Simulizi za Mkatekumeni: Kikao changu na Waziri Mkuu Mwigulu

Simulizi za Mkatekumeni: Kikao changu na Waziri Mkuu Mwigulu

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,436
Reaction score
4,756
Habari za Usiku huu;

Kama Unavyoona sa hivi ni usiku wa manane. Nimeamka usingizini, nimechukua chombo changu cha kazi na nimeingi kazini.

Hili ni andiko la kwanza katika Mtiririko wa Simulizi za Mkatekumeni ambapo nitakuwa nikiwaletea maandiko ya Ndoto mbalimbali ambazo nitakuwa ninaziota hasa zile ambazo zitakuwa na wahusika ambao ni viongozi wa nchi au Dunia.

Nitajitahidi mara zote nitakapoleta andiko basi liwe kweli limetoka katika Ndoto na liwe uncensored.

Leo Tarehe 5 Machi 2026 katika ndoto yangu ya Usiku huu ambayo imehitimu mnamo saa kumi kamili ya asubuhi nimeota njozi.Katika njozi hiyo Nilikuwa katika kikao na Mwigulu Nchema kama Waziri Mkuu na kikao hicho tulikuwepo watu wanne ambapo ni Mimi Mkatekumeni, Mwanaharakati Maria Tsehai na Mtanzania mwingine mwanama ambaye sijaweza kumtambua nani.

Mjadala ulianza kwa sauti ya utulivu. Maria hakuwa yule mkalimkali mwenye Hasira wa Mwigulu hakuwa yule mshambamshamba anayejipendekeza. Wala yule dada wa tatu hakuonekana kuwa na hali au hisia yoyote tofauti. Hata hivyo katika kikao hicho sijui kwa sababu ilikuwa ndoto mimi nilikuwa kama mind reader, chief listener na focust of attention. Lakini Pia nilikuwa na hoja nzito uelewa mpana na nilikuwa naongea kama mtu mwenye Mamlaka.

Mtu wa kwanza kuzungumza alikuwa Mwigulu Nchemba. Alieleza mambo mengi sana kuhusu uongozi na utawala aligusia hali ya nchi,changamoto, maono na malengo yake kama waziri mkuu. Alipomaliza nilimpokea Juu kwa Juu na nikamwambia; "Mh, Waziri Najua hapa tuko wachache na baadhi ya tunayosema hapa yanaweza fika kwenye Media ila kwa kuwa tuko wenyewe naomba kwanza nianze kwa kukwambia kwamba 'YOU HAVE NO CLUE what it means to be a PRIME Minister'.

Kwa Ukali kabisa
Nilimwambia Sielewi Rais aliona nini kwake mpaka akamteua kuwa Waziri Mkuu. Nikamwambia anajua ilivyoheshima kuteuliwa kuwa waziri Mkuu? Unafahamu kwamba Waziri Mkuu Ndiye Kiongozi Pekee mwenye mamlaka ya kiutendaji ndani ya Tanzania Bara?Unafahamu kwamba Waziri Mkuu ndiye kiongozi Pekee mwenye mamlaka makubwa ndani ya Tanzania Bara kuliko Hata Rais? Unafahamu kwamba Waziri Mkuu Ndio kiongozi Pekee ambaye anaweza Ku override maamuzi ya Rais?Unafahamu kwamba Waziri Mkuu ndiye kiongozi Pekee ambaye RAIS analazimika kumsikiliza na kwamba Kama hakubaliani naye inabidi amfute uwaziri Mkuu?"

Nilipomaliza kumlima hizo spana Maria Sarungi aliniambia nipunguze ukali wa maneno na kuniomba nisiumuudhi wala kutumia maneno makali kwani naweza fanya kikao kikaharibika.

Nilishangazwa na Upole wa Maria Sarungi hata hivyo nilishangazwa zaidi Mwigulu aliposema tusijali. Alisema Tuendelee kuongea maana katika uongozi ni mara chache sana wanapata nafasi ya kuambiwa kwa ukali, kukosolewa kwa ukali hasa in Private. Anasema kwamba anatamani sana kama Mkatekumeni angekuwa sehemu ya Washauri wake kwani namna yake ya kuongea ndio ambayo viongozi wanataka.

Mwigulu alikiri kwamba Uongozi una changamoto na kuna wakati kiongozi unakosea sio kwa sababu huwezi ila ni kwa sababu haiwezekani na hakuna atakayekwambia haiwezekani na washauri na wasidizi wako daima watakwambia kile ambacho kinakukufurahisha.

Alinitazama kwa macho ya Pleading akiniomba niwe sehemu ya washauri wake nami nikamwambia tu kwamba. Nikiwa mshauri wake nitamchosha sana itapendeza zaidi kama nikiwa mshauri wa washauri wake maana hata washauri nao huhitaji washauri ili wawe kushauri ushauri mzuri. Alifurahi sana akasema tu kwamba ataomba tu vikao vyetu na washauri wake basi viwe vinakuwa recorded il anapokuwa Barabara na Dereveva wake awe anawekewa kama Audio asikilize namna tunavyojadiliana kushauriana kuhusu masuala mbalimbali na atakuwa anatupa masuala ya kujadili kila mara kuhusu mustakabali wa nchi.

Baada ya kumaliza hapo aliniomba niendelee kusemu kile nilitaka kusema ili na wengine wapate nafasi pia ya kusema na kuuzliza maswali.

Basi niliendelea kumwambia "Unapokuwa Waziri mkuu unakuwa hauna anasa ya kukosea, unakuwa hauna anasa ya kuwa kikaragosi, unakuwa hauna anasa ya kuingia kwenye mijada isiyokuwa na TIJA. Unapokuwa waziri Mkuu unapaswa kuwa katika Mijadala ya kisera na kimsimamo. Kila wazo, kila fikra na kila kauli unayotoa ni lazima iwe imepimwa katika mizania ya Kisera(Policy) na kimkakati(Strategy).

Ni lazima ulazimishe mijaala ya kisiasa iwe centred kwenye Sera za nchi. Watu wanapokujadili au kuijadili wajadili kwa kusema. Hii sera ni nzuri/mbaya. Huu uamuzi ni mzuri au mbaya. Hizi hatua zilizofanyika ni nzuri au mbaya. Na mijadala inapofanyika Ujitahidi kusikiliza na sio kujibu, majibu yako yawe ama kwa Vitenda au kwa kutoa Taarifa sahihi ili watu waelewe zaidi maana baadhi ya matatizo yanasababishwa na watu kukosa uelewa"

Kwa kuwa mimi ndio nilikuwa Muota ndoto nilipewa nafasi ndefu zaidi ya kuongea hivyo niliendelee kumueleza kwamba unapofikiri kuhusu mustakabala wa nchi usifikiri kuhusu Short term Goals ni lazima ufikirie zaidi ya Umaarufu wa sasa hivi, Ni lazima ufikirie zaidi ya mafanikio ya sasa hivi,ni lazima ufikirie zaidi ya ushindi wa kisiasa na ni lazima ufikirie zaidi ya mafanikio yako. Kama Waziri Mkuu ni lazima ufikiri labda miaka 20 ijayo, miaka 100 ijayo au hata miaka 1,000 ijayo kama unaweza.

Nilimsisitizia umuhimu wa kufanya Long term thinking na mbinu za kufanya Long term thinking. Nilimpa Mbinu moja Rahisi sana. Nilimwambia "Think about the Children" Hii mbinu ya Kufikiria kuhusu watoto ni nzuri sana. Ni nzuri sana kwa viongozi wakubwa wa nchi kufikiria kwani inawsaidia kuweza kuweka mambo katika mizania ya long term.

NIlimweleza yafuatayo kuhusu mbinu hii. Nilimwambia unapozungumza na viongozi wenzako walioko Juu yako na hata walioko chini yako, unapozungumza na watumishi wa umma, unapozungumza na wananchi wa kawaida, wasomi, wafanyabiashara na watu wote maarufu kama kiongozi jitahidi mijadala yenu yote ilenge Watoto wenu.

Watazame hawa wote kama wazazi wenye watoto ambao wako tayari kufanya lolote kwa ajili ya kuwapa watoto wao maisha yenye furaha.

Sasa unapowatazama na mnapojadiliana kuhusu masuala ya kisera na maendelea muwaze juu ya watoto wenu. Mnataka watoto wenu wasome katika shule zai aina gani? Wale vyakula vya aina gani, walalae katika mazingira ya aina gani? Wacheze michezo ya aina gani? Watakapokuwa watu wazima wafanye kazi/shughuli za aina gani? Waishi maisha ya aina gani? Waendeshe magari ya aina gani?Walipwe mshahara kiasi gani? Wafanye biashara gani? n.k. Wafikirie watoto wako na watoto wengine? Jiulize wawe na marafiki wa aina gani? Majirani wa aina gani? Waoe mwanamke wa aina gani? Waolewe na mwanaume wa aina gani?

Kwa hakika Kama Viongozi wote, watumishi wote na wananchi wote wakifanya mambo kwa kufikiria watoto wao na aina ya dunia ambayo wanataka watoto wao waishi maamuzi mengi mabaya hayatafanyika. Rushwa itapungua, uzembe na ubadhirifu utapungua, umaskini utapungua, chuki za kisiasa zitapungua.

Nilimaliza kwa kumwambia Mwigulu kwamba yeye kama Waziri Mkuu Watoto wote wa Tanganyika ni watoto wake na anapaswa kufikiri kuhusu hao watoto katika kila kauli yake, maamuzi yake na uendeshaji wa nchi.

Baada ya kumaliza kuongea alifuata Maria Tsehai ambaye kwanza alianza kumuulza kuhusu masuala mbalimbali ya kisera na udaku. Alimuuliza kuhusu Matukio ya Oktoba 29 alimuuliza kuhusu tume ya Jaji Chande na hata kugusia kidogo kuhusu suala la Serikali kushtakiwa ICC na kwingine DUniani. Mwigulu alimtazama sana Maria huku Machozi yakiwa yanamlengalenga akasema - Kuna mambo nawaambia ambayo natamani yasisikike Popote ila ndio ukweli. Kila aliyehusika katika Matukio ya Oktoba 29 anaumia, analia na kuomboleza. Rais anaumia na kuomboleza, Mawaziri wanalia na kuomboleza, Polisi wanalia na kuomboleza, wanajeshi wanalia na kuomboleza, Usalama wa Taifa wanalia na kuomboleza, viongozi waliohusika na hata ambao hawakuhusika wanalia na kuomboleza. Wengi wanatamani ile siku iwe ni ndoto tu na yaliyotokea yawe ni ndoto tu. Wanatamani labda wasingekuwa viongozi wakati yale yanatokea.

Alimwambia Maria kwamba huenda watu wasikiri wazi, wala kusema kwa uwazi ili wanaumia na kujuta sana. Wanajaribu kufikiri kama kuna namna wangeweza kufanya ili yale yaliyotekea yasitokee. Hata hivyo alisisitiza Jambo moja. Alisema kwamba unapokuwa kiongozi kuna maamuzi ambayo unafanya ambayo unatamani usifanye. Kuna maamuzi yanafanyika ambayo wewe huwezi kukubaliana nayo ila uongozi na nafasi yako unakutaka ukubaliane nayo. Unapokuwa kiongozi kuna wakati unajiuliza Je, Kama mimi nisipofanya Uamuzi huu nani aufanye? Kuna uamuzi ambao unatakiwa uufanye kwa sababu wewe ni RAIS sasa kama wewe usipoufanye nani aufanye? Je huyo mwingine ambaye utamuachia afanye una uhakika gani kwamba atafanya uamuzi sahihi iwapo wewe umeshindwa? Inapofikia Hatua hiyo huwa unalazimika kufanya uamuzi.

Mwigulu akasema Tarehe 29 Oktoba watu wengi sana walifanya maamuzi magumu. Maamuzi ambayo yaliwakumbusha wajibu wao wa msingi wa kujiuliza Kama sio mimi Je nani anapaswa kuamua kuhusu hili?Je atafanya uamuzi sahihi? Uamuzi sahihi ni upi? Alisema tunaweza tusiwatambue watu hao ili uzalendo wao na kujitoa kwao kulikuwa kwa kiwango cha Juu sana na watabaki katika Historia.

Alimwamba Maria kwamba wewe ulikuwa mtandaoni ukiwahamasisha watu kwa sababu uliamini kwamba uko sahihi ila Je unafahamu kwamba kuna watu ambao walikuwa wanatumia upepo wenu ili kufanikisha Sinister Objectives?Unafahamu kwamba labda kama maamuzi yaliyofanyia yasingefanyika tungekuwa na madhara makubwa zaidi?

Mwigulu alimaliza kwa kusema.nTunawaheshimu sana wanaharakati na wapinzani pale mnapokuja na Hoja za Kutufanya tufanye kazi vizuri ila mnapochagua kwamba nchi ianguke ili tu mpate nafasi ya kutawala inakuwa vigumu sana kuwaelewa iwapo kweli mna nia njema na nchi yetu.nTunashindwa kuwaelewa iwapo kweli ninyi ni wazalendo na mnaelewa changamoto za nchi yetu. Mnaweza kutamani aina ya siasa za nchi nyingine ila Je kwanini msiamue tu kuchukua uraia wa hizo nchi halafu mfurahia hio siasa na mfumo wao wa kisiasa huko badala ya kujaribu kuleta mambo ya kule kwao hapa kwetu?Jaribuni tu kama mko Kenya mtukane viongozi wa Kenya au kama Mko Marekani mtukane viongozi wa Marekani. Mvunje sheria za nchi kwa kisingizio cha kudai haki muone kama wataacha kuwachukulia hatua.

Alisema kwamba Serikali ilijifunza kitu na inataka sana kufanya mambo yaende sawa. Wanaomba wapewe nafasi..

Baada ya Mwigulu kusema hivyo yule mshiriki wa tatu alitoa naye maoni na ushauri wake akisema Serikali iangalie namna ya kufuta Kesi ya Lissu, kuwaachiwa wale waliopotezwa ama kutekwa na kuachia uhuru wa kisiasa. Mwigulu akamtazama Dada yule na kumwambia.

Kwenye Suala la Tundu Lissu, mahakama ndio yenye mamlaka. Serikali kupitia Jeshi la Polisi imetimiza wajibu wake. Tundu Lissu ni mtuhumiwa ka watuhumiwa wengine na anafanya kazi nzuri ya kujitetea na tuamini kwamba mahakama itatenda haki. Serikali haina lengo la kuingilia mchakato wa kimahakama ingawa imepokea maombi, maelekezo na hata mkandamizo wa nje ya nchi wa kutaka kumuachia ila kwa sasa hivi serikali bado haiwezi kuingilia mchakato wa kimahakama.

Kuhusu waliotekwa na kupotezwa Mwigulu alisema Hata yeye mwenyewe hajui wapo wapi watu hao na wamekamatwaje na nani?Amekiri kwamba Jambo hili linampa hofu hata yeye na ukimya wa vyombo vya Ulinzi na usalama una maana kwamba bada hawajapata uelekeo na taarifa sahihi. Anasema Tuhuma na kunyoosheana vidole ni kwingi ila akasema serikali inaendelea kufauatilia na kama kweli wametekwa na wapo mahali basi na yeye atajitahidi kuhakikisha wanaachiliwa ila kwa sasa hata yeye anakosa kauli ya kusema.

Kama nilivyoeleza mwanzoni hii ni ndoto katika ndoto hii alikuwepo Nchemba, Maria, Mimi Mkatekumeni na Mwananchi mmoja ambaye sijamfahamu bado. Pamoja na kwamba ni ndoto ila naamini ina ujumbe ambao unaweza Pita mchujo wa Moderators wa JF na iwapo utapita basi RASMI nitakuwa nikiwaletea Ndoto zangu kila nitakapoziota. Muda na wakati kama huu.

Nawatakieni SIKU NJEMA..

Mungu awabariki

Mimi wenu

Mkatekumeni
 
Habari za Usiku huu;

Kama Unavyoona sa hivi ni usiku wa manane. Nimeamka usingizini, nimechukua chombo changu cha kazi na nimeingi kazini.
huu.

Nawatakieni SIKU NJEMA..

Mungu awabariki

Mimi wenu

Mkatekumeni
Asante, amen
P
 
Back
Top Bottom