby nikwamba tu nahisi ni kwaajili ya kukata mda mrefu pale ndani bila kujinyoosha halafu pia baby naomba niendelee kufanya mazoezi kama mwanzo"

"Ooh Hilo halina shida lakini tutakua tunafanya wote kabla ya kwenda kazini kwangu"

"Suma jamani..!."

"Niite mume wako sio Suma Tena"

"Sawa mume wangu"

Basi walipiga story nyingi na kupanga mambo mengi sana Hadi wanafika nyumbani kwao.

Waliingia ndani na kumkuta mama yao kama kawaida yake anapenda sana kufatilia tamthilia , walimsalimia kisha Aisha akaingia chumbani Suma pia alimuaga mama yake kua anaenda kuoga kisha aje kula chakula, Suma alipoingia ndani akamkuta Aisha amejilaza kitandani akamuuliza.

"Enhe vipi kujilaza hapo umeoga na kuhusu kula pia?"

"Baby yaani sijiskii kula Chochote Wala hata kuoga pia"

"Hee we Aisha amka bwana tukaoge wote basi maana wewe unataka kunifanya mie mjinga"

Aisha aliamka na kwenda kuoga pamoja na kipenzi chake baada ya kutoka bafuni Suma alimlazimisha sana aende kula lakini Aisha alikataa, Suma alitoka sebleni na kukwambia mama yake kuhusu Aisha mama yake akamwambia.

"Sio Hali ya kawaida na hafanyi kusudi Kuna kitu kinamsumbua"

"Mama kitu Gani hiko mbona mie nahisi kua ananidekea tu?"

"Hapana Aisha sasa hivi ni mjamzito lakini mwenyewe hajajua sababu hajawahi kubeba mimba na hii hali wengie wanakua bado hawajajua sababu ya kuwa mara ya kwanza kubeba mimba"

"Mama unataka kusema Aisha ana mimba yangu?"

"Shiii usiongee Kwa nguvu hivyo Sasa ataskia, Sasa sikia sitaki huyo mtoto azaliwe nnje ya ndoa nataka umuoe Aisha mwanangu mmekaa Kwa muda mrefu sana lakini tudhihirishe kama tayari ni halali kwako"

"Aaha mama Hilo mbona halina shida nitazungumza nae na litakwisha tu"

Suma alichukua chakula na kuingia nacho chumbani kwaajili ya kumlisha Aisha maana alikua hapendi kabisa kula chakula, alipoingia chumbani akamkuta tayari Aisha ameshalala alimwamsha hivyo hivyo na kujaribu kumpa chakula Kwa kufosi Hadi akatapika Aisha akamwambia Kwa ukali.

"Kwanini unilazimishe kula wakati sitaki Suma ona sasa ukijiona nimechoka usinichoshe Suma"

Suma aliweka chakula pembeni na kumsafisha Aisha kisha akamwambia.

"Nisamehe sana mke wangu Kwa kukulazimisha kula lakini nataka ule uwe na nguvu usipokula utakuaje na nguvu na hiyo...unatakiwa kula"

"Niwe na nguvu ya Nini Yani Kwani hapa Sina nguvu?"

"Basi mpenzi nisamehe sana naomba nikukumbatie mpenzi ili upumzike"

Aisha anavyopenda kudeka Sasa hakujibu chochote akalala Kwenye kifua Cha Suma huku akiwa anatabasamu, Suma alijiwazia sana na kusema.

"Mmh kama kuishi na mjamzito ndio hivi yataka moyo sana ehe ni hatari sana"

Basi walipitiwa na usingizi lakini wakati wengine wanalala wakiwa na furaha lakini upande mwingine ni hali ya tofauti sana, Nadya alipojifungua aliambiwa ameathirika na virusi vya ukimwi na hakujua hivyo virusi amevipata Kwa nani maana ametoka na wanaume tofauti hivyo hakutambua nani mzima nani mgonjwa lakini mawazo yake yalimuondoa kabisa Suma sababu jinsi alivyokua anamuona Suma ni mwanaume wa tofauti mwenye kujali sana na mwenye hisia na malengo ya kweli hivyo Moja Kwa Moja hakutaka kumshutumu Kwa Hilo na wazo lake Moja Kwa Moja likadondokea Kwa Isaya hivyo alimlaani sana Isaya kwa kurejea kwake.

Muda wote alikua ni mtu mwenye kilio na mwenye maumivu sana alitamani kumpata Suma lakini alivyoondoka alimwachia Kila kitu chake hadi simu na hakua anajua kama Kwenye simu ambayo alikua anatumia Suma kulikua na namba za marafiki zake Hilo hakua anajua hivyo ndo ilizidi kumuumiza.

Na kama kawaida ukiwa unawaza mambo mengi lazima wazo Moja utakubaliana nalo hivyo asubuhi mapema Nadya aliamka na kujiandaa Kisha akamchukua na mtoto pia akamuweka Kwenye gari na kutoka nae.

Safari yake ilikomea Kwenye car wash ambayo walikua wanafanya kazi Suma na wenzake alipaki gari kando wakati anasogea Kwenye eneo la ndni Kwa kuangalia labda atamuona mtu yoyote mara akasikia sauti Kwa nyuma.

"Madam mbona umepaki gari mbali isogeze ndani tulioshe".

"Hapana ndugu yangu sijaja kuosha gari Kuna mtu nimekuja kumuulizia au kuwauliza"

"Nani huyo?"

"Kuna kijana mmoja alikua anafanya kazi hapa anaitwa Suma na mwingine anaitwa Juma mwingine anaitwa Rama kama sikosei unawafahamu?"

"Madam hàyo majina Kwa hapa sijawahi kuyaskia"

Nadya alizidi kuumia na aliweza kukubaliana nae mapema sababu aliona mabadiliko makubwa sana pale hivyo hayo majibu ya huyo kijana yalimwaminisha Moja Kwa Moja kuwa hao vijana hawawezi kubaki Tena hapo wakati tayari wenye pesa washaingilia kati hivyo ikabidi tu ageuke na kutaka kuondoka lakini Ghafla akaisika sauti nyingine Kwa mbali.

Kwa upande wa Aisha na Suma pia waliamka mapema sana na walikua wanafanya mazoezi ya kukimbia lakini Aisha alivyokumbuka kuwa alitaka kugongwa na gari akamwambia Suma.

"Baby wakati nafanya haha mazoezi mwanzo nilikoswa na gari na mdada mmoja hivi sasa Kwa tahadhari naomba tuwe tunaenda kufanya mazoezi pale gym"

"Aisha gym Tena jamani ila Sawa kama upendavyo lakini sio Leo Tena"

"Bado muda baby tafadhali twende"

Suma hakutaka kumkasirisha Aisha hivyo walienda hapo gym na kuanza kufanya mazoezi mara Aisha alimuona Samuel haraka akazima mashine na kwenda kumkumbatia Samuel na kumuuliza.

"Samuel ulipotea machoni mwangu"

"Aah Aisha Mimi nipo hapa Kila siku wewe ndio uliziba kabisa kuja hapa na Kila nikipiga simu Yako iko bize tu"

"Nikweli kabisa lakini Leo nipo na mume wangu hapa anaitwa Suma, baby huyu ni rafiki yangu ambae aliniokoa ike siku ambayo nilitaka kugongwa"

"Ooh asante Kwa kumuokota Aisha wangu"

"Usijali ilitokea wakati mie nimeona hivyo ikabidi tu nimsaidie"

Basi walipiga story nyingi Kisha Aisha na Suma wakaondoka lakini wakiwa Kwenye gari Suma akamwambia.

"Aisha sijapenda kumkumbatia yule kijana"

"Ooh umeona wivu?"

"Ndio na sitaki ijirudie"

"Basi Sawa nimekuelewa na sitarudia Tena baby"

"Ohk sawa lakini Aisha kwanini tusifunge ndoa tuishi Kihalali kama mke na mume?"

"Ooh Sawa hilo halina shida baby ni wewe tu ila sitaki ndoa ya sherehe sitaki kuona watu wengi macho yangu yana aibu sana"

"Usijali kuhusu hilo nitashughulikia"

Mambo ya Suma na Aisha yametaradadi huku kwa Nadya mambo magumu sana..
baada ya Nadya kusikia ile sauti aligeuka na kumuona Juma alifurahi sana na kutamani hata kumkumbatia lakini hakuweza sababu ya mambo flani, Juma akamuuliza.

"Madam ukatususa kabisa au ulisafiri?"

"Juma Nina mazungumzo marefu na wewe naomba kama hauna kazi twende Kwenye gari tukazungumze"

Juma hakua mbishi walifatana huku wanapiga story za zamani huku wakielekea Kwenye gari, waliingia Kwenye gari, Juma alimuona mtoto akashtuka na kumuuliza.

"Madam huyu mtoto wako?"

"Ndio ni mtoto wangu"

"Hongera sana ni mzuri sana"

"Ndio kafanana sana na baba yake"

"Sawa madam niambie"

"Juma kwanza naomba sana unisamehe sana kwasababu niliwafanya kuwa Kwenye wasiwasi mkubwa sana baada ya kumuondoa rafiki yenu kwenu, namaniisha kua nilikua naishi na Suma nyumbani kwangu kama rafiki na mwisho wa siku tukaanzisha mahusiano ambayo yaliota mizizi Hadi kupelekea kunipa zawadi ya huyu mtoto lakini..."

"Madam inamaana ulikua unaishi na Suma pika pakua?"

"Ndio Juma yaani alikua kila kitu kwangu na nilimpata baada ya ile siku kuagana na kaka yake sijui kua anakuja kumchukua lakini hakuja nilipita hapa nikamkuta amekaa mwenyewe nikamsaidia kwenda nae kwangu lakini nikajikuta tu naanza kumpenda"

"Ooh kwahiyo huyu mtoto wa Suma? Dah brother kajizaa kabisa Yani Sasa Suma Yuko wapi?"

"Juma nimekuja kwako sababu nataka uniambie maana Suma aliondoka kwangu kwa hasira kutokana na nilikua simfanyii mambo mazuri na siku ambayo aliondoka sikua natarajia kama ataondoka lakini kuondoka kwake kumenipa mashaka sana sababu hakuwahi kutaka kutumia pesa zangu Kwa ufujaji na pia hakua na tamaaa hata kidogo na alivyoondoka ameacha Kila kitu ambacho nilimpatia ndio kitu ambacho kinaniaminisha kua Suma alikua kwangu kwaajili ya mapenzi na sio pesa lakini sijamuona Tena"

"Pole sana madam siku ambayo aliondoka alikuja kuniaga na kusema kuwa anarudi Kijijini kwao na alisema anaishi Tabora sijui Kijiji Gani ila nilipojaribu kumuhoji alijibu tu kua amejeruhiwa"

"Ndio nilimuumiza sana Suma lakini nilikua nataka kumpa taarifa kua ana mtoto wake kwangu"

"Hongera sana na pole lakini ameondoka kama alivyokuja hakua na simu Wala Nini."
Nadya alichoka sana baada ya kusikia vile.

Suma baada ya kumrudisha mke wake Aisha nyumbani kwao akaoga haraka na kuelekea kazini lakini akiwa njiani alikua na furaha sana akasema.
"Najua kua Aisha hataki watu wengi Kwenye ndoa yetu lakini lazima marafiki zangu waje namba ya Juma ninayo Wacha nimpigie nimpe taarifa hizi.."

Suma alichukua simu yake na kuandika namba ya Juma kisha akapiga iliita bila ya kupokelewa alipiga Tena pia haikupokelewa alipiga zaidi ya mara tatu lakini haikua na majibu yoyote Yale akaweka simu Kando na kuendelea kuendesha gari.

Ghafla simu yake ikaita na alivyopokea akasikia sauti ya Aisha ikidai kua amemmisi, Suma alitabasamu kisha akamwambia.

"Aisha kipenzi nipo naendesha gari nikifika nitakupigia baby"
simu ilikatwa kisha Suma akasema.
"mwaka huu mbona nitakoma na hii mimba..."

ITAENDELEA.........

Jina la simulizi ni Penzi langu, unadhani taarifa za Nadya kuwa ana mtoto zitapokelewaje na Suma? Na vipi kuhusu Aisha akizisikia wakati nae ni mja mzito? Mambo ni bam bam [emoji3059][emoji3059][emoji3059]
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 11

ILIPOISHIA.......

Ghafla simu yake ikaita na alivyopokea akasikia sauti ya Aisha ikidai kua amemmisi, Suma alitabasamu kisha akamwambia.

"Aisha kipenzi nipo naendesha gari nikifika nitakupigia baby"
simu ilikatwa kisha Suma akasema.
"mwaka huu mbona nitakoma na hii mimba..."

ENDELEA NAYO.....

Suma alifika dukani kwake na kuendelea na biashara zake, alikuaa anauza duka la spea za boda boda magari biashara zingine mbalimbali ila mwenyewe alikua anakaa Kwenye duka la spea.

Upande wa Juma na Nadya walifika muafaka Kwa kumwambia atamtafuta Suma na akipata taarifa zake atamwambia, Nadya alikubaliana na Juma Kisha akaondoka zake na kumwacha Juma Kwenye sintofahamu akiwaza kuwa inamaana Suma alikua anatembea na madam boss halafu alikua hasemi kama ndie anaetembea nae.
Juma aliamua kuondoka zake kuelekea dukani kwake maana hapo alifika kuwapa hai tu marafiki zake.

Upande wa Aisha alikua amekaa sebleni na mama yake Suma walikuta wanapiga story zao mara simu yake ikaita akapokea.

"Hallow mambo Aisha"
"Poa nani wewe?"
"Mimi Samuel uliniachia namba Yako baada ya kutokea gym"
"Ooh samahani nilikua nimesahau kabisa vipi lakini uko poa?"
"Niko poa lakini nataka unisaidie kitu kimoja Aisha"
"Kitu Gani hiko?"

Mara Ghafla simu ikakata Aisha alimpigia lakini haikua ikipatikana akaiweka simu kando mama Suma akamuuliza.

"Ni nani huyo?"
"Ni rafiki yangu alitaka kuzungumza kitu lakini Ghafla tu simu imekata"
"Labda itakua imezima chaji"
"Ndio labda"

Basi wakiendelea na story zao lakini ghafla Aisha alijisikia kutapika akatoka mbio mbio hadi nnje mama yake Suma alimfata na kumuuliza.

"Aisha unaumwa?"
"Mama nimekua nikijiskia vibaya Sana Kwenye wiki hizi"
"Twende hospital basi ukajue Nini shida"
"Yani mama ukizungumza mambo ya hospital Mimi napona kabisa Yani maana sitaki kabisa kwenda hospital"
"Kwanini Sasa ,na ukikaa bila ya kwenda hospital utajuaje Nini kinakusumbua?"
"Mama lakini Mimi..."
"Nimegundua kua wewe ni muoga wa sindano ndio maana hutaki kwenda hospital"
Aisha alicheka kidogo Kisha akamwambia.

"Mama mie hata siogopi sindano basi tu sitaki kwenda"
"Hapana Aisha nenda kajue tatizo Nini ukikaa bila ya kujua tatizo utazidi kujiumiza"

Aisha aliingia chumbani kwake na kumuacha mama Suma pale nnje alicheka sana na kusema.
"mmh hizi mimba za kizazi hiki zinadeka Sana yaani hospital tu unakasirika hivi mmh sie enzi zetu ukifanya fyoko umebamizwa na mbao ya kichwa haijalishi una mimba Wala mtoto lakini sasa hivi mmh lakini nashukuru Mungu mwanangu amenidhihirishia kua yeye ni kidume Cha mbegu."

Mama Suma alikua anazungumza mwenyewe baada ya Aisha kuingia ndani.

Suma akiwa bize na wateja mara simu yake ikaita akachukua simu yake na kupokea Kisha kaunza kuzungumza.

"Oya juma mambo vipi ndugu yangu?"
"safi wewe ni Suma sindio?"
"Ndio mzee vipi uko poa?"
"kidogo Sana Suma umeondoka zako umetuacha wapweke hutaki hata salamu ndugu yangu"
"Hapana Juma sikuwahi kuondoka maana dah..ila sikia Juma nitakuja dukani kwako Leo si Bado upo pale pale?"
"Ndio nipo pale pale, ila kama utakuja itakua vizuri Sana maana Nina jambo nataka kukushirikisha"
"Poa basi nitakupigia simu badae"

Simu ilikatwa na Suma alikua na nuru na tabasamu zito usoni kwake.

Upande wa Nadya muda wote alikua anamtazama mtoto wake aliekua analia sana, Nadya akamsogelea mwanae na kumwambia.

"Najua unalia Sana mwanangu sababu ya kutomuona baba Yako lakini hivi karibuni tu utakutana na baba Yako naamini atafurahi Sana baba Yako na naamini atakupenda Sana vumilia kidogo mwanangu"

Nadya alikua anazungumza kwa uchungu Sana Kila anapomtazama mtoto wake na pia hakuwahi kumpa maziwa yake tangu alipomzaa Kwa kuogopa kumuambukiza maradhi aliyonayo.

Muda ulizidi kusogea na hatimae ilikua yapata saa mbili usiku Suma alimpigia simu Juma na kumwambia kua anamfata, Juma alikubali na baada ya nusu saa Suma alifika ana ndinga yake akashuka wakasalimiana Tena Kwa mara nyingine wakiwa na furaha Sana Juma akamuuliza.

"Enhe umepata jimama jingine Nini naona mambo sio mabaya unaanza kunenepa Tena na vipi kuhusu safari ya kijijini?"

"Juma ni story ndefu lakini wacha tu nifupishe sijapata jimama lingine ila sema yule mpenzi wangu wa kule kijijini alirudi mjini na kwao maisha safi kabisa hivyo kama bahati tu ile siku ambayo nimetoka kwako hapa naelekea station nikakutana nae basi kilichoendelea mwenyewe unajua"

"Duh Suma unabahati Sana hivi umeogeshewa maji Gani mbona hiyo bahati siipati Mimi?"

"Achana na hayo Juma kwanza nataka kukwambia kitu kabla ya kuchelewa nikwamba nakualika ndoa Mimi na mpenzi wangu tunataka kuowana mke wangu ana ujauzito tayari hivyo amekua msumbufu Sana hakua anataka sherehe ila nimeona hata rafiki zangu nyie nisiwapuuze"

"Duh unataka kuowa Suma na yule mwanamke wako.."

"Mwanamke wangu yupi juma?"

"Nakutania tu Mimi kaka nakutakia maisha mema na marefu na mke wako mpendwa"

"Asante Sana lakini mbona huna dalili ya kufunga hata duka au hufungi mida hii?"

"Nafunga saa 5 Hadi 6 huko"

"Eeh sawa Juma Wacha mie niende maana hapa simu unavyoona inaita muda wote ni yeye Huyu ameanza kunisumbua"

"Eeh Suma we tutafutie na wenzio dawa tupendwe kama wewe sio vizuri"
Juma alikua anazungumza kwa utani Kwa rafiki yake.

Suma aliaga na kuondoka zake na kumwacha Juma akizidi kuchanganikiwa akawa anajiuliza.

"Nifanye Nini sasa maana kwanza namuonea huruma yule mtoto pia namuonea huruma huyo mwanamke aliyenae Sasa maana ni mpenzi wake wa zamani Sana na wametoka mbali Sana Hadi kufikia hatua ya kutaka kupata mtoto he akipata taarifa hizi maana inaonesha wazi kua Suma hajui Chochote kuhusu madam boss kama anamtoto wake aah nifanye Nini sasa mimi aah..!"

Juma alikua anawaza nini cha kufanya Kwaajili ya mashemeji zake, kweli kabisa ukiwa upande mmoja upande huu lazima ukuumize kichwa sasa Juma alikua njia panda na haelewi Nini afanye na wapi atetee.

Maisha yaliendelea hivyo hatimae Aisha na Suma walifunga ndoa Yao haikua na sherehe lakini ilipita salama majirani na marafiki walifika kuwa sabahi na baada ya shughuli kupita salama Kila mmoja akaondoka kwenda kwake.

Baada ya siku kadhaa Suma akamwambia Aisha waende hospital maana tayari Aisha alianza kukonda kutokana na kutokula chakula Kwa wakati, walipofika hospital daktari akamchunguza Aisha Kisha akatoa majibu kua Aisha anaujauzito wa miezi mitatu na anatakiwa kuhudhuria kliniki haraka iwezekanavyo.

Aisha alishtuka Sana baada ya kuambiwa kuwa ni mjamzito baada ya kutoka Kwa daktari na kuingia kwenye gari Aisha alianza kulia Suma akambeleza na kumuuliza kwanini analia Aisha akamjibu.

"Najua baadhi ya wanawake wanapoteza dira zao pindi wanapokua na ujauzito sababu wanaume zao wanakua bize na wanawake wengine naogopa Sana kuumia nikiwa kwenye Hali hii Mimi"

"Aisha wewe ni mke wangu na nimegundua kua mjamzito kabla na nilitaka tuje hospital kwaajili ya kuthibitisha na wewe umsikie daktari Kwa maskio Yako, hivyo usijali Aisha wewe ni mke wangu na nitakua na wewe kwenye shida na raha kama ilivyokua mwanzo nakupenda Sana huna sababu ya kuwaza Tena nipo karibu Yako muda wote Chochote unachohitaji nitafanya"

Aisha alimkumbatia Suma Kwa furaha Sana na kumbusu mabusu yasiyo na idadi Kisha Suma akawasha gari na kuondoka maeneo hayo.

Baada ya kuambiwa kua anatakiwa kuanza kliniki hivyo mwezi wa nne kwake ulivyoingia tu ile siku ya tarehe Moja Aisha na Suma walijiandaa vizuri na kumuaga mama Yao Kisha wakapanda kwenye gari kuelekea kliniki.

Na kwa upande wa Nadya pia hiyo tarehe ilikua siku ya kumpeleka mtoto wake kliniki hivyo nae alijiandaa yeye na mwanae na kuondoka zake.

Katika eneo la hospital upande wa kupimwa watoto Aisha alikua wa kwanza sababu alifika na mume wake hivyo alikua wa kwanza kwenda kumuona daktari.

Baada ya kumpima daktari aliwapa ushauri ambao ulikua mzuri kufatwa na mama mjamzito kipindi chote Cha miezi tisa Kuhudhuria kliniki na mara baada ya kujifungia pia.

Baada ya kumaliza kuongea Suma na mke wake walitoka Kwa daktari lakini wakiwa wanatembea kwenye korido waweze kufika kwenye sehemu ya kupaki gari mara ghafla Aisha alijiskia kutapika hivyo alimuacha Suma pale na kuelekea washroom.

Suma alisimama kwa muda hadi alihisi kuchoka ikabidi akae kwenye sehemu ambayo wamekaa wa mama na watoto zao ambao wanasubiria foleni ya kwenda kuwapima watoto zao mara ghafla alishikwa mkono na baada ya kufika sehemu yenye kificho alimuona Nadya akiwa na mtoto, Suma akamuuliza.

"Nadya ni wewe kweli?"
lakini hapakua na maficho kiasi hiko wakati Suma anaendelea kumuhuliza Nadya baadhi ya maswali Aisha alirudi alipomuacha mume wake hakumkuta akamuuliza mdada mmoja kamwambia kua Kuna mdada ameenda nae huko nyuma ya Jengo.

Aisha alipiga hatua Hadi kwenye nyuma ya Jengo Hilo akamuona Suma akiwa anamshika Nadya mara amgeuze sura yake mara amguse paji la uso kama anapima joto, Nadya akamkabidhi Suma mtoto, Suma alimpokea na kuanza kumtazama Kwa makini huyo mtoto kweli alikua amefanana nae sana, Sasa alivyotaka kuzungumza kitu Kwa Nadya hakuwepo Tena pale, Suma alianza kutazama huku na huko lakini hakumuona wakati mambo yote hayo yanaendelea Aisha alikua anaona akaamua kurudi kwenye gari.

Suma alimtafuta sana Nadya lakini alivyotoka kwenye parking akaona gari la Nadya ndio linaondoka.

Suma alishindwa kujizuia kabisa kuhusu kile kilichotokea kwanza alikua anawaza nini atamueleza Aisha Hadi amuelewe na kwanini Nadya aje kipindi hiko kigumu kwake ukweli alikua amechanganikiwa sana.

Suma alisogea Hadi ilipo gari alifungua mlango na kupanda akamkuta Aisha ameshusha siti amejifanya amelala lakini hakua amelala hata kidogo.

Suma akitaka kumuamsha Aisha lakini bado alikua anaogopa, Aisha aliamka mwenyewe na kumuuliza shida nini? na vipi mbona watoto Tena?"

"Aah Aisha naomba tukazungumze nyumbani hili jambo"

"Tuzungumze nyumbani, huyu mtoto umempata wapi, naomba nieleze hapa hapa na kama vipi mpeleke huyu mtoto Kwa mama yake"

"Aisha nakupenda sana mpenzi wangu najua wewe ni muelewa sana naomba nielewe kipenzi changu"

ITAENDELEA........

Sitaki aje mtu anibanie pua "Mbona fupiii?" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji2091][emoji2091]
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 12

ILIPOISHIA.......

"Tuzungumze nyumbani? Huyu mtoto umempata wapi, naomba nieleze hapa hapa na kama vipi mpeleke huyu mtoto Kwa mama yake"

"Aisha nakupenda sana mpenzi wangu najua wewe ni muelewa sana naomba nielewe kipenzi changu"

ENDELEA NAYO......

Aisha alikua anaumia sana moyoni sababu alijua fika kua yule mtoto ni wa Suma na Hana namna aliamua kushuka kwenye siti ya mbele na kukaa nyuma huku akilia sana, Suma hakujua Nini afanye kwaajili ya kumpooza Aisha akimtazama mtoto Bado mdogo ikabidi tu ambebe ili aendeshe gari.

Walifika nyumbani kwao Aisha alikua wa kwanza kushuka kwenye gari na kuingia chumbani kwake na kujifungia mlango huku Suma akifuatia akiwa na mtoto, mama yake akamuuliza.

"Suma imekuaje, mwenzio umemfanya Nini mbona amekua vile macho yamemvimba inaoanekana wazi kua alikua analia na huyu mtoto vipi?"

"Mama naomba nisaidie kwanza huyu mtoto, nimechoka sana"

Mama yake alimchukua mtoto kisha Suma akaelekea chumbani lakini Aisha alikua amejifungia Kwa ndani Suma alimuomba sana amfungulie alimwambia maneno yote mazuri, mapenzi ni mapenzi tu nyie, Aisha alifungua mlango na kumkumbatia Suma huku bado akiwa analia, Suma alifunga mlango na kumsogeza Aisha wake kitandani na kumwambia.

"Najua unaumia sana Aisha lakini sikua nataka haya yote yatokee mpenzi lakini nilishindwa tu kujizuia naomba sana nisamehe"

"Suma unataka kunambia kua yule mtoto ni wako?"

"Aisha Kwa asilimia zote yule mtoto ni wangu, naomba nielewe pia nisamehe sana, maana niliwahi kukuambia namna nilivyokukosea wakati tukiwa mbali mbali na niliwahi kukuomba msamaha kwa usaliti wangu na leo ndio nimeletewa mtoto niliyempata wakati nikikusaliti, narudia tena nisamehe mke wangu"

"Sawa Suma nimekuelewa na nimekusamehe sababu nakupenda sana"

"Nafurahi sana kusikia hivyo mke wangu"

Basi waliweza kumaliza tofauti Yao Kwa siku hiyo, Aisha alikua anambeba mtoto yule vizuri na kuhakikisha kua anapata Kila hitaji ambalo anahitaji kupewa mtoto.

Siku Moja Suma alichukua begi ambalo Nadya aliweka nguo za mwanae kwaajili ya kumbadilisha, Suma alichukua na kuaga kuwa anaenda kununua nguo za kubadilisha mtoto, wote walikubaliana nae lakini alipokua kwenye gari Suma alianza kupekua pekua kwenye baadhi ya mifuko na akakuta karatasi yenye waraka mkubwa sana ikabidi awe na shauku kubwa sana ya kutaka kujua waraka huo unahusu Nini akawasha gari na kutoka nalo nnje ya geti Kisha akapaki na kuanza kusoma..

"kwako mpendwa Suma
kuondoka kwako kwenye maisha yangu ilikua mateso makubwa sana kwangu, najua nilikua nimekukosea sana kwa mambo niliyokua nayafanya lakini nilikua nafanya vile ili ushindwe na uondoke sababu sikua na nguvu ya kukufukuza sikutaka ujiskie vibaya, najua kama umenichunguza umegundua mengi sana kuhusu mimi, Suma nisamehe kwa yote ambayo unajua ni mabaya kwangu na kusema ukweli nilikua nimekudanganya kua nimeachwa na mwanaume wangu haikua kweli japokua nikweli amekua akinisaliti alipokua huko nnje ya nchi na aliposema kua anarudi ndio nikaamua kukufanyia mambo ya ajabu na baada ya kurudi kwake sikuwahi kuwa na furaha hata kidogo sababu alikua mbinafsi sana na hakuwahi kuonesha kama ananijali alikua bize na wapenzi wake wa huko nnje japokua kabla ya kuondoka aliniachia baadhi ya vitu akanitafutia kazi nzuri lakini vyote havikutosha Mimi nilihitaji uwepo wake lakini hakuwepo nikaanza kutoka na vijana tofauti hatimae nikakupata wewe.

Suma ulikua mpole sana mwenye mapenzi ya dhati na sio mwenye tamaa ukweli ulistahili kuoneshwa heshima yako najua ulishanambia kua unampenzi unaempenda lakini bado sikutaka kushindwa kwako sababu niliona kitu Cha tofauti Hadi nikiwa na wewe lakini nilijali sana pesa zangu na ubinafsi bila ya kujali moyo wako.

Niachane na hayo kwanza nataka kuzungumza kuhusu mtoto Suma, nilitelekezwa baada ya yule mwanaume kugundua kua Nina ujauzito na sikua na mwanaume mwingine zaidi yako nikaanza kukutafuta Kila sehemu lakini sikukupata mpaka nilipojifungua mtoto ndio alikua faraja yangu sababu sura yake ni Yako hivyo alikua ananitazama sana pindi napokua nalia nilitamani kumtupa

nafsi ikanisuta nikatamani kumpeleka kwenye vituo vya watoto yatima nafsi ikanisuta nikasema kua wewe upo hai kwanini usiwe baba Bora kwake nikamtafuta rafiki yako Juma lakini nae alinambia kua hajui ulipo hivyo nikajipa Imani kua siku yoyote tunaweza kukutana na kukukabidhi mtoto wako.

Suma mlee vyema mwanao, huyo ni mtoto wako pekee Mimi nimeathirika sikutaka kumuathiri na mtoto pia hata wewe usiwe na wasiwasi wewe ni mzima kabisa, maana aliyeniambukiza ni aliyekua mpenzi wangu baada ya kurudi na nitabaki kukupenda siku zote Suma mtunze mtoto wetu aje kupata elimu Bora na maisha Bora pia kwaheri."

Suma baada ya kumaliza kusoma waraka huo alikua amechoka sana na Mara baada ya kumaliza kusoma ujumbe huo simu yake ikaanza kuita na baada ya kuita aliipokea na alishtuka sana baada ya kupokea taarifa za msiba wa Nadya, alizidi kuumia maana tayari alishapoteza matumaini.

kwakua hakua mbali na nyumbani kwao aliingia ndani na kuwakuta Aisha na mama yake wamekaa na mtoto akiwa amelala Suma alimsogelea mtoto na kumbeba Kisha akamkumbatia Kwa nguvu sana huku akitetemeka sana Aisha akamuuliza.

"Suma imekuaje huoni kua mtoto amelala, mbona hivyo?"

"Aisha, mama huyu mtoto tayari yatima mama yake amejiua, Aisha mama yake hayupo Tena duniani junior mwanangu ona mama yako amejiua junior wangu kwanini akuache ukiwa mdogo hivi kwanini lakini?"

Suma alilia kiume kiasi kwamba hata Aisha alishindwa kujizuia maana Suma alikua analia kwa hisia kali sana.

Siku zilienda mtoto aliendelea kukua vizuri sana na pia tumbo la Aisha pia lilikua kadiri siku zilivyozidi kusogea.

Aisha kwakua tayari alikua ameshawazoea rafiki zake na Suma siku Moja baada ya Suma tu kuondoka kazini Aisha alipanda kwenye gari nyingine na kuelekea dukani Kwa Juma Kisha akamkuta Juma na kupiga story baada ya hapo akawa anamuuliza baadhi ya maswali, Juma alikua anamkubali sana huyo mwanamke kwanza mcheshi halafu pia anasifa ya upole hadi kwenye uzungumzaji wake hivyo Juma alikua anajibu Kila anachouliza mke wa Suma, basi Baada ya kumaliza jambo lake akamuaga na kuondoka zake Juma akaanza kuzungumza mwenyewe kama kawaida yake.

"Suma akimpoteza na huyu mwanamke basi hatokuja kupata Tena mwanamke mzuri na mstaarabu kama huyu binti mrembo anazungumza vizuri eeh namimi Wacha niowe maana Kila siku nasifia wanawake za watu eeh Mungu nipe mwanamke mie hata ukinipa kurumbembe gegedu ilimradi tu nipate heshima, sitaki hata mwanamke mzuri Mimi nataka wa kuishi nae mwenye kujua thamani ya maisha na kuheshimiana tu"

Mara akashtushwa na sauti iliyosikika
"Kaka kama kawaida yako unaongea mwenyewe tu yaani we utazeeka vibaya sana"

"Aah Rama we acha tu yani nilikua naongea na shemeji yangu Aisha hapa alikuja kuniona basi nimetokea tu kumpenda Bure yule dada mkarimu na mpole"

"Aah mke wa Suma kile chombo mwanangu sana yaani ukizungumza nae tu kama hujapandwa na hisia je anapokua faragha Yani navuta picha tu hapa na ile suati ya kubembeleza"

"Eeh Rama basi acha kusifia sana hivyo"

"Haya mwanangu lete story maana nimekuja kukuona tu umekua adimu sana ofisini kwetu"

"Aah Niko bize sana Yani..."
Waliendelea kupiga story zao za kuhusu kazi.

Siku moja usiku wakiwa wamelala na walikua wanalala na mtoto wao junior maana Aisha alikua anampenda sana, unajua Kuna kitu mda mwingine mtoto anakifanya Cha ajabu Hadi unajikuta tu unashangaa au unapata hisia za kitu flani hivyo usiku huo junior alikua amekumbatiwa na Aisha lakini Ghafla akajitoa na kusogea kwa baba yake na mara baada ya junior kusogea kando Aisha hakuchukua hata dakika tano alianza kuhisi maumivu ya tumbo sana huku akitetemeka sana.

Suma aliamka na kumbeba Junior kumpeleka Kwa bibi yake kisha akambeba Aisha na kuelekea nae hospital.

Baada ya madaktari kumpokea na kumpima akaonekana kua tayari muda wa kujifungia umewadia hivyo haraka wakaandaa vifaa kwaajili yake.

Wakiwa Labor Aisha alikua anaugua kwa maumivu sana madaktari walimpa nasaha kua aendelee kua mvumilivu na kuweza kufata kile wanachomuelejeza daktari akamwambia.

"Pia Aisha jitahidi sana kuvuta pumzi ndefu kisha ishushe Kwa nguvu kila kitu kitakua Sawa lakini ukiwa muoga utampoteza mtoto maana tayari ameshaanza kutoka.."

Aisha alijitahidi sana na kuvuta pumzi kwa nguvu zote kisha akashusha Kwa nguvu pia mara alisikika mtoto akilia lakini Aisha alionekana hayupo Sawa kabisa madaktari walianza kuchanganyikiwa sana maana Aisha alikua na hali mbaya sana macho yalikua yamemtoka sana na pia hakua akilia Tena Kwa maumivu Wala hata kufanya chochote hivyo hivyo alivyotulia ndivyo alivyo, daktari akaweka mkono kwenye pua yake akashtuka na kumwambia.

"Hapumui Tena jamani fanya haraka tujaribu kuokoa maisha yake".

Haraka madaktari walishirikiana kwenye suala zima la kumuwekea mfumo wa kupumulia na hapo sasa walianza kuona matumaini, wote walimshukuru Mungu kwa kunyoosha mikono yao juu kwa tabasamu.

Baada ya madaktari kumaliza zoezi zima la kumsaidia Aisha walitoka labor na kumkuta Suma akiwa nje anasubiria majibu kuhusu taarifa yoyote mana wanasema ukiwa labor ni nusu mfu na nusu uhai kutokana na maumivu makali ambayo hupitia mama mjamzito pindi anapojifungua hivyo Suma alikuaa anasubiria kauli yoyote kutoka Kwa daktari japokua hakutamani kumpoteza yoyote kati Yao sababu alimpenda sana Aisha wake na alitegemea kupata mtoto mzuri sana na Aisha na mwenye sifa zote ambazo anazo Aisha.

Wakati yupo pale nje anaenda kulia na kushoto mbele na nyuma bila kuelewa Chochote mara daktari ambae alikuaa ameteuliwa kwaajili ya kumsaidia Aisha alimuita Suma ofsini kwake.

"Samahani kaka naomba uje ofsini kwangu"
Suma hakupoteza muda alimfata Kwa haraka sana daktari, na baada ya kufika akamuuliza kabla ya daktari kuanza kumuelezea.

"Daktari mke wangu anaendeleaje na vipi kuhusu mwanangu wapo sawa?"

"Tulia ndugu yangu kama wamgekua na tatizo nisingekua na utulivu wa kukuita ofsini muda huu lakini nimekuita hapa sababu Nina taarifa njema"

"Sawa daktari nakusikiliza lakini samahani kwa kua msumbufu"

"Sawa Hamna shida mana najua jinsi unavyojiskia ngoja niende Kwenye majibu Yako Moja Kwa Moja ni kwamba mke wako tumeweza kumsaidia kwa uwezo wa Mungu alifanikiwa kujifungua salama japokua Kuna tatizo lilitokea katikati ya safari lakini tumemsaidia na Sasa Yuko sawa kabisa"

"Ooh asante Mungu wangu"
Suma alifurahi sana na kumshukuru Mungu na kumpongeza daktari na kumuuliza.

"Naweza kumuona?"

"Kwa sasa hivi amepumzika lakini baadae utamuona akiwa Sawa"

Suma alitoka nje akiwa na furaha sana alitoa simu yake na kumpigia simu mama yake kuwa Aisha amejifungua salama, mama yake pia alifurahi sana Suma alikata simu na kuanza kuwapigia rafiki zake hasa Juma ndio alikuaa anamkubali sana maana Juma ndie alikuaa mkaidi sana kwake.

Ilikua usiku wakati mambo yote hayo yanaendelea lakini Hadi kufikia asubuhi Juma alikua tayari amefika hospital na baada ya kufika muda wa kuona wagonjwa Suma na Juma waliingia wodini na kumkuta Aisha akiwa amekaa anacheza na mwanae.

Suma alipomuona mke wake alifurahi sana na na kutamani kumkumbatia lakini alikua ameshika mtoto hivyo hakupata nafasi hivyo alimbusu mtoto na mke wake pia Kisha akamwambia.

"Oole sana mke wangu Kwa maumivu uliyipitia wakati wa kujifungua nilikua nakuombea sana ujifungue salama mke wangu"

"Asante mume wangu nahisi nguvu ya maombo Yako ndio yameniweka hai"
Suma alifurahi sana Juma pia alimpa hongera shemeji yake na muda mchache tu mama yake Suma alifika hospital kumuona Aisha alimsalimia na kumpa pole Kisha akamwambia Aisha.

"Mwanangu Aisha pole sana hatimae Sasa umekua na uoga wote umeisha sindio mama?"

Aisha alikua anaona aibu hata kumtazama mume wake, Juma na Suma wakaona kua mama Yao anataka kuwafukuza tu kimafumbo hivyo walitoka na kuwaacha peke yao.

ITAENDELEA......
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 13

ILIPOISHIA.......

"Mwanangu Aisha pole sana hatimae Sasa umekua na uoga wote umeisha sindio mama?"

Aisha alikua anaona aibu hata kumtazama mume wake, Juma na Suma wakaona kua mama Yao anataka kuwafukuza tu kimafumbo hivyo walitoka na kuwaacha peke yao.

ENDELEA NAYO......

Wakiwa pale Aisha akaongea
"Mama sikua najua maumivu anayopitia mjamzito lakini Jana mmh nimeona Wacha tu yani sijui kama nitazaa tena"
mama Suma alicheka sana Kisha akamwambia..

"Wakati wenzio tunaanza tulikua tunasema hivyo lakini mwisho wa siku tunaongeza watoto maana Hali hii tunakua tumeshaizoea na haikimbiliki"

"Sawa mama nimemmis junior wangu mlete kwanza"

Walibadilishana watoto pale Aisha alimkumbatia junior yaani junior alifanana sana na Suma yaani ukimtazama huulizi kabisa, ila mtoto wa Aisha alifanana sana na Aisha mwenyewe sababu alikua wa kike hivyo alifanana sana na mama yake.

Baada ya kupiga story nyingi muda wa kutazama wagonjwa uliisha hivyo walitoka wodini na kumuachia Aisha na mtoto wake, daktari aliingia na kumpima baadhi ya vipimo kisha akamwambia.

"Presha yako iko kawaida kwa sasa na hauna shida yoyote ile hivyo ikiendelea hivi hadi jioni tunaweza kukuruhusu"

"Asante sana daktari"

"Usijali ila mtoto wako ni mzuri sana kama wewe mwenyewe"

"Asante "
daktari alitoka na kumwacha Aisha apumzike.

Suma na mama yake wakiwa wamekaa pale nje wakijadili mambo kadhaa, Juma aliweza kuwaaga na kuondoka zake Suma akabaki na mama yake na mwanae junior akazungumza.

"Mama natamani kufanya surprise kwaajili ya Aisha na mwanangu"

"Unataka kufanya Nini?"

"Mama nataka kumfanyia Aisha ajionee mwenye furaha sana akiwa na mimi hivyo nataka nifanye kitu kama Cha tofauti hivi kwake"

"Mwanangu wala hata usijali, fanya Chochote ambacho utahisi kitakua kizuri Kwa mkeo Mimi sina hata neno"

Basi Suma aliwarudisha nyumbani mama yake na mtoto wake Kisha akatoka kuelekea kununua baadhi ya vitu akarudi navyo kisha akaanza kusaidiana na vijana ambao alikua amewapata wakapamba kwenye ukuta kwa mauwa mazuri na kila kitu vinavyohusika na mapambo kisha baada ya kumaliza akawalipa hao vijana kisha wakaondoka zao Suma akamwambia mama yake.

"Ni sherehe ndogo kwaajili ya mke wangu kabla ya 40"

"Suma ila usiwaalike rafiki zako iwe ni sisi kama sisi maana mtoto bado kuonekana na watu tofauti hadi amalize 40"

"Usijali mama"
Suma alitoka na kuelekea hospital na kwa bahati tayari Aisha alikua amepewa ruhusa hivyo alimsaidia baadhi ya vitu na kupeleka kwenye gari kisha Aisha pia alifika kwenye gari na wakaondoka zao.

Walipofika Suma alimkaribisha mke wake kwa furaha sana Aisha alifurahi na kumshukuru mume wake lakini kila kilichoandaliwa Aisha alijizuia kula hivyo walikula wenyewe Suma na mama yake.

Siku zilienda sana hadi siku ya 40 wakafanya kasherehe ka mtoto waliwaalika marafiki na baadhi ya majirani wengi sana na maisha mengine yakaendelea.

Aisha aliwapigia simu wazazi wake na kuwaeleza kuhusu kupata mtoto mama yake alilia machozi ya furaha sana na kutamani kumshika mjukuu wake, Aisha alimuonesha mama yake mtoto sababu walikua wanazungumza kupitia video call hivyo baada ya kumuonesha mtoto alikua amelala mama yake akamwambia.

"Mwanangu yaani alivyotulia kama ulivyokua wewe wakati uko mdogo mzuri sana binti yangu"

"Mama sifa zikizidi utaaribu hahahaha"
mara mdogo wake akachukua simu na kumwambia.

"Ndio dada wewe mzuri na jinsi alivyomsifia mama mwanao kama mapacha natamani sana kucheza nae"

"Usijali mdogo wangu nitakuja nae"
Basi Baada ya kuongea mengi Aisha alikata simu.
alipotaka kuweka simu yake kando mara simu yake ikaita akapokea.

"Hallow Habari"
"Safi naona namba ngeni"
"Ndio ni Mimi Samuel za siku nyingi?"
"Samuel mbona umekua kama mzimu ndugu yangu, kwanza ile siku nilikua niko makini kusikiliza lakini Ghafla tu ulikatika kwenye simu"
"Nikweli ila nilikua kwenye misheni yangu muhimu na Sasa ni Kwa miezi kadhaa sijafanikiwa ila nataka tuonane niweze kukushirikisha jambo labda utanisaidia kitu, maana nimeshatimiza nusu ya jambo langu"
"Sawa Samuel ukiwa tayari we nijulishe nipo tayari kukusaidia"

Simu ilikatwa na kumfanya Aisha mwenye mawazo maana akikumbuka jinsi alivyokua anamtazama akawa anajiuliza tu mwenyewe.
"Au ananitaka huyu mpuuzi, aah ila nilishamwambia kua Nina mume wangu na alishamuona hivyo kama atasema ananipenda nitamkomesha hapo hapo."
yalikua mawazo ya Aisha kuhusu Samuel..

Akiwa kwenye mzunguko wa mawazo hayo mara mlango ukafunguliwa akaingia Dan akasema surprise
Aisha alishtuka sana baada ya kugeuka akamuonya Dan akamkumbatia kwa furaha kisha akamuuliza.

"We kijana ulikua wapi lakini mbona simu Yako ilikua haipatikani?"

"Aisha sikua nimekuaga sababu ilikua ghafla sana ila umerudi tu wewe hapa siku ambayo nataka kuja kusalimia baba yako akanituma mambo flani hivyo ikabidi nifanye hivyo ndio maana sikuwepo"

"Jamani Dan sijapenda yaani nimekosa msimamizi kwenye matukio memgi muhimu yaliyopita"

"Nisamehe lakini sasa nipo hapa kama babu wa Binti yako, anaitwa nani kwanza?"

"Anaitwa Maira"

"Wao waoo waoo Jina zuri kama mwenyewe huyu Binti utasema kama hakunyi"
Aisha alicheka sana kwa mazungumzo ya Dan.

Baada ya story tofauti aliamua kuaga na kuondoka zake.
Upande wa Suma akiwa Kwenye mizunguko yake siku Moja ilikua mida ya jioni akiwa kwenye mitaa kadhaa akiwa na Juma mara ghafla wakaona vitu vinatolewa nje na kutupwa huku mwanaume akimuomba sana baba mwenye nyumba amvumilie lakini huyo mwenye nyumba hakua na huruma kabisa na hao watu, Suma alipaki gari na kutaka kushuka kwenye gari Juma akamshika mkono na kumuuliza.

"We unaenda wapi, hivi we umekua na huruma kiasi hiko eeh yule jamaa sindio alikuja siku ile kukutukana pale kazini na kuturushia nguo zako japokua wewe hukuwepo ila sisi ndio tulishuhudia Sasa unaenda wapi?"

"Juma ni sawa alinifanyia hivyo lakini bila yeye kumbuka mimi na wewe tusingejuana na kumbuka yeye ndio alinipa chachu ya kuendelea kupambana"

Juma alichukia sana maneno ya Suma alimuacha afanye anachotaka, Suma alipiga hatua hadi pale na kuwasalimia kisha kuuliza juu ya kinachoendelea, kwanza yule kaka alipomuona aliona aibu lakini mke wake alifurahi kuona ujio wake na kuchangamkia fursa.

Alimsimulia kila kitu kisha Suma aliita gari ya usafiri na kupakia kila kitu na kisha wakaelekea kwenye nyumba moja nzuri sana ambayo walijenga tayari yeye na Aisha, walipofika akawambia.

"Brother na shemeji mtakaa hapa kwa muda kisha nitawatafutia nyumba ya kuishi"

"Suma tunashukuru sana kwa msaada wako bila wewe sisi tungezidi kudhalilika"

"Shemeji usijali hata hivyo bila ya kaka hapa kunisaidia leo nisingekua hapa nasema asante sana kwa kunipokea siku niliyokuja hapa jijini"
Suma alitazama saa yake na kusema.

"Natamani kuwasaidia kuingiza vitu ndani lakini nimechelewa sana muda huu.."

"Usijali hapa tulipofikia tutamalizia sisi wewe wahi tu nyumbani"
Suma alitoa pesa kama elfu50 na kumkabidhi kaka yake huyo na kuondoka zake.

Baada ya Suma kuondoka zake mke wake na yule jamaa akaanza kuzungumza.

"Mume wangu ona sasa kijana uliyemsaidia ukamuondoa kwako kwa hasira ona leo ndio ametusaidia je angekua na moyo wa kutosamehe ingekuaje so angetucheka na kutudhalilisha?"

"Kweli na sasa nimeamini kua tenda wema uende zako usingoje shukran na sababu hujui kesho yako na sasa nimeamini kua malipo ni hapa duniani, leo bila juyu kijana sijui hata ningekua mgeni wa nani"

"Usijilaumu sana lakini pia hilo ni funzo tosha usije kurudia tena makosa ambayo umeyafanya"

"Kweli kabisa mke wangu nitajirekebisha"

Upande wa Suma na Juma walikua wanazozana tu.
"Suma umeacha kunisaidia Mimi ambae hadi keo naishi nyumba ya kupanga unaenda kumsaidia yule jamaa, kusema ukweli bado nitaendelea kukulaumu Kila siku"

"Aah Juma jamani usiwe hivyo rafiki yangu lakini nafanya kwa kulipa fadhila tu kwao kwanini unakua hivyo pia binadamu tunasaidia hatupaswi kutazama makosa ya nyuma kuwa nini kilitendeka"

"Nishushe hapo Suma sitamani kuendelea na hii safari"
Suma alisimamisha gari na Juma akashuka na kutokomea gizani, Suma aliendesha gari hadi nyumbani kwao na baada ya kuwasalimia vipenzi vyake wakiwa wanapata chakula Suma akaanza kuongea.

"Mama na mke wangu nataka kuwaambia jambo Moja ambalo limetokea keo najua sijawashirikisha lakini nataka kuwajuza kitu".

"Kitu Gani hiko Suma?"

Wote waliuliza kwa shauku ya kutaka kujua.
"Aah nilipofika hapa mjini wakati ule natokea kijijini, kuna brother wangu nilimsaidia kurekebisha gari yake na baada ya kuniona na kile kifurishi changu akajiuliza baadhi ya mambo nikamwambia kua mimi mgeni akanisaidia kunipeleka kwake nililala kwake siku moja na siku ya pili akanipeleka kazini hapo ambapo nilikutana na Juma na wale wengine na siku ile nikijifanya kutaka kurudi lakini sikuweza kupakumbuka ikabidi nirudi nilipotoka kabla ya kufika pale maeneo ya kazi walitokea vibaka na kunipora pesa ambayo nilitegema nitaamka nayo kwaajili ya chakula na sikua na jinsi basi nikarudi kulala pale pale palikua na baridi sana sababu hapakua na uzio wa aina yoyote Ile, nililla pale hadi asubuhi na yule brother alikuja kunitazama akanikuta, akajilaumua sana kwa kutonifata na akaniahidi kua atanifata jioni ya siku hiyo sababu usiku ulipita alihisi kua nimepitia mengi magumu, mimi nilimkubalia sababu alisisitiza sana kua nisilale pale Tena.

Lakini hadi inafika jioni hatimae usiku lakini hakutokea nikaja kusaidiwa na mama yake junior ndio ambaye alinipeleka nyumbani kwake tuliishi kama ndugu lakini alianza kubadilika na kunitaka kimwili nili...."

"Suma achana na hizo story twende kwa huyu aliyekusaidia usifike mbali kuhusu mama wa huyu mtoto"

"Sawa basi siku iliyofata yule kaka alikuja pale ofsini maana tayari ilikua ofisi yetu aligomba sana na kunitukana sana na kuwarushia nguo zangu na kuondoka zake na mimi kwa kua sikua nimerudi tena pale siku nilipokutana na Juma akanisimulia Kila kitu, lakini mbali na hayo yote mama nimejikuta namsamehe baada ya leo kuwakuta wanafukuzwa kwenye nyumba waliyokua wamepanga nikaamua kuwasaidia na kuwapeleka kwenye ile nyumba yetu Aisha wakae kwa muda ila nisamehe kwa kuto kuwashirikisha hili"

Mama yake akamuuliza.
"Mbali na hayo yote lakini umewasaidia lakini sisi tuseme Nini wakati wewe ndio umepita hayo yote kama umefanya maamuzi yako ni wewe ila ungemshirikisha mwenzio na kwenye maamzi ya kufanya hivi usirudie tena"

"Sawa mama nimekuelewa, mama Maira wangu unasemaje kuhusu Hilo?"

"Sina usemi wowote ule, nipo pamoja na wewe"
basi walikula chakula na kuingia chumbani kupumzika zao.

Maisha Yao yaliendelea kua na furaha watoto wao pia waliendelea kukua vizuri sana.

Hatimae Maira alitimiza mwaka mmoja wakati huo junior alikua na mwaka mmoja na miezi kadhaa, Aisha alianza kufanya mazoezi tena na akiwa kwenye mazoezi hayo tena simu yake iliita na baada ya kupokea akasikia sauti ikisema.

"Aisha Nina jambo nataka kukueleza muda huu naomba ufike gym Mimi Samuel"
Aisha alikata simu na baada ya muda mfupi alifika hapo gym na kukutana na Samuel baada ya salamu nyingi Aisha akamwambia.

"Samuel umebadilika sana aise umekuaje sijui"

"Nikweli kabisa sababu nilikua nafanya mazoezi ya nguvu sana pia nikatoka nikaenda nje huko kwaajili ya kujifua vizuri kama naweza kupambana na watu wabaya"

"Mmh umefanikisha kwa asilimia ulizohitaji sawa niambie unachotaka kunambia mana nilikua narejea nyumbani"

ITAENDELEA......

Je! Unadhani Samuel anataka kumwambia nini Aisha? Tukutane mchana sehemu ya mwisho ya simulizi hii, na ukipata jawabu ya jambo analotaka kulisema Samuel basi nitakuonesha majina ya simulizi mpya na kukupa offer ya kuichagua unayotaka nianze nayo, kura yako moja tu itakua imetosha. Changamkia fursa hio[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 15 - final

ILIPOISHIA.......

Dan alimtandika sana na kumwambia
"Sasa sikia nitakupa kila kitu ili uwatoroshe ila kila unachofanya nitakua nakuona hivyo hata uende wapi kila kitu nimeandaa kwaajili Yako hivyo ukijifanya mjanja kila kitu kitakua kibaya kwako sitaki kukuuwa ila utapata mateso makali sana"

ENDELEA NAYO......


"Samahani kaka naomba usiniuwe"

"Siwezi kukuuwa ila fanya kaka ninavyotaka"
Yule mjamaa alikubali na walikaa nae kwa siku kadhaa kisha siku ambayo aliwaahidi kuwa atawatorosha alifika kwenye eneo husika haraka na kuanza haraka zake katika hizo harakati walifanikiwa kutoroka watatu lakini mmoja aliweza kupigwa risasi na alifariki hapo hapo na wale waliobakia wakawa wanajilaumu sana kwa kumpoteza mwenzao.

Yule jamaa aliwapeleka moja kwa moja kwa Dan sababu alishamchimbia mkwala kuhusu kama atakimbia.
huku njiani aliwambia kuwa amepata chimbo hivyo baada ya kuwafikisha hapo na kuonana na Dan walimlaumu sana yule ambae amewatorosha na kumtukana sana sio Aisha sio Samuel wote walikua na hasira sana juu ya walichowafanyia, Aisha alikua anawabana sana sehemu zao za siri ili wapitie hata nusu ya maumivu ambayo alikua nayo kwa kipindi chote baada ya kuambiwa wazazi wake wamefariki upande wa Samuel pia alikua na hasira sana juu yao sababu aliambiwa hao ndio waliowaua wazazi wake kitu ambacho hata wao walikataa Dan aliwasimulia ishu nzima ilivyokua walimluamu sana Kisha akawaambia.

"Nilifanya hivyo sababu ya kuokoa maisha ya mabosi wangu hata mngekua nyie mungemsababishia matatizo makubwa mtu ambae amenitoa kwenye shida hiyo kitu haipo kabisa ndio maana nikaamua kuwaokoa Kwa staili hiyo"

Aisha alivyoona anacheleweshwa kwa maneno mengi alichukua bastola na kuwapiga wawili na kubaki wawili yule jamaa na mmoja wapo ambae ametoka gerezani akaanza kumlaumu yule jamaa.

"Sasa mwanangu ndio umekuja kutuuza hivi bora ningebaki gerezani ningeendelea kula ugali na maharage na kuitumikia nchi yangu Kwa kufanya kazi za kijamii Sasa umeniletea hapa ili nitangulie mbinguni sio poa mwanangu nakumaind kinoma Yani na nakuambiaje huu moto uliouwasha leo kaa mbali na mimi hata ukiniona huko mbinguni usinisogelee maana nitakufanyia kiti kibaya sana boya wewe"

Aisha baada ya kuwafyatulia risasi wale wawili alitoka nnje akabaki Samuel na Dan, Dan alitoa karatasi nyeupe na kumpatia Samuel na kumwambia asisome hapo akasome pindi atakapokua pamoja na Aisha, kisha akampa ruhusa ya kumuuwa mmoja kati ya hao, Samuel alifyatua risasi kwa mmoja na kumgeukia Dan kumrejeshea bastola, Dan aligeuza kwa yule jamaa na kumfyatulia risasi na kumwambia Samuel aondoke eneo hilo kabla ya polisi kuingilia kati na kumkamata yeye, Samuel aliamua kuondoka eneo hilo, Dan alitoa simu yake na kupiga polisi na alipomaliza alijiua baada ya muda polis walifika kwenye eneo husika na kukuta Dan ameshika karatasi ikiwa na maelezo mafupi na pia alikua ameshika simu hivyo kiongozi alichukua ile karatasi na kusoma maelezo yote kisha akasema.

"Hizi maiti kumbe ndio zile ambazo zimetoroka gerezani na hawa nao pia wanahusika kwenye vifo vya wazazi wa Binti Aisha, hili ni jambo la kushtukiza kwanini wajiuwe pamoja lazima kuna jambo nyuma yao"

Maiti zote zilikusanywa na kuingizwa kwenye gari na kuondoka nazo.

Upande wa hotelini Aisha anaonekana akiwana na uoga sana juu kile alichokifanya alikua anakunywa sana pombe mara simu yake ikaita Aisha alipokea na kuzungumza..

"Nani wewe?"
"Aisha Mimi Samuel nataka kukuambia jambo uko wapi?"
"Nipo hotelin hapa"
"Nielekeze hoteli Gani?"

Aisha alimpa maelekezo sehemu alipo kisha Samuel alifika kwa haraka sana na kumkuta Aisha anakunywa pombe kama kichaa Samuel akamwambia..

"Aisha kaka Dan ametuachia ujumbe kwenye hii karatasi na amesema nisiisome hii barua mwenyewe nikutane na wewe tusome pamoja"

"Ohk soma Samuel nakusikiliza"
"Kwenu ndugu zangu wapendwa mimi ni kaka yenu Dan nimeandika barua hii kwa ajili ya kutaka kuwaaminisha kuwa msiwe na wasiwasi najua sasa mioyo yenu imefurahi kwa kulipa kisasi ambacho mlikua mnatamani sana kukilipa lakini haya mimi nimeamua kujiuwa sababu nilikua ni Moja wa watu wabaya hasa Samuel nisamehe sana kwa kuwalaghai wazazi wako na kuwasababishia kifo bila makubaliano kuanzia sasa ishini kwa amani na furaha kwasasa nawapenda sana na hii ibaki kuwa siri yenu Nawapenda sana"

Samuel baada ya kumaliza kusoma ujumbe huo alijikuta anaumia sana na kujiuliza
"Inamana aliniondoa kwa haraka na kujiuwa kabisa nilimzoea kwa siku chache sana lakini alikua mkarimu sana lakini naomba Mungu ampumzishe Kwa amani huko alipo"

Aisha pia alikua analia sana baada ya kuskia ujumbe huo.

Mpaka inafika asubuhi wakiwa pale pale mara simu ya Aisha ikaita alipomtazama alikua mume wake anampigia simu alipokea na kuanza kulia Suma akamuuliza.

"Aisha mke wangu unalia nini mbona unanifanyia niwe na wasiwasi mke wangu tatizo Nini?"

"Suma nimekukumbuka sana mume wangu na watoto wetu"

"Mimi Aisha wangu umeniacha na watoto kila siku wanalia kwaajili yako simu yangu haukua ukipokea tena wala hata sms zangu hakuwahi kujibu shida Nini hasa"

"Suma tutakuja kuzungumza nitakaporudi nakupenda sana lakini pia nisamehe sana"
Aisha alikataa simu na kuizima kabisa, kisha akamwambia Samuel.

"Samuel wazazi wangu wapo nnje ya nchi nataka twende mimi na wewe ili wakakuombe msamaha najua hawataweza kurudi huku sababu tayari wameshazoea mazingira ya kule hivyo kama utakua tayari naomba tujiandae Kwa safari"

Samuel hakua na pingamizi na lile suala walijiandaa kisha Aisha aligharamia kila kitu kuhusu safari yao na kuondoka Tanzania bila ya kumwambia Suma kama anaondoka.

Baada ya kufika kwenye nchi husika Aisha alimkaribisha Samuel wakaingia ndani na kumkuta mama yake akiwa anatazama tv Aisha akamshtua mama yake Kwa sauti.
"Surprise...!"

Mama yake hakuamini kumuona Aisha akiwa hapo alimkumbatia kwa furaha sana na kumuuliza.

"Unaendeleaje mwanangu na huyu mgeni ni nani na watoto wanaendeleaje?"
maswali ya mama yake Aisha yalikua mengi kiasi kwamba Aisha alishindwa ajibu lipi na aliache lipi.

Kabla ya kuanza kutaka kuzungumza mara baba yake na mdogo wake walifika Aisha kama kawaida alimkumbatia baba yake na kumsalimia na mdogo ake pia kisha wakiwa wamekaa wanataka kuzungumza mara ghafla mlango uligongwa.

Baba yake Aisha alienda kufungua mlango na baada ya kufungua akakutana na askari wa hapo nchini akazungumza.

"Kuna raia wawili wameingia humu ndani mda mchache uliopita hawakufanyiwa uchunguzi kama ni raia kutoka wapi?"

Samuel na Aisha walitoka na kuonesha vitambulisho vyao kisha wale polisi wakaondoka baada ya kujiridhisha lakini walidai watakuja tena kama kuna tatizo limetokea, baada ya kuondoka baba yake Aisha akauliza.

"Aisha kuna nini kimetokea mbona unataka kutuingiza kwenye matatizo shida nini?"

"Baba na mama huyu mnaemuona hapa ni kijana ambae wazazi wake waliuawa badala yenu nyie, hivyo nimemleta kwenu kwaajili ya kumuomba msamaha"

"We mtoto unaongea ujinga Gani?"

"Mume wangu nikweli alichokisema Aisha hivi nani anaeweza kujitolea kufa yeye badala yako na wala huusiani nae hata kidogo eeh, kumbuka mume wangu hata yeye ni mtoto alitakiwa awe na wazazi wake lakini tumemfanya awe mpweke sana maskini, baba naomba utusamehe sana kwa kilichotokea najua hatuwezi kulipa kwa kile ambacho kimetokea lakini kauli ya kudhihirisha msamaha huu utatuponya hata wazazi wako pia kama walikua wamechukia watakunjua roho zao kwaajili yetu na kuhitaji tuishi kwa amani bila malumabano"

"Mama usijali kuhusu hilo nimewasemehe kwa moyo mmoja lakini nina ombi moja kwenu kama mtaliafiki"

"Ombi gani kijana sema tunakusikiliza"

"Naomba kama mtanikubali niwe mmoja ya familia wenu"

Mama yake Aisha alitabasamu na kumwambia
"Hee hilo tu wala hata usijali kijana wangu jisikie amani kabisa"

Basi walifurahi pamoja lakini baba yake Aisha alikua bado ana hasira akamuuliza Aisha.
"Nimekuuliza kuna nini kimetokea hadi polis waje hapa?"

"Baba tumelipa kisasi kwa walioshiriki kufanya mauwaji na Dan ndio alifanya yote na hata yeye pia amejiua na kukiri hata yeye amehusika"

Baba yake Aisha alichoka sana kwa kile alichokisikia na baada ya muda mfupi polisi walikua tena na safari hii waliwachukua Samuel na Aisha kwenda kutoa maelezo mafupi na walipoachiwa wakati wanarudi Samuel alikua anafuraha sana kumwambia Aisha..

"Natamani tusirudi Tanzania kwanini tusiishi huku?"

"Hapana Samuel siwezi kuishi huku sababu Tanzania kuna familia yangu najua kua hata hii ni familia yangu lakini nimeolewa tayari siwezi kuishi na wazazi tena"
Samuel alibaki kimyaa tu.

Baada ya siku kadhaa Aisha aliaga kua anaondoka na Samuel pia hivyo waliondoka pamoja tena kama walivyoenda.

Aisha alifika nyumbani kwake na kufungua geti la nyumba yao akawakuta watoto wake wanacheza na baba yao kwa furaha sana lakini lilipofunguliwa tu geti wote waligeuka na kutazama getini na wote wakaanza kumkimbilia mama yao, Suma pia alimkimbilia. Aisha aliwaacha watoto na kumkumbatia mume wake kwa furaha sana na mabusu kama yote Suma hakuamini kama Aisha amerudi tena kwake akamwambia.

"Siamini kama ungerudi Aisha wangu"

"Suma sikua na sababu maalum ya kukuacha Suma naomba nisamehe sana mpenzi wangu"

"I miss you Aisha na naomba tusahau yote yaliyopita na tuanze upya"

Aisha hakutaka kumkumbusha yaliyopita na baada ya kuridhika na mazungumzo yao ya kimahaba wakawabeba watoto wao na kuingia ndani wakiwa nafuraha.

Aisha akisema
"Baada ya keo nataka twende kwa mama maana tangu aondoke sijawahi kuongea nae"

"Hata mimi pia sijawahi kumtafuta"
basi pale walipiga story nyingi kisha Aisha alipoingia chumbani akakuta mabadiliko sana maana tayari watoto walishatengezewa vitanda vyao, Aisha alifurahi sana kwakua watoto walikua wameshalala waliwalaza kwenye vitanda vyao Kisha Aisha akamwambia Suma.

"Umekua ukinijali siku zote sikua najua kama hata watoto ungeweza kuwajali hivi na wapo wawili na vile wana utundu, Suma nakupenda sana"

"Aisha yote nimefanya kwaajili ya kujisafisha kwako kwa kile nilichokifanyia kipindi Cha nyuma na tukiachana na hayo sasa keo siwezi kuacha upumzike sababu nimekumiss sana mke wangu"

Aisha alitabasamu na kumtazama kwa madeko mume wake na vile Suma hana kona kona fasta tu wakajikuta kitandani, wakifanya usafi wa chumba. [emoji23][emoji12]

Siku iliyofata walijiandaa vizuri kisha Aisha alimpigia simu Samuel na Suma alimpigia simu Juma na marafiki zake wengine kisha wakakodi Kosta hadi anapoishi mama yake.

Na ilikua siku ya kuzaliwa mama yake Suma hivyo ilikua furaha sana kwa wote.
Siku hiyo walimtambulisha mwana familia mpya ambae ni Samuel pia Suma na Juma pia walisameheana kuhusu ugomvi wa kumsaidia kaka yake ambae alimsaidia na mwisho Suma akasema.

"Nawashukuru sana ndugu zangu kwa kuwa na sisi kuanzia mwanzo wa shughuli hadi hapa mwisho na kitu kingine pia naomba niwashukuru Juma na marafiki zangu wakina Rama na wengine pia kwa kunipokea na kunisapoti kwa kila njia sina cha kuwalipa zaidi ya kuwatakia mafanikio zaidi na umri mrefu wa kuendelea kufurahia Nawapenda sana"

WEMA HULIPWA NA WEMA HATA UBAYA HULIPWA NA WEMA PIA KIKUBWA KUWA NA MOYO WA HURUMA KWA BINADAMU WENZETU SABABU HUWEZI IJUA KESHO YAKO MUNGU HUTOA MITIHANI NA YEYE NDIO HUTUTATULIA PIA KIKUBWA NI IMANI NA MOYO WA MATUMAINI


MWISHO
 
Back
Top Bottom