Sina amani naye japo nampenda huyu binti

Bin Shaib

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2019
Posts
1,346
Reaction score
1,221
Bwana wetu Yesu asifiwe wapendwa, Asalaam naalykum kwa waisilam wote natumaini mu wazima wote.

Moja kwa moja nizame ndani ya maada wapendwa. Mimi ni kijana ambaye natarajia kuingia kunako ndoa ikimpendeza Mungu wangu,
Umri wangu miaka 25

Kuna binti ambae tulikutana kwa mazingira fulani tukazoeana na tunaishi naye mitaa ya karibu japo kuna umbali kidogo, baadae alichukua namba yangu bila mi kujua, baadae ndo kuanza kuchati pamoja na mazungumzo kwa njia ya simu na ana kwa ana hadi kufikia binti kunitamkia kuwa anahitaji me niwe mme wake wa ndoa na ananipenda ,, basi sikumpa jibu la kumaanisha nikamwambia poa ikimpendeza Mungu tutakuwa pamoja.

Nimekaa naye hivo huku nikiendelea kumchunguza basi nami moyo wangu ukazidi kumpenda kila kukicha na nipo radhi kumuoa japo hapa katikati ilitokea changamoto fulani ambayo nikawa najiuliza saana, kuna kuna jamaa ambae tunasali nae kanisa moja naye akawa anamtaka kwamba anahitaji kumuoa na binti akawa ananitumia zile chating za jamaa akimuomba anahitaji kuwa naye.

Binti akanithibitishia kuwa anipenda mie na akamtumia jamaa sms kuwa mi ndo ntakuwa mumewe au baba watoto wake,, lakini sijajua kama jamaa bado wanaendelea naye katika harakati hizo.

Changamoto ya huyu binti:
Au niseme asili yake ambayo nishaiona kwake ni mtu ambae anapenda kuongea na kila mtu halafu ni mwongeaji sana halafu marafiki wengi wa kiume na kuchati anachat sana kila wakati yaani chaji yake huwa inaisha mara nyingi kwa kuchat hata nikiwa nae sms mara kwa mara zinaingia kwake, hiyo hali inanitia shaka je atakuwa mwaminifu kweli kama mimi nilivyo mwaminifu kwake?

Je, ntaiweza kweli hii hali maana mpaka tusha elewana me nikipata mahari nimchukue mtoto niweke ndani,,

Wadau kwa hili limekaaje?
 
Kahangaike na mke wa Mjomba tuu jamaa angu.
Kwani kwa mjomba hujaondoka bado tuu
 
Alichukua namba Yako bila wewe kujua......

Anachat akiwa na wewe...?

Hapo kuna mawili. Tandika kofi Moja hatarious awe na adabu ama mteme akakalie wengine huko mbele ya safari.
Kwanini wanawake hua mnaencourage sexual violence?

As in hapa umetoa ushauri huyu jamaa akampige kofi huyo binti na maoni yako wanashare wanawake wengi nilioongea nao. Mmoja aliwahi sema kwamba siku nyingine mwanamke anaamka anakua anatamani kupigwa.
 
Alichukua namba Yako bila wewe kujua......

Anachat akiwa na wewe...?

Hapo kuna mawili. Tandika kofi Moja hatarious awe na adabu ama mteme akakalie wengine huko mbele ya safari.
Vp mkuu kuna ulazima wa kumwambia kuwa sipendezwi na tabia yake?

Maana nakumbuka siku moja tupo tunaongea kwa njia ya simu kumbe kaongeza round speaker ananiskilz huku anachat,nikaskia vibatan vinasikika ndo nikamwambia harafu upo unachati?

Ndo kuomba msamaha nimsamehe basi nikamwambia haina shida tukaendelea na mazungumzo yetu.
 
Miaka 25 mkristo,unataka kuoa ili iweje???????

Mwanamke anaweza kuzoea wanaume elfu lkn akipata mmoja mjanja mjanja ni lazima atagongwa kimasihara refer uzi wa kula tunda kimasihara..

Halafu hautakaa ujue
 
Miaka 25 mkristo,unataka kuoa ili iweje???????

Mwanamke anaweza kuzoea wanaume elfu lkn akipata mmoja mjanja mjanja ni lazima atagongwa kimasihara refer uzi wa kula tunda kimasihara..

Halafu hautakaa ujue
Nisawa lakini me kumula kimasihara inawezekana lakini naogopa mahusiano yangu na Mungu wangu.
 
Mueleze mze tabia usizopenda kwake kama hizo za kuchati chati kama mtoa huduma na wanasema hakuna urafiki baina ya jinsia mbili tofauti ipo siku yatatokea ya kutokea tu.
naungana na huyu jamaa. unapokua mwanaume ni vizuri ukawa na principles zako na aina ya msichana unaemtaka. kama ana tabia fulani huipendi mueke wazi, kama anaweza kujirekebisha ajirekebishe., kama hawezi basi mwambie tu muachane, kwanini ukae na kitu usichokipenda moyoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…