Sina amani naye japo nampenda huyu binti

Asante kwa mawazo yako mkuu me ntajitahidi kama niwakubadilika atabadilika, Shukrani mkuu
 
Nisawa lakini me kumula kimasihara inawezekana lakini naogopa mahusiano yangu na Mungu wangu.

Nadhani wewe unapaswa upate mwanamke mshika dini na sio huyo chakalamu..Tafuta wa kufanana nae huyo sio size yako na yeye anajua kbs kwa kichaa chake anahitaji mwanaume kama wewe nice boy.

Anaenda kufanya ujinga wake huko anapumzika kwako religion boy

Kwahiyo mzee hapana ngono mpaka ndoa au dini kwenye mambo mengine tu ila mahusiano fresh tu???
 
Kwa hiyo mkuu yaweza kuwa ni shetani anataka kuniharibia maisha?
Acha mawazo potofu, maisha unapanga wewe unataka uishi vipi, fikra za shetani kukuharibia maisha zitakuharibu, shetani anaweza kuwepo au asiwepo lakini uwezo wa kukuharibia maisha hana.

Ushauri kuhusu huyo binti na tabia yake ya kuchati ukiwa nae, kwanza hakuheshimu, kwasababu kwa mtu anayeheshimu mahusiano yake hawezi kuonesha tabia ambayo inahisiwa ni ya kimalaya, unaonekan hujawahi kumwambia hupendezwi na hiyo tabia.

Mwanamke anakujaje from nowhere anakuambia umuoe?na wewe unataka kumuoa?, 25 lakini uko obsessed na ndoa? Tuliza mpira huyo binti asikufanye uwe pressured na ndoa, tulia endelea kumchunguza vizuri.
 
Ni kweli mkuu kwa ninavyo jijua mimi na Mungu wangu nahitaji mwanake mwenye hofu ya Mungu ndo tutaendana, nikimwangalia huyu nahisi bado hajamshika Mungu sawasawa.
 
Ni kweli mkuu kwa ninavyo jijua mimi na Mungu wangu nahitaji mwanake mwenye hofu ya Mungu ndo tutaendana, nikimwangalia huyu nahisi bado hajamshika Mungu sawasawa.
Kweli kabisa ndege wafananao huruka pamoja umemshika mungu tafuta mshika mungu mwenzako lasivyo utakutana na kitu kitakacho kutoa kwenye njia.
 
Nakazia hapo.
 
Sawa mkuu nimekuelewa na ubarikiwe kwa ushauri wako ngoja nizidi kumchunguza yasije nitokea puani.
 
Wewe una miaka 25...

Bila shaka mwanamke ana miaka 25 au chini ya hapo, umri sahihi kabisa wa 'nyege ndoa' kwa wanawake...

Ndio umri wanawake wengi wanapigwa mimba sababu tu wanataka ndoa...

Usioe mwanamke kwenye range hiyo maana huwa hawajaamua mtu sahihi wa kuwa nao...
 
Yeye binti atakuwa kwenye miaka 19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…